MLANGO 12

SALA YA IDI

Sala ya Idul-Fitri na Idul-Adh-ha (sikukuu kubwa) asili yake ni faradhi; na mmoja katika shuruti zake muhimu ni kuhudhuria Mtume (s.a.w.) au mmoja katika Ma-Imamu kumi na wawili au Naibu wao mahsusi. Kwa vile sharti ya sala hiyo wakati huu haikutimu, basi sala hiyo sasa ni suna tu.

Sala hiyo unaweza kusali peke yako na kwa jamaa pia; ni bora na ina thawabu nyingi kusali kwa jamaa. Wakati wa kusali sala za Idi ni wakati wa kutoka jua hadi adhuri.

Namna ya kusali:

Sala za Idi ni rakaa mbili tu. Baada ya kunuia na kutamka Takbeeratul Ihram, katika hali ya kusimama (Qiyaam) uta soma Sura ya AL-HAMDU na baadaye Sura moja ya Qur’ani, (Ni bora kabisa kusoma Sura ya AL-AALA (S87) inayo anza kwa SAB-BI-HIS-MA, RAB-BIKAL-AALA). Ukiisha maliza Sura hiyo, utatamka takbira mara tano, na baada ya kila takbira utafanya Qunuut (unyanyue mikono yako juu sawa na uso wako kama tulivyoeleza katika mlango wa14 wa kitabu cha sala). na utasoma dua ifuatayo. Tena utatamka takbira ya sita na utakwenda rukuu tena sajdah mbili. Hapo utainuka kwa rakaa ya pili na utasoma Sura ya Al-Hamdu na baadaye Sura moja ya Qur’ani (Ni bora sana kusoma Sura ya WASH-SHAMSI. Na baadaye utatamka takbira nne mara hii, na baada ya kila takbira utafanya Qunuut, na utasoma dua ifuatayo. Tena utatamka takbira ya tano, na utakwenda rukuu, tena sajda mbili; baadaye utakaa utasoma 'Tashah-hud' na baadaye utamaliza sala kwa kutoa salaam kama desturi. Unaweza vile vile katika sala ya Idi baada ya 'Alhamdu,. katika rakaa ya kwanza usome Sura ya Wash-shamsi na katika rakaa ya pili baada ya 'Alhamdu' usome Sura ya 'Ghaa-shiya' inaanzia Hal ataaka hadee-thul ghaa-shiya.

DUA YA QUNUUT

ÇóááøÜåõãøó Çóåúáó ÇáúßöÈúÑöíÇÁö æóÇáúÚóÙóãóÉö¡ æóÇóåúáó ÇáúÌõæÏö æóÇáúÌóÈóÑõæÊö¡ æóÇóåúáó ÇáúÚóÝúæö æóÇáÑøóÍúãóÉö¡ æóÇóåúáó ÇáÊøóÞúæì æóÇáúãóÛúÝöÑóÉö¡ ÇóÓúÇóáõßó ÈöÍóÞøö åÐóÇ Çáúíóæãö ÇáøóÐí ÌóÚóáúÊóåõ áöáúãõÓúáöãíäó ÚíÏÇð¡ æóáöõãÍóãøóÏ Õóáøóì Çááåõ Úóáóíúåö æóÂáöåö ÐõÎúÑÇð æóÔóÑóÝÇð æóãóÒíúÏÇð¡ Çóäú ÊõÕóáøöíó Úóáì ãõÍóãøóÏ æóÂáö ãõÍóãøóÏ¡ æóÇóäú ÊõÏúÎöáóäí Ýí ßõáøö ÎóíúÑ ÇóÏúÎóáúÊó Ýíåö ãõÍóãøóÏÇð æóÂáó ãõÍóãøóÏ¡ æóÇóäú ÊõÎúÑöÌóäí ãöäú ßõáøö ÓõæÁ ÇóÎúÑóÌúÊó ãöäúåõ ãõÍóãøóÏÇð æóÂáó ãõÍóãøóÏ ÕóáóæÇÊõßó Úóáóíúåö æóÚóáóíúåöãú¡ ÇóááøÜåõãøó Çöäøí ÇóÓúÇóáõßó ÎóíúÑó ãÇ ÓóÃóáóßó ãöäúåõ ÚöÈÇÏõßó ÇáÕøÇáöÍõæäó¡ æóÇóÚõæÐõ Èößó ãöãøóÇ ÇÓúÊÚÇÐó ãöäúåõ ÚöÈÇÏõßó ÇáúÕøÇáöÍõæäó .

Ikiwa mtu anasali sala za Idi kwa jamaa, lazima asisome Qara-at (sura ya Alhamdu na sura nyingine) kama anavyosali sala za fardhi kwa jamaa kila siku, kwa kuacha kusoma Qaraat tu, huku amsikie Imaamu anazisoma; vitendo na masemo yaliyobaki yote lazima atende na ayasome yeye.

Ikiwa Maamumu kafika wakati ambapo Imaam ameshazisoma baadhi ya Qunuut basi akienda Imaam katika rukuu yeye azitimize zile Qunuuti asizoziwahi, ijapokuwa katika kila Qunuut akisema SUB-HAANAL-LAAh, au AL-HAMDU-LIL-LAAH. pia itatosha na baadaye amfuatie Imaam.

Ikiwa mtu katika sala ya Idi kafika wakati ambao imaam yupo katika rukuu, basi baada ya nia na kusema Takbeeratul  Ihraam  tu,  amfuate  Imaam  (aingie  katika rukuu).

Ni sunna baada ya sala ya magharibi, isha, usiku, kuamkia Idul-Fitri na baada ya Idul-Fitri kuzisoma takbeeraa hizi : Al-laa-hu akbar, Al-laa-hu-akbar, Laa-ilaa-ha il-Ial-laa-hu wal-laahu-akbar, Al-laa-hu-akbar, walil-laa-hil-hamd, Al-laa-hu-akbar alaa maa hadaa-naa.

Na ikiwa Idul-Adh-ha basi Takbeeraa hizo ni sunna kuzisoma baada ya sala kumi (10) kuanzia sala ya adhuhuri siku hiyo mwezi kumi (mfungo tatu) hadi sala ya asubuhi ya mwezi kumi na mbili; lakini utaongeza Takbeeraa ya sikukuu hii maneno haya: AI-laa-hu akbar, Alaa maa razaqa-naa min bahee-matil an-aam, wal-hamdu-lillaahi alaa maa ab-laa-naa.

Na ikiwa Mwenyezi Mungu amemjaalia mtu awepo Hija katika Mina siku hiyo, basi Takbeera ufululize hadi baada ya sala ya asubuhi ya tarehe kumi na tatu (mfungo tatu). Mwenyezi Mungu "atujalie sote tuwepo huko kila mwaka. Amin.

Mwenyezi Mungu amesema katika Qur’ani: Wali-tuk-milul-iddata, wali-tukab-birul-laaha ala maa hadaa-kum, wala-allakum tash-ku-ruun (2:185). (Na pia anakutakieni mtimize siku za mwezi huu (wa kufunga), anakutakieni kumtukuza Mwenyezi Mungu kwa kuwa amekuongozeni kwenye dini, ili mpate kumshukuru kwa neema hiyo na neema zote).

Katika hadithi inayotokana na Al-Imaam Ar-Ridha (a.s.), Imaam wa nane, imesema hivi: "Kwa ajili ya hii, katika sala ya Idi imefanywa takbira nyingi zaidi kuliko sala zote zingine; kwa sababu, takbira, hakika, ni taadhima kwa Mola na kumtukuza kwa namna alivyotuahidi na kutupa afya, kufuata alivyosema Mwenyezi Mungu katika Qur’ani.

ÑóÈøóäóÇ ÊóÞóÈøóáú ãöäøóÇ Åöäøóßó ÃóäÊó ÇáÓøóãöíÚõ ÇáúÚóáöíãõ

ÓõÈúÍóÇäó Çááåö æó ÇáúÍóãúÏõ öááåö æó áÇó Åöáóåó ÅöáÇøó Çááåõ æó Çááåõ ÃóßúÈóÑõ


[1] Subh-Saadiq ni weupe wa mchana unaonekana kwenye mstari wa upeo wa macho upande wa mashariki wenye kutanuka 'kwa upana, na kuzidi kua mweupe mpaka linapotoka jua, na ndio wakati ambapo huwa haramu kula na kila kinachovunja Saumu kwa mwenye kutaka kufunga.

Magharibi: Kwa kawaida magharibi ni wakati jua linapozama na kufichika upeo wa macho, na kwa sharia ni wakati ule wekundu unaonekana upande wa mashariki baada ya kuzama juu ufike sawa na utosi mbinguni

[2] Tazamo lapili". maana yake tazamo la haramu juu ya mwanamke asie wako. Binadamu inapoanguka nadhari yake ya kwanza kwa ghafla, au kwa kusahau, au kosa kujua, juu ya mwanamke (asie wake) au kitu kilichoharamishwa kutazama, na akitazama tena mara ya pili, basi hiyo tazamo la pili ni haramu, asitazame.

[3] Alama za ubalehe ni moja katika hizi tatu : (a) Kutoka manii (shahawa) macho au usingizini. Alama za kupambanua (kufafanua) manii, kwa mtu mzima (asiye mgonjwa) ni tatu. Kwanza, bidii ya moyo inapotoka shahawa. Pili, kumwaga kwa nguvu (kufoka). Tatu, ulegevu wa mwili baada ya kutoka. (b) Kuwa nywele nene (za kukwaruza) chini ya kitovu, juu ya dhakari. (c) Kutimia umri miaka kumi na tano (15). Na alama ya ubalehe wa mtoto wa kike ni kuingia miaka ya kumi katika umri.

[4] Tazama Mafaatihul-Jinaan, uk. 179

[5] Tazama Mafaatihul-Jinaan, uk. 184

[6] Tazama Mafaatihul-Jinaan, uk. 186

[7] Tazama Mafaatihul-jinaan, uk. 428/430.