MLANGO 7

DUA NA AMALI ZA USIKU

Sasa tutaeleza baadhi ya sunna za mwezi huu mtukuu ambazo ni thawabu sana kuzifanya; na ambazo zimepokewa kutoka kwa Mtume wetu (S.A.W.) na Ahlul-Baiti wake (A.S.).

DUA ZA KILA USIKU

(1) Dua Za Kufutoria  :Ukisoma dua zifuatazo kabla ya kufuturu utapata thawabu nyingi:

(a)Al-llaa-humma laka sumtu wa ala riz-qikaa af-tartu wa alay-ka ta-wak-kal-tu.

(b)Soma sura nzima ya al-Qadri (In-na an-zal-na).

(c)Kwenye tonge la kwanza, anzia na Bismillahi, na ufuatie  maneno haya:  Yaa Wa-si-al-magh-firati Igh-fir-lee.

(d) Soma dua hili ambalo Ameerul-mumeneen Ali (A.S.) alikuwa akisoma wakati wa kufuturu: Bismil-lahi, alla-humma laka sumnaa wa ala riz-qi-ka af-tar-naa; fata-qabbal minnaa, Inna-ka an-tas-sa-mee-ul-aleem.

Katika hadithi tukufu nyingi za Mtume (S.A.W.) na Ma-Imamu (A.S.) imesemwa kwamba kufuturia vitu vitamu, kama halua, sukari mawe au tende, kuna thawabu nyingi na pia ni suna ya Mtume (S.A.W.).

Vile vile kufuturu kwa maji ya moto kuna fadhila nyingi na faida kwa roho na kiwiliwili.

Imaam Muhammad al-Baaqir (A.S.) amesema: "Kutanguliza sala (za magharibi na Isha) kabla ya kufuturu kuna thawabu nyingi sana; huandikwa sala hizo thawabu za sala katika hali ya saumu".

Lakini ikiwa mtu anakungojea, au umeshikwa na nja  hutaweza kusali kwa utulivu, hapo bora kufuturu kwanza. Ujitahadhari usichelewe kusali 'katika nyakati za fadhila,

Thawabu ya Kufuturisha

Amehadithia Imaam As-Sadiq (A), kwamba, "Katika mwezi wa Ramadhani, Sudair As-Sairafi alikwenda kwa baba yangu (Imaam Muhammal Al-Baaqir, (A) Imaam wa tano. Akamuliza Imaam, 'Ee Sudair, je wajua siku gani hizi?' Akajibu, 'Ndiyo, nakufidia baba yangu, siku hizi ni siku za Ramadhani, kwani ni nini?' Akamwambia Imaam (A), 'Je unaweza kuweka huru watu kumi katika watoto wa Nabi Ismail (A) kila usiku katika siku hizi?' Akajibu Sudair, 'Nakufidia baba yangu na mama yangu, sina mali kiasi hicho'. Akaendelea Imaam Al-Baaqir (A) kuipunguza hata akafika kuweka huru mtu mmoja tu, na kila mara Sudair akamjibu, 'Siwezi'. Basi akamwambia, 'Je, huwezi kumfuturisha Mwislamu mmoja kila siku?' Akajibu, 'Naweza si mmoja tu, bali hata kumi'. Akamwambia Imaam (A), 'Hiyo ndiyo ninayotaka (ndio shabaha yangu), Ee Sudair. Kumfuturisha ndugu yako Mwislamu ni sawa (thawabu yake) kama kumweka huru mmoja katika watoto wa Mtume Ismail'".

Imepokewa hadithi kwa Al-Imaam As-Saadiq (A), "Mwenye kumfuturisha Mumin mmoja, Mwenyezi Mungu huwaweka Malaika sabini wamtakase (wammuombee aghufiriwe) mpaka mwakani usiku kama ule".

(2)Asome dua hii yenye maneno machache, lakini maana zake adhimu. Basi mwenye kusoma dua hii kila usiku

katika mwezi wa Ramadhani ataghufiriwa madhambi ya

miaka sitini:

Al-laa-hum-ma Rab-ba shah-ri Ramadhan, al-lla-dhi an-zal-ta fee-hil Qur-aan; waf-tar-adh-ta ala ibaa-dika fee-his-siyaam; Sali-li alaa Muhamadin wa aali Muhammad; war-zuq-nee Haj-ja bay-tikal ha-raam, fee aami hadha wa fee kul-li aam; wagh-fir-lee til-kadh dhu-nuu-bal-idhaam; fa-in-nahu la-yagh-firu-haa ghay-ruka; ya Rah-maanu, ya Al-laam.

(3)Asome kila usiku dua mashuhuri inayoitwa Duaul-Iftitaah.   Mwanzo wake ni hivi: Al-laa-humma in-nee af-ta-ti-huth-thanaa-abi-ham-dik.[4]

(4)Wakati wa kula daku asome dua mashuhuri na adhimu ya Sahar, inayoanza kwa maneno haya: Allaahum-ma In-nee as-alu-ka min ba-haa-ika bi-ab-ha-hu, wa kul-lu ba-haa-ika ba-hee.[5] Na baada ya kuisoma, amuombe Mwenyezi Mungu kila mambo mema anayotaka; Na anapotaka kula daku asiache kabisa kusoma sura ya al-Qadri.

Imepokewa hadithi kwamba Mtume (S.A.W.), amesema, "Hakika Mwenyezi Mungu na Malaika wake huwarehemu walao daku (katika mwezi wa Ramadhani) na wenye kuomba kughufiriwa, wakati wa daku, basi msiache kula daku ijapokuwa kinyweo cha maji.

(5) Abu Hamza Thumali (R.) amesema kwamba Imaam Zaynul-Abideen (A.) alikuwa akisali sehemu ya usiku; na ukifika wakati wa daku akimwomba Mwenyezi Mungu kwa maneno haya : Ilaa-hi, laatu-addib-ni bi ukuu batik[6] (mpaka mwisho). Dua hii inajulikana kwa jina la sahaba huyu Bwana Abu Hamza Thumaali (R). Hakika dua hiyo ni hazina ya elimu na maarifa.

(6)Kuoga (Ghusl) katika usiku wa witri (1, 3, 5, 7, na kadhalika) kuna thawabu sana. (Kwa namna ya kuoga tazama Kitabu chetu cha Sala uk33).

AMALI  ZA USIKU ZA LAYLATUL-QADRI

Usiku ambao taadhima yake haina mfano; usiku ambao fadhila yake haiwezi kukadiriwa; Usiku ambao utukufu wake hauna kifani. Ni usiku ambao Qur’ani tukufu iliteremshwa na Mwenyezi Mungu; usiku ambao ni bora kuliko miezi elfu; ibada katika usiku huo ni sawa na ibada ya miezi elfu.

Mwenyezi Mungu anasema katika usiku huo hivi:

ÈöÓúãö Çááåö ÇáÑøóÍúãäö ÇáÑøóÍöíãö
ÅöäøóÇ ÃóäÒóáúäóÇåõ Ýöí áóíúáóÉö ÇáúÞóÏúÑö* æóãóÇ ÃóÏúÑóÇßó ãóÇ áóíúáóÉõ ÇáúÞóÏúÑö* áóíúáóÉõ ÇáúÞóÏúÑö ÎóíúÑñ ãøöäú ÃóáúÝö ÔóåúÑò * ÊóäóÒøóáõ ÇáúãóáóÇÆößóÉõ æóÇáÑøõæÍõ ÝöíåóÇ ÈöÅöÐúäö ÑóÈøöåöã ãøöä ßõáøö ÃóãúÑò *ÓóáóÇãñ åöíó ÍóÊøóì ãóØúáóÚö ÇáúÝóÌúÑö

"Tumeiteremsha Qurani katika usiku huo wa Laylatul-Qadr. Na nini kitakufahamisha wewe maana ya Laylatul-Qadr? Usiku wa laylatu! Qadr ni bora kuliko miezi elfu. Usiku huo huteremka Malaika na Jibrilu (A) pamoja na hukumu zote za mwaka mzima kwa idhini ya Mola wao. Amani (usiku) huo mpaka mapambazuko ya Alfajiri"

Usiku huo ni usiku ambao hubainishwa kila jambo la hekima. Mwenyezi Mungu anasema: "Kwa yakini tumeiteremsha (Quran) katika usiku uliobarikiwa; bila shaka sisi ni waonyao. Katika (usiku) huu hubainishwa kila jambo la hekima na maslaha" (44:3-4). Usiku huu ndio Mwenyezi Mungu huweka mambo ya viumbe wake mpaka mwaka mmoja. Kwa mfano, kila atakayezaliwa, atakaye kufa. atakaye tajirika, atakaye kuwa masikini, atakaye kuwa na cheo, atakaye dhalilika, atakaye shinda, atakaye shindwa, atakaye ongoka, atakaye kupotea, atakaye pona, atakaye kuwa mgonjwa, na mambo mengi kama hayo ambayo humsibu binadamu.

Amali nzuri usiku huo ni kusali, kutoa zaka, kutenda kila jambo zuri la khayri; kwani ukitenda usiku huu ni bora kuliko amali ya miezi elfu isiopo kati yao Laylatul-Qadr. Usiku huu huteremka Malaika pamoja na AR-RUUH ambaye ni Malaika alie adhimiwa kuliko Malaika wote, kwa amri ya Mwenyezi Mungu wanafika kwa Al-Imaam Al-Mahdi (A), na wanamwonesha kila alichokadiriwa yeye na watu wote na Mola, mwaka ujao mpaka Laylatul. Qadr ijayo.

Kama ilivyo katika hadithi ya Laylatul Qadr hii, juu ya utukufu wake, na jinsi inavyokuwa inayo manzila na cheo, lakini bado hatuijui, na maarifa ya kuwekwa hiyo siku, na siku gani kwa hakika hiyo haikubaynishwa. Lakini inatumainiwa kuwa ni moja katika usiku wa tarehe kumi na tisa (19), ishirini na moja (21), ishirini na tatu (23). ishirini na tano (25) na ishirini na saba (27); na labda zaidi inatumainiwa sana kuwa katika usiku wa tarene ishirini na moja na ishirini na tatu (21 na 23), Hadithi nyingi za Maimamu wetu (A.S.) zilizopokewa zinatilia nguvu sana kwamba Lay-latul-Qadr ni usiku mmoja katika usiku hizo mbili (21 au 23). Mara nyingi watu wamewaomba Al-Imaam (A) awaainishiye (dhihirishie) siku ipi katika hizo mbili? Imaam hakuainisha, na akajibu, "Itakudhuru nini ukifanya mambo mazuri (Ibada) usiku mbili hizi?".

Imepokewa kwa Imaam Al-Baaqir (A) kutokana kwa baba zake watukufu.(A.S.) kwamba wamesema hivi, "Mtume (S.A.W.) amekataza mtu kutojali usiku wa Ishirini na moja na Ishirini na tatu, na amekataza kulala mtu usiku hizo". Vile vile amesema (A) kwamba "Mtume (S.A.W.) alikuwa akikunja 'matandiko yake na akikaza kitambaa cha kiunoni (mshipi) katika siku kumi za mwisho wa mwezi wa Ramadhani (alikuwa akikesha kwa Ibada) na akiwafanya watu wake wa nyumbani wakeshe usiku wa Ishirini na tatu na akiwarushia maji usoni mwa wenye kulala. Na alikuwa Bibi Fatima (a.s) hamwachi mtu yoyote katika watu wake wa nyumbani kulala usiku huo, na akiwatibu kwa kula kidogo (akiwaeleza kama kula kidogo hupunguza usingizi; na ukila sana huleta usingizi mwingi), na akijiweka tayari kwa Ibada ya usiku tangu mchana.

Ala kulihali, usiku wa AI-Qdri haimfalii mtu kuupuuza kulala, bali akeshe kwa Ibada ya Mwenyezi Mungu kwa kusali, kutubia, kufanya dhikri (kutoa uradi) na kila amali za suna zilizowekwa na kupangwa kwa usiku huu. Usijidanganye nafsi yako kwa kusema nimechoka au ninaumwa kichwa na kuonesha uchovu. Kwa sababu haya yote hutokana na adui wetu mkubwa shetani, kukukosesha mafanikio na manufaa yote ya kheri za usika huu. Kama alivyosema Bibi Fatima (a.s), "Mwenye kunyimwa ni yule mwenye kujinyima kheri zote za usiku huu". Basi, ndugu zangu, msikose yote haya kwani hujui mwakani utakuwapo hai, upate kufidia uliyo yakosa !!

Maelezo na Utaratibu wa Amali za Laylatul Qadr

(1)Kuoga (Ghusl) usiku wa 19, 21 na 23. Ni bora uoge  wakati linapozama  jua, hata  upate kusali  sala ya magharibi na Isha kwa hiyo ghusli, lakini utawadhe pia.

(2)Ukeshe  kucha usiku   zote tatu  za Laylatul-Qdri  kuomba  dua,  kunyenyekea,  kuomba  kughufiriwa.

Imepokewa hadithi tukufu inayosema kwamba kila mwenye kukesha kucha Mwenyezi Mungu atamghufiria madhambi yake yote hata yakiwa kwa idadi ya nyota zote, au majabali, au kiasi cha maji ya bahari zote (utaghufiriwa dhambi zako binafsi na Mola, si za watu kama umemwibia mtu).

(3)Usali  raka mbili katika usiku wa Laylatul-Qadr (19,   21, 23).   Katika kila  rakaa, baada  ya Sura  ya AL-

HAMDU,  soma  Sura   (Qul-Huwal-Laah)   mara  saba  na ukiisha maliza hiyo sala, hapo hapo soma mara sabini (70)

hivi;   As-tagh-firul-Laa-ha  wa   Atuu-bu-Ilay-hi.  Imepokewa hadithi tukufu inasema, 'Mwenye kuzisali hizi rakaa

mbili kama ilivyo elezwa. basi kabla ya kuondoka mahala pake Mwenyezi Mangu atamghufiria yeye na wazee wake.

(4)Usome usiku wa mwezi  19, 21 na 23 mara mia moja (100) . As-tagh-firul-laah rab-bee wa atubu-ilayh.

(5)Usiku wa 19 na 21.usome mara mia moja (100): Al laa-hum-mal-an, qata-lata, Ameeril-mu-mineen.

(6)Ufunue Qur’ani tukufu. uiweke wazi mbele mikononi mwako na usome dua hii: "Al-la-hum-ma in-nee as-alu-ka biki-taa-bikal, munzali wa maa fee-hi wa fee-his-mu-kal  ak-baru  wa  as-maa-ukal  hus-naa  wa  maa  yukhaa fu wayur-jaa an taj-alanee min uta qaa-ika minan -naar". Baadaye uombe maombi yako yote.

(7)Tena   uifunge Qur’ani   na uiweke  juu  ya  kichwa chako (Tahadhari isianguke) na useme maneno haya: "Al-laa-hum-ma, Bi-haqqi ha dhaal-qur’aan wa Bihaqi man ar sal-taho bih wa Bihaq qi kul-li mu-mi-nin ma-dah-tahu feeh wa Bi-haq-qika, alay-him, falaa ahada a’ rafu Bi-haq-qika minka". Tena sema mara kumi hivi: Bika yaa Allaahu; mara kumi, Bi-Muhammadin (S.A.W.); mara kumi, Bi-Aliy-yin (a.s); mara kumi, Bi-Faa-timata (a.s); mara kumi, Bil-Hasani (a.s); mara kumi, Bil-Husaini (a.s); mara kumi, Bi-Aliy-yibnil-Husain (a.s); mara kumi, Bi-Muhammadi bin-Aliy-yln (a.s); mara kumi, Bi-Jafa-ribni-Muhammadin (a.s); mara kumi, Bi-Muusabni-Jafarin (a.s); mara kumi Bi-AIiy-yibni Muusa (a.s); mara kumi, Bi-Muhammadi-bni-AIiy-yin (a.s); mara kumi, Bi-Aliy-yibni-Muhammadin (a.s); mara kumi Bil-Hasanibnl-Aliy-yin (a.s) Hapo inuka katika hali ya kusimama mkono mmoja umeikamata Qurani ilioko juu ya kichwa, basi sema mara kumi Bl-Huj-ja (a.s); tena taja moyoni haja zako zote na utake kwa Mwenyezi Mungu baraka ya usiku huu wa Lay-latu Qadri.

 (8)Kumzuru Imaam Husain (A) katika usiku wa Lay. Latul-Qadri. Imepokewa hadithi tukufu inayosema kwamba, "Huita muitaji (Malaika) kutoka mbingu ya saba kwenye. Arshi hivi, 'Bila shaka Mwenyezi Mungu amemghufiria mwenye kuhudhuria (kuizuru) kaburi tukufu la Imaam Husain (a.s)". Basi zipo Ziyara mahsusi nyingi katika vitabu vya Ziyara, na ukisoma Ziyara mashuhuri kwa jina la Ziyaaratul Waaritha itatosha. Ziyara hii inaanzia kwa maneno haya: "As-salaamu alay-ka, yaa waa-ritha Aa-dama saf’wa-til-Iaah"[7]

(9) Usali rakaa mia (100) katika kila usiku wa 19, 21 na 23. Kusali huko kuna thawabu mno, na bora kusali hivi. Katika kila rakaa, baada ya sura ya "AL-HAMDU", soma sura ya -QUL-HUWAL-LAAHU mara kumi. Vile vile unaweza kusali raka mia hizo kwa (kukidhi) kulipa sala zako za fardhi uloziwacha kusali kwa udhuru fulani fulani muda wa mwaka; kwa mfano ikiwa unadaiwa sala ya siku sita itakuwa rakaa mia moja na mbili (102) Kuanzia sala ya adhuhuri ya siku ya kwanza mpaka asubuhi ya siku ya saba.

HADHARI Sala  ya sunna   yeyote haijuzu   kusali kwa mafungu zaidi ya rakaa mbili, utazisali kama sala za asubuhi; vile vile huwezi kusali kwa Jamaa kabisa, isipokuwa sala za Idi na Salatu-Istisqaa" (Sala ya kuombea mvua tu).

(10) Usome usiku wa mwezi ishirini na tatu (23) Sura za Qurani zijazo: AL-ANKA-BUUT. (J.20: S.29), Ar-Ruum (J.25: .30), na AD-DU-KHAAN (J25:S.44). Katika hadithi tukufu amesema Imaam As-Sadiq (A): "Ninaapa, mwenye kuzisoma zile sura mbili (za mwanzo) usiku huu, ni mtu wa Peponi"

AMALI ZA KUMl YA MWISHO WA MWEZI

(l)Kuanzia usiku wa kumi la tatu mpaka mwisho wa mwezi mtukufu (usiku wa 21 mpaka mwisho) soma dua hii kila usiku. "A'udhu bi-jalali waj-hikal-Kareem, an yan-qadhi-ya an-nee shahru Ramadhan au yatlual-Fajru min lay-latee ha-dhi-hee walaka qi-balee dhan-bun au fabi-atun tuadh-dhi-buni alayh".

(2) Imaam Zaynul-Abedeen (A), "Imaam wa nne, alikuwa akisoma dua hii usiku wa ishirini na saba (27) kila mara, nayo ni hii: al-laa-hum-mar-zuq-nee at tajaa-fiya an daa-ril-ghu-ruur wal-inaa-bata Ilaa daa-ril-khu-luud wal is-tia-dada lil-mawti qabla hu-luu-lil-fawt.

(Ewe Mola wangu nipe uwezo wa kujitenga na mambo usiyoyapenda yenye kunidanganya humu (duniayani) na nifanye mambo mema ya kuniokoa huko akhera na adhabu yako, na nijiweke tayari kwa kufa kabla haikunijia mauti, (maana yake nifanye amali njema hata ikinijia mauti nisiwe na wasiwasi ya kukosa kutubia).

Usiache kuoga "GHUSL" usiku huu, na kukesha pia kwa Ibada, kama unaweza.

 (3) Usome Dua ya Al-Widaa (ya kuuaga mwezi mtukufu wa Ramadhani) katika usiku wa mwisho, kama ilivyopokewa katika hadithi ya Al-Imaam Jaafar bin Muhammad As-Sadiq (a.s) Imaam wa sita; nayo ni hii: Al-laa-ham-ma laa tajal-hu aa-kbiral-ahdi min siyaa-mee li-shah-ri Ramadhan wa audhu bika an-yat-lua fajru haa dhi-hi?-lay-lati il-laa wa qad ghafarta-lee. Basi Mwenyezi Mungu atakughufiria kabla ya asubuhi na atakujalia na kuruzuku utubiye madhambi yako.

Haya yote ni badhi ya dua na sala zilizopokelewa katika hadithi tukufu, na mwenye kutaka zaidi atapata katika vitabu vya Dua na Ziyara kama Mafaateehul-Jinaan na zinginezo.