MLANGO 4

SHURUTI ZA KUFUNGA NA KUSIHI KWAKE

Huwa wajibu kufunga saumu juu ya watu wote kwa shuruti hizi:-

1. Kwa kila Mwislamu aliye balehe,[3] mwanamume au mwanamke, ni wajibu afunge.

Na siwajibu kufunga kwa mtoto ijapo mwenye akili na anayepambanua;lakini huyo mtoto akifunga ni thawabu sana, na inawapasa wazee wa wazoeze watoto wao kufunga, ili wawe tayari kutimiza wajibu wao wakiwa wakubwa (balehe). Mtoto yeyote akibalehe

wakati wa Ramadhani siku' yeyote ile itampasa kufunga siku zote zilizobaki za mwezi tangu kubalehe, na siku zilizopita (kabla ya kubalehe) ikiwa hakuzifunga haidhuru neno (kwani haikuwa fardhi juu yake). Ikiwa amebalehe kabla ya Alfajiri, ni fardhi juu yake siku hiyo aanze kufunga, na ikiwa baada ya Alfajiri kabalehe na siku ile amefunga kwa thawabu tu, hapo ni lazima juu yake aendelee na hiyo saumu na haruhusiwi kufuturu mchana.

2. Katika shuruti za kufunga ni kuwa na (Akili) si wajibu (fardhi) mwenda wazimu kufunga.

3. Awe na siha (asiwe na ugonjwa wa kumdhuru saumu wakati anapojizuia kula na kunywa.

Mwenyezi Mungu   amesema katika  Qur'an tukufu:

Ýóãóä ßóÇäó ãöäßõã ãøóÑöíÖðÇ Ãóæú Úóáóì ÓóÝóÑò ÝóÚöÏøóÉñ ãøöäú ÃóíøóÇãò ÃõÎóÑó

Na atakayekuwa mgonjwa kwa maradhi yale ambayo akifunga saumu itamdhuru au anahofia kumdhuru, au akifunga atachelewa kupona au ugonjwa utamzidi, kwa njia zote hizi haruhusiwi kufunga bali itampasa azilipe saumu baadaye.

Ikiwa mtu anajua kuwa saumu haimdhuru, hata akimwambia daktari kama itamdhuru, lazima afunge; na ikiwa anahakika au anawaza kwamba saumu akifunga itamdhuru, haruhusiwi kufunga, hata daktari akimwambia kwamba haitamdhuru; na akifunga saumu yake haitasihi; lazima ailipe saumu ile baadaye.

4. AL-IQAA-MA : Awe katika mji wake (asiwe safarini) au mahala (mji) ambapo haimpasi kupunguza sala zake, kwa mfano ikiwa katika safari kafika mahala na akanuia kukaa siku kumi (10) au zaidi basi kwa sharia, mtu huyo huitwa MUQEEM na itamlazimu afunge saumu ya Ramadhani.

Mwenyezi Mungu amesema juu ya jambo hili: Faman sha-hida min-kumush-shah-ra fal-ya-sum-hu wa-man kaana maree-dhan aw alaa safar-in faid-da-tun min ay-yaa-min ukhar. yu-ree-dul-laa-huu bikumul-yus-ra; walaa yu-ree-du bi-kumul-us-ra "Atakayekuwa katika mji (wala si mgonjwa. wala hayupo safarini) katika huu mwezi wa Ramadhani afunge. Na mwenye kuwa mgonjwa mwezi mzima au baadhi ya siku zake, au yuko safarini basi wote hawo wazilipe baadaye saumu; walizoziacha. Mwenyezi Mungu anakutakieni yaliyo mepesi; wala hakutakieni yaliyo mazito (Kwa sababu hiyo amekuamrisheni msifunge katika ugonjwa na safari(.

Ikiwa shuruti za upungufu (Qasr) wa sala zimetimia (Tazama kitabu cha Sala, uk. 98). basi msafiri haruhusiwi kufunga. Hukumu hii inachukuliwa kwa namna zote.za safari, kama vile, kusafiri kwa mguu, mnyama, reli, meli, au kwa ndege. Kusafiri katika mwezi wa Ramadhani haikatazwi hasa ikiwa ni kwa ajili ya kazi. Lakin ikiwa ni kuikimbia saumu, safari hiyo ni makruhu. Hata hivyo ni lazima wote hawa wazilipe funga (saumu) zao baadaye. Ikiwa msafiri ameshafikia masafa tutayotaja, akifunga saumu basi haitasihi; bali atakuwa ameasi na lazima alipize baadaye saumu yake. Zimepokewa hadithi nyingi za Mtume (S.A.W.) na Maimamu (A.S.) kukataza dhahiri kufunga katika safari kama hivi:

"AS-SAIMU FI SHAHRI RAMADHAN FIS-SAFAR, KAL-MUF-TIR FEEHI FIL-HADHAR", yaani "Kufunga saumu katika mwezi wa Ramadhani katika safari, ni kama yule ambaye hakusafiri na hakufunga ingawa hana budi kufunga".-

 Amesema Mtume (S.A.W.) katika hadithi mbili kwamba "Mwenyezi Mungu amenituza mimi na umma (wafuasi) pia, zawadi ambayo hakumtuza mtu yoyote katika umma wowote walio tangulia, na ni heshima kutokana na Mola juu yetu'. Wakasema watu, "Kitu gani hicho, Yaa Rasuul-lal-Laah?", Akajibu, "Kufuturu (Kutokufunga), katika safari na kupunguziwa sala pia, na asiyefuata hayo basi atakuwa amerejesha tuzo kwa Mola !".

Katika, hadithi moja Imaam Al-Baaqir (Imaam wa tano A) amesema hivi, "SAMMA RASUU-LUL-LAAH (S.A.W.) QAW-MAN SAA-MUU HEENA AFTARA WA QAS-SARA USAA-TUN. Mtume (S.A.W.) aliwaita wale watu waasi (USAAT); ambao walisafiri naye wakifunga wakati ambapo Mtume alikuwa akifuturu. Kwa hiyo wamekuwa waasi mpaka siku ya Qiyama.

Imeelezwa katika Saheeh Muslim hadithi inayotokana na Jabir bin Abdullah, inasema, "Mwaka wa kuiteka Maka, Mtume (S.A.W.) alitoka Madina katika mwezi wa Ramadhani wakati watu wote walikuwa wamefunga. Hata alipofika mahala paitwapo Kuraa Gha-mi, mchana kabisa, Mtume akataka bakuli la maji, akalinyanyua hata wote wakaliona; na akafuturia kwa yale maji. Baadaye akapashwa habari kwamba baadhi ya watu (waliofuatana naye) hawakufuturu (hawakuvunja saumu yao), Mtume (S.A.W.) akasemS kuwa mwenye kufanya vile (ambaye hakufungua saumu yake) basi amefanya dhambi na uhalifu naye ni MUASI.

Ikiwa mwenye saumu kafanya safari baada ya adhuhuri, basi lazima siku hiyo aitimize mpaka magharibi, saumu yake itasihi, lakini ikiwa anasafiri kabla ya adhuhuri wakati wowote ule, akifika kwenye "Had-dut-Tarakh-Khus" (mahali ambapo majumba ya huo mji atokao hayaoni au sauti ya adhana ya mji haisikiki) itampasa afuturu, na akifuturu kabla ya kufika mahali hapo Itampasa alipe kaffara pia.

Ikiwa msafiri amefika mji wake kabla ya adhuhuri au mahala ambapo amepakusudia kukaa siku kumi au zaidi, na hakutenda mambo yavunjayo saumu siku hiyo, basi lazima siku hiyo afunge, na ikiwa amewahi kufanya moja katika yavunjayo saumu, kufunga siku hiyo kwake si fardhi, atailipa tu.

5.  Mwanamke asiwe katika hedhi na nifasi(ujusi) kwa sababu haitasihi saumu yake.

Hata kama ikimjia kwamuda mdogo kabla ya magharibi, saumu ya siku hiyo lazima ailipe pia.

6. AL-ISLAM:Uislamu ni shuruti moja katika shuruti za kukubaliwa saumu   na ibada  zote. Ijapokuwa juu ya kafiri pia ni wajibu kufunga na kufanya ibada zote, lakini kwa vile yeye si Mwislamu basi haitasihi na kukubaliwa ibada zake.

     Mwenyezi Mungu anaamrisha watu wasali lakini shuruti  (watawadhe au  watayammamu).   Basi kafiri pia inampasa afunge, lakini shurati za kusihi hiyo saumu yake ni kukubali Uislamu, na Kafiri anaweza kusilimu.

7.  Nia ni makusudio ya kutenda, nayo ni fardhi kwa kila ibada na ni sharti katika ibada zote.Lazima kunuia kujizuia na kila kinacho batilisha Saumu, na si lazima wakati wa nia kuzikumbuka zotekwajina,inatoshakuwekaniayakujitenganakilakinachoharibunakubatilishasaumu. Kuweka nia ni wajib. Ikiwa kwa mfano, siku moja kabla ya kuingia Ramadhani mtu bila ya Nia ya kufunga akalala naasizindukane ila baada ya magharibi ya usiku wa pili wa mwezi wa Ramadhani, basi kukosa kula na kunywa siku

hiyo moja ya Ramadhni bila ya Nia haitasihi, na lazima baadaye ailipe.

Mtu anaweza kila usiku wa Ramadhani kuweka nia ya kufunga kesho yake, na nzuri usiku wa mwezi mosi Ramadhani aweke nia ya mwezi mzima.

WAKATI WA KUWEKA NIA

    Wakati wa kuweka nia ya saumu ni kutoka mwanzo wa usiku hadi adhana ya asubuhi (Alfajiri) kwa saumu za fardhi, ama saumu za sunna huanzia mwanzo wa usiku, hadi kiasi cha kunuwia kumebaki kufikia magharibi, ikiwa mpaka wakati ule hakutenda kitu cha kuvunja saumu, basi hapo aweke nia ya saumu, na saumu itasihi. Ikiwa mtu bila ya kuweka nia kabla ya alfajiri akalala, na akaamuka kabla ya adhuhuri na hapo akiweka nia, saumu yake itasihi, ikiwa saumu ya fardhi au ya sunna lakini akizindukana baada ya adhuhuri, basi hapo hawezi kuweka nia ya saumu ya fardhi. Ikiwa kabla ya alfajiri kanuwia na akalala na asiamke ila baada ya magharibi, saumu hiyo itasihi haidhuru neno.

8. AL-KHU-LUUS: Lil-Laahi Ta'Aala, maana yake, kufunga kwake iwe Lil-Laahi, T'aala tu, au akiingiza Riya (kwa kujipendeleza) tu hapa saumu yake haitasihi.

Walioruhusiwa Wasifunge

   Wapo baadhi ya watu ambao wamesamehewa wasifunge. Nao ni hawa:

(1 na 2) (a) Mzee na kizee ambao si wagonjwa lakini kufunga saumu kwao ni takalifu sana; wasifunge lakini watoe fidia kwa kila siku 'Mud' moja (3/4 kilogram). (b) Ikiwa hawawezi kabisa kufunga basi kutoa hiyo fidia si lazima. bali ni bora.

(3)  Hivyo hivo hukumu hii kwa mgonjwa wa kiu (ambaye hawezi kustahmili kiu kabisa): (a) Ikiwa takalifu sana, atoe fidia 'Mud' moja. (b) Ikiwa hawezi kabisa, basi kutoa hiyo fidiya si lazima. bali ni bora. (Na hata hivyo asifanye fujo kwa kunywa maji). Na baadaye akiweza azilipe saumu hizo.

 (4)Mwanamke mwenye mimba aliye karibukuza (a) Ikiwa anahofia mimba yake asifunge, lakini atoe fidia 'Mud' moja kwa kila siku; nabaadae atazilipa saumu hizo

 (b) Ikiwa anahofia nafsi yake, asifunge,wala hanafidia lakini baadae azilipe saumu.

(5)Mwanamke mwenye kumnyonyesha aliye na maziwa machache (akiwa anamnyonyesha mwanawe au mwana wa mwingine.

(a) Ikiwa kufunga kutamdhuru mtoto anyoyae, basi asifunge, lakini atoe fidia 'Mud' moja kwa kila siku. (b) Ikiwa saumu itamdhuru yeye binafsi. asifunge, nani bora atoe fidia pia; na baadae azilipe saumu zote alizo ziacha kwa sababu zote mbili hizo.