Rudi nyuma Yaliyomo endelea

Hakika wale wanaoficha yale aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu miongoni mwa ubainifu na uongofu, baada ya kuwa tumewabainishia watu ndani ya kitabu, watu hao Mwenyezi Mungu anawalaani na kinawalaani kila (kiumbe) chenye kulaani" (Qur. 2:159)

Na pia kauli nyingine ya Mwenyezi Mungu isemayo:-

"Hakika wale wanao yaficha yale aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu katika kitabu na wanayauza kwa thamani ndogo y a dunia •watu hao hawali matumboni mwao isipokuwa moto, na wala Mwenyezi Mungu hatawasemesha siku ya Qiyama na wala hatawatakasa, na watapata adhabu kali" (Qur. 2:174)

256

Basi je si inawapasa watu hawa watubie kwa Mwenyezi Mungu na waukubali ukweli ili Mwenyezi Mungu akubali toba yao kabla wakati haujawapita???

Kwa hakika yote haya kwangu mimi yalithibitika baada ya utafiti na uchunguzi, nikiwa na dalili zisizo na shaka kwa haya niyasemayo, wao wamejaribu bila mafanikio kuyatakasa matendo ya Masahaba ambao walirudi kinyume nyume kwa visigino vyao, basi kauli zao zimekuja zikipingana zenyewe kwa zenyewe na zinapingana na historia.

Laiti wao wangeliimata haki japo kuwani chungu hakika wangestarehe na hiyo ingekuwa ni sababu ya kuwa na umoja katika umma huu, umoja ambao umeparaganyika na kusababisha ugomvi si kwa lolote isipokuwa kwa kutaka kuunga mkono kauli zao au kuzikanusha.

Sasa basi, ikiwa baadhi ya Masahaba wa mwanzo siyo waaminifu katika kunakili hadithi tukufu za Mtume, wakawa huzibatilisha zile zisizokubaliana na matakwa yao khususan hadithi hizo zikiwa ni miongoni mwa usia aliousia Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.) wakati wa kufariki kwake, kwani Bukhari na Muslim wameandika ya kwamba Mjumbe wa Mwenyezi Mungu ameusia mambo matatu wakati wa kifo chake.

"Waondoweni washirikina katika bara Arabu, wapeni wajumbe kama nilivyokuwa nawapa, kisha msimulizi wa hadithi hii anasema: Jambo la tatu nimelisahau.

Taz: Sahih Bukhari Juz. I uk. 121 Babu Jawazil-wafai Minkitabil-Jihad, Sahih Muslim Juz. 5 uk. 75 Kitabul-Wasiyyah.

Basi je katika hali kama hii inaingia akilini ya kwamba Masahaba waliokuwepo ambao waliusikia usia wa Mtume juu ya mambo matatu wakati wa kufa kwake, wanaweza kusahau

257

usia wa jambo la tatu, hali ya kuwa ndiyo wao hao hao waliokuwa wakihifadhi kasida za mashairi marefu baada tu ya kuyasikia maramoja? Haiwezekani, lakini kilichopo ni kwamba siasa ndiyo iliyowalazimisha wasahau wasikumbuke. Hakika huu ni unyonge mwingine miongoni mwa unyonge waliokuwa nao masahaba hawa.

Na kwa kuwa wasia muhimu wa Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, bila shaka ulikuwa ni kumpa Ukhalifa Ali ibn Abi Talib ndiyo maana msimulizi wa hadithi hakuutaja.

Pamoja na yote hayo mchunguzi yeyote juu ya mas-ala haya ataikuta harufu ya wasia juu ya Ali inanukia licha ya kufichwa na kutotajwa, kwani Bukhari ameandika ndani ya sahihi yake, Kitabul-Wasaya, kama ambavyo Muslim pia ameandika ndani ya sahihi yake "Palizungumzwa mbele ya mama Aisha ya kwamba Mtume aliusia juu ya Ali".

Taz: Sahih Bukhari Juz. 3 uk. 68 Babu maradhi Nnabi wa Wafatih, Sahih Muslim Kitabul-Wasiyyah.

Angalia nijinsi gani Mwenyezi Mungu anavyoidhihirisha Nuru yakejapokuwa madhalimu wataifunika.

Narudia kusema, "Ikiwa Masahaba hawa siyo waaminifu katika kunukuu wasia wa Mjumbe wa Mwenyezi Mungu basi baada ya hapo hakuna lawama kwa wale waliowafuatia (Masahaba) wala wale waliowafuatia hawa.

Na ikiwa mama Aisha ambaye ni mama wa waumini hawezi hata kulitaja jina la Ali na wala nafsi yake haifurahii kheri yoyote kwa Ali kama alivyoyaeleza haya Ibn Saad ndani ya Tabaqat[28] yake naye Bukhari ndani ya Sahihi yake, Babu maradhi Nnabi wa Wafatih, na iwapo mama Aisha anasujudu kumshukuru Mwenyezi Mungu pindi aliposikia kuwa Ali

258

amefariki basi ni vipi itatarajiwa kutoka kwake utajo wa usia juu ya Ali hali ya kuwa mama Aisha anatambulika kwa wote juu ya uadui wake na kero yake dhidi ya Ali na wanawe na watu wa nyumba ya Mtume?

Lahaula wala Quwata Ilia Billahi l-Aliyil-Adhim.

259

MSIBA ULIOTUFIKA UMETOKANA NA KUFANYA IJTIHADI DHIDI YA NASSI

Ndani ya uchunguzi (niliofanya) nimegundua ya kwamba msiba ulioufika umma wa Kiislamu umetokana na Ijtihada ambayo waliifanya Masahaba dhidi ya Nassi (maagizo ya Qur'an au Mtume) yaliyo bayana, na kwa sababu hiyo mipaka ya Mwenyezi Mungu ikabomoka na Sunna za Mtume zikapotea, na hatimaye wanachuoni na Maimamu wakawa wanakisia kwa kutumia Ijtihadi zilizofanywa na Masahaba na wakati mwingine (akafikia hatua ya kuyapinga maagizo ya Mtume pindi yanapopingana na tendo la mmoja wa Masahaba. Na sitakuwa ninatia chumvi wa kusema kwamba hata andiko la Qur'an walilipinga kwani hapo kabla nimetangulia kueleza namna gani walivyofanya licha ya kuwepo maelekezo juu ya kutayamam ndani ya kitabu cha Mwenyezi Mungu na Sunna ya Mtume iliyothibiti, basi licha ya yote hayo kuwepo wao walifanya jitihada zao, wakasema kuwa sala itaachwa kusaliwa ikiwa patakuwa hapana maji kwa ajili ya udhu na (huyu) Abdallah Ibn Omar alitoa sababu zake za kufanya Ijtihadi yake kama tulivyoonesha pahala pengine ndani ya uchunguzi wetu.

Na miongoni mwa Masahaba waliofungua hii milango (ya Ijtihadi) ni Khalifa wa pili ambaye alitumia maoni yake dhidi ya andiko la Qur'an baada ya kifo cha Mtume (s.a.w.) akazuwia fungu la wale wenye kutiwa nguvu imani zao, fungu ambalo Mwenyezi Mungu amelifaradhisha kwao kutoka ndani ya zaka, na yeye akasema, "Sisi hatuna haja nanyi"

260

Ama Ijtihadi yake kuhusu maagizo ya Mtume ni nyingi mno hazina idadi, kwani yeye alifanya Ijtihadi yake hata katika zama za uhai wa Mtume mwenyewe na alimpinga mara nyingi.

Hapo kabla tumeashiria upinzani wake alioufanya katika siku ya sulhu ya Hudaibiyyah, na pale alipozuwia yasiandikwe maagizo ya Mtume na akasema, "Kinatutosha kitabu cha Mwenyezi Mungu", Kadhalika lipo tukio jingine lililotokea baina yake na Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.) bila shaka litatupa picha iliyowazi jinsi alivyo Omar ambaye alijihalalishia kumjadili na kumpinga Mtume. Tukio hilo ni lile la Mtume kubashiria pepo, pale Mjumbe wa Mwenyezi Mungu alipomtuma Abuhurairah na akamwambia, "Utakayekutana naye hali ya kuwa anashuhudia kwamba hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu, moyo wake ni wenye kuyakinisha jambo hilo, basi mbashirie pepo", basi Abuhurairah akatoka ili akambashirie huyo atayekutana naye Umar akamfuata na kumzuia kufanya hivyo na akampiga mpaka akaanguka chini. Abuhurairah akarudi mpaka kwa Mjumbe wa Mwenyezi Mungu hali ya kuwa analia na akamweleza Mtume tendo alolitenda Omar. Mjumbe wa Mwenyezi Mungu akamwambia Omar, "Ni kitu gani kilichokufanya utende hivyo"? Omar akasema, "Je wewe ndiye uliyemtuma ambashirie pepo yule atakayesema Lailuha Illa ll ah hali yakuwa moyo wake ni wenye kuyakinisha hivyo". Mjumbe wa Mwenyezi Mungu akasema "Ndiyo", Omar akasema, "Usifanye hivyo, kwani mimi hakika nachelea watu watategemea "Lailaha Illallah"!

Na huyu mwanawe Abdallah ibn Omar anachelea watu watategemea kutayammamu, basi yeye akawaamuru waache sala, laiti wangeliziacha Nassi kama ziliyyo na wasizibadilishe kulingana na Ijtihadi zao zisizo na faida ambazo zinapelekea kufuta sheria na kuvunja heshima ya mambo matukufu ya Mwenyezi Mungu na kuugawa umma katika madh-hebu mbali mbali mengi maoni yenye kutofautiana na farka zenye uhasama,

261

Na- -miongom "mwa mitazamo mbali mbali ya Omar kumuhusu Mtume na Sunna yake, tunafahamu ya kwamba yeye alikuwa haamini hata siku moja kwamba Mtume anayo Ismah, (amehifadhiwa kutokana na makosa) bali alikuwa akimuona kwamba ni mtu tu anayekosea na kupatia.

Na kutokana na msingi huu hapa ndiyo ile fikra ya wanachuoni wa Kisunni ilipokuja nayo ni kwamb  Mjumbe wa Mwenyezi Mungu ana Ismah katika kubalighisha (Qur'an tu, na yasiyokuwa Qur'an anakosea na wanatolea ushahidi juu ya jambo hilo kwamba Omar aliyasahihisha maoni ya Mtume mara nyingi katika matukio kadhaa!!!

Basi iwapo Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.) - kama waonavyo baadhi ya watu wasiojua kitu - anayakubali mazumari ya shetani ndani ya nyumba yake hali ya kuwa kalala chali na wanawake wanapiga madufu, shetani naye anacheza na kufurahia pembeni yake mpaka alipoingia Omar ibn Khatab shetani yule akakimbia na wanawake wale nao wakayaficha madufu chini ya makalio yao, kisha Mjumbe wa Mwenyezi Mungu akamwambia Omar, "Hatakuona shetani ukipita njia fulani isipokuwa atapita njia nyingine isiyokuwa yako."

Kwa hiyo siyo ajabu kwa Omar ibn Khatab kuwa na nafasi ndani ya dini au kuipa nafasi nafsi yake ya kumpinga Mtume katika mambo ya kisiasa na hata katika mambo ya dini kama

ilivyotangulia hapo kabla juu ya lile tukio la kuwabashiria pepo waumini.

Na kutokana na fikra ya Ijtihadi na kutumia rai dhidi ya Nassi, kilianza au kilitengenezeka kikundi cha Masahaba wakiongozwa na Omar ibn Khatab. Na bila shaka tumekwishawaona ni jinsi gani siku ile ya msiba ule wa siku ya Alkhamisi walivyokinga mkono na kuitia nguvu rai ya Omar dhidi ya maagizo baya na ya Mtume.

262

Na kwa ajili hiyo pia tunaona kwamba watuTiawa hata siku moja hawakuikubali Nnasi (maagizo) ya Ghadir ambayo Mtume (s.a.w.) alimsimika Ali kuwa ndiyo Khalifa wake kwa Waislamu, na wao wakaitumia nafasi ya kufanya ijtihadi zao kuyapinga maagizo ya Mtume wakati wa kifo chake, kwani mkutano wa Saqifah ukawa ni wa kumchagua Abubakr yakiwa ni matokeo ya ijtihadi hii.

Na baada ya mambo kuwakalia vizuri na watu kuyasahau maagizo ya Mtume kuhusu Ukhalifa, hapo ndipo walipoanza kufanya ijtihadi katika kila jambo mpaka wakathubutu kukilemaza kitabu cha Mwenyezi Mungu, wakaipuuza mipaka ya Mwenyezi Mungu, wakazibadilisha hukmu za Mwenyezi Mungu. Hivyo basi madhila yaliyomfika Fatmah Zahra (yalikuja) baada ya madhila yaliyomfika mumewe kwa kunyang'anywa Ukhalifa, kisha ukafuatia msiba wa kuuawa watu waliokataa kutoa zaka, na yote hayo ni matokeo ya kufanya ijtihadi dhidi ya maandiko au maagizo ya Mwenyezi Mungu na Mtume. Hatimaye Ukhalifa wa Umar ibn Khatab ulikuja ukiwa ni matokeo halisi ya ijtihadi hiyo, kwani Abubakr alijitahidi kwa maoni yake akayapuuza mashauriano ambayo hapo kabia alikuwa akiyatolea ushahidi wa kusihi kwa Ukhalifa wake, na Umar naye akaongeza maji ndani ya unga pale alipotawalia mambo ya Waislamu, akahalalisha mambo aliyoyaharamisha Mwenyezi Mungu na Mtume wake[29] Na akaharamisha mambo aliyohalalisha Mwenyezi Mungu na Mtume wake.[30]

Alipokuja Uthman baada ya Umar yeye alikwenda mbali zaid katika kufanya ijtihadi, akazidisha kuliko waliomtangulia

263

mpaka ijtihadi yake ikayaathiri maisha ya kisiasa na dini kwa jumla, yakafanyika mapinduzi matokeo yake akatoa uhai wake kwa thamani ya ijtihadi yake.

Na pindi Imam Ali (a.s.) alipotawalia mambo ya Waislamu alikuta kuna kazi ngumu ya kuwarejesha watu kwenye Sunna tukufu ya Mtume na kwenye uzio wa Qur'an. Alijaribu kwa juhudi zake kuondosha bid'a ambazo ziliingizwa ndani ya dini, lakini baadhi ya watu walipiga kelele wakasema, "Iko wapi Sunna ya Omar?"

Mimi nakurubia-kuamini na kuamua kwamba, wale waliompiga vita Imam Ali na wakamkhalifu, hapana shaka walifanya hivyo kwa kuwa yeye Imam Ali (a.s.) aliwalazimisha kufuata njia ya sawa na aliwarejesha kwenye maagizo sahihi. Kwa ajili hiyo akaziua bid'a zote na ijtihadi zote ambazo zilikuwa zimeambatanishwa na dini kwa muda wote wa robo karne, na watu walikwisha zizowea hasa wale wenye tamaa ya dunia ambao mali ya Mwenyezi Mungu waliifanya kuwa ni ya kupeana wao kwa wao, na waja wa Mwenyezi Mungu wakawafanya kuwa ni watumwa. Walijilimbikizia dhahabu na fedha, na wakawanyima wanyonge haki zao za msingi hata zile ndogo mno ambazo Uislamu umeziweka.

Bila shaka katika kila zama tunawakuta Wastakbari wanapendelea kufanya ijtihadi na kuzitilia mkazo kwa sababu huwapa nafasi ya kuyafikia malengo yao kwa kila njia. Amma maandiko ya Mwenyezi Mungu na Mtume huwa yanazuwia njama zao na  kuweka kizuizi baina yao na kile wanachokikusudia.

Kisha ijtihadi imepata watu wa kuitetea katika kila zama na kila mahali, hata hao wanyonge wenyewe, kutokana na kuwepo wepesi wa utekelezaji wa mambo na kukosa kuwa na Iltizam. Na kwa kuwa maagizo ya Mwenyezi Mungu na Mtume yanayo Iltizam na yanaondoa uhuru wa kujiamulia na hii kwa

264

watu wa siasa huwa wanaiita kuwa ni hukumu au utawala wa siasa kali "kwa lugha kileo" ya kidini wakimaanisha - hukumu za Mwenyezi Mungu. Ama ijtihadi kwa kuwa ndani yake kuna uhuru unaovuka mipaka na hakuna Iltizam ya mipaka ya sheria basi wao huita kuwa ni hukumu au utawala wa kidemokrasia yaani maamuzi ya wananchi.

Kwa hiyo basi wale waliokusanyika ndani ya Saqifah baada ya kifo cha Mtume (s.a.w.) walipuuza serikali yenye hukumu za Mwenyezi Mungu alizoziasisi Mjumbe wa Mwenyezi Mungu juu ya msingi wa maandiko ya Qur'an, na wakabadilisha kwa kuweka serikali ya kidemokrasia ambayo wananchi ndiyo watakaomchagua wamuonaye kuwa anafaa kuwaongoza. Masahaba hao hawakuwawakifahamu neno "Demokrasia" kwa kuwa neno hilo siyo la kiarabu, lakini walichokuwa wakikifahamu wao ni nidhamu ya "Shuraa."

Kwa hiyo wale ambao hawaikubali Nassi ya Ukhalifa (leo hii) wao ni watetezi wa demokrasia, na wanajifakharisha kwa

1). Licha ya hivyo, hakika hata hiyo aina ya uchaguzi •wa Shuraa haikupatikana, kwani waliofanya uchaguzi huo hawakuwa na haki ya kumiliki uwakilishi kwa niaba ya umma (wa kiislamu) kwa namna yoyote ile kutokana na kukosekana kwa walio wengi miongoni mwa watu muhimu kwa Waislamu ambao wanayo haki ya kuchagua. Hivyo basi mambo yalifanyika kama ilivyokuja ndani ya ushairi unaonasibishwa kuwa ni wa Amiri lmuuminina Ali akimwambia Abubakar kama ifuatavyo: Iwapo wewe umetawalia mambo yao kwa kutumia Shuraa, yatawezekana vipi mambo Il-hali hawapo wahusika wa Shuraa? Na iwapo umetumia hoja ya udugu dhidi ya khasimu yao, basi asiyekuwa wewe ni bora mno kwa Mtume tena yu karibu mno.

265

jambo hilo wakidai kwamba Uislamu ndiyo wa mwanzo kuiona nidhamu hii, na wao pia ndio watetezi wa ijtihadi na kufanya mabadiliko ndani ya dini hali ya kuwa leo hii ndiyo wao walio karibu mno na tawala za kimagharibi. Kwa ajili hiyo leo hii tunazisikia serikali za kimagharibi zinawasifia watu hawa na kuwaita kuwa ni Waislamu walioendelea tena wenye msimamo wastani.

Amma Mashia watetezi wa "Theocracy" au hukumu ya Mwenyezi Mungu, na ambao wanaipinga ijtihadi dhidi ya Nassi na wanatofautisha baina ya hukumu ya Mwenyezi Mungu na Shuraa, kwani Shuraa kwao wao haina uhusiano na Nassi, bali shuraa na ijtihadi hupatikana katika mambo ambayo hakuna Nassi ndani yake. Je, huoni kwamba Mwenyezi Mungu ndiye aliyemchagua Mtume wake Muhammad, lakini pamoja na hayo amemwambia: "Washauri katika mambo". (Qur. 3:159)

Ama yale mambo yanayohusiana na kuchagua viongozi ambao watawaongoza viumbe Mwenyezi Mungu amesema:

" Na Mola •wako ndiye anayeumba akitakacho nu ndiye anayemchagua amtakaye wao hawana hiyari" (Qur. 28:68)

Kwa hiyo pale Mashia wanapozungumzia kuwa Ukhalifa ni wa Imam Ali baada ya Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, hapana kingine isipokuwa huwa wanashikamana na maagizo ya Mwenyezi Mungu na Mtume hali kadhalika wanapowashutumu baadhi ya Masahaba, si jinginelo bali huwatuhumu wale waliobadilisha maagizo na kuweka ijtihadi, na kwa ajili hiyo wameipoteza hukumu ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake na wakawa wamefungua mwanya katika Uislamu ambao hauja-fungika hadi leo.

Na kwa ajili hii vile vile tunazikuta serikali za kimagharibi na wanafikra wao wanawakejeli Mashia na kuwaita kuwa ni wenye chuki za kidini na pia wanawaita kuwa wasio na

266

maendeleo kwa sababu tu ya wao kuirejea Qur'an ambayo inakata mkono wa mwizi na kumpiga mawe mzinifu, na inaamrisha kufanya jihadi katika. njia ya Mwenyezi Mungu. Yote hayo kwao wao ni hukumu za kiimla na kishenzi na kwa kupitia uchunguzi huu nimefahamu kwamba, ni kwa nini baadhi ya wanachuoni wa Kisunni waliufunga mlango wa ijtihadi tangu karne ya tatu hijiriya, basi huenda ilitokea hivyo kutokana na hii ijtihadi kuuvutia umma huu maangamizi na masaibu, mambo ya kuchukiza na vita vya kumwaga damu ambavyo vikiunguza vibichi na vikavu, na pia ijtihadi hiyo iliubadilisha umma bora uliotolewa kwa watu na kuwa umma wenye kugombana wao kwa wao na kuuana, unoongozwa na mambo ya vurugu na kutawaliwa na ukabila unaogeuka kutoka kwenye Uislamu na kurudi. kwenye Jahiliyyah. Kuhusu Mashia ambao walibakia na mlango wa ijtihadi wazi muda wote ambapo maandiko na maagizo ya Mwenyezi Mungu na Mtume yakiwa yapo na thabiti, na haiwezekani kwa yeyote yule kuyabadilisha na juu ya msingi huo pia wamesaidiwa kwa kuwepo Maimamu kumi na wawili ambao wamerithi elimu ya babu yao Mtume s.a.w. na wamekuwa wakisema kwamba "Hapana lolote isipokuwa linayo hukumu ya Mwenyezi Mungu na hapana shaka Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.) amelibainisha.

Pia tunafahamu ya kwamba Masunni walipokuwa wamefuata uongozi wa Masahaba wenye kufanya ijtihadi ambao walizuwia kuandikwa Sunna ya Mtume, walijikuta wenyewe wakilazimika kufanya ijtihadi pale inapokosekana Nassi kwa kutumia maoni na kiasi na kufunga mlango wa mianya na sababu nyingine zisizokuwa hizo.

Kadhalika tunafahamu kutokana na yote hayo kwamba Mashia walishikamana na Imam Ali ambaye ndiye mlango wa mji wa elimu, na ni yeye ambaye alikuwa akiwaambia "Niulizeni jambo lolote lile, kwa hakika Mjumbe wa Mwenyezi Mungu amenifundisha milango elfu moja ya elimu, ambayo kila mlango

267

unafunguliwa milango (mingine) elfu moja".

Taz: (1) Tarikh Dimishq ya Ibn Asakir Juz. 2 uk. 484 Tarjumaya Imam Ali Ibn Abi Talib. (2) Maqtalul-Husein cha Al-Khawarzami juz. 1 uk. 38, (3) Al-Ghadir cha Al-Ammi Juz. 3uk. 120.

Wakati huo huo wasiokuwa Mashia walishikamana na Muawiyah ibn Abi Sufiyan ambaye alikuwa haijuwi Sunna ya Mtume isipokuwa kidogo, na alikuwa ndiye Imamu wa kundi potofu lakini wakamfanya kuwa amirijeshi wa waumini baada ya kifo cha Imam Ali, na ndipo alipofanya mambo ndani ya dini ya Mwenyezi Mungu kwa namna aonavyo zaidi kuliko waliomtangulia.

Masunni wao wanasema kuwa alikuwa ni mwandishi wa wahyi na kwamba yeye alikuwa miongoni mwa wanachuoni na Mujtahidina, lakini ni vipi wanahukumu juu ya ijtihadi yake hali ya kuwa ndiye mtu aliyemtilia sumu na kumuua ImamHasan ibn Ali Bwana wa vijana wa peponi? Lakini huenda wao watasema kuwa tendo hili pia ni miongoni mwa ijtihadi yake kwani alijitahidi akakosea!

Ni vipi wanamhukumu kuwa ni mwenye kufanya ijtihadi hali ya kuwa alichukua Baia yake mwenyewe binafsi kwa nguvu toka kwa umma kisha akafanya hivyo hivyo kwa mwanawe Yazid, na akaigeuza nidhamu ya shuraa na kuwa ni Ufalme wa Kaizari.

Ni vipi basi wanamzingatia kuwa mwenye kufanya ijtihadi na kumpa malipo hali ya kuwa hapana shaka kwamba ni yeye (Muawiyah) ndiye aliyewalazimisha watu wamlaani Imam Ali na watu wa kizazi cha nyumba ya Mtume juu ya mimbari kwa muda wote wa miaka sitini na tendo hili likawa ni Sunna inayofuatwa katika kipindi hicho chote?

Bali inakuwaje wanamuita kuwa ni mwandishi wa wahyi

268

... hali ya kuwa katika muda wa miaka ishirini na tatu ya kushuka kwa wahyi juu ya mjumbe wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.) yeye Muawiya alikuwa ni mwenye kumshirikisha Mwenyezi Mungu katika kipindi cha miaka kumi na moja miongoni mwa miaka hiyo ishirini na tatu, na aliposilimu baada ya fat’hi Makka hatujaipata hadithi isemayo kuwa aliishi Madinah, hali ya julikana pia kuwa Mtume Mtukum hakurudi kuishi Makah baada ya Fat’hi hivyo basi ilikuwaje Muawiya apate fursa ya kuwa mwandishi wa wahyi.

Lahaula wala quwata illa Billah L-Aliyyil-Adhim! Siku zote suali linarudi kuwa "Ni lipi kati ya makundi mawili ndilo lililo kwenye haki, na ni lipi kati ya makundi hayo liko kwenye batili, basi imma watakuwa Mashia ndiyo madhalimu na hawako kwenye haki na imma Muawiya na wafuasi wake ndiyo madhalimu na hawako kwenye haki.

Hapana shaka kwamba Mjumbe wa Mwenyezi Mungu amebainisha kila kitu isipokuwa baadhi ya wanaodai kuwa ni wafuasi wa Sunna ya Mtume wanaitafutia dosari, na hapana shaka kwamba imenibainikia wakati nikifanya utafiti na kupitia kumtetea Muawiyah kuwa kwa hakika wale wanaomtetea ni wale wafuasi wake na wafuasi wa Banu Umayyah na siyo kama wanavyodai kwamba wao ni wafuasi wa Sunna ya Mtume, na khususan iwapo utafuatilia misimamo yao, kwani wao wanawachukia wafuasi wa Ali na huwa wanasherehekea siku ya Ashura kuwa ni sikukuu [31]kadhalika wanawatetea Masahaba waliomuudhi Mjumbe wa Mwenyezi Mungu katika uhai wake na baada ya kufa kwake na pia makosa ya Masahaba hao wao hujaribu kuyatakasa na kuyafanya kuwa ni matendo sahihi.

269

Ewe Bwana waona ni jinsi gani mnadai kwamba mnampenda Ali na watu wa nyumba ya Mtume na wakati huo huo mnawaombea radhi kwa Mwenyezi Mungu maadui zao na waliowaua? Yupi mnampenda Mwenyezi Mungu na Mtume wake na kisha mnawatetea waliobadilisha hukumu za Mwenyezi Mungu na Mtume wake, na wakafanya jitihada zao na kuawili kwa kufuata maoni yao ndani ya hukumu za Mwenyezi Mungu?

Ni vipi basi mwampa heshima mtu ambaye hakumpa heshima Mjumbe wa Mwenyezi Mungu bali alimsingizia Mtume kuwa anaweweseka na autuhumu uongozi wake?!

Ni jinsi gani mnawafuata wasimamizi waliosimikwa na dola ya Banu Umayyah au dola ya Banu Abbas kwa ajili ya mambo ya kisiasa, na mnawaacha Maimamu waliotamkwa na Mjumbe wa Mwenyezi Mungu kwa idadi yao[32] na majina yao[33]

Ni vipi basi mnamfuata mtu ambaye hakumfahamu ipasavyo Mtume na mnamuacha ambaye ndiye mlango wa mji wa elimu na ndiye ambaye kwa Mtume (s.a.w.) daraja yake ni kama ile ya Haruna kwa Musa?!

*Ni nani aliyeanzisha Istilahi ya Ahlus-Sunnah Wal-JamaaPl

Hapana shaka, nimefanya uchunguzi ndani ya historia, lakini sijakuta isipokuwa ni kwamba, wao waliafikiana kuuita ule mwaka ambao Muawiyah alitwaa madaraka kuwa "Ni mwaka wa umoja" na hiyo ilikuja kutokana na umma kugawanyika makundi mawili baada ya mauaji ya Uthman, kundi moja la Mashia wa Ali najingine wafuasi wa Muawiyah. Na pindi Imam Ali (a. s.) alipouawa, Muawiyah akatawala baada ya sulhu aliyoipitisha yeye pamoja na Imam Hasan ndipo

270

Muawiyah akawa Amirul-Muuminin, na hapo ndipo mwaka huo ulipoitwa "Mwaka wa Umoja" (Aamul-Jamaah) kwa hiyo basi kuitwa "Ahlus-Sunnah Wal-Jamaah" kunajulisha juu ya kuwa mfuasi wa Sunna ya Muawiyah na kushikamana juu ya misingi yake, na wala haimaanishi kuwa ni kufuata Sunna ya Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, kwani Maimamu wanaotokana na kizazi chake (Mtume) ndiyo wanaoifahamu na ni wajuzi mno wa Sunnah ya Babu yao kuliko Maimamu wanaotokana na waachwa huru (Banu Umayyah).

Na ilivyo ndivyo ni kwamba wenye nyumba ndiyo wajuao kilichomo nyumbani mwao, na watu wa Makkah ndio wajuao vichochoro vya Makkah, lakini sisi tumewakhalifu Maimamu kumi na wawili ambao Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.) aliagiza tuwafuate na badala yao tumewafuata maadui zao.

Licha ya sisi kukiri kuwepo na kusihi kwa hadithi ambayo Mjumbe wa Mwenyezi Mungu amewataja ndani ya hadithi hiyo Makhalifa kumi na wawili na wote ni Maquraishi, lakini siku zote sisi tunakomea kwa Makhalifa wanne. Labda Muawiyah aliyetupatia jina la "Ahlus-Sunna Wal-Jamaa" alikuwa akikusudia tujumuike kwenye. Sunna aliyoianzisha ya kumtukana Ali na watu wa nyumba ya Mtume, Sunna ambayo iliendelea kwa miaka sitini na hakuna aliyeweza kuiondosha isipokuwa Omar ibn Abdil-Aziz "Mwenyezi Mungu ampe radhi yake". Na hapana shaka kwamba baadhi ya wanahistoria wanatusimulia kwamba Banu Umayyah walikula njama ya kumuuwa Omar ibn Abail-Aziz hali ya kuwa yeye ni miongoni mwa Banu Umayyah kwa ajili tu ya kuiua hiyo Sunna ambayo ni ya kumlaani Ali ibn Abi Talib.

Enyi watu wangu najamaa zangu, kwa kufuata misingi ya muongozo wa Mwenyezi Mungu, hebu tuelekee kwenye uchunguzi wa kuitafuta haki, tuiweke chuki pembeni, kwani sisi ni kafara ya Banu Umayyah na Banu Abbas, na ni kafara ya historia yenye kiza na pia sisi ni wahanga wa fikra iliyoganda,

271

fikra ambayo wametupandikizia hao waliotangulia. Hapana shaka sisi ni wahanga wa hila na vitimbi vya Muawiyah ambavyo alisifika navyo, pia Amr ibn Al-Aas na Mughirah ibn Shu'bah na watu kama hawa.

Kwa hiyo basi chunguzeni undani wa historia yetu ya Kiislamu ili muweze kuupata ukweli halisi. Naye Mwenyezi Mungu atakupeni malipo yenu mara mbili, kwani huenda Mwenyezi Mungu akaunga umoja wa umma huu kupitia kwenu ambao ulipotoka baada ya kifo cha Mtume wake na ukatawanyika na kuwa makundi sabini na tatu, basi njooni muunganishe chini ya bendera ya "Lailaha Illallah Muhammadun Rasulullah", (na) kuwafuata watu wa nyumba ya Mtume ambao yeye Mjumbe wa Mwenyezi Mungu ametuamuru kuwafuata akasema, "Musiwatangulie mutaangamia, wala musiwape mgongo mutaangamia, na wala musiwafundishe, bila shaka wao ni wajuzi mno kuliko ninyi"

Taz: Addurul-Manthoorcha Suyuti Juz. 2uk. 60, Usudul-Ghabah Juz. 3 uk. 137, As-Sawaiqul-Muhriqa cha ibn Hajar uk. 148, Yanabiul-Mawaddah uk. 41 na 355, Kanzul-Ummal Juz. 1 uk. 168, Maj-Mauz-Zawaid Juz. 9 uk. 163.

Lau tutafanya hivyo, basi hapana shaka Mwenyezi Mungu ataondosha hasira yake na ghadhabu yake kwetu sisi, na atatubadilishia amani baada ya khofu yetu na atatumakinisha katika ardhi na kutupatia urithi ndani yake na angetudhihirishia walii wake Imam Mahdi (a.s.) ambaye kupitia kwake Mtume wa Mwenyezi Mungu ametuahidi kuwa ataijaza ardhi yetu usawa wa uadilifu kama ambavyo imejazwa dhulma na ujeuri na hapana shaka Mwenyezi angeitimiza nuru yake ulimwenguni kote.

272

MWITO KWA MARAFIKI KUJA KUFANYA UTAFITI

Mabadiliko yalikuwa ndiyo mwanzo wa mafanikio ya kiroho, kwani nilihisi raha ya nafsi na ukunjufu wa moyo kuyaendea madh-hebu ya haki niliyoyagundua au unaweza kusema kuwa "Uislamu halisi" ambao hauna shaka ndani yake. Furaha kubwa na fahari vilinifuni kakutokana na neema aliyonineemesha Mwenyezi Mungu kwa uongofu na mwongozo. Sikuweza kunyamaza na kuficha yale yote yaliyokuwa yakinipeketa kifuani mwangu na nikajiambia mwenyewe, "inanibidi niudhihirishe ukweli huu kwa watu kwani neema ya Mola wako isimulie." Nayo ni miongoni mwa neema kubwa, au ni neema kubwa mno duniani na akhera na yeyote anayenyamazia haki ni shetani bubu. Na hakuna kingine baada ya haki isipokuwa ni upotofu.

Kilichonizidishia yakini ndani ya hisia zangu ili kuwajibika kuueneza ukweli huu, ni kule kutokuwa na dhambi kwa Massuni ambao wanampenda Mtume (s.a.w.) na Ahli Bayt wake, na yatosha kuwaondolea tandabui iliyofumwa na historia mbele yao ili waifuate haki. Jambo hili ndilo lililonifika mimi binafsi.

Mwenyezi Mungu anasema: "Namna hiyo ndivyo mlivyokuwa hapo kabla, basi Mwenyezi Mungu akakuneemesheni" (Qur. 4:94)

Basi, niliwaita marafiki wanne miongoni mwa Waalimu

273

ninaofanya kazi pamoja nao chuoni, wawili kati yao walikuwa wakifundisha mafunzo ya dini na watatu akifundisha Kiarabu, na huyu wa nne alikuwa mtaalamu wa falsafa ya Kiislamu. Wote hawa wanne hawakuwa wakitoka Qafsah bali walikuwa ni kutoka Tunis, na Jammal na Sausah.        '

Niliwaita wawe pamoja nami katika utafiti wa maudhui hii ya hatari, na niliwaonesha kuwa mimi nashindwa kufahamu baadhi ya maana za mambo fulani na nimechanganyikiwa, pia ninayo mashaka ndani ya baadhi ya mambo. Walikubali kuja nyumbani kwangu baada ya kazi, nami nikawaacha wanasoma kitabu kiitwacho "Al-Murajaat" kwa msingi kuwa, mtunzi wa kitabu hicho anadai vitu vya ajabu na ni vigeni katika dini. Watatu miongoni mwao walikipenda sana kitabu hicho, ama yule wa nne ambaye husomesha Kiarabu yeye alituacha baada ya vikao vinne au vitano na alisema: "Sasa hivi wazungu wanakwenda mwezini ninyi bado munatafiti mambo ya Ukhalifa wa Kiislamu."

Hatukuwahi kukimaliza kitabu hicho ndani ya kipindi cha mwezi mmoja isipokuwa hao watatu walikuwa tayari wamekwisha kuona ukweli, na kwa hakika niliwasaidia mno kuufikia ukweli huu kwa njia fupi kulingana na upana wa ufahamu uliojengeka kwangu katika kipindi cha uchunguzi. Nilionja utamu wa uongofu na niliufurahia mustaqbali (wangu) nikaanza kuwaita mara kwa mara baadhi ya marafiki wa Qafsah ambao vipindi vya masomo vilikuwa vikiniunganisha nao Msikitini au mahusiano yaliyokuwa kwa njia ya Twariqah za Kisufi, na baadhi ya wanafunzi wangu ambao walikuwa wakiambatana nami.

Haukupita mwaka ila tulikuwa tumefikia idadi kubwa (ya watu) tunaowatawalisha Ahlul-Bait, tunamtawalisha mwenye kuwatawalishawao na tunamfanya kuwa adui mwenye kuwafanyia uadui, tunafurahi katika sikukuu zao na

Rudi nyuma Yaliyomo endelea