Rudi nyuma Yaliyomo endelea

Ama tukio la tatu ambalo lilimtokea Abubakar mwanzoni mwa Ukhalifa wake na katika tukio hilo Omar alimkhalifu

239

(Abubakar) na aliyabadilisha maandiko ya Qur'an na Sunna ya Mtume ni lile tukio la Khalid ibn Walid ambaye alimuuwa Malik ibn Nuwairah na akamtendea uchafu mkewe ndani ya usiku ule ule (aliomuuwa mume).

Omar alikuwa akimwambia Khalid "Ewe adui wa Mwenyezi Mungu umemuua mtu Muislamu kisha umemtendea uchafu mkewe, wallahi nitakupiga kwa mawe." Taz: Tarikh TabariJ. 3 uk. 280, Jarikh Abul-Fida Juz. 1 uk. 158, Tarikh Yaqubi Jnz. 2 uk. 110, Al-Isabah Fimawifatis-Sahaba Juz. 3 uk. 336.

Lakini Abubakar alimtetea (Khalid) na akasema: "Ewe Omar mwachie amefasiri na amekosea, wacha kumsema sema Khalid."

Hii ni fedheha nymgine iliyotendwa na Sahaba mkubwa ambayo imesajiliwa na historia, na tumtajapo (Sahaba huyu) humtaja kwa heshima na utukufu, bali tumempa Laqabu ya "Saifullahil-Mas-lul" yaani upanga wa Mwenyezi Mungu ulio nje ya ala.

Niseme nini juu ya Sahaba anayefanya matendo kama haya, anamuua Malik ibn Nuwairah ambaye ni Sahaba mtukufu bwana wa ukoo wa Bani Tamim na Bani Yar'buu na ni mtu wa kupigiwa mfano kwa murua (wake), ukarimu na ushujaa.

Hapana shaka, wanahistoria wamesimulia ya kwamba, Khalid ibn Walid alimfanyia khiana Malik na watu wake baada ya kuwa wameweka silaha chini na wakasali jamaa akawatia kamba. Na miongoni mwao akiwemo Layla binti Min-Hal mke wa Malik ambaye alikuwa mwanamke mashuhuri kwa uzuri miongoni mwa wanawake wa Kiarabu, na inasemekana ya kwamba hakupata kuonekanwa mwanamke mzuri kuliko yeye, kwa hiyo Khalid akafitinika kwa uzuri wake. Malik akamwambia Khalid, "Ewe Khalid ungetupeleka kwa Abubakar

240

yeye ndiye awe mwenye kutuhukumu". Abdallah ibn Omar na Abu Qatadah Al-Ansari waliingilia kati wakamsisitiza Khalid awapeleke kwa Abubakar, lakini Khalid akapinga akasema:

"Mungu hatonisamehe iwapo sitakuua" Basi Malik alimgeukia mkewe Layla na akamwambia Khalid "Anayenuia ni huyu hapa" yaani mkewe. Basi Khalid akaamuru shingo ya Malik ikatwe na akamkamata Layla mke wa Malik kisha akamuingilia usiku ule ule. Taz: Tarikh Abul-Fida Jiiz. 1 uk. 158, Tarikh Al-Yaqubi Juz. 2 uk. 110, Tarikh ibn Shahnah Hamish ya Al-Kamil Juz. 11 uk. 114, Wafiyatul-Aayan Juz. 6 uk 14.

Niseme nini juu ya Masahaba hawa ambao wanahalalisha aliyoyaharamisha Mwenyezi Mungu na wanaua nafsi za Waislamu kwa ajili ya matamanio ya nafsi na wanahalalisha tupu alizoziharamisha Mwenyezi Mungu, kwani ndani ya Uislamu haolewi mwanamke aliyefiwa na mumewe isipokuwa baada ya eda ambayo ameieleza Mwenyezi Mungu ndani ya kitabu chake kitukufa. Lakini Khalid matamanio yake aliyafanya kuwa ndiyo mungu wake akaangamia. Je, kwa Khalid eda ina kiwango gani (cha kuheshimiwa) baada ya kumuua mume wake (Layla) hali ya kuwa kamtia kifungoni na kwa dhulma? Pia akawaua watu wake hali ya kuwa ni Waislamu (na alifanya yote haya) mbele ya ushuhuda-wa Abdallah ibn Omar na Abu Qatadah ambaye alikasirika mno kutokana na matendo ya Khalid, na aliondoka akarudi Madina na akaapa kwamba (kamwe) hatokuwa ndani ya uongozi uliopo (chini ya) Khalid ibn Walid. Taz: Tarikh Tabari Juz. 3 uk. 280, Tarikh Yaqubi Juz. 2 uk 110, Tarikh Abul-Fida, Al-Isabah Juz. 3 uk. 336.

Yatutosha kuhusu Qadhia hii mashuhuri kukiri kwa Ustadh Haikal ndani ya kitabu chake kiitwacho "As-Sidiq Abubakar" chini ya anuani isemayo "Maoni ya Umar na hoja yake" amesema:- "Amma Omar alikuwa ni mfano wa uadilifu thabiti, yeye alikuwa akimuona Khalid kwamba alimfanyia uadui Muislamu na kumtenda tendo chafu mkewe kabla ya kumalizika

241

eda yake, basi haifai kwa mtu kama huyo kubakia ndani ya uongozi wa jeshi ili asije rudia kosa kama hili na hatimaye kuharibu mambo ya Waislamu na kuichafua heshima yao mbele ya Waarabu", (anaendelea Ustadh Haikal) anasema, "Haifai kabisa kuachwa bila ya kuadhibiwa kutokana na yale aliyoyafanya kwa Layla".

Basi 1-au itasihi kwamba yeye alijitahidi akakosea kuhusu jambo la Malik - kitu ambacho Omar hakukikubali- basi yatosha kuadhibiwa kwa yale aliyoyatenda kwa mkewe (Malik), basi haiwezi kuleta udhuru kwamba yeye ni upanga wa Mwenyezi Mungu na kwa ajili hiyo asiadhibiwe kwa mujibu wa sheria. Na ungekuwa ni mfano mbaya wa kupigiwa Waislamu katika kuheshimu kitabu cha Mwenyezi Mungu, ndiyo maana Omar hakuacha kumrudia Abubakar na kumsisitiza mpaka akamwita Khalid na akamlaumu ....." Taz: Kitabu Siddiq Abubakr cha Ustadh Haikal uk. 151.

Hebu tumuulize Ustadh Haikal na walio kama yeye miongoni mwa wanachuoni wetu ambao wanapotosha (mambo) kwa msingi wa kulinda heshima ya Masahaba, hebu tuwaulize "Ni kwanini Abubakar hakumuadhibu Khalid"? Ikiwa Omar -kama alivyosema Ustadh Haikal ya kwamba alikuwa ni mfano wa uadilifu madhubuti, basi ni kwanini (Omar) alitosheka tu na (adhabu) ya kuondolewa kwenye uongozi wa jeshi na wala haikusimamishwa adhabu ya kisheria dhidi ya Khalid kulingana na kosa alilotenda? Hii isijekuwa ni mfano mbaya unaopigiwa Waislamu katika kuheshimu kitabu cha Mwenyezi Mungu kama alivyoeleza? Je, wao walikiheshimu kitabu cha Mwenyezi Mungu na wakasimamisha adhabu (alizoziweka) Mwenyezi Mungu? Sivyo kabisa hiyo ni siasa, na ni kipi kitachokujulisha hiyo siasa ni kitu gani? Ni kufanywa maajabu na hakika ya mambo kugeuzwa'na maandiko ya Qur'an kupigwa ukutani.

Hebu tuwaulize baadhi ya wanachuoni wetu ambao wanasimulia ndani ya vitabu vyao kwamba Mjumbe wa

242

Mwenyezi Mungu (s.a.w.) alikasirika mno pale Usamah alipomjia na kumuombea msamaha yule mwanamke mwenye sharafu aliyeiba.

Mtume (s.a.w) alisema, "Ole wako, wamuombea tumsamehe adhabu miongoni mwa adhabu za Mwenyezi Mungu Wallahi lau Fatumah Binti Muhammad angekuwa ndiye aliyeiba ningemkata mkono wake, bila shaka waliangamizwa waliokuwa kabla yenu, pindi anapoiba mtu mwenye sharafu humuacha na anapoiba mnyonge humuadhibu kwa mujibu wa sheria."

Ni vipi wanachuoni hawa wananyamazia mauaji ya Waislamu wasio na hatia, na wake zao kuingiliwa katika usiku ule ule hali ya kuwa wameghubikwa na huzuni za vifo vya waume zao, ni bora lau wangenyamaza lakini wao wanajaribu kulitakasa tendo la Khalid kwa kuunda uzushi na kumtengenezea sifa na mambo mema mpaka wakampa Laqabu ya kuwa ni upanga wa Mwenyezi Mungu ulio nje ya ala (tayari kumshambulia adui).

Mmoja kati ya rafiki zangu ambaye alikuwa akipendelea utani na kugeuza maana alinishangaza nilipokuwa namuelezea sifa za Khalid ibn Walid katika siku za ujinga wangu nikamwambia "Bila shaka yeye ni upanga wa Mwenyezi Mungu ulio nje ya ala", yeye akanijibu akasema: "Yeye ni upanga wa shetani uliopooza". Nilimshangaa siku hiyo, lakini baada ya uchunguzi Mwenyezi Mungu amenifungulia macho yangu na kututambulisha daraja ya watu hawa ambao walikalia Ukhalifa na wakabadilisha hukumu za Mwenyezi Mungu na wakachupa mipaka ya Mwenyezi Mungu na kuivunja.

Na huyu Khalid ibn Walid anacho kisa (alichokifanya) katika zama za uhai wa Mtume (s.a.w.), pindi Mtume alipomtuma kwenda kwa Bani Judhaima ili awalinganie Uislamu, na wala hakumuamuru kuwapiga vita, (watu hawa) hawakuwezakutamkavemaneno "Aslamna" yaani tumesilimu,

243

'badala yake wakasema Sabaana Sabaana, basi Khalid akaanza kuwauwa na kuwashika mateka na hao mateka akawatoa kwa wenzake na akawaamuru wawauwe, baadhi yao walikataa kuwaua pale ilipowabainikia kwamba wamesilimu, na waliporudi (Madina) walimueleza Mtume (s.a.w.)juu ya jambo hilo.

Mtume (s.a.w.) alisema: "Ewe Mwenyezi Mungu najitakasa kwako kutokana na yale aliyoyafanya Khalid ibn Walid alisema hivi mara mbili. Taz: Sahih Bukhari Juz. 4 uk 171 mlango usemao: Idhaa Qadhal-Hakim Bijaurin Fahuwa Raddun.

Na hatimaye Mtume alimtuma Ali ibn Abi Talib aende kwa Bani Judhaimah akiwa na mali akafidia damu na mali zao zilizoharibiwa, mpaka akafidia vyombo vya mbwa, na Mjumbe wa Mwenyezi Mungu alielekea kibla hali ya kuwa amesimama amenyoosha mikono yake mbinguni hadi ikaonekana sehemu ya kwapani kwake akasema: "Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi najitakasa kwako kutokana na. yale aliyoyatenda Khalid ibn Walid, mara tatu. Taz: Siratu Ibn Hisham Juz. 4 uk. 53 Tabaqat ibn Saad, Usudul-Ghabah Juz. 3 uk. 102.

Tunauliza, uko wapi basi uadilifu wa Masahaba usemwao, ikiwa Khalid ibn Walid naye kwetu sisi ni miongoni mwa watukufu wetu mpaka tumempa Laqabu ya "Upanga" wa Mwenyezi Mungu, hivi kweli Mola wetu alikuwa akiunyoosha upanga wake na kuuwezesha dhidi ya Waislamu na watu wasiokuwa na hatia na pia kuvunja heshima ya vitu vitakatifu? Katika jambo hilo kuna utata kwani Mwenyezi Mungu anakataza kuuwa nafsi na anakataza maovu na machafu na ujeuri, lakini yeye (Khalid) katika wakati huo huo ananyoosha panga la ujeuri ili kuwafanyia khiyana Waislamu, kumwaga damu yao, kuharibu mali zao, kuwateka wanawake zao na watoto wao. Kwa hakika huu ni uzushi na uongo ulio wazi

244

(kumwita Khalid kuwa ni upanga wa Mwenyezi Mungu na kuwa ni muadilifu). Umetakasika ewe Mola wetu na sifa njema ni zako umetukuka na kutakasika mno kutokana na hayo, utakatifu ni wako, hukuumba mbingu na nchi na vilivyomo kwa mchezo, hiyo ni fikra ya wale ambao wamekufuru, basi ole wao waliokufuru kutokana na moto.

Vipi ilifaa kwa Abubakar hali ya kuwa ni Khalifa wa Waislamu kusikia madhambi hayo yanayoangamiza kisha akayanyamazia bali akamtaka Omar asimsemeseme Khalid na akamkasirikia Abu Qatadah kwa sababu yaupinzani wake kwa tendo la Khalid? Hivi kweli alikuwa ameyakinisha kwamba Khalid alikuwa amefanya Taawili na akakosea basi kutakuwa na jibu gani kwa waovu baada ya tukio kama hili watendapo yaliyoharamishwa kisha wadai kuwa wameyatenda kwa kuyaawili?

Ama mimi siamini kwamba Abubakar alikuwa ni mwenye kuawili (kujitahidi) kuhusu jambo la Khalid ambaye Omar alimuita kuwa ni adui wa Mwenyezi Mungu, na maoni ya Omar ilikuwa ni kwamba (Abubakar) amuuwe Khalid kwa sababu amemuua mtu Muislamu na ampige kwa mawe kwa sababu amemzini mke wa Malik. Lakini hapakuwa chochote dhidi ya muuaji huyu muovu bali alitoka akiwa ni mshindi dhidi ya Omar ibn Khatab kwani Abubakar alisimama upande wake hali ya kuwa anamfahamu vilivyo Khalid kuliko mwingine yeyote.

Wanahistoria wameandika kwamba, Abubakar alimtuma tena Khalid baada ya tukio hili baya aende Yamamah mji ambao alitoka akiwa mshindi na alifuatishia kumuoa msichana kama vile alivyomfanyia Layla kabla damu za Waislamu hazijakauka wala damu za wafuasi wa Musailamah nazo hazijakauka. Abubakar alimkemea mno kwa tendo lake hili kuliko alivyomkemea juu ya tendo lake alilomfanyia Layla. Taz: As-Siddiqu Abubakar cha Ustadh Haikal uk. 151 na kuendelea.

245

Hapana shaka kwamba binti huyu mwingine, naye alikuwa na mume, Khalid akamuuwa na kumtenda binti tendo chafu kama alivyomfanya Layla mke wa Malik, vinginevyo asingestahiki kukemewa mno na Abubakar kuliko alivyomkemea kuhusu tendo lake la mwanzo, kwani wanahistoria wanaitaja barua ambayo Abubakar alimpelekea Khalid ibn Walid na ndani yake iliandikwa kama ifuatavyo:-

"Naapa ewe Khalid bila shaka wewe huna maana, unaoa wanawake hali ya kuwa kwenye uwanja wa nyumba yako kuna damu ya watu mia mbili miongoni mwa Waislamu haijakauka. Taz: Tarikh Tabari Juz. 3 uk. 254, Tarikh Al-Khamis uk. 343.

Khalid alipoisoma barua hii akasema, "Hii ni kazi ya.Al-Asar akiwa na maana ya Omar ibn Khatab.

Hizi ni sababu muhimu zilizonifanya niwaepuke Masahaba kama hawa na wafuasi wao wanaobadilisha maagizo na kuunda simulizi za kubuni ili tu wayatakase matendo ya Abubakar, Omar, Uthman, Khalid ibn Walid, Muawiya, Amru ibn Al-Aas na ndugu zao.

Ewe Mwenyezi Mungu hakika mimi nakuomba msamaha na ninatubia kwako, Ewe Mwenyezi Mungu mimi najitakasa kwako kutokana na matendo ya watu hawa na maneno yao ambayo yamekwenda kinyume na hukumu zako na yakavunja heshima ya vitu vyako vitakatifu na yakavuka mipaka yako. Unisamehe makosa yaliyotangulia ikiwa ni pamoja na kuwatawalisha wao kwani nilikuwa miongoni mwa watu wajinga, na kwa hakika mjumbe wako amesema, "Haombewi udhuru mjinga kwa ujinga wake". Ewe Mwenyezi Mungu hakika viongozi wetu na wakubwa wetu wametupoteza njia na wakatuzuwilia (kuuona) ukweli, wakatuonesha Masahaba waliogeuka kinyume, ya kwamba hao ndiyo viumbe bora baada ya Mjumbe wako, na hapana shaka kwamba baba zetu na babu zetu walikuwa ni wahanga wa uzushi na udanganyifu

246

uliokusudiwa na Banu Umayyah na Banu Abbas waliokuja baada ya Banu Umayyah. Ewe Mwenyezi Mungu wasamehe wazee wetu wewe ndiwe ujuwaye mambo ya siri na yaliyofichikana vifuani, kwani heshima yao na kuwatukuza kwao Masahaba haikuwa isipokuwa ni kwa nia njema kwamba (Masahaba hao) ni watetezi na wapenzi wa Mjumbe wako Muhammad (s.a.w.)... nawe ewe Bwana wangu unalijua penzi lao na penzi letu (namna lilivyo) kwa kizazi kitukufu che Mtume (chenye) Maimamu ambao umewaondoshea uchafu na umewatakasa mno wakiongozwa na Bwana wa Waislamu na Amirjeshi wa Waumini ambaye ni kiongozi wa watu mashuhuri wateule, na ni kiongozi wa wachamungu Bwana wetu Ali ibn Abi Talib.

Unijaalie ewe Mwenyezi Mungu niwe miongoni mwa wafuasi wake wenye kushikamana na kamba ya kuwatawalisha, na wenye kufuata njia yao, na wenye kupanda ndani ya Safina yao, (na unijaalie) miongoni mwa wenye kushikamana na kishiko chao imara, na unijaalie miongoni mwa wenye kuingia katika milango yao na wenye kudumu ndani ya mapenzi yao, wenye kuzitumia kauli zao na matendo yao na unijaalie miongoni mwa wenye kushukuru kwa fadhila zao na upaji wao.

Ewe Mwenyezi Mungu (nakuomba) unifufue ndani ya kundi lao, hakika mjumbe wako (s.a.w.) amesema: "Mtu atafufuliwa pamoja na yule aliyekuwa akimpenda".

2). Hadithi ya Safinah.

Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.), amesema:-

"Bila shaka mfano wa watu wa nyumba yangu kwenu ninyi ni mfano wa Safina ya Nuh kwa watu wake, yeyote mwenye kuipanda ataokoka na mwenye kuipa mgongo atazama" Taz: Mustadrak Al-Hakim Juz. 3 uk. 151, Tal-Khi Adhahabi, Yanabiul-Mawaddah, As-sawaiqul-Muhriqah c}

247

ibn Hajar uk. 184na234, Tarikh Al-Khulafaa cha Suyuti, na Aljamius-Saghir, Is-aafur-Raghibin.

"Na bila shaka mfano wa watu wa nyumba yangu kwenu ni mfano wa mlango wa msamaha kwa Banu Israil, yeyote mwenye kuingia mlango huo atasamehewa". Taz: Majmauz-Zawaid cha Haithami Juz. 9 uk 168.

Ibn Hajar ndani ya kitabu chake kiitwacho As-Sawaiqul-Muhriqas ameiandika hadithi hii kisha akasema, "Na kufananishwa kwao na Safina ya Nuhu ni kwamba, mwenye kuwapenda na kuwatukuza kwa kushukuru neema ya ubora 'wao na kuchukua uongofu wa wanachuoni wao ataokoka kutokana na kiza cha khitilafu mbali mbali, na mwenye kulipa mgongo jambo hili atazama ndani ya bahari ya kukufuru na ataangamia ndani ya jangwa la upotofu, na kufananishwa kwao na mlango wa msamaha ni kwamba, hapana shaka Mwenyezi -Mungu Mtukufu amejaalia kuingia ndani ya mlango huo ambao ni mlango wa Arihaa au kuingia Baitul-Muqaddas kwa unyenyekevu, na kuomba msamaha ndiyo sababu ya kusamehewa, na ameujaalia umma huu mapenzi ya (kuwapenda) watu wa nyumba ya Mtume kuwa ni sababu ya msamaha na kuokoka".

Aah, laiti mimi (ningepata nafasi ya) kumuuliza ibn Hajar hiva yeye alikuwa miongoni mwa wale waliopanda Safina hii au walioingia ndani ya mlango huu na wakachukua uongofu wa wanachuoni (wao), au yeye ni miongoni mwa wale wasemao wasiyoyatenda na wanakwenda kinyume na kile wanachokiamini. Na watu wengi wasiojua kitu pindi ninapowauliza kuhusu (Ahlul Bait) na kutoa hoja dhidi yao, wao husema," Sisi ni wa mwanzo mno kwa (kuwapenda) Ahlul Bait na Imam Ali kuliko mwingine asiyekuwa sisi kwani sisi, tunawaheshimu Ahlul-Bait na tunawatukuza na hakuna (miongoni mwetu) anayepinga ubora wao na heshima yao!

248

Naam wanasema kwa ndimi zao mambo yasiyokuwemo ndani ya nyoyo zao au wanawaheshimu na kuwatukuza lakini hapo hapo wanawafuata maadui zao na wanafanya Taqlid ya hao na wale waliowaua na kuwakhalifu.

Au wao mara nyingi wanakuwa hawafahamu Ahlul Bait ni kina nani, na ukiwauliza, ni nani Ahlul Bait? Kwa haraka sana watajibu: "Ni wakeze Mtume ambao Mwenyezi Mungu amewaondolea uchafu na amewatakasa mno."

Kuna mmoja wao aliniondolea mushkeli huu pale nilipomuuliza na akanijibu huku akisema:- "Ahlus-Sunna wote wanawafuata Ahlul-Bait" Nilistaajabu na kisha nikasema, "Munawafuata vipi"? Akasema: "Mjumbe wa Mwenyezi Mungu amesema: chukuweni nusu ya (maarifa ya) dini yenu kutoka kwa hiki kijanajike chekundu yaani Aisha" Basi sisi tumechukua nusu ya dini yetu kutoka kwa Ahlul-Bait.

Na kwa msingi huu yanaeleweka maneno yao juu ya kuwaheshimu na kuwatukuza Ahlul-Bait. Ama pindi utakapowauliza kuhusu Maimamu kumi na wawili hakuna wamjuaye isipokuwa Ali, Hasan na Husein, pamoja na kwamba hawakiri Uimamu wa Hasan na Husein, na wakati huo huo wao wanamtukuza Muawiyah ibn Abi Sufiyan ambaye alimtilia sumu Hasan na akamuua, na (huyu Muawiyah) wanamuita kuwa ni "Mwandishi wa Wahyi" na amri ibn Al-as (wote hawa wanawatukuza) kama wanavyomtukuza Imam Ali.

Hakika hali kama hii ni yenye kupingana na kuchanganya mambo, kuchanganya haki na batili na ni kuufunika mwangaza kwa kiza, vinginevyo, itawezekanaje ndani ya moyo wa muumini lichanganyike pendo la kumpenda Mwenyezi Mungu na shetani kwa pamoja?

Mwenyezi Mungu amesema ndani ya kitabu chake kitukufu:- "Hutawakuta watu wanaomuamini Mwenyezi

249

Mungu na siku ya mwisho wanawapenda wale wanaompinga Mwenyezi Mungu na Mtume wake hata wakiwa ni baba zao au watoto wao au ndugu zao au jamaa zao, hao ndiyo ambao (Mwenyezi Mungu) ameandika nyoyoni mwao imani na akawatia nguvu kwa roho itokayo kwake na atawaingiza katika mabustani yapitayo mito ndani yake watakaa humo daima, Mwenyezi Mungu amewaridhia na wao wamekuwa radhi naye hao ndiyo kundi la Mwenyezi Mungu, fahamuni (ya kwamba) bila shaka kundi la Mwenyezi Mungu ndilo lenye kufaulu" (Qur. 58:22)

Kadhalika amesema: Mwenyezi Mungu mtukufu:- "Enyi mlioamini, msiwafanye adui zangu na adui zenu kuwa ni marafiki, munawapa upendo kwa ajili ya urafiki hali ya kuwa wao wamekwishaipinga haki iliyokujieni" (Qur. 60:1')

3). Hadithi isemayo:

Atakayefurahishwa kuishi maisha niliyoishi mimi.

Amesema Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.):-"Yeyote atakayefurahishwa kuishi maisha (niliyoishi) mimi na kufa kama kifo changu na kuishi ndani ya pepo ya milele, basi na amtawalishe Ali baada yangu mimi, na (pia) amtawalishe aliyetawalishwa naye, na afaate nyayo za Ahlul-Bait wangu baada yangu kwani wao ni kizazi changu. wameumbwa kwa udongo nilioumbiwa mimi, na wamepewa fahamu yangu na elimu yangu, ole wao wenye kupinga ubora wao katika umati wangu, wenye kukata maungamano yao kwangu, basi Mwenyezi Mungu asiwape Shafaa yangu" Taz: Mustadrak Al-HakimJuz. 3uk. 128,At-Tabramfil-Jamil-Kabir,Al-Isabah cha Ibn Hajar Al-asqalani, Kanzul-Ummal Juz. 6 uk. 155, Al-Manaqib cha Khawar-zami uk. 34, Yanabiul-Mawaddah uk. 149 Hil-Yatul-Auliyaa Juz. 1 uk. 86, Tarikh Ibn Asakir Juz. 2uk. 95.

250

Hadithi hii kama tunavyoiona, ni miongoni mwa hadithi zilizowazi ambayo haikubali Taawili na wala haimuachii Muislamu namna yoyote ya hiyari bali inakata kila hoja dhidi yake, na ikiwa Muislamu hakumtawalisha Ali na hakufuata nyayo za Ahlul-Bait ambao ni kizazi cha Mtume, basi atakuwa ameharamishiwa shafaa uombezi wa Babu yao ambaye ni Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.).

Na inafaa kuashiria hapa ya kwamba, wakati wa uchunguzi niliokuwa nikiufanya, kwanza niliingiwa na mashaka juu ya kusihi kwa hadithi hii na nilistushwa na maonyo na makemeo yaliyomo kwa yeyote mwenye kwenda kinyume cha Ali na Ahlul-Bait na khususan kwa kuwa hadithi hii haikubali Taawili. Mashaka yaliniondoka pindi niliposoma ndani ya kitabu kiitwacho Al-Isabah kilichoandikwa na Ibn Hajar Al-as-Qalani, baada ya kuiandikika hadithi hii amesema:-

"Mimi nasema kuwa ndani ya sanad ya hadithi hii yumo Yahya ibn Yaala al-Muharibi naye ni dhaifu". Basi kwa kauli hii Ibn Hajar akawa ameniondolea baadhi ya mishkeli iliyokuwa akilini mwangu kwani nilikuwa nadhani kwamba Yahya ibn Yaala al-Muharibi ni mzushi wa hadithi na wala siyo muaminifu, lakini Mwenyezi Mungu Mtukufu alitaka kuniweka kwenye ukweli uliokamilika, kwani siku moja nilisoma kitabu kiitwacho, ''MunaqashatuAqaadiyahfiMaqalatiIbrahimaAl-Jab-han" uk. 26. Kitabu hiki kikaniweka kwenye hali iliyo bayana, pindi kilipobainisha kwamba Yahya ibn Yaala Al-Muharibi ni miongoni mwa watu Waaminifu ambao Masheikh wawili wa hadithi Bukhari na Muslim wamewategemea nami binafsi nilifuatilia nikakuta Bukhari ameandiKa hadithi zake ndani ya mlango wa "Ghaz-watul-Hudaibiyyah" ndani ya juzuu ya tatu ukurasawa31.

Vile vile Muslim ndani ya sahihi yake ameandika hadithi ya Yahya katika mlango wa Hudud ndani ya Juzuu ya 5 ukurasa

251

119, na Dhahabi mwenyewe - pamoja na ugumu wake amemueleza kuwa ni mkweli, yaani ameeleza hadithi zake ni mur'sali zinazokubalika na Maimamu wa "Jarhi na Taadil" wamemuhesabu kuwa yu miongoni mwa watu waaminifu na Masheikh wawili wamemtolea hoja. Basi ni wa nini uzushi huu na kumpaka matope na kugeuza ukweli kisha kumtuhumu mtu muaminifu ambaye waandishi wa Sihah wametoa hoja kupitia kwake?

Alaa! ni kwa kuwa ameeleza ukweli halisi juu ya kufuata nyayo za Ahlul-Bait, hivyo basi malipo yake toka kwa Ibn Hajar yakawa ni kumdhalilisha na kumfanya kuwa ni dhaifu. Lakini Ibn Hajar hakujua kama baada yake wako wanachuoni mabingwa wanaompa changamoto juu ya kila jambo dogo na kubwa na wataiumbua chuki yake na ujinga wake kwani wao wanang'ara kwa nuru ya Utume na wanafuata uongofu wa Ahlubait.

Na baada ya hayo nimefahamu ya kwamba baadhi ya wanachuoni wetu wanajaribu kwa juhudi zao kuufunika ukweli ili mambo ya Masahaba na Makhalifa yasije yakaumbuka, Masahaba ambao walikuwa ndiyo maamiri wao na vigezo vyao. Kuna wakati utawakuta wanageuza maana ya Maula katika hadithi ya "Mankuntu Maulahu" badala ya kuwa Aula (mstahiki) wanafanya kuwa mpenzi, mtetezi. Wanachuoni wa Kisunni wanasema kuwa hadithi hii ni sahihi, lakini ni wajibu kuiawili (kuipa tafsiri) imaanishe maana ya mpenzi na mtetezi na wanafanya hivi ili kuupasisha Ukhalifa wa Abubakar, Umar na Uthman, vinginevyo itakuwa ni wajibu Ali (a.s.) awe ni mwenye kustahiki Ukhalifa kuliko wote. Kwa hiyo utaona ndani yake kuna mambo, ikiwemo kupotoka Masahaba wengi waliompa baia Abubakar, na kusema hivi kwao ni kauli isiyofaa.

Hii ndiyo kauli ya wanachuoni wa Kisunni kama walivyonieleza wengi wa wanachuoni wetu wa Tunis.

252

Nilipowaambia kwamba Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.) kabla ya (kuisema) hadithi hii alipokuwa akiwahutubia aliwauliza "Je mimi siyo bora kwenu kuliko nafsi zenu?" Wakasema "Bila shaka (wewe ni bora kwetu kuliko nafsi zetu) hapo ndipo Mtume aliposema, "Basi yeyote ambaye mimi nilikuwa mtawalia mambo yake basi huyu hapa Ali ni mtawalia mambo yake" Baadhi yao walinijibu wakisema, "Hiyo ni miongoni mwa ziyada zilizozidishwa na Mashia." Na nilipowauliza, "Hivi kweli inaingia akilini, kwamba Mtume (s.a.w.) awakusanye mamia ya watu miongoni mwa Mahujaji katika joto kali linalounguza eti tu kwa ajili ya kuwaambia kwamba Ali (a.s.) ni mpenzi na msaidizi wa Waislamu? Hivi kweli inaingia akilini? Basi walinyamaza hawakujibu kitu.

Kuna wakati mwingine wanazipinga na kuzikanusha zile hadithi ambazo zinapingana na madh-hebu yao hata kama zimeandikwa ndani ya vitabu vyao Sahihi na Musnad zao. Mfano wa hilo ni ile hadithi isemayo, "Makhalifa baada yangu ni kumi na wawili wote wanatokana na Maquraish", na katika riwaya nyingine "Wote wanatokana na Bani Hashim". Hadithi hii wameiandika wote Bukhari na Muslim na pia Sihahi zote za Kisunni, lakini pamoja na hali hii wao wanakanusha kuwa kwamba wote hawa ndiyo wale Maimamu kumi na wawili wanaotokana na Ahlubait ambao Mashia Ithnaasharia ndiyo wanaosema kuwa ni Maimamu na watawalia mambo ni wao.

Masunni kwa upande wao huwahesabu wale Makhalifa wanne na humuongeza juu ya hawa Khalifa Omar ibn Abdul-Aziz na inakuwa idadi yao ni watano na hapo wanasimama kwa sababu wao hawamuhesabu Muawiyah wala mwanawe Yazid wala Mar-wan ibn Al-Hakam na wanawe kuwa nao ni miongoni mwa Khulafaur-Rashiduna, na kwa kutowahesabu hao kuwa miongoni mwa Khulafaur-Rashiduna. Hii ni hali halisi.

253

Kwa hiyo idadi ya Makhalifa kumi na wawili kwa Masunni inabakia ni utata usiokuwa na ufumbuzi labda wakubaliane na kauli ya Mashia!

Na kuna wakati mwingine huwa wanafuta nusu ya hadithi au theluthi mbili ili waibadili kwa kuweka "kadha wa kadha"!! Mfano wa hilo ni ile hadithi isemayo, "Hakika huyu ni ndugu yangu na ni wasii wangu na ni Khalifa wangu baada yangu, msikilizeni na mumtii" Hadithi aliyoisema Mtume hali ya kuwa ameshika shingo ya Ali, na ni hadithi ambayo imeandikwa na Tabari ndani ya Tarikh yake na Ibn Al-Athir ndani ya Kamil yake, vile vile Kanzul Ummal, Musnad Imam Ahmad,' na Siratul-Halabiyah na Ibn Asakir, lakini mchapishaji aliyechapisha kitabu cha tafsiri ya Tabari Juz. 19 uk. 121 hakuiacha hadithi hii kamilifu kama alivyoitamka mwenyewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, bali ameondosha maana yake yote na akaibadili ikabakia "Hakika huyu ndugu yangu na kadha wa kadha". Akasahau kwamba Tabari ameiandika hadithi hii kwa ukamilifu ndani ya kitabu chake cha historia Juz. 2 uk. 319-321 hakika huo ndiyo uaminifu wa elimu.

Huenda mwanachuoni huyu hakuwa na ujanja wa kuikanusha hadithi hii, na aliona kuwa ndani yake kuna maagizo ya Mtume yaliyowazi kuhusu Ukhalifa wa Imam Ali baada ya Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.), kwa hiyo akakusudia kuyafunika maagizo haya na kuyabadilisha kwa kuandika kadha wa kadha. Masikini (mtu) huyu alidhani kwamba anaweza kufunika nuru ya jua wakati yeye atakapofumba macho yake, au anaweza kuwatosheleza wasomaji na wanataaluma kwa kusema kwake "kadha wa kadha". Sivyo kabisa, hayo ni maneno ayasemayo yeye!!

Wakati mwingine Masunni huwa wanawatilia mashaka wapokezi wa kuaminika kwa sababu tu wamesimulia mambo ambayo nafsi zao haziyapendi, mfano wa hilo ni pale

254

wanapomtuhumu Yahya ibn Yaala Al-Muharib, ambaye ni miongoni mwa wapokezi (wa hadithi) wanaoaminika ambao Bukhari na Muslim wametoa hoja kupitia hadithi zake. Lakini Ibn Hajar Al-Asqalani amemtuhumu na kumwita kuwa ni dhaifu, si kwa sababu yoyote ila tu ni kwa kuwa amesimulia hadithi ya Wilayah ambayo ndani yake Mtume (s.a.w.) aliwaamuru Masahaba wake wamtawalishe Ali na Ahlul Bait.

Na kwa mujibu wa Hadithi (ilivyo) siyo ajabu kwa Ibn Hajar na walio kama yeye ambao wanajaribu kwa bidii zao kuufuta ukweli ambao Muawiyah ibn Abi Sufiyan alitoa kila anachokimiliki katika dhahabu na fedha kwa lengo la kuufuta ukweli lakini hakufaulu, basi ni vipi itawezekana kwa Ibn Hajar kuufuta ukweli kwa njia ya kuwatuhumu wasimulizi wanaoaminika? Bila shaka Muawiya alikuwa na mali nyingi, hila, nguvu, madaraka na kitisho, lakini pamoja na yote hayo alishindwa vibaya na kufedheheka kisha zama zikamfunika akawa hajulikani, wakati ambapo nuru ya Imam Ali inasambaa siku zote. Basi ni vipi inawezekana kwa Ibn Hajar na walio kama yeye kutia mashaka kuhusu ukweli wa Ahlu-Bait kwa kiasi cha kufanya tuhuma dhidi ya wapokezi (wa hadithi) ambao ni waaminifu tena wanaotegemewa?

Katu haitawezekana"kabisa nuru ya Mwenyezi Mungu kuzimwa kwa vinywa!!...

Wakati mwingine watu hawa huiandika hadithi ndani ya chapa ya mwanzo kwa ukamilifu na katika chapa zingine huiondoa bila ya kuashiria sababu za kuiondoa, licha ya kwamba wasomi hufahamu sababu za kufanya hivyo. Mfano wa hilo ni kitendo alichokitenda Muhammad Husein Haikal ndani ya kitabu chake kiitwacho "Hayatu Muhammad", kwani ndani ya chapa ya kwanza uk. 104 amesema: "Iliposhuka kauli ya Mwenyezi Mungu isemayo "Waandhir Ashiratakal-Aqrabina" yaani -Waonyejamaazako wa karibu-}kisha akakielezakile kisa

255

kama walivyokieleza wanahistoria, na mwishoni Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.) alisema: "Hakika huyu ni ndugu yangu na ni wasii wangu na ni Khalifa wangu kwenu ..." Lakini yeye (Muhammad Haikal) katika chapa ya pili akaiondosha riwaya hii pia ndani ya chapa zilizofuatia bila ya maelezo wala ufafanuzi mambo ambayo yanaashiria kwa ukaribu au umbali uliosababisha kuondosha sehemu ya hadithi hii ya Mtume (s.a.w.). Japokuwa Sheikh Muhammad Jawad Mughniyyah -ukweli halisi anao mwenyewe - amenakili tukio hili ndani ya kitabu chake kiitwacho "As-Shiatu fil-Mizan" amesema kwamba "Muhammad Husein Haikal aliondosha sehemu hii (ya hadithi) kwa kupokea maelfu ya pauni" Na kwa kuwa Haikal hakuikanusha habari hii na wala hakutoa sababu za kuondosha sehemu hiyo iliyotajwa, basi bila shaka unabainika ukweli wa Sheikh Muhammad Jawad Mughuniyyah na pia ufuatiliaji wake juu ya mambo yanayotendeka!

Kwa msingi huu sisi tunasema kuwaambia watu hawa na wengine kama hawa ambao wanaziuza aya za Mwenyezi Mungu kwa thamani ndogo ya dunia, "Muogopeni Mwenyezi Mungu na museme kauli zilizo sawa sawa na kumbukeni kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu aliposema:-

Rudi nyuma Yaliyomo endelea