Rudi nyuma Yaliyomo endelea

Na lau Ali Ibn Abi Talib na Masahaba waliomfuata wangelifahamu ya kwamba Abubakar anayo daraja hii ya imani, basi isingejuzu kwao kuikhalifu Baia yake. Na lau Fatumah Az-Zahra angelifahamu ya kwamba Abubakar anayo daraja hii ya imani basi asingemkasirikia na kujizuwia kumsemesha na kujibu salamu yake na asingeomba dua dhidi yake katika kila sala. Taz: Al-Imamah Was-Siyasah Juz. 1 uk. 14, Rasailul-Jahidh uk. 301, Aalaamun-Nisaa Juz. 3 uk. 1215.

Kisha Bibi Fatumah asingelimzuia Abubakr kuhudhuria mazishi yake - kama ilivyokuja ndani ya usia wake na lau Abubakar angelifahamu kuwa yeye anayo daraja hii ya imani, basi asingetamani wakati wa mauti yake ya kwamba lau asingekuwa ameikashifu nyumba ya Bibi Fatumah (a.s.).

Na kwamba siku ya Saqifa angeliuacha Ukhalifa shingoni

221

kwa mmoja kati ya watu wawili, yaani Umar au Abu Ubaidah. Taz: Tarikh TabariJuz. 4 uk. 52 Al-Imamah Was-Siyasah Juz. 1 uk. 18, Jdrikh Al-Masoudi Juz. 1 uk. 414.

Kwa hiyo basi mtu ambaye yuko katika daraja kama hii ya imani na hiyo imani yake inashinda imani ya umma wote, hawezi kujuta mwishoni mwa uhai wake kwa yale aliyomfanyia Fatumah na kujuta alipomuunguza Al-Faja-a Assalmi na kwa kutawalia Ukhalifa, kama ambavyo hawezi kutamani asiwe mtu na awe kapi au kinyesi cha mnyama.

Hivi kweli imani ya mtu kama huyu ni sawa na imani ya umma wa Kiislamu bali iko juu zaidi ya imani ya umma wa Kiislamu?

Na tutakapoichukua ile hadithi isemayo: "Lau ningekuwa mwenye kujifanyia mwandani, basi ningelimfanya Abubakr kuwa mwandani wangu".

Hadithi hii ni kama ile iliyotangulia kwani (tunajiuliza) kwani alikuwa wapi Abubakar siku ya "Muakhatus-Sughra"[24] huko Makka kabla ya Hijra na siku ya "Muakhatul Kubra"[25] huko Madina baada ya Hijra na katika zote mbili, na mara mbili zote Mjumbe wa Mwenyezi Mungu alimfanya Ali kuwa ni nduguye na akasema, "Wewe ni ndugu yangu duniani na akhera"[26]

Mtume hakumshughulikia Abubakar alimnyima udugu wa akhera kama vile alivyomnyima Ukhalil "umwandani".

222

Na mimi sitaki kuirefusha maudhui hii ninatosheka na mifano hii miwili ambayo nimeileta kutoka ndani ya vitabu vya Kisunni, ama kwa Mashia wao hawazikubali hadithi hizo moja kwa moja na wanazo dalili zilizo wazi ya kwamba ziliwekwa katika zama zilizokuja baada ya Abubakar.

Kwa hiyo basi ikiwa tutaacha (kutaja) fadhila na ubora wao na tukachunguza maovu (yaliyotendwa) bila shaka hatuwezi kupata ovu hata moja lililotendwa na Ali ibn Abi Talib wakati ambapo kwa wasiokuwa yeye tutakuta maovu mengi yaliyoandikwa ndani ya vitabu vya Kisunni kama vile sihahi (sita) na vitabu vya sira na historia.

Na kwa msingi huu inapatikana Ijmai ya pande zote mbili inayomuhusu Ali peke yake kama inavyotia nguvu jambo hilo historia na kwamba Baia sahihi haikuwa kwa mwingine isipokuwa kwa Ali peke yake.

Imam Ali aliikataa baia (yao baada ya kifo cha Athuman) lakini Muhajirina na Ansari wakamlazimisha na kuna watu fulani hawakufanya baia kwa Imam Ali lakini hakuwalazimisha wambai wakati huo huo baia ya Abubakar ilikuwa ni (tukio la) . ghafla, Mwenyezi Mungu aliwakinga Waislamu kutokana na shari yake, kama asemavyo Omar ibn Khatab - na Ukhalifa wa Umari ulipatikana kwa usia wa Abubakr, nao Ukhalifa wa Uthman (ulikuwa ni tukio la) unyonge kihistoria, na hiyo ni kwa kuwa Omar alipendekeza kamati ya watu sita (kujadili) suala la Ukhalifa (baada yake) na akawalazimisha wamchague mmoja wao na akasema, "Watakapo afikiana watu wanne na wawili wakapinga basi wawili hawa wauawe, na kama watu hawa sita watagawanyika makundi mawili kila upande ukawa na watu watatu, basi chukueni maoni ya watu watatu ambao Abdurahman ibn Auf atakuwa pamoja nao, na iwapo muda utamalizika na watu hawa sita wakawa bado hawajaafikiana, basi wote hawa muwaue". Kisa hiki ni kirefu na ni cha

223

kustaajabisha, lakini cha muhimu ni kwamba Abdur-rahman ibn Auf alimchagua Ali na kisha kumuwekea masharti kwamba awaongoze kwa mujibu wa kitabu cha Mwenyezi Mungu na Sunna ya Mjumbe wake na sunna ya Masheikhe wawili (yaani) Abubakr na. Omar. Imam Ali aliikataa sharti hii na Uthman akaikubali na yeye akawa Khalifa kisha Ali alitoka katika-baia hiyo hali ya kuwa tangu mwanzo alifahamu matokeo yake yatakuwaje, na hapana shaka alilizungumzia jambo hilo ndani ya khutba yake ijulikanayo kama "Khut-batus-shaqshaqyah."

Na baada ya Imam Ali (a.s.) Muawiya aliukalia Ukhalifa na akaubadilisha ukawa ni Ufalme wa Kaizari. Banu Umayyah wakawa wanapokezana, na baada yao wakaushika Banu Abbas mwana kumrithi baba, basi hakuja Khalifa isipokuwa kwa maagizo ya Khalifa aliyetangulia kwa yule ajaye au kwa nguvu ya upanga na silaha na hapakuwa na baia iliyo sahihi katika historia ya Uislamu kuanzia zama za Makhalifa (wa mwanzo) mpaka zama za Kamal Ataturki aliyemalizia Ukhalifa wa Kiislamu. Baia sahih ilikuwa ni ya Amir-ul-Muuminina Ali Ibn Abi Talib.

4. Hadithi zilizokuja kuhusiana na Imam Ali zinawajibisha kumfuata.

Miongoni mwa hadithi nilizozichukuwa na zikanilazimisha nimfuate Imam Ali ni zile zilizoandikwa ndani ya sihahi za Kisunni na vikatilia nguvu usahihi wa hadithi hizo. Ama Mashia wao wanazo nyingi mno lakini - kama ilivyo ada, mimi sitatoa dalili wala kutegemea hadithi isipokuwa zile ambazo pande zote mbili wameafikiana na miongoni mwa hadithi hizo ni hizi zifuatazo:-

a: Hadithi isemayo "Mimi ndiyo mji wa elimu na Ali nidyo rnlango wake".

224

Hadithi hii peke yake inatosha kubainisha kiigizo kinachopasa kukifuata baada ya Mtume (s.a.w.) kwani mwenye elimu ndiye anayefaa kufuatwa yaani yeye anastahiki mno kuwa kiigizo kuliko mjinga,

Mwenyezi Mungu amesema: "Waambie, hivi wanalingana wale wanaofahamu na wale wasio fahamu" (Our. 39:9)

Na amesema vile vile kwamba:- "Je aongozaye kwenye haki ndiye mwenye haki ya kufuatwa au yule asiyeongoka (mwenyewe) isipokuwa kwa kuongozwa (ndiye anayestahiki)9 (Our. 10:35)

Hapana shaka mwenye maarifa ndiye anayeongoza na asiye na maarifa anastahiki kuongozwa na anahitajia mno uongofu kuliko mwingine yeyote.

Na kuhusu maelezo haya, historia imetuandikia ya kwamba Imam Ali yeye ni mwenye maarifa zaidi kuliko Sahaba yeyote kwa jumla, na wao Masahaba walikuwa wakimrejea Imam juu ya mas-ala yote mazito, nasi kamwe hatukupata kufahamu ya kwamba yeye Imam Ali aliwahi kuuliza kwa Sahaba yeyote, bali Abubakar anasema:- Mungu asinibakishe kwenye tatizo ambalo Abul-Hassan hayupo.

Omar naye anasema;- "Lau asingelikuwa Ali basi Umar angeliangamia" Taz: AI-Istiabu Juz. 3 iik. 39, Manaqib Al-Khawarzami uk. 48, Ar-Riyadhun-Nadhrah Juz. 2 uk. 194.

Ibn Abbas naye anasema:- "Elimu yangu na elimu ya Masahaba wa Mtume ukilinganisha na elimu ya Ali ni kama tone moja ndani ya bahari saba." Imam Ali mwenyewe anasema:- "Niulizeni kabla hamjanikosa, namuapa Mwenyezi Mungu hamtaniuliza jambo lolote litakalokuwa mpaka siku ya kiyama isipokuwa nitakuelezeni na niulizeni juu ya kitabu cha Mwenyezi Mungu, basi namuapa Mwenyezi Mungu, hapana aya yoyote isipokuwa mimi nafahamu kuwa ilishuka usiku au

225

mchana, katika ardhi tambarare au mlimani." Taz: Ar-Riyadh An-Nadhrah Juz. 2uk. 198, Tarikh Al-Khulafa cha Suyut Al-ItqanJuz. 2 uk. 319, Fat-h Al-Bari Juz. 8 uk. 485, Tah-Dhibut-Tahdhib Juz, -7 uk. 338.

Wakati huo huo Abubakar alipoulizwa maana "Al-Abb" iliyoko ndani ya kauli ya Mwenyezi Mungu isemayo " Wafakihatan •wa Abban Mataan Lakum Walian-Amikum" Akasema, "Ni mbingu gani itakayonifunika na ardhi ipi itakayonibeba iwapo nitasema kitu nisichokijua ndani ya kitabu cha Mwenyezi Mungu?"

Na Omar ibn Al-Khatab naye anasema:-."Watu wote wana elimu isipokuwa Omar hata wanawake wenye bangili miguuni."

Sihahi za Kisunni na vitabu vyao vimeafikiana juu ya ubora wa Ali (a.s.) na kutangulia kwake katika elimu kuliko Masahaba wote, kwa mfano tu rejea maelezo yaliyomo ndani ya Al-Istiabu Juz. 3 uk. 38-45 utakuta kauli za Masahaba wenyewe wakimtanguliza Imam Ali juu yao.

Na aliulizwa Omar ibn Al-Khataab (afafanue) aya fulani iliyomo ndani ya kitabu cha Mwenyezi Mungu, matokeo yake akamkemea muulizaji na akampiga kwa mjeledi mpaka akamtoa damu kisha akasema, "Musiulize mambo, mkidhihirishiwa yatawakera." Na aliulizwa juu ya "Kalalah" hakuweza kufahamu.

Tabari ameandika ndani ya tafsiri yake kuhusu Omar kwamba amesema:- "Kwangu mimi kuifahamu maana ya Kalalah ni bora mno kuliko kupata majumba ya Shamu".

Vile vile ibn Majah ameandika ndani ya Sunan yake kutoka kwa Omar ibn Al-Khatab amesema:- "Mambo matatu lau Mtume angeliyabainisha kwangu ingekuwa bora mno kuliko dunia na vilivyomo; Kalalah, Riba na Ukhalifa".

226

Sub-hanallah,! haiwezekani kwa Mjumbe wa Mwenyezi Mungu kuwa aliyanyamazia mambo haya akakosa kuyabainisha.

b: Hadithi isemayo: - "Ewe Ali wewe kwangu mimi unayo daraja kama ya Harun kwa Musa isipokuwa hapana Nabii baada yangu". Taz: Sunan Ad-Darami Juz. 1 uk. 54, Tafsiri ibn Kathir Juz. 4 uk. 232 Ad-Durul-Manthoor J. 6 uk. 111.

Hadithi hii ambayo iko wazi kwa wenye akili, ndani yake kuna kuhusishwa Amirul-Muuminina Ali na Uwaziri, Uwasii na Ukhalifa.

Kwa hiyo kama alivyokuwa Haroon ni Waziri, Wasii, na Khalifa wa Musa alipoghibu na kwenda kwenye Miqat ya Mola wake, basi ni hivyo hivyo daraja ya Imam Ali naye ni kama Harun amani imshukie yeye na Mtume wetu. Kwa hiyo Imam Ali (a.s.) ni mfano halisi wa Harun isipokuwa Utume ambao hadithi yenyewe imeuvua, na ndani yake pia ni kwamba Imam Ali ni Sahaba bora mno kuliko Masahaba wengine wote, na inavyofahamika ni kwamba hadithi hii inakubalika kwa Waislamu wote.

c: Hadithi isemayo:- "Yeyote ambaye mimi nilikuwa mtawalia mambo yake, basi huyu Ali ni mtawalia mambo yake, ewe Mwenyezi Mungu mpende atakayemtawalisha Ali, na umpinge atakaye mpinga, na umsaidie atakayemsaidia, na umdhalilishe atakaye mdhalilisha na uizungushe haki pamoja naye popote atakakozungukia".

Hadithi hii peke yake inatosha kuyapinga madai ya kuwatanguliza Abubakar na Omar na Uthman kwa msingi wa kwamba (Ali) alisimikwa na mwenyewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu awe ni mtawalia mambo ya waumini baada ya Mtume, na hapana mazingatio yoyote kwa yule anayefasiri hadithi hii kwa maana ya mpenzi na msaidizi kwa kuitoa kutoka kwenye maana ya asili aliyokusudia Mtume na yote hayo (yanafanyika)

227

ili kulinda heshima ya Masahaba, kwani Mjumbe wa Mwenyezi Mungu aliposema kuhutubia siku hiyo kukiwa na joto kali alisema: "Je hamshuhudii kwamba mimi ni bora zaidi kwa Waumini kuliko nafsi zao?" Wakasema, "Bila shaka wewe ni bora ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu." Hapo ndipo aliposema:- "Basi yeyote, ambaye mimi nilikuwa mtawala wa mambo yake, huyu Ali ni mtawala wa mambo yake..." Hii ni Nassi (maagizo) yaliyowazi katika kumrithisha Ali Ukhalifa juu ya umma wake, na wala haiwezekani kwa mtu mwenye akili adilifu isipokuwa ni kuikubali maana hii na kupinga ile tafsiri ya baadhi ya watu iliyolazimishwa ili kulinda heshima na utukufu wa Mtume kabla ya kulinda utukufu wa Masahaba. Kwani tafsiri yao hii ni kudharau na kupuuza hekima ya Mtume ambaye alikusanya kundi kubwa la watu katika joto kali najua utosini eti awambie kuwa Ali ni kipenzi cha Waumini na ni msaidizi wao. Je watu hawa wanaogeuza maandiko kwa lengo la kuhifadhi heshima ya wakubwa zao na mabwana zao, wataufasiri namna gani ule mkusanyiko wa watu waliompongeza Imam Ali jambo ambalo Mjumbe wa Mwenyezi Mungu aliliamuru?

Mtume alianza na wakeze ambao ndiyo mama wa Waumini, na kisha wakaja Abubakar na Omar wakasema, "Hongera ewe mwana wa Abu Talib, leo kumekupambazukia na kukuchwea hali ya kuwa umtawalia wa mambo ya kila muumini mwanamume na mwanamke." Na ukweli historia inashuhudia kwamba, wale wanaogeuza (maana halisi iliyokusudiwa) ni waongo, na ole wao kwa yale wayaandikayo, amesema Mwenyezi Mungu: "Bila shaka kuna kundi miongoni mwao wanauficha ukweli hali ya kuwa wanafahamu" (Qur. 2:146)

d: Hadithi isemayo:- "Ali anatokana na mimi na mimi natokana na Ali, na wala hawezi mtu kutekeleza (jambo) kwa niaba yangu isipokuwa mimi mwenyewe au Ali" Taz: Suncm

228

Ihn Majah, Jnz. I uk. 44, Khasaisim-Nasai uk. 20, Sahih TirmidhiJnz. 5 uk. 300, Ar-RiyadhuAn-NadhrahJ. 2 uk. 229.

Hii ni hadithi nyingine tukufu iliyowazi ikieleza kwamba Imam Ali ni mtu pekee ambaye Mjumbe wa Mwenyezi Mungu alimpa ustahiki (wa kutenda) kwa niaba yake, na hadithi hii Mtume aliisema wakati alipomtuma Imam Ali akawasomee watu sura Al-Baraa siku ya hija badala ya Abubakar na Abubakar alirudi hali ya kuwa analia huku akisema, "Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, kuna kitu kimeshuka kwa ajili yangu?"Mtume (s.a.w.) akasema, "Mwenyezi Mungu ameniamuru hivyo, hawezi kutekeleza (jambo) kwa niaba yangu isipokuwa mimi mwenyewe au Ali."

Na hadithi hii inaitia nguvu ile (hadithi) nyingine aliyoisema Mjumbe wa Mwenyezi Mungu kumwambia Ali katika munasaba mwingine pale aliposema: "Wewe Ali utaubainishia umma wangu yale mambo ambayo watahitilafiana ndani yake baada yangu". Taz: Tarikh Damishq ya ibn Asakir Juz. 2 uk. 488, Kunuzul-Haqaiq chaAl-Mawi uk. 203, Kanzul-Ummal Juz. 5 uk. 33.

Basi ikiwa (mtu mwingine) hawezi kutekeleza jambo kwa niaba ya Mjumbe wa Mwenyezi Mungu isipokuwa Ali, na ni yeye ndiye atakayeubainishia umma (wa Kiislamu) yale mambo watakayo hitilafiana ndani yake baada ya Mtume, basi itakuwaje amtangulie mtu ambaye hafahamu maana ya "Al-Abb" na yule asiyefahamu maana ya "Al-Kalalah", kwa hiyo naapa ya kwamba miongoni mwa misiba iliyoukumba umma wa Kiislamu na kuuzuia usiweze kutimiza jambo muhimu ambalo Mwenyezi Mungu aliuchagulia umma huu. Na hii haitakuwa ni hoja dhidi ya Mwenyezi Mungu wala dhidi ya Mjumbe wa Mwenyezi Mungu wala Amirul-Muuminin Ali ibn Abi Talib, bali hoja iliyowazi itakuwa dhidi ya wale walioasi na kubadilisha.

229

Mwenyezi Mungu amesema:-

"Na wanapoambiwa njoni kwenye yale aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu, na (mje) kwa Mtume, wao husema, yanatutosha yale tuliyowakuta nayo baba zetu, je hata kama baba zao -walikuwa hawajui kitu wala hawakuongoka. ?" (Qur. 5:104)

e: Hadithi ya Ad-Dar Yaumul-Indhar.

Mjumbe wa Mwenyezi Mungu amesema hali ya kuwa akimuashiria Ali:

"Hakika huyu ni ndugu yangu, wasii wangu na Khalifa wangu baada yangu, basi msikilizeni na mumtii."

Taz: Tarikh Tabari Juz. 2 uk. 319, Tarikh Ibn Athir Jiiz. 2 uk. 62, Siratu Al-Halabiyah Juz. 1 uk. 311 Shawahidut-Tanzil cha Al-Haskani Juz. 1 uk. 371 Kanzul-Ummal Juz. 15 uk. 15. Tarikh ibnAsakir Juz. 1 uk. 85 Tafsir Al-Khazin ya Alaud-Dini Shafii Juz. 3 uk. 371, Hayatu Muhammad cha Husain Haikal, chapa ya kwanza mlango wa Waandhir Ashira Takal-Aqrabina.

Hadithi hii pia ni miongoni mwa hadithi sahihi walizozinakili wanahistoria mwanzoni tu mwa kutumwa kwa Mtume na wakaiweka kuwa ni miongoni mwa miujiza ya Mtume (s.a.w.), lakini siasa ndiyo iliyobadili na kupotosha ukweli na hali halisi, na siyo ajabu hali hii kutokea kwani yaliyotokea katika zama hizo zenye giza yanajirudia leo katika zama zenye mwanga. Huyu Muhammad Husain Haikal ameiandika hadithi hii kwa ukamilifu ndani ya kitabu chake kiitwacho "Hayatu Muhammad" (yaani maisha ya Muhammad) ndani ya ukurasa wa 104 chapa ya kwanza ya mwaka 1354 A.H. na katika chapa ya pili na zilizofuatia katika hadithi hiyo hiyo kumeondolewa ile kauli ya Mtume isemayo (wasii wangu na Khalifa wangu baada yangu); vile vile ndani ya Tafsiri ya

230

Tabar Juz. ya 19 ukurasa 121 wameondosha ile kauli ya Mtume isemayo (wasii wangu na Khalifa wangu) na wakabadilisha kwa kauli isemayo: "Hakika huyu ni ndugu yangu na hivi na hivi." wakasahau kwamba Tabari ameitaja hadithi hiyo kwa ukamilifu ndani ya kitabu chake cha historia juzuu ya pili ukurasa wa319.

Angalia ni vipi wanavyopotosha maneno kutoka mahala yanapostahiki na wanayageuza mambo, wao wanataka kuizima nuru ya Mwenyezi Mungu kwa vinywa vyao na Mwenyezi Mungu ataitimiza nuru yake..,

Na wakati nilipokuwa nikifanya utafiti, nilitaka nisimame juu ya msingi uliowazi, basi niliitafuta ile chapa ya kwanza ya kitabu kiitwacho "Hayatu Muhammad" na nilikipata, namshukuru Mwenyezi Mungu, lakini baada ya tabu na mashaka na ili nigharimu kiasi kikubwa lakini la muhimu ni kwamba niliuona ule upotoshaji, na kilinizidishia yakini kwamba watu waovu wanajaribu kwa juhudi zao kuufuta ukweli uliothibiti kwa sababu tu ni hoja yenye nguvu inayowaunga mkono makhasimu wao!

Lakini mtafiti mwenye uadilifu pindi anapoona kitu miongoni mwa upotoshaji na udanganyifu kama huu huzidi kujitenga na watu kama hao na bila shaka huwa anafahamu kwamba hawana hoja isipokuwa kupotosha na kutia uongo na kugeuza ukweli kwa gharama yoyote ile.

Hapana shaka kwamba wameajiri waandishi wengi na kuwamiminia mali nyingi, kama ambavyo wamewamiminia sifa kemkem na shahada za vyuo vikuu za uongo ili wawaandikie yale wayatakayo miongoni mwa vitabu na maqala zinazowashutumu Mashia na kuwakufurisha, na waitetee kwa juhudi zao zote heshima ya baadhi ya Masahaba waliogeuka kinyume nyume kwa visigino nyao hata kama sifa hiyo ni batili, na (Masahaba hao) ndiyo waliobadilisha haki kuwa batili baada

231

ya Mjumbe wa Mwenyezi Mungu." Vivyo hivyo walisema wale waliokuwa kabla yao mfano wa kauli yao hii, nyoyo zao zimefanana, bila shaka tumezibainisha hoja zetu zote kwa watu wenyekuyakinisha mambo". (Qur. 2:118)

232

HADITHI SAHIHI ZINAZO LAZIMISHA KUWAFUATA AHLUL-BAIT

1). Hadithi ya Vizito Viwili:

Mjumbe wa Mwenyezi Mungu amesema: "Enyi watu nimeacha kwenu vitu ambavyo mkivichukua kamwe hamtapotea, kitabu cha Mwenyezi Mungu na kizazi changu watu wa nyumba yangu". Na pia amesema: "Inakaribia kuwa atanijia Mjumbe wa Mola wangu nami nitaitika, na kwa hakika mimi ninaacha kwenu vizito viwili cha kwanza ni kitabu cha Mwenyezi Mungu, ndani yake muna uongofu na nuru, na watu wa nyumba yangu, nakukumbusheni Mwenyezi Mungu juu ya watu wa nyumba yangu, nakukumbusheni Mwenyezi Mungu juu ya watu wa nyumba yangu."

Taz: Sahih Muslim, Babu Fadhail Ali Juz. 5 uk. 122, Sahih Tirmidh.hiz. 5 uk. 328, Mustadrak Al-Hakim Juz. 3 uk. 148, Musnad Imam Ahmad Ibn Hambal Juz. 3

uk. 17.

Tukiangalia kwa makini ndani ya hadithi hii tukufu ambayo sihahi za Ahlus-Sunnah zimeiandika, tunakuta ni Mashia peke yao tu ndiyo waliovifuata vizito viwili "Kitabu cha Mwenyezi Mungu na kizazi kitukufu cha Mtume", ambapo Ahlus-Sunnah Wal-Jamaa wamefuata kauli ya Umar isemayo;

"Kinatutosha kitabu cha Mwenyezi Mungu".

233

Laiti wao wangekifuata kitabu cha Mwenyezi Mungu bila ya kukifasiri kufuatana na matamanio yao. Ikiwa Omar mwenyewe hafahamu maana ya "Alkalala" iliyomo ndani ya kitabu cha Mwenyezi Mungu wala hakuifahamu aya ya kutayammamu na hukumu nyinginezo, basi itakuwaje hali ya mtu aliyekuja baada yake na kamfuata bila ya kufanya ijtihadi kwa mujibu wa maoni yake kuhusu maandiko ya Qur'an? Na kwa namna hali ilivyo huenda watanijibu kwa kutumia hadithi iliyopokelewa kwao (Masunni) nayo ni ile isemayo "Nimekuachieni kitabu cha Mwenyezi Mngu na Sunna zangu."

Na hadithi hii kama itasihi, na ni sahihi kwa mujibu wa maana yake kwani maana ya kizazi kufuatia kauli yake Mtume ndani ya hadithi ya vizito viwili iliyotangulia ni kuwarejea Ahlul-Bait wangu ili wakufundisheni:

Kwanza: Sunna zangu au wakunukulieni hadithi sahihi kwani wao wametakasika kutokana na uongo na kwamba Mwenyezi Mungu amewahifadhi kwa aya ya utakaso.

Pili: Hi wawafasirieni maana zake na makusudio yake, kwani kitabu cha Mwenyezi Mungu peke yake (kama kilivyo) hakitoshelezi kuwapeni uongofu, ni mara ngapi baadhi ya vikundi vinatoa hoja kwa kutumia kitabu cha Mwenyezi Mungu hali ya kuwa vimo ndani ya upotovu, kama yalivyokuja maelezo ya mwenyewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu aliposema? "Ni mara ngapi msomaji wa Qur'an (husoma) Qur'an nayo ikawa inamlaani" basi kitabu cha Mwenyezi Mungu kimenyamaa kimya na kimebeba namna nyingi, na ndani yake kuna (aya) Muhkam na Mutashabih na hapana budi zifahamike kwa kuwarejea wale waliobobea katika elimu kama isemavyo Qur'an, na kuwarejea Ahlul-Bait kwa mujibu wa tafsiri ya Mtume.

Mashia wao katika kila kitu wanawarejea Maimamu Maasum wanaotokana na Ahlul-Bait wa Mtume, na wala

234

hawafanyi Ijtihadi isipokuwa katika jambo ambalo halina Nassi ndani yake.

Ama sisi tunarejea kwa Masahaba katika kila kitu sawa sawa katika tafsiri ya Qur'an au katika kuthibitisha Sunna na tafsiri yake, na hapo kabla tumekwishakufahamu hali za Masahaba na yale waliyoyatenda na waliyoyaeleza na kujitahidi ndani yake kwa mtazamo wao dhidi ya maandiko yaliyowazi, nayo ni mengi kwa mamia na haiwezekani kuwategemea watu mfano wao baada ya kupatikana mengi kutokana nao.

Na tutakapowauliza wanachuoni wetu, "Ni Sunna gani mnayoifuata"? Moja kwa moja watatujibu kuwa, "Ni Sunna ya Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.)".

Na ukweli wa historia haukubaliani na hilo, kwani ni wao hao hao waliopokea mapokezi yasemayo kwamba mwenyewe Mtume amesema, "Shikamaneni na Sunna zangu na Sunna za Makhalifa wangu viongozi baada yangu, zishikeni kwa magego". Kwahiyo Sunna wanayoifuata kwa kiwango kikubwa ni Sunna ya Makhalifa, na hata hiyo Sunna ya Mtume waisemayo ni ile iliyopokelewa kupitia watu hawa.

(Cha ajabu) ni kwamba sisi ndani ya vitabu vyetu tumeandika ya kuwa Mtume aliwazuwia (Masahaba) wasiandike Sunna zake ili zisije zikachanganyika na Qur'an, na ndiyo alivyofanya Abubakar na Umar wakati wa Ukhalifa wao, kwa hiyo baada ya maelezo haya haitabakia hoja yoyote ndani ya kauli yetu kwamba "Nimekuachieni Sunna zangu"[27]

235

Mifano michache nimeitaja ndani ya uchunguzi huu lakini hii inatosha kuirudi hadithi hii kwani miongoni mwa Sunna za Abubakar na Omar na Uthman zinaipinga Sunna ya Mtume na kuibatilisha kitu ambacho kiko wazi.

Iwapo tukio la kwanza lililo tokea baada tu ya kifo cha , Mjumbe wa Mwenyezi Mungu na likasajiliwa na Ahlus-Sunnah Wal-Jamaa pamoja na wanahistoria ni lile la Bibi Fatuma Zahra kumkasirikia Abubakar ambaye (Alizuwia mirathi ya Bibi Fatumah) kwa kutolea ushahidi wa hadithi isemayo " Sisi Mitume haturithiwi tunacho kiacha ni sadaka"

Bibi Fatumah (a. s.) aliipinga hadithi hii na akaibatilisha kwa mujibu wa kitabu cha Mwenyezi Mungu, akatoa hoja kwa kusema kuwa baba yake (yaani) Mtume (s.a.w.) hawezi kupingana na kitabu cha Mwenyezi Mungu ambacho kiliteremshwa kwake kwani Mwenyezi Mungu anasema:

"Mwenyezi Mungu anakuusieni juu ya watoto wenu, mwanaume apate sawa na sehemu ya wanawake wawili" (Qw. 4:11)

Na hii aya inawakusanya Manabii na wasiokuwa Manabii, pia akampa hoja ya kauli ya Mwenyezi Mungu isemayo:

"Na Suleiman akamrithi Daudi" (Qur. 27:16) Na wote hawa wawili ni Manabii.

Na pia kauli ya Mwenyezi Mungu isemayo:

"Basi nipe mrithi kutoka kwako, atakayenirithi na kuwarithi kizazi cha Yaqub na umfanye mwenye kukuridhisha ewe Mola wangu" (Qur. 19:5-6).

Na tukio la pili ni lile lililotokea kwa Abubakar katika zama za Ukhalifa wake, na likasajiliwa na wanahistoria miongoni mwa Masunni, pale Abubakar alipohitilafiana na mtu wa karibu yake ambaye ni Omar ibn Khatab. Tukio hilo ni lile

236

ambalo kwa muhtasari ni ule uamuzi wake wa kuwapiga vita wanaozuwia kutoa zaka na kuwauwa, kwani Omar alikuwa akimpinga na kumwambia, "Mimi nimesikia Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.) anasema, nimeamuriwa niwapige vita watu mpaka waseme Lailaha Illallah Muhammad Rasulullah basi, mwenye kusema hivyo mali yake na damu yake imehifadhika tokana nami na hesabu yake iko kwa Mwenyezi Mungu.

Hii ni Nassi aliyoiandika Muslim ndani ya Sahih yake ya kwamba, "Mjumbe wa Mwenyezi Mungu alimpa Ali bendera siku ya Khaibar kisha Ali akasema ni juu ya msingi wa jambo gani nikawapige vita? Mtume (s.a.w.) akasema wapige mpaka washuhudie ya kwamba hapana Mola apashwaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allah na kwamba Muhammad ni Mjumbe wa Mwenyezi Mungu wakifanya hivyo basi watakuwa wameizuwia damu yao na mali zao kutokana nawe isipokuwa kwa haki inayostahiki na hesabu yao ni juu ya Mwenyezi Mungu." Taz: Sahih Muslim Juz. 8 uk. 51 Kitabul-Iman.

Lakini Abubakar hakukinaishwa na hadithi hii yeye akasema: "Wallahi nitawapiga vita wanaotenganisha baina ya sala na zaka kwani zaka ni haki ya mali". Au alisema, "Wallahi lau watanizuwilia sadaka waliokuwa wakiitowa kwa Mjumbe wa Mwenyezi Mungu basi ningewapiga kwa kuizuia.

Omar ibn Khatab baadaye aliridhika na hali hiyo na akasema, "Nilimuona, Abubakar ameng'ang'ania jambo hilo mpaka nami Mwenyezi Mungu akakifungua kifua changu.

Mimi sielewi ni vipi Mwenyezi Mungu hufungua vifua vya watu kwa kuikhalifu Sunna ya Mtume wao!

Hii ni taawili itokanayo na wao wenyewe ili tu wajihalalishe kuwapiga vita Waislamu ambao Mwenyezi Mungu ameharamisha kuwauwa pale aliposema ndani ya kitabu chake

237

kitukufu: "Enyi mlioamini! mtakaposafiri katika njia ya Mwenyezi Mungu basi hakikisheni wala musimwambie anayekutoleeni salamu: Wewe si Muumini. Je, mnataka mafao ya dunia hii hali ya kuwa kwa Mwenyezi Mungu kuna mafao mengi zaidi. Hivyo ndivyo mlivyokuwa ninyi zamani na Mwenyezi Mungu, akakuneemesheni. Basi chunguzeni sawa sawa. Hakika Mwenyezi Mungu anazo habari za mnayoyatenda. (Qur. 4:94)

Watu hawa waliomkatalia kumpa zaka Abubakar zaka zao, hawakupinga msingi wa wajibu wa kutoa zaka, lakini walichelewa kufanya hivyo ili wachunguze mambo yalivyo Mashia wao wanasema, "Bila shaka watu hawa walishitushwa na Ukhalifa wa Abubakar kwani wako miongoni mwao ambao walikuwa pamoja na Mjumbe wa Mwenyezi Mungu katika Hija yake ya mwisho na wakasikia toka kwa Mtume lile tangazo la juu ya Ali ibn Abi Talib kuhusu Ukhalifa. Walifanya uzito wakingojea uhakika lakini Abubakar alitaka wanyamaze wanyamaze wasifuatilie ukweli. Na kwa kuwa mimi sitoi ushahidi wala hoja kwa maneno wasemayo Mashia basi naliacha jambo hili kwa yoyote anayeona umuhimu wake ili alifuatilie.

Kwa msingi huu sitaacha kutaja kisa cha Thaalaba, ya kwamba Mjumbe wa Mwenyezi Mungu katika zama za uhai wake kilimtokea kisa cha huyu Thaalaba ambaye alimuomba Mtume amuombee dua ya utajiri na akang'ang'ania mno kuombewa dua hiyo, na akamuahidi Mwenyezi Mungu kwamba atatoa sadaka, Mjumbe wa Mwenyezi Mungu akamuombea na Mwenyezi Mungu akamtajirisha kutokana na fadhila zake. Hatimaye mji wa Madina na viunga vyake ukawa ni mdogo kwake kwa wingi wa ngamia na mbuzi ikamlazimu awe mbali (na mji) na hakuweza kuhudhuria sala ya ljumaa. Na pindi Mtume alipowatuma watumishi wa idara ya zaka (yule Thaalaba) alikataa kuwapa chochote katika zaka akasema:- "Hii sasa ni kodi au mfano wa kodi" Lakini pamoja na hali hii

238

Mjumbe wa Mwenyezi Mungu hakumpiga vita bali ilishuka Qur'an juu ya mtu huyu ikasema: "Na miongoni mwao (hao wanafiki) wako waliomuahidi Mwenyezi Mungu kuwa akitupa katika fadhila zake tutatoa sadaka na tutakuwa miongoni mwa watendao mema, lakini alipowapa hizo fadhila walizifanyia ubakhili nawakageuka na hukuwaki puuza". (Qur. 9:75-76)

Thaalaba alikuja (kwa Mtume) baada ya kushuka aya hii, akamtaka Mjumbe wa Mwenyezi Mungu aikubali zaka yake (lakini) Mtume alikataa kama riwaya inavyoeleza.

Sasa ikiwa Abubakar na Umar wanafuata Sunna ya Mtume, upinzani huu ni wa nini na (mbona) wanahalalisha kumwaga damu ya Waislamu wasio na hatia (isipokuwa) kwa kuzuwia kutoa zaka. Ama wale wanaomtakia udhuru Abubakar (kwa tendo lake la kuwapiga vita waliozuwia zaka) na wale wanaotaka kulihalalisha kosa lake kwa kulipa tafsiri ya kwamba zaka ni haki ya mali, basi hawatabakia wao wala yeye na udhuru wowote baada ya kisa cha Thaalaba ambaye aliipinga zaka na kuona kuwa ni kodi (lakini Mtume hakumfanya kitu). Lakini nani ajuaye, kwani huenda Abubakar alimkinaisha sahibu wake Omar kwamba ni wajibu kuwauawa wanaozuwia kutoa zaka ili usienee wito wao katika nchi za Kiislamu kwani wito wao ungeweka hai lile tamko la Ghadir Khum ambalo lilimweka Ali kwenye kiti cha Ukhalifa.

Na kwa ajili hiyo Mwenyezi Mungu akakikunjua kifua cha Omar Ibn Khatab kama anavyodai mwenyewe ili akubaliane kuwa piga vita wanao zuwia zaka na yeye huyo Omar ndiye ambaye alionya kuwa angewaua wale wapinzani wa baia waliokuwa ndani ya nyumba ya Fatumah na kwamba angewachoma kwa moto yote hayo ni kwa ajili ya kutaka achukue toka kwao baia kwa ajili ya sahibu yake.

Rudi nyuma Yaliyomo endelea