Rudi nyuma Yaliyomo  

274

tunahuzunika katika Ashura na kufanya vikao vya maombolezo, yote haya ni kwa msaada wa Mwenyezi Mungu.

Barua yangu ya mwanzo ambayo inabeba khabari za kuuona kwangu ukweli, niliiandika kwa Sayyid Al-Khui na Sayyid Muhammad Baqir As-Sadr na ilikuwa katika munasaba wa Idi ya Ghadir kwani kwa mara ya kwanza tuliisherehekea katika mji wa Qafsah.

Mambo yangu yakatangaa kwa watu maalum na wengine wote ya kwamba mimi nimekuwa Shia na kwamba mimi nalingania watu kwenye Ushia yaani kuwafuata watu wa nyumba ya Mtume (s.a.w.). Na hapo zikaanza tuhuma mbali mbali na uvumi ukavuma nchini ya kwamba mimi ni jasusi la Israel ninafanya kazi ya kuwatia mashaka watu katika dini yao, na kwamba mimi na watukana Masahaba, pia mimi ni mtu wa fitna na mengineyo. Katika mji mkuu wa Tunis, niliwasiliana na marafiki wawili, Rashid Al-Ghannushi na Abdul-Fattah Moro, upinzani wao dhidi yangu ulikuwa mbaya mno, na katika mazungumzo yaliyofanyika baina yetu ndani ya nyumba ya Abdul-Fattah, mimi nilisema, "Ni wajibu wetu kama Waislamu kuvirejea vitabu vyetu na historia yetu", na nilitoa mfano wa Sahih Bukhari ambayo ndani yake mna mambo ambayo akili haiyakubali wala dini haikubaliani nayo.

Walifura kwa hasira zao na wakaniambia: "Wewe ni nani hata umkosoe Bukhari"? Mimi nilitoa juhudi zangu zote niwatosheleze ili tupate kuingia ndani ya utafiti wa maudhui za kielimu. Wote wawili walilikataa jambo hilo wakasema: "Ikiwa wewe umekuwa Shia usitufanye sisi kuwa Mashia! sisi tuna jambo muhimu mno kuliko hilo la Ushia, nalo ni kuipinga serikali ambayo haihukumu kwa mujibu wa sheria za Kiislamu." Nilisema ni faida gani mtapata mtakapofika kwenye ngazi ya uongozi wa serikali, mtafanya vibaya zaidi ya waliopo leo hii maadamu hamjui hakika ya Uislamu. Mawasiliano yetu yaliishia hapo.

275

Hali hii ilifuatiwa na uvumi mwingi dhidi yetu kutoka kwa baadhi ya watu na wakaeneza uvumi wa ajabu kwa watu wa kawaida kwa lengo la kuwaweka mbali na mimi na pia kunisingizia kwa namna zote ili watu wanitenge - Mwenyezi Mungu mtukufu awasamehe.

Hatimaye tulianza kutengwa na baadhi ya vijana na Masheikh ambao niwafuasi wa Tariqa za kisufi, na tuliishi ndani ya kipindi kigumu tukajiona kama wageni miongoni mwa ndugu zetu najamaa zetu ndani ya nchi yetu. Lakini Mwenyezi Mungu Mtukufu alitubadilishia watu bora kuliko wao, kwani baadhi ya vijana walikuwa wakija kutoka miji mingine wakiutafuta ukweli, nami nilikuwa nikitoa upeo wa nafasi niliyonayo kuwatosheleza juu ya ukweli wa njia ya Ahlul-Bait (a.s/) na pia uhakika wa kihistoria. Basi vijana wengi waliiona haki kutoka mji mkuu wa Tunis, na pia miji ya Qairawan, Susah ria Sayidi Buzaid. Nilipokuwa katika safari yangu ya kwenda Iraqi wakati wa kipupwe nilipitia Ulaya na nikakutana na baadhi ya marafiki zangu huko Ufaransa na Holland na nilizungumza nao juu ya maudhui hii ya Ukhalifa, namshukuru Mwenyezi Mungu kwamba nao waliona haki na kufuata.

Hakika furaha yangu ilikuwa ni ya hali ya juu mno pindi nilipokutana na Sayyid Muhammad Baqir As-Sadri katika mji mtukufu wa Najaf nyumbani mwake na palikuwa na kikundi cha wanachuoni na ndipo Sayyid alipoanza kunitambulisha kwao ya kwamba mimi ni mbegu ya wafuasi wa Ahlul-Bait wa Mtume (s.a.w.) katika nchi ya Tunisia, kama ambavyo aliwatambulisha pia kwamba yeye alilia kwa furaha pindi ilipomfikia barua yangu iliyobeba bishara ya kufanyika kwa mahfali yetu kwa mara ya kwanza kuadhimisha sikukuu ya Ghadir njema. Nilimfahamisha pia juu ya mambo yanayotusibu ikiwemo upinzani na uzushi dhidi yetu na kutengwa. Sayyid alisema katika utangulizi wa maneno yake "Ni lazima mstahamili mashaka kwa sababu njia ya Ahlul-Bait ni ngumu na ina

276

matatizo, kuna mtu alikuja kwa Mtume (s.a.w.) akamwambia, "Hakika mimi nakupenda ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu"! Mtume akamwambia yule mtu "Basi jibashirie balaa nyingi" Akasema (tena .yule mtu) "Pia nampenda Ibn Ami yako Ali" Mtume akasema "Jibashirie kuwa na maadui wengi" yule mtu akasema "Na ninawapenda Hasan na Husein" Mtume akamwambia jiandae kwa umaskini na balaa nyingi". Sasa je sisi tumetanguliza nini katika (kutetea) njia ya haki ambayo Abu Abdillah Husein (a.s.) alijitolea nafsi yake, watu wake, watoto wake na wafuasi wake kwa thamani ya njia hiyo. Kama ambavyo kipindi chote cha historia Mashia wamejitolea kwa thamani ya kuwatawalisha kwao watu wa nyumba ya Mtume (s.a.w.), ni lazima ewe ndugu yangu kustahmili baadhi ya taabu na kujitolea katika njia ya haki, kwani Mwenyezi Mungu akimuongoa mtu mmoja kupitia kwako ni bora kwako kuliko dunia na vilivyomo."

Vile vile Sayyid Sadri alinipa nasaha nisijitenge, bali aliniamuru nijikurubishe zaidi kwa ndugu zangu Ahlus-Sunnah Wal-Jamaa kila wanapojaribu kunitenga, kadhalika aliniamuru nisali nyuma yao ili mawasiliano yasikatike, na niwaone kuwa wao hawahusiki na lolote katika mambo yaliyotokea, kwani wao ni wahanga wa habari za propaganda za uzushi na historia iliyopotoshwa, na kwamba watu ni maadui wa kitu wasichokijua.

Kwa hakika Sayyid Al-Khui naye alinipa nasaha kama hiyo hiyo kama ambavyo Sayyid Muhammad Ali Tabatabai Al-Hakim naye siku zote alikuwa akitumia nasaha zake ndani ya barua zake nyingi ambazo zilikuwa na athari kubwa ndani ya mwenendo wa ndugu ambao tayari walikwishauona uongofu.

Kwa hiyo basi ziyara zangu kuutembelea mji mtukufu wa Najaf na wanachuoni wa Najaf katika minasaba mingi ziliongezeka, kisha niliapa kuwa kila mwaka nitaitumia likizo yangu ya kipindi cha kipupwe ndani ya uwanja wa Haram ya

277

Imam Ali ili nipate kuhudhuria mafunzo ya Sayyid Muhammad Baqir As-Sadri, mafunzo ambayo nilifaidika nayo sana na yalininufaisha mno, vile vile niliapa kuyazuru maeneo (ya kumbukumbu) za Maimamu kumi na wawili.

Kwa hakika Mwenyezi Mungu aliyatimiza makusudio yangu kwa kuniwafikisha hata kumzuru Imam Ridha ambaye kaburi lake liko Mash-had ambao ni mji ulioko karibu na mpaka wa Urusi huko Iran, na huko nilijitambulisha kwa wanachuoni mashuhuri na nilifaidika nao sana.

Pia Sayyid Al-Khui ambaye sisi tulikuwa tukifuata fatwa zake alinipa ruhusa ya kuwa muwakilishi wake katika matumizi ya Khumsi na Zaka na kuwapa wale walioiona haki huku kwetu kile wanachokihitajia miongoni mwa vitabu na misaada na mengineyo.

Nilitengeneza maktaba inayojitosheleza kwa rejea muhimu ambazo zinahusika katika uchunguzi, na ilikuwa imekusanya vitabu vya pande zote mbili na ilikuwa inaitwa "Maktabatu Ahlil-Bayt (a. s.)" na kwa hakika inanufaisha wengi.

Mwenyezi Mungu aliiongezea furaha yetu kuwa furaha mbili na mafanikio yetu kuwa mafanikio ya namna mbili, kwani kabla ya miaka kumi na tano, Mwenyezi Mungu aliturahisishia mambo kwa kumfanya Meya wa mji wa Qafsah aafiki kuupa jina la Imam Ali ibn Abi Talib (a.s.) mtaa niliokuwa nikikaa. Sitaacha kumshukuru kwa uoni huu mtukufu, kwani yeye ni miongoni mwa Waislamu wenye juhudi na anayo mapenzi makubwa kwa Imam Ali, na kwa hakika nilimzawadia kitabu cha Muraja'ati naye anawasiliana nasi kwa mapenzi na heshima kubwa, Mwenyezi Mungu amlipe wema na ampe yale anayoyakusudia.

Wako baadhi ya watu wenye chuki ambao walijaribu kuuondoa ule ubao unaooneshajina la mtaa wetu lakini njama

278

zao hazikufaulu, kwani Mwenyezi Mungu alikwisha taka kuudumisha. Hatimaye barua nyingi zikawa zinatufikia kutoka kila pembe ya ulimwengu na juu yake liko jina la "Mtaa wa Imam Ali ibn Abi Talib (a.s.)" ambaye jina laketukufu liliubarikia mji wetu mzuri.

Kwa kutumia nasaha za Maimamu wa Ahlul-Bait na vile vile nasaha za wanachuoni wa Najaf tukufa, tulikusudia hasa kujikurubisha kwa ndugu zetu wa madh-hebu mengineyo na tukaulazimu umoja na tukawa tunasali kwa pamoja, na kwa sababu hii basi chuki ilipungua na tukaweza kuwakinaisha baadhi ya vijana kupitia masuali yao kwetu jinsi tunavyosali, tunavyotawadha na itikadi yetu.

279

UONGOFU WA HAKI

Katika moja ya miji iliyoko kusini mwa Tunisia, kulikuwa na hafla ya harusi, hivyo wanawake fulani walikuwa wakizungumza juu ya mwanamke mmoja ambaye ni mke wa mwanaume fulani. Bibi Kizee mmoja aliyekuwa kakaa katikati yao akisikiliza mazungumzo yao, alishangazwa kuwa mwanamke yule ni mke wa Bwana yule, walipomuuliza sababu ya kushangazwa kwake, alisema kwamba yeye amewanyonyesha mume yule na mke yule kwa hiyo wao ni ndugu wa kunyonya.

Wanawake hawa walizichukua habari hizi za kutisha hadi kwa waume zao na wakazifanyia kazi, matokeo yake mzazi wa yule mwanamke alikiri kuwa Binti yake alinyonyeshwa na Bibi kizee yule ambaye ni maarufu kwa wote kuwa ni mnyonyeshaji, kama ambavyo mzazi wa yule mwanaume naye alikiri kwamba mwanawe alinyonyeshwa na Bibi yule yule.

Basi hapo palizuka kutokuelewana.baina ya familia hizi mbili, wakapigana kwa fimbo, kila mmoja wao akiutuhumu upande mwingine kuwa umesababisha msiba ambao huenda utawaingiza ndani ya ghadhabu na adhabu ya Mwenyezi Mungu, na khasa kwa kuwa ndoa hii imeshafikisha miaka kumi na huyu mwanamke amekwisha zaa watoto watatu. Aliposikia habari hizi alirudi nyumbani kwa baba yake na alisusa kula na kunywa na akataka kujinyonga kwa sababu hakuweza kuvumilia pigo

280

hili na ni jinsi gani yeye aliolewa na nduguye hali ya kuwa hajuwi. Kuna idadi kadhaa ya watu walijeruhiwa kati ya koo mbili hizi, na mmoja kati ya wazee wakubwa aliingilia kati akasimamisha vita hii na akawanasihi waende kwa wanachuoni ili kuomba fatwa ya jambo hili huenda wakapata ufumbuzi.

Basi wakawa wanazunguka katika miji mikubwa yajirani wakiwauliza wanachuoni wa miji hiyo juu ya ufumbuzi wa tatizo hili, na kila walipowasiliana na mwanachuoni fulani na kumueleza jambo hili, aliwaambia kuwa ndoa hiyo ni haramu na ni lazima Bibi na Bwana watenganishwe moja kwa moja na pia waachie huru mtumwa au kufunga miezi miwili, na Fat-wa nyinginezo.

Walifika pia Qafsah na wakawauliza wanachuoni wa hapo lakini jawabu likawa ni lile lile kwani, wafuasi wa madh-hebu ya Malik wote wanaharamisha kunyonyeshwa japo tone moja wakifuata maoni ya Malik ambaye aliyafanyia kiasi maziwa kwa pombe kwani kinacholewesha ni haramu ikiwa ni kingi au kidogo basi kunyonyesha kunaharamisha japo kwa tone moja la maziwa.

Kilichotokea hapo Qafsa ni kwamba mmoja wa watu waliohudhuria kikao cha fatwa hiyo aliwachukua pembeni akawaonesha nyumba yangu huku akiwaambia, "Muulize Tijani Qadhia kama hizi kwani yeye anayafahamu madh-hebu yote nimekwishamuona anajadiliana na wanachuoni hawa mara nyingi na anawashinda kwa hoja madhubuti."

Hivi ndivyo alivyonieleza mume wa mwanamke yule neno kwa neno pindi nilipomuingiza ndani ya maktaba yangu, na akanisimulia tukio lote kwa urefu mwanzo hadi mwisho, na akasema, "Ewe Bwana wangu! hakika mke wangu anataka kujinyonga na wanangu wametelekezwa nasi hatujui ufumbuzi wa tatizo hili, na wametuelekeza tuje kwako, na kwa hakika nimebashiria kuwa itakuwa kheri pindi nilipo onaunavitabu hivi

281

vingi ambavyo sija pata kuviona- maishani mwangu mfano wake, basi huenda kwako kutakuwa na ufumbuzi".

Nilimletea kahawa kisha nikatafakari kidogo halafu nikamuuliza, kuhusu ni mara ngapi alinyonya kwa huyo mama, akasema, "Sifahamu, lakini mke wangu alinyonya mara mbili au mara tatu kwa huyo mwanamke na Baba yake mke wangu alishuhudia kwamba alimchukua bintiye mara mbili tu au mara tatu kumpeleka kwa Bibi huyo mwenye kunyonyesha" mimi nikamwambia, "Ikiwa hivi usemavyo ni sahihi hapana kitu juu yenu na ndoa yenu ni sahihi na ni halali".

Bwana yule masikini alijitosa kwangu akawa anakibusu kichwa changu na mikono yangu huku akisema, "Mwenyezi Mungu akupe kheri kwa hakika umefungua mlango wa utulivu mbele yangu" hapo hapo akanyanyuka kwa haraka na wala hakuimaliza kahawa yake wala hakutaka nimfafanulie na wala hakutaka dalili isipokuwa aliniomba ruhusa atoke ili akamfahamishe mkewe, wanawe watu wake na jamaa zake

Katika siku iliyofuata alirudi akiwa na watu saba na akawatambulisha kwangu huku akisema, "Huyu ni mzazi wangu, na huyu ni mzazi wa mke wangu, na huyu wa tatu ni chifu wa kijiji, wanne ni Imam wa Sala ya ljumaa na jamaa na huyu wa tano ni kiongozi wa Dini wa sita ni Mzee wa Jumuiya, na huyu wa saba ni Mkuu wa shule, na tumekuja ili utufafanulie kuhusu tatizo lile la kunyonya na ni vipi umehalalisha?

Wote niliwaingiza maktaba na nikawa nayasubiri majadiliano yao, nikawaletea kahawa kisha nikawakaribisha. Wakasema, "Sisi tumekujia ili tukujadili kuhusu kuhalalisha kwako Qadhiya ya kunyonya wakati Mwenyezi Mungu ameiharamisha ndani ya Qur'an, naye Mjumbe wa Mwenyezi Mungu ameiharamisha kwa kauli yake aliposema, "Inakuwa haramu kwa kunyonya kama ambayo inakuwa haramu kwa sababu ya nasaba". Kadhalika Imam Malik ameharamisha.

282

Mimi nilisema, "Enyi mabwana zangu, ninyi mashaallah ni watu wanane na mimi ni mtu mmoja, iwapo nitazungumza basi huenda nisikukinaisheni na majadiliano yetu yatapotea hewani, ila mimi napendekeza kwenu mumchague mmoja wenu ili nijadiliane naye nanyi mutakuwa mahakimu baina yangu na yeye!

Fikra hii iliwafurahisha na wakaiona nzuri, na mambo yao wakamkabidhi yule kiongozi wa Dini hali ya kuwa wanasema kwamba, "Yeye ni mjuzi mno kuliko wao na ni mwenye uwezo." Yule bwana alianza kwa kuniuliza ni vipi ninahalalisha jambo aliloliharamisha Mwenyezi Mungu na Mtume wake na Maimamu.

Nikasema, "Najilinda kwa Mwenyezi Mungu kutokana na kufanya hivyo! lakini Mwenyezi Mungu ameharamisha kwa aya ambayo ni "Mujmal" na hakubainisha ufafanuzi wa jambo hilo, bali ufafanuzi wake umewakilishwa kwa Mtume wake ambaye ameweka wazi makusudio ya aya, (kwamba) ni unyonyeshaji upi na mara ngapi".

Akasema, "Imam Malik ameharamisha kunyonya japokuwa tone moja."

Mimi nikasema "Hilo nalijua", lakini Imam Malik yeye siyo hoja juu ya Waislamu, isipokuwa unasemaje juu ya Maimamu wengine?

Alijibu akasema: "Mwenyezi Mungu awawie radhi, kwani wote wanataraji kutoka kwa Mtume (s.a.w.)." Nikasema "Kwa hiyo nini hoja yako mbele ya Mwenyezi Mungu kutokana na wewe kumfuata Imam Malik ambaye maoni yake yanakwenda kinyume na maagizo ya Mtume (s.a.w.)?"

Akasema, hali ya kuwa amechanganyikiwa, "Subhanallah, mimi sijui kwamba Imam Malik ambaye ni Imam wa Darul-Hijra, anakhalifu maagizo ya Mtume." Wote waliokuwepo hapo

283

walichanganyikiwa kutokana na kauli hii, na walinishangaa kwa ujasiri huu dhidi ya Imam Malik kitu ambacho hapo kabla hawakupata kukifahamu kwa mtu asiyekuwa mimi pale pale niliwahi nikasema, "Hivi Imam Malik alikuwa miongoni mwa Masahaba"? Akasema: "Hapana" nikasema "Je, alikuwa katika Tabiina"? akasema "Hapana bali alikuwa miongoni mwa waliowafuatia Tabiina."

Nikasema, "Basi ni yupi aliyekaribu zaidi na Mtume ni yeye au Imam Ali ibn Abi Talib?"

Akasema, "Imam Ali yuko karibu zaidi kwani yeye ni miongoni mwa Khulafaur-Rashidina."

Mmoja wa watu waliokuwa wamehudhuria hapo akasema, "Sayyidna Ali Karramallahu Waj-Hahu yeye ndiye mlango wa mji wa elimu"

Basi mimi nikasema, "Ni kwa nini basi mmeuacha mlango wa mji wa elimu na mmemfuata mtu ambaye hayuko miongoni mwa Masahaba wala Tabiina, bali amezaliwa baada ya fitna na baada ya mji wa Mjumbe wa Mwenyezi Mungu kukaliwa na jeshi la Yazid na wakafanya mjini humo waliyoyafanya, wakawauwa Masahaba wema, na wakavunja heshima ya mambo matakatifu, wakaibadilisha Sunna ya Mtume kwa bidaa walizozua basi ni vipi baada ya yote haya mtu atakuwa na utulivu wa moyo kwa Maimamu hawa ambao waliridhia utawala waliokuwa wakitawala kwa sababu tu ya wao kutoa Fat-wa zinazoafikiana na matamanio ya watawala hao?

Mmoja wao akazungumza akasema, "Sisi tumesikia kwamba wewe ni Shia na unamuabudu Imam Ali." basi mwenzake aliyekuwa pembeni yake akampiga kwa ngumi iliyomuumiza na akamwambia, "Nyamaza, huoni aibu kusema maneno kama haya kwa mtu mheshimiwa kama huyu, kwa hakika mimi nimewafahamu wanachuoni siku nyingi lakini

284

mpaka sasa jicho langu halijawahi kuona maktaba mfano wa maktaba hii, na huyu mtu anazungumza kwa kutumia maarifa na ukweli kwa yale ayasemayo"!

Mimi nilimjibu kwa kusema "Mimi ni Shia na hii ni sawa, lakini Mashia'hawamuabudu Imam Ali bali badala ya kumfuata Imam Malik wao wanamfuata Imam Ali kwa kuwa yeye ni mlango wa mji wa elimu kwa mujibu wa ushahidi wenu mlioutoa sasa hivi.

Yule kiongozi wa Dini akasema, "Watu walionyonya ziwa moja Imamu Ali amehalalisha waowane?"

Nikasema: "Hapana, lakini yeye anaharamisha ikiwa kunyonya kutakapofikia mara kumi na tano mfululizo tena kunyonya kunakoshibisha au kama kutakuza nyama na mfupa."

Uso wa yule mzazi wa mke ukachanua (kwa furaha) na akasema, "Namshukuru Mwenyezi Mungu, basi Binti yangu hakunyonya isipokuwa mara mbili au tatu tu, na bila shaka ndani ya kauli hii ya Imam Ali ndimo ilimo salama yetu kutokana na maangamivu haya, na hii ni huruma ya Mwenyezi Mungu kwetu baada ya kuwa tulikata tamaa".

Yule kiongozi wa Dini akasema, "Tupe dalili juu ya kauli hii ili tutosheke".

Nikawapa kitabu cha Min-Hajus-Salihina cha Sayyid Alkhui, na akawasomea yeye mwenyewe mlango wa kunyonyesha, wakafurahia mno khasa mume ambaye alikuwa akikhofu kwamba (huenda) nisiwe na ushahidi unaotosheleza. Kisha wakanitaka niwaazime kitabu hicho ili wapate kutolea hoja kijijini kwao, nikawapa na wakatoka hali ya kuwa wakiniaga na kuniombea huku wakitaka radhi.

Kiasi tu cha wao kutoka, walikutana na mmoj a wa maadui (zetu) akawachukua hadi kwa baadhi ya wanachuoni waovu,

285

wakawatisha na kuwahadharisha kwamba mimi ni kibaraka wa Israel na kwamba kitabu cha Minhajus-Salihina ambacho niliwapa chote ni upotofu mtupu, na kwamba watu wa Iraqi ni watu wa kufru na unafiki, na kuwa Mashia ni majusi (wanaoabudu moto) wanahalalisha kuoa madada kwa hiyo siyo ajabu kwa mimi kuhalalisha ndoa ya dada wa kunyonya, na mengineyo miongoni mwa tuhuma na fitna, basi aliwashika akiwahadharisha mpaka wakabadili msimamo baada ya kuwa walikinaika na maelezo yangu, wakamlazimisha mume yule apeleke madai ya talaka kwenye Mahakama ya mwanzo mjini Qafsah, na huyo rais wa Mahakama hiyo aliwataka waende mji mkuu wa Tunis na wawasiliane na Mufti wa Jamhuri ili aweze kutoa ufumbuzi wa tatizo hili.

Bwana yule alikwenda na akabakia huko kwa muda wa mwezi mmoja kamili mpaka ikawezekana kumuona Mufti na akamsimulia kisa chake mwanzo mpaka mwisho.

Yule Mufti alimuuliza kuhusu wanachuoni waliomwambia kuwa ndoa ile ni halali na sahihi. Yule Bwana alijibu kwamba, "Hakuna aliyesema kuwa ndoa hiyo ni halali isipokuwa mtu mmoja tu naye Tijani Samawi."

Mufti aliliandika jina langu kisha akamwambia yule Bwana, "Wewe rudi, nami nitatuma barua kwa rais wa Mahakama ya Qafsah, na kweli barua ilikuja toka kwa Mufti wa Jamhuri na wakili wa mume akaisoma na kumjulisha mume huyu kuwa "Mufti wa Jamhuri ameiharamisha ndoa hii".

Hivi ndivyo alivyonisimulia mume wa mke yule ambaye unyonge na kuchanganyikiwa vilionekana (wazi) juu yake kutokana na taabu nyingi, hali ya kuwa akiomba msamaha kwa kero na usumbufu alionisababishia. Mimi nilimshukuru kwa wema wake huku nikistaajabu ni vipi Mufti wa Jamhuri anaibatilisha ndoa sahihi katika Qadhiya kama hii.

286

Nilimtaka aniletee barua yake aliyoipeleka Mahakamani ili niitangaze ndani ya magazeti ya Tunisia na nibainishe kwamba Mufti wa Jamhuri hayafahamu madhehebu ya Kiislamu na wala hajui tofauti zake za Kifiqhi kuhusu mas-ala ya kunyonyesha.

Yule mume akasema kuwa, hawezi kuyaona mafaili ya Qadhiya yake licha ya kuniletea barua toka kwake, basi hapo tukaachana.

Baada ya siku kadhaa ulinijia mwito toka kwa rais wa Mahakama akiniamuru nilete kitabu na dalili juu ya kutokubatilika ndoa baina ya watu wawili walionyonya ziwa moja. Mimi nilikwenda hali ya kuwa nimebeba rejea kadhaa nilizokuwa nimezichagua toka hapo mwanzo, na ndani ya kila kitabu niliweka kipande cha karatasi katika mlango wa kunyonyesha ili iwe rahisi kuufungua ukurasa huo mara moja.

Nilikwenda katika siku na saa iliyotajwa, na Katibu wa Mahakama akanipokea na kuniingiza ndani ya ofisi ya rais wa Mahakama, nikawakuta humo rais wa Mahakama ya mwanzo, rais wa Mahakama ya kanda na wakili wa Jamhuri na wajumbe watatu wote wamevalia mavazi maalum ya kutolea hukumu kana kwamba wako ndani ya kikao rasmi. Vile vile nilimuona mume wa mke amekaa mkabala wao mwishoni mwa ukumbi, nikawasalimia wote na wote walikuwa wakiniangalia kwa chuki na dharau.

Nilipoketi, yule rais alinisemesha kwa lugha kavu akasema, "Wewe ndiyo Tijani Samawi?" nikasema "Ndiyo" Akasema, "Wewe ndiye uliyetoa fatwa kwamba ndoa iliyoko katika shauri hili ni sahihi?"

Nikasema, "Hapana, mimi siyo mufti, lakini Maimamu na wanachuoni wa Kiislamu ndiyo waliotoa fatwa ya uhalali na kusihi kwake."

287

Akasema, "Kwa ajili hiyo ndiyo tumekuita, na wewe sasa umo ndani ya mzingo wa tuhuma, iwapo hutathibitisha madai yako kwa kutumia dalili basi tutakuhukumu kifungo na hutatoka hapa isipokuwa ni gerezani moja kwa moja." Na hapo kweli nilitambua kwamba nimo ndani ya mzingo wa tuhuma, siyo kwa kuwa mimi nimetoa fat-wa katika shauri hili, lakini ni kwa kuwa baadhi ya wanachuoni waovu wamewaambia Mahakimu hawa kuwa mimi ni mtu wa fitna, na kwamba mimi ninawatukana Masahaba na ninaeneza Ushia kuwafuata Ahlu-lbait wa Mtume, na huyu rais wa Mahakama alikwisha mwambia kwamba iwapo utaniletea mashahidi wawili basi nitamtupa gerezani".

Zaidi ya hapo ni kwamba, jamaa miongoni mwa ndugu Waislamu waliipotosha fatwa hiyo na kuifanya isieleweke kwa watu makhsusi na watu wa kawaida na badala yake ikaeleweka kwamba, mimi nahalalisha kuoa madada na hiyo (eti) ndiyo kauli ya Mashia - kwa mujibu wa madai yao.

Yote hayo niliyafahamu kabla na niliyakinisha wakati rais wa mahakama alipokuwa akinionya kuwa atanitia gerezani, basi hapana kilichokuwa kimebakia mbele yangu isipokuwa ni kuwapa changamoto na kujitetea nafsi yangu kwa ushujaa wote, ndipo nilipomwambia yule rais: "Je, naweza kuzungumza wazi wazi bila ya khofu?"

Akasema, "Ndiyo, wewe huna wa kukutetea, "Mimi nikasema "Kabla ya yote, mimi sijajipa cheo cha umufti, lakini huyu hapa mbele yenu mume wa huyo mke muulizeni, ni yeye ndiye alinijia nyumbani kwangu akagonga mlango wangu na akaniuliza, basi ulikuwa ni wajibu wangu kumjibu kwa kile ninachokifahamu na nilimuuliza kuhusu idadi ya kunyonya (kulikonyonywa), na aliponijulisha ya kwamba mkewe hakunyonya isipokuwa mara mbili basi pale pale nilimpa hukumu ya Kiislamu kuhusu shauri hilo, mimi siyo miongoni mwa

288

wanajitahadi wala wanaoweka sheria.

Yule rais akasema, "Ni ajabu, sasa hivi wewe unadai kwamba unaujuwa Uislamu na sisi eti hatuujui"!

Mimi nikasema, "Mwenyezi Mungu anisamehe, mimi sikukusudia hivyo, lakini watu wote hapa wanayafahamu madh-hebu ya Imam Malik na wametosheka naye, na mimi (kwa upande wangu) nimeyafanyia utafiti kila madh-hebu na nikaupata ufumbuzi wa shauri hili".

Rais akasema, "Ni wapi ulipoupata ufumbuzi?" Nikasema, "Kabla ya kufanya jambo lolote je naweza kuuliza swali moja ewe Bwana rais?"

Akasema, "Uliza ukitakacho". Nikasema, "Nini kauli yenu kuhusu madh-hebu (mengine) ya Kiislamu"?

Akasema, "Yote ni sahihi, kwani wote wanataraji kutoka kwa Mtume, na ndani ya khitilafu zao kuna rehma."

Mimi nikasema, "Kama ni hivyo, basi muhurumieni huyu masikini, hali ya kuwa ninamuashiria yule mume wa mwanamke yule, ambaye sasa hivi amemaliza muda wa zaidi ya miezi miwili hali ya kuwa kajitenga na mkewe na wanawe, wakati ambapo kuna wanachuoni wa madh-hebu ya Kiislamu ambao wamekwisha litatua tatizo lake".

Akasema hali ya kuwa na ghadhabu, "Lete dalili ya kutosha usifanye mchezo, sisi tumekupa nafasi ujitetee nafsi yako na sasa umekuwa mtetezi wa mtu mwingine".

Nikamtolea kitabu cha Minhajus-Salihina cha Sayyid Khui kutoka mkobani mwangu na nikasema, "Haya ni madh-hebu ya Ahlul-Bait na ndani yake imo dalili".

Basi alinikatisha kwa kusema, "Achana na madh-hebu ya Ahlu-Bait, sisi hatuya Jui na wala hatuyaamini".

289

Toka mwanzo nilikuwa nikingojea kutokea kitu kama hiki, kwa hiyo baada ya utafiti na uchunguzi siku hiyo nilikuwa nimeleta rejea nyingi za Kisunni ambazo nilizipanga vema, kwa namna nijuavyo niliiweka sahih Bukhari katika daraja la kwanza, kisha sahih Muslim, na baada yake nikaweka kitabu cha fatwa chaMahmud Shaltut, kitabu cha Bidayatul-Muj-Tahidi kitabu kiitwacho Nihatul-Muqtasid. cha Ibn Rushd, kitabu kiitwacho Zaadul-Masir fi Ilmit-Tafsir cha Ibn Al-Jauzi na rejea nyinginezo miongoni mwa vitabu vya Kisunni.

Hivyo basi, wakati rais alipokataa kuangalia ndani ya kitabu cha Sayyid Alkhui nilimuuliza ni kitabu gani ambacho yeye anakiamini, alisema, "Bukhari na Muslim."

Nikatoa Sahih Bukhari na nikaufungua ule ukurasa unaohusika kisha nikasema, "Tafadhali ewe Bwana hebu soma," Akasema, "Somawewe"?

Mimi nikasoma, "Ametusimulia fulani naye kutoka kwa fulani, toka kwa (mama) Aisha Mama wa Waumini, amesema, Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.) alifishwa na wala hakuharamisha kutokana na kunyonya isipokuwa mara tano na kuendelea".

Basi yule rais akakichukua kitabu toka kwangu, na akasoma yeye binafsi kisha akampa Wakili wa Jamhuri aliyekuwa pembeni mwake, naye akasoma na akampa anayefuatia, wakati ambapo mimi nilitoa Sahih Muslim na nikamuonesha hadithi zile zile kisha nilifungua kitabu cha fatwa cha Sheikh Shal-tut wa Az-Har, naye hapana shaka kabisa, ameeleza ikhitilafu za Maimamu kuhusu mas-ala ya kunyonyesha, kwani wako ambao wamesema kuwa, kunyonyesha kunakoharamisha ni kule kunakofikia mara kumi na tano na wengi wamesema mara saba, na miongoni mwao wameharamisha kama ni zaidi ya mara tano, isipokuwa Malik ambaye ameikhalifu Nassi (maandiko) na akaharamisha japo

290

kwa tone moja.

Kisha Shaltut amesema, "Mimi ninaungana na maoni ya kati kwa kati ninasema mara saba na zaidi."

Baada ya rais wa Mahakama kuona yote hayo akasema, "Inatosha." Kisha akamgeukia yule mume wa mke na kumwambia, "Nenda kaniitie baba wa mkeo ili aje ashuhudie mbele yangu kwamba mkeo alinyonyeshwa mara mbili au tatu na ikithibiti hivyo utamchukua mkeo leo hii."

Masikini yule aliruka kwa furaha, ndipo Wakili wa Jamhuri alipoomba ruhusa yeye na wajumbe waliohudhuria ili wakaendelee na kazi zao, naye rais akawaruhusu.

Pindi kikao kilipokuwa kimebakia kwetu tu, rais alinigeukia hali ya kunitaka radhi akasema: "Nisamehe ewe Ustadh, hakika watu wamenipotosha kuhusiana nawe, wamesema mengi ya ajabu juu yako, nami hivi sasa nimefahamu kwamba wao ni mahasidi na wana malengo maovu dhidi yako, wanakutakia wewe shari."

Moyo wangu ulifurahia mno mabadiliko haya ya haraka na nikasema "Kila sifa njema anastahiki Mwenyezi Mungu ambaye amejaalia nusra yangu kupitia mikononi mwako ewe Bwana wangu rais."

Yeye akasema, "Nimesikia kwamba wewe unayo maktaba kubwa, je katika maktaba hiyo kimo kitabu kiitwacho "Hayatul-Hayawani lkubra" cha Ad-Dumair?

Nikasema, "Ndiyo" akasema, "Je, unaweza kuniazima kitabu hicho kwani imepita miaka miwili ninakitafuta" Nikasema "Umekipata ewe bwana wangu wakati wowote ukitaka."

Akasema, "Je, unao wakati unaokuruhusu uje kwenye maktaba yangu ili tuzungumze na niweze kufaidika kutoka

291

kwako?" Nikasema, "Mwenyezi Mungu anisamehe, mimi ndiyo nifaidike kutokana nawe kwani wewe ni mkubwa kuliko mimi kwa umri na cheo, nami ninazo siku nne za mapumziko katika wiki nitakuwa rehami wa maelekezo yako.

. Basi tuliafikiana siku ya Jumamosi katika kila wiki, kwa kuwa siku hiyo hakuna vikao vya Mahakama.

Na baada ya kuniomba nimuachie kitabu changu cha Bukhari na Muslim na kitabu cha Fatwa cha Mahmud Shaltut ili aihariri ile Nassi, alisimama na kunitoa ofisini akanisindikiza mwenyewe.

Nilitoka kwa furaha nikimshukuru Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa ushindi huu, kwani niliingia hali ya kuwa ni mwenye khofu nikitishiwa kufungwa gerezani, na (sasa) ninatoka hali ya kuwa rais wa mahakama akiwa amebadilika na kuwa rafiki mpenzi anayeniheshimu na akinitaka tuketi naye ili afaidike kutoka kwangu. Kwa hakika hizo ni miongoni mwa baraka za (kufuata) njia ya watu wa nyumba ya Mtume ambao mwenye kushikamana nao hapati khasara, na hupata amani mwenye kuwategemea.

Yule mume akaizungumza khabari hii kijijini kwake na ikaenea katika kila kijiji kilicho jirani baada ya mke kurejea nyumbani kwa mumewe na shauri lile kumalizika kwa ndoa ile kuwa halali. Basi watu wakawa wanasema kwamba mimi ni mjuzi mno kuliko wote na ni mjuzi mno kuliko hata Mufti wa Jamhuri. Yule mume alikuja nyumbani akiwa na gari kubwa, akaniita niende kijijini mimi na familia yangu yote na akaniambia kwamba watu wote wanasubiri kufika kwangu na watachinja kondoo watatu ili kufanya' sherehe ya faraja.

Nilimtaka radhi kutokana na shughuli zangu mjini Qafsah na nikamwambia nitawatembeleeni wakati mwingine pindi apendapo Mwenyezi Mungu."

292

Naye rais wa Mahakama akawazungumza marafiki zake na shauri hili likawa mashuhuri, Mwenyezi Mungu akavishinda vitimbi vya wakaidi, na baadhi yao walikuja niomba radhi.

Kwa hakika Mwenyezi Mungu alizifungua nyoyo za baadhi yao wakaongoka na wakawa miongoni mwa mukhlisina.

Hiyo ni fadhila ya Mwenyezi Mungu humpa amtakaye, naye Mwenyezi Mungu ni mwingi wa fadhila.

Na maombi yetu ya mwisho ni kuwa kila sifa njema anastahiki Mwenyezi Mungu, kisha rehma za Mwenyezi Mungu zimshukie Bwana wetu Muhammad na ziwashukie kizazi chake walio wema waliotakasika.

293

Rejea Zilizotumika:

Vitabu vya Tafsir;

1. Qur'anTukufa

2. Tafsiri ya al-Tabari

3. Al-Durr al-Manthur fi al-Tafsiri hi al-Ma'thur ya al-Suyuti.

4. Tafsir al-Mizan ya al-Tabatabai.

5. Al-Tafsir al-Kabir ya al-Fakhr al-Razi.

6. Tafsir Ibn Kathir.

7. Zad al-Maseer fi Ilm al-Tafsir ya Ibn al-Jawzi

8. Tafsir al-Qurtubi.

9. Shawahid al-Tanzil ya al-Haskani.

10. Al-Hawi Lil Fatawi ya al-Suyuti.

11. Al-Itqan fi Ulum al-Qur'an.

Vitabu vya Hadithi:

1. Sahih Bukhari.

2. Sahih Muslim.

3. Sahih Tirmidhi.

4. Sahih Ibn Majah.

5. Mustadrak al-Hakim.

6. Musnad al-Imam Ahmad ibn Hanbal.

7. Sunan Abi Dawood.

8. Kanz al-Ummal.

9. Muwatta'al-Imam Malik. 10. Jami' al-Usul cha Ibn al-Athir.

294

11. Al-Jami' al-Saghir na al-Jami' al-Kabir vya al-Suyuti.

12. Minhaj al-Sunnah cha Ibn Taymiyah.

13. Majma al-Zawa'id cha al-Haythami.

14. Kunuz al-Haqa'iq cha al-Manawi.

15. Fath al-Bari fi Sharh al-Bukhari.

Vitabu vya Historia:

1. Tarikh al-Umam wa al-Muluk cha al-Tabari.

2. Tarikh al-Khulafa cha al-Suyuti

3. Tarikh al-Kamil cha Ibn al-Athir.

4. Tarikh Dimashq cha Ibn Asakir.

5. Tarikh al-Masudi [Muruj al-Dhahab]

6. Tarikh al-Ya'qubi.

7. Tarikh al-Khulafa cha Ibn Qutaybah.

Kinachojulikana kama Imamah wa al-Siyasah.

8. Tarikh Abi al-Fida'.

9. Tarikh Ibn al-Shuhnah.

10. Tarikh Baghdad.

11. Al-Tabaqat al-Kubra cha Ibn Sa'd.

13. Sharh Nahj al-Balagha cha Ibn Abi al-Hadid.

Vitabu vya Sirah:

1. Sirat Ibn Hisham.

2. Al-Sirah al-Halabiyah.

3. Al-Isti'ab.

4. Al-Isabah fi Tamyeez al-Sahabah.

6. Hilyat al-Awlia cha Abi Nu'aym.

7. Al-Ghadir fi al-Kitab wa al-Sunnah cha al-Amini.

8. Al-Ta'rifcha Ibn Tawus.

9. Al-Fitnah al-Kubra cha Taha Husayn.

295

10. Maisha ya Muhammad cha Muhammad Hasanain Haykal.

11. Al-Riyadh al-Nadirah cha al-Tabari.

12. Al-Khilafah wa al-Mulk cha Abu al-Aala al-Mawdudi.

Vitabu Mbalimbali:

1. Is'afal-Raghibeen.

2. Tahdhib al-Tahdhib.

3. Tadhkirat al-Khawass cha Ibn al-Jawzi.

4. Al-Bidayah wa al-Nihayah cha Ibn Kathir.

5. Sirr al-Alamin cha al-Ghazali.

6. Al-Sawa"qal-Muhriqah Ibn Hajar al-Haythami.

7. Al-Manaqib al-Khawarizmi.

8. Yanabi'al-Mawaddah cha al-Qanduzi al-Hanafi.

9. Al-Nass wa al-Ijtihad cha Sharafal-Din al-Musawi.

10. Al-Muraja'at cha Sharafal-Din al-Musawi.

11. Al-Saqifah cha Shaykh al-Muzaffar.

12. Fadak cha al-Sayyid Muhammad Baqir al-Sadr.

13. Al-Siddiq Abu Bakar cha Husain Haykal.

14. Munaqashah' Aqaidiyya fi Maqalat Ibrahim al-Jabhan.

14. Lisan al-Arab cha Ibn Manzur.

16. SharhNahj al-Balaghah cha Muhammad Abduh.

17. Abu Hurayrah cha Sharafal-Din al-Musawi.

18. Al-Saqifah wa al-Khilafah cha Abdul Fattah Abdul Maqsud.

19. Shaykh al-Mudirah cha Mahmud Abu r-ayyah.

296

Rudi nyuma Yaliyomo