Rudi nyuma Yaliyomo endelea

Sahih Bukhar Juz. 1 uk. 54).

Mashaallah; Huyu Abdullah alijifanya kuwa ni kiongozi wa Umma huu akatoa Fat-wa kwa matamanio yake na vile atakavyo, na siyo vile hukmu za Mwenyezi Mungu alizoziteremsha ndani ya Qur'an zinavyotaka, licha ya Abu Musa Al-Ash-ari kutoa ushahidi wa aya ya kutayamam, kwani Abdullah anasema, "Lau tutawaruhusu kufanya hivyo...."

Wewe ni kama nani (Ewe Abdullah)? Kiasi kwamba unahalalisha na kuharamisha, unaruhusu na kukataza kama upendavyo. Naapa kwa hakika wewe kuhusu jambo hili umefuata mwendo wa aliyekutangulia, na umezidi kuwajeuri na kuyatia nguvu maoni yake ambayo alikuwa akitolea Fat-wa ya kuacha kuswali wakati maji yanapokosekana na wala hakukinaishwa na hoja ya Ammar ibn Yasir aliyoitowa kupitia

168

Sunna ya Mtume (s.a.w.) kama ambavyo Musa al-Ash-ari aliyoitoa kupitia aya ya Qur'an!! Je, Baada ya yote haya, hivi kweli wanachuoni wetu wanaweza kudai kwamba Masahaba ni kama nyota basi yeyote tutakayemfuata tutaongoka!!

(Je, Munastaajabu kwa hadithi hii na munacheka na wala hamlii, hali yakuwa mumeghafilika)!! (Qur'an, 53:59)

3). Masahaba wanashuhudia wenyewe:

Anas Ibn Malik amesimulia kwamba, "Mjumbe wa Mwenyezi Mungu aliwaambia Ansar, Hakika ninyi baada yangu mutaona ubinafsi mkubwa, basi subirini mpaka mkutane na Mwenyezi Mungu na Mtume wake kwenye Haudh." Anas akasema, "Hatukusubiri." (Taz: Sahih Bukhari Juz. 2 uk. 135)

Na imesimuliwa kutoka kwa Al-Alau ibn Al-Musayyab naye toka kwa baba yake Amesema: "Nilikutana na Al-Bar-raa ibn Azib (r.a.) nikamwambia, Hongera, wewe ulikuwa Sahaba wa Mtume na ulimpa Baia chini ya mti, akasema: Ewe mtoto wa ndugu yangu, wewe hutambui ni mambo gani tuliyoyazusha baada yake. (Taz: Sahih Bukhari Juz.3 uk.32 mlango wa Ghazuwatul-Hudaibiyah).

Basi ikiwa Sahaba huyu ni miongoni mwa waliotangulia (kusilimu) arnbao walimpa Baia Mtume chini ya-mti (siku ya Hudaibiyah) na Mwenyezi Mungu aliwaridhia na akayafahamu yaliyomo ndani ya nyoyo zao, akawapa ushindi kwa zama za karibu, anashuhudia juu ya nafsi yake na wenzake kwamba wao walizusha mambo baada ya Mtume. Ushahidi huu ndiyo uthibitisho wa yale aliyoyasema Mtume (s.a.w.) na kuyaeleza yakuwa Masahaba wake baada yake watazusha na watageuka nyuma. Je, inawezekana kwa mtu mwenye akili baada ya maelezo haya akausadiki uadilifu wa Masahaba wote kabisa

169

kwa mujibu wa kauli ya Ahlus-sunna Wal-Jamaa. Na yeyote asemaye kauli kama hii bila shaka atakuwa anapingana na akili na maandiko, na wala hatabakia na kipimo chochote cha kufikiri akitegemeacho mtu anayefanya uchunguzi ili aweze kuufikia ukweli.

4). Ushahidi wa Masheikh wawili (Abubakr na Umar) Juu ya nafsi zao wenyewe:

Bukhari ameandika ndani ya Sahih yake katika mlango unaotaja sifa za Umar ibn al-Khatab amesema: "Pindi Umar alipopigwa upanga akawa anaugua ibn Abbas alimwambia: Ewe Amirul-Muuminin hata kama umefikwa na hayo bila shaka wewe ulishirikiana vema na Mjumbe wa Mwenyezi Mungu kisha ulitengana naye hali ya kuwa amekuridhia, na ulishirikiana vema na Abubakr, halafu ulitengana naye hali yakuwa amekuridhia, kisha ulishirikiana vema na masahaba wao na iwapo utatengana nao, basi bila shaka utatengana nao hali ya kuwa wamekuridhia."

Umar akasema, "Ama ulivyosema kuhusu usuhuba (ushirikiano) wangu kwa Mjumbe wa Mwenyezi Mungu na kuwa kwake radhi hakika hayo ni neema ya Mwenyezi Mungu aliyonineemesha, na ama usuhuba wangu kwa Abubakar na radhi yake kwangu si kingine bali ni neema ya Mwenyezi Mungu Mtukufu aliyo ninemesha, ama huzuni yangu ulionayo, hiyo ni kwa sababu yako na jamaa zako, namuapa Mwenyezi Mungu lau ningekuwa na kilima cha dhahabu ningejikomboa kwa kilima hicho kutokana na adhabu ya Mwenyezi Mungu Mtukufa kabla sijamuona". (Taz: Bukhari Juz.2 uk.201).

Pia historia imesajili kauli ya Umar isemayo; "Laiti mimi ningekuwa kondoo wa watu wangu, wakaninenepesha wapendavyo nikishanenepa vizuri, wakatembelewa na baadhi ya wanaowapenda, (wakanichinja) kisha sehemu yangu fulani

170

wakaichoma na wakanikata vipande vipande kisha wakanila na wakanitoa nikiwa ni uchafu na nisingekuwa mtu.

(Taz: Min-Hajus-Sunnah cha ibn Taimiyah Juz. 3 uk. 131, Hil-Yatul-Auliyai cha Abu Nuaim Juz. 1 uk.52.

Vile vile historia imesajili tukio kama hili kumhusu Abubakr; kuna wakati Abubakr alimuangalia ndege aliyekuwa juu ya mti akasema: "Ni furaha kubwa uliyonayo, Ewe ndege unakula matunda na unatua juu ya mti na wala huna hesabu wala adhabu, hakika napenda ningelikuwa mti pembezoni mwa njia, ngamia akipita anile na anitoe nikiwa uchafu na wala nisingekuwa mtu.

(Taz: Tarikh Tabari uk.41, Ar-ri Yadhun-Nadhrah Juz. 1 uk.134, Kanzul Ummal uk.361 Min-Hajus-Sunnah cha ibn Taimiyyah Juz. 3 uk. 120).

Na kuna mara nyingine tena alisema: "Laiti mama yangu asingenizaa, laiti ningekuwa pumba ndani ya tofali." Hayo ni baadhi ya maandiko niliyoyaleta kama mfano na siyo yote.

Na hiki hapa kitabu cha Mwenyezi Mungu kinawabashiria waja wake walioamini kwa kusema:-

"Fahamuni ya kwamba, mawalii 'wa Mwenyezi Mungu hawana khofu juu yao 'wala hawahuzuniki. (Hao) ni wale ambao wameamini na walikuwa wachaji Mungu wanayofuraha Duniani na Akhera. Hapana mabadiliko katika maneno ya Mwenyezi Mungu, hayo ndiyo mafanikio makubwa". (Qur. 10:

62, 63, 64.)

Na kinasema tena:-

"Bila shaka wale ambao •wamesema kuwa Mola -wetu ni Allah kisha wakawa na msimamo, basi huteremka juu yao Malaika (na kuwaambia) msikhofu na wala

171

msihuzunike, na jibashirieni kupata pepo ambayo mulikuwa mukiahidiwa, sisi ni wasimamizi wenu ndani ya maisha ya Dunia na Akhera, na humo mutapata chochote ambacho nafsi zenu zinakitamani, na humo mutapata mukitakacho, ni Takrima itokayo kwa (Mola) mwingi wa kusamehe, mwingi wa Rehma." (Qur. 41:30-32)

Basi ni vipi Masheikh hawa wawili Abubakar na Umar wanatamani wasiwe miongoni mwa binaadamu ambaye Mwenyezi Mungu amemtukuza kuliko viumbe wake wengine?

Na iwapo Muumini wa kawaida ambaye anao msimamo wa (Dini) katika maisha yake huwa anateremkiwa na Malaika na kumbashiria daraja yake aliyonayo peponi, basi hawezi kuogopa adhabu ya Mwenyezi Mungu wala hahuzuniki kwa matendo aliyoyaacha nyuma yake duniani na anayo furaha maishani mwake hapa duniani kabla hajafika Akhera, sasa inakuwaje kwa Masahaba hawa wakubwa ambao ni viumbe bora baada ya Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (kama tulivyofunzwa) ni vipi wanatamani wawe takataka na kapi za ngano?

Hivyo basi, lau Malaika wangekuwa wamewabashiria pepo kamwe wasingetamania kupata kilima chenye dhahabu ili wapate kujikomboa kutokana na adhabu ya Mwenyezi Mungu kabla ya kukutana naye.

Mwenyezi Mungu Anasema:

"Na lau kila mtu aliyejidhulumu angekuwa amemiliki vyote vilivyoko ardhini, bila shaka angevitoa vyote ili ajikomboe, na pindi watakapoiona adhabu watajitahidi kuficha majuto yao lakini hawawezi na patahukumiwa baina yao kwa uadilifu na wala hawatadhulumiwa." (Qur. 10:54)

172

Pia amesema Mwenyezi Mungu:

"Na lau wale waliojidhulumu wangemiliki vyote vilivyoko ardhini na vingine mfano kama huo, wangevitoa kujikomboa kutokana na adhabu mbaya ya siku ya Qiyama na yatawadhihirikia kwa Mwenyezi Mungu mambo ambayo hawakuyatazamia, na utawadhihirikia ubaya wa yale waliyoyachuma na yatawazunguka yale waliyokuwa wakiyafanyia mzaha."(Qur. 39:47-48).

Mimi kwa hakika natamani kwa moyo wangu wote aya hizi zisiwakumbe masahaba wakubwa mfano wa Abubakr Siddiq na Umar Al-Farouq... .

Isipokuwa mara nyingi nimekuwa natulizana mbele ya maandiko kama haya ili nichunguze sehemu zinazoathiri uhusiano wao na Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (s.w.t.), kutokana na wao kwenda kinyume na maamrisho yake na matakwa yake mwishoni mwa umri wake Mtukufa Mtume (s.a.w.) hali ambayo ilimkasirisha na kumfanya awaamuru wote watoke ndani. Vile vile naweka mbele matukio yaliyopita baada ya kufariki Mtume na aliyofanyiwa binti ya Mtume bibi Fatmah miongoni mwa maudhi hali yakuwa Mtume (s.a.w.) amesema, "Fatumah ni sehemu ya mwili wangu, mwenye kumkasirisha hakika amenikasirisha mimi[18]

Naye Bibi Fatumah alisema kuwaambia Abu Bakr na Umar, "Nakuapieni Mwenyezi Mungu Mtukufu, Je, ninyi hamjamsikia Mjumbe wa Mwenytezi Mungu akisema, Ridhaa ya Fatumah ni katika Riadhaa yangu, na kuchukia kwa Fatumah ndiyo kuchukizwa kwangu, basi yeyote mwenye kumpenda binti yangu Fatmah hakika amenipenda mimi, na mwenye kumridhisha Fatmah basi ameniridhisha mimi, na mwenye

 

173

kumkasirisha Fatumah amenikasirisha mimi." Wakasema, "Ndiyo tumeyasikia (hayo) kwa mjumbe wa Mwenyezi." Fatumah akasema, "Basi mimi ninamshuhudisha Mwenyezi Mungu na Malaika wake kwamba ninyi mumenichukiza Mimi na wala hamukuniridhisha. Na pindi nitakapokutana na Mtume Wallahi nitawashitaki."

(Taz: Al-Imamah Was-Siyasa cha ibn Juz.l uk.20, Fadakun Fit-Tarikh uk. 92).

Hebu tuachane na riwaya hizi ambazo zinaumiza moyo, kwani huenda ibn Qutaybah naye ni miongoni mwa wanachuoni wa Kisunni waliojitokeza katika fani nyingi na anazo tungo nyingi za tafsiri, hadithi, lugha, nahau na historia, basi huenda ameshakuwa Shia kama alivyoniambia mtu fulani miongoni mwa wapinzani pale nilipomuonesha kitabu cha (ibn Qutaibah) kiitwacho, "Tarikh Al-Khulafa".

Na madai kama haya ndiyo wanayoyakimbilia baadhi ya wanachuoni wetu wanapokosa njia, basi Tabari huku kwetu ni Shia, na Imam Nasai ambaye alitunga kitabu kinachohusu sifa makhususi za Imam Ali ni Shia, ibn Qutaibah naye ni Shia hadi Twaha Husein ambaye ni miongoni mwa wanachuoni wa zama zetu naye ni Shia, eti tu kwa kuwa ametunga kitabu chake kiitwacho, "Al-Fitnatul-Kubra". (fitna kubwa) na humo akaeleza hadithi ya Ghadir, na akayakubali mambo mengi yenye ukweli basi naye kawa Shia!!!

Lakini ukweli halisi wote hawa hawakuwa Mashia, bali wanapozungumza kitu kuhusu Mashia, hawawataji Mashia isipokuwa kwa sifa mbaya, pia (wanachuoni hawa) wanatetea uadilifu waMasahaba kwa kila njia inayowezekana. Lakini mtu yeyote anayeeleza ubora wa Imam Ali ibn Abi Talib na akakiri juu ya mambo yaliyofanywa na Masahaba wakubwa basi tunamtuhumu kuwa ni Shia. Na inatosha tu kusema mbele ya mmoja wao wakati unapomtajaMtume, (ukasema), "SalaLlahu

174

Alaihi Waalihi Was-Salama" au useme, "Ali alaihis-Salaam" tayari utaambiwa wewe ni "Shia".

Na kwa msingi huu, siku moja nilimwambia mmoja wa wanachuouni wetu katika hali ya majadiliano, "Una maoni gani juu ya Bukhari"? Akasema, "Yeye ni miongoni mwa Maimamu wa hadithi, na kitabu chake ni sahihi mno kwetu sisi kuliko vitabu vingine baada ya kitabu cha Mwenyezi Mungu na wanachuoni wetu wamekubaliana juu ya hilo."

Basi mimi nikamwambia, "Bila shaka Bukhari ni Shia akacheka kwa kicheko cha dharau kisha akasema, "Haiwezekani Bukhari akawa Shia."

Mimi nikasema, "Je, siyo wewe uliyesema kwamba kila asemaye" Ali Alaihis-Salaam ni Shia?" Akasema, "Bila shaka nimesema." Basi nikamuonesha yeye na waliokuwa pamoja naye Sahih Bukhari tena mahala pengi kila linapokuja jina la Ali husema Alaihis-Salaam, na FatmahAlaihas-Salaam, na Husein ibn Ali Alaihimas-Salaam.[19]Basi alichanganyikiwa asijuwe alisemalo.

Narejea tena kwenye ile riwaya ya ibn Qutaibah ambayo amedai kwamba Bibi Fatumah(a.s.) aliwakasirikia Mabwana Abubakr na Umar, basi iwapo wewe utakuwa na mashaka nayo, mimi siwezi kuitilia shaka Sahihi Bukhari ambayo huku kwetu ni kitabu Sahihi mno baada ya kitabu cha Mwenyezi Mungu, nasi tumejilazimisha wenyewe kuwa ni kitabu sahihi, hawa Mashia wanawajibika kukitolea hoja dhidi yetu ili watulazimishe kukubali hoja zao kwa kutumia kitu ambacho sisi wenyewe tumejilazimisha (kuwa ni sahihi), na namna hii ndiyo uadilifu kwa watu wenye akili.

175

Basi huyu hapa Bukhari ameandika ndani ya mlango uitwao, "Ubora waQaraba (Jamaa) wa Mjumbe wa Mwenyezi Mungu" kwamba, Mjumbe wa Mwenyezi Mungu amesema, "Fatumah ni sehemu itokanayo na mimi, basi yeyote mwenye kumkasirisha, amenikasirisha mimi."

Pia ameandika katika mlango wa "Ghaz-wah Khaibar" kutoka kwa Bibi Aisha amesema, "Fatumah (a. s.) bint ya Mtume alipeleka ujumbe kwa Abubakr akimtaka ampe mirathi yake (aliyoacha) Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, Abubakr akakataa kumpa Fatumah chochote katika mirathi hiyo, Fatumah akamkasirikia Abubakr kuhusu jambo hilo akamsusa na hakumsemesha tena hadi (Fatumah) alipofariki. (Taz: Sahih BukhariJuz.3uk.39.)

Matokeo ya mwisho kuhusu kisa hiki ni ya aina moja, Bukhari ameyataja kwa mukhtasari naye ibn Qutaibah ameyataja kwa urefu, matokeo hayo ni haya: Kwamba Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.) hukasirika Fatumah anapokasirika na huwa radhi pindi Fatumah anapokuwa radhi, na (hali iliyopo ni) kwamba Fatumah amefariki hali ya kuwa amemkasirikia Abubakr na Umar.

Sasa iwapo Bukhari amesema kwamba Fatumah alifariki hali yakuwa amemkasirikia Abubakr na hakumsemesha hadi alipofishwa, basi ni wazi maana (iliyopo) ni moja tu, na iwapo Fatumah ambaye ni mwanamke bora kuliko wote ulimwenguni kama alivyobainisha Bukhari ndani ya (Kitabul-Istiidhan) katika mlango wa (Man Naaja Bayna Yadayn-Nas). Pia iwapo Fatumah ndiye mwanamke pekee katika umma huu ambaye Mwenyezi Mungu amemuondolea uchafu na kumtakasa kikamilifu, basi hawezi kukasirika kwa jambo lisilokuwa la haki, na ndiyo maana Mwenyezi Mungu na Mjumbe wake wanachukia kwa kuchukia kwake Fatumah, na kwa ajili hiyo Abubakar alisema: "Mimi na jilinda kwa Mwenyezi Mungu kutokana na kuchukia kwake na

176

kuchukia kwako Ewe Fatumah." Kisha Abubakar alilia mno mpaka karibu nafsi yake itoke, na huku Fatumah akisema, "Wallahi nitamuomba Mwenyezi Mungu dhidi yako ndani ya kila sala nitakayoisali." Abubakr alitoka hali yakuwa analia huku anasema, "Sina haja na Baia yenu tengueni Baia yangu".

(Taz: TarekhAl-Khula-faa ambacho ni maarufu kwa Jina laAl-Imamah Was-Siyasah cha ibn Qutaibah Ad-Dainuri Juz. 1 uk.20).

Lakini wengi wa wanahistoria na baadhi ya wanachuoni wetu wanakiri kwamba Fatumah (a.s.) alimkasirikia Abubakr kuhusu qadhia ya zawadi ya shamba aliyopewa na baba yake na mirathi na sehemu ya Qaraba wa Mtume (s.a.w.) (kwani madai ya Fatumah yalikataliwa mpaka akafariki hali yakuwa amemkasirikia, isipokuwa (wanahistoria hao na wanachuoni' wanapotaja) matukio haya hupita wima na wala hawataki kusema kitu kuhusiana nayo ili tu kulinda heshima ya Abubakr kama ilivyo kawaida yao kwa kila jambo linalomgusa kwa karibu au kwa mbali. Miongoni mwa maajabu niliyoyasoma kuhusiana na maudhui hii ni kauli ya baadhi yao baada ya kutaja sehemu ya tukio kwa urefu husema: "Haiwezekani Fatumah kudai kitu kisichokuwa haki yake na haiwezekani kwa Abubakr kumzuwilia Fatumah haki yake."

Na kutokana na mizani hii ya ajabu, mwanachuoni huyu alidhani kwamba ametatua tatizo na amewakinaisha watafiti na maneno yake haya ni sawa na kauli ya msomaji asemaye:

"Haiwezekani Qur'an kusema jambo lisilo la kweli, pia haiwezekani kwa Banu Israil kuabudia ndama."

Hakika tumepata mtihani kwa kuwa na wanachuoni »wanaosema wasiyoyajua na wanaoamini vitu viwili vinavyopingana kwa wakati mmoja, (ajabu mwanachuoni) akasisitiza kwamba Fatumah alipeleka madai na Abu Baker akayapinga madai yake, basi ima Fatumah awe ni muongo

177

(Mwenyezi Mungu apishe mbali) hawezi kuwa hivyo, au basi Abu Bakar awe amemdhulumu Fatmah, na hakuna aina nyingine ya tatu ya ufumbuzi na suala hili kama wanavyotaka baadhi ya wanachuoni wetu.

Na ilivyoshindikana kwa dalili za kiakili na za maandiko kuwa Fatumah ni muongo kutokana na maneno ya Mjumbe wa Mwenyezi Mungu yaliyothibiti aliposema: "Fatumah ni sehemu iliyotokana nami, yeyote mwenye kumuudhi, basi atakuwa kaniudhi mimi". Bila ubishi muongo yeyote hawezi kustahiki mfano wa kauli hii itokayo kwa Mtume (s.a.w.), kwani hadithi hii kwa dhati yake inajulisha juu ya "Ismah" kuhifadhika kwa Bibi Fatumah kuwa hasemi uongo na mambo mengine machafu. Kama ambavyo ile aya ya utakaso nayo inajulisha juu ya "Ismah" yake, na hapana shaka kwamba iliteremka kwa ajili ya Bibi Fatumah, mumewe na wanawe wawili Hasan na Husein (a.s.) (na hili ni kwa ushahidi wa Bibi Aisha mwenyewe. (Taz: Tarekh Al-KhulafaiJuz.l uk. 20.

Kwa hiyo basi hakuna kinachobakia isipokuwa ni watu wenye akili wakubaliane kwamba Bibi Fatumah (a.s.) alidhulumiwa. Kukanusha madai ya Bibi Fatumah nijambo jepesi kwa mtu aliyeruhusu kumchoma moto iwapo wapinzani waliomo nyumbani mwake hawatotoka nje ya nyumba na kwenda kuwapa Baia Mabwana hao. (Taz: Tarekh A l-Khulafai Juz.luk.20).

Na kutokana na (matatizo) yote haya ndiyo maana unamuona (Fatumah a.s.) hakuwaruhusu kuingia nyumbani mwake walipomuomba ruhusa. ama pale Imam Ali alipowaingiza ndani, yeye aligeuzia uso wake kuelekea ukutani na hakuwa radhi kuwaangalia. (Taz: Rarekh Al-Khulafa, Juz. 1 uk.20).

Kwa hakika Bibi Fatumah alifariki na akazikwa usiku kwa mujibu wa usia wake ili tu asijehudhuria yeyote miongoni

178

mwao[20] na kaburi lake limebakia katika hali ya kutofahamika mahali lilipo hadi leo hii. Kwa hiyo mimi najiuliza ni kwanini wanachuoni wetu wanaunyamazia ukweli huu wala hawataki kuufanyia utafiti, wala hata kuuelezea na wanatupatia picha ya Masahaba wa Mjumbe wa Mwenyezi Mungu kama kwamba wao ni Malaika wasiokosea wala kutenda dhambi.

Na ikiwa utamuuliza mmoja wao ni vipi Khalifa wa Waislamu Sayyidna Uthman Dhun-Nurain aliuawa, atakujibu kwamba, Wamisri (ambao ni makafiri) walikuja na wakamuuwa, basi maudhui hii hukamilika kwa sentensi mbili tu. Lakini nilipopata fursa ya kufanya uchunguzi na kuisoma historia nikakuta kwamba, walio mstari wa mbele katika wauaji wa Uthman ni hao hao Masahaba wakiongozwa na Ummul-Muuminina Aisha ambaye alikuwa akinadi auawe na kuihalalisha damu yake mbele ya watu na alikuwa akisema:

"Muuweni mpumbavu amekufuru."[21]

Pia tunamkuta Tal-ha, Zuberi na Muhammad Ibn Abi Bakr na wengineo miongoni mwa Masahaba mashuhuri, walimzingira na wakamzuia asinywe maji ili tu wamlazimishe kujiuzulu.

Wanahistoria wanatusimulia kuwa ni hao hao Masahaba ndiyo waliomzuwilia Uthman asizikwe ndani ya eneo la Makaburi ya Waislamu, na akazikwa (Hash Kaukab) bila ya kukoshwa wala kusaliwa, Sub-hanallah! basi ni vipi tuambiwe kuwa aliuawa kwa kudhulumiwa na kwamba waliomuuwa siyo Waislamu?

Ni kisa kingine kinachofanana na qadhia ya Bibi Fatumah na Abubakr, kwa hiyo ima Sayidna Uthman atakuwa ndiye

179

aliyedhulumiwa na ikiwa hivyo basi (itabidi) tuwahukumu Masahaba waliomuua au walioshiriki mauaji yake kwamba wao ni wauaji tena waovu kwa sababu wamemuua Khalifa wa Waislamu kwa dhulma na uadui na wakalifuatia jeneza lake wakalipiga kwa mawe na wakamdhalilisha akiwa hai na baada ya kufa, au Masahaba hawa walihalalisha mauaji ya Uthman kutokana na mambo aliyoyatenda ambayo yanapingana na Uislamu kama ilivyoelezwa ndani ya vitabu vya historia. Hakuna namna nyingine ya kati na kati itakayosawazisha isipokuwa kama tutaikanusha historia na tukachukua upotofu (usemao) kwamba "Wamisri ambao walikuwa makafiri ndiyo waliomuua" (Uthman).

Na katika namna zote mbili kuna kanusho madhubuti kwa ile kauli inayohusu uadilifu wa Masahaba wote bila kubakisha, basi (kama ni hivyo) ima Uthman atakuwa siyo muadilifu au waliomuua siyo waadilifu (kwani) wote hawa ni miongoni mwa Masahaba na kwa sababu hiyo yanabatilika madai yetu (ya uadilifu wa Masahaba wote).

Kinachobakia ni madai ya wafuasi wa nyumba ya Mtume wasemao kwamba, uadilifu uko kwa baadhi miongoni mwao na kwa wengine hakuna.

Na tunajiuliza kuhusu vita ya Jamal ambayo moto wake uliwashwa na Ummul-Muuminin Aisha, kwani yeye mwenyewe ndiye aliyeiongoza, ni vipi Umul-Muumina Aisha anatoka nje ya nyumba yake ambayo Mwenyezi Mungu ameamrisha kukaa ndani yake aliposema:

"Kaeni majumbani mwenu wala msioneshe mapambo yenu kama walivyokuwa wakionesha mapambo yao wanawake wa zama za Jahiliya: (Qur. 33:33)

Sisi tunauliza, ni kwa haki gani iliyomfanya Ummul-Muuminina ahalalishe kumpiga vita Khalifa wa Waislamu Ali

180

ibn Abi Talib ambaye ni walii wa kila Muumini mwanaume na mwanamke7

Kama ilivyo kawaida na kwa ufafanuzi wanachuoni wetu wanatupatia jawabu ya kwamba, Bibi Aisha alikuwa hampendi kwa sababu Ali alimuashiria Mjumbe wa Mwenyezi Mungu ampe talaka katika lile tukio la "Ifki", na wanachuoni wetu hawa wanataka kutukinaisha ya kwamba tukio hili (iwapo litasihi) ambalo ni ishara ya Ali kwa Mjumbe wa Mwenyezi Mungu amuache Bibi Aisha, linatosha kabisa kumfanya amuasi Mola wake na kubomoa stara aliyowekewa na Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.) hatimaye akapanda ngamia ambaye Mjumbe wa Mwenyezi Mungu alimkataza kumpanda na alimhadharisha kwamba atabwekewa na mbwa wa Hauab.? [22]

Lakini Bibi Aisha alikata masafa marefu kutoka Madina hadi Maka na kutoka Maka akaenda hadi Basra, akahalalisha mauaji ya watu wasio na hatia na akampiga vita Jemedari wa waumini pamoja na Masahaba waliompa Baia na kusababisha mauaji ya maelfu ya Waislamu kama walivyoeleza wanahistoria. (Taz: Tabari, Ibn Al-Athir, Almadaini na wengineo miongoni mwa wanahistoria waliohadithia matukio ya mwaka •wa thelathini na sitaA.H.)

Yote haya ni kwa sababu Bibi Aisha alikuwa hampendi Imam Ali ambaye alimuashiria Mtume ampe talaka, lakini pamoja na hali hiyo Mtume hakumtaliki. Basi chuki yote hii ni ya nini na hapana shaka kwamba wanahistoria wameandika msimamo wa uadui usiyoweza kutafsirika aliokua nao Bibi Aisha kwa Imam Ali. Kuna kipindi Bibi Aisha alikuwa akirudi Madina kutoka Maka, akiwa njiani alijulishwa kuhusu kuuawa kwa Uthman, basi alimrahi sana. Lakini alipofahamu kwamba watu wamempa Baia Imam Ali, alikasirika na kusema, "Natamani mbingu ingeliifunika ardhi kabla mwana wa Abu

181

Talib hajatawalia kiti cha Ukhalifa." Kisha akasema tena, "Nirudisheni". Hapo ndipo alipoanza kuwasha moto wa fitnah ili kumpindua Imam Ali ambaye hakutaka hata kumtaja jina lake kama walivyoandika wanahistoria kuhusu Bibi Aisha.

Basi Je, Umul-Muuminina Aisha hakusikia kauli ya Mtume (s.a.w.) kwamba, "Kumpenda Ali ni imani, na kumbughudhi ni unafiki,[23] kiasi kwamba baadhi ya Masahaba wamesema; "Tulikuwa hatuwatambui wanafiki isipokuwa kwa kumbughudhi kwao Ali."

Je, Ummul-Muuminina hakuisikia kauli ya Mtume (s.a.w.) aliposema, "Yule ambaye mimi nilikuwa nikitawalia mambo yake, basi Ali ni mtawala wa mambo yake." Hapana shaka alisikia yote hayo lakini hakumpenda Ali wala hakuweza kutaja hata jina lake, bali aliposikia kuwa Ali amefariki alisujudu sijda ya kumshukuru Mwenyezi Mungu. (Taz: Tabari, ibn Al-Athir na wanahistoria wengine walioandika matukio ya mwaka wa arobaini A.H.)

Na tuyaachilie mbali yote haya, mimi sitaki kuichambua historia ya Ummul-Muuminina Aisha, lakini nikitakacho nikuleta ushahidi unaohusu Masahaba kwenda kinyume na misingi ya Uislamu, kukhalifu kwao amri za Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.) na inanitosha fitna (aliyoizua) Ummul-Muuminina kuwa ni dalili moja ambayo wanahistoria wamekubaliana juu yake, wamesema kuwa, "Pindi mama Aisha alipoyapita maji ya Hauab mbwa wa mahali hapo walimbwekea wakimkumbusha lile onyo na katazo la Mumewe ambaye ni mjumbe wa Mwenyezi Mungu kupanda ngamia (wa fitna), basi Mama Aisha alilia na kusema, "Nirudisheni, nirudisheni."

Lakini Tal-ha na Zubair wakamletea watu khamsini waliowapa rushwa, wakamuapia Mama kwa Mwenyezi Mungu

182

' ya kwamba hapa sipo kwenye maji ya Hauab, basi Mama (akadanganyika) akaendelea na Safari yake mpaka Basra. Wanahistoria wanaeleza kwamba, huo ndio ulikuwa ushahidi wa kwanza wa uongo ndani ya Uislamu. (Taz: Tabari, Ibn Al-Athir Al-Madam na wengineo walioyataja matukio ya mwaka •wa thelathini na sita).

Tuambieni Enyi Waislamu, Enyi wenye akili pevu inayoweza kufumbua fumbo hili, Je, hawa ndiyo Masahaba watukufu ambao sisi tunahukumu kuwa ni waadilifu na kuwafanya kuwa ndiyo viumbe bora baada ya Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.)? Wanaoshuhudia ushahidi wa uongo kitendo ambacho Mjumbe wa Mwenyezi Mungu amekihesabu kuwa ni miongoni mwa madhambi makubwa yanayoangamiza, ambayo yanampeleka mtu motoni.

Suala hili siku zote linajirudia na kukaririka, Je, ni yupi yuko katika haki na ni yupi yuko katika batili (upotofu), basi imma Ali pamoja na wote aliokuwa nao ni madhalimu na hawako katika haki,   imma Aisha na aliokuwanao na Twalha na Zubair na waliokuwa pamoja nao ni madhalimu na hawakuwa juu ya haki, hakuna mtazamo mwingine wa tatu. Mchunguzi muadilifu simuoni isipokuwa ataelekea kwenye haki ya Ali ambaye, "Haki inazunguka pamoja naye popote azungukiapo," na kuiponda fitna ya "Umul-Muuminina Aisha na wafuasi wake ambao waliuwasha moto wa fitna na hawakuuzima mpaka ulipokuwa umeunguza vibichi na vikavu na athari zake zimebakia mpaka leo.

Hi kuongezea uchunguzi na ili moyo wangu utulie nasema, ' "Bukhari ameandika ndani ya Sahih yake katika Kitabul-Fitnah, ambayo inavuma kama yanavyovuma mawimbi amesema:

"Pindi Tal-ha na Zubair na Aisha walipokwenda Basra, Ali

183

alimtuma Ammar ibn Yasir na Hasan ibn Ali wakaenda Al-kufah, kisha wakapanda juu ya mimbar, Hasan ibn Ali alikuwa juu kabisa ya mimbar na Ammar ibn Yasir alisimama chini kidogo ya Hasan, basi tulikusanyika kwa ajili yake, nami nilimsikia Ammar anasema: "Bila shaka Aisha amekwishakwenda Basra, Wallahi yeye ni mke wa Mtume wenu hapa duniani na kesho Akhera, lakini Mwenyezi Mungu Mtukufu amekupeni mtihani ili abainishe. Je, Mtamtii yeye Mwenyezi Mungu au Aisha? (Taz: Sahih Bukhari Juz. 4 uk. 161).

Pia Bukhari ameandika ndani ya Sahihi yake, Kitabus-Shurut Babu Majaa Fi Buyuut Az-Wajin-Nabi amesema:

Mtume (s.a.w.) alisimama akahutubia, hatimaye aliashiria yaliko makazi ya Aisha kisha akasema, hapa ndipo, itapoanzia fitina, hapa ndipo itapoanzia fitna, hapa ndipo itapoanzia fitna, wakati itakapochomoza pembe ya shetani." (Taz: Sahih Bukhar uk.128).

Kadhalika Bukhari ameandika ndani ya Sahih yake mambo ya ajabu na ya kushangaza juu ya tabia isiyo nzuri ya Bibi Aisha (aliyokuwa) akimfanyia Mtume (s.a.w.) kiasi kwamba Baba yake alimpiga na kumvujisha damu.

Na baada ya yote haya, najiuliza ni vipi mama Aisha alistahiki heshima zote hizi (apewazo) kwaAhlus-Sunnah Wal-Jamaa, hapana kingine isipokuwa kwa kuwa ni mke wa Mtume, lakini wake wa Mtume ni wengi na miongoni mwao wako waliobora kuliko Aisha kwa mujibu wa utambulisho wa Mwenyewe Mtume. (Taz: Sahih tir-midhi, Al-Istiiabu Tarjuma ya Safiyyah, Al-Isabah Tar-Juma ya Safiyyah Ummul-Muumimna).

Labda kwa vile yeye ni binti wa Abubakr na yeye ndiye aliyeisimamia kwa kiwango kikubwa kampeni ya kukanusha wasia wa Mtume kwa Ali kiasi kwamba pindi alipoambiwa kwamba Mtume aliusia kwa Ali akasema, "Nani aliyesema

184

hivyo kwa hakika Mtume alikuwa kaegemea kifuani pangu, aliomba dishi la maji ghafla alidhoofika na kufa."

Au kwa sababu alimpiga Ali vita isiyo na huruma, na baada ya Ali akawafanyia hivyo hivyo wanawe mpaka alizuwia jeneza la Hasan Bwana wa vijana wa peponi na akakataza asizikwe pembezoni mwa Babu yake Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.) akasema (Bibi Aisha), "Msimuingize nyumbani mwangu mtu nisiyempenda." Mama Aisha alisahau kauli ya Mtume kuhusu Hasan na nduguye, "Hasan na Husein ni mabwana wa vijana wa peponi." Au kauli ya Mtume isemayo:

"Mwenyezi Mungu ampende awapendaye (Hasan na Husein) na Mwenyezi Mungu amkasirikie anayewabughudhi wao". Au aliposema: "Mimi nampiga vita anayekupigeni vita, na nitampa amani mwenye kukupeni amani." Basi na kauli nyinginezo nyingi ambazo sitozieleza - Ni kwanini (wasistahiki sifa hizi) hali ya kuwa wao ni pambo la umma huu.

Rudi nyuma Yaliyomo endelea