Rudi nyuma Yaliyomo endelea

Haishangazi kwani amekwisha sikia mengi zaidi ya hayo kuhusu haki ya Ali, lakini licha ya maonyo ya Mtume (s.a.w.) kwa mama Aisha, hakukubali isipokuwa (akaendelea) kumpiga vita Imam Ali na kuwahimiza watu wampinge na kuzikanusha fadhila zake na ubora wake.

Na kwa ajili hiyo, Banu Umayyah walimpenda na kumuweka kwenye daraja hiyo kubwa na wakasimulia mengi juu ya fadhila za mama Aisha, ambazo zimeenea kila pahali, mpaka wakamfanya kuwa ndiyo rejea kubwa ya (dini katika) umma wa Kiislamu kwani Eti yeye peke yake anayo nusu ya maarifa ya Dini.

Na huenda nusu ya pili ya dini wamemuhusisha nayo Abu Hurairah ambaye kapokea (na kusimulia) kwa (manufaa ya Banu Umayyah) mambo wayapendayo, ndipo nao walipomsogeza karibu yao na kumpa ugavana wa mji wa Madina na kumjengea jumba kubwa la Aqiqi, ambapo hapo

185

kabla alikuwa mtu duni kisha wakampa Laqabu ya "msimulizi wa Uislamu."

Na kwa ajili hiyo ikawa nijambo rahisi kwa Banu Umayyah kupata Dini yao iliyo kamilika ambayo ndani yake hakuna kitabu cha Mwenyezi Mungu wala Sunna ya Mtume wake, bali kilichomo ni yale mambo ambayo nafsi zao zinayataka na kuimarisha ufalme wao na nguvu zao. Na stahiki ya Dini hii (ya Banu Umayyah) ni kuwa imejaa mchezo na upuuzi na uzushi, na kutokana na hali hii ukweli halisi ukafutwa na pahali pake pakakaa kiza.

Bila shaka waliwalazimisha watu kufuata misingi ya dini yao na kuwadanganya mpaka dini ya Mwenyezi Mungu kwao wao ikawa ni kitu cha mzaha miongoni mwa mizaha, wakakosa kuithamini na wala watu hawakumuogopa Mwenyezi Mungu kama walivyokuwa wakimuogopa Muawiyah.

Pindi tuwaulizapo wanachuoni wetu kuhsu sababu za Muawiyah kumpiga vita Imam Ali, vita kali iliyo sababisha Waislamu wagawanyike kwenye Usunni na Ushia, na Uislamu nao ukabomoka na usiungike hadi leo, wakati ambapo Muhajirina na Ansari walikwisha kumpa Baia Ali, wao hujibu kama ilivyo kawaida yao tena kwa urahisi tu husema, "Hapana shaka Ali na Muawiyah ni Masahaba watukufu, wote walifanya ijtihadi, Ali alifanya jitihada na akapatia hivyo ana ujira mara mbili, na Muawiyah alijitahidi akakosea basi anao ujira mmoja, nasi hatuna haki kutoa hukumu dhidi yao, na Mwenyezi Mungu amesema. "Hao ni Umma ambao umeshapita, wanayo yao waliyoyachuma, nanyi munayo yenu mliyoyachuma, na wala hamtaulizwa kwa yale waliyokuwa wakiyatenda."

Hivi ndivyo ilivyo, inahuzunisha! majibu yetu yanavyokuwa ni kama unavyoona yanapotosha, akili haikubali na wala dini wala sheria haikubaliani nayo. "Ewe Mwenyezi Mungu najitakasa kwako kutokana na maoni potofu na kuteleza

186

kwa kufuata matamanio na najilinda kwako na upotofu wa shetani na najilinda kwako asinifikie."

Ni vipi akili iliyosalama itaamua kuwa jitihada ya Muawiyah itampa ujira mmoja kwa kumpiga vita Imam wa Waislamu, na kwa kuwauwa Waislamu wasiyokuwa na hatia na kwa maovu na machafu aliyoyafanya ambayo hakuna awezaye kudhibiti hesabu yake isipokuwa Mwenyezi Mungu.

Hapana shaka Muawiyah ni mashuhuri mbele ya wanahistoria kwa mauaji yake dhidi ya wapinzani wake, na jinsi wanavyomsifia kutokana na matumizi ya njia yake mashuhuri (katika kutekeleza mauaji) nayo ni kuwalisha (wapinzani wake) Asali iliyotiwa Sumu, - na alikuwa akisema, "Hakika Mwenyezi Mungu anao askari ndani ya asali."

Ni vipi wanachuoni wetu hawa wanaohukumu kuwa alifanya ijtihadi na kumpa ujira hali yakuwa hapana shaka, kwamba Muawiyyah alikuwa ni Imamu wa kundi potofu? Kwani ndani ya hadithi mashuhuri ya Mtume ambayo imeandikikwa na wanachuoni wote wa hadithi wa Kisunni na Kishia na wengineo (Mtume kasema), "Nakuhurumia Ewe Ammar, litakuua kundi potofu" na hawajakhitilafiana Waislamu wawili kwamba aliyemuua Ammar na jamaa zake kuwa ni Muawiyah, basi vipi wanahukumu juu ya ijtihadi yake naye ndiye aliyemuuwa Hujr ibn Adiyi na jamaa zake ndani ya kifungo na akawazika huko "Murju Adh-raa katika jangwa la Shamu, kwa sababu tu wamekataa kumtukuana Ali ibn Abi Talib.

Ni vipi basi wanamtaka awe Sahaba muadilifu wakati ndiye aliyemtilia sumu Hasan ibn Ali Bwana wa vijana wa peponi na akamuua.

Ni vipi wanamtakasa hali yakuwa alichukua Baia kutoka kwa Umma wa Waislamu kwa nguvu, kwanza kwa nafsi yake kisha na mwanawe Yazid muovu, na akabadili utaratibu wa mashauriano na kufanya kuwa ufaime wa Kaisari?

187

(Taz: Al-Khilafatu Wal-Mulk, cha Maudud na Yaumul-Islam cha AhmadAmin.

Namna gani wanahukumu juu ya ijtihad yake na kumpa ujira, hali yakuwa aliwalazimisha watu wamlaani Ali juu ya mimbari yeye na watu wa nyumba ya Mtume ambao ni kizazi cha Mtume, na akawaua Masahaba waliokataa kufanya hivyo, laana hiyo ikawa ni sunna inayofuatwa, watu huzeeka wakiifanya na watoto wadogo nao hukua hali yakuwa wanafanya hivyo. "La haula Wala Quwwata Illah Billahil-aliyyil-Adhim".

Swali siku zote lina rudi na kukaririka, "Ewe Bwana ni nani kati ya makundi mawili aliye juu ya haki na ni yupi kati yao yuko kwenye upotufu?

Basi Imam Ali na wafuasi wake ni madhalimu na hawako kwenye haki, au Muawiyah na wafuasi wake ni madhalimu na hawako kwenye haki?

Kwa hakika Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.) alikwishaweka wazi kila kitu.

Katika namna zote mbili bila shaka Masahaba wote kuwa waadilifu bila ya kumtoa hata mmoja nijambo lisilowezekana wala halikubaliani na mantiki.

Maudhui zote hizi zina mifano mingi ambayo hawezi kudhibiti idadi yake isipokuwa Mwenyezi Mungu, na lau ningetaka kuingia kwa undani na kuzitafiti kila upande ningehitajia vitabu vingi, lakini nilitaka kufanya mukhtasari, na' nikachukua baadhi ya mifano tu kwa ajili ya utafiti huu. Namshukuru Mwenyezi Mungu kwamba utafiti huu utakuwa ni wenye kutosheleza kubatilisha madai ya watu wangu ambao walizigandisha fikra zangu muda mrefu na wakanidumaza nisifahamu hadithi wala kuyachambua matukio ya kihistoria kwa kutumia mizani ya akili na vipimo vya kisheria ambavyo

188

Qur'an na sunna tukufu ya Mtume vimetufunza.

Na kwa sababu hiyo basi nitaipinga nafsi yangu na kulipangusa vumbi la ung'ang'anizi walilonifunika, ili nijikomboe kutokana na vifungo na minyororo waliyonifunga nayo kwa zaidi ya miaka ishirini.

Kielelezo changu nawaambia kwamba, "Laiti watu wangu wangejua alivyonisamehe Mola wangu na akanifanya kuwa miongoni mwa waliokirimiwa. Oh! Laiti watu wangeuvumbua ulimwengu wasiyo ujua na wanao ufanyia uadui bila ya kuufahamu!

189

MWANZO WA KUBADILIKA

Nilibakia nimechanganyikiwa na kupigwa butwaa kwa muda wa miezi mitatu, hata usingizini nilikuwa navutana na fikra na mchanganyiko wa mawazo, naihofia nafsi yangu kutokana na baadhi ya Masahaba niliokuwa nikihakiki historia yao, na kuchunguza baadhi ya mfarakano wa kutatanisha katika mienendo yao. Kwani mafunzo niliyokwishayapata muda wote wa maisha yangu yananitaka kuwaheshimu na kuwatukuza Mawalii wa Mwenyezi Mungu na wacha Mungu miongoni mwa waja wa Mwenyezi Mungu ambao humdhuru yeyote awasemaye kwa ubaya au kuwakosea adabu hata kama hawapo au wamekufa.

Nilipata kusoma hapo zamani ndani ya kitabu kiitwacho, "Hayatul-Hayawan Al-kubra" cha Ad-Dumairi ya kwamba kuna mtu fulani alikuwa akimshutumu Umar ibn Al-Khatab, walikuwako jamaa zake ndani ya msafara huo wakimkataza, basi alipokwenda kujisaidia haja ndogo akaumwa na nyoka mweusi akafa pale pale. Wakachimba kaburi ili wamzike, humo kuburini wakamkuta nyoka mweusi, kisha wakachimba makaburi mengine na ndani ya kila kaburi walimkuta nyoka mweusi, basi mtu mmoja mwenye maarifa miongoni mwao akawaambia, "Mzikeni vyovyote mupendavyo, kwani hata kama mutaichimba ardhi yote basi mtamkuta nyoka mweusi, na hii ni kwakuwa Mwenyezi Mungu anataka amuadhibu duniani kabla ya huko Akhera kutokana na kosa lake la

190

kumshutumu SayyidnaUmar."

Na kwa ajili hii utanikuta naitosa nafsi yangu ndani ya utafiti huu mzito, hali ya kuwa ni mwenye khofu ninababaika, khususan kwa kuwa mimi nimejifunza katika kitengo cha "Az-Zaituni" ya kwamba uhakika ulivyo, mbora wa Makhalifa ni Sayyidna Abubakr As-Sidiq kisha baada yake ni Sayyidna Umar ibn al-Khatab Al-Farouq, ambaye kupitia kwake Mwenyezi Mungu huitenganisha haki na batili. kisha baada yake ni Sayyidina Uthman ibn Affan Dhun-Nurain ambaye Malaika wa Mwenyezi Mungu mwingi wa Rehma walimstahi na kisha baada yake ni Sayyidna Ali ambaye ndiye mlango wa mji wa Elimu, kisha baada ya hawa wanne, waliobaki ni Masahaba sita miongoni mwa kumi waliobashiriwa pepo, nao ni Tal-ha, Zubair, Saad, Said, Abdur-rahman na Abu Ubaidah. Na Baada ya hawa wanakuja Masahaba wote, na mara nyingi walipokuwa wakinifunza hutoleaushahidi wa aya ya Qur'anTukufu isemayo:

"Hatutofautishi baina ya yeyote miongoni mwa Mitume wake," inayo wajibisha kuwaheshimu Masahaba waliobakia kwa aina ile ile ya heshima bila kumtia dosari yeyote kati yao.

Na kwa msingi huu nilichelea nafsi yangu, nikamuomba Mwenyezi Mungu mara nyingi anisamehe nikikusudia katika msamaha huo niache kuendelea na utafiti wa mambo kama haya ambayo yananifanya niwatilie mashaka Masahaba wa Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, zaidi ya hivyo yananifanya niitilie Mashaka dini yangu.

Lakini muda wote nilipokuwa nikizungumza na baadhi ya wanachuoni, nilikuta mambo yanayopingana ambayo hayakubaliki kiakili, walianza kunionya kwamba mimi ninafanya utafiti juu ya mazingira na hali za Masahaba, jambo hili ni hatari huenda Mwenyezi Mungu akanipokonya neema yake na kuniangamiza.

191

Kutokana na upinzani wao na kukanusha kwao kila nilisemalo utashi wangu wa kielimu na pupa yangu ili nifikie uhakika ilinilazimu kuitosa upya nafsi yangu ndani ya utafiti na nikapata nguvu ya ndani iliyonishinikiza sana.

192

MAJADILIANO NA MWANACHUONI

Kuna mwanachuoni mmoja nilimwambia: "Ikiwa Muawiyah aliwauwa watu wasiokuwa na hatia na kuwavunjia heshima, nanyi mnasema kwamba alijitahidi akakosea na atapata ujira mmoja. Na iwapo Yazid ndiye aliyewaua watoto wa Mtume na akaruhusu jeshi lake liukalie mji wa Madina, na (kwa tendo hili) ninyi mnasema kwamba alifanya ijtihadi akakosea na atapata ujira mmoja, kiasi kwamba baadhi yenu wamesema kuwa, "Husein (a.s.) aliuawa kwa upanga wa Babu yake" ili walitakase tendo la Yazid.

Basi ni kwanini nami nisifanye jitihada katika utafiti kitu ambacho kinanipa msukumo wa kuwatilia mashaka masahaba na kuwatoa baadhi yao miongoni mwao, na hili jambo (nilifanyalo mimi) huwezi kulilinganisha na mauaji aliyoyafanya Muawiyah na mwanawe Yazid kwa kizazi kitukufu cha Mtume. Basi nami iwapo nitapatia nitapata ujira mara mbili na nikikosea nitapata ujira mara moja, kwani ninapowakosoa baadhi ya Masahaba sikusudii kuwatukana wala kuwashutumu na kuwalaani, bali ninachokikusudia ni kufika kwenye ukweli ili nilitambue lile kundi lenye uokovu kutokana na makundi potofu.

Huu ni wajibu wa kila Muislamu, na Mwenyezi Mungu Mtukufu ndiye ajuaye siri na kila kilichojificha moyoni."

Yule mwanachuoni alinijibu kwa kusema; "Ewe mwanangu hapana shaka kwamba mlango wa Ijtihadi

193

umekwishafungwa siku nyingi."

Nikamwambia, "Ni nani aliufunga"? Akasema, "Maimamu wanne."

Nikasema kwa kujiamini, "Al-Hamdulillahi! ikiwa Mwenyezi Mungu na Mjumbe wa Mwenyezi Mungu siyo walioufunga wala Makhalifa waongofu tulioamriwa kuwafuata, basi si makosa kwangu mimi nikijitahidi kama walivyojitahidi wao." Akasema: "Huwezi kufanya Ijtihadi mpaka uzifahamu Elimu (fani) kumi na saba, miongoni mwa hizo ni: Tafsiri, Lugha, Nahau, Sarifi, Balagha, Hadithi, Historia na nyinginezo."

Nilimkatiza kwa kusema, "Mimi sintafanya Ijtihadi ili niwabainishie watu hukmu za Qur'an na Sunnah, au ili nianzishe Madh-hebu katika Uislamu sivyo kabisa, lakini ili tu nifahamu nani yuko katika haki na nani yuko kwenye upotofu, na ili kufahamu kama Imam Ali yuko katika haki au Muawiyah kwa mfano. Haihitajii kufuzu Elimu hizo kumi na saba, inatosha nisome maisha ya kila mmoja wao na mambo waliyoyafanya ili niutambue ukweli."

Akasema: "Jambo gani la muhimu linakufanya utake kuyajuwa hayo? "Hao niwatu waliopita wanayao waliyoyatenda nanyi munayenu muliyoyatenda na wala hamtaulizwa ni mambo gani walikuwa wakiyatenda." Nikasema: "Je, unaisoma aya hii Wala Ta-saluna, kwa kuitia fataha Ta' au kuitia dhamma (yaani) Wala Tus-aluna: ? Akasema, "Tus-saluna, kwa Dhama".

Mimi nikasema: "Al-Hamdulillah lau ingekuwa kwa fataha uchunguzi ungezuilika, maadam ni kwa dhamma basi maana yake ni kwamba Mwenyezi Mungu Mtukufu hatatuadhibu kwa yale waliyoyafanya, na hilo ni kama kauli yake Mwenyezi Mungu isemayo, "Kila nafsi imefungika kwa yale iliyoyatenda" na "Mtu hatapata (malipo) ila kwa yale aliyoyatenda". Na Qur'an Tukufu imetuhimiza kuchunguza

194

khabari za watu waliopita ili tupate mazingatio kutokana na kahabari hizo, na bila shaka Mwenyezi Mungu ametusimulia mambo juu ya Fir-aun, Hamana, Namruda, Qaruni na Mitume waliotangulia na mataifa yao siyo kwa lengo la kutuliwaza tu, bali kwa lengo la kutujulisha ukweli kutokana na upotofu.

Amma kauli yako uliposema ni jambo gani la muhimu linalokusukuma kutaka kufanya uchunguzi (wa hayo)? Mimi najibu kuwa, ninao umuhimu wa kuchunguza.

Kwanza: Ili nimfahamu walii wa Mwenyezi Mungu nipate kumpenda, na nimjue adui wa Mwenyezi Mungu ili awe adui yangu. Na jambo hili ndilo ambalo Qur'an inanitaka kulifanya bali imenilazimisha.

Pili: Ni muhimu kwangu kufahamu ni jinsi gani nitamuabudu Mwenyezi Mungu na nitajikurubisha kwake kwa Faradhi alizozifaradhisha kama atakavyo yeye Mwenyezi Mungu na siyo kama atakavyo Malik au Abu Hanifa, au wengineo miongoni mwa wanajitihada, kwani mimi nimemkuta Malik anasema kuwa ni karaha kusoma Bismillahi Rahmani Rahiim katika Sala, wakati ambapo Abu Hanifa anasema kuwa ni wajibu, na wengine nao wanasema kuwa Sala inabatilika kama haikusomwa Bismillah, na kwa kuwa Sala ni nguzo ya dini, inapokubaliwa basi mema mengine nayo hukubaliwa na ikikataliwa, na mengine nayo hukataliwa, basi mimi sitaki Sala yangu iwe batili.Vile vile Mashia wanasema kuwa, miguu ipakwe wakati wa (kutia) udhu, na Masunni wanasema ikoshwe na wakati huo huo tunasoma ndani ya Qur'an (kama ifuatavyo) "Pakeni vichwa vyenu na miguu yenu" na iko wazi kuwa ni kupaka, basi vipi bwana wangu unamtaka Muislamu mwenye akili akubali kauli ya huyo na aipinge ya yule bila kufanya uchunguzi na (kupata) dalili? Akasema: "Nijuu yako kuchukua kutoka kila Madh-hebu lile jambo linalokuathiri, kwani yote ni Madh-hebu ya Kiislamu na wote wanataraji kutoka kwa

195

Mjumbe wa Mungu.

Nikasema, "Naogopa kuwa miongoni mwa wale aliowasema Mwenyezi Mungu kuwa; Je, umemuona anayefanya matamanio yake kuwa ndiye Mungu wake, na Mwenyezi Mungu akamuacha apotee pamoja na kuwa ana ujuzi, na akapiga muhuri juu ya masikio yake na moyo wake na kumuwekea kifuniko juu ya macho yake, basi ni nani atakayemuongoza baada ya Mwenyezi Mungu, Je, hamzingatii". (Qur. 45:23)

Ewe Bwana wangu mimi siamini kwamba Madhehebu yote yako kwenye msingi wa haki maadam tu moja Una halalisha kitu hiki na jingine linaharamisha kitu kile kile, haiwezekani kitu kimoja kuwa haramu na halali kwa wakati mmoja, na Mtume hakujipinga mwenyewe katika hukmu zake kwani huo ni wahyi utokao ndani ya Qur'an. "Na lau ingekuwa (hii Qur'an) haikutoka kwa Mwenyezi Mungu basi wangekuta ndani muna hitilafunyingi". (Qur. 4:82).

Na kwa kuwa (hayo) madh-hebu manne ndani yake kuna hitilafu nyingi, basi (ujuwe) hayakutoka kwa Mwenyezi Mungu, wala kwa Mtume wake kwani Mtume hapingani na Qur'an".

Na Sheikh huyu alipoona maneno yangu yana nantiki na hoja yangu inakubalika alisema:

"Nakusihi kwa ajili ya Mwenyezi Mungu Mtukufu, shaka yoyote itakayokupata usijaribu kuwashukia Makhalifa waongofu kwani wao ndiyo nguzo ya dini, na ukizibomoa nguzo jengo lote litaanguka.....

Nikasema, "Astaghfirullah!" Ewe Bwana wangu, basi Mtume atakuwa na nafasi gani ikiwa wao ndiyo nguzo za Uislasmu?

Akajibu; "Mjumbe wa Mwenyezi Mungu ndiyo jengo lenyewe na yeye ndiyo Uislamu wote".

196

Nilitabasamu kutokana na jawabu hili na nikasema, "Astaghafirullah"! kwa mara nyingine tena Sheikh unazungumza bila ya kufahamu, eti ya kwamba Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.) hawezi kusimama isipokuwa kwa kuwategemea hawa (Makhalifa) wanne, (kinyume na kauli yako) Mwenyezi Mungu anasema: "Ni yeye Mwenyezi Mungu aliyemtuma Mjumbe wake kwa uongofu na dini ya haki ili aipe ushindi juu ya dini zote, na Mwenyezi Mungu anatosha kuwa shahidi". (Qur. 48:28)

Kwa hakika alimtuma Muhammad na ujumbe bila ya kumshirikisha yeyote miongoni mwao hawa wala wasiokuwa hawa, na hapana shaka Mwenyezi Mungu amesema (kama ifuatavyo) kuhusu jambo hili: "Kama tulivyomtuma kwenu Mjumbe anayetokana nanyi, akusomeeni aya zetu na akutakaseni na akufundisheni kitabu na hekima, na akufundisheni mambo ambayo mlikuwa hamyajui" (Qur. 2:151)

Akasema: "(Majibu niliyokupa) hayo ndiyo tuliyojifunza kutoka kwa Masheikh wetu na Maimamu wetu, nasi katika zama zetu (tulipokuwa tukisoma) tulikuwa hatuwaulizi wala kujadiliana na Masheikh wetu kama ilivyo kwenu leo hii katika zama mpya, kwani mmekuwa na shaka katika kila jambo hata dini munaitilia mashaka na (kwa kweli) hizi ndizo dalili za Qiyama kwani Mtume (s.a.w.) amesema, "Hakitasimama Qiyama isipokuwa kwa viumbe waovu."

Mimi nikamwambia "Ee! Bwana wangu vitisho hivi ni vya nini? Mimi najilinda kwa Mwenyezi Mungu kutokana na kuitilia shaka dini au kuingiza mashaka katika dini, bila shaka namuamini Mwenyezi Mungu pekee asiyekuwa na mshirika, na Malaika wake na Mitume wake (nawaamini) na ninaamini kwamba Bwana wetu Muhammad ni mja wake na ni Mjumbe wake, naye ndiye mbora wa Mitume na Manabii na ndiyo wa mwisho wao na mimi ni katika Waislamu, basi vipi wewe

197

unanituhumu kwa tuhuma hiyo?"

Ninakutuhumu kwa mengi zaidi (kuliko haya niliyokuambia) na hii ni kwa sababu wewe unamshuku Bwana wetu Abubakr na Bwana wetu Umar, wakati Mtume (s.a.w.) amesema lau itapimwa imani ya umma wangu ikalinganishwa na imani ya Abubakr, basi imani ya Abubakar ingekuwa nzito".

Na amesema Mtume (s.a.w.) kuhusu haki ya Sayyidna Umar, "Nilioneshwa umma wangu hali umevaa kanzu haikufika vifuwani, na nilioneshwa Omar hali akiwa anaiburura kanzu yake, wakasema, umeitafsiri vipi ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu? Akasema: Ni dini." Leo unakuja wewe katika karne ya kumi na nne utie mashaka kuhusu uadilifu wa masahaba na hasa Abubakr na Omar?

Je wewe hujui kwamba watu wa Iraq ndiyo wavurugaji na ndiyo wenye kufru na unafiki?

Basi niseme nini kuhusu mwanachuoni huyu anayedai kuwa na elimu, mwanachuoni ambaye amechotwa na fahari mbaya, aliyeyabadilisha majadiliano yaliyokuwa kwa njia nzuri na kuyafanya kuwa zogo na uzushi na kueneza urongo mbele ya mkusanyiko wa watu walioathirika kwake, ambao macho yao tayari yalikwishawiva na kufura kwa hasira na nikaona nyuso zao zina alama ya shari.

Basi hakuna nilichofanya isipokuwa niliondoka haraka na nikaenda nyumbani, nikawaletea kitabu cha Muwatta ya Imam Malik na Sahih Bukhari kisha nikasema, ewe Bwana wangu, hakika aliyenitia mashaka haya ni mwenyewe Mtume wa Mwenyezi Mungu, halafu nikakifunguwa kitabu cha Muwatta, na ndani yake Malik anasimulia kwamba, "Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.) amesema kuhusu haki ya mashahidi wa Uhud; "Hawa nashuhudia juu yao (kwa wema waliofanya)," Abubakr akasema, "Ewe Mjumbe wa Mwenyezi

198

Mungu sisi siyo miongoni mwa ndugu zao (nasi upate kushuhudia) tumesilimu kama walivyosilimu, na tumepigana jihadi 'kama walivyopigana," Mtume wa Mwenyezi Mungu akasema, yote uliyosema ni sawa, lakini mimi sijui ni yepi mutayoyazua baada yangu!" Abubakr akalia, kisha akasema, hakika tutakuwa hivyo baada yako?" Taz: Muwattaya Imam Malik Juz. 1 uk. 307, Al-Maghaziya Waqidi uk. 310.

Kisha nikafungua Sahih Bukhari na ndani yake (tukakuta kama ifuatavyo), siku moja Umar ibn Khatab aliingia nyumbani kwa Hafsa na humo alikuwemo Asma Binti Umeis, Umar alipomuona Asma akasema (kumuuliza Hafsa) ni nani huyu, akasema, ni Asma Binti Umais, Umar akasema, huyu ni Mhabesh au Mbahriyah, Asma akasema ndiyo, Umar akasema sisi tumekutangulieni kuhama (Maka) kwa hiyo sisi tunayo haki zaidi kwa Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, Akasema sivyo kabisa ulivyosema, ninyi mlikuwa pamoja na Mjumbe wa Mwenyezi Mungu yeye akiwalisha wenye njaa miongoni mwenu, na sisi tulikuwa ndani ya makazi au nchi ya mbali yenye kero (huko) Uhabeshi na yote hayo (yalitukuta) kwa ajili ya (kutaka) radhi ya Mwenyezi Mungu na Mjumbe wake, namuapa Mwenyezi Mungu mimi sitokula chakula wala kunywa kinywaji mpaka nimwambie Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, na tulipokuwa huko tulikerwa na kutishwa, na kutokana na maneno uliyoniambia sasa hivi) nitamueleza Mtume nimuulize (nani bora sisi au ninyi naapa sitasema uongo wala kupotosha wala sitaongeza chochote juu ya haya uliyoyasema. Basi (Asma) alipokuja kwa Mtume (s.a.w.) akasema, Ewe Nabii wa Mungu Omar amesema kadha wa kadha, mimi sikumwambia (kitu) isipokuwa (nilisema) kadha wa kadha.

Mtume (s.a.w.) akasema:- "Yeye hana haki zaidi kwangu mimi kuliko ninyi, na yeye na wenzake wanayo hijra moja tu wakati ninyi enyi watu wa Safina mnazo hijra mbili." Akasema;

nilimuona Abu Musa na watu wa Safina (Wahajiri wa Uhabeshi)

199

wakinijia mfululizo kuniuliza hadithi hii, basi hapana kitu chochote duniani walichokifurahia wala kilichobora ndani ya nafsi zao kuliko maneno aliyoyasema Mtume kwa ajili yao" Taz: Sahih Bukhari Juz. 3 uk. 387 mlango unaohusu vita vya Khaibar.

Baada ya yule Sheikh na watu waliohudhuria hapo kuzisoma hadithi hizi, nyuso zao ziliwabadilika wakawa wanatazama na wao kwa wao wakisubiri jawabu la Sheikh aliyegongwa (na hadithi), basi hakuna kilichojitokeza kwake isipokuwa alinyanyua macho yake kama alama ya kustaajabu kisha akasema, "Waambie, Ewe Molawangu nizidishie Elimu."

Mimi nikasema, ikiwa kama Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.) ndiye wa kwanza kumtilia mashaka Abubakr na hakukubali kumshuhudia (wema wake) kwa sababu tu hajui ni jambo gani atakalolizusha baada yake, na iwapo Mjumbe wa Mwenyezi Mungu hakukubali kumboresha Omar ibn Al-Khatab juu ya Asma bint Umais, bali Mtume alimboresha Asma juu ya Omar, mimi pia ninayo haki ya kuwa na mashaka na kutokumboresha yeye mpaka kwanza nibaini na kuufahamu uhakika, na ni wazi kabisa kwamba hadithi hizi mbili zinapingana na zile hadithi zilizokuja kuhusu Abubakr na Omar isitoshe zinazibatilisha kwani na hizi mbili zinaingia akilini kuliko zile zinazodaiwa kuwa ni zenye kuwapa ubora.

Basi jamaa waliokuwepo hapo wakauliza kwa kusema, "Jambo hilo linakuja vipi?" Mimi nikasema "Hakika Mjumbe wa Mwenyezi Mungu hakumshuhudia Abubakr na alichomwambia ni kwamba, hakika mimi sijui ni mambo gani mutayazua baada yangu! jambo hili linaingia akilini sana, na Qur'an Tukufu imelikariri (mara nyingi) na historia nayo ni shahidi kwamba wao walibadilisha (mambo) baada ya Mtume, na ndiyo maana Abubakar alilia, kwani hapana shaka alibadili (mambo) na akamkasirisha Bibi Fatmah binti ya Mtume (s. a.w.)

200

kama tulivyo eleza hapo kabla na aliendelea kubadili (mambo) mpaka akajutia kabla ya kufa na akatamani laiti asingekuwa mtu.

Ama ile hadithi isemayo, "Lau itapimwa imani ya umma wangu kulinganishwa na imani ya Abubakr, basi imani ya Abubakr ingeshinda imani zingine." Hadithi hii ni batili wala haingii akilini, na wala haiwezekani kwa mtu ambaye umri wake wa miaka arobaini aliutumia katika kumshirikisha Mwenyezi Mungu na akiabudia sanamu akawa na imani kubwa kuliko umma wote wa Muhammad, wakati ndani ya umma huu wamo mawalii wema wa Mwenyezi Mungu, na mashahidi na Maimamu ambao walitumia muda wao wote wakipigania dini ya Mwenyezi Mungu, basi anayo nafasi gani Abubakr kutokana na hadithi hii? Na lau kama itasihi ni kwanini mwishoini mwa uhai wake alikuwa akitamani asingekuwa mtu. Na lau pia imani yake ingeshinda imani za umma wote basi Bibi Fatmah binti ya Mtume ambaye ni mwanamke bora kuliko wote asingemkasirikia na kuomba dua kwa Mwenyezi Mungu dhidi ya Abubakr katika kila sala aliyokuwa akisali.

Mwanachuoni yule hakurudisha jawabu lolote, lakini baadhi ya wanakikao walisema, "Bila shaka Wallahi hadithi hii imezua mashaka mioyoni mwetu", hapo hapo yule Sheikh akasema kuniambia "Hivi ndivyo unavyotaka hakika tayari umekwishawatia mashaka watu hawa katika dini yao." Kwa bahati nzuri mmoja wao alinitoshelezea jawabu kumjibu yule Sheikh akasema, "Siyo hivyo Sheikh, haki iko pamoja naye, maishani mwetu sisi hatujasoma kitabu chochote kwa ukamilifu, tumekufuateni na kuambatana nanyi katika imani ya upofu bila kujiuliza, na sasa imetubainikia kuwa ayasemayo Al-Haj ni Sahihi, wajibu wetu ni kusoma na kuchunguza!!" Baadhi ya waliokuwepo hapo waliafikiana naye katika maoni yake haya, na kwa kweli hali hii ilikuwa ni ushindi kwa upande wa haki, na wala haukuwa ni ushindi wa kutumia nguvu na shinikizo,

201

lakini ni ushindi wa kiakili, hoja na dalili "Waambie leteni hoja zenu kama ninyi ni wasema kweli."

Mazingira haya yalinipa msukumo na kunipa nguvu ya kuingia kwa undani katika uchunguzi, yalinifungulia milango yote nikaingia kwajina la Mwenyezi Mungu, kwa kumtegemea Mwenyezi Mungu na katika mila ya Mjumbe wa Mwenyezi Mungu hali ya kuwa nikitarajia kutoka kwa Mola Mtukufu anipe taufiki na uongofu, kwani ni yeye ndiye aliyeahidi kumuongoa kila anayefanya utafiti kuitafuta haki, na yeye Mwenyezi Mungu haendi kinyume na ahadi yake.

Utafiti uliendelea kwa makini miaka mitatu, kwa sababu nilikuwa nakariri niliyokuwa nimeyasoma baadhi ya wakati, kwa kukisoma kitabu mwanzo wa ukurasa hadi ukurasa wa mwisho wa kitabu.

Nilisoma kitabu kiitwacho "Al-Murajaat" cha Imam Sharafud-Din, nikakirudia mara nyingi, na kwa hakika kilifungua mbele yangu mwangaza uliosababisha niongoke nikakifungua kifua changu kwa kuwapenda watu wa nyumba ya Mtume.

Pia nilisoma kitabu kiitwacho "Al-Ghadir" nikakirudia mara tatu kutokana na yaliyomo miongoni mwa mambo ya haki iliyowazi mno, nikasoma kitabu cha Fidak cha Sayyid Muhammad Baqir As-Sadri, pia kitabu cha Saqifah kilichoandikwa na Sheikh Muhammad Ridha Al-Mudhafar, na kutokana na vitabu hivi viwili nilifahamu siri nyingi za ndani na zikawa wazi. Vile vile nilisoma kitabu kiitwacho "An-Nas -wal-Ij-tihadi" basi hapa ndipo yakini ikaongezeka, hatimaye nikasoma kitabu kiitwacho "Abuhurairah cha Sharafud-din, na kingine kiitwacho "Shaikhul-Muzira" kilichotungwa na Sheikh Mahmud Abur-Rayyah wa Misri na nikafahamu ya kwamba Masahaba waliobadili mambo baada ya Mjumbe wa Mwenyezi Mungu wamegawika mafungu mawili, kuna fungu moja walibadilisha hukmu kutokana na nguvu za utawala

202

walizokuwa nazo, na wengine walibadili hukumu kwa kuweka hadithi za uongo kumzushia Mtume (s.a.w.).

Baada ya vitabu hivyo nilisoma kitabu kiitwacho Al-Imam As-Sadiq Wal-Madhahibul-Arbah kilichoandikwa Asad Haidar, na humo nilifahamu tofauti baina ya elimu ya kipawa na elimu ya kutafuta, nilifahamu tofauti iliyopo baina ya hekima ya Mwenyezi Mungu ambayo humpa amtakaye na kulelewa katika mazingira ya elimu na kujitahidi kwa njia ya maoni kitu ambacho kimeutenga umma wa Kiislamu na ile roho halisi ya Uislamu.

Nilisoma vitabu vingine vingi vya Sayyid Jaafar Murtaza Al-Amili na Sayyid Murtaza Al-Askari, Sayyid Tabatabai Sheikh Muhammad Zainud-Din, Fairuz Abad, Ibn Abil-Hadid Al-Muutazili katika Sherhe yake ya Nahjul-Balagha na Fitnatul Kubra cha mwandishi Taha Husain. Na miongoni mwa vitabu vya historia nilisoma Tarikh At-Tabari, Tarikh ibn Al-Athir, Tarikh Al-Masoudna Tarikh Al-Yaaqubi, nilisoma vitabu vingi nikakinaika kwamba Shia Imamiyyah wako kwenye haki, nikawa Shia na nikaipanda Safina ya watu wa nyumba ya Mtume (s.a.w.) kwa baraka za Mwenyezi Mungu, nikashikamana na kamba ya kuwatawalisha, kwani namshukuru Mwenyezi Mungu, nilipata (viongozi) badala ya baadhi ya Masahaba ambao kwangu mimi ilikwishathibiti kwamba wao walirudi kinyume nyume kwa visigino vya miguu yao na hapana aliyeokoka miongoni mwao isipokuwa wachache. Nikawabadilisha hawa na mahala pao nikawaweka Maimamu wa nyumba ya Mtume, Maimamu ambao Mwenyezi Mungu amewaondoshea uchafu na amewatakasa kikamilifu, na akafaradhisha kuwapenda kuliko watu wote.

Walivyo Mashia sivyo kama wanavyodai baadhi ya Wanachuoni wetu eti kuwa wao ni Wafursi (Waajemi) ambao Sayyidina Omar alivunja jeuri yao na utukufu wao na heshima yao katika vita ya Qadisiya, ndiyo maana wanamchukia na kumbughudhi!

203

Watu hawa wasiyo jua nimepata kuwajibu kwamba, kuwa mfuasi wa watu wa nyumba ya Mtume siyo jambo linalowahusu Wafursi bali Mashia wapo Iraq, Hijaz, Syria na Lebanon na kote huko ni Waarabu, kama ambavyo Mashia wapo Pakistani, India, Afrika na Amerika na wote hawa siyo Waarabu wala si Wafursi.

Na lau tutatosheka na Mashia wa Iran basi hoja (yangu) itakuwa bora zaidi, kwani nimewakuta hawa Wafursi wanasema kuwa, Maimamu (wao) ni kumi na wawili na wote ni Waarabu tena Maquraishi katika Bani Hashim na ni kizazi cha Mtume (s.a.w.) kwa hiyo lau Wafursi wangekuwa na chuki ya kuwachukia Waarabu kama wanavyodai baadhi ya watu, basi wangelimfanya Salman Al-Farisi kuwa ndiyo Imam wao kwa kuwa anatokana nao, tena ni Sahaba Mtukufu ambaye cheo chake kinafahamika kwa wote sawa sawa Mashia na Masunni.

Rudi nyuma Yaliyomo endelea