Rudi nyuma Yaliyomo endelea

4). Aya ya khushui (unyenyekevu):

Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

"Je, wakati haujafika kwa wale walio amini kwamba, nyoyo zao zinyenyekee kwa kumkumbuka Mwenyezi Mungu na kwa mambo ya haki yaliyo teremka, na wala wasiwe kama wale waliopewa kitabu hapo kabla na muda wao (wa kuondokewa na Mitume) ukawa mrefu, kwa hivyo nyoyo zao zikawa ngumu na wengi wao wakawa waasi. (Qur. 5 7:16)

Ndani ya kitabu kiitwacho Ad-Durul-Ma-nthoor kilichoandikwa na Jalalud-Dini As-Suyut Amesema: "Pindi Masahaba wa Mtume (s.a.w.) walipofika Madina, wakapata

149

maisha mazuri ambayo hawakuwa nayo baada ya kuwa walikuwa katika shida basi 'kwao wao ikawa wamezembea (kutenda) baadhi ya wajibu uliokuwa juu yao, hivyo wakakemewa na ikashuka kauli ya Mwenyezi Mungu isemayo:

"Je, wakati haujafika kwa wale walioamini"? Na katika riwaya nyingine itokayo kwa Mtume (s.a.w.) inasema kwamba, "Mwenyezi Mungu aliziona nyoyo za Muhajirina kuwa ni nzito (hata) baada ya miaka kumi na saba tangu kushuka Qur'an, basi akateremsha kauli yake, "Je, wakati haujafika kwa 'wale •walioamini?"

Ikiwa hawa ndiyo Masahaba ambao ndiyo wabora mno kuliko watu wengine (kama wasemavyo Ahlul-Sunnah •wal-Jamaa) nyoyo zao hazikuwa na unyenyekevu katika kumtaja Mwenyezi Mungu na kile alichokiteremsha katika haki kwa muda wote wa miaka kumi na saba mpaka Mwenyezi Mungu akawaona wana nyoyo nzito, akawakemea na kuwaonya kutokana na ugumu wa nyoyo zao zinazowakokota kuwapeleka kwenye uovu, basi hapana lawama yoyote kwa vigogo wa Kiquraishi waliochelewa halafu wakasilimu katika mwaka wa saba Hijriyah na baada ya Makkah kuingia mikononi mwa Waislamu.

Basi hii ni baadhi ya mifano niliyoileta kutoka ndani ya kitabu kitukufu cha Mwenyezi Mungu, inatosha kuwa ni dalili kwamba siyo kweli kuwa Masahaba wote ni waadilifa (kama wasemavyo Ahlis-Sunna Wal-Jamaa.

Na tukifanya uchunguzi katika hadithi za Mtume (s.a.w.), basi bila shaka tutakuta mifano mingi lakini kwa mukhtasari nitaleta baadhi tu ya mifano, na itakuwa ni juu ya mwenye kutaka kufanya utafiti atafiti zaidi kama analitaka jambo hilo.

150

MAONI YA MTUME KUHUSU MASAHABA

1). Hadithi ya Haudh (Birika):

Mtume wa Mwenyezi Mungu amesema: "Nitakuwa nimesimama (siku ya Qiyama) halafu watanijia watu, na nitakapowafahamu, atatokea mtu kati yangu na wao atasema:

(kuwaambia), twendeni, mimi nitasema waende wapi? Atasema motoni, nitasema wamefanya nini hawa? Atasema, hakika wao walirudi baada yako kinyumenyume. Basi sintawaona wenye kuokoka miongoni mwao isipokuwa kikundi kidogo.[11]

Na amesema Mtume (s.a.w.): "Mimi ni mtangulizi wenu kwenye hodhi, yeyote atakayepitia kwangu atakunywa na atakayekunywa, milele hatahisi kiu, bila shaka watanifikia watu mbali mbali ambao mimi nawafahamu na wao wananifahamu kisha patawekwa kizuizi baina yangu na wao, mimi nitasema, hao ni Sahaba wangu, patasemwa, hakika wewe hujui mambo waliyoyazusha baada yako, basi mimi nitasema: Aangamie aliye badilisha (dini) baada yangu. "[12]

Yeyote mwenye kufanya mazingatiao ndani ya hadithi hizi nyingi walizoziandika wanachuoni wa Kisunni katika vitabu vyao, hawezi kuwa na shaka kwamba Masahaba wengi kwa

151

hakika walibadilisha na kugeuza (dini) bali waliritadi na kurudi nyuma kwa visigino vyao baada ya Mtume (s.a.w.) isipokuwa wachache ambao Mtume (s.a.w.) amewaeleza kuwa ni kikundi kidogo, na haiwezekani kwa hali yoyote ile kuziweka hadithi hizi kwenye kundi la tatu ambalo ni la wanafiki kwani maandiko yanasema: "Nitasema Masahaba wangu", na hali "hii ni kwa sababu wanafiki hawakubadilika baada ya Mtume (s.a.w.) vinginevyo basi (kama wangebadilika) mnafiki angelikuwa muumini baada ya kufariki Mtume (s.a.w.) kama ambavyo hadithi hizi ni kielelezo na ni tafsiri ya kile tulicho kisajili hapo kabla miongoni mwa aya tukufu ambazo zimezungumzia juu

ya kugeuka kwao na kuritadi na kuonywa kwao juu ya adhabu kali.

2). Hadithi inayohusu kuwafuata Wayahudi na Wakristo:

Amesema Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.):

"Bila shaka mutafuata nyendo za waliokutangulieni shubiri kwa shubiri na dhiraa kwa dhiraa (Hatua kwa hatua au kidogo kidogo) hata kama wataingia ndani ya shimo la kenge mutawafuata", tukasema, "Ewe Mjumbe wa Mwenyezi Mungu,

ni Wayahudi na Wakristo"? Mtume akasema, "Ni nani basi (Kama siyo hao"?[13]

Basi kwa yeyote anayefanya utafiti anawajibika kujiuliza pindi anapoisoma hadithi hii ambayo usahihi wake unakubalika kwa Waislamu wote ya kwamba, Masahaba ambao ndio waliokusudiwa katika hadithi hii walifanya mambo gani miongoni mwa matendo ya Wayahudi na Wakristo kiasi kwamba Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.) akawataja kwa

152

sifa ya kuwa watawafuata Shubiri kwa Shubiri na dhiraa kwa dhiraa hata kama wataingia ndani ya shimo la kenge nao wataingia.

Ndani ya Qur'an na katika historia sahihi inaeleweka wazi kuwa Wayahudi walimuasi Mjumbe wa Mwenyezi Mungu Nabii Musa (a.s.), wakaiasi amri yake, wakamuudhi na wakaabudia ndama alipokuwa hayupo, kisha walifanya njama dhidi ya Harun nduguye Musa (a.s.) na walikaribia kumuua, na kwa ajili hiyo walipewa adhabu ya unyonge na umaskini na wakastahiki adhabu ya Mwenyezi Mungu, yakiwa ni malipo (yao) kwa matendo waliyokuwa wakiyafanya. Waliritadi baada ya kuamini kwao na wakafanya njama dhidi ya Mitume wa Mwenyezi Mungu, na kila alipowafikia Mtume kwa jambo ambalo nafsi zao hazipendi, basi baadhi yao walimpinga na wengine walimuua, kiasi kwamba mambo yalifikia kuwa Mayahudi kupanga njama dhidi ya Bwana wetu Isa (a.s.) na walimsononesha mama yake Mtukufu (Bibi Mariam) na hawakutulia mpaka waliopomuua na kumsulubu kama wanavyodai wao,[14] kisha wakahitilafiana baada ya hayo na wakafarakana kuhusu Nabii Isa, kwani miongoni mwao wako wasemao kuwa yeye alikuwa ni muongo na ni mzushi, na wengine walivuka mipaka na kumpa daraja ya uungu, wakasema kuwa ni mtoto wa Mungu.

Na ili kuipa uthibitisho hadithi hii, ninayo haki ya kuwaona Masahaba kwamba wao vile vile waliasi amri ya Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.) katika mambo mengi, na miongoni mwa hayo, ni pale walipomzuia asiwaandikie maandiko ambayo yatawalinda wasipotee, na katika hayo ni pale walipomshutumu

153

kwa kumpa uamiri wa jeshi Usamah ibn Zaid, na wakakataa kutoka pamoja naye hata baada ya kifo cha Mtume (s.a.w.) na bila shaka Mjumbe wa Mwenyezi Mungu alimlaani kila aliyegoma (kutii amri hiyo) miongoni mwa watu aliowateua (kufuatana na Usamah).

Na katika mambo waliyoasi ni pale walipohitilafiana na kuzozana ndani ya Saqifa Bani Saidah juu ya suala la kumtawalisha Khalifa, na hawakumkubali Khalifa aliyetangazwa na Mjumbe wa Mwenyezi Mungu katika siku ya Ghadir Khum ambaye ni Ali ibn Abi Talib kama wanavyodai Mashia, na wanao ushahidi kutoka ndani ya vitabu vya hadithi vya Kisunni na vile vya historia (ushahidi ambao) hauwezekani kubadilishwa. Si hivyo tu bali walimuonya Binti yake Mtume Bibi Fatmah Az-Zahra mwanamke bora kuliko wanawake wote kwamba, wangelichoma moto nyumba yake kama watu wanaopinga baia (ya Abubakr) wasingetoka (ndani ya nyumba hiyo) kwa nguvu. Kwa hakika inaingia akilini mno kwa mtafiti muadilifu kuyakubali maandiko yaliyo wazi juu ya ukhalifa wa Ali ibn Abi Talib, kwa kuwa haingii akilini kwamba Mjumbe wa Mwenyezi Mungu afariki bila ya kumbainisha mtu yeyote (atakayechukua mahali pake), Mtume ambaye hakutoka nje ya Madina kwenda vitani au safarini isipokuwa huacha Khalifa. Na inaingia akilini pia kwamba, mtafiti muadilifu aikubali kauli ya Imam Sharafud-Din iliyomo ndani ya Kitabu chake kiitwacho "Al-Murajaat"pale alipomwambia Sheikh wa Az-Zahr Sheikh Salim Al-Bishri:

"Mmekubali, (Mwenyezi Mungu akupeni amani), ya kwamba Masahaba walichelewa kwenda kwenye jeshi la Usamah na wakawa wazito wakati huo pamoja na kuwa waliamuriwa wafanye upesi tena haraka, na mumekubali kwamba Masahaba walimshutumu Mtume s.a.w. kwa kumpa uamirijeshi Usamah, licha ya wao kusikia na kuyafahamu maelekezo ya Mtume kwa kauli na vitendo vya kumpa Usamah

154

uamirijeshi, na mumekubali juu ya kumtaka kwao Abu Bakr amuuzulu Usamah hata baada ya Mtume (s.a.w.) kuwa alichukizwa na shutma yao juu ya kumpa kwake uamiri na kwa sababu hiyo akatoka hali ya kuwa ana homa kajiinamia na kajifunika nguo, kisha akawakemea katika hotuba yake akiwa juu ya mimbari, kitu ambacho mumesema lilikuwa ni miongoni mwa matukio ya kihistoria, na kwamba Mtume alitangaza wazi wazi kuwa Usamah alikuwa anastahiki uamiri jeshi huo aliopewa na Mtume. Na mmekubali kuwa Masahaba walimtaka Khalifa (Abu Bakr) apuuze ujumbe huo (wa Kijeshi) alioutuma Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.) na aitengue bendera aliyoifunga Mtume kwa mkono wake Mtukufu, hali ya kuwa waliona ni jinsi gani Mtume alivyosisitiza kupelekwa haraka jeshi hilo na maelekezo mengi juu ya wajibu huo. Pia mumekubali kuhusu baadhi ya Masahaba aliowateua Mtume (s.a.w.) ndani ya jeshi hilo na kuwaamuru waende chini ya uongozi wa Usamah, walivyogoma.

Na mumeyakubali haya yote kama walivyoyaeleza waandishi na wakaafikiana watu wa hadithi na wahifadhi wa athari (kumbukumbu za Kiislamu) na mumesema kwamba wao walikuwa na udhuru kwa hilo. Mukhtasari wa yote muliyoyataja katika udhuru wao ni kwamba, wao katika mambo haya walitanguliza mbele maslahi ya Uislamu kwa mujibu wa mtazamo wao na siyo kama yalivyowajibisha maagizo ya Mtume, nasi hakuna tulichokidai (mahala hapa) zaidi ya haya."

Kwa maelezo mengine iwapo tutajiuliza, basi tutakuwa katika mzunguko ufuatao:

Je, wao katika ibada zao walikuwa wakizifanya kwa mujibu wa maagizo yote ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake au baadhi tu ya maagizo hayo? Ninyi mmechagua tamko la kwanza nasi tumechagua tamko la pili, basi kukiri kwenu sasa hivi kwamba hawakutii maamrisho hayo ya Mtume

155

kunakithibitisha kile tulichokichagua sisi. Na kuwa kwao na udhuru au kutokuwa na udhuru nijambo lililo nje ya maudhui inayochunguzwa kitu ambacho kiko wazi.

Na kwa kuwa imethibiti kwenu kwamba wao walitanguliza mbele maslahi ya Uislamu kuhusu jeshi la Usamah kama ulivyo mtazamo wao wa kutii maagizo ya Mtume, basi ni kwa nini hamsemi kwamba wao walitanguliza mbele maslahi ya Uislamu kuhusu Ukhalifa baada ya Mtume (s.a.w.) kama ulivyo mtazamo wao ili tu wayatii maagizo ya Ukhalifa yaliyoagizwa siku ya Ghadiri na mfano wa hayo.

Mmetoa udhuru kuhusu shutuma ya walioshutumu kupewa uamirijeshi Bwana Usamah, kwamba watu hao hapana kilichowafanya washutumu isipokuwa ni ule umri mdogo aliokuwa nao (Usamah) wakati walikuwepo miongoni mwao watu wazima na wazee, na mkasema, hakika nafsi za wazee na watu wazima hao hazikukubali kwa jumla na kwa maumbile yake kuongozwa na vijana basi ni kwa nini msitoe sababu kama hii hii kuhusu wale waliokataa kutii maagizo ya Ghadiri yanayompa uamiri (Ukhalifa) Ali juu ya watu wazima na wazee na hali ya kuwa ni kijana. Kwa hukumu ya dharura katika maelezo yao ni kwamba siku aliyokufa Mtume waliuona umri wake (Ali) kuwa ni mdogo kama walivyoouona umri wa Usamah kuwa ni mdogo siku Mtume (s.a.w.) alipomtawalisha juu yao katika umri ule, na kuna tofauti kubwa baina ya Ukhalifa na Uamirijeshi wa kikosi.

Iwapo nafsi zao zote zilikataa kuongozwa (na Usamah) kwa sababu ya umri mdogo katika kikosi kimoja, basi nafsi hizo zilikuwa na haki ya kukataa kuongozwa na mtu mwenye umri mdogo katika muda wote maishani mwake katika mambo yake yote ya dunia na akhera. Kwa msingi wa yale mliyoyaelezea kwamba nafsi za wazeee na watu wazima hao kwa tabia zake zinapinga kuongozwa na vijana wenye umri mdogo ni jambo

156

lisilokubalika ikiwa makusudio yenu ni kutoipa mpaka hukumu hii, kwani nafsi za waumini wazee waliokamilika katika imani zao hazipingi kumtii Mwenyezi Mungu na Mtume wake katika suala la kuongozwa na vijana wenye umri mdogo, wala katika mambo mengine, amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

"Naapa kwa Mola wako, kamwe hawawezi kuwa ni waumini mpaka wakufanye wewe kuwa ni muamuzi wao kwa yale wanayozozana baina yao, kisha wasiwe na uzito ndani ya nafsi zao katika yale uliyoyaamua na wasalimu amri mara moja".

"Nachochote anachokupeni Mtume basi kichukuweni na anachokukatazeni basi komeni."

Maelezo haya tumeyanukuu kutoka ndani ya kitabu kiitwacho Al-Murajaat (Barua Na.92).

3). Hadithi ya Bitanataini(vikundi viwili):

Amesema Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.):

"Mwenyezi Mungu hakumtuma Mtume yeyote wala hakumpa Ukhalifa Khalifa yeyote isipokuwa anakuwa na makundi mawili, kundi moja linamuamrisha mema na kumhimiza, na kundi jingine linamuamrisha shari na kumsisitiza juu ya shari hiyo, basi maasum ni yule aliye hifadhiwa na Mwenyezi Mungu.(2)

Hadithi hii ndani yake kuna dalili iliyowazi ya kwamba Masahaba walikuwa wamegawika mafungu mawili na tukitaka kuipanua maudhui hii bila shaka tutayakinisha zaidi kwamba baadhi ya Masahaba walikuwa wakimuelekeza Mtume kufanya yasiyokuwa mema.

1).Bitanah maanayake ni: Ni mtu aliye karibu mno kwa mtu mwingine; mwenye kujua siri zake.

2). Sahih Bukhari Juz. 4 uk. 173, Musnad Imam Ahmad Juz.Suk. 29.

157

Na mfano wa hilo ni hadithi aliyoiandika Al-Khatib ndani ya Tarikh Al-Baghadad katika Juzuu ya kwanza na Ibn Jariri amesema kuwa hadithi hiyo ni sahihi:-

Amesema: "Kuna watu miongoni mwa Maquraishi walikuja kwa Mtume (s.a.w.) wakasema. Ewe Muhammad bila shaka sisi nijirani zako na tumewekeana nawe ahadi, na kwa hakika kuna watu katika vijana wetu wamekujia wewe wala hawana haja ya Uislamu wala kutaka kujifunza, bali hakuna lolote ila wamekimbia kutoka katika miliki zetu." Mtume akamwambia Abubakr, Wasemaje? Akasema, "Wasemavyo ni kweli wao ni jirani zako na umewekeana nao ahadi." Uso wa Mtume ukabadilika kwa maelekezo aliyoyatoa Abubakr kisha Mtume akamwambia Omar, "Wasemaje, "Akasema, "Wasemavyo ni kweli, hakika wao nijirani zako na umewekeana nao ahadi." Basi uso wa Mtume ukabadilika kwa maelelekezo ya huyu Bwana mwingine.[15]

Na kisa hiki ni uthibitisho wa hadithi ya Bitanatain, kwani walichokiashiria Abubakr na Omar siyo katika kheri wala mema vinginevyo uso wa Mtume (s.a.w.) usingebadilika.

Imam Ahmad Ibn Hanbal ndani ya Musnad yake na Muslim ndani ya Sahih yake wameandika: "Nilimsikia Omar akisema, Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.) aligawa mgao fulani, basi mimi nikamwambia wako wanaostahiki mno kuliko hawa (ambao ni) Ahlus-Suffah.[16] Mjumbe wa Mwenyezi Mungu akasema, "Ninyi munanitaka nifanye uchafu na munanitaka niwe bakhili na mimi siyo bakhili. "[17]

158

Na hiki ni kisa kingine kilichowazi kwamba Umar Ibn Khatab hakuwa katika kikundi cha wanaoamrisha mema.

Bali yeye ni miongoni mwa wale wanaotaka uovu na kuamrisha ubakhili kwa mujibu wa maelezo yaliyomo ndani ya hadithi ya Mtume (s.a.w.).

4). Hadithi ya kushindania Ulimwengu:

Amesema Mtume (s.a.w.); "Mimi ni Mwenye kuwatangulieni na ni shahidi juu yenu, na bila shaka mimi namuapa Mwenyezi Mungu nakiangalia kidimbwi changu sasa hivi na kwa hakika nimepewa funguo za hazina ya ardhi nami namuapa Mwenyezi Mungu sihofii kwenu kwamba mtafanya ushirikina baada yangu lakini nawahofia kuwa mutashindania ulimwengu. Taz: Sahih Bukhari Juz.4 uk. 100 -101.

Amesema kweli mjumbe wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.), kwa hakika walishindania ulimwengu mpaka wakazichomoa panga zao kupigana na wakakufurishana wao kwa wao, na baadhi ya hawa masahaba walikuwa mashuhuri kwa kukusanya na kuhifadhi dhahabu na fedha wakati baadhi ya Waislamu wanakufa kwa njaa. Na wanahistoria kama vile Al-Mas-oodi ndani ya Muroojud-Dhahabi na Tabari na wengineo wanatusimulia kwamba utajiri wa Zuberi peke yake ulifikia dinari alfu khamsini na farasi alfu moja na watumwa alfu moja na alikuwa na milki nyingi za ardhi katika mji wa Basra, Kufah, Misri na miji mingineyo. Taz: Muroojud-Dhahabi cha Al-Mas-oodi Juz. 2 uk. 341.

Naye Abdur-Rahman Ibn Auf alikuwa na farasi mia moja , ngamia alfu moja, mbuzi elfu kumi na robo ya thamani ya mali yake iliyogawiwa kwa wakeze baada yakifo chake ilifikia themanini na nne Taz: Rejea iliyotangulia.

Naye Uthman Ibn Affan siku aliyokufa aliacha dinari laki moja na alfu khamsini ukitoa mifugo, ardhi na mashamba

159

yasiyokuwa na idadi. Ama Zaid ibn Thabiti yeye aliacha dhahabu na fedha ambazo zilikuwa zikivunjwa kwa mashoka mpaka mikono ya watu ikawa na malengelenge.

Hii ni baadhi ya mifano michache, na ndani ya historia kuna ushahidi mwingi ambao hatutaki kuingia katika uchunguzi wake sasa hivi na tunatosheka na kiasi hiki cha dalili juu ya ukweli wa ile hadithi kwamba, wao Masahaba dunia iliwapambia machoni mwao na yakawafurahisha mapambo yake, wakajilimbikizia mali nyingi juu ya hesabu ya Waislamu wanyonge.

160

MAONI YA BAADHI YA MASAHABA KUHUSUWENZAO

1). Ushahidi wao wenyewe juu ya kuibadilisha Sunna ya Mtume

Imesimuliwa toka kwa Said Al-Khudri amesema:

"Mjumbe wa Mwenyezi Mungu alikuwa akitoka siku ya Idi Al-Fitri naAl-Adh-ha kwenda kuswali, basi kitu cha mwanzo alichokuwa akikianza ni sala kisha husimama mbele ya watu, na hali yakuwa wao wamekaa katika safu zao, basi huwapa mawaidha na kuwausia na kuwapa muongozo na endapo anataka kukatisha somo hulikatisha, au kuamrisha kitu huamrisha, kisha huondoka. Abu Said amesema, watu waliendelea kufanya hivyo mpaka nilipotoka pamoja na Mar-wan akiwa ndiyo Amiri wa Madina katika siku kuu yaAl-Adh-Ha au Al-Fitri, basi pindi tulipofika mahali pa kusalia, hapo kulikuwa na mimbari aliyoijenga Kathir ibn As-Sili, bwana Mar-wan akataka kupanda kwenye mimbari hiyo kabla ya kuswali, mimi nikaivuta nguo yake naye akaivuta kisha akapanda akahutubia kabla ya kuswali, basi mimi nikamwambia, "Wallahi mumebadilisha",   akasema,   "Ewe,   Baba   Said yamekwishaondoka uyajuwayo." Akasema, "Kwa hakika watu walikuwa hawakai nasi baada ya kusali ndiyo maana tumeifanya Khutba kabla ya kusali." (Taz: Sahihi Bukhari Juz.l uk.122

161

katika Kitabul-Idain Mlango wa Al-Khuruju Ilal-Musala Bighair Mimbar.

Kwa hakika nimefanya uchunguzi juu ya sababu zilizokuwa zikiwafanya Masahaba hawa waigeuze Sunna ya Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.), nikagundua kuwa, Banu Umayyah na wengi wao wakiwa ni miongoni mwa Masahaba wa Mtume (s.a.w.), wakiongozwa na Muawiyah ibn Abi Sufiyan (mwandishi wa Wahyi) kama wanavyomwita wenyewe, huyu alikuwa akiwalazimisha watu wamtukane Imam Ali ibn Abi Talib, na wamlaani katika mimbari msikitini, kama walivyoeleza hayo wanahistoria.

Muslim ameandika ndani ya Sahih yake katika mlango wa Fadhail Ali ibn Abi Talib kama ifuatavyo: Muawiyah aliwaamuru wafanyakazi wake katika kila mji kuifanya laana hiyo ya (kumlaani Imam Ali a.s.) kuwa ni sunna inayosemwa na makhatibu juu ya mimbari, na pindi baadhi ya Masahaba walipoona uchungu kutokana na tendo hilo na wakamkemea, Muawiyah aliamuru wauawe na wachomwe moto. Miongoni mwa waliouawa ni sahaba mashuhuri Bwana Hujru ibn Adiyi Al-Kindi na j amaa zake na baadhi yao walizikwa hai kwa sababu tu ya wao kukataa kumlaani Imam Ali na kupinga jambo hilo.

Naye Abul-ala Al-Maududi ameandika ndani ya Kitabu chake kiitwatocho, Al-khilafatu Wal-Mulku - "Ukhalifa na ufaime" Akimnukuu Al-Hasan Albasri amesema:-

"Mambo manne alikuwa nayo Muawiyah, lau asingekuwa nayo isipokuwa jambo moja, basi lingetosha kuwa ni lenye kumwangamiza.

1). Kuchukua Ukhalifa bila ushauri wakati wapo Masahaba bora zaidi kuliko yeye.

2). Kumrithisha Ukhalifa mwanawe (Yazid) aliyekuwa

162

mlevi, anaye kuvaa hariri na kupiga zumari.

3). Kumfanya Ziyad kuwa ni mtoto wake wakati Mjumbe wa Mwenyezi Mungu amesema, "Mtoto ni wa kitanda na yule mzinifu mwanaume atapatajiwe".

4. Kumuua Hujru ibn Adiyi Al-Kindi na jamaa zake Hujru, basi Ole wake kwa kumuua Hujru, Oh!! Ole wake kwa kumuua Hujru na jamaa wa Hujru. Taz: Abul-Aala Al-Maudud, Kitabu Al-Khilafatu Wal-Mulku uk. 106.

Baadhi ya waumini miongoni mwa Masahaba walikuwa wakikimbia kutoka Misikitini baada ya kumaliza kusali ili tu wasijehudhuria Khutba ambayo itahitimishwa kwa kumlaani Ali (a.s.) na watu wa nyumba yake, na kwa ajili hii basi, Banu Umayyah waliibadilisha Sunna ya Mjumbe wa Mwenyezi Mungu wakatanguliza Khutba kabla ya Sala ili watu wote wahudhurie na walazimike kusikiliza japo hawapendi.

Ajabu kubwa kwa Masahaba hawa ambao walikuwa hawaoni vibaya kubadili Sunna ya Mtume (s.a.w.) na hata hukmu za Mwenyezi Mungu ilimradi tu watimize malengo yao machafu, chuki yao iliyojificha na tamaa zao mbaya, na wakamlaani mtu ambaye Mwenyezi Mungu amemuondolea uchafu na kumtakasa mno na akawajibisha kumuombea Rehma kama anavyoombewa Mjumbe wake. Vile vile Mwenyezi Mungu na Mtume wake wamewajibisha kumpenda mpaka Mtume (s.a.w.) amesema, "Kumpenda Ali ni dalili ya imani na kumbughudhi ni dalili ya unafiki." Taz: Sahih Muslim Juz. 1 uk.61.

Lakini Masahaba hawa walibadili na kugeuza na wakasema tumesikia natumeasi, na badala ya wao kumuombea Rehma Ali a.s.kumpenda na kumtii, wao walimtukana na kumlaani kwa muda wa miaka sitini kama inavyoelezea ndani ya vitabu vya historia.

163

Basi kama watu wa Musa (a.s.) walifanya njama dhidi ya Harun (a.s.) na wakakaribia kumuua, hakika baadhi ya Masahaba wa Muhammad (s.a.w.) walimuua Harun wake Ali a.s. na wakawafuatilia wanawe na wafuasi wake kila upande na kila mji, wakayafuta majina yao katika diwani na wakazuwia mtu yeyote asiitwe kwajina lake, Hawakutosheka na hayo bali waliwalazimisha Masahaba wenye utakaso wa moyo wafanye hayo kwa nguvu na dhulma.

Nami Wallahi husimama hali yakuwa nimechanganyikiwa sijuwi la kufanya, pale ninaposoma Sihahi zetu (vitabu vyetu) na mambo yaliyoandikwa humo juu ya mapenzi ya Mtume kwa nduguye na ibn ami yake Ali (a.s.), na jinsi alivyomtanguliza mbele kuliko Sahaba yeyote mpaka Mtume akasema; "Wewe (Ali) kwangu mimi unayo daraja ya Harun kwa Musa, isipokuwa hapana Nabii baada yangu." Taz: Sahih Bukhari, Juz. 2 uk. 305, Muslim Juz.2 uk.360, Mus -TadrakyaAl-HakimJuz.3 uk. 109.

Pia alimwambia: "Wewe unatokana na mimi, nami natokana nawe" Taz: Sahih Bukhari Juz. 2 uk. 76, Sahih Tirmidh Juz. 5 uk. 300, Sunan ibnMajah Juz. 1 uk. 44. Na alisema Mtume:

"Kumpenda Ali ni dalili ya imani na kumbughudhi ni dalili ya unafiki." Taz: Sahih Muslim Juz. 1 uk. 61, Sunan An-Nasai Juz. 6 uk. 116, Sahih Tirmidh Juz. 8 uk. 306. Na alisema Mtume, "Mimi ni mji wa elimu na Ali ndiyo mlango wake." Taz. Sahih Tirmidhi Juz. 5 uk. 201, Mus-TadrakyaAl-Hakim Juz. 3 uk. 126.

Na alisema: "Ali ni Walii wa kila Muumini baada yangu"

Taz: Musnad ImamAhmadJuz.5 uk.25, Mus-TadrakAl-Hakim Juz. 3 uk.134, Sahih Tirmidh Juz. 5 uk.296.

Pia Mtume (s.a.w.) alisema: "Yeyote ambaye Mimi nilikuwa mtawala wake, basi huyu hapa Ali ni Mtawala wake, Ewe Mwenyezi Mungu mtawalishe atakaye mtawalisha na umpinge atakayempinga." Taz: Sahih Muslim Juz.2 uk.362 MustadrakAl-HakmJuz. 3 uk. 109, MusnadAhmadJuz. 4 uk.28.

164

Na lau tungetaka kusimulia fadhila ambazo Mtume (s.a.w.) amezitaja kumhusu Ali (a.s.), na ambazo wameziandika wanachuoni wetu hali yakuwa wamekiri juu ya usahihi wake, basi jambo hilo lingelazimu kuandika kitabu maalum. Basi ni vipi Masahaba walijifanya kuwa hawayajui maagizo haya na wakamtukana Ali na kumfanyia uadui, wakamlaani juu ya mimbari na ni vipi wakampiga vita na kisha kumuua.

Hakika Mimi najaribu kupata nanma ya kuwatakasa watu hawa, lakini sipati isipokuwa nawaona ni watu walioipenda dunia na kuishindania, au ni unafiki au waliritadi na kurudi nyuma kwa visigino. Ninajaribu kuwabebesha jukumu hili wale Masahaba wasio na hadhi yeyote na baadhi ya wanafiki,'lakini inasikitisha sana kwamba hawa waliofanya haya wanahesabiwa kuwa ni miongoni mwa masahaba wakubwa, wenye hadhi na Mashuhuri, kwani wa kwanza kutoa onyo la kuiunguza nyumba ya Ali (a.s.) na waliomo ni Omar ibn Khatab, na wa kwanza kumpiga vita (Ali a. s.) ni Zuberi. Ummul-Muuminin Aisha Bint Abubakr, Muawiyah ibn Abi Sufiyan na Omr Ibn Al-As na wengi mfano wa hawa.

Kwa hakika mimi nastaajabu sana na huenda kustaajabu kwangu kusifikie mwisho kama anavyoniunga mkono juu ya hili kila mwanafikra aliyehuru na mwenye akili (ya kuchambua mambo) ni vipi wanachuoni wa Kisunni wamekubaliana juu ya uadilifu wa Masahaba wote na kuwaombea radhi na pia kuwaombea Rehma wote, hawamtoi yeyote miongoni mwao kiasi kwamba baadhi ya wanachuoni hao wamesema "Mlaani Yazid wala usizidishe (chochote)." Basi ana nafasi gani Yazid kutokana na maafa hayo (aliyoyasababisha) ambayo hayakubaliwi na Dini wala,akili?

Mimi siridhiki na Ahlus-Sunnah Wal-Jamaa, ikiwakweli wao wanafuata Sunna ya Mtume, basi ni vipi wanamhukumu kuwa ni Muadilifu mtu ambaye Qur'an na Sunna (ya Mtume)

165

vimemhukumu juu ya uovu wake, kuritaddi kwake na kukufuru kwa mtu huyo, na hapana shaka kwamba mjumbe wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.) amesema, "Yeyote mwenye kumtukana Ali hakika amenitukana mimi, na yeyote atakayenitukana mimi bila shaka amemtukana Mwenyezi Mungu, na mwenye kumtukana Mwenyezi Mungu atamtupa kifudi fudi motoni." (Taz: Mus-Tadrak-Alhakim Juz. 3 uk. 121, Khasaisun-Nasai uk. 24, Musnad Imam Ahmad Juz.6 uk. 32, Manaqib-Alkhawarzami uk.81,

Ariyad-Dhu Anadhrah ya Tabari juz. 2 uk. 219, Tarikh-As-Suyutuk. 73.

Haya ndiyo malipo ya mtu atakaye mtukana Ali (a.s.), basi unamfikiriaje mtu atakayemlaani na kumpiga vita? Wana

hali gani wanachuoni wetu kuhusu ukweli wote huu au kuna vifuniko kwenye nyoyo?

Na useme. Ewe Mola! najikinga kwako uniepushe na wasiwasi wa mashetani, na ninajikinga kwako wasinifikie.

2). Masahaba hata Swala waliibadilisha:

Amesema Anas ibn Malik: "Hapana kitu nilichokifahamu vyema miongoni mwa mambo yaliyokuwepo katika zama za Mtume (s.a.w.) kuliko Sala, akasema, Je, siyo kwamba mumepoteza vitu fulani ndani yake.

Na Az-Zuhri amesema, niliingia kwa Anas ibn Malik huko Damscus nikamkuta analia, nikamwambia, "Ni Jambo gani linalokuliza,?" Akasema, hapana kitu nikijuacho vyema miongoni mwa vitu nilivyovidiriki isipokuwa hii Sala ambayo imekwishapotezwa. (Taz: Sahih Bukhari Juz. 1 uk. 74).

ili mtu yeyote asije dhani kwamba Taabiina (waliofuata baada ya Masahaba) ndiyo waliobadilisha mambo yaliyobadilishwa baada ya fitna hizo na vita, napenda nikumbushe kwamba mtu wa kwanza aliyeibadilisha Sunna ya Mtume ndani ya Sala ni Khalifa wa Waislamu Uthman ibn

166

Affaan na vile vile Ummul-Muumina Aisha.

Wameandika Masheikh wawili Bukhari na Muslim ndani ya Sahih zao ya kwamba: Mjumbe wa Mwenyezi Mungu alisali rakaa mbili Mina, na Abubakr baada ya Mtume, na Omar baada ya Abu Bakr na Uthman mwanzoni mwa Ukhalifa wake kisha baadaye alisali rakaa nne. (Taz: Sahih Bukhari Juz.2 uk.154 Sahihi Muslim Juz. 1 uk.260).

Vile vile Muslim ameandika ndani ya Sahih yake:

Amesema Az-Zuhri, "Nilimwambia Ur-wah, ana nini Aisha mbona anakamilisha Sala katika Safari"? akasema, "Yeye ameawili (amebadilisha) kama alivyoawili Uthman." (Taz. Sahih Muslim Juz.2 uk. 143 Kitabu Salatil-Musafirina).

Sub-hanallah!! Hivi kuna Taawili yoyote inayofuta Sunna ya Mtume kuliko hii na mfano wa hii miongoni mwa Taawili? Je, kuna mtu yeyote atakayemlaumu Abu Hanifa, au kumlaumu mmoja wa Maimamu wa Madhehebu ya watu waliogeuza, wakahalalisha na kuharamisha kufuatana na Taawili zao na Ij-tihadi zao hali yakuwa katika kufanya hivyo wanafuata Sunna za Masahaba hawa?

Na Umar Ibn Khatab alikuwa akifanya Ij-tihadi na Taawili mbele ya nasi zilizowazi katika Sunna za Mtume ball mbele ya maandiko yaliyowazi ya Qur'an Tukufu, basi anahukumu kwa mujibu wa maoni yake kama ilivyo kauli yake, "Mut-a mbili zilikuweko katika zama za Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, nami nazizuwia na nitatoa adhabu kwa mwenye kuzitenda.

Na anasema (Umar) kumwambia mtu mwenye Janaba na hakupata maji ya kuoga, "Usiswali" ajabu!! licha ya kuwepo kauli ya Mwenyezi Mungu ndani ya Sura Al-Maidah isemayo;

"Na iwapo hamtapata maji, basi fanyeni Tayamam kwa udongo safi". (Qur., 5:6)

167

Bukhari ameandika ndani ya Sahihi yake katika mlango usemao, pindi mtu mwenye Janaba akiichelea nafsi yake Amesema:- "Nilimsikia Shaqiq ibn Salamah akisema, nilikuwa mbele ya Abdullah na Abu Musa, basi Abu Musa akamwambia Shaqiq, waonaje Ewe Abu Abdur-Rahman iwapo mtu akipatwa na Janaba na akakosa maji atafanya nini? Abdullah akasema, Hawezi kuswali mpaka apate maji. Abu Musa akasema, basi utaifanya nini kauli ya Ammar wakati Mtume (s.a.w.) alipomwambia ukiwa na Janaba na hukupata maji inakutosha upige mapigo mawili (juu ya udongo), Mtume akamfunza kutayamam. Abdullah akasema, Je, wewe huoni kwamba Umar hakutosheka na kauli hiyo. Abu Musa akasema, haya basi tuachane na kauli ya Ammar sasa utafanya nini kuhusu aya hii (Qur.5:6)?   Abdullah   hakufahamu   akisemacho (alichanganyikiwa) hatimaye akasema, bila shaka sisi tunaona lau tutawaruhusu kufanya hivyo kuna mashaka kwamba itakapokuwa kuna hali ya baridi kwa mmoja wao ataacha kutumia maji na atatayamamu. Mimi nikamwambia Shaqiq, Kilichomchukiza Abdallah ni hiki. Akasema: "Ndiyo". (Taz:

Rudi nyuma Yaliyomo endelea