Rudi nyuma Yaliyomo endelea

Kwa hakika ninapoeleza baadhi ya mambo waliyotenda baadhi ya Masahaba kwa Mjumbe wa Mwenyezi Mungu nabakia ni mwenye kushangaa tena mwenye kuchanganyikiwa, kinachonishangaza si tabia za Masahaba tu kumwelekea Mtume lakini mtazamo wa wanachuoni wa Kisunni ambao siku zote unatuonesha kuwa Masahaba wote wako kwenye haki, na haiwezekani kuwakosoa kwa namna yoyote ile, kwa ajili hiyo wanamzuia mwenye kutafiti kuufikia ukweli na anabakia anahangaika ndani ya fikra zinazopingana.

Zaidi ya hayo yaliyotangulia ninaleta baadhi ya mifano ambayo itatupatia picha halisi juu ya Masahaba hawa na hapo tutaufahamu msimamo wa Mashia kuhusu Masahaba.

Bukhari ameandika ndani ya sahihi yake Juz. 3 uk. 47 miango wa subira juu ya maudhi, na kauli ya Mwenyezi Mungu mtukufu isemwayo "Bila shaka wenye kusubiri watatekelezewa malipo yao" kutoka katika kitabul-adabi amesema, "Ametusimulia Aamash amesema, "Nimemsikia Shaqiq anasema, Abdallah amesema, Mtume (s.a.w.) aligawa mgao kama baadhi ya migao aliyokuwa akigawa, basi mtu mmoja

131

miongoni mwa maansari akasema namuapa Mwenyezi Mungu hakika mgao huu haukukusudiwa kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, mimi nikasema kwa hakika mimi nitamwambia jambo hili Mtume (s.a.w.), basi nikamfuata Mtume hali ya kuwa yuko kati ya Masahaba wake nikamkabili nikamwambia, jambo hili lilimuumiza Mtume, uso wake ulibadilika na akakasirika mpaka nikatamani laiti nisingemwambia kisha Mtume akasema kwa hakika Musa aliudhiwa zaidi kuliko hivyo lakini alisubiri."

Vile vile Bukhari ameandika katika kitabu hicho hicho yaani Kitabul-Adab katika Babut-Tabassum Wad-dhahak.

Amesema, "Ametusimulia Anas 'ibn Malik amesema, nilikuwa natembea pamoja na Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.) hali yakuwa amejifunika shuka ya Kinajirani yenye pindo nene, basi bedui mmoja akakutana na Mtume akamvuta shuka yake kwa nguvu sana, Anas akasema: Niliangalia kwenye bega la Mtume (s.a.w.) nikaliona limeathirika kutokana na pindo la shuka kwa sababu ya kuvutwa kwa nguvu sana alikofanya yule Bedui, kisha bedui yule akasema. Ewe Muhammad toa amri nipewe mali ya Mwenyezi Mungu uliyonayo, basi Mtume alimgeukia (kumtazama) kisha akacheka halafu akaamuru apewe."

Kama ambavyo Bukhari ameandika ndani ya Kitabul-Adab katika mlango uitwao "Asiyewakabili wafu kwa lawama" Amesema: Bibi Aisha amesema, "Mtume (s.a.w.) alifanya jambo fulani na akaliruhusu (lifanywe), baadhi ya watu hawakulifanya. Habari hiyo ikamfikia Mtume (s.a.w.), basi akatoa hotuba akamtukuza Mwenyezi Mungu kisha akasema, wana nini watu walioacha kufanya kitu ninachokifanya mimi, namuapa Mwenyezi Mungu kwa hakika mimi namfahamu zaidi Mwenyezi Mungu kuliko wao nami namcha zaidi kuliko wao!..."

132

Naapa, kwa hakika wale wanaoitakidi kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.) matamanio yanampindisha na kumpotosha njia ya haki, akagawa mgao ambao hakusudii radhi ya Mwenyezi Mungu bali anafuata matamanio yake na vile apendavyo, na wale ambao wanaacha kufanya mambo aliyoyafanya Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, hali yakuwa wanaitakidi kuwa wao ni wacha Mungu mno na wanamfahamu zaidi Mwenyezi Mungu kuliko Mjumbe wake, kiasi kwamba baadhi ya watu wanawaweka katika daraja la Malaika na kuhukumu kwamba wao ni viumbe bora baada ya Mjumbe wa Mwenyezi Mungu na kwamba Waislamu wanatakiwa kuwafuata na kuziandama sera zao, si kwa lolote isipokuwa tu kwa kuwa ni Masahaba wa Mjumbe wa Mwenyezi Mungu. Lakini watu hawa hawastahiki kabisa utukufu huo.

Na hali hii (kwa kweli) inapingana na Masunni ambao hawamsalii Mtume (s.a.w.) na kizazi chake isipokuwa huongeza juu yao Masahaba wote, wakati ambapo Mwenyezi Mungu Mtukufu amekwisha kukitambulisha cheo chao (Mtume na kizazi chake) na akawapa daraja yao kisha akawaamuru (Masahaba) wamsalie Mtume wake na watu wa nyumba yake waliotakasika ili kuwafanya wawe watiifu na wanyenyekevu na waitambue daraja ya watu hawa mbele ya Mwenyezi Mungu, basi (kama ni hivyo) ni kwa nini sisi tunawaweka (Masahaba) juu kuliko daraja yao na tunawalinganisha na watu ambao Mwenyezi Mungu amewatukuza na kuwaboresha juu ya walimwengu wote?

Hebu niwache nihitimishe (kwa kueleza) kwamba, Banu Ummayyah na Banu Abbas ambao waliwafanyia uadui watu wa nyumba ya Mtume, wakawatenga, kuwatawanisha na kuwauwa wao na wafuasi wao, waliitambua maana halisi ya daraja na ubora mkubwa wa Ahlul-Bait. Basi ikiwa Mwenyezi Mungu haikubali sala ya Muislamu ila kwa kuwasalia wao, ni kwa nini basi wanautetea uadui wao na kupotoka kwao dhidi

133

ya Ahlul-Bait? Na kwa ajili hiyo utawaona wamewalinganisha Masahaba kwa Ahlul-Bait (katika kuwasalia) ili kuwapotosha watu waone kuwa Masahaba na Ahlul-Bait ni sawa tu katika daraja. Na hasa iwapo tutafahamu ya kwamba mabwana wao na wakubwa wao ni baadhi ya Masahaba ambao waliwaajiri watu wanyonge wa akili miongoni mwa Masahaba wa Mjumbe  wa Mwenyezi Mungu au miongoni mwa taabiina ili tu wasimulie hadithi za uongo zinazohusu fadhila za Masahaba na hasa wale waliofaulu kukalia kiti cha Ukhalifa na wakawa moja kwa moja ndiyo sababu ya wao Banu Umayyah na Banu Abbas kuufikia utawala na kufanya wapendavyo dhidi ya Waislamu. Historia ni shahidi mwema juu ya haya niyasemayo, kwani Umar Ibn Al-Khatab ambaye ni mashuhuri kwa kuwaadhibu magavana wake kwa kiasi cha dhana tu tunamuona ni mpole mno kwa Muawiyyah Ibn Abi Sufiyan wala hamuadhibu kabisa. Na huyu Muawiyyah alitawalishwa na Abu Bakr, na Umar alipokuja akamkubali kwa muda wote wa uhai wake na wala hakuthubutu hata kumkemea au kumlaumu licha ya mashitaka ya watu wengi waliokuwa wakienda kumshitakia kuhusu Muawiyah na wakimwambia, "Kwa hakika Muawiyah anavaa dhahabu na hariri vitu ambavyo Mtume wa Mwenyezi Mungu ameviharamisha kwa wanaume." Basi Umar alikuwa akiwajibu, "Mwacheni kwa kuwa yeye ni Kisra wa Waarabu." Hivyo basi Muawiyah aliendelea kutawala zaidi ya miaka ishirini na hakuna yeyote aliyethubutu kumkosoa wala kumuuzulu, na alipotawalia Uthman Ukhalifa wa Waislamu alimuongezea (Muawiya) madaraka mengine yaliyomuwezesha kuupora utajiri wa Waislamu, na kuchukua uongozi kwa nguvu, kisha kufanya apendavyo na kuwalazimisha Waislamu wale kiapo cha utii kwa mwanawe Yazid aliyekuwa muovu na mlevi, na hiki ni kisa kingine kirefu ambacho sikukikusudia kukieleza kwa urefu ndani ya kitabu hiki, lakini jambo muhimu ni kutambulisha mwenendo wa masahaba hawa ambao walikalia Ukhalifa na moja kwa moja wakaandaa kusimama kwa dola ya Bani

134

Umayyah ili kuwaridhisha Maquraish ambao hawakutaka Utume na Ukhalifa uwe ndani ya Bani Hashim.

Kwa maelezo zaidi soma:

(1) Al-Khilafatu Wal-Mulk; Abul Aala-al-Maududi.

(2) Yaumul-Islam: AhmadAmin.

Kwa hakika dola ya Banu Umayyah ina haki bali ni wajibu wake iwashukuru wale wote ambao waliiandalia utawala, na shukurani ya chini kabisa ni kuajiri wapokezi wa hadithi wa kulipwa watakaosimulia fadhila za Mabwana zao na wakati huo huo kuwakweza zaidi kuliko Makhasimu wao ambao ni Ahlul-Bait kwa sifa na ubora wa aina mbali mbali ambao Mwenyezi Mungu anashuhudia kuwa, (sifa hizo na ubora huo waliopewa hao Masahaba) iwapo utaufanyia utafiti kwa mujibu wa dalili za kisheria, kiakili na kimantiki hapana chochote cha kutajwa kitakachobakia, isipokuwa tu kama akili zetu zitakapokuwa na kasoro tukaamini mambo yanayopingana.

Kwa mfano, tunasikia mengi juu ya uadilifu wa Umar ambao umevuka mpaka hadi ikasemwa "Umekuwa muadilifu mno mpaka umelala" naimesemwa pia kuwa, "Umar amezikwa wima ili uadilifu wake usijekufa pamoja naye". Basi yalivyo ya Umar kuhusu uadilifu unaweza kusimulia ukasimulia-ukasimulia.... .hulaumiwi.

Historia sahihi inatueleza kwamba katika mwaka wa ishirini Hijiriyah ilipomlazimu kutoa, yeye hakufuata sunna ya Mtume wa Mwenyezi Mungu, wala hakufuata mipaka yake kwani Mtume (s.a.w.) aliweka usawa baina ya Waislamu wote katika mgao huo hakumboresha yeyote juu ya mwingine, na Abubakr alimfuata Mtume kwa jambo hilo muda wote wa Ukhalifa wake. Lakini Umar Ibn Al-Khatab alianzisha njia mpya akawaboresha (Waislamu) waliosilimu mwanzoni juu ya wengine, na akawaboresha Muhajirina miongoni mwa Maquraishi juu

135

ya Muhajirina wengine. Akawatanguliza Muhajirina wote juu ya Maansari wote, na aliwafadhilisha Waarabu juu ya wasiokuwa Waarabu na alimboresha mtu huru juu ya mtumwa[4] na akaliboresha kabila la Mudhar juu ya kabila la Rabiah. akafaradhisha kabila la Mudhar wapewe mia tatu na Rabia mia mbili[5] na aliwaboresha kabila la Ausi juu ya Khazraj. [6]

Basi uko wapi usawa na uadilifa Ewe mwenye akili? Na tunasikia juu ya elimu ya Umar Ibn Al-Khatab mambo mengi yasiyo na idadi mpaka imesemwa kwamba yeye ndiye mjuzi mno kuliko Masahaba (wengine) na imesemwa kuwa yeye alimuwafiki Mola wake katika mengi miongoni mwa maoni yake ambayo Qur'an ikishuka kuyaunga mkono katika aya nyingi ambazo Umar na Mtume (s.a.w.) walitofautiana.

Lakini historia sahihi inatujulisha kwamba Umar hakuiafiki Qur'an hata baada ya kushuka kwake, pale alipoulizwa na Sahaba mmoja katika zama za Ukhalifa wake akasema: "Ewe Amirul-Muuminina mimi nimepatwa na janaba lakini sikupata maji", Umar akamwambia, "Usisali". Hapo Ammar Ibn Yasir akalazimika kumkumbusha kutayamam [7]lakini Umar hakukinaika kwa hilo na akamwambia Ammar "Tutakubebeshajukumu kwa yale uliyojibebesha."

Basi yu wapi Umar yeye na aya ya kutayamam iliyoteremshwa ndani ya kitabu cha Mwenyezi Mungu na iwapi Elimu yake na Sunna ya Mtume (s.a.w.) ambaye amewafundisha namna ya kutayammam kama ambavyo amewafundisha (namna ya) kutawadha. Na Umar yeye mwenyewe mara nyingi anakiri katika rnatukio kadhaa kwamba yeye si mjuzi, bali watu wote ni wajuzi kuliko yeye hata yule mwanamke mwenye mimba, na

136

akisema mara nyingi, "Lau si Ali, basi Umar angeliangamia", na alifikwa na mauti akafa na hakuwahi kutambua hukumu ya "Al-Kalalah" ambayo alihukumu kwa hukumu nyingi tofauti tofauti kama inavyoshuhudia historia.

Vile vile tunasikia mambo mengi juu ya uhodari wa Umar na ushujaa wake na nguvu zake mpaka imesemwa kwamba Maquraishi waliogopa pindi Umar aliposilimu, na nguvu ya Waislamu iliimarika kwa kusilimu kwake, na imesemwa kwamba Mwenyezi Mungu aliupa nguvu Uislamu kupitia kwa Umar Ibn Al-Kataab, na imesemwa kuwa Mjumbe wa Mwenyezi Mungu hakudhihirisha wazi wito wake isipokuwa baada ya kusilimu Umar.

Lakini historia thabiti na sahihi haituoneshi chochote juu ya uhodari huu na ushujaa, wala hakuna mtu yeyote miongoni mwa watu mashuhuri au hata watu wa kawaida ambao Umar Ibn Khataab aliwauwa katika makabiliano ya ana kwa ana au katika vita kama vile Badr au Uhud au Khandaq na vinginevyo, bali kinyume chake ndiyo sahihi, na historia inatusimulia kwamba, yeye alikimbia pamoja na wengine waliokimbia katika vita ya Uhud na vile vile alikimbia siku ya (vita ya) Hunain. Pia Mtume (s.a.w.) alimtuma ili akaufungue (alete ushindi) katika mji wa Khaibar na alirudi bila ushindi na hata katika vikosi vidogo vidogo ambavyo alishiriki, hakuwa kiongozi bali aliongozwa na cha mwisho ni kile cha Usamah ambacho yeye alikuwa mwenye kuamrishwa chini ya uongozi wa kijana Usamah ibn Zaid.

Basi yako wapi madai ya uhodari na ushujaa wa Umar (ukilinganisha) na ukweli huu unaoonekana wazi? Tunasikia mambo mengi juu ya ucha Mungu wa Umar na namna alivyokuwa akilia kwa kumuogopa Mwenyezi Mungu, mpaka imesemwa kwamba yeye alikuwa anakhofu kuwa Mwenyezi Mungu atamuadhibu japo itatokea nyumbu akaanguka njiani

137

kutokana na (Umar) kutomtengenezea nyumbu huyo njia nzuri ya kupita huko Iraq.

Lakini masimulizi ya historia yaliyothibiti yanatueleza kwamba, Umar alikuwa mkali tena mgumu (wa tabia) haoni vibaya na haogopi, kwani akimpiga yeyote aliyemuuliza suali juu ya aya moja tu ya kitabu cha Mwenyezi Mungu mpaka humtoa damu pasina kosa lolote alilolifanya mtu huyo, bali zaidi ya hapo mwanamke akiharibu ujauzito wake kwa kiasi tu cha kumuona Umar kutokana na woga na tisho alilokuwa nalo Umar.

Na ni kwa nini Umar hakuona vibaya pale alipounyoosha upanga wake kumuonya kila yule atakayesema kuwa (Mtume) Muhammad amekufa, na akaapa kwa Mwenyezi Mungu kuwa Mtume hakufa bali kaenda kuzungumza na Mola wake kama alivyofanya Musa ibn Imran, na akaonya kuwa yeyote atakayesema kuwa Mtume amekufa ataikata shingo yake[8] Basi ni kwanini asimukhofu Mwenyezi Mungu (kutokana na tendo hili)?

Na ni kwanini asione kuwa ni vibaya wala asimukhofu Mwenyezi Mungu juu ya onyo lake la kutaka kuiunguza kwa moto nyumba ya Fatmah Az-Zahra iwapo tu hawatatoka ndani ya nyumba hiyo kwenda kufanya Baia (kula kiapo cha utii) watu waliopinga Baia ya Abu Bakr,[9] haliyakuwa aliambiwa kuwa ndani ya nyumba hiyo yumo Fatmah, basi yeye alijibu akasema, "Hata kama yumo Fatmah" (tutaichoma moto).

Umar alithubutu kuwa dhidi ya kitabu cha Mwenyezi Mungu na Sunna ya Mtume wake, akahukumu katika zama za Ukhalifa wake hukumu zinazokwenda kinyume na Qur'an na Sunnah Tukufu ya Mtume[10]

138

Ukowapi uchamungu wake ukiulinganisha na matukio ya kweli tena yanayoumiza moyo Enyi! waja wema wa Mwenyezi Mungu???

Kwa hakika nimemtaja Sahaba huyo mkubwa tena mashuhuri kama mfano tu na nimeacha mambo mengi kusudi nisirefushe maelezo, lakini lau ningetaka kufanya kwa upana ningejaza vitabu vingi, bali kama nilivyosema ninataja hivi kama mfano na siyo yote.

Maelezo niliyoyataja ni sehemu ndogo tu inayotupatia dalili iliyowazi juu ya hali halisi ya Masahaba (walivyo) na pia msimamo unaopingana wa wanachuoni wa Kisunni, kwani wao wanawazuia watu kuwakosoa na kuwatilia mashaka na wakati huo huo ndani ya vitabu vyao wanasimulia mambo yanoyoleta shaka na tuhuma kwa Masahaba. Na lau wanachuoni wa Kisunni wasingetaja mfano wa mambo kama haya wazi wazi yanayochafua na kutia doa heshima ya Masahaba katika uadilifu (usemwao) kuwa wanao, hakika wangetupumzisha na taabu hii ya mkanganyiko.

Kwa hakika mimi naukumbuka mkutano wangu pamoja na mwanachuoni mmoja katika mji Mtukufu wa Najafa itwaye Sayyid Asad Haidar ambaye ndiye mtunzi wa kitabu kiitwacho, "Al-Imamu S-Sadiq Wal-Madhahibul-Arbaa" na katika mkutano huo tulikuwa tukizungumzia juu ya Usunni na Ushia, basi akanisimulia kisa cha mzazi wake ambaye alipokuwa Hijja alikutana na mwanachuoni wa Kitunisia miongoni mwa wanachuoni wa Zaitunah, na tukio hili lilitokea miaka hamsini iliyopita. Baina yao kulifanyika majadiliano kumuhusu Amirul-Muuminina Ali ibn Abi Talib, ambapo yule mwanachuoni wa Kitunisia alikuwa akimsikiliza mzazi wangu akitaja dalili za Uimamu wa Imamu Ali (a.s.) na kustahiki kwake Ukhalifa, akataja dalili nne au tano. Na alipokwisha zitaja yule mwanachuoni wa Zaitunah alimuuliza mzazi wangu, "Je, unazo

139

dalili zingine zisizokuwa hizi?" Akasema: "Hapana." Basi yule Mtunisia akasema, "Hebu toa 'tasbihi' yako na uanze kuhesabu." Basi yule mwanachuoni wa Kitunisia akaanza kuzitaja dalili zinazohusu Ukhalifa wa Imam Ali (a.s.) mpaka zikafikia mia moja, ambazo mzazi wangu alikuwa hazifahamu. Naye Sheikh Asad Haidar aliongeza akasema, "Lau Ahlil-Sunnah Wal-Jamaa watasoma ndani ya vitabu vyao, basi wasingekuwa na usemi isipokuwa ule tuusemao sisi na tofauti hii ingemalizika tangu siku nyingi."

Naapa kwamba huu ni ukweli usio kwepeka iwapo tu mtu atakuwa huru kutokana na chuki yenye kupotosha na kibri chake na kisha akazirejea dalili zilizowazi.

140

1). MAONI YAQUR'AN KUHUSU MASAHABA

Kabla ya yote sina budi nieleze kwamba bila shaka Mwenyezi Mungu Mtukufu ndani ya kitabu chake Kitukufa mahala pengi amewasifu Masahaba wa Mtume wa Mwenyezi Mungu ambao walimpenda Mtume, wakamfuata na kumtii bila ya tamaa na hawakupinga wala kujikweza, wala kufanya majivuno, bali walimfuata kwa kutaka radhi ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake, basi hao Mwenyezi Mungu amewaridhia nao wamemridhia na sifa hii hapati isipokuwa yule anayemuogopa Mola wake.

Kundi hili la Masahaba ndilo lile ambalo Waislamu wanatambua heshima yao kutokana na msimamo wao na matendo yao walipokuwa na Mtume (s.a.w.). Waislamu wanawapenda, wanawaheshimu na kukitukuza cheo chao na kuwaombea radhi kila wanapowataja.

Utafiti wangu (nilio ufanya) hauhusiani na kundi hili la Masahaba ambao wao ndiyo kitovu cha heshima na utukufu kwa Masunni na Mashia, kama ambavyo utafiti wangu hauhusu kundi la Masahaba ambao ni Mashuhuri kwa unafiki na ambao wanalaaniwa na Waislamu wote Sunni na Shia.

Lakini uchunguzi wangu unalihusu kundi hili la Masahaba ambao Waislamu wamekhitilafiana juu yao, na Qur'an ilishuka kuwakemea na kuwaonya katika baadhi ya matukio, na ndiyo

141

wale ambao mjumbe wa Mwenyezi Mungu aliwahadharisha katika minasaba mingi au alionywa kutokana nao.

Naam, ikhtilafu iliyopo baina ya Shia na Sunni iko katika kundi hili la Masahaba, kwani Mashia wanayakosoa maneno yao na vitendo vyao na wanautilia mashaka uadilifu wao, wakati ambapo Ahlus-Sunna Wal-Jamaa wanawatukuza bila kujali mambo yaliyo kinyume (cha sheria ya dini) yaliyothibiti (kuwa waliyatenda).

Kwa hiyo basi utafiti wangu unahusika na kundi hili la Masahaba ili kwa kupitia utafiti huu niweze kuufikia ukweli ulivyo au sehemu ya ukweli huo.

Nimeyasema haya ili mtu yeyote asijedhani kuwa mimi nimezipuuza zile aya ambazo zimewasifu Masahaba wa Mjumbe wa Mwenyezi Mungu na nikazionesha zile tu zinazowapinga, bali mimi kwa hakika katika utafiti wangu nimegundua kwamba ziko aya zinazowasifu, ndani yake kuna maana ya lawama au kinyume chake.

Na huenda sitaikalifisha nafsi yangu kwa juhudi kubwa kama nilivyofanya katika kipindi cha miaka mitatu ya uchunguzi huu, bali nitatosheka kwa kutaja baadhi ya Aya tu ziwe mfano kama ilivyo kawaida, na hivi ni kwa ajili ya (kutaka) kufanya mukhtasari, na ni juu yao wale watakao upana zaidi kufanya juhudi ya utafiti, na kulinganisha kama nilivyofanya mimi ili kuongoka kwao kuwe kumetokana na juhudi na mchujo wa fikra, kitu ambacho Mwenyezi Mungu anakitaka kipatikane kwa kila mtu na ndivyo hali halisi inavyotaka ili mtu apate kukinaika barabara na asije akababaishwa na upepo mkali. Na inaeleweka moja kwa moja kwamba uongofu unaopatikana kwa kukinai nafsi ni bora mno kuliko ule unaopatikana kutokana na

athari za nje. Mwenyezi Mungu amesema alipokuwa akimsifu Mtume wake:

142

"Na Mola wako amekukuta ukiwa unahangaika akakuongoza." (Qur. 93:7)

Yaani: Amekukuta unaitafuta haki akakuongoza kwenye haki

Na amesema tena:

"Na wale waliofanya juhudi kwa ajili yetu basi tutawaongoza kwenye njia zetu" (Qur. 29:69).

i). Muhammad Mjumbe wa Mwenyezi Mungu

Mfano wa kwanza juu ya jambo hilo ni ile aya isemayo:

"Muhammad ni Mjumbe wa Mwenyezi Mungu."

Mwenyezi Mungu Amesema:

"Muhammad ni Mjumbe wa Mwenyezi Mungu, na walio pamoja naye wana nguvu mbele ya makafiri, na wanahurumiana wao kwa wao. Utawaona wanarukuu na kusujudu wakitafuta fadhila na radhi za Mwenyezi Mungu. A lama zao ziko katika nyuso zao kwa athari ya kusujudu. Huu ndio mfano wao katika Torati. Na mfano wao katika Injili ni kama mmea uliotoa chipukizi lake, kisha ukalitia nguvu ukawa mnene, ukasimama sawa juu ya ubuwa wake, akawafurahisha wakulima, ili kuwakasirisha kwa ajili yao makafiri. Mwenyezi Mungu amewaahidi walioamini na wakatenda mema miongoni mwa msamaha na ujira mkubwa. " (Qur. 48:29)

Aya hii tukufu yote inamsifu Mjumbe wa Mwenyezi Mungu na Masahaba walio pamoja naye, ambao wamesifika kwa sifa alizozitaja Mwenyezi Mungu kuwa wao ni wakali mbele ya Makafiri na ni wenye huruma wao kwa wao, na inaendelea aya hii Tukufu katika kuwasifu watu hawa na kutaja sifa zao mpaka inamalizika kwa kueleza ahadi ya Mwenyezi

143

Mungu Mtukufu kuwa atatoa msamaha na malipo makubwa siyo kwa masahaba wote waliotajwa lakini kwa baadhi yao ambao wameamini na kutenda mema. Basi lile tamko lisemalo:

"Miongoni mwao" Alilolitaja Mwenyezi Mungu Mtukufu linajulisha kuwa ni "Baadhi" na limeweka wazi .kwamba miongoni mwao Masahaba msamaha wa Mwenyezi Mungu na radhi zake hawatavipata, na pia limejulisha kuwa baadhi ya Masahaba hawakuwa na sifa ya imani na matendo mema. Hivyo basi aya hii ni miongoni mwa zile aya zinazowasifu na kuwakosoa kwa wakati mmoja, kwani imekisifu kikundi fulani cha Masahaba na kuwakosoa wengine.

Jambo la kusikitisha na kuhuzunisha ni kwamba watu wengi wanaitolea ushahidi aya hii tukufu juu ya Isma ya Masahaba "kuwa hawatendi makosa" na ni waadilifu na kuifanya aya hii ni hoja dhidi ya Shia, wakati ambapo aya hii ni hoja iliyo wazi dhidi yao na inawaunga mkono Mashia katika kuwagawa Masahaba kuwa kuna Sahaba aliyeamini kisawasawa na akawa mkamilifu wa imani na matendo mema, basi Mwenyezi Mungu akamuahidi msamaha na radhi yake na malipo makubwa. Na kuna Sahaba mwingine aliyesilimu na imani ikawa haijaingia kisawasawa katika moyo wake, au aliamini na kutenda mema katika zama za uhai wa Mtume s. a.w. lakini huyo huyo aligeuka kinyume nyume, basi huyu hawezi kumdhuru Mwenyezi Mungu kwa lolote lile, na Mwenyezi Mungu amemuonya kuwa matendo yake yataporomoka kwa kiasi tu cha kupaza sauti yake juu ya sauti ya Mtume, basi je, unadhani ana hali gani yule aliyemuasi Mwenyezi Mungu na Mtume wake na akapotea upotovu ulio wazi? Kisha unamfikiriaje yule ambaye hakuhukumu kwa hukumu aliyoteremshiwa au alibadilisha hukumu ya Mwenyezi Mungu akahalalisha kile alicho kiharamisha Mwenyezi Mungu na akaharamisha kile alichokihalalisha Mwenyezi Mungu na akafuata maoni yake na matamanio yake katika yote hayo.

144

2). Aya ya kugeuka nyuma:

Mwenyezi Mungu anasema:

"Na Muhammad hakuwa ila ni Mtume tu. Wamekwishapita kabla yake Mitume. Je, akifa au akiuawa ndiyo mtageuka kurudi nyuma? Na atakayegeuka na akarudi nyuma huyo hatadhuru kitu Mwenyezi Mungu. Na Mwenyezi Mungu atawalipa wanaomshukuru. (Qur. 3:144)

Aya hii tukufu iko wazi mno kwamba Masahaba watageuka nyuma baada tu ya kufariki Mtume, na hawatabakia ila wachache. Kama ilivyotambulisha aya katika maelezo ya Mwenyezi Mungu juu yao yaani: Wenye kubakia ambao hawatageuka ndiyo wale wenye kushukuru, kwani wenye kushukuru hawawi ila ni wachache kama inavyotujulisha kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu isemayo:

"Ni wachache katika waja wangu wanaoshukuru". (Qur. 34:13)

Vile vile ni kama zilivyotambulisha hadithi Tukufu za Mtume ambazo zinafasiri huku kugeuka na ambazo tutazitaja baadhi yake. Na iwapo Mwenyezi Mungu Mtukufu katika aya hii hakubainisha adhabu ya wale watakaogeuka nyuma akatosheka kwa kuwasifu wenye kushukuru ambao wastahiki malipo yake. Lakini kinachofahamika moja kwa moja ni kwamba wenye kugeuka hawastahiki malipo mema ya Mwenyezi Mungu na msamaha wake, ni kama alivyotilia mkazo Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.) katika hadithi nyingi, hapo baadaye tutazichambua baadhi yake ndani ya kitabu hiki apendapo Mwenyezi Mungu.

Na haiwezekani kufasiri aya hii tukufu kuwa inawahusu Tulaiha, Sajah na As-wad-Al-ansa, eti tu kwa kutaka kulinda heshima ya Masahaba kwani watu hawa waligeuka wakaritadi

145

kutoka kwenye Uislamu na wakadai LJtume katika uhai wa Mtume (s.a.w.) naye aliwapiga vita akawashinda. Kama ainbavyo haiwezekanani kuifasiri aya tukufu kuhusu tukio la Malik ibn Nuwairah na wafuasi wake ambao walizuia kutoa zaka katika zama za Abu Bakr kutokana na sababu nyingi tu na miongoni mwa hizo ni hizi zifuatazo:

Kwanza. walizuia zaka na hawakumpa Abu Bakr ili kufanya subira mpaka wafahamu ukweli wa mambo kwani wao walikuwa wamehiji na Mjumbe wa Mwenyezi Mungu katika Hija ya kuaga na walimpa Baia yao Imam Ah ibn Abi Talib kule Ghadir Khum baada tu ya Mjumbe wa Mwenyezi kumsimika Ukhalifa, ambapo Abu Bakr mwenyewe alikuwa amempa Imam Ali Baia yake. Mara ghafla (Malik na. watu wake) wakashitukizwa na Mjumbe wa Khalifa Abu Bakr aliyewapasha habari ya kifo cha Mjumbe wa Mwenyezi Mungu na wakati huo huo akawataka watoe zaka kwa niaba ya Khalifa mpya ambaye ni Abu Bakr. Kisa hiki ni kirefu na historia haikielezi kwa undani kwa kulinda heshima ya Maswahaba, lakini sehemu tu ya kisa hicho ni kwamba: "Malik na wafuasi wake walikuwa Waislamu hilo hlishuhudiwa na Umar na Abu Bakr mwenyewe, vile vile idadi kadhaa miongoni mwa Masahaba ambao wote walimkemea Khalid ibn Walid kwa tendo lake la kumuua Malik ibn Nuwairah. Nayo historia inashuhudia kwamba Abu Bakar alimlipa Mutamim ambaye ni ndugu wa Maliki fidia kutoka katika Baitui Mali ya Waislamu na akamwomba radhi kutokana na mauaji yale. Na inafahamika kwamba, mwenye kuritadi akatoka katika Uislamu ni wajibu kumuuwa na wala halipwi

fidia kutoka katika Baitui mali na wala haombwi radhi kwa kuuawa kwake.

Jambo la muhumu ni kwamba ile aya ya kugeuka, inawakusudia Masahaba waliokuwawakiishi na Mtume (s.a.w.) hapo mjini Madina, na inawaashiria kugeuka kwao mara tu

146

baada ya kifo cha Mtume (s.a.w.) bila kutoa mwanya. Nazo hadithi za Mtume (s.a.w.) zinabainisha wazi juu ya jambo hilo kitu ambacho kinaondoa shaka na tutaliangalia suala hih hivi punde Mwenyezi Mungu apendapo na historia ni shahidi bora juu ya kugeuka kulikotokea baada ya kifo cha Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.). Na mwenye kuyasoma matukio yaliyotokea baina ya Masahaba wakati wa kifo cha Mtume basi hapatabakia kwake shaka yoyote juu ya kugeuka huko kulikotokea miongoni mwao na hakuna aliyesalimika isipokuwa wachache.

3). Aya ya Jihadi:

Mwenyezi Mungu anasema:

"Enyi mlioamini mna nini mnapo ambiwa: Nendeni katika njiaya Mwenyezi Mungu, mnajitia uzito katika ardhi? Je, mmeridhia maisha ya dunia kuliko ya Akhera? Lakini starehe za maisha ya dunia kulinganisha na ya akhera ni chache. Kama hamuendi atakuadhibuni adhabu chungu na atawaleta watu wengine wala ninyi hamtamdhuru chochote, na Mwenyezi Mungu ni muweza wa kila kitu." (Qur. 9:28-39)

Pia aya hii iko wazi kwamba, Masahaba walikuwa wazito kwenda kwenye Jihad na walichagua maisha ya dunia licha ya wao kufahamu kuwa ni starehe ya muda mfupi mpaka wakalazimisha Mwenyezi Mungu Mtukufu awakemee na awaonye kwa adhabu kali na kubadilishwa mahali pao waje waumini wenye kusadiki.

Onyo hili la kubadilishwa (na kuletwa) wasiokuwa wao limekuja mara nyingi ndani ya aya nyingi, jambo ambalo linafahamisha dalili iliyo wazi kwamba wao walifanya uzito kwenda kwenye Jihad mara nyingi kwani imekuja katika kauli

147

ya Mwenyezi Mungu kwamba:

"Na mkirudi nyuma, (Mwenyezi Mungu) atabadilisha (alete) watu wengine wasiokuwa ninyi kisha hawatakuwa kama ninyi" (Qur. 47:38)

Na kama ilivyokauli ya Mwenyezi Mungu Mtukufu:

"Enyi mlio amini, atakayeiacha miongoni mwenu Dini yake, basi hivi karibuni Mwenyezi Mungu ataleta watu ambao atawapenda nao watampenda, wanyenyekevu kwa Waislamu (wenzao) wenye nguvu juu ya makafiri. Wataipigania Dini ya Mwenyezi Mungu na wala hawataogopa lawama ya anayewalaumu, hiyo ndiyo fadhila ya Mwenyezi Mungu, humpa amtakaye na Mwenyezi Mungu ni mwenye wasaa, mwenye kujua." (Qur. 5:54)

Na lau tungetaka kuzieleza aya tukufu zilizopo, ambazo zinaitia nguvu maana hii na kuweka wazi uhakika wa mgawanyo wausemao Mashia kuhusu aina hii ya Masahaba, basi ingelazimu kuandika kitabu maalum, na bila shaka Qur'an Tukufu imeeleza juu ya jambo hilo kwa kutumia maelezo mafupi yenye ufahamisho wa kina pale iliposema:

"Na wawepo miongoni mwenu watu wanaolingania wema na kukataza maovu, na hao ndio watakaotengenekewa. Na wala musiwe kama wale waliofarikiana na kukhitilafiana baada ya kuwafikaia dalili zilizo wazi, na hao ndio watakaokuwa na adhabu kubwa. Siku ambayo nyuso zitanawiri na nyuso zingine zitasawijika wataambiwa: Je, mlikufuru baada ya kuamini kwenu? Basi onjeni adhabu kwa vile mlivyokuwa mnakufuru. Ama wale ambao nyuso zao zitanawiri watakuwa katika Rehema ya Mwenyezi Mungu. Wao humo watakaa milele." (Qur. 3:104, 105, na 106)

148

Na aya hizi kama ambavyo haifichikani kwa kila mwenye kuchunguza kwa undani, zinawaambia Masahaba na kuwahadharisha wasifarakane na kuhitilafiana baada ya kuwafikia ubainisho, na zinawaonya juu ya adhabu kubwa na kuwagawa mafungu mawili, fungu moja litafufuliwa siku ya Qiyama likiwa na nyuso zenye kunawiri na hao ndiyo wenye kushukuru ambao wamestahiki huruma ya Mwenyezi Mungu na fungu jingine watafufuliwa wakiwa na nyuso zilizosawijika na hawa ndiyo ambao waliritadi baada ya kuamini, na Mwenyezi Mungu Mtukufu amewaonya kwa adhabu kubwa.

Bila shaka inaeleweka kwamba, Masahaba walifarakana baada ya Mtume, wakahitilafiana na wakawasha moto wa fitna mpaka jambo hili likawafikisha kwenye mauaji na vita zilizomwaga damu, kitu kilichosababisha Waislamu wageuke na kubakia nyuma na hatimaye maadui zao kuwa na tamaa (ya kuwavuruga).

Na aya hiyo iliyotajwa haiwezekani kuifanyia Taawili'na. kuigeuza kutoka kwenye Maf-Hum yake inayotangulia kueleweka akilini.

Rudi nyuma Yaliyomo endelea