Rudi nyuma Yaliyomo endelea

Hatimaye Umar ibn Al-Khatab akamuendea Abubakr akasema: "Huyu siye Mjumbe wa Mwenyezi Mungu wa haki?"

Abubakr akasema, "Bila shaka ni Mtume wa haki". Kisha Umar alimuuliza Abubakr maswali yale yale aliyomuuliza Mjumbe wa Mwenyezi Mungu naye Abubakr akamjibu majibu yale yale na akamwambia, "Ewe bwana bila shaka yeye ni Mjumbe wa Mwenyezi Mungu na hawezi kumuasi Mola wake naye ndiye mwenye kumlinda hivyo basi shikamana naye."

Na Mjumbe wa Mwenyezi Mungu alipomaliza kutia saini mkataba wa Sul-hu ya Hudabiyah aliwaambia masahaba wake: "Simameni mchinje na mnyoe." Basi wallahi hakuna miongoni mwao aliyesimama mpaka akasema mara tatu na ilivyokuwa hapana yeyote miongoni mwao aliyetekeleza amri yake aliingia kwenye hema lake kisha akatoka na wala hakumsemesha yeyote kati yao akachinja mnyama wake na akamuita kinyozi wake akamnyoa.

Masahaba wake walipoiona hali hiyo, walisimama wakachinja na wakawa wananyoana wao kwa wao karibu wauane wao kwa wao. Kisa hiki wamekiandika waandishi wa sera na Tarikh, kama ambavyo amekiandika Bukhari ndani ya sahih yake katika kitabus-shurut, babu-shurut fil-jihad juz.2 uk. 122 (pia) Sahih Muslim katika babu Sul-hul-hudaibiyah Juz. 7..

113

Kwa ujumla hiki ndicho kisa cha Sul-hu ya Hudaibiyyah nacho ni miongoni mwa matukio ambayo Mashia na Masunni wameafikiana na wamelitaja tukio hilo waandishi wa sera kama vile Tabari, ibn Al-athir na ibn Saad na wengineo kama vile Bukhari na Muslim.

Nami hapa ninao msimamo wangu; haiwezekani nisome maelezo kama haya yaliyopita hivi punde kisha nisiathiarike wala kushangazwa na matendo ya Masahaba hawa kwa Mtume  wao.

Hivi mtu mwenye akili atakubaliana na kauli ya wale wasemao kwamba Masahaba (r.a.) walikuwa wakitii maamrisho ya Mjumbe wa Mwenyezi Mungu na kuyatekeleza, wakati tukio hili linawasuta na linapinga wanayoyakusudia.

Hivi kweli mtu mwenye akili anaweza akafikiria kwamba matendo haya dhidi ya Mtume (s.a.w.) nijambo dogo linalokubalika au linalosameheka?

Mwenyezi Mungu anasema: "Naapa kwa Mola wako, hawawi waumini mpaka wakufanye wewe uwe muamuzi katika yale wanayozozania baina yao. Kisha wasione uzito katika nafsi zao kwa yale uliyoyaamua na wasalimu amri mara moja. (Qur. 4:65)

Basi je Umar ibn Al-Khatab alisalimu amri mara moja mahali hapo na hakuona uzito ndani ya nafsi yake kwa maamuzi aliyoyaamua Mtume (s.a.w.)? Au katika msimamo wake alikuwa na mashaka juu ya amri ya Mtume? Na hasa pale aliposema. "Je wewe siyo Mtume wa Mwenyezi Mungu wa haki? Naje siyo wewe uliyekuwa ukituambia..." mpaka mwisho wa maneno yake.                            '

Naje hivi alisalimu amri mara moja baada ya Mjumbe wa Mwenyezi Mungu kumjibu maswali hayo kwa majibu yanayokinaisha. Sivyo kabisa hakika hakutosheka na majibu

114

ya Mtume (s.a.w.) na akaendakumuulizaAbubakr (r.a.) maswali yale yale. Je,'hivi alikubali hata baada ya Abubakr (r.a.) kumjibu na kumpa nasaha na akamtaka ashikamane na Mtume? Mimi sijui kama alikubali au alitosheka na majibu ya Mtume au majibu ya Abubakr (r.a.). Kinyume chake ni kwamba, ni kwa nini tena Umar anasema yeye mwenyewe kwamba "Nilifanya mambo mengi kwenye tukio hilo ..." Na sijui ni sababu ipi iliyowafanya wengine waliobakia miongoni mwao wapinge baada ya hapo, pindi Mjumbe wa Mwenyezi Mungu alipowaambia, "Chinjeni kisha mnyoe." Hakuna yeyote miongoni mwao aliyetii amri hiyo mpaka Mtume akakariri mara tatu bila mafanikio.

Subhana-llah Mimi nakurubia kutokuamini nikisomacho, hivi kweli inafikia hali hii kwa Masahaba kumfanyia Mtume? Kwa hakika lau kisa hiki kingelikuwa kimesimuliwa na Mashia peke yao, basi ningeyachukulia hayo waliyoyasema kuwa ni uzushi wao dhidi ya Masahaba watukufu, lakini kisa hiki kwa usahihi na umashuhuri wake kimenakiliwa pia na wanachuoni wote wa hadithi wa Kisunni.

Kwa kuwa mimi niliilazimisha nafsi yangu kukubali yale waliyoafikiana Mashia na Masunni, basi nilijikuta ninasalimu amri na kuchanganyikiwa ilikuwaje hali hii!! Niseme nini, na nitawatakasa vipi Masahaba hawa ambao waliishi na Mjumbe wa Mwenyezi Mungu karibu miaka ishirini tangu kuanza Utume mpaka siku ya Hudaibiyyah, il-hali wanaona miujiza yake na nuru ya Unabii, na Qur'an ikiwafundisha usiku na mchana, vipi waishi na Mtume na jinsi gani wazungumze naye. Ilifikia hali ambayo Mwenyezi Mungu aliwaonya kuwa matendo yao mema yataharibika iwapo watanyanyua sauti zao juu ya sauti ya Mtume.

Ninalazimika kufikiri kwamba Umar ibn Khatab ndiye aliyewachochea wengine na kuwafanya wapinge amri ya Mtume na zaidi ya hapo ukiongeza kukiri kwake kwamba yeye siku

115

hiyo alifanya mambo ambayo hakutaka kuyataja na ameyakariri mahala pengi akisema: "Nimekuwa nikifunga, kutoa sadaka, kusali na kuwaacha huru watumwa kwa kuchelea maneno yangu niliyoyasema ..." hadi mwisho kama ilivyovyosimuliwa toka kwake kuhusu tukio hili. (Taz: Siratul-Halabiyyah Babu sul-hil-Hudaibiyyah Juz. 2 uk. 706.)

Maelezo haya yanatujulisha kwamba Umar mwenyewe alikuwa akitambua upeo wa msimamo aliokuwa nao siku hiyo, kwa hakika ni kisa cha ajabu lakini cha kweli.

116

2). Masahaba na msiba wa Siku ya Alhamisi

Ujumla wa kisa chenyewe ni kwamba, Masahaba walikuwa wamekusanyika ndani ya nyumba ya Mjumbe wa Mwenyezi Mungu siku tatu kabla ya kufariki kwake, basi Mtume akawaamuru wamletee mfupa wa begani na wino ili awaandikie maandiko yatakayowalinda wasipotee, lakini Masahaba walihitilafiana miongoni mwao, wako walioiasi amri yake na wakamtuhumu kuwa anaweweseka, basi Mjumbe wa Mwenyezi Mungu alikasirika na akawatoa nyumbani mwake bila ya kuwaandikia chochote.

Hebu soma sehemu kidogo ya kisa hiki kwa ufafanuzi. Ibn Abbas amesema "Siku ya al-hamisi, hiyo siku ya al-hamisi ilikuwa na tukio gani? Mtume wa Mwenyezi Mungu yalimzidia maumivu yake akasema, njooni nikuandikieni maandiko ambayo hamtapotea baada yake, Umar akasema bila shaka Mtume kazidiwa na maumivu nanyi mnayo Qur'an, kinatutosha kitabu cha Mwenyezi Mungu, basi hapo watu waliokuwemo ndani ya nyumba ya Mtume wakahitilafiana na kuzozana miongoni mwao, wako wanaosema sogeeni ili Mtume akuandikieni maandiko ambayo hamtapotea baada yake na wengine wanasema alivyosema Umar, walipozidisha zogo na kuhitilafiana mbele ya Mjumbe wa Mwenyezi Mungu akawaambia niondokeeni." Kwa ajili hii Ibn Abbas alikuwa akisema "Msiba mkubwa kuliko yote ni yale majibizano

117

yaliyotokea baina ya Mtume na kuwaandikia maandiko kwa sababu ya kuhitilafiana kwao na zogo lao. (Taz. Sahih Muslim Juz. 5 uk. 75 mwishoni mwa kitabul-Wassiyyah).

Tukio hili ni sahihi na la kweli halina shaka ndani yake, wanachuoni na wanahadithi Wakishia wameliandika katika vitabu vyao, kama ambavyo wanachuoni, wanahadithi na wanahistoria wa Kisunni wameliandika ndani ya vitabu vyao nalo linanilazimisha mimi nitimize kile nilichojilazimisha nafsi yangu.

Mpaka hapa nasimama hali ya kuwa nimechanganyikiwa kuufasiri msimamo wa Umar ibn Al-Khatab dhidi ya amri ya Mjumbe wa Mwenyezi Mungu.Ni amri ipi hiyo? Ni ile ya kuulinda umma huu usipotee, na hapana shaka maandiko haya ndani yake kulikuwa na kitu kipya kwa ajili ya Waislamu ambacho kingewaondoshea kila aina ya mashaka.

Hebu tuachane na kauli ya Mashia isemayo kwamba Mtume alitaka kuandika jina la Ali kuwa ni Khalifa wake, na Umar akalitambua jambo hilo kisha akamzuia Mtume asiandike.

Huenda (Mashia) wasitukinaishe kwa madai yao haya ambayo kimsingi hayaturidhishi, lakini je kunapatikana tafsiri nyingine inayoingia akilini kuhusu tukio hili lenye kutia uchungu ambalo lilimkasirisha Mtume mpaka akawafukuza Masahaba na likamfanya Ibn Abbas alie hadi machozi yake yakazilowanisha changarawe na akaliita kuwa ni msiba mkubwa? Masunni wanasema kwamba Umar alihisi ukali wa maradhi ya Mtume hivyo alimhurumia na alitaka ampumzishe, lakini sababu hii haikubaliki kwa watu wa kawaida sembuse wanachuoni? Mimi nilijaribu mara nyingi kumtakia udhuru Umar, lakini uhakika wa tukio lenyewe unanizuia kufanya hivyo, hata kama neno anaweweseka litabadilishwa "Mwenyezi Mungu apishe mbali" liwe tamko la "Maradhi yamemzidia" bado hatutapata kitu kitakachoitakasa kauli ya Umar aliposema:

118

"Munayo Qur'an na kinatutosha kitabu cha Mwenyezi Mungu."

Basi je, yeye alikuwa anaifahamu mno Qur'an kuliko Mjumbe wa Mwenyezi Mungu ambaye ameteremshiwa au kwamba Mjumbe wa Mwenyezi Mungu hazingatii akisemacho? Haiwezekani!! Au (tuseme) kwamba Mtume kwa amri yake hiyo alikuwa anataka kuleta hitilafu na kutokuelewana? "Namuomba Mwenyezi Mungu anisamehe."

Lau sababu ya Masunni ingekuwa sahihi, basi hilo lisingefichikana kwa Mtume na asingekosa kuifahamu nia nzuri ya Umar, na Mjumbe wa Mwenyezi Mungu angelimshukuru kwa ajili hiyo na angemkurubisha badala ya kumkasirikia na akasema "Niondokeeni"!!

Kwa hakika mimi najiuliza ni kwa nini wao waliitii amri yake alipowafukuza kutoka ndani ya chumba cha Mtume mbona hawakusema kuwa anaweweseka? Walipotambua ya kwamba bila shaka walikuwa wamefanikisha njama yao ya kumzuia Mtume kuandika maandiko yale, basi hawakuona tena sababu yoyote ya kuwafanya wabakie hapo, na dalili ya hilo ni kuwa wao walizidisha mzozo na kuhitilafiana mbele ya Mtume (s.a.w.) na wakagawika makundi mawili, wapo miongoni mwao wanaosema sogeeni kwa Mtume awaandikieni hayo maandiko, na miongoni mwao wako wanaosema alivyosema Umar yaani "Mtume anaweweseka."

Na suala hili halikuwajepesi kiasi cha kumuhusu Omar peke yake!!

Lau mambo yangekuwa hivyo basi. Mtume wa Mwenyezi Mungu angelimnyamazisha na kumkinaisha kwamba yeye Mtume hatamki jambo kwa matamanio yake na wala haiwezekani kuzidiwa na maumivu katika kuuongoa Umma usipotee, lakini jambo hili lilikuwa nyeti na likapata watetezi kama kwamba walikuwa wameafikiana mapema na ndiyo maana

119

walizidisha zogo na kuhitilafiana wakasahau au wakajisahaulisha kauli ya Mwenyezi Mungu isemayo:

"Enyi mulioamini musipaze sauti zenu juu ya sautiya Mtume na wala msisemezane naye kwa sauti ya nguvu kama mnavyosemezana ninyi kwa ninyi, visije vitendo vyenu vikakosa thawabu na haliya kuwa hamtambui." (Qur. 49:2)

Na katika tukio hili walivuka mipaka ya kupaza sauti na kumsemesha kwa nguvu hadi wakamtuhumu Mtume (s. a.w.) kuwa anaweweseka. Mwenyezi Mungu apishilie mbali. Kisha wakazidisha zogo na kuhitilafiana na kukawa na vita vya maneno mbele ya Mtume (s.a.w.), mimi nakurubia kuamini kwamba wengi wao waliunga mkono kauli ya Umar na ndiyo maana Mjumbe wa Mwenyezi Mungu aliona kuwa hakuna mafanikio katika kuandika maandiko hayo kwa sababu alifahamu kuwa wao hawakumuheshimu na wala hawakutii amri ya Mwenyezi Mungu kuhusiana naye yaani, kutokupaza sauti zao mbele yake. Na iwapo wao wanaiasi amri ya Mwenyezi Mungu basi hawawezi kutii amri ya Mtume wake.

Hekima ya Mtume ilikuwa ni kutokuwaandikia maandiko yake kwani alituhumiwa kuhusu maandiko hayo bado yuko hai, basi mambo yangekuwaje kuhusu maandiko hayo baada ya kufa kwake? Bila shaka wenye kumtuhumu wangesema, "Ni maneno ya mwenye kuweweseka."

Huenda wangetilia shaka hata baadhi ya hukmu alizoweka Mjumbe wa Mwenyezi Mungu katika kipindi cha maradhi aliyofia, kwani itikadi yao kuhusu kuweweseka kwake ilikuwa na nguvu.

Namuomba Mwenyezi Mungu anisamehe, na ninatubia kwake kutokana na kauli hii mbele ya Mtume mtukufu. Basi ni vipi nitaikinaisha nafsi yangu na dhamiri yangu iliyo huru

120

kwamba Umar ibn Khatab alifanya jambo la kusameheka wakati ambapo wenzake na waliokuwepo hapo walilia kwa ajili ya kilichotokea mpaka machozi yao yakalowesha mchanga na wakaiita siku hiyo kuwa ni msiba kwa Waislamu.

Kwa ajili hii niliamuwa kuzikataa sababu zote zilizotolewa ili kulitakasa tendo hilo, na nilijaribu kulipinga tukio hili na kulikanusha ili niepukane na maafa yake, lakini Vitabu vimelinakili na kulithibitisha na kulifanya kuwa ni tukio sahihi na havikufaulu kufanya vyema katika utetezi wake.

Ninakurubia kukubaliana na mtazamo wa Mashia katika kulifasiri tukio hili kwani mtazamo huo unazo sababu za kimantiki na unadalili nyingi.

Bado nakumbuka jawabu la Sayyid Muhammad Baqir As-Sadr nilipomuuliza, ni jinsi gani alivyofahamu Sayyidna Umar miongoni mwa Masahaba kile ambacho Mtume anataka kukiandika, nacho ni kumpa Ali Ukhalifa kwa mujibu wa madai yenu (ninyi Mashia).

Sayyid As-Sadr akasema, "Umar hakuwa peke yake aliyetambua makusudio ya Mtume lakini masahaba wengi walitambua kile alichokitambua Umar, kwani Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.) alikwisha kuwaambia jambo kama hili pale aliposema, "Hakika mimi ninaacha kwenu vizito viwili, kitabu cha Mwenyezi Mungu na kizazi changu watu wa nyumba yangu vitu ambavyo mukishikamana navyo kamwe hamtapotea baada yangu." Na katika kipindi cha maradhi yake hayo akawaambia, "Njooni niwaandikieni maandiko ambayo kamwe hamtapotea baada yake." Waliokuwepo hapo akiwemo Umar walifahamu kwamba Mjumbe wa Mwenyezi Mungu anataka kutilia nguvu kile alichokieleza ile siku ya Ghadir Khum kwa maandiko, nacho ni kushikamana na kitabu cha Mwenyezi Mungu na kizazi chake Mtume (s.a.w.) na Bwana wa kizazi hicho ni Ali, basi ni kama kwamba Mtume (s.a.w.) alitaka

121

kusema "Shikamaneni na Qur'an na mshikamane na Ali." Na hilo alikwishalisema katika matukio mengi kama walivyoyaeleza wanachuoni wa hadithi.

Maquraishi wengi walikuwa hawamridhii Ali kwa sababu eti ni mdogo kwao na kwamba yeye ndiye aliyewavunja wenye kibri (miongoni mwa Maquraishi) wao, akawakatisha tamaa na kuwaua mashujaa wao, lakini hawakuonesha jeuri mbele ya Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (kama Umar) kwa kiwango kilichotokea katika sulhu ya Hudaibiyyah, na pia upinzani mkali (aliouonesha) kwa Mtume pale alipo msalia Abdallah ibn Ubayi mnafiki na mahala pengine ambapo historia imeandika. Na tukio hili ni miongoni mwa hayo mengi, nawe utaona kwamba ule upinzani wa kuandika maandiko katika kipindi cha maradhi ya Mtume uliwachochea wengine kuthubutu kumpinga Mtume na hatimaye kuzidisha zogo mbele ya Mtume (s.a.w.).

Bila shaka kauli hii ilikuja ikiwa ni upinzani kamili wa makusudio ya hadithi, kwani kusema munayo Qur'an. kinatutosha kitabu cha Mwenyezi Mungu ni kinyume na madhumuni ya hadithi ambayo inawaamuru washikamane na kitabu cha Mungu na kizazi cha Mtume vyote kwa pamoja. Hivyo basi kama kwamba makusudio yao ni kuwa kinatutosha kitabu cha Mwenyezi Mungu tu, hatuna haja na kizazi cha Mtume.

Hapana tafsiri nyingine inayoingia akilini isiyokuwa hii kulingana na tukio hili isipokuwa kama itakuwa muradi ni kumtii Mwenyezi Mungu tu bila ya Mtume wake, na maana hii vile vile ni batili na haingii akilini.

Nami nikiweka kando kuegemea upande mmoja na ubinafsi uliovuka mpaka na kuipa maamuzi akili iliyosalimika na fikra iliyohuru, ninaegama kwenye ufumbuzi huu, na hili jepesi kuliko kumtuhumu Umar kwamba yeye ni wa mwanzo

122

kuipinga sunna ya Mtume kwa kusema kwake kuwa kinatutosha kitabu cha Mwenyezi Mungu.

Pia iwapo kuna baadhi ya watawala walioikataa sunna ya Mtume kwa madai kuwa inapingana, basi hali hiyo imefuatia mambo yaliyopita ndani ya historia ya Waislamu. Pamoja na kuwa mimi simbebeshi Umar peke yake lawama ya tukio hili na kule kuukosesha Ummah mwongozo na ili nibaki kuwa mwadilifu upande wa haki, nambebesha yeye na waliokuwa upande wa rai yake miongoni mwa Masahaba watukufu ambao walisema usemi kama wake na kuunga mkono msimamo wake ili kupinga amri ya mjumbe wa Mungu.

Kwa hakika mimi nashangazwa na mtu anayesoma tukio hili na akapita tu kama kwamba hapakuwa kitu pamoja na kuwa tukio hili ni miongoni mwa misiba mikubwa kama alivyoliita ibn Abbas, na nashangazwa mno na watu ambao wanajaribu kwa juhudi zao kulinda heshima ya sahaba na kulitakasa kosa lake hata kama heshima hiyo itakuwa iko dhidi ya heshima na utukufu wa Mjumbe wa Mwenyezi Mungu na ni dhidi ya Uislamu na misingi yake!!

Ni kwa nini tunaukwepa ukweli na tunajaribu kuufuta pindi unapokwenda kinyume cha matakwa yetu? Ni kwa nini hatukubali kuwa Masahaba ni watu kama sisi nao wana matamanio na wanakosea na kufanya vizuri kama sisi.

Siachi kushangaa isipokuwa ninapokisoma kitabu cha Mwenyezi Mungu ambacho kinatusimulia visa vya Manabii (a.s.) na mambo waliyopambana nayo toka kwa watu wao licha ya kushuhudia miujiza ya Mtume wao:

(Ewe Mola wetu usizipotoshe nyoyo zetu baada ya kuwa umetuongoa na utupe rehma kutoka kwako, bila shaka wewe ni mpaji.)

Namna hivi nimekuwa nikifahamu rejea ya msimamo

123

wa Mashia kwa Khalifa wa pili ambaye wao Mashia humbebesha sehemu kubwa ya jukumu la misiba iliyotokea katika maisha ya Waislamu tangu siku ya msiba ule wa siku ya Al-hamisi msiba ambao uliunyima umma yale maandiko ya uongofu ambayo

Mtume (s.a.w.) alitaka kuwaandikia.

Haiwezekani kukwepa ukweli kwamba, mwenye akili ni yule aliyeijuaa haki kwanza kabla ya kuwajua watu anaowatakia udhuru, Ama wasio ijuwa haki isipokuwa kupitia kwa watu sisi hatuna cha kuzungumza juu yao.

3). Masahaba katika Jeshi la Usamah:

Kisa hiki kwa ujumla ni kwamba Mtume (s.a.w.) aliandaa jeshi ili kulikabili jeshi la Warumi siku mbili kabla ya kufariki kwake na akampa uamirijeshi Usamah ibn Zaid ibn Harith aliyekuwa na umri wa miaka kumi na minane. Katika jeshi hi!i Mtume (s. a.w.) aliwatayarisha wakuu wa Kimuhajirina na Ansari kama vile Abubakr, Umar, Abu-Ubaidah na wengineo miongoni mwa Masahaba wakubwa mashuhuri. Miongoni mwao wapo waliopinga uamirijeshi wa Usamah na wakasema "Itakuwaje tuongozwe na kijana ambaye bado hajakomaa."

Kabla ya hapo waliwahi kupinga uamirijeshi wa Baba yake na walisema mengi juu ya jambo hilo na walikosoa mno (hali hiyo) iliomfanye Mtume (s. a.w.) akasirike sana kuhusiana na upinzani wao na kukosoa kwao. Hivyo basi Mtume (s.a.w.) alitoka akiwa mgonjwa hali amefunga kitambaa kichwani akiyumba kati ya watu wawili huku miguu yake inakokota chini kutokana na taabu ya maradhi aliyonayo. Basi akapanda kwenye mimbari akamshukuru Mwenyezi Mungu na kumtukuza kisha akasema:

"Enyi watu ni maneno gani yaliyonifikia kutoka kwa baadhi yenu kuhusu uamirijeshi wa Usamah, basi ikiwa

124

mutakebehi kwa kumpa kwangu uamiri Usamah kwa hakika mulikwishakebehi kumpa kwangu uamiri baba yake kabla ya mwanawe basi namuapa Mwenyezi Mungu kwa hakika yeye Zaid anastahiki kuwa amiri na bila ya shaka mwanawe baada yake anastahiki uamiri huo.

(1) Tabaqat cha ibn SaadJuz 2 uk. 190

(2) Tarikh Ibn Al-athir uz 2 uk. 317

(3) Tarikh At-Tabari Juz 3 uk. 226

(4) As-Siratul-Halabiyyah Juz. 3 uk.207

Kisha Mtume (s.a.w.) akawa anawahimiza wafanye haraka akawambia "Liandaeni jeshi la Usamah nendeni najeshi la Usamah upelekeni ujumbe wa Usamah," alikariri jambo hilo mbele ya masikio yao na hali ya kuwa ni wazito. Kwa hakika tendo kama hili linanilazimisha nijiulize: "Ni kwa nini wamethubutu kuwa dhidi ya amri ya Mwenyezi Mungu na Mtume wake? Na ni uasi gani huu kuhusu haki ya Mtume Mtukufu ambaye siku zote alikuwa na hamu kubwa juu yao ili waongoke na nimpole na mwenye huruma kwa waaminio."

Sikufikiria kama ambavyo Mtu mwingine naye hawezi kufikiria tafsiri nyingine inayokubalika juu ya uasi huu na ushupavu huu. Kama ilivyo kawaida wakati wa kusoma matukio kama haya yanayogusa heshima ya Masahaba kwa karibu au kwa mbali najaribu kukanusha na kupuuza matukio kama haya lakini haiwezekani kupinga na kupuuza kitu ambacho wameafikiana wanahistoria na wanahadithi katika wanachuoni wa Kisunni na Kishia.

Bila shaka nilikuwa nimemuahidi Molawangu kwamba nitakuwa muadilifu, sitang'ang'ania madhehebu yangu na sitathamini kisichokuwa kweli, na ukweli hapa ni mchurugu kama isemwavyo, na Mtume (s.a.w.) alikwishasema kuwa "Sema kweli hata kama ni juu ya nafsi yako na sema kweli japokuwa ni chungu".

125

Ukweli uliopo ndani ya tukio hili ni kwamba masahaba hawa waliopinga uamiri wa Usamah walikwenda kinyume na amri ya Mola wao na waliikhalifu amri iliyo wazi haina shaka wala tafsiri nyengine, na wala hawana udhuru wowote kwa tendo lao hilo na wala hawana udhuru isipokuwa udhuru baridi wanaoutafuta baadhi ya watu ili kulinda heshima ya masahaba na "Salafus-Salih, " mtu mwenye akili iliyo huru kwa vyovyote vile hawezi kuzikubali nyudhuru hizi, isipokuwa kama atakuwa miongoni mwa wasiofahamu wala kutumia akili au akawa miongoni mwa wale ambao chuki imewapofua macho yao ambao hawatenganishi baina ya faradhi ambayo ni wajibu kuitii na katazo ambalo ni wajibu kuliacha. Kwa hakika nilifikiri kwa muda mrefu ili labda nitawapatia udhuru unaokubalika kwa watu hawa lakini sikupata ufumbuzi.

Nilizisoma nyudhuru za Masunni juu ya watu hawa, kwamba wao walikuwa ndiyo wazee wa Kiquraish na ndiyo wakubwa zao, na walikuwa wa mwanzo kusilimu wakati ambapo Usamah ni mdogo na wala hakushiriki katika vita ili kuutukuza Uislamu kama vile vita vya Badri, Uhud, na Hunayn na hakuwa wa mwanzo kusilimu, kwa umri alikuwa mdogo wakati Mtume wa Mwenyezi Mungu alipompa uamirijeshi na maumbile ya nafsi za watu wote yanapinga iwapo miongoni mwao kuna wazee na watu wazima kuongozwa na vijana na kwa maumbile yake yanakataza kuwa chini ya uongozi wa vijana na ndiyo maana walipinga uamirijeshi wake na walimtaka Mtume (s.a.w.) ambadilishe kwa kumpa mwingine miongoni mwa Masahaba wakubwa.

Kwa hakika huo ni udhuru usiotegemea dalili ya kiakili wala kisheria na wala haiwezekani kwa Muislamu yeyote aliyeisoma Qur'an na akazifahamu hukumu zake isipokuwa ataukataa udhuru huu kwani Mwenyezi Mungu mtukufu anasema:

126

"Na kile anachokupeni Mtume kichukueni na kile anachokukatazeni komeni (msikifanye)". (Qur: 59:7)

Na amesema tenaj

"Haiwi kwa muumini mwanaume 'wala muumini mwanamke pindi Mwenyezi Mungu na Mtume wake wanapokata shauri wawe na hiyari katika shauri hilo na yeyote mwenye kumuasi Mwenyezi Mungu na Mtume wake hakika amepotea upotofu ulio wazi kabisa". (Qur: 33:36.)

Basi je ni udhuru gani watakao ukubali watu wenye akili. baada ya aya hizi zilizowazi? Niseme nini juu ya watu ambao walimkasirisha mjumbe wa Mwenyezi Mungu hali ya kuwa wanafahamu kuwa Mwenyezi Mungu hughadhibika pindi Mtume anapoghadhibika, na hayo ni baada ya wao (Masahaba) kumtuhumu Mtume kuwa anaweweseka na bila woga wakasema waliyoyasema mbele yake na wakazidisha zogo na kuhitilafiana hali ya kuwa Mtume ni mgonjwa akalazimika kuwafukuza toka chumbani mwake. Je yote haya hayakuwatosha?

Na badala ya wao kujikosoa na kutubia kwa Mwenyezi Mungu na kumtaka awasamehe kwa hayo waliyoyafanya na wamuombe Mtume  awaombee msamaha kama ilivyowafundisha Qur'an, kinyume chake waliongeza maji ndani ya unga kama mithali isemwavyo huko kwetu. Hivyo basi wakawa watovu wa nidhamu kwa Mtume aliyekuwa mpole kwao na mwenye huruma, hawakumpa haki yeyote wala kutambua heshima yake, wakamkebehi kwa kumpa uamiri Usamah baada ya siku mbili tu toka walipomtuhumu kuwa anaweweseka. Kabla jeraha bado halijapona, walimlazimisha atoke akiwa katika hali waliyoieleza wana historia kuwa alikuwa hawezi kutembea kutokana na uchungu wa maradhi, tena anayumba akiwa kati ya watu wawili. Kisha Mtume (s.a.w.)

127

akawa anaapa kuwa Usamah anastahiki kuwa amiri, na vile vile Mtume anaongeza kutujulisha kwamba "Ni hao hao Masahaba waliompinga alipompa uamiri Zaid ibn Harith hapo kabla. Mtume aliyasema hayo kwa lengo la kutujulisha kwamba wao Masahaba wanayo mambo mengi na ushuhuda mwingi kuwa wao hawakuwa miongoni mwa wale ambao huwa hawaoni uzito katika nafsi zao kwa yale aliyoyakatia shauri Mtume na wakasalimu amri mara moja, bali walikuwa miongoni mwa wabishi wanaomjadili na kujifanya wanayohadhi ya kukosoa na kupinga hata kama watakwenda kinyume na hukumu za Mwenyezi Mungu na Mtume wake.

Na miongoni mwa mambo yanayotujulisha juu ya upinzani uliyowazi ni kwamba, licha ya mambo waliyoyashuhudia ikiwemo kukasirika kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu na kuikabidhi bendera ya uamiri yeye mwenyewe kwa mkono wake mtukufu, na kuwaamuru wafanye haraka kuondoka, lakini wao walikuwa wazito na hawakuenda mpaka Mtume akafariki hali ya kuwa ndani ya moyo wake kuna huzuni juu ya umma wake uliofikwa na msiba ambao utaufanya umma wake urudi nyuma kwa visigino vyake na kuingia motoni na hawataokoka na moto huo isipokuwa wachache ambao Mtume wa Mwenyezi Mungu amewafananisha na kikundi kidogo cha ngamia waliosahauliwa na mchungaji.

Ikiwa tutataka kukifanyia mazingatio kisa hiki, basi bila shaka tutamkuta Khalifa wa pili ndiye chimbuko halisi la tukio hilo, kwa sababu baada ya kifo cha Mjumbe wa Mwenyezi Mungu yeye ndiye aliyekwenda kwa Khalifa Abubakr na akamtaka amuuzulu Usamah na kumbadilisha kwa kuweka amiri mwingine. Khalfa Abubakr akamwambia, "Mama yako amekula hasara ewe mwana wa Khatab waniamuru nimuuzulu na hali ya kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu alimtawalisha?"

Taz: (1) Tabaqat al-kubra cha Ibn Saad Juz. 2 uk, 190 (2) Tarikh At-Tabari juz 3 uk. 226

128

Vipi Umar hakutambua ukweli huu ambao Abubakr aliutambua? Au tuseme ndani ya jambo hili kuna siri nyingine ambayo haikutambulikana kwa wanahistoria? Au tu ni kwamba wanahistoria ndiyo waliouficha ukweli kwa kulinda heshima ya Umar kama ilivyo kawaida yao na kama walivyoibadilisha ibara ya "Anaweweseka" pakawekwa tamko "Maradhi yamemzidia"?

Kinachonishangaza  kwa  Masahaba  hawa waliomkasirisha Mtume siku ya Al-hamisi na kumtuhumu kuweweseka na kuchanganyikiwa na wakasema, "Kinatutosha kitabu cha Mwenyezi Mungu." Na wakati huo huo kitabu cha Mwenyezi Mungu kinawaambia ndani ya aya zake:

"Waambie ikiwa ninyi munampenda Mwenyezi Mungu basi nifuateni, Mwenyezi Mungu atakupendeni". (Qur. 3:31)

Eti kama kwamba wao (wanajiona kuwa) wanakijua mno kitabu cha Mwenyezi Mungu na hukumu zake kuliko yule aliyeteremshiwa. Ndiyo maana baada ya siku mbili tu tangu ule msiba wenye machungu na ni kabla ya siku mbili tu Mtume afariki wanamkasirisha zaidi walipomkebehi kwa kumpa Usamah uamiri na wala hawakutii amri yake alipowataka watoke waungane na jeshi la Usamah. Katika ule msiba wa mwanzo (uliotokea siku ya al-hamisi) Mtume alikuwa mgonjwa amelala kitandani, basi katika msiba huu wa pili, Mtume alilazimika atoke hali kafunga kitambaa kichwani akiwa amejifunika shuka na anayumba kati ya watu wawili, miguu yake inakokota chini akawahutubia hotuba kamili akiwa juu ya mimbari, hotuba ambayo alianza kwa kumpwekesha Mwenyezi Mungu na kumtukuza ili awajulishe kwamba yeye hakuwa anaweweseka. Kisha akawatambulisha kufahamu kwake kebehi yao na hatimaye akawakumbusha tukio jingine walilomkebehi miaka minne iliyopita, basi je baada ya yote hayo bado tu

129

wanaamini kuwa Mtume anaweweseka au kwamba maradhi yamemzidia kiasi kwamba hawezi kufahamu anachokisema?

Ewe Mwenyezi Mungu umetakasika na umetukuka, ni vipi watu hawa wanafanya ushupavu mbele ya Mtume wako hawaridhii na maamuzi aliyoyapitisha, na wanampinga kwa nguvu zote bila kusita hata alipowaamuru kuchinja na kunyoa mara tatu na hakuna yeyote aliyekubali miongoni mwao. Na katika tukio lingine walimvuta kanzu yake na kumzuia asimswalie Abdallah ibn Ubayi wakamwambia, "Hakika Mola wako amekukataza kuwasalia wanafiki!!" Kama kwamba wao ndio wanaomfundisha kile alichoteremshiwa wakati ambapo (Ewe Mwenyezi Mungu) umesema ndani ya Qur'an yako:

"Na tumekuteremshia ukumbusho (Qur'an) ili uwabaimshie mambo yaliyoteremshwa kwao. "

(Qur.l6-.44)

Pia umesema:

"Hakika sisi tumekuteremshia kitabu kwa haki ili uhukumu baina ya watu kwa yale aliyokuonesha Mwenyezi Mungu". (Qur. 4:105)

Na umesema na kauli yako ni ya haki:

"Kama tulivyomtuma Mtume kwenu anayetokana nanyi anakusomeeni aya zetu na kuwatakaseni na kuwafundisheni  kitabu na hekima na anawafundisheni mambo mliyokuwa hamuyajui". (Qur. 2:151).

Watu hawa wanashangaza, wanajiweka kwenye daraja juu kuliko ya Mtume na wakati mwingine hawatii amri yake na mara nyingine wanamtuhumu kuwa anaweweseka na kuzidisha zogo mbele yake bila ya heshima wala adabu, na kuna wakati mwingine wanampinga kwa kumpa uamiri Zaid ibn Harith na baada yake alimpa uamiri mwanae Usamah ibn Zaid.

130

Ni mashaka gani yatakayobakia kwa wenye kutafiti baada ya yote haya kwamba Mashia wako kwenye haki wanapoidhibiti mienendo ya baadhi ya Masahaba kwa alama ya kuuliza na wakawa wakali kutokana na mienendo hiyo kwa ajili tu ya kumheshimu na kumpenda Mtume na watu wa nyumba yake.

Mimi sikutaja mengi ambayo (Masahaba) walikhalifu isipokuwa mambo manne au matano na nimefanya hivyo kwa sababu ya kufupisha na hayo niliyoyataja yawe ni mfano tu, lakini wanachuoni wa Kishia wamehifadhi mamia ya mambo ambayo Masahaba walikhalifu maelekezo yawazi. Wanachuoni hawa Wakishia hawakutoa dalili isipokuwa zile zilizoandikwa na wanachuoni wa Kisunni ndani ya Sihahi zao na Musnad zao.

Rudi nyuma Yaliyomo endelea