Rudi nyuma Yaliyomo endelea

93

kweli. "Yeyote anayeacha utajo wa (Mola) mwingi wa rehma tunamuwekea shetani kuwa ndiye rafiki yake". (43:36)

Vile vile umesema "Na hakuwa Muhammad ila ni Mtume, wamepitakabla yake Mitume wengi, basi endapo akifa au akiuawa mtageuka mrudi nyuma? Na atakayegeuka akarudi nyuma, huyo hatamdhuru kitu Mwenyezi Mungu, na Mwenyezi Mungu atawalipawanaomshukuru." (3:144)

Na hapana shaka hali waliyoifikia Umma wa Kiislamu katika kuporomoka, kubakia nyuma, unyonge na umasikini ni dalili isiyo na shaka kwamba wako mbali mno na njia iliyoonyooka, na hapana shaka kwamba watu wachache au kundi la watu wachache miongoni mwa sabini na tatu haliathiri chochote katika mwendo mzima wa maisha ya Umma kwa jumla.

Bila shaka mjumbe wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.) alikwisha sema "Amrisheni mema na mukataze maovu vinginevyo Mwenyezi Mungu atawapa uwezo watu waovu juu yenu, wema wenu watakapoomba hawatajibiwa." Ewe Mola wetu tumeyaamini uliyoyateremsha na tumemfuata Mtume, basi utuandike pamoja na mashahidi. Ewe Mola wetu, usizipotoshe nyoyo zetu baada ya kutuongoa na utupe rehma kutoka kwako, hakika wewe ni mpaji. Ewe Mola wetu, sisi tumejidhulumu wenyewe na iwapo hutatusamehe na kutuhurumia, basi tutakuwa miongoni mwa watu wenye kupata hasara.

Hatimaye nilisafiri kwenda Madina nikiwa na barua kutoka kwa rafiki yangu Bashiri kwenda kwa mmoja wa ndugu zake ili nikafikie kwake kwa muda nitakaobakia huko, na kabla ya hapo alikwishazungumza naye kwa simu. Huyu bwana alinipokea na kunikaribisha nyumbani kwake, baada ya kufika nilikwenda kumzuru mjumbe wa Mwenyezi Mungu, hivyo basi nilikoga na kujitia manukato, nikavaa nguo zangu nzuri zilizo safi, na kulikuwa na watu wachache wanaozuru hapo

94

ukilinganisha na msimu wa Hijja, hivyo niliweza kusimama mbele ya kaburi la mjumbe wa Mwenyezi Mungu na lile la Abubakr na Omar jambo ambalo sikuweza kulifanya wakati wa msimu wa Hijja kutokana na msongamano. Pia nilijaribu kuugusa mlango mmoja wapo kwa ajili ya kutabaruku basi askari aliyekuwa kasimama hapo alinikemea, na kila mlango ulikuwa na askari analinda,

Niliposimama kwa muda mrefu hali ya kuwa ninaomba na kuzifikisha salamu walizonipa rafiki zangu, askari waliniamuru niondoke nami nilijaribu kuzungumza na mmoja wao lakini sikufaulu.

Nilirejea kwenye Raudha tukufu, nikaketi na kusoma Qur'an tena kwa vizuri nikarudia mara kadhaa, na ikawa nawaza kama kwamba Mjumbe wa Mwenyezi Mungu ananisikiliza na nikajiambia moyoni mwangu, je yawezekana kuwa Mtume amekufa kama watu wengine? Basi kwa nini katika sala zetu tunasema "Salamu zikushukie ewe Mtume na rehma za Mwenyezi Mungu na baraka zake?" Matamko ambayo yanayo ibara ya mwenye kusemeshwa? Na iwapo Waislamu wanaitakidi kuwa Sayyidna Khidhr (a.s.) hakufa na humrejeshea salamu kila anayemsalimia ball masheikh wa Tariqa za kisufi wanaamini kabisa kuwa Sheikh wao Ahmad Al-Tijani au Abdul-Qadir Al-Jailani huwajia wazi wazi wakiwa macho na wala siyo usingizini basi ni kwanini tunamnyima Mjumbe wa Mwenyezi Mungu utukufu kama huu wakati yeye ndiye mbora wa viumbe wote? Nafsi yangu ilijipunguzia uzito wa wazo hili na kusema:

Waislamu hawazuii uwezekano huo isipokuwa Mawahabi ambao nilikwishaanza kuwachukia kwa sababu ya jambo hili na sababu zingine, miongoni mwazo ni ukatili walionao ambao nimeuona na ukali dhidi ya waumini wanaokwenda kinyume na itikadi zao.

Nilitembelea uwanja wa makaburi ya Baqii na nilikuwa nimesimama huku nikiziombea roho za watu wa nyumba ya

95

Mtume, karibu yangu alikuweko Mzee mmoja mwenye umri mkubwa sana analia nami nilitambua kuwa ni Shia kwa mujibu wa kilio chake.Mzee huyu alielekea kibla na akaanza kuswali, mara ghafla askari alimjia kwa haraka kama kwamba alikuwa akimfuatilia nyendo zake akampiga teke hali ya kuwa yuko katika sijida akaanguka chali, masikini Mzee huyu akazimia kwa dakika chache na yule askari akaanza kumpiga, kumtukana na kumshutumu.

Nilimhurumia mzee yule na nikadhani kuwa amekufa, hasira zikanipanda, basi huruma zangu zilinilazimisha niseme kumwambia yule askari, "Ni haramu kwa nini unampiga huku anasali?" Lakini alinikemea huku akisema "Nyamaza wala usiingilie nisije nikakufanya kama nilivyomfanya (mzee huyu)" Nilipoona macho yake kuwa yana sura ya uovu nilijiepusha naye hali ya kuwa nimeikasirikia nafsi yangu ambayo ilishindwa kumsaidia mtu aliyedhulumiwa, na pia nimewakasirikia Wasaudia ambao wanawatendea watu mambo wayatakayo wao bila ya kuwepo mtu wa kuwazuwia, kuwadhibiti wala kuwakemea.

Baadhi ya Mahujaji walikuwepo hapo wengine walisema, "Lahaula •wala Qnwata illa Billahi" na wengine walisema "anastahiki kufanyiwa hivyo kwa sababu anaswali makaburini jambo ambalo ni haramu" Basi mimi sikuweza kuvumilia na nikamkemea huyu aliyesema hivi na kumwambia "Nani alikwambia kuwa kusali makaburini ni haramu?" Alijibu akasema, "Mjumbe wa Mwenyezi Mungu kakataza jambo hilo."

Nilisema bila kujali "Mnamzulia Mjumbe wa Mwenyezi Mungu" Lakini nikaogopa wasije wakanifanyia njama watu hawa wakamwita askari na akanipiga, basi nikasema kwa upole, "Ikiwa mjumbe wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.) amekataza jambo hilo, ni kwa nini mamilioni ya Mahujaji na wanaozuru wanakhalifu katazo lake na wanafanya haramu kwa kusali

96

karibu na kaburi la Mtume, Abubakr na Umar katika msikiti mtukufu wa Mtume na (kuna makaburi) ndani ya misikiti mingi ya Waislamu katika ulimwengu wa Kiislamu, na hebu tujaalie kuwa ni haramu kuswali karibu ya makaburi, basi ndiyo tutatatua tatizo hilo kwa ukali na ukatili namna hii? Au tutatatua kwa upole na huruma? Hebu nipeni nafasi nikusimulieni kisa cha yule Bedui aliyekojoa ndani ya msikiti wa Mtume wa Mwenyezi Mungu mbele yake na mbele ya Masahaba wake bila haya wala aibu, na baadhi ya Masahaba waliposimama hali ya kuwa wamezinyoosha panga zao wamuuwe, Mtume wa Mwenyezi Mungu aliwazuwia na akasema, "Mwacheni musimkatize bali mwagieni maji juu ya mkojo wake, kwa hakika mumetumwa ili murahisishe mambo na siyo mlete uzito, mubashirie wala msiwafukuze watu". Hapana walichokifanya masahaba hao ila kutii amri yake na ndipo Mtume wa Mwenyezi Mungu alipomuita yule Bedui akamkalisha karibu yake, akaongea naye kwa upole na heshima na akamfahamisha kuwa mahali pale ni nyumba ya Mwenyezi Mungu haifai kuinajisisha. Yule bedui alisilimu baada ya hapo akawa anakuja msikitini katika hali ya mavazi mazuri na safi mno. Mwenyezi Mungu amesema kweli pale alipomwambia Mtume wake "Lau ungekuwa mkali mwenye moyo mgumu wote wangelikukimbia. (3:159)

Baadhi ya watu waliathirika walipokisikia kisa hiki, mmoja wao akaniita faragha pembeni akaniuliza, "Wewe unatoka wapi"? Nikamwambia: "Tunisia," akanisalimia na kuniambia "Ndugu yangu nakunasihi kwa ajili ya Mwenyezi Mungu ulinde ulimi wako wala usiseme namna hivi mahala hapa kabisa nakunasihi kwa ajili ya Mwenyezi Mungu." Nilizidi kukasirika na kuwachukia watu hawa ambao wanadai kuwa wao ni walinzi wa Haram mbili takatifu kisha wanawatendea ubaya kiasi hiki wageni wa Mwenyezi Mungu na wala hawezi mtu yeyote kutoa rai yake au kusimulia hadithi ambazo

97

haziafikiani na riwaya zao au zenye itikadi isiyokuwa yao.

Nilirudi nyumbani kwa rafiki yangu mpya ambaye sikuwahi kulitambua jina lake, akaniletea chakula chajioni na akakaa mbele yangu. Kabla hatujaanza kula aliniuliza kuwa "Nilikwenda wapi?" Nami nikamsimulia kisa changu mwanzo hadi mwisho na nilimwambia kuwa "Ndugu yangu ni wazi kabisa nimeanza kuwachukia Mawahabi na kuwapenda Mashia." Uso wake ulibadilika na akaniambia, "Ole wako usizungumze tena maneno kama haya." aliniacha na hakula pamoja nami, nilimsubiri sana mpaka usingizi ukanishika na nilizindukana mapema kutokana na adhana ya msikiti wa Mtume nikakiona chakula bado kiko pale pale kama nilivyokiacha hivyo nikatambua kuwa mwenyeji wangu hakurudi tena.

Nilitia shaka kutokana na hali hiyo na nikaogopa huenda akawa ni miongoni mwa majasusi, basi nikaamka kwa haraka na nikaondoka hapo nyumbani sikurudii tena nikaimaliza kutwa nzima ndani ya Msikiti Mtukufu wa Mtume nikifanya ziyara na kuswali na nilikuwa nikitoka kwa ajili ya kukidhi haja na kutawadha.

Baada ya sala ya alasiri nilimsikia khatibu mmoja akisomesha katikati ya watu wenye kuswali, nikaenda hapo na nikatambua kupitia kwa mmoja wa watu waliokuwa wameketi hapo kwamba huyo alikuwa Qadhi wa Madina.

Nilimsikiliza akifasiri baadhi ya aya za Qur'an na alipomaliza darasa lake akataka kutoka nikamsimamisha nikamuuliza, "Bwana wangu, unaweza kunijulisha maana ya aya iliyoko katika kauli ya Mwenyezi Mungu isemayo: "Hakika Mwenyezi Mungu anataka kuwaondoleeni uchafu enyi watu wa nyumba ya Mtume na kukutakaseni sana sana (33:33), basi ninani hawa Ahlul Bayt waliokusudiwa ndani ya aya hii?

Alinijibu kwa haraka akasema "Ni wakeze Mtume, na aya hiyo imeanza kwa kuwataja, Enyi wake wa Mtume ninyi si

98

kama yeyote miongoni mwa wanawake iwapo mtakuwa wacha Mungu".

Mimi nikamwambia, "Kwa hakika wanachuoni wa Kishia wanasema kwamba aya hiyo inawahusu Ali, Fatmah, Hasan na Hussein, nami niliwapinga na nikawaambia kwamba mwanzo wa aya inasema: Enyi wake wa Mtume, wao wakanijibu kwamba ilipokuwa wanazungumziwa wao mfumo wa aya wote ulikuwa kwa kutumia nuni ambayo nidhamiri ya kike, na Mwenyezi Mungu akasema, "Lastunna, initaqaitunna, falatakh-dhaana, waqar-nafi buyutikunna, •wala Tabar rajna, waaqimna, waatinaz-zakah, wa-ati-ina-llaha warasulahu lakini kipande hiki kilipokuwa kinawarejea watu wa nyumba ya Mtume mfumo wa aya ukabadilika Mwenyezi Mungu akasema:

"Liyudh-hiba an-kum, •wayutah-hirakum" basi alinitazama na hali ya kuwa anatoa miwani yake na akasema "Ole wako na fikra hizi zenye sumu, bila shaka Mashia hufasiri maneno ya Mwenyezi Mungu kwa mujibu wa matamanio yao na wanazo aya zinazomuhusu Ali na wanawe ambazo sisi hatuzijuwi pia wanayo Qur'an maalum wanayoita kuwa ni msahafu wa Fatimah, mimi nakutahadharisha wasije kukuhadaa."

Mimi nikamwambia "Usihofu Ewe Bwana wangu, mimi ninayo tahadhari na ninafahamu mambo yao mengi, lakini nilitaka tu kuthibitisha". Akasema, "Wewe unatokea wapi? Nikamwambia "Tunisia" akasema "Unaitwa nani?" Nikasema "Al-Tijam" Alicheka katika hali ya kujifakharisha na akasema "Hivi unamjua huyu Ahmad Al-Tijani ni nani?" Nikasema "Yeye ni Sheikh wa Tariqa".

Akasema "Huyu ni kibaraka wa wakoloni wa Kifaransa, na Wafaransa waliimarika huko Al-geria na Tunisia kwa msaada wake, na ukitembelea Paris nenda kwenye Maktaba ya Taifa na ukasome mwenyewe kamusi ya Kifaransa katika mlango wa herufi (A), basi utaona kwamba Wafaransa wamempa nishani

99

ya Utumishi bora huyo Ahmad Al-Tijani, ambaye aliwatumikia kwa utumishi usiyo na kipimo."

Nilistaajabishwa mno na maneno yake nikamshukuru kisha nikamuaga na nikaondoka. Nilibakia Madina kwa wiki moja kamili, ambapo nilisali sala arobaini na nikayatembelea maziyara yote na nilikuwa mchunguzi mno wakati nilipokuwa huko na sikuzidisha kitu isipokuwa kuwa mbali na mawahabi na kuwachukia.

Niliondoka Madina yenye Nuru kuelekea Jordan mahala ambapo nilikutana na marafiki ambao nilijuana nao wakati wa Hija niliyokwisha ieleza hapo kabla.

Nilikaa nao kwa muda wa siku tatu, nikakuta kuwa wanachuki dhidi ya Shia zaidi kuliko ile iliyoko kwetu Tunisia, basi masimulizi ni yale yale tu, na uvumi ni huo huo na hakuna yeyote niliyemuuliza dalili ila alisema kuwa yeye amesikia tu habari zao na sikumpata hata mmoja miongoni mwao aliyekaa na Shia na kusoma kitabu cha Shia wala hajakutana na Shia maishani mwake.

Kutoka huko nilikwenda Syria, na nilipokuwa mjini Damascus niliutembelea Msikiti wa Banu Umayyah na pembezoni mwake kuna mahala kilipo kichwa cha Sayyidina Hussein, vile vile nilitembelea kaburi la Salahud-din Al-Ayubi na lile la Bibi Zainab.

Na kutokea Beirut nilikatisha moja kwa moja hadi Tripoli na safari ilidumu muda wa siku nne baharini, na katika kipindi hicho nilipumzika kimwili na kimawazo, nikaleta kumbukumbu ya safari ambayo ilikuwa karibu kumalizika, nikajikuta ninapata natija ya kuwapenda na kuwaheshimu Mashia, na wakati huo huo kuzidi kujitenga na kuwachukia Mawahabi ambao nimekwishafahamu ubaya wao.

100

Nikamshukuru Mwenyezi Mungu kwa neema aliyonineemesha na hali ya kuwa namuomba aniongoe kwenye njia ya haki.

Nikarudi nyumbani nikiwa na shauku na mapenzi kwa familia yangu, watu wangu, rafiki zangu na wote niliwakuta hawajambo, na nilikumbana na vitabu vingi nilipokuwa nikiingia nyumbani mwangu vitabu ambavyo viliwasili kabla yangu na nilitambua chanzo chake.

Nilipovifungua vitabu hivyo ambavyo vilikuwa vimejaa ndani ya nyumba nilizidi kuwapenda na kuwaheshimu watu hao ambao hawakhalifu ahadi yao na hapa vilikuwa vingi mno kuliko vile nilivyozawadiwa huko.

101

KUANZA UTAFITI

Nilifurahi sana na nikavipanga vitabu hivyo katika chumba maalum ambacho nilikiita kuwa ni maktaba. Nilipumzika kwa siku kadhaa, na nilipokea ratiba ya nyakati za kazi kwa kuanza mwaka mpya wa masomo nami kazi yangu ilikuwa ni siku tatu mfululizo za kusomesha na siku nne za mapumziko kwa wiki,

Nilianza kuvisoma vile vitabu nikasoma kitabu cha Aqidayalmamiyah, naAs-lus-shiahwa Usuluha. Nafsi yangu ilitua kutokana na itikadi hizo na fikra hizo ambazo ndiyo mtazamo wa Mashia, kisha nilisoma kitabu cha Al-Murajaat cha Sayyid Sharafud-din Al-Musawi. Sikusoma isipokuwa kurasa chache bali kitabu hiki kiliniteka na kikanipa mvuto nikawa sikiachi isipokuwa mara chache, na wakati mwingine nilikichukua hadi chuoni.

Kitabu hicho kilinishangaza mno kutokana na uchambuzi uliomo wa Mwanachuoni wa Kishia na pia kutatua mishkeli aliyokuwa nayo yule mwanachuoni wa Kisunni ambaye ni Sheikh wa chuo cha Az-har. Makusudio yangu niliyakuta ndani ya kitabu hicho kwani kitabu hicho si kama vitabu vingine ambavyo mwandishi huandika akitakacho pasina kuwa na mpinzani wala mwenye kukijadili. Lakini Al-Murajaat ni majadiliano baina ya Wanachuoni wawili kutoka madh-hebu mawili yanayo tofautiana ambayo kila mmoja wao anamuona

102

mwenziwe kuwa yuko juu ya upotofu katika kilajambo dogo na kubwa. Katika swala hilo la majadiliano wanategemea rejea mbili za msingi kwa Waislamu wote ambazo ni Qur'an tukufu na Sunnah sahihi ambayo ni yenye kukubalika katika vitabu sahihi vya Kisunni:

Kwa kweli kitabu hicho kilikuwa kinawakilisha wajibu wangu kama mtafiti anayetafuta ukweli na kuukubali popote atakapoukuta, na kwa msingi huu basi kitabu hiki kilikuwa kinafaa mno na kwangu mimi kina ubora mwingi.

Nilisimama   nikaduwaa  pindi   kilipokuwa kikiwazungumzia masahaba pale walipokosa kuzitii amri za Mtume na kuleta mifano mingi juu yajambo hilo, na miongoni mwake ni lile tukio la msiba wa siku ya Al-Khamisi, kwani nilikuwa sifikirii kabisa kwamba Sayyidna Omar Ibn Al-Khatab angeweza kupinga amri za Mtume wa Mwenyezi Mungu na kumtuhumu kuwa anaweweseka. Na hapo mwanzoni nilidhani kwamba riwaya hiyo inatoka katika vitabu vya Mashia, nilizidi kushangazwa na kuchanganyikiwa nilipomuona yule mwanachuoni wa Kishia ameinakili kutoka ndani ya sahihi Bukhari na Sahihi Muslim na nikajisemeza mwenyewe, "Iwapo nitalikuta jambo hili ndani ya sahihi Bukhari, basi nitaangalia nini cha kufanya."

Nilisafiri hadi mji mkuu wa nchi yetu na huko nilinunua Sahih Bukhari, Sahih Muslim, Musnad ya Imam Ahmad, Sahihut-Tirmidh na Muwatta ya Imam Malik na vitabu vinginevyo mashuhuri, na sikusubiri kurudi nyumbani, bali njia nzima baina ya Tunis na Qafsah nikiwa ndani ya basi nilikuwa nikizifungua kurasa za Sahih Bukhar na kutafuta tukio la msiba wa siku ya Al-Khamisi hali ya kuwa natamani nisilione tukio hilo, bila kutarajia nikalikuta.

Nikalisoma mara nyingi lakini lilikuwa kama alivyolinakili Sayyid Sharafud-din, nikalijaribukulikanusha tukio

103

hilo lote na kuwa Sayyidna Omar ndiye aliyetenda tendo hilo la hatari, lakini itawezekana vipi kwangu mimi kupinga kitu ambacho kimetajwa ndani ya Sihahi zetu nazo ni zile Sihahi za Ahlis-Sunnah Wal-Jamaah ambazo tumejilazimisha wenyewe na kushuhudia juu ya usahih wake?

Hivyo basi kuvitilia mashaka au kuvipinga sehemu fulani italazimu kutupilia mbali na kwa kufanya hivyo italazimu kuzitupilia mbali itikadi zetu zote. Na lau mwanachuoni huyo wa Kishia angekuwa ananukuu kutoka katika vitabu vyao basi kamwe nisingeamini, amma alivyonakili kutoka katika Sihahi za Kisunni jambo hilo halina nafasi ya kupingwa kwa kuwa sisi tumezilazimisha nafsi zetu wenyewe kuwa hivyo ni vitabu sahihi mno baada ya kitabu cha Mwenyezi Mungu. Jambo hilo limekuwa ni lazima vinginevyo itabidi kuzitilia mashaka sihahi hizo na hapo ndipo tutakapobakia bila ya hukumu yeyote ya Kiislamu tunayoitegemea kwa sababu hukumu zilizokuja ndani ya kitabu cha Mwenyezi Mungu ni Mujmal na siyo Mufassar (hazijafafanuliwa) na kwa kuwa sisi tuko mbali na ile zama ya Utume na tulirithi dini yetu kutoka kwa baba, tokea kwa babu tena kwa njia hii hii ya sihahi hizi, basi kwa hali yoyote ile haiwezekani kuvitupa vitabu hivi.

Nilijilazimisha mwenyewe kwa kuweka ahadi wakati nikiingia katika utafiti huu mrefu na mgumu kwamba nitegemee hadith sahihi ambazo Masunni na Mashia wameafikiana, na nizitupilie mbali hadithi ambazo zimepokelewa na kundi moja kinyume na lile jingine, kwa njia hii ya kati na kati nitakuwa nimejitenga na upendeleo, ung'ang'anizi wa kimadhehebu na chuki za kitaifa na kwa wakati huo huo naikata kamba ya mashaka ili niufikie mlima wa yakini nao ni njia ya Mwenyezi Mungu iliyonyooka.

104

MWANZO WA UTAFITI WA KINA

MTAZAMO WA SHIA NA SUNNI JUU YA MASAHABA

Miongoni mwa utafiti uliomuhimu ambao mimi nauzingatia kuwa ndiyo jiwe la msingi katika utafiti wote unaoongoza kufikia kwenye ukweli, ni ule utafiti unaohusu Maisha ya Masahaba, mambo yao waliyoyafanya na waliyokuwa wakiyaitakidi, hiyo ni kwa sababu wao ndiyo nguzo ya kila kitu, na tumeipokea dini yetu kutoka kwao na kupitia kwao tutaondokana na kiza ili tuzifahamu hukumu za Mwenyezi Mungu.

Wanachuoni wa Kiislamu wametangulia katika kuwachunguza Masahaba na mienendo yao, na kwa ajili ya jambo hili wametunga vitabu vingi kama vile Usudul-Ghabah, Al-Isaabah Fimaarifatis-Sahabah, Miizannul-itidal, navingine kwa kuwapima na kuchanganua maisha ya Masahaba, lakini vitabu hivyo ni kwa mujibu wa mtazamo wa Kisunni.

Lipo tatizo ambalo linabainisha kwamba wanachuoni wa hapo mwanzo wengi wao walikuwa wakiandika na kusimulia kwa namna inayokubaliana na maoni ya watawala wa Kibani Umayyah na Bani Abbas ambao wao walikuwa wanatambulikana kwa uadui wao dhidi ya watu wa nyumba ya

105

Mtume (s.a.w.) bali na kila anayewafuata na kupita katika muongozo wao. Na kwa ajili hii basi siyo uadilifu kutegemea kauli zao bila ya kauli za wanachuoni wengine wa Kiislamu ambao tawala hizo ziliwakandamiza, kuwatawanya na kuwaua kwa sababu ya wao kuwa ni wafuasi wa watu wa nyumba ya Mtume na ndiyo waliokuwa chimbuko la mapinduzi dhidi ya tawala hizo za kidhalimu zilizopotoka.

Na tatizo la msingi katika yote hayo ni Masahaba, kwani wao ndiyo waliohitilafiana kuhusu lile suala la Mjumbe wa Mwenyezi Mungu kuwaandikia yale maandiko ambayo yangewalinda wasipotee mpaka siku ya Qiyamah. Kuhitilafiana kwao huku ndiko kuliko unyima umma wa Kiislamu fadhila hii na kuutumbukiza ndani ya upotofu mpaka ukagawanyika, kufarakana, kugombana na kisha ukashindwa na nguvu zake zikatoweka.

Na ni hao hao Masahaba ambao walihitilafiana kuhusu ukhalifa na wakagawanyika baina ya kundi linalotawala na jingine pinzani, na hilo likasababisha umma kubakia nyuma na kugawanyika (baadhi yao) kuwa wafuasi wa Muawiya na wengine kuwa wafuasi wa Ali (a.s.).

Ni masahaba hao hao waliohitilafiana katika tafsiri ya kitabu cha Mwenyezi Mungu na hadithi za Mjumbe wa Mwenyezi Mungu na ndipo yalipotokea madhehebu, makundi vikundi vidogo vidogo hatimae yakazuka mafunzo yaliyojulikana kwa jina la Il-mul-Kalami na fikra nyingine tofauti, pia kukajitokeza falsafa aina kwa aina zilizochochewa na tamaa za kisiasa tu zenye kufungamana na tamaa za kuhodhi madaraka.

Waislamu wasingegawanyika wala kuhitilafiana katika jambo lolote lau siyo Masahaba, na tofauti yeyote iliyokwishaanza na inayoanza hivi sasa kwa hakika inarudi kwenye hitilafu yao juu ya masahaba.

106

Mola wao ni mmoja, Qur'an moja, Mtume mmoja na Qibla moja. Waislamu wote wanaafikiana juu ya hayo na tofauti zao zimeanzia kwa Masahaba ndani ya Saqifa bani Saidah kuanzia siku ya kwanza baada ya Mtume kufariki na (tofauti baina yao) ikaendelea mpaka leo hii na itaendelea mpaka Mwenyezi Mungu mwenyewe atakapotaka.

Nami nimegundua wakati wa mazungumzo yangu pamoja na wanachuoni wa Kishia kwamba, kwa mujibu wa mtazamo wao ni kuwa Masahaba wamegawanyika kwenye makundi matatu:

Kundi la kwanza: Ni la wale masahaba wema ambao walimtambua Mwenyezi Mungu na Mjumbe wa Mwenyezi Mungu kwa maarifa ya kweli kabisa na wakamuunga mkono kwa dhati na kusuhubiana naye kwa ukweli katika kauli na utakaso wa moyo katika matendo, na wala hawakugeuka baada yake, bali waliimarika juu ya ahadi waliyomuahidi bila shaka Mwenyezi Mungu mtukufu amewasifu ndani ya kitabu chake kitukufu mara nyingi na mahali pengi. Naye mjumbe wa Mwenyezi Mungu amewasifu mara nyingi na mahali pengi pia, na Mashia huwataja Masahaba hawa kwa heshima na kuwatukuza kama ambavyo Masunni nao huwataja kwa heshima na kuwatukuza pia.

Na kundi la pili: Ni la wale Masahaba ambao waliingia ndani ya Uislamu wakamfuata Mjumbe wa Mwenyezi Mungu imma kwa kupenda au kwa kuogopa, hawa walikuwa wana msimbulia Mtume wa Mwenyezi Mungu kwa kusilimu kwao na katika baadhi ya nyakati wao walikuwa wakimuudhi na hawafuati maamrisho yake na makatazo yake, bali waliyapa maoni yao nafasi dhidi ya hukumu zilizowazi mpaka Qur'an ilikuwa inashuka ili kuwakemea na mara nyingine ilishuka kuwatisha. Mwenyezi Mungu aliwafedhehesha katika aya nyingi, pia Mtume aliwahadharisha katika hadithi nyingi.

107

Mashia hawawataji Masahaba hawa ila kwa mujibu wa matendo yao bila ya kuwaheshimu wala kuwatukuza kama wale wa mwanzo.

Amma kundi la tatu la Masahaba: Ni wanafiki ambao walimfuata Mjumbe wa Mwenyezi Mungu ili kumfanyia vitimbi, wakadhihirisha Uislamu, wakaficha ukafiri, wakajisogeza ili wauvuruge Uislamu na Waislamu wote. Bila shaka Mwenyezi Mungu ame teremsha sura kamili kwa ajili yao na akawataja mara nyingi mahali pengi na kuwaonya kuwa wataingia katika tabaka la chini kabisa ndani ya moto.

Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.) amewataja na kuwahadharisha na kuna baadhi ya Masahaba wake aliwafahamisha majina ya wanafiki hao na alama zao. Na Shia na Sunni wanaafikiana juu ya kuwalaani na kujitenga nao.

Na wapo aina maalum ya Masahaba ambao japokuwa walikuwa miongoni mwa Masahaba, lakini wao wanazo sifa pekee mbali na Masahaba wengine kwani wanayo Qaraba (udugu) kwa Mtume na ubora wa kimaumbile, kiroho na mambo mengine maalum aliyowahusisha nayo Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Hapana yeyote mwenye kuwafikia katika daraja hiyo.

Hawa ndiyo wale watu wa nyumba ya Mtume (s.a.w.) ambao Mwenyezi Mungu amewaondolea uchafu na kuwatakasa mno. (Qur. 33:33) Na akawajibisha kuwasalia kama alivyowajibisha sala hiyo kwa Mtume wake, pia amewajibisha khumsi kwa ajili ya Mtume wa Mwenyezi Mungu na wao. (Qur. 8:41)

Vile vile akawajibisha kwa kila Muislamu awapende na (mapenzi hayo) ndiyo malipo ya Utume wa Muhammad. (Qvr. 42:23)

Wao ndiyo wenye mamlaka ambao Mwenyezi Mungu

108

ameamuru kuwatii (Qur. 4:59). Nao ndiyo waliobobea katika elimu, ambao wanafahamu taawili ya Qur'an na wanazijua aya Mutashabih naMuh-kam (Qur. 4:59). Hao pia ndiyo wale wenye kumbukumbu (Ahlud-Dhikr) ambao mjumbe wa Mwenyezi Mungu amewalinganisha na Qur'an katika ile hadithi ya vizito viwili na akawajibisha kushikamana navyo[1] pia akawalinganisha na Safina ya Nabi Nuhu ambayo mwenye kuipanda ataokoka na mwenye kuikengeuka ataangamia. [2]

Masahaba walikuwa wakifahamu utukufu wa watu wa nyumba ya Mtume (s.a.w.), wakiwatukuza na kuwaheshimu, na Mashia wanawafuata uongozi wao na kuwatanguliza juu ya kila sahaba, na wanazo dalili sahihi zilizo wazi.

Amma Ah-lus-Sunnah Wal-Jamaa, bila shaka wao pamoja na kuwaheshimu kwao watu wa nyumba ya Mtume (s.a.w.) na kuwatukuza na kuwaboresha, wao hawakiri mgawanyiko huu wa Masahaba, wala hawaamini kwamba kuna Masahaba wanafiki, bali kwa mtazamo wao Masahaba wote ni viumbe bora baada ya Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.) na kama kutakuwa na mgawanyo, basi huo utakuwa ni katika mlango wa kuzidiana ubora kama kutangulia kusilimu na kujitolea ndani ya Uislamu, hivyo basi huwaboresha Khulqfaur-Rashiduna[3] kwa daraja ya kwanza kisha wale sita miongoni mwa wale waliobashiriwa pepo na hii ni kwa mujibu wa maoni yao.

Ndio maana utawaona pindi wamsaliapo Mtume na Aali zake huongezea na Masahaba wote bila kumtoa yeyote. Hiki

109

ndicho nikijuacho toka kwa wanachuoni wa Kisunni na nilichokisema mwanzo ndicho nilichokisikia toka kwa wanachuoni wa Kishia yaani kuwagawa Masahaba mafungu manne na hili ndilo lililonipelekea niufanye utafiti wangu wa kina uanzie somo hili kuhusu Masahaba na nilimuahidi Mwenyezi Mungu iwapo ataniongoa nijiepushe na jazba ili nisifungamane na upande wowote bila upinzani na nisikilize kauli toka pande zote mbili kisha nifuate iliyokuwa bora. Na rejea yangu ndani ya utafiti huo ni:

(1) Kanuni sahihi za kimantiki, yaani nisitegemee isipokuwa lile jambo ambalo wote wameafikiana juu ya tafsiri ya kitabu cha Mwenyezi Mungu na sunna sahih ya Mtukufu Mtume.

(2) Akili: ambayo ni neema kubwa miongoni mwa neema za Mwenyezi Mungu juu ya mwanadamu, kwani kwa akili hiyo Mwenyezi Mungu amemtukuza na kumboresha juu ya viumbe wengine. Je huoni kwamba Mwenyezi Mungu mtukufu pindi anapotoa hoja dhidi ya waja wake huwataka watumie akili kwa kusema: "Je hawafikiri, je hawafahamu, je hawazingatii, je hawaoni n.k.

Na kimsingi, Uislamu wangu uwe ni kumuamini Mwenyezi Mungu, Malaika wake, Vitabu vyake, Mitume wake na kwamba Muhammad ni Mja wake na ni Mjumbe wake, na kwamba Uislamu ndiyo dini (sahihi) mbele ya Mwenyezi Mungu na wala nisimtegemee katika utafiti huo yeyote miongoni mwa Masahaba hata akiwa na ukaribu kiasi gani au ana daraja kubwa kiasi gani, kwani mimi siyo miongoni mwaBanu Umayyah wala Banu Abbas wala Banu Fatmah, na wala siyo Sunni wala Shia na sina uadui wowote na Abubakar wala Umar wala Uthman wala Ali na hata yule Wah-shi aliyemuua Bwana wetu Hamza maadam alisilimu na Uislamu unafuta yaliyotendwa kabla yake, na bila shaka mjumbe wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.) alimsamehe.

110

Kwa kuwa nafsi yangu nilikwisha kuiingiza ndani ya utafiti huu kwa lengo la kuufikia ukweli, na kwa kuwa nimejiepusha na fikra zote zilizotangulia kwa nia njema kabisa, basi sasa hivi naanza uchunguzi huu juu ya Masahaba nikitaraji baraka za Mwenyezi Mungu.

1). Masahaba siku ya Sulhu ya Hudaibiyyah

Kisa chenyewe kwa jumla ni kwamba: Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.) katika mwaka wa sita A.H. alitoka akikusudia kufanya umra akiwa pamoja na Masahaba elfu moja na mia nne. Akawaamuru panga zao wazitie ndani ya Ala, kisha akavaa Ihram yeye na Masahaba wake mahala paitwapo "Dhil-Halifah." Wakawatanguliza ngamia kwa ajili ya kuchinja ili kuwatambulisha Maquraishi kwamba yeye amekuja Makkah kufanya Umrah na siyo kwa ajili ya vita. Lakini Maquraish kwa kiburi chao waliogopa iwapo Waarabu watasikia kuwa Muhammad ameingia kwa nguvu mjini Makkah na kuvunja nguvu zao. Basi walimtumia ujumbe ulio ongozwa na Suhail Ibn Amr Ibn abdi Wuddi Al-Amiri, wakamtaka safari hii arudi alikotoka na kwamba mwaka ujao watamuachia Makkah kwa siku tatu.

Kwa hakika walimpa masharti magumu ambayo Mjumbe wa Mwenyezi Mungu aliyakubali kutegemeana na mas-lahi ambayo Mola wake mtukufu alimfunulia.

Hata hivyo baadhi ya Masahaba jambo hili alilofanya Mtume halikuwapendeza, wakampinga kwa nguvu mno, na Umar Ibn Khatab akamjia Mtume na kumuambia "Je, wewe siyo Mtume wa Mwenyezi Mungu wa haki?" Mtume akasema, "Bila shaka mimi ni Mtume wa Mwenyezi Mungu wa haki."

112

Umar akasema "Je sisi hatuko kwenye haki na adui yetu yuko kwenye batili?" Mtume akasema, "Bila shaka ndivyo" Umar akasema, "Basi ni kwa nini tunaonyesha udhaifu katika dini yetu?" Mjumbe wa Mwenyezi Mungu akamwambia: "Bila shaka mimi ni Mjumbe wa Mwenyezi Mungu na siwezi kumuasi naye ndiye mwenye kunilinda," Umar akasema, "Je, si ulikuwa ukituambia kwamba tutaingia kwenye nyumba tukufu na tutaitufu?" Mtume akasema, "Bila shaka nilisema, lakini je nilikuambia tutaingia mwaka huu?" Umar akasema, "Hapana" Mtume akasema, "Basi bila shaka utaingia na utaitufu."

Rudi nyuma Yaliyomo endelea