Rudi nyuma Yaliyomo endelea

(Sayyid aliendelea kusema) "Wiki iliyopita nimesoma ripoti rasmi ya serikali ya Misri ikielezea kifo cha aliyekuwa

76

rais wa nchi hiyo Jamal Abdun-Nasir, kwamba: "Watu wanane wamejiuwa mara tu waliposikia habari za kifo chake, kuna aliyejitupa kutoka juu ya nyumba na kuna aliyejiingiza mwenyewe chini ya gari moshi n.k. na wako wengi mno waliojeruhiwa na kupagawa kwa ajili ya huzuni hii. Mifano hii niitajayo ni ya hisia za kimaumbile ya kibinadamu ambayo kuna wakati huwazidi wenye nayo, na watu hao ni Waislamu bila shaka wamejiua kwa ajili ya kufa Jamal Abdun-Nasir hali ya kuwa amekufa kifo cha kawaida, kwa msingi wa tukio hili hatuna haki kuwahukumu Masunni kuwa ni wenye makosa. Hivyo basi sio haki wala uadilifu kwa ndugu zetu Masunni kuwahukumu ndugu zao Mashia kuwa wanamakosa kwa kumuhuzunikia Bwana wa mashahidi, nao Mashia wameishi na wanaendelea kuishi katika hali ya mateso mpaka leo na kwa hakika Mjumbe wa Mwenyezi Mungu mwenyewe alimlilia Husein kiasi kwamba Jibril naye alilia kutokana na kilio cha Mtume Mtukufu (s.a.w.).

Nikasema "Ni kwa nini Mashia wanayapamba makaburi ya mawalii wao kwa dhahabu na fedha jambo ambalo ni haramu katika Uislamu?" Sayyid As-Sadri alijibu: "Tendo hilo siyo kwa Mashia peke yao na wala siyo haramu, bali iko Misikiti ya ndugu zetu Masunni sawa iwe Iraq au Misri au Uturuki au penginepo katika nchi za Kiislamu imepambwa kwa dhahabu na fedha na pia Msikiti wa mjumbe wa Mwenyezi Mungu huko Madina tukufa na nyumba ya Mwenyezi Mungu tukufu huko Makkah ambayo kila mwaka huvalishwa vazi la dhahabu jipya linalogharimu mamilioni ya fedha, kwa hiyo hili siyo la Mashia peke yao.

Nikasema "Wanachuoni wa Kisaudia wanasema kuwa, kujipangusa (kugusa) kwenye makaburi na kuwaomba watu wema na kutabaruku kwao ni kumshirikisha Mwenyezi Mungu basi nini maoni yenu?"

Sayyid Muhammad Baqir As-Sadri alijibu: "Kuyagusa

77

makaburi na kuwaomba wenye makaburi hayo kwa nia ya kwamba wanadhuru na kunufaisha hii bila shaka ni shirki, na hapana shaka kwamba Waislamu wanampwekesha Mwenyezi Mungu na wanafahamu kwamba ni Mwenyezi Mungu peke yake ndiye mwenye kudhuru na kunufaisha na wao wanawaomba mawalii na maimamu ili wawe ni wasila kwake na hii siyo shirki. Vilevile Masunni na Mashia wanakubaliana juu ya hilo tangu zama za Mtume mpaka leo, isipokuwa Mawahabi ambao ni wanachuoni wa Saudia uliowataja na ndiyo ambao wameikhalifu Ij-mai ya Waislamu kwa madh-hebu yao mapya yaliyojitokeza mno katika kame hii. Kwa hakika hawa wamewafitini Waislamu kutokana na itikadi yao hii na wamewakufurisha na kuhalalisha kumwaga damu zao, kwani wao huwapiga wazee miongoni mwa Mahujaji wa nyumba tukufu ya Mwenyezi Mungu kwa kadiri ya mmoja wao kusema:

"Assalaamu Alaika ya Rasulallah na hawamruhusu yeyote kugusa kaburi (dharihi) yake tukufu."

Sayyid akaendelea kueleza, "Yalipata kutokea majadiliano kati yao (wanachuoni wa Kiwahabi) na wanachuoni wetu lakini hata baada ya kuoneshwa ukweli waliendelea na ubishi na wakatakabari mno. Sayyid Sharafud-din ambaye ni miongoni mwa wanachuoni wetu wa Kishia alipokwenda kuhiji kwenye nyumba tukufu ya Mwenyezi Mungu zama za mfalme Abdul-Aziz Al-Suud alikuwa miongoni mwa wanachuoni walio alikwa kwenda kwenye jumba la mfalme ili kumpa mkono wa sikukuu ya "Iddul-Udh-ha". Kama ilivyokuwa kawaida ya huko, ilipofika zamu yake kupeana mkono na mfalrne, (Sayyid) alimpa (mfaime huyo) zawadi ambayo ilikuwa ni msahafa uliofungwa ndani ya ngozi, naye akaubusu na kuuweka kwenye paji lake la uso kwa kuuheshimu na kuutukuza. Hapo ndipo Sayyid Sharafud-din alipomwambia mfaime "Ewe mfalme, kwa nini unaibusu ngozi na kuitukuza wakati hiyo ni ngozi ya mbuzi?"

78

Mfaime akajibu "Mimi nimeikusudia Qur'an tukufu • ambayo imo ndani ya ngozi na sikukusudia kuitukuza ngozi." Basi Sayyid Sharafud-din akasema "Vema ewe mfalme, basi ni hivyo hivyo tufanyavyo sisi tunapoyabusu madirisha ya chumba cha Mtume au milango yake. Sisi pia tunafahamu kabisa kwamba hivyo ni vyuma havidhuru na wala havinufaishi, lakini huwa tunakikusudia kilichopo nyuma ya vyuma hivyo na mbao hizo, kwa hiyo sisi hukusudia kumtukuza Mjumbe wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.) kama wewe ulivyoikusudia Qur'an kwa kuibusu ngozi ya mbuzi ambayo imefunika Qur'an."

Basi waalikwa walitoa takbira "A llahu Akbar" kwa kumfurahiya Sayyid na wakasema umesema kweli na jambo hilo lilimlazimisha mfalme huyo, katika zama zake awaachie Mahujaji watabaruku kwa athari za Mtume (s.a.w.) mpaka alipokuja (mfalme) ambaye alifuatia baada yake akarudia katika uamuzi ule wa zamani. Basi hapa tatizo lao siyo kwamba, khofu yao ni kuwa watu watamshirikisha Mwenyezi Mungu, kwa kiwango fulani tatizo lao ni la kisiasa limewekwa ili kuwapinga Waislamu na kuwaua ili kuimarisha ufalme wao na utawala wao dhidi ya Waislamu, na historia ni shahidi mkubwa kwa mambo waliyo watendea ummati Muhammad (s.a.w.).

Na nilimuuliza kuhusu Tarika za masufi, akanijibu kwa ufapi kwamba ndani ya Tariqa hizo kuna mambo ambayo ni mema na mengine si mema. Ama yaliyomema ni kuilea na kuizowesha nafsi taabu ya maisha na kujitenga na mambo ya starehe za dunia yenye kupita na kuipandisha kwenye daraja za ulimwengu wa kiroho. Amma yasiyokuwa mema ni kujitenga na kuacha hali halisi ya maisha na kuifanya dhikiri ya Mwenyezi Mungu iishiye kwenye idadi ya matamshi n.k.

Na inastahiki kusema kwamba, Uislamu na mafunzo yake yote ni mema.

79

MASHAKA NA MKANGANYIKO

Majibu ya Sayyid Muhammad Baqir As-Sadr yalikuwa na ufafanuzi na yenye "kutosheleza lakini itawezekanaje kupenya haraka ndani ya nafsi ya mtu kama mimi ambaye katika umri wake wa miaka ishirini na tano ameishi juu ya msingi wa kuwatukuza masahaba na kuwaheshimu na hasa wale Khulafaur-Rashiduna ambao mjumbe wa Mwenyezi Mungu ametuamuru tushikamane na sunna yao na kufuata uongozi wao wakitanguliwa na Sayyidna Abubakr As-Sidiq, kisha Sayidna Umar Al-Faruq, nami sikuwahi kusikia watu hawa wakitajwa toka nilipofika Iraq bali nimekuwa nikiyasikia yakitajwa majina mengine mapya nisiyoyajua kabisa na nimekuwa nikisikia Maimamu kumi na wawili kwa idadi na pia madai kwamba mjumbe wa Mwenyezi Mungu kabla hajafariki alitamka kuwa. Imam Ali awe Khalifa wake basi ni vipi nitayaamini mambo hayo?

Hivi kweli Waislamu tena masahaba watukufu ambao ni viumbe bora baada ya Mjumbe wa Mwenyezi Mungu wanaweza kukubaliana dhidi ya Imam Ali Karramallah Waj-hahu, nasi masheikh wetu wametufundisha tangu utotoni kwamba Masahaba walikuwa wakimuheshimu Imam Ali na wakiitambua haki yake kwani yeye ndiye mume wa Fatmah Az-Zahra naye ndiye mzazi wa Hasan na Husein na ndiye mlango wa mji wa Elimu.

80

Na hali ni ile ile kwa upande wa pili, Sayyidna Ali anaitambua haki ya Abubakr As-Sidiq ambaye alisilimu kabla ya watu wote, naye ndiye mwenza wa Mjumbe wa Mwenyezi Mungu katika pango. Mwenyezi Mungu Mtukufu amemtaja ndani ya Qur'an na Mjumbe wa Mwenyezi Mungu alimtawalisha Uimamu katika sala wakati alipokuwa mgonjwa na isitoshe Mtume (s.a.w.) alisema, "Lau ningelikuwa mwenye kumfanya mtu fulani kuwa mwandani wangu, basi ningemfanya Abubakr awe mwandani wangu."

Juu ya yote hayo Waislamu walimchagua (Abubakr) awe khalifa wao na vivyo hivyo, Imam Ali anaitambua haki ya Sayyidna Omar ambaye Mwenyezi Mungu aliutukuza Uislamu kupitia kwake pia Mjumbe wa Mwenyezi Mungu akamwita kuwa ni "Farouq" ambaye anatenganisha baina ya haki na batili, na ni kama ambavyo anaitambua pia haki ya Sayyidna Uthman ibn Aflan ambaye Malaika wa Mwenyezi Mungu walimstahi na ni yeye aliyeliandaa jeshi la Usrah, na ni Mjumbe wa Mwenyezi Mungu aliyempa jina la "Dhun-Nurain"

Ni kwa nini basi ndugu zetu Mashia hawayajui yote haya au wanajifanya hawayajui na kisha wanawafanya watukufu hawa kuwa' ni watu wa kawaida ambao wanaoweza kupotoshwa na tamaa za kidunia na wakaacba kufuata haki, kisha wakaiasi amri ya Mtume baada ya kufariki kwake wakati hawa ndiyo ambao walikuwa wakishindana kutekeleza amri zake. Wakiwaua watoto wao na baba zao na jamaa zao katika njia ya kuutukuza Uislamu na kuutetea. Kwa hiyo mtu anayemuuwa baba yake na mwanawe kwa ajili ya kumtii Mwenyezi Mungu na Mtume wake hawezi kabisa kudanganywa na tamaa za kidunia kwa lengo la kupata madaraka ya ukhalifa na kisha wapuuze na kuipa mgongo amri ya mjumbe wa Mwenyezi Mungu.

Naam, kwa ajili ya yote hayo sikuyaamini maneno yote wayasemayo Mashia licha ya kwamba nilikuwa nimekubaliana

81

nao katika mambo mengi na nilibakia katika mkanganyiko na mashaka ambayo waliyaingiza wanachuoni wa Kishia ndani ya akili yangu, kwani maneno yao yanaingia akilini na ni yenye mantiki inayokubalika. Kutokana na kukanganyikiwa kulikonipata, sikuamini kabisa kwamba Masahaba (r.a.) wamewekwa katika daraja hii na wakawa ni watu wa kawaida tu kama sisi ambao Nuru ya utume haikuwakosha na wala uongofu wa Muhammad haukuwabadilisha tabia. Ewe Mola wangu itakuwaje hali hii, hivi kweli inawezekana Masahaba wakawa katika hali hii waisemayo Mashia?

Jambo la muhimu ni kwamba mashaka haya na mkanganyiko huu ndicho chanzo cha unyonge na ndiyo mwanzo wa kuthibitisha kwamba kuna mamboambayo yamefichwa na hapana budi kuyachunguza ili kuweza kuufikia ukweli.

Rafiki yangu Mun-im alikuja na tukasafiri hadi Kar-bala huko niliishi katika mazingira ya tukio la masaibu ya Sayyidna Husein kama wanavyoishi Mashia wake, na hapo ndipo nilipotambua kwamba Sayyidna Husein hajafa bado, kwani watu wanasongamana na kuzunguka kwenye kaburi lake kama vipepeo huku wakilia kwa huzuni na majonzi. Sijapata kuona mfano wake na ni kama kwamba Hussein ameuawa sasa hivi. Niliwasikia wahadhiri wanaziamsha hisia za watu kwa kusimulia tukio la Karbala kwa kulia na kuomboleza, kiasi kwamba msikilizaji hawezi kuizuia nafsi yake ila atalia, basi kwa hakika nililia, nikalia nikaiacha huru nafsi yangu kama kwamba ilikuwa imefungwa, na nilihisi raha kubwa katika nafsi ambayo sikuifahamu kabla ya siku hiyo, pia nilijiona kama kwamba nilikuwa kwenye safu ya maadui wa Husein na ghafla nimegeuka na kuwa upande wa wafuasi wake na Masahaba wake ambao wanajitolea roho zao. Kuna khatibu mmoja alikuwa akieleza kisa cha "Huru" ambaye ni mmoja wa viongozi waliopewa jukumu la kumpiga vita Husein, lakini alisimama katika uwanja wa vita akitetemeka kama kuti, na baadhi ya

82

wenziwe walipomuuliza kuwa "Je wewe unaogopa kufa?"

Huru alijibu, "Wallahi hapana, lakini ninaihiyarisha nafsi yangu baina ya pepo na moto." Kisha hapo hapo akampiga farasi wake akaenda kwa Husein akamwambia: "Ewe mwana wa Mtume wa Mwenyezi Mungu naweza kutubia?" Basi baada ya kusikia hayo sikuweza kujizuwia bali nilianguka chini hali ya kuwa ninalia kama kwamba ninachukuwa nafasi ya tendo la "Huru" na ninamuomba Husein "Ewe mwana wa Mjumbe wa Mwenyezi Mungu naweza kutubia? Nisamehe Ewe mtoto wa Mjumbe wa Mwenyezi Mungu". Sauti ya khatibu yule ilikuwa inaathiri, hivyo basi sauti za watu zilipaa kwa kulia sana na wakati huo rafiki yangu alisikia kilio changu akanikumbatia hali ya kuwa analia na kunipakata kifuani kama mama anavyompakata mwanawe huku akirudia rudia kusema "Ewe Husein! Ewe Husein!"

Kipindi hicho kilikuwa ni wakati na muda niliokifahamu kilio cha kweli na nikahisi machozi yangu kuwa yameukosha moyo wangu na mwili wote toka ndani na hapo pia ndipo nilipoifahamu hadithi ya Mtume isemayo, "Lau mungelifahamu mambo niyajuwayo mimi, basi mungecheka kidogo na mungelia sana." Kutwa nzima ya siku hiyo nilikuwa mwenye huzuni, na rafiki yangu alijaribu kuniliwaza na kunipa baadhi ya viburudisho, lakini nilikuwa sina hamu navyo kabisa, nilichokifanya ilikuwa ni kumuomba anieleze tena kisa cha mauaji ya Sayyidna Husein, kwani sikupata kukisikia japo kidogo zaidi ya kuwa masheikh wetu wanapotusimulia kisa hicho husema kwamba wanafiki na maadui wa Uislamu waliomuuwa Sayyidna Omar na Sayyidna Uthuman na Sayyidna Ali ndiyo waliomuua Sayyidna Husein, na hakuna tukijuacho isipokuwa muhtasari huu tu, bali tulikuwa tunasherehekea siku ya Ashura kwa kufahamu kwamba "ni moja ya sikukuu za Kiislamu. Na katika Sikukuu hiyo hutolewa Zaka za mali na kupikwa vyakula vinono vya aina mbali mbali pia watoto nao

83

hupita wakiwaomba pesa watu wazima ili waweze kununua. Hal-wa na vifaa vya kuchezea.

Naam katika baadhi ya miji kuna aina ya desturi ambazo miongoni mwazo ni wakazi wa maeneo hayo huwasha moto na siku hiyo hawafanyi kazi wala hawaowi na wala hawasherehekei, lakini tunaziita kuwa ni desturi tu ambazo hazina maelezo wala tafsiri yake, na wanachuoni wetu husimulia hadithi mbali mbali zinazoelezea ubora wa siku ya Ashura na baraka zilizomo na rehma nyingi za ajabu!

Baada ya kuzuru kaburi la Imam Husein (a.s.) tulizuru kaburi (dharih) ya Abbas ambaye ni ndugu yake Husein, nami nilikuwa simfahamu Abbas kuwa ni nani, rafiki yangu alinisimulia kisa cha ushujaa na uhodari wa Abbas. Hapo pia tulikutana na wanachuoni wengi ambao siwakumbuki majina yao kikamilifa, isipokuwa baadhi ya Laqabu zao kama vile, Bah-rul-ulum na Sayyid Al-hakim, Kashiful-ghitaa na Ali-Yasin, Tabatabai, Fairuz Abaad, Asad Haidar na wengineo ambao nilibahatika kuonana nao.

Ukweli na usemwe, "Kwa hakika ni wanachuoni wachamungu ambao wamefunikwa na haiba na heshima, na Mashia wanawaheshimu sana na huwa wanatoa Khums ya mali zao kwa wanachuoni hao ambao huzitumia Khums hizo kuendeshea Vyuo vya elimu na kuasisi Madrasah na viwanda vya uchapishaji, vile vile huzitumia kuwapa wanafunzi wanaokuja hapo kusoma kutoka nchi mbali mbali za Kiislamu. Wanachuoni hao wanajitegemea wenyewe wala hawana uhusiano na watawala wa Serikali kwa namna yoyote ile kinyume na walivyo wanachuoni wetu ambao hawatoi Fatwa wala kusema kitu isipokuwa kwa mujibu wa maoni ya watawala wanaodhamini maisha yao na wanamstaafisha wamtakaye na kumpa cheo wamtakaye.

Kusema kweli ni ulimwengu mpya nilio uvumbua au

84

alionionesha Mwenyezi Mungu na nimeliwazika nao baada ya kuwa nilikuwa nikiuchukia na niko pamoja nao baada ya kuwa nilikuwa naupinga, kwa hakika ulimwengu huu umenipatia fikra mpya na umenipa hali ya kupenda kuchunguza, kutafiti na kusoma mpaka niupate ukweli unaohitajika, ukweli ambao siku zote umekuwa ukinipitia akilini nilipoisoma hadithi tukufu ya Mtume wa Mwenyezi Mungu aliposema, "Wana wa Israil walifarakana wakawa makundi sabini na moja, na Manaswara wamefarakana mpaka wakafikia makundi sabini na mbili, na Umati wangu watafarakana na kuwa makundi sabini na tatu na yote yataingia motoni isipokuwa kundi moja."

Hatuna la kusema juu ya dini yingine nyingi ambazo kila moja inadai kuwa ndiyo ya kweli na nyingine si za kweli, lakini nashangaa na kustajaabu na kuchanganyikiwa ninapoisoma hadithi hii, na huku kustaajabu kwangu na kushangaa kwangu na kuchanganyikiwa si kwa sababu ya hadithi yenyewe lakini (ninaowashangaa na kuwastaajabu na kunichanganya mawazo) ni Waislamu wenyewe ambao huisoma hadithi hii na kuirudia rudia katika hotuba zao na kuiacha bila kuchanganua wala kutafiti maana yake ili walibainishe lile kundi lenye kuokoka kutokana na makundi yaliyopotoka.

Cha ajabu ni kuwa kila kundi linadai kuwa wenyewe ndiyo pekee wenye kuokoka wakati ambapo mwisho wa hadithi imekuja kama ifuatavyo: "(Masahaba) wakasema ni kina nani hao watakao okoka ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu?" Mtume akasema, "Ni wale ambao watakuwa kama nilivyo mimi na sahaba wangu." Hapana kundi ila (linadai kuwa) limeshikamana na Kitabu na Sunna, na hakuna kundi la Kiislamu ambalo linadai kinyume na hivyo. Kwa hiyo lau Imamu Malik ataulizwa au Abu Hanifa au Imamu Shafii au Ahmad ibn Hanbal ila kila mmoja wao atadai kwamba yeye anashikamana na Qur'an na Sunna sahihi.

85

Madh-hebu haya ya Kisunni na tukiongeza na kundi la Mashia ambao nilikuwa nikiamini kuwa ni waovu na wamepotoka, nao ni kundi jingine linalodai pia kwamba limeshikamana na Qur-an na Sunnah sahihi iliyo nakiliwa toka kwa watu wa nyumba ya Mtume waliotakasikia, na wenye nyumba, ndio wanaofahamu kilichomo ndani mwao kama wasemavyo (Mashia).

Basi je inawezekana wote hawa wawe kwenye haki kama wanavyodai? Jambo hili haliwezekani kwani hadithi tukufu inamaanisha kinyume cha hivyo isipokuwa kama hadithi hiyo itakuwa ni ya uongo, na hili haliwezekani kwa sababu hadithi yenyewe ni mutawatiri kwa Masunni na Mashia. Au basi hadithi hii iwe haina maana yoyote na haijulishi lolote? Na haiwezekani kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu kusema kitu kisichokuwa na maana na hakijulishi chochote kwani Mtume hasemi kwa matamanio ya nafsi yake na hadithi zake zote zimejaa hekima na mazingatio.

Kilichobakia kwetu ni kukiri lipo kundi moja lililoko kwenye haki, na yaliyobakia ni upotofu. Basi hadithi hii inaniletea mkanganyiko kama ambavyo inavyoniletea (hali ya kumfanya mtu) atafiti na kufuatilia kwa yule atakaye kuiokoa nafsi yake.

Kwa ajili hii basi iliniingia shaka na utata baada ya mimi kukutana na Mashia, kwani ni nani ajuaye, huenda wao wako kwenye haki na wanasema kweli! na ni kwa nini nisifanye utafiti na kufuatilia?

Nao Uislamu umenilazimisha kupitia Qur-an yake na Sunna yake nifanye utafiti, nilinganishe na nizingatie. Mwenyezi Mungu anasema, "Na wale wanaojitahidi kwa ajili yetu tutawaongoza kwenye njia zetu" 29:69 na amesema tena kwamba, "Wale ambao husikiliza kauli (zisemwazo) wakafuata zile zilizo njema hao ndiyo aliowaongoa Mwenyezi Mungu na

86

hao ndiyo wenye akili "39:18 na bila shaka Mjumbe wa Mwenyezi Mungu amesema, "Fanya utafiti kuhusu dini yako mpaka isemwe kuwa wewe ni maj-nun".

Kwa hiyo kufanya utafiti na kulinganisha ni wajibu wa kisheria juu ya kila mukallaf. Kwa ajili ya uthibitisho huu na kutokana na azma ya kweli niliahidi mwenyewe nafsi yangu kufanya utafiti na kulinganisha na niliwaahidi hivyo marafiki zangu Mashia huko Iraq wakati nilipokuwa nawaaga kwa kuwakumbatia tena mwenye huzuni kwa kutengana nao. Kusema kweli niliwapenda na wao walinipenda, niliwaacha wapendwa hao watukufu wenye moyo safi waliojitolea wakati wao kwa ajili yangu si kwa ajilinyingine kama walivyosema siyo kwa khofu fulani wala tamaa fulani, bali kutafuta radhi za Mwenyezi Mungu Mtukufu. Imekuja (riwaya) katika hadithi tukufu kwamba, "Mwenyezi Mungu akimuongoa mtu mmoja kupitia kwako ni bora kwako kuliko kila kitu kinachoangaziwa na jua".

Niliondoka Iraq baada ya kukaa huko siku ishirini nikiwa ndani ya mazingira ya Maimamu na Mashia wao, siku hizo zilipita mfano wa ndoto tamu ambayo aliyelala hutamani asiamke mpaka aikamilishe.

Basi niliondoka Iraq nikiwa ni mwenye huzuni kutokana na uchache wa muda, nilihuzunika kwa kutengana na nyoyo nilizozipenda ambazo zinazotaharika kwa kuwapenda Ahlul-bait. Nikaelekea Hijaz hali ya kuwa naikusudia nyumba tukufu ya Mwenyezi Mungu na kaburi la Bwana wetu Mtukufu wa daraja kwa wale wa mwanzo na wa mwisho, sala na salamu za Mwenyezi Mungu zimshukie yeye na ali zake wema walotakasika.

87

SAFARI YA KWENDA HIJAZ

Niliwasili Jeddah na nikakutana na rafiki yangu Bashir ambaye alifurahi kwa kufika kwangu, akanikaribisha nyumbani kwake, akanikirimu kwa takrima kubwa na alikuwa akitumia wakati wa mapumziko yake katika matembezi pamoja nami kwa gari lake.

Tulikwenda sote Umra na tukaishi huko siku kadhaa katika ibada na Uchamungu, na nilimuomba radhi kwa kuchelewa kwangu kwani nilikuwa Iraq. Nilimsimulia juu ya uvumbuzi wangu mpya au ushindi mpya naye alikuwa ni mtu aliyefungukiwa, pia ni mtambuzi akasema: "Bila shaka mimi nasikia kwamba katika wao wamo baadhi ya wanachuoni wakubwa nawanayo wayasemayo, lakini wanavyo vikundi vingi vyenye kufru vilivyopotoka vinavyotusababishia matatizo mengi wakati wa msimu wa Hijja."

Nilimuuliza ni yepi matatizo ambayo wanayasababisha? Alijibu: "Wao wanasali kwenye makaburi, huingia Baqii kwa wingi na wanalia na kuomboleza na mifukoni mwao huchukua vipande vya mawe na kuvisujudia, na wanapokwenda kwenye kaburi la Sayidna Hamzah lililoko Uhud, basi huko huweka jeneza na kujipiga na kulia kama kwamba Hamza amekufa katika muda huo na kwa ajili hiyo basi serikali imezuwiya kuingia sehemu zenye makaburi."

Nilitabasamu na nikasema "Kwa sababu hii unawahukumu kwamba wamekwenda kinyume cha Uislamu?"

88

Akasema: "Na mengineyo, kwani wao huja kumzuru Mtume lakini wakati huo huo husimama kwenye kaburi la Abubakar na Umar na kuwatukana na kuwalaani na miongoni mwao wako ambao hutupia uchafu na najisi kwenye kaburi la Abubakar na Umar."

Kauli hii ilinikumbusha kisa nilichokisikia toka kwa mzazi wangu baada tu ya yeye kurejea kutoka Hija, lakini yeye alisema kwamba wao hutupia uchafu kwenye kaburi la Mtume, hapana shaka mzazi wangu hakulishuhudia jambo hilo kwa macho yake kwani yeye alisema: "Tuliwaona askari wajeshi la Saudia wakiwapiga baadhi ya Mahujaji kwa fimbo, na tulipo-wakemea kwa tendo hilo la kuwadhalilisha Mahujaji wa nyumba tukufu ya Mwenyezi Mungu, walitujibu kuwa hawa siyo Waislamu wao ni Mashia wamekuja na uchafu ili wautupie kwenye kaburi la Mtume". Mzazi wangu alisema, "Hapo tuliwalaani na kuwatemea mate hao Mashia.

Na sasa na mimi nayasikia toka kwa rafiki yangu ambaye ni Msaudia mzaliwa wa mjini Madina kwamba wao huja kuzuru kaburi la Mtume lakini wao hutupia najisi juu ya kaburi la Abubakr na Umar. Nilizitilia mashaka riwaya zote mbili kwani mimi nimehiji na nimeona kwamba chumba kitukufu ambacho ndani yake limo kaburi la Mtume, Abubakr na Umar kimefungwa na haiwezekani kwa mtu yeyote kukisogelea ili kugusa mlango wake au dirisha licha ya kutupiavitu ndani yake.

Kwanza hakuna upenyo, na pili wapo walinzi imara miongoni mwa askari washupavu ambao hupokezana kulinda na kuchunga mbele ya kila mlango, na mikononi mwao wanafimbo ambazo humpiga kila anayesogelea na au kujaribu kuchungulia ndani ya chumba. Ninadhani kwamba, miongoni mwa baadhi ya askari hao wako wanao wakufurisha Mashia na ndiyo waliowatupia tuhuma hii ili kuhalalisha tendo lao la kuwapiga ili kuwachochea Waislamu nao wawapige, na au kwa

89

uchache wanyamaze dhidi ya kuwanyanyasa (Mahujaji) hao na waeneze uvumi warudipo katika nchi zao kwamba Mashia wanambughudhi Mtume wa Mwenyezi Mungu na wanatupia najisi kwenye kaburi lake na kwa njia hiyo wanapiga ndege wawili kwajiwe moja.

Na hali hii inafanana na ile aliyoisimulia mheshimiwa mmoja miongoni mwa watu ninaowaamini alisema kwamba, "Tulikuwa tunatufu Al-Kaaba, basi mara kijana mmoja alishikwa na maumivu makali ya tumbo kutokana na msongamano akatapika, askari waliokuwa wakilinda Hajarul-As-wad walimpiga na wakamtoa akiwa katika hali ya kuhuzunisha wakamtuhumu kwamba alikuja na najisi ili kuichafua Al-Kaaba na wakatoa ushahidi dhidi yake akauawa siku ile ile.

Maelezo haya yakawa yanazunguka kichwani mwangu na nilibakia naifikiria kwa kitambo hoja ya yule rafiki yangu Msaudia inayowakufurisha Mashia hawa. Kwa kweli mimi sikusikia lolote isipokuwa wanalia, kujipiga vifua, wanasujudu juu yajiwe, wanaswali kwenye makaburi, na ndipo nikajiuliza je katika matendo haya liko la kumkufurisha mtu anayeshuhudia kwamba hapana Mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu na kwamba Muhammad ni Mja wake na ni Mjumbe wake, isitoshe anasali sala (tano), anatoa zaka, anafunga Ramadhani, anahiji Makka na anaamrisha mema na kukataza maovu.

Sikutaka kumpinga rafiki yangu na kuingia naye katika majadiliano ambayo hayana faida, basi nikatosheka kwa kusema "Mwenyezi Mungu atuongoe kwenye njia yake iliyonyooka sisi na wao na awalaani maadui wa dini ambao wanaufanyia vitimbi Uislamu na Waislamu."

Nilikuwa kila ninapoitufu nyumba kongwe (Al-Kaaba) katika Umra na kila wakati wa kuzuru Makka tukufu, kisha kukawa hakuna watu wengi wanaotufu miongoni mwa wenye

90

kufanya Umra, niliswali na kumuomba Mwenyezi Mungu mtukufa kutoka katika kila kiungo changu anifungulie moyo wangu na aniongoze kwenye ukweli.

Nilisimama kwenye Maqam Ibrahim (a. s.) na nikasoma aya tukufu ya Qur'an isemayo "Na ipiganieni dini ya Mwenyezi Mungu kama inavyostahiki, yeye ndiye aliyekuumbeni wala hakuweka juu yenu mambo mazito katika dini, nayo ni mila ya " baba yenu Ibrahim yeye ndiye ahyekuiteni kuwa ni Waislamu tangu mwanzo na katika hili Mtume awe shahidi juu yenu na ninyi muwe mashahidi juu ya watu (waliotangulia) basi salini sala na toeni zaka na shikamaneni pamoja kwa ajili ya Mwenyezi Mungu yeye ndiye Mola wenu Mola mwema mno na ni msaidizi mwema mno (22:78).

Kisha nikaanza kumzungumza bwana wetu Ibrahim au baba yetu Ibrahim kama ilivyomuita Qur'an nikasema, "Ewe Baba yangu! ewe uliyetuita Waislamu angalia! watoto wako wamekhitilafiana baada yako, wamekuwa Mayahudi, Wakristo, na Waislamu. Ama Wayahudi wamekhitilafiana baina yao wakawa makundi sabini na moja nao Wakristo wamekhitilafiana makundi sabini na mbili, Waislamu nao wamekhitilafiana makundi sabini na tatu, na yote yako katika upotofu kama alivyoeleza mwanao Muhammad (s.a.w.), na kwamba kundi moja limebakia kwenye ahadi yako ewe Baba yangu!!"

(Niliendelea kusema), "Je, huo ndio utaratibu wa Mwenyezi Mungu kwa waja wake kama wasemavyo Qadariyyah, kwamba:- Mwenyezi Mungu Mtukufu ndiye yeye alieiandikia kila nafsi iwe Yahudi au Mkristo au Muislamu au Mul-hid au Mshirikina au kuipenda dunia na kujitenga na mafundisho ya Mwenyezi Mungu, yote hayo ni kwa sababu wamemsahau Mwenyezi Mungu basi naye akawasahaulisha nafsi zao. Kwa hakika akiliyangu hainikubalii kusadiki kwamba Qadhaa na Qadar ndiyo iliyoamua hatima ya mtu, bali karibu

91

nikate shauri kwamba Mwenyezi Mungu ndiye aliyetuumba na akatuongoza na akatufahamisha mabaya na mema, na akawatuma kwetu Mitume wake ili watubainishie yanayotutatiza na watujulishe haki kutokana na batili lakini mtu mwenyewe ndiye yaliyemzuga maisha ya dunia na mapambo yake.

Mtu kwa ubinafsi na ujeuri wake, kwa ujinga wake na kujitosa kwake katika mambo yasiyo na faida, na kwa inadi yake na uhasama wake na kwa dhulma yake na kuvuka kwake mpaka ameiacha haki na amemmata shetani na akajitenga na Mwenyezi Mungu, amepotea njia na kula kisicholiwa. Bila ya shaka Qur'an tukufu imekwishalieleza hilo vyema na kulieleza kwa mukhtasari kama ifuatavyo: "Kwa hakika Mwenyezi Mungu hawadhulumu watu kitu chochote lakini watu wanajidhulumu wenyewe (10:44). Ewe baba yetu Ibrahim hawana lawama Mayahudi ambao waliipinga haki kwa kufanya dhulma baina yao pindi ukweli ulipowafikia, basi umma huu aliouokoa Mwenyezi Mungu kupitia kwa mwanao Muhammad, na akautoa kwenye giza na kuupeleka kwenye nuru na kuufanya kuwa ni Umma bora uliotolewa kwa watu, Umma huu nao vile vile umehitilafiana na kufarakana na kukufurishana wao kwa wao na hali ya kuwa Mjumbe wa Mwenyezi Mungu aliwatahadharisha na kuwatanabahisha juu ya hilo na akawasisitiza mno mpaka akasema "Sio halali kwa Muislamu kumnunia nduguye Muislamu zaidi ya siku tatu" umegawanyika na kufarakana na umekuwa vijidola vidogo vidogo vinavyofanyiana uadui vyenyewe kwa vyenyewe na kupigana wao kwa wao na huyu hamjui yule na kumnunia maisha yake yote.

Umma huu una nini Ewe baba yetu Ibrahim baada ya kuwa ulikuwa ni umma bora kuliko umati zingine na ulitawala dunia yote na ukawafikishia watu uongofo, elimu, maarifa na maendeleo, ghafla leo hii umekuwa ni umma mdogo na dhaifu

92

mno, ardhi yao imeporwa na wananchi wake wametawanyika na Msikiti wao Mtakatifu umekaliwa na kupokonywa na Wazayoni na wala hawawezi kuukomboa. Utakapozitembelea nchi zao hakuna utakachokiona isipokuwa umasikini uliopea, njaa inayoua, ardhi kame, maradhi mabaya, na tabia mbaya na wako nyuma kifikra na kiteknolojia, dhulma na ukandamizaji umejaa na kuna uchafu na wadudu.

Itakutosheleza tu (hali hii) iwapo utalinganisha vyoo vya umma viko namna gani huko Ulaya na kwetu sisi vikoje. Msafiri anapoingia kwenye vyoo vyote vya Ulaya atavikuta ni visafi vinanga'ara kama kioo na ndani yake muna harufu nzuri, wakati ambapo katika nchi za Kiislamu msafiri hawezi kuingia katika vyoo kutokana na mvundo wake na najisi na kunuka kwake, nasisi ndiyo ambao Uislamu umetufundisha kwamba "Hakika Usafi ni sehemu ya Imani na uchafu unatokana na shetani". Hivi je imani imehamia Ulaya na shetani anaishi kwetu? Kwa nini Waislamu wamekuwa wanahofu kudhihirisha itikadi yao hata katika miji yao? Ni kwa nini Muislamu hawi hata muamuzi wa mwili wake kiasi kwamba hawezi hata kufuga ndevu wala kuvaa mavazi ya Kiislamu wakati ambapo watu waovu wanajidhihirisha kwa kunywa pombe na zinaa na kuvunja heshima za watu na Muislamu hawezi tena kuwazuia bali hata kuwaamrisha mema na kuwakataza mabaya. Kuna habari zilizonifikia kwamba katika baadhi ya nchi za Kiislamu kama vile Misri na Morocco wapo wazazi ambao huwatuma mabinti zao wakafanye umalaya kutokana na umasikini uliokithiri na shida nying.i lahaula •wala Quwata Ilia Bilahi Alaliyil-adhim, Ewe Mola wangu kwa nini umekuwa mbali na umma huu? Na umeuacha (umma) unahangaika katika giza hapana! hapana! Nakuomba unisamehe Ewe Mola wangu na ninatubia kwako. Bali umma huu wenyewe umekaa mbali na utajo wako na umechagua njia ya shetani, nawe Ewe Mola ambaye hekima yako na Qudra yako vimetukuka umesema na kauli yako ni ya

Rudi nyuma Yaliyomo endelea