Rudi nyuma Yaliyomo endelea

Mmoja wao aliniuliza, "Ni madh-hebu gani yanayofuatwa huko Tunisia?" Nilisema, "Madh-hebu ya Malik"Nikawaona baadhi yao wanacheka lakini sikujali. Akauliza, "Je, madh-hebu ya Jaafariyyah munayafahamu?" Nikasema: Vema Insha-allah jina hili jipya ni kitu gani? hapana sisi hatufahamu isipokuwa madh-hebu manne na yasiyokuwa hayo siyo Uislamu.

Alitabasamu hali ya kuwa anasema "Samahani madh-hebu ya Jaafariyah ndiyo Uislamu halisi, hivi hufahamu kwamba Abu Hanifa amesoma kwa Imam Jaafar As-Sadiq? Na kwa ajili hiyo Abu Hanifa anasema "Lau si miaka miwili, basi Nuuman angeangamia."

59

Nilinyamaza na sikuwa na jawabu, kwa hakika amenifahamisha jina jipya ambalo kabla ya leo nilikuwa sijalisikia lakini nilimshukuru Mwenyezi Mungu kwamba huyu Imam wao Jaafar As-Saadiq hakuwa mwalimu wa Imam Malik, nami nikasema "Sisi ni Malik na siyo Mahanafii." Akasema "Bila shaka madh-hebu hizi ni nne baadhi yao wamesoma kwa baadhi yao (wamesomeshana) kwani Ahmad Ibn Hanbal amesoma kwa Shafii na Shafii kasoma kwa Malik na Malik amesoma kwa Abuhanifa, na Abuhanifah naye kasoma kwa Jaafar As-Sadiq hivyo kwa ajili hii basi wote ni wanafunzi wa Jaafar Ibn Muhammad, naye ndiye mtu wa kwanza kufungua Chuo Kikuu cha Kiislamu ndani ya Msikiti wa babu yake ambaye ni mjumbe wa Mwenyezi Mungu (s.a.a.) na kwake (huyu Jaafar Ibn Muhammad) wamesoma zaidi ya wanachuoni wa hadithi na Fiqhi wapatao elfu nne." Nilimshangaa mvulana huyu hodari ambaye ameyahifadhi maneno ayasemayo kama vile mmoja wetu anavyohifadhi sura fulani ya Qur'an, pia alinishangaza zaidi wakati alipokuwa akinitiririshia baadhi ya vitabu vya rejea za historia ambazo amehifadhi idadi ya juzuu na milango yake, na aliendelea nami mfululizo kama kwamba yeye ni Mwalimu anamsomesha mwanafunzi wake, kwa kweli nilihisi kuwa mimi ni dhaifu mbele yake na nikatamani lau ningetoka pamoja na rafiki yangu badala ya kubakia na wavulana hao." Hapana yeyote miongoni mwao aliyeniuliza kitu kuhusu Fiqhi au Historia isipokuwa nilishindwa kujibu. Aliniuliza "Ni nani ninayemqalid miongoni mwa Maimamu?" nikasema "Imam Malik" akasema "Ni vipi unamfuata mtu ambaye amekwisha kufa? Na baina yako na yeye kuna karne kumi na nne, ikiwa utataka kumuuliza kuhusu mas-ala mapya hivi kweli atakujibu?"

Nilifikiri kwa kitambo na kisha nikasema "Na wewe Jaafari wako amekwisha kufa pia tangu karne kumi na nne hivyo unamqalid nani?" Yule mvulana alijibu kwa haraka yeye na wenzake "Sisi tunamqalid Sayyid Al-Khui, yeye ndiye Imam

60

wetu." Mimi sikuelewa Je, Khui ndiye aliyekuwa mjuzi mno au Jaafari? Nilibakia pamoja nao hali ya kuwa najaribu kubadilisha maudhui, •basi nikawa nawauliza kuhusu kitu chochote kitakacho wasahaulisha wao kuniuliza mimi, hivyo basi nikawauliza kuwa Najaf ina wakazi wangapi, na ni masafa kiasi gani kutoka Najaf hadi Baghdad na je kuna nchi zingine wazijuazo zaidi ya Iraq. Ikawa kila wakinijibu mimi huwauliza swali jingine ili tu niwashughulishe wasiniulize kwani nilishindwa (kuwajibu) na nilihisi kuwa nilikuwa na upungufu, lakini sikukiri (hilo mbelo yao) japokuwa moyoni nilikuwa nimekiri kwani utukufu, heshima na elimu waliyonipachika huko Misri hapo imekuwa kama mvuke na imeyeyuka, hasa baada ya kukutana na hawa wavulana nilitambua ile hekima isemayo:

"Mwambie yule anayedai kuwa yeye ni mwanafalsafa kwamba wewe umefahamu kitu kidogo na mambo mengi hujayafahamu."

Niliona kwamba akili za wavulana hawa ni kubwa kuliko akili za hao Masheikh niliokutana nao (huko Misri) katika chuo cha Az-har na pia ni kubwa kuliko akili za wanachuoni wetu ninaowafahamu huko Tunisia.

Sayyid Al-Khui aliingia akiwa amezungukwa na wanachuoni wenye haiba na utulivu, na wavulana hawa walisimama na wakamfuata Sayyid na kuubusu mkono wake, mimi nilibakia nimesimama mahali pangu, Sayyid alipoketi wote wakaketi na akawa anawasalimu kwa kusema "Mas-saakumullahu Bil-kheir" akimuambia kila mmoja miongoni mwao na hujibu hivyo hivyo hata alipofika kwangu nikamjibu kama nilivyosikia.

Baada ya hapo rafiki yangu aliniashiria nimkurubie Sayyid baada ya kumnongoneza akanikalisha kuliani kwake kisha baada ya kusalimiana rafiki yangu aliniambia "Msimulie Sayyid ni mambo gani mnayoyasikia kuhusu Shia huko Tunisia?"

61

Nikasema "Ndugu yangu zinatosha hizo hekaya tunazozisikia huku na kule, jambo la muhimu ni mimi mwenyewe kufahamu nini wanachokisema Mashia nami ninayo baadhi ya maswali ambayo nataka majibu yake wazi wazi."

Rafiki yangu akanisisitiza na kutilia mkazo nimsimulie Sayyid ni itikadi gani tuliyo nayo juu ya Mashia nikasema:

"Mashia kwetu sisi ni waovu mno dhidi ya Uislamu kuliko Mayahudi na Wakristo, kwa sababu hawa wana muabudu Mwenyezi Mungu na wanaamini Utume wa Nabii Musa (a.s.) wakati ambapo tunayoyasikia kuhusu Mashia ni kwamba, wao wanamuabudu Ali na kumtukuza, na miongoni mwao kuna kundi linalomuabudu Mwenyezi Mungu lakini wao humpa Ali daraja ya Utume wa Mwenyezi Mungu". Pia,nilikisimulia kisa cha Jibril ni namna gani alivyofanya khiyana ya uaminifu kama wasemavyo kwamba, badala ya kupeleka Utume kwa Ali yeye aliupeleka kwa Muhammad (s.a.w.).

Sayyid aliinamisha kichwa chake kidogo kisha akanitazama na akasema, "Sisi tunashuhudia kwamba hapana Mola apaswaye kuabudiwa isipokuwa Mwenyezi Mungu na kwamba Muhammad ni mjumbe wa Mwenyezi Mungu (Mwenyezi Mungu amteremshie sala na salamu yeye na Aali zake walio wema waliotakasika) na Ali ni mja miongoni mwa waja wa Mwenyezi Mungu".

Aliwageukia waliokuwepo hapo hali ya kuwa akisema na kuniashiria "Tazameni masikini hawa ni namna gani unavyowapotosha uvumi wa uongo, na jambo hili siyo geni nimekwisha sikia zaidi ya hayo kutoka kwa watu wengine, Lahaula Walaquwwata Illa Billahil-A liyyil adhim".

Kisha akasema: "Je umesoma Qur'an?" Nikasema, "Nimehifadhi nusu yake kabla sijafika miaka kumi ya umri wangu." Akasema, "Je unafahamu kwamba vikundi vyote vya Kiislamu pamoja na hitilafu ya madh-hebu yao, wanaafikiana

62

kuhusu Qur'an na hii Qur'an tuliyonayo sisi ndiyo ile ile muliyonayo ninyi."

Nikasema, "Ndiyo jambo hili nalifahamu" Akasema "Kwa hiyo basi hujaisoma kauli ya Mwenyezi Mungu mtukufu isemayo, Muhammad hakuwa isipokuwa ni Mtume kwa hakika wamepita kabla yake Mitume" (3:144), pia kauli yake isemayo "Muhammad ni mjumbe wa Mwenyezi Mungu na wale walio pamoja naye ni wenye nguvu dhidi ya makafiri. (48:29) kadhalika kauli nyingine isemayo: "Muhammad si baba wa yeyote katika wanaume wenu, lakini ni mjumbe wa Mwenyezi Mungu naye ndiye mwisho wa Manabii". (35:40)

Nikasema, "Bila shaka ninazifahamu aya hizi." Yeye akasema "Basi yu wapi Ali? Ikiwa Qur'an yetu inasema kwamba Muhanunad ndiye mjumbe wa Mwenyezi Mungu basi uongo huu unatokea wapi?"

Nilinyamaza na sikuwa na jawabu, naye aliongeza kusema "Amma khiyana ya Jibril Mwenyezi Mungu amlinde, hili ni jambo baya zaidi kuliko lile la mwanzo kwa sababu Muhanunad umri wake ulikuwa ni miaka arobaini wakati Mwenyezi Mungu alipomtuma Jibril (a.s.) kwa Muhamad na Ali alikuwa ni mvulana mwenye umri wa miaka sita au saba, basi ewe Bwana ni vipi Jibril atakosea na asiweze kupambanua baina ya Muhammad ambaye ni mtu mzima na Ali ambaye ni mvulana?"

Kisha nilinyamaza kwa muda mrefu, nikiyafikiria maneno yake hali ya kuwa nawaza na kuchambua na nimeyapenda mazungumzo yenye mantiki ambayo yameniingia moyoni na kuondoa kizibo machoni mwangu, na nikajiuliza ndani kwa ndani ni vipi sisi hatukuweza kutatua mambo haya kwa kutumia mantiki hii? Sayyid Al-Khui aliendelea kusema:

"Nakuongezea zaidi ya kwamba Mashia ndiyo kundi pekee kati ya makundi ya Kiislamu linalosema kuwa Mitume na Maimamu

63

ni Maasum, kwa hiyo iwapo Maimamu wetu (a. s.) wamelindwa wasikosee nao ni watu kama sisi, basi itakuwaje kwa Jibril ambaye ni Malaika mwema na Mola mtukufa amemwita kuwa Roho mwaminifu". Mimi nilisema, "Basi uzushi huu umetokea wapi?" Akasema Unatoka kwa maadui wa Uislamu ambao wanataka kuwatenganisha Waislamu na kuwagawanya na kuwachonganisha wao kwa wao, kinyume cha hivyo ni kwamba Waislamu ni ndugu sawa sawa wakiwa ni Mashia au Masunni, kwani wao wanamuabudu Mwenyezi Mungu peke yake na hawamshirikishi na chochote na Qur'an yao ni moja na Mtume wao ni mmoja na kibla yao ni moja na wala Shia na Sunni hawatofautiani isipokuwa katika mambo ya Kifiqhi kama ambavyo Maimam wa Madh-hebu za Kisunni wenyewe wanatofautiana kati yao, Malik anamkhalifu Abu Hanifa na huyu naye anamkhalifu Shafii na kadhalika.

Nikasema: "Kwa hiyo yote yanayosemwa juu yenu ni uzushi mtupu?" Akasema, Al-hamdulilah wewe ni mtu mwenye akili na unafahamu mambo na umekwishaiona miji ya Kishia na umetembea ndani yao basi hivi umeona au kusikia chochote katika uzushi huo?" Nikasema, "Sikusikia wala kuona isipokuwa mambo mazuri, nami kwa hakika namshukuru Mwenyezi Mungu mtukufu aliyenitambulisha kwa Ustadh Mun-im ndani ya boti kwani yeye ndiye sababu ya kuja kwangu Iraq na kwa hakika nimefahamu mambo mengi ambayo nilikuwa siyajui". Rafiki yangu Mun-im alicheka huku akisema, "Na miongoni mwa hayo (usiyoyajua ni kuwepo kwa kaburi la Imam Ali....." Mimi nikamkatiza na kumuwahi hali ya kuwa ninasema "Bali nimejifunza mambo mapya hasa kutoka kwa wavulana hawa, na nimetainani lau kama ningepewa fursa ili nijifimze kama wao katika Chuo cha Elimu hapa."

Sayyid akasema1 "Karibu, nafasi ni yako, ikiwa wewe unataka kusoma Chuo kitakudhamini nasi tupo kwa ajili ya kukuhudumia". Rai hii ilipokelewa na wote waliohudhuria hapo

64

na hasa rafiki yangu Mun-im ambaye uso wake ulionyesha furaha.

Nikasema, "Mimi nimeoa na nina watoto wawili" Akasema, "Sisi tutabeba jukumu la kila mambo yako yanayokulazimu kuanzia makazi, chakula na kila utakachohitajia, jambo muhimu ni kusoma."

Nilifikiri kidogo na nikajisemeza moyoni "Siyo busara mimi kuwa mwanafinzi baada ya kumaliza miaka mitano nikiwa mwalimu ninafundisha na miezi, na siyo jambo rahisi kulichukulia uamuzi jambo kama hili kwa haraka."

Nilimshukuru mno Sayyid Al-Khui kwa ahadi hii (ya kukubali kubeba jukumu) na nikasema "Nitafikiria kuhusu maudhui hii kwa undani baada ya kurejea kwangu toka umra kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu, lakini nina haja ya baadhi yavitabu."

Sayyid akasema, "Mpeni vitabu". Basi kilinyanyuka kikundi cha wanachuoni na wakafungua makabati na punde nilijikuta mbele yangu kuna mijalladi (volume) sabini na kila mmoja aliniletea aina ya vitabu na akasema, "Hii hapa zawadi yangu" niliona kwamba siwezi kubeba idadi hii kubwa ya vitabu hasa kwa kuwa ninaelekea Saudi Arabia ambako hawaruhusu kuingia kitabu chochote katika nchi yao, kwa kuchelea kuenea kwa itikadi ambazo zinakwenda kinyume na Madh-hebu yao, lakini sikupenda kuikosa bahati ya vitabu hivi ambavyo sijawahi kuipata hapo kabla maishani mwangu.

Basi nikamwambia rafiki yangu na wote waliokuwepo hapo kwamba "Safari yangu ni ndefu, inapitia Damascus, Jordan hadi Saudi Arabia, na wakati wa kurudi itakuwa ndefu zaidi kwani nitapita Misri, Libya hadi Tunisia na zaidi ya kuwa mzigo mzito nchi nyingi zinazuwia kuingiza vitabu".

65

Sayyid akasema "Tuachie anuani yako nasi tutabeba jukumu la kukutumia". Niliiona rai hii ni nzuri na niliipenda, nikachukua kadi yangu binafsi yenye anuani yangu ya Tunisia nikampa nikamshukuru kwa wema wake.

Nilipomuaga nikasimama ili nitoke, alisimama pamoja nami hali ya kuwa anasema, "Nakuombea Mwenyezi Mungu akupe salama na utakapofika kwenye kaburi la babu yangu mjumbe wa Mwenyezi Mungu mfikishie salamu zangu".

Watu wote waliathirika nami niliathirika mno hali ya kuwa nayaona macho yake yanatiririka machozi na nikasema moyoni "Haiwezekani mtu huyu kuwa miongoni mwa watu wanaokosea, na haiwezekani mtu huyu kuwa miongoni mwa watu waongo, bila shaka haiba yake, heshima na unyenyekevu wake vinaonesha kweli kwamba yeye anatokana na kizazi kitakatifu, sikuwa na lakufanya isipokuwa niliushika mkono wake nikaubusu bila kujali kwamba alikuwa akiuzuwiya.

Watu wote walinyanyuka niliposimama na wakaniombea salama, na baadhi ya wale wavulana waliokuwa wakijadiliana nami walinifuata na kunitaka anuani yangu ili tuwasiliane nikawapa.

Kwa mara nyingine tena tulielekea mji wa "Kufah" kwa mwaliko wa mmoja wa watu waliokuwa pale kwenye kikao na Sayyid Khui, naye ni rafiki wa yule rafiki yangu Mun-im jina lake ni Abu Shubar.

Tulifika kwake tulikesha usiku wote pamoja na jumla ya vijana wenye taaluma miongoni mwao wakiwa wanafunzi wa Sayyid Muhammad Baaqir Sadir, walinishauri niende nikamzuru Sayyid Baaqir Sadir, waliniahidi kuwa wao watapanga utaratibu wote wa kukutana naye siku iliyofuata.

Rafiki yangu Mun-im aliona ni wazo zuri, isipokuwa alisikitishwa na kutoweza kwake kuhudhuria kwa kuwa alikuwa

66

na kazi mjini Bughdad iliyomlazimu aende. Tulikubaliana nibakie nyumbani kwa Sayyid Abuu-Shubar siku tatu au nne mpaka atakaporudi Mun-im ambaye alituacha baada ya sala ya asubuhi, nasi tulilala alipoondoka. Kwa hakika nilifaidika sana na wanafunzi wale niliokesha nao. Nilistaajabishwa na aina tofauti ya elimu wazisomazo ndani ya Hauza, kwani wao kando na elimu za dini ya Kiislamu kama vile Fiq'hi, Sharia, Tauheed, wanasoma na elimu ya uchumi pia elimu ya kijamii siasa, historia, lugha tofauti na elimu ya Sayari na nyinginezo.

67

KUKUTANA NA SAYYID MUHAMMAD BAQIR AS-SADR

Nilifuatana na Sayyid Abu-Shubbar kwenda kwa Sayyid Muhammad Baqir As-Sadri na tukiwa njiani alikuwa akinienzi na kunipa maelezo yanayohusu wanachuoni mashuhuri pia juu ya Taqlid na mengineyo. Tuliingia nyumbani kwa Sayyid Muhammad Baqir As-Sadri na palikuwa pamejaa wanafunzi wengi wao wakiwa ni vijana wenye vilemba, Sayyid alisimama na kutusalimia kisha walinitambulisha kwake naye akanikaribisha na kunikalisha pembeni yake halafa akaanza kuniuliza habari za Tunisia na Algeria pia kuhusu wanachuoni mashuhuri kama vile Al-Khidhri Hussein na Tahir Ibn Asfur na wengineo.

Nilinufaika kwa mazungumzo yake licha ya ile haiba aliyonayo na heshima wampayo watu wanaoketi pamoja naye, nilijikuta sina uzito wowote na ni kama kwamba nilifahamiana naye toka hapo kabla na nilifaidika kutokana na kikao hicho kwani nilikuwa nikisikiliza maswali ya wanafunzi na majibu ya Sayyid.

Katika kipindi hicho nilifahamu faida ya kuwaqalid wanachuoni walio hai ambao hujibu utata wowote pale pale na kwa uwazi na nikayakinisha vile vile kwamba Mashia ni Waislamu wanaomuabudu Mwenyezi Mungu na wanauamini Utume wa Mtume wetu Muhammad (s.a.w.) kwani baadhi ya

68

shaka zilikuwa zikinihadaa, shetani naye akinitia wasiwasi ya kwamba niliyoyaona hapo kabla ilikuwa ni kuigiza tu na huenda ni kile kitu wakiitacho Taqiyyah (ndicho wanionyeshacho) yaani wao hudhihirisha kile wasichokiamini, kwa haraka mno shaka hii inaondoka na ule wasiwasi nao unadhoofika kwa kuwa haiwezekani kwa hali yoyote ile wote niliowaona na niliowasikia ambao ni mamia ya watu waafikiane juu ya kuigiza na ni kwa nini waigize na mimi ni nani hata (wafanye wasiyoyaamini)? Na nina umuhimu gani kwao hata liwafanye watumie Taqiyyah hii, kisha vitabu vyao vya zamani hivi ambavyo vimeandikwa tangu karne nyingi na vitabu vipya ambavyo vimechapishwa kwa miezi michache tu iliyopita pia vipo na vyote vinampwekesha Mwenyezi Mungu na kumtukuza Mtume wake Muhammad (s.a.w.) kama nilivyolisoma jambo hilo katika utangulizi wake nami sasa hivi niko ndani ya nyumba ya Sayyid Muhammad Baqir-As-Sadri ambaye ni Mar-jaa mashuhuri nchini Iraq na nje ya Iraq pia kila litajwapo jina la Mtume Muhammad wote kwa sauti moja wanasema "Allahuma salli ala Muhammad waali Muhammad."

Ulifika wakati wa sala na tulitoka kwenda Msikitini na ulikuwa karibu ya nyumba ys Sayyid na yeye Sayyid Muhammad Baqir As-Sadri akatusalisha sala ya Adhuhuri na Alasiri, nilijihisi kama kwamba mimi ninaishi miongoni mwa Masahaba watukufu. Sala hizo mbili zilikuwa zikifaatwa na dua nzito iliyosomwa na mmoja wa watu waliokuwa wakiswali humo na alikuwa na sauti ya huzuni.

Na kila akimaliza kusoma dua wote husema kwa sauti za juu: "A llahumma sall Ala Muhammad •waali Muhammad" Du'a yote ilikuwa imejaa sifa na utukufu wa Mwenyezi Mungu mtukufu kisha sifa za Mtume Muhammad na ali zake wema waliotakasika.

Baada ya sala Sayyid alikaa kwenye Mihrab, baadhi yao walianza kumsalimia na kumuuliza kwa siri na wengine wazi

69

wazi, naye alikuwa akiwajibu kwa siri baadhi ya Mas-ala ambayo nilitambua kwamba yanahitajia kujibiwa kwa siri kwani yanahusiana na mambo binafsi naye muulizaji anapopata jawabu alikuwa akiubusu mkono wa Sayyid kisha huondoka na hii ni dalili ya kumpongeza (kumshukuru) mwanachuoni huyu ambaye anatatua matatizo yao na anashirikiana nao katika taabu zao, tulikuwa pamoja na Sayyid na kwa mara nyingine ambapo alinitendea wema na alinipa mapokezi mazuri ambayo yalinisahaulisha watu wangu na jamaa zangu na nikahisi kwamba lau ningebakia pamoja naye kwa mwezi mmoja ningekuwa Shia kutokana na tabia yake na unyenyekevu wake na ushirikiano wake mzuri, kwani kila nikimwangalia yeye hutabasamu na kuanza kunisemesha na kuniuliza, je. kuna kitu fulani kimenipungukia basi nilikuwa simwachi kwa muda wote wa siku nne isipokuwa wakati wa kulala, licha ya wageni wengi na wanachuoni waliokuwa wakifika kwake toka nchi mbali mbali.

Niliwaona Wasaudia huko na sikudhania kabisa kwamba katika nchi ya Hijaz wako Mashia, pia wanachuoni wa Bahrain na wengine toka Qatar na Imarat na kutoka Lebanon, Syria, Iran, Afghanistan na Turkey na pia toka Afrika nyeusi. Na Sayyid alikuwa akizungumza nao na kuwakidhia haja zao na walikuwa wakitoka hali ya kuwa ni wenye faraha.

Hapo sitaacha kueleza tukio nililoliona na nilishangaa namna lilivyotatuliwa, nami nalitaja kwa ajili ya kumbukumbu ya kihistoria kutokana na umuhimu wake mkubwa ili Waislamu wapate kufahamu ni kwa kiasi gani wamepata hasara kwa kuacha hukumu ya Mwenyezi Mungu.

Kuna watu wanne walikuja kwa Sayyid Muhammad Baqir As-Sadr na nadhani Wairaq nilifahamu hilo kutokana na lahaja yao. Mmoja wao alirithi makazi fulani toka kwa babu yake aliyefariki miaka mingi iliyopita na huyu bwana akapauza mahali hapo kwa mtu mwingine ambaye alikuwepo (siku hiyo)

70

na baada ya kupita mwaka tangu kuuzwa mahala hapo, kuna ndugu wawili walikuja kuthibitisha kwamba wao ni warithi wa Kisheria wa Mar-hum yule, na wote wanne walikaa mbele ya Sayyid na kila mmoja wao akatoa nyaraka zake na ushahidi alionao.

Baada ya Sayyid kusoma nyaraka zao na akazungumza nao kwa muda wa dakika chache aliwaamulia tatizo lao kwa uadilifa, akampa yule mnunuzi haki ya kutumia mahala pale na akamtaka yule muuzaji awape wale ndugu wawili fungu lao kutoka kwenye thamani aliyoichukua kisha wote walisimama na kuubusu mkono wa Sayyid na wakakumbatiana.

Nilishangazwa na hali hii na sikuamini, ndipo nilipomuuliza Abu Shubbar "Je tatizo hili ndiyo limemalizika?" Akasema, "Limekwisha na kila mmoja amechukua haki yake" Subhanallah!! kiurahisi namna hii na kwa muda mchache kama huu, dakika chache zinatosha kusuluhisha ugomvi? Kwa hakika tatizo kama hili nchini kwetu linachukua muda wa miaka kumi kwa uchache na baadhi yao hufariki na watoto wao kuendelea kulifuatilia tatizo, na gharama za mahakama na watu wa kuwatetea huweza wakati mwingine kugharimu ile thamani ya makazi yenyewe, na huanzia mahakama ya mwanzo kisha mahakama ya Hakimu Mkazi na hatimaye kwenda mahakama ya rufaa na mwisho wote huwa hawaridhiki baada ya kuwa wamesumbuka, kutaabika, kupoteza pesa na rushwa, hatimaye uadui na chuki (hujitokeza) miongoni mwa ndugu na jamaa."

Abu Shubbar alinijibu "Hata sisi hali ni ile ile au zaidi" mimi nikasema "Vipi" akasema, "Watu wanapopeleka mashitaka yao kwenye mahakama za kiserikali basi hali inakuwa kama hiyo uliyoisimulia ama wakiwa ni watu wanaomqalid Mar-jaa wa kidini na wanafuata hukumu za Kiislamu, basi hawapeleki mashitaka yao isipokuwa kwa Mwanachuoni huyo naye huwatatulia kwa dakika chache kama ulivyoona. Na ni nani

71

mwenye hukumu nzuri kuliko MwenyeziMungu kwa watu wenye akili? Sayyid Sadr hakuchukua kwao japo senti moja, na lau wangekwenda  kwenye  Mahakama  za  Serikali wangenyanyasika." Nilicheka kutokana na maelezo haya ambayo kwetu pia inatendeka na kisha nikasema "Subhanallah!! Mimi bado siamini haya niliyoyaona na lau nisingeshuhudia kwa macho yangu kamwe nisingesadiki" Abu Shubbar akasema, "Usipinge ndugu yangu hili uliloliona ni dogo ukilinganisha na matukio mengine ambayo yana utata mkubwa na husababisha damu kumwagika, lakini pamoja na hali huyo Mar-jaa huweza kuyasuluhisha kwa muda mchache."

Nilisema hali ya kuwa nastaajabu, "Kwa hiyo ninyi hapa Iraq munazo serikali mbili, serikali ya Dola na Serikali ya watu wa dini," akasema, "Sivyo tuliyonayo ni Serikali ya Dola peke yake lakini Waislamu wa Kishia ambao wanawaqalid Mar-jaa wa kidini hawajishughulishi na Serikali isiyo ya Kiislamu, wao wanaitii katika mambo ya uraia, kodi, haki za nchi na mazingira binafsi, na lau Muislamu mwenye kushika dini atagombana na mmoja wa Waislamu wasioshika dini basi atalazimika kupeleka tatizo lake kwenye Mahakama za Serikali kwani huyu mwingine hawezi kuridhia kuamuliwa na Wanachuoni wa kidini, na ama waliohitilafiana wakiwa ni watu wenye kushika dini, basi hapo hakuna tatizo, na kile atakachokiamua Mar-jaa wote watakikubali. Na kwa msingi huu matatizo ambayo huhukumiwa na Mar-jaa hutatuliwa siku hiyo hiyo, wakati ambapo matatizo mengine (yanayohukumiwa kwingine) huendelea kwa miaka mingi."

Kwa hakika hili ni tukio lililoitingisha nafsi yangu, zile hisia za kuiridhia hukumu ya Mwenyezi Mungu Mtukufu na nikaifahamu ile maana ya kauli ya Mwenyezi Mungu iliyoko katika kitabu chake kitukufu aliposema: "Na asiye hukumu kwa mujibu wa hukumu aliyoiteremsha Mwenyezi Mungu watu hao ni makafiri, na asiye hukumu kwa mujibu wa hukumu

72

aliyoiteremsha Mwenyezi Mungu watu hao ni madhalimu, na asiye hukumu kwa mujibu wa hukumu aliyoiteremsha Mwenyezi Mungu watu hao ni mafasiki (5:44, 45, 47). Mwenyezi Mungu Mtukufo amesema kweli.

Kama ambavyo pia liliamsha katika nafsi yangu hisia za kuchukia na kuwapinga wadhalimu hawa ambao wanazibadilisha hukumu adilifu za Mwenyezi Mungu kwa kuleta hukumu na kanuni za wanadamu ambazo ni za kijeuri na wala yote hayo hayawatoshi bali wanazikosoa bila aibu na kuzikebehi hukumu za Mwenyezi Mungu, na wanasema kuwa ni za kikatili na kishenzi kwa kuwa zinaweka adhabu ya kumkata mkono mwizi na kumpiga mawe mzinifu na kumuuwa muuwaji.

Basi nadharia hii ya kigeni imetujia kutoka wapi (na ikawa) dhidi ya mirathi yetu hapana shaka hiyo ni nadharia toka nchi za Magharibi na kwa maadui wa Uislamu ambao wameona kuwa kuzitumikisha hukumu za Mwenyezi Mungu kutamanisha kuwaangamiza wao moja kwa moja kwa kuwa wao ni wezi, mahaini wazinifu na ni waovu na wauaji. Na lau hukumu za Mwenyezi Mungu zingetekelezwa dhidi yao basi tungeepukana na watu wote wa aina hii.

Katika kipindi hicho cha kuwepo Najaf yalikuwa yakifanyika mazungumzo kati yangu na Sayyid Muhammad Al-Baqir na nilikuwa nikimuuliza kila jambo dogo na kubwa kufuatia mambo niliyokuwa nimeyafahamu kupitia kwa marafiki zangu ambao walinisimulia mengi juu ya itikadi yao na kile wakisemacho juu ya Masahaba (r.a.) na kile wanachokiamini kuhusu Maimamu kumi na mbili yaani Ali na wanawe na mambo mengine ambayo sisi tunahitilafiana nao.

Nilimuuliza Sayyid juu ya Imam Ali na ni kwa nini wanamshuhudia kwenye adhana kwamba yeye ni walii wa Mwenyezi Mungu? Alinijibu akasema "Kwa hakika Amirul-muuminina Ali amani ya Mwenyezi Mungu imshukie, yeye ni

73

mja miongoni mwa waja wa Mwenyezi Mungu ambao amewachagua na kuwatukuza ili waendeleze jukumu zito la ujumbe baada ya Mitume, na watu wa namna hii ni mawasii wa Mitume kwani kila Nabii anayewasii wake na Ali ibn Abitalib ni wasii wa Muhammad, nasi tunamboresha juu ya masahaba wengine kwa vile Mwenyezi Mungu na Mtume wake wamemboresha. Na kuhusu hali hii sisi tunazo dalili za kiakili na zingine ni zile za Qur'an na Sunna, na dalili zote hizi haiwezekani kuingiwa na shaka kwani ni mutawatir kwa njia zetu na hata kwa njia za Ahlu-Sunnah wal-Jamaa, pia wanachuoni wetu wametunga vitabu vingi juu ya jambo hilo lakini ilipokuwa utawala wa Banu-Umaiyyah umesimama kidete kufuta ukweli huu na kumpiga vita Amirul-Muuminina Ali na wanawe na kuwaua, na mambo yakafikia kumtukana na kumlaani juu ya mimbari za Waislamu na kuwalazimisha watu kwa nguvu wamtukane na kumlaani, ndipo Mashia wake na wafuasi wake (r.a.) wanashuhudia kwamba Ali ni walii wa Mwenyezi Mungu na haifai kwa Muislamu kumtukana walii wa Mwenyezi Mungu, na walifanya hivyo ili kuonesha upinzani wao kwa Tawala dhalimu. Ili utukufu uwe ni wa Mwenyezi Mungu na Mtume wake na waumini na ili (kushuhudia huko) kuwe ni msukumo wa kihistoria kwa Waislamu wote katika vizazi vyote wapate kufahamu ukweli juu ya Ali (a.s.) na uovu wa maadui zake. Wanachuoni wetu wameendelea kushuhudia kwamba Ali (a.s.) ni walii wa Mwenyezi Mungu katika adhana kwa kupendekeza kuwa ni jambo jema na wala siyo kuwa ni sehemu ya adhana au Iqamah, basi iwapo muadhini au mwenye kuqim atanuwia kuwa ni sehemu ya Adhana, Adhaaa na Iqama yake vitabatilika. Na mambo mustahabu ndani ya Ibada na matendo ni mengi mno na Muislamu hupata thawabu kwa kuyatenda wala haadhibiwi kwa kuyaacha, kwa mfano imekuja kwamba ni mustahabbu baada ya kushuhudia kwamba hapana Mola apasiwaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu, na kwamba Muhammad ni mjumbe wake, Muislamu

74

aseme nashuhudia kwamba pepo ni kweli na moto ni kweli (upo) na kwamba Mwenyezi Mungu atawafufua waliomo makaburini."

Mimi nikasema "Wanachuoni wetu wametufundisha kwamba, ukweli halisi ni kuwa khalifa bora mno ni Sayyidna Abubakar As-Sidiq, kisha Sayyidna Umar, Al-Faruq kisha Sayyidna Uthman na kisha Sayyidna Ali Mwenyezi Mungu awe radhi nao wote." Sayyid alinyamaza kisha akanijibu, "Wanao uhuru wa kusema wapendavyo, lakini hawawezi kulithibitisha hilo kwa dalili za kisheria, kisha kauli hii inakhalifu maelezo yaliyomo ndani ya vitabu vyao sahihi vya kutegemewa, ndani ya vitabu hivyo imeelezwa kwamba mtu mbora mno kuliko watu wote ni Abubakr kisha Omar kisha Othman na wala Ali hayumo bali wamemfanya kuwa ni mtu wa kawaida tu, isipokuwa ametajwa na wanachuoni wa baadaye kwamba ni mustahabbu kumtaja miongoni mwa Ma-Khalafatur-Rashiduna."

Baada ya hilo nilimuuliza juu ya udongo wanao utumia kusujudu juu yake ambao wanauita "Tur-batul-Husaniniyyah" alinijibu akasema "Kabla ya yote inakupasa ufahamu kwamba sisi tunasujudu juu ya udongo na wala hatusujudii udongo kama baadhi ya watu wanavyodhani na hatimaye kuwazushia uongo Mashia. Sijda ni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu Mtukufu peke yake, na kilichothibiti kwetu sisi na kwa Masunni ni kwamba, kilichobora ni kusujudu juu ya ardhi au kitu kilichoota ardhini kisicholiwa, na wala haisihi kusujudu juu ya kitu kinginecho na Mjumbe wa Mwenyezi Mungu alikuwa akitandika udongo na akitumia jamvi lililotengenezwa kwa udongo na makuti na husujudu juu yake, na aliwafundisha Masahaba wake (r.a.) wakawa wanasujudu juu ya ardhi na changarawe, na akawakataza yeyote kati yao asisujudu kwenye ncha ya nguo yake, mambo haya kwetu sisi yanajuli'kana bila haja ya dalili.

75

Imam Ali ibn Husein ambaye ni mashuhuri kwa jina la Zainul Abidina (a.s.) naye ni bwana wawanaosujudu alichukua udongo wa kaburi la baba yake Abu Abdillah (Imam Husein a.s.) kwa kujua kwamba huo ni udongo uliotakasika na ambao damu za mashahidi zimemwagika juu yake, na Mashia wake wakaendelea kufanya hivyo mpaka leo, basi sisi hatusemi kwamba kusujudu hakusihi isipokuwa juu ya udongo huo, bali tukisemacho ni kwamba, Sijda inasihi juu ya udongo wowote na jiwe lolote lenye tahara kama inavyosihi kusujudu juu ya jamvi na kilichotengenezwa kwa makuti ya mtende na mfano wa hicho."

Nikamuuliza Sayyid kuhusu kumbukumbu ya Saydna Husein (r.a.), "Je, ni kwa nini Mashia wanalia na kujipiga wenyewe mpaka damu inawatoka hali ya kuwa jambo hili katika Uislamu ni haramu, kwani Mtume (s.a.w.) amesema: "Si miongoni mwetu atakayejipiga mashavu na kuchana mifuko na akalingania mwito wa kijahiliya."

Sayyid akajibu, "Hadithi hii ni sahihi lakini haiendani na maombolezo ya Abdillah (Husein ibn Ali a.s.) kwani mtu anaelingania kisasi kwa Husein huyo yuko katika njia ya Husein, na katika mwito wa Husein na wala siyo mwito wa kijahiliya. Kisha ieleweke kuwa Mashia ni watu, miongoni mwao kuna mwanachuoni na mjinga, na wanahisia za kimaumbile ya kibinadamu, hivyo basi endapo miongoni mwao kuna ambaye hisia zake za kimaumbile zimechemka na kumshinda kwa ajili ya kukumbuka jinsi alivyokufa kishahidi Abu Abdilahi na yale aliyotendewa yeye na watu wa nyumba yake na waliyotendewa masahaba wake kwa kuuwawa kikatili, kuwavunjia hadhi yao ya kibinadamu na kuchukuliwa mateka, bila shaka wenye kufanya hayo watalipwa mema kwa nia zao, kwa kuwa (wamefanya kwa) ajili ya Mwenyezi Mungu, na Mwenyezi Mungu humlipa mtu ujira kulingana na nia yake.

Rudi nyuma Yaliyomo endelea