Rudi nyuma Yaliyomo endelea

Hapa sita acha kueleza kwamba darasa walizokuwa wakizifanya ni za kiroho, kwani Sheikh alikuwa akizifungua kwa kusoma aya chache za kitabu cha Mwenyezi Mungu kwa Taj-wiid, kisha baada ya kumaliza huanza kusoma Qasida na humfua wale muridi ambao wamehifadhi Mad-hi na Dhikri ambazo nyingi miongoni mwa hizo ni za kuishutumu Dunia na kupendelea Akhera, na ndani yake zina mafunzo ya uchamungu, baada ya hapo Murid wa kwanza aliyekaa kuliani mwa Sheikh hurudia kusoma aya chache za Qur'an, na anaposema "Sadaqallahul-Adhim" Sheikh huanzisha upya Qasida na wote hushiriki kuiimba basi hivyo hivyo hupokea waliohudhuria kusoma japo aya moja, na hushirikiana' hivyo mpaka wote waenee, na huwa wanayumbayumba kulia na kushoto kwa kufuata sauti ya Mad-hi hizo na hatimaye Sheikh hunyanyuka na Muridi nao hunyanyuka pamoja naye na hufanywa duara

20

yeye Sheikh huwa katikati yake na huanza kufanya dhikiri kwa kusema "AAH AAH AAH" naye Sheikh akizunguka katikati yao hali ya kumuelekea kila mara mmoja miongoni mwao mpaka panakuwa mtikisiko mkubwa kiasi cha kuufananisha na ngoma, na huruka baadhi yao huku na huko kama wamepatwa na kichaa na sauti za kuimba huwa kubwa zilizopangika, lakini zinakera na mwisho utulivu hurejea baada ya shida na taabu, kwa Sheikh kusoma Qasida ya mwisho, kisha wote hukaa baada ya kukibusu kichwa cha Sheikh na mabega yake mmoja baada ya mwingine.

Nami nilishirikiana nao katika harakati hizi nikiwafuatisha tu lakini bila ya ridhaa yangu, na kwa kufanya hivyo nilijikuta nikipingana na itikadi yangu niliyokuwa nimechagua nayo ni kutokumshirikisha Mwenyezi Mungu kutokutawasal kwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu basi nilianguka chini nikawa karibu kulia hali ya kuwa nimechanganyikiwa mawazo yamegawanyika baina ya fikra mbili zinazopingana, fikra ya kisufi ambayo ni undani wa kiroho anaoishi nao mtu na humjaza undani wake hisiya za kitawa na kujikurubisha kwa Mwenyezi Mungu kwa njia ya mawalii wake wema na waja wake wenye uchamungu, na fikra (nyengine) ya Kiwahabi ambayo ilinifundisha kuwa yote hayo ni kumshirikisha Mwenyezi Mungu na Mwenyezi Mungu hausamehi ushirikina.

Na iwapo Muhammad mjumbe wa Mwenyezi Mungu (S.A.W.) hanufaishi kitu wala hapafanywi Tawasul kwa Mwenyezi Mungu kupitia kwake, basi wana daraja gani mawalii hawa na watu wema'waliokuja baada yake?

Japokuwa (nilikuwa na) cheo kipya alichonipa Sheikh kwani nilikwishakuwa wakili wake katika mji wa Qafsah ndani ya nafsi yangu sikukubaliana moja kwa moja ingawa wakati mwingine nilikuwa nikielekea kwenye Tarika za kisufi na siku zote nikihisi kuwa ndani ya nafsi yangu kumejificha heshima kubwa kwa hii twarika kwa ajili ya Mawalii wa Mungu na watu

21

wema miongoni mwa waja wa Mungu, lakini nikipinga na kujadili kwa kutumia kauli ya Mwenyezi Mungu isemayo "Wala usimuombe pamoja na Mwenyezi Mungu mwingine" (28:88). Na ikiwa mtu ataniambia kwamba Mwenyezi Mungu mtukufu anasema: "Enyi mulio amini mcheni Mwenyezi Mungu na tafuteni wasila wa kumfikia" (5:35) nitamjibu kwa haraka kama walivyonifunza wanachuoni wa Kisaudi. "Wasila ni matendo mema"

Jambo la muhimu ni kwamba katika kipindi hicho niliishi hali ya kuwa nimechanganyikiwa fikra yangu ikiwa ni yenye kutatizwa, na wakati mwinyine baadhi ya Murid (Wafuasi wa Tariqa) wakija nyumbani kwangu na tunakesha na tukifanya dhikri (ile ya Aah,.,,,.)

Basi majirani walianza kunung'unika kutokana na sauti zinazokera amabazo zinatokea kooni kwa kufanya dhikri ya "Aaah" lakini walikuwa hawanidhihirishii mimi jambo hilo bali wao humlalamikia  mke wangu kupitia kwa wanawake zao, na nilipotamabua hilo niliwaomba hawa wafanye hafla hizo katika moja ya nyumba zao, na nikawaomba radhi kwa kuwaambia kwamba mimi huenda nikasafiri nje ya nchi kwa muda wa miezi mitatu na niliwaaga ndugu na jamaa nikaazimia (safari) hali ya kuwa nimetegemea kwa Mwenyezi Mungu bila ya kumshirikisha na chochote.

22

SAFARI YENYE MAFANIKIO

23

NIKIWA MISRI

Sikukaa sana Tripoli ambao ni Mji mkuu Wa Libya isipokuwa kiasi cha kupata visa kutoka kwa Balozi wa Misri ili niweze kuingia katika ardhi ya Kinanah (Misri),

Na huko nilikutana na baadhi ya marafiki zangu wakanisaidia (kupata visa) Mwenyezi Mungu awalipe mema kwa juhudi zao hizo, na wakati nikiwa njiani kuelekea Cairo, safari ambayo ni ndefu inayochukua muda wa siku tatu mchana na usiku, nilipanda ndani ya gari ya kukodi ambayo nilishirikiana na Wamisri wanne wanaofanya kazi Libya na walikuwa wakirudi nchini kwao.

Tukiwa safarini nilikuwa nikiwazungumzisha na kuwasomea Qur'an basi walinipenda mno na kila mmoja wao akanitaka nifikie nyumbani kwake, nami nilimchagua mmoja wao ambaye nafsi yangu iliridhika naye kutokana na uchamungu wake na jina lake akiitwa Ahmad, alinikaribisha na kunipokea ipasavyo, Mwenyezi Mungu amlipe mema.

Nilikaa muda wa siku ishirini mjini Cairo, na katika kipindi hicho nilimtembelea mwanamuziki aitwaye Farid Al-Atrash katika jumba lake lililoko kando kando ya mto Nile, tangu hapo mwanzo nilikuwa nikimpenda kutokana na maelezo niliyokuwa nimeyasoma ndani ya magazeti ya Misri yanayouzwa huko kwetu Tunisia kuhusu tabia yake na unyenyekevu wake, na sikuwa na bahati ya kukaa naye muda mrefu isipokuwa

24

dakika ishirini tu kwani alikuwa akitoka kuelekea uwanja wa ndege ili asafiri kwenda Lebanon, na nilimtembelea sheikh Abdul-Basit Muhamad Abdus-Samad, ambaye ni msomaji mashuhuri wa Tajwid nami nilikuwa nikimpenda mno, na nilibaki pamoja naye kwa muda wa siku tatu.

Wakati tukiwa naye nilikuwa nikifanya majadiliano na nduguze na marafiki zake kuhusu maudhui mbali mbali, nao walikuwa wakifurahiwa na hamasa yangu na ukunjufu wangu na maarifa yangu mengi hivyo basi wakizungumzia juu ya mambo ya sanaa kwangu ni kama nyimbo. Na wakizungumza juu ya uchamungu na Tasawuf, niliwaeleza kuwa mimi ni mwana Tarika ya Tijaniyah na pia Madaniyyah, na wakizungumza kuhusu ulimwengu wa Magharibi, mimi huwasimulia habari za Paris, Londoni, Ubelgij, Holland, Italia na Hispania ambazo nilizitembelea wakati wa likizo ya kiangazi, na wakiongea habari za Hijja, basi mimi huwajibu kwamba mimi nilikwisha hiji na sasa nakwenda Umrah, na niliwasimulia •sehemu ambazo

hawazifahamu hata watu waliokwisha Hijji mara saba, kama vile pango la Hiraa na pango la Thaur na madhabahu ya Nabii Ismail (a.s.).

Na iwapo watazungumza habari za Sayansi na Teknolojia mimi nitawatosheleza shauku yao kwa kuwapa mifano na Istilahi mbalimbali na wakiongea juu ya Siasa basi mimi huwakatiza kwa mtazamo nilionao hali ya kusema:

"Mwenyezi Mungu amrehemu Nasir Salah Din Al-Ayyub ambaye alijiharamishia kutabasamu sembuse kucheka, na pindi watu wa karibu yake walipomlaumu na wakamwambia mjumbe wa Mwenyezi Mungu alikuwa ni mwenye tabasamu wakati wote aliwajibu, "vipi mimi munanitaka nitabasamu wakati Msikiti wa Aqsa unakaliwa na maadui wa Mwenyezi Mungu hapana Wallah} sitatabasamu mpaka niukomboe au nife kwa ajiliyake."             ,

25

Na wakati huo Masheikh wa Azhar walikuwa wakihudhuria vikao hivyo na wakifurahiwa na mambo niliyoyahifadhi miongoni mwa hadithi na aya (za Qur'an) na hoja zenye nguvu nilizokuwa nazo, basi walikuwa wakiniuliza kuhusu chuo nilichosoma hivyo mimi hujifahamisha kwa kuwaambia kwamba nimemaliza masomo yangu katika chuo kikuu cha Zaituniyah ambacho kimeasisiwa kabla ya  Azhar tukufu, nanikiongeza kwamba hao Fatimiyya walio iasisi Azhar walitokea katika mji wa Mah-diyyah nchini Tunisia.

Pia nilifahamiana na wanachuoni wengi wakubwa katika chuo kikuu cha Az-har ambao walinizawadia baadhi ya vitabu, na siku moja nilipokuwa ndani ya ofisi ya mmoja wa wasimamizi wa mambo yanayohusu chuo cha Az-har, alikuja mjumbe fulani wa Baraza la Mapinduzi la Misri na akamtaka ahudhurie mkutano wa Waislam na wakuu wengine kwenye shirika kubwa mno miongoni mwa mashirika ya Reli Kairo baada ya matokeo ya uharibifu yaliyofanyika baada ya vita vya mwezi June vya Waarabu na Waisraeli. Akakataa kwenda isipokuwa nifuatane naye na huko kwenye kikao nilikaa katika meza ya wageni waheshimiwa kati ya wanachuoni wa Misri na Abu Shanadah na wakanitaka nihutubie mbele ya wageni waalikwa nami nililifanya hilo kwa wepesi kwa kuwa nimezowea kutoa mihadhara Misikitini na katika kamati za Utamaduni nchini mwangu.

Jambo muhimu kuliko yote niliyoyasimulia katika mlango huu ni zile hisia zangu zilianza kutakabari na nikapandwa na baadhi ya majivuno na nikadhani kabisa kwamba mimi nimekwisha kuwa Mwanachuoni na ni kwa nini nisihisi hivyo hali ya kuwa Wanachuoni wa Chuo cha Az-hari walinishuhudia kwa hilo na wako miongoni mwao waliosema:

inapasa mahala pako pawe ni hapa katika chuo cha Az-har.

Na miongoni mwa mambo yaliyoniongezea fahari na majivuno ni kwamba mjumbe wa Mwenyezi Mungu

26

ameniruhusu kuingia na kuona vitu alivyoviacha kama alivyodai muangalizi wa Msikiti wa Sayyidina Hussein ulioko Cairo na aliniingiza peke yangu kwenye chumba ambacho hakifunguliwi na mwingine isipokuwa yeye na aliufunga mlango baada yangu na akanifungulia sanduku na akatoa kanzu ya mjumbe wa Mwenyezi Mungu (S.A.W.) basi nikaibusu, na kanionyesha baadhi ya mabaki mengineyo na nilitoka humo huku nikilia nikiwa nimeathirika juu ya upendeleo wa Mtume (S.A.W.) alionifanyia mimi binafsi na khasa huyu mwangalizi hakunidai pesa yoyote, bali alikataa na akachukua kidogo tu baada ya kumsisitiza achukue, na alinipongeza na kunibashiria kwamba mimi ni miongoni mwa waliokubaliwa mbele ya mtukufu Mtume(s.a.w.w.).

Na huenda tukio hili liliathiri katika nafsi yangu na likanifanya niwe ninafikiri mno kwa siku kadhaa yale mambo wayasemayo Mawahabi kwamba Mtume (S.A.W.) amekwisha kufa basi mambo yake yamekwisha kama ilivyo kwa watu wengine basi sikuiafiki fikra hii, bali niliyakinisha upotofu wa itikadi hii kwani ikiwa shahidi aliyeuawa katika njia ya Mwenyezi Mungu si maiti bali yuhai na anaruzukiwa mbele ya Mola wake, basi vipi isiwe kwa Bwana wa mwanzo na wa mwisho (Mtume Muhammad S.A.W.) na jambo hili liliongeza hisiya na nguvu na mwanga wa mafunzo niliyoyapata hapo nyuma katika uhai wangu miongoni mwa mafunzo ya masufi ambao huwapa Mawalii wao na Masheikh zao uwezo na athari katika kutenda mambo na wanakiri kwamba Mwenyezi Mungu peke yake ndiye ambaye aliyewapatia uwezo huu kwa kuwa wao walimtii na wakayapenda mema yaliyoko kwake.

Je? siye Mwenyezi Mungu (s.w.t.) aliyesema ndani ya hadith Qud'si kwamba "Mja wangu nitii utakuwa kama mimi utakiambia kitu kuwa kitakuwa".

Ushindani wa ndani kwa ndani ulianza kunivuta, na muda wa kubakia kwangu Misri ulimalizika baada ya kuwa

27

nilikuwa nikizuru Misikiti mingi katika kipindi hicho na nilisali katika Misikiti yote katika Misri kutoka ile ya Madh-hebu ya Malik hadi ile ya Abuhanifah na ile ya Shafii na Ahmad ibn Hanbal kisha kwa Bibi Zainab na Sayyidina Husein kama ambavyo nilitembelea zawiya ya Tijani na kuhusu hiyo ninayo mengi ya kusimulia ambayo itachukua muda mrefu kuyafafanua nami nimeona ni bora kufanya muhtasari.

28

MKUTANO NDANI YA BOTI

Nilisafiri kwenda Alexandria katika siku maalum, mahali ambapo huegesha boti za Misri zinazosafiri kwenda Beirut, na nilijikuta mwili na fikra vimechoka, na nilijilaza juu ya kitanda changu, basi nikalala kidogo, na boti ilikuwa imeng'oa nanga kiasi cha saa mbili au tatu zilizopita na niliamshwa na sauti ya jirani yangu aliyesema "Yaonyesha huyu ndugu amechoka".

Nilisema "Ndiyo, safari ya kutoka Cairo kwenda Alexandria imenichokesha kwani niliamka mapema ili niweze kufika kwa wakati uliyopangwa hivyo basi jana sikulala isipokuwa kidogo."

Na kutokana na Lahaja yake nilitambua kuwa siyo Mmisri, na udadisi wangu kama ilivyo kawaida yangu ulinishawishi nitake kumfahamu, basi nikajitambulisha mimi kwanza ndipo nilipofahamu kwamba yeye ni Muiraq na ni Mwalimu katika Chuo Kikuu cha Baghdad na jina lake ni Mun-im na alikuja Cairo kuwasilisha maandiko yake ya shahada ya udaktari katika Chuo cha Azhar,

Basi tulianza mazungumzo yanayohusu Misri na ulimwengu wa Kiarabu wa Kiislamu na kuhusu kushindwa kwa Waarabu na ushindi wa Wayahudi na mazungumzo yenye kuhuzunisha, basi mimi nilisema katika msingi wa maneno yangu kuwa sababu ya kushindwa huku ni kugawanyika kwa Waarabu na Waislamu kwenye dola ndogo ndogo na vikundi na Madh-

29

hebu mengi licha ya wingi wao kwa idadi, basi hawana uzito wala mazingatio katika mtazamo wa maadui zao.

Tulizungumza sana kuhusu Misri na Wamisri na tulikuwa tukiafikiana juu ya sababu za kushindwa nami niliongezea kwamba mimi ninapinga mgawanyiko huu ambao wakoloni wanautilia mkazo miongoni mwetu ili iwe rahisi kwa kututawala na kutudhalilisha nasi bado tunatofautisha baina ya Mad-hab ya Malik na Mahanafi na nilisimulia kisa cha kuhuzunisha  kilichonipata wakati nilipoingia katika Msikiti wa Mahznafi mjini Cairo na nikasali nao sala ya Alasiri kwa jamaa mara gafla baada ya sala, mtu aliyekuwa kasimama pembeni yangu akaniambia kwa hasira "Kwa nini hufungi mikono katika Sala'? Mimi nikamjibu kwa heshima na adabu kwamba, "Wafuasi wa Malik hawafungi mikono nami ni Malik" akaniambia  "Nenda kwenye Msikiti wa Malik na ukaswali huko", basi nilitoka hali ya kuwa nimechukia tena mwenye uchungu kutokana na tendo hili lililoniongezea tatizo juu ya tatizo,

Basi mara yule Mwalimu wa Kiiraq akatabasamu na kuniambia kuwa yeye ni Shia. Kutokana na habari hii nilichanganyikiwa  na nikasema bila kujali kwamba, "Lau ninge jua  kuwa wewe ni Shia basi nisingezungumza nawe" akasema, "Kwa nini?"

 Mimi nikasema, "Ninyi siyo Waislamu kwani nyinyi

mnamuabudu Ali ibn Abi talib, na walio afadhali miongoni mwenu wanamuabudu Mwenyezi Mungu lakini nao hawaamini utume wa Mtume Muhammad (s.a.w.) na wanao mshutumu Jibril na wanasema kuwa, yeye alifanya khiyana badala ya kupeleka utume kwa Ali akaupeleka kwa Muhammad." Na niliendelea kuzungumza mambo kama haya wakati ambapo rafiki yangu alikuwa akitabasamu na wakati mwingine alikuwa

akisema, "lahaula Walaquwata Illa Billah" Ishara ya kuonyesha

30

kushangazwa. Nilipomaliza maneno yangu aliniuliza tena, "Wewe ni mwalimu unayesomesha wanafunzi?" Nikasema, "Ndiyo" akasema "Basi ikiwa fikra za Waalimu ziko katika hali hii hapana lawama kwa watu wengine wa kawaida ambao hawana elimu". Nikasema, "Unakusudia nini?" Alijibu, "Samahani, lakini ni wapi ulikoyapata madai haya ya urongo?" Nikasema, "Katika vitabu vya historia ambavyo ni mashuhuri kwa watu wote". Akasema, "Tuachane na watu wote lakini ni kitabu gani cha historia ulichokisoma?"

Nilianza kuorodhesha baadhi ya vitabu kama vile FaJ-rul-Islam na Dhuhal-Islam na Dhuhri Al-Islam vya Ahmad Amin na vyenginevyo. Akasema, "Tangu lini Ahmad Amin amekuwa ndiyo hoja dhidi ya Mashia, akaongeza kusema hakika uadilifu na ukinzani ulio sawa ni kuyabainisha mambo kutoka katika rejea zao asilia zilizo mashuhuri". Mimi nikasema, "Basi nitawajibika vipi kubainisha jambo ambalo linaeleweka kwa watu wote?"

Yeye akasema, "Huyu Ahmad Amin yeye mwenyewe alizuru Iraq nami nilikuwa miongoni mwa walimu waliokutana naye huko Najaf, na tulipomlaumu kuhusu maandiko yake juu ya Shia, aliomba radhi kwa kusema kuwa, mimi sina chochote ninachokijua juu yenu, na kwa hakika sijawahi kukutana na Shia hapo kabla na hii ndiyo mara yangu ya kwanza kukutana na Shia."

Sisi tulimwambia, "Huenda udhuru ulio utowa ni jambo baya zaidi kuliko kosa ulilolitenda kwani ni vipi ulikuwa hujui chochote kutuhusu siye nawe ukaandika kila kitu kibaya dhidi yetu?"

Kisha aliendelea akasema, "Ewe ndugu yangu sisi tutakapoyahukumu makosa ya Wayahudi na Wakristo kwa kutumia Qur'an tukufu ambayo kwetu sisi ni hoja madhubuti, basi mtazamo wetu huu utakuwa dhaifu kwa sababu wao

31

hawaikubali Qur'an, na hoja yetu itakuwa madhubuti yenye nguvu tu ikiwa tutayabainisha makosa yao kwa mujibu wa vitabu vyao wanavyoviamini na hili litakuwa katika mizani ya "Ameshuhudia shahidi kutoka kwao wenyewe". (12:26)

Maneno yake yalitua ndani ya moyo wangu kama yanavyoshuka maji katika moyo wa mtu mwenye kiu na nilijikuta ninabadilika kutoka katika hali ya mpinzani na kuelekea kwenye hali ya mtu mwenye kutafuta na kuchunguza, kwani (maneno yake) niliyahisi kuwa ni yenye mantiki iliyosalimika na ni hoja yenye nguvu, basi sikuwa na budi isipokuwa lau nitatulia kidogo na kumsikiliza, nandiponilipomwambia, "Kwa hiyo nawe ni miongoni mwa wanao itakidi ujumbe wa Mtume wetu Muhammad (s.a.w.)?"

Akanijibu, "Na Mashia wote ni kama mimi wanaitakidi hivyo na ni juu yako wewe ndugu yangu kulithibitisha hilo wewe mwenyewe ili usiwe na shaka na jambo hili na usiwadhanie nduguzo Mashia dhana mbali mbali kwani baadhi ya dhana ni makosa" Na aliendelea kusema, "Na ikiwa kweli unataka kujua ukweli na kuyaona hayo kwa macho yako na moyo wako Uyakinishe basi mimi nakualika utembelee Iraq na ukutane na Wanachuoni wa Kishia na watu wa kawaida na ndipo Utakapo ufahamu uongo wa watu wenye dhamira mbaya".

Nikasema, "Hakika matumaini yangu yalikuwa kwamba siku moja niitembelee nchi ya Iraq ili nione kumbukumbu zake mashuhuri  za Kiislamu ambazo ziliachwa na watawala wa Kibani abbas hasa hasa Harun Rashid lakini kwanza uwezo Wangu wa mali hautoshi kwani nimeupanga kuniwezesha kufanya  umra, pili paspoti yangu niliyonayo hainiruhusu kuingia lraq" Yeye akasema: "Kwanza nilipokuwa nimekualika kutembelea  Iraq hiyo ilikuwa na maana kwamba mimi nitabeba jukumu Ia matumizi ya safari yako kutoka Beirut hadi Baghdad kwenda na kurudi na makazi yako huko Iraq utakuwa pamoja

32

nami nyumbani kwangu wewe ni mgeni wangu, na pili kuhusu paspoti ambayo haikuruhusu kuingia Iraq, hilo tumwachie Mwenyezi Mungu mtukufu, kama amekukadiria kuizuru Iraq basi hilo litawezekana hata bila ya pasipoti na tutajitahidi kupata viza ya kuingia Iraq tutakapofika Beirut".

Nilifurahi sana kupata bahati hii na nikamwahidi rafiki yangu kwamba apendapo Mwenyezi Mungu kesho nitampajibu.

Nilitoka katika chumba cha kulala na nikapanda juu ya boti ili nivute hewa mpya hali ya kuwa nafikiria kwa makini fikra mpya na akili yangu imekwenda na mandhari ya bahari ambayo imetandaa upeo wangu wa macho na huku namhimidi na kumtakasa Mola wangu aliyeumba ulimwengu na nikimshukuru kwa kunifikisha mahala hapa na nikimuomba Mwenyezi Mungu anilinde kutokana na shari na watu wenye shari na anihifadhi kutokana na kupotoka na kukosea.

Mawazo yangu yalifika mbali wakati nilipokuwa nikiyakumbuka mbele ya macho yangu matukio niliyokutana nayo na nilikumbuka hali ya mafanikio tangu utotoni mwangu mpaka siku hiyo, na nilikuwa nikiota mustaqbali bora na nikihisi kama kwamba Mwenyezi Mungu na Mtume wake wamenizunguka kwa ulinzi makhususi niligeuka upande wa Misri ambayo sehemu ya pwani yake ilikuwa bado ikionekana katika wakati wote hali ya kuwa naiaga nchi hiyo ambayo ndani yake nimeibusu kanzu ya mjumbe wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.) nacho ni kitu pekee cha thamani kubwa kilichobakia katika kumbukumbu nilizo kutana nazo nchini Misri.

Hatimaye nilianza kuyakumbuka maneno mageni ya yule Shia ambaye aliingiza kwangu furaha kubwa itakayoithibitisha ndoto yangu iliyokuwa ikinipitia tangu nilipokuwa mdogo, nayo si nyingine ball ni kuizuru nchi ya Iraq, nchi ambayo inanikumbusha mahakama ya Al-Rashid na Maamuni ambaye ndiye muanzilishi wa Darul-Hikmah ambayo

33

wasomi wa elimu mbali mbali wakienda kutoka nchi za magharibi zama za maendeleo makubwa ya Kiislamu.

Zaidi ya hayo Iraq ni nchi ya yule kiongozi wa kiroho bwana wangu Sheikh Abdul-Qadir Jaylani ambaye sifa zake zimeenea ulimwengu wote na Tariqa yake imeingia katika kila mji na nguvu ya Tariqa yake imeshinda kila Tariqa. Basi kwa mara nyingine haya hapa tena mapenzi yatokayo kwa Mwenyezi Mungu ili kuithibitisha ndoto hii. Hivyo nilianza kuwaza na kuogelea katika bahari ya mawazo na matumaini mpaka kiliponizindua kipaza sauti cha boti ambacho kinawatangazia wasafiri waende kwenye mgahawa ili wakajipatie chakula cha jioni nami nilikwenda mahali palipotajwa, basi watu walikuwa wakisongamana kama kawaida yao wanapokuwa katika kila mkusanyiko, na kila mmoja anataka kuingia kabla ya mwenziwe na makelele yakawa mengi na pia fujo.

Mara ghafla yule Shia alinishika nguo yangu na kunivuta taratibu nyuma hali ya kuwa anasema, "Njoo ndugu yangu usijisumbue sisi tutakula baadaye bila ya kusukumana na kwa hakika nilikuwa nakutafuta kila mahali".

Kisha aliniuliza, "Je umekwisha Swali?" Nikasema "Bado sijaswali" Akaniambia njoo basi tuswali kisha tuje kula wakati hawa jamaa wamemaliza fujo na makelele (yao).

Niliipenda rai yake na nikafuatana naye mpaka mahali ambapo hapakuwa na watu ambapo nilitawadha na kumtanguliza yeye awe Imamu, lakini nilikuwa nimekusudia kumchunguza namna anavyoswali nami baadaye nitarudia kuiswali swala yangu, na mara alipoqim sala ili kutekeleza faradhi ya Magharibi na kuanza kusoma visomo vya sala na kuomba dua, kiasi kwamba mtazamo wangu ulibadilika. Na kwa hakika niliwaza kwamba mimi ninaswali nyuma ya mmoja wa masahaba watukufu ambao ninasoma habari zao kuhusu uchamungu wao.

34

Baada ya kuwa (yule Shia) amemaliza kuswali aliomba dua ndefu ambayo nilikuwa sijaisikia dua kama hiyo nchini kwetu wala katika nchi ninazozifahamu, na nilikwa nikituliza (moyo) na kumrahi kila alipomswalia mtume na ali zake na kumsifu vile anavyostahiki.

Na baada ya sala niliona machoni mwake kuna athari za machozi kama ambavyo nilimsikia akimuomba Mwenyezi Mungu anifungulie maono yangu na aniongoe.

Tulielekea kwenye mgahawa ambao ulikwisha anza kuwa hauna watu wanaokula nasi tukaingia, basi (yule Shia) hakukaa mpaka alipokwisha kunikalisha mimi na tukaletewa sahani mbili za chakula, nikamuona anabadilisha sahani yake kwa sahani yangu, kwani sehemu yangu ilikuwa na nyama chache kuliko sehemu yake na akaanza kunihimiza kula kama kwamba mimi ni mgeni wake na akinifanyia wema na kunisimulia masimulizi yanayohusu kula na kunywa na adabu za kukaa kwenye meza ya chakula, (masimulizi) ambayo hapo kabla sijawahi kuyasikia.

Nilifurahishwa na tabia yake na alitusalisha sala ya Isha na kuomba dua ndefu mpaka aliniliza kwa dua hiyo nami nikamuomba Mwenyezi Mungu mtukufu aibadilishe dhana yangu juu yake kwani baadhi ya dhana ni makosa, lakini ni nani ajuaye?

Nililala hali ya kuwa naota Iraq na Al-fulela-ulela na niliamka kwa mwito wake alipokuwa akiniamsha kwa ajili ya Swala ya Alfajiri na tulisali na tukaketi tukizungumza neema za Mwenyezi Mungu juu ya Waislamu.

Tulirudi tena kulala na nilipoamka nilimkuta amekaa kitandani kwake na mkononi mwake ameshika tasbihi anamdhukuru Mwenyezi Mungu, nafsi yangu iliburudika kwa ajili yake na moyo wangu ukatulizana kwa ajili yake nami nikamuomba Mola wangu anisamehe.

35

Tulikuwa tukila ndani ya mgahawa wakati tuliposikia kipaza sauti kinatangaza kwamba boti inakurubia kuinyia pwani ya Lebanon na huenda tukawa katika bandari ya Beirut baada ya saa mbili kwa uwezo wake Mwenyezi Mungu basi aliniuliza, "Je umefikiria kwa undani na umeamua nini1"7

Nikasema, "Mwenyezi Mungu atakaponiwepesishia kupata viza ya kuinyia Iraq, mimi sina kipingamizi na nikamshukuru kwa mwaliko wake", Tuliteremka Beirut ambapo tuliumaliza usiku ule na kutoka Beirut tulisafiri hadi Damascus ambapo tulipofika tu tulielekea Ubalozi wa Iraq na nikapata viza kwa haraka mno kiasi ambacho sikutegemea na tulitoka huko na hali ya kuwa ananipongeza na kumuhimidi Mwenyezi Mungu kwa msaada wake.

36

ZIYARA YA IRAQ KWA MARA VA KWANZA

Tulisafiri kutoka Damascus hadi Baghdad katika gari moja kubwa lenye kipoza hewa linalomilikiwa na shirika kubwa la kimataifa la Al-Najaf hali ya joto ilikuwa digrii 40% ya hapo Baghdad, na tulipofika tu mara moja tulielekea nyumbani kwake katika mtaa wa Jamillah, na niliingia ndani ya nyumba iliyokuwa na kipoza hewa na nikapumzika kisha aliniletea kanzu ambayo wao wanaiita "Dishdashah".

Alileta matunda na chakula na watu wa nyumbani mwake waliingia na kunisalimia kwa adabu na heshima na baba yake alikuwa akinikumbatia kama kwamba ananifahamu tangu hapo mwanzo, ama mama yake alisimama mlangoni akiwa amevaa baibui nyeusi akanisalimia na kunikaribisha.

Rafiki yangu aliniomba radhi kuhusu mama yake (kwa kutonipa mkono) kwani wao Mashia kupeana mkono na mwanamke asiye maharam kwao ni haramu. Nilistaajabu mno na nikijisemesha mwenye (moyoni) "Hawa ndio tunaowatuhumu kwamba wametoka nje ya dini lakini wao ndiyo wanao ihifadhi dini zaidi kuliko sisi".

Na nimeona katika masiku ya safari nilipokuwa pamoja naye tabia bora na utukufu wa nafsi, utu na unyenyekevu na ucha Mungu ambao sikuufahamu hapo kabla.

Nilijihisi kuwa mimi siyo mgeni bali kama kwamba niko

37

nyumbani mwangu.

Usiku tulipanda juu ya paa la nyumba ambapo palikuwa pametandikwa kwa ajili yetu ili tulale na sikupata usingizi hadi usiku wa manane, na weweseka je naota au niko macho ni kweli kwamba mimi  niko Baghdad karibu ya Sayyid yangu Abdul-Qadir Al-Jailan? Rafiki yangu alicheka hali ya kuwa anauliza  wanasema nini Watunisia juu ya huyu Abdul-Qadir AI-Jailani?

Nilianza kumsimulia kuhusu karama ambazo twasimuliwa na kwamba yeye ni Qutbud-Dairah, kama ambavyo Muhammad ni mjumbe wa Mwenyezi Mungu na ni Bwana wa Mitume, basi Abdul-Qadir ni bwana wa mawalii na unyayo wake uko juu ya kila walii naye anasema: "Watu wote wanaitufu nyumba (Al-kaaba) mara saba nami nitaitufu pamoja na mahema yangu",

Kwa hiyo nilijaribu kumkinaisha kwamba Sheikh Abdul-Qadir huwa anawajia baadhi ya muridi wake na wapenzi wake wazi wazi na kuwaponya maradhi yao na kuwafariji kutokana na matatizo yao na niliisahau au tuseme nilijisahaulisha itikadi ya Kiwahabi ambayo niliathirika nayo kwamba yote hayo (niyasemayo) ni kumshirikisha Mwenyezi Mungu na nilipohisi kwamba rafiki yangu hahamasiki nilijaribu kukinaisha nafsi yangu kwamba niliyoyasema siyo sahihi na nikamuuliza nini maoni yake.

Rafiki yangu alisema hali ya kuwa anacheka "Usiku huu lala na pumzika kutokana na machovu yaliyokupata safarini na kesho apendapo Mwenyezi Mungu tutamzuru Sheikh Abdul-Qadir". Nilifurahi kwa habari hii na nikatamani alfajiri ingechomoza wakati huo huo lakini machovu -yalikuwa yamenizidi, basi hatimaye nililala usingizi mzito hadi sala ya asubuhi ilinipita kwani niliamka baada ya kuchomoza jua. Yule rafiki yangu alinijulisha kuwa alijaribu mara kadhaa kuniamsha bila mafanikio akaniacha ili nipumzike.

38

ABDUL-QADIR AL-JAILAN NA MUSA AL-KADHIM

Baada ya kifungua kinywa tulikwenda kwa Sheikh na niliiona Maqaam ambayo muda mrefu nimekuwa nikitamani kuizuru na nilitembea kwa haraka kama kwamba mimi nina hamu ya kumuona na niliingia kwa pupa na majonzi kama kwamba nitajitupa miguuni pake na rafiki yangu alikuwa akinifuata kila nilipokwenda, nilichanganyika na watu waliokuwa wakizuru (hapo) ambao walifurika kwenye Maqaam hiyo kama wanavyofurika Mahujaji kwenye nyumba ya Mwenyezi Mungu tukufu, miongoni mwa watu hao walikuwemo waliokuwa wakirusha pipi, na wenye kuzuru sehemu hiyo huzigombea kuziokota, nami nikakimbilia kuchukua mbili kati ya hizo nikala moja kwa haraka ili nipate baraka na nyingine nikaificha mfukoni mwangu kwa ajili ya kumbu kumbu.

Niliswali huko na kuomba dua chache kisha nikanywa maji na nilijiona kama nakunywa maji ya zamzam na nilimtaka rafiki yangu anisubiri kidogo ili niandike postakadi chache nilizozinunua huko kuwapelekea marafiki zangu wa Tunisia na postakadi zote zilikuwa na picha ya Quba la kijani la Sheikh Abdul-Qadir Al-Jailan na kwa kufanya hivyo nilikuwa nataka kuwaonesha marafiki zangu na ndugu zangu walioko Tunisia

39

juu yajuhudi zangu kubwa zilizonifikisha kwenye Maqam hiyo ambayo wao hawajafika.

Baada ya hapo tulikula chakula cha mchana katika mgahawa uitwao MAT-AM SHAABI ulioko katikati ya mji, kisha rafiki yangu alinichukua katika taxi mpaka Kadhimiyyh. Jina hili nililitambua pindi rafiki yangu alipotaja kumwambia dereva wa Gari, na tulifika huko.

Na tuliposhuka kwenye gari tukitembea tulichanganyika na idadi kubwa ya watu wakielekea tuendako, wake kwa waume na watoto na wamebeba baadhi ya mizigo, hali hii ilinikumbusha msimu wa Hijja na nilikuwa sijaelewa ni upande gani unaokusudiwa mpaka yalipojitokeza Maqubah na minara ya dhahabu inayong'ara na hapo nilitambua kwamba huu ni msikiti miongoni mwa misikiti ya Mashia kwa kuwa hapo kabla nilikuwa nikifahamu kwamba wao huipamba misikiti yao kwa dhahabu na fedha, jambo ambalo Uislamu umeliharamisha, na nilihisi vibaya kuingia msikiti huo isipokuwa tu kwa kuchunga hisia ya rafiki yangu nilimfuata bila kupenda.

Tuliingia kupitia mlango wa kwanza na hapo nilianza kuona Wazee wakiishika na kuibusu milango nami nilijiliwaza kwa kusomaubao mkubwa ulioandikwa "Ni marufuku kuingia wanawake wasiokuwa na Hijab" maandishi hayo yaliambatana na hadith ya Imam Ali isemayo, "Kunawakati utawafikia watu, wanawake watatoka nje hali ya kuwa wamevaa nguo zinazoonyesha (miili yao)...." mpaka mwisho wa hadithi.

Rudi nyuma Yaliyomo endelea