Yaliyomo endelea

Kisha nikaongoka

MUHAMMAD AL-TIJANI AL-SAMAWI

UTANGULIZI

بسم الله الرحمن الرحـيم

الحمدلله رب العالمين والصلوة والسلام علي خير خلقه محمد وآله الطاهرين

Kitabu kilichopo mikononi mwako ni tafsiri ya Kitabu cha Kiarabu, kiitwacho Thummah-tadaytu, kilichoandikwa na Shaykh Muhammad Tijani Samawi wa Tunisia. Katika Kitabu hiki ameelezea kuhusu safari yake kuelekea kwenye Imani ya Kishi'a. Kitabu hiki kimekuwa maarufu katika ulimwengu wa Kiislamu na tayari kimetafsiriwa katika lugha za Kiingereza, Urdu na Kifarsi. Maulamaa wengi katika Afrika ya Mashariki wametuomba kukitafsiri kitabu hiki katika lugha ya Kiswahili pia.

Nilimuomba Shaykh Musabah Shabani Mapinda kukitafsiri kitabu hiki katika lugha ya Kiswahili kutoka kwenye asili yake

ya lugha ya Kiarabu. Namshukuru kwa kukubali ombi langu na kuifanya kazi hii kwa moyo mmoja. Nimeiangalia pamoja naye tafsiri hii kwa makini kuhakikisha kuwa maudhui yake ya asili hayakupotoshwa katika lugha ya Kiswahili.

Mission inasikitika kusema kuwa miaka mingi sasa  imepita hadi kitabu hiki kupelekwa kwa wachapaji. hata hivyo tunamshukuru Allah Subhanahu wa Ta'ala na wale wote wanaotuunga mkono kwa njia moja au nyingine kwa kufanikisha kuchapishwa kitabu hiki. Tunamuomba Mwenyezi Mungu

(s.w.t.) awalipe malipo mema hapa Duniani na  baadae huko Akhera. Amin.

Shaykh Tijani Samawi ameandika vitabu vitatu zaidi  baada ya kitabu hiki; na Shaykh wetu Shaykh Musabah Shabani ametafsiri pia vitabu viwili vifuatavyo kwa lugha ya  Kiswahili:

7. Fas'alu Ahladhdhikr (Waulizeni  wanaofahamu)

 2. Li Akuna Ma 'as-Sadiqin (Niwe pamoju na Wakweli)

Vitabu hivi viwili vimekwishapangwa katika Kompyuta na kama wasomaji watakipenda hiki kitabu cha  hivi sasa, tutakuwa na ari ya kufanya mipango ya kuvichapisha "Inshallah".

Mission inatoa shukurani zake za dhati kwa Mfasiri na kwa wale wote waliosaidia kwa njia moja au nyingine katika uchapishaji wa kitabu hiki.

Dar-es-Salaam 15 Shaban 1420

24 November 1999

Sayyid Saed Akhtar Rizviy Mhubiri mkuu

ZAWADI

Kitabu changu ni kidogo hakina mikogo ndani yake, nacho (kinahusu) kisa cha safari, kisa ambacho ni cha uvumbuzi mpya, siyo uvumbuzi (unaohusu) ulimwengu wa kiufundi na mazingira, lakini kinahusu (uvumbuzi) wa Dunia ya kiitikadi katika wingi wa madhehebu na falsafa za kidini.

Na ilipokuwa uvumbuzi unategemea kwanza, akili iliyosalimika na fahamu madhubuti ambayo ndio iliomtenganisha mtu na viumbe wengine.

Basi mimi ninakitoa zawadi kitabu changu kwa kila mwenye akili iliyosalimika ambayo itachambua na kuifahamu haki kutokana na mkusanyiko wa batili na atayapima maneno kwa mizani ya uadilifu na kuunga mkono kile kinachokubalika kiakili, na kulinganisha maneno na mazungumzo, kisha atabaini hoja inayokubalika kiakili kutokana na ile isiyokubalika kiakili na hoja yenye nguvu kutokana na hoja dhaifu.

Mwenyezi Mungu anasema:-

"Wabashirie waja wangu ambao wanasikiliza maneno na kufuata yale yaliyo mazuri mno, hao ndiyo ambao Mwenyezi Mungu amewaongoza, nawao ndiyo wenye akili."

Basi kwa wote hawa natoa zawadi ya kitabu changu hiki hali ya kuwa nikitaraji kutoka kwa Mwenyezi Mungu mtukufu atufungulie fahamu zetu kabla ya macho yetu na atuongoe na azitie nuru nyoyo zetu na atuonyeshe haki kuwa

ni haki waziwazi nasi tuifaate, na atuonyeshe upotofu kuwa ni upotofu bila kificho ndani yake na tujiepushe nao, na atuingize katika waja wake wema kwa hakika yeye ni mwenye kusikia, mwenye kujibu (maombi).

KWA JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHEMA MWENYE KUREHEMU

DIBAJI

Sifa zote njema anastahiki Mwenyezi Mungu Mola wa walimwengu, ambaye amemuumba mtu kutokana na udongo akamuweka katika umbo bora, na akamfadhilisha juu ya viumbe wengine na (akawaamuru) Malaika wake watakatif'u wamsujudie, na akamtukuza kwa (kumpa) akili ambayo hubadilisha shaka yake na kuwa yakini, na akamjaalia macho mawili na ulimi na midomo miwili na akamuonyesha njia mbili, kisha akamtumia Mitume wenye kubashiria mema na wenye kuonya maovu ili wamzindue na wamlinde kutokana na upotovu wa ibilisi aliyelaaniwa, na akamuagiza kuwa asimuabudu shetani kwani shetani ni adui aliyedhahiri kwake na (akamuagiza) amuabudu Mwenyezi Mungu peke yake na afuate njia iliyonyooka, hali ya kuwa ni mwenye kutambua uongofu na imani na Elimu ya yakini, hatimaye (akamuagiza) kuwa katika itikadi yake asifuate jamaa na ndugu na wazazi waliotangulia, ambao waliwafuata waliokuwa kabla yao bila ya dalili iliyowazi wala hoja, basi ni nani mwenye kauli njema kuliko yule anayelingania (watu) kwa Mwenyezi Mungu na akatenda mema na akasema bila shaka mimi ni miongoni mwa waliojisalimisha (kwa Mwenyezi Mungu).

Na (kisha) Rehma za Mola wangu na salamu zake na baraka zake zimshukie (Mtume) aliyetumwa kuwa  ni rehma kwa walimwengu, mtetezi wa wenye kudhulumiwa na wenye kudhalilishwa, muokozi wa Wanaadamu kutoka kwenye upotovu wa wajinga na kumuelekeza kwenye uongofu wa waumini (naye) ni Bwana wetu na msimamizi wetu Ibn Abdillahi, ambaye ndiye Mtume wa Waislam.

Na ziwashukie ali zake wema watakatifu ambao Mwenyezi Mungu amewateua juu ya viumbe  wengine ili wawe ni kigezo cha waumini, na mnara  wa wenye  kutambua na ni alama ya wakweli na wenye utakaso wa moyo, na  (Mwenyezi Mungu) amewajibisha ndani ya Qur'an tukufu kuwapenda, baada ya kuwa amewaondolea uchafu na    kuwajalia  kuwa miongoni mwa Maasumina, na akamuahidi kuokoka mwenye kupanda safina yao, na  mwenye kuwapa mgongo atakuwa miongoni mwa wenye kuangamia, na (Rehma na amani   ziwashukie Masahaba wake Mtume) wenye baraka, ambao walimtetea na wakamsaidia na  wakamtukuza na wakajitole nafsi zao kwa ajili ya kuinusuru dini, na wakaifahamu haki   kisha wakampa ahadi ya utii kwa yakini, na walisimama  imara baada  yake katika njia ya haki na wala hawakugeuza wala kubadilisha na walikuwa miongoni mwa wenye kushukuru, basi Mwenyezi Mungu awalipe mema kwa kuutumikia uislaam  na Waislamu na (pia rehma na amani) ziwashukie Waliowafuatia  na wapitao njia ya uongofu wao mpaka siku ya kiyama,

Mola wangu nikubalie (kazi yangu) kwa hakika wewe ni mwenye kusikia mwenye kujua, na uukunjue moyo wangu kwani wewe ndiyo mwenye kuongoa kwenye yakini ya kweli na fungua mfundo wa ulimi wangu kwani wewe ndiye mwenye kutoa hekima kwa yule umtakaye miongoni mwa waja wako wenye kuamini Mola wangu nizidishie Elimu na unikutanishe na watu wema.

HALI YA MAISHA YANGU KWA UFUPI

Bado nakumbuka namna baba yangu mzazi alivyonichukua kwenda naye kwenye Msikiti ulioko mtaani, ambamo husaliwa sala ya Tarawehe katika Mwezi wa Ramadhani, na umri wangu ulikuwa miaka kumi, na akanitanguliza kwa watu wanaosali ambao kunifurahia kwao (nijambo ambalo) halikufichikana.

Tangu hapo kabla nilikuwa nafahamu kwamba Mwalimu alikuwa amepanga nisalishe sala ya Tarawehe siku mbili au tatu. Kwa kawaida ilikuwa nikiswali nyuma ya sala ya jamaa pamoja na kundi la watoto wa mtaani nami nikisubiri Imam (wa msikiti ule) afikie kwenye nusu ya Qur'an inayofuatia yaani katika surah MAR-YAM, na Baba yangu mzazi alikuwa anahima tujifunze Qur'an katika Madrasa na nyumbani katika vipindi vya usiku vilivyokuwa vikisimamiwa na Imam wa Msikiti mkuu ambaye ni jamaa yetu aliyekuwa kipofu na amehifadhi Qur'an tukufu, basi mimi nilikuwa nimehifadhi nusu ya Qur'an katika umri huo mdogo, kwa hiyo Mwalimu alitaka kudhihirisha ubora wake na juhudi yake kupitia kwangu, akanifundisha vituo vya kusimama katika kusoma na akanikaririsha mara nyingi ili athibitishe kuwa nimeifahamu.....

Baada ya kufaulu kwangu Mtihani na kumalizika sala na kisomo katika sala yajamaa tena vizuri kama alivyokuwa

akitarajia mzazi wangu na mwalimu, watu wale walinifuata wakinibusu na kufurahiwa na wakimshukuru mwalimu aliyenifunza na kumpongeza mzazi wangu, na wote wakimshukuru Mwenyezi Mungu juu ya neema ya Uislamu na baraka za Sheikh.

Huenda kumbukumbu ya mambo niliyo niliyo pata baada ya tukio hilo haitafutika katika maisha yangu kutokana kufurahiwa kwa watu na mimi na umashuhuri ambao ulivuka mtaa wetu na kuenea mji wote, na masiku hayo ya Ramadhani yaliweka athari ya kiitikadi katika maisha yangu na  athari hiyo imebakia mpaka leo, na hali hiyo ni kwa kuwa kila nilipokuwa nikiteleza, basi nilihisi nguvu ya ajabu inanisukuma  na kunirejesha kwenye umadhubuti, na kila nilipohisi unyonge na uzembe wa kibinafsi hasi kumbukumbu hizo huninyanyua  na kuniweka kwenye daraja za juu kiroho na huwasha miali  ya imani katika dhamira yangu ili niweze kuyabeba  majukumu.

Na ni kama kwamba jukumu hilo alilonibebesha mzazi wangu na (tuseme) zaidi mwalimu wangu, juu ya kuonyoza sala ya jamaa katika umri ule mdogo, lilinifanya siku zote nione kuwa mimi sijaweza kufikia kiwango ninacho kikusudia, au niko chini ya kiwango kitakiwacho kwangu,

Kwa hiyo niliutumia muda wa utoto wangu na ujana wangu katika muongozo kwa kiwango fulani bila ya kuepukana na mchezo na utashi unaotawaliwa wakati mwingi na utoto na kupenda kujua na kuiga, hali ya kuwa uangalizi wa kiungu ukinizunguka ili niwe mwenye kutambulikana baina ya ndugu zangu kwa umakini na utulivu na  kutokuteleza katika maasi na maovu.

Sitaacha kueleza kwamba mama yangu (Mwenyezi Mungu amrehenmu) alikuwa na athari kubwa katika maisha yangu, kwa hakika ndiye aliyeyafungua  macho yangu kwa kunifundisha sura fupi fupi za Qur'an tukufu kama ambavyo

alinifunza sala na Tahara, na kwa hakika alinisimamia   kwa uangalizi wa pekee kwani mimi ndiye mwanawe wa kwanza.

Na alikuwa akimuona mke mwenzie ndani ya nyumba hiyo hiyo ambaye alimtangulia kwa miaka mingi na ana  watoto wengi ambao wako waliokuwa wakimkaribia (Mama yangu) kwa umri, hivyo basi alikuwa akisimamia malezi yangu na mafunzo yangu kama kwamba anafanya ushindani na mke mwenzie na watoto wa mum ewe.

Najina la Tijani alilonipa Mama yangu lina ubora wa kipekee kwa familia zote za Wasamawi ambao wameikubali Tarika ya Tijaniya na wamedumu nayo tangu mmoja wa watoto wa Sheikh Sayed Ahmad Tijani alipozuru mji wa Qafsah akitokea Algeria na akafikia katika nyumba ya Msamawi, basi wengi miongoni mwa watu wa mjini hasa familia za watu wenye elimu na matajiri wakaikubali Tarika hii ya Kisufi na wakaipupia, na kwa ajili ya jina langu nimekuwa ni mwenye kupendwa katika mji wa Wasamawi ambao unakaliwa na zaidi ya familia Ishirini na pia nje yake ni miongoni mwa wale ambao wanayo maungamano na Tarika ya Tijaniyah. Kwa ajili hiyo wengi wa wazee waliokuwa wakisali ambao walikuwepo katika yale masiku ya Ramadhani niliyoyataja walikuwa wakibusu kichwa changu na mikono yangu hali ya kuwa wakimpongeza mzazi wangu na wakimuambia:

"Hizi ni miongoni mwa baraka za Bwana wetu Sheikh Ahmad Tijani" Kwa kweli inafaa kusema kwamba Tarika ya Tijaniyah imeenea kwa wingi huko Morocco, Algeria, Tunisia, Libya, Sudan na Misri, na kwamba wanaokubali Tarika hii wanayo namna fulani ya kuishikilia Itikadi yao kwani hawazuru Makaburi ya Mawalii wengine kwa kuwa (Wanaamini kwamba) Mawalii wote wamesoma kutoka kwa baadhi yao kwa kuachiziana isipokuwa Sheikh Ahmad Tijani yeye amechukua elimu yake moja kwa moja toka kwa mjumbe wa Mwenyezi

Mungu (S.A.W.)japokuwa amekuja baada ya zama za utume kwa karne kumi na tatu, na wanasimulia kwamba yeye Sheikh Ahmad Tijani alikuwa akieleza kuwa mjumbe wa Mwenyezi Mungu (S.A.W.) alimjia akiwa macho siyo usingizini, kama ambavyo wanasema kwamba dua kamili aliyoitunga Sheikh wao ni bora kuliko khitimisho la Qur'an tukufu mara arobaini,

Ili tusije tukatoka nje ya kufupisha maelezo, tunaishia hapa kuhusu taarifa ya Tijaniyah tutawarudia tena Mwenyezi Mungu apendapo katika sehemu nyingine ya kitabu hiki.

Kwa hiyo basi nililelewa na kukulia katika itikadi hii kama ilivyo kwa vijana wengine wa mjini kwetu, sisi sote Al-hamdulilah tukiwa ni Waislam katika Ahli Sunnah wal-Jamaah ndani ya madh-hebu ya Maliki Ibn Anas ambaye ni Imam wa mji wa Hijra (Madina) isipokuwa tumegawanyika katika Tarika za kisufi ambazo ni nyingi mno huko kaskazini mwa Afrika, kwani katika mji wa Qafsah peke yake kuna Tarika za Tijaniyyah, Qadiriyah, Rahmaniyah, Salamiyah na Aisawiyah, na kila Tarika inao wafuasi wanaohifadhi kasida zake na dhikri zake na nyiradi zake ambazo hufanywa katika hafla na mikesha katika Minasaba ya ndoa au khitani au mafanikio au nadhiri, na japokuwa yako baadhi ya mambo yasiyokubalika (katika sheria) tarika hizi zimefanya kazi kubwa kuhifadhi mambo matukufu ya dini na kuwaheshimu mawalii na watu wema.

10

SAFARI YA KWENDA KUHIJI NYUMBA TUKUFU YA MWENYEZI MUNGU.

Umri wangu ulikuwa miaka kumi na minane wakati Jumuiya ya Taifa ya maskauti wa Tunisia iliponiita kwa ajili ya kwenda kushiriki kwenye mkutano wa Maskauti wa nchi za Kiarabu na Kiislamu, (mkutano) ambao ulifanyika katika mji mtakatifu wa Makkah nami nikiwa ndani ya ujumbe wa watu sita mashuhuri wa Jamhuri ya Tunisia.

Nilijikuta kuwa mimi ndiye rndogo kwa umri miongoni mwa wajumbe waliotumwa na mwenye elimu-ndogo kuliko wote, kwani wawili kati yao walikuwa ni miongoni mwa walimu wakuu wa shule na mtu wa tatu alikuwa ni mwalimu katika mji mkuu (wa nchi yetu) na mtu wa nne alikuwa mwandishi wa habari na mtu wa tano sikufahamu cheo chake, bali nilifahamu tu kuwa yeye ni mmoja wa jamaa za Waziri wa Elimu katika zama hizo.

Safari yetu haikuwa ya moja kwa moja, tulishuka Athens ambao ni mji mkuu wa nchi ya Ugiriki mahali ambapo tulimaliza siku tatu na kutoka hapo tulikwenda Aman mji mkuu wa Jordan, na tulikaa hapo siku nne, na baada ya hapo tulifika Saudia, ambapo tulishiriki mkutanoni na tukafanya ibada za Hijja na Umra.

Hisia zangu zilikuwa hazielezeki wakati nilipokuwa naingia katika nyumba tukufu ya Mwenyezi Mungu kwa mara

11

ya kwanza na moyo wangu ulikuwa kama unataka kuzivunja mbavu ambazo zinauzunguka kutokana na kudunda kwa nguvu hali ya kuwa unataka kutoka ili wenyewe uione nyumba hii kongwe ambayo umekuwa ukiiota kwa muda mrefu, machozi yalinitiririka mpaka nikadhania hayatakatika na nilijiona kama kuwa Malaika wananibeba juu ya Mahujaji wote ili nifikie kwenye paa la Kaaba tukufu na ninaitikia wito wa Mwenyezi Mungu nikiwa huko "LABBAIKALLAHUMMA LABBAIK" ewe Mwenyezi Mungu huyu mja wako amekuja kwako.

Nilibaini hali ya kuwa nasikia Tal-biyah za Mahujaji ya kuwa watu hawa wamemaliza umri wao hali ya kuwa wakijiandaa na wakifanya matayarisho na kukusanya mali ili waje hapa, ama mimi kuja kwangu kulikuwa ni kwa ghafla bila ya maandalizi yatokanayo nami, na ninakumbuka kwannba mzazi wamgu alipoiona tiketi ya ndege na akayakinisha kuwa nitasafiri kwenda Hijja alilia hali ya kuwa ananibusu na kuniaga huku anasema:

"Hongera ewe mwanangu kwa hakika Mwenyezi Mungu ametaka uhiji kabla yangu nawe ukiwa katika umri huu basi wewe ni mtoto wa Sayyid Ahmad Tijani, niombee kwa Mwenyezi Mungu katika nyumba yake anikubalie toba yangu na aniruzuku kuhiji nyumba yake tukufu".

Kwa ajili hiyo nilidhania kwamba Mwenyezi Mungu ndiye aliye niita na akaniweka katika himaya yake na akanifikisha mahali hapo ambapo watu wanakufa bila kupafikia hali ya kuwa ni  wenye simanzi na masikitiko, basi inanistahikia mno mimi kufanya Talbiya, na nilikuwa nikitufu mno na kusali sana na kufanya Saayi (Baina ya Safa na Marwa).

Hata maji ya zamzam nikiyanywa kwa wingi, na kupanda katika mlima mahala ambapo watu hushindana kufika kwenye pango la Hira na juu ya mlima Nnur, nami hakuna aliyenishinda isipokuwa kijana mmoja wa Kisudani. Hivyo basi

12

nilikuwa wa pili katika wawili (Thaniya th-nain) na  niligaagaa ndani yake kama kwamba ninagaagaa ndani ya mapaja ya  Mtume mtukufu (S.A.W.) na ninaivuta pumzi  zake, Aah…. kumbukumbu zilizoje ambazo zimeacha ndani ya nafsi yangu athari   kubwa ambayo kamwe haitafutika!!

Majaaliwa mengine ya Mwenyezi Mungu, yalimfanya kila anionaye miongoni mwa wajumbe anipende na kutaka anuani yangu ili kuwasiliana, na kwa hakika wenzangu ambao walinidharau tulipokutana nao kwa mara ya kwanza tukiandaa safari katika mji mkuu wa Tunis walinipenda na nilihisi hivyo na nikavumilia kutokana na kujua kwangu toka mwanzo kwamba watu wa kaskazini (ya nchi yetu) wanawadharau watu wa kusini na wanawazingatia kuwa hawajaendelea, lakini ghafla mtazamo wao ulibadilika wakati wa safari na mkutanoni na katika Hijja, na nilizing'arisha nyuso zao kwa mambo niliyokuwa nimeyahifadhi miongoni mwa Qasida na Mashairi na zawadi nilizopata katika mashindano ambayo yalifanyika katika mnasaba na nilirejea nchini kwangu nikiwa na zaidi ya anuani ishirini za marafiki wa mataifa rnbali mbali.

Tulikaa Saudia kwa muda wa siku ishirini na tano na tulikuwa tukikutana na wanachuoni na kuwasikiliza katika mihadhara yao, na kwa hakika niliathirika kwa baadhi ya itikadi za Kiwahabi ambazo nilizipenda na nikatamani Waislamu wawe katika itikadi hizo, kwa wakati huo nilidhani kuwa Mwenyezi Mungu amewachagua kutoka miongoni mwa waja wake kwa ajili ya kulinda nyumba yake tukufu, hivyo basi wao ni watakatifu na wanajua kuliko kiumbe mwengine wa Mwenyezi Mungu duniani, na Mwenyezi Mungu amewatajirisha kwa (kuwapa) petroli ili waweze kuwahudumia mahujaji ambao ni wageni wa Mwenyezi Mungu napia kulinda usalama wao.

Na wakati wa kurudi nchini kwangu kutoka Hijja nilikuwa nimevaa vazi la Kisaudia, na nilisitukizwa na mapokezi

13

aliyokuwa ameyaandaa mzazi wangu, kwani kulikuwa na watu wengi waliokusanyika kituoni wakiongozwa na Sheikh wa Tarika ya Aisawiyah na Sheikh wa Tarika ya Tijaniyah na Sheikh wa Tarika ya Qadiriyah wakiwa na ngoma na dufu.

Walinizungusha katika mitaa ya mji wakifanya Tahlil na Takbira na kila tukipita kwenye msikiti baadhi ya wakati walinisimamisha kwenye kizingiti chake na watu wakiwa pembeni yangu wakishindana kutaka kunibusu na hasa wazee wenye umri mkubwa walikuwa wakinibusu hali ya kuwa wanalia kwa shauku ya kutaka kuiona nyumba ya Mwenyezi Mungu na kusimama kwenye kaburi la mjumbe wake nao walikuwa hawajazoea kumuona Haji mwenye umri kama wangu kama ambavyojambo hili walikuwa hawajaliona katika Qafsah kabla yangu.

Niliishi maisha ya furaha katika wakati wote huo na nyumbani kwetu walikuja watu wakubwa mashuhuri wa mjini kunisalimia na kunipongeza na wakiniombea na mara nyingi walikuwa wakinitaka niwasomee fatiha na dua mbele ya mzazi wangu, basi wakati mwingine nilikuwa naona haya na nikijipa moyo mara nyingine naye mama yangu kila mara alikuwa akiingia baada ya waliokuja kuniona wanapotoka ili awashe ubani na kunifanyia kago ili kunikinga kutokana na shari za mahasidi na kuniepusha na vitimbi vya mashetani.

Baba yangu alifanya karamu kwa muda wa siku tatu mfululizo kwa ajili ya wana Tarika wa Tijaniyah, kila siku akichinja Kondoo na watu walikuwa wakiniuliza kila mambo makubwa na madogo na majibu yangu yote, aghlabu yalikuwa yakishikamana na kuwapenda na kuwasifu Wasaudia na kazi wanayoisimamia katika kueneza Uislam na kutetea Waislamu.

Wakazi wa mjini wakanipa jina la "Haji" basi ikawa litajwapo jina hili haliendi kwingine isipokuwa kwangu, na baada

14

ya hapo nikawa maarufu mno hasa hasa ndani ya makundi ya watu wa dini kama vile "Jaftiaatu Ikh-wanil-Musli-mina".

Nilikuwa nikizunguka katika Misikiti na kuwakataza watu kubusu makaburi na kujipangusia kwenye mbao, na nikijaribu juhudi zangu zote kuwakinaisha kwamba kufanya hivyo ni kumshirikisha Mwenyezi Mungu, na utendaji wangu wa kazi ulizidi kupanuka, kwani nilikuwa nikitoa mafunzo ya kidini ndani ya Misikiti siku ya ljumaa kabla ya khutba ya Imam na nikihama kutoka Msikiti wa Abu Yaaqub kwenda Msikiti Mkuu, kwani sala ya ljumaa katika Misikiti hiyo husaliwa kwa nyakati tofauti wakati ambapo ya kwanza husaliwa wakati wa adhuhuri, ya pili husaliwa wakati wa Alasiri.

Na ni mara nyingi wengi wa watu waliokuwa wakihudhuria masomo hayo niliyokuwa nikiyatoa siku ya Jumapili ni wanafunzi wa shule ya Sekondari ambayo nilikuwa nikisomesha somo la Teknolojia na ufundi, na walikuwa wakishangazwa na jambo hili na wakizidi kunipenda na kuniheshimu kwani nilikuwa nawapa wakati mwingi kuwaondolea ndani ya fikra zao utando (wa fikra mbaya) / zilizogandamizwa na baadhi ya waalimu wa falsafa za kikafiri na wasioamini Mungu na Wakomunisti na wengine wengi zaidi ya hao.

Hivyo basi walikuwa wakingojea kwa shauku wakati wa mafunzo hayo ya kidini, na miongoni mwao wakija nyumbani, na nilinunua vitabu vya dini na nikavisoma kwa bidii ili niwe katika kiwango cha kuweza kujibu maswali mbali mbali.

Katika mwaka huo niliohiji vile vile nilikamilisha nusu ya dini yangu, kwani mama yangu (Mwenyezi Mungu amrehemu) alipendekeza aniozeshe kabla ya kufa kwake, naye ndiye aliyewalea watoto wote wa mumewe na akahudhuria harusi zao basi shauku yake ilikuwa anataka kuniona nimeoa, na Mwenyezi Mungu alimkubalia kile alichokitamania nami

15

nilitii amriyake kwa kumuoa msichana mmoja ambaye nilikuwa sijamuona hapo kabla, na mama yangu alihudhuria kuzaliwa kwa mwanangu wa kiume wa kwanza na wa pili, na alifariki hali ya kuwa ameniridhia kama ambavyo baba (Mwenyezi Mungu amrehemu) alikuwa amemtangulia mama kabla ya miaka miwili na alihiji nyumba tukufu ya Mwenyezi Mungu na akatubia toba ya kweli kabla ya kufariki kwake miaka miwili.

Katika kipindi ambacho Waislamu na Waarabu walikuwa wakinyanyasika kutokana na kushindwa katika vita vyao dhidi ya Israel, Mapinduzi ya Libya yalifaulu na akatuchomozea yule kijana ambaye ndiye Kiongozi wa Mapinduzi hali ya kuwa akizungumza kwa niaba ya Waislamu, na akisalisha watu Msikitini na kutoa mwito kuikomboa Quds, kwa hakika alinivutia kama ambavyo aliwavutia vijana wengi Waislamu katika nchi za Kiarabu na Kiislamu na alitulazimisha kupenda kuangalia (uwezekano) wa kuandaa safari ya mafunzo kwenda Libya, na tulikusanya watu arobaini" miongoni mwa watu wasomi na tulifanya ziyara ya nchi ndugu mwanzoni kabisa mwa mapinduzi,

Tulirejea toka huko hali ya kuwa ni wenye kufurahishwa na mambo tuliyoyaona tukitazamia mustaqbali ambao tulitarajia kuwa utakuwa ndiyo suluhisho Ia Umma wa Kiarabu na Kiislam ulimwenguni kote.

Muda wote huu uliopita mawasiliano ya barua na baadhi ya marafiki yalikuwa yakiendelea na mapenzi pia yakizidi, na mahusiano yangu na baadhi yao yaliimarika na walisisitiza niwatembelee, basi nilijiandaa na nikayapanga mambo kwa ajili ya safari ndefu itakayomaliza likizo ya kiangazi ambayo hudumu miezi mitatu, na njia ilikuwa inapitia   libya kwa barabara kisha Misri na kutoka hapo hadi Lebanon kupitia Baharini hadi Syria na Jordan na hatimaye Saudia, napo ndipo penye makusudio ya kufanya umra na kuimarisha mafungamano na Mawahabi

16

ambao nimewatangaza mno miongoni mwa vijana wasomi na ndani ya Misikiti ambayo ndani yake Ikhwanul-Muslimina ni wengi.

Umaarufu wangu ulivuka mipaka ya mji wangu ukafika mpaka kwenye miji mingine ya jirani, basi huenda akapita msafiri akasali sala ya ljumaa na kuhudhuria darasa zile na kwenda kulizungumzia katika jamii yake, na habari zikamfikia Sheikh Ismail Al-Hadifi, kiongozi wa Tarika mashuhuri ya kisufi katika mji wa Tuzer ambao ni mji mkuu wa Al-Jarid.

Na Sheikh huyu ana wafuasi na Murid, katika Jamhuri nzima ya Tunisia na nje ya nchi yake miongoni mwa watu wafanyao kazi Ufaransa na Ujerumani.

Wito wa kumzuru Sheikh huyo ulinifikia kupitia kwa watumishi wake walioko Qafsah, ambao waliniandikia barua ndefu wakinishukuru katika barua hiyo kutokana na kuhudumia kwangu Uislamu na Waislamu na wakidai kwamba jambo hilo haliwezi kunikurubisha kwa Mwenyezi Mungu japokuwa kidogo maadamu siko katika Tarika ya Sheikh mtambuzi na kwa mujibu wa hadithi ambayo ni mashuhuri kwao (isemayo):

''"Asiyekuwa na Sheikh basi Sheikh wake ni shetani" vile vile wanasema kwamba "Ni lazima uwe na Sheikh atakayekuonyesha njia vinginevyo elimu yako uliyonayo ina upungufu"

Walinibashiria kwamba (Sahibuz Zaman) wakimlenga Sheikh Ismail ameniteua kutoka miongoni mwa watu ili niwe msiri wake.

Nilifurahi sana kutokana na khabari hizi na nililia kwa kuathirika na majaaliwa haya ya Mola ambayo yanaendelea kuninyanyua kutoka daraja ya juu hadi ya juu zaidi, na kutoka (mahali) pazuri hadi pazuri zaidi, kwani mimi hapo zamani maishani mwangu nilikuwa nikimfuata Sayyid yangu Al-Hadi

17

Al-Haf-Yan ambaye ni Sheikh wa Tasawufu na husimuliwa kuwa na karama na mambo yasiyo ya kawaida na nilikuwa katika vipenzi wake wakubwa, kama ambavyo nilifuatana na Sayyid yangu Saleh Bas-saih, na Sayyid yangu Jailani na wengineo miongoni mwa watu wa Tariqa wa miaka ya hivi karibuni, basi nilingojea mkutano huo (na Sheikh Ismail) kwa shauku.

Nilipoingia nyumbani kwa Sheikh nilikuwa nikiziangalia nyuso za watu kwa hamu kubwa, na ukumbi ulikuwa umejaa wanamuridi na miongoni mwao wamo Masheikh waliovaa mavazi meupe sana, na baada ya kusalimiana Sheikh Ismail alitutokea na wote wakasimama wakambusu mkono wake kwa heshima kubwa na yule wakili akanikonyeza kunijulisha kuwa huyu ndiye Sheikh mwenyewe basi sikuonyesha hamasa yoyote kwani mimi nilikuwa nikimsubiri asiyekuwa huyu niliyemuona kwa kuwa nilikuwa nimeunda picha ya kimawazo kufuata karama na miujiza ambayo wakili wa Sheikh na wafuasi wake waliingiza katika akili yangu, na nilimuona ni Sheikh wa kawaida tu hana haiba wala utukufu na katikati ya kikao yule wakili alinitambulisha kwake naye akanikaribisha na kunikalisha kuliani kwake na nikapewa chakula.

Baada ya kula na kunywa hadhara ile ilianza na akanitambulisha upya yule wakili ili nichukue ahadi na nyiradi kutoka kwa Sheikh.

Na baada ya hapo wote walinipongeza, kunikumbatia na kuniombea baraka, na nilitambua kutokana na mazungumzo yao kwamba wao wanasikia mambo mengi juu yangu, na huu upendo wao kwangu ulinifanya nijione na kunisukuma nipinge baadhi ya majibu ya Sheikh aliyokuwa akiyatoa kwa waulizaji na nikitetea maoni yangu kwa kutumia Qur'an na Sunna.

Baadhi ya waliohudhuria hapo walichukizwa na huu uingiliaji kati na wakauzingatia kuwa ni utovu wa adabu mbele

18

ya Sheikh na wao wamezoea kutozungumza mbele yake isipokuwa kwa idhini yake.

Sheikh aligundua chuki ya watu waliokuwepo hapo basi akaondosha kwa uerevu hali ya kuwa akisema: "Yeyote ambaye mwanzo wake ulikuwa wenye kuungua basi mwisho wake ni wenye kung'ara". Na wote waliohudhuria hapo walielewa kuwa ni dalili kutoka kwa Sheikh yakuthibitisha ufanisi wa mustakbal wangu.

Lakini Sheikh yule wa Tarika alikuwa mwerevu na mzoefu, hivyo hakunipa nafasi ya kuendeleza ufidhuli unaokera, na alitusimulia kisa cha mtu mmoja mcha Mungu ambaye walikaa katika darasa lake baadhi ya watu wenye Elimu, basi alimwambia mmoja wao kuwa "Simama uende ukaoge" yule mtu mwenye Elimu alikwenda akaoga na akaja kukaa kwenye darasa, yule mchamungu akamwambia tena mara ya pili "Simama ukaoge" yule mwenye Elimu alisimama akarudia kuoga vizuri kwa kadri inavyowezekana akidhania kuwa kuoga alikooga mara ya kwanza kulikuwa siyo sahihi na akaja ili akae basi yule Sheikh mchamungu akamkemea na akamwamuru akaoge upya, yule mwenye Elimu akapiga kelele akasema, "Ewe bwana wangu hakika nimeoga kwa mujibu wa Elimu yangu na juhudi yangu, na hapa kilichobakia ni vile atavyonijaalia Mwenyezi Mungu kupitia mikononi mwako!

Basi hapo yule Sheikh mchamungu akamwambia "Sasa kaa"

Basi mimi nilitambua kuwa anayekusudiwa katika kisa hicho ni mimi kama ambavyo walifahamu hivyo waliokuwepo hapo walinilaumu baada ya Sheikh Ismail kutoka kwa ajili ya mapumziko na wakanitaka ninyamaze na niwe na heshima mbele ya Sheikh ambaye ndiye "Sahibu Zaman" ili matendo yangu mema yasije yakaharibika, na walitoa ushahidi wa aya tukufu ya Qur'an isemayo"-

19

"Enyi mlioamini musipaze sauti zenu kuliko sauti ya Mtume wala musiseme naye kwa sauti ya nguvu kama munavyosemezana ninyi kwa ninyi ili vitendo vyenu visije kukosa thawabu na hali ya kuwa hamtambui." (Qur'an, 49:2)

Basi nilitambua heshima yangu na nikafuata maelekezo na nasaha (nilizopewa) na Sheikh alinikumbusha zaidi na nilikaa kwake siku tatu na muda wote huo nilikuwa nikimuuliza maswali mengi, baadhi ya maswali hayo nilimuuliza kumjaribu na Sheikh huyo alikuwa akilitambua hilo, basi hunijibu kwa kusema: Bila shaka Qur'an ina maana za dhahiri na zingine za ndani zaidi hadi daraja saba" pia alinifungulia kabati lake ambalo alinionyesha daftari  lake maalum ambalo ndani yake umo mfululizo wa majina ya watu wema na wachamungu (mfululizo ambao) unafikia kwa Abul-Hasan As-Shadhiliy unaopitia kwa mawalii wengi waliotajwa hadi kufikia kwenye sanad ya Imam Ali Ibn Abi twalib Mwenyezi Mungu ametukuza uso wake na amemuwii) radhi.

  Yaliyomo endelea