rudi nyuma Yaliyomo endelea

13. SABABU ZILIZOTOLEWA KWA KUHARAMISHA UANDISHI WA HADITH ZA MTUME S.A.W.W.

1. Sababu ya kwanza iliyotolewa ni khofu ya watu kushindwa kutofautisha baina ya Quran na Hadith za Mtume s.a.w.w. ambazo zingalisababisha uharibifu (tahrif) wa maandiko ya Quran, madhambi yasiyo samehewa.

Mazungumzo haya, ambayo hayawezi kukubalika, yamekanushwa na Ustadh Abu Riyyah katika maneno yafuatayo:

"Mtu kama huyo anaweza kuwashawishi watu wa kawaida, lakini haiwezi kukubalika kiutafiti. Kwa sababu itakuwa ikimaanisha kuwa ufasaha wa Quran unasimama sawasawa na ufasaha wa Hadith za Mtume s.a.w.w.

Kile anachokimaanisha hapa ni muujiza wa ufasaha wa Quran unavyo tambulikana miongoni mwa watu, hatuwezi kudai kuwa wao wangalikuwa chini ya upotofu kwa kuzichanganya aya za Quran kwa Hadith za Mtume s.a.w.w., ambazo zipo chini kwa kulinganishwa na ufasaha wa Quran. Msimamo kama huu, kwa hakika unamfanya mtu akipingana na muujiza wa Quran.

Zaidi ya hayo, kuamini katika uwezekano wa kuchanganyika kwa Aya za Quran na Hadith ni sawa na kuamini katika uwezekano wa kuja kupotea kwa maandiko ya Quran. Imani kama hiyo inakanushwa kwa sababu uhalisi wa Quran upo unathibitishwa na Allah swt katika Quran: Sura Hijr, 15:9.

Tunaweza kusema zaidi ya hayo kuwa kikundi cha Sahaba walikuwa wamehifadhi moyoni mwao Quran nzima, na kwa uangalifu mkubwa na upendo wao mkubwa juu ya Quran. Hatuwezi kamwe kuwafikiria kuwa wao walikuwa na hatari ya kuchanganyikiwa baina ya Quran na Hadith. Sisi twaweza kusema kuwa labda kulikuwapo na hatari ya uwezekano tu, na uwezekano huo hauwezi kupewa uzito sawa na madhara na hatari za kutoziandika Hadith. Madhara yaliyokuwa yameshajulikana kuanzia awali kabisa Shabaha hawakukubaliana miongoni mwao katika siku za awali kuhusu baadhi ya Shariah za Kiislamu na ilikuwa ni dhahiri kuwa athari za ufarakano huo ungelikuwa na hatari kubwa iwapo Hadith za Mtume s.a.w.w. zingalikuwa hazikuandikwa. Lakini hatari hiyo ilitokea tu. Baina ya tishio la zamani na hatari fulani, iliwabidi wao walitilie mkazo swala la uandishi wa Hadith, ingawaje, kimsingi swala la kutoruhusu uandishi wa Hadith halikuwa na uzito wowote.

2. Maelezo ya pili yatolewayo na Abu Riyyah yanasema baada ya kukubalia uharamisho wa kuandika Hadith ulitokana na Mtume s.a.w.w. kwamba Mtume s.a.w.w. alitaka maamrisho ya Shariah yawe katika mipaka iliyodhibitiwa na alipinga kueneza zaidi kwa maamrisho ya Shariah (adillah). Haya, kwa mujibu wake, ni sababu ambayo pia inatokana na nyakati zinginezo ambapo Mtume s.a.w.w. alichukia kuulizwa maswali. Sababu hiyo hiyo ipo inatumika katika hali ambapo Hadith ambazo zilikuwa sahihi katika kipindi fulani na ambapo haikuruhusiwa kufuata hapo baadaye.

Sisi tunachukulia maelezo hayo kuwa ni dhaifu mno, kwani haiwezekani kamwe kudai kuwa Mtume s.a.w.w. alipinga kwa kuenea Hadith halali kisheria zikitumika kama misingi ya kanuni halali za shariah. Je, itawezekanaje kwetu sisi kukubaliana nayo wakati Quran na Hadith kwa pamoja zinawajibika kujibu mahitaji katika sura mbalimbali ya Shariah kwa ajili ya siku ya Kiyama na siku zote kutoa maongozi kwa mwanadamu? Pamoja na hayo, sisi tutaelezea tena kwa mara ya pili kuwa sisi hatuamini ya kwamba Mtume s.a.w.w. alitoa amri ya kuharamisha uandishi wa Hadith.

3. Al-Awzai anatoa maelezo mengineyo, anaandika: "Sayansi ya Hadith ni tukufu pale inapoenezwa kwa mdomo tu, inawafanya watu wakumbushana daima Hadith. Lakini, pale inapoandikwa, nuru yake inafifia na pia huweza kufikia mikono ya watu wasiostahili kupatiwa."

Sisi tunaweza kuonyesha kuwa ingawaje kuenezwa kwa Hadith kwa mdomo kuna faida ya kukumbusha watu yaliyomo ndani mwa Hadith, utumiaji wake kama halisi, na pekee, njia za kuzirekodi hizo zipo mashakani. Kwa hakika, faida kama hizo ziliambatana na madhara makubwa mno. Hata hivyo, hii ndiyo sababu mojawapo ambayo al-Awzai ameibuni, na ipo inashukiwa iwapo ikizingatiwa na wale waliokuwa wameharamisha uandishi wa Hadith.

  1. Ibn Abd al-Birr, anaandika wakati wa kutoa maelezo kama hayo:

Uandishi wa Hadith uliharamishwa ili watu wasitegemee mno yale yaliyoandikwa na wao, wakiepukana na huzihifadhi. Katika hali kama hiyo, desturi ya kuhifadhi moyoni Hadith ingalikuwa imepotea.

Wazo kama hilo pia haliwezi kukubalika, kwa sababu madhara yaliyotokana na kushindwa kuziandika Hadith yalikuwa ni makubwa mno kwa kulinganishwa na faida iliyotokana na kupigwa marufuku kwa uandishi wa Hadith. Ustaarabu na utamaduni wa mwanadamu umekuwa ukilindwa kwa kupitia maandishi na wala si kwa kusema tu, ingawaje kuhifadhi Hadith kwenyewe ni tabia nzuri na yenye maana.

5. Sababu nyingine imetolewa pamoja na haya ni kwamba iwapo Hadith zingalikuwa zimeandikwa basi watu wangalikuwa wameiacha Quran huku wakizipatia Hadith umuhimu wote.

Mazungumzo hayo pia hayawezi kuchukuliwa kuwa ni kinga, kwani jambo kama hilo linaweza kusemwa iwapo Hadith itakayomaanishwa itakuwa ni zile zisemwazo kwa mdomo tu, na Quran kwa upande wa pili. Ni kweli kabisa kuwa kupitia umuhimu wote Hadith ni upotofu ambao wale wafanyao hivyo waonywe na wachukue umuhimu kama huo katika Quran. Lakini uharamisho wa uandishi wa Hadith, umeleta uharibifu usioweza kutegemewa katika utamaduni wa Islam, kwa njia hiyo si ya kupatikana kwa matokeo sahihi.

6. Abjad al-'ulum anaandika:

"Sahaba na Tabi'un, kwa sababu ya uhalisi wa imani yao na kuwapo kwao karibu na kipindi cha Mtume s.a.w.w., na kutokuwapo kwa mabishano na uwezekano wa kuwaelekea watu waliotegemewa, hawakuwa na hitajio la kuziandika Hadith na shariah.Lakini vile Islam ilipoanza kuenea penginepo, wao walianza kuzikusanya na kuziandika Hadith, Fiqh na tafsiri ya Quran.'

Kile anachokitaka kukisema huyu mwandishi siyo sababu ya kupinga kwa baadhi ya Sahaba kwa ajili ya uandishi wa Hadith, bali ni maelezo tu- nayo pia siyo sahihi- ni kwa nini Hadith hazikuandikwa; sababu yake halisi ilikuwa ni kupingwa kwa uandishi wa Hadith, na wala si kutohitajika kama vile anavyodai mwandishi huyo. Zaidi ya hayo, ueneaji wa Islam ulitokea katika miaka ya ishirini au zaidi ya miaka hamsini baada ya kifo cha Mtume s.a.w.w. Uandishi na ukusanyaji wa Hadith ulicheleweshwa hadi kufikia nusu ya karne ya 2 A.H./8 A.D. mbali na nukta hizo mbili inaeleweka kuwa sifa hii ya kumzulia Mtume s.a.w.w. ilianza katika maisha yake, na hatimaye iliweza kuongezeka kwa sababu ya kutokuwepo kwa Hadith zilizoandikwa. Pia ilikuwa ni wajibu wa Sahaba, ambao walitofautiana miongoni mwao katika mambo ya Shariah, kuzuia kukua kwa upotoshi na tofauti kwa kuanza kuziandika Hadith.

  1. Sababu hasa ambayo ipo nyuma ya kuharamishwa kwa uandishi wa Hadith, ambayo mimi ninaamini, imeelezwa na mwanachuo mashuhuri aitwaye Sayyid Jaafar Murtadha na imethibitishwa kwa ushahidi uliopo:-

Kulikuwapo na madhehebu mawili miongoni mwa Mayahudi. Dhehebu moja waliamini katika uandishi wa Hadith, ambapo dhehebu la pili halikuafiki hivyo, waliamini katika kutoandika chochote kile isipokuwa Taurati peke yake. Kundi hili la pili liliitwa Qurra (wasomaji). Haya yapo yamedokezwa na Dhadha katika kitabu chake cha fikara za Dini ya Kiyahudi. Ka'aba al-Ahbar Myahudi aliyesilimu (katika zama za Umar) alitokana na kundi hilo la pili. Mara moja Umar alimwuliza swali kuhusu mashairi ya vitu avisemavyo kuhusu Waarabu, kuwa kikundi cha kizazi cha Ismail, walikuwa wamehimili Biblia katika nyoyo zao na walizungumza kwa busara.....Labda inawezekana kuwa Khalifa alilichukua wazo hilo (la kutoandika chochote kile isipokuwa Quran tu) kutoka kwa Ka'b al-Khalifa na vile vile alikuwa akiheshimiwa kwa ushauri wake.

Zaidi ya hayo, uharamisho juu ya uandishi wa Hadith ulikuwa ukienda vyema pamoja na Siasa za tawala, kwani waliweza kuyazima malalamiko dhidi yao na kuendelea kuimarisha utawala wao. Kwa hakika hatua kama hiyo inawezekana kuwa na matokeo ya upotezi wa sehemu ya Hadith izungumziayo juu ya haki za wapinzani na ustahiki na ambayo ilifaa kuletea nguvu sehemu walizokuwa wamezidhibiti.

Mtunzi huyo, kama vile taarifa yake ionyeshavyo, anadhani zipo sababu mbalimbali zilizosababisha kuharamishwa kwa Hadith, moja na muhimu kabisa ni kushawishiwa kwa mawazo ya Ahl al-Kitab juu ya Khalifa wa pili, ambaye, inavyoonekana, alipenda kusoma vitabu vyao kuanzia wakati aliposilimu.

Uthibisho unaothibitisha ushawishi huu ni riwaya ya Urwah ibn al-Zubayr, isemayo kuwa Khalifa alikuwa amenuia kukusanya 'sunan' na hata pia aliwasiliana na Sahaba wengineo juu ya mpango wake huo. Wao walikubaliana nalo, lakini alibadilisha mpango wake huo kwa kusema kuwa watu wa Ahl al- Kitaab waliviacha vitabu vitukufu na kuanza kuvifuata vile walivyokuwa wameviandika na hivyo yeye hakutaka kufuata kitakachotokea juu ya Quran kama hivyo ilivyokuwa imetokea.

Ni jambo la kuweza kutokea kuwa maelezo hayo ya Khalifa yaliletwa na Ka'b al-ahbar, aliyetokana na kikundi cha Qurra, ambaye alijiepusha na kuandika chochote kile mbali na Tawrati. Ka'b alikuwa na njama mbaya dhidi ya Islam; ingawaje Khalifa alikuwa hana nia kama hizo, naye, kwa bahati mbaya, alishindwa kuona kwa kupitia ulaghai wa Ka'b.

Mabishano ya Umar dhidi ya uandishi wa Hadith yalirudiwa na wengineo. Abu Burdah anaripoti kutokea baba yake aliyesema: "Banu Israil waliandika vitabu na kukiacha Kitabu cha Allah." Hakam ibn Atiyyah anaripoti kutokea Muhammad (bila shaka, Muhammad ibn Sirin) kuwa alizoea kusema: "Imenukuliwa kuwa Banu Israil walipotoshwa kwa sababu ya vitabu walivyovirithi kutokea mababu zao."

Mwanachuoni mwingine anaandika:

"Moja ya ushawishi mkubwa wa Mayahudi juu ya Waislamu ulikuwa ni kuepukana na desturi ya kuandika Hadith.

Imeandikwa katika Talmud, "Nyinyi hamna haki ya kuandika mambo ambayo munayazungumzia tu. "Huwezi kupinga kuwa Waislamu hawaku shawishiwa na Ka'b al-ahbar katika swala hili, ingawaje wao waliileta mbele katika sura ya Hadith ya Mtume s.a.w.w. Ushahid wake ni amri iliyotolewa na Khalifa baada ya kuzichoma Hadith alizokuwa amezikusanya:

"Mathnat (au Mishnah) kama Mathnat ya Ahl al-Kitab." Maneno haya pia yanatuonyesha vile alivyokuwa ameshikamana pamoja na desturi za Mayahudi.

Abu Ubayd katika Gharib al-Hadith, anaandika:

"Mimi nilimwuliza mwanachuo wa Taurati na Injili kuhusu neno 'Mathnat.' Yeye alinijibu: "Mapadre wa Kiyahudi na waalimu wa Kiyahudi waliviandika baadhi ya vitabu baada ya Musa, mbali na vitabu vitukufu, na ambavyo wao waliviita kwa jina la 'Mathnat.'

Ni dhahiri kuwa Khalifa alikuwa akiufuata mfano wa Mayahudi ambao wao walikuwa katika kambi mbali na iliyoelezwa hapa. Abu Ubayd anaendelea kusema:

Baada ya kupata maelezo hayo, mimi nimeelewa maana ya riwaya hii. Na hii ndiyo iliyokuwa sababu Abd Allah ibn Amr ibn al-As alikuwa akichukia kukichukua chochote kile kutokea kwa Ahl al-Kitaab, ingawaje yeye alikuwa na baadhi ya vitabu alivyovipata wakati wa kampeni ya Yarmuk (kutokea Makanisa ya Kiyahudi).

Abu 'Ubayd anaongezea:

"Ni lazima, uharamisho (wa uandishi na usambazaji) haukuhusiana na Hadith na Sunnah za Mtume s.a.w.w., kwa sababu itawezekanaje kuharamisha uandishi wa Hadith wakati ambapo wengi wa Sahaba wenyewe walikuwa wakinakili Ahadith.

Hii inatuonyesha waziwazi kuwa Umar aliharamisha uandishi wa Hadith za Mtume s.a.w.w. na Sunnah zake kwa sababu yeye alichukulia msimamo kama ule wa maandishi yaliyokuwa yametolewa na waalimu wa Kiyahudi. Kwa hivyo, badala ya kuangalia na kuchunga kuenea kwa imani za Isra'iliyyat, yeye alikuwa ameshawishiwa nayo, ushawishi ambao ulisababisha katika kuangamizwa kwa Sunnah za Mtume s.a.w.w. Vile vile ni lazima iongezwe kuwa Abd Allah ibn Amr mwenyewe alikuwa mmoja wa waenezaji wa 'Isra'iliyyatambaye kamwe alikuwa si mtu aliyechukiwa mbele yao. Ilikuwa ni kwa sababu ya elimu yake ya Tawrati kwamba watu walimwambia awaeleze tabia ya Mtume mmoja.

Kile kilichotokea, katika mtizamo wetu, ni hivi: "Hadith za Mtume s.a.w.w. kwa ujumla hazikuandikwa hadi kufikia mwishoni mwa karne ya 1 A.H./7 A.D., ingawaje baadhi ya Sahaba walipendelea uandikaji wake na vile vile wengineo walikuwa na vibao vilivyokuwa vimeandikwa Hadith. Uandikaji wa hapa na pale ulianza kutokea katika karne ya 2 A.H. /8. A.D. , lakini ukusanyaji na uandikaji wa Hadith ulianza kwa nguvu mwishoni mwa karne ya 2 A.H./8 A.D., na hasa katika karne ya 3A.H./8 9 A.D. Ingawaje inawezekana kuwa wakusanyaji walikuwa na mkusanyiko usio na utaratibu (kwani walikuwa wakikusanya chochote kile walichokipata bila ya kufanyia utafiti juu ya usahihi wake au ni nani aliyeileza), ni dhahiri kuwa wingi wa Hadith walizozikusanya zilikuwa zimetokana na kutamkwa tu.

Ushahidi uliopo ni kwamba uandishi mdogo kabisa-ambao hauwezi kulinganishwa na kazi kubwa ya ukusanyaji wa Hadith-zipo dalili kidogo kabisa zenye kuonyesha kuwa kulikuwepo na uandishi wa Hadith katika karne ya 2 A.H./88 A.D. Hivyo inaweza kusemwa kuwa Hadith hazikuwa zikiandikwa kwa kipindi kirefu na zilikuwa zikisemwa kwa midomo tu bila ya kuandikwa katika kipindi hicho.

14. MATOKEO YA KUTOZIANDIKA HADITH:

Kulitokea matokeo mabaya kwa sababu ya kutokuwa na Hadith zilizoandikwa wakati wa kuzieneza. Hapa sisi tutajaribu kuzizungumzia baadhi yao.

1. Upoteaji mkubwa mno wa Hadith:

Haya yalikuwa ni matokeo ya kutoandikwa kwa Hadith. Kwa Sahaba, uhifadhi moyoni ulileta matokeo ya kuhifadhika kwa idadi kubwa ya Hadith, na pia tukubali kuwa kulisababisha katika kupotea Hadith chungu nzima kwani kuhifadhi moyoni ni njia isiyoaminika katika kuhifadhi. Kukiri na kukubali kwa Muhaddithun (waliohadithia) katika jambo hili ni ushahidi ulio bora kabisa kwa ajili ya hayo.

Ibn Qulabah anasema, "vitabu na maandiko ni bora kabisa kuliko kupotea kwa fahamu na hatimaye kusahau." Yahya ibn Sa'id anaandika, "mimi niliwaona Wanazuoni katika hali ya kuchukia uandishi wa Hadith. Laiti tungalikuwa tukiziandika, basi sisi tungalikuwa tunayo elimu kubwa mno ya Sa'id ibn Musayyab na vile vile mashauri yake." Yahya hapa anasikitikia upoteaji wa idadi kubwa ya Hadith zilizosimuliwa na Sa'id na vile vile mashauri yake yote kwa sababu ya kutoziandika.

Urwah ibn al-Zubayr anaandika, "mimi niliandika idadi kubwa ya Hadith na hapo baadaye niliziteketeza. Sasa ninaona kuwa laiti nisingeziteketeza badala yake ningelikuwa nimetoa mali na fidia ya watoto wangu kwa kuzibakiza. Hisham bin Urwah anaelezea "Baba yangu alivichoma vitabu vyake vyote alivyokuwanavyo katika tukio la Harrah (mnamo mwaka 63 A.H./ 283 A.D. ambapo jeshi la Syria liliposhambulia mji wa Madinah na kuuteketeza mji huo); baadaye aliniambia, 'Laiti ningalikuwa nimeviweka, kwa hakika ingalikuwa bora kabisa kwangu kubakia na Hadith kuliko mali na watoto nilionao kwa hivi sasa." Pia Yahya ibn Sa'id alikuwa akisema kama hayo. Taarifa hizo zinatuonyesha vile baadhi ya watu walivyokuwa wakisikitika kwa kuteketeza vitabu vyao kutokana na sababu moja au nyingine.

Mu'ammar asema, "mimi nilimsimulia baadhi ya Hadith Yahya ibn Kathir. Yeye aliniambia kumwandikia Hadith fulani fulani. Lakini mimi nilimwambia kuwa sisi tulichukia maandishi ya Ilm. Yeye aliniambia, "Andika, kwani usipoandika, utapoteza yote."

Al-Mansurr asema, Laiti ningalikuwa nimeziandika Ahadith..........Kwani nimekwisha zisahau kwa idadi sawa na zile nizikumbukazo. Laiti ningalikuwa nimeziandika! Sasa nipo ninazikumbuka nusu tu ya Hadith ya zile nilizokuwa nimezisikia."

Ibn Rushd anaandika, "iwapo Wanzuonini wasingalikuwa wamehifadhi elimu kwa kuandika na iwapo wasingalikuwa wameweza kutofautisha katika uhalisi na uzushi, basi elimu yote ingalikuwa imeshapotea na kusingalikuwapo na mwelekeo wowote ule wa Din. Mungu awajaze jazaa iliyo bora kabisa. Mwanzo wa kuandikwa kwa Hadith, mbali na kucheleweshwa kwake, yalikuwa ni maendeleo yaliyokuwa yamekaribishwa, khususan ilifuatia baada ya kuhifadhi Hadith moyoni zikiwemo halisi na zile zilizozuliwa.

Rashid Ridha anaandika, "sisi tuna uhakika kuwa sisi tumeshasahau na kupoteza idadi kubwa ya Hadith za Mtume s.a.w.w. kwa sababu Wanazuoni hawakuziandika Hadith walizokuwa wakizisikia. Lakini kile kilichopotea hakikuhusiana na Quran wala hakikuhusiana na maswala ya dini." Baada ya kuukubali ukweli wa kupotea kwa Hadith, yeye anajaribu kutuonyesha kutokuwapo kwa umuhimu wake kwa kusema kuwa kila kilichopotea hakikuwa juu ya Quran wala hakikuhusiana na maswala ya Dini.

Mawazo kama hayo hayawezi kukubaliwa: Je, inawezekanaje kwa kitu kiwe ni Hadith ya Mtume s.a.w.w. na papo hapo kisiwe na uhusiano na maswala ya Dini? Vyovyote vile, yeye anatuthibitishia kuwa baadhi ya Madhehebu ya Kiislamu hawana mafunzo yote ya Mtume s.a.w.w. ambayo yalihifadhiwa na Ahl al-Bayt a.s. yake.

Ibn Abd al-Birr aandika, "leo hakuna yeyote achukiae kuandika Hadith. Iwapo Hadith hazitaandikwa basi idadi kubwa ya elimu itaweza kupotea bure."

Umar ibn Abd al-Aziz asema, "Wakati nilipotoka Madinah mimi ndiye niliye kuwa mwenye elimu zaidi kuliko wote, lakini kufikia Syria mimi nilikwisha sahau nilichokijua."

Yazid ibn Harun alisema, "Mimi nilihifadhi Hadith elfu sabini kutoka Yahya ibn Sa'id. Lakini nilisahau nusu ya Hadith hizo pale nilipougua ugonjwa."

Ibn Rahewayh anaandika:"Mimi nilikuwa nimehifadhi moyoni mwangu Hadith elfu sabini na niliweza kujikumbusha zaidi ya Hadith laki moja. Mimi nilikuwa sikisikii chochote kile isipokuwa nilikiweka katika hifadhi yangu moyoni. Lakini baada ya muda mimi nilisahau yote."

Al-Sha'bi anasema, "Hadi sasa mimi sijaandika hata ukurasa mmoja, na hadi leo hakuna yeyote aliyenielezea Hadith hata moja ambayo ilikuwa imeandikwa bali aliisimulia kwa mdomo tu, na wala sikupenda kusimuliwa kwa mara ya pili. Pamoja na hayo nimekuja kusahau mimi kiasi kikubwa cha elimu (ilm), kiasi kwamba iwapo mtu yeyote atakuwa na elimu hiyo basi atakuwa mwanachuo mkubwa katika zama zake." Ishaq ibn Mansur anaandika,"Mimi nilimwuliza Ahmad ibn Hanbal kuhusu wale waliochukia kuandika 'ilm. Yeye alisema kuwa baadhi walichukia na baadhi waliipendelea. Mimi nilidokeza iwapo 'ilm isingaliandikwa basi ingalipotea kabisa. Yeye alikubaliana akisema, 'iwapo kusingaliandikwa kwa 'ilm,' je tungalikuwa na nini hivi leo."

Ahmad ibn Hanbal anasema, "Baadhi walitusimulia kutoka fahamu zao na wengineo kutokea vitabuni. Hadith zilizotakana na vitabu zilithaminiwa zaidi." Ahmad mwenyewe kamwe hakusimulia Hadith ila kutokea vitabuni tu.

Ibn Salah anaandika, "Iwapo Hadith isingalikuja kuandikwa, basi 'ilm yote ingalikuja kupotea katika zama zilizoifuatia."

Taarifa hizo zinatosheleza kuelezea maelezo yetu.

2. Uenezaji wa uongo na masingizio:

Uovu mwingine wa matokeo ya kutoandika Hadith ni kukua kwa Hadith zilizozuliwa na za uongo. Haikuwezekana kudhibiti hali halisi ya Hadith na muundo wake halisi. Hapo mwanzoni, kama inavyoeleweka, watu hawakuupa umuhimu wa sanad (mfululizo wa watu waliosimulia Hadith) kwani hali ya kuaminiana ilikuwapo zamani na ilikuwa imeenea kote. Siku hizi, Wanazuoni wa Hadith, ili kukwepa kukiri kuwa kulikuwapo jambo kama hili la ukweli wa kihistoria, wanasema kuwa hapakuwapo na Hadith zozote zilizozuliwa katika zama za Sahaba. Lakini katika uchunguzi na utafiti uliofanywa siku hizi, imethibitishwa kuwa baadhi ya watu kama Abu Hurayrah, walizua Hadith nyingi mno. Ni kweli kuwa zilifanywa jitihada nyingi katika kuzitofautisha Hadith zilizo halisi na zile zilizo za uongo, lakini haya yalikuwa yametokea katika kipindi ambapo idadi kubwa ya makundi yalijitokeza katika jamii pamoja na mambo ya Imani na Siasa hadi kwamba utofautisho wa halisi (thiqah) pia ulikuwa ukitofautiana na watu walivyokuwa wakielewa. Ni dhahiri kuwa jitihada kama hizi zinaweza kuleta matokeo ya uthamini sahihi wa Hadith na mapotoshi ya aina gani yaliyokuwapo.

Juu ya kuandika somo hili, abu Riyyah anasema, "Wakati Ahadith za Mtume s.a.w.w. zilipoachwa kuandikwa na Sahaba hawakuchukua hatua kuzikusanya, milango ya masimulizi ya Hadith kwa midomo ilifunguliwa kwa ajili ya wacha Mungu na vile vile hali hiyo kwa ajili ya waongo, wapotofu na wazushi, ambao walisimulia chochote kile walichokitaka bila ya kuwa na woga wa yeyote."

Mwandishi mwingine anaandika, "Moja ya sababu ya kuchomoza kwa waliokuwa wakibuni Hadith ni kwa sababu ya kutoziandika Hadith na Sahaba waliridhika kwa kusimuliwa kimdomo tu bila ya maandiko yoyote."

Abu al-Abbas al-Hanbali (716 A.H./1316 A.D.) anaandika:

Moja ya sababu ya kutofautiana kimashauri miongoni mwa maulamaa ni Hadith na maelezo yanayotofautiana. Baadhi yao wanafikiria kuwa Khalifa Umar ibn Khattab ndiye aliyehusika, kwa sababu Sahaba walimwomba ruhusa ya kuandika Hadith, lakini, yeye aliwazuia, mbali na kutambua ukweli wa amri ya Mtume s.a.w.w. ya kuandika hotuba yake ya Hijja ya mwisho kwa ajili ya Abu Shat na vile vile Mtume s.a.w.w.alikuwa amesema: "Ikamateni elimu yenu kwa kuiandika.'Iwapo kila Sahaba angaliandika alichokisikia kutoka kwa Mtume s.a.w.w., basi Sunnah zingalinakiliwa bila ya kuwapo na msimulizi zaidi ya mmoja (mfululizo wa wanaosimulia) baina ya Mtume s.a.w.w. na (kizazi kilichofuatia) Ummah."

Ni jambo la kuvutia sana kwa kuangalia kuwa Abu al-Abbass alishutumiwa kuwa ni rafidh (aliyeasi) na tashayyu (kuwa Shiah) kwa sababu ya maelezo yake hayo!

Abu Riyyah katika maelezo yake mengineyo, yeye anajitokeza katika kukana imani kuwa Mtume s.a.w.w. ndiye alitoa amri ya kutoandikwa kwa Hadith, anasema:

"Je ni sahihi kuwa Mtume s.a.w.w. atakuwa amepuuzia nusu ya kila alichofunuliwa, akiicha bila kuhifadhiwa katika mioyo ya watu, ambamo mmoja wao anakumbuka, na mwingine, anasahau wakati huo huo na mwingine anaongezea atakacho kwa yale yasiyoandikwa......? Je uangalifu wa Sahaba upo wapi vile walivyoijali Quran? Hakuna kingine chochote kile kwa sababu ya dharau isipokuwa ni matokeo ya kutoandikwa huku kwa nusu ya ufunuo na wao wote ni wenye madhambi katika swala hili."

Ibrahim ibn Sa'id ameelezea zaidi kuwa uandishi wa Hadith ulianza pale ambapo palipogunduliwa kuandikwa kwa Hadith za uongo na uzushi. Yeye anasema, "Kama isingalikuwa kutokezea kwa Hadith kutokea Mashariki, sisi tusingalikuwa tumeandika Hadith hata moja, wala kusingaliruhusiwa kuandikwa kwake."

Habari kama hiyo pia imeelezwa na Ibn Shihab al-Zuhri. Hata hivyo, Hadith ziliandikwa kwa kuchelewa mno. Uchelewesho huo unaweza kuonekana kutokana na ukweli kuwa sahih ya al-Bukhari alichaguliwa miongoni mwa Hadith laki saba na Abu Hanifa alizikubali Hadith 150 tu kati ya Hadith milioni moja!

  1. Kusimulia Hadith kwa kutoa maana tu na wala si kwa

maneno yake

Mojawapo ya athari za kutoandika kwa Hadith ni kule kusahauliwa kwa maneno halisi ya Hadith na lilikuwa ni jambo la kawaida kutokea masimulizi yaliyokuwa juu ya maana tu. Ni jambo la kawaida pia kwa mtu aliyesikia Hadith miaka ishirini iliyopita kuielezea kwa maana yake tu wakati aisimuliapo. Kuongezwa na kupunguzwa ni mambo ya kawaida katika hali kama hizo. Hata hivyo, iwapo Hadith zingalikuwa zimeanza kuandikwa kuanzia hapo mwanzoni, uwezekano wa janga kama hilo lingalikuwa dogo.

Imran ibn al-Husayn anasema:

"Kwa kiapo cha Mungu, nilitaka kusimulia Hadith za Mtume s.a.w.w. kwa mfululizo wa siku mbili, lakini kile kilichonizuia kilikuwa ni kuwaona kwangu wale waliosikia Hadith kama mimi, lakini wao walisimulia Hadith katika sura isiyokuwa ya halisi.(Kusimulia kwa kuelezea maana tu).Nami nilikuwa nikiogopa nisije nikasimulia Hadith kama wao. Lakini nakuambia, wao wanafanya makosa mengi katika kusimulia Hadith, ingawaje ni bila ya kunuia."

Sufyan anasema:

"Mimi nilisikia kupitia wasimulizi wa Hadith kutokea Bara' ibn Azib kutokea Mtume s.a.w.w. kuwa: "Nilimwona Mtume s.a.w.w. akiinua mikono yake alipokuwa akiianza sala." Na pale nilipokwenda Kufah, nilimwona msimulizi Ibn Abi Layla, akiongezea maneno "Hapo baadaye hakurudia hivyo' katika hayo. Inaonekana kuwa fahamu zake zilikuwa nzuri pale alipokuwa Makkah. Mimi niliambiwa kuwa fahamu zake zimepata mabadiliko kidogo."

Ibn al-Jawzi, katika kuelezea habari za wasimulizi wa Ahdith zenye uzushi, anaandika:

Aina ya kwanza ni wale, ambao chini ya ushawishi wa utawa, polepole walipuuzia kuhifadhi Hadith pia kuzitambulisha Hadith na wale, katika hali ya makosa walisimulia Hadith kutokana na hifadhi zao baada ya vitabu vyao kupotea au kuungua au kuzikwa. Aina hii ya watu mara nyingi walisimulia Hadith mursal kama marfu', mawqul kama musnad na mara nyingi waliziingiza Hadith za hapa kuingia pale na za pale kuingizwa hapa.

4. Ufarakano miongoni mwa Waislamu:

Matokeo mengineyo ya kutoandika Hadith ni kugawanyika na kufarakana kwa mashauri ya Waislamu katika mambo ya halali (Shariah), hadi kufikia ufarakano wao katika fatawa na imani. Na haya yalitokana na Hadith zilizotofautianan, ndivyo ilivyokuwa hali ya Waislamu katika nyakati hizo. Kufuatia ushindi wa awali, Islam ilienea katika maeneo mapya. Sahaba na Tabiun ambao walielekea sehemu mbali mbali zilizokuwa mpya, kila mmoja wao alichukua sehemu ile tu ya Hadith ambayo alisikia kutokea kwa Mtume s.a.w.w. au Sahaba. Kutoka Madinah, baadhi yao walikwenda Makkah na Yemen, baadhi yao walikwenda Syria na Palestina, na baadhi yao waliishi katika miji ya Iraq kama vile Kufah na Basrah.

rudi nyuma Yaliyomo endelea