rudi nyuma Yaliyomo  

Matokeo ya hayo, ni kwamba kila mmoja wao alichukuliwa msimamo wake kwa mujibu wa Ahdith alizokuwanazo. Bila ya kujua Ahdith walizonazo wengineo, kila mmoja wao alifuata fatawa tofauti. Ufarakano huu ulipotambuliwa katika kipindi cha Tabiun, wao walianza kusafiri ili kuzuru miji tofauti, na hivyo ndivyo 'Safari ya kutafuta Hadith' (al-rihlah talab al-Hadith) ilivyokuja kubuniwa.

Wingi wa safari hizi zilitokea katika karne ya 2 A.H./8 A.D. na 3 A.H./9 A.D. , na hata baada ya hapo sababu ya uhakika nyuma yao ilikuwa kutawanyika kwa Hadith kwa kupitia miji tofauti na Wanazuoni waliotembea huko na huko katika kutafuta na kuleta namna moja ya Hadith baina ya Hadith za sehemu moja na nyingine; lakini wakati mwingine ilitokea kwamba Hadith moja iliweza kusimuliwa tofauti katika sehemu zinginezo - jambo ambalo mfano wake tumeulezea hapo awali.

Sisi twaambiwa kuwa Abd Allah ibn Mubarak alisafiri hadi Yemen, Misri, Syria na Kufah kwa madhumuni ya kukusanya Hadith.

Abu Hatim al-Razi anaandika:

"Safari zangu za awali zilinipeleka katika kutafuta Hadith, zilinichukua miaka saba. Mimi nilipiga hisabu ya umbali niliosafiri kwa miguu nikapata jumla ya 'Parasang' (parasang moja ni sawa na takriban maili nne hivi) elfu moja. Basi mimi nilikuwa nikiendelea kuongezea hivyo hivyo hadi zilipokuwa zikifikia parasang elfu moja......Mara nyingi nilisafiri kutoka Makkah kwenda Madinah na kutoka Misri hadi Ramlah, kutoka hapo hadi Asqalan, Tabariyyah, Demascus, Homs......

Ibn Musayyat anasema: "Mimi nilikuwa nikisafiri usiku na mchana katika kutafuta Hadith moja." Safari hizi zilikuwa zimeenea sana hadi al-Khatib alikusanya maandiko juu ya somo hilo kwa kukipatia jina la al-rihlafi talab al - Hadith na vile vile al-Ramhurmuzi aliandika sura juu ya somo hilo katika kitabu chake al-Muhaddith al-fadhil.

Safari hizi za kutafuta Hadith zilikuwa muhimu mno hadi Yahya ibn Muin ilimbidi aseme: "Kuna aina nne ya watu ambao hawawezi kutegemea kukomaa kwao....mmoja wao ni yule ambaye atabakia mjini mwaka akiandika Hadith hapo, na hakusafiri hadi miji mingine katika kutafuta Hadith."

Matatizo kama hayo, ambayo ni matokeo yenyewe ya kutoandika Hadith, hayakutokea katika swala la Quran.Iwapo Hadith za Mtume s.a.w.w. zingalikuwa zimeshaanza kuandikwa kutokea miongoni, kwa ushirikiano wa Sahaba wote kwa pamoja, Vyuo vyote vya Kisheriah - na hata kiitikadi na kisiasa - zilizotokezea hapo baadaye basi zisingaliweza kuwapo. Vyuo vyote hivi vinategemea imani zao juu ya Ahdith. Je kwa kiasi gani Hadith hizo zilikuwa Sahihi? Je kwa kiasi gani zilikubaliwa na wengine? Kwa kiasi gani wengineo walikubalia maagizo yake iwapo masimulizi yalitegemea maana tu? Haya ni maswali ambayo hayakupatiwa majibu.

Abu Suhrah anaandika:

Wakati Umar alipofariki na Sahaba walipoondoka kwenda miji tofauti, kila mmoja wao alianzisha Chuo cha Sharia kwa ajili yake na hivyo kila mmoja wao aliifuata njia yake. Ulipofika wakati wa Tabiun, kila mji ulikuwa na Chuo chake cha Sharia na mitazamo yao ilikuwa tofauti na mbali na zingine kama vile miji yenyewe ilivyokuwa mbali na nyingine.

Siku moja, al-Mansur alimwambia Malik ibn Anas, juu ya nia yake ya kutumia muwatta Malik kama ndiyo Shariah ya Dini, kwa kutegewa na Waislamu wote wa miji hiyo na kufundisha na kufuata yaliyokuwamo na kujiepusha na chochote kile (kama ndiyo mamlaka ya Shariah), na hivyo ingalifanyika kwa kutengeneza nakala zaidi ya hivyo kwa ajili ya miji yote. Malik alimwambia, "Ewe Amir al-Muminiin, usithubutu kufanya hivyo. Watu hawa wanazo itikadi zao, wakiwa wamesikia kila Ahadith na kuzisimulia, na kila mmoja wao anaamini katika kile alichokuwanacho. Waache peke yao watu wa kila mji pamoja na kila walichojichagulia wao wenyewe."

5. Kuenea kwa Ra'y:

Athari nyingine ya kushindwa kwa uandikaji wa Hadith ilikuwa ni kutokezea na kutumika zaidi mno kwa ra'y (hukumu zisizo halisi au hukumu za kibinafsi) miongoni mwa Mahakimu wa Kiislamu, kwa sababu kila mmoja wao alikuwa na kiasi kidogo tu cha Hadith alizokuwa akiweza kuzifikia, kwani mno ama zilipotea au hazikuweza kufikiwa.

Watu walishindilia kutoa fatawa wakati ambapo wao walikuwa hawana kiasi cha kutosheleza cha Hadith kuwasaidia katika hatua hiyo. Kwa hivyo wao iliwabidi kuchagua njia ya ra'y ili kuweza kuwajibu watu. Zaid ya hayo, wengineo walikuwa ni mabingwa katika ra'y kwa sababu ya kutokuwa na imani katika Hadith, na hii ni wazi kwa kutokezea kwa sababu ya ukosefu wa Hadith zilizoandikwa.

Wakati fulani, katika mji mmoja hukumu ilitegemea Hadith iliyokuwapo, ambapo pengine hukumu ilikuwa inategemea uamuzi wa kibinafsi. Kwa bahati mbaya, baada ya muda fulani, zile hukumu za ra'y zilijipatia nafasi za mamlaka halisi ya hukumu kwa ajili ya wengine ambao wao pia hawakuwa na ufikio wa kutosheleza katika Hadith, wao walipendelea kufuatilia ra'y za mababu zao badala ya wao kubuni maamuzi yao ya kibinafsi (vile walivyokuwa .wakipendelea wao wenyewe). Kutanda huku kwa tabia ya ra'y kwa kufikia kiasi hiki miongoni mwa Ahl al-Sunna kulitokana na kutokuwapo na kutosheleza kwa Hadith, ambavyo kwa upande wa pili ulitokana na kupotea kwa idadi kubwa mno ya Hadith za Mtume s.a.w.w. na Sunnah zake.

15. UHARAMISHO WA KUSIMULIA HADITH:

Sisi tumezungumzia hapo awali vile uandihi wa Hadith ulivyoharamishwa na kile kilichotokea athari yake. Mazungumzo yetu hapa yanaelezea ukweli kuwa kama vile historia inavyoelezea, baadhi ya Sahaba walijaribu hata kuzuia kusimulia Hadith kwa mdomo pia.Wao walizuia uandishi wa Hadith kwa kisingizio cha Quran kulindwa, na wao waliharamisha kusimulia kwa mdomo pia kwa kisingizio cha kuwazuia watu wasitilie mkazo mambo mengine isipokuwa Quran tu, kama kwamba azma yao ilikuwa kuifanya Hadith ionekane kuwa ni kitu kisicho na maana wala kisipewe umuhimu wowote na vyovyote vile, kuna uwezekano wa kuwapo kwa sababu za kisiasa katika hatua hizo.

Qurzah ibn Ka'b anasema:

Sisi tuliondoka Madinah kwenda Iraq.Umar alitusindikiza hadi kufikia nje ya Mji. Yeye alituambia, "Je mnajua kwa nini mimi nimekuja nanyi hadi hapa?" Sisi tulijibu, "Labda` umekuja kutuaga, kwani sisi ni Sahaba wa Mtume s.a.w.w." Umar alisema, "Mimi nimekuja kuwaambieni kuwa nyie muuweke mkazo wenu zaidi juu ya Quran na kwamba musizisimulie Hadith za Mtume s.a.w.w. kwa zaidi, ila kidogo tu. Sasa endeleeni kwani mimi ni mshiriki wenu katika swala hili."

Qurzah anaongezea katika riwaya nyingine:

Pale mimi nilikuwa nimeketi miongoni mwa watu waliokuwa wakisimuliana Hadith. Ilionekana kuwa mimi ndiye niliyekuwa nikizijua Hadith nyingi kuliko wao. Lakini nilijikalisha kimya pale nilipokumbuka ushauri wa 'Umar.'

Katika mapokezi ya al-Dhahabi, yeye anaripotiwa akiwa amesema, wakati wao waliponiomba kusimulia Hadith za Mtume s.a.w.w., mimi niliwaambia kuwa Umar ameniharamishia kufanya hivyo.

Vile vile imeripotiwa kuwa wakati Khalifa alipomtuma Abu Musa al-Ashari kwenda Iraq, alimwambia, "Usiwashughulishe watu katika Hadith. Mimi ni mshiriki wako katika swala hili."

Riwaya hizi zinatuonyesha majaribio yaliyofanywa katika kuzuia kuenezwa kwa Hadith Mtume s.a.w.w., si pekee kwa maandishi tu. Ibn Asakir anaripoti haya yaliyosemwa na Ibrahim ibn Abd Rahmaan:

Haki ya Mungu, Umar hakufariki kabla ya kuwaita Sahaba wa Mtume s.a.w.w. kama vile Hudhayfah ibn al-Yamani, Abu al-Darda, Abu Dhar, Aqabah ibn Amir na ......Yeye aliwaambia: "Je ni Hadith zipi hizi ambazo nyinyi mnazieneza pembe zote?" Wao walimjibu, "Je, wewe unatuzuia kusimulia Hadith?"

Kwa mujibu wa riwaya iliyorikodiwa na al-Tabarani, Ibrahim ibn Abd Rahman alikuwa na uzoefu wa kusema:

"Umar alimwita Abd Allah ibn Mas'ud, Mas'ud al-ansari na Abu Darda. Yeye aliwaambia, "Je, ni Hadith zipi hizo za Mtume s.a.w.w. ambazo mnazisimulia kwa kupita kiasi?" Na kuanzia hapo aliwazuia Madinah tu hadi kufariki kwake (waliwekwa chini ya kifungo)."

Ni dhahiri kuwa watu hawa walikuwa ni miongoni mwa watu maarufu kabisa katika Sahaba wa Mtume s.a.w.w., Ahl al-Sunnah hawana shaka juu ya watu kama hawa juu ya usadikifu wa watu kama Hudhayfah, Abu Darda na Ibn Mas'ud hadi kuwa alipomtuma Iraq, aliwaandikia, "Mimi nimependelea faida yenu kuliko hasara yangu kwa kuwatumieni Ibn Mas'ud kwenu nyinyi."

Ibn Sazm amechukizwa mno na shutuma hiyo dhidi ya Khalifa, lakini, hakuthubutu kushutumu tendo la Khalifa, yeye anazusha mashaka kuhusu ukweli wa riwaya. Yeye anasema: "Hadith hii ni mursal, na yenye mashaka kwa sababu ya mmoja wa watu katika mfululizo wa wasimulizi ni Shu'bah. Hivyo haiwezi kuchukuliwa kuwa ni uthibitisho." Lakini sisi twaelewa kuwa Hadith hiyo ipo imepokelewa kwa kupitia mifululizo ya wasimulizi. Zaidi ya hayo, Ibn Haytham, katika Majma al-Zawaid (Vol. 1 uk. 147), baada ya kuitenga Hadith hii ni sahihi, ameandika: "Msemo huo wa Umar ni sahihi (inayosadikiwa) na ipo imesimuliwa kwa kupitia mifululizo ya masimulizi mengi."

Hata hivyo, Ibn Hazm, wakati akiichambua Hadith, anasema:

Riwayah hii kwa uthibitisho ni uongo; kwani aliyesema itatubidi tuseme kuwa amejitoa katika mipaka ya Islam, kwa sababu jitihada zake zililenga katika kufunika na kupuuzia Hadith za Mtume wa Allah swt.

Mwandishi wa al-Sunnah qabl al-tadhwin anaandika:

Ukweli kuwa kuwekwa mahabusu (habs) kwa Sahaba (katika Madinah) kulitokana na wao kusimulia Hadith za Mtume s.a.w.w. , sivyo sahihi. Kwa sababu Abu Hurayrah alikuwa mmoja wa watu wa aina hiyo, na ambapo yeye hakuwekwa mahabusi (na Umar).

Habari ya hapo juu si ya kweli, kwa sababu Abu Hurayrah mwenyewe alikuwa ni mmoja wa wale waliopigiwa marufuku na Umar katika kusimulia Hadith za Mtume s.a.w.w. Abu Hurayrah alitekeleza maamrisho ya Umar na hivyo aliweza kusimulia Hadith kidogo mno katika uhai wa Umar.

Imekamilika, wal hamdu lillah.

rudi nyuma Yaliyomo