rudi nyuma Yaliyomo endelea

“Wakati Islam ilipoenea katika sehemu mbalimbali, na miji ya Islam ilipopanuka, tabi'un walisambaa mote humo. Baada ya muda, mkuu wao alipofariki dunia na hivyo ndivyo ilivyokuwa imekuja kuathiri ukusanyaji wa Hadith. Wanazuoni walianza kuhisi haja ya kuziandika Hadith na kuzihifadhi kwa njia ya kuziandika. Katika maisha yangu, lilikuwa ni jambo la maana la kuziandika Hadith, kwa sababu kukariri tu kuna uwezekano mkubwa wa kuweza kuja kupoteza fahamu au kuzipotoa. Baada yao, kulitokezea kipindi cha wataalamu wa Hadith kama Ibn Jurayj na Malik ibn Anas. Inasemekana kuwa mtu wa kwanza katika kukusanya Hadith alikuwa Rabi ibn Subay wa Basrah. Baada yahuyo, zoezi kama hili lilikuwa ni la kawaida.

Kutokana na taarifa hizo, tunaweza kumalizia kuwa, kotekote, kulikuwapo na vipindi vitatu katika mpitilio wa Hadith za kutamkwa. Kipindi cha kwanza kilichukua/kilidumu mwanzoni hadi mwishoni mwa karne ya 1 A.H. /7 A.D. katika kipindi hiki uandishi wa Hadith haukuwapo wala haukujaribiwa isipokuwa tu katika hali chache ambapo Sahaba walijaribu kuziandika kwa kwenda kinyume na amri ya Makhalifa. Katika kipindi cha pili, kuanzia mwanzoni mwa karne ya 2 A.H./8 A.D. hadi kwa kufikia katikati, kulitokezea uandishi na ukusanyaji wa Hadith katika hali isiyokuwa kamilifu na pia mambo yaliyoandikwa yaliweza kukusanywa. Katika kipindi cha tatu, kilichoanzia katikati ya karne ya 2 A.H./8 A.D., uangalifu mkubwa ulielekezwa katika ukusanyaji na uandikaji wa Hadith ikiwa ni shughuli muhimu kimsingi. Vitabu vichache mno vilivyoandikwa katika kipindi hiki vinaweza kupatikana na baadhi ya mikusanyiko ya zamani sana pia vinaweza kupatikana na baadhi ya mikusanyiko ya zamani sana pia vinaweza kupatikana- kama vile musannaf Ibn Abi Shaybah, musannaf ya Abd al-Razzaq na Muwatta ya Malik ibn Anas yalikuwa yameanzishwa katika sehemu ya pili ya karne ya 2 A.H./8 A.D.

Kwa mujibu wa ripoti ya al-Dhahab, musnad ya kwanza ilikusanywa na Nu'aym ibn Hammad. Yahya al-Hamani huko Kufah na al-Musd huko Basrah nao ndio waliokuwa wa kwanza miongoni mwa Wanazuoni wa miji hii katika kukusanya musnad.

  1. SABABU ZA UCHELEWESHO KATIKA UANDISHI WA

HADITH

Inafahamika vyema kabisa kuwa Mtume s.a.w.w., kuanzia mwanzoni kabisa mwa Utume wake, aliupatia umuhimu zaidi kuhusu uandishi wa Qurani. Kimatokeo Qurani ikawa ipo mbali na makosa au mabadiliko (tahrif). Hata hivyo, katika hali ya Hadith kwa mujibu wa imani yetu mbali na ruhusa au amri ya Mtume s.a.w.w. kwa kuhusiana na uandishi wa Hadith na mbali na ukweli kwamba Hadith zilikuwa zimeandikwa katika zama za uhai wa Mtume s.a.w.w. , sio kwamba tu kuwa haukupewa umuhimu kwa kazi, pia iliweza hata kupingwa. Upingamizi huo ulisababisha matatizo mengi kuhusiana na Hadith, ambayo tutayaona hapo mbeleni.

Uchelewesho huo wa kuziandika Hadith na matokeo yenye hatari yalifanya kikundi kimoja kumtupia lawama na 'udhubillah Mtume s.a.w.w. Wao walitambua wazi kuwa upingamizi wa uandishi wa Hadith iwapo itatokea kwa Mtume s.a.w.w. , basi haitaweza kulaumiwa, kwani Mtume s.a.w.w. hawezi kulaumiwa; hata hivyo, iwapo wataielezea kwa wengine basi itatoboa udhaifu wao. Kwa hivyo, walimwelekezea Mtume s.a.w.w. kuwa ndiye aliyekataza kuandikwa kwa Hadith.

5. RIWAYA YA ABU SA'ID:

Riwaya ifuatayo imenakiliwa kwa mamlaka ya Abu Sa'id al-Khudhri:

"Musiandike chochote kile kutoka kwangu isipokuwa Qurani tu, na yeyote yule aliyekwisha andika chochote kile basi ni lazima ayateketeze yote."

Taarifa hiyo ni wazi na yenye maana isiyofahamika. Maana inayotakiwa kuelezwa ni kwamba hakuruhusiwi kuandikwa kwa Hadith. Kwa mujibu wake, mtu yeyote aliyekuwa ameandika chochote kile basi lazima akiteketeze. Ni sawa kabisa kwa sababu ya uwazi wa ubainishi wake, vile vile pamoja na sababu zinginezo, ndiyo maana sisi hatuwezi kuikubali uhakiki wa taarifa hiyo au nyinginezo kama hizo. Sababu zetu za kutokubaliana na Hadith hiyo ya juu ni kama zifuatazo:

  1. Kwanza, iwapo sisi tutaikubalia Hadith hii basi hatuwezi kuifungia kipindi cha muda. Iwapo uandishi wa Hadith ulikatazwa na haram, basi ni haram katika kila zama. Hata hivyo, sisi twaona wanaoinakili Hadith hii, wao wenyewe hawakuifuatilia na wao hatimaye waliziandika na kuzikusanya Ahadith. Uandishi huu, kama ilivyoonekana hapo juu, ulianza katikati ya karne ya 2 A.H./8 A.D., na kukosekana kwa utiifu wa Hadith inatuonyesha kuwa hao wanainakili Hadith walikuwa hawakuichukulia kama sahihi na kweli; kwani hao walijua kuwa chochote kile kilichoharamishwa na Shariah haiwezi kubadilishwa kikawa halali. Jambo la kuvutia humu ni kwamba wao wameirekodi hata Hadith hii, ambavyo wao hawakuifuatilia, kwa kalamu zao zilizobarikiwa! Je, itawezekanaje sisi kuiamini kuwa ni sahihi na kweli?
  2. Pili, waandishi hawa hawa pia wamezinakili Hadith zinginezo zinazozungumzia kuruhusiwa kuandikwa kwa Hadith, na iwapo sisi tutazichukulia Hadith zote mbili kuwa ni sawa katika maelezo na maelekezo, basi itatulazimu kuziachia mbali Hadith zote mbili hizo kwa sababu ya kupingana kwao kwenyewe. Kwa hivyo, katika hali kama hii Hadith hizi zote mbili zinapoteza ustahi wa kuaminika; navyo hata sisi, kwa kudhania tu, hatuwezi kamwe hata kutumia njia zinginezo kusadikisha Hadith ambayo ipo inakataza uandishi wa Hadith za Mtume s.a.w.w.
  3. Tatu, Abu sa'id al-Khudhri, ambaye anatajwa hapo juu kwa wingi katika kuinakili taarifa hiyo, pia anatoa taarifa nyingine inayopingana na ile ya kwanza, yeye anasema: "Katika siku hizo, sisi tulikuwa hatuandiki chochote kile isipokuwa Qurani na tashahud."

Nukta mbili zinaweza kufahamika kwa kujua sababu zake kutokana na taarifa za Abu Sa'id. Kwanza, Abu Sa'id haelezi kuwa kutoandika kwao Hadith kulitokana na amri ya Mtume s.a.w.w. kwani kama ingalikuwapo, basi angalionyesha hayo, hadi hapo isemwe kuwa maelezo kama hayo hayakuazimiwa hapa. Uwezekano huu wa pili uliotolewa, ingawaje unaweza kuchukuliwa kwetu sisi, inaonekana ya mbali mno. Na nukta ya pili ni kuongezwa kwa neno tashahhud katika taarifa hii, kitu ambacho hakipatanishi pamoja na kusudi la uharamisho wa kuandika isipokuwa Quran tu. Ni jambo la kutilia maanani kwamba Hadith nyingine kutoka kwa Ibn Mas'ud, neno istikharah limeongezwa pamoja na tashahhud.

Kwa kuhusiana na Hadith hii, inawezekana kukaulizwa, je, ni kwa nini Mtume s.a.w.w. aruhusu uandishi wa tashahhud pekee yake, ambapo inatambuliwa kuwa kutapotea vile wakati uendeleavyo, hayo pia yaliweza kutokea pamoja na Hadith zinginezo, baadhi yao ambazo zilikuwa na maongozo muhimu kabisa ya Shariah za Dini. Na katika upande wa pili, iwapo kulikuwapo na madhara yoyote katika kuziandika Hadith, basi madhara hayo pia yaliweza kutokezea katika kuandika tashahhud au chochote kile. Kwa hivyo, haikubaliki kimantiki kudai kuwa Mtume s.a.w.w. ndiye aliyeharamisha kuandikwa kwa Hadith.

  1. Nne, kile kinachoweza kukusanywa kutokana na historia- ambacho sisi tutalisemea kwa zaidi hapo mbeleni - Abu Bakr, na hata Khalifa wa pili, walipendekeza kuandikwa kwa Hadith mwanzoni mwa Ukhalifa wao. Hata hivyo, hapo baadaye wao waliharamisha kwa kutolewa kwa sababu zao. Hao Makhalifa kamwe hawakusema kuwa kazi kama hiyo ilikuwa imeharamishwa na Mtume s.a.w.w. Zaidi ya hayo wao waliposhauriana na Sahaba wengineo kuhusu kuandika Hadith, nao pia walipendezewa na shauri hilo. Hii pia linatuthibitishia kuwa hapa kutolewa amri na Mtume s.a.w.w. ya kuharamisha kuandika kwa Hadith.
  2. Katika mojawapo ya Hadith Abu Basir anaripotiwa akiwa amemwambia Abu Sa'id al-Khudhri: "Sisi twaandika chochote kile tukisomacho." Abu Sa'id alimwambia: "Je, wataka kuyakusanya ili ukitengeneze Kitabu? Mtume s.a.w.w. ametuelezea Hadith nasi pia twakuambia wewe, nawe pia kama sisi ni lazima uzikariri tu kwa mdomo bila ya kuandika."Nukta mbili hapa zinastahili kuchunguzwa. Kwanza, Abu Sa'id hasemi kuwa Mtume s.a.w.w. ndiye aliyeharamisha uandikwaji wa Hadith. Pili, sababu aitoayo kwa kutoziandika Hadith ni sawa na zile zilizoripotiwa kutokea kwa Khalifa wa pili, ambaye naye pia hamsemi Mtume s.a.w.w. kuwa ndiye aliyeharamisha uandishi wa Hadith. Katika hali yoyote ile, ni jambo la kuyakinisha kuwa Mtume s.a.w.w. kamwe hakuharamisha uandishi wa Hadith.
  3. Sita, kuna taarifa katika Hadith, moja kwa moja baada ya kutajwa hiyo ya juu, na kuwapo kwake pia kunatudalilishia kule kutothaminiwa kwake:
  4. "Simulieni (chochote kile utakacho) kutokea Waisraili. Hakuna madhara ndani yake." Kuanzia mwanzoni kabisa, kwa upande mmoja Mtume s.a.w.w. anafahamika kwa kuchukizwa mno katika kusikia hadithi za Mayahudi (hujulikana kama Israiliyyat) -na kwa upande wa pili, Wanazuoni wa Kiislam wamekwisha zitambua madhara ya mawazo yanayoenezwa nayo, inaweza kusemwa kuwa Hadith hiyo nzima ni kazi ya uzushi mtupu. Hadith hii inawataka Waislam kwa upande mmoja, waziandike Hadith za Mtume s.a.w.w., na hatimaye kwamba zitaweza kusahauliwa pole pole; na upande wa pili, inawapatia leseni ya bure ya kuunganisha chochote kile wakitakacho kutoka kwa Mayahudi, Haya ndiyo maazimio maovu kabisa za Hadith kama hizi za kuzuliwa. Je, kunaweza mtu yeyote mwenye akili timamu akasema kuwa Mtume s.a.w.w. ndiye aliyetoa amri kama hiyo?

    Ipo Hadith nyingineyo kutokea Abu Sa'id al-Khudhri ambayo inatuletea uwezekano wa Mtume s.a.w.w. kutomruhusu Abu Sa'id kuandika Hadith kutokana na sababu maalum, ingawaje, katika mtazamo wetu, uwezekano wa kuruhusiwa katika swala hili pia ni kwamba Hadith hii vile vile ni uzushi. Abu Sa'id asema:"Mimi nilimwomba Mtume s.a.w.w. ruhusa ya kuandika Hadith, lakini yeye alikataa kunipa idhini." Je kwa sababu zipi ?

    Hadith hii inatuunga mkono katika uwezekano wa Mtume s.a.w.w. kwa kumkatalia ruhusa ya kuandika Hadith katika swala la Abu Sa'id. Wakati inapozingatiwa katika nuru ya Hadith, ambazo sisi tutazinakili hapo mbeleni, ambapo Mtume s.a.w.w. yupo anaripotiwa kwa kutoa idhini kwa watu wengineo basi uwezekano huu utajipatia nguvu zaidi.

  5. KUTOKUBALIKA KWA HADITH ZA ABU HURAYRAH
  6. :

Kuhusiana na hayo, kuna Hadith kutoka kwa Abu Hurayrah ambayo pia imehusika. Abu Hurayrah asema:

"Mtume s.a.w.w. alitufikia wakati tulipokuwa tunaziandika Hadith. "Je, mwaandika nini?" Aliuliza Mtume s.a.w.w. mimi nilijibu: "Haya ni mambo ambayo sisi tumeyasikia kutoka kwako."

Mtume s.a.w.w. alisema: "Je, munataka kuandika kitabu mbali na Kitabu cha Allah swt? Hakuna kilichopotosha mataifa isipokuwa tu pale wameandika kitabu mbali na Kitabu cha Allah (Quran)"

Hadith hii pia haikubaliki kwa sababu zifuatazo:

  1. Kwa sababu ya wengi waliokwisha kutoa sababu zao katika masomo yao na ambazo sisi pia tumeziona kuwa zinaweza kukubalika baada ya kuchunguzwa, hivyo usadikifu ('adalah) wa Abu Hurayrah hauwezi kukubaliwa. Vile vile inawezekana kuwa Hadith hii imezuliwa na wengine halafu wakaja kumtaja Abu Hurayrah kuwa ndiye aliyeiripoti.
  2. Pili, mazungumzo yaliyomo ni sawa kabisa, kama vile yalivyokuwa yametolewa na Khalifa Umar wakati alipokuwa ameamua kuziandika Hadith na baadaye kughairi. Lakini Khalifa mwenyewe kamwe hakumsingizia Mtume s.a.w.w. Wakati ambapo Abu Hurayrah, au wale wote wengineo wakimsingizia Mtume s.a.w.w., hawakutupatia mwanya wa kubishana nao kwa madai yao (kwani madai yao ni kuwa Mtume s.a.w.w. tu ndiye aliyeyasema, hivyo hakuna ubishi juu yakauli ya Mtume): Khalifa Umar kama vile tutakavyoona hapo mbeleni, alifikia maamuzi hayo baada ya kuzingatia mambo fulani fulani.
  3. Tatu, mazungumzo yaliyomo na yanayonekana katika Hadith hii ingawaje inaonekana kuwa inayo mizizi katika kauli ya Mtume s.a.w.w. ambayo itazungumzwa hapo mbeleni, inazungumzia juu ya Mtume s.a.w.w.. kuharamisha vitabu vya Mayahudi na Wakristo, na wala si kuharamishwa Hadith za Mtume s.a.w.w. ambazo ni kitu kilicho kamili baada ya Quran.
  4. Nne, je inawezekana kwa Mtume s.a.w.w. kuharamisha kuandikwa kwa Sunnah, ambayo ndiyo inayofuatia baada ya Quran? Au aliharamisha kuwa hivyo isibakie sambamba na Quran? Je, ni nafasi ipi iliyo ya Sunnah ya Mtume s.a.w.w. isiokuwa ubavuni mwa Quran? Je, ni ukweli unaoweza kupingwa kuwa Quran na Sunnah ndivyo kwa pamoja vinafanya Shariah za Kiislam?
  5. Ipo Hadith nyingine ivutiayo, ambayo inadhihirisha tabia ya udanganyifu wa Hadith kama hizo, nayo ni ile iliyonakiliwa na Abu Hurayrah. Baada ya kuelekezea kama taarifa tuliyonayo ipo, inaendelea kuongezea mambo mengi ambayo yanatudhihirishia upotofu katika upande wa Abu Hurayrah, au mzushi aliyezusha juu yake. Kwa mujibu wa Hadith hii, Mtume s.a.w.w. aliwasikia watu wameziandika Hadith zake. Papo hapo, alikwenda juu ya Mimbar na baada ya kumsifu Allah swt alisema:

    "Ni aina gani ya vitabu hivi ambavyo nimesikia mmeviandika? Kwa hakika mimi ni mwanadamu tu. Yeyote aliyeandika chochote kile, basi ni lazima aniletee mimi."

    Hadith hiyo kwa wazi wazi inakanusha Sunnah ya Mtume s.a.w.w. kwani Mtume s.a.w.w. yupo anakana uwezekano na uhalali wake wa utume kwa kusema kuwa yeye alikuwa ni mtu kama watu wengine wa kawaida. Hili ni jambo ambalo mtu yeyote hawezi kulikubali kwani ni uzushi mtupu.

    Jambo la kuvutia zaidi ni kuhusu kusema kwa Mtume s.a.w.w. hapa ('mimi ni mwanadamu') ipo imeelezwa katika Hadith nyingine kuwa hayo yalisemwa na kikundi cha watu wa Quraysh kuhusu Abd Allah ibn Amir ibn al-As, ambaye alikuwa ameandika Hadith za Mtume s.a.w.w. Hapo Mtume s.a.w.w. hatilii maanani maoni yao kwa hakika yupo anayakanusha. Anasema:"Mimi hakuna nilisemalo isipokuwa ni haki tupu."

  6. Tano, ipo imeripotiwa kutoka Abu Hurayrah mwenyewe kuwa hakuna mtu yoyote yule anayemzidi katika kunakili Hadith, isipokuwa Abdallah ibn Amribn al-As, kwa sababu huyu alikuwa akiziandika wakati ambapo Abu Hurayrah hakuwa akifanya hivyo. Taarifa hii inaonyesha kutokuwapo kwa uharamisho Abdallah aliziandika Hadith zote, ambapo zipo sababu za kibinafsi zilizomfanya Abu Hurayrah asiziandike. Hivyo, inatuonyesha wazi wazi kuwa hapakuwepo na amri yoyote yenye kuharamisha kuandikwa kwa Hadith za Mtume s.a.w.w.; wote waliotaka kuziandika waliziandika, na yeyote asiyetaka kuziandika hakuziandika lakini kwa sababu zao binafsi bila ya kuzuiwa.
  7. Sita, katika ripoti nyingineyo Abu Nuhayk, mwanafunzi wa Abu Hurayrah, asema:
  8. "Mimi nilikuwa nikiviazima vitabu kutoka kwa Abu Hurayrah, nilinakili, na kumchukulia (makala zangu) Abu Hurayrah na kumsomea. Kwa kila Hadith nilikuwa nikimwuliza iwapo amewahi kumsikia Mtume Mtukufu s.a.w.w. akiisema, naye alikuwa akiitikia."

    Hadith hii pia inaonyesha uongo wa Hadith isemayo kuharamishwa uandishi wa Hadith, ambayo amesingiziwa Abu Hurayrah.

  9. Imeripotiwa na Hamman ibn Munabbih, mwanafunzi wa Abu Hurayrah kuwa alikusanya mus-haf iliyokuwa na Hadith zote zilizokuwa zimenakiliwa na mwalimu wao katika uhai wake.
  10. Hayo pia yanatuonyesha kupingana na Hadith hiyo, kwani isingewezekana kwa Abu Hurayrah kunakili Hadith inayoharamisha uandishi wa Hadith wakati ambapo wanafunzi wake wameziandika Hadith mbele yake na katika uhai wake, au tuseme labda kuwa Abu Hurayrah hakutekeleza Hadith ipigayo marufuku uandishi wa Hadith kwa kunakili Hadith na kuzifundisha.

    Vile vile ipo Hadith nyingineyo iliyoripotiwa na Zayd ibn Thabit kwamba siku moja alimwendea Muawiya, ambaye alimwuliza kuhusu Hadith fulani. Hapo Muawiya alimwambia mtu fulani kuiandika. Hapo Zayd alisema: "Mtume Mtukufu s.a.w.w. ametuambia tusiandike Hadith ya aina yoyote ile."

    Sisi twaamini kwa uhakika uliowazi kuwa Hadith zilikuwa zimeandikwa na Tab'un na Tabi'in na baadhi ya wanazuoni wa Sunni, wanathibitisha kutotegemewa kwa Hadith kama hizo. Hapo mbeleni katika kulichambua swala hili, sisi tutaona uthibitisho utakaoonyesha sababu za kweli katika kuharamisha uandishi wa Hadith za Mtume Mtukufu s.a.w.w. Uhakika na uthibitisho huu unaonyesha kuwa sahihi kwa kumsingizia Mtume s.a.w.w. kwa taarifa kama hizo.

    Pia imeripotiwa kuwa Ibn Mas'ud alielezea katika usia wake kuwa mkusanyo (sahifa) wa Hadith zilizofanywa naye, ziteketezwe.Katika sura hii, haionyeshi wazi iwapo tendo hili lilikuwa limejibu amri ya Mtume Mtukufu s.a.w.w. Labda inawezekana, alikuwa akifuata amri ya Makhalifa. Pili, kama vile tutakavyozungumza hapo mbeleni, tendo hilo linaelezea kuhusu kuteketeza riwaya na mapokezi ya Mayahudi (Israilliyyat) na wala si Hadith za Mtume s.a.w.w.

    Vile vile imeripotiwa kuwa Abu Musa al-Ash'ari aliziteketeza Hadith zilizokuwa zimeandikwa na mtoto wake. Tukichukulia utiifu wa Abu Musa kwa Khalifa wa Pili, labda inaweza kusemwa kuwa tendo lake hili lilikuwa bila shaka chini ya ushahidi kuonyesha kuwa Abu Musa alitenda kwa kuvutiwa na uharamisho huo wa Mtume s.a.w.w. kuhusu Hadith.

    Moja ya kitu kinachoonyesha kutokuwa halisi kwa mapokezi hayo yaliyozuliwa juu ya Mtume s.a.w.w. kuharamisha uandishi wa Hadith, ni kauli aliyoitoa Umar kuhusiana nalo kwa nia yake ya kutaka kukusanywa kwa Hadith za Mtume s.a.w.w. Umar anaripotiwa akiwa amesema: "Mimi nilinuia kuziandika Sunnah za Mtume s.a.w.w. Lakini lilikuja wazo akilini mwangu kuwa watu waliopita walikuwa wameandika baadhi ya vitabu na walikuwa wakivitegemea mno, hatimaye wao waliacha kukitegemea Kitabu cha Allah swt. Kwa kiapo cha Mungu, mimi sitakubaliana na chochote kile kitakachoweza kukifunika (kuachwa) Kitabu cha Allah (Quran)."

    Katika riwaya ya hapo juu, inaonyesha kuwa Khalifa wa Pili alinuia kuandika Hadith hapo awali. Katika baadhi ya tafsiri ya riwaya hii inaelezea kuwa aliwashauri Sahaba wengine kuhusu swala hili nao pia walilikubalia (kuandika Sunnah za Mtume s.a.w.w.); lakini hapo baadaye yeye alilibadilisha shauri lake hilo kwa sababu zake alizozitaja, na wala si kwamba Mtume s.a.w.w. ndiye anayehusika katika kuharamisha.

    Jambo lingine ambalo linaloweza kuonekana kama uthibitisho wa kukanusha uhalisi wa Hadith isemayo juu ya uharamisho wa kuandika Hadith, ni maneno aliyoyasema Mtume s.a.w.w. siku ya Alhamisi ya mwisho katika maisha yake (yaani kabla ya kufariki). Siku hiyo, walikusanyika Sahaba wote katika kitanda chake Mtume s.a.w.w. na hapo Mtume s.a.w.w. aliwaambia: "Nileteeni wino na karatasi ili niweze kuwaandikieni mambo fulani fulani ambayo hapo baadaye nyie mnapashwa kujitahadharisha msitumbukie katika makosa." Hapo baadhi ya watu wakiongozwa na Umar walipinga hayo wakisema "Kitabu cha Allah kinatosheleza kwetu sisi." Riwaya hii inatuonyesha kuwa uandishi wowote mbali na Quran haukupigwa marufuku tu, bali hata ulichukuliwa na Mtume s.a.w.w. kuwa ni lazima ili kuokoa Ummah kuangukia makosa na upotofu. Wakati Mtume s.a.w.w. alipokuwa akiulizia vifaa vya kuandikia na kikundi cha Sahaba - kikiongozwa na Khalifa wa Pili kwa mujibu wa al-Shahristani katika al-milal wa al-nihal- walimpinga Mtume s.a.w.w., kwani Mtume s.a.w.w. alikuwa akielewa wazi maafa yatakayotokea hapo baadaye kutokea tukio au kisa hiki. Hapo mbeleni sisi tutachambua kwa undani zaidi yaliyokusanywa na kusemwa na wanazuoni wa Sunni kuhusu athari mbaya zilizotokana na kutoandikwa kwa Hadith lakini ni lazima tujiulize "Je, ni sahihi kwa kumdhania Mtume s.a.w.w. katika kuharamisha kuziandika Hadith zake, jambo ambalo limeleta maovu makubwa katika utamaduni wa Kiislamu na kusababisha Sunnah za Mtume s.a.w.w. kuchezewa na Hadith hizo za kuzuliwa? Je, ni kweli kuwa Mtume s.a.w.w. ndiye anayehusika moja kwa moja katika upotofu huu na madhara yote yaliyotokea?"

  11. HADITH ZA MTUME S.A.W.W. KATIKA KURUHUSU
  12. UANDISHI WA HADITH

    Hadith zimepokelewa kutoka Mtume s.a.w.w. ambamo yeye ameruhusu uandishi wa Hadith kijumla au kuruhusu kikundi fulani. Hadith hizi, zenyewe, zinatosheleza kukanusha Hadith zilizotangulia zinazozungumzia kuhusu kuharamishwa kwa uandishi wa Hadith, au tuseme haikosi, kuleta vurugu la riwayaat (wingi wa riwaya) katika hali yoyote, zinashindwa kubakia na uhai wao (hujjiyyah);kwani idadi ya Hadith hizi ni kubwa mno, na kwa kutilia maanani ya makanusho yaliyonayo dhidi ya Hadith zinazozua juu ya kutoandika Hadith, basi uhalisi wa Hadith kama hizi ni zenye kusadikiwa kabisa. Hadith hizi si kwamba zinazoruhusu kuandika Hadith bali pia zinatuamrisha kuziandika Hadith za Mtume s.a.w.w.

    Hadith ifuatayo imenakiliwa kupitia mfululizo wa upokezi kuwa kulikuwapo na mtu aliyemlalamikia Mtume s.a.w.w. juu ya udhaifu wake wa kuhifadhi mambo katika akili yake. Mtume s.a.w.w. alimwambia: "Chukua msaada wa mkono wa kulia (i.e. kuandika) dhidi ya udhaifu wa hifadhi ya akili yako."

    Mtume s.a.w.w. yupo anaripotiwa akisema:

    "Ikamateni (hifadheni, iandikeni) elimu kwa njia ya kuandika."

    Imeripotiwa kutoka Rafi' ibn Khadij kuwa yeye alisema: "Sisi tulimwuliza Mtume s.a.w.w. ,'Je tunaweza kuandika baadhi ya mambo ambayo twayasikia kwako?' Mtume s.a.w.w. alijibu, 'Andika hayo na wala hakuna madhara ndani yake.' Imeripotiwa kwa mamlaka ya Amr ibn Shu'ayb kuwa baba yake alimwuliza Mtume s.a.w.w.: "Sisi tukisikia mambo kutoka kwako ambayo hatuwezi kuhifadhi akilini mwetu kwa kipindi kirefu, je, tunaruhusiwa kuyaandika?" Hapa Mtume s.a.w.w. alijibu: Naam, muyaandike"

    Imeripotiwa kupitia mifululizo ya wanaonakili, kutoka Abdallah ibn Al-As kwa kusema: "Mimi nilimwuliza Mtume s.a.w.w.: 'Je, tunaweza kuandika kile tukisikiacho kutoka kwako? Mtume s.a.w.w. alijibu, 'Naam.' Mimi niliulizia. 'Bila ya kujali wewe ukiwa umeghadhabika au mpole? Mtume s.a.w.w. alijibu, "Naam mimi sizungumzi chochote kile isipokuwa haki tupu, hata kama nikiwa nimeghadhabika au nikiwa nimefurahishwa."

    Katika Hadith nyingine, msimulizi anaripotiwa kwa kumwuliza Mtume s.a.w.w. "Je, twaweza 'kuikamata' elimu?" Mtume s.a.w.w. alijibu: "Naam."

    Huyo huyo Abd Allah ibn Amr anaripotiwa kuwa,"Nilikuwa nimezoea kuandika chochote kile nilichokisikia kutoka kwa Mtume s.a.w.w. kwa ajili ya kurekodi. Baadaye Ma- Qureyshi walinizuia kufanya hivyo, na mimi pia niliachilia kuandika. Baadaye, mimi nilimwelezea Mtume s.a.w.w. swala hilo. Naye alisema, "kwa kiapo cha Mungu ambaye anayamiliki maisha yangu, mimi kamwe sitamki chochote kile isipokuwa haki tupu."

    Imeripotiwa na Amir al-Muminiin Ali ibn Abi Talib a.s. kuwa Mtume s.a.w.w. alisema: "Andikeni elimu (ilim) kwani mutafaidi nacho humu duniani na akhera vile vile. Eleweni kuwa elimu haikubali mmiliki wake ateketee."

    Hadith nyingine mashuhuri ya Ma-Imam wa Ahl al-Bayt a.s. ambayo imesimuliwa na chanzo cha Sunni na Shia, inaelezea maandiko (sahifah) juu ya upanga wa Mtume s.a.w.w. Al-Imam al-Sadiq a.s. anaripotiwa akiwa amesema:

    "Kulikuwapo na Sahifah katika mpini wa upanga wa Mtume s.a.w.w. yakisomwa: "Amelaaniwa yule anayeiba mipaka ya ardhi. Amelaaniwa yule ajifanyiaye marafiki mbali na mawali wake." Au alisema, "amelaaniwa yule ambaye anakana neema za Mola wake aliyempatia."

    Abu Hurayrah anaripotiwa akisema: "Hakuna yoyote yule anayeweza kuelewa zaidi yangu kuhusu Hadith za Mtume s.a.w.w. isipokuwa Abd Allah ibn Amr, kwa sababu yeye alikuwa akiyaandika kwa mkono wake, na kuhifadhi akilini mwake, ambapo mimi nilikuwa nikiyahifadhi tu bila ya kuyaandika. Naye huyo alikuwa amepatiwa idhini na Mtume s.a.w.w. kwa ajili ya kuziandika Hadith zake."Abd Allah ibn amr anaripotiwa kwa kusema: "Mimi nataka kusimulia Hadith zako na iwapo wewe utaniruhusu mimi nitaweza kuutumikisha mkono wangu (i.e. katika kuandika) ili kuusaidia moyo wangu (i.e. kuhifadhi). Na Mtume s.a.w.w. alisema, 'iwapo ni Hadith zangu, basi lazima uchukue msaada wa mkono wako.''' Yeye pia anaripotiwa kuwa na sahifah ambayo ilijulikana vyema kama al- Sahifat al-Sadiqah, ingawaje wengine wanakana kama ilikuwa na Hadith za Mtume s.a.w.w. Al-Mughirah ibn Shu'bah anaripotiwa kwa kuthibitisha kuwa Abd Allah ibn Amr alikuwa na Sahifah iliyoitwa al-Sahifah al-Sadiqaah.

    Katika Hadith nyingine, Mtume s.a.w.w. anaripotiwa akisema: "Wakati mumin anapokufa, karatasi alimoandika elimu (ilim) itabakia daima na itakuwa ni pazia baina yake na moto wa Jahannam Siku ya Qiyama."

    Al-Tirmidhi ameripoti kuwa Sa'id ibn Ubadah alikuwa na sahifah ambamo alikusanya idadi kubwa ya Hadith za Mtume s.a.w.w. Mtoto wake pia alikuwa anayo mazoea ya kunukuu Hadith kutoka sahifah hiyo. Kwa mujibu wa riwayah za al-Bukhari, ilikuwa ni nakili ya sahifah ya Abdallah ibn Awfi ambaye alizoea kuandika Hadith ndani mwake kwa mikono yake mwenyewe.

    Samurah ibn Jundab pia alikusanya Hadith nyingi katika kitabu chake kikubwa na mtoto wake, Sulayman, aliyerithi, alizoea kunakili Hadith kutokea humo. Bila shaka yalikuwa ni maandiko haya ambayo Ibn Sirin anayasemea: "Katika risalah aliyoiacha Samurah kwa mtoto wake, humo kuna kiwango kikubwa mno cha ilimu.

    Imeripotiwa na Anas akisema huku amenyooshea mkono kwa mus-haf: "Hizi ni Hadith ambazo mimi nimezisikia kutoka kwa Mtume Mtukufu s.a.w.w. Mimi niliziandika na nilimpatia Mtume s.a.w.w. (kwa ajili ya uthibitisho wake)."

    Al-Imam Jaafer al-Sadiq a.s. anasimulia kutokea Mababu zake a.s. kwamba Mtume s.a.w.w. alisema: "Wakati unapoandika Hadith, andika pamoja na sanad yake (ufululizo wa upokezi wake). Iwapo itakuwa ni kweli, basi utagawana thawabu zake; na iwapo zitatokezea kuwa ni za uongo, basi madhambi yake yatamwia aliyesema."

    rudi nyuma Yaliyomo endelea