rudi nyuma Yaliyomo endelea

Kwa hivyo basi hadithi hii tukufu ni katika dalili za kuonyesha ulazima wa kuwepo Imamu katika kila zama, na hili ni jambo lililowazi kwa watu wenye busara.

8) Hadithuth thaqalain inaonyesha kuwa Ahlul bait (a.s) ni maasumu.

Hii hadithi tukufu inaonyesha kuwa Qurani na Ahlul bait ni maasumu kwani imemdhaminia mwenye kuvifwata (hivi viwili) kwamba hatopotea wala kuangamia, bila ya kumwekea sharti lolote. Ni wazi kuwa haingetoa dhamana hii lau kama havingekuwa maasumu.[88]

Kuna hadithi nyingi za thaqalain zilizotamka waziwazi kwa maneno haya, kwa ibara tofauti tofauti.

a) Miongoni mwazo ni,

((ايها الناس اني تارك فيكم ما إن اخذتم به لن تضلوا: كتاب الله وعترتي اهل بيتي)).

“Enyi watu hakika mimi ninaacha kati yenu ambavyo mkishikamana navyo hamtapotea kamwe, Kitabu cha Mwenyezi Mungu na kizazi changu (ambacho ni) Ahlubaiti wangu”.[89]

b) Na Miongoni mwazo ni;

((ما ان تمسكتم به لن تضلوا: كتاب الله عزوجل وعترتي اهل بيتي)).

“Ambavyo mkishikamana navyo hamtapotea kamwe, Kitabu cha Mwenyezi Mungu Mwenye Nguvu na Aliyetukuka, pamoja na kizazi changu Ahlu baiti wangu”.[90]

c) Na Miongoni mwazo ni zile zilizotamka wazi wazi,

((هذا علي مع القرآن والقرآن مع عليّ لا يفترقان حتى يردا علي الحوض)).

“Huyu Ali yuko pamoja na Qurani, nayo Qurani iko pamoja na Ali, hawatatengana hadi watakaponijia huko hodhini (mwa kauthar)”.[91]

d) Na miongoni mwazo ni dua ya Mtume Mtukufu (s.a.w.a) aliyomsomea Ali (a.s) kwa kusema”.

(الّلهم ادر الحق معه حيث كان)).

“Ewe Allah, ipitishe haki pamoja naye popote alipo”.[92]

Hizi ni pamoja na dalili nyinginezo, kama vile ayatut tathir inayoonyesha na kuthibitisha umaasum wa Ahlul bait, pamoja na hadithi mutawatir zinazoon-yesha kuwa hao ni maasumu.

e) Na Miongoni mwazo ni hadithi aliyoipokea Alhaakim kwa isnadi yake kutoka kwa Abu Dhar ya kwamba alisema:

قال رسول الله(ص) : ((انما مثل اهل بيتي فيكم مثل سفينة نوح من ركبها نجا ومن تخلف عنها غرق)).

“Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.a) amesema “Hakika mfano wa Ahlubaiti wangu kati yenu ni mfano wa jahazi ya Nuhu, aliyeipanda aliokoka na aliyebaki nyuma (bila kuipanda) alighariki.”[93]

f) Na miongoni mwazo ni aliyoipokea Attabarani kutoka kwa Abu Said, aliyesema kwamba,

قال رسول الله(ص): ((وانما مثل اهل بيتي فيكم مثل باب حطة في بني اسرائيل من دخله غفر له))

“Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.a) amesema, “kwa hakika mfano wa Ahlubaiti wangu ni mfano wa mlango wa “hittah” kwa wana wa sraeli, aliyeingia (ndani yake) alisame- hewa (madhambi yake).”[94]

Seyyid Sharafudin (r.a) amesema kwamba, “sababu hasa ya kufananishwa kwa Ahlulbait na mlango wa hitta ni kwa kuwa Mwenyezi Mungu Aliyetukuka, Aliufanya mlango huo kuwa ni dhihirisho mojawapo la unyenyekevu mbele ya utukufu wake na utiifu mbele ya hukumu yake na kwa hivyo, hii ikawa ndio sababu ya kupata maghfira (msamaha), Vile vile (Mwenyezi Mungu) Amejaalia pia utiifu wa umma huu kwa Ahlulbait wa Mtume wake (s.a.w.a) na kuwafwata Maimamu hao kukuwa ni dhihirisho mojawapo la unyenyekevu mbele yake na utiifu mbele ya hukumu. Na kwa hivyo hii ikawa ndio sababu ya kupata maghfira. Hii ndio sababu ya wao kufananishwa na mlango huo.

Hata hivyo baadhi ya maulama wa kisunni wamekiri jambo hili, miongoni mwao akiwa Razi, Ibn Hajar Alhaitami, Aljalalus suyuti, Assanad na wengineo.[95]

Ibnu Abil Hadid amemnukuu Abu Muhammad Ibnu Muttawaih kutoka kwenye kitabu cha “Alkifaya” akisema, “Hakika Ali (a.s) ni maasumu hata ingawa sio kwa isma (umaasumu) ya wajibu, na wala isma sio sharti kwa Imamu lakini dalili za kisheria (Quran na hadithi) zimethibitisha ya kwamba yeye ni maasumu na mwenye yakini, na ya kwamba hili ni jambo linalomhusu yeye pekee, wala maswahaba wengine hawakupewa. Tofauti katika maneno yetu iko wazi tunaposema “Zaid ni maasumu” na tunaposema “Zaid ni maasumu kiwajibu, kwa kuwa yeye ni Imamu na katika masharti ya Imamu ni kwamba awe ni maasu-mu”. Kauli ya kwanza inaambatana na dhehebu letu la (kisunni) na kauli ya pili inaambatana na dhehebu la Imamiya (mashia)”.[96]

Jua ya kwamba, Qurani imekuwa maasumu kwa kuwa imetoka kwa Mwenyezi Mungu Ambaye hapa-twi na kosa katika vitendo vyake na wala katika kuiteremsha Qurani, au katika kuwateremshia Mitume (a.s) wahyi wake na katika kuwafikishia watu, kwani lengo la kuwaongoza watu ni kuwafikisha kwenye maslahi yao halisi na ya hakika. Basi, ikiwa Mwenyezi Mungu atafanya kinyume cha hayo atakuwa amefanya kinyume cha hekima yake tukufu.

Vivyo hivyo umaasumu (isma) wa Maimamu ni kwa kuwa elimu yao imetokana na Mtume (s.a.w.a) na Mwenyezi Mungu na kwa hivyo elimu zao haziwezi kupatwa na makosa wala kasoro, kwani wao wame-teuliwa na Mwenyezi Mungu ili kuwaongoza watu na kuwatakasa, na kama tujuavyo makosa na upotofu hayasaidii katika kulifikia lengo hili tukufu na wala hayanasibiani na hekima ya Mwenyezi Mugu.

Kwa hivyo basi Qurani na kizazi kutukufu cha Mtume (s.a.w.a) ni maasumu, na vyote viwili vimehi-fadhiwa kutokana na makosa, na kuvifwata kunamhi-fadhi mtu katokana na kuangamia. Hii ikiwa ni fadhila ya kipekee, na iliyomakhsusi kwa hivi viwili tu.

9) Uhusiano wa kizazi kitukufu na Mwenyezi Mungu

a) Kauli yake Mtume (s.a.w.a) isemayo:

((هما حبل ممدود من السماء بينكم وبين الله عزوجل))

“Viwili hivi ni kamba iliyonyooshwa toka binguni iliyoko baina yenu na Mwenyezi Mungu Mwenye Nguvu na Aliyetukuka.”

b) Na kauli yake (s.a.w.a)

((سبب منه بيد الله وسبب بايديكم))

“Upande mmoja wake (kamba hii) uko mikononi mwa Mwenyezi Mungu na upande mwengine uko mikononi mwenu.”

c) Na kuali yake (s.a.w.a)

((انهما لن يفترقا حتى يردا علي الحوض))

Hakika hivi viwili havitatengana kamwe hadi vita-kaponijia huko hodhini (mwa kauthar)”.

d) Na kauli yake (s.a.w.a)

((ما ان تمسكتم بهما لن تضلوا))

“Mkishikamana navyo hamtapotea kamwe”

e) Na kauli yake (s.a.w.a)

((هذا علي مع القرآن والقرآن مع علي لا يفترقان)).

“Huyu Ali yuko pamoja na Qurani, nayo Qurani iko pamoja na Ali (Hivi viwili) havite-ngani.”

f) Au kauli yake (s.a.w.a)

((فلا تقدموهما فتهلكوا ولا تقصروا عنهم فتذهبوا))

((Basi msiwatangulie msije mkahiliki na wala msibaki nyuma yao msije mkaangamia”.

g) Vlie vile kule kuwafananisha na jahazi ya Nuhu (a.s.) au kuwafananisha na nyota, pamoja na kauli yake isemayo.

((انهما خليفتي رسول الله (ص) ))

“Hakika” hivi viwili ni makhalifa wa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.a).

Hizi pamoja na nyinginezo nyingi ni dalili zionye-shazo wazi ukaribu wa kizazi kitukufu mbele ya Mwenyezi Mungu, na ya kuwa walikuwa wakiongo-zwa na Mwenyezi Mungu.

Huu uhusiano nao na Mwenyezi Mungu na ukaribifu wao mbele yake ndio uliowafanya kuwa tofauti na watu wengine. Na ndio sababu twasema kuwa Uimamu wao haukuwa sawa na Ukhalifa wa makhalifa wa ndugu zetu masunni, kwa sababu ya tofauti ya kiasili iliyoko baina ya Uimamu huu na Ukhalifa huo.

Uimamu kwetu una asili moja na Utume, bali tofauti iliyoko baina yao ni wahyi uliyomakhsusi kwa Mitume. Ama Mwongozo wa Mwenyezi Mungu wa kighaibu (kwa njia isiyokuwa ya wahyi) ungali unaendelea, nao Maimamu waongofu wamechukua majukumu yote ya Mtume (s.a.w.a) aliyotwikwa na Mwenyezi Mungu.

Hii ni kinyume cha Uimamu (Ukhalifa) kwa ndugu zetu masunni. Kwani wao wanauchukulia kuwa utawala na uongozi wa dhahiri, bila ya kulazimisha umaasumu na uadilifu katika Imamu (Khalifa).

Hata hivyo hadithuth thaqalain imetuthibitishia kuwa Uimamu una maana ile ile iliyotajwa katika kizazi kitukufu cha Mtume(s.a.w.a).Basi wao Maimamu wamechukua vyeo vile vya Mtume (s.a.w.a) kama vile uongozi wa kidini na uongozi wa kisiasa, ila tu tofauti iliyoko baina yao na Mtume (s.a.w.a) ni kwamba wao wanachukua sheria za uislamu kutoka kwa Mtume (s.a.w.a) na wanamfuata yeye (s.a.w.a) katika mambo yote na wanaongozwa kwa nuru yake na ni Makhalifa wake katika umma wake. Basi wanachukua majukumu yake yote ikiwa miongoni mwayo, ni utawala wa hukuma (serikali).

Kwa hivyo basi, maana halisi ya Uimamu kwetu ina tofautiana na maana halisi ya Uimamu kwa ndugu zetu masunni. Hadithi inatusaidia pamoja na dalili za kiakili zinazo kubaliwa na wenye akili wote, kuthibitisha jambo hili, na ndio sababu mashia ithnaasharia wakatofautiana na waislamu wengineo katika kuitakidi kudumu na kuendelea kuwepo uhusiano wa kighaibu na mwongozo wa Mwenyezi Mungu kwa ajili ya kuendelea kuwepo kizazi kitoharifu cha Mtume (s.a.w.a).

Imamu wetu wa nane, Imam Ali Ridha (a.s) amasema.”

((ان العبد اذا اختاره الله عزوجل لامور عباده شرح صدره لذلك واودع قلبه ينابيع الحكمة وألهمه العلم إلهاماً فلم يعي بعده بجواب ولا يُحيّر فيه عن الصواب)).

“Mja anapoteuliwa na Mwenyezi Mungu, Mwenye Nguvu na Aliyetukuka ili kuyasimamia mambo ya waja wake, humpanulia kifua chake kwa ajili yake (kazi hii) na huweka moyoni mwake chemchemu za hekima, na humfunulia elimu sawa sawa (kwa njia ya) ilhamu (kiasi cha kuwa) hashindwi katika kutoa jawabu, na wala hapatwi na shaka na jawabu iliyo ya haki”.[97]

10) Wajibu wa kuwafuata Ahlulbait ni sawa na wajibu wa kukifuato Kitabu cha Mwenyezi Mungu

Lililo la wajibu ni kuwafuata Ahlulbait kama ilivyowajibu kukifuata Kitabu Kitukufu (Quran). Hili ndilo linalo kusudiwa na hadithuth thaqalain. Basi haitoshi kuwaheshimu tu na kudhihirisha mapenzi na mahaba bila ya kuwafwata. Dalili ya haya tusemayo, ni kule kufanywa Ahlul bait kuwa kizito cha pili pamoja na Quran, pamoja na kauli yake Mtume (s.a.w.a).

((فلا تقدموهما ولا تقصروا عنهما)).

“Basi msiwatangulie na wala msibaki nyuma yao” na kauli yake,

((ما ان تمسكتم بهما لن تضلوا))

“Mkishikama navyo hamtapotea”.

Na ni wazi kuwa kushikamana na kizazi ni kutenda kufuatana na kauli zao na maagizo na makatazo yao na kuufuata mwenenda wao Mtukufu.

Hii ndio sababu tunamuona Taftazani ananukuliwa akisema baada ya kuitaja hadithi hii, “Je huoni kuwa (Mtume(s.a.w.a)) aliwataja pamoja na Kitabu cha Mwenyezi Mungu Aliyetukuka (kwa kusema) kuwa kushikamana navyo viwili kunamuokoa mtu kutokana na kupotoka. Kushikamana na kitabu hakumaanishi ila tu kuchukua katika elimu na mwongozo wake na (hiyo ndiyo maana ya kushikamana na) kizazi vile vile!![98]

Imepokewa kuwa Ibnu Hajar amesema kuwa, Mtume (s.a.w.a) aliwahimiza watu kuwafuata, kushi-kamana nao na kuchukua elimu kutoka kwao.[99]

Na hii inamaana kuwa maamrisho na makatazo yatokanayo na kizazi kitukufu ni lazima yafuatwe kama ilivyo wajibu kuyafuata maamrisho na makatazo ya Qurani tukufu.

Ikidaiwa kuwa maamrisho na makatazo yao ni hayo hayo maamrisho na makatazo ya Qurani tukufu, sisi tutajibu kwa kusema, maamrisho na makatazo yao ni mapana zaidi, kwani huenda wakati mwengine yakatoka kwa unwani kuwa wao ni Mawalii(viongozi) juu ya mambo yote ya umma, nayo nikufuatana na hadithi iliyotuamrisha sisi kufuata maamrisho yao na kuacha makatazo yao bila ya kupunguza wala kuongeza chochote, na hiyo ndiyo maana ya “wilaya mutlaqa” yaani uongozi usio kuwa na mipaka.

Mwandishi wa Abaqatul Anwar amefaidisha na kufanya wema aliposema: “Hakika hadithi (hii) inamaaniisha kuwa ni wajibu kuwafuata Ahlul bait katika maneno yao, vitendo, hukumu na itikadi zote. Na ni dhahiri kuwa cheo hiki na cha namna hii hakiwezi kupatikana ila tu kwa yule ambaye amefikia daraja ya Uimamu na Uongozi mkuu (wa cheo cha juu kabisa) baada ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.a).[100]

Naye Seyyid Sharafu Din amesema “Zimepokewa hadithi nyingi zilizo mutawatiri na sahihi zinazoonye-sha na kuelezea wajibu wa kukifuata kizazi cha Mtume (s.a.w.a) .

Na hasa hadithi zilizopokelewa kwa njia za upokezi za kizazi kitoharifu, (yaani kwanye vitabi vya hadithi vya kishia).[101]

Kwa hivyo basi kuifasiri hadithi hiyo eti kuwa inauusia umma kukipenda na kukiheshimu kizazi hicho kitoharifu na wala sio (kwamba kuna uwajibu wa) kuwafuata, kunapingana na yaliyomo kwenye hadithi hiyo kama vile kukitaja kwenye hukumu moja na Quran na kukiweka sawa nayo na kuwazuia watu kukitangulia au kubaki nyuma ya kizazi hicho, kuam-risha kushikamana nacho, na kuchukua kutokana nacho hakumpi mtu nafasi ya kuifasiri hadithi hii kama walivyoifasiri. Hii nipamoja na dalili nyingi-nezo, zinazomzuia mtu kuifasiri vivyo.

Kwa hivyo basi sababu hasa ya kusema kuwa Quran na kizazi kitoharifu, vimejaaliwa kuwa Maima-mu katika kuwaongoza watu imefahamika. Hili ni jambo lililowazi katika hadithuth thaqalain, kama alivyosema Imam Ja’afar Swadiq (a.s.),

((وقد امر رسول الله (ص) ان يقتدى بالقرآن وآل محمد وذلك حيث قال في آخر خطبة: اني تارك فيكم الثقلين الثقل الاكبر والثقل الاصغر اما الاكبر فكتاب ربي واما الاصغر فعترتي اهل بيتي فاحفظوني فيهما فلن تضلوا ما ان تمسكتم بمهما)).

“Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.a) alishaamuru kuwa ifuatwe Qurani (pamoja) na Aali Muhammad (kizazi chake) pale aliposema katika hotuba yake ya mwisho (kabla ya kufarikiana na dunia)” Hakika mimi ninaacha kati yenu viwili vizito, kizito kikubwa na kizito kidogo. Ama kikubwa ni Kitabu cha Mola wangu na ama kidogo ni kizazi changu (ambacho ni) Ahlubaiti wangu. Basi nihifadhini katika (kuviangalia) vitu hivyo viwili, kwani hamtapotea kamwe mtakapo-kuwa mmeshikamana navyo.”

11) Kutopingana kwa hadithuth thaqalain na ile iliyopokewa katika Majmauz Zawaid

Jua ya kwamba hadithi iliyopokelewa kwenye kitaba cha Majmauz Zawaid kutoka kwa Abu Huraira ya kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.a) alisema;

اني خلفت فيكم اثنين لن تضلوا بعدهما ابداًً: كتاب الله ونسبي ولن يفترقا حتى يردا علي الحوض)).

“Hakika mimi ninaacha kati yenu vitu viwili, (ambavyo) baada yavyo hamtapotea kamwe, Kitabu cha Mwenyezi Mungu na nasaba yangu. Na havita-tengana kamwe hadi vitakaponijia Kwenye hodhi (ya kauthar)”. Hadithi hiyo haipingani kamwe na hadithi zilizomutawatir (nyingi) zinazoonyesha kuwa Mtume (s.a.w.a) aliacha Kitabu na kizazi, kwani umekw-ishajua Kuwa kizazi (Al-itra) ni Jamaa wa karibu wa Mtume, kwa hivyo basi kutumia neno nasaba (katika hadithi ya Abu Huraira) kunachukuliwa kuwa kusudio lake ni wale wa karibu. Na kusudio hili la wale jamaa wa karibu linajulikana kuto kana na kanuni iitwayo “Munasabatul hukmi wal maudhu”, (Mnasaba wa hukumu na maudhui – yaani, kuangalia hukumu imetolewa kwa mnasaba gani ili kufahamu maudhui ya hukumu na hukumu yenyewa) kusudio lake sio kuwafuata jamaa wote wa karibu ambako kutamfanya mtu aongoke, bali kusudio lake ni jamaa maalum ambao ni maasum, kama zionyeshavyo hadithi nyingi ambazo tulizoashiria na kuzitaja baadhi yake hapo awali.

Vile vile baadhi ya hadithi zinazosisitiza kushi-kamana na Kitabu cha Mwenyezi Mungu na Sunna za Mtume (s.a.w.a) hazipingani na hadithi mutawatir zinazosisitiza juu ya kushikamana na Kitabu na kizazi, kwani sunna ya hakika na iliyosahihi haipatikani ila tu kutokana na kizazi kiongofu. Kwa hivyo, hakuna mgongano wala mpingano kati ya hadithi hizo ikiwa hadithi hii itakuwa imethibiti kuwa imetoka kwa Mtume (s.a.w.a) Ama hadithi iliyopokelewa kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.a) ya kwamba alisema,

((مهما اوتيتم من كتاب الله فالعمل به لا عذر لاحد في تركه فان لم يكن في كتاب الله فبسنة مني ماضية فان لم يكن مني سنة ماضية فما قال اصحابي إن اصحابي بمنزلة النجوم في السماء فايهما اخذتم به اهتديتم)).

“Kwa kiasi chochote kile mlichopewa (kili choko) katika Kitabu cha Mwenyezi Mungu basi yeyote yule hana udhuru wa kutokitenda. Na ikiwa hakipo ndani ya Kitabu cha Mwenyezi Mungu. basi (kitapatikana) katika Sunna yangu na ikiwa hakikupatikana katika Sunna yangu basi(kitapatikana) katika yale wasemayo maswahaba wangu. Hakika maswahaba wangu ni mfano wa nyota zilizo binguni, yeyote (kati yao) mtakayemfuata, mtaongoka.”[102] Hiyo hadithi haikuba-liki kwa sababa nyingi. Nazo ni kama zifuatazo:

Kwanza Maulamaa wakubwa wa kisunni wameta-mka wazi wazi kuwa hadithi hii ni dhaifu. Mwandishi wa kitabu cha “Abaqatul Anwar” amewataja baadhi yao katika utangulizi wa kitabu chake. Miongoni mwao (aliowataja) wakiwemo Ahmad Ibnu Hambal, Albazzaz, Addaru Qutni Ibnu Hazm, Albaihaqi, -hata ingawa yeye mwenyewa anainakili hadithi hiina Ibnu Asakir, Ibnul Jauzi, Ibnu Duhya, Abu Hayyan, Adh-dhahabi, Ibnul Haitham, Ibnu Hajar Al-asqalani na wengineo katika wale waliosema waziwazi kuwa hadithi hio sio sahihi au kuwa ni dhaifu au kuwa Mtume (s.a.w.a) alizuliwa (hadithi hii).[103]

Kwa hivyo basi hadithi hii dhaifu haina nguvu na uwezo wa kuipinga hadithuth thaqalain iliyomutawatir na isiyo kuwa na shaka ndani yake kuwa imetoka kwa Mtume Mtukufu (s.a.w.a).

Pili:

Pamoja na kuwa hadithi hiyo ni dhaifu pia inapingana na ijmai (makubaliano na maafikiano ya maulama wote) na akili pia, kama anavyosema Allama Mir Husein “Hakika hadithun nujum (hadithi ya nyota) inaonyesha kuwa maswahaba wote wa Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.a) walikuwa wema, ambapo, kufuatana na ijmai sivyo hivyo kamwe. Vile vile inaonyesha kuwa wote ni wenye kuungoza umma (katika njia iliyonyooka) ambapo sivyo pia, kwani kikundi kikubwa kati yao kiliwapoteza watu wengi. Vile vile inaonyesha kuwa maswahaba wote wanastahiki kufuatwa na umma na hilo pia ni jambo lisiloweza kuwa sahihi kamwe kwani wengi wao walikuwa ni watu wenye kasoro ambazo ziliwafanya wasistahiki hilo”.

Hadi kufikia kusema, “Zimeteremka aya katika Kitabu cha Mweneyezi Mungu Mwenye Nguvu na Aliyetukuka, zinazoelezea wazi wazi hali za kikundi kikubwa cha maswahaba, na hasa aya zilizoko katika sura ya Anfal Bara-ah, Ahzabi Jum-ah na ya Munafi-quun. Basi je Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.a) anaweza akawateuwa maswahaba wote wake kuwa viongozi wa umma na hali kama hii?”.

Mpaka kufikia kasema, “zimepokewa hadithi nyingi kutoka kwa Mtume (s.a.w.a) zenye kuwalaumu na kuwashusha daraja baadhi ya maswahaba, utakazozi-pata kwenye Sihahu na Masanid[104] zenye kutegemewa. Miongoni mwazo ni “hadithul haudh.” (Hadithi ya hodhi) “hadithul irtidad” (hadithi ya kuritadi kwa maswahab) na hadithi isemayo “msirudi baada yangu makafiri”, hadithi isemayo kuwa “ushirikina ndani yenu umejificha zaidi ya kutambaa kwa sisimizi”, hadithi isemayo “sijui mtakayoyafanya baada yangu”, hadithi isemayo, “mtaufuata mwenendo wa mayahudi na manaswara”, na “hadithut tanaafus” (Hadithi ya kushindana), hadithi isemayo, “katika maswahaba kuna ambaye hatoniona (huko peponi) nami pia sito-mwona”, hadithi isemayo “katika maswahaba wangu kuna wanafiki”, hadithi isemayo, “wenye kunizulia uwongo wamezidi”, na nyingi nyinginezo ambazo zinawalaumu baadhi ya maswahaba. “Na zipo hadithi katika vitabu vya ndugu zetu masunni zinazoonyesha waziwazi kuwa Mtume (s.a.w.a) alikataza na kuzuia kufuatwa maswahaba kama hao. Katika baadhi yazo, ame sema.

((ان من اقتداهم في النار))

“Hakika mwenye kuwafwata hao ataingia motoni.”

Hadi kufikia kusema.

((وقال الحنفي: تكون بين اصحابي فتنة يغفر الله لهم لسابقتهم ان اقتدى بهم قوم من بعدهم كبهم الله تعالى الى نار جهنم.))

“Naye Alhanafi amesema (amepokea), “kutatokea fitna baina ya maswahaba wangu, Mwenyezi Mungu atawasamehe kwa yale waliyo yatanguliza. Watu watakao kuja baada yao wakiwafuata Mwenyezi Mungu awatumbukize katika moto wa Jahanam.”[105]

Tatu: lau kama tutakubali kuwa hadithi hii ni sahihi, lakini tunapata kuwa haipingani na hadithuth thaqalain kwani inaingia na kuambatana na yale yote yaliyo tajwa kwenye hadithi ya thaqalain, kwa kuwa imewaamuru (waislamu) kutenda, kufuatana na Kitabu cha Mwenyezi Mungu na kusema kuwa mwenye kupuuza kutenda hayo hana udhuru (wa kutoa). Kisha ikiwa ufafanuzi kuhusu kitu haupatikani katika Kitabu cha Mwenyezi Mungu, basi (hadithi), imeamuru kuwa ifuatwe sunna ya Mtume (s.a.w.a.). Na ikiwa sunna haipatikani (hadithi) ikaturejesha kwa maswahaba. Na ni wazi kuwa sunna sahihi na ya hakika wako nayo Ahlul bait wa Mtume (s.a.w.a) na kuwafuata hao ni wajibu wa daraja ya mbele. Basi Ahlul bait wanapo-kuwepo hakuna nafasi ya kuwafuata maswahaba.

Nne: Hakuna awezaye kukanusha tofauti iliyo-kuwepo baina ya maswahaba katika kuzinukuu huku-mu za Mwenyezi Mungu na mambo mengineyo kuto-kana na kutojua kwa wengi wao. Hata wao wenyewe walikiri kuwa hawakuwa na elimu. Hivyo basi itawezekanaje kwa Mtume(s.a.w.a) kuwafanya kuwa marejeo ya umma katika maongozo ya kidini pamoja na kuthibiti ujahili wao na kuhitilafiana baina yao.

Haya, tukiongeza pia vitendo vya haramu walivyo-tenda baadhi yao, kama vile kuuza pombe, kuchukua riba katika biashara, na vinginevyo, vilivyotajwa katika Kitabu cha “Abaqatul Anwar”.[106] Audhubillah!! kutokana na kumnasibishia Mtume wa Mwenyezi Mungu(s.a.w.a) mambo kama hayo, (Mtume) aliye-teuliwa na Mwenyezi Mungu ili kuwaongoza watu.

Mtume(s.a.w.a) ametukuka na ametakasika kutokana na kunasibishiwa mambo kama hayo. Hii ni kufuatana na hukumu ya akili na hadithi zilizomutawatir, ikiwa miongoni mwazo ni hadithuth thaqalain, ambayo kama ujuavyo, iliubainishia umma njia iliyonyooka isiyo kuwa na upotofu. Basi mwenye kuipuuza hiyo njia kwa madai hayo, kwa hakika atakuwa ameiacha njia iliyonyooka na kujiingiza kwenye upotofu, husuda, chuki na ushindani, hayo yote ni miongo ni mwa mambo ambayo yaliyokatazwa na Mwenyezi Mungu na Mtume wake (s.a.w.a), naye akatilia mkazo kwa kusema,

rudi nyuma Yaliyomo endelea