rudi nyuma Yaliyomo endelea

“Amirul muminin Ali (a.s) aliulizwa maana ya kauli yake Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.a) (aliyosema) “Hakika mimi ninaacha kati yenu vizito viwili, Kitabu cha Mwenyezi Mungu na (itrah) kizazi changu”. Ni nani itrah (kizazi)? Akasema “Ni mimi, Hasan, Husein na Maimamu tisa, wa tisa kati yao ndiye Mahdi na Qaim, (kamwe) hawa tengani na Kitabu cha Mwenyezi Mungu, nacho hakitengani nao, hadi watakapomjia Mtume wa Mwenyezi Mungu kwenye hodhi yake (ya kauthar)”.[72]

Kwa hivyo ni wazi kuwa “itrah” (kizazi) ni Ahlul bait, nao ni Maimamu watoharifu na maasumin [73] watukufu (a.s).

6) Quran na Ahulbait ndio kamba ya Mwenyezi Mungu

Qurani ni kamba ya Mwenyezi Mungu kama Asemavyo Mwenyezi Mungu;

(واعتصموا بحبل الله جميعاً ولا تفرقوا)

“Na shikamaneni kwa kamba ya Mwenyezi Mungu nyote, wala msitengane”.

Kuna riwaya nying zinazoshuhudia jambo hili. Miongoni mwazo, ni riwaya aliyoipokea Abu Said Alkhidri kutoka kwa Mtume (s.a.w.a) ya kwamba alisema,

((اني اوشك ان ادعى فاجيب واني تارك فيكم الثقلين: كتاب الله وعترتي كتاب الله حبل ممدود من السماء الى الارض وعترتي اهل بيتي وان اللطيف الخبير اخبرني انهما لن يفترقا حتى يردا علي الحوض فانظروا كيف تخلّفوني فيهما)).

“Huenda nikaitwa na (Mola wangu) nami nikajibu, nami ninaacha kati yenu vizito viwili, Kitabu cha Mwenyezi Mungu na kizazi changu. Kitabu cha Mwenyezi Mungu ni kamba iliyonyooshwa kutoka mbinguni hadi ardhini nacho Kizazi changu ni Ahlubait wangu (watu wa karibu wa nyumbani kwangu). Naye Mwingi wa huruma Aliyemjuzi wa yote amenijulisha kwamba havitotengana kamwe mpaka vitakaponijia kwenye hodhi (ya kauthar). Basi angalieni mtakavyo-vitendea baada yangu”.[74]

Vile vile kamba ya Mwenyezi Mungu inawaku-sanya Ahlulbait (a.s), kwa kuwa wamefanywa kuwa sawa na Quran katika hadithuth thaqalain, na kwa kuwa wameteuliwa na Mwenyezi Mungu kuwaongoza watu. Basi kushikamana nao ni sawa na kushikamana na kamba ya Mwenyezi Mungu ambayo inatuzuia na kupotoka na kuangamia.

Katika Tafsiru Alaur Rahman’ baada ya kuitaja aya hii,

((واعتصموا بحبل الله جميعاً…))

“Na shikamaneni kwa kamba ya Mwenyezi Mungu nyote…”

Mwandishi amesema, “yaani jizuieni kutokana na kuanguka, kwa kushikamana na kamba ya Mwenyezi Mungu mkiwa katika hali ya umoja, na (pia) kwa kushikamana na) kile ambacho amekijaalia kuwa ni chenye kuwahifadhi (na kuwazuia) kutokana na kuanguka kwenye upotofu. Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.a) ameshatu julisha kuwa ni nani wanaoitwa kamba, ambayo mwenye kushikamana nayo hapotei, katika kauli yake kwenye hadithuth thaqalain isemeyo:

((ما ان تمسكتم بهما لن تضلوا كتاب الله وعترتبي اهل بيتي))

“Ambavyo mkishi kamana navyo hamtapotea kam-we, (navyo ni) Kitaba cha Mwenyezi Mungu na kizazi changu (ambao ni) Ahlubait wangu”. Neno kamba limetumika katika (maana) kuonyesha kuwa kutoshi-kamana nayo kutamfanya mtu kuanguka kwenye upotofu mkubwa na kuangamia.”[75]

Dalili nyingine inayo tuthibitishia kuwa neno kamba halikutumiwa makhsusi kwa Qurani, bali lime-wakusanya pia Ahlul bait, ni kuwa, Mtume(s.a.w.a) amekusanywa kwenye maana hii katika aya

]وكيف تكفرون وانتم تتلى عليكم آياته وفيكم رسوله ومن يعتصم بالله فقد هدى الى صراط مستقيم[

“Na mnakanushaje, hali nyinyi mnasomewa Aya za Mwenyezi Mungu, na Mtume wake yuko pamoja na nyiye? Na mwenye kumshika Mwenyezi Mungu sawa sawa basi yeye amekwishaongozwa katika njia iliyonyooka”

Katika aya hizi ni dhahiri kuwa kushikamana na aya za Mwenyezi Mungu na kumfwata Mtume (s.a.w.a) ni sawa na kushikamana na kamba ya Mwe-nyezi Mungu, kama alivyosema Mwenyezi Mungu katika aya iliyotangulia, kwamba kushikamana navyo ni kushikama na Mwenyezi Mungu, kwa hivyo basi kama vile Mtume (s.a.w.a) ni mfano wa kamba ya Mwenyezi Mungu, vile vile kizazi chake kitukufu chenye kuchukua cheo chake (baada yake) ni mfano wa kamba ya Mwenyezi Mungu.

Haya pamoja na kuongezea riwaya nyingi zilizoe-lezea wazi wazi jambo hili. Miongoni mwazo ni riwaya iliyopokewa kwenye Abaqatul Anwar kutoka kwa Sheikh Suleiman Al-hanafi Alqanduzi katika tafsiri ya aya “Na shikamaneni kwa kamba ya Mwenyezi Mungu nyote…” alisema kuwa “Ath-tha’alabi amepokea kwa sanadi yake (silsila ya wapokezi) kutoka kwa Aban Ibnu Taghlib kutoka kwa Ja’afar Swadiq (R.a.) ya kwamba alisema.

((نحن حبل الله الذي قال الله عزوجل: واعتصموا بحبل الله جميعاً ولا تفرقوا)).

“Sisi ndio kamba ya Mwenyezi Mungu ambayo Mwenyezi Mungu Mwenye Nguvu na Aliyetukuka Amesema. “Na shikamaneni kwa kamba ya Mwenyezi Mungu nyote na wala msiachane”.

Vile vile mwandishi wa Kitabul Manaqib ame-pokea kutoka kwa Said Ibnu Jubair (R.a) kutoka kwa Ibnul Abbas (r.a) ya kwamba alisema:

((كنا عند النبي صلى الله عليه وسلم اذ جاء اعرابي فقال يا رسول الله سمعتك تقول: واعتصموا بحبل الله فما حبل الله الذي نعتصم به؟ فضرب النبي صلى الله عليه وآله وسلم يده في يد عليّ وقال: ((تمسّكوا بهذا هو حبل الله المتين)).

“Tulikuwa pamoja na Mtume (s.a.w.a) alipokuja bedui mmoja wa kiarabu na kumwambia “Ya Rasulallah, nilikusikia ukisema “Na shikamaneni na kamba ya Mwenyezi Mungu”. Basi ni ipi kamba ya Mwenyezi Mungu ambayo tutashikamana nayo? Mtume (s.a.w.a) akaupigisha mkono wake kwenye mkono wa Ali na kusema “Shikamaneni na huyu, yeye adiye kamba ya Mwenyezi Mungu iliyoimara”.[76]

Na miongoni mwazo ni hadithi aliyoipokea Annumani kwa isnadi yake kutoka kwa Hariiz Ibnu Abdillah kutoka kwa Abu Abdillah Ja’afar Swadiq Ibnu Muhammad (a.s) kutoka kwa baba yake kutoka kwa babu zake (a.s) kutoka kwa Ali (a.s) ya kwamba alisema,

((خطب رسول الله في مسجد الخيف – وهي خطبة مشهورة في حجة الوداع – قال فيها: … الا واني مخلف فيكم الثقلين: الثقل الاكبر والثقل الاصغر: الثقل الاكبر القرآن والثقل الاصغر عترتي اهل بيتي هما حبل ممدود بينكم وبين الله جل وعز ان تمسكتم به لن تضلوا سبب منه بيد الله وسبب بايديكم)).

“Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.a) aliho tubia kwenye msikito wa Alkhiif – (Nayo ni hotuba mashu-huri katika hijjatul wida’a (hijja yake ya mwisho) – na kusema” …. Tambueni kuwa mimi ninaacha kati yenu vizito viwili, kizito kikubwa na kizito kidogo. Kizito kikibwa ni Quran, na kizito kidogo ni kizazi changu (ambao ni) Ahlubaiti wangu. Navyo (viwili hivi) ni kamba iliyonyooshwa baina yenu na baina ya Mwenyezi Mungu Aliyetukuka na Mwenye Nguvu. Mkishikamana nayo hamtapotea kamwe. Sehemu moja yake iko mikononi mwa Mwenyezi Mungu na sehemu (nyingine) iko mikononi mwenu”.[77]

Na miongono mwazo ni hadithi aliyoitaja Ibnu Abil Hadid, ya kwamba Mtume (s.a.w.a) alisema,

((خلّفت فيكم الثقلين كتاب الله وعترتي اهل بيتي حبلان ممدودان من السماء الى الارض لا يفترقان حتى يردا علي الحوض)).

“Nemeacha kati yenu viwili vizito (kama) makhalifa (wawili) Kitabu cha Mwenyezi Mungu na kizazi changu (amboa ni) Ahlubait wangu, (hivi viwili) ni kamba mbili zilizonyooshwa toka binguni hadi ardhini, (na) havitatengana mpaka vitakapanijia huko hodhini (mwa kauthar). [78]

Kwa hivyo basi, la wajibu kufanya katika kuleta umoja na kuondosha utengano na ufarikiano, ni kushikamana na vizito viwili na kuzuia utengano kabisa, kwani hivi ndivyo vinavyoleta umoja, kama ilivyo kuwa katika zama za Mtume (s.a.w.a) umoja ulipatikana kwa kushikamana na Mtume wake (s.a.w.a). Yatupasa basi, sisi waislamu, kuamka kutoka usingizini na kushikamana na sababu muhimu na ya asili ya umoja wetu. Ndipo tutakuwa tumepata umoja wa kweli tulioamrishwa kuwa nao katika aya tukufu, na umoja huu utakuwa umeondoa umoja wa juu juu, hata ingawa ni umoja unaofaa, unaostahiki kuwepo.

Kisha kuiita Qurani na kizazi kwa jina la kamba ya Mwenyezi Mungu kunaonyesha wazi uhusiano mkubwa vilivyonao na Mwenyezi Mungu, kwa hivyo mwenye kushikamana navyo atakuwa kwa hakika ameshikamana na Mwenyezi Mungu. Na kunaonyesha pia kuwa kushikamana na kamba ya Mwenyezi Mungu ndio njia ya pekee ya kujihifadhi kutokana na upotovu.

7) Kutotengana kwa Qurani na kizazi kitukufu milele:

Qurani na kizazi kitukufu cha Mtume Muhammad (a.s) ni vyenye kuandamana daima kama mapacha wawili na havitotengana kamwe na vitadumu kuwepo. Hadithi nyingi za thaqalain (vizito viwili) zimesema wazi wazi jambo hili. Kwa mfano kauli yake Mtume (s.a.w.a) isemayo,

((الا وانهما لن يفترقا حتى يردا علي الحوض))

“Tambueni kuwa viwili hivi havitatengana kamwe hadi vitakaponijia huko hodhini (mwa kauthar)” Na mfano wa kauli yake nyingine,

((وان اللطيف الخبير اخبرني انهما لن يفترقا))

“Na hakika Mjuzi wa yaliyofichika na yaliyodhahiri Amenijulisha ya kwamba havitatengana kamwe”.

Hizi zilikuwa habari za ghaibu na bishara kuhusu kubaki kwa Qurani na kizazi kitukufu hadi siku ya kiyama. Bishara ya kuonyesha kuwa Qurani tukufu na kizazi, vitadumu kuwepo na hakuna wakati ambao havitakuwepo. Kama vile Qurani ni muujiza wa milele, vile vile kizazi cha Mtume (s.a.w.a) ni muujiza wa milele na kamwe hakitakosekana ardhini (hiki kizazi).

Kuna hadithi nyingi pia zilizotamka waziwazi jambo hili, mfano wake ni ile iliyopokewa na Sheikh Suleiman Alhanafi Alqanduzi kwa isnadi yake kutoka kwa Imam Hasan (a.s) ya kwamba alisema,

((خطب جدي(ص) يوماً فقال بعد ما حمد الله واثنى عليه: معاشر الناس اني ادعى فاجيب واني تارك فيكم الثقلين كتاب الله وعترتي اهل بيتي ان تمسكتم بهما لن تضلوا وانهما لن يتفرقا حتى يردا علي الحوض فتعلّموا منهم ولا تعلموهم فانهم اعلم منكم ولا تخلو الارض منهم ولو خلت لانساخت باهلها)).

“Siku moja babu yangu (Mtume) (sawa) alihotubia. Baada ya kumhimidi Mwenyezi Mungu na kumsifu, alisema” Enyi watu, hakika mimi nitaitwa (na Mola wangu) nami nitajibu, nami ninaacha kati yenu viwili vizito, Kitabu cha Mwenyezi Mungu na kizazi changu (ambao ni) Ahlubaiti wangu, mkishikamana navyo hamtapotea kamwe. Navyo havitatengana kamwe hadi vitakaponijia kwenye hodhi (ya kauthar). Basi jifun-disheni kutoka kwao na wala msiwafundishe kwani wao ni wajuzi zaidi yenu, na kamwe ardhi haitobaki bila wao. Lau kama itabaki bila wao, basi itaangamia pamoja na watu wake”.[79]

Hili ni jambo linalokubaliana na akili, kwani ardhi kubaki bila Hujja wa Mwenyezi Mungu (ambaye ni Mtume (s.a.w.a) au Imamu) ni kinyume cha hekima ya Mwenyezi Mungu, hekima ya kutaka kutimiza hoja (yaani itmamul hujja) zake, (kwani Mwenyezi Mungu hawezi kuwaadhibu viumbe vyake kabla ya kuwatumia mwongozo kamili na kuwaonyesha jinsi ya kutekeleza kufwatana na mwongozo huo. wakiwa Mitume na Maimamu ndio waalimu na wafafanuzi wa mwongozo huu, ambapo watu wakiwa watakosa kuufwata watakuwa hawana hoja na dalili ya kujitetea mbele ya Mwenyezi Mungu kwani ameshatimiza na kukamilisha hoja zake kwa kuwapa mwongozo). Kuna hadithi nyingi zinazo elezea jambo hili. Miongoni mwazo ni hadithi zisemazo kuwa:

a) Ahlul bait ni amani kwa watu wa ardhini

Katika kitabu kiitwacho “Fadhailu Ali Ibni Abi Talib” cha Ahmad Ibnu Hambal amepokea kwa isnadi yake kutoka kwa Ali (a.s) ya kwamba alisema,

((قال رسول الله ((النجوم امان لاهل السماء اذا ذهبت النجوم ذهب اهل السماء واهل بيتي امان لاهل الارض فاذا ذهب اهل بيتي ذهب اهل الأرض)).

“Mtume wa Mwenyezi Mungu amesema, “Nyota ni amani kwa watu wa mbinguni, zitakapoondoka nyota (basi) watu wa mbinguni wataondoka (na kuangamia). Nao Ahlu baiti wangu ni amani kwa watu wa ardhini, watakapoondoka Ahlu baiti wangu (basi) watu wa ardhini wataondoka (na kuangamia)”.[80]

Na katika “Aamal” cha Sheikh Attusi kwa Isnadi yake kutoka kwa Ibnu Abbas, ya kwamba alisema,

((قال رسول الله(ص): ((النجوم امان لاهل السماء واهل بيتي امان لامتي فاذا ذهب النجوم ذهب اهل السماء واذا ذهب اهل بيتي ذهب اهل الارض)).

“Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.a) amesema, “Nyota ni amani kwa watu wa mbinguni, na Ahlubaiti wangu ni amani kwa umma wangu, zitakapoondoka nyota, (basi) watu wa mbinguni wataondoka na wata-kapoondoka Ahlubaiti wangu (basi) watu wa ardhini wataondoka (na kuangamia)”.

b) Ukhalifa wa Makhalifa wa Mtume (s.a.w.a) na Mahujja wa Mwenyezi Mungu utaendelea hadi siku ya kiama

Alhamwani amepokea kwa isnadi yake kutoka kwa Abdullah Ibnul Abbas ya kwamba alisema:

((قال رسول الله: ان خلفائي واوصيائي وحجج الله على الخلق بعدي لاثنا عشر اولهم اخي وآخرهم ولدي. قيل يا رسول الله ومن اخوك؟ قال: علي بن ابي طالب. قيل: فمن ولدك؟ قال: المهدي الذي يملأ الارض قسطاً وعدلاً كما مُلئت جوراً وظلماً والذي بعثني بالحق بشيراً لو لم يبق من الدنيا الا يوم واحد لطوّل الله ذلك اليوم حتى يخرج فيه ولدي المهدي فينزل روح الله عيسى بن مريم فيصلي خلفه وتشرق الارض بنور ربها ويبلغ سلطانه المشرق والمغرب)).

“Kwa hakika Makhalifa wangu na Mawasii wangu na Mahujja wa Mwenyezi Mungu kwa viumbe baada yangu (watakuwa) kumi na wawili wa mwanzo wao ni ndugu yangu na wa mwisho wao ni mwanangu”. Akaulizwa “Ya Rasulallah, na ni nani ndugu yako?” Akasema, “Ali Ibnu Abi Talib” akaulizwa, “Na ninani mwanao?” Akajibu, “Almahdi ambaye ataijaza ardhi kwa usawa na uadilifu baada ya kujazwa kwa ujeuri na dhulma. Naapa kwa yule Aliyeniteuwa kwa haki kuwa mbashiri, lau kama ardhi itakuwa haijabakisha ila siku moja, Mwenyezi Mungu Atairefusha hiyo siku ili Amdhihirishe mwanangu Almahdi. Basi (siku hiyo) Atamshusha Isa Ibnu Maryam (kutoka mbinguni) naye ataswali nyuma yake (Almahdi) na hapo ardhi itanawiri kwa nuru ya Mola wake, na utawala wake (Almahdi) utafika mashariki na magharibi.”[81]

Almuwaffaq Ibnu Ahmad (mmoja katika maulama wakubwa wa kisunni) amenukuu hadithi kutoka kwa Salman Almuhammadi[82] ya kwamba alisema”.

دخلت على النبي(ص) واذا الحسين على فخذه وهو يقبل عينيه ويلثم فاه وهو يقول: ((أنت سيد بن سيد واخو سيد وابو السادة انت امام بن امام اخو امام وابو الائمة، انت حجة بن حجة اخو حجة ابو حجج تسعة من صلبك تاسعهم قائمهم)).

“Nilimtembelea Mtume (s.a.w.a) nikampata Husein akiwa (ameketi) mapajani mwake, huku (Mume) (s.a.w.a) anayabusu macho yake na mdomo wake na kumwambia, “wewe ni bwana, mwana wa bwana (seyyid), ndugu wa bwana, na baba wa mabwana. Wewe ni Imamu, mwana wa Imamu, ndugu wa Imamu, na baba wa Maimamu. Wewe ni Hujja mwana wa Hujja ndugu wa Hujja baba ya mahujjah tisa watokanao na kizazi chako, wa tisa wao akiwa ndiye Alqain (Almahdi).”[83]

Muslim katika kitabu chake “Sahihu Muslim” amepokea kwa isnadi yake kutoka kwa Jabir Ibnu Samura ya kwamba alisema”.

سمعت النبي(ص) يقول: ((لا يزال امر الناس ماضياً ما وليهم اثنا عشر رجلاً)) ثم تكلم النبي (ص) بكلمة خفيت علي فسألت ابي: ماذا قال رسول الله (ص) فقال: قال: ((كلهم من قريش)).

“Nilimsikia Mtume (s.a.w.a) akisema, “Mambo ya watu yataendelea kutangamana madamu watu kumi na wawili wanawatawala”, kisha Mtume wa Mwenyezi Mungu alitamka neno ambalo sikulipata, basi nilimu-uliza baba yangu “Je, Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.a) amesema nini?” akasema “Amesema, “wote watatokana na Qureish”.[84]

Alhamwini amepokea kwa isnadi yake kutoka kwa Nafii ya kwamba alisema”,

سمعت رسول الله(ص) يقول: ((لا يزال الدين قائماً حتى تقوم الساعة ويكون عليكم اثنا عشر خليفة كلهم من قريش)).

“Nilimsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.a) akisema “Dini itaendelea kuwepo hadi siku ya kiama, na wataendelea kuwatawala Makhalifa kumi na wawili wote wanaotokana na Qureish.”[85]

Pamoja na riwaya nyingi nyinginezo.

Na hii ndiyo sababu tunamuona Samhudi ananakiliwa kwenye kitabu cha “Jawahirul Aqdain” kutoka kwenye kitabu cha “Tanbihatuth thaqalain” akisema kuwa “Hii inaonyesha kuwepo kwa watu wanaostahiki kushikamanwa nao, miongoni mwa Ahlul bait na kizazi kitoharifu, katika kila zama wanapokuwepo hadi siku ya kiyama. Na ndio sababu hadithi zikasisitiza katila kushikamana nao, kama zilivyosisitiza kuhusu Quran tukufu. Na hiyo ndiyo sababu, kama tutakavyoelezea baadaye, wakawa ni amani kwa watu wa ardhini, ambapo wa kiondoka nayo ardhi itaondoka”.[86]

Vile vile Ibnu Hajar katika kitabu chake “Assawaiqul Muhriqa”, na katika hadithi zinazosisitiza katika kushikamana na Ahlul bait, kuna ishara kuwa wata-endelea kushikamanwa nao hadi siku ya kiyama, kama Qurani tukufu ilivyo, na ndiyo sababu wakawa ni amani kwa watu wa ardhini”.[87]

rudi nyuma Yaliyomo endelea