rudi nyuma Yaliyomo endelea

Pili: Mtume (s.a.w.a) alimwamuru Imam Ali Ibnu Abi Talib (a.s) peke yake kuandika na wala hakuna yeyote mwengine katika zama zake aliyejua aliyoku-wa ameandika. Kisha alimwusia kuwa kitabu hiki kiwe mikononi mwa Maimamu kumi na wawili baada yake. Basi inauwajibikia umma wote wa kiislamu kuchukua elimu inayo husu halali na haramu, na yote wanayohitajia katika dini yao kutoka kwake Ali (a.s) na Maimamu watokanao na kizazi chake, kwani wao ndio wasiri wa Mtume (s.a.w.a) na ndio hazina ya elimu yake na wahifadhio dini yake.

Tatu: Kitabu hiki kilikuwa mikononi mwao Maimamu (a.s). Imam Muhammad Baqir (a.s) na Imam Ja’afar Swadiq (a.s) waliwaonyesha baadhi ya maswahaba wao na wengineo katika wafuasi wa dhehebu la kisunni, ili kuitimiza hoja, na ili kuwaon-dolea shaka mioyoni mwao”.

Katika sehemu nyingine Seyyid Burujurdi ana-endelea kusema. “Basi inawajibika kuchukua hadithi katoka kwao, kwani zinaaminika zaidi kuliko za wengineo”.[49]

3) Wajibu wa Kushikamana na Quran na kizazi kitukufu(a.s).

Hadithi hii inatufunza ya kwamba ni wajibu kwa waislamu kushikamana na Qurani tukufu na kizazi, vyote viwiti kwa pamoja. Kwa hivyo basi kushika-mana na kimoja na kukiacha kingine ni kosa kwani maagizo ya hadithi ni kushikamana na vyoze viwili.

Basi watu wameamrishwa kushikamana na Qurani kama walivyoamwrishwa kushikamana na kizazi cha Mtume Mtukufu (s.a.w.a). Katika baadhi ya riwaya imepokewa kuwa alisema:

((وقد تركت فيكم ما ان تمسكتم به لن تضلوا بعدي كتاب الله بين ايديكم تقرؤونه صباحاً ومساءً وفيه ما تلقون وما تدّعون).

“Nimeacha kati yenu ambacho mkishikamana nacho hamtapotea kamwe baada yangu, Kitabu cha Mwenyezi Mungu kilicho kati yenu, mnakisoma asubuhi na jioni. Ndani nwake mna yote mnayokutana nayo na yote mnayodai…”[50]

Kurejeshwa kwenye Qurani kunaonyesha kuwa inabayana na ufafanuzi wa kutosha, na hii si kutokana na jambo jengine, ila tu ni kwa kuwa, maana dhahiri ya maneno yake ni hoja, kwa hivyo maana ya dhahiri ya maneno yake na aya zake za Muhkamat (zilizo dhahiri) ni nuru na uongofu. Naam, ufafanuzi wa lazima unaachiwa Mtume (s.a.w.a) na kizazi chake kitukufu, kwani Qurani tukufu, haikutoa maelezo yote kuhusu swala, zaka, hijja na mambo mengineo.

Vile vile kufafanua daraja za mafunzo yake na mambo yanayohusiana na akhlaq na jamii na mengi-neyo yote, ni jukumu lililo mikononi mwa kizazi kitoharifu(a.s). Kwa vyovote vile, haijuzu kuacha kuirejelea Qurani kwa kudai kuwa umeshi kamana na kizazi cha Mtume (s.a.w.a), kwani kizazi chenyewe kimeifanya Quran tukufu kuwa ndio kipimio cha haki, zinapo hitilafiana riwaya na hadithi za Mtume (s.a.w.a) na pia na kime kuwa kikiirejelea Qurani katika kupambanua baina ya hadithi zilizodhaifu na zilizosahihi. Kisha kizazi kitukufu kilitilia mkazo kuwa watu wairejelee Qurani na kuitegemea, na kuwahimiza katika mambo mengi yenye uhusiano na Qurani, kama vile kuisoma Qurani na kuizingatia. Kuhusiana na haya, yatutosha kauli yake Amirul muuminin Ali (a.s) aliyosema.

((واعلموا ان هذا القرآن هو الناصح الذي لا يغش والهادي الذي لا يضل والمحدث الذي لا يكذب وما جالس هذا القرآن احد الا قام عنه بزيادة او نقصان: زيادة في هدىً ونقصان من عمىً واعلموا انه ليس لاحد بعد القرآن من فاقة ولا لأحد قبل القرآن من غنى فاستشفوه من ادوائكم واستعينوا به على لأوائكم فان فيه شفاءً من اكبر الداء وهو الكفر والنفاق والغي والضلال فاسألُوا الله به وتوجهوا اليه بحبه ولا تسألوا به خلقه انه ما توجه العبادُ الى الله تعالى بمثله)).

“Tambueni kuwa hii Qurani ni mtoaji nasaha asiye hadaa, na mwongozaji asiyepoteza, na mzungumzaji asiyedanganya. Hakuna anayeketi karibu na hii Qurani, ila tu husimama akiwa na ziyada (katika jambo) na upungufu (katika jambo). Ziada katika uongofu na upungufu katika upofu (na upotofu). Tambueni, kuwa, hakuna mwenye haja, (na ufukara) baada ya kuwa na Quran, na hakuna mwenye utajiri kabla ya kuwa na Qurani. Basi jitibuni kwayo kutokana na maradhi yenu, na itegemeeni katika shida zenu, kwani ndani yake kuna tiba ya ugonjwa mkuu zaidi, nao ni ukafiri, unafiki udanganyifu na upotofu. Basi, muombeni Mwenyezi Mungu kwayo na mumuelekee kwa kui-penda, na wala msiwaombe viumbe vyake kwayo. Hakika waja hawakumwelekea Mwenyezi Mungu kwa njia bora mfano wake (Qurani).

“Na jueni kuwa Qurani ni mtetezi atakaye kubaliwa utetezi wake (siku ye kiyama) na mzungumzaji anayesadikiwa. Na (Jueni) kuwa atakayetetewa nayo siku ya kiyama atakubaliwa (na Mwenyezi Mungu) na ambaye Qurani itashuhudia maovu yake (mbele ya Mwenyezi Mungu) siku ya kiyama itasadikiwa (na kukubaliwa)”.[51]

Vile vile yatutosha kauli yake Imam wetu Ja’afar Sadiq (a.s) aliyosema,

((ثلاثة يشكون الى الله عزوجل: مسجد خراب لا يُصلى فيه اهله وعالم بين جهّال ومصحف معلق قد وقع عليه الغبار لا يُقرأ فيه)).

“Vitu vitatu vitashitaki kwa Mwenyezi Mungu Mwenye Nguvu na Aliyetukuka, (siku ya kiyama), msikiti ulioharibika ambao watu wake hawaswali ndani yake, na mwana chuoni katikati ya wajinga (wasiotaka kusoma) na Msahafu uliotundikwa, uliojaa mavumbi, usiosomwa”.[52]

Na kauli yake (a.s) nyingine:

((ان هذا القرآن فيه منار الهدى ومصابيح الدُجى فليَجْلُ جالٍ بَصَرَه ويفتح للضياء نظره فان التفكر حياة قلب البصير كما يمشي المستنير في الظلمات بالنور)).

))Haikika ndani mwa hii Qurani kuna nuru ya uon-gofu, na taa (zinazowaka) na kuondosha kiza, basi na atembeze mtembezaji macho yake na ayafungue ili kuupokea mwangaza (wake) kwani tafakari ndio uhai wa moyo wenye busara (na ayatembeze macho) kama yule anayetaka nuru yake atembeavyo gizani”[53]

Tambueni kuwa mwenye kutosheka tu nakuwataja Ahlul bait(a.s) bila ya kufwata maagizo na makatazo ya Qurani na mwelekezo wake, basi atakua hajachukua kutoka kwa Ahlulbait (a.s) kikamilifu, kwani wao hawaridhishwi kamwe na mtu kuiacha na kuipuuza Qurani.

Vile vile haifai kutosheka na Qurani pekee, kwani ufafanuzi kuihusu Quran kiupana pamoja na hukumu na elimu za Qurani zote ziko kwao, Ahlul bait (a.s).

Haya ni pamoja na haja iliyoko ya kuwepo kwao katika kuimarisha uadilifu, malezi bora, utakaso na kuondoa kuhitilafiana (baina ya waislamu) pamoja na mambo mengineo katika ulimwengu.

Kushikamana na Qurani bila ya kushikamana na Ahlulbait sio kushikamana kikamilifu na Qurani, kwani aya za Qurani zenyewe zinatuele keza katika kuwatawalisha juu ya mambo yetu yote na kuwatii na inatuelekeza katika wajibu wa kuwapenda, kwani kila moja wapo (Qurani na Ahlulbait) – kama ilivyo katika baadhi ya hadithi – inaifafanua nyengine na kuafikiana nayo.[54]

Kwa hivyo basi, la wajibu ni kushikamana na vyote viwili, na hili ndilo jambo lililotiliwa mkazo katika hadithuth thaqalain, isemayo:

((ما ان تمسكتم بهما لن تضلوا بعدي))

“Mkishikamana navyo (vizito viwili) hamtapotea kamwe baada yangu” pamoja na riwaya nyingi nyingi-nezo.

4) Sababu ya kuiita Qurani na kizazi vizito viwili (Thaqalain)

kuiita Qurani na Ahlul bait kuwa ni vizito viwili (Thaqalain) huenda ikawa ni kwa lengo la kutaka kuonyesha kuwa ni vitu vyenye thamani na utukufu sana. Hata hadithi yenyewe yaelezea binafsi kuhusu utukufu wa Quran na cheo kitukufu cha Ahlul bait (a.s).

Imenakiliwa kutoka kwenye kitabu cha Abaqatul Anwar kutoka kwa Ibnul Athir ya kwamba ameandika kwenye kitabu chake cha Annihaya kuwa “chochote kilicho hatari na chenye thamani huitwa “thaqal” (kizito). Basi ameviita vizito viwili (Thaqalain) ili kuonyesha utukufu wa cheo cha vitu hivi viwili na kwa hivyo neno kizito lafaa kusomwa kwa kutamta fatha mbili (Juu ya herufi mbili za mwanzo – yaani – ثَقَلُ (Thaqal)”.

Qurani ni tukufu zaidi ya Kitabu chochote kilichoteremshwa na Mwenyezi Mungu, nayo ni muujiza wa milele, itaendelea kuwepo madamu jua lipo. Nayo ni ufunuo (wahyi) usiopatwa na ubatilifu kabla yake wala baada yake, na ni nuru na uongofu.

Vile vile, kizazi, hakina mfano katika sifa, elimu na fadhila tukufu. Kama ilivyo makosa kuwalinganisha Mitume watukufu (a.s) na watu wa kawaida, vile vile ni makosa kuwalinganisha Ahlul bait (a.s) na watu wengineo wa kawaida, kwani wao ni mahujja[55] wa Mwenyezi Mungu juu ya viumbe vyake na wao ni hazina ya elimu yake.

Amirul muuminin Ali ibnu Abi Talib (a.s) katika maneno yake mafupi, (yaliyoko kwenye kitabu cha Nahjul balagha) kuhusu Ahlul bait (a.s) kwa kusema:

((انهم موضع سره ولجأ امره وعيبة علمه وموئل حكمه وكهوف كتبه وجبال دينه بهم اقام انحناء ظهره واذهب ارتعاد فرائصه… لا يقاس بآل محمد(ص) من هذه الامة احدٌ ولا يسوّي بهم من جرت نعمتهم عليه ابداً هم اساس الدين وعماد اليقين اليهم يفيء الغالي وبهم يلحق التالي ولهم خصائص حق الولاية وفيهم الوصية والوراثة الآن اذ رجع الحق الى اهله ونقل الى منتقله)).

“Wao ni wasiri wake (Mwenyezi Mungu) na maficho (sanduku) ya mambo yake, na chemchemi ya elima yake na marejeo ya hekima zake, pango za vitabu vyake na milima ya dini yake. Kwa kupitia kwao amenyoosha kupinda kwa mgongo wa dini na kuondosha kutetemeka kwa viungo vyake (dini) …… Hakuna katika umma huu anayeweza kulinginanishwa nao, na kamwe hawezi kusawazishwa nao yule anayetawaliwa na fadhila zao. Wao ndio msingi wa dini na nguzo ya imani. Aliyewatangulia (na kupita mipaka) yampasa kuwarejelea, na aliyebaki nyuma yampasa kuwafikia. Wana sifa zote za kustahiki uwalii (uongozi) na wao ndio wenye wasia (wa Mtume (s.a.w.a) na urithi (wake). Huu ndio wakati ambao haki imemrudia mwenyewe (anayeistahiki) na kunakiliwa hadi kwenye mahala pake.”[56]

Huenda mtu akadai, kama alivyosema Zamakhshari, kuwa neno thaqalain limetumiwa kwenye hadithi kwa lengo la kuvifananisha vizito viwili na majini (yaani) kama wanavyoitwa (watu na majini) thaqalain (ndani ya Qurani) kumaanisha dunia, vile vile thaqalain (Quran na Ahlul bait) limetumika kumaanisha dini.[57]

Na huenda ikawa makusudio ya kutumia neno hili thaqalain, ni kuonyesha kuwa kutenda na kushikamana na vizito viwili na kutii na kuchunga haki zao na kuviangalia ni jambo zito. (Hii ni) kama walivyofasiri baadhi ya wajuzi wa lugha ya kiarabu, na wajuzi wa hadithi tukufu kama alivyo nukuu Alhamwini kutoka kwa Ibnul Abbas, ya kwamba, “Aliulizwa maana ya kauli ya Mtume (s.a.w.a) “Hakika mimi ninaacha
((اني تارك فيكم الثقلين)) kati yenu thaqalain (vizito viwili)?” akasema “kwa kuwa kushikamana navyo nikuzito (Thaqiil)”.[58]

Na katika riwaya nyingine vile vile kutoka kwake, amesema, “kwa kuwa kushikamana navyo na kutenda kufwatana navyo ni kuzito (thaqiil).”[59]

Maneno haya vile vile yametajwa katika kitabu cha Abaqatu; Anwar kama ilivyopokewa kutoka kwa Al-azhari kwenye kitabu cha Tahdhibul lugha na kwenye vitabu vingine pia.[60]

Kwa hivyo basi, kufuatana na kauli hii neno (ثِقْلُ) (Thiqlu) lenye kasra – lina maana ya mzigo mzito au mojawapo ya vitu vizito, lakini hii ni kinyume cha maana dhahiri ya hadithi, kwa kuwa (ikifasiriwa vivyo) itakuwa ina sifia hali ya hivi vitu viwili, na ilhali dhahiri ya hadithi inawajibisha hii kuwa sifa ya vitu vivyo (wala siyo sifa ya hali yavyo) kwa kuwa vyenyewe ni vizuri na vyenye utukufu na cheo.

5) Maana ya Al-itrah (kizazi).

“Al-itra” (kizazi) kama lilvyotajwa katika Annihaya na katika vitabu vinginevyo ni jamaa wa karibu wanaomhusu mtu.

Kwa hivyo basi neno hili haliwa kusanyi wasio kuwa jamaa wa karibu wanaomhusu mtu, mbali na wasio kuwa jamaa wa karibu, bali kinacho kusudiwa hapa kufuatana na mnasaba wa hukumu na maudhui[61] sio yeyote yule, katika jamaa wa karibu kwani sifa zao zilizotajwa kwenye hadithi- kama kuwafanya kuwa ni sawa na Quran tukufu na mizani ya haki na uongofuhazitusaidii katika kulitumikisha neno hili kuwakusanya wote. Kwa hivyo basi wanaokusudiwa – kama ilivyo tajwa waziwazi kwenye riwaya chungu nzima – ni Ahlul bait waliotajwa katika Qurani tukufu kuwa wametoharishwa (kutokana na madhambi) nao ni Maimamu Maasumu waliowatoharifu.

Ibnu Abil Hadid amesema kuwa “Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.a) alishabainisha kuwa ninani kizazi chake (itrah) aliposema”.

((اني تارك فيكم الثقلين))

“Hakika mimi ninaacha kati yenu thaqalain (vizito viwili)” kisha akasema;

((وعترتي اهل بيتي))

“Na kizazi changu (ambao ni) Ahlubaiti wangu” (yaani watu wa nyumba yangu). Kisha akabainisha katika sehemu nyingine kuwa ni nani Ahlubaiti wake, alipowakusanya chini ya shuka, ilipoteremka aya

انما يريد الله ليذهب عنكم الرجس اهل البيت ويطهركم تطهيراً

“Hakika Mwenyezi Mungu Anataka kakuondo-leeni uchafu enyi watu wa nyumba (ya Mtume) na (anataka) kukutakasenikabisa kabisa” na kusema;

((الّلهم هؤلاء اهل بيتي فاذهب الرجس عنهم))

“Ewe Allah, hawa ndio Ahlubait wangu, basi waondolee uchafu”.[62]

Aljurjani Ash-shafii; (Aliyefariki katika mwaka wa 365 H.) amepokea kutoka kwa Abu Said ya kwamba alisema, “Hii aya – ayatut tat-hir’ – (aya ya kutakaswa kwa Ahlulbait), iliteremshwa kuwahusu watu watano… Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.a) Ali, Fatima, Hasan na Husein (a.s)”[63]

Adh-dhahabi katika Talkhisul mustadrak amepokea kutoka kwa Ummu Salama ya kwamba alisema,

((في بيتي نزلت انما يريد الله ليذهب عنكم الرجس اهل البيت ويطهركم تطهيراً فارسل رسول الله (ص) الى عليّ وفاطمة والحسن والحسين فقال: ((الّلهم هؤلاء اهل بيتي)) قالت ام سلمة: ((يا رسول الله ما انا من اهل البيت؟ قال: لا انك إلى خير وهولاء اهل بيتي الّلهم اهلي احق)).

Hakika Mwenyezi Mungu Anataka kukuondoleeni uchafu enyi watu wa nyumba (ya Mtume) na (anataka) kukutakaseni kabisa kabisa”. ilitermka nyumbani kwangu. Basi Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.a) akawatumania Ali, Fatima, Hasan na Husein (a.s), na kusema, “Ewe Allah hawa ndio Ahlubaiti wangu”. Ummu Salama akamwambia (Mtume (s.a.w.a)) “Ya Rasulallah, Je, mimi si katika Ahlulbait?” akamjibu “Hakika wewe u katika kheri, na hawa ndio Ahlubaiti wangu. Ewe Allah Ahlubati wangu ndio wenye haki zaidi”.[64]

Na kuna riwaya nyingi nyinginezo zinazoonyesha kuwa Ahlul bait katika ayatut tathir wanao kusudiwa ni watu makhsusi.

Na hivyo ndivyo ilivyo pia katika riwaya zinazoifasiri “ayatul mubahala” (aya ya kuapizana kwa Mtume (s.a.w.a) na wakristo wa Najran) ambazo vile vile zinaelezea kuwa makusudio hasa ya Ahlul bait ni akina nani.

Muslim amepokea kwa isnadi yake, kwamba “ayatul mubahala[65] ilipoteremka Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.a) alimwita Ali, Fatima, Hasan na Husein (a.s) na kusema.

((اللهم هؤلاء اهل بيتي ـ اهلي ـ))

“Ewe Allah hawa ndio Ahlu baiti wangu, Jamaa wangu (wa nyumbani)”.[66]

Na ndio sababu imetajwa kwenye kitabu cha Abaqatul Anwar kukiri kwa maulama wa dhehebu la kisunni kuwa hadithuth thaqalain inazungumza kuhusu Maimamu watokanao na Ahlulbait (wala haiwahusu watu wengine).

Miongoni mwa maulama hawa ni Alhakim Attirmidhi, aliyesema kuwa, “Basi kauli ya Mtume wa Mwenyezi, Mungu (s.a.w.a) kuwa

((لن يفترقا حتى يردا علي الحوض))

“Havitatengana kamwe mpaka vitakaponijia huko kwenye hodhi (ya kauthar)” na kauli yake kuwa

((ما ان اخذتم به لن تضلوا))

“Mkishikamana nacho hamtapotea kamwe”, inawa-husu Maimamu. Basi wao ni maseyyid (mabwana) na wala haiwahusu wengine”.[67]

Na miongoni mwao ni Sibtu Ibnil Jauzi, alipoitaja hii hadithi katika Tadhkiratul khawass, chini ya unwani ya (ذكر الائمة) “Tunayoyataja kuwahusu Maimamu”.[68]

Na miongoni mwao ni Alkanji Ash-shafii katikakifaya tut Talib (baada ya kuitaja riwaya ya Zaid Ibnu Arqam na tafsiri yake ya Ahlulbait, kuwa ni wale walioharanmishiwa kula sadaka) alisema kuwa – “Hii tafsiri ya Zaid kuwahusu Ahlul bait hairidhishi, kwani amesema “Ahlulbait ni wale ambao wameharamishiwa kula sadaka baada yake – (yaani baadaye Mtume sawa) – ilhali kuharamishiwa kwao sadaka sio tu baada ya kufariki kwa Mtume(s.a.w.a), bali hata katika uhai wake. Vile vile kuharamishwa huku hakuwahusu tu waliotajwa (katika hadithi) bali kunawahusu hata Bani Muttalib”. mpaka akafikia kusema, “Bali lililo sahihi ni kuwa Ahlul bait ni Ali, Fatima, Hasan na Husein (a.s) kama alivyopokea Muslim kwa isnadi yake kutoka kwa Bibi Aisha (aliyeseme).

((ان رسول الله خرج ذات غداة وعليه مرط مرَّجل من شعر اسود فجاء الحسن بن علي فادخله ثم جاء الحسين فادخله معه ثم جاءت فاطمة فادخلها ثم جاء عليّ فادخله ثم قال انما يريد اللهُ ليذهب عنكم الرجس اهل البيت ويطهركم تطهيراً )).

“Siku moja asubuhi, Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.a) alitoka akiwa amejifinika kwa shuka iliyoshonwa kwa sufi nyeusi; Hasan ibnu Ali akamjia, (Mtume) akamwingiza (ndani ya shuka). Kisha akaja Husein, akamwingiza (pia). Kisha akaja Fatima, akamwingiza (pia). Kisha akaja Ali, akamwingiza (vile vile) : Kisha akasema “Hakika Mwenyezi Mungu (Anataka) kukuon-doleeni uchafu enyi watu wa nyumba (ya Mtume) na (Anataka) kukutakaseni kabisa kabisa”.

Na hii ni dalili ya kuonyesha kuwa Ahlulbait ni wale ambao Mwenyezi Mungu Aliwaita kwa kauli yake Ahlulbait ambao Mtume (s.a.w.a) aliwaingiza ndani ya shuka”.[69]

Kuna maulamaa wengine wengi waliokiri (kuwa Ahlulbait katika hadithuth thaqalain ni Maimanu Maasumin), walio tajwa, majina yao pamoja na maneno yao (yaani maulamaa) kwenye kitabu cha Abaqatul Anwar.[70]

Haya, bila ya kutaja riwaya nyingi zilizo mutawatir[71] katika vitabu vyetu zinazohusiana na mlango huu, ambazo miongoni mwazo ni riwaya aliyoipokea Ibnu Babaweihi katika kitabu cha “Uyunu Akhbarir Ridha (a.s)” kutoka kwa Imam Ja’afar Swadiq (a.s) kutoka kwa babu zake watukufu (a.s) kutoka kwa babu yake, (ambaye ni) Imam Husein (a.s) ya kwamba alisema”,

((سُئل اميرالمؤمنين (ع) عن معنى قول رسول الله ((اني مخلف فيكم الثقلين: كتاب الله وعترتي)) مَن العترة؟ قال: انا والحسن والحسين والائمة التسعة تاسعهم مهديهم وقائمهم لا يفارقون كتاب الله ولا يفارقهم حتى يردوا على رسول الله حوضه)).

rudi nyuma Yaliyomo endelea