rudi nyuma Yaliyomo endelea

“Ninawahakikishieni kuwa nitawatolea hoja (yangu) kwa kitu ambacho hawezi mwarabu kati yenu na wala muajeni kati yenu kutoa hoja zaidi yake”, kisha akase-ma “Nawaapizeni (nyote) kwa (Jina la) Mwenyezi Mungu, enyi kikundi (cha waliopo hadharani) Je, kuna yeyote kati yenu aliyempwekesha Mwenyezi Mungu kabla yangu?” Wakajibu “Twaapa kwa (Jina la) Mwenyezi Mungu ya kwamba hakuna (yeyote kati yetu)” mpaka akafikia kusema “Basi nawaapizeni kwa (Jina la) Mwenyezi Mungu, je mnajua ya kwamba Mtume Mtukufu (s.a.w.a) alisemu kwambu, “Hakika mimi ninaacha kati yenu viwili vizito; Kitabu cha Mwenyezi Mungu na kizazi changu, hamtapotea kamwe mkidumu kushikamana navyo, na kamwe havitoachana mpaka vitakaponijia hodhini (mwa kauthar)?” wakajibu “Twaapa kwa (Jina la) Mwenyezi Mungu kuwa ndio (tulimsikia akisema vivyo)”.[30]

Vile Vile Amirul Muuminin (a.s) alitoa hoja kwa kutumia hadithi hii katika Msikiti wa Mtume (s.a.w.a) katita ukhalifa wa Uthman mbele ya kikundi cha maswahaba, nao wakamjibu kwa kusema.

((نشهد ان رسول الله (ص) قال ذلك))

“Tunashuhudia kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu alisema hivyo”.[31]

Vile Vile Imam Hasan bin Ali (a.s) alitoa hoja kwa kutumia hadhithi hii ili kuthibitisha kuwa yeye ndiye aliyekuwa na haki ya kuwa khalifa na Imamu wa waislamu. Sheikh Suleiman Alqanduzi katika Kitabu cha Yanabiul Mawadda amenukuu kutoka kwenye Kitabu kiitwacho Almanaqib, hadithi kutoka kwa Hisham ibnu Hassaan, ya kwamba alisema.

((خطب الحسن بن علي(ع) بعد بيعة الناس له بالامر فقال ((نحن حزب الله الغالبون ونحن عترة رسوله الاقربون ونحن اهل بيته الطيبون ونحن احد الثقلين اللذين خلّفهما جدّي (ص) في امته ونحن ثاني كتاب الله فيه تفصيل كل شيء لا يأتيه الباطل من بين يديه ولا من خلفه)).

“Hasan ibnu Ali (a.s) alihotubia watu baada ya wao kumkubali kuwa khalifa na kusema, “sisi ndio kundi la Mwenyezi Mungu lenye ushindi, sisi ndio kizazi cha karibu cha Mtume wake sisi ndio Ahlubait wake walio wema. Sisi ndio kizito kimoja katika vizito viwizi alivyo viacha babu yangu (mpendwa) (s.a.w.a) katika umma wake. Na sisi ndio wa pili baada ya Kitabu cha Mwenyezi Mungu, (ambamo) ndani yake kuna upambanuzi wa mambo yote, haikifikii batili, mbele yake wala nyuma yake”.

SEHEMU YA TATU

Matamshi ya hadithi kama yalivyo kuja vitabuni

1) Katika hijja ya mwisho

((اني اوشك ان ادعى فاجيب واني تارك فيكم الثقلين كتاب الله عزوجل حبل ممدود من السماء الى الارض وعترتي اهل بيتي وان اللطيف الخبير اخبرني انهما لن يفترقا حتى يردا علي الحوض فانظروني بما تخلفوني فيهما.))

a) “Huenda nikaitwa (na Mola wangu) nami nikajibu, nami ninaacha kati yenu viwili vizito, Kitabu cha Mwenyezi Mungu Mwenye Nguvu na Aiyetukuka, ambacho ni kamba iliyonyooshwa toka binguni hadi ardhi. Na kizazi changu (ambao ni) Ahlubaiti wangu. Hakika Mjuzi wa (yote) yaliyofichika na yaliyodhahiri amenijulisha kuwa havitatengana kamwe mpaka vita-kaponijia huko hodhini (mwa kauthar) basi angalieni vile mtakavyovitendea baada yangu”.[32]

((اإني قد تركت فيكم ما ان اخذتم به لن تضلوا بعدي الثقلين احدهما اكبر من الآخر)).

b) “Hakika mimi ninaacha kati yenu ambavyo mki-vichukua (na kushikamana navyo) kamwe ha mtopo-tea baada yangu, navyo ni vizito viwili, kimoja kati yavyo ni kikuu kuliko kinginecho”.

Na katika hijja ya mwisho katika sehemu iitwayo Ghadir khum aliongeza maneno haya (kwa kusema):

((فانظروا كيف تخلفوني فيهما فانهما لن يفترقا حتى يردا علي الحوض)) ثم قال: ((ان الله عزوجل مولاي وانا مولى كل مؤمن)) ثم اخذ بيد علي فقال: ((من كنت مولاه فهذا وليّه))

c) “Basi angalieni mtakavyo vifanyia baada yangu, kwani, kamwe havitotengana hadi vitakaponija kwenye hodhi”, kisha akasema, “Hakika Mwenyezi Mungu Mwenye Nguvu na Aliyetukuka ni Bwana wangu, nami ni bwana wa kila muumini”. Kisha akaushikia mkono wa Ali na kusema “Ambaye mimi ni bwana wake, basi huyu Ali ni bwana wake”.[33]

2) Katika Ghadir Khum

قال في غدير خم ايضاً:((اذكركم الله في اهل بيتي اذكركم الله في اهل بيتي اذكركم الله في اهل بيتي)).

“Nakukumbusheni Mwenyezi Mungu katika Ahlu-baiti wangu, nakukumbusheni Mwenyezi Mungu katika Ahlubaiti wangu, nakukumbusheni Mwenyezi Mungu katika Ahlubaiti wangu”.[34]

3) Katika hotuba ya Mwisho siku aliyoaga dunia

Katika siku aliyoaga dunia na kurudi kwa Mola wake alisema katika hotuba yake ya mwisho:

((اني تركت فيكم امرين لن تضلوا بعدي ان تمسكتم بهما كتاب الله عزوجل وعترتي اهل بيتي فان اللطيف الخبير قد عهد الي انهما لن يفترقا حتى يردا علي الحوض كهاتين ـ وجمع مسبّحتيه ـ ولا اقول كهاتين ـ و جمع مسبّحته والوسطى ـ فتمسكوا بهما ولا تقدموا فتضلوا)).

a) “Hakika mimi ninaacha mambo mawili kati yenu, mkishikamana nayo hamtapotea kamwe baada yangu Kitabu cha Mwenyezi Mungu Mwenye Nguvu Aliyetukuka, na kizazi changu (ambao ni) Ahlubaiti wangu, kwani mjuzi wa yaliyoficha na yaliyodhahiri Amenijulisha kwamba (Mambo haya mawili) hayato-tengana kamwe mpaka yatakaponijia katika hodhi (ya kauthar) kama hivi viwili – (akavishikanisha vidole vyake viwili vya shahada) – na wala sisemi kama hivi viwili (akakishikanisha kidole cha shahada na kidole cha kati) basi shikamaneni nayo (mawili) na wala msiwatangulie (Ahlubaiti wangu) msije mkapotea”.[35]

((قد تركت فيكم ما ان تمسكتم به لن تضلوا بعدي كتاب الله بين ايديكم تقرؤونه صباحاً ومساءً وفيه ما تلقون وما تدّعون الاّ تنافسوا ولا تحاسدوا ولا تباغضوا وكونوا إخواناً كما امركم الله الا ثم اوصيكم بعترتي اهل بيتي)).

b) “Nimekwishaviacha kati yenu ambavyo mkishi-kamana navyo hamtapotea kamwe baada yangu, Kitabu cha Mwenyezi Mungu kilicho mikononi mwenu, mnakisoma asubuhi na jioni, na ndani yake kuna yale mnayokutana nayo na yale mnayodai. Kwa hivyo msishindane wala msihusudiane wala msichukiane, na kueni ndugu kama alivyokuamrisheni Mwenyezi Mungu kisha nawa usieni kizazi changu (ambao ni) Ahulbaiti wangu”.[36]

((فلا تقدموهما فتهلكوا ولا تعلموهما فانهما اعلم منكم))

c) ((Basi misivitangulie (vizito viwili) msije mka-angamia na wala msivifunze kwani vina elimu zaidi kuwaliko nyinyi)).[37]

((فلا تسبقوا اهل بيتي بالقول فتهلكوا ولا تقصروا عنهم فتذهبوا فان مثلهم فيكم كمثل سفينة نوح من ركبها نجا ومن تخلف عنها هلك ومثلهم فيكم كمثل باب حطة في بني اسرائيل من دخله غفر له الا وان اهل بيتي امان امتي فاذا ذهب اهل بيتي جاء امتي ما يوعدون. الا وان الله عصمهم من الضلالة وطهرهم من الفواحش واصطفاهم على العالمين الا وان الله اوجب محبتهم وامر بمودتهم...))

d) “Basi msiwatangulie Ahlubaiti wangu kwa kauli msije mkaangamia na wala msibaki nyuma yao msije mkapotea kwani mfano wao kati yeni ni mfano wa safina ya Nuhu (a.s) aliyeipanda aliokoka na aliye-baki nyuma (bila kungia) aliangamia. Na mfano wao kati yenu ni mfano wa mlango wa Hitta (msamaha) katika wana wa Israeli, aliyeuingia alisamehewa. Tambueni kuwa Ahlubaiti wangu ni amani kwa umma wangu, basi watakapoondoka Ahlubaiti wangu (ardhini) kitawajia umma wangu kile walichoahidiwa (yaani kiyama); Tambueni kuwa Mwenyezi Mungu Amewa-hifadhi hawa kutokana na upotofu na kuwatakasa kutokana na machafu na kuwachagua juu ya walim-wengu wote. Tambueni kuwa Mwenyezi Mungu Amewajibisha kuwapenda wao (na Ameamuru kuwa wapendwe).[38]

((اني تارك فيكم الثقلين كتاب الله عزوجل وعترتي اهل بيتي الا وهما الخليفتان من بعدي ولن يفترقا حتى يردا علي الحوض)).

e) “Hakika mimi ninaacha kati yenu Viwili vizito Kitabu cha Mwenyezi Mungu Aliyetukuka na kizazi changu(ambao ni) Ahlubaiti wangu. Tambueni kuwa viwili hivi, ndivyo makhalifa wawili baada yangu na havitatengana kamwe, baada yangu mpaka vitakapo-nijia huko hodhini (mwa kauthar)”.[39]

((اني تركت فيهم خليفتين كتاب الله واهل بيتي وانهما لن يفترقا حتى يردا علي الحوض))

f) “Hakika mimi ninaacha kati yao makhalifa wawili, Kitabu cha Mwenyezi Mungu na Ahlubaiti wangu, navyo havitoachana kamwe mpake vitakapo-nijia hodhini.”[40]

((اني تارك فيكم الخليفتين: كتاب الله حبل ممدود ما بين السماء والارض وعترتي أهل بيتي وانهما لن يفترقا حتى يردا عليّ الحوض)).

g) “Hakika mimi ninaacha kati yenu makhalifa wawili, Kitabu cha Mwenyezi Mungu (ambacho) ni kamba (ya Mwenyezi Mungu) iliyonyooshwa baina ya mbingu na ardhi, na kizazi changu (ambao ni) Ahlubaiti wangu, nao (makhalifa wawili) hawato-tengana kamwe hadi watokapo nijia hodhini (mwa kauthar).[41]

((وان اللطيف الخبير نبّأني انهما لن يفترقا حتى يردا علي الحوض فسألت ذلك لهما ربي فلا تقدموهما فتهلكوا ولا تقصروا عنهما فتهلكوا ولا تعلموهم فانهم اعلم منكم من كنت اولى به من نفسه فعلي وليه اللّهم وال من والاه وعاد من عاداه)).

h) “Kwa hakika Mjuzi wa yaliyofichika na yaliyo-dhahiri amenijulisha kuwa havitatengana kamwe mpaka vitakaponijia kwenye hodhi. Basi niliviombea haya kwa Mola wangu, kwa hivyo msivitangulie msije mkaangania na wala msibaki nyuma msije mkaanga-mia, na wala msiwafunze (Ahlubait wangu) kwani wao wanajua zaidi yenu. Ambaye mimi ni bwana wake basi Ali ni bwana wake. Ewe Allah mpende ampendaye (Ali) na mfanyie uadui amfamyiae uadui.”[42]

4) HUKO JUHFA

katika hotuba yake (s.a.w.a) huko Juhfa, Ghadir khum alisema;

((ألست اولى بكم من انفسكم قالوا بلى يا رسول الله)) قال ((فاني سائلكم عن اثنين: القرآن وعترتي))

“Je si mimi ninazitawala nafsi zenu zaidi ya mnav-yozitawala nyinyi nafsi zenu?” wakajibu “Ndiyo, ya Rasulallah” akasema “basi mimi nitawaulizeni kuhu-siana na vitu viwili (siku ya kiyama), Qurani (tukufu) na kizazi changu”.[43]

SEHEMU YA NNE

Maana ya hadithi

Tunajifunza kutokana na hadithi hii tukufu mambo yafwatayo:-

1– Mtume(s.a.w.a) aliwajulisha waislamu kifo chake.

Mtume Mtukufu (s.a.w.a) aliwajulisha waislamu kuhusu kifo chake. Hadithi nyingi zinaonyesha maana hii, kama vile kauli yake tukufu aliyoisema;

((اني اوشك ان ادعى فاجيب))

“Hakika mimi huenda nikaitwa (na Mola wangu) nami nikajibu.”

Na kauli yake:

((ان الله عزوجل اوحى اني مقبوض))

“Hakika Mwenyezi Mungu, Mwenye Nguvu na Aliyetukuka ameniteremshia wahyi (kunijulisha) kuwa mimi nitafariki”. Pamoja na kauli nyingi nyinginezo.

Hizi hadithi zinaonyesha kuwa Mtume Mtukufu (s.a.w.a) alipozungumza maneno hayo alikua katika hali ya kubainisha wadhifa wa umma baada ya kufa kwake, ili usibaki katika hali ya kupuuzwa, jambo lisilomstahiki Mtume(s.a.w.a) kwani mfano wake, ambaye ni mwanzilishi wa uislamu, atawezaje kuridhia kuuacha uislamu na waislanu hivi tu, bila ya mwelekeo, baada ya kupitio mateso na misiba katika kuuasisi uislamu na serikali ya kiislamu? Kamwe, hekima ya Mwenyezi Mungu pamoja na elimu ya Mtume Mtukufu (s.a.w.a) haimruhusu yeye (s.a.w.a) kufanya vivyo.

2) Kutotengana kwa Qurani na kizazi cha Mtume (s.a.w.a)

Kuviacha vitu viwili (yaani Kitabu cha Mwenyezi Mungu na kizazi cha Mtume Mtukufu (s.a.w.a) ) katika umma ni sawa na kuvifanya kuwa makhalifa wake. Basi Quran na kizazi chake Mtume (s.a.w.a) ni makhalifa wawili wa Mtume Mtukufu (s.a.w.a) katika ummu. Vinachukua cheo cha Mtume (s.a.w.a) vinapo-dumu kuwa pamoja na kutofarikiana, na hii ndio sababu tunaona kwenye hadithi nyingi Mtume (s.a.w.a) akiviita makhalifa, kama alivyopokea Ahmad katika kitabu chake cha Musnad kutoka kwa Zaid ibnu Thabit, aliyesema, “Mtume wa Mwenyezi Mungu alisema:

((اني تارك فيكم خليفتين))

“Hakika mimi ninaacha kati yenu makhalifa wawili”.[44]

Vile vile imepokewa kutoka kwa Abu Sa’id Alkhidri ya kwamba alisema, “Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.a.) alihotubia na kusema:

((يا ايها الناس اني تركت فيكم الثقلين خليفتين))

“Enyi watu, hakika mimi nimeacha kati yenu vizito viwili, vikiwa (kama) makhalifa wawili”. [45]

Au kwa riwaya nyingine;

((اني مخلّف فيكم الثقلين))

“Hakika mimi ninaviacha viwili vizito kuwa makh-alifa kati yenu”.[46]

Na kwenye riwaya nyingine alisema:

((قد خلفت فيكم الثقلين))

“kwa hakika nimeviacha viwili vizito kuwa makhalifa kati yenu”.[47]

Lengo la kukifanye kizazi chake (s.a.w.a) kuwa khalifa na kukiachia cheo chake si jengine ila tu, ni kukipa majukumu yake, na hii kwa njia nyingine inathibitisha uimamu na uongozi wa kizazi chake (s.a.w.a) juu ya umma wake.

Kwa hivyo basi, hadithi hii inatuthibitishia vilevile uongozi wao katika mambo ya kisiasa kama inavyo-thibitisha uongozi wao katika mambo ya kielimu na mengineo. Inatuthibitishia pia wajibu wa kuwafuata kiujumla, na wala haikushurutisha jambo lotote lile katika kuwafuata. Imetuthibitishia pia uharamu wa kuwatangulia au kubaki nyuma (yao).

Lakini, ni sikitiko kubwa kuona kuwa umma wa kiislamu uliwaacha na kuwapuuza Ahlulbait (Baada ya kuwa Mtume Mtukufu (s.a.w.a) ametilia mkazo sana.) na wala hawakujali haki zao, kwani hawaku-unyenyekea uimamu na uongozi wao, bali walifanya yale waliyoya fanya baada ya kuwa Mtume (s.a.w.a) amemteuwa na kumuainisha Imamu katika sehemu nyingi na hasa katika siku yake ya kuaga dunia.

Zaidi ya hayo hawakuchukuo hukumu na sheria za Mwenyezi Mungu na wala adabu na sunna za Mtume (s.a.w.a) walibaki bila kuziandika hadi baada ya nusu ya karne ya pili ya hijriya takriban, ali po kuja khalifa Umar ibnu Abdul Aziz na kuifuta sheria hii, kwa kuona kuwa hadithi tukufu zina potea. Ndipo maula-maa wa kisunni wakaanza kuandika hadithi za Mtume Mtukufu (s.a.w.a) ziilizobaki (kama vile Malik na Ahmad ibnu Hambal na Bukhari na wengineo (kwa utaratibu huo) baada ya kuzisahao nyingi kati ya hizo au baada ya kufariki kwa kwa waliokuwa wamezihi-fadhi. Baadhi ya wachunguzi wa hadithi wamesema ya kwamba “Hadithi wanazozitegemea (ndugu zetu masunni) katika kutoa hukumu za sheria hazizidi mia tano”.

Na kwa hivyo sunna (hadithi) za Mtume Mtukufu (s.a.w.a) kwa ndugu zetu masunni zilikuwa hazijaku-sanywa wala hawakuzijua kabla ya nusu ya karne ya pili, na hali ya kuwa sunna kamili ilikuwa pamoja na Ahlul bait (a.s) tangu kuaga dunia kwa Mtume (s.a.w.a).

Kwa hivyo basi, nini sababu ya kuiacha na kuipuuza elimu ya Ahlulbait, ilhali walikuwa wakina-kili sunna ya Mtume (s.a.w.a) kama ilivyo kuwa, kwa ukamilifu.

Almuhaqqiqul wahiid (Muhakiki wa aina yake) Seyyid Burujurdi (r.a) amesema ya kwamba, “Kuna hadithi nyingi zilizopokelewa kutoka kwa Ahlul bait (a.s) zisemazo kuwa wana kitabu kilichoandikwa kwa imla[48] ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.a) na kwa khati za Imam Ali bin Abi Talib (a.s), ambacho ndani yake kuna Sunna zote za Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.a) na yote aliyoamrishwa na Mwenyezi Mungu kuyafikisha kwa umma wake, katika mafunzo na hukumu za kidini.”

Kisha alitaja baadhi ya riwaya hizi zenye kuon-yesha kuwepo kwa kitabu kwa imla ya Mtume (s.a.w.a) na kwa hati ya Ali (a.s) na kusema, “Inadhihiri kutokana na hadithi hizi mambo yafwatayo”.

Kwanza: Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.a) hakuuacha umma baada yake bure, bila ya Imamu wa kuwaongoza, wala bayana ya kutosha, bali aliwacha-gulia Maimamu, watukufu, waongozao na kuihifadhi dini, kisha akawapa mafunzo yanayomhusu Mwenyezi Mungu, faradhi za kidini, sunna na adabu, halali na haramu, hekima na athari, na yote wanayoyahitajia watu hadi siku ya kiama, hata ikiwa mtu atamkwaruza mwenzake amewaelezea ni kiwango gani cha faini (dia) kinachofaa kutolewa. Wala hakumruhusu yeyote kuhukumu au katoa fatwa kwa kutumia rai na maoni yake au kwa kutumia Qiyas (kufananisha hukumu za sheria kama wafanyavyo ndugu zetu masunni) kwani hakuna maudhiu au jambo lolote lisilokuwa na hukumu thabiti itokayo kwa Mwenyezi Mungu, Aliye Mjuzi Mwenye Hekima, bali Mtume (s.a.w.a) alimju-lisha Imam Ali Ibnu Abi Talib (a.s) sheria na hukumu zote na kumuamuru kuwa aziandike na kuzihifadhi. Na kuwakabidhi Maimamu (a.s) katika kizazi chake. Basi Ali (a.s) aliandika kwa hati yake (tukufu) na kuwakabidhi waliokusudiwa (yaani Maimamu).

rudi nyuma Yaliyomo endelea