rudi nyuma Yaliyomo  

((اني سائلكم عن اثنين: القرآن وعترتي))

“Hakika mimi nitawaulizeni kuhusu vitu viwili, Qurani na kizazi changu”.[107]

12) Hadithuth thaqalain inathibitisha kuwa Uimamu ni wa kizazi pekee

Hadithuth thaqalain inaonyesha kuwa kizazi cha Mtume (s.a.w.a) kilipata Uimamu baada tu ya Mtume (s.a.w.a) kuaga dunia bila ya kupita muda na kwa hivyo hilo ndilo linalofaa kufuatwa kama tuonavyo katika hadithi zilizomutawatir zinazoonyesha kuwa Mtume (s.a.w.a) alimfanya Imam Ali (a.s) kuwa wasii khalifa na walii (kiongozi) baada yake.

Na hii ndio sababu Seyyid Murtadha (r.a) katika Kitabu cha Shafii ananukuliwa akisema “Hadithi hii inaonyesha kuwa Amirul Muumini Ali (a.s.) alikuwa ndiye Imamu baada ya Mtume (s.a.w.a) pasipo kupita muda”.[108]

13) Mwenye kushikamana na Qurani na kizazi kitukufu, huyo ndiye mwenye kuongoka

Mwenye kushikamana na Qurani na kizazi cha Mtukufu Mtume (s.a.w.a) huyo ndiye aliyeongoka kufuatana na kauli ya Mtume (s.a.w.a) aliye mkweli na mwaminifu, katika hadithuth thaqalain iliyomu-tawatir. Na wala haifai kumwita mpotofu au raafidhi (mkataa haki) mwenye kushikamana navyo, kwani Mtume (s.a.w.a) hakosei katika kauli yake. Kuna hadithi nyingi zionyeshazo kuwa mashia, wafuasi wa Ahlul bait (a.s) ndio watakaofuzu siku ya kiama. Basi (ndugu yangu) usighafilike.

Kwa kumalizia ninamuomba Mwenyezi Mungu awajaalie ndugu zetu waislamu kutafakari katika hadithuth thaqalain, iliyomutawatir na inayokubaliwa na maulama wa madhehebu yote ya kiislamu.

Kwani hadithi hiyo ni nuru ambayo Mtukufu Mtume(s.a.w.a) aliwaangazia waislamu ili wasije wa-kapotea wala kufarikiana, baada ya kuondoka kwake.

Ewe Allah, tujaalie sisi na waislamu wote ulimwe-nguni, kushikamana na Kitabu Kitukufu na Kizazi Kitoharifu, Amina ya rabbal alamina.

Seyyid Muhsin

Alkharrazi

Mji wa Qum Almusharrafa

Tarehe 21 Ramadhen 1416 H.