rudi nyuma Yaliyomo endelea

Siku moja alipokuwa Imam Hasan AS akipita njiani akiwa amempanda farasi, akakutana kwa ghafla na mtu mmoja kutoka Shamu. Bila ya kusita, Mshamu akaanza kumtukana na kumvunjia heshima Imam. Imam akamsikiliza kwa makini mpaka akamaliza. Kisha akamwambia kwa maneno mazuri na kwa upole:

"Nafikiri umekosea. Ukiniruhusu nitakufurahisha na kukuridhisha. Chochote unachotaka nitakupa. Ikiwa umepotea njia nitakuongoza. Ikiwa unahitajia msaada wa kubeba mizigo yako, nitaamrisha mizigo yako ifikishwe mpaka nyumbani kwako. Ikiwa una njaa nitakushibisha. Ikiwa unahitajia nguo nitakuletea. Ikiwa ni maskini na mhitaji, niko tayari kugharamia maisha

203

yako. Ikiwa unataka usalama, mimi nitakupa. Na ikiwa una haja yoyote, sitachelewa kukutimizia. Afadhali ufuatane nasi katika msafara wetu, kwani tuna kila kitu cha kukuandalia."

Mtu wa Shamu alivutiwa sana na maneno matamu ya Imam ambayo hakuyatazamia. Kwa sababu ya kuona haya sana, machozi yakamdondoka kidevuni mwake. Hapohapo mwanga wa maarifa ukamulika katika moyo wake, na hisia ya mapenzi ikachemka katika moyo wake. Kisha akakubali Uimamu wa Imam Hasan AS kwa moyo safi kabisa na akasema:

"Mimi mpaka hivi punde tu nilikuwa nikiamini kwamba wewe na baba yako ni watu wabaya kabisa, lakini sasa ninahisi kwamba huo moyo wangu uliokuwa umejaa chuki na uadui dhidi yenu, sasa umejaa mapenzi na ikhlasi. Hakika hakuna mtu mwingine anayestahiki cheo hiki kitukufu isipokuwa wewe tu."

13 - KUVUNJA AHADI

207

Majukumu Mbalimbali

Binadamu hutambua majukumu yake ya kila aina katika vipindi mbalimbali vya maisha yake wakati inapotafakari juu ya masuala tofauti ya kimaisha na inapoyapima mambo kwa kutumia akili yake. Ana wajibu wa kuzikubali taratibu zote alizowekewa katika naisha yake na kuzifuata kanuni zilizowekwa kwa ajili ya kumkamilisha na kumfanikisha. Kwa ufupi, ni lazima "mwendo wake ukubaliane na mahitaji halisi ya mwili na •oho yake. Ni lazima tukubali wajibu wetu katika vipengee vyote vya kimaada na kiroho. Akili na dhamiri ya mtu zinamwambia juu ya wajibu huo na zinamtaka itekeleze majukumu yake kwa uthabiti na ukamilifu ili cudhamini ustawi wajamii. Vivyo hivyo, akili na dhamiri ya. mtu zinamwonya aepukane na mambo yote yanayosababisha kupanguka mfumo wa maisha, na kuzorotesha na kuanguka utu wake. Kuwa na jukumu kunasaidia sana kukuza sifa njema za kiroho na kimaadili, kumpatia mtu uhuru wa kweli na (umwonyesha sera inayoafikiana na mfumo sahihi. majukumu ya namna kwa namna yameenea katika vipengee vyote vya maisha ya mtu, hivyo, anapaswa kuyatekeleza mpaka mwisho wa uhai wake. Mtu anayekubali na kujitwika jukumu lolote lile anawajibika kulitekeleza kufuatana na uwezo wake.

Kutojali wajibu na kukiuka mpaka wake ni dalili ya kutojua kanuni za maisha na ni chanzo cha maafa na

208

kushindwa katika mustakabali. Hakuna kosa kubwa kama kutaka kuzipuza nyadhifa zetu, au kutofuata kanuni za lazima kwa kudhania kuwa ni uhuru wa mtu, au kujifikiria kwamba mtu ana uhuru wa kufanya alitakalo bila ya kujali utaratibu wowote. Kutokuwa na hisia ya kuwa na wajibu kunaleta madhara makubwa katika jamii, kunaleta hitilafu kati ya pande mbili za watu, na husababisha kutokea mgawanyiko katikajamii ambao hauwezi kuungwa tena. Hivyo, ni marufuku kuvuruga wajibu wa watu wengine kwa ajili ya kuridhisha matamanio yetu. Wale waliotegeka katika mtego wa matamanio hupendelea zaidi maslahi yao ya kibinafsi na hufuatia matakwa yao kuliko kutekeleza wajibu wao, bali huyapa umuhimu zaidi matakwa yao ya kinafsi. Watu kama hao huanza kuharibika katika mazingira kama hayo, wala hawawezi kamwe kuwa wanadamu wakamilifu.

Dk. Carl amesema:

"Binadamu asiyefuata sheria haweza kabisa kufanana na mwewe anayeruka katika anga pana, bali anafanana zaidi na mbwa aliyekimbia kwa bwana wake akijikuta anazurura huku na huko kati ya magari mengi yanayopita barabarani. Bila shaka mtu kama huyo anaweza kutenda kwa mujibu wa matamanio yake na kwenda popote pale kama mbwa. Lakini yeye huwa ni mpotevu zaidi, kwa sababu hajui aende wapi na ajilinde vipi kutokana na hatari inayomzunguka.

"Sisi tunajua kwamba kuna kanuni za kimaumbile, hivyo, ni lazima tufikirie kwamba maisha ya mwanadamu yamewekewa kanuni na misingi. Sisi

209

tusidhani kwamba tuko mbali na mfumo wa maumbile na tuko huru kutenda kwa mujibu wa matakwa yetu. Hatutaki kuelewa kwamba uongozi wa maisha kama vile uendeshaji wa gari unapaswa kutiiwa sheria zake. Lakini leo tunadhani kwamba shabaha ya mwanadamu ni kula, kunywa, kulala, kushibisha hamu ya kijinsia, kumiliki gari na redio, kwenda sinema, kucheza dansi na kuchuma mali tu. Kila mtu anaishi kama vile anavyopenda, akivuta sigara, akistarehe kwa uzembe na akilewa.

"Jambo lililo muhimu zaidi kuliko kitu chochote kingine kwa jamii ya wanadamu ni nidhamu. Nidhamu hii haiwezi kudumu kama sheria zake hazifuatwi. Wenye kutegemea uwezo wao wa kidhati na juhudi zao, huyatazama mambo ya kimaisha kwa mtazamo wa akili na mantiki, na huwa na uwezo kamili katika kutekeleza majukumu yao mbalimbali. Huupanga utaratibu wa maisha yao kufuatana na msingi wa uaminifu na ukweli, na huyapokea majukumu yao kwa mikono miwili. Pindi wanaposhindwa hufurahi pia, kwa sababu kushindwa huko kunatokana na juhudi zao za kutekeleza majukumu yao.

Ni lazima tuutafute ufanisi katika furaha ya kweli, na tuitafutie roho utulivu. Wale wanaoutikia mwito wa dhamiri zao watapata utulivu kamili wakati wa dhiki na masaibu. Kutosheka moyoni ni malipo mema yanayotolewa kwa ajili ya kutekeleza wajibu; na hisia hiyohiyo ya furaha inayotoka moyoni ndiyo inayomfanya mtu atambue wajibu wake.

210

Thamani ya Ahadi na Ubaya wa Kuzivunja

Wajibu mkubwa kabisa wa mtu katika maisha yake ni kutekeleza ahadi na mapatano aliyoahidi kutekeleza. Kila mtu awe ni mfuasi wa dini au itikadi yoyote ile, anajua ubaya wa kuvunja ahadi na uzuri wa kuweka ahadi katika mambo yote ya kibinafsi na kijamii. Utambuzi wa haja ya kutekeleza ahadi ni rasilimali ya kimaumbile ya mwanadamu na utekelezaji wake hutokana na malezi sahihi ya kipawa hicho. Utambuzi huo hudhamini ufanisi na mafanikio ya mtu. Hapana shaka kwamba msingi unaowekwa katika dhamiri ya mtu udogoni mwake unaathiri katika kiwango cha kutoa matunda kwa wingi au kwa uchache. Hivyo, hapa panaonekana waziwazi umuhimu wa kuzingatia malezi sahihi yanayosimamisha msingi wa tabia njema ya mtu, kutumia vizuri matokeo ya maana na ya thamani ya malezi mema, na kujiepusha na mambo yanayotia doa msingi wa maumbile ya mtu.

Kimaadili, mapatano yoyote wanayoafikiana watu wawili, yawe ya kikauli au kimaandishi, yana thamani na yanapaswa kuheshimiwa, hata kama hayakudhaminiwa kisheria au si rasmi. Kuvunja ahadi ni sawa na kutoka katika uungwana. Ni kitendo cha kishenzi kwenda kinyume na mapatano pasina kuwepo makubaliano baina ya pande mbili kabla yake.

Mshairi mashuhuri wa Kiajemi, Buzurgmehr, amesema:

"Kuvunja ahadi humweka mtu mbali mno na

211

uungwana."

Mtu anayepotoka kwenye njia iliyonyooka kwa kuvunja ahadi kwa urahisi, hupanda mbegu ya kuchukiwa na kukataliwa na watu kwa sababu ya mwendo wake mbaya. Mtu kama huyo hujitia katika fedheha ya daima kwa kusema maneno yanayopingana ili kuficha aibu kubwa ya kimaadili. Lakini mwisho wake hatapata faida yoyote ila ni kuthibitisha unafiki na uwongo wake.

Kwenda kinyume na mapatano huleta fitina na ugomvi katika jamii kuliko kitu chochote kingine, na kuenea kwake husababisha kudhoofika na kuanguka kwa jamii. Mafungamano yasiyo onekana kati ya watu hudhoofishwa na tabia ya kuvunja ahadi. Hapana shaka kwamba kutokuwepo uaminifu na uelewano katika mazingira fulani huharibu nidhamu ya maisha kwa kadiri kwamba watu huwa hawaaminiani, na hata rafiki mmoja huwa hamwamini rafiki mwenzake. Kati ya maadili maovu ya siku hizi ambayo yamewachafua watu kwa namna mbalimbali, udanganyifu na uvunjaji wa ahadi ndio uliotia fora. Tabia ya watu kujionyesha kuwa ni wazuri ndiyo iliyoshika mzizi sana. Katika jamii wanapatikana watu ambao mbali ya kutotekeleza na kutojali ahadi na mapatano yoyote yale, huamini kwamba udanganyifu na ujanja wao ni aina moja ya uerevu na ni chombo cha kujiendeleza! Kwa bahati mbaya, hila hiyo imewaambukiza watu wengine wengi.

Kutimiza ahadi ni njia mojawapo inayoleta uelewano kati ya watu na ni msingi wa ufanisi wa jamii. Huweka athari yake juu ya kila kipengee cha maisha ya

212

watu na ni chanzo cha kutoa natija nzuri ya mafanikio na maendeleo.

Katika zama za utawala wa dhalimu Hajjaj bin Yusuf, walikamatwa baadhi ya Khawariji na wakaletwa mbele yake. Hajjaj akachungua utetezi wao na kila mmoja akamhukumu adhabu fulani. Ilipofika zamu ya kutolewa hukumu ya mtu wa mwisho, ikasikika sauti ya adhana. Hajjaj akajitayarisha kwenda kusali na akamkabidhi mfungwa huyo mlinzi mmoja na kumwambia: "Mweke kwako usiku wa leo, na kesho mlete kwangu nimhukumu."

Mlinzi akatoka kwenye kasri ya Hajjaj pamoja na mtuhumiwa. Walipokuwa njiani, mtuhumiwa akamwambia mlinzi: "Mimi simo katika kikundi cha Khawariji, na nakataa tuhuma hiyo. Mimi nina matumaini kamili juu ya huruma na rehema za Mwenyezi Mungu kwa sababu nimefikishwa mbele ya Hajjaj bila ya kufanya kosa lolote. Sasa nakuomba kwa hisani yako niruhusu usiku huu nikae na ahli na watoto wangu na niwape wasia wangu. Na mimi nakupa kauli kwamba kesho nitarejea kwako asubuhi na mapema."

Mlinzi alimyamaza kimya, lakini alipoombwa sana na mfungwa huyo, akaridhika na akampa ruhusa ya kwenda kwake. Lakini mara tu baada ya kuondoka, akaanza kuingiwa na hofu na wasiwasi na akajuta kumruhusu. Akawaza moyoni mwake: "Kwa kumkubalia mfungwa huyo, nitamhamakisha Hajjaj na kujitia matatani." Usiku huo aliupitisha kwa wasiwasi mpaka asubuhi. Asubuhi na mapema, mlango ukagongwa, na alipoufungua alishangaa kumwona

213

mfungwa amefika. Alipoona hivyo, hakuweza kuficha mshangao wake. Akamwuliza mfungwa: "Kwa nini umerejea kama ulivyoahidi?" Mfungwa akasema:

"Yeyote anayetambua Utukufu na Uwezo wa Mwenyezi Mungu na akamweka Mola wake kushuhudia ahadi aliyoweka, ni lazima atimize ahadi hiyo."

Mlinzi akampeleka mfungwa kwa Hajjaj na akamwelezea kisa chote kilichotokea. Ingawa Hajjaj alikuwa katili na dhalimu, lakini alivutiwa mno na imani na uaminifu wa mfungwa huyo, hivyo, akatoa amri afunguliwe. Kisha akamwuliza mlinzi: "Je, unapenda nikutunze mfungwa huyu?" Mlinzi akajibu: "Ukinifanyia hisani hiyo nitakushukuru sana." Hajjaj akamtunza mlinzi mfungwa huyo, na mlinzi baada ya kutoka nje ya kasri ya Hajjaj pamoja na mfungwa huyo, akamwachilia huru.

Ikiwa kwa mfano, shirika moja litadharau wajibu wake na litaipuza mikataba yake iliyofunga, hapana shaka kwamba kutotekeleza mikataba hiyo kutaharibu heshima na itibari yake. Mwisho wa shirika kama hilo linaloshindwa kutekeleza mikataba yake ni kuvunjika na kufilisika tu. Hakuna kitu kinachothibitisha na kuimarisha jamii kama kuaminiana. Ikiwa maingiliano ya watu yatasimama juu ya msingi wa kuaminiana na kila mmoja atasadiki kauli ya mwenziwe kama vile unavyothaminiwa waraka rasmi, basi hapana shaka kwamba maisha yenye ufanisi yatapatikana katika jamii hiyo. Ikiwa watu watatekeleza mikataba yao na watatimiza ahadi zao kwa kuchukulia kuwa ni wajibu usioweza kukataliwa, hapana shaka, wataaminiana na

214

watathaminiana. Kwa mfano, ikiwa mwuzaji atampa mnunuaji bidhaa alizonunua katika wakati aliomwahidi, au ikiwa mdaiwa atalipa deni lake siku ile aliyoahidi, basi kutokana na kuwepo hali kama hiyo, ugomvi mwingi utaondoka na thamani ya maisha itapanda na kuwa bora zaidi.

Sharti la kwanza kabisa la kuandikiana mkataba ni mtu kuangalia uwezo wake na kukwepa kufunga mkataba au kuweka ahadi ambayo huna uwezo wa kuitimiza. Kwa hivyo, ikiwa mtu ataahidi kutekeleza jambo fulani na akashindwa kulitimiza, atastahiki kulaumiwa na watu.

Uislamu Wakataza Kuvunja Ahadi

Binadamu anahitaji mwendo wa kiakili katika mazingira ya maisha ili aweze kuwa na sifa za ubinadamu halisi. Mafanikio ya kwanza ya jamii ya wanadamu yanategemea kuwepo umoja na usawa kati yao. Kwa hivyo, inampasa kila mtu arekebishe tabia yake ifuatane na msingi wa ukweli na uaminifu, na ajiepushe kabisa na kila jambo linalosababisha utengano kati ya watu. Ikiwa katika jamii moja thamani ya kutimiza ahadi au mapatano itatokana na imani na maadili yake mema, basi hapana shaka kwamba mapatano hayo yatakuwa madhubuti kuliko waraka wowote.

Kuvunja ahadi kunachukiwa mno katika Uislamu kwa kadiri kwamba Waislamu hawaruhusiwi kuvunja ahadi hata kama wameifunga na watu waovu na

215

mafisadi.

Imam Baqir AS amesema:

"Mwenyezi Mungu Mtukufu hakumruhusu mtu yeyote kwenda kinyume katika mambo matatu: Kuweka amana ya mwema au mwovu; kutimiza ahadi ya mwema au mwovu; na kuwatendea mema wazazi wema au

waovu.

(al-Kafi,]?.. 2,uk.l62)

Qur'ani Tukufu inawasifu waumini kwa sifa hii:

"Na ambao ni waangalifu kwa amana zao na ahadi

zao (al-Mu'minuun, 23:8)

"Na timizeni ahadi, kwa hakika ahadi itaulizwa."

(Banilsrail, 17:34)

Mtume Muhammad SAW ametaja kuvunja ahadi kama ni alama mojawapo ya unafiki:

"Mwenye kuwa na sifa nne (zifuatazo) ni mnafiki;

na hata akiwa nayo mojawapo kati ya hizo pia atasifika kwa unafiki isipokuwa aiache: Mwenye kusema uwongo anapozungumza; mwenye kuvunja ahadi anapoahidi;

mwenye kufanya hiana anapoaminiwa; na mwenye kufisidi anapogombana."

(Biharu 'l-Anwar,]2.. 15, uk. 243)

Katika waraka wa mwongozo aliomwandikia Malik Ashtar, gavana wa Misri, Imam Ali AS ameandika:

"Jihadhari usiwasimange raia zako kwa hisani

216

ulizowafanyia, wala usijione bora kwa ajili ya kazi unazowafanyia, na unapowaahidi usiende kinyume na ahadi zako. Hakika masimango huharibu hisani, na kujiona huondoa nuru ya haki, na kuvunja ahadi husababisha kuchukiwa na Mwenyezi Mungu na watu. Mwenyezi Mungu anasema: 'Ni chukizo kubwa mbeleya Allah kusema msiyoyatenda."1 (61:3)

(Mitstadriku 'l-Wasa'il,]-z.. 2, uk. 85)

Imam Ali AS amesema:

"Kutimiza ahadi hufuatana na uaminifu, nami sikijui kinga kinachokinga vizuri zaidi kuliko kutimiza ahadi."

(Ghuraru 'l-ffikam, uk. 228)

Uislamu umeupa umuhimu mkubwa ulezi wa watoto na umefafanua maamrisho kamili juu ya wajibu wa kimaadili wa wazazi. Ikiwa hawatafuata misingi ya kimaadili na hawatatekeleza wajibu wao, hawataweza kuwakuza watoto wao kwa sifa njema za kitabia, kwani athari ya matendo ni muhimu zaidi kuliko maneno na maonyo. Mtume amekataza kabisa kuwaahidi watoto bila ya kutimiza ahadi hizo. Amesema:

"Mtu asimwahidi mwanawe asipoweza kutimiza."

(Nahju 'l-Fasahah, uk. 201)

Dk. Alindi amesema:

"Nililetewa kumtibu mvulana wa miaka kumi na sita ambaye alikuwa akizidi kuiba siku baada ya siku. Kijana huyo alipokuwa na umri wa miaka saba au nane, siku moja babake alimlazimisha ampe bandia yake binti wa

217

mwajiri wake, hali ya kuwa bandia hiyo aliipata baada ya kusubiri kwa miezi mingi na kutumia juhudi zake zote kuweza kufanikiwa kupewa bandia hiyo kama tunzo. Kwa bahati, wakati babake alipomlazimisha ampe mtoto mwingine bandia yake, alimwahidi kwamba angemnunulia nyingine badala yake, lakini hakutimiza ahadi hiyo kwa kuwa alipuuza na alisahau. Siku moja, mtoto huyo aliyevunjika moyo wake na kutokwa na tamaa, aliiba kipande kimoja cha chokleti kutoka kwenye kasha la mamake. Siku aliyoletwa kwangu alikuwa amevunja mlango na kioo na akaiba. Haikuwa kazi ngumu kumrekebisha mwendo wake; nami nikafanikiwa kumbadilisha kwa sababu wazazi wake ndio waliofanya kosa la kisaikolojia hata mtoto akawa hivyo. Lau mwendo wake ungeendelea hivyo, basi mtoto huyo angekuwa mhalifu wa hatari badala ya kuwa mtu shupavu mwenye kujiamini."

(Ma Wa Farzandane Ma)

Imam Ali AS ameonyesha namna ya mtu kusuhubiana na mwenzake:

"Ukimchagua mtu kuwa rafiki yako, basi kuwa mtumishi wake na mwonyeshe uaminifu wako wa kweli na moyo safi."

(Ghuraru 'l-Hikam, uk. 323)

Anayestahiki kuwa rafiki ni yule mtu aliye na sifa nzuri za uungwana na ambaye urafiki wake unaweza kuburudisha na kutukuza roho ya mwenzake.

Mtume Mtukufu amesema:

218

"Mwenye furaha kayaya kuliko watu wote ni yule mwenye kuingiliana na watu watukufu na ambaye huendeana na watu bila ya kuwadhulumu, huzungumza nao bila ya kuwadanganya, na huahidiana nao bila ya kuvunja. Hakika mtu kama huyu amekamilisha murua wake, amedhihirisha uadilifu wake, na anastahiki udugu na urafiki wake."

Dk. Samuel Smiles amesema:

"Ukiishi pamoja na watu wenye roho safi na tukufu, utahisi kwamba nguvu ya ndani ya roho na tabia yako hukupeleka kwenye utukufu. Kufanya urafiki pamoja na watu walio na akili, murua na uzoefu mkubwa zaidi kuliko sisi kuna thamani kubwa mno, kwa sababu kusuhubiana nao hutia roho mpya katika nafsi (ya mtu), hutufunza mwendo na sira ya maisha, na hurekebisha mawazo na maoni yetu juu ya wengine. Ikiwa watu hao ni wathabiti zaidi kuliko sisi, nasi pia tutakuwa wathabiti kutokana na kuingiliana na kukaa nao. Tutafaidika na nguvu zao za kiroho, kwani usuhuba wao huzidisha nguvu zetu za kiroho, hukuza malengo yetu ya duniani, na hututayansha kutekeleza mambo yetu ya kimaisha na kuwasaidia watu wengine. Kufanya urafiki na mtu mzuri hutoa matunda mema na mazuri, kwa sababu tabia njema ni kama taa inayoangaza pembezoni na karibu nayo."

Kwa kuzingatia maelezo ya juu, wajibu wa kila mtu kufuatana na ahadi, mapatano na makubaliano yake unafahamika waziwazi.

14 - KHIANA

221

Kuaminiana na Kutekeleza Wajibu

Hisia ya kuaminiana ni msingi wa jamii iliyo nzima na imara. Jamii inaweza kuwa na furaha na ufanisi vakati mzizi wa uaminifu unaposhika barabara kati ya vatu. Lakini watu wanapokiuka mipaka ya wajibu wao la wakafanyiana khiana, hapo uzima wa kijamii huanza cudhoofika.

Kuna kanuni mbalimbali zinazoratibu vipengee vyote vya maisha ya mwanadamu. Kila mtu ana mchango wake katika kanuni hizo kwa kuwajibika kwake kiakili, kimaumbile na kidini kuzifuata ili kwamba maisha ya wanadamu yang'are kwa uaminifu na kuaminiana. Haiwezekani kabisa kufuta wajibu wa ntu katika kamusi ya maisha yake au mtu kuyasahau yale aliyofadhiliwa na Mwenyezi Mungu na jamii na "kuyafanya hayana maana. Kimaumbile binadamu hana budi ila kuishi kijamii na wenzake, na kwa kuwa kunakuwepo haki na wajibu katika uhusiano kati ya vatu, hivyo, hulazimika kufuata utaratibu wa sheria ili kuhifadhi mfumowajamii kutokana na machafuko na natatizo. Kuishi huko kwa ushirikiano na wenzake unarahisisha njia ya ufumbuzi wa matatizo yao. Ingawa kutekeleza majukumu ni kazi ngumu inayohitaji kujitolea na kuvumilia matatizo, na binadamu daima hupendelea kupata ufanisi na mafanikio bila ya kutaabika kwa kuwa ni sifa yake ya kiasili, lakini ni lazima tufahamu kwamba raha haipatikani ila kwa

222

kutekeleza wajibu, kama vile walivyosema wahenga:

"Raha ni malipo ya kutimiza wajibu."

Mtu mmoja anaweza kuwa na sehemu katika majukumu ya watu wengine kwa kadiri fulani, kwa sababu anapokwenda kinyume na wajibu wake husababisha athari mbaya katika maoni na fikra za watu, na vivyo hivyo, husababisha kutokea mabadiliko katika mwendo na matendo yao. Ufanisi wa kijamii una thamani zaidi kuliko ufanisi wa mtu binafsi, bali ni msingi na chanzo cha ufanisi wa watu. Kunyima haki za watu hakupatani na roho ya uadilifu wa jamii, bali huvunja muundo wa kijamii. Ni wajibu wa kila mtu kuheshimu roho, uhuru na heshima ya mwenzake. Watu ambao wanatambua wajibu wao kwa jamii na wanalipa kwa dhati fadhila wanazofanyiwa, mbali na kuaminiwa na watu na kupata mafanikio katika mashindano ya maisha, husababisha watu wengine pia wazidi kupata ustawi na ufanisi na kufanikiwa katika maendeleo yao.

Dk. Samuel Smiles ameandika:

"Wajibu ni kama deni alilonalo mtu. Yeyote anayetaka kuepukana na fedheha ya kupoteza itibari na kufilisika kimaadili ni lazima alipe deni lake. Na si rahisi kulipa ila kwa kukusudia kikwelikweli, kujitahidi na kujishughulisha kimatendo katika mambo ya kimaisha kwa muda mrefu. Kutekeleza wajibu ni kazi ya pekee iliyo muhimu kwa mtu tangu siku anayoingia katika uwanja wa maisha mpaka siku anayotoka. Kila palipo na uwezo na nguvu, wajibu huwa hapo pia, kwa sababu binadamu ni kama mtumishi mwenye wadhifa wa kutoa huduma na faida kwa ajili yake na wengine. Ni wajibu

223

unaotokana na hisia ya kutaka uadilifu na mapenzi. Hatuwezi kuchukulia kuwa ni faradhi ya kidini au itikadi tu, bali ni msingi na kigezo kwa ajili ya kulinganisha na maisha yake. Athari na alama za utekelezaji wa wajibu hudhihirika katika mwendo na amali za mtu ambavyo ni kioo cha dhamiri na nia (hiari) yake. Hisia ya kutambua wajibu ni neema na kipaji kikubwa kabisa kwa mataifa ya dunia. Kila taifa lenye watu wenye hisia hiyo tukufu huweza kuwa na matumaini juu ya utukufu na ubora wao katika mustakabali. Lakini ikiwa taifa moja litakosa hisia hiyo na badala yake litapenda anasa, ubinafsi na ufakhari, basi ni lazima taifa hilo lenye mkosi lililiwe, kwa kuwa kwa mujibu wa kanuni ya kimaumbile ni lazima liangamie karibuni au baadaye!"

Khiana na Hatari Zake

Hatuwezi kukataa kabisa kwamba kuna visababu mbalimbali vinavyosababisha ufisadi na upotofu katika jamii ya leo, lakini tunapochungua vyema masuala ya kimaadili na kinafsi kuhusu visababu hivyo vinavyoharibu na kudunisha jamii, tunaona kwamba chanzo muhimu kabisa cha mkosi huo ni kutawala khiana katika fikra za watu na kuenea katika mambo yote ya maisha yao. Hatari inayoikabili jamii ya leo kutokana na kuenea khiana na ambayo huharibu uzima wa kiroho wajamii ni kubwa na ya kusikitisha mno.

Khiana au kutokuwepo uaminifu huchafua kioo cha roho na huufanya mwendo wa hisia na fikra uende kombo na upotoke.

224

Sifa hii huota mzizi katika moyo wa mtu wakati matamanio yake yanapopindukia mpaka, hivyo, badala ya kupata maongozi ya imani na akili, fikra zake za kishetani humwamrisha akubali uduni na udhalilifu.

Kila mtu katika mazingira yake anahitajia kuaminiwa na wengine. Huenda mhunzi au mfanyabiashara mmoja akapata faida nyingi kwa kufanya khiana na akaweza kuficha kwa ujanja fedheha hiyo kwa muda fulani, lakini mwisho wake siku moja pazia hilo litafunguliwa na atapoteza itibari yake ambayo ndiyo rasilimali yake iliyo kubwa kabisa na vilevile kuharibu heshima na utukufu wa tabaka lake.

Mwenye kufanya khiana huugua aina moja ya maradhi ya kinafsi kwa kuwa hukitazama kila kitu kwa ubaya. Chanzo cha kusumbuliwa na wasiwasi na uduni huo ni lazima kitafutwa katika dhati yake.

Ni wazi kwamba utulivu wa roho na ustawi wa umma hutegemea usalama. Hali ya fujo na kutokuwepo usalama inayotawala katika mazingira ya jamii kutokana na kuenea khiana ni sawa na kuuawa kwa malaika wa uadilifu na kuangamizwa msingi wa muundo wa uhai wa taifa hilo. Naam, mahali pasipokuwepo amani na usalama, huwa hapana uhuru, udugu wala ubinadamu pia. Khiana haihusiki na mambo mahsusi tu, bali ina maana pana na inahusika na amali zote za mtu. Tunapochunguza kila kauli na amali, tunaona kwamba kila moja ina kiwango maalumu ambacho kikipindukia husababisha mtu atoke katika uaminifu na muamana na apige hatua katika njia ya khiana na udanganyifu.

Inasemekana kwamba mkuu mmoja alimwusia haya

225

mwanawe:

"Ewe mwanangu! Baki maskini na mhitaji na waachie wengine watajirike kwa kufanya hila na khiana. Ishi bila ya kutaka cheo au madaraka, na waachie wengine wang'ang'anie vyeo vikuu na madaraka kwa macho makavu. Vumilia taabu na shida, na waachie wengine wapate muradi wao kwa kudanganyana na kupendekezana. Usijali kuingiliana na kukaa na watu wakubwa, na waachie wengine washindane katika kujipendekeza kwao. Ni afadhali uvae nguo ya murua na uchaji, kwani nywele zako zitakapokuwa nyeupe na utakapokuwa huna hata doa moja nyeusi katika jina na utukufu wako, hapo mshukuru Mwenyezi Mungu kwa kuwa tayari kuyapokea mauti kwa moyo wa furaha na

amani."

Uaminifu ni rasilimali ya uungwana. Mwaminifu ni mtu anayeaminiwa na watu ambaye huishi maisha yaliyojaa utukufu. Huhifadhi amana za watu katika hali yoyote ile. Huo mwendo wake ndio unaompatia uzoefu katika mambo mbalimbali na humwongoza katika njia ya maisha ya uaminifu.

Uislamu Walaani Khiana

Mwenyezi Mungu amezitaja sheria alizowatungia waja Wake kama ni amana, na amekataza kabisa kufanya khiana ya aina yoyote:

"Enyi mlioamini! Msimfanyie khiana Allah na Mtume na mkakhini amana zenu na hali mnajua."

(al-Anfaal, 8:27)

226

Vilevile Mwenyezi Mungu amesema:

"Hakika Allah anakuamrisheni kuzirudisha amana kwa wenyewe."

(an-Nisaa',4:5S)

Imam AliAS amesema:

"Kikomo cha khiana ni kumfanyia khiana rafiki mpendwa na kuvunja ahadi."

(Ghuraru 'l-Hikam, uk. 505)

Vilevile amesema:

"Mtu mwovu kuliko wote ni yule asiyeamini kuweka amana wala hajizuii kufanya khiana."

(Ghuraru 'l-Hikam, uk. 446)

"Jihadharini na khiana kwani ni dhambi mbaya kabisa; na kwamba mwenye kukhini ataadhibiwa katika Moto kwa khiana yake."

(Ghuraru 'l-Hikam, uk. 150)

Imam Sadiq AS amemwusia sahaba wake mmoja hivi:

"Halahala na kusema ukweli na kurejesha amana kwa mwema au mwovu, kwani sifa mbili hizi ni ufunguo wa riziki."

(Safinatu 'l-Bihar,]z. 1, uk. 41)

Uislamu ukiwa na utaratibu wa kudumu na maamrisho matukufu unawaita watu wote watekeleze wajibu na majukumu yao ili waweze kuishi maisha yenye

227

ufanisi na uthabiti, na unausia sana kuhifadhi amana za watu.

Imam Zaynul Abidin AS amesema:

"Halahala na kuweka amana. Naapa kwa yule aliyembaathi Muhammad kwa haki kuwa Mtume, kwamba lau mwuaji wa babangu Husayn bin Ali angenipa upanga ule aliomwulia kumwekea amana, nisingemfanyia khiana."

(Amali as-Saduq, uk. 149)

Kufanya khiana kunachukiwa na kunashutumiwa mno katika Uislamu kwa kadiri kwamba ikiwa katika masharti maalumu mtu atafanya khiana katika amana za watu, basi atahukumiwa kwa kosa la wizi na ufisadi na atakatwa mkono. Uislamu umeweka sheria kali sana kumwadhibu mwenye kufanya khiana ili kwamba heshima na haki za jamii ziheshimiwe na usalama wa umma uhifadhiwe. Lengo ni kuhuisha roho ya kutambua wajibu katika jamii na kuandalia uwanja wa kutokeza jamii bora na inayofaa.

Kwa kuwa kila kitendo cha kihalifu na kisichofaa ni chanzo cha kumwangusha mwanadamu, na kina athari mbaya katika maisha ya mwenye kutenda, hivyo, mwisho wake humsibu matokeo mabaya katika dunia hiihii.

Mtume Mtukufu amesema:

"Mwenye kutenda kitendo kiovu atalipwa (hapahapa) duniani."

(Nahju 'l-Fasahah, uk. 592)

228

Dk. Rose Keen amesema:

"Kila kosa ninalofanya katika maisha yangu litasimama dhidi yangu, litanyima raha na furaha na litachafua uwezo wangu wa kufahamu na kutambua. Lakini kinyume chake, kila juhudi niliyoifanya na kuionyesha, na kila ukweli niliouonyesha kwa maneno na vitendo utafuatana na kuambatana nami, na utanipa nguvu na hima ya kufikia matumaini na malengo yangu. Kanuni ya kimakanika (mechanical law) inayosema kwamba kanitenzi (action) na kanizuizi (reaction) zina ukubwa sawa kila moja inahusika pia katika elimu ya maadili. Amali njema na mbaya, kila moja ina athari ya kutenda na kutendewa kwa mwenyewe. Vilevile athari hiyo huwaathiri wale wanaomfuata."

(Akhlaq)

Imam Ali AS amesema:

"Uaminifu katika (kuweka) amana ni alama ya usafi wa mwenye imani."

(Ghuram 'l-Hikam, 453)

Vilevile amesema:

"Khiana ni dalili ya upungufu wa uchaji na utovu wa dini."

(Ghuraru 'l-Hikam, uk. 53)

Imani ni silaha ya kujitetea kwa ajili ya roho na ni kitu cha pekee kinachoweza kupenya ndani ya roho ya binadamu na kudhibiti vyema amali za mtu. Nguvu za ajabu za imani huyazindua majukumu ya kibinafsi na kijamii, huuzuia ufisadi kuenea katika mazingira,

229

huishawishi jamii kuelekea kwenye mwenendo mwema, na huzuia kufurika kwa mabaya na khiana. Kwa hivyo, wazazi wana wajibu muhimu wa kuratibu mustakabali wa ufanisi wa watoto wao, kuangalia tabia zao za mwanzo, kuhuisha imani ya Mwenyezi Mungu katika nyoyo zao, na kuimarisha sifa njema katika shakhsia zao.

Imam Sajjad AS amesema:

"Una wajibu wa kumlea (mwanao) kwa adabu nzuri, kumwongoza kwa Mola wake Mtukufu, na kumsaidia katika kumtii."

(al-Wafi, uk. 127)

Dk. Raymund Peach ameandika:

"Haitoshi kufuata dini katika ukoo kijuujuu tu. Hapana; wazazi waangalie kwa makini na kwa mtazamo wa imani.mwendo, vitendo na hisia zote za watoto. Ondoeni madaha na ugumu katika dini na badala yake tieni misingi mitukufu ya dini ndani ya nyoyo zao safi. Mkifanya hivyo, imani na uthabiti wa watoto wenu utahifadhika katika wakati wa hatari kabisa wa maisha yao na utawazuia wasishindwe, wasiangamie na wasipotee."

rudi nyuma Yaliyomo endelea