rudi nyuma Yaliyomo endelea

Miongoni mwa majukumu yetu ya kimsingi katika ulimwengu wa maingiliano ni kuwa na moyo wa kusahau na kusamehe makosa na mabaya ya watu wengine. Kudumu kwa uhusiano kati ya watu

178

kunahitajia kuvumiliana kwao.

Utulivu wa hali ya juu kabisa unapatikana wakati watu wanapoendeana vizuri na wanapoishi kwa masikilizano.

Tusilisahau jambo hili kwamba hakuna mtu yeyote katika dunia hii asiyekuwa na aibu na upungufu fulani. Watu wenye kuwa na vipawa kamili na makini barabara ni wachache sana. Hata watu watukufu kabisa katika jamii wana dosari fulani. Kwa sababu hii, kila mtu anatakiwa kwa kadiri fulani avumilie jambo asilotazamia kutoka kwa mwingine na ayasamehe makosa na mabaya ya wengine, kwani mara nyingi amani na masikilizano hayapatikani ila kwa njia ya kusamehe, na mapenzi hayapatikani ila kwa maelewano.

Kila mtu ana mwendo wake maalumu unaotokana na hali yake ya kimaadili na kinafsi. Msamaha ni mojawapo kati ya sura nyangavu kabisa ya utukufu na udhibiti wa nafsi, na ni aina moja ya ushujaa na uungwana. Mwenye kuwa na sifa hiyo kwa kadiri ya kutosha na mbali ya kuwa na nguvu akasamehe, hufaidika kwa kuwa na uhakika na usafi wa moyo ambao hauwezi kulinganishwa na kitu chochote kingine. Kusamehe kunaitukuza na kuiimarisha roho ya mtu, na ni kipawa ambacho kwacho hububujika upole na wema. Kusamehe humtoa mtu kwenye kifungo cha ubinafsi. Ingawa ni shida sana kusahau madhara na mabaya ya wengine na moyo huumia sana mwanzoni, lakini kwa kadiri mtu atakavyovumilia katika njia hiyo ndivyo atakavyoweza kupunguza sana masumbufu yake ya rohoni na mwisho wake akawa ni mtu msamehevu.

179

Hapana shaka kwamba kusamehe kunaweka athari nzuri katika moyo wa adui kwa kadiri kwamba huweza kuleta mabadiliko katika fikra na mwendo wake. Chuki nyingi zimeondoshwa kwa kusamehe, na uadui mkali na wa kizamani umeondoshwa na mahali pake kukaa usafi wa moyo na upendo. Adui mchokozi hulainika na husalimu amri mbele ya mtu aliyejizatiti kwa silaha hii kali na kwa fikra za kiungwana.

Mwanachuoni mmoja amesema:

"Kimojawapo kati ya vipawa vikubwa kabisa vya binadamu ambavyo wanyama wengine hawakufaidika navyo ni hisia ya kusamehe makosa ya wengine. Mtu anayekuudhi huwa kwa wakati huohuo hukupa fursa nzuri ya kumsamehe na kuona utamu wake. Tumefunzwa kuwasamehe maadui zetu lakini hatukuambiwa tusiwasamehe marafiki zetu. Hivyo, ni wazi kwamba ni lazima tusahau mabaya tuliyotendewa na wengine. Unapomlipizia kisasi adui wako huwa ni sawa naye, lakini unapomsamehe huwa ni bora kuliko yeye, kwani yeye huwa ni mwovu, nawe huwa ni msamehevu. Huenda tusifanikiwe tunapotaka kulipiza kisasi, lakini kusamehe ni njia bora kabisa ya kulipiza kisasi. Kwa kusamehe tunaweza kuwashinda maadui zetu bila ya kupigana na kuwafanya wainamishe vichwa vyao mbele ya utukufu wetu. Kwa hivyo, kuacha chuki na kukwepa uadui ni shambulio kubwa kabisa lenye kuwashinda mahasimu wetu. Tunapotendewa maovu, tuwatendee mema, kwani kulipa mema kwa mabaya uliyofanyiwa ni siasa ya kidini ambayo kwayo

180

hupatikana amani duniani."

Madhara Yatokanayo na Uadui

Kati ya anuwai ya maradhi ya hatari ya kimaadili yanayompata mtu, hakuna hata moja yaliyokuwa na madhara makubwa kwake kama maradhi ya chuki na uadui. Uadui ni miongoni mwa maafa makubwa ya ufanisi na utulivu unaotokana na tabia mbaya ya hasira na ambao kwao huvuruga uthabiti wa kiroho wa mtu. Huenda kutokana na sababu fulanifulani hamaki ya mwenye hasira ikapoa kwa muda, lakini hamaki hiyohiyo ikawa ni moto uliofunikwa chini ya majivu ambao unaweza kutoa cheche za chuki na uadui zitakazounguza na kuteketeza mazao ya ufanisi na utulivu.

Kama vile ambavyo kusamehe kunaonyesha utukufu na umakini wa nafsi ya mtu na kunaleta usalama na umoja, vivyo hivyo, uadui na uhasama unaonyesha roho ya chuki na ni chanzo cha mfarakano na ugomvi. Ingawa uhasama hufanywa ili kutuliza misukosuko ya ndani, lakini madhara anayopata mtu kwa kulipiza ubaya kwa ubaya huwa ni makubwa zaidi kuliko madhara anayopata kwa njia nyingine, kwani maudhi licha ya kuwa ni shida kuvumilia, mwisho wake huondoka, lakini uhasama unapoota mizizi huchoma moyo wa mtu kama miba ya sumu na humkera daima. Isitoshe, uadui hauwezi kuondoa ubaya, bali hulipanua na kulichimba zaidi donda. Kwa kawaida, uhasama humfanya hasimu ajitetee zaidi na alipize kisasi.

181

Wakati mwingine matokeo ya uadui huwa machungu mno kwa kadiri kwamba huwa hayumkiniki kurekebisha uharibifu unaotokana nao. Huenda mtu katika umri wake wote akaungua moyo wake na akateseka roho yake kutokana na kosa kubwa alilofanya la kuweka chuki, kutotumia akili na kutofikiria matokeo mabaya ya kufanya ugomvi. Katika kamusi ya maisha ya baadhi ya watu, hakuna neno 'samehe' kabisa, bali 'uadui' na mishabaha na minyambuliko yake ndiyo iliyojaa humo. Kinyongo na hasira kali hutumia nguvu zote katika kulipiza kisasi na kujenga chuki kati ya watu. Tabia ya kupandwa na hasira haraka huandalia uwanja wa chuki. Mtu mwenye moyo dhaifu na mwepesi wa kuhamaki havumilii kusikia akikosolewa au akichambuliwa hata kidogo. Kinyume chake, watu wenye nyoyo safi na madhubuti huchukulia kukosolewa na kuchambuliwa kwao kuwa ni fursa nzuri ya kujirekebisha.

Mwanachuoni mmoja amesema:

"Kushikwa na hasira sana ni dalili ya kutopevuka akili ya mtu, kwani huenda mtu anayekosoa huwa hana nia ya kumtukana au kumdharau mwenzake mwenye moyo dhaifu na mwepesi wa kukasirika. Hata kama kitendo hicho kitaonekana ni cha kutukana na kudharau, lakini huenda hakukusudia hivyo. Kwa hivyo, hakuna haja ya kuudhika na kulalamika. Uchambuzi uliokusudiwa kuudhi na kudharau, kama una ukweli na unaonyesha kosa lenyewe, basi huwa ni zinduo na funzo kwa mwenye akili badala ya kuwa chukio. Lakini uchambuzi usiokuwa na msingi na ukweli usitiwe

182

maanani, kwani unatokana na husuda na ubaya. Kitendo cha kuchambua bila ya msingi wowote ni kitendo cha kitoto, kichuki na kiwivu chenye lengo la kujitukuza kwa kuwadharau wengine. Hata hivyo, tusikereke na watu kama hao."

Moyo wa kuweka kisasi ni dalili ya unyonge wa nafsi. Maudhi na maonevu waliyoyapata udogoni mwao au waliyoyaona katika mazingira yao ya kijamii huweka athari mbaya na kinyongo katika nyoyo zao kwa kadiri kwamba nafsi zao husumbuliwa na aina moja ya chuki iliyotia fora. Kwa ufupi, kisasi ni njia mojawapo wanayoitumia wenye kujihisi duni ili kufidia kushindwa kwao. Hutumia visingizio mbalimbali kuwakera wengine na hutenda uhalifu wa hatari kulipiza kisasi! Njia mojawapo inayosaidia kusahau mabaya ya watu ni kuzingatia shabaha takatifu na aali ya maisha. Mwenye roho safi ni yule anayetazama malengo matukufu na yaliyo bora na huyapuuza mabaya na upinzani anaouona.

Sisi wenyewe ndio wenye hiari ya kudhibiti taathira ya ubaya katika roho, kubadilisha fikra moja kwa fikra nyingine, na kujibu ubaya kwa uzuri. Kwa hivyo, tunaweza kupunguza nguvu za taathira mbalimbali juu ya fikra zetu kwa kutegemea nguvu za matakwa yetu, na kwa njia hiyo tukapata nguvu za kutosha kuweza kuvunja hisia ya chuki ambayo huzisumbua roho zetu. Hakuna mtu atakayeweza kutusaidia tutakaposhindwa kutekeleza wajibu wetu.

Kisasi kina maumbo tofauti na kinajidhihirisha katika sura mbalimbali. Baadhi ya watu huvaa nguo za

183

urafiki na uongozi ili kuwaelekeza wapinzani wao kwenye mambo yatakayowafikisha kwenye mwisho mwovu na wenye misukosuko ili kwa njia hiyo waweze kulipiza kisasi kwa ujanja kabisa!

Mwanachuoni mmoja wa Magharibi ameandika:

"Chuki na uadui ni matokeo ya upumbavu hasa panapokosekana sababu maalumu. Tunaweza kuyatatua mambo mengi kwa urafiki, lakini ubinafsi hautuachii. Hutokea mara nyingine tukavunja urafiki kwa sababu ya adha ndogo kabisa tu, wakati tunaelewa kwamba kosa lao halikuwa kubwa hivyo hata wasistahiki kusamehewa. Kwa kweli, tutawezaje kuvumilia maonevu hayo juu ya wengine?"

Radiamali ya Imam Sajjad AS

Maisha ya viongozi wetu wa kidini yanatoa mafunzo ya utukufu, ubora na ubinadamu; na sifa zao za kiroho zinadhihirika katika sura bora kabisa.

Siku moja wakati masahaba walipokuwa kwa Imam Sajjad (Zaynul Abidin) AS, akaingia kwa ghafla mtu mmoja mwenye moyo mweusi ambaye alianza kumtukana Imam kwa maneno machafu sana. Imam akamsikiliza kwa utulivu na makini mpaka aliponyamaza na kuondoka barazani. Kisha Imam akawaambia masahaba zake:

"Nitapenda mnifuate kwenda kujibu maneno ya bwana huyo." Masahaba wakamtii na wakafuatana na Imam.

Imam alipofika mlangoni kwa bwana huyo,

184

akamwita. Bwana huyo mjeuri akajiandaa kwa ugomvi na akatoka nje ya nyumba. Imam akamwambia:

"Ewe ndugu yangu! Maneno uliyonituhumu kama yana ukweli, namwomba Mwenyezi Mungu anisamehe;

na kama hayana ukweli, namwomba Mwenyezi Mungu akusamehe na akuhurumie!"

Maneno matamu na ya upole ya Imam yaliathiri moyo mgumu wa bwana huyo na kuondoa kero aliyokuwa nayo moyoni mwake: Alama ya mabadiliko na majuto ilionekana usoni mwake, na machozi ya majuto yalimdondoka kidevuni mwake. Kisha akamwambia Imam kwa sauti laini iliyojaa adabu:

"Utukufu na ubora wako umesalimika na tuhuma hizo zisizokustahili. Mimi mwenyewe ndiye ninayestahili maneno hayo niliyoyasema."

(Kitabu 'l-Imhad, uk. 257)

Kwa njia hii, Imam Zaynul Abidin AS aliwafunza kimatendo wafuasi wake funzo la kusamehe, na aliwaonyesha namna msamaha ulivyoweza kuleta mabadiliko na ufanisi katika moyo wa mtu huyo.

Imam Ali AS amesema:

"Kutosamehe ni aibu mbaya kuliko zote, na kuharakiza kisasi ni dhambi kubwa kuliko zote."

{Ghuraru 'l-Hikam, uk. 537)

Vilevile Imam Ali AS amewasifu waungwana wanaosamehe makosa ya wengine, kwa kusema:

"Ni murua wa watukufu kusamehe makosa kwa haraka."

(Ghuraru 'l-Hikam, uk. 768)

185

Qur' ani Tukufu inawausia Waislamu wasamehe:

"... Na wasamehe na waachilie mbali. Je, nyinyi

hampendi Allah akusameheni? Na Allah ni Mwingi wa

msamaha, Mwenye kurehemu."

{an-Nuur, 24:22)

Mwenyezi Mungu anasema:

"Mazuri na mabaya hayawi sawa. Zuia (ubaya unaofanyiwa) kwa mema, tahamaki yule ambaye baina yako na yeye kuna uadui atakuwa kama ni rafiki mwandani."

(Fussilat, 41:34)

Mambo mazuri na mabaya hayawi kamwe sawasawa katika dunia hii. Hivyo, ni afadhali kulipa ubaya kwa amali njema kabisa ili kwamba yule aliyekufanyia ubaya na uadui awe ni rafiki yako wa karibu sana.

Msamaha huwa na thamani kubwa sana wakati mtu anapokuwa na uwezo na nguvu za kulipiza. Imam Sadiq AS ameihesabu sifa hii tukufu kuwa ni miongoni mwa sifa njema za Mitume na wachaji:

"Msamaha wakati wa (kuwepo) uwezo (wa kulipiza ubaya) ni miongoni mwa mienendo ya Mitume na wacha Mungu."

(Safinatu 'l-Bihar, jz. 2, uk. 702)

Amirul Muuminin Ali AS ameutaja msamaha kama ni silaha bora kabisa ya kuwapigia wapinzani:

"Mlaumu nduguyo kwa (kumfanyia) mema, na jiepushe na shari yake kwa kumfadhili."

(Nahju 'l-Balaghah, uk. 1150)

186

Imam Ali AS amefichua uhakika wa ndani wa maana ya kinyongo na chuki kwa kutoa usemi mfupi:

"Moyo wa mwenye kinyongo ni mgumu kuliko nyoyo zote."

(Ghuraru 'l-Hikam, uk. 178)

Mwanasaikolojia mmoja ameandika:

"Chuki ni hasira mbaya sana na haina huruma katika ugomvi. Mwenye chuki huwa tayari kutenda uovu mkubwa kwa kosa dogo tu. Ingawa wenye kuweka chuki huonekana wapole, wenye adabu na wenye ndimi tamu, lakini nyoyo zao ni kama volkano iliyolala lakini ndani mwake huchemka lava ya chuki na kisasi na hungoja fursa ya kwanza kulipuka na kuteketeza msitu na nyika, na rafiki na adui sawasawa."

(Ravankavi)

Wahaka na adhabu ya roho daima humtesa mwenye chuki. Imam Ali AS amesema:

"Kinyongo huadhibu nafsi na huzidisha adhabu yake."

(Ghuram 'l-Hikam, uk. 85)

Dk. Dale Carnegie ameandika:

"Tunapowafanyia chuki maadui zetu, huwa tunawafanya wadhibiti usingizi, chakula, mkandamizo wa damu, siha ya mwili na hata furaha na starehe zetu. Sisi wenyewe ndio tunaowapa nguvu za kutudhibiti. Chuki haiwasumbui wao hata kidogo, bali hugeuka mchana na usiku wetu kuwa balaa na Jahannamu kwa

187

ajili yetu."

(How to Win Friends and Influence People)

Wataalamu wa leo hufanya uchunguzi wao wa kisaikolojia juu ya maradhi ya kiakili na dhamiri ya mgonjwa, kisha hutibu. Imam Ali AS amesema:

"Dhamiri zinapotibiwa ndipo siri zinapojitokeza na kuonekana."

{Ghurant 'l-Hikam, uk. 490)

Sifa mojawapo ya kinafsi ya watu wenye chuki ni kwamba hawaoni raha mpaka wachukue kisasi juu ya maadui zao hapo ndipo moto wa ndani unapozimika."

Imam Ali AS amesema:

"Chuki ni moto wa ndanindani usiozimika ila kwa ushindi."

(Ghuraru 'l-Hikam, uk. 106)

Mwanasaikolojia mmoja ameandika:

"Kwa kawaida, mwenye chuki huwalazimisha wengine kunyamaza na kutii kwa kutumia ufidhuli na kitisho. Mwendo huo wa kuwaonea na kuwashinda wengine huonekana ni wa kawaida, wa halali na wa lazima kwa kadiri kwamba ikiwa mwenye chuki na kisasi atavumilia na atasamehe badala ya kuchukua kisasi, basi atajilaumu sana na kujiona mnyonge na dhaifu.

"Mimi namjua afisa mkuu wa kijeshi ambaye siku moja gari lake liligongana na baiskeli ya maskini mmoja. Maskini alianguka pamoja na majagi mawili ya mtindi aliyoyaweka nyuma ya baiskeli. Majagi yakavunjika,

188

mtindi ukamwagika na kutapakaa njia nzima na magurudumu mawili ya baiskeli yakapindana. Huenda makosa yalikuwa ni ya mpanda baiskeli, lakini kwa vyovyote vile, maskini huyo alistahiki apewe pole katika hali hiyo ya kusikitisha, si kwamba atukanwe na atolewe maneno makali na afisa huyo aliyepandwa na hamaki. Ingawa mpanda baiskeli aliumia lakini alikuwa jasiri, akajikokota na hakukaa kimya, bali akaanza kumjibu na kumtukana kwa maneno machafu sana akitoa bughudha zote zilizokusanyika moyoni mwake kwa miaka mingi aliyoonewa. Rafiki yangu alitaka kushuka garini kumpiga ngumi na kumtia adabu yule mwuza mtindi mjeuri aliyethubutu kumtukana afisa wa kijeshi. Mimi na rafiki yangu mwingine tuliokuwa garini tulimzuia, naye akatulia baada ya kumkataza. Lakini katika muda wote huo tuliokuwa wageni wa afisa huyo usiku ule, alitulaumu na alijilaumu mwenyewe kwa nini hatukumwacha amwonyeshe kilichomtoa kanga manyoa. Kwa ufupi, hakutusamehe wala hakujisamehe mwenyewe kwa kosa la udhaifu wake wa kumwachilia mbali na kumsamehe kwa nguvu mpanda baiskeli huyo." (Ravankavi)

Chuki hukoka moto wa hamaki. Imam Ali AS amesema:

"Chuki huwasha hasira."

(Ghuraru 'l-Hikam, uk. 21)

Mwandishi wa Ravankavi ameandika:

"Mwenye chuki asipopata matakwa yake hata kama

189

hayana maana, huhamaki sana na hatulii mpaka urushe sumu yake."

Moyo wa mtu hupoa anapokuwa hana hamaki wala uchungu. Imam Ali AS amesema:

"Mwenye kuondoa chuki hutuliza moyo na akili yake."

(Ghuraru 'l-Hikam, uk. 666)

Katika makala moja ya elimunafsi iliyochapishwa katika jarida moja, mwandishi ameandika:

"Mtu akijiepusha haraka na uasi, hasira na chuki, basi atasalimika na ugonjwa wa kiakili ambao hutia tashwishi roho ya mtu."

(Selection Joumal)

Kwa ufupi, mtu mwenye furaha na raha ni yule ambaye moyo wake umesafika kutokana na kinyongo na uadui.

Imam Ali AS amesema:

"Mja mwenye furaha ni yule ambaye moyo wake hauna chuki wala wivu."

(Ghuraru 'l-ffikam, uk. 399)

Ni lazima tukumbushe hapa jambo moja, kwamba Uislamu hautoi ruhusa baadhi ya vitendo viovu kusamehewa wala kuachiliwa vivi hivi. Ilivyokuwa sheria za Kiislamu zimeutilia mkazo mahsusi ulinzi wa mfumo wa jamii, hivyo, ikiwa mwendo mwovu na uasi wa mtu mmoja utaharibu mambo ya kijamii na kuhatarisha amani, hapo itabidi achukuliwe hatua ya kutiwa adabu,

190

kama vile kutekeleza sheria za kisasi na hududi.

12 - HAMAKI

MAKI193

Faida ya Kujidhibiti

Muundo wa siri na wa kushangaza wa binadamu imezatitiwa kwa nguvu mbili kubwa ziitwazo akili na rada. Akili ni mwanga unaotokana na utukufu wa roho;

layo huamua maisha ya mtu na huhesabiwa kama ni citambulisho halisi cha shakhsia yake. Akili ni taa inayoangaza kila uwanja wa kiza cha maisha, na ni nwenge unaotumulikia njia iliyopotoka ya maisha na kutuongoza kwenye njia iliyonyooka.

Binadamu ana wajibu wa kujitahidi kuzizoeza vizuri hisia za kila aina alizonazo katika umbile lake ili azizuie zisikiuke mpaka. Kipawa cha kiakili hutuonyesha ciwango cha amali za hisia ili tuweze kutumia hazina na 'asilimali hizo katika kiwango sahihi, na ili kwamba naumbile yetu ya kishari yasilazimike kufuata naamrisho yake. Hapana shaka kwamba akili inapo angaza katika mazingira ya upendo, nyota za ;humu hudhihirika katika mbingu ya maisha. Lakini ikiwa mtu atazitii hisia zake (potofu), basi shakhsia na uhuru wake utadhoofika pia na atashindwa katika nedani ya maisha.

Irada (azma) ambayo ni sehemu kubwa kabisa ya naadili na chombo cha kutekelezea makusudio na matakwa, inahusika kikamilifu na ufanisi na mafanikio 'a mtu, na huzihifadhi shakhsia na roho kutokana na uchafu na ubaya.

Sharti muhimu la kupata mafanikio katika maisha

194

ni kuwa na azma madhubuti ili mtu aweze kumudu kukabiliana kwa ushupavu na matukio na matatizo yanayoathiri maisha yake. Kwa kadiri tutakavyojitahidi kuikuza irada hiyo ambayo ni kiini cha mafanikio, ndivyo tutakavyoweza kujizatiti kwa mema na uvumilivu, na kuzifanya roho zetu ziwe makini na imara na zisiweze kuyumbishwa na upotofu.

Mwanafikra mmoja wa Magharibi amesema:

"Kuna maelezo mazuri yanayotoa maana muhimu ya sifa ya akili yenye makini, nayo ni 'nguvu ya kunadhimu'. Nguvu hiyo ni kama 'chombo cha kuzuia mgongano' wa gari. Leo magari mengi ya kisasa na yaliyo na thamani kubwa yametiwa chombo hicho ambacho kazi yake ni kuzuia athari za ajali ya gari, mtikisiko na utelezi unaotokana na kuwepo njia zenye mashimo na miinuko. Chombo hicho huwafanya wasafiri wasichoke bali wahisi raha kabisa hata wakipita kwenye njia mbaya sana.

"Mhalifu ni mtu aliyekosa makini na akili timamu. Wewe unaposhindwa wakati huo kuidhibiti akili yako huwa huna hiari yako mwenyewe. Akili isiyodhibitiwa na mwenyewe mbali na kuwa haifai wala haina athari huwa ni hatari pia. Akili kama hiyo haiwezi kuwa na faida wala maendeleo, bali huwa ni yenye kuleta madhara na uharibifu. Vijito vinavyobubujika katika milima huwa na sauti kali zaidi kuliko mto mkubwa wa Missisippi. Watu wenye maadili bora na madhubuti pia ni kama mito mikubwa inayopita taratibu na bila ya sauti katika ardhi tambarare."

Tabia ya kuhamaki sana inahitajiwa kudhibitiwa

195

kwa nia imara, kwani isipodhibitiwa huasi, hupindukia mpaka na huzoea, na katika baadhi ya nyakati humsumbua mtu na kumlazimisha aamue jambo kwa haraka bila ya kufikiria, na husababisha matokeo mabaya sana.

Athari Mbaya za Hamaki

Hamaki ni mojawapo kati ya hali ya kinafsi inayopotosha mwendo mwema kwenye mkondo wake ulionyooka. Ghadhabu inapoitawala misingi ya maisha na kumvaa mtu, roho yake huwa na tabia ya kuasi. Uwanja huwa wazi kwa ajili ya kushambulia sifa hii mbaya ambayo humkera mtu vibaya sana kama iwezekanavyo, kwa sababu pazia la hamaki huliziba mtazamo wa akili na huvunja nguvu za kutambua na kupambanua. Wakati mwingine mwenye hamaki hupata majojo na misukosuko mingi kwa kadiri kwamba huonekana katika sura yake ya kihayawani. Hukosa kutambua uhakika na huruma na hutenda vitendo vinavyotisha vya kihalifu kwa kadiri kwamba huenda yeye mwenyewe akapata hasara ya daima. Anapokuja kutambua matokeo mabaya ya hamaki hiyo huwa amekwishatumbukia katika shimo refu.

Tabia ya kuhamaki hufuatana na majuto, kwa sababu baada ya kupoa na kutulia hujihisi amelainika mno na hujuta kwa aliyoyafanya. Hujilaumu mbele ya 'mahakama ya akili na dhamiri', na baada ya hapo moyo wake hujaa masikitiko na huzuni.

Hamaki si tu kwamba hufanya roho ijae ghamu na

196

majonzi, bali hata mwili ambao ni makao ya usalama na utulivu wa nafsi,huathirika na kusononeka.Ndimi kali za ghadhabu zinapowaka katika mwili wa binadamu, husukuma damu kwa nguvu katika moyo, kisha hupeleka katika mishipa, huwivisha uso wake, hutetemesha mwili na kukifanya kila kiungo kuwa tayari kuchukua kisasi. Hamaki husababisha maradhi ya akili, kifua kikuu na kutokwa damu. Ulevi na sigara ni miongoni mwa vitu vinavyomfanya mtu kupandwa na hamaki na kuingia sumu katika damu yake.

Hapana shaka kwamba ni lazima mtu awe na hamaki kwa kiasi cha mahitaji. Hamaki isiyokiuka mpaka ni jambo la lazima kwa mtu na ni alama ya ushujaa. Hasira inayomfanya mtu asimame imara dhidi ya uonevu na atetee haki na ukweli ndiyo inayostahiki kusifiwa.

Hisia ya kulipiza kisasi ni miongoni mwa mambo yanayoharibu maisha na kuleta utengano kati ya watu. Kwa kawaida, hisia hii ya kishari hufuatana na ghadhabu. Ikiwa tutataka kulipiza kisasi kwa kila jambo baya tunalofanyiwa na tutataka kutuliza hisia yetu ya kisasi kwa kuumiza miili na roho za watu, basi hapana shaka maisha yetu yote yatakuwa katika kugombana na kuzozana tu! Isitoshe, roho zetu zitadhoofika na tutatokwa na hima.

Kila mtu hufanya makosa katika maisha yake. Ikiwa kukosea kwetu kutamfanya mtu atuhamakie, njia bora kabisa ya kumfanya atusamehe ni kukiri makosa yetu.

Dk. Dale Carnegie ameandika:

"Inapobainika kwetu kwamba tunastahili kutiwa

197

adabu, je, si bora kwetu kukubali na kukiri makosa yetu? Je, kujilaumu kwetu si kwepesi zaidi kuliko kukaripiwa na wengine? Fanyeni haraka kukubali makosa yenu kabla ya wengi kuanza kukufokeeni na kukutukaneni. Mkifanya hivyo, basi kuna uwezekano wa asilimia tisini kusamehewa na kuhurumiwa. Kila mpumbavu anaweza kuficha makosa yake; na wapumbavu wote wanafanya hivyo. Lakini mtu mwenye kukiri makosa yake atakuwa ni mtu mtukufu katika jamii na atahisi utamu wa utukufu huo. Tutakapokuwa na hakika kwamba haki ipo upande wetu, basi ni lazima tuwahakikishie wengine kwa upole na uangalifu. Lakini tutakapofanya kosa lolote, basi tukiri kwa haraka na kwa kinagaubaga. Kwa hakika, mambo yasiyo sawa ni mengi kuliko yale yaliyo sawa kwa sharti kwamba tuwe na macho ya kuyatazama. Baada ya kukiri makosa yetu tutayaona matokeo yake ya kushangaza, bali hata tutaona utamu wake ni mwingi zaidi kuliko kuficha kwake!"

Msamaha humulika furaha ya kweli na hujaza mapenzi na hisia ya kibinadamu katika moyo wa mtu. Mtu anapomsamehe mwenzake humlazimisha adui wake amwachilie na amnyenyekee. Msamaha huleta amani na kuaminiana, huangaza nuru kati yao, humfanya adui asahau uhasama wake na afikirie kufanya urafiki na mapenzi.

Maarifa na uzoefu ni nyenzo za kuondolea ukali na kurekebisha maadili. Maarifa yanapopanuka, kiwango cha fikra na mawazo pia hukunjuka. Watu wenye uzoefu mwingi na wanavyuoni wakubwa huwa na nguvu

198

zaidi ya kupambana na udanganyifu wa nafsi na huwa ni watu wavumilivu pia. Huwa na moyo mkubwa wa kusamehe makosa kuliko watu wengine.

Viongozi wa Kidini Watuongoza

Hakuna dawa iliyo mujarabu zaidi kutibu haya maradhi ya hatari ya kiroho kama mafundisho ya Mitume na viongozi wa kidini. Ingawa matibabu ya madaktari na wanasaikolojia katika uwanja huu ulitoa natija, lakini hayakuwa kamili.Viongozi wetu wa kidini wametufunza maneno ya maana, wametuonya juu ya matokeo ya hatari ya hamaki, na wametuelezeajuu ya faida na haja ya kujidhibiti na kuvumilia.

Imam Sadiq AS amesema:

"Jiepusheni na ghadhabu, kwani huleta mashaka."

Dk.Marden ameandika:

"Kwa kawaida, hamaki iwe imesababishwa na jambo lolote lile, humfanya mwenye hamaki kuona hasara yake baada ya kupoa kwake. Kwa sababu hii, mwenye hamaki anapopima hamaki yake siku ya pili yake, hulazimika amwombe radhi yule aliyemhamakia. Ikiwa mtajizoesha uamuzi wa siku ya pili mwamue leo, mtaweza kupunguza matatizo ya hamaki kufikia kiwango cha chini kabisa."

(Piruzi Fikr)

Imam Sadiq AS amesema:

"Hamaki huziba (nuru ya) moyo wa mwenye hekima. Asiyeweza kuidhibiti hamaki yake hawezi

199

kuitawala akili yake."

(Usulu 'l-Kafi,]z. 2, uk. 305)

Kufuatana na uchunguzi wa madaktari, hamaki na hasira huleta matokeo mabaya sana, na hata huweza kumaliza maisha ya mtu.

Amirul Muuminin AS amesema:

"Mwenye kuiacha hamaki yake ipande, huharakisha mauti yake."

(Ghuraru 'l-ffikam, uk. 625)

Dk. Marden ameandika pia:

"Je, wale watu wenye nyoyo dhaifu wanajua kwamba huenda siku moja kufazaika kwao kutakomesha maisha yao? Labda wasifikirie hivyo, lakini ni lazima wajue kwamba wakati mwingine watu wenye nguvu na afya kamili hupoteza maisha yao. Mara nyingi imeonekana kwamba ukali wa hamaki husababisha akapata pigo la moyo na kufa.

"Hamaki huondoa hamu ya kula, hutatiza msago wa chakula tumboni, husumbua akili ya mtu kwa masaa mengi na hata huendelea kwa siku nyingi, huharibu mfumo wa mwili, na mwisho wake huchafua roho na nguvu za kiakili.... Vilevile huenda hamaki ikatia sumu maziwa anayenyonyeshwa mtoto."

(PimziFikr)

Dk. Mann amesema:

"Utafiti wa kifiziolojia uliofanywa juu ya hamaki umeonyesha kwamba wakati mtu anapohamaki viungo

200

vyake vyote huathirika. Hutokea mabadiliko katika mapigo ya moyo, tezi jasho, utumbo, ubongo na utokaji wa osmososi. Kutoka adrenalini katika tezi adrenalini ni muhimu sana kwa sababu hamoni hiyo hurekebisha kiasi cha sukari na chumvi katika damu ambayo husisimua mwili."

(Usule Ravanshinasi)

Imam Ali AS amesema:

"Jihadhari na hamaki, kwani mwanzo wake ni wendawazimu na mwisho wake ni majuto."

Vilevile amesema:

"Hamaki ni moto uliokokwa, mwenye kuipoza hamaki huuzima (moto wake), na mwenye kuiachilia huwa ni wa kwanza kuungua humo."

(Ghuram 'l-Hikam, uk. 71)

Imam Ali AS ametuusia tuwe na subira na uvumilivu ili tuweze kukabiliana na hasira na hamaki, kwa sababu tunavihitajia hivyo kuepukana na maumivu yake.

Amesema:

"Jilindeni kutokana na ukali wa hamaki na jiandaeni kupambana nao kwa kuvunja hamaki na kwa kuvumilia."

(Ghurani 'l-Hikam, uk. 133)

Vilevile amesema:

"Kujidhibiti wakati wa kushikwa na hasira humsalimisha mtu wakati wa maangamizo."

(Ghuram 'l-Hikam, uk. 463)

201

Imam Baqir AS amesema:

"Kitu gani kilicho kiovu zaidi kuliko hamaki wakati mtu aliyepandwa na hamaki hutoa roho iliyoharamishwa na Mungu?"

(fl/-^,jz.3,uk.l48)

Bw. John Markoist ameandika:

"Wako watu wenye hamaki kali ambao mawazo ya kutenda kitendo cha kijinai huwapitia haraka katika bongo zao kama filamu. Ukali mno kama huo ni tabia ya.kinafsi ya watu wa aina hiyo ambao wanapowaza juu ya jinai moja huitenda haraka. Watu kama hao wanaitwa wauaji wa papo hapo."

(Cheh Midanam)

Mtume Mtukufu SAW ametoa mwongozo mzuri wa kufanya wakati mtu anapopandwa na hamaki:

"Ikiwa mmoja wenu atapandwa na hamaki, kama amesimama akae chini, na kama amekaa alale. Na kama hamaki haikupoa baada ya kufanya hivyo, basi atawadhe kwa maji baridi au aoge kwani moto hauzimiki ila kwa maji."

(Ahyau 'l-'Ulumu 'd-Din,]z. 3, uk. 151)

Bw. Victor Pusheh ameandika:

"Ikiwa mtoto atakuwa mkali sana, unaweza kumtuliza bila ya kumtolea ukali kwa kumwosha kwa maji baridi au kwa kumviringa kwa kitambaa cha majimaji."

(Rahe Khoshbakhti)

202

Dk. Gilbert Roben ameandika:

"Usafi wa mwili una umuhimu mkubwa kwa upande wa maadili na tabia. Kuoga kwa maji vuguvugu wakati wa asubuhi na usiku na vilevile baada ya kumaliza kazi ya mchana husafisha na huchangamsha mwili, huondoa uchapwa na ukimwa na humburudisha mtu. Tunaweza kusema kwamba matokeo ya kimwili ya kuoga yana thamani sawasawa na ya kitabia yake."

{Cheh Midanam)

Kwa hakika, maisha ya viongozi wa kidini ni kama taa inayotumulikia njia ya maadili mema ambayo inatubidi tuyafuate. Tunaweza kutambua uvumilivu na udhibiti wao wa nafsi kwa kutazama tabia zao na namna walivyowatendea maadui zao. Maisha yao ni mafunzo makubwa kwetu. Hapa inatosha kutoa kisa kimoja kuwa kama mfano wenyewe:

rudi nyuma Yaliyomo endelea