rudi nyuma Yaliyomo endelea

Ikiwa mwangaza wenye kutoa uzima wa mapenzi utazimika katika upeo wa maisha, giza la kutisha la upweke na la kuvunja moyo litatanda katika roho ya mtu. Sura ya maisha itakunjana na kujawa na majonzi kwa kadiri kwamba watakaoiona watachukia kuishi!

Binadamu ameumbwa kimaumbile kama mtu wa kijamii; kuchanganyika na kuingiliana na wenzake ni sehemu muhimu ya maisha yake. Kwa kawaida, hitilafu za kifikra humfanya mtu ajitenge na jamii, azoee kukaa peke yake na akwepe kuingiliana na watu. Wale wanaowakimbia watu, wakajitenga na wakazoea kukaa peke yao huwa wana upungufu fulani katika fikra zao;

kwani hili ni jambo linaloeleweka wazi kwamba mkiwa hana raha wala furaha. Kama vile ambavyo kuna mahitaji mengi ya kimwili ambayo ni lazima yakidhiwe, vivyo hivyo, roho ina matakwa mengi ambayo ni lazima kwayo iridhishwe. Nafsi ina kiu cha ahaba, hivyo, binadamu yuko daima mbioni kutafuta kile

150

kitakachotosheleza hiyo haja yake ya ndani.

Binadamu amekuwa akihitajia sana mapenzi na nyonda tangu siku ya kwanza alipoweka mguu wake duniani na kuanza kuishi mpaka dakika za mwisho wakati kitabu chake cha uhai kilipofungwa. Wakati mashaka ya maisha yanapomlemea sana, na matukio ya kusikitisha yanapomchoma moyo wake, na hatimaye masaibu yanapotaka kukata mshipa wa matumaini, hapo mtu huwa na kiu kali sana ya mapenzi ambayo yataupa matumaini moyo wake. Utulivu wa dhamiri yake hauwezi kupatikana ila kwa mahaba, kwani kama kuna marhamu yoyote inayoweza kutuliza mashaka na masaibu ya mtu, basi hiyo ni marhamu ya mapenzi tu. Ukilinganisha na hisia nyinginezo za mwanadamu, huba au upendo unaweza kuhesabiwa kama ni hisia inayong'ara kuliko zote na ni chimbuko la asili la maadili mema. Mapenzi yanahawilika, na njia bora kabisa ya kuvuta mapenzi ya wengine na kuwapenda watu ni kuwatolea roho yako safi, na kuamini kwamba huna wadhifa mwingine mbele ya wenzako isipokuwa kuwapenda. Kuonyesha mahaba kwa wengine peke yake ni muamala wenye faida. Ikiwa mtu atajitolea kuonyesha utukufu wake kwa kutoa johari hiyo iliyolundikwa kwenye hazina ya moyo na kumpa mtu mwingine, basi atapata mara nyingi kuliko hiyo. Mtu mwenyewe ana ufunguo wa nyoyo za watu. Mtu anayetaka kuingia katika hazina zenye kima za mahaba, itabidi moyo wake ububujike roho safi na utakaswe kutokana na sifa mbaya zinazochafua roho.

Wanafalsafa wanasema: "Ukamilifu wa kila kitu

151

unadhihirika katika dhati yake, na dhati ya mwanadamu ni mapenzi." Upendo huo wa kiroho na mapenzi yanayovutana kati ya nyoyo za wanadamu ndiyo msingi unaosimamisha ushirikiano, mapenzi na maelewano kati ya watu.

Dk. Carl ameandika:

"Ili jamii iweze kupata mafanikio, inabidi watu wake washikamane kama matofali ya jengo moja. Lakini saruji gani inayoweza kuwashikamanisha watu barabara? Mapenzi ni saruji ya pekee iliyo na ushikamano madhubuti. Ni mapenzi hayohayo ambayo mara nyingine unayaona kati ya watu wa nyumbani, lakini hayatoki nje ya mfumo wa ukoo nyumbani. Asili ya mapenzi ina sehemu mbili, moja inausia mtu awapende watu, na nyingine inamtaka mtu mwenyewe awe anastahiki kupendwa na wengine. Ikiwa mtu mwenyewe hatafanya hima kuacha tabia zake mbaya, hataweza kupendwa. Tunaweza kufikia shabaha yetu tutakapofanya mapinduzi katika nafsi zetu na kujitoa katika utumwa wa aibu ambazo zinatutenganisha na watu wengine. Hapo patawezekana jirani mmoja kumtazama jirani mwenzake kwa macho ya mapenzi, na mwajiri na mwajiriwa wakapendana. Mapenzi tu ndiyo yanayoweza kuweka nidhamu katika jamii ya wanadamu kama vile silika ilivyoweza kuweka nidhamu katika jamii za sisimizi na nyuki katika kipindi cha mamilioni ya miaka."

(Rah Wa Rasme Zindagi)

152

Majivuno Yaleta Machukio Makubwa

Huba ya dhati au kujipenda ni silika muhimu katika maumbile ya mwanadamu. Silika hii ni muhimu kwa ajili ya maendeleo ya maisha. Chanzo cha mtu kupenda na kushindania kuishi kinaanza hapohapo. Ingawa hii hazina asilia ni nishati yenye kutoa faida na sifa nyingi njema zinazoweza kukuzwa humo, hata hivyo, inapopindukia mpaka na kujitokeza bila ya maana, hupata fursa ya kustawi na kupotoka kwenye njia yake na kuwa ni chanzo cha mienendo mibaya na upotofu wa kila aina.

Hatari ya mwanzo kabisa kwa maadili mema ni mtu kujipenda nafsi yake kupita kiasi kwa kadiri kwamba hapabaki nafasi ya kupendana na watu wengine. Tabia hii ya ubinafsi humzuia mtu asikiri makosa yake wala asikubali ukweli ambao utavunja majivuno yake.

Profesa Robinson amesema:

"Mara kwa mara imetokea kwamba tunazibadilisha wenyewe itikadi zetu bila ya taabu au matatizo yoyote. Lakini akitokea mtu kutuonyesha makosa yetu, papo hapo tunabadilika, tunaikataa tuhuma hiyo na tunajitetea. Sisi tunaikubali kwa urahisi itikadi fulani, lakini akitokea mtu kutaka kutusahihisha, tunaanza kujitetea kama wendawazimu. Hapana shaka kwamba kile tunachokiogopa si kupokonywa itikadi yetu, bali ni kuvunjwa ubinafsi wetu. Ikiwa mtu atatuambia kwamba saa zetu zinaenda nyuma au magari yetu ni ya modeli ya zamani, huenda tukahamaki kwa kadiri hiyohiyo kama

153

akituambia kwamba elimu yetu juu ya jedwali ya sayari ya Marikhi, au faida za dawa ya aspirini, au ustaarabu wa mafirauni wa Misri si sawa!"

Maradhi makubwa kabisa ya ufanisi wa binadamu na adui mwovu kabisa ni majivuno na takaburi (kiburi). Hakuna tabia mbaya inayochukiwa sana kama takaburi. Kujiona ni sifa ambayo hukata mfungamano wa kindugu na kimapenzi na hugeuza kuwa ni utengano na uhasama. Mwenye kujivuna hujifungulia mlango wa kuchukiwa na watu. Kama vile ambavyo mtu mmoja hutegemea apendwe na aheshimiwe na wengine, vivyo hivyo, mtu huyo anategemewa awapende na ahifadhi heshima za wengine pia; na ajiepushe kabisa na kila jambo linalokwenda kinyume na maingiliano mazuri au linalosababisha kuharibika mapenzi. Bila shaka kutozijali hisia za watu huleta matokeo mabaya, nayo ni kutukanwa na kudharauliwa mringaji mwenyewe.

Haki za watu huheshimiwa katika jamii. Kila mtu huheshimiwa vizuri kwa kadiri ya heshima na hadhi yake. Mtu anayejifunga katika kuta nne za majivuno na nafsi yake ikatawaliwa na ghururi, hatajali kamwe mambo na hali ya wengine isipokuwa atazingatia matakwa yake tu. Kwa hivyo, atajaribu kwa inadi na kukera kujifanya mashuhuri na msifiwa, na kuitwika jamii ubora wake wa kujinata. Tabia hiyo ya kukera na kutarajia jambo lisilostahili husababisha kutokea ukinzani mkubwa baina ya matakwa na matamanio ya mwenye kutakabari na mwendo wa watu wa kumchukia. Radiamali kali ya jamii humsumbua sana mwenye kujitwaza na humbidi avumilie kwa roho ya

154

hasira na moyo wa mashaka jambo asilotarajia.

Dhana mbaya ni athari isiyozuilika ya ndweo. Miali ya dhana mbaya ya mwenye kujiona daima huwaka na huwadhania wote kuwa ni wenye kumchukia na kumtakia mabaya. Kudharauliwa kwake na kupata mapigo ya daima kutokana na maringo yake hakumsahaulishi kamwe. Anayevimbisha kichwa chake husumbuliwa na fikra zake bila ya mwenyewe kutaka;

kila akipata fursa hutaka kuifanyia chuki jamii, na huwa hawezi kuona raha madhali machafuko na machemko ya ndani mwake hayatulii.

Shetani wa majivuno na maringo hutokeza katika dhamiri ya mtu baada ya kuugua maradhi ya kinafsi ya kujihisi duni. Maradhi hayo hugeuka kuwa kidonge duni ambacho kwa sababu ya kuwa kiharibifu na chauma, huenda kikawa ni chanzo cha hatari nyingi na uhalifu wa kila aina. Kidonge duni humfanya mwenye kujinata afanye ukatili na udhalimu.

Tukiisoma historia ya dunia, suala hili litadhihirika kwetu kwamba kikundi ambacho daima kilikuwa kikisimama dhidi ya Mitume wa Mwenyezi Mungu na kikikataa kukubali haki kilikuwa ni cha wenye kutakabari na kujiona. Vilevile mauaji mengi ya umati na mashambulizi ya kikatili yaliyofanywa katika vita vya dunia ambayo yalikaribia kuwaangamiza watu wote duniani, yalitokana na kikundi cha watawala wenye ghururi na takabari.

Watu wengi waliolelewa katika koo duni na wakapata vyeo katika jamii huwa ni wajeuri. Kwa njia hii hutaka kufidia uduni waliolelewa nao katika koo

155

hizo. Hujiona ni watu bora kuliko wengine, na hutaka kutumia ghururi na ubinafsi wao kujitangazia ubora wao. Wasomaji wetu wanaweza kuwatambua watu wa aina hii miongoni mwao.

Mtu mwenye thamani na hadhi kweli hatakuwa na haja ya kujivuna au kujionyesha mbele ya watu wakati wowote ule, kwa sababu anaelewa vyema kwamba kujiona si msingi wa ubora, na ghururi haimfai mtu yeyote wala haimfikishi mtu yeyote kwenye kilele cha utukufu na ufakhari.

Mwanachuoni mmoja amesema:

"Yawekeeni kikomo matumaini yenu na kiteremsheni kiwango cha mategemeo yenu. Jiepusheni na tamaa za roho na jiwekeni mbali na kiburi na majivuno. Fungueni mafundo ili nafsi zenu ziwe na uzima zaidi!"

Viongozi wa Kidini Wafunza Unyenyekevu

Mojawapo kati ya maadili mema ambayo yanaweza kuwa ni ufunguo wa mapenzi na njia bora kabisa ya kuvuta upendo na urafiki ni unyenyekevu. Mnyenyekevu anapotekeleza wadhifa wake wa kimaadili hupandisha juu thamani ya utukufu wake, na kwa njia hiyo miali ya kupendwa kwake huzidi kupenya katika nyoyo za watu. Ni lazima tujue kwamba kuna tofauti kubwa sana baina ya unyenyekevu na majisifu, na kila moja ina hesabu yake mbali. Unyenyekevu ni katika mwendo mzuri na ni dalili ya utukufu wa nafsi, ubora wa shakhsia na utulivu wa roho. Lakini majisifu

156

yanatokana na uharibifu wa maadili na ni alama ya kukosa hadhi.

Luqman mwenye hekima alipokuwa akimwusia mwanawe maneno murua alimwonya juu ya ghururi kwa kumwambia:

"Wala usiwatazame watu kwa upande mmoja wa uso, wala usitembee katika nchi kwa maringo, hakika Allah hampendi kila mwenye kujivuna na kujisifu"

(Luqman, 31:18)

Amirul Muuminin Ali AS amesema:

"Lau Mwenyezi Mungu angeruhusu kiburi kwa waja Wake, basi angewaruhusu Manabii na Mawalii Wake. Lakini Mwenyezi Mungu amewakataza kuwa na kiburi na amewaridhia kuwa na unyenyekevu. Hivyo, huweka videvu vyao juu ya ardhi (kumnyenyekea Mwenyezi Mungu), huzisugua nyuso zao kwenye ardhi, na huwanyenyekea waumini."

Wenye kujiona huchukiwa na jamii na hukosa pia rehema za Mwenyezi Mungu.

Mtume Mtukufu amesema:

"Jiepusheni na kiburi, kwani mja anapotakabari, Mwenyezi Mungu husema: 'Mwandikeni mja huyu miongoni mwa waasi.'"

(Nahju 'l-Fasahah, uk. 12)

Imam Sadiq AS ametaja kwa ufupi asili ya kinafsi ya ndweo na majivuno:

"Hakuna mtu anayeugua kiburi ila kwamba amehisi uduni (dhila) nafsini mwake."

(al-Kafi,]z.3,uk.461)

157

Bwana McBrid ameandika katika kitabu chake kiitwacho 'Uqdae Hiqarat:

"Kutakabari mtu au taifa kunamaanisha kuwadharau na kuwadunisha watu wengine na mataifa mengine. Karibu chuki, uhasama na ugomvi wote wa leo unatokana na hisia ya uduni. Kwa hakika, mzizi wa fikra kama hiyo ni aina moja ya jaribio lisilo sawa la kufidia hisia ya udhalili. Hakuna mtu mwenye moyo safi na heshima atakayejiona bora kuliko watu wengine au bora kuliko matabaka na makabila mengine."

Watu wanaojiona na wanaotakabari huona mienendo yao yote kuwa ni mizuri na aibu zao huziona ni mema yao.

Imam Musa bin Jaafar AS amesema:

"Maringo na majivuno yana vidato; kimojawapo ni kumpambia mja amali yake mbaya akaiona nzuri na akaipenda na kufikiria kwamba amefanya vizuri."

(Wasa'ilu 'sh-Shi'ah, jz. 1, uk. 74)

Mtungaji wa kitabu kiitwacho Ravan -kavi ameandika:

"Mwenye kujiona huziona kasoro zake ni bora na aibu zake ni nzuri. Kwa mfano, akimhamakia upesi mdogo wake huona ana hadhi yenye nguvu! Kuna uzuri gani mtu awe kama haluwa? Akiwa mwembamba huchukulia kuwa ni mtu mwenye hisia nyingi na roho tukufu, na watu wanene huwa ni watu wa kuchekesha wasioweza kusema kinagaubaga na wasio na hisia!! Lakini yeye mwenyewe anapokuwa mnene huchukulia ni alama ya afya na roho nzima katika mwili mzima! Na

158

huwachukulia watu wembamba kuwa ni kama majipu, hivyo, amali zao haziwezi kutabiriwa wala haiwezekani kuwategemea, n.k."

Hapa tunanukulu baadhi ya semi zilizojaa maana na hekima za Imam Ali AS kuhusu kutakabari na kujiona:

"Jihadhari na kujipenda (kujiona) mwenyewe, kwani utazidiwa na wenye kukuchukia."

{Ghuraru 'l-Hikam, uk. 147)

Wanasaikolojia wa leo wanaamini kwamba mwenye kutakabari huugua aina moja ya udhaifu wa akili na uwendawazimu.

Jambo hili limekwishasemwa na Imam Ali AS:

"Kiburi huharibu akili."

(Ghuraru 'l-Hikam, uk. 26)

"Mwenye kudhoofisha fikra zake huimarisha ghururi yake."

(Ghuraru 'l-Hikam, uk. 651)

"Unyenyekevu ni kiini cha akili, na majivuno ni kiini cha ujinga."

(Ghuraru 'l-Hikam, uk. 102)

"Kiburi ni maradhi ya ndani."

(Ghuram 'l-Hikam, uk. 478)

"Mwenye kuona bora mwendo wake, hushindwa kurekebisha nafsi yake."

(Ghuram 'l-Hikam, uk. 677)

159

Mtu mwenye kiburi na ubinafsi hatafanikiwa kamwe kujirekebisha mwenyewe na kuiinua shakhsia yake.

Dk. Helen Shakhter amesema:

"Njia nyingine tunayoitumia kuwavutia watu licha ya kutofanikiwa kwetu ni kujisifu wenyewe. Tunajidai kuwa tumefanikiwa katika kazi tulizozitaka kuzifanya na katika mafanikio tuliyoyategemea. Au tunajiridhisha kwa kuyahusisha mafanikio tusiyoyapata na kazi muhimu tusizoweza kuzitekeleza kwa kazi ndogo tulizotekeleza. Tunazifanya kuwa ni kubwa sana ingawa ni ndogo tu. Watu kama hao wanajidanganya na wanajifurahisha nafsi zao kwa kujisifu na kusema uwongo kwa kadiri kwamba hupoteza fursa ya kujitahidi na kufanikiwa."

(Roshde Shakhsiyyat)

Mtu anayejitia katika utumwa wa majivuno hawezi kuziona kasoro zake na kuzithamini sifa njema za wengine.

Imam Ali AS amesema:

"Mwenye kujipenda nafsi yake haoni aibu zake, na lau angejua mema ya wengine angetengeneza dosari na hasara zake."

(Ghuraru 'l-ffikam, uk. 95)

Uislamu huongoza kwenye ustaarabu bora wenye kuhuisha, hivyo, hubatilisha kila sifa iliyo kinyume na uadilifu; na sifa ya pekee tu unaoitambua ni ile inayokubaliana na usafi wa moyo na uchaji.

160

Imam Ali AS amesema:

"Jikingeni kwa Mwenyezi Mungu kutokana na ulevi wa utajiri, kwani una nishai (ulevi) inayochelewa kutoka."

(Ghuraru 'l-Hikam, uk. 138)

Siku moja tajiri mmoja alikwenda katika baraza la Mtume Muhammad SAW. Baadaye akaja maskini mmoja na akakaa karibu na tajiri huyo. Tajiri akakusanya nguo zake alipomwona maskini amekaa ubavuni mwake. Mtume Mtukufu akamwambia tajiri:

"Unaogopa umaskini wake ukuguse?"

Tajiri akajibu: "Hapana!"

Akamwuliza: "Unaogopa sehemu ya mali yako aipate yeye?"

Akajibu: "Hapana!"

Akamwuliza: "Unaogopa nguo zako ziingie uchafu?"

Akajibu: "Hapana!"

Mtume Mtukufu akamwuliza: "Basi kwa nini umezikusanya nguo zako na umekikunja kipaji chako?"

Tajiri akasema:" Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Utajiri wangu na mali zangu zimenifumba macho yangu nisitambue uhakika, na zimenifanya niyaone mazuri yale mabaya yangu. Kwa kufuta kosa hilo lisilofaa, natoa nusu ya mali zangu kumpa maskini huyu."

Mtume Mtukufu akamwuliza maskini: "Je, unaikubali tunzo hiyo?"

Maskini akakataa, na alipoulizwa sababu yake, akasema: "Naogopa nami pia nisiwe na sifa mbaya kama yake baada ya kuwa na utajiri mwingi."

161

Kwa hivyo, ikiwa mtu mwenye kutakabari na kuvimbisha kichwa chake atapenda kupata furaha na ufanisi, basi aazimie barabara kujirekebisha mwenyewe, na kuitoa tabia hiyo mbaya yenye kuchafua shakhsia yake kutoka katika pango lake. Asipoiondoa tabia hiyo, basi atasumbuka katika maisha yake yote.

10 - UDHALIMU

165

Nafasi ya Uadilifu katika Jamii

Mapitio ya historia mbalimbali na uchunguzi juu ya kuzuka harakati (za ukombozi) unatuongoza kwenye ambo la kuvutia sana, nalo ni hili kwamba katika vipindi mbalimbali vya historia, neno takatifu la 'uadilifu" lilikuwa ni kiini cha mapambano na chimbuko la mapinduzi kati ya mataifa yote. Watu ambao walishindwa kuvumilia ukandamizaji na udhalimu iliopita mipaka, roho zao zilihamasishwa na tamaa ya .;upata uadilifu na hisia zao zilisisimishwa kwa kadiri kwamba walithubutu kuanza mapambano yao dhidi ya itawala wa kishetani. Watu walijitahidi bila ya kuchoka la hawakusita hata kidogo kutoa mhanga roho zao ili mradi waipate johari hiyo ya kima na wazipindue awamu za kiza na za kishenzi.

Lakini kwa bahati mbaya, mengi kati ya mavuguvugu na mapambano hayo hayakutoa matunda mazuri au ushindi halisi. Kwa ufupi, harakati hizo pia hazikuweza kufikia makusudio au malengo yake.

Siri ya kushindwa na kutofanikiwa kwao hubainika tukizingatia jambo hili, kwamba wakati mwendo wa lamii moja unapopotoka kwenye kiini cha maumbile na kilicho haribika, (jamii) huwa haiwezi kuupokea uadilifu au kukubali kuwa na insafu. Uadilifu hauwezi kuenea ila baada ya kutimizwa masharti fulanifulani, na yasipopatikana masharti hayo, sura halisi ya uadilifu pia itadhihirika katika upeo wa maisha.

166

Kwanza, jamii inahitaji sheria zilizotungwa juu ya msingi wa uadilifu. Haki za matabaka ya watu wote ziwe zinazingatiwa kwa ukamilifu na ziwe zinakwenda sambamba na maslahi ya umma. Mafanikio yatapatikana katika utekelezaji wake kama yatakuwepo malezi ya kimsingi na maadili mema.

Uadilifu ni sheria asilia inayoonekana katika ulimwengu mzima. Njia ya safari ya ulimwengu imepangwa kwa mujibu wa uadilifu, na ni muhali kwenda kinyume na sheria hiyo ya kimaumbile. Ulinganifu wa kushangaza na ushirikiano kati ya viungo vya mwili ni dhihirisho safi kabisa la kuwepo uadilifu sahihi katika mifumo adhimu wa uumbaji. Hivyo, tunapozichungua nafsi zetu wenyewe ndipo tunapoujua mfumo wa ulimwengu wote.

Msawazo ulioko katika mfumo wa ulimwengu ni mizani ya kimaumbile, lakini kwa kuwa binadamu ana uhuru wa kufikiri na kuamua, hivyo, inabidi msingi wa uadilifu katika jamii aupange kwa hiari yake mwenyewe. Katika baadhi ya mambo, akili ya mtu haihitaji mwongozo wa kidini, kwa kuwa yeye peke yake anaweza kutambua ukweli na kuamua mwenyewe. Akili huthamini amali nzuri na huchukia amali na mwendo usiofaa.

Uadilifu una umuhimu mkubwa sana katika maisha ya wanadamu, kwa kuwa ni chimbuko la mema yote. Kwa ufupi, uadilifu ni hali inayomfanya mtu afanye kazi zinazostahiki na nzuri. Uadilifu ni chanzo kikubwa kabisa kuwaunganisha wanadamu, kukuza mapenzi katika nyoyo za watu, na kuleta umoja na muungano

167

katika jamii.

Plato, mwanafalsafa mashuhuri wa Kiyunani, amesema:

"Wakati wowote uadilifu unapotokeza katika nafsi ya mtu, miali yake huangaza katika vipaji vyake vyote, kwa sababu sifa zote njema na maadili mema ya binadamu hububujika kutoka katika chemchemi ya uadilifu, na humwezesha mtu kutekeleza amali zake katika sura bora kabisa inayostahiki. Na huko ni kufikia kilele cha ufanisi na mafanikio na kupata ukuruba na Mwenyezi Mungu."

Ikiwa tutasema kwamba uadilifu ni msingi wa mwanzo wa maisha yaliyopangika ya kijamii, hatutakuwa tumetia chumvi. Kusimamishwa uadilifu hufungua sura mpya katika maisha ya wanadamu, hutia roho mpya katika mwili uliokufa wa jamii, na hung'arisha mno mazingira ya maisha kwa kuyafanya yapendeze. Shamba la jamii lililostawi kwa miti na mimea ya uadilifu na insafu huweza kuishi na kuyashinda maradhi na matatizo yake.

Miali lunguzayo ya Udhalimu

Matokeo ya madhara ya udhalimu katika kuiangusha na kuivuruga jamii na kuharibu usalama wa kimaadili ni makubwa mno na hayawezi kukataliwa kwa kadiri kwamba hata wale wasiomini dini yoyote hawawezi kukataa ukweli huu. Udhalimu unapotia fora, uhusiano na mifungamano ya watu hukatika, na hitilafu, utengano na migogoro hutawala katika mfumo mzima

168

wa jamii. Vitendo vya kimabavu na kidhalimu mwisho wake hufunga ukurasa wa tawala dhalimu na huzibatilisha starehe na ufakhari wao. Tukichungua kidogo historia ya maisha ya madhalimu ambao waliteseka kwa sababu ya vitendo vyao, tutapata ibra kubwa sana! Inatosha hapa kutoa mfano mmoja katika historia ya madhalimu:

Muhammad bin Abdul Malik alikuwa na cheo kikubwa katika tawala za makhalifa wa Bani Abbasi. Waziri huyo aliyekuwa katili na moyo mgumu alitengeneza tanuri la chuma ambalo alichomeka misumari mirefu ndani yake ili kuwaadhibu wafungwa. Wafungwa wasio na bahati walifungwa katika tanuri hilo la mateso na lenye kutisha. Tanuri lilikuwa likikokwa moto na kuwaua wafungwa kwa ukatili mkubwa.

Mutawakkil aliposhika ukhalifa alimwuzulu waziri huyo cheo chake na akamtia katika jela hiyohiyo aliyoijenga mwenyewe. Abdul Malik alipoona kwamba siku zake zinamalizika, akaomba karatasi na kalamu, na akamwandikia khalifa barua yenye beti mbili zenye maana hii:

Dunia kama njia, kila siku kupitia, Mfano kama njozi, kwenye huo usingizi, Usihuzunike, powa, wengine watapasiwa.

Mutawakkil aliposoma beti hizo (zenye kumwonya kwamba utawala wake pia utamtoka), akatoa amri afunguliwe. Lakini alichelewa, kwani alikuwa amekwishatoa roho kwa namna ya kikatili kabisa (kama

169

alivyokuwa akiwatoa wengine)!

(Muruju 'dh-Dhahab,']z.4, uk. 88)

Naam; watu wanaofikiri kwamba dunia ni medani ya mashindano ya kuishi, huwakandamiza wanyonge ili waimarishe nguvu zao na wahifadhi utukufu na vyeo vyao. Vilevile hawasiti hata kidogo katika kufanya vitendo vya kikatili na vilivyo kinyume na ubinadamu. Lakini katika kipindi kisichokuwa kirefu, cheche za moto wa ghadhabu na hasira hutoka katika vifua, zikifuatiwa na harakati na vuguvugu kubwa la mapinduzi na umwagikaji wa damu.

Hakuna tabaka maalumu linalozalisha madhalimu. Kila mtu awe na cheo au hadhi yoyote ile, maadamu atataka kufaidika na fursa za watu wengine kwa kuwaonea na kutumia njia isiyo ya haki na halali, ni dhalimu.

Kwa bahati mbaya, leo udhalimu umetia fora katika jamii. Ndimi za moto wa udhalimu zinachoma mavuno ya maisha ya jamii, na zinahatarisha kuziangusha nguzo za ustaarabu wa wanadamu. Madhalimu wanavuruga haki za jamii ya wanadamu kwa kadiri ya uwezo na nguvu zao. Huwanyang'anya watu wasio na ulinzi mali na utajiri wao bila ya kujali kitu. Kitu cha pekee kinachoonekana katika jamii hiyo ni sanamu isiyo na roho ya malaika wa uadilifu.

Mapambano ya Dini dhidi ya Udhalimu

Our'ani Tukufu inatangaza ukuba wa madhalimu

170

katika aya hii:

"Na (wakazi wa) miji hiyo tuliwaangamiza walipodhulumu, na tukawawekea miadi ya maangamizo yao"

(al-Kahf, 18: 59)

Viongozi wa kidini walijishughulisha sana katika kuweka uthabiti wa jamii, na shabaha yao ya asili ilikuwa ni kuimarisha uadilifu. Waliubadilisha mwendo wa jamii kufuata harakati dhidi ya udhalimu, waliziteka ngome za dhuluma, walizidhalilisha tawala za kishenzi, waliutambua udhalimu kama ni dhambi isiyosameheka, na wakawakataza sana watu wasiusogelee mpaka wake kwa kadiri kwamba wakahesabu ushirikina (shirk) kuwa ni aina moja ya udhalimu.

Mwenyezi Mungu anasema:

"Kwa hakika tuliwatuma Mitume Wetu kwa dalili waziwazi na tukateremsha pamoja nao Kitabu na mizani (ya kupambanua uadilifu na uonevu) ili watu wasimame kwa uadilifu..."

(al-Hadiid, 57:25)

Kwa kuwa shabaha hasa ya Uislamu ni kusimamisha uadilifu katika kila kipengee cha maisha, hivyo, umefanya kwamba ni wajibu kwa wafuasi wake watendeane uadilifu na insafu bila ya kujali cheo au hadhi ya mtu. Vivyo hivyo, Uislamu umepiga marufuku uonevu na udhalimu wa kiasi chochote kile wasifanyiwe watu wa kikundi chochote kile.

Mwenyezi Mungu anasema:

171

"Enyi mlioamini! Kuweni kwa ajili ya Allah wasimamizi shahidi wa uadilifu, wala uadui wa watu usikushawishini kutofanya uadilifu. Fanyeni uadilifu! Huo ni karibu zaidi ya takwa, na mcheni Allah, hakika Allah anazo habari za yale mnayoyatenda."

(al-Maaidah, 5:8)

Kuhusu kutumia uadilifu katika hukumu na uamuzi, Mwenyezi Mungu anasema:

"Na mnapohukumu baina ya watu, hukumuni kwa uadilifu..."

(an-Nisaa', 4:58)

Mtu asiyekuwa na uadilifu uliosisitizwa katika sheria ya Kiislamu, hana haki ya kukaa juu ya kiti cha mahakama na hukumu hata kama atakuwa nazo sifa nyinginezo nzurinzuri.

Wadhifa mmojawapo ulio muhimu na wa kimsingi kwa wazazi ni kuwafanyia insafu na usawa watoto wao. Ili sifa ya uadilifu ishike barabara katika dhamiri za watoto na tabia zao zisizowee kudhulumu na kuasi, njia bora kabisa ya kuwalea watoto ni kuwafanyia uadilifu na kuwatendea sawasawa. Watoto wanaokua katika mazingira ya nyumbani ambapo huona uonevu na upendeleo wa wazazi, hawataweza kabisa kuinukia na sifa za uadilifu na insafu, bali hapana shaka yoyote kwamba watakuwa na roho ya kudhulumu na kuonea, na mwendo wao katika jamii utakuwa ni wa kuvunja sheria, kuonea, kughusubu haki za watu kwa kadiri kwamba wazazi wenyewe watakula matunda machungu

172

ya utovu wa uadilifu wa wanao.

Kwa sababu hiyohiyo, Mtume Mtukufu alilitilia mkazo jambo hili muhimu la kinafsi na kimalezi na akawausia wafuasi wake kulifuata:

"Wafanyieni uadilifu watoto wenu katika kutoa zawadi kama vile mtakavyopenda wakufanyieni uadilifu kwa mema na mapenzi."

(Nahju 'l-Fasahah, uk. 66)

Betrand Russell ameandika:

"Nafsi ya mtu ni kama mvuke unaopanda daima. Shabaha ya malezi ni kuyafanya matatizo ya nje yachukue sura ya tabia, fikra na hisia za upendo katika akili ya mtoto. Uadilifu haupatikani kwa kupiga, kudekeza, kutesa wala kufikiri. Uadilifu ni dhana ambayo tujaribu kuitia katika fikra na tabia za mtoto kidogokidogo. Malezi sahihi ya kiadilifu hupatikana tunapowachanganya watoto hao na watoto wengine. Watoto hufahamu haraka maana ya uadilifu wanapokuwa wanacheza pamoja mahali ambapo pana mchezo mmoja tu. Kwa mfano, inapokuwepo baiskeli moja tu huazimana kwa zamu, ingawa kila mtoto hupenda aichezee peke yake. Ajabu ni kuwa wanapokuwa watoto wakubwa pamoja nao, watoto wadogo huacha tabia hiyo ya ubinafsi. Mimi siamini kwamba hisia ya uadilifu ni ya kimaumbile, lakini nilipoona jinsi uadilifu ulivyokua kwa haraka kati ya watoto, nilishangaa. Bila shaka ni lazima uadilifu wa kweli uwepo ili usikuwepo upendeleo kati yao. Ikiwa mtawapenda baadhi ya watoto kuliko watoto wengine,

173

basi muwe waangalifu yasije mapenzi yenu yakaharibu mgawanyo wa furaha kati yao. Ni kanuni inayokubaliwa kwamba watoto wapewe bandia sawasawa. Jaribio la kuwashawishi watoto kufanya uadilifu kwa kuwatia adabu ni kazi bure."

(Dar Tarbiyaf)

Mtume Mtukufu amesema:

"Mcheni Mwenyezi Mungu na adiliana na watoto wenu kama vile mpendavyo wakutendeeni wema."

(Nahju 'l-Fasahah, uk. 8)

Amirul Muuminin Ali AS alimpa nasaha ifuatayo Muhammad bin Abu Bakr alipomteua kuwa gavana wa Misri:

"Wafanyie (Wamisri) uadilifu, endeana nao kwa upole, changamka nao, na fanya insafu katika kuwatazama pia ili kwamba watukufu wasitazamie dhuluma kutoka kwako wala wanyonge wasikate tamaa ya kuona uadilifu kutoka kwako."

(Nahju 'l-Balaghah, uk. 877)

Mabalozi wa Mwenyezi Mungu ni waasisi wa uadilifu na waratibu wa sera ya ukamilifu wa mwanadamu. Katika zama za ukhalifa wa Imam Ali AS, siku moja Aqil alikwenda kwa ndugu yake mtawala. Baada ya kumwelezea matatizo yake na umaskini wake, akamshika nduguye (Imam Ali) ampe karibu mani moja (ratili mbili) ya ngano zaidi kuliko sehemu yake kutoka Baitul Maal (Idara ya Hazina). Imam Ali AS badala ya

174

kumkubalia akamsogezea kipande cha chuma kilichoyayushwa ili kumwonya. Aqil akapiga kelele. Hapo Imam akamwambia:

"Ewe Aqil! Mamako akulilie! Unapiga kelele hivyo kuogopa kipande cha chuma tu kilichoyayushwa na mtu, lakini mimi nitavumilia vipi moto utakaowashwa kwa ghadhabu za Mwenyezi Mungu? Je, inafaa wewe upige kelele kwa sababu ya kuungua mwili, nami nivumilie adhabu ya roho?"

Baada ya kusema hayo, akaongeza: "Wallahi! Hata kama nitapewa dunia nzima pamoja na utajiri wake wote ili kwamba nimnyang'anye siafu ganda la shayiri alilonalo mdomoni mwake, sitafanya hivyo kamwe! Dunia unayoina ni nzuri na inavutia kwako, kwangu mimi ni duni na haina thamani kuliko ganda hilo hata kutaka kumuudhi siafu."

Imam Husayn bin Ali AS amesajili katika daftari ya historia maana ya uadilifu na msingi wa ubinadamu kwa kuongoza harakati kubwa dhidi ya udhalimu ambayo ingali iking'ara katika kurasa za historia ya wanadamu.

11 - CHUKI NA UADUI

177

Kwa Nini Tuyasahau Mabaya?

Hapana shaka yoyote kwamba binadamu hawezi kujitenga na jamii, akakata uhusiano wake na wanadamu wenzake, na akajiweka kando peke yake. Kwa sababu binadamu ni kiumbe mwenye kuhitajia, na mahitaji yake hayana kikomo. Kwa hivyo, kufuatana na kanuni ya kimaumbile na haja, ni lazima maisha ya mtu yategemee jamii ili kwa ushirikiano na wanajamii wenzake aweze kuyatatua matatizo ya maisha moja baada ya jingine. Kwa upande mwingine, maisha ya kijamii yana masharti yake ya kila aina. Mara tu mtu anapotia mguu wake katika uwanja wa jamii, sheria na shuruti huja pia. Hutokeza nyadhifa na desturi ambazo kwazo huleta mafanikio kwa kutekelezwa kwake kwa ukamilifu. Maisha ya kijamii ambayo ni miongoni mwa misingi athirifu katika kujenga shakhsia ya mtu, hayastahili kukomea katika mazingira ya kifizikia. Yanapaswa maingiliano yawe yanatokana na ufungamano wa nafsi, na ushirikiano na uhusiano wa kidhahiri uwe unalingana na hali ya kiroho. Jamii inapokuwa na moyo wa umoja, uhusiano kati ya watu hufungamana imara na huwa ni muhali kuharibika maisha ya masikilizano.

rudi nyuma Yaliyomo endelea