rudi nyuma Yaliyomo endelea

122

Mhenga aliulizwa: "Jambo gani ni gumu kabisa kuliko yote, na jambo gani ni rahisi kabisa kuliko yote?" Akajibu: "Jambo lililo gumu kabisa ni mtu kujijua mwenyewe, na jambo lililo rahisi kabisa ni kutoa aibu zawengine!"

Kikundi cha Watoao Aibu

Baadhi ya watu wana tabia mbaya ya kupenda kupeleleza udhaifu na aibu za wengine na kuchungua siri za watu. Huwachambua na huwasengenya kwa kejeli na mzaha watu wengine ilhali wao wenyewe wana aibu na udhaifu mwingi ulioshinda mema yao. Wanazipuuza aibu zao na wanazifumbia macho, na badala ya kuzisafisha nafsi zao wenyewe ndio kwanza wanazitafuta aibu na dosari za wengine.

Kutoa aibu ni katika sifa ambazo huharibu maisha na hushusha hadhi ya kimaadili.

Mambo yanayomshawishi mtu kuwahizi na kuwatolea watu aibu zao yanatokana na aina moja ya hisia ya udhalilifu na uduni ambayo huchochewa na huimarishwa na majivuno na ubinafsi. Uharibifu unaotokea katika maadili na roho za watu kutokana na tabia hiyo huwafanya watoe uamuzi usio sahihi juu ya watu wengine na wao wenyewe kujifikiria kuwa ni watu jasiri na sawa.

Wakosoaji wanapoteza bure uwezo wao wa kuyachunga mambo yasiyopendwa na akili, kwa sababu hutumia jitahada zao katika kuwachungua marafiki zao na kupeleleza vitendo vyao ili wazipate aibu na dosari

123

zao na waanze kuwachambua na kuwasema. Huendelea kutumia mbinu hiyo ya uharibifu mpaka pale wanapopata fursa ya kuwaumbua na kuwatweza watu. Hapana shaka kwamba kwa kudadisi na kupeleleza kwao mienendo ya wengine, kunawanyima fursa ya kutosha ya kuchunguza tabia na vitendo vyao wenyewe, na kwa sababu hii, hushindwa kufuata mwendo mwema na safi. Kwa kawaida, watu kama hao hukosa unyofu na haya kwa kadiri kwamba wanapojichafua katika mwendo huo huona si lazima kwao kuweka heshima ya mtu yeyote, na hata huwa hayumkiniki kuingiliana kwa moyo safi na marafiki walio karibu nao sana. Mwambi anapokwenda kwa rafiki yake hutoa aibu za watu wengine, lakini anapopata uwanja wa kushambulia, haachi kumkosoa, kutoa aibu na kumchambua rafiki yake mbele ya wengine. Kwa hivyo, mtu mwenye tabia ya kutoa aibu za watu hawezi kujipatia marafiki wa kweli ambao watampenda na watamfurahisha moyo wake kwa mapenzi na upole wao.

Mwanadamu mwenyewe ndiye mwenye kujenga heshima na utukufu wake. Mwenye kuvunja heshima ya wengine, hapana shaka atajivunjia heshima yake mwenyewe.

Huenda mtafuta aibu za watu asifahamu matokeo mabaya ya tabia yake, lakini akipenda au asipende hataweza kuepukana na radiamali na bidhaa ya matusi na ufidhuli wake. Tabia hii husababisha nyoyo za watu kuvunjika, huleta chuki na hata uadui, na matokeo yake ni juto la Firauni. Wahenga wamesema: "Maneno si kama njiwa ambaye anaporuka hurejea tena tunduni

124

mwake." (Hivyo, maneno yakikudondoka hayarejei tena mdomoni mwako!)

Mtu anayetaka kuishi na kuingiliana vizuri na watu, inampasa azijue nyadhifa zake. Siku zote awe anaangalia mema na mazuri ya watu, na avisifu na kuvithamini vitendo vyema.

Katika maisha ya kijamii, mtu anatakiwa ageuze mwendo na tabia ambazo zinavunja heshima za watu na misingi ya urafiki. Sakubimbi atakayeacha kutoa aibu za marafiki zake, atajenga msingi madhubuti wa mapenzi ya kidhati kati yake na marafiki zake. Usafi wake wa moyo na unyofu wake utaimarika zaidi atakapoiona aibu ya rafiki yake, lakini badala ya kutoa aibu hiyo mbele ya watu wengine, atatafuta fursa nzuri ya kumtanabahisha rafiki yake juu ya aibu hiyo na kumwomba ajirekebishe. Wakati wowote mtu akitaka kumwonesha rafiki yake makosa yake, itambidi atumie maarifa maalumu ili asije kukasirika na kuchukiwa.

Mwalimu mmoja wa maadili amesema:

"Unaweza kumjulisha mwenzako juu ya kosa lake bila ya kutaka kumwambia kwa kumtazama, kubadilisha sauti au kwa ishara ya viungo vyako. Kwa sababu ikiwa utamwambia: 'Umekosea,' hatakubali kwa kuwa utakuwa umetusi kinagaubaga akili yake, uwezo wake wa kufikiri na kutia dosari kujiamini kwake. Kwa kitendo hicho utamfanya akupinge na asibadilishe fikra zake wakati wowote. Huenda ukamtolea hoja za Plato na Aristotle lakini hutaweza kugeuza maoni yake ya ndani kutokana na kitendo chako cha kumwumiza moyo wake. Unapozungumza usijaribu kabisa kuanza

125

kwa maneno haya: 'Mimi nakuthibitishia.... Mimi nitakupa hoja zangu', n.k. kwa sababu maneno haya yanamaanisha kwamba wewe ni mwerevu zaidi kuliko yeye. Kitendo cha kusahihisha fikra za watu kwa mara nyingi huwa ni kazi ngumu, basi kwa nini ujitie zaidi matatani kwa kutumia mbinu isiyofaa na kujiwekea vizuizi vigumu zaidi? Unapotaka kuthibitisha jambo moja, angalia kwamba wengine wasitambue makusudio yako, na tumia maarifa na uhodari ili wengine wasifahamu unalolikusudia. Kumbuka msemo wa yule mshairi mashuhuri unaosema: 'Wafunzeni wengine bila ya kuwa wafunzaji.'"

Uchunguzi wa Mafunzo ya Kidini

Qur'ani Tukufu inatangaza mwisho mbaya wa wale wenye kuumbua na kutoa aibu za watu, na inawaonya juu ya adhabu watakayopata kutokana na tabia hiyo:

"Ole kwa kila mwenye kumwumbua na kumsema

mtu.

(al-Humazah, 104: 1)

Ili kuhifadhi umoja wa jamii, Uislamu unawajibisha kuheshimu misingi ya adabu ya maisha na unakataza tabia ya kuumbua na kuambaamba ambayo husababisha utengano na kuvunjika uhusiano wa ki'rafiki. Ni lazima Waislamu wawekeane heshima zao na wajiepushe kabisa na tabia ya kuhiziana, kudharauliana na kutukanana.

Imam Sadiq AS amesema:

126

"Yatakikana muumini awe ni kiburudisho cha (roho ya) muumini (mwenzake) kamavile maji baridi yanavyokata na kutuliza kiu."

(o/-^/(Jz.2,uk.247)

Imam Baqir AS amesema:

"Inatosha kuthibitisha aibu ya mtu anayeona aibu za watu wengine bila ya kuona yake mwenyewe, au anayewagombeza watu jambo ambalo yeye mwenyewe anashindwa kuliacha, au anayemwudhi rafiki yake kwa

jambo lisilomhusu."

(al-Kafi,]z.2,\±.459)

Haifai kuingiliana na kusuhubiana na watu wenye kutoa aibu za watu. Imam Ali AS amesema:

"Jihadhari na kuingiliana na wenye kutafuta aibu za watu, kwani hutasalimika na mazungumzo yao ya kutoa

aibu."

(Ghuraru 'l-Hikam. uk. 148)

Ingawa kwa kawaida mtu huwa hayuko tayari kuchambuliwa au kukosolewa, lakini ni bora kwake asikilize kwa makini na furaha ukosoaji sahihi wa makosa yake, kwani kwa kutanabahishwa huko makosa yake ataweza kujirekebisha na kusafisha roho yake.

Imam Ali AS ameonyesha nukta muhimu juu ya maudhui hii pale aliposema:

"Mtu bora kuliko wote mbele yako ni yule mwenye kukuonyesha aibu zako na kuisaidia nafsi yako."

(Ghuram 'l-Hikam, uk. 558)

127

Dk. Dale Carnegie ameandika:

"Ni lazima sote tukubali kwa furaha kukosolewa, kwani hatuwezi kutumainia zaidi ya robo tatu ya matendo na mawazo yetu yawe sahihi na sawasawa. Hata Einstein ambaye ni mwanafikra mkubwa kabisa katika zama hii, anakiri kwamba asilimia tisini na tisa ya fikra (nadharia) zake hazikuwa sahihi. Kila wakati mtu anapoanza kunichambua, ikiwa siwi mwangalifu, basi huanza kujitetea haraka bila ya kujua anataka kusema nini. Hivyo, kila ninapofanya kosa hilo, hujilaumu mwenyewe. Sote tunachukia kukosolewa na tunafurahi tunaposifiwa. Hatuangalii kama kukosolewa au kusifiwa huko kulikuwa ni sawasawa au la. Sisi hatukuzaliwa na ushahidi wala mantiki bali ni viumbe wenye hisia (za uchungu na furaha). Akili na mantiki yetu ni kama hori inayosukumwa huku na huko katika bahari yenye kina kirefu cha hisia zilizochafuka. Wengi wetu kwa hivi sasa tuna dhana nyingi zilizo nzuri juu yetu, lakini baada ya kupita miaka arobaini tunacheka tunapotazama nyuma na kujilinganisha na namna tulivyo leo."

(How to Win Friends and Influence People)

Imam Ali AS amesema:

"Mwenye (kutaka) kutafuta aibu za watu, aanze na zake."

(Ghurani 'l-Hikam, uk. 659)

Dk. Helen Shakhter ameandika:

"Ingekuwa bora badala ya kupinga matendo na maneno yasiyofaa ya wengine, tuwasaidie na

128

tuwaongoze tunapoweza. Na lililo wajibu kuliko hilo ni kujisaidia sisi wenyewe, yaani tuweke makosa na aibu zetu mbele yetu na tuzisahihishe bila ya kujionyesha au

kuogopa."

(Roshde Shakhsiyyat')

Mtu anapokuwa mtumwa wa ujinga na upumbavu wake, huzificha aibu zake badala ya kuzisahihisha.

Amirul Muuminin AS amesema:

"Inatosha mtu kujifanya mpumbavu mwenyewe kwa kutazama aibu za watu wengine huku akizificha zake."

(Ghurani 'l-Hikam, uk. 559)

Dk. Auibuty ameandika:

"Mara nyingi kutokana na ujinga wetu mwingi tunazidharau aibu zetu na tunazifunika kwa pazia la ujinga na kutojua ili tujidanganye wenyewe. Nijambo la kushangaza kweli kuona watu wanajaribu kuzificha aibu zao zisionekane na wengine, lakini hawafikirii kuzisahihisha. Ikitokea kwamba mojawapo kati ya aibu zao ikaonekana na wasiweze kuificha, hutoa maelt'u ya visingizio ili kujiridhisha wenyewe na kuwadanganya wengine. Hutaka kuonyesha kwamba aibu zao ni ndogo na si muhimu, lakini wanasahau kwamba aibu hata kama ni ndogo, siku moja itakuwa kubwa kama vile ambavyo mbegu ndogo huwa ni mti mkubwa baada ya

kupita siku nyingi."

(DarJostojue Khoshbakhti)

Kwa maoni ya wataalamu wa elimunafsi (saikolojia)

129

wa leo, uchunguzi wa nafsi ni njia ya kujua ugonjwa na kutibu maradhi mbalimbali.

Imam Ali AS amesema maneno matamu na yenye kuvutia kuhusu utambuaji na utibabu wa maradhi ya kinafsi kwa njia ya mtu mwenyewe kujichungua:

"Ni lazima kwa mwenye akili kuichungua nafsi yake na kuziona dosari zake katika dini, maoni, maadili na adabu; kisha azikusanye (azihifadhi) katika kitabu na achukue hatua ya kuziangamiza."

(Ghurani 'l-Hikam, uk. 448)

Njia ya Kujichungua na Kujijua

Mwandishi wa kitabu kiitwacho, Ravank-avi ametoa mwongozo ufuatao kwa ajili ya kuchungua nafsi yako na kuweza kujijua mwenyewe:

"Kaa kwa raha na utulivu katika chumba kilicho kimya kabisa. Weka saa moja usije kusumbuliwa na mtu yeyote. Ni bora mahali hapo pawe patulivu zaidi na wewe usiwe na haraka, kwa sababu kazi unayoitaka kuifanya sharti lake la lazima ni kwamba mawazo yako yasisikie sauti yoyote. Kwa maana nyingine, fikra zako zisijali kitu isipokuwa kile unachokusudia, na mawazo yako yasibabaishwe na mahitaji ya kimwili.

"Chukua karatasi nyingi za bei rahisi na kalamu moja unayoweza kuandikia kwa raha. Sababu ya kusema karatasi rahisi ni kukuwezesha kuzitumia kwa wingi bila ya kuwa na wasiwasi wa gharama zake, na nimetaja kalamu unayoweza kuandikia kwa raha kwa

130

sababu wakati utakapoanza kujichungua utasumbuliwa na maelfu ya mambo ya kinafsi, hivyo, utahitajia kalamu nzuri ili isikusumbue.

"Andika orodha ya kila aina ya hisia (nzuri au mbaya) uliyokuwa nayo siku hiyo au siku moja kabla yake.

"Baada ya kuandika orodha hiyo ya hamaki na furaha za siku hiyo, irudie mojamoja na andika fikra yoyote itakayokujia juu ya kila hisia bila ya kuficha kitu na bila ya kujali urefu wake.

"Baada ya kuandika vitendo, fikra na hisia za furaha na hamaki za siku hiyo kwa utaratibu huo, zitazame taathira na radiamali za ubinafsi, upweke na majivuno mbele yako. Kisha fikiria kila kitendo, fikra na hisia hizo na kila moja uliza swali hili:

"'Kitendo chenye hisia hii kimechochewa na tabia gani?'

"Shabaha hasa ya uchunguzi huu wa kinafsi ni kubadilisha shakhsia ya kiroho ya mgonjwa kwa kadiri kwamba nishati amirifu na nzuri za nafsi yake ziweze kuziondoa hali zake za kihamaki na ukinzani wa kiroho. Kwa njia hiyo, atajihisi ni mtu mpya, atapata thamani mpya na malengo mapya katika maisha yake. Kwa hakika, atakuwa amefuata mwendo mpya unaotofautiana na wa zamani."

8 - UHASIDI

133

Tamanio la Kushangaza na Potofu!

Katika ulimwengu huu uliojaa taharuki na vioja, binadamu huwa daima katika harakati na pirikapirika akiogelea katika mawimbi ya matatizo na masaibu. Maisha yake hufuatana na mashaka na matatizo, isipokuwa tu awe anachuma maua adimu katika bustani la maisha au awe anapata matumaini na matarajio yake moja baada ya moja. Madhali uzi wa uhai wa mtu haukukatwa kwa mkasi wa mauti, basi kila siku huwa na matumaini, huhangaika na hutafuta mafanikio. Taa ya matumaini ndiyo inayomwangaza mwenye matumaini, na matumaini hayohayo ndiyo yanayomgeuzia maisha yake machungu kuwa matamu.

Mtu mmoja huwa na tamaa ya kupata utajiri mkubwa na hutumia jitahada zake zote kuweza kuupata. Mwingine hutaka cheo na umashuhuri na huhangaika sana mpaka apate matakwa yake. Matakwa ya kila mtu yanategemea mahitaji yake ya kimwili na ukamilifu na usalama wa roho yake, lakini mawazo ya kila mtu yanatofautiana kabisa kutokana na namna ya kufikiri na kufahamu kwao kulivyo. Ni lazima tulizingatie hapa jambo hili la kimsingi, kwamba matakwa na matamanio huzalisha ufanisi na mafanikio wakati yanapoafikiana na mahitaji ya kiroho, yanapotimiza mahitaji ya kifikra, na yanapopandisha na kukuza kiwango cha maarifa. Vivyo hivyo, ikiwa taa inayong'ara ya mtu itaangaza maisha yake, basi atatoka

134

kwenye giza la kutisha la masaibu na mashaka.

Huenda mara nyingine mojawapo kati ya silika za kimwili kama vile uroho au ubarakala ikaasi na kuwa ni chanzo cha masumbuko ya mtu. Uhasidi ni mojawapo kati ya matunda ya silika za kimwili (kihawaa) ambao hujidhihirisha kwa kutamani vibaya, kuitia pingu dhamiri njema na tambuzi, na kumzuia mtu kuyapata matarajio halisi ya maisha yake. Mwenye kijicho hawezi kumtazama mwenzake akistarehe au akifanikiwa; moyo wake humchoma na husononeka kila anapowaona wenzake wananeemeka.

Socrates amesema:

"Mwenye kinyongo au kijicho hukonda anap-owaona wengine wamenenepa."

Maskini hasidi; anaupoteza umri wake wote akilia ngoa na kujiunguza nafsi yake. Huwatakia wenzake ubaya na hutumia kila njia ya ujanja na ulaghai ili wasifanikiwe.

Mwandishi mmoja mashuhuri ameandika:

"Roho zetu ni kama jangwa lisilo na ngome wala ukuta ambapo wezi wa furaha na mafanikio huweza kuingia kwa urahisi. Upepo mdogo kabisa huzitia wahaka na wasiwasi nyoyo zetu. Maadui wengi wa tamaa na hawaa huingia majumbani mwetu na kila mmoja hutuamrisha na hutusugua roho zetu. Kila mjinga hujua kwamba anapoumwa sana na kichwa inambidi aende kwa daktari kutibiwa, lakini yule mwenye kuugua uhasidi inambidi ateketee moyoni mwake!"

Ni kawaida kwa hasidi kuyafanyia kijicho mafanikio

135

na matakwa ya watu. Hujaribu kutumia majina na hila mbalimbali ili kuwapokonya baraka zao, na bila ya kufikiri hata kidogo hujifanya chambo cha tabia zake chafu.

Wakati mwingine hasidi hufunua roho yake kwa kuendelea kutangaza uwongo, na anapoona kwamba kwa njia hiyo hatosheki na ushakii huo na mazingira hayaafikiani na matakwa yake, basi huenda akavuka mipaka ya uhuru wa watu kwa kuzikandamiza roho zao kwa faida ya matamanio yake mabaya yasiyo na mpaka.

Je, ni kweli kwamba tamaa kama hiyo inahesabiwa kuwa ni miongoni mwa matakwa ya mwanadamu halisi na inalingana na utu wake?

Licha ya hasidi kutoka katika ubinadamu hata hudidimia na hudunika zaidi kuliko mnyama, kwa sababu hufurahia masaibu ya wengine. Mtu kama huyo hawezi kuwa mwungwana kweli. Kwa hivyo, mtu anayefurahia na kushangilia ukosaji na shida za wengine kuwa ni mafanikio yake, utamweka katika kikundi gani?

Hasidi Huungua kwa Kutopata na Kutofanikiwa

Mapenzi ya kijamii ni sababu muhimu kabisa ya mtu kupata maendeleo na mafanikio mazuri katika maisha yake. Yule mtu anayeonyesha ustahiki wake na sifa zake njema ndiye anayeweza kutawala nchi ya nyoyo na kupanda ngazi ya maendeleo kwa kunufaika kwa msaada na ushirikiano wa jamii na kupata ufunguo wa mafanikio. Mtu mzuri kwa tabia na amali ni kama

136

taa inayong'aa yenye kuongoza fikra na maendeleo ya jamii. Usafi wake wa moyo una taathira kubwa katika muundo wa maadili ya watu.

Kwa kuwa kijicho kina sura mbaya, hivyo, hujitangaza chenyewe kuwa ni adui wa tabia na sifa nzuri na kuzuizi kati ya watu. Kijicho hakimpi mtu fursa ya kupendwa na watu anaoingiliana nao wala kushukiwa na jaha. Hivyo, mwenye kijicho hukosa fursa za ushirikiano na neema ya mapenzi. Hasidi huonyesha waziwazi ubaya wake unaotokana na vitendo vya tabia yake mbaya, na kwa sababu hiyo hulaaniwa na huchukiwa sana na watu. Dhaa na huzuni ambazo huingia moyoni mwake kutokana na uhasidi, huikandamiza roho yake na hukoka moto mkali kuteketeza maisha yake.

Ni jambo linalofahamika kabisa kwa nini moyo wa mwenye wivu daima huona uchungu na huwa hauna raha wakati wowote. Kwa sababu, kinyume na anavyopenda yeye, upaji wa neema za Mwenyezi Mungu hauna kikomo, hivyo, kutu ya huzuni huwa haiwezi kutoka kabisa katika moyo wake. Kwa hakika, mfano wa ngoa au husuda ni kama kimbunga kinachoing'oa mizizi ya miti madhubuti ya akili na mema kwa kadiri kwamba hasidi huwa hana kizuizi chochote cha kimaadili au kidhati kumzuia kufanya kitendo chochote cha kihalifu.

Qabil alipoona kwamba dhabihu ya Habil ilikubaliwa na Mwenyezi Mungu na yake ilikataliwa, moyo wake ukazidi kuona uchungu hata akaamua kumwua ndugu yake, na akatekeleza mpango huo wa

137

kihaini. Kilio cha ngoa kilimjaa moyoni mwake kwa kadiri kwamba akasahau mapenzi ya kindugu, huruma na upole wa kiutu katika wakati huo wa hatari nyingi. Akauvuruga ubongo wa Habil na akautupa mwili wake mtakatifu katika mchirizi wa damu kwa kosa la usafi wa moyo na ikhlasi tu! Dunia ya siku hiyo iliyokuwa kimya na iliyoduwaa ilishuhudia tambiko la kwanza la uhasidi kwa kutokea jinai kubwa na ya kutisha ya kuuawa mwana na Adam. Hasidi alipokwishatenda ukatili wake akajuta juto la Firauni kwa ubaya alioufanya, lakini majuto hayo hayakuwa na faida, kwani dhamiri yake ilikuwa ikimtesa katika muda wote ambapo roho ilikuwemo mwilini mwake. Kama ungekuwepo utambuzi wa uhakika katika fikra za Qabil na mawazo yake yangekuwa safi, basi angetafuta sababu ya kutopata mafanikio ya haki katika dhati yake.

Bwana Shcopenhauer, mwanachuoni wa Kijerumani, amesema:

"Wivu au uhasidi ni miongoni mwa hisia za hatari kubwa kwa mtu, hivyo, unapaswa uchukuliwe kama ni adui wa kutisha mno wa ufanisi na ifanywe hima ya kuutokomeza."

Uhasidi ukishamiri katika jamii, migogoro na ugomvi wa kila aina pia huzidi. Mazingira kama hayo yanayochafuliwa na ugonjwa wa uhasidi huwa ni kizuizi mbele ya kila maendeleo badala ya kuwepo urekebisho na uboreshaji wa vipengee dhaifu vya maisha. Chuki, uchungu na upinzani wa mahasidi huwa ni kizuizi katika kufanya marekebisho yoyote, na matokeo ya mienendo hiyo huwa ni kuvuruga nidhamu ambayo ni kiini cha

138

ia maendeleo ya watu watukufu kwa manufaa ya watu wa kati, na ni sababu ya kuwekwa kando wale watu ambao wangeweza kuwa viongozi wa kesho wa umma."

utulivu na ustaarabu kuiangamiza jamii hiyo.

Dk. Carl amesema:

"Uzimbezimbe ulaumiwe uhasidi, kwa sababu ndio unaozuSehemu kubwa ya uhalifu unaotendwa kwa ukatili wa kila aina katika jamii ya kisasaunatokana na kijicho. Tukichungua kwa makini undani wa uhalifu huo tutaona waziwazi uhakika wenyewe.

Dini HukatazaUhasidi

Our'ani Tukufu inasema:

"Wala msitamani vile ambavyo Allah amewafadhilisha baadhiyenu kuliko wengine."

(an-N^aa', 4:32)

Ingawa ni kawaida katika maumbile ya mtu kutaka manufaa, lakini ni lazima matakwa hayo ya manufaa yawe katika mpaka wa sheria, yafuatane na msingi wa uhuru na mantiki ya akili, na yakubaliane na maslahi ya jamii ya wanadamu.

Kwa hivyo, Mwenyezi Mungu anapombariki mtu mmoja neema fulani, mwingine hana haki ya kumpokonya au kumvurugia neema hiyo kwa sababu ya kuwa na maumbile ya kutaka manufaa na kutaka kutuliza kijicho chake, bali inambidi atumie njia sahihi kuweza kupata matakwa yake. Kama vile alivyotuo-

139

nyesha Muumba wetu, ni lazima tuyatafute matakwa na mafanikio yetu katika jitahada. Mwenyezi Mungu kutokana na fadhila Zake za kudumu, anataka kuturahisishia njia ya masumbuko na mushkili ili tuweze kufikia malengo yetu.

Ikiwa nishati ya kifikra na hazina ya kihisia ya hasidi zitatumiwa mahali pake panapotakikana ili aweze kufikia shabaha yake, basi hapana shaka yoyote atapambazukiwa na mwanga wa matumaini na mafanikio, kwa sharti kwamba azitumie kuifuata shabaha yake kwa kupiga hatua za hima katika njia iliyojaa miiba na vizuizi, na kwa kutegemea nishati za kufuzu za Mwenyezi Mungu.

Zimepokewa hadithi (riwaya) nyingi kutoka kwa viongozi wa kidini zinazotutahadharisha juu ya tabia hiyo mbaya na kutuonya tusijichafue nayo. Inatosha kuzingatia sehemu moja ya maneno ya Imam Sadiq AS kuhusu suala hili. Katika hadithi hiyo, Imam ameashiria jambo muhimu sana la kinafsi:

"Asili ya kijicho ni upofu wa moyo na ukanyaji wa fadhila na neema za Mwenyezi Mungu. Sifa hizo ni mabawa mawili ya ukafiri. Kijicho humtia mwanadamu katika uchungu wa daima na humwangamiza kabisakabisa asiokoke kamwe!"

(Mwstadraku 'l-Wasa' il, jz. 2, uk. 428)

Dk. Mann ameandika:

"Jawabu ya baadhiya watu juu ya mashindano (ukinzani) yao ya kinafsini ni kukataa kuwemo ukinzani wowote humo. Kuhusu watu kama hao, tunawaambia

140

kwamba wameyagandamiza makusudio na matakwa yao. Mtoto anayeona wivu kukubali kuwepo nduguye mdogo huwa ameigandamiza fikra yake inayomuudhi. Kugandamiza kwa maana iliyowazi zaidi hapa ni kukataa kitu kilichokuwepo au kutokijali kitu kilichokuwepo. Kwa kawaida, kile tunachokigandamiza na kukitoa mawazoni mwetu huwa ni kitu kinachotughasi na kutuchoma."

(Usule Ravanshinasi)

Malezi mabaya katika mazingira ya nyumbani ni sababu mojawapo ya kutokea uhasidi. Wazazi wanapompenda mwanao mmoja kuliko mwingine, kutokana na kutojali huko, husababisha mtoto aliyenyimwa mapenzi awe na fundo la moyo na roho yake iasi. Chimbuko la uhasidi kati ya baadhi ya watoto huanza hapohapo, na wanapoinukia huharibikiwa na husumbuliwa maisha yao. Vilevile ikiwa nguzo za jamii hazisimamishwi juu ya msingi wa uadilifu na insafu, na ikiwa ubaguzi na udhalimu unatawala katika mambo yote, basi roho za watu huelekezwa katika mwendo wa kuasi na kuhalifu, na moto usioonekana wa uhasidi huwaka katika roho na nyoyo zao.

Mtume Mtukufu amekataza kila aina ya uonevu na utovu wa uadilifu ili kuwazuia watu wasiharibike kwa uhasidi na sifa mbaya. Amesema:

"Watendeeni sawasawa watoto wenu mnapowapa zawadi."

(Nahju 'l-Fasahah, uk. 366)

141

Bertrand Russel amemdondoa mwandishi wa The Fairchild Family akiandika yafuatayo kuhusu njia za kuyakwepa madhambi ya siri ya moyo:

"Lucy anajiona ana mwendo mzuri. Mamake anasema kwamba ingawa mwendo wake ni mzuri lakini fikra zake si sahihi, na anamdondoa Armiya akisema kwamba moyo umejaa ulaghai na uchafu kuliko kitu chochote kile. Kisha Lucy anapewa daftari ndogo arekodi humo zile fikra chafu kabisa zinazomtokezea moyoni mwake ingawa yeye mwenyewe anaonekana kuwa na mwendo mzuri na mtulivu. Wakati wa kula chakula cha asubuhi, wazazi wake walimpa dada yake kaseti na kaka yake gilasi, lakini yeye hakupewa kitu. Kwa hivyo, Lucy akaandika katika daftari yake kwamba wakati huo ilimjia fikra mbaya sana, nayo ni hii, kwamba wazazi wake hawampendi kama wanavyowapenda ndugu zake wawili. Wazazi walimfunza Lucy mafunzo muhimu, naye akaamini kwamba ni lazima akabiliane na aishinde fikra kama hiyo kwa kutumia uwezo wa nidhamu ya kimaadili. Lakini mbinu hiyo haikuleta faida isipokuwa fikra hiyo ikabaki katika moyo wake mpaka katika miaka ya baadaye ambapo ikatokeza athari yake iliyokwenda zigizaga."

Imam Ali AS ametaja madhara ya kimwili ya kijicho:

"Naustaajabia mghafala wa mahasidi juu ya uzima wa miili yao."

(Ghuraru 'l-Hikam, uk. 494)

142

Dk. Frank Haurk amesema:

"Toeni uhasidi katika bongo zenu. Uhasidi ni majonzi ya hisia za kiroho zisizofanikiwa na ni mashetani wa rohoni. Mashetani hao si tu kwamba hawaridhiki na kuchafua hali ya mtu peke yake, bali huwa ni chanzo cha kuzidi seli za sumu katika mwili. Matokeo yake ni kuumia mwili na kuzuia mzunguko wa damu. Kwa kufanyika sumu mwilini, neva za fahamu hudhoofika na huleta hasara kubwa kwa nishati za mwili na roho. Madhara yake mengine ni kuvunja moyo, kupotoa malengo matukufu na kudhoofisha kiwango cha kipawa cha akili. Ni lazima (mashetani hao wa uhasidi) watengwe mbali na maisha, wahesabiwe kuwa ni maadui wauaji, na wafungwe katika jela iliyo mbali na maisha. Mwenye kufuata haya, ataona makusudio yake yakiimarika zaidi, na kutokana na nguvu za makusudio yake aliyoyapata ataweza kuishi na kuyashinda matatizo yote."

Imam Ali AS amesema:

"Kijicho huuangamiza mwili."

(Ghurani 'l-Hikam, uk. 32)

Na mahali pengine ametaja madhara yake ya kinafsi:

"Jihadharini na uhasidi, kwani huitia ila nafsi."

(Ghuraru 'l-Hikam, uk. 141)

Mwanasaikolojia mmoja ameandika:

"Hapana shaka wivu uliotia fora ni mojawapo kati ya maumivu makali yanayosumbua sana roho ya mtu na

143

yanayosababisha makosa mengi na uonevu mwingi. Tunajua kwamba idadi kubwa ya amali za hasidi hazifanywi kwa kupenda yeye mwenyewe, bali zinafanywa kwa kutii maamrisho ya uhasidi wa kiifriti." (Ravankavi)

Imam Zaynul Abidin AS alimwomba Mwenyezi Mungu hivi:

"Ewe Mwenyezi Mungu! Teremsha rehema na baraka kwa Muhammad na Aali za Muhammad; na nipe kifua kilichohifadhika na uhasidi, ili kwamba nisimwonee wivu yeyote kati ya viumbe Vyako juu ya fadhila Zako; wala nisione kijicho juu ya neema Zako ulizompa yeyote kati ya viumbe Vyako- ziwe ni neema za dini au dunia, afya au takwa, nyingi au nyepesi, ila kwamba nitamani bora zaidi kwa ajili yangu lakini kutoka Kwako Peke Yako, (Ewe) usiye na mshirika."

(Sahifah Kamilah, dua ya 22)

Tusikubali kuachia matamanio machafu na matarajio duni yanayofanya maisha ya binadamu machungu yazuie ukamilifu na utukufu wa roho zetu, bali ni lazima tuzielekeze fikra zetu kwenye malengo aali, na daima tutamani sifa na tabia bora za kiutu. Kwa sababu kuwa na matarajio mazuri na yanayofaa na kujitahidi katika kugeuza mwelekeo wa fikra, kutaleta natija nzuri na mwisho wake kutamfikisha binadamu kwenye malengo na matarajio mema.

Amirul Muuminin AS amesema:

"Shindaneni katika maadili yanayovutia, matumaini

144

makubwa na mawazo matukufu ili mpate jazaa kubwa." (Ghuraru 'l-Hikam, uk. 355)

Dk.Marden amesema:

"Ikiwa utazingatia fikra zako juu ya sifa unazotamani, mwisho wake utazipata. Tabia ni zao la fikra ya kimaumbile. Ikiwa umetamani uvivu na starehe, basi utakuwa mvivu na mtu wa anasa. Ikiwa una mtazamo mbaya na kila kitu unakiona cheusi mbele yako, unaweza kujiokoa kutokana na udhaifu huo katika muda mfupi tu. Njia yake ni kufikiria kinyume na mtazamo huo, yaani fikiria vitu vinavyokupa nishati na uchangamfu katika dunia. Ikiwa utatamani kuwa na murua, shikilia katika kutamani huko ili dhamiri yako iwe tayari kupokea sifa nzuri hizo, na hapana shaka utakuwa na murua. Usiogope kukariri matumaini na malengo yako, yachore matakwa yako katika fikra zako na mwambie kila mtu kwamba unataka kuyapata matumaini hayo; na katika muda mfupi tu utaona jinsi ubongo wako utakavyokuvuta kama sumaku kwenye malengo hayo."

(Piruzi Fikr)

Dk. Mann anafafanua zaidi jambo hili:

"Tumejaribu na kuvumbua katika baadhi ya mambo kwamba kutafakari juu ya amali moja kunasababisha amali hiyo ifanyike kidogo kabla yake. Kwa mfano, ikiwa utafikiria kufumbata mkono wako, misuli ya mkono wako itaanza kuvutika na neva itajikunja kwa kadiri kwamba utaweza kupima kwa chombo maalumu

145

kiitwacho ducolanometer. Watu wengine pia wamejifunza na wanaweza kuyafanya malaika yao yasimike. Wengine wameweza kuifanya mishipa midogo ya mikono yao ikunjane kwa kufikiri sana kwamba mikono yao imo ndani ya maji ya barafu. Fikra zao zimeathiri sana kwa kadiri kwamba utafikiri kama kweli mikono yao ilitiwa ndani ya maji baridi. Vilevile watu wengine waliweza kuzidisha au kupunguza ukubwa wa mboni zao za macho kwa kukaza fikra zao juu ya mboni na kuziamrisha zizidi au zipungue ukubwa wake."

(Usule Ravanshinasi)

Kutambua uhakika kunasaidia sana katika tafakuri na matakwa ya mtu. Pazia la tamaa ndilo daima linaziba maono ya fikra na kuyaweka katika giza na dhaa. Inafaa kwanza kioo cha fikra na akili king'arishwe kwa uchaji (takwa) ili uhakika uweze kuonekana hapo. Kisha kwa nia imara na jitahada za nguvu, ni lazima zisafishwe alama za kijicho na tamaa za sumu kwenye kiini cha moyo! Baada ya hapo, ni lazima ikatwe minyororo ya chuki na bughudha iliyokuwa ikiibana roho, ili roho ijikomboe katika majonzi na badala yake hisia ya kuwatakia wengine mema na kheri iwe ni tabia ya lazima kwa kila mwanadamu.

9 - TAKABURI

149

Mwangaza wa Mapenzi katika Upeo wa Maisha

Upeo wa maisha ya wanadamu huangazwa kwa nuru ya mapenzi. Mapenzi yana taathira kubwa na ya kudumu na yamna nguvu kubwa katika maendeleo ya kimaada na kiroho ya mwandamu. Nguvu hizo huanzia kwenye mkondo wa maumbile ndani ya dhamiri ya mtu na ya maana na kumalizikia katika hazina kubwa isiyo na kikomo.

rudi nyuma Yaliyomo endelea