rudi nyuma Yaliyomo endelea

Mojawapo kati ya sababu kubwa ya misiba ya jamii ni kuenea ujanja na ria na kutokuwepo uaminifu kati ya matabaka mbalimbali ya watu. Unafiki unapoingia katika muundo wa jamii na ukatawala katika nyoyo za watu, licha ya kuvurugika na kuharibika tabia za watu, jamii hiyo pia huelekea katika njia ya maangamizo na upotofu.

Mwanachuoni mashuhuri wa Kiingereza amesema:

"Maadili ya wanasiasa na wanajamii wa zama zetu yanaharibika na kupotoka. Leo maoni yanayotolewa katika vyumba vya kukaribisha wageni yanatofautiana na yale yanayotolewa hadharani. Ushabiki wa watu unasifiwa katika mikutano ya hadhara, lakini katika mikutano ya faragha huchekwa na hufanyiwa masihara. Kubadilishabadilisha dhamiri na fikra katika zama hizi kumezidi kuliko wakati wowote ule, na shabaha na misingi yao daima hugeuzwa na kubadilishwa kufuatana na maslahi yao. Kujionyesha na kujigamba kutatoka katika kikundi cha sifa mbaya kidogokidogo. Ikiwa watu wa tabaka la juu watazoea kufanya ria na kujigeuzageuza, basi watu wa tabaka la chini pia hawatabaki nyuma katika kuchukua sifa mbili hizo. Siku zote watu wa tabaka la chini huchukua maadili na

96

mwendo wa watu wa tabaka la juu kama kielelezo chao, na huwaiga katika usongombwingo na unafiki. Umashuhuri unaosifiwa siku hizi badala ya kuonyesha sifa njema za mtu, aghlabu huwa ni kusifu sifa zake mbaya. Methali moja ya Kirusi inasema: 'Aliye nao uti wa mgongo madhubuti, hatapata cheo kamwe.' Lakini uti wa mgongo wa yule mwenye kupenda umashuhuri ni mlaini na unapindika, na huweza kuupinda mgongo wake upande wowote ule unapovuma upepo wa umaarufu. Umashuhuri unaopatikana kwa kuwadanganya watu, kuficha ukweli mbele ya umma na kusema na kuandika kufuatana na maumbile na raghba ya matabaka tofauti ni mbaya; na mbaya kuliko wote ni ule umashuhuri unaopatikana kwa kutumia migongano ya kitabaka katika jamii. Umashuhuri huu ni mwovu na mbaya kwa maoni ya kila mtu mwema na mwenye dhamiri; na mtu aliyepata umashuhuri kwa njia hiyo hana uzito wala thamani yoyote!"

Uaminifu na usafi wa moyo ni miongoni mwa alama za ubinadamu na dhamiri safi, na ni mwendo aali na bora kabisa wa maisha. Sifa hii tukufu ambayo hutokana na roho takatifu humpa mtu shakhsia madhubuti, huleta umoja na amani, huimarisha na huisawazisha jamii. Bila shaka mtu mwenye kuwa na sifa hii huwa na mapenzi makubwa juu ya marafiki zake walio waaminifu, na kiwango cha mapenzi hayo huwa ni sawa na machukio aliyonayo kwa kuingiliana na wanafiki.

97

Unguzeni Hiyo Nyumba ya Unafiki!

Wakati Uislamu ulipokuwa ukienea kwa haraka, kikundi cha wanafiki ambacho kilikuwa kikiona msimamo wao dhaifu ulikuwa hatarini, kilijitokeza mbele kuliko vikundi vyote vya upinzani ili kuhujumu msingi wa utawala wa Kiislamu. Wanafiki hao walifunga mikataba na Mtume Mtukufu kidhahiri tu, kwani walipojaribiwa kimatendo walishindwa kutekeleza majukumu yao, na walikuwa wakiwafanyia masihara Waislamu wengine. Mafisadi na wahujumu hao wachache ambao hawakuwa na hadhi ya kidini wala kimaadili, walishindwa kutambua imani na ikhlasi ya watu juu ya Mtume Mtukufu. Kiongozi wa kikundi hicho alikuwa akiitwa Abu Aamir Rahib, ambaye kabla ya Mtume Muhammad SAW kuhamia Madina, alikuwa ni kiongozi wa kidini wa Mayahudi na Wakristo. Yeye mara kwa mara alikuwa akiwabashiria watu kuja kwa Mtume Mtukufu, naye akawa ni miongoni mwa watu wa mwanzo kusilimu. Lakini alipoona kwamba hadhi yake ya zamani ilikuwa ikimtoka na watu hawakuwa wakimjali kwa sababu ya kuzidi kwa nguvu za Mtume, hakuweza kuvumilia hali hiyo. Hivyo, akahamia Makka ambapo alikuwa akichochea dhidi ya Uislamu, na akashiriki katika vita vya Badr na Uhud kwa upande wa washirikina. Kisha akakimbilia Roma ambapo daima alikuwa akipanga njama za hatari ili kuikata mizizi ya mti uliostawi wa Uislamu.

Ili kutekeleza njama yake, kwanza, Abu Aamir

98

aliwaamrisha marafiki zake katika Madina wajenge msikiti. Kwa kuwa hakujawezekana kujenga msikiti bila ya kupata ruhusa ya Mtume Mtukufu, hivyo, kiongozi mmojawapo wa wanafiki akatumwa kuchukua ruhusa hiyo kwa kutumia visingizio mbalimbali; na alipopata ruhusa hiyo akaanza kujenga msikiti polepole. Mtume Mtukufu aliporejea kutoka vita vya Tabuk, wajenzi wa msikiti huo wakamwalika (Mtume Mtukufu) kuubariki, wakitegemea kwamba kwa kuhudhuria kiongozi wa Kiislamu katika msikiti huo, wangeweza kutekeleza azma zao mbaya. Lakini Mtume Mtukufu alipopashwa habari juu ya njama yao, hakwenda msikitini. Kwa amri ya Mwenyezi Mungu akauita msikiti huo "Dharara" (dhara na udhia) ambao ulikusudia kuwa ni kitovu cha njama za wanafiki na makao ya ufisadi; na akapiga marufuku usikuwepo mkusanyiko wowote hapo. Kwa njia hiyo, njama yao ya kihaini ikavunjwa kabisa, na kwa amri ya Mtume Mtukufu nyumba hiyo ya unafiki ikatiwa moto!

Qur'ani Tukufu imewalaani na kuwashutumu vikali sana wanafiki; na katika aya mbalimbali imekishambulia sana kikundi hiki chenye mwendo mbaya. Mwenyezi Mungu amesema:

"Na katika watu wako wanaosema: 'Tumemwamini Allah na sikuya Akhera (Ufufuo);'na hali wao si wenye kuamini. Wanataka kumdanganya Allah na wale waliomini, na hawadanganyi ila nafsi zao, lakini hawafahamu. Nyoyoni mwao mna maradhi, na Allah amewazidishia maradhi (yao), na adhabu inayoumiza inawangojea kwa sababu ya kusema kwao uwongo. Na

99

wanapoambiwa: 'Msifanye ufisadi ardhini;' husema:'Sisi ni warekebishaji (wasuluhivu) tu.' Jueni kwamba wao ndio mafisadl, lakini hawafahamu."

(al-Baqarah, 2:8-12)

Sifa ya unafiki ni athari ya aina moja ya maradhi ya kiroho, udhalilifu na uduni. Amirul Muuminin Ali AS amesema:

"Jihadharini na wanafiki, kwani wao ni wapotevu na wanapoteza (watu). Nyoyo zao zina maradhi lakini nyuso zao ni safi."

(Ghuraru 'l-Hikam, uk. 146)

Dk. Helen Shakhter amesema:

"Baadhi ya watu wanapinga jambo fulani kwa lengo la kujitokeza na kupata umaarufu tu. Itikadi zao hazitokani na uchunguzi na tafakuri zao wala wao wenyewe hawaziamini, bali wanaona ni afadhali kwao kusema maneno yasiyo na maana na kupinga kuliko kubaki wasijulikane. Kwa sababu hakuna taabu kubwa kwao kuliko kuvumilia hali ya kutoendekezwa. Ajabu ioje ya baadhi ya watu ambao wanapoona kwamba hawaendekezwi, mara huenda njia ya unafiki na hutenda mambo yasiyofaa."

(Roshde Shakhsiyyat)

Imam Ali AS amesema:

"Maneno ya mnafiki ni matamu lakini moyo wake ni maradhi."

(Ghurani 'l-Hikam, uk. 60)

100

llivyokuwa ndumakuwili hana tegemeo madhubuti katika maisha yake, hivyo, maisha yake siku zote huwa ni ya kufazaika na kuyumbayumba. Mtume Mtukufu SAW ametoa taswira nzuri ya mnafiki kwa kusema:

"Mfano wa mnafiki ni kama kondoo anayebabaika kati ya makundi mawili ya kondoo."

(Nahju 'l-Fasahah, uk. 562)

Vilevile Mtume Mtukufu ametoa alama tatu za kauleni:

"Na mnafiki ana alama tatu: anaposema husema uwongo, anapotoa ahadi huvunja, na anapoaminiwa hufanyahiana."

(Bihani 'l-Anwar, jz. 15, uk. 30)

Imam Baqir AS amesema:

"Ni uovu mno kwa mja kuwa na nyuso mbili na ndimi mbili. Humsifu nduguye mbele yake lakini humsengenya nyuma yake. Akifanikiwa humwonea wivu, na akipata mashaka humtupa."

(Biharu 'l-Anwar.jz. 15, uk. 172)

Sifa nyingine ya wanafiki ni kujitetea wenyewe na kuwapinga wengine. Imam Ali AS amesema:

"Mnafiki hujisifu mwenyewe na huwakejeli watu wengine."

(Gliurani 'l-Hikam, uk. 88)

Dk. Samuel Smiles ameandika:

"Watu wenye kufanya ria daima hujishughulisha na

101

nafsi zao na hawawajali kamwe watu wengine. Hujipendelea mno nafsi zao, hujifikiria wenyewe na hujizingatia nafsi na hali zao tu kwa kadiri kwamba mwisho wake nafsi zao zilizo duni huziona ni ulimwengu na miungu yao."

(Akhlaq)

Imam Sadiq AS amemdondoa Luqman akimwusia mwanawe haya:

"Mnafiki ana alama tatu: ulimi wake hukinzana na moyo wake, moyo wake hukinzana na vitendo vyake, na dhahiri yake hukinzana na batini yake."

(Bifiani 'l-Anwar, jz, 15, uk. 30)

Mawazo, fikra na hali za ndani ndizo zinazodhihirisha sura halisi ya mtu. Ikiwa mtu atafunika kifuniko cha hila na ria juu ya maisha yake, hatapata mafanikio yoyote, na mwisho wake azma yake halisi itadhihirika.

Mtu mmoja alimwuliza Imam Sadiq AS: "Mtu mmoja alikuja kwangu na kuniambia kwamba ananipenda sana. Vipi nitajua kama kweli ananipenda sana?" Imam akamjibu; "Tahini moyo wako. Ukimpenda, basi anakupenda. Tazama moyo wako. Ukimkataa mwenzako, basi mmoja wenu ana hila."

(al-Wafi, jz. 3, uk.106)

Dk. Marden amesema:

"Ikiwa mnadhani kwamba mnaweza kujijulisha kwa watu kwa maneno yenu tu, basi mnajidanganya. Watu

102

wengine hawakudhanieni nyinyi kwa kipimo chenu wenyewe, bali wanakupimeni kwa hali na dhamiri zenu. Watu wanaozungumza nanyi hutambua fikra zenu, kama ni thabiti au dhaifu, safi au chafu. Hata wakati mnapokaa kimya, hutambua matumaini na makusudio yenu kwa njia ya miali inayotoka upande wenu. Na maoni yao juu yenu huwa imara sana kwa kadiri kwamba hawawi tayari kuyabadilisha hata mkipinga vipi.

"Mara kwa mara tunawasikia baadhi ya watu wakisema: 'Sipendi kuuona uso wa mtu fulani.' Mtu mwenye kusema maneno hayo huwa amemwona fulani huyo akicheka au akichangamka na watu, lakini juu ya hayo humchukia, kwa sababu amezisoma na amezihisi fikra zake mbaya za moyoni. . . . Athari hizo tofauti zinatokana na mnururisho wa kifikra. Sisi wenyewe pia huhisi vivyo hivyo juu ya watu wengine. Yale tunayoyafikiri na kuyahisi huwa yanatawanyika kutoka upande wetu katika sura ya mawimbi yasiyoonekana."

(Pimzi Fikr)

Imam Ali amesema:

"Dhamiri safi ni ushahidi bora zaidi wa ukweli kuliko lugha fasihi."

(Ghurani 'l-Hikam, uk. 501,)

Ni lazima izingatiwe kwamba unafiki unaokusudiwa ni wa kidini au wa kimaadili katika tabia na mwendo wa mtu. Uislamu unaitaka jamii ya Kiislamu iwe na umoja kamili; na unawaongoza Waislamu waishi maisha yaliyojaa mapenzi na uaminifu na yasiyokuwa na unafiki

na na.

6 - USENGENYAJI

105

Jamii Iliyochafuliwa kwa Madhambi

Hapana shaka kwamba jamii ya leo inaugua maradhi ya kila aina ya upotofu wa kiroho na imezama katika bahari kubwa ya ufisadi. Kwa kiwango kilekile ambacho suhula za kimaada zimeleta maendelea na ustawi wa maisha, maadili mema pia yamezorota na kuharibika katika jamii. Mashaka ya kijamii yamezidj siku baada ya siku, na mazingira ya kijamii yameingia sumu na kuumia sana. Watu ambao walikuwa daima wakijitahidi ili kuyakimbia mashaka na misukosuko, sasa wanakimbilia kwenye ufisadi; wanatenda maovu na wanafuata mwendo mbaya ili kujipunguzia matatizo na usumbufu wao wa kiroho. Ni muhali kabisa kuweza jua la ufanisi kuangaza katika mfumo wa maisha ya jamii kama hii.

Utasema kana kwamba watu wamevunja miiko yote ya kijamii na wanashindana katika kurejea nyuma na kufurutu ada! Tunapoangalia vizuri, tunaona kwamba suhula na vyombo vya maendeleo vinatumiwa kinyume. Kwa ufupi, madhihirisho ya vitu vyenye kulaghai ndiyo yaliyofanywa kiini cha matumaini. Msingi mchafu wa kishetani ndio uliofunika uso wa jamii kwa vazi linalochukiza na kuifanya jamii iwe na sura ya kutisha.

Afadhali kati ya utajiri wote huo na gharama zisizo na kifani zinazotumiwa katika njia ya upotofu na uharibifu, sehemu ndogo yake ingetumiwa kwa ajili ya kukuza maadili mema. Ingawa kanuni za kimaadili ni

106

thabiti na hazibadiliki, lakini katika jamii yetu daima huwa katika hali ya kubadilika na kugeuka katika sura mbalimbali na rangi tofauti! Ni dhahiri kwamba ikiwa watu hawautambui wema kama ni kigezo cha shakhsia yao, basi hapana shaka kwamba wema hautathaminiwa, na wengi wao wataathiriwa na mazingira. Watu hao wataifuata hali yoyote itakayotokea katika maisha bila ya kuogopa matokeo yake mabaya. Hapo ndipo tunapojua kwamba ustaarabu kama huo hauwezi kuleta maadili sahihi wala kudhamini ufanisi na maslahi ya jamii.

Mwanachuoni mashuhuri wa Kifaransa, Dk. Carl, amesema:

"Sisi tunaihitajia dunia ambayo kila mtu ataweza kupata tena mahali panapofaa pasipotenganishwa mambo ya kimaada na kiroho na tutakapoweza kujua tuishi vipi. Kwa sababu tumekwishaelewa kidogokidogo kwamba ni hatari kupita kwenye njia ya maisha bila ya kuwa na dira au kiongozi. Ni ajabu kwamba kuelewa kwetu hatari hiyo hakukutufanya tutafute njia za kuunda miundo ya maana ya maisha. Ukweli ni kwamba idadi ya watu walioielewa hatari hiyo hivi sasa ni ndogo sana. Leo watu wengi wanaishi katika mawazo yao na wamelewa na suhula za kimaada walizopata kutokana na maendeleo ya teknolojia. Hawako tayari kusamehe hata fursa moja waliyopata kutokana na ustaarabu mpya, bali wanayapitisha maisha yao katika mkondo wa matamanio kama vile ambavyo maji ya mito yanavyoteremka katika ziwa, upwa au bonde. Huyapitisha maisha yao katika kila aina ya ufisadi na

107

uduni na kuyaridhisha matamanio yao kwa starehe na tamaa. Watu wanajitafutia mahitaji mapya kwa ajili yao na wanakidhia mahitaji hayo kwa uroho mwingi. Lakini kuna matamanio mengine ambayo huwa ni rahisi zaidi kwao kuyaridhisha kwa kusengenya, kulaghai na kuzungumza mambo ya upuuzi. Hayo machafuko ya kifikra ambayo watu wengi wanajifurahisha nayo ni hatari kama ulevi."

Kusengenya ni mojawapo kati ya ufisadi mkubwa wa kijamii. Katika mjadala wetu huu, hatuna haja ya kuelezea maana yake ya kiistilahi, kwani kila mtu, awe mjuzi au maamuma, anaifahamu maana yake kwa urahisi.

Madhara ya Kusengenya

Madhara ya kwanza ya kusengenya ni kuharibika thamani ya maisha na shakhsia ya kiroho ya mtu mwenyewe. Watu waliotoa nyoyo zao kwenye njia ya kimaumbile, huwa wamepoteza fikra makini na nidhamu ya kimaadili. Wasengenyaji huziumiza nyoyo za watu kwa kutoa siri na aibu zao. Kumsema mtu hubomoa kasri kubwa ya wema. Huharibu kwa haraka sana maumbile na tabia safi ya binadamu, na huchoma na huangamiza mizizi ya utukufu na ubora katika nyoyo. Kwa ufupi, hii hulka mbaya inabadilisha mwendo wa fikra safi na inaufungia moyo madirisha ya fahamu na akili! Tukichungua upande wa jamii, tutaona kwamba ghiba imepiga pigo kubwa kwenye mwili wa jamii. Imechukua nafasi muhimu katika kutia chuki na

108

uhasama. Kama kuteta kutaendelea, basi heshima na itibari za taifa zitapakwa matope na kutatokea utengano na mwanya mkubwa katika umoja wa jamii ambao hautaweza kuzibwa kamwe.

Ni jambo la kusikitisha kukiri hapa huu ukweli mchungu kwamba leo mabaraza ya kusemanasemana yamestawi kilamahali kwa kadiri kwamba hakuna baraza lolote asiposemwa mtu. Kuwepo kwa uhusiano kati ya matukio ya dunia na urahisi wa mawasiliano kumesababisha kutokea na kutapakaa kwa haraka upotofu wa kiroho kati ya watu wa matabaka mbalimbali ya jamii. Kutokana na athari mbaya ya kuenea usengenyaji, roho za watu zimetia dhana mbaya fikra za watu kwa kadiri kwamba uaminifu na kuaminiana kumeondoka. Kwa hivyo, ikiwa sifa njema na aali ya roho haitaangaza katika jamii, uaminifu hautapatikana tena. Jamii inayokosa neema ya maadili mema, itakosa pia mazuri ya maisha.

Chanzo cha Ugonjwa Huo wa Kiroho na Dawa Yake

Ingawa usengenyaji ni dhambi ya kimatendo, lakini una uhusiano wa moja kwa moja na nafsi ya binadamu na ni alama ya mchafuko wa hatari wa roho. Hivyo,ni lazima litafutwe chimbuko lake katika moyo.

Wataalamu wa elimu ya maadili wametaja sababu kadhaa zinazosababisha usengenyaji, na muhimu zaidi kuliko zote ni: uhasidi, hamaki, ubinafsi na dhana mbaya. Athari zote zinazotokeza nje na kazi zote

109

zinazofanywa na mtu ni matokeo ya hali mbalimbali zilizomo moyoni mwake. Kukusanyika mojawapo kati ya sifa hizo mbaya, huwasha moto wenye miali mikali ndani ya moyo wa mtu na husababisha ulimi wa kusengenya uanze kufanya kazi, kwa kuwa ulimi ni siri ya ndani.

Sifa mbaya inapoota mizizi katika moyo, husababisha macho ya mtu yasione na huitawala fikra yake asteaste. Kushadidi kuenea usengenyaji kunatokana na kukaririwa kitendo hicho na kutozingatiwa matokeo yake mabaya, kwa sababu tunaona kwamba watu wengi ambao wanajiepusha na maasi mengine huwa hawana hofu ya kutenda dhambi kubwa kama hii. Kurejearejea kitendo hicho na udhaifu wa kutumia akili humfanya mtu afike katika hali ambayo humshinda kujizuia na tamaa ya nafsi yake licha ya kujua madhara yake. Ingawa kwa upande wa elimu binadamu amefikia daraja ya kutambua uhakika, na kwa mujibu wa kimaumbile yupo katika kutafuta ukamilifu, lakini kutokana na tabia yake ya kuwasema watu, huwa hayuko tayari kuvumilia taabu ndogo kabisa (ya kutosengenya) ingawa anapenda kupata ufanisi. Kwa hivyo, mtu kama huyo hushutumiwa kwa uduni wake.

Watu wasiojilazimisha kuhifadhi heshima za wengine huwa ni muhali kwao kufuata misingi ya maadili mema. Watu wenye kuufanya uwanja wa maisha yao kuwa ni jaa la matamanio yao na huzikiuka haki za watu wengine bila ya kujali, wanastahili balaa na misiba.

110

Ulegevu na udhaifu huo wa misingi ya kimaadili unatokana na imani dhaifu, kwa sababu uthabiti na ustawi wa maadili mema unategemea imani. Ikiwa nguvu za imani hazitakuwa tegemeo la mtu, maadili mema hayataweza kudhamini utekelezaji wake.

Kila mtu kufuatana na silika na kipawa chake huwa na mbinu ya kuwaokoa watu kutokana na upotofu na kuwaondolea mashaka yao ya kimaadili. Lakini njia bora kabisa yenye kuathiri ni kuwapa watu motisho ya kujirekebisha wenyewe, kuzizindua hisia nzuri, kuutikia sawasawa mwito wa kimaumbile, na kuzitumia hazina safi za kifikra katika njia ya ufanisi na saada. Kwa kuzingatia matokeo mabaya ya sifa mbaya na kwa kuimarisha azma ya kuepukana na maadili mabaya, tunaweza kuushinda uasi wa nafsi zetu na kuliondoa giza nyoyoni mwetu na badala yake kuzing'arisha kwa

sifa tukufu.

Bwana Jago ameandika haya katika kitabu chake

kiitwacho Qudrate Iradeh:

"Tunapotaka kupambana na tabia mbaya, ni lazima kwanza tuyasawiri moyoni mwetu matokeo yake mabaya, kisha faida zitakazopatikana kutokana na kuacha tabia hiyo. Tena tusawiri nyanja mbalimbali za maisha, na tuyakumbuke matukio mbalimbali yaliyotutokea kutokana na kuacha ada hiyo. Kila wakati tutakapotazama taswira hiyo katika mawazo yetu, tutaona raha ya kuiacha tabia hiyo na kuushinda

ushawishi huo."

Kwa kuwa kipawa cha kujikamilisha kimewekwa katika nafsi ya binadamu, na nchi ya mwili imedhibitiwa

111

kwa silaha kamili za kujitetea, hivyo, itabidi kwanza kitambuliwe chanzo cha ubaya, kisha (ubaya huo) uondoshwe moyoni na uangamizwe kwa nguvu barabara, na kiwekwe kizuizi mbele ya matamanio yasiyo na mpaka.

Vitendo vya watu vinadhihirisha utukufu wao wa kweli. Thamani ya muundo wa nafsi ya kila mtu inadhihirishwa na mwendo wake. Ikiwa mtu anataka apate ufanisi, ni lazima kitendo chake ambacho ni athari ya nafsi yake kiwe kitukufu na safi ili kibaki kama athari ya thamani na inayong'ara katika maisha yake yote. Ajue katika kila hali kwamba Mwenyezi Mungu anaangalia amali zake, na aogope matokeo mabaya ya dhambi na adhabu ya Akhera. Awe na hakika kabisa kwamba kitendo chake, hata kiwe kidogo vipi, kinarekodiwa kwa uangalifu mno na chombo kikubwa na cherevu cha ulimwengu.

Mwanafalsafa mmoja amesema:

"Msiseme kwamba ulimwengu hauna akili, umekufa au hauna hisia, kwani kwa kusema huko mtajithibitisha wenyewe kama hamna akili. Kwa kuwa nyinyi mmetokana na ulimwengu, hivyo, kama haukuwa na akili na hisia, nyinyi pia msingekuwa navyo."

Kwa kadiri hiyohiyo ambayo jamii huhitajia mahitaji ya dharura ya maisha ili kuweza kuendelea, vivyo hivyo, huhitajia sana unyofu na usafi wa moyo kwa ajili ya uhusiano wa kiroho. Ikiwa watu watatekeleza majukumu yao ya kijamii, watafaidika mno na maadili mema na wataendelea katika njia ya ukamilifu. Ni lazima tuziimarishe fikra bora zikabiliane na fikra zenye

112

kudhuru ili nafsi zetu ziweze kujikinga kutokana na sumu zake. Kuzihifadhi na kuzidhibiti ndimi zetu kutokana na usengenyaji ni hatua ya kwanza kufikia kwenye lengo la ufanisi unaodumu daima. Ni lazima mabadiliko na mapinduzi ya kiroho kati ya watu yaende sambamba na utapakaaji wa ufisadi. Ni lazima pia roho ya kuheshimu haki za wanadamu wenzetu izinduliwe, na misingi ya kiimani na kibinadamu iimarishwe. Tujitahidi kwa kadiri ya uwezo wetu kupiga hatua ya kimsingi kuimarisha nguzo za kimaadili ambazo kwazo zinaegemewa na jamii yetu. Ikiwa harakati za kiroho zitaanza kati ya watu, hapana shaka yoyote kwamba watu watakuwa tayari kuamini ukweli kwa haraka na kwa dhati, na matokeo yake ni kutekelezwa vizuri kanuni za kijamii na kimaadili.

Dini Hupambana na Maadili Fasidi

Our'ani Tukufu inatoa picha ya maana halisi ya usengenyaji katika jumla ndogo na fasihi:

"Je, mmoja wenu anapenda kula nyama ya nduguye aliyekufa?"

(al-Hujaraal, 49:12)

Kama vile ambavyo ni tabia ya kibinadamu kuchukia kula nyama ya mfu, vivyo hivyo, ni lazima akili ya mwanadamu ichukie kufanya ghiba. Viongozi wa kidini walijitahidi sana kurekebisha sifa na tabia za kinafsi kama vile walivyopambana na ushirikina na dhana mbaya.

113

Mtume Mtukufu amesema:

"Mimi nimetumwa kukukuzieni na kukukamilishieni maadili mema."

Kwa hivyo, kwa kutumia mantiki makini na sera yenye saada, akawaongoza watu kwenye maadili mema na akakataza kabisa na kupiga marufuku kukiuka mwenendo mwema.

Si tu kwamba kumsema mtu na kusikiliza mtu akisemwa ni dhambi, bali kwa mujibu wa sheria ya Kiislamu, kila Mwislamu anapaswa kutetea heshima ya mwenye kusemwa.

Mtume Mtukufu amesema:

"Ukiwepo katika baraza ambapo mtu mmoja husengenywa, basi msaidie mtu huyo, au wakataze wasengenyaji, au ondoka hapo."

(Nahju 'l-Fasahah, uk. 48)

Mahali pengine amesema:

"Mwenye kumtetea nduguye anayesemwa kwa ubaya wakati hayupo, hustahiki kwa Mwenyezi Mungu kuepushwa na Moto."

(Nahju 'l-Fasahah, uk. 613)

Mtume Mtukufu amesema pia:

"Mwenye kumsengenya Mwislamu, Mwenyezi Mungu hatazikubali funga na sala zake za mchana na usiku arobaini mpaka asemehewe na msengenywa .... Na mwenye kumsema Mwislamu katika mwezi wa Ramadhani, hatapewa thawabu ya kufunga."

(Biham 'l-Anwar, jz. 16, uk. 179)

114

Mtume wa Uislamu amewasifu Waislamu kwa sifa hii:

"Mwislamu ni mwenye kuwasalimisha Waislamu kutokana na mikono na ulimi wake."

Ni wazi kwamba yule mwenye kutumia ulimi wake kumsema Mwislamu, hutoka nje ya mpaka wa wema na huhalifu mwenyewe utu wake. Wanavyuoni wote wanaafikiana kwamba kusengenya ni miongoni mwa madhambi makubwa, kwa sababu licha ya msengenyaji kwenda kinyume na maamrisho ya Muumba, hukiuka haki za watu kwa kuwaumbua.

Kama vile ambavyo mwili usiokuwa na roho hauwezi kujitetea na kuuhifadhi mwili wake, vivyo hivyo, mtu asiyekuwepo huwa hana uwezo wa kutetea heshima na hadhi yake anaposemwa. Kwa hivyo, kama ilivyo kwamba ni lazima roho za watu ziheshimiwe, vivyo hivyo, ni lazima pia heshima zao zisivunjwe.

Chanzo cha kuwasengenya na kuwaumbua watu kinatokana na matatizo ya kinafsi.

Imam Ali AS amesema:

"Kusengenya ni juhudi za mtu dhaifu."

(Ghuraru 'l-Hikam, uk. 36)

Dk. Helen Shakhter amesema:

"Kila haja isipokidhiwa husababisha wasiwasi; na kila tukiwa na wasiwasi hutufanya tuwe waangalifu katika vitendo vyetu. Lakini vitendo vya watu wote haviwi sawasawa katika kuondoa wasiwasi wao uliowaingia kutokana na kukosa kupata mahitaji yao ya kijamii. Mtu anapoona kwamba watu wengine

115

hawamjali kama anavyotazamia, huwakimbia, hujitenga nao na huona afadhali asiingiliane nao kwa kuogopa asidharauliwe. Au akiwa pamoja na kikundi cha watu, hukaa pembeni kimya akiudhika roho yake na kuogopa. Au hufanya masihara yasiyo na maana au hucheka burebure. Au huwasema wasiokuwepo, hushindana na waliokuwepo na hupinga kila linalosemwa ili kwa njia hiyo apate kujionyesha kwao."

(Roshde Shakhsiyyat)

Dk. Mann ameandika:

"Ili kufidia kutofaulu kwetu na kuficha aibu zetu, mara nyingine tunajaribu kuwatupia lawama wengine ili kwa njia hiyo tuweze kuhifadhi heshima zetu. Kwa mfano, tunapofeli katika mtihani, tunamlaumu mwalimu au tunatoa ila katika maswali yenyewe. Tusipofanikiwa kupata cheo fulani, tunaishusha hadhi ya cheo hicho au tunaivunja hadhi ya mwenye kushika cheo hicho. Na mara nyingine tunawalaumu wengine kuwa ndio waliosababisha kushindwa kwetu, wakati ukweli ni kwamba hawakuhusika kabisa."

(Usule Ravanshinasi)

Kwa hivyo, tunafikia natija hii kwamba ni lazima tuimarishe mienendo mema kwa juhudi za kinafsi na usafi wa moyo. Tuanze kujirekebisha, kujisahihisha na kujisafisha wenyewe, ili upatikane uwanja wa furaha na utanisi katika vipengee vyote vyajamii yetu.

7 - KUTOA AIBU

119

Kutojijua Mwenyewe

Mojawapo kati ya aibu kubwa ya kitabia ambayo hairekebishiki ni mtu kutoona aibu zake. Aghlabu upotofu na ubaya unatokana na ujinga na ujahili. Mara nyingi sifa na tabia mbaya zinaposhika mzizi katika moyo wa mtu kutokana na ughafilifu wake, husababisha kusimama shina la mashaka na misiba katika maisha yake. Mtu anapokuwa mtumwa wa ujinga wa nafsi yake, roho ya wema hufa moyoni mwake, huwa mtumwa wa matamanio na tamaa mbalimbali, na hukosa furaha na ufanisi wa daima. Katika hali hii, jitahada yoyote au uongozi wowote wa kimaadili hushindwa kutoa natija.

Sharti la kwanza la kurekebisha nafsi ni kuzijua aibu zake mwenyewe, kwa sababu mtu anapozijua aibu na dosari zake huweza kuikata minyororo ya mabaya na machafu yake na akajiokoa kutokana na hatari ya aibu zisizopendeza ambazo humtumbukiza katika taabu na mashaka. Ni muhimu sana mtu azichungue sifa zake za kinafsi ili aweze kuikuza roho yake, kwani hakuna njia nyingine ghairi ya hii ambayo inaweza kumfikisha kwenye ukamilifu wa kiroho na kimaadili. Kujichunguza nafsi humpa mtu uwezo wa kuziona sifa mbaya na pia nzuri za roho yake, na kuwatoa maafriti kutoka katika mashimo ya roho yake. Kwa njia hii, mtu huweza kusafisha kabisa uchafu wa ndani na kukifanya kioo chake cha ndani king'are.

Ikiwa kwa sababu ya upuuzi wetu hatutaweza

120

kuona sura zetu hasa katika kioo cha vitendo vyetu, tutakuwa tumefanya kosa kubwa lisilosameheka. Kabla ya lolote lile, ni wajibu kwetu kwanza kuzichungua hali zetu za kiroho na kuziona waziwazi sura zetu za ndani, ili tuweze kuzitambua aibu zilizoota mizizi na kustawi katika dhamiri zetu bila ya sisi wenyewe kufahamu. Sisi wenyewe tu ndio tunaoweza kuikata mizizi ya sifa mbaya katika nafsi zetu kwa kufanya uchunguzi na jitihada, na tukazizuia (nafsi) zisidhihirishe ubaya wake katika mazingira ya maisha yetu. Hapana shaka kwamba kuitakasa na kuirekebisha nafsi sijambo rahisi, bali kunahitaji kuvumilia taabu kwa muda mrefu na kusubiri sana. Ili kuikata mizizi ya mazoea yenye hatari na madhara, na badala yake kupandisha sifa njema na mpya, ni lazima tuzitafute aibu zetu wenyewe-jambo ambalo linalazimu mtu kuwa na azma madhubuti katika kumwongoza kutekelezajambo hilo. Kila tutakapoweza kuzidhibiti tabia zetu na kuziwekea utaratibu maalumn ndivyo zitakavyonyooka na kudarijika nguvu zetu za kiakili. Kila hatua itakayochukuliwa katika njia hii itakuwa na athari zenye manufaa na zenye kudumn ambazo zitadhihirika mwisho wa kazi hiyo.

Mwanachuoni mashuhuri aitwaye Profesa Carl, ameandika:

"Ukitaka sera ya maisha iwe na maana, basi njia bora kabisa yenye faida ni kuzipanga kazi zake za kila siku kila asubuhi, na kuzichungua natija ya kazi hizo kila usiku. Kama vile tunavyopanga kazi zetu: tuanze saa ngapi na tumalize saa ngapi, tuonane na nani, tule nini, tunywe nini na mapato yetu yawe kiasi gani, vivyo hivyo,

121

tupange kwamba tutoe misaada gani kwa watu wengine na tuweke wastani wa namna gani katika kazi zetu. Maadili machafu ni machafu kama mwili mchafu. Watu wengi wamezoea kabla ya kulala na baada ya kuamka kufanya mazoezi ya viungo vyao ili vilainike. Mazoezi ya kifikra hayana umuhimu mdogo kuliko mazoezi ya kimwili, hivyo, ingekuwa bora kama watu hao wangetumia pia dakika chache kila siku kuziimarisha nishati zao za kimaadili, kifikra na kinafsi. Kwa kutafakari kila siku juu ya mwendo wako na kujitahidi kuifuata vyema sera uliyoipanga, unaweza kwa wakati huohuo kuziimarisha akili na azma zako. Kwa njia hiyo, utaivuka mipaka ya ujinga na utapiga mbizi katika kilindi cha akili ambapo kila mtu huweza kuiona sura yake mwenyewe bila ya kificho chochote. Mafanikio yetu katika kutekeleza kanuni za maisha zinategemea sana maisha yetu ya ndani kama vile ambavyo tajiri na mtafiti wanavyopanga kwa uangalifu daftari na nyaraka zao za utafiti. Ni lazima kila mtu, awe maskini au tajiri, mzee au kijana, msomi au mjinga, arekodi kila siku mazuri na mabaya aliyoyafanya. Kwa kutekeleza kwa uvumilivu utaratibu huo ndipo miili na roho zetu zitakapoweza kubadilika kidogokidogo."

Mtu wa maana mwenye mawazo maangavu huzipitisha jitihada na nishati zake katika mikondo inayofaa. Mtu mwenye heshima ya kiasi chochote kile ana haki ya kuheshimiwa na wengine; hivyo, hujiepusha kabisa na mambo yanayowaudhi watu, kwa sababu kitambulisho bora kabisa cha mwungwana ni tabia yake ya kila siku inayoonekana kwa kuingiliana na watu.

rudi nyuma Yaliyomo endelea