rudi nyuma Yaliyomo endelea

Huenda mtu anayedhaniwa vibaya akapotoka katika tabia yake nyoofu na akaathiriwa na ufisadi.

Imam Ali AS amesema:

"Dhana mbaya hufisidi mambo na huchochea maovu."

(Ghuram 'l-Hikam, uk. 433,)

Dr.Marden ameandika:

"Baadhi ya matajiri huwashuku sana waajiriwa wao kwamba huenda wakaiba, na mwishowe huiba. Kushuku kama huko hata kama kusitamkwe kunaathiri kwa kutia sumu roho ya mwajiriwa na kumfanya aibe."

(Piruzi Fikr)

Imam Ali AS amesema:

"Jihadhari na ghera (inayotokana na kushuku) mahali si pake, kwani humtia mzima maradhi na humshuku asiyekuwa na hatia."

(Ghuraru 'l-Hikam, uk. 152}

Mwenye kuugua dhana mbaya, mwili na roho yake huugua pia.

Imam Ali'AS amesema:

"Humwoni mwenye kushuku kuwa mzima."

(Ghuram 'l-Hikam, uk. 835}

Dk. Carl ameandika haya kuhusu maudhui hii:

68

"Baadhi ya tabia hupunguza nguvu za kuishi, kama vile kulaumu kila kitu na kushuku. Kwa sababu tabia hiyo ya kinafsi isiyofaa huathiri vibaya mfumo mkuu wa huruma na tezi za mwilini, na inaweza kusababisha ugonjwa kwa mwili pia."

(Rah Wa Rasme Zindagi)

Dr. Marden ameandika:

"Dhana mbaya huharibu siha ya mtu na hudhoofisha mwendo mzuri. Roho zilizo makini hazitazamii jambo baya kabisa, bali daima hutegemea kukabiliana na jambo jema, kwa sababu zinajua kwamba jambo jema ni hakika ya daima na jambo baya si kitu isipokuwa ni udhaifu wa jema; kama vile ambavyo kiza chenyewe si kitu pekee bali ni hali ya kutokuwepo mwanga. Kwa hivyo, daima tafuteni mwanga, kwani mwanga huondoa kiza katika nyoyo zenu."

(Pintzi Fikr)

Mtu mwenye dhana mbaya huwa ana maradhi ya wasiwasi na huwaogopa watu.

Imam Ali AS amesema:

"Yule ambaye dhana yake si nzuri humwogopa kila mtu."

(Ghurani 'l-Hikam, uk. 712)

Dk. Farmer ameandika:

"Yule anayeogopa kuelezea fikra na mawazo yake katika mikutano au tafrija ambapo kila mtu huelezea

69

itikadi yake, mtu huyo huogopa kutangaza maoni yake. Vivyo hivyo, yule mtu anayeepuka kukutana na marafiki zake katika mitaa mipana au mahali pa hadhara na badala yake hupita kwenye vichochoro na njia zenye watu wachache, mtu kama huyo ni mwoga au moyo wake hutawaliwa na dhana mbaya."

(Raze Khoshbakhti)

Chanzo kimojawapo cha dhana mbaya ni kumbukumbu mbaya zinazomsumbua mtu moyoni mwake ambazo humfanya ashuku bila ya mwenyewe kutambua.

Imam Ali AS amesema:

"Nyoyo zina kumbukumbu mbaya ambazo huchukiwa na akili"

(Ghuraru 'l-Hikam, uk. 29)

Dk. Helen Shakhter amesema:

"Watu wasiojiamini nafsi zao huwa ni wepesi kuhamaki na husumbuka wakipata misiba midogo tu. Kumbukumbu za misiba hiyo na usumbufu huo hubaki katika nyoyo zao na huwaathari katika fikra na miendo yao bila wenyewe kufahamu. Kwa mfano, huwa na huzuni, ukali na shaka lakini hawajijui kwa nini wamepatwa na maradhi hayo ya kiroho. Sababu yake ni kwamba kumbukumbu mbaya na zinazoumiza hujificha kalika nyoyo zetu na hazidhihiriki kwa urahisi. Kwa maana nyingine, ni kawaida mtu kujisahaulisha na kujiepusha na makumbusho yanayohuzunisha na kutaka asikumbuke tena. Lakini hao maadui wa ndani

70

hawaachi chuki zao na maovu yao, na kuzifanya amali, tabia na roho zetu zifuate matakwa yao. Wakati mwingine tunaona mwendo na amali na tunasikia maneno yetu wenyewe au ya wengine ambayo yanatushangaza kwa kukosa maana. Lakini tukiyachunguza tunaona kwamba vitendo hivyo au maneno hayo yanatokana na kumbukumbu mbaya zilizofichika katika nyoyo zetu."

(Roshde Shakhsiyyat)

Watu duni na wenye tabia mbaya hujilinganisha na tabia za watu wengine, hivyo, huziona tabia zao kwa wengine.

Imam Ali AS amegusia kuhusu tabia hiyo pale aliposema:

"Mwovu hamdhanii vizuri mtu mwingine kwa kuwa haoni kwake ila tabia yake mwenyewe."

(Ghuraru 'l-Hikam, uk. SO)

Dk. Mann ameandika:

"Kumtupia mtu lawama ni kutoa fikra, hisia na uchungu wako moyoni na kumsingizia mwingine. Hii ni aina moja ya radiamali ya kuficha makosa na kujitetea ili kujitoa katika mashaka na fadhaa. Tabia hii hufanywa na mtu bila kutambua kwamba ni aina moja ya usingiziaji. Tabia hiyo ya kuwatupia lawama wengine inapozidi, hupoteza afya yake na huugua wazimu. Tabia hii ni matokeo ya mtu anapohisi amefanya kosa fulani, hivyo, huwasingizia wengine kosa hilo ili kujitetea mwenyewe."

(Usule Ravanshinasi)

71

Mtume Mtukufu alipohamia Madina, mwenyeji mmoja akamwendea na kumwambia: "Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Wenyeji wa mji huu ni watu wema sana. Umefanya vizuri kuja hapa." Mtume Mtukufu akasema: "Umesema kweli." Baada ya muda mdogo akaja mtu mwingine na kumwambia: "Wenyeji wa mji huu ni watu wabaya. Afadhali usingekaa na watu hao." Mtume akasema: "Umesema kweli." Sahaba mmoja aliyekuwepo hapo alishangaa alipoona kwamba Mtume Mtukufu amesadikisha kauli mbili zinazotofautiana, hivyo, akamwuliza sababu yake. Mtume Mtukufu akajibu: "Kila mmoja katika watu wawili hao amesema kwa mujibu wa dhamiri na tabia yake mwenyewe juu ya wenyeji wa hapa. Hivyo, wamewadhania wengine kwa sifa hiyohiyo waliyokuwa nayo wenyewe. Kwa sababu hii, kauli za wote wawili ni sawasawa." Yaani kila mmoja amewasifu wenyeji wa Madina kwa sifa aliyokuwa nayo mwenyewe.

Ni lazima tufahamu hapa kwamba muradi wa dhana mbaya iliyokatazwa ni maelekeo na upotofu wa moyo katika kudhania vibaya, kushadidia dhana hiyo na kutekeleza yale unayodhania. Lakini dhana zinazopita moyoni na ambazo hazishughulikiwi hazipo katika hiari ya mtu. Na kwa kuwa mtu hana uwezo wa kuzizuia dhana hizo, hivyo, hazina hukumu ya kisheria.

Kufuatana na hayo tuliyoandika, ilivyokuwa chimbuko la maisha machungu na yasiyo na mafanikio ya dhana mbaya yanatokana na dosari hiihii kubwa, hivyo, inapaswa kutafutwa sababu ya maradhi hayo au itafutwe dawa yake.

4 - UWONGO

Thamani na Umuhimu wa Maadili

Mojawapo kati ya misingi na shuruti za maisha ya kijamii na ukamilifu wa kila taifa ni maadili. Maadili yamezaliwa pamoja na maisha ya binadamu na umri wake ni sawa na ya jamii ya wanadamu. Hakuna mtu yeyote aliye na akili timamu ambaye anaweza kukana umuhimu na wajibu wa maadili katika kuleta utulivu na usalama wa roho; au akakataa faida yake katika kuimarisha msingi wa ustawi wa jamii na marekebisho ya umma. Ni nani asiyependa uaminifu na wema au akatafuta furaha na saada katika uhaini na ulaghai? Katika kusifu maadili inatosha kusema kwamba hata taifa lisiloendelea au ustaarabu usioamini dini yoyote unatukuza na kuheshimu sifa za kimaadili, na unahisi kwamba inabidi ufuate utaratibu wa sheria zake katika kukabiliana na maisha yanayokwenda zigizaga. Katika kipindi kirefu cha maisha ya binadamu ambacho kimemwonyesha anuwai ya njia za kufuata, kitu alichoona kila mahali na katika kila kundi na taifa ni sura moja ya msingi wa kimaadili.

Samuel Smiles, mwanachuoni mashuhuri wa Kiingereza, amesema:

"Maadili ni mojawapo kati ya nguvu zinazoendesha ulimwengu huu. Yanapokuwa katika upeo wa madhihirisho yake, hujenga maumbile ya mwanadamu katika umbo aali, kwa sababu maadili ni kitambulisho cha ubinadamu halisi. Watu wenye mafanikio na fursa

76

mahsusi katika maisha yao huwatukuza na huwaheshimu wanadamu wenzao ili kuwavutia, na bila shaka watu huwaamini na huwafuata wao kwa kuwa wanaamini kwamba kila kizuri cha dunia kinamilikiwa na watu hao, na wasipokuwepo wao kusingewezekana kuishi katika dunia hii. Ikiwa kipawa anachozaliwa nacho mtu kinawavutia watu na wakakisifu, basi inapasa maadili yaheshimiwe na yatukuzwe; kwa sababu, kwanza, maadili ni matokeo ya kifikra, na pili, ni athari ya nguvu za moyo, na sote tunajua kwamba moyo ndio unaohukumu na kuendesha maisha yetu yote katika muda wote wa uhai wake. Watu waliofikia kilele cha ubora na utukufu, huwa ni kama mienge inayomulika njia ya ubinadamu na kuangaza mazingira ya kimaadili ya ulimwengu, na kuwaongoza watu kwenye njia ya utukufu na uchaji. Ikiwa watu wa jamii moja hawatakuwa na adabu na tabia njema hata kwamba watakuwa na haki na uhuru mwingi wa kisiasa, hawataweza kamwe kufikia kwenye maendeleo na utukufu. Ikiwa taifa moja linataka kuishi kwa ubora na utukufu, si lazima ardhi yake iwe kubwa, kwa sababu huenda taifa moja likawa na ardhi kubwa na watu wengi lakini likakosa utukufu na ukamilifu. Ni lazima tujue kwamba ikiwa wakati wowote taifa moja litaharibikiwa na maadili yake, basi watu wake wataangamia pia."

(Akhlaq)

Kwa upande wa kinadharia, maneno hayo yanakubaliwa na wote; lakini kwa upande wa kimatendo, wanadamu wanahitalifiana kwa masafa

77

marefu baina ya elimu na amali. Wanabadilisha maadili mema kwa matamanio ya kihayawani na daima wanatafuta raha na starehe zinazolaghai ambazo zinajitokeza katika maisha kama mapovu yanavyo tokeza juu ya maji.

Binadamu ametoka katika kiwanda cha uumbaji akiwa na maumbile yanayokinzana. Moyo ni medani ya mapambano baina ya sifa nzuri na mbaya. Hatua ya kwanza katika kuusafisha moyo ni kuzishinda nguvu mbili za ghadhabu na matamanio ambazo ndizo zinazomtawala mtu na kuanzisha nguvu nyinginezo za kihayawani. Ni lazima zizuiliwe nguvu hizo zisitumiliwe vibaya na kupita kiasi, na maelekeo ya hamaki na yenye kudhuru yabadilishwe yawe mazuri na yenye manufaa. Hapana shaka kwamba mwanadamu hutumia vizuri hisia zake katika mkondo wa maisha yake, lakini matokeo yake mema na mazuri yataweza kubainika atakaposalimu amri mbele ya akili.

Mwanasaikolojia mmoja amesema:

"Hisia za binadamu zimefanana na tanki yenye sehemu mbili. Sehemu moja ina nguvu ya kusukuma, na sehemu nyingine ina nguvu ya kukinza (kuzuia). Nguvu yoyote itakayoweza kuishinda sehemu ya ukinzani, itakuwa na uwezo wa moja kwa moja juu yetu, nasi tutatii amri yake."

Wale waliosawazisha nguvu zao za ndani na wakayalinganisha matakwa ya moyoni pamoja na kibali cha akili—au kwa ufupi, wakapatanisha akili na moyo basi hapana shaka yoyote huwa wamepita katika njia ya ufanisi na saada kwa hiari na uhuru na bila ya

78

kutetereka, ingawa rijia hiyo hupita katika misukosuko na mashaka. Ni kweli kwamba leo maendeleo yanakwenda kwa kasi, na mwanadamu kwa kutumia vipawa vyake vya kifikra ameweza kufikia kina kirefu baharini. Lakini misiba yote hayo na mapinduzi yanayotokea katika ustaarabu wa sasa, yameifanya jamii ya wanadamu ikumbwe katika mawimbi ya matatizo na balaa na isukumwe katika machafuko na misukosuko. Sababu yake ni kushindwa kiroho na kupotoka kwenye njia ya maadili mema.

Dk. Joel Roman ameandika:

"Sayansi imeendelea katika zama hizi, lakini tabia na hisia zetu za kimaumbile zimesimama katika zama za kale. Wakati wowote zitakapoendelea pamoja na akili na elimu, tutaweza kusema kwamba ustaarabu wa mwanadamu  ambao ni tunda la fikra na matakwa mema umeendelea na kustawi pia."

Naam, ustaaratou ambao hautoi haki ya kutawala kwa maadili mema na badala yake hubatilisha hukumu zake, kwa mujibu "wa hukumu ya sheria ya usawa, mwisho wa ustaarabu kama huo ulioingia sumu ni kuangamia tu. Kuwepo upungufu, balaa na misiba katika jamii moja ni ishara kwamba jamii hiyo inahitajia kanuni za kimaadili. Maadili hukipa pumzi ya uzima kiwiliwili dhaifu na kichoofu cha ustaarabu na nguvu za kuishi.

Anuwai ya Madhara ya Uwongo

Kwa kadiri ambavyo kusema kweli ni kuzuri na

79

kunanufaisha, vivyo hivyo, kusema uwongo ni kubaya na kunadhuru. Ukweli ni sifa bora kabisa na uwongo ni sifa duni kabisa. Ulimi hufumbua moyo na hufafanua hisia za ndani; kwa hivyo, ikiwa uwongo unatokana na uhasidi na uhasama, basi ni matokeo ya kuvuja nguvu za hatari za ghadhabu. Na ikiwa uwongo unatokana na tamaa au tabia, basi ni athari mbaya na inayowaka ya uchu (wa kijinsia).

Ikiwa ulimi utaingia sumu na maneno yakawa machafu, basi heshima ya msemaji itapeperushwa kama majani yanavyopeperushwa na upepo mkali, naye atakuwa chambo cha uharibu na utukufu wake utaanguka. Uwongo huimarisha roho ya uhaini na uchafu katika mwanadamu na huzima moto wa dhamiri katika kiini cha moyo. Uwongo hutingisha misingi ya umoja na mfungamano, na husababisha kuenea kwa unafiki katika jamii. Sehemu kubwa ya upotofu ni natija ya maneno na madai yaliyo kinyume na uhakika ambayo hutolewa na watu wenye tamaa na mabarakala. Watu hao hufunika sura halisi ya ukweli kwa kusema maneno ya udanganyifu ili wajipatie fursa na matakwa yao. Huwafunga mazuzu pingu za utumwa kwa kuwaroga kwa maneno matamu.

Kusema uwongo hakumpi mwongo fursa ya kutafakari. Kwa kuwa mwongo hudhani kwamba hakuna mtu anayejua siri yake, hivyo, hafikiri juu ya matokeo ya njia yake fupi. Kwa sababu hii daima hufanya makosa na maneno yake hukinzana. Hali hii humfanya afedheheke, apoteze heshima yake, aone haya na apate aibu kubwa. Basi ni kweli ule usemi

80

unaosema: "Mwongo hakumbuki vizuri!"

Sababu mojawapo inayoeneza tabia hii mbaya ambayo kwa hakika huyatia sumu maadili ya jamii ni kule kutumiwa uwongo kwa jina la "uwongo wa kimaslahi!" Jina hilo ni kama pazia linalopendeza ambalo linafunika uchafu huo. Kwa kawaida watu wanapotaka kuthibitisha kwamba uwongo wao uliotia chumvi ni wa haki, hutoa kisingizio hicho, wakisahau kwamba akili na sheria zimeruhusu uwongo wa kimaslahi kufuatana na masharti maalumu tu. Kwa mfano, kama kuna hatari ya kupotea roho, mali au heshima ya Mwislamu, ni lazima itumiwe kila njia iwezekanayo ili kuzuia hatari inayoikabili roho au mali ya Mwislamu, hata kama ni kwa kusema uwongo. Lakini kwa wakati huohuo hakuruhusiwi kuvuka mpaka wa dharura (au kiwango kinachojuzu). Ikiwa kiwango cha maslahi kitazidishwa kukidhi maslahi ya kibinafsi na matakwa ya mtu na kikachukuliwa kama ni ushahidi madhubuti katika mambo yote, basi kila uwongo utakuwa ni wa kimaslahi.

Mwandishi mmoja mashuhuri ameandika:

"Kila kitu kina sababu yake; na unaweza kutafuta sababu ya kila jambo ukapata. Hata wahalifu wanapolaumiwa huweza kutoa sababu na visingizio mbalimbali kutetea uhalifu wao. Hapana shaka kwamba kila uwongo unaosemwa duniani ni wa kimaslahi; au kwa maana nyingine, kila uwongo una faida yake. Uwongo usiokuwa na faida kwa mwongo hauna maana kwake, hivyo, hauna madhara mengi kwake. Kimaumbile, binadamu hukiona chema kila kitu

81

kinachomletea manufaa ya kibinafsi. Kwa hivyo, akiona kwamba akisema kweli atahatarisha manufaa yake ya kibinafsi, au akiwaza kwamba akisema owongo atapata faida, basi hapana shaka yoyote kwamba atasema uwongo, kwa sababu huona kwamba kuna fitna na ushari katika kusema ukweli, na manufaa na maslahi katika kusema uwongo."

Lapasa jambo hili kutiwa maanani, kwamba uwongo ni shari kubwa. Ikiwa shari moja inaondoka kwa kusema uwongo unaoruhusiwa, basi huwa ni kwa sababu ya kuondosha shari kubwa kwa shari ndogo. (Heri nusu shari kuliko shari kamili.)

Uhuru wa kusema ni muhimu zaidi kuliko uhuru wa fikra, kwa sababu ukitokea upotofu katika fikra, ni mwenye fikra hiyo tu ndiye atakayedhurika. Lakini uhuru wa kusema unahusika na maslahi ya jamii nzima, na manufaa au madhara yake yanawaathiri watu wote.

Ghazali amesema:

"Ulimi ni miongoni mwa neema kubwa na ni miongoni mwa viungo vilivyoumbwa na Mwenyezi Mungu kwa uzuri na umahiri. Ingawa ukubwa na uzito wa kiungo hicho ni mdogo, lakini utii na uasi wake ni mkubwa na mzito, kwa sababu ukafiri na imani ya mtu hudhihirika kwa ushahidi wa ulimi. Na hivi ni vikomo viwili vya uasi na utumwa .... Mwenye kuepukana na shari ya ulimi ni yule ambaye huufunga kwa hatamu ya dirii, na haufungui ila katika mambo yenye manufaa katika dunia na Akhera."

(Kimiyai Sa'adaat)

82

Ili kuwahifadhi watoto wadogo wasipate maradhi ya kusema uwongo, ni lazima tujiepushe kusema uwongo wowote mbele yao au kusema jambo lolote lililo kinyume na uhakika, kwa kuwa ni kawaida kwa watoto wadogo kuiga usemaji na utendaji wa wale watu walio karibu nao daima. Ikiwa katika mazingira ya nyumbani ambayo ni muhimu kabisa katika kuwafunza watoto wadogo, kusema uwongo kutakuwa ni kama kunywa maji, na maneno na vitendo vya wazazi vitakuwa kinyume na ukweli na adabu njema, basi hapana shaka yoyote kwamba watoto watakaokua humo hawatakuwa wasemao kweli abadani.

Bwana Morris T. Yash amesema:

"Tabia ya kutafakari juu ya ukweli, kusema kweli na vilevile kutafuta ukweli ni mwendo wa wale tu ambao tangu udogoni wamelelewa hivyo."

Uwongo katika Mtazamo wa Dini

Qur'ani Tukufu inasema waziwazi kwamba mwongo yuko nje ya jamii ya Waislamu:

"Wanaozua uwongo ni wale wasioziamini aya za

Allah, na liao ndio waongo (liasa)!"

(an-Nahl, 16:105)

Aya hii inamaanisha kwamba waumini hawawezi kuwa waongo.

Mtume Muhammad SAW amesema:

"Halahala na ukweli, kwani ukweli huongoza kwenye wema, na wema huongoza kwenye Pepo. Mtu

83

haachi kusema ukweli na kutafuta ukweli mpaka aandikwe ni mkweli mbele ya Mwenyezi Mungu. Na jihadharini na uwongo, kwani uwongo huelekeza kwenye ufisadi, na ufisadi huelekeza kwenye Moto. Mtu haachi kusema uwongo na kufuata uwongo mpaka aandikwe ni mwongo mbele ya Mwenyezi Mungu."

(Nahju 'l-Fasahah, uk. 418)

Mojawapo kati ya sifa za waongo ni hii kwamba, husita na huchelewa kuamini maneno ya watu wengine na husadiki kwa taabu maneno ya wengine.

Mtume Mtukufu SAW amesema:

"Watu wenye kuwasadiki upesi wengine ni watu wenye kusema kweli kuliko wengine; na watu wenye kuwakadhibisha zaidi wengine ni watu wenye kusema uwongo kuliko wote."

(Nahju 'l-Fasahah, uk. 118)

Dk. Samuel Smiles ameandika:

"Baadhi ya watu hupima tabia zao mbaya sawa na tabia za wengine. Lakini ni lazima tujue kwamba kwa hakika watu wengine ni kioo cha tabia zetu, hivyo, kila zuri au baya tunaloliona kwa wengine ni muakisho wa uzuri na ubaya wa maumbile yetu wenyewe."

(Akhlaq)

Watu wenye ushujaa wa kimaadili hawajitatizi katika uwongo wala hawajipaki uchafu wake. Katika dhamiri na ndani mwa nafsi ya mwongo, kuna hali moja ya kinafsi ambayo humpotosha kwenye njia nyoofu ya

84

kusema kweli. Watu wenye kujihisi uduni na udhaifu wao hutegemea uwongo. Uwongo ni kimbilio la waoga na watu dhaifu.

Amirul Muuminin Ali AS amesema:

"Lau vitu vingeainishwa (kwa ulingano wao), ukweli ungekuwa pamoja na ushujaa, na uwongo ungekuwa pamoja na uwoga."

(Ghuraru 'l-Hikam, uk. 605)

Dk. Raymond Peach amesema:

"Uwongo ni silaha bora kabisa ya kujitetea kwa watu dhaifu na ni njia ya haraka kabisa ya kuepukana na hatari. Uwongo ni radiamali ya udhaifu na unyonge katika baadhi ya mambo. Tukimwuliza mtoto mdogo:

'Wewe umechukua pipi hizi?' au 'Wewe ndiye uliyevunja chombo cha maua?' Ikiwa mtoto huyo atajua kwamba akikiri kosa lake atatiwa adabu kali, moyo wake utamwambia ajitetee na kumfanya akatae." (Ma Wa Farzandane Ma)

Imam Ali AS ametaja matunda ya kusema kweli katika usemi mfupi huu:

"Msema kweli hujichumia vitu vitatu: kuaminiwa, kupendwa na kuheshimiwa."

(Ghuraru 'l-Hikam, uk. 876)

Uislamu hutambua kusema kweli kama ni kipimo cha utukufu wa mtu.

Imam Sadiq AS amesema:

"Msidanganywe na sala na saumu zao, kwani

85

huenda mtu akawa amezoea kusali na kufunga na endapo ataziacha ataona taabu. Hivyo, wajaribuni katika kusema ukweli na kuweka amana."

(Usulu 'l-Kafi, jz. 1, uk. 460^

Imam Ali AS amesema:

"Tabia mbaya kabisa ni kusema uwongo."

(Ghuraru 'l-Hikam, uk. 110)

Dk. Samuel Smiles ameandika haya kuhusu maudhui hii:

"Kati ya tabia na sifa zilizo duni kabisa, kusema uwongo ni kubaya kuliko zote. Ukweli na uaminifu ni lazima uwe ni lengo la pekee la mwanadamu katika vipindi vyote vya maisha yake, na katika hali yoyote ile usifidiwe kwa ajili ya malengo mengine."

(Akhlaq)

Uislamu umesimamisha msingi wa imani juu ya ratiba zote za kimaadili na za urekebishaji na kuihesabu imani kuwa ni msingi wa furaha na ufanisi. Descartes amesema kwamba maadili bila ya imani ni kama kasri iliyojengwa juu ya matope. Mwanachuoni mwingine amesema pia:

"Maadili pasina dini ni kama mbegu iliyopandwa kwenye jiwe au magugu ambayo hukauka na hufa. Maadili bora kabisa yasipopata uhai wake kutoka katika dini, yataonekana kama wafu mbele ya mtu mzima na kamili."

Dini hutawala nchi mbili za akili na moyo, na kwa

86

sababu hiyo ni makao ya suluhu na vita. Hisia za kidini hupunguza hisia za kimaada, na hujenga ukuta madhubuti baina ya mwanadamu na anuwai ya mabaya. Mwenye kutegemea imani, daima huwa na utulivu, usalama na lengo maalumu. Kipimo na kiini cha hadhi ya mwanadamu katika Uislamu ni imani na tabia njema ambazo Uislamu hujitahidi kuziimarisha na kuzihifadhi. Imani ndiyo inayoipa thamani na itibari kauli ya Mwislamu. Kwa mujibu wa sheria ya Kiislamu, kiapo katika masharti maalumu huchukua nafasi ya ushahidi na huwa ni njia mojawapo ya kumaliza daawa. Vivyo hivyo, Uislamu umefanya ushahidi kuwa ni njia moja ya kuthibitisha haki za kijamii.

Kwa hivyo, ni wazi kwamba uwongo ukichukua sura ya kutisha katika hali mbili hizo, madhara yake yatakuwa makubwa na makosa na madhambi yake hayataweza kusameheka. Kipimo cha uzito wa dhambi ya kusema uwongo hutegemea kadiri ya madhara yaliyosababishwa. Kwa kuwa ushahidi wa uwongo una madhara zaidi, hivyo, dhambi yake ni kubwa zaidi.

Uwongo ni chombo cha kwanza kinachompeleka mtu kwenye maovu mengine.

Imam Hasan Askari AS amesema:

"Maovu yote yamewekwa katika nyumba moja, na ufunguo wake ni uwongo."

(Jami'u 's-Sa'adaat,jz. 2, uk. 318)

Ili kufafanua maudhui hii, tunakutanabahisha kwa hadithi ifuatayo:

Mtu mmoja alikwenda kwa Mtume Mtukufu SAW

87

kumwomba amnasihi kwa jambo ambalo litamletea saada na furaha. Mtume akamkubalia na akamjibu kwa usemi huu mfupi: "Jiepushe na uwongo na jizatiti kwa ukweli."

Bwana huyo akapata jawabu yake, na akaomba ruhusa kwenda zake. Lakini baadaye akakiri: "Mimi nilizama katika matope ya sifa chafu, lakini baada ya kupata nasaha hiyo ilinibidi nijisafishe kabisa na uchafu huo. Kwa sababu kama katika mazungumzo yangu ya kila siku ningeulizwa jambo fulani na nikasema ukweli wake, baadhi ya siri zangu zingefichuka na ningefedheheka; na kama ningeficha uhakika na nikasema uwongo, ningekuwa nimehalifu amri ya Mtume Mtukufu. Kutokana na kushika kwangu na kutekeleza nasaha hiyo ya Mtume Mtukufu nikaokoka kutokana na matope hayo, na madoa meusi ya madhambi yangu yakasafika katika moyo wangu."

Naam,yule mwenye kusema kweli na kufuata mwendo wa ukweli ataokoka na maisha ya taabu na mashaka, na mwenge wa moyo wake utamuangaza daima. Atasalimika na wasiwasi na hofu, na mawazo yake yatapata utulivu na kumkinga na fikra zinazosumbua.

Kwa mtazamo wa kidini au wa kidunia, uchunguzi wa hali ya kijamii na uzingatio juu ya matokeo maovu ya uwongo, unatoa mafunzo makubwa kabisa kwa mtu mwenye kutafakari na kupenda utukufu. Matokeo ya kusema uwongo ni kiboko kinachomtanabahisha kila mtu. Ukamilifu halisi unapatikana katika imani na maadili mema. Mahali pasipokuwepo ukamilifu wa

88

kweli hapawezi kupatikana utulivu na ufanisi hapo.

5 - UNAFIKI

91

Tujitahidi Kuhifadhi Shakhsia Yetu

Msingi muhimu kabisa wa ufanisi na saada na pambo bora kabisa linalompatia mtu utulivu ni shakhsia. Hii ni johari yenye kima inayompatia mtu utukufu na heshima na humpandisha katika daraja ya juu kabisa ya ufakhari na adhama. Kwa kuwa watu wote ni wa jamii moja ya wanadamu, hivyo wote ni sawasawa, lakini kila mmoja wao hutofautiana na mwenziwe kiakili, kifikra na kitabia. Kile kinachomtofautisha kila mtu na kumpa thamani na hadhi ni shakhsia. Kinyume na sifa nyingi nyinginezo zinazotuathiri kwa njia isiyo dhahiri, athari ya shakhsia ni ya dhahiri na isiyoweza kuharibika.

Binadamu amewekwa katika ulimwengu huu ili ajitahidi kwa dhati kustawisha sifa njema na hazina za maisha yake, kuzidisha kiwango cha maarifa yake na kupanua fikra na mawazo yake; na kwa njia hii, nishati za nafsi yake ziwe na nguvu na zipevuke kwa ukamilifu ili mwishowe aweze kutekeleza wadhifa wake wa kiutu katika uso wa dunia.

Ni lazima iwe ni shabaha ya kila mtu kuweka msingi wa shakhsia madhubuti na makini katika nafsi na kuzitumia nguvu za ndani katika njia ya kupata ufanisi. Kadiri mtu atakavyoonyesha jitahada zaidi katika njia hii, ndivyo atakavyoweza kuwa na matumaini zaidi ya kupata mafanikio yake. Kwa sababu hakuna kitu chochote kinachoweza kumpatia mtu ufanisi kama

92

kuwa nayo shakhsia tukufu ambayo pia huweza kumpatia maslahi na manufaa kwa ajili yake. Shakhsia aali humwezesha mtu kuogelea katika bahari iliyochafuka.

Bwana Schopenhaure amesema:

"Tofauti kati ya shakhsia ni jambo la kawaida kabisa, na taathira zake katika furaha na huzuni za watu ni zaidi kuliko zile taathira tofauti zinazotokana na sheria zilizotungwa na binadamu. Fursa za kibinafsi, kama vile kuwa navyo akili iliyokomaa, uendeshaji mzuri na hisia safi na nyororo, haviwezi kabisa kulinganishwa na fursa zinazopatikana katika kipindi cha maisha, kama vile kuwa na vyeo na daraja. Mtu mwenye akili anayeishi katika upweke na ukiwa anaweza kutumia wakati wake wote katika furaha kwa kutegemea fikra na mawazo yake, walakini mtu mjinga hataweza kujiepusha na ugonjwa unaomkera mwili na roho yake hata kama atatumia kila aina ya starehe au a.tatumia pesa nyingi mno. Nguvu na uwezo, na akili pevu na hisia safi ni miongoni mwa vitu muhimu sana vinavyomfikisha mwanadamu karibu na shabaha yake na kumfungulia milango ya ufanisi na furaha. Kwa sababu hii, inatubidi tuvistawishe na tuvikuze zaidi vitu hivi vya nafsini kuliko vile vinavyopatikana kutoka nje."

Kila tabia na sifa ina mchango wake katika kuamua mustakabali wa mtu, na kila hisia na fikra inaathiri tabia na sifa hizo. Kwa sababu hii, mwendo wa kila mtu hubadilika daima- ama hutukuka na kukamilika, au hudhoofika na kuanguka.

Kwa hivyo, hatua ya kwanza katika kuiimarisha na

93

kuikamilisha shakhsia yake ni kujifunza mbinu ya kutumia uwezo na vipawa alivyonavyo moyoni mwake, kupambana na aina yoyote ya kizuizi kinachozuia hatua yake ya kujikamilisha, na kuvua nguo ya uduni na uchafu mwilini mwake. Lakini mtu asipoitambua thamani yake hasa, hatafanikiwa kamwe kuihuisha nafsi yake, wala haiwezekani aweze kupata mabadiliko yoyote yenye faida kwa ajili yake na akaweza kujisalimisha mawazo yake na machafu, bali badala ya kwenda kwenye njia ya ukamilifu atafuata njia ya uangamivu.

Maneno na matendo ya mtu yasipochimbuka kwenye kiini cha moyo na kwenye moyo mweupe, hayawezi kuwa na thamani yoyote. Alama ya maneno yenye "shakhsia madhubuti" huonekana wakati maneno hayo yanapowakilisha roho, yanapofafanua nafsi, yanapofumbua siri ya moyo, na wakati alama za utukufu na ukamilifu zinapong'ara katika maneno yake. Lakini kinyume chake, wakati maneno (na matendo) yanapotofautiana na nia yake ambayo ni alama ya "shakhsia dhaifu", matokeo yake huwa ni mabaya na machungu kabisa katika maisha yake.

Unafiki ni Sifa Mbaya Kabisa ya Kimaadili

Unafiki ni miongoni mwa sifa mbaya kabisa ya kimaadili ambayo inachusha katika hali yoyote ile. Tabia ya mwanadamu ambayo inapendelea uhuru na ufanisi na ina uwezo wa kupanda kwenye kilele cha

94

utukufu na ustawi, inapochafuliwa kwa kusema uwongo na kuvunja ahadi, hupanua uwanja mkubwa kwa ajili ya kukua kwa unafiki na uzandiki, na kusababisha maradhi mabaya sana kushika mahali pake. Unafiki ni kizuizi kikubwa na chenye nguvu kinachofunga njia ya kutokeza sifa nzuri na kutafuta ukweli katika dhamiri ya mtu. Hapana shaka kwamba kitu chochote kinachozuia ustawi na maendeleo ya nafsi kamilifu huwa kinapingana na maisha ya ufanisi na mambo ya kukamilisha roho.

Unafiki ni ugonjwa wa hatari unaopoteza heshima na thamani ya mtu, na unaleta utovu wa adabu na uharibifu wa maadili. Unafiki huleta dhana mbaya na wasiwasi katika kiini cha moyo badala ya nguvu ya kujiamini ambayo ni lazima kwa ajili ya mafanikio ya maisha.

Mtu laghai ambaye upotofu wake umetia fora, hutumia ujanja maalumu kujionyesha kwamba anampenda kila mtu na anataka wema wake tu. Anapoona kwamba kuna uhasama na kutokusikilizana baina ya watu wawili, huingiliana na hujipendekeza na kila mmoja wao. Hujitia ni mpenzi na rafiki wa mmoja na humpinga na humlaumu mwingine, na kwa hakika huwa hana uhusiano wa kiroho na kidhati na yeyote kati yao. Huwaambia uwongo wote wawili na huwafanyia ria. Hujionyesha anaafiki itikadi za watu kwa kujidai na kufanya ria na hukataa kudhihirisha haki na kusema kweli wakati hasa unapotakikana. Hizi ni katika sifa za ndumakuwili. Hatari ya mnafiki ni kubwa kwa mara nyingi zaidi kuliko ya adui mkubwa.

95

Mwanachuoni mmoja amesema:

"Miongoni mwa sifa za maadui ni hii kwamba dhahiri na batini yao ni maadui, kwa sababu uadui hauna rangi mbili. Afadhali marafiki pia wangekuwa ni watu thabiti na wasiojionyesha. Hapana shaka kwamba marafiki wanafiki ni wabaya zaidi kuliko maadui wauaji."

rudi nyuma Yaliyomo endelea