rudi nyuma Yaliyomo  

Maana yake “Enyi mlio amini kwanini mna sema msiyo yafanya zikaandikwa shahada katika shingo zenu na mkaulizwa siku ya kiyama.”

Aya hizi mbili na sura mbili alizozitaja hazimo ndani ya Qur’ani ina maana zilitoweka kufatana na rai yake. Ukiongezea na mifano tuliyo tangulia kuitaja, kwani katika njia ya kuikusanya Qur’ani kama walivyo pokea Ahlu Sunna na katika njia ya kuandikwa kwake na kutokana na kauli yao ya kuwa kuna (naskhu ttilawa) yaani visomo vili vyo futwa) katika aya nyingi sawa kufutwa hukumu ya aya au haikufutwa, yote haya yanapelekea kukiri kuwepo mabadiliko ndani ya Qur’ani na kawepo upungufu pia.

7. Ibnu maaja ametoa hadithi kutoka kwa mwana Aisha mkewe mtume (s.a.w) amesema iliteremka aya ya rajmi na aya ya kunyonyeshwa mtu mzima mara kumi, na aya hizi mbili zilikuwa kwenye nyaraka chini ya kitanda changu, alipokufa mtume (s.a.w) tukawa katika hali ya kushughulikia kifo chake akaingia mnyama akazila nyaraka hizo. Vile vile riwaya hii ameipokea Addamiiry katika kitabu Haayatul-Hayawaan chini ya neno Daajin.()

Maulamaa wetu katika sehemu mbalimbali wamekuwa wakijadiliana na wale wasemao ya kuwa Qur’ani imegeuzwa, na kubatilisha kauli zao hizo. Ili kuyapatahayo waweza kurejea katika vitabu tulivyo vitaja hapo mwanzo. Pamoja na yote hayo, tuliyo yataja ni baadhi tu ya mifano kwani tuna vyanzo vingine ambavyo tukiyakusanya yote basi itatulazimu kutunga vitabu vingi ili kubainisha kauli zao zote, zinazo zungumzia kugeuzwa kwa Qur’ani. Pamoja na yote hayo tuliyo yabainsha, uzuishi huu umekuwa ukiendelea bila kukoma.

Na mimi nina itakidi na kuamini yakuwa tunayo yaandika nakuyaeleza kubatilisha uzushi huu yatawanufaisha wachache Sana nao ni wale watafiti na wenye nyoyo za Ikhlas na ambao wanapenda kuitafuta haki. Ama walio wengi si watafutaji wa haki bali wao hung’ang’ania waliyo nayo hata kama ni batili na katika ung’ang’’anizi wao hufikia hatua ya kuliita jua kuwa ni jiwe jeusi na si jua.

Pamoja na hayo juhudi zetu ni kuwafafanulia wale wenye kuutafuta na kuutaka ukweli, na kwa kufanya hivyo huwenda Mwenyezi Mungu akamnufaisha nao mwenye kutaka kuongoka.

MFANO WA PILI UZUSHI WA KUKOSEA JIBRILU KUTEREMSHA WAHYI KWA MOHAMMAD(S.A.W)

Moingoni mwa mambo ya msingi katika itikadi ya waislamu ni kuwa Mwenyezi Mungu alimtuma Mtume Mohammad (s.a.w.) kwa viumbe wote na akauthibitisha utume kwa mohammad. Na dalili za Qur’ani zinathibitisha hivyo. Mwenyezi Mungu anasema “Ewe mtume hakika sisi tume kutuma ukiwa ni mwenye kushuhudia na mwenye kubashiria na mwenye kuonya”.() Kisha amesema “Mohammad ni Mtume wa Mwenyezi Mungu”() na katika aya nyingine amesema “yeye (Mwenyezi Mungu) ndie alie mtuma Mtume kwa watu wasio jua kusoma anaetoka miongoni mwao”.()

Na jambo hili liko wazi kwa waislamu ya kuwa Mutume alitumwa na Mwenyezi Mungu na ni mtume wa mwisho, ikiwa atatokea anaedai ya kuwa Mtume Mohammad hakuwa ametumwa na Mwenyezi Mungu bali Jibrilu ambae ni kiunganishi kati ya Mwenyezi mungu na watu alifanya khiyana akapeleka utume kwa Mohammad badala ya kuupeleka kwa Ally bin Abi Twaalib (a.s.) hapana shaka mwenye kusema hivyo atakuwa kafiri na atakuwa ametoka kwenye uislamu, na waislamu watamlaani kwani atakuwa amekwenda kinyume na dalili za Qur’ani, pili atakuwa amepinga dharura moja wapo kati ya dharura za dini, tatu atakuwa amemtuhumu yule alie itwa na Mwenyezi Mungu kuwa ni muaminifu nae ni Jibrilu, nne atakuwa amemnasibishia Mwenyezi Mungu ya, kuwa Jibrilu alikosea naye akamnyamazia. Tano atakuwa amemtuhumu Mtume(s.a.w) yakuwa alichukua haki ya mtu mwingine. Sita atakuwa amefungua mlango wa shaka katika wahyi wote na Maudhui yake. Kwa Sababu mwenye kufanya khiyana katika kufikisha, inawezekana vile vile kufanya khiyana katika maudhui ya wahyi huo pia.

Kwa hivyo basi kunasibishwa akida kama hii tuliyo itaja kwa kundi lolote inatosha kulitoa kundi hilo katika uislam na haya ndio wanayo yanasibisha masunni kwa mashia na kusisitiza hivyo.

Baada ya Kazinukuu kauli zao tutazijadili ili tuone jinsi wanavyo wanasibishia mashia kauli hizo na tutaona athari zitokanazo na kauli zao hizo.

Kama maneno hayo yangekuwa yanasemwa na mtu wa kawaida kusinge kuwa na tatizo kiasi hicho lakini jambo la kuhuzunisha ni kaona kuwa wasemao maneno kama haya ni watu wenye nafasi zao, na nimiongoni mwa watu ambao maneno yao husomwa kila siku na niwanafikra wa kiislam walio mashuhuri kama wafuatao.

(1) Fakhru-Rrazi:

Aliwanasibishia hayo mashia katika Tafsiri yake ya aya hii.

((áóÇ íóãóÓøõåõ ÅöáøóÇ ÇáúãõØóåøóÑõæäó))

Maana yake “Hawaigusi Qur’ani isipokuwa walio twahirishwa”()

Na ninapenda kukukumbusha wewe msomaji yakuwa Ahlu Sunna hukitaja kikundi fulani na wakakinasibisha na mashia wakati ambapo ni kikundi kinacho jitegemea kisicho na uhusiano wawote na mashia na hufanya hivyo ili kuonyesha ya kuwa yanayo husishwa na kikundi hiki ni mambo makubwa na ili yaenee na ili ionekane kuwa hiyo ni rai ya mashia wengi. Kwa fano kuwaita (muhammadiya) kuwa ni kikundi cha mohammad wakikinasibisha kwa Mohammad bin Abdullah mtoto wa Imam Hassan mjukuu wa mtume wakati ambapo kikundi hiki hakipo kamwe.

Mambo haya amejaribu kuyataja Ibnu Taahir katika kitabu (Al-Firak baynal-firak) na kila mwenye maarifa ya vitabu vya kiislamu atafahamu ninani Fakhru-rrazi katika upande wa kielimu. Anapotaka kaihusisha habari fulani au rai fulani na mtu fulani isidhaniwe kuwa jambo hilo au rai hiyo hakuithibitisha au ametegemea kuenea kwa jambo hilo au rai hiyo, na ikiwa atafanya hivyo ina maana nafasi yake ya kifikra itatoweka. Na jambo alilo wahusisha nalo mashia tutaona usahihi wake hapo baadae.

2. Al-Kurtubi Al-Maaliky katika Tafsiri yake al-Kabiir.

Vile vile huyu bwana ni kama yule tulie muelezea mwanzo simtu mdogo na Tafsiri yake ni miongoni mwa Tafsiri zilizo muhimu na daraja lake la elimu ni la juu kwani ni nadra sana kukuta maudhui fulani ya Qur’ani ime andikwa ambapo hayakutajwa ndani ya Tafsiri yake. Basi ni upi msimamo wa msomaji ikiwa atayaona maneno ya huyu bwana aliyo wanasibisha nayo mashia?

3. Ibnu Taymiya:

Katika kitabu chake (minhaaju – Sunna) juzu ya kwanza amesema alipo kuwa akili nganisha kati ya mayahudi na mashia “mayahudi wanamchukia Jibrilu na wanasema yeye ni adui yetu katika malaika vile vile marawaafidhi wanasema alikosea Jibrilu kupeleka wahyi kwa Mohammad … na mtu huyu anayo mengi mazito aliyo wanasibishia mashia na nina muomba Mwenyezi Mungu awalipe mashia ikiwa ni ya kweli hayo waliyo husishwa nayo. Na amlipe bwana huyu ikiwa aliyo wahusisha nayo mashia hayata kuwa na ukweli wowote bali yali kuwa ni madai yasiyo na ukweli.

Sijawahi kuona mtu alie thubutu kuigawa kufru na imani kuliko mtu huyu. Baada ya hawa mabwana tuliowataja walifuatia wale walio fuata nyayo zao kama Aljabhani katika kitabu chake (Tabdiidu – Adhwalaam) na muhibbu ddini – Al-Khatiib na wengineo.

Kama ambavyo wakaanza wengine kuritibisha athari juu ya madai ya kuwa mashia sio waislamu kutokana na itikadi yao hiyo na khatib Al-baghdadi katika kitabu chake (Al-firaq baynal firaq) akaelezea ya kuwa “Haijuzu kumsalia shia wala haijuzu kusali nyuma yake na mnyama alie chinjwa na shia si halali kuliwa na haifai kumuoza shia binti wa kisunni na si halali kuoa kwao ikiwa binti huyo ana itikadi kama za mashia”() na hivi hivi ndivyo alivyo eleza pia mwenye kitabu kiitwacho (Al-ankihatul-faasida). Dr. Amir na wengine walio watangulia katika kikundi cha salafiyya walio kuwa ni mamufti wa miji ya kiislam. Na mas’ala haya yamekuwa mashuhuri hakuna haja ya kuyaeleza zaidi. Na mwisho tuna sema mabwana hawa mambo waliyo wahusisha nayo mashia kama ni ya kweli na Sahihi basi hakuna haja ya kutafuta dalili ya kuonyesha ukafiri wa yule mwenye kupinga dharura moja wapo kati ya dharura za dini kama hii, lakini kwa jambo hili tunasema.

1. Ni vigezo gani walivyo vitegemea juu ya madai yao hayo ya kuwahusisha mashia na kauli ya kukosea kwa Jibrilu katika kushusha wahyi kwa Mtume Mohammad? Sisi tuna wataka watuonyeshe vigezo hivyo na ni haki yetu kuwadai hawa walio toa madai haya chanzo moja wapo kati ya vitabu vyetu ambamo yanapatikana maneno hayo, na je wanaweza katupatia vitabu hivyo? Ikiwa hawawezi kupata chanzo cha maneno hayo ndani ya vitabu vyetu je wako tayari kuacha na kujiepusha na uzushi wao huo? Je wataona haya juu ya madai hayo.

Na dhana kubwa ni kuwa hawawezi kujizuia kutoa madai hayo kwani vitu vinavyo wapa msukumo wa kufanya hivyo vina fahamika.

2. Hata kama wangepata kitabu kimoja kinacho sema hivyo je ni Sahihi kuunasibishia ushia na mashia wote kauli kama hiyo kwa Sababu mtu mmoja kasema hivyo? Wakati vitabu vyote vya mashia vina pingana na jambo hilo? Na ukitaka uthibitisho soma vitabu vyao vya fikhi, na akida wimejazana katika maktaba na vina sema wazi ya kuwa Mwenyezi Mungu alimtuma Mtume Mohammad(s.a.w) na akamfanya kuwa ni Mtume wa mwisho na kwamba Jibrilu ni Muaminifu katika wahyi utokao kwa Mwenyezi Mungu na Qur’ani ina thibitisha ya kuwa Jibrilu ni mtiifu kisha muaminifu.

Mwanazuoni huyu aitwae Al-Karkhii ambaye ni miongoni mwa maimamu wa madhehebu ya Hanafi. Anasema Qur’ani na Sunna ikiwa vitapingana na kauli za wanazuoni wa kihanafi ni lazima kufanyiwata awiili (yaahi Qur’ani na Sunna).

Je Ahlu Sunna wanaridhia tutangaze yakuwa wao wanahukumu ya kuwa Qur’ani ni lazima ifuate kauli zao? Naje ikiwa tuta sema kauli kama hii je ita onekana ni kauli ya mantiki? Yenye kukubaliana na akili? kuna kauli nyingi kwa Ahlu Sunna zinazo nasibishwa kwa mtu mmoja mmoja katika hukumu na itikadi, hukumu ambazo zinatofauti kubwa na hazi wiani na mwendo wa kiislamu. Kwa mfano rai ya Bukhari ya kuwa “Maziwa ya ng’ombe yana Sababisha kupatikana uharamu, yaani ikiwa watu wawili watashirikiana kunywa maziwa ya ng’ombe moja Watakuwa ndugu wa kunyonya” je ni Sawa kauli kama hii kuinasibisha kwa masunni wote? Pamoja na yote hayo sisi tuna wataka angalau watoe ushahidi wa mtu mmoja anaesema ya kuwa Jibrilu alikosea au alifanya khiyana na kuupeleka wahyi kwa Mtume Mohammad (s.a.w) kama upo ushahidi tuna waomba watu onyeshe.

3. Ni jambo lililowazi kwamba imam Ally (a.s) alikuwa na Mtume wakati wote kwani ni mtu alie kuwa na mapenzi sana na Mtume kwani hata malezi yake yalifanywa na Mtume (s.a.w) na tukiiangalia historia yake tunakuta kuwa ni mtu aliejitolea kumtetea Mtume na dini ya Allah na alikuwa ni nafsi ya Mtume kwa dalili ya Qur’ani. Ikiwa ni kweli utume ulikuwa ni wa Ally mbona hatuoni kwamba Ally alikata mawasi-liano na Mtume au kutoa maneno mabaya dhidi ya Mtume? Je unadhani mashia pamoja na maulamaa wao walio bobea na wasio hesabika hawayafahamu hayo isipokuwa anae yafahamu ni Jabhani na wenzie tu watu ambao Mwenyezi Mungu aliwapiga mihuri juu ya nyoyo zao? Kama kweli wangekuwa wanaitakidi hivyo wange ona athari zake kati ya uhusiano ulio kuwepo kati ya Mtume na wasii wake (a.s.).

4. Imam Ally (a.s.) ulipo teremshwa wahyi alikuwa na umri kati ya miaka saba au kumi kutokana na riwaya mbili zilizo pokelewa. Je unadhani inawezekana kutumwa Mtume akiwa na umri wa miaka saba au kumi? Na je kunamfano wowote wa mtume kabla ya Mtame Mohammad (s.a.w) aliepewa utume akiwa na Umri kama huu na je hili ni katika mambo magumu yasiyoweza kufahamika?

Ni ajabu iliyoje kwa watu hawa wasio na elimu na wasio fahamu maneno ya Allah!

5. Qur’ani tukufu inasema:

(æóãóÇ ÃóÑúÓóáúäóÇ ãöäú ÞóÈúáößó ÅöáøóÇ ÑöÌóÇáðÇ )

“Hatukuwatuma kabla yako isipokuwa watu walio kamilikas katik. Aya hii limetumika neno “Rijaalan” neno hili hutumika kumuashiria mtu aliefikia utu uzima kisheria yaani aliefikia kubalighe na mwenye miaka kati ya ishirini na tano. Na Imam kama tulivyo tangulia kusema alikuwa ni mtoto. Na mengine mengi ambayo yalitakiwa yaangaliwe vizuri kabla ya kutangaza uzushi huu ndani ya jamii. Katika kitabu chetu (Hawiyatu shia)() tulibatilisha madai hayo.

Baada ya yote hayo tunasema misikiti yetu na vipaza sauti vyetu hupaza sauti ya adhana siku zote wakati wa sala tano pembe zote za dunia hunadi na kusema.

((ÃÔåÏ Çäø ãÍãøÏÇð ÑóÓõæáõ Çááå))

“Ninashuhudia ya kuwa Mohammad ni Mtume wa Mwenyezi Mungu. Je adhana zote hizi zitolewazo si dalili tosha ya kubatilisha uzushi huu? Watasema ya kuwa nyinyi mnasema hayo kwenye adhana kwa takiya na hapa tunawajibu kabla hawaja yasema hayo. Tunasema yakuwa katika adhana zetu tuna dhihirisha kauli ifuatayo “Nina shuhudia ya kuwa

((ÃÔúåóÏõ Ãäø ÚóáíÇð æóáöíøõ Çááå))

Ally ni walii wa Mwenyezi Mungu” na hatu tumii takiya. Basi tunge yadhihirisha hayo katika misikiti yetu iliyopo ulaya kama tunge kuwa tunaogopa kuyadhirisha kwenye misikiti iliyopo kwenye bara La asia au sehemu zenye waislamu wengi.

Kama ambavyo tungeweza kuyadhihirisha hayo katika nchi ambazo zilitawaliwa na mashia kama misri iliyo hukumiwa na faatimiya au iraq iliyo hukumiwa na buwayhiyiin au Iran ambayo ni dola la kishia au sehemu zingine zisizo hizo tungeweza kutangaza hilo bila ya khofu yoyote mbona hatufanyi hivyo? Je wanaweza kutujibu. Na ina onekana ni watu wanao pandikiziwa na watu wenye shubuha au wenyelengo la kuufarakanisha umma wa kiislamu na kuvunja umaja wao.

Jibu ni hapana, kwa sababu wao hawataki ukweli, na kama kweli wangekuwa ni watafutaji wa ukweli wasinge thubutu kusimama juu ya uzushi kama huu.

Japokuwa hawakosekani baadhi wenye dhamira nzuri ya kupinga uzushi kama huu kwa mfano shekh Muhammad Al-ghazali katika kitabu chake (Difau anil-Akida) na Dr. Abdul-Waahid Katika kitabu chake (Bayna shia wa Sunna).

MFANO WA TATU: KUVUKA MIPAKA KATIKA ITIKADI YA MAIMAMU

Vitabu vya Ahli Sunna katika fani zao mbali mbali zenye Uhusiano na elimu za kiislamu wamekuwa wakiwatuhumu mashia ya kuwa wanavuka mipaka katika Imani zao kwa Maimamu wao, kiasi kwamba wanawapa daraja wasizo zistahiki, na wanavuka mipaka katika kuwasifia. Na huenda baadhi yao wamekuwa wakitutuhumu ya kuwa tunasema kuwa wao wanafahamu mambo ya ghaibu kwa dhati zao (yaani kwa uwezo wao wenyewe) na kuwa wanao uwezo kibinafsi wa kugundua yaliyomo, na kwamba sisi tunawapa utawala wa kuviendesha viumbe vyote kwa kuviathiri kwa dhati zao na mengine mengi. Kwa ufupi wanadai ya kuwa tunawatoa Maimam wetu kwenye hali ya ubinadam wa kawaida na tunawa weka nafasi ya juu zaidi.

Katika sehemu hii nita anza kwa kuashiria ya kuwa watu wengi wasomao fikra za mashia huwa hawasomi fikra zilizo andikwa na mashia wenyewe bali husoma fikra zilizo andikwa na maadui zao au zilizo andikwa na watu ambao hawajaiva kifikra vizuri katika kufahamu mifumo ya dini na hawajaiva vizuri kiasi cha kuwa na uwezo wa kupambanua istilahi zake au fikra zake, au ni watu walio jichanganya na kushindwa kupambanua kati ya kuwa maimamu huletewa ujuzi kutoka kwa mwenyezi Mungu kwa njia hii au ile. Kama wanavyo jaribu kuonyesha ndugu zetu masunni ya kuwa waoa ni watu wa kawaida) na kati ya kuwa wanajua kwa dhati zao bila kujulishwa. Hizi ndizo sababu ilizowafanya kukosea katika kufahamu rai za mashia.

Ninapenda kuligusia jambo lingine nalo ni kuwa baadhi ya waandishi wana weza kuiona rai fulani ambayo ni moja tu kati ya nyingi na ni ya mtu mmoja au kundi fulani ambalo halipo tena (yaani limekwisha toweka) akaichukua rai hiyo na kuinasibisha na mashia wote. Kama ambavyo baadhi ya waandishi wanaweza kuiona riwaya fulani pamoja na kuwa wao si watu wenye ujuzi na maarifa ya uwanja huu wa riwaya kiasi kwamba baada ya kuiona riwaya hiyo akaifuatilia na kujua kama kuna riwaya nyingine inayo ipinga au inayo toa tafsiri yake au Ufafanuzi wake na kubainisha mambo yaliyo fungika ndani ya riwaya niyo. Yeye akachukua hatua ya kuiandika bila uchunguzi na natija yake ikawa ni kutoa hukumu ambazo hazipo ndani ya uislamu au hukumu zisizo za kweli.

Na pengine huwenda akawepo mwenye ujuzi wa elimu hizo lakini ndani ya moyo wake kuna magonjwa kiasi kwamba akatumia njia isiyo ya haki kuiandika na kutoa hukumu zisizo faa mfano wa aliye sema “Hakuna apasaye kuabudiwa” Bila kusema “isipokuwa Allah”. Pamoja na yote hayo nita onyesha katika sehemu hii japo kwa muhtasari rai za mashia katika maudhui haya. Zikiwa ni dalili tosha ya kuthibitisha msimamo wao juu ya suala hili, na mwisho nita nukuu rai za Ahli Sunna kwa Maimam wao ili tuone ni watu gani wanao vuka mipaka.

(1) Shia Imamiyya wametoa dalili inayo dhihirisha ukafiri wa maghulati na kwamba wao hawana uhusiano wowote na kikundi hicho na miongoni mwa dalili hizo ni kauli ya Mwenyezi Mungu, aya ya sabini na saba ya Suratul – Maaida. Mwenyezi Mungu amesema:

((Þõáú íóÇ Ãóåúáó ÇáúßöÊóÇÈö áóÇ ÊóÛúáõæÇ Ýöí Ïöíäößõãú ÛóíúÑó ÇáúÍóÞøö æóáóÇ ÊóÊøóÈöÚõæÇ ÃóåúæóÇÁó Þóæúãò ÞóÏú ÖóáøõæÇ ãöäú ÞóÈúáõ æóÃóÖóáøõæÇ ßóËöíÑðÇ æóÖóáøõæÇ Úóäú ÓóæóÇÁö ÇáÓøóÈöíáö)).

Maana yake.

“Sema: (ewe Mohammad) Enyi watu wa kitabu msivuke mipaka katika dini yenu kwa kuyachukua yasiyo ya haki wala msiyafuate matamanio ya watufulani walio potea kabla na wakawapoteza wengi na wakapotea kunako njia ya kweli”

2. Imam Ally (a.s.) amesema “Wameangamia kwa ajili yangu watu wawili: mwenye kunipenda na akavuka mipaka na mwenya kunichukia na akawa ni mwenye kusema”.()

(3) Pia Imam Swaadiq(a.s.) amesema: “Hatukuwa sisi ispokuwa ni watumwa wa Mwenyezi Mungu ambao alituumba na akatuchagua, na ninaapa kwa jina la Mwenyezi Mungu, mbeleya Mwenyezi Mungu hatuna hoja na wala hatuwezi kuepukana nae. Hakika sisi tutakufa na tutasimamishwa na tutaulizwa. Yeyote mwenye kuwapenda maghulati atakuwa ame tuchukia na mwenye kuwachukia Maghulati atakuwa ametupenda, maghulati ni makafiri na mufawidha ni washirikina.

Mwenyezi mungu awalaani maghulati kwani wali kuwa kama manasara walikuwa kama kadaria walikuwa kama murjia walikuwa kama Haruriyya”()

(4) Pia maulamaa wetu kwa pamoja wamekuba liana ya kuwa maghulati ni najisi na haifai kuiosha maiti yao. Pia haijuzu kuzika maiti yao, na ni haramu kuwapa zaka. Pia haijuzu wao kuwaoza binti wa kiislamu na haijuzu wao kumrithi muislamu isipo kuwa inajuza muislamu kuwarithi.()

(5) Shekh Mufiid katika kitabu chake (Sharhul-Akaidi Saduq) amesema: “Maghulati ni miongoni mwa watu wanaojionyesha ya kuwa ni waislamu, nao ni wale walio mnasibishia Amirul-muuminina Ally(a.s.) pamoja na maimamu katika kizazi chake uungu na utume na wakawatukuza ndani ya dini na dunia kiasi kwamba wakafikia hatua ya kuvuka mipaka na kutoka kwenye njia ya sawa. Kwa hiyo wao ni watu walio potea na ni makafiri. () Na dalili hizi tulizo zitanguliza ni kama vielelezo vinavyo bainisha rai ya mashia katika suala hili. La kuhusu maghulaati na kuhusu kuvuka mipaka katika imani ya maimamu. Na sidhani yakuwa wale wanao watuhu mu mashia kuwa wanavuka mipaka hawaja ziona dalili hizi, bali yaliwashinda matamanio yao kiasi kwamba wakawanasibishia mashia kuwa wamevuka mipaka. Na Mwenyezi Mungu ndio mwenye kutegemewa kwa yale wayasemayo.

Na tutaonyesha kwa ufupi mwendo wa fikra za Ahli sunna ili tuone je kwao kuna hali ya kuvuka mipaka katika masuala ya imam au hapana?

(1) Bwana Alauddini Dadeh katika kitabu chake (muhaadharatul-Awaail wa musaamaratul Awakhir) amesema “Kulitokea tetemeko la Ardhi katika mji wa madina, Omar akapiga juu ya Ardhi kwa upanga wake na akasema “tulia Ardhi” ikatulia” na tetemeko likatoweka. Na amesema vile vile maji ya mto Naili yalipungua na mtawala wa misri kwa wakati huo alikuwa Omar binil-Aasi, watu wa misri wakataka kumtosa bibi harusi ndani ya mto Naili kama kawaida yao, Omar binil-Aasi akawazuia na akamuandikia omar binil Khataab barua. Omar binil-Khataab katika Jibu lake akamtumia barua iliyokuwa imeandikwa mambo fulani akaitupia kwenye mto naili na mto ukafurika. Kisha ametaja tukio la vita vya mlimani (sariyatul Jabal) na la kuzima moto kuliko fanywa na khalifa Omar, Mwisho akasema hakika Omar Alikuwa na uwezo wa kuvitawala vitu vinne, Maji, Hewa, mchanga, na moto, na hii ndio maana ya (wilaya takwiniya) utawala katika viumbe na kuviathiri atakavyo, je Riwaya kama hizi zilitoa hisia fulani kwa Ahli Sunna baada ya kuzisoma ndani ya vitabu vyao? Ukweli ni kuwa ni hapana lakini kama ingepokelewa kutoka kwa mmoja wapo kati ya Maimam wa Ahlul Bayti ingeonekana kuwa, ni ghuluw (kupita mipaka) na ni kufru.

2. Ibnu Jawzi katika manaqib Ahmad bin Hambal kutoka kwa Ally bin Ismaaili amesema. Niliona katika ndoto kana kwamba kiama kimesimama na watu wakija kwenge kivuko na hapo haruhusiwi yeyote kuvuka mpaka aje na muhuri – na pembeni mwake kuna mtu amekaa akiwapigia mihuri. Nikasema ni nani huyo? Waka jibu hi Ahmad bin Hambal.

3. Al-Makiy ametaja katika kitabu chake (Manaaqib Abi Hanifa) ya kuwa amesema. Abu hanifa aliona katika ndoto ya kuwa yuko kwenye bustaani akiwa na kipande cha karatasi huku akiandika ijazaa ya watu fulani akaulizwa sababu ya kufanya hivyo akajibu. (Hakika Mwenyezi Mungu amekubali matendo yangu na madhehebu yangu na amenifanya niwe muombezi wa uma wangu na nina andika ijaza zao, akaulizwa wale unao waandikia ijaza, elimu zao yapasa ziwe zimefikia kiwango gani? Akasema wakielewa ya kuwa Tayamamu haijuzu kwa kutumia majivu).

4. Pia khatiib Al-Baghdad katika Taarekh yake juzu ya kumi na nne amesema kwa sanadi ya kutoka kwa Abi umama kutoka kwa Mtume (s.a.w) amesema Niliingia peponi… kisha akasema nilipokuwa mlangoni kikaletwa kiganja cha miizaani nikawekwa juu yake na umma wangu ukawekwa upande wa pili upande wangu ukawa mzito zaidi kuliko umma wangu.

Kisha akaletwa Abubakar akawekwa upande mmoja na umma wangu upande mwingine upande wa Abubakar ukawa mzito kuliko umma wangu. Kisha akaletwa Omar akawekwa upande na Umma wangu upande mwingine upande wa Omar ukawa mzito kuliko umma wangu kisha miizani ikainuliwa) Ikiwa na maana ya utukufu wa mabwana hawa juu ya umma wa mtume. Na maneno haya ameyapokea Hakiim Attir midhi kwenye kitabu chake (Nawaadirul-Usuul).

5. Pia Al-abiidy Al-Maaliky katika umdatul tahkiik, amesema: Mtume (s.a.w) alipokuwa karibu na Mwenyezi Mungu alipo kwenda miiraaji alishikwa na woga akiwa mbele ghafla akasikia sauti ya Abubakar moyo wake ukaingiwa na utulivu na akalewazika kwa kusikia Sauti ya swahibu wake.

Mpaka hapa nina waambia wale wanao tutuhumu kwa kuvuka mipaka kwa kusema tunavyo vitabu vyenu vinavyo elezea mambo kama haya bila kuongeza chochote na hatutaki kupoteza wakati wetu kwa kuya nukuu yote hayo na hatutaki kutekeleza malengo yenu ya kuyaandika mambo hayo na kuyaeneza kati ya waislamu badala ya kuzishughuli sha kalamu zenu kwa kutetea dini au kueneza mafundisho mazuri ya dini. Na sina shaka ya kuwa malengo ya watu wengi walio andika mambo hayo ni watu walio pandikiziwa shubuha zikawafanya wawe na lengo la kuufarikisha umma wa kiislamu. Na ni watu ambao ndani ya nyoyo zao kumejaa hikidi (kinyo ngo) ambazo ilikuwa ni lazima ziondoke hikidi hizo kwa sababu ya kuamini kwao. Na hikidi hizo zinge ondoka kama wangekuwa na malengo mazuri ya kuwaita watu kwenye neno laailaha illallah.

Na asitie dhanna yeyote ya kuwa tunayasema haya kwa kuogopa. Kwani hakuna sababu ya kutufanya tuogope na hatuna matumaini ya kuwa mtarudi nyuma na kufanya insaafu.

Isipokuwa wachache wenye nyoyo safi na wenye kuitaka haki. Kwa ajili yao tuna toa juhudi (tunafanya juhudi) na kuya andika haya ili waweze kunufaika huku tukimuomba Mwenyezi Mungu alie tuhimiza na kutuadabisha kwa kusema “Hakika umma wenu ni umma mmoja nami ni mola wenu, basi ni abuduni”. Ewe Mola hakika sisi tunakuabudu na wala hatu kushirikishi na chochote na tuna kiamini kitabu chako na Mtume wako Mohammad (s.a.w) na dini yako wewe ni Mola wetu na Mtawala wetu (Walii wetu) tuenezee (tupe) Rehma zako ewe Mwingi wa kurehemu.

rudi nyuma Yaliyomo