Yaliyomo endelea

UKWELI NI HUU

MTUNZI: SHEKH AHMAD WAAILIY

MTARJUMI: ABDULMAJID NASSIR

KWA JINA LA MWENYEZI MUNGU MWINGI WA REHMA MWENYE KUREHEM

UADUI NA UZUSHI DHID YA USHIA

Kila mwenye kufuatilia historia ya ummah au kikundi fulani, atakubali ya kuwa hakuna ummah au kikundi kilicho zushiwa mambo fulani au kugeuzwa maana ya mafundisho yake tofauti kama ushia.

Hakika mashia na ushia wamezushiwa mambo mengi yaliyo mabaya, pengine wamenasibishiwa mambo ya aibu ambayo hawanayo. Wakati mwingine wamenasibishiwa mambo ya watu wengine, na sihiv-yo tu kwani wamekuwa wakihusishwa na mambo ya maadui zao. Katika kurasa hizi chache tuta kutajieni kwa ufupi baadhi ya mifano juu ya mambo tuliyo yataja.

Niwengi walio alezea na hata kuandi ka vitabu kwa mapana no marefu juu ya maudhui haya. Kwa hiyo katika kijitabu chetu hiki tuta yaelezea kwa ufipi.

Hata kama ingekuwa kwamba malengo ya wale wanao andika kuhusu ushia na itikadi za kishia wanafanya hivyo kwa malengo mazuri au wanafanya hivyo kwa lengo la kutafuta ukweli. Yangetosha yale yaliyo andikwa na mashia wenyewe. Au yangetosha majibu yao waliyo wajibu waulizaji kubainisha ukweli wa itikadi zao na hata kubatilisha shubuha na kuondoa kiza kilicho kusudia kuficha historia yao na usahihi, wa itikadi zao (mashia).

Lakini inavyo onekana malengo ya wale wanao andika kuhusu ushia na mashia yako mbali na kuta-futa ukweli. Isipokuwa ni majaribio ya wazi wanayo yafanya ili kufuta na kubadilisha mafundisho na ukweli ulivyo. Na ni majaribio ya kutaka kuwabana mashia na ushia na kuwatoa katika jengo la uislamu kwa thamani yoyote ile.

Pamoja na majaribio yao ya muda mrefu hawaja weza kufanikiwa. Lakini pamoja na kutofanikiwa kwao bado wanaendeleza juhudi zao kwa nguvu zao zote ili kuona kuwa ushia na mashia wanawatoa ndani ya uislamu.

Baadhi ya jumuia zinasisitizia jambo hili kwa malengo yasiyo dhahiri na hata wale walio ajiriwa ili kufanya kazi hii pia wanasisitiza bila ya kudhihirisha malengo yao hayo na hata hao wafanyao kazi hii wamepotezwa kwa kupandikiziwa fikra potovu dhidi ya ushia na wakazijenga imani zao ya kuwa ushia sio uislamu. Wakaamini hivyo na kuyajengea dhana nzuri yale waliyopandikiziwa, na waka endeleakuamini hivyo na kufanyakazi bila kufanya utafiti juu ya mambo hayo.

Na baadhi ya watu walio lelewa katika uzushi huo waliyachukua mambo hayo kama urithi mtukufu. Kiasi kwamba inawawia vigumu kutia shaka juu ya mambo hayo ili wasiziudhi dhamira zao za dini ambazo wamelelewa nazo juu ya kuwazulia mashia na kuitakidi ya kuwa yanayo nasibishwa na mashia ni mambo yasiyo na shaka.

Ni wachache ambao dhamira zao nzuri na kuwa na ghera na dini yao imewafanya wahisi hatari na matokeo mabaya katika umma wa kiislam kwa kuenezwa uzushi kama huu. Wakapaza Sauti zao juu ya mambo haya na kuwaita waislamu wawafanyie uadilifu (insaafu) mashia.

Na wakafanya juhudi na majaribio ya kusahihisha sifa mbaya walizo pachikwa kinyume cha uislamu mbele ya madhehebu zingine za kiislam.

Majaribio yao yalikuwa ni Kuonyesha ya kuwa baadhi ya mambo yanayo nasibishwa kwa mashia hayana uhusiano wowote na ushia na mashia. Isipo kuwa ni mambo ya watu fulani au vikundi fulani ambavyo tiyari vimekwisha futika.

(Yani hovipotena katika ulimwengu huu) pia wali-jaribu kuonyesha kwamba baadhi ya rai za mashia ni Ijitihadi za maulamaa ambao walikosea katika ijiti-hadi zao na inabidi washauriwe ili waepukane na rai hizo.

Baadhi waliwalingania waislamu kuyanyamazia mambo hayo na kuongeza mashambulizi yao kwa nijia ya taratibu ili kuwafuta katika historia na kufanya hivyo ni kwa ajili ya kuunganisha na kuhifadhi jengo la uislamu ili lisiharibike.

Pamoja na majaribio yote hayo sijamuona yeyote kati ya hawa alie fikiria kurejea na kusoma vitabu walivyo virithi ambavyo vimeandikwa kwa ajili ya kuwashutumu mashia na wakafanya utafiti juu ya ukweli wa yale yaliyo andikwa ndani ya vitabu hivyo ili waweze kuona usahili wa hayo yaliyo andikwa.

Na ili aone kuwa, je, yaliyo andikwa ni kutokana na matakwa ya waandishi. Na hayana ukweli wowote bali yame vishwa tu Sura ya dini au itikadi? Au kuwa, waliyo nayo wao ndani ya vitabu vyao ni ukweli usio na shaka na usio hitaji kufanyiwa mjadala wowote wala utafiti?

Nime tangulia kusema hapo kabla ya kuwa ni wachache sana walio toa wito wa kuwafanyia (insaafu) mashia, na Sauti zao zikombioni kutoweka au kufifizwa ndani ya anga hili pana na refu na amani yao inakaribia kuyayuka katika mawimbi haya makali yanayotoa wito wa kuuteketeza ushia na mashia na kuwatoa katika uhai kiukamilifu. Yanafanyika hayo wakati ambapo tunawaona ahlu sunna pamoja na madhehebu zao wanakwenda mbio kumvuta angalau mtu mmoja awe katika safu yao. Na wanatoa pesa na juhudi kubwa kufanikisha hilo, lakini wao hao hao wana kwenda mbio na kusisitiza kuwatoa waislamu milioni miatatu walio mashia katika umma wa kiislamu kwa vigezo ambavyo mwenyezi mungu hakuvitere-mshia dalili ndani ya kitabu kitukufu.

Navyo ni vigezo ambavyo ikiwa watafiti watajika lifisha na wakafanya uchunguzi au utafiti juu ya ukweli wake au usahihi wake watagundua yakuwa ni vigezo vilivyo tegemea matakwa yao binafsi. Si vigezo vyenye dalili, na kwamba, natija waliyo ipata inatokana na msingi dhaifu. Kama ambavyo hawa kuangalia kwa upana na kuona ya kuwa matendo wayafanyayo yatatoa natija mbaya katika umma wa kiislamu. Kwa ufupi matendo hayo yanawaandalia njia wale wenye kutaka kuwagawa waislamu na kuufarakanisha umma wa kiislam. Kwa malengo ya Kuzinufaisha nafsi zao, na wenye kutaka kuingiza shaka katika nyoyo za baadhi ya watu ya kuwa uislamu sio dini ya umoja, bali ni dini inoyo lingani’a utengano, na ukiongezea ya kuwa kwa kufanya hivyo mwenyezi mungu atatuepusha na kutunyima Rehma zake na tawfiki yake. Na mwenyezi mungu ana sema “wamemsahau mwenyezi mungu akawasahaulisha nafsi zao”. ()

SABABU ZA UADUI DHIDI YA MASHIA

Katika kulielezea tatizo hili tujiulize kama ambav-yo wengine wamekuwa wakijiuliza Sababu na siri ya kuwa na msimamo dhidi ya mashia na ushia.

Katika kujibu Swali hili nitaelezea kwa ufupi sababu ambazo zimenidhihirikia nikitarajia ya kuwa sababu hizi zitatosha kiasi fulani kuonyesha Sababu ya uadui wanao fanyiwa mashia.

1. Tangu ulipoanza ushia katika zama za Mtume (s.a.w) na baadhi ya watu wakafahamika kuwa ni mashia, watu hao kwa wakati huo walijulikana kwa jina la (shiiatu Ally) (yaani wafuasi wa Ally) kwa mfano. Salmani, na Abu dhari, miqdad binil As’wad na Amar bin Yassir na wengineo, ulianza ushia ukiwa umewajumuisha watu fulani tu kwani kuanzakwake kulitokana na tathmini ya Mtume (s.a.w) kwa Ally(a.s.) na tathmini hii ili kuwa ni kumtofautisha Ally na wengine na haya tuna yashuhudia katika msimamo wa mtume (s.a.w) kumuelekea Ally(a.s.) na yote hayo yalitokana na mambo mbali mbali aliyo yafanya Ally katika kuutumikia uislam. Amma kuhusu dalili ni kuwa kuna aya kati ya sabini hadi miatatu katika Qur’ani tukufu kama alivyo eleza Abdullah bin Abbas na jamaa wengine ya kuwa aya hizi zinamuelezea Ally peke yake juu ya mambo aliyo yafanya na aya zingine zinamuelezea yeye pamoja na wengine. Na vitabu vya Asbaabu nnuzul, vimebainisha idadi kamili ya aya hizo na kueleza kila aya na muhusika wake. Pia katika hadith za Mtume kuna dalili nyingi ambazo zinahusiana na Ally wamezithi-bitisha wanazuoni wa Hadithi.

Ama misimamo ya Ally katika vitabu vya historia ni mingi sana kwani kuna matukio mengi ndani ya historia yaliyo fanywa na Ally matukio ambayo husisimua nyoyo na kushangaza, kiasi kwamba kila mwenye kuyasoma ataungana na Ally kimoyo na kifikra. Na mambo haya ndio yaliyo wapelekea baadhi ya maswahaba kuwa karibu na Ally. Na wakawa ni watu wenye kumpenda na wenyekumtu kuza kuliko wengine. Na maswahaba wengine wakawa na msimamo wa upinzani. Na wakafahamika kuwa ni kikundi cha upinzani. Na upinzani huo uli dhihirika zaidi baada ya upande wa upinzani kuchukua utawala na kujizatiti kwa kila uwezo dhidi, ya Ally kama ambavyo unajiimarisha upande unao tawala dhidi ya mpinzani wake.

2. Sababu ya pili ni kuwa. Kutokana na kuwa madeni ya Ally bin Abbi twalib (a.s.) yalikuwa ni mazito kwa ajili ya kumwaga damu za makuraishi na washirikina. Ukianza na vita vidago hadi vikubwa, vita ambayo vilifikia thamanini na tatu(83) ukiviju-muisha vyote kwa ujumla, Utakuta kuwa nafasi ya Ally katika vita hivyo ili kuwa ni kubwa zaidi. Kwa mfano katika tukio la badri. Nusu ya walio uliwa katika jeshi la mushrikina waliuliwa kwa upanga wa Ally (a.s.) na katika tukio la uhudi walio uliwa na Ally walikuwa ni watu kumi na nane(18) pia ukiongezea na nyumba za waarabu aliowajeruhi watu wake, japo kuwa vili kuwa ni vita vya kiislam dhidi ya ukafiri kiasi kwamba hapakuwa na sababu nyingine iliyopelekea kuwepo kwa vita kati ya Ally na watu hao isipokuwa uislamu lakini zile damu zilizo mwagwa katika vita hivyo hazikuhusishwa na uislamu bali zili husishwa moja kwa moja na mtume (s.a.w) na familia yake, yaani wao ndio wanao beba majukumu ya damu hizo.

Na akabebeshwa majukumu hayo Ally baada ya mtume (s.a.w.) na hayakuishia kwa Ally tu bali yalizidi kupanuka na kawajumuisha hata wale walio kuwa na mahusiano nae. kutokana na sababu hiyo mashia wa Ally (wafuasi wa Ally) wakaanza kupata misukosuko ya ulipizaji kisasi uliyo vishwa sura mbalimbali, zikamwagwa damu zao wakanyang’anywa haki zao na kuvunjiwa heshima zao na mwisho waka andamwa na milolongo ya tuhuma na uzushi dhidi yao. Na tuhuma moja wapo kati ya nyingi walizo tuhumiwa nazo nikuwa mashia si waislam. Na yote hayo yalifanywa na watawala wa kikuraishi ambao utawala wao ulidumu kwa muda mrefu.

Na tunaweza kusema kuwa hiyo ilikuwa ni kazi iliyo fanywa ili kuwaangusha mashia kazi iliyo tokana na wale walio jeruhiwa katika matukio tuliyo yaeleza hapo kabla.

3. sababu ya tatu inatokana na kuenea nadhariya ya shia kuhusu utawala na kuwa ni nani mwenye haki ya utawala baada ya mtume. Na hapo ikadhihiri hali ya kisiasa katika upande huu na ikajenga hali ya mapam-bano ya fikra na nadharia katika upande huu. Waandishi wa pande zote mbili wakaanza kuandika juu ya suala hili na kila upande ukijikusanyia nyenzo na uwezo wa kifikira na hapo yakaanza mapambano kati ya pande hizi mbili. Upande mmoja ukijitetea na upande mwingine ukifanya mashambulizi nao ni upande ulio kwenye utawala. Ama upande wenye kutawaliwa ambao maranyingi hufuata dini ya watawala ndio upande wenye nguvu na wenye nyenzo kiasi kuwa, haiwezekani kulinganishwa kati ya nyenzo zitumikazo pande hizi mbili kwani miongoni mwa nyenzo zilizotumika ni waandishi walio andaliwa na kupewa majukumu ya kafanya mashambulizi yasiyo na huruma. Kiasi kwamba misingi ya uamini fu na maadili ya uandishi katika historia ikavunjwa. Na maadili ya uandishi, manenomazuri pia yakatoweka. Na yaka badilishwa yote hayo kuwa ni matusi ambayo hata uislamu kamwe hauyaridhii. Na hali hii iliendelea kiasi ikafika mahala pa kusikitisha, ambapo kila muislamu mwenye wivu na dini yake atasikiti-shwa na hali hiyo. Na matokeo yake ilikuwa ni kukithiri uzushi mwingi dhidi ya mashia. Na hali hii ikaendelea tokea kipindi hicho hadli leo hii. Na huwenda hivi sasa imezidikuota mizizi inonyo onekana kutokana na mambo mawili yanayo toa msukumo kama mali na hikdi (chuki). Vitu ambavyo vimezidi kuwapa msukumo waandishi na kuzidi kuwasha moto kwa kuni zilizo imara ili usiweze kuzimika na Allah peke yake ndie mwenye uwezo wakuwakunjulia waislamu Rehma zake na kuwa Okoa kutokana na moto huu.

Sababu ya nne (4) ni kukinaika kikamilifu katika ulimwengu wa kiislam ya kuwa utawala ulikuwa khasa wa Ahli Sunna peke yao, na hali za kijografia na kiitikadi zili saidia kulifanya jambo hili liote mizizi. Hali hii inayo maelezo marefu. Hatuhitaji kuielezea kwa kirefu katika kurasa zetu hizi isipo kuwa tuna ashiria tu.

Ni jambo lililo wazi ya kuwa utawala unao uwezo wa kukusanya nguvu zote kufanikisha jambo hili, na hivindivyo ilivyo fanyika, kwani watawala walitumia hali iliyo kuwepo kiasi wakawatenga mashia na utawala kwa kutumia njia tofautitofauti.

Na hali hiyo ilipelekea kuota mizizi utawala upande wa Ahli Sunna na kuwafanyia uadui mashia, uadui ambao ulitokana na wale walio kimbilia madaraka nakuchukua utawala wa kiisham.

Sababu ya tano(5): inafahamika wazi jinsi fikra na fiqhi ya kishia zinovyo fungamana na dalili aya au hadithi na kutobadilisha dalili kwa kuzingatia vigezo vingine. Kama kutoifanyisha kazi dalili aya au Hadithikiwa itapingana na maslahi. Au kutoifanyisha kazi dalili ikiwa itapingana na rai ya madhehebu. Maana ya maneno haya ni kuwa hana nafasi yeyote atakae taka kuibadilisha dalili ya Qur’an au sunna ili mradi tu iwafikiane na matakwa yake au maslahi yake.

Wakati ambapo tunaona upande wa pili wakipanua maana ya dalili na kuzifungulia milango rai zao wanazo kusu diakuzitekeleza ziingie katika mafhum yao hayo kwa ajili ya kufikia maslahi yao kwa malipo yoyote yale, hata ikiwa ni kwa madhara ya dini. Kwa hivyo basi kutozichukua watu fikra za ushia kulitokana na Sababu hizi ukiongezea na sababu zingine zilizo changia pia. Kisha wakazidi kuwa mbali na fikra na fikhi ya kishia kwa kuzihujumu fikra hizi huku wakitoa madai kuwa haziambatani na Qur’ani na sunna ambazo haifai kuzikiuka kama Madai ambayo nyuma yake kulikuwa na maslahi, hata kama yame vishwa nguo nyingine na yaka onekana katika Sura ile.

Waanzilishi wa fikra hii potovu waliacha nyuma vitabu vingi vilivyobaki kama urithi ulio rithiwa, na ambao ilikuwa Si rahisi kuepukana nao. Wafuasi wa urithi huu wakafanya kazi ya kumshambulia kila mwenye kuupinga hata kama ni fatwa inayo ambatana na Haki, na kukubaliwa na waislam wote. Hii ni baadhi tu ya mifano na nyenzo mbali mbali zilizope-lekea kupatikana hali hii ya kuwazulia mashia na ushia, kwa uzushi mwigi tunao usikia. Na ili kuwa ni lazima kutokana na haya tuliyo yataja kudhoofika harakati za mashia kifikra na kijamii. Kwani masha-mbulizi yalikuwa yakiwalenga na yenye kufuatana katika zama na hali tofauti.

Vyombo vya habari vimo mikononi mwa maadui zao kama vile magazeti vitabu redio, television na vinginevyo. Pia mitaala ya masomo ni njia nyingine iliyo tumika na inayo tumika kuzishambulia fikra za ushia na kuziendeleza fikra za upande wa pili. Vile vile fursa za kujijenga zimefunguliwa kwa wanao beba fikra za kisuni, na zimefungwa kwa wale wabebao fikra za kishia bali hata wale wenye kuwafanyia upole mashia. Isipo kuwa tu mtu mmoja mmoja aliefanya harakati na kuhangaika huku na kule na kufanikiwa kujitengenezea maisha yake kwa juhudi zake chache. Na kama si Allah kuihifadhi Madhehebu na fikra za Aali muhammad hatahiki kikundi tukionacho kingetoweka na kuangamia.

Sababu ya sita(6)

Ikiwa tutachukulia kwamba msomaji hakuzitilia maanani Sababu tulizo zitaja hapo kabla kama vigezo na dalili za hujuma hizi zinazo fanywa siku zote dhidi ya mashia katika karne zilizo pita ita bakia Sababu moja tu kama ifu atavyo:

Kuwekewa vikwazo mashia tangu siku za mwanzo ambavyo vilitokana na tawala zilizo pita Sababu yake ilikuwa ni hali ya kisiasa iliyo lenga kuwafuta katika ramani ya ulimwengu kwa kuwaondoa maimamu wao kwenye utawala. Na ilikuwa ni lazima kutengenezwe visingizio kama tulivyo ashiria hapo awali. Na visingizio muhimu ni visingizio vya itikadi na baada ya muda mrefu ukachipukia umma uliolishwa na kulelewa katika hali ya kuwachukia mashia. Malezi ambayo vyombo vya habari ndivyo vilikuwa vikiya eneza ili wachukiwe, etikwa madai kuwa “Mashia wako kinyome na dini ya kiislam.” Na umma huu ukawa ukiendelea kuzaliana na kukua na kurithishana mambo haya. Nao ni urithi wa kuitakidi ya kuwa yale mambo yanayo nasibishwa na mashia ni mambo ya kweli wakati ambapo tunayakuta mambo hayo ni upotovu na uzushi usio na ukweli wowote.

Na watu hawa kutokana na ghera yao kwa dini yao ya kiislamu inawafanya wawe na msimamo dhidi ya mashia hasa ukizingatia kuwa bado kuna waandishi wengi wanaoendelea kuzitumia kalamu zao kucho-chea moto wakitaka kuonyesha muungano wao na fikra (dhenebu) iliyo kuwa ikitawala. Vile vile kwa ajili ya ghera ya maslahi yake na nafasi yake ya utawala. Vitu ambavyo huenda vitakuwa mbioni kutoweka na kupotea ikiwa haki itazungumzwa au kusahihishwa njia Iliyopo au huenda watakuwa hatarini ikiwa watawafanyia insafu mashia. Na msimamo wa watu wa sham (siria) kwa Imam Nasai hauko mbali na kumbu kumbu zetu wakati walipo muuliza kati ya Ally na muawiya ni yupi bora? Akawajibu “Na atawezaje muawiya kufikia kuwa sawa sawa (cheo kimoja) na Ali, seuze kuwa bara zaidi yake.” Kutokana na maneno haya watu wa Sham(Siria) kutokana na kufadhilishwa Ally juu ya muawiya walimponda ponda imam huyo hadi kumu uwa.

Pamoja na yote hayo inabakia amana ya historia na jukumu la Uandishi na kauli ya haki vikiwaita wanafikra na wafuasi halisi wa dini kuidhihirisha haki na kuyaandika mambo kama yalivyo, na vinawaita katita kuhisi umuhimu wa kulinda maslahi ya umma wa kiislamu na kuinua heba yake na kuunganisha neno lake na kulifanya jepesi lile lililo fanywa kuwazito na kutaka raadhi za Allah na maisha mazuri ya Akhera. Kwani faida zitokanazo na umoja wa waislamu ikiwa zitathibiti, basi hilo ndilo tumaini la kila nafsi iliyo epukana na machafu ya (ubaguzi) asabiya na akamtakasia nia Mwenyezi Mungu hata kama ni jambo zito kupatikana. Na historia inatuon-yeha kuwa mafanikio hayapatikani bila kupambana na matatizo mbalimbali yaliyo mazito hasa ukizingatia kuwa ukweli umedhihiri kutokana na kuenea vyombo vya habari na kupatikana vyombo vilivyo wafahamisha watu fikra za kishia. Na pia kuwepo maingiliano kati ya waislamu.

Yote haya tuliyo yataja tumeyataja kwa sababu ya kuondoa giza lililo tanda katika umma wa kiislamu, na kwa sababu ya kufahamu hali halisi ilivyo kuwa. Kwani kama madai hayo yangekuwa na ukweli ingetosha kuithibitisha hiyo Qur’ani inayo daiwa kuwanayo mashia tofauti na Qur’ani waliyonayo waislam wengine pamoja na kuwa zimepita karne kumi na nne tangu yaanze madai hayo hawaja weza kuithibitisha Qur’ani hiyo. Na ikiwa hakuna uwezekano wa kupatikana kopy mojawapo ya Qur’ani hiyo basi ndivyo hivi vitabu mama vya kishia vinapatikana, pia vitabu vya fiqhi ya kishia vinapatikana, yewezekana kuvirejea na kupata ukweli wa fikra zao zilizo wazi. Na hata fanya hivyo ila yule alie Shupavu na mwenye kuitaka haki.

Kwa hivyo basi sababu hii kwa mukhtasari ni kuwa uadui dhidi ya mashia na ushia na kuwazulia mashia ni jambo lililo tokana na nia ya wale walio kusudia kuwa toa mashia katika jamii ya kii slamu.

BAADHI YA UZUSHI UNAO NASIBISHWA NA MASHIA

Baada ya utangulizi huu nitaelezea maudhui yenyewe ambayo ndio malengo yangu. Nayo ni kutoa baadhi ya mifano ya mambo yanayo nasibishwa kwa mashia kwa lengo la kuwatoa kwenye uislamu na kuwafanya wawe ni wenye kuchukiwa kwa waislamu. Na nita taja mifano mitatu tu kama vielelezo na kipimo cha hayo mengine waliyo nasibishiwa.

MFANO WA KWANZA MADAI YA KUGEUZWA KWA QUR’ANI

Qur’ani tukufu ni kitabu cha Mwenyezi Mungu kilicho teremshwa ambacho hakikuingiliwa na baatili kabla ya kuteremshwa na baada ya kuteremshwa. Kitabu ambacho ndio msingi wa utamaduni wetu na ni katiba yetu na chemchem ambayo umma hurejea kwake. Na Qur’ani nikitabu kitakatifu kwa kila muislamu na nikitabu ambacho hakilinganishwi na chochote. Ni jambo lililo wazi yakuwa Qur’ani ndio chimbuko la msingi la sheria za kiislamu ambapo tunakuta kuwa vyanzo vyote vya sheria ndani ya uislamu marejeo yake ni Qur’ani. Kwa hivyo basi ikiwa kutakuwa na madai ya kugeuzwa kwa Qur’ani au kuwepo mabadiliko ndani ya Qur’ani mabadiliko ya kuzidi aya au kupungua, au kugeuzwa kwa baadhi ya sentensi, hawezi muislamu yeyote kuwa na uhakika ya kuwa sheria za kiislamu ni Sahihi na Salama. Kwani kauli kama hizi tiyari zinakitia kitabu hiki ila (kasoro).

Wakati ambapo tunakuta Mwenyezi Mungu akisema ((Hakika sisi tumeuteremsha ukumbusho (yaani Qur’ani) na Hakika ukumbusha huo tuta uhifadhi)).

Kutokana na nafasi ya Qur’ani katika nafsi za waislamu na utukufu wake, kikundi chochote au madhehebu yoyote yatakayo thubutu na kudai ya kuwa Qur’ani ilifanyiwa mabadiliko yatakuwa ni madhehebu ya ajabu katika umma na madai kama hayo itakuwa ni sababu ya kuchukiwa kwa hivyo basi jambo la kwanza lililo tengenezwa na kuzushwa na tawala zilizopita na kuwapa mawakala wao jukumu la kulieneza, ni kuwanasibishia mashia kauli ya kuwa Qur’ani ilifanyiwa mabadiliko. Na inshaallah tuta ona ukweli wa maneno hayo. Pia tutaziona kauli za masunni juu ya Suala hili ili kuona usahihi wa yale wanayo nasibishiwa mashia.

Kuna kauli nyingi za maulamaa wetu na mufassirina wetu zinazopinga madai haya kunasibishwa na ushia na kubatilishwa uzushi mwingi katika vitabu vingi vya kishia.

Kiasi kwamba huwezi kupitia kitabu chochote kinacho zungumzia elimu za Qur’ani na maudhui zake isipo kuwa utakuta kuna kurasa kadhaa zimetengwa maalumu kwa ajili ya kubatilisha madai ya kuwa Qur’ani ili badilishwa.

Sio lengo langu kuorodhesha yote yaliyo andikwa katika maudhui haya isipo kuwa ni kuashiria kwako msomaji baadhi tu ya vyanzo vinavyo onyesha rai za mashia kwa uwazi na nitataja tu baadhi ikiwa ni dalili kwa hayo niliyo yasema, kwa kiasi kinachotosha.

Rai za maulamaa wote wa kishia ni kuwa Qur’ani tukufu imehifadhiwa haikuingiliwa na mabadiliko yoyote kama kuzidi aya au kupungua katika sura zake na hata herufi zake, bali Qur’ani tuliyo nayo ndio ileile iliyo teremshwa kwa Mtume Muhammad (s.a.w.a) tuionayo kwenye majalada mawili na iliyo enea katika jamii ya kiislamu. Na unaweza kuyathibitisha maneno haya kwa kurejea katika utangulizi wa Tafsiru Attibyaan ya shekh Tuusi, pia utangulizi wa Tafsiru majmaul-bayaan ya shekh Tabrasi. Pia Tafsir “Kashful ghitaa” ya shekh ustaadhul fuqahaa shekh Jaafar. Katika mlango wa bahthul-Qur’ani. Pia waweza kurejea kwenye kitabu “Hakkul-Yakiin” cha mulla muhsinil – Faidh alie mashhuri kwa jina la Al-muhaddithul-Kaashaani. Pia rejea kwenye kitabu “Aalau-rrahmaani” cha shekh Muhammad Jawad Albalaghi, pia waweza kasoma “Al-bayaani fi – mukaddimat Tafsiril-Qur’ani” cha ayatullah Abil-Kaasim Khui na hiyo ndio rai ya shekh mufiid na shekh Bahai na Kaadhi Nurullah, nasi hawa tu bali muhakkikina wote.

Amma kawli inayo nasibishwa kwa shekh kulaini thiqatul-islam katika kitabu cha “Al-Kaaf” ya kuwa amepokea riwaya zinazo zungumzia kuwepo mabadi-liko ndani ya Qur’ani yeye mwenyewe anazipinga riwaya hizo na ana sisitiza mambo yafuatayo. Hadith zinazo elezea kugeuzwa kwa Qur’ani alizitaja kwenye mlango wa Hadithi zilizo nadra, na maana yake ni kuwa ni hadithi chache katika vitabu vya hadithi na ni hadithi ambazo hazitumiki. Kwa sababu hadithi kama hizi zikitofauti ana na Qur’ani na Sunna Sahihi Au hadithi zenyewe zikawa Sahihi lakini zikapingana na hadithi zingine zilizo mutawaatir. (mashuhuri) hadithi kama hizo huwa hazitumiki na haya ndio wayasemayo maulamaa wetu. (Katika mlango wa attaadilu wa tarjiihu) yaani ikiwa kuta kuwa na makundi mawili ya hadithi zinazo pingana na kundi moja linanguvu zaidikuliko lingine litatumika kundi ambalo hadithi zake zina nguvu zaidi na hizi ni istilahi za elimu ya usul. Na kwa kuwa riwaya zinazo elezea kugeuzwa kwa Qur’ani zinapingana na kitabu na Sunna na zinapingana na kauli mashuhuri na zenye nguvu zaidi ikaamuliwa kutotumiwa hadithi hizo.

Kisha ametaja katika kupambanua kati ya Riwaya sahihi na isiyo Sahihi lakufanywa ni kuipima na Qur’ani na Sunna Sahihi ikiwafikiana na vitu hivyo wiwili huchukuliwa na ikipingana navyo huachwa na hapa kuna dalili ya kuwa Shakh Kulaini hazipi uzito riwaya hizo isipo kuwa yeye alizipokea kama walivyo zipokea Bukhari na muslim, riwaya zinazosema kuwa Qur’ani ime badilishwa.

Vile vile ametaja riwaya ya Saadul-Khair iliyopo kwenye kitabu “Raudhatul-Kaafi” Riwaya ambayo imeeleza wazi kutokuwepo upungufu ndani ya Qur’ani kama riwaya ifuatayo “Akasema imam Baakir (a.s.) kumwambia Saadul-Khair na miongoni mwa kukipuuza kwao kitabu ni kuzibakiza herufi zake na kubadilisha hukumu zake”() na riwaya hii inabainisha wazi kukamilika kwa herufi za Qur’ani.

Sio kila mpokezi wa riwaya huyataja madhumuni ya riwaya kama inavyo fahamika katika elimu mbali mbali.

Hizi ni baadhi tu ya fikra zinazo elezea kubadili shwa kwa Qur’ani tukufu na msimamo wa mashia juu ya suala hili ukowazi na tunazo dalili nyingi zinazo thibitisha ya kuwa mashia hawasemi ya kuwa Qur’ani imegeuzwa. Ispo kuwa wasemao ya kuwa Qur’ani ilibadilishwa kwa maana ya kuzidi au kupungua maneno na aya ni wengine.

Ama kugeuzwa Kwa maana ya kubadilishwa maana ya maneno na aya na hata Sababu za kateremshwa aya fulani, mashia wanayo rai iliyo wazi juu ya jambo hili nayo ni kuwa wanakubali ya kuwa mabadiliko kwa maana ya kugeuzwa maana ya maneno, na ya baadhi ya aya na hata ya Sababu Nnuzuul- yali tokea katika riwaya nyingi, mabadiliko ambayo yalifanywa na mufassiriina kwa Sababu ambazo ziko wazi.

Na tutataja kundi la maulamaa wa Ahli Sunna wanaosema ya kuwa Qur’ani imepungua katokana na vitabu vyao.

Jambo la kushangaza ni kuwa masunni wenyewe ndio wasemao ya kuwa Qur’ani ilibadilishwa na kauli zao ziko wazi juu ya kupungua kwa Qur’ani waliyo nayo waislamu. Uki achilia mbali ya kuwa wanaratibisha athari za kauli hizo au hapana. Kwani imezoeleka ya kuwa wao siku zote wamekuwa hawarati bishi athari za kauli hii katika sehenu nyingi na hapa si mahala pa kutegemea kama dalili juu ya tusemayo lakini haya yanamazungumzo yake katika sehemu nyingine huenda tukayataja insha-Allah.

Nina kariri ya kuwa kauli zao ziko wazi juu ya kuzidi au kupungua kwa Qur’ani lakini wao hao hao wanawatuhumu wenzao kwa jambo hilo kama tutakavyo ona katika mifano tutakayo itoa.

Kwanza tutatoa kauli zao kisha tutaashiria vitabu ambavyo kauli hizo zinapatikana kwa mwenye kutaka kufanya utafiti zaidi.

(1) Suyuuti katika kitabu chake (Al itikaanfi ulumil-Qur’ani) amesema katika mlango wa idadi ya sura, maneno, na herufi za Qur’ani katika riwaya iliyo pokelewa kutoka kwa Omar binil-Khataab ya kuwa alikuwa akisema kwamba Herufi za Qur’ani ni milioni moja ishirini na Saba elfu.() Na riwaya hii ameitoa Tabarani kwa Sanadi iliyokubaliwa na ikiwa imeinuliwa katoka kwa Omar binil-Khataab.

(2) Vile vile muandishi wa (muntakhab Kanzul-Ummaal, ametaja katika riwaya yake kutoka kwa Zur bin Hubaish amesema: ubay aliniambia”Ewe Zur vipi unaisoma suratul- Ahzaab? nikamjibu. Suratul Ahzaab ni aya Sabini na tatu. Akasema ilikuwa Sura hii kama Suratul-Baqara au zaidi ya Al-baqara kutokana na riwaya hizi mbili tunafaidika ya kuwa hii ndio rai ya khalifa kama alivyo sema katika riwaya yake ya kuwa herufi za Qur’ani zilizoko ni chini ya theluthi ya herufi zote.

Na riwaya ya pili iliyo tolewa na ubay inaonyesha ya kuwa Suratul-Ahzaab iliopo ni chini ya theluthi ya sura iliyo teremshwa.

3. pia Ahlu Sunna wamesema ya kuwa Suratul-Al-hafd, na Al-Khal-I ni miongoni mwa Sura ndogo ndogo ambazo hazimo ndani ya Qur’ani nanisura ambazo Khalifa Omar binil-Khattab alikuwa akizitumia kwenye kunuti zake nazo ni kama zifuatazo:

((Çááøåãø ÅäøÇ äóÓÊóÚíäõßó æóäóÓÊóÛÝöÑõßó æäõËäí Úóáóíúßó æóáÇ äóßúÝõÑõßó æäóÎúáóÚõ æäóÊúÑõßõ ãóäú íõÝÌöÑõßó))

Maana yake.

“Ewe mola Hakika sisi tuna kuomba msaada. Na tunakuomba msamaha. Na tunakusifu. Na wala hatukukufuru. Na tunajiepusha na kumuacha mwenye kukuasi”

((Çááøåõãø ÅíøÇßó äóÚÈõÏõ æóáóßó äõÕóáøí æóäóÓúÌõÏõ æÅáóíúßó äóÓúÚì æäóÍúÝóÏõ äóÑúÌõæú ÑóÍúãóÊóßó æäóÎúÔóì äöÞãóÊóßó Åäø ÚÐÇÈßó ÈÇáßÇÝöÑíäó ãõáúÍóÞõ))

Maana yake. Ewe Mwenyezi Mungu wewe tu ndie tunae kuabudu na kwa ajili yako tuna Sali na kusujudu na kwako ndiko tunako kimbilia tunataraji rehma zako na tunaogopa adhabu zako. Hakika adhabu yako itawapata makafiri”()

Angalia katika kitabu cha Suyuti kwenye mlango wa idadi ya sura. Imepokelewa riwaya hii katika njia nyingi pamoja na kuwa sura hizi mbili hazimo ndani ya Qur’ani.

4. Imam Ahmad bin Hambali ametaja katika musnad Juzuu ya kwanza kwa Sanadi yake kutoka kwa Ibnu Abbas kutoka kwa Omar binil Khattaab ya kuwa amesema “Hakika mwenyezi mungu alimtuma mohammad na haki na akamteremshia kitabu na miongoni mwa aliyo mteremshia ni aya ya (Rajmi) ((kumpiga mzinifu mawe)) mtume (s.a.w.) akawapiga mawe wazinifu nasi tukawapiga mawe baada yake na tulikuwa tukisoma kama ifuatavyo.

((æóáÇó ÊóÑÛóÈõæÇ Úä ÂÈÇÆößõã Åä ßóÝóÑÇ Èößõã Ãä ÊóÑúÛóÈõæÇ Úä ÂÈÇÆößõã))

Maana yake ((Na wala msijiepushe na wazazi wenu ikiwa watakukufuruni kujiepusha na wazazi wenu)) na aya hii haimo ndani ya Qur’ani.()

5. Suyuti katika kitabu chake Al-itikaan ametaja riwaya ya (Naafiu) kutoka kwa mtoto wa Omar amesema “Asiseme yeyote ya kuwa nimeichukua Qur’ani yote. Nilipi linalo kujulisha ya kuwa ni yote. hakika ilitoweka sehemu kubwa ya Qur’ani, lakini mwenye kusema aseme yakuwa hakika nimechukuwa katika Qur’ani iliyo dhihiri.()

Vile vile imepokelewa kutoka kwa mwana Aisha mkewe mtume (s.a.w.) amesema: Suratul-Ahzaab ilikuwa ikisomwa katika zama za mtume (s.a.w.) aya miambili. Alipo andika othmani msahafu hatukusoma isipo kuwa kama ilivyo hivi sasa. Na riwaya hizi mbili ziko wazi Kabisa juu ya Suala hili.()

6. Imam Muslim amepokea katika kitabu chake Sahihi Muslim juzuu ya tatu kwa Sanadi yake kutoka kwa Abi harbi bin Abi aswad ya kuwa baba yake mussa Al-ash-ari ali sema kuwambia mahufadhi Wa Qur’ani basra (sisi tulikuwa tukiisoma sura fulani tukiifananisha kwa urefu wake na uzito wa maneno yake, na suratul-Baraa. Na nimeisahau isipo kuwa ninakumbuka sehemu hii:

((áóæú ßóÇäó áÇÈúäö ÂÏóã æÇÏöíóÇä ãä ãÇá áÇÈúÊóÛì æÇÏíÇð ËÇáöËÇð æáÇ íóãúáóÃõ ÌóæúÝõ ÇöÈúä ÂÏã ÅáÇø ÇáÊõÑÇÈ))

“Law kama mwana adam angekuwa na mapango mawili ya mali ange taka apate la tatu na hakuna kinachoweza kulijaza tumbo la mwana adam isipo kuwa udongo”.

Vile vile tulikuwa tukisoma Sura tukiifananisha na mojawapo ya sura za Al-musabbihaati na nimeisahau isipo kuwa Sehemu hii

((íÇ ÃíøåÇ ÇáÐíä ÂãäæÇ áöãó ÊóÞõæáõæäó ãóÇ áÇó ÊóÝúÚóáõæäó ÝóÊõßÊóÈõ ÔóåóÇÏóÉñ Ýí ÃÚúäÇÞößõã ÝóÊõÓúÃóáõæäó ÚóäúåóÇ íóæúã ÇáÞöíóÇãóÉö))

  Yaliyomo endelea