rudi maktaba >Maadili >

Rudi nyuma Yaliyomo endelea

Ulaya ya mashariki nako (kwa walahidi) wanadai kuondoa sheria zilizowekwa na dini kuhusu ndoa na kuchukua mfumo wa ‘ndoa ya pamoja’ uliopendekezwa Uingereza. Na nadharia hizi hivi sasa zinaenezwa kwetu; je kwa kiasi gani tutaweza kuzipinga?

Jibu: Uthabiti wetu na upingaji wa nguvu dhidi ya nadharia hizi za kikoloni ni lazima ushikamane na dini na desturi zake.

Mwanamke huchinjwa vipi?

Huku akiwa amefanikiwa na shuka nzito yenye nembo za kijani na weupe, wamemchukua mwanamke, na kumpeleka kichinjioni ili asihisi maumivu ya kifo. Wametumia neno ‘uhuru’ wakampokonya mwanamke uhuru wake, na mwili wake wakaufanya bidhaa yenye kuvutia kwenye mashirika ya biashara ya ngono! Ndiyo ni kweli kwamba hawakumtungika msalabani, lakini wamemfungia njia ili afuate mwenyewe kwenye biashara ya utumwa na ajiuze mwenyewe kwa wateja.

Wametumia neno ‘penzi lisilo la kuingiliana’ wakamsukuma msichana mdogo kwenye makao ya haramu na kumfanya achukue tembe za kuzuia mimba ndani ya madaftari ya hesabu anapoingia chuo kikuu kusoma.

Wametumia neno ‘kufanya kazi’ wakawapeleka wake za watu kwenye mikono ya wanaume baki vichochoroni bure!

Na wametumia neno ‘mchanganyiko wa ki-heshima’ kwa kuunda kizazi lanisi, kisicho na mwenendo wala afya nzuri, na mamilioni ya wanaharamu kwa mwaka mmoja tu!

Lau ningeliambiwa nichague jina la enzi hizi zetu ningechagua ‘Enzi za upotofu na uchizi uliosindikwa ndani ya maneno matamu”.

Hebu angelieni huku na huko, hivi kweli kuna fikra iliyobaki bila ya kusindikwa (kutiwa) ndani ya maneno matamu?

Zamani neno ‘zinaa’ liliwaogyofiya wasichana kama makali ya kisu; wakalibadilisha neno hilo kwa neno ‘uhuru wa mapenzi’ ili asiogope!

Neno ‘msago’, wakalibadilisha kwa ‘penzi la penzi’ ili liwe tamu na lipendwalo!

Neno ‘mwanaharamu’ lilikuwa lina aibu kwenye jamii, hivi sasa limekuwa ‘mtoto wa kimaumbile’ ili asionewe haya na mtu yeyote!

Basi, kama yalivyobadilika maneno, na mtazamo wa jamii pia umebadilika. Mwanzo mtazamo wa jamii ulikuwa mzuri, wenye mshikamano kisha ukawa umepotea, umezama kwenye taabu na masumbufu.

Zamani msingi wa jamii ulisimamia kwenye imani, mapenzi na utangano, uchu na uhalifu. Hivi ndivyo mwanaadamu walivyomuuwa kwa mwanadamu.

Ee chonde wanaadamu!

Safari ya ki-chizi inaelekea wapi?

Safari hiyo inayoanzia kwenye Mini inaishia wapi?

Jambo hili si gumu kama hesabu, tujumlishe, tutoe au tugawanye ndipo tupate majibu, la; majibu ni hali halisi kama tunavyoiona hivi sasa kwenye jamii ya kisasa inayoishi kwenye enzi hizi za upotofu wa kijinsiya na ufuska.

Kwa mtazamo wa haraka haraka tunapoangalia ndani ya jamii za kisasa tutagundua mambo yenye kuogofya yafuatayo:

Safari yenyewe hawaanzii kwenye Mini kama inavyodaiwa, bali inaanza pale mwanamke anapoanza kujionyesha nywele na sehemu zingine.

Kisha safari hiyo huendelea mpaka kufikia kwenye Mini ambayo itaonyesha miguu.

Kisha inaendelea mpaka kufikia kwenye Micro, ambayo iko senti mita ishirini na nne juu ya magoti.

Haishii hapo, kisha inaingia kwenye ‘stesheni’ ya Short (bukta) karibu na kwenda uchi

Kutoka hapo inasimama kwenye ufuo wa bahari kwa kustarehe kijinsiya kufanya mapenzi na kuoga maji ya moto (k.v. Sauna n.k.)

Kisha inafikia kwenye vilabu vya watembea uchi (Niudists) kama walivyozaliwa.

Kisha wiki nzima kwenye vilabu vya ngono zisizo za kawaida na kwenye maandamano ya mashoga na wanawake wanaopenda jinsiya na wake wenzao wakidai haki zao za kufanya mapuuzi kwa uhuru!

Kutoka hapo anafikia kwenye kujianika uchi na wenda-uchi wenzake kwa muda mrefu mabarabarani, viwanjani na hata kwenye mabwawa ya kuogelea.

Kuishi hatua za mwisho mwisho ni uvutaji wa bangi , hashish na ‘unga’ (heroin)

Mwisho wa safari ni kuharibika akili, wazimu na kujiua kwa pamoja .

Safari hii mbaya haichukui muda mrefu kufika, lakini kwa kweli inachukuwa maisha ya watu wengi mno katika jamii. Isitoshe ni safari moja lakini yenye vituo kumi ambavyo mtu lazima avipitie vyote kimoja baada ya kingine bila ya kuviacha vingine kwa sababu ‘orodha’ yake ni moja tu haiepukiki.

Wasomi wa elimu ya maadili wanasema: “Ngono inapelekea mtu kufanya nyingine, tendo la haramu ni sumaku ya kuvutia lingine la haramu, na kuvama kwenye maAsya kuna sababisha kuvama zaidi kwenye maAsya”. Na kama wasomi hao hamuwaamini, macho yenu je?

Hebu njooni, kisha tuinue shingo zetu kidogo tuiangalie jamii hii ya kisasa ‘ya viwanda’ ambayo inatukuza mitambo tu bila ya kujali gharama ya utu wa binadamu ambao umezidi kuzorota siku baada ya siku mbele ya moshi wa viwanda. Hebu njooni tuangalie takwimu zinavyoonyesha.

Nchini Ufaransa kuingiliana ngono, kinyume na maumbile kunafanywa bila ya kuona haya. Wanasema wake nchini humo “Baada ya yote hayo, tuna wanaume wengi wa nje tunaowazalia watoto” Nchini humo, mtu haoni vibaya kujichua, kufanya ulawiti, kuingiliana na wanyama na midomoni ambako huko ndiko kunapendezwa. Na huko Merekani, nako, mwanamke kwenda uchi ndiyo maendeleo na kunakubalika na kupigwa picha za jinsiya sehemu moja moja imekuwa pia ndio maendeleo.

Katika ripoti ya kila mwaka, imeelezwa kwenye mwaka 1965 ya manispaa ya mji wa San Fransisco, jimbo la Carlifornia kuzidi kwa makosa ya kijinsiya na kwamba, matoleo ya picha chafu za kijinsiya na watumishi wa nyumbani na wahudumu wa mahoteli walio vifua na mapaja wazi wanapohudumu wamezidi mno. Vilevile pana wasichana wanaojionyesha mili yao uchi, mihadarati, na ulawiti kwa wanaume wamefikilia nusu milioni mwaka huu.”

Safari hiyo ya wendawazimu inaendelea nchini Marekani, hebu angalia”

“Maofisi wa polisi walivamia ghafla jumba moja jipya liliopo mjini Atlanta, Georgia wakafanya msako, na wakapata mafaili ambayo inakisiwa kuwa ni ya kilabu cha kubadilishana wake! Msemaji wa polisi alinukuliwa akisema kwamba: “Kuna jarida linalotolewa na kilabu hicho lisemalo kwamba mlango wa kilabu u wazi kwa makapera na walioowa, wake kwa waume, na kwamba kilabu hicho kina matawi yake mjini New York, Chicago, Dallas, Orlando na Florida”.

Polisi mwingine naye anasema: “Kitendo cha kubadilishana wake kinazidi kuongezeka siku baada ya siku katika kilabu hicho.

Huko Sovieti safari hiyo potofu inaishia kwenye talaka, kwenye gazeti litokalo nchini humo la Pravda kuna makala maalum iliyoandikwa na mtaalamu wa mambo ya jamii Dkt Kharshev isemayo: “Katika kila watu kumi, watu tisa huwachana kwenye nchi za umoja wa kisovieti na sababu kubwa ni kuharibika kwa tabia na ulevi wa kupita kiasi. Na asilimia themanini ya uhalifu unaotendwa na vijana wadogo unatokana na kusambaratika kwa familia, vilevile wengi wanaoana hawaishi pamoja zaidi ya miaka mitatu au hata baadhi yao kwa miezi au wiki chache tu.”

Nchini Uingereza, ripota moja wakike wa jarida moja la kiarabu, ameeleza kwamba siku moja alikwenda nchini humo na kupokewa uwanja wa ndege na rafiki yake wa siku nyingi: alipomuona tu kitu cha kwanza alichokigundua kwa rafiki yake huyo ni kubadilika kwa sura yake ambayo mwanzoni ilikuwa nzuri na kuonekana mzee! Akataka kujua sababu iliyomfanya azeeke mapema hivyo akiwa na umri wa miaka ishirini na mitano tu; alimjibu: “Ah, kwa sababu ya matatizo mengi ya kisaikolojia”. Akamuuliza: “kulikoni, mumeo kakuwacha na kuchukua mrembo mwingine nini?” Akajibu! “Ndio kaniacha, lakini siyo kwa ajili kapata mrembo mwingine, la bali mwanamume kama yeye! Yule mwandishi alishangaa mno: “Nini? Mwanamume kama yeye?“ Akajibu: “Ndiyo, amekuwa mlawiti.”

Mwandishi huyo anaongeza: “Wimbi linaloikumba jamii ya Uingereza ni hilo la mapenzi ya waume kwa waume, na utaweza kufahamu hilo kwa kuangalia matangazo yake kwenye majarida. Ikiwa zamani mwanamume alikuwa akitaja sifa anazotakiwa awe nazo mwanamke anayetaka kumuoa, ama hivi leo atatoa sifa za mvulana anayetaka kumuoa! Zamani msichana anapotafuta mchumba hujitaja sifa zake gazetini, mathalan, msichana, umri miaka kumi na nane rangi ya nywele: kahawia, elimu: chuo kikuu: angependa kuolewa na mume aliye chini ya miaka thelathini n.k leo hii mvulana ndiye anayejitangaza, mathalan, umri miaka ishirini rangi ya nywele; nyeusi, rangi ya macho; kijani. Elimu: mwanafunzi wa mwaka wa tatu wa chuo kikuu, angelipenda ‘kuolewa’ na mume asiyezidi miaka hamsini… n.k.!

Je, si nilikwambia safari ya upotofu ni moja tu, mtu hawezi kufuata njia amoja akaacha nyingine!

Barua ya haraka kwa msichana wa karne ya ishirini na moja.

Kwako msichana wa karne ya ishirini na moja.

Wale wanaopigania uhuru hawakupiganii wewe, ati mwanamume fulani apigania uhuru wako kama unavyofahamu, sivyo, bali hao wenye njaa wanapigana wapate uhuru kwenye mwili wako wakuvutia, au ati mwanamke fulani atake uwe huru kwa sababu yeye yuhuru, la hasha, anachotaka ni kukuingiza wewe uwe pamoja naye katika pepo hiyo na mapochopocho, yeye anapotea na ataka wewe pia uanguke kwenye shimo la maovu kama yeye ili umuondolee hisia zake za kujiona yuko peke yake katika maovu hayo.

Hebu peleleza maisha yao hasa hao wanaopigania uhuru ugundue ukweli ulivyo: kwa hakika wote hao wana maovu yao wanataka kujificha uovu wao chini ya joho tukufu, na inaweza kuwa wana kasoro katika namna ya kufikiri au kwenye mambo mengine.

Pengine mtu anaweza kuwa kama Bw. Sartre anayepigania ‘uhuru’ akiulizwa nini maana ya uhuru, anasema: “Ni mwanamke awe na uhuru wa kufanya mapenzi na kila mtu.” Anapoulizwa ‘hata mkeo’ Anajibu, ndiyo, hata mke wangu akipenda kufanya hivyo.” Baadaye watu walipo yachunguza maisha yake ya utotoni waligundua kuwa alikuwa na kasoro.

Au pia inawezekana mwanamume akiwa ni wa aina nyingine mathalan, aina ya wale ambao mkewe au mabinti zake wana kasoro, au anataka tu tustarehe na wanawake wengi kwa masaa tu na kuwapokonya maua ya maisha.

Au pia inaweza kuwa ni kwa sababu nyingine; almuradi ni lazima utambue kuwa hakuna ‘anayekupigania’ uwe huru. Na jichunge sana usijaribu kuingia kwenye janga lolote, kwani utapotea.

Ukitawaliwa udhihirishe uso, nywele au mguu wako ‘kidogo’, usisadiki kwamba yataishia hapo tu bali yatafikia mahali ambapo hapana mwisho mwema. Unataka nikupe dalili?

Hebu chukua jarida lolote dukani uliangalie, kwa haraka kitu utakachokiona ni wasichana wadogo ambao kila mmoja wao aweza kuwa ‘mama’ na akaishi maisha matulivu ya ndoa, lakini wameufuata mwito wa kuonyesha nyuso, nywele na miguu ‘kidogo’ na wakaukubali mara tu baada ya muda mfupi walipogundua, tayari wameshakuwa ‘wasichana wanaohitajika wakati wa haja’, Ee Mungu azirehemu enzi za utawa (za zamani)!

Na msichana anapokuwa chombo cha kutumiwa kwa matamanio ya wengine anapoteza thamani yake, hata wewe rafiki wajua vizuri hilo. Na hata mwanamume anayemtafuta msichana kama huyu humpenda kwa muda mchache tu unaoteketea mara moja tu na kuwacha moshi mzito unaompoteza msichana huyo, na anapokufa hakuna hata mtu mmoja atakayemlilia. Ndiyo, ni kweli kwamba pengine utajisikia hamu ya jinsiya na ikawa inaweza kupatikana lakini ole wako usikubali kujiingiza kwenye hiyo. Kwani njaa yako yaweza kuwa ya uwongo na kuukosa heshima yako ya kike ni ukweli kabisa. Na mwanamke anapoukosa uwanawali wake basi haupati tena, au sivyo!

Dada mpendwa, wakikuhadaa ufanye kazi kiwandani au ya safari na utapata mshahara mkubwa uweze kukidhi mahitaji yako na ya watoto usiwasadiki kwani nia yao si wewe uchume bali nia yao wakupate kumbuka ya kwamba asilimia themanini ya wanawake wafanyao kazi viwandani nchini Merekani wamesinywa na kazi, kama ripoti zinavyoonyesha.

Na kumbuka pia ya kwamba mwandishi wa kike maarufu, Helen Michel amesema kwa uhuru, maendeleo ya ki uchumi na nafasi za kimataifa alizozipata mwanamke wa Ufaransa hazijamkwamua kutokana na matatizo yake mazito na wala hazikubadilisha hali yake na kuweza kupeleka jahazi la maisha.

Isitoshe, hakuna anayekupenda sana zaidi ya Mwenyezi Mungu aliyekuumba kwa hivyo usitende ila yale anayoyasema.

Kuiga: Maafa ya Ulaya Mashariki

Watu wa Ulaya mashariki walipojitenga na dini tu, hadhi yao ikaporomoka wakawa ni wenye kuiga tu. Wengine nao walipofika mwezini, vijana wetu nao wakavutiwa sana na hilo wakasoma magazeti yao ili wapate ramani iliyowafikisha huko mwezini lakini hawakuipata, ila tu waliambulia bimbiriza – mavi, habari za vijana wa Pop Music na, fikra ya uhuru, wao wakadhani mambo haya ndiyo ramani ya kufika mwezini. Wakaacha kila kitu. Wakavaa mavazi ya kike! Jee hii si aibu?

Hapana, maadam Waamerika wanafanya basi si aibu, si wao wamefika mwezini? Hayo ndiyo maneno yao.

Wengine wamefika kwenye safari ya Mars, vijana wetu pia wakavutiwa na lilo, wakasoma magazeti yao, wakapewa, wakipata “Sandwichi za kisaikolojia” zenye alama nyekundu na manjano wakadhani kula sandwich hizo ishirini kunatosha kumpeleka mtu kwenye Mars, wakamiminika madukani kuzinunua kwa fujo, mwishowe walicheza shere dini na maadili mema.

Walisikiliza idhaa zao wakasikia kwamba “kwa hakika hakuna misingi thabiti au ukweli unaopelekea kuwa na tabia njema, bali tabia zenyewe zinabadilika kutokana na jinsi hali za kijamii zinavyogeuka chini ya athari za kiuchumi, na kwamba fikra za binaadamu ni chombo kinachofuata maada tu (dunia) na vivyo hivyo mfumo wa kitabia ni chombo kingine cha ki-maada tu.”

Vijana wetu wakashikamana na fikra hizo kama wahyi ulioshuka, wakawa wanaishi na familia na jamii zao kwa kutumia falsafa hiyo mbovu, wakaanguka kwenye mlizamu (mfereji wa maji ya mvua) badala ya kutua mwezini na kwenye Mars. Ikawa kisa chao hiki kinafanana na kisa cha bwana mmoja aliyepata madaraka makubwa katika jamii, wenzake wakataka kujua sababu hasa iliyomfanya apate madaraka hayo, baada ya kipindi kidogo cha uchunguzi wao, mmoja wao akadai kwamba amegundua sababu, akawaambia wenzake, “nimegundua sababu iliyomfanya mwenzetu awe na madaraka ni kuwa kila anapoketi mahali huchezesha kidole chake gumba cha mguu kwa vidole vyake vya mkono na kulia! wenzake hao wakaingilia kujichezeachezea vidole vyote vya miguu, wakiwa na ndoto ya kubeba wadhifa mkubwa kama mwenzao!”

Kupanga uzazi… Kwa nini?

Mnamo mwaka 1965 huko Bombay, India, kulianzishwa shirikisho la kimataifa la kupanga uzazi (Family Planning), ambalo baadhi ya nchi za kiislamu zilijiunga. Sababu walizozitoa za kuanzishwa kwa shirikisho hilo ni kama ifuatayo.

Tatizo la makazi

Ongezelo kubwa la watu duniani kila mwaka halilingani na uzalishaji mdogo wa chakula duniani, kwa hivyo ni lazima kupunguza ongezeko hilo ili kujiepusha na njaa.

Umuhimu wa malezi ya watoto

Familia inayoweza kulea watoto watano mathalan katika hali ya kawaida , itaweza kulea watoto wawili kwa vizuri zaidi.

Kuinua hali ya maisha

Familia yenye kipato cha chini haiwezi kukidhi mahitaji ya lazima kwa idadi kubwa ya watu iliyonayo.

Kumkomboa mwanamke kutokana na majukumu ya ulezi katika kupanga uzazi kuna uhusiano mkubwa baina ya mwanamke kuzaa sana kukombolewa kwa sababu mke mwenye mtoto mmoja anaepukika na ulezi wa mtoto kwa zaidi ya miaka mitano, hivyo anakuwa amepumzika na majukuma yake.

Hizi ndizo sababu kuu wanazozitoa hao wanaopigania na kusimama upangaji uzazi. Nasi tunajibu hapa kwa ufafanuzi:

Kuhusu tatizo la ongezeko la wakaazi, hilo halipo ila kwao hao wanaodai hivyo, dunia, kama tujuavyo, ina uwezo wa kuzalisha chakula maradufu ya mahitaji ya wakaazi wake; kwa hiyo hakuna hoja ya kwamba ni dharura kupigana vita kumaliza watu kwa ajili ya maisha yao!

Kuhusu malezi ya watoto, haya ni madai ya fitna tu kwani malezi ya watoto hayana uhusiano wowote na kuzaa watoto wengi au wachache kwani familia ikiwa nzuri inaweza kulea idadi yoyote ya watoto, na ikiwa mbaya haiwezi kulea hata mtoto mmoja. Isitoshe, kukata kizazi ni kosa kubwa kwa jamii ya watu, kwani inawezekana, pengine yule mtoto, aliyezuiliwa na mamake asijaliwe, angelikuwa mtu mkubwa sana katika jamii kama angeachiliwa aishi. Angalia, lau Abu Talib, babaye Ali bin Abi Talib angefunga kizazi chake baada ya kuzaliwa Aqil (kakake Ali) je ni kosa kubwa kiasi gani angeliifanyia jamii ya watu.

Ama kuhusu kuinua hali ya maisha, inaweza kuwa hoja sahihi kama watu kuangalia kwa makini na kwamba mikutano ya kimataifa iweze baada ya kulipa umuhimu suala la ‘kupanga uzazi’ wangelipa kipaumbele suala la kuongeza makao ili yalingane na jinsi watu wanavyoongezeka.

Na kuhusu suala la kuhusisha upangaji wa uzazi na ‘kumkomboa’ mwanamke ni kweli lakini nani kasema kwamba inapasa mwanamke ajikomboe na majukumu na wajibu wake? Kuzaa kwa mpango si jambo lililo chini ya uwezo wa mwanamke tu, bali ni jambo lilio chini ya uwezo wa jamii, na jaribio lolote la kuzuia wasizaliwe watu wema kwa jamii ni kwenda kinyume na ubinaadamu wote ambapo huko kumkomboa mwanamke kwa maneno mengine, tayari anakombolewa kwa kuwaweka vifaa ili kumrahisishia kazi.

Hizi ndio sababu wanazozitoa, (tulizozijua) kwa ajili ya kupanga uzazi. Na maadam sababu hizi hazina hoja ya nguvu, basi nasi ni haki yetu kuuliza swali hili: hawa wanaofanya kampeni ya kupanga uzazi wanakusudia nini? Je kweli wanataka mwanamke aende kulingana na ratiba iliyopangwa ya malezi mazuri zaidi ili aweze kutoa huduma nzuri zaidi?

Mmoja kati ya viongozi wao, katika nchi moja ya Kiarabu anajibu “kwa hakika kazi ya kufanya kampeni ya upangaji uzazi lengo lake kubwa ni kuondoa desturi walizonazo watu; na ili tuweze kufanya kazi hii barabara ni lazima tuondoe zile fikra zinazokwamisha mpango huu”

Lakini bwana huyu hayaweki wazi maneno yake juu ya hizo anazoziita ‘fikra’ hizo ni fikra za kiislamu, na desturi hizo ni yale maadili na tabia za familia za kiislamu.

Ama njia ya kuziondoa ni kujaribu kutia shaka ndani ya Uislamu na kuileta misingi ya mambo kimaada (kidunia), ya kilahidi badala ya maadili ya kiislamu. Jambo la kushangaza ni kwamba wale wanaoshadidia mambo ya kupanga uzazi hawaoni umuhimu wowote wa kuenea ukahaba, kama ambavyo zile nchi zinazokampenia upangaji uzazi hazijaribu hata mara moja kuzuia ukahaba.

Je nini maoni ya uislamu katika kupanga uzazi?

Bila shaka uislamu haukubali kupanga uzazi kwa ‘mwito’ wowote ule. Kuna wale wanaopotosha hadith ya Mtume (s.a.w) isemayo: “Oaneni mzaane ili mpate kuwa wengi, kwani mimi nitajifaharisha kwa watu wa umma zingine siku ya kiyama hata kwa mimba iliyoharibika.” Watu hawa wanadai kuwa makusudio ya Mtume kusema ‘mpate kuwa wengi’ siyo wengi wa idadi bali wa aina fulani. Ndiyo, ni kweli uislamu unataka kupanga, lakini nani aliyesema uislamu unataka kupunguza kwa mpango, na si kuongeza lakini kimpango?

Ama ile hadith ya Mtume makusudio yake si ‘aina’ (kama wanavyodai) itakuwa na uhusiano gani basi juu ya kujifaharisha Mtume na aliposema mpate kuwa wengi na aliposema hata mimba iliyoharibika?

Kuhusu suala la ongezeko la wakaazi, uislamu umekuja na masuluhisho ya aina mbili

Ufafanuzi wa ki-ujumla

Ufumbuzi maalum wa hali halisi

Kabla hatujafafanua juu ya ufumbuzi wa kwanza ni lazima tukubali kwamba Uislamu umeruhusu baadhi ya familia kupanga uzazi.

Katika maoni ya Uislamu, Mwenyezi Mungu ameumba ardhi kulingana na wanadamu walivyo na daima kuna uhusiano baina ya mwili wa ardhi na mwili wa binaadamu kiasi kwamba haijatokea na wala haitatokea siku ambayo ardhi haitamtosha mwanaadamu vilevile, mazao ya dunia daima yanazidi mahitaji ya mwanaadamu hata kama watazaana kwa wingi. Qur’an inasema:

“Na Mwenyezi Mungu amekuumbieni wake kwa jinsi yenu, na akakujaalieni kutoka kwa wake zenu watoto na wajukuu, na akakuruzukuni vitu vizuri vizuri. Basi je, wanaamini yasiyokuwa ya haki na kuzikataa neema za Mwenyezi Mungu?” (16:72)

Neema za ardhi hazitakuwa chache kuliko mahitaji ya binaadamu isipokuwa ugawaji mbaya na mpango mbaya wa miji kisiasa ndiyo mambo yaliyosababisha ugumu wa maisha ya baadhi ya watu. Kuna baadhi ya nchi tajiri zenye ardhi zenye rutuba, madini na utajiri wa mali asili, na hali watu wake wanaishi maisha ya dhiki na mfumko mkubwa wa bei.

Pia kuna nchi zingine maskini zenye ardhi kame zinapatana na nchi tajiri lakini watu wake wanataabika na ukosefu wa chakula, njaa na vifo.

Ufumbuzi wake ni mdogo tu, zile nchi tajiri zifunguwe milango yake kwa nchi masikini na mipaka ya kisiasa iondolewe na mashirikisho ya kimataifa yasimamie chakula, hilo litafanya watu wote waishi kwenye ardhi moja wakistarehe na kuneemeka.

Nani aliyesema Amerika lazima kila mwaka iteketeze tani chungu nzima za ngano ya zaidi; ambapo kuna watu duniani kiasi cha milioni moja wanaokufa kwa njaa na ukata?

Nani aliyesema mataifa dunia yatumie milioni ya mapesa katika mashindano ya kujilimbikizia silaha bila ya kujua hatima yake, na hali kuna watu wanashindwa kupata mkate na tone la maji.

Takwimu za uchumi wa kijeshi na mashindano ya silaha duniani zinaonyesha kwamba gharama za matumizi ya kijeshi duniani zinazidi, kwa kiwango kikubwa, kuliko gharama za maisha katika sekta za kiafya, kielimu, chakula na kijamii. Tarakimu hizo zinafafanua kwamba matumizi ya kijeshi duniani katika mwaka 1966 na 1967 yalifikia dola milioni mia moja na themanini na mbili ($182) kila mwaka, na kwamba kiwango hiki kitapanda hadi kufikia dola milioni mia nne na tisini na tisa ($499) kabla ya kufikia mwaka 1977.

Na kulingana na takrimu za shirika la UNESCO, Gemini News Service, England, matumizi ya kijeshi ya dunia yanazidi matunzo ya kielimu dunia kwa wastani wa asilimia arubaini (40%)

Miongoni mwa mambo yaliyofichuliwa na UNESCO ni kama ifuatayo:

Gharama za kumsomesha shuleni mtoto mmoja kwa mwaka hazizidi dola mia moja ($100) ambapo gharama zinazotumika kwa mwanajeshi mmoja tu praveti zinafika dola elfu saba na mia nane ($7800)

Msaada (huo) anaotoa mtu katika nchi tajiri kuzipatia nchi masikini hauzidi hata dola nane ($8), ambapo kwa wastani anagharamika zaidi ya dola mia moja na sabiini ($170) kwa matumizi ya kijeshi!

Misaada ya kijeshi inayopokea nchi maskini kutoka nchi tajiri imeongezeka.

Hii ni kuongezea kwamba bado kuna utajiri mwingi sana wa mali asili ambazo haujavumbuliwa au haujatumika, utajiri ambao wataalamu wanakisia kwamba utakapogunduliwa utaweza kumuongezea mahitaji zaidi ishirini elfu ya wakaazi duniani kwa kila wanachokihitaji.

Hebu tuangalie utajiri ulioko baharini:

Kadri idadi ya watu inavyoongezeka duniani ndiyo matumizi ya nchi asili yanavyozidi kuongezeka kwa kasi na kwa wingi mno na watu wanaelekea zaidi baharini ambamo mna hazina kubwa sana ambayo bado haijatumika. Hivi sasa zaidi ya tani milioni hamsini za samaki huvuliwa kila mwaka na hiyo ni sehemu ndogo tu kama tone la utajiri ulioko baharini ambao kwa ujumla unaweza kufikia tani bilioni ishirini, mbali na mimea ipatikanayo baharini. Bidhaa zinazopatikana baharini zikitumiwa vizuri unaweza kuondoa tatizo la ukosefu wa Vitamin, Protini na mafuta katika chakula cha binaadamu.

Isitoshe, baharini mna hazina isiyokwisha ya madini mbalimbali wachilia mbali hazina za meli na majahazi yaliyozama ambazo ni kidogo sana kulinganisha na hazina zilizomo humo.

Chini ya bahari kunapatikana mabilioni ya tani za chuma na manganese, Nicel (madini kama fedha), shaba na madini nyingi mbalimbali. Uvumbuzi wa hivi karibuni umeonyesha kwamba kuna hazina ya kutosha ya mafuta baharini, na dhahabu iliyomo chini ya bahari ikiwa itagawanywa itatosheleza kila mtu duniani kupata tani tatu.

Isitoshe, maji ya bahari yanaweza kuzalisha umeme katika siku zijazo

Ikiwa utajiri wa dunia ni mkubwa kiasi hiki kwa nini basi kuwe na kutaka kukata kizazi? Uislamu unaposema ‘la’ hakuna kupanga uzazi hautegemei hoja tasa, bali ukweli ulivyo kwa dunia na watu wenyewe.

Ah! Mangapi mazuri yatapatikana lau uislamu utarudi?

Kuna mamia ya watu wanaokufa njaa nchini ya kivuli cha ulahidi. Mamia wengine wananyimwa kibali cha kuingia kwenye maisha kwa ajili ya kile wanachokiita ‘kupanga uzazi’

Lakini, kwa sababu uislamu hauamini kama wanavyoamini watu wa ki-maada wa kisasa kwamba, mwanaadamu ni manyasi ya jangwani anayetoka tumboni kwa mama yake, si muhimu, awe na njaa, kiu, au hata afe..!

Kwa matazamo ya uislamu, mwanaadamu ana heshima yake maalum kubwa zaidi ya heshima ya dunia, hata kilenge kilicho tumboni kina heshima yake. Kwa hivyo utaratibu wa kiislamu umetosheleza kila mtu maisha mazuri vyovyote itakavyokuwa.

Uislamu, kwa kiasi kikubwa, unafanya juhudi kumuandalia kila mtu shughuli njema ili aweze kuitosheleza familia yake, na asipopata kazi basi mtu aliye karibu naye amsaidie kimaisha, si kwa huruma na hisani, la, bali ni wajibu uliofaradhiwa na uislamu

Na kukiwa na familia maskini isiyo na uwezo na haina jamaa zakusaidia basi dola ya kiislamu ndiyo itakayowasimamia mahitaji yao ya kimalezi, kiafya na kijamii.

Maadam uislamu hautambui mipaka ya kikoloni baina ya dola za kiislamu, au hata mipaka ya duniani, na maadam mwanaadamu kwa mtazamo wa kiislamu ni ‘mwanaadamu’ basi nchi haziwezi kuwa na matatizo kwa wingi wa makazi. Hebu tupige mfano, mathalan nchi ya Misri imezidiwa na watu kisha nchi ishindwe kuwatosheleza mahitaji ya lazima ya watu wake, hakuna tatizo, wafungulieni wamisri mipaka ya Sudan ambayo ina ardhi kubwa na hali nzuri ya hewa kisha muwagawanyie pesa za mafuta za Libya kisha muwaache wajiendeleze…!

Hii ni kwa upande wa kutatua matatizo ya kiislamu ki-ujumla.

Ama kuhusu kutatua matatizo yaliyopo hivi sasa, kile kinachotoa uislamu ni rahisi kupatikana. Ardhi ya Kiislamu kama tujuavyo si ndogo bali ni kubwa na masafa yake yanatosha kwa kuishi na kuwaajiri watu wote duniani, isitoshe, ardhi hiyo si maskini kwa sababu ina madini, maji na rutuba. Mwenyezi Mungu ameumba petroli sehemu nyingine na nchi nyingine hakuweka, vilevile kwingine ameweka mito na kwingine hakuweka; naye alipoumba hivi hakuweka mipaka bali alimwambia ‘hii ardhi ni kwa ajili yenu, shikaneni na muishi kwa amani’ bali watu ndio walioweka mipaka umma mmoja wakaufanya ziwe ishirini, na taifa moja wameligawanya kwenye mataifa ishirini.

Nasi si wajinga kiasi kwamba tupendekeze ufumbuzi wa tatizo la wingi wa watu kwa njia ya kuondoa mipaka ghafla katika nchi za kiislamu, kwa sababu zoezi hilo si rahisi hivi sasa, kama si muhali. Lakini pia sisi si wajinga kiasi kwamba tuamini kwamba haiwezekani kukusanya pesa za Kiislamu zinazotumika mahotelini kwa ufuska kwa ajili ya kufungua viwanda vikubwa ambavyo vitawaajiri mamilioni ya watu kwenye mji wa Kiislamu wanaotafuta chochote na hawakipati!

Kwa hivyo basi sisi tunapinga ‘kupanga kizazi’ kwa maana ya kuzuia watu wazaane kwa sababu hizo, upingaji huu unaukosea umma wa kiislamu ambao unabeba majukumu mazito ya ulimwengu, ya kuutoa kwenye udhalili na kuweka kwenye uadilifu, uhuru na amani, na kisha kumtoa mwanaadamu kumpeleka kwenye anga ambao hajaijua upeo wake, na hatuamini kama watu milioni mia nane wanatosha kutekeleza majukumu haya.

Jambo la kushangaza ni kwamba propaganda za ‘upangaji uzazi zinaongezeka upande wa mashariki ya nchi za kiislamu kila kunapokuwa na mapambano kati ya nguvu za kikoloni, kilahidi na waislamu, na hasa wanapohisi kuwa nguvu hizo zinashindwa kutokana nguvu za watu za waislamu.

Na jambo jingine la kushangaza utafiti juu ya ongezeko la wakazi katika nchi za kiislamu kwanza huonekana kwenye magazeti ya kikoloni nchi za mashariki na magharibi kisha unaonekana katika magazeti ya nchi za kiislamu na watu wakavalia ujinga?

Lakini msisahau kwamba Ulaya mashariki na ulimwengu wa kiyahudi wanafanya juhudi kubwa ya kuongeza uzazi badala ya kupanga!

WAsya kwa mwanamke mu’min

Katika historia yetu adhimu, mwanamke ana sehemu kubwa na ya kijasiri, ambayo mara nyingine yamuonyesha akiwa kwenye uwanja wa mapambano, na wakati mwingine kwenye medani ya kupambana na ubatili, kuanzia bibi Maryam, bibi Khadija, bibi Fatima, bibi Zainab, Ummu Ammar na wengineo.

Kwa kweli mwanamke, pamoja na kazi zake za kawaida bado ana kazi kubwa ya kupambana na kubeba mas’uliya (majukumu). Wanawake wangapi walioviporomosha viti vya enzi vya mataghuti? Wanawake wangapi wameshinda madhalimu? Na kwa sababu hiyo, si ajabu kuwa katika Qur’an, neno kali dhidi ya ufalme na utaghuti lilitamkwa na mwanamke pale aliposema:

“(Malkia) akasema:

“Hakika wafalme wanapoingia mji (wa watu) huuharibu na wanawafanya watukufu wake kuwa dhalili; hivi ndivyo wanavyofanya (daima).” (27:34)

Ewe mwanamke mu’min!

Daima kumbuka kuwa Mungu wako na Mungu wa mwanamume ni mmoja, na uwezo aliokupa wewe ndio aliompa mwanamume. Majukumu mamoja, haki moja na marejeo yenu mwishowe ni mamoja tu.

Ama tofauti za ki-maumbile zilizoko kati yenu, hazimaanishi kwamba wewe ni madini ya feruzi (isiyo na thamani) na yeye ni almasi. Nyote mwatokana na Adam na Adam atokana na udongo.

“Enyi watu! Hakika tumekuumbeni kutokana na mwanamume na mwanamke. Na tumekufanyeni mataifa na makabila (mbali mbali) ili mjuane. Hakika ahishimiwaye zaidi miongoni mwenu mbele ya Mwenyezi Mungu ni yule amchaye Mungu zaidi..” (49:13)

Kuwa mume siyo fahari na ubora kama vile ambavyo kuwa mke si udhalili na aibu, bali kuwa hivyo ni njia tu ya kujuana na hivyo kuweza kushirikiana katika kubeba majukumu. Kama vile ambavyo haifai kwa mtu wa kabila fulani ajione bora kuliko mtu wa kabila nyingine kwa ajili ya nasaba na ukoo wake, au watu wa nchi fulani wajiona bora kuliko watu wengine kijografia au kilugha, basi hata kwa mwanamke si haki ajione bora kuliko mwanamke mwingine au kinyume chake, ila kwa kumcha Mungu tu.

“…Kwa hakika aliye mbora zaidi kwa Mwenyezi Mungu ni yule amchaye Mungu zaidi.” (49:13)

Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) pia amesema mara nyingi: “Nawausia juu ya wanawake.” Kwa hivyo basi, ni lazima kwa mwanamume mtilie manani sana mwanamke, kwani kuwapenda wanawake ni katika imani, na kadri mtu anavyozidi kuwa na imani kama asemavyo Mtume (saw) ndivyo anavyozidi kuwapenda wanawake. Siyo penzi dhaifu la kimwili basli penzi tukufu la kidini!

Rudi nyuma Yaliyomo endelea