rudi nyuma Yaliyomo  

WAFUASI HALISI WA AHLUL-BAYT a.s. NA SIFA ZAO

77. Imam Muhammad al-Baqir a.s. alimwambia Ja’bir, Al-Kafi, j. 2, uk. 74

“Je inatosheleza kwa mtu kujiita Shia na mfuasi wetu ati kwa kudhihirisha mapenzi yetu, Ahlul Bayt ? Kamwe sivyo hivyo !, Kwa kiapo cha Allah swt, huyo mtu kamwe hawezi kuwa mfuasi wetu isipokuwa yule ambaye amejawa khofu ya Allah swt na kumtii ipasavyo. Ewe Ja’abir! Wafuasi wetu hawawezi kutambuliwa isipokuwa kwa sifa zifuatazo watakazokuwanazo kama unyenyekevu, kujitolea; uadilifu; kumsifu Allah kupita kiasi; kufunga saumu na kusali; kuuwatii wazazi; kuwasaidia masikini, wenye shida, wenye madeni, na mayatima wanaoishi karibu naye; kusema ukweli; kusoma Qur’an; kuuzuia ulimi kusema chochote kuhusu watu isipokuwa kwa mapenzi; na kuwa mwaminifu kwa majamaa kwa maswala yote …….”

78. Amesema Sulayman Ibn Mahran kuwa yeye alimtembelea Imam Ja’afer as-Sadique a.s. wakati ambapo baadhi ya wafuasi (Mashiah) walikuwa karibu naye na alimsikia Imam a.s. akiwaambia, Al-Amali, cha Saduq, uk. 142 :

“(Mujiheshimu) muwe kama vito vya thamani kwa ajili yetu na wala kamwe musiwe wenye kutuaibisha sisi. Waambieni watu kuhusu mema, na muizuie ndimi zenu zisizungumze mneno maovu na mambo yasiyo na maana.”

79. Amesema al-Imam as- Sadique a.s. , Al-Kafi j. 2, uk. 56

“Kwa hakika, sisi huwapenda wale walio na busara, wenye kuelewa, wenye elimu, wenye kufanya subira, waaminifu na wenye imani. Kwa hakika Allah swt aliwajaaliwa Mitume a.s. kwa tabia njema. Kwa hivyo yeyote yule aliye na sifa hizo basi amshukuru Allah swt, lakini yule ambaye hana hayo basi amlilie Allah swt,Aliye Mkuu na Mwenye uwezo, na Amwombe hayo. “

Ja’abir kwa unyenyekevu alimwuliza Imam a.s. ndiyo yapi hayo, na Imam a.s. alimjibu: “Nayo ni: Ucha-Mungu, kutosheka, subira, kushukuru, kuvumilia, tabia njema, furaha, hima, bidii,shauku, mkarimu, mkweli na mwaminifu katika amana.”

80. Amesema Al-Imam Muhammad al-Baquir a.s., Al-Kafi, j.2, uk.75

“ Yeyote yule anamtii Allah swt basi ni mpenzi wetu, na yeyote yule asiyemtii Allah swt basi ni adui wetu (sisi Ahlul-Bayt)…..”

MADHAMBI NA ATHARI ZAKE

81. Amesema Mtume Muhammad s.a.w.w. , Bihar al- Anwar ,j.77,uk.79 na

Mustadrak Al-Wasail ,j.11, uk. 330 :

“Msitazame udogo wa dhambi, lakini muangalie muliyemuasi (Allah swt).”

82. Amesema Al-Imam Amir-ul-Muminiin Ali ibn Abi Talib a.s., Bihar al- Anwar ,j. 70, uk.18

“Iwapo mtu anapenda kujiona vile alivyo mbele ya Allah swt, basi ajitathmini kwa madhambi na maasi yake mbele ya Allah swt; basi kwa kipimo hicho ndivyo alivyo huyo mtu mbele ya Allah swt.”

83. Al-Imam as- Sadique a.s. aliwauliza watu ni kwa nini wanamwudhi Mtume s.a.w.w. Basi mmoja wa watu alimwuliza Imam a.s. vipi, naye Imam a.s. aliwaambia, Usul-i-Kafi , j.1, uk.219 :

“ Je hamujui kuwa matendo yenu yapoyanajulishwa kwa Mtume Mtukufu s.a.w.w. na pale aanapoona madhambi dhidi ya Allah swt miongoni mwao, basi husikitishwa mno. Kwa hivyo musimuudhi Mtume wa Allah swt na badala yake munatakiwa kumfurahisha (kwa kutenda mema).”

84 Amesema Ali ibn Abi Talib a.s. , Ghurur al-Hikam, uk. 235

“Kukosa kusamehe ni kasoro moja kubwa kabisa na kuwa mwepesi katika kulipiza kisasi ni miongoni mwa madhambi makubwa kabisa.”

  1. Kutokea Asbaghi bin Nabatah kutokea kwa Ali ibn Abi Talib a.s. amesema, Al-Khisal,cha as-Sadduq, j.2, uk. 360
  2. “Amesema Mtume s.a.w.w. kuwa Allah swt anapoikasirikia Ummah na kama hakuiadhibu basi bei za vitu vitapanda juu sana yaani maisha yatakuwa ghali, maisha yao yatakuwa mafupi, biashara zao hazitaingiza faida, mazao yao hayatukuwa mengi, mito yao haitakuwa imejaa maji, watanyimwa mvua (itapungua), na watatawaliwa na waovu miongoni mwao.”

    (Yaani Hadith hiyo juu inatubainishia kuwa iwapo kutakuwa na jumuiya ambayo imejitumbukiza katika madhambi basi wanabashiriwa kupatwa na mambo saba hayo yaliyotajwa. )

  3. Al-Imam al-Baqir a.s. amesema kuwa amekuta katika kitabu cha Al-Amir al-Muminiin Ali ibn Abi Talib a.s. akisema kuwa Mtume s.a.w.w. amesema: Safinat –ul-Bihar, j.2, uk.630
  4. “Wakati zinaa itakapokithiri katika jumuiya basi idadi za mauti za ghafla zitakithiri; na patakapokuwa na uovu basi Allah swt atawatumbukiza katika maisha ya ghali na hasara. Wakati watu watakapoacha kulipa zaka , basi ardhi itazinyakua baraka zake kutokea mazao, matunda, madini na vitu vyote kama hivyo. Wakati watakapotenda bila haki kwa mujibu wa Shariah, basi itakuwa sawa na kumsaidia dhalimu na ugaidi. Na watakapozikiuka ahadi zao, basi Allah swt Allah swt atawafanya maadui wao kuwasaliti na kuwakandamiza. Wakati watakapoacha uhusiano pamoja na ndugu na jamaa zao, basi yote yale wayamilikiayo yatakwenda mikononi mwa waovu. Na wakati watakapojiepusha na kutoa nasiha ya mambo mema na kuyakataza maovu na kama hawatawafuata waliochaguliwa Ahl-ul-Bayt a.s., basi Allah swt atawasalitisha kwa walio wenye shari miongoni mwao na katika hali hii, wataomba duaa lakini hazitakubalika.”

  5. Amesema Al-Imam Ali ibn Abi Talib a.s. , Bihar al- Anwar , j.70,uk.55
  6. “Machozi hayaishi illa kwa nyoyo kuwa ngumu, na nyoyo haziwi ngumu illa kukithiri kwa madhambi.”

  7. Allah swt alimwambia Mtume Dawud a.s.: Ithna-Ashariyyah, uk.59

“Ewe Dawud ! Wabashirie habari njema wale watendao madhambi kuhusu msamaha wangu, ambayo inajumuisha kila kitu kilichopo humu duniani, ili wasikate tamaa ya msamaha wangu; na waonye wale watendao mema kwa adhabu zangu ili wasije wakajifanyia ufakhari kwa utii wao, kwani ufakhari ni dhambi mbaya kabisa.”

ELIMU NA THAMANI YAKE

89. Amesema Mtume s.a.w.w. , Bihar al- Anwar , j.2, uk. 25

“Waalimu pamoja na wanafunzi wanashirikiana katika kuulipwa mema wakati watu wengine hawabahatiki..”

90. Amesema Mtume s.a.w.w. , Bihar al- Anwar , j.2, uk. 121

“Yeyote yule aienezaye Din kwa watu bila ya yeye mwenyewe kuwa na ilimu ya kutosha, basi anaidhuru Din zaidi kuliko vile anavyoitumikia.”

91. Amesema Ali ibn Abi Talib a.s. , Nhjul Balagha, semi nam. 482

“Thamani ya kila kitu ni katika ubora wake.”

Yaani thamani ya mtu ni katika ilimu yake. Cheo na utukuzo wake utakuwa katika kiwango cha ilimu aliyonayo. Macho yetu hayaangali sura, urefu ukubwa wa mwili wa mtu bali humthamini kwa kufuatana na kiwango cha ilimu aliyonayo. Hivyo inatubidi sisi sote tujitahidi katika kutafuta na kuipata ilimu kwa kiasi tuwezacho.

92. Amesema Mtume Muhammad s.a.w.w. katika Bihar al- Anwar ,j.2, uk.36

“Elimu ni amana ya Allah swt juu ya ardhi hii na wanazuoni ndio wenye amana hii. Hivyo yeyote yule atebdaye kwa mujibu wa ilimu yake, basi kwa hakika ameiwakilisha amana vile ipasavyo …”

93. Al-Imam Muhammad Baqir a.s. amesema:, Bihar al- Anwar , j.78, uk. 189

“Jitafutieni ilimu kwa sababu kujifunza ni matendo mema na kusoma kwenyewe ni ‘ibada.”

94. Al-Imam Ali ibn Abi Talib a.s. amesema: , Bihar al- Anwar ,j.1,uk.179

“Mtu ambaye anatafuta ilimu, ni sawa na mpiganaji vita katika njia ya Allah swt.”

95. Amesema al-Imam as- Sadique a.s. katika Bihar al- Anwar ,j.2, uk.92

“Uichunge sana ilimu yako na utazame ni kwa nani unaitoa.”

96. Amesema al-Imam as- Sadique a.s. katika Al-Kafi,j.1, uk.36

“Muitafute ilimu na kuipamba kwa subira na ukuu ; na uwe mnyenyekevu kwa yule ambaye anaitafuta ilimu kutoka kwako”

97. Amesema al-Imam as- Sadique a.s. katika Al-Kafi, j. 1, uk. 35

“Yeyote yule ajifunzae ilimu na kutenda vilivyo, na kuifundisha kwa ajili ya Allah swt, basi Malaika watatmukuza mbinguni .”

98. Amesema Mtume Muhammad s.a.w.w. katika Bihar al- Anwar , j.1, uk. 204

“Wema wa duniani humu pamoja na Aakhera ni pamoja na ilimu.”

ILIMU NA FADHILA ZA KUJIFUNZA

99. Amesema Mtume Muhammad s.a.w.w. katika Bihar al- Anwar , j.1, uk. 184

“Yeyote yule atafutaye ilimu ni sawa na mtu anayefunga saumu mchana na akikesha macho usiku kucha akifanya ibada. Iwapo atajifunza ilimu kwa sehemu fulani, basi itakuwa kwake ni afadhali kabisa hata kuliko kuwa na dhahabu ya ukubwa wa mlima Abu Qubais na ambayo itagawiwa sadaqa katika njia ya Allah swt.”

100. Al-Imam Zaynul ‘Aabediin a.s. amesema katika Usul-i-Kafi, j.1, uk. 35

“Iwapo watu wangalikuwa wakitambua kile kilichopo ndani ya kutafuta ilimu, basi wao wangaliitafuta hata kama itawabidi kusafiri na hata kuhatarisha maisha yao katika kuipata.”

101. Ali ibn Abi Talib a.s. amesema Qurar-ul-Hikam, uk. 348

“Kutafuta ilimu haitawezakana wakati mwili unastareheshwa.” (yaani mtu hataki kutaabika)

102. Amesema al-Imam as- Sadique a.s. katika Bihar al- Anwar ,j.2, uk.152

“Hifadhini maandiko na vitabu vyenu kwa sababu hautapita muda mutakapovihitaji.”

103. Ali ibn Abi Talib a.s. amesema katika Al-Kafi, j.1, uk.30

“Kwa hakika, kukamilika kwa Din ni kule kuitafuta ilimu na kuitekeleza ipasavyo, na muelewe waziwazi kuwa kutafuta ilimu ni faradhi zaidi kwenu nyinyi kuliko kutafuta mali na utajiri.”

104. Amesema al-Imam al-Hassan ibn Ali ibn Abi Talib a.s. katika Bihar al- Anwar ,j. 78, uk.111

“Wafundisheni watu wengine ilimu muliyonayo na mujaribu kujifunza ilimu waliyonayo wengineo.”

105. Amesema Mtume Muhammad s.a.w.w. katika Bihar al- Anwar , j.1, uk.167

“Fadhila za ilimu zinapendwa zaidi na Allah swt hata kuliko fadhila za ibada.”

ILIMU NA FADHILA ZA KUIFUNDISHA

106. Amesema Mtume Muhammad s.a.w.w. katika Ithna-Ahariyyah, uk. 11

“Mtu yeyote aliyekuwa na ilimu kuhusu swala fulani na akaificha pale atkapoulizwa basi Allah swt atamkasirikia kwa ghadhabu za moto.”

(yaani mtu anapokuwa na habari ambazo zitamsaidia mtu aliyepatwa na shida na ikaweza kumsaidia kuimarisha hali yake, badala ya kumsaidia yeye akaificha, basi hapo kwa hakika ametenda dhambi kubwa.)

107. Amesema Mtume Muhammad s.a.w.w. katika Bihar al- Anwar, j.92, uk. 19

“Qur’an tukufu ni chuo kikuu ; hivyo jielimisheni kiasi muwezavyo kutokea chuo hiki.”

108. Amesema Mtume s.a.w.w. katika Sunan-i-ibn-Majah, j.1, uk.88

“Kwa hakika, kile kitakachoendelea kumfikia mtu hata baada ya kufa kwake, miongoni mwa matendo yake mema ni : ilimu ambayo yeye amewafundisha na kuieneza kwa wengineo, mtoto mwema aliyemwacha, kuacha Qur’an Tukufu ikapatikana.”

109, Amesema al-Imam Ali ar-Ridha a.s. katika Ma’anil Akhbaar, uk.180 na ‘Uyun-il-Akhbaar –ir- Ridha, j. 1, uk.207

“Rehema za Allah swt ziwe juu ya yule ambaye anazihuisha amri zetu.”

Na halikuwapo mtu akamwuliza Imam a.s. ni vipi wanaweza kuhuisha amri zao, na Imam a.s. alimjibu: “Anaweza akijifunza ilimu zetu na akawafundisha watu. Kwa hakika, iwapo watu wangelikuwa wamezijua faida na mema ya semi zetu, basi kwa hakika wangalitufuata sisi.”

UTUKUFU NA UMUHIMU WA WANAZUONI

110. Amesema Mtume Muhammad s.a.w.w. katika Bihar al- Anwar , j.2, uk. 49

“Yapo makundi mawili ya Ummah wangu kwamba wanapokuwa wachamungu, Ummah wangu utakuwa sahihi na wakati watakapokuwa wameingiliwa na ufisadi, basi Ummah wangu utageuka kuwa waovu.”

Kwa hayo Mtume Muhammad s.a.w.w. aliulizwa kuhusu waliokuwa wakimaanishwa. Alijibu : “Wanazuoni wa Din na watawala.”

111. Amesema Imam Muhammad al-Baqir a.s. katika Bihar al- Anwar , j.1, uk. 222

“Utakapokuwa umekutana na Mwanazuoni basi uwe mwenye kutaka kujua mengi kuliko kujifanya msemaji zaidi, na ujifunze namna ya kusikiliza na namna ya kuzungumza vyema, na wala usimkatize kauli yake yoyote atakayokuwa akizungumza.”

112. Amesema Mtume Muhammad s.a.w.w. katika Ithna-Ashariyyah, uk. 245

“Ewe ‘Ali ibn Abi Talib ! Malaika Jibraili alitaka alitamani kuwa mwanadamu kwa sababu saba zifuatazo:

1. Sala za Jama’a

2. Uhusiano pamoja na wanazuoni

3. Kudumisha amani miongoni mwa watu wawili

4. Kuwahurumia na kuwahishimu mayatima

5. Kuwatembelea na kuwajua hali wagonjwa,

6. Kuhudhuria na kushiriki katika mazishi

    1. Kuwagawia maji mahujjaji

Kwa hivyo nyinyi pia muwe watu wa kuzipenda na kuvitekeleza vitu hivyo.”

113. Ali ibn Abi Talib a.s. amesema katika Nahjul Balagha, semi nam. 265

“Iwapo matamshi ya watu wenye busara yatakuwa katika malengo yao, basi huwa kama matibabu, lakini yanapokuwa siyo sahihi basi ni sawa na ugonjwa.”

114. Amesema al-Imam Hassan al ‘Askari a.s. katika Al-Ihtijaj, j.2, uk. 155

“Maulamaa wa Kishia’h ni walinzi wa mishikamano ya Islam. Kwa hivyo, yeyote yule katika wafuasi wetu anayechukua jukumu hili basi ni bora kuliko kupigana vita dhidi ya Waroma (kwa sababu huyu analinda mishikamano ya imani zetu).

115. Amesema al-Imam ‘Ali ar-Ridha a.s. katika Bihar al- Anwar , j.2, uk.5

“Jihadharini kuwa hakimu wa kidini wa kweli ambaye anapatia watu mema na huruma, na kuwahifadhi dhidi ya maadui wao, kuwazidishia neema za Peponi na kuwapatia ridhaa za Allah swt kwa ajili yao (kwa kupitia hidaya).”

116. Al-Imam ‘Ali ibn Abi Talib a.s. amesema katika Bihar al- Anwar ,j.2, uk. 43

“ …. Malipo kwa Mwanazuoni ni zaidi kuliko malipo ya mtu afungaye saumu nyakati za mchana na kusali nyakati za usiku na akipigana vita vya jihadi kwa ajili ya Allah swt. Na, wakati mwanazuoni anapokufa, basi kutatokezea pengo katika Islam ambalo haliwezi kuzibwa illa kwa aina yake tu.”

117. Al-Imam ‘Ali ibn Abi Talib a.s. amesema katika Nahjul Balagha,semi nam.147

“Ewe Kumayil ! Wale wanaojilimbikizia utajiri na mali ni watu waliokwisha kufa hata kama watakuwa bado hai, wakati maulamaa (wanazuoni) wenye elimu watabakia hadi hapo dunia itakapokuwa ikibakia. Hata kama watakuwa lakini mafunzo na mifano yao itabakia mioyoni mwa watu.”

118. Amesema al-Imam Husayn a.s. katika Tuhaful ‘Uqul, uk. 172

“ ….. Kwa hakika, njia ya masuala ya Waislamu na hukumu za Shariah zipo katika mikono ya Wanazuoni wakimungu ambao ndio wenye amana za Allah swt katika mambo ayatakayo na yale asiyoyataka …”

KUWA MAKINI KUHUSU AKHERA

119. Amesema Mtume Muhammad s.a.w.w. katika Bihar al- Anwar, j.1, uk. 203

“Wafuasi wa Mtume Isa a.s. walimwuliza ni watu gani wawafanye marafiki wao, naye a.s. aliwajibu: “Pamoja na wale ambao wanapokuwa nanyi humkumbusha Allah swt, mazungumzo yao hukuzidishieni ilimu na matendo yao huwavutieni ninyi kutenda matendo mema kwa ajili ya Aakhera.”

120. Al-Imam ‘Ali ibn Abi Talib a.s. amesema katika Qurar-ul-Hikam, uk. 335

“Kusiwepo na shughuli ya aina yoyote ile ambayo itakuzuia kutenda matendo kwa ajili ya Aakhira, kwa hivyo, muda wa kufanya hivyo upo mdogo sana.”

121. Al-Imam ‘Ali ibn Abi Talib a.s. amesema katika Qurar-ul-Hikam, uk. 274

“Yeyote yule atakayeiuza Aakhera yake kwa maisha ya humu duniani, basi kwa hakika amepoteza yote kwa pamoja.”

122.. Al-Imam ‘Ali ibn Muhammad al-Hadi a.s. amesema katika Bihar al- Anwar, j. 78, uk. 370

“Kumbuka pale utakapokuwa kitandani ambapo mauti imekukalia kichwani na huku umezungukwa na ndugu na majamaa zako, na hapo hakuna mganga anayeweza kukuepusha na kifo hicho wala hakuna rafiki anayeweza kukusaidia.”

T A W B A

123. Amesema Mtume Muhammad s.a.w.w. katika Al-Mahajjat-ul-Baydha

“Majonzi makubwa ya watu wa Jahannam ni kuahirisha kwao Tawba”

124. Amesema al-Imam Muhammad al-Baqir a.s. katika Was’il al-Shiah,,j.16, uk.74

“Yeyote yule anayefanya Tawba ni sawa na yule mtu ambaye hana mzigo wowote wa madhambi ya aina yoyote ile.”

125. Al-Imam ‘Ali ibn Abi Talib a.s. amesema katika Qurar-ul-Hikam, uk. 240

“Wapo waahirishaji ambao huahirisha kufanya Tawba hadi hapo mauti inapowafikia.”

126. Mtume Muhammad s.a.w.w. alimwambia Al-Imam ‘Ali ibn Abi Talib a.s. , katika Bihar al- Anwar,j.77, uk.63

“Ewe ‘Ali ! Amebarikiwa yule ambaye anatazwa na Allah swt wakati pale anapolia kwa ajili ya kutaka msamaha wa madhambi ambayo hakuna mwingine ajuaye illa Allah swt tu.”

(Baadhi ya Ahadith zinasisitiza kuwa haimpasi mtu kuwaambia watu wengine juu ya madhambi yake mwenyewe. Hivyo inambidi aungame madhambi yake kwa Allah swt tu na wala si kwa mtu mwingine.)

127. Amesema Mtume Muhammad s.a.w.w. katika Bihar al- Anwar ,j.3, uk. 314

“Katika kila sehemu ya tatu ya usiku na usiku wa kuamkia Ijumaa kuanzia usiku uingiapo( hadi alfajiri) Allah swt huwauma Malaika mbinguni ili kuita: ‘Je yupo mwenye kuomba ili nimtimizie ombi lake ?’ Je yupo yeyote mwenye kufanya tawba ili nimrejee ? Je yupo aombaye msamaha ili nimsamehe ?’ “

Tanbihi: Katika utamaduni wa Kiislamu, tunafundishwa kuwa kulala katika usiku wa kuamkia Ijumaa kunaitwa usingizi wa masikitiko ; kwa sababu Siku ya Qiyama watu watakuwa wakisikitika mno kwa kulala usiku hizo.

128. Amesema al-Imam as- Sadique a.s. katika Bihar al- Anwar, j.92, uk.216

“Fungeni milango ya madhambi kwa kumwomba Allah swt , na mufungue milango ya utiifuu kwa kusema Bismillah-ir-Rahmaan-ir-Rahiim.”

KULINDA HESHIMA YA WAUMINI

129. Amesema al-Imam Muhammad al-Baqir a.s. katika Bihar al- Anwar , j.74, uk. 301

“Ni faradhi kwa kila Mwislamu kusitiri na kuzificha aibu sabini (70) za Mwislamu mwenzake (ili kulinda heshima yake).”

(Makosa na kasoro zake zote zishughulikiwe kibinafsi na wala zisienezwe na kutangazwa kwa watu wengine).

130. Al-Imam ‘Ali ibn Abi Talib a.s. amesema katika Bihar al- Anwar, j.74, uk.165

“Kubali msamaha akuombao Nduguyo Mwislamu na kama hakufanya hivyo, jaribu kumvumbulia hivyo.”

131. Al-Imam ‘Ali ibn Abi Talib a.s. amesema katika Mustadrak Al-Was’il al-Shiah’il-ush-Shiah, j.12 , uk.305 na 14155

“Hali mbaya kabisa ya uhaini ni kutoboa habari zilizo siri.”

132. Al-Imam ‘Ali ibn Abi Talib a.s. amesema katika Ghurar-ul-Hikam, uk. 322

“Kumuonya kwako aliyetenda makosa miongoni mwa au mbele ya watu ni kumdhalilisha.” (Inakubidi uongee naye katika faragha).”

133. Amesema al-Imam as- Sadique a.s. katika Al-kafi,j.2, uk. 192

“Katika matendo yote aypendayo Allah swt, ni kule kumletea furaha Mwislamu kwa mfano : kumshibisha, kumwondolea majonzi yake, au kumlipia madeni yake.”

M A T E N D O M E M A

134. Amesema Mtume Muhammad s.a.w.w. katika Bihar al- Anwar ,j.76, uk. 43

“Kwa kufanya usuluhisho na amani miongoni mwa watu wawili (kwa kulinganisha) ni borai kuliko ibada za sala na saumu zake mwenyewe.”

135. Al-Imam ‘Ali ibn Abi Talib a.s. amesema katika Nahjul-Balagha, uk. 511 ,Semi na. 248

“Iwapo mtu atakufikia wewe kwa mema, basi inakubidi uhakikishe kuwa fikira zake zinabakia kweli.”

136. Amesema Mtume s.a.w.w. katika Bihar al- Anwar ,j.96, uk. 119

“Yeyote yule awaongozaye watu kwa taqwa (atalipwa) sawa na yale ayatendayo (aliyeongozwa) hayo matendo mema..”

137. Amesema al-Imam as- Sadique a.s. katika Al-Khisal cha Saduq, uk. 323

“Yapo matendo sita ambayo Mwislamu Momiin anaweza kufaidika nayo hata baada ya kufariki kwake:

    1. Kumwacha nyuma mtoto atakaye mwombea maghfira,
    2. Kuacha Mus.-hafu sharifu ambao watu watakuwa wakisoma,
    3. Kuchimba kisima cha maji kitakachokuwa kikiwafaidisha watu,
    4. Mti alioupanda yeye,
    5. Sadaka aliiyoitoa katika kusababisha maji yakatirika vyema,
    6. Ahadith na Sunnah nzuri atakazokuwa ameacha nyuma yake na zikifuatwa na watu.

138. Amesema Mtume s.a.w.w. katika Bihar al- Anwar, j. 76, uk. 126

“Iwapo isingalikuwa vigumu kwa Ummah wangu basi ningalikuwa nimewaamrisha kupiga miswaki kwa kila Sala.”

DHULUMA NA UONEVU

139. Amesema Mtume Muhammad s.a.w.w. katika Thawab-ul-A’amaal, uk. 309

“Siku ya Qiyama, mwitaji ataita:’ Je wako wapi wadhalimu na wasaidizi wao na wale wote waliowatengenezea wino au waliowatengenezea na kuwakazia mifuko yao au waliowapatia wino kwa ajili ya kalamu zao ? Kwa hivyo, wakusanye watu wote hawa pamoja nao !’ “

140. Al-Imam ‘Ali ibn Abi Talib a.s. amesema katika Nahjul-Balagha, uk. 347

“Kwa kiapo cha Allah swt, Iwapo nitapewa umiliki wa nchi sana pamoja na yale yote yaliyomo chini ya mbingu zilizo waz ili nimuasi Allah swt kwa kiasi cha mimi kunyofoa punje moja ya shairi kutoka kwa sisimizi, basi mimi kamwe sitafanya hivyo.”

141. Amesema al-Imam Muhammad al-Baqir a.s. katika Al-Kafi, j.2, uk. 330

“Zipo aina tatu za dhuluma: moja, ni ile ambayo Allah swt anasamehe, pili, ile ambayo Allah swt haisamehe, na tatu ni ile ambayo Allah swt haipuuzii.

Hivyo, dhuluma ambayo Allah swt haisamehe ni ukafiri dhidi ya Allah swt. Na dhambi ambalo Allah swt anaisamehe ni kile mtu anachojifanyia dhidi yake mwenyewe na Allah swt. Lakini dhambi ambalo Allah swt haipuuzii ni ile ambayo inavunja haki za watu. “

Ufafanuzi:

Aina ya tatu ya dhuluma ni ile ambayo mtu hukiuka na kuvunja haki za watu. Njia saheli ya kutaka kusamehewa ni kwanza kumridhisha yule ambaye haki zake zimekiukwa na kuvunjwa. Iwapo mtu huyo atamsamehe yule aliyemvunjia haki zake, basi hapo dhuluma hiyo itageuka kuwa dhuluma dhidi yake binafsi. Na hapo ndipo ataweza kuwa mstahiki wa kuomba msamaha wa Allah swt.

142. Al-Imam ‘Ali ibn Abi Talib a.s. amesema katika Tasnif Ghurarul Hikam, j. 2, uk.36 :

“Dhuluma husababisha miguu kupotoka, inaondoa baraka na kuangamiza umma au taifa.”

143. Al-Imam ‘Ali ibn Abi Talib a.s. amesema katika Nahjul-Balagha, Barua na 53

“Hakuna kitu kinachovutia na kuharakisha kuondolewa kwa neema za Allah swt spokuwa kuendekea kwa dhuluma, kwa sababu Allah swt anazisikiliza dua za madhulumu na huwa yuko tahadhari pamoja na madhalimu.”

Haki za Waislamu wenzako

144. Amesema Mtume Muhammad s.a.w.w. katika Bihar al- Anwar ,j.75, uk. 150 :

“Yeyote yule anayemhuzunisha Mwislamu mwenzake basi kamwe hawezi kumfidia hata kama atamlipa dunia nzima kwani haitatosha (ispokuwa iwapo atatubu na kumfurahisha Mwislamu huyo).”

145. Al-Imam Musa al-Kadhim a.s. amesema katika Bihar al- Anwar j.2, uk.75

“Moja ya faradhi miongoni mwenu kuelekea Mwislamu mwenzenu ni kutokumficha kitu chochote ambacho kinaweza kumfaidisha humu duniani au Aakhera.”

146. Al-Imam Al-Hassan ‘Ali ibn Abi Talib a.s. amesema katika

“Watendee watu vile utakavyopenda wewe kutendewa.”

147. Al-Imam ‘Ali ibn Abi Talib a.s. amesema katika Ghurarul-Hikam, uk.181

“Alla swt humrehemu mtu ambaye anahuisha yaliyo haki na kuangamiza na kuteketeza yale yaliyo batili, au hukanusha dhuluma na kuimarisha uadilifu.”

148. Amesema al-Imam as- Sadique a.s. katika Tuhfatul-Uqul, uk. 277

“Tabia hizi nne ni kutokea tabia za Mtume s.a.w.w. : haki, ukarimu, subira na kuvumilia katika shida, na kusimamia haki ya Mumiin.”

149. Al-Imam ‘Ali ibn Abi Talib a.s. amesema katika Nahjul-Balagha, barua na 53. :

“Kwa hakika ni watu wa kawaida ndio walio nguzo za Din, nguvu ya Waislamu na hifadhi dhidi ya maadui. Hivyo mwelekeo wako daima uwe kuelekea wao na uwanynyekee.”

150. Amesema al-Imam as- Sadique a.s. katika Al-Kafi, j.2, uk. 170

“Allah swt haabudiwi zaidi ya thamani kuliko kutimiza haki ya Mumiin.”

151. Amesema Mtume Muhammad s.a.w.w. katika Bihar al- Anwar, j. 67, uk. 72

“Yeyote yule anayemuudhi Mumiin, basi ameniudhi mimi.”

152. Amesema Mtume Muhammad s.a.w.w. katika Mustadrak al-Was’il, j. 17, uk. 89

“Yeyote yule atakayemdhulumu Muumin mali yak pasi na hakie, basi Allah swt ataendelea kumghadhibikia na wala hatazikubalia matendo yake mema atakayokuwa akiyatenda; na hakuna hata mema moja itakayoandikwa katika hisabu zake nzuri hadi hapo yeye atakapofanya tawba na kuirudisha hiyo mali kwa mwenyewe.”

Salaam -- kusalimiana

153. Amesema Mtume Muhammad s.a.w.w. katika Bihar al- Anwar , j. 76, uk. 4:

“Pale munapokutana miongoni mwenu basi muwe wa kwanza kwa kutoa salaam na kukumbatiana; na munapoachana, muagane kwa kuomeana msamaha.”

154. Al-Imam Hussein ibn ‘Ali ibn Abi Talib a.s. amesema katika Bihar al- Anwar, j. 78, uk. 120

“Thawabu sabini (70 ) ni kwa ajili ya yule ambaye anaanza kutoa salaam na thawabu moja ni kwa ajili ya yule anayeijibu hiyo salaam.”

( Wakati watu wawili wanapoonana, mtanguliaji katika kutoa salaam hupata thawabu zaidi.)

NEEMA NNE ZA ALLAH swt

Ali ibn Abi Talib a.s. amesema kuwa Mtume Muhammad s.a.w.w. amesema kuwa kila asubuhi Mwislamu anatakiwa azikumbuke neema nne za Allah swt. Hofu yangu ni kwamba asipozikumbuka, kuna hatari ya kuzipoteza neema hizo:

Namshukuru Allah swt ambaye amenisaidia kumtambua Yeye na hakuuacha moyo wangu gizani.

Namshukuru Allah swt ambaye ameniweka pamoja na wafuasi wa Mtume Muhammad s.a.w.w.

Namshukuru Allah swt ambaye ameiweka riziki yangu kwake Yeye na si mikononi mwa watu.

Namshukuru Allah swt ambaye amezifunika dhambi zangu na aibu zangu na hakunidhalilisha mbele ya watu.

AHADITH MCHANGANYIKO

1. Amesema Mtume Muhammad s.a.w.w. katika Yanabiul Mawaddah, uk. 584 na 485 :

“Mimi ni mbora wa Manabii na Ali a.s. ni mbora wa Mawasii. Mawasii wangu baada yangu ni kumi na wawili. Wa kwanza wao ni Ali a.s. na wa mwisho wao ni Mahdi a.s.”

2. Allah swt amesema katika Al-Qur’an , Sura al-Ahzab, 33 Ayah 33

‘Allah anataka kukuondoleeni uchafu, enyi watu wa Nyumba (ya Mtume ) na kukutakaseni kabisa kabisa.’

3. Allah swt amesema katika Al-Qur’an , Sura al-Ahzab, 33 Ayah 56

‘Hakika Allah na Malaika Wake wanamteremshia Rehema Mtume, basi enyi Waumini (Waislamu) msalieni Mtume na muombeeni Amani’

4. Amesema Mtume Muhammad s.a.w.w. katika Yanabiul Mawaddah, uk 42,

217 :

“Mimi nawaachia nyinyi Makhalifa wawili; Kitabu cha Allah swt : ni kamba iliyonyoshwa kutoka mbinguni mpaka ardhini, na Jamaa zangu wa Nyumba yangu (Ahlul-Bait a.s.)”

5. Amesema Mtume Muhammad s.a.w.w. katika Yanabiul Mawaddah, uk 30/31

“Mfano wa Ahlul Bait zangu kwenu ni kama mfano wa jahazi ya Nuh a.s. , mwenye kupanda jahazi hiyo ameokoka na mwenye kuiachilia, kapotea.”

6. Amesema Mtume Muhammad s.a.w.w. katika Sahih Muslim, Kitabu Al-

Fadhail, mlango wa Fadhail Ali a.s. kwa kiingereza ni j.4, uk. 1286, Hadith

nambari 5920 :

“….Enyi watu ! …. Ninawaachia nyinyi vizito viwili : Cha kwanza ni Kitabu cha Allah swt chenye uongozi na mwangaza basi shikamaneni na Kitabu cha Allah swt …. Na watu wa Nyumba yangu (Ahlul Bait a.s. )”

7. Amesema Mtume Muhammad s.a.w.w. Musnad Bin Hanbal, j. 4; uk. 437 :

“Hakika Ali ni kiongozi wa kila Mumiin baada yangu.”

8. Amesema Mtume Muhammad s.a.w.w. katika At-Tirmidhi, j.5, uk. 66 Na.3786

“Enyi Watu ! Mimi hakika nimekuacheni vitu viwili navyo ni Kitabu cha Allah swt (Qur’an ) na watu wa ukoo wa Nyumba yangu (Ahlul-Bait a.s.). Mkivichika viwili hivyo milele hamtapotea.”

9. Al-Imam ‘Ali ibn Abi Talib a.s. amesema

“Mkipata neema chache msirudishe kwa uchache wa shukurani.”

10. Allah swt amesema katika Qur’an : Sura Al-Imran, 3 Ayah 179 :

‘Wala usidhani wale waliouawa katika njia ya Allah swt kuwa ni wafu, bali wahai wanaruzukiwa kwa Mola wao.’

11. Al-Imam ‘Ali ibn Abi Talib a.s. amesema :

“Changanyikeni na watu kiasi ambacho kama mkifa watawalilia na mkiishi watatamani kuwa nanyi.”

12. Amesema Mtume Muhammad s.a.w.w. katika Al-Ghadiir :

“Siku ya Ghadiir Khum ni Idi bora mno kwa Ummah wangu.”

13. Allah swt amesema katika Qur’an : Sura Ayah

‘Shikamaneni na kamba ya Allah na wala msifarakane.’

rudi nyuma Yaliyomo