rudi nyuma Yaliyomo endelea

1412.  Allah swt anatuambia katika Qur'an Tukufu, Sura Aali ‘Imran

( 3 ) Ayah ya 159 kuwa: [85]

Hivyo kutokana na Rehema itokayo kwa Allah  kuwa wewe umekuwa mlaini kwao na kama ungalikuwa mkali na mwenye moyo mgumu bila shaka wangalikukimbia. Basi uwasamehe wewe na uwaombe msamaha na ushauriane (kwa kuwaridhisha tu ) nao katika mambo. Na unapoazimia mtegemee Allah, Hakika Allah huwapenda wamtegemeao.

Aya hii tukufu imewateremkia kuhusu wale ambao walikwenda kinyume na amri ya Mtume Muhammad sa.w.w. katika Vita vya Uhud ambapo kulisababisha Waislamu kushindwa.  Watu hao walikuwa ni hamsini na wawili (52) kwa idadi ambao waliwekwa na Mtume s.a.w.w. kulinda pakuingilia huko bondeni na aliwaambia : “ Iwapo sisi tutashinda au kushindwa, nyinyi kamwe musisogee wala kuondoka  hata hatua moja kutoka sehemu hii iliyo nyeti.”

Mbinu hii ya Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. ikiwa pamoja na baraka za Allah swt na moyo wa kujitolea mhanga wa vijana wa Kiislamu wenye imani halisi, iliwafanikisha kuwashinda maadui ambao walikimbia. Wailsamu baada ya maadui kukimbia, walianza kukusanya mali iliyopatikana vitani hapo katika uwanja wa mapigano.

Mara hawa watu hamsini na wawili walipopata habari kuwa Waislamu wameshinda na wanakusanya mali iliyopatikana vitani, wote, isipokuwa kumi na wawili tu, waliacha ngome zao wazi na kukimbilia mali huku wakiwa wamevunja amri ya Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. iliyokuwa imewakataza wasiondoke hapo walipo katika sura yoyote ile ama iwe ya ushindi au kushindwa.  Kwa kuona haya, Khalid ibn Walid, ambaye alikuwa ni kamanda wa jeshi la makafiri, alikwenda hapo bondeni akiwa na jeshi la wapanda farasi mia mbili (200 ) wakiwa wamejiandaa kwa silaha. Makafiri hao waliwashambulia kwa ghafla Waislamu kumi na wawili na kuwaua wote na wakatokezea kwa nyuma kushambulia jeshi la Waislamu. Katika mapigano haya, Mashujaa sabini ( 70 ) wa jeshi la Waislamu waliuawa, akiwemo Hamzah ush-Shuhadaa ( kiongozi wa mashahidi).  Na Mas’ab ibn Umair vile vile wapiganaji wengi walijeruhiwa akiwemo Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. pamoja na Al-Imam ‘Ali ibn Abi Talib a.s.  Kwa hakika kuvunja amri ya Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. kwa hao wachache kulileta maafa makubwa kwa upande wa Waislamu.  Watu walitegemea kuwa Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. atatoa amri kali kabisa dhidi ya hawa wachache; lakini sivyo na badala yake kuliteremka Ayah tukufu ikisema:

1413.  Qur'an Tukufu, Sura Aali ‘Imran ( 3 ), Ayah ya 159,kuwa:

‘…Basi uwasamehe wewe na uwaombe msamaha na ushauriane (kwa kuwaridhisha tu ) nao katika mambo….’

1414. Kwa kuiteremsha Ayah hii, Allah swt alimwamuru Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. atoe msamaha kwa waliokuwa wamekosa.

1415.  Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. amesema:

“Bora ya tendo lililo mbele ya Allah swt ni kusamehe mtu ambaye amekukosea, kuwapenda ndugu na jamaa ambao wameukata uhusiano pamoja nawe, na kuwa mkarimu kwa yule ambaye aliwahi kukunyima. “ Na hapo Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. aliisoma Ayah hii ya Qur’an:

1416.  Qur'an Tukufu, Sura  Al- A’araf  (7) Ayah ya 199,

‘Uchukulie kusamehe na kuamrisha mema na kujiepusha na majaheli’  [86]

1417. Al-Imam ‘Ali ibn Abi Talib a.s. katika mkataba aliokuwa amemwandikia Malik-i-Ashtar, aliandika:

“Zijazeni nyoyo zenu kwa  huruma, uwema na kuwapenda waliochini yenu. Na kamwe musitendee kama wanyama walafi na waroho, kujifanya kama munawalea kwa kuwatenga, kwani wao wapo wa aina mbili: ama wao ni nduguzo katika imani au wapo sawa katika kuumbwa. Wao wanapotoka bila ya kujua na kasoro zinawaghalibu, wanakosa makosa ama kwa makusudi au bila kukusudia.  Kwa hivyo nawe pia uwasamehe  kwa kutegemea naye Allah swt atakusamehe, kwani wewe umekuwa na uwezo dhidi yao, na Yule aliyekuchagua wewe yu juu yako, na Allah swt  yupo juu ya yule aliyekuweka katika wadhifa huu.” [87]

1418.  Amesema al-Imam Muhammad al-Baqir a.s. :

“Kusikitika baada ya kutoa msamaha ni afadhali ya kufurahi baada ya kuadhibu.” [88] 

1419.  Amesema Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. katika  Hadith ‘Arbain, ananakili Marehemu Deilami:

“Siku ya Qiyama, mpiga mbiu atasimama na kusema: ‘Yeyote aliye na malipo yake kwa Allah swt basi asimame.’  Lakini hakuna watakao simama isipokuwa wale tu ambao walikuwa ni wasamehevu.  Anaendelea kusema ‘Je hao hawakusikiaga ahadi iliyokuwa imetolewa na Allah swt :

1420.  Qur'an Tukufu,Surah Ash-Shuura  ( 42 ), Ayah 40, [89]

‘Na malipo ya uovu mfano wa huo. Lakini anayesamehe na kusahihisha; ujira wake uko kwa Allah swt. Hakika Yeye hawapendi wenye kudhulumu.’

1421.  Qur'an Tukufu,Sura An-Nahl (16) Ayah 126,

‘Na mkilipiza, basi lipizeni sawa na vile mlivyoonewa, na kama mkisubiri basi hiyo itakuwa bora kabisa kwa wafanyao subira’.

1422.  Baada ya ufunuo wa Ayah hiyo, Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. alisema : “mimi nitakuwa mwenye subira.” [90]

1423.  Qur'an Tukufu, Surah  Fat-h   (48 ) Ayah 1-2,

‘Bila shaka tumekwishakupa kushinda kuliko dhahiri. Kwamba Allah  alinde kwa ajili yako (dhidi) ya yale yaliyopita kabla ya (wafuasi wako) kasoro zako na yale yanayokuja …’ [91]

1424.  Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. aliisoma Ayah ifuatayo :

Qur'an Tukufu, Surah Bani- Israil (17 ) Ayah 81,

‘ Na sema : ‘Ukweli umefika; na uongo umetoweka; Kwa hakika uongo ndio wenye kutoweka.’ [92]

1425. Vile vile Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. alimsamehe mtumwa wa Kihabeshi, Wahshi, ambaye ndiye aliyekuwa amemwua Bwana Hamza, babake mkubwa wa Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. . Alimsamehe wakati ambapo alikuwa na uwezo kamili wa kumwadhibu na kulipiza kisasi. Kwa hakika hii ndiyo iliyokuwa kanuni ya mtu ambaye alikuwa akiwaambia watu wote kuwa huruma ipo imefungamana katika tabia tatu:

1426. Qur’an tukufu inawatakata Wailsamu waigize tabia na mwnenendo kama Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. na ndiye awe kiigizo chao :

1427.  Qur'an Tukufu, Surah  Ahzab (33 ) Ayah 21,

Kwa hakika mnao mfano mwema kwa Mtume wa Allah, … [93]

Kwa mujibu wa Ayah hiyo, iwapo sisi tutapenda kuwa Waislamu wema, basi itatubidi kuzifuata tabia na mienendo yote ya Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. .

1428.  Amesema al-Imam Muhammad al-Baqir a.s.

“Allah swt hakubakiza chochote kile ambacho waja Wake watakihitaji hadi Siku ya Qiyama, isipokuwa vyote vipo katika kitabu kitakatifu cha Qur’an na ambayo yote yamefikishwa kwa Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w.. Yeye amewekea mipaka kwa kila kitu, na kuweka uthibitisho kwa ajili yake.  Kwa wale watakaopita mipaka yake, Allah swt ameainisha adhabu za kutubu za Kidini.” [94]

1429.  Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. alisema :

“Tofauti baina ya Waislamu na jamii zingine ni kwamba watu wote ni sawa mbele ya Shariah za Allah swt.  Islam haitofautishi baina ya tajiri na masikini, au baina ya mwenye nguvu na mnyonge.  Kwa kiapo cha Allah swt ! Lau Fatima binti ya Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. angalikuwa amefanya uizi, basi Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. angalimkata mkono wake pia.” [95]

AHADITH MCHANGANYIKO

1430.  Amesema Mtume Muhammad s.a.w.w. katika Yanabiul Mawaddah, uk. 584 na  485 :

“Mimi ni mbora wa Manabii na Ali a.s. ni mbora wa Mawasii. Mawasii wangu baada yangu ni kumi na wawili. Wa kwanza wao ni Ali a.s. na wa mwisho wao ni Mahdi a.s.”

1431.  Allah swt amesema katika Qur'an Tukufu , Sura al-Ahzab, 33 Ayah 33,

‘Allah anataka kukuondoleeni uchafu, enyi watu wa Nyumba (ya Mtume ) na kukutakaseni kabisa kabisa.’

1432.  Allah swt amesema katika Qur'an Tukufu , Sura al-Ahzab, 33 Ayah 56,

‘Hakika Allah na Malaika Wake wanamteremshia Rehema Mtume, basi enyi Waumini (Waislamu) msalieni Mtume na muombeeni Amani’

1433. Amesema Mtume Muhammad s.a.w.w. katika  Yanabiul Mawaddah, uk 42, 217 :

“Mimi nawaachia nyinyi Makhalifa wawili; Kitabu cha Allah swt : ni kamba iliyonyoshwa kutoka mbinguni mpaka ardhini, na Jamaa zangu wa Nyumba yangu (Ahlul-Bait a.s.)”

1434. Amesema Mtume Muhammad s.a.w.w. katika Yanabiul Mawaddah, uk 30/31

“Mfano wa Ahlul Bait zangu kwenu ni kama mfano wa jahazi ya Nuh a.s. , mwenye kupanda jahazi hiyo ameokoka na mwenye kuiachilia, kapotea.”

1435.  Amesema Mtume Muhammad s.a.w.w. katika Sahih Muslim, Kitabu Al-Fadhail, mlango wa Fadhail Ali a.s. kwa kiingereza ni : J.4, uk. 1286, Hadith  nambari 5920 :

“….Enyi watu ! …. Ninawaachia nyinyi vizito viwili : Cha kwanza ni Kitabu cha Allah swt chenye uongozi na mwangaza basi shikamaneni na Kitabu cha Allah swt  …. Na watu wa Nyumba yangu (Ahlul Bait a.s. )”

1436.  Amesema Mtume Muhammad s.a.w.w. Musnad Bin Hanbal, j. 4; uk. 437 :

“Hakika Ali ni kiongozi wa kila Mumiin baada yangu.”

1437.  Amesema Mtume Muhammad s.a.w.w. katika

At-Tirmidhi, j.5, uk. 66 Na.3786

“Enyi Watu ! Mimi hakika nimekuacheni vitu viwili navyo ni Kitabu cha Allah swt (Qur’an ) na watu wa ukoo wa Nyumba yangu (Ahlul-Bait a.s.). Mkivichika viwili hivyo milele hamtapotea.”

1438.   Al-Imam ‘Ali ibn Abi Talib a.s. amesema 

“Mkipata neema chache msirudishe kwa uchache wa shukurani.”

1439.  Allah swt amesema katika Qur'an Tukuf, Sura Al-Imran, 3, Ayah 179 :

‘Wala usidhani wale waliouawa katika njia ya Allah swt kuwa ni wafu, bali wahai wanaruzukiwa kwa Mola wao.’

1440.   Al-Imam ‘Ali ibn Abi Talib a.s. amesema :

“Changanyikeni na watu kiasi ambacho kama mkifa watawalilia na mkiishi watatamani kuwa nanyi.”

1441.  Amesema Mtume Muhammad s.a.w.w. katika Al-Ghadiir :

“Siku ya Ghadiir Khum ni Idi bora mno kwa Ummah wangu.”

1442. Allah swt  amesema katika Qur'an Tukufu, Surah…, …., Ayah….,

‘Shikamaneni na kamba ya Allah na wala msifarakane.’

SEMI MCHANGANYIKO

1443.  “Uwe mpole na mwenye huruma kwa wale walioko chini yako au 

       amri yako.”

1444. “Uchukue tahadhari na wala usidanganyike na ving’aavyo.”

1445. “Umwie ndugu yako kwa uwema hata kama ametokezea kwako

kukudhuru. Yeye anapo puuzia au kuukanusha udugu nawe, umwijie kindugu, utokezee awapo katika shida na ujaribu sana ili uweze kumsaidia katika hali hiyo. Awapo mchoyo au bahili kwako na akupuuzapo pale uwapo na mahitaji ya msaada wa kifedha, uwe mkarimu na umsaidie kifedha kwa kiasi uwezacho. Iwapo yeye ni mjuvi na mkatili kwako, basi wewe uwe mpole na umhali yeye. Iwapo anakudhuru, uyakubalie hoja zake. Uishi nae kama kwamba wewe ni mfaidika. Lakini uwe mwangalifu sana kuwa wewe usiwe hivyo kwa wasio stahiki na walio waovu.  

1446. “Usiimarishe urafiki na maadui wa marafiki wako kwani na rafiki yako atakugeuka wewe na kujitokezea mbele yako kama adui pia.”

1447. “Umshauri na kumpatia mawaidha mema na bora sana rafiki yako hata kama yeye hatapendelea hivyo.”

1448. “Uimarishe vyema na kusawazisha hasira, kwa sababu mimi sijawahi kuona  faida yoyote ile iliyo zaidi kuliko kujizuia hivyo.”

1449.  “Usimkorofishe mtu ambaye akufikiriaye wewe kuwa u mzuri na mwema na wala usijaribu kumfanya ajaribu kukugeuka.

1450.  “Usiwe mbaya kwa watu wa nyumbani mwako (mke, watoto na wakutegemeao) na wala usiwe kwao kwa ghadhabu na mkatili yungali hai.”

1451.  “Usimkimbilie yule akupuuzaye.”

1452.  “Kamwe usiwaijie kwa ubaya wale waliokufanyia hisani.”

1453.  “Masikini ni yule ambaye hana marafiki. Yeyote yule akunashaye haki na kujiona kuwa maisha yake yanamzonga na zenye kumtatanisha basi ni mtatanishi.”

1454.  “Uhasiano ulio bora kabisa ni ule kati ya mtu na Allah swt.”

1455.  “Uahirishe matendo yako maovu kwa kipindi kirefu kwani wewe unaweza kuyatenda popote pale utakapo penda (kwa hivyo kwa nini uwe na haraka ya kutenda?)”

1456.       “Uchukue mambo mema kutoka kila tawi la elime kama vile nyuki atafutavyo asali (utamutamu) kutoka kila ua  zuri.

1457.  “Kumbuka kwa chochote kile kilivyo kidogo ambacho umepatiwa na Allah swt  kitakuwa ni chenye manufaa zaidi na huduma zaidi kwako na ni yenye heshima kwa uwingi usio na maana. Uelewe vyema kuwa kiasi chochote kile mtu mwingine atakacho kukupatia ni sehemu mojawapo ya kiasi alichomjaalia Allah swt .”

1458. “Hasara uipatayo wewe kutokana na ukimya wako unaweza kufidiwa kwa urahisi, lakini hasara itakayotokana na kusema kupita kiasi na kusema ovyo itakuwa vigumu kuyarudia. Je hauoni kuwa njia iliyo bora ya kuyalinda maji katika bwawa ni kwa kuufunga mdomo wake ?” 

1459.  “Kulinda na kuhifadhi kile ulichonacho na kilicho chako ni afadhali kuliko kuomba na kutamani vile walivyonavyo wengine.”

1460.  “Marejeo yatokanayo na kazi za mikono au uhodari wa ufundi kwa njia ya heshima na utukufu ingawaje hata kama ikiwa ni kidogo, ni heri ya utajiri ambao wewe unaweza kuupata/kuulimbika kwa kufanya madhambi maovu.”

1461.  “Hakuna mhifadhi bora wa siri zako kuliko wewe mwenyewe.”

1462.   “Kwa mara nyingi mtu anajaribu kila njia kujipatia kitu ambacho ndicho chenye kumletea madhara yeye. Na mara nyingi mtu hujitakia mabaya ya madhara mwenyewe.”

1463.  “Yule aliyenatabia ya kusema sana, ndiye afanyaye makosa mengi.”

1464.  “Yule ambaye huwa na tabia ya kufikiri na kuyadhatiti mambo, huendeleza nguvu zake za kina na fikara na nuru ya macho.”

1465.  “Riziki inayopatikana kwa njia isiyo halali ni njia ovu kabisa ya kupata riziki.”

1466.  “Kwa kujijumuisha pamoja na awatu wema, wewe utaendeleza uwem katika tabia yako na kwa kujiepusha na makundi ya waovu, basi uwema ilivyo bora.”

1467.  “Iwapo huruma au upole wako utatokezea kutendwa kwa ukatili na uonevu basi ukomeshaji na kutilia mkazo mkali ndiyo huruma na uwema ilivyo bora.”

1468.  “Kamwe usitumainie uzushi kwani ndizo rasilimali za wajinga au wapumbavu.”

1469.  “Busara ndilo jina la mkondo wa kukumbuka uzoefu na kuitumia. Uzoefu uliyo bora zaidi ni ule ambao ukupatiao tahadhari iliyo bora na mawaidha yaliyo bora.”

1470.  “Kila mmoja ajaribuaye siye ndiye afanikiwae.”

1471. “Yeyote yule atakaeiaga (kufa) hii dunia, basi ajue kuwa  hatarudipo tena.”

1472.  “Karibuni utakipata kile alichokuidhinishia Allah swt kwa ajili yako.”

1473.  Allah swt Amesema katika Qur'an Tukufu, Surah Az-Zumar, 39 , Ayah 13 - 15 :

“Mimi naogopa adhabu ya siku kama nikimuasi Mola wangu.

Sema: “Namuabudu Allah swt kwa kumuitikadi kuwa yeye tu ndiye Allah swt .”

“Basi nyinyi abuduni mnachopenda kisichokuwa yeye.” (khiari yenu, lakini Allah swt atakulipeni tu); Sema: “Hakika watakao pata hasara ni wale walizotia hasarani nafsi zao na watu wao siku ya Qiyama. Angalieni! Hiyo ndiyo hasara iliyo dhahiri.”

FADHAIL  ZA  IMAM  ALI  a.s.

1474. Kutokea ‘Ala, amesema yeye: “Mimi nilimwuliza ‘Aysha kuhusu ‘Ali ibn Abi Talib. Mimi nilimwuliza Mtume s.a.w.w. kuhusu yeye.  ‘Ayesha alijibu, naye akasema kuwa ‘Ali ni mtu bora kabisa katika Wanadamu, na hakuna mwenye shaka yoyote ile isipokuwa ni mpagani tu.

1475.  Na kutoka ‘Ali ibn Abi Talib a.s., kasema: “Aliniambia Mtume Muhammad s.a.w.w.  ‘Wewe ni bora wa viumbe vya Allah swt, na hakuna mwenye shaka yoyote ile isipokuwa atakuwa ni kafiri’

1476. Na kutoka kwa Hudhaifa: “Alisema  Mtume Muhammad s.a.w.w.  kuwa ‘ ‘Ali ni bora wa Wanaadamu. Yeyote yule anayekataa haya kwa hakika ni kafiri.’

1477.  Kutokea kwa  Imam ‘Ali ibn Abi Talib a.s. alisema: “Alisema Mtume Muhammad s.a.w.w. , ‘uadui, chuki na bughudha dhidi ya ‘Ali ibn Abi Talib ni ukafiri na uadui dhidi ya Bani Hashim ni unafiki.’”

1478.  Na kutokea kwake, kutokea Mtume Muhammad s.a.w.w. akasema: “ Hakuna ampendaye ‘Ali ibn Abi Talib a.s. isipokuwa ni mumiinhalisi, na hakuna amchukiaye ‘Ali isipokuwa ni kafiri.”

1479.  Na kutokea Imam ‘Ali ibn Abi Talib a.s. ,  alisema: “Amesema Mtume Muhammad s.a.w.w.  kuwa yeyote yule atakaye msema vibaya ‘Ali ibn Abi Talib, basi ajue kuwa amenisema mimi vibaya hivyo, na yeyote yule anisemaye mimi vibaya, basi amemsema hivyo Allah swt (na hilo ni dhambi kuu ).”

1480.  Amesema Al-Imam  Ali ibn Abi Talib a.s. kuwa Mtume Muhammad s.a.w.w. amesema: “Kwa hakika Allah swt alitazama kuelekea dunia hii na akanichagua mimi kutoka watu wa dunia; na kwa mara nyingine tena aliangalia duniani na kukuchagua wewe kutoka watu wa dunia; na kwa mara ya tatu alipoangalia akawachagua Maimamu a.s. kutokea vizazi vyako miongoni mwa watu wote wa dunia hii; na kwa mara ya nne alipoangalia akamchagua binti yangu Fatimah kutokea wanawake wote wa dunia hii.”

1481.  Kutokea Ja’abir, anasema kuwa  Mtume Muhammad s.a.w.w. amesema: “ Ali ibn Abi Talib a.s. ni bora miongoni mwa watu wa dunia. Yeyote yule aliye na shaka, basi ni kafiri.”

1482. Amesema Ibn ‘Abbas kuwa Mtume Muhammad s.a.w.w. amesema: “ ‘Ali ibn Abi Talib a.s. ni mlango wa Hitta [96]   Yeyote yule atakayeingia ndani mwake basi kwa hakika ndiye mumiin wa kweli, na yeyote atakayetoka kutoka humo ni kafiri.”

1483. Al-Imam Muhammad al-Baquir a.s. kutokea baba yake amesema kuwa Mtume Muhammad s.a.w.w.  aliulizwa kuhusu hali ya watu, naye akajibu “ bora kabisa na Mcha Mungu halisi na ambaye aliye karibu kabisa nao ambay yuko karibu nami ni Ali ibn Abi Talib a.s. , na hakuna Mcha-Mungu halisi miongoni mwenu, na ambaye yupo karibu nami kuliko Ali ibn Abi Talib a.s.”

1484.  Jami’ bin ‘Omair, alisema kuwa yeye alimwuliza ‘Ayesha kuhusu daraja la ‘Ali ibn Abi Talib a.s. mbele ya Mtume Muhammad s.a.w.w. ?  Yeye alijibu: “ Kwa hakika ni mtu mwenye kuheshimiwa mno mbele ya Mtume Muhammad s.a.w.w.”

Yeye alimwuliza tena kuhusu nafasi ya Ali ibn Abi Talib a.s. katika macho ya Mtume Muhammad s.a.w.w. . Alijibiwa kuwa “Ni mtu mwenye kuheshimiwa mno mbele ya Mtume Muhammad s.a.w.w. .”

1485.  Na kutokea Ibn ‘Umar amesema kuwa Mtume Muhammad s.a.w.w. amesema : “Bora wa mtu miongoni  mwenu ni ‘Ali ibn Abi Talib a.s.  na bora wa vijana wenu ni  Al - Hassan na Al -Husayn

1486.  ‘Urwah anaripoti kutoka ‘Ayesha kuwa: Amesema Mtume Muhammad s.a.w.w. “Kwa hakika nimeahidiwa na Allah swt kuwa yeyote yule atakayeinuka dhidi ya ‘Ali ibn Abi Talib a.s. basi kwa hakika ni kafiri na kwa hakika ataingia Jahannamaunguzwe na moto.  ‘Aisha  akasema kuwa “Mimi niliisahau hadith hii siku ya (vita vya) Jamal, hadi hapo nilipoikumbuka au nilipokumbushwa tukiwa Basra (Iraq), nami namwomba Allah swt anisamehe, na sitegemei kuwa miongoni mwao.”

1487.  Abu Salim bin Abu al-Jaada amesema kuwa yeye alimwomba Ja’abir azungumze chochote kuhusu ‘Ali ibn Abi Talib a.s. .  Ja’abir kasema: “’Ali ibn Abi Talib a.s. alikuwa bora miongoni mwa wanadamu.”  Mimi nilimwuliza tena “Je unasemaje kuhusu mtu atakayemchukia ‘Ali ibn Abi Talib a.s.”  Yeye alinijibu: “Hakuna atakayemchukia ‘Ali ibn Abi Talib a.s. isipokuwa kafiri.”

1488.  Hashim bin Barid alisema kuwa ‘Abdullah ibn Mas’ud alisema : “Mimi nilijifunza Sura 70 za Qur’an Tukufu kutokea kinywani mwa Mtume Muhammad s.a.w.w.  na Surah za Qur’an zilizobakia nilijifunza kutokea mbora wa Ummah wetu yaani Ali ibn Abi Talib a.s.”

1489.  Muhammad bin Salim al-Bazzar anasema kuwa yeye alikuwa pamoja na Said bin al-Musayyib katika  Masjid-i-Nabi, siku ya Ijumaa, ndipo alipotokezea mhubiri kutoka kabila la Banu Omayyah  (laana za Allah swt ziwafikie juu yao )  na akapanda juu ya mimbarna akaanza kumtusi Ali ibn Abi Talib a.s.  kwa kusema: “Kwa hakika, Allah swt hakumtukuza Ali ibn Abi Talib a.s. kwa mapenzi yake ba dala yake amefanya hivyo kwa kuhofu uchochezi wake.” Kwa hayo Said bin Al-Musayyib alimlaani na kumwambia: “Kwa hakika wewe unasema uongo mtupu” [97]  Na hapo alimtupia nguo aliyokuwa akijifunika juu ya mdomo wa mhubiri huyo. Hapo watu walipomwambia kuwa itakuwaje iwapo Abu Muhammad wakati Imam huyo anatokana na Banu Omayyah ?  Hapo Said alijibu: “Kwa kiapo cha Allah swt ! Mimi sijui nilichokisema, lakini mimi nilimsikia Mtume Muhammad s.a.w.w. akisema haya kutokea makbara haya nami ndipo nilipoyarudia kuyasema.”

1490. Ummi Hani binti Abu Talib a.s. kasema kuwa Mtume Muhammad s.a.w.w. kasema kuwa: “Bora wa viumbe vya Allah swt  katika mtazamo wake Allah swt, ni yule anayelala kaburini mwake na kamwe hakumshuku 'Ali ibn Abi Talib a.s.  na kizazi chake ni bora wa vizazi katika viumbe vyote.”

1491.  Ja’abir anasema kuwa “Hakuna anayeshuku fadhail za ‘Ali ibn Abi Talib a.s.  isipokuwa ni kafiri na kasema kuwa “Kwa kiapo cha Allah swt sisi kamwe tulikuwa hatuwajui wanafiki, katika zama za Mtume Muhammad s.a.w.w.  isipokuwa kwa yule mwenye chuki dhidi ya ‘Ali ibn Abi Talib a.s.”

1492.  Said bin Ja’abir alise kuwa yeye alikuwa akimwongoza Ibn ‘Abbas baada ya yeye kupoteza nuru ya macho yake, kutokea Msikitini, na aliwapita kundi la watu waliokuwa wakimtukana ‘Ali ibn Abi Talib a.s.  na aliniambia kuwa nimchukue hapo.

Hivyo mimi nilimfikisha kwao.  Kufika hapo alisema “Ni nani miongoni mwenu anayemkashifu Allah swt ?! Kwa hakika yeyote yule anayemkashifu Allah swt  amekuwa kafiri. Na ni yupi yule anayemkashifu ‘Ali ibn Abi Talib a.s. ?  Na kwa hakika hili limetokea” akasema.  Ndipo alipoendelea kusema: “Nashuhudia Allah swt, kwa kiapo cha Allah swt, mimi nilimsikia Mtume Muhammad s.a.w.w. akisema ‘Yeyote yule anayemkashifu ‘Ali ibn Abi Talib a.s. basi amenikashifu mimi  na kwa hakika anayenikashifu mimi basi ajue kuwa amemkashifu  Allah swt na yule anayemkashifu Allah swt, Mtume wake basi watatakiwa kutoa maelezo yake.” Na hapo ndipo  Ibn ‘Abbas aligeuka.

1493.  Amesema Mtume Muhammad s.a.w.w. : “Muzirembeshe vikao vyenu kwa mazungumzo na makumbusho ya ‘Ali ibn Abi Talib a.s.  kwa dhikr ya ni dhikr zangu na dhikrzangu ndizo dhikr za Allah swt na dhikr za Allah swt ni ‘ibadah. Na mwenye kufanya ‘ibadah huingia Peponi.”

MAADILI YA ISLAM:

Nafs  aina na sifa zake

Masomo ya akhlaq- maadili katika Islam ni mojawapo ya bora ya sayansi na inamwelekeza asomaye hadi katika elimu ya kujielewa nafsi yake mwenyeweambayo Islam inaamini kuwa ni faradhi. Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. amesema: “Yeyote yule aliyeitambua nafsi yake (mwenyewe) basi kwa hakika ametambua Allah.”

Hivyo hivyo kuna mapokezi mengi ya habari kuhusu umuhimu wa somo hili hata Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. amebainisha kuwa: “Mimi nimetumwa kuja kukamilisha maadili.

Tuanze kuzichambua aina za nafsi alizonazo mwanadamu vile alivyo:

Hapana shaka kuwa mwanadamu hana nafs zaidi ya moja, lakini hii nafsi au  inayo masharti fulani fulani. Kwa hiyo, hali ya kuonyesha kama ‘nafsi ya kujilaumu’ ‘au nafsi ya kuamrisha’ ‘nafsi inayotosheka’ (kama vile vielezwavyo katika Qu’rani), na hivyo haidhihirishi idadi ya nafsi. Upande mwingine, yote haya ni miongoni mwa ngazi za sifa ambazo zinaleta kwa ukamilifu na ustawi wa hali ya nafsi, pamoja na yale yanayoozesha nafsi na kuleta maovu.

1494.  NAFSI SAFI AU THABITI (Thabit.)

Katika Qur’an Tukufu, Surah Ash Shua’raa, 26, Ayah 89, aina mbili hizo za masharti za nafsi zinaelezwa:-

“Isipokuwa mwenye kuja kwa Allah swt na moyo safi”

Uhalisi huu ni aina ya moyo, na moyo halisi (safi) ni ule ambao haufungamani na upande wa kuhangaika wala upande ule wa wapotofu.

Imenakiliwa kutoka kwa Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. kuwa: “Moyo ulio msafi- halisi ni ule  ambamo hakuna chochote kile isipokuwa Allah swt  tu”

Katika hali hii, Nafsi imetunukiwa hatua mojawapo ya umuhimu kuwa kamilifu. Hivyo inamaanisha kuwa hakutakuwa na mapenzi mbali na ile ya Allah swt tu.

Kuna habari nyigine iliyonakiliwa kutoka kwa Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. ambamo twaambiwa:

“Imani ya mtu haitokamilika hadi hapo mimi niwe mpenzi wake kuliko hata baba, mama, watoto wake, mali yake na hata kuliko maisha yake.”

Ndivyo hivyo, nafsi safi ni nafsi ambamo hakuna mapendo mengine yoyote yale isipokuwa Allah swt  na wale wapendwao kwa ajili ya Allah swt (Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w.  na Ahali yake a.s.)

1495.  NAFSI YENYE KUTUBU (al-Nafs al- Muniib).

Sharti lingine la moyo au Nafsi ni kutubu na hivyo huitwa moyo wenye kutubu au nafsi yenye kutubu. Hivyo huwa daima inarudi kwa Allah swt, Qur’an Tukufu, Surah Qaaf, 50, Ayah 33:

“Anayemuogopa ( Allah swt Mwingi wa kurehemu), na hali ya kuwa humuoni na akaja kwa moyo ulioelekea ( kwa Allah swt).”

Kuwa na khofu ya Allah swt pale mtu awapo peke yake ni mojawapo ya masharti bora ya nafsi, na hii ina maanisha kuwa nafsi imemtambua Allah swt kiasi kile kuwa hakutakuwa na tofauti yoyote itakapokuwa pekee yake au katika kundi la watu. Hata kama hakutakuwa na mtu yeyote karibu nayo, basi ile khofu ya Allah swt imo ndani yake thabiti.

Hii haipo katika kundi la zile nafsizilizo ghafilika katika maasi na matendo maovu wakiwa katika kundi la watu au wakati wengine watakapokuja julishwa, na hawatajizuia nayo na hata kama iwapo watakapopewa habari zilizo bainika. Hii ni ile aina ya nafsi ambayo haielewi kuwa Allah swt yupo anaangalia yote na Aliye dhahiri popote pale na kwa hakika aina hii ya nafsi haipo pamoja na Allah swt na wala haitorudi kamwe kwa Allah swt.

1496.  NAFSI MWONGOZI (al- Nafs al- Muhtadi).

Sharti lingine la nafsi ni ile iongozwayo. Qur’an Tukufu, Surah Attaghaabun, 64, Ayah 11,inatuambia:

“Haufiki msiba wowote ila kwa idhini ya Allah swt. Na anayemuamini Allah swt huuongoza moyo wake. Na Allah swt ni Mjuzi wa kila kitu.”

Mtu ambaye moyo wake ukiwa umeongozwa na kujitosa katika habari ya imani na sheria Tukufu za Allah swt, yeye anaielewa njia yake vyema kabisa. Zile imani atakazokubalia na matendo yake yampasa kuyatenda huwa ni dhahiri kwake kuelewa vyote hivyo kwa uadilifu.

1497.  NAFSI ILIYO RIDHIKA (al-Nafs al- Mutmai’na)

Sharti lingine lijulikanalo vyema la moyo au nafsi ni kuridhika. Amesema Allah swt katika Qur’an Tukufu, Surah Ar-Raa’d, 13, Ayah 28

“ Sikiliza: Kwa kumkumbuka Allah swt nyoyo hutulia.”

Na vile vile mwishoni mwa Qur’an Tukufu, Surah al-Fajr, 89, Ayah 28,twaambiwa:

“Ewe nafsi yenye kutua”!

“Rudi kwa Mola wako, hali ya utaridhika na umemridhisha.”

Nafsi iliyo ridhika ni ile iliyokwisha ridhika, ina maanisha kuwa mtu yupo anapigana vita vikali na matakwa yake na kwa kuyatimiza yale yaliyo fardhi kwake katika dini na kujiepusha na yale yaliyoharamishwa, na anajipa umuhimu kwa kuelimisha na kuikamilisha nafsi yake hadi hapo yeye hapindukii kutii chochote kile isipokuwa Allah swt tu. Ni marufuku kwake kuelekea pale penye madhambi na huwa ni mwenye kupenda amani na utulivu na huwa ni mwenye kujiridhikia mwenyewe hadi hapo yeye huwa thabiti kama jabali madhubuti. Hakuna madhambi, matakwa ya ubinafsi, tamaa, mvutano wa dunia, mapenzi ya mali au cheo yatakayoweza kuja kumpotosha yeye na kumwelekeze pengine na vile vile hakuna sheitani atakayeweza kumghalibu na kumpotosha yeye.

Hali ya juu kabisa ya sharti hili kama ilivyokuwa katika Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. na ma - Imamu a.s. waliokuwa halisi kuwa hata mawazo ya kutaka kutenda madhambi hayakutokea kamwe.

1498.  NAFSI YA TAHADHARI YA UADILIFU (al-nafs Al

Muttaqi ):

Sifa nyigine ya nafsi inajulikana kama uangalifu wa uadilifu wa nafsi, nafsi ambayo imejaa kwa khofu na tahadhari. Hali hiyo inatokana na nyakati fulani kwa kupotoshwa na (kwa akili na ) huzungukwa na uchafu na ubovu ili nafsi iingie sharti sawa sawa na itahadharishwe na madhambi. Nafsi ikiwa katika hali  hiyo huitwa nafsi ya tahadhari ya uadilifu.

Qur’an Tukufu, Surah Al Hajj, 22, Ayah 32 :

“Ndio hivyo! Na anayetukuza ibada za Allah swt, anayezihishimu alama za (dini ya ) Allah swt, basi hili ni jambo la katika utawala wa nyoyo.”

Kwa mtu yule ambaye imani yake inafikia kiwango hiki cha Taqwa kiwango cha tahadhari ya uadilifu, huheshimu na kumthamini Allah swt na yale yote yaliyotolewa ishara nae kama Dini, Msikiti, shariah, waumini wake, Makkah, Al-Ka’abah Tukufu n.k. Kwa ufupi chochote kile kinachohusika na Allah swt huwa kina kuwa na umuhimu na

ta‘adhima kubwa kwa mtu kama huyu wa namna hii. Na hii ndiyo kwa hakika matokeo ya  taqwa

rudi nyuma Yaliyomo endelea