rudi nyuma Yaliyomo endelea

“Hali yoyote katika hizi na vyovyote vile ambavyo mwanamme humwaga maji yake, inachukuliwa kuwa ni zinaa (na imeharamishwa).”

894.            Amesema Mtume Muhammad  Mustafa s.a.w.w., Al-Kafi,

J. 2, Uk. 270:

“Amelaaniwa! Amelaaniwa yule mtu ambaye anafanya tendo la kuwaingilia wanyama.”

895.            Amesema Mtume Muhammad  Mustafa s.a.w.w., Kanz-ul-

'Ummal, J. 5, Uk. 316 ;

“(Zinaa miongoni mwa jamii moja) mwanamme kwa mwanamme au mwanamke kwa mwanamke (ni zinaa).”

ULAWITI.

896.  Amesema al-Imam as- Sadique a.s. katika Al-Kafi :

“Kuingiza (uume) mwanzoni mwa nafasi ya haja kubwa ni dhambi kubwa kabisa hata kuliko kuingizia katika sehemu ya mbele ya siri ya mwanamke. Kwa hakika Allah swt ameangamiza ummah mzima wa Mtume Lut[67] a.s. kwa sababu wao walijiingiza katika laana ya ulawiti. Allah swt kamwe hakumteketeza hata mtu mmoja kwa dhambi za zinaa.”

897.  Amesema Mtume Muhammad s.a.w.w. ,Wasa’il al-Shiah :

“Mtu yeyote anayetenda ulawiti pamoja na kijana wa kiume atapatwa na janabah (uchafu) ambao hautaweza kutakasishwa hata kwa maji ya dunia nzima. Allah swt atamghadhabikia na kumlaani vikali. (Yaani Allah swt atazichukua rehema na baraka kutoka kwake na kumlipa Motoni i.e. Jahannam). Kwa hakika ni mahala pabaya kabisa !  Pepo (Jannah) zitakuwa zimemkasirikia mno. Na mtu ambaye anakubali kulawitiwa kwa nyuma, basi Allah swt  humweka ukingoni mwa Jahannam (motoni penye moto mkali kabisa) na atamweka huko hadi hapo atakapo maliza kuwahoji watu wote. Hapo ndipo atakapo mwamrisha kuwekwa Motoni. Atapitia adhabu moja baada ya pili hadi kuzimaliza adhabu zote za Jahannam na hadi atakapofikia daraja la chini kabisa. Na kamwe hataweza kutoka hapo.”

898.  Al-Imam ‘Ali ibn Abi Talib a.s. amesema katika Al-Kafi

“Ulawiti ni moja ya Madhambi Makuu na inaadhibu pale mtu mmoja anapompanda mtu  bila ya kumwingilia. Na iwapo atamwingilia kwa nyuma basi hiyo itakuwa ni kufr (ukafiri).”

899.  Hudhaifa ibn Mansur anasema :

“Mimi nilimwuliza  al-Imam as- Sadique a.s. kuhusu Dhambi Kuu.

900.  Amesema al-Imam as- Sadique a.s. katika Wasa’il al-Shiah :

“Kubana kwa sehemu za kiume baina ya mapaja mawili kwa njia isiyoruhusiwa.”

901.  Nikamwuliza tena,

“Je ni mtu gani anayetenda dhambi la ulawiti ?”

902.  Al-Imam as- Sadique a.s. alinijibu :

“Yule ambaye amekufuru kwa Allah swt kwa yale aliyoteremshiwa Mtume Muhammad s.a.w.w. (Qur’an tukufu ).”

903.  Amesema Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. kwa kumjibu Abu Basir kuhusu Qur’an Tukufu, Surah Hud, 11, Ayah 82, isemayo :

‘Basi ilipofika amri yetu, Sisi tuliibinua (mji) juu chinii, na kuwateremshia mvua ya mawe magumu ya udongo uliopikwa, tabaka juu ya tabaka.’

904.  Al-Imam as- Sadique a.s. alimjibu:

“Yupo mtu ambaye anaiaga hii dunia huku akisadiki kuwa ulawiti ni halali, lakini Allah swt anampiga kwa jiwe moja ambalo liliwadondokea watu wa Mtume Lut a.s.[68]

Walivyoadhibiwa Umma wa Mtume Lut a.s.

905. Qur’an tukufu imeelezea aina tatu za adhabu zilizoteremshiwa umma wa Mtume Lut a.s. .

906.  Baada ya kutaja adhabu hiyo ya tatu, imeelezwa katika Sura Hud, 11 : 83 

‘(Mawe hayo ya udongo uliopikwa) yalikuwa yametiwa alama (za adhabu) za Mola wako; Na wala haipo (maangamizo ya miji) mbali kutoka wadhalimu (wengine kama hawa watu wa umma huu wanaofanya machafu haya)’

907.  Imam ‘Ali ar-Ridha a.s. amesema : katika  Fiqh-i-Ridha

“Jiepusheni na ulawiti na zinaa, na huu ulawiti ni chafu na mbaya kabisa  kuliko zinaa. Madhambi haya mawili ndiyo vyanzo vya mabaya sabini na mbili ya humu duniani na Aakhera.”

908.  Qur’an tukufu imetumia neno ‘utovu wa adabu, uchafu’ kwa ajili ya zinaa kwa njia ambayo imetumika vile vile kwa ajili ya ulawiti. Twaambiwa katika Surah A’araf, 7, : Ayah 80 - 81

‘Na (Sisi tulimpeleka) Lut, wakati alipowaambia watu wake:”Je ! Mwatenda jambo chafu ambalo halikutendwa na yeyote kabla yenu katika ulimwengu.’

“Nyinyi mnawaendea wanaume kwa hamu (ya kufanyiana uchimvi) badala ya wanawake; Ama nyinyi ni watu wafujaji.’

909.  Kumtazama kijana mdogo wa kiume kwa macho ya ashiki au uzinifu ni Haraam kabisa, hususan kijana ambaye bado hajaota nywele za usoni mwake. Madhara na adhabu za mtazamo wa ashiki au uzinifu vinazungumziwa kwa mapana na marefu katika maudhui yanayozungumzia zanaa.  Vile vile Mtume Amesema Mtume Muhammad s.a.w.w. katika Wasa’il al-Shiah

“Jiepusheni na kuwatazama kwa macho ya ashiki au uzinifu vijana wa matajiri na watumwa, hususan wale ambao hawajaota hata ndevu. Kwa sababu uchokozi unaofanywa kwa mitazamo ya aina hiyo ni mbaya kabisa kuliko uchokozi wa kuwatazama hivyo wasichana wadogo walio katika hijabu.”

910.  Ni haraam kumbusu kijana wa kiume kwa kuashiki.  Amesema al-Imam as- Sadique a.s. katika  Al-Kafi kwa kumnakili Mtume Muhammad s.a.w.w. :

“Iwapo mtu atambusu kijana wa kiume kwa kuwa ashiki, basi Siku ya Hukumu (Siku ya Qiyama) , Allah swt atamfunga mdomoni mwa mtu huyo hatamu ya moto.”

911.  Al-Imam ar-Ridha a.s. amesema katika Fiqh-i-Ridha :

“Wakati mtu anapombusu kijana wa kiume kwa kuwa ashiki (mapenzi au nyege) basi Malaika wa mbinguni na Malaika ardhini , Malaika wa Rehema na Malaika wa adhabu  wote kwa pamoja humlaani huyo mtu. Na allah swt humtolea hukumu yake kwenda Motoni (Jahannam). Loh ! mahala pakutisha mno.”

912.  Amesema Mtume Muhammad s.a.w.w. katika Mustadrakul

     Wasail:

“Allah swt atamwadhibu Motoni (Jahannam) kwa maelfu ya miaka mtu ambaye anambusu kijana wa kiume kwa ashiki au matamanio ya mapenzi.”

913.  Wanazuoni wanasema kuwa wanaume wawili kulala pamoja chini ya blanketi au shuka moja bila mavazi kunawapa adhabu kwa mujibu wa Sharia za Kiislamu, navyo pia ni miongoni mwa madhambi makuu.

914.  Amesema Mtume Muhammad s.a.w.w. ,Wasa’il al-Shiah :

“Tengenezeni vitanda vya kulalia tofauti  kwa ajili ya watoto wenu wanaozidi umri wa miaka kumi. Ndugu wawili wa kiume au ndugu wawili wasichana au ndugu na dada yake wasilazwe pamoja katika kitanda kimoja."

915.  Kwa mujibu wa Al-Imam ‘Ali ibn Abi Talib a.s.,

“Mtu aliyetenda dhambi kama hili, mwili wake uchomwe moto hata baada ya kuuawa kwa njia nyingine. Yaani akishauawa kwa adhabu atakayoiamua Qadhi, basi baada ya kuuawa mwili wake uchomwe moto.

916. Tunakuleteeni hadith ya Al-Imam ‘Ali ibn Abi Talib a.s. aliyoisema :

“Mtu yeyote anayestahili kuuawa mara mbili kwa kupigwa mawe basi huyo ni mlawiti.”

917. Ni lazima ujilikane wazi wazi kuwa mwanamme yeyote anayemlawiti kijana wa kiume (anamwingilia sehemu za haja kubwa), basi wafuatao watakuwa wame haramishwa kwake :

918.  Imam Jaafer Sadiq a.s. amesema:

 "Allah swt ameweka adhabu sita kwa wale watendao zinaa xe "zinaa "ambapo adhabu za aina tatu wanazipata humu humu duniani na zinazobakia hizo tatu wanazipata huko Akhera. 

Adhabu hizo zilizowekewa humu duniani ni:-

·  Wanapoteza nuru 

·  Wanakuwa maskini

Maisha yao yanakuwa mafupi.

Adhabu tatu zilizowekewa Akhera ni:-

·  Allah swt atakuwa amewakasirikia mno

·  Watahesabiwa siku ya Qiyama xe "Qiyama "kwa Sharia kali

·  Wataishi milele Jahannam.

919.  Mtume Mtukufu s.a.w.w. amesema:

"Manukatoxe "Manukato" ya Jannat yataweza kusikika hadi umbali wa miaka. Hata hivyo yule mtoto ambaye amekanushwa na wazazi yaani wazazi wamesema sio mtoto wao tena, na mtu yule ambaye haonyeshi huruma kwa jamaa zake na yule mtu mzee anafanya zinaa, hao ndio watu hawataweza kusikia manukato ya Jannat."

(2413) Iwapo mwanamme aliyebaleghe atafanya Ulawiti xe "Ulawiti "na kijana wa kiume, basi mama, dada na binti wa mtoto huyo atakuwa haramu kwa ajili yake. Na Sharia kama hii itatumika wakati ambapo mtu ambaye amelawitiwa xe "amelawitiwa "ni mwanamme mtu mzima, au wakati mtu anayelawiti xe "anayelawiti "ni kijana ambaye hajabaleghexe "baleghe".  Lakini iwapo mtu atakuwa na shaka iwapo kikofia cha uume wa mwanamme  xe "uume wa mwanamme  "umeingia katika sehemu za haja kubwa au haikuingia, basi katika sura hiyo mwanamke katika kikundi cha hapo juu hawatakuwa haramu kwa ajili yake.

(2414) Iwapo mwanamme atamuoa mama xe "mama "au dada xe "dada "wa kijana mvulana, na akamlawiti huyo mvulana baada ya ndoa kwa misingi ya tahadhari hao watakuwa ni haramu kwa ajili yake.

       

USAFI KATIKA ISLAM.

920.            Amesema Mtume Muhammad  Mustafa s.a.w.w., Al-Ithna-

'Asheriyyah, Uk. 92:

“Kuna mema matatu ambayo Allah swt huyapenda katika watu:

Ufupi katika uzungumzaji,

usingizi mfupi, na

 ulaji mdogo;

Na mambo matatu ambayo hayamfurahishi Allah swt:

Kuzungumza kupita kiasi

Kulala kupita kiasi, na

 Kula kupita kiasi.”

921.            Mtume Muhammad  Mustafa s.a.w.w. Amesema, Kanz-ul-

'Ummal, Hadithi no. 26002:

“Jaribuni kuwa wasafi kila muwezavyo. Kwa hakika Allah swt ameweka misingi ya Islam juu ya usafi; hivyo kamwe mtu mchafu hawezi kuingia Jannat mpaka awe msafi.”

922.     Al Imam Amiril Muuminin 'Ali ibn Abi Talib a.s., AmesemaGhurar-ul-Hikam, Uk. 356:

“Kula kupita kiasi kunasababisha wingi wa magonjwa.”

923.            Amesema Al Imam Musa al-Kadhim a.s., Khisal-i-Sadduq,

Uk. 125:

“Zipo Sunnah tano kuhusu kichwa na tano zingine kuhusu mwili.

Sunnah tano zinazohusiana na kichwa ni:

Kuosha mdomo,

kunyoa mashurubu,

kuchana nywele,

kupitisha maji kupita mdomo na

pua.

Sunnah tano zinazohusiana na mwili ni:

Kukaa jando,

kunyoa nywele za sehemu za siri,

kunyoa nywele kwenye mabega,

kupunguza na kukata makucha, na

 kusafisha na kuosha sehemu za siri (kwa maji au kwa karatasi, kwa kitambaa, au chochote kile kinachoweza kukufaa n.k.)”

924.     Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. alimwambia Al Imam Hasan

ibn ‘Ali ibn Abi Talib a.s., Wasa'il  ush-Shi'ah, J. 24, Uk. 245:

“Je nikufundishe mema manne ambayo hautahitaji dawa ya matibabu ya aina yoyote ?

“Naam” alijibu Al Imam Hasan ibn ‘Ali ibn Abi Talib a.s. 

Kwa hayo Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. alimjibu:

Usikae kula chakula hadi uwe una njaa;

Na usiondoke juu ya meza ya chakula bila ya kubakiza njaa kidogo;

Tafuna chakula chako vyema mdomoni mwako;

Na unapotaka kwenda kulala, uende ukajisaidie haja.

Iwapo utatekeleza haya basi kamwe hautahitaji matibabu ya aina yoyote.”

BIASHARA NA UHUSIANO WA KIJAMII.

925.            Mtume Muhammad  Mustafa s.a.w.w., Amesema Bihar al-

Anwaar, J. 103, Uk. 89:

“Iwapo mtu atanunua mali ambayo katika vyakula ambacho ni muhimu katika jamii na akakificha kwa siku arobaini kwa matumaini kuwa bei yake itapanda miongoni mwa Waislam, na kama atafanikiwa kukiuza kwa bei ya juu hicho chakula basi kama fedha zote atazigawa katika sadaka kwa na wenye kuhitaji misaada maskini, basi hiyo haitapunguza adhabu yoyote mbele ya Allah swt kwa kile alicho kitenda (kuhujumu uchumi).”

926.     Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s., amesema Bihar al-Anwaar,

J. 103, Uk. 93:

“Yeyote yule anayefanya biashara bila ya kuzingatia sheria na kanuni za Islam, basi kwa hakika ataingia katika riba, (bila ya yeyemwenyewe kujijua).”

 

927.     Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. ananakili kutoka Mtume

Muhammad  Mustafa s.a.w.w.  kuwa Amesema, Khisal-i-Sadduq,

J. 1, Uk. 286:

“Yeyote yule aliye katika biashara na anayenunua na kuuza vitu lazima ajiepushe mambo matano, ama sivyo asinunue wala asiuze kitu chochote:

Riba,

Kula kiapo,

Kuficha ubaya na kasoro za mali,

Kusifu kitu kama hakistahili hivyo wakati wa kuuza; na

kutafuta kasoro au ubaya wakati wa kununua.[69]

928. Al Imam Muhammad al-Baquir a.s. Amesema, Al-Kafi, J. 5,

Uk. 78:

“Yeyote yule anayetafuta riziki humu duniani ili aondokane na shida za kutegemea watu katika mahitaji yake, na ili kuwalisha na kuwasaidia wananyumba wake, na kueneza mapenzi yake kwa majirani zake basi atakutana na Allah swt siku ya Qiyamah huku uso wake ukiwa uking’ara kama mwezi.”

KUGHUSHI KATIKA BIASHARA.

929.            Mtume Muhammad  Mustafa s.a.w.w., amesema Safinat-ul-

Bihar, J. 2, Uk. 318:

“Yeyote yule anaye lala huku akiwa amepanga njama dhidi ya Muislam mwenzake moyoni mwake, basi amelala katika adhabu za Allah swt, na atabakia katika hali hiyo hadi pale afanye Tawba.”

930.            Mtume Muhammad  Mustafa s.a.w.w. Amesema, Wasa'il ush-

Shi'ah, J. 17, Uk. 283:

“Na yeyote yule anayemlaghai ndugu yake Mwislam, basi Allah swt humwondoshea riziki kwa wingi na huharibu maisha yake na kumwachia katika hali yake mwenyewe.[70]

931.            Amesema Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s., At-Tahdhib, J. 7,

Uk. 13:

“Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. ameharamisha kuchanganywa kwa maji katika maziwa wakati wa kuuza.”

932.     Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. Amesema,

“Yeyote yule anayewaghushi Waislam kwa ujumla basi huyo hayupo nasi.”

933.            Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w., amesema Bihar al-

Anwaar, J. 103, Uk. 80:

“Mtu yeyote anaye walaghai Waislam wenzake katika kununua au kuuza kitu chochote, hayupo miongoni mwetu, na siku ya Qiyamah atainuliwa akiwa miongoni mwa Wayahudi, kwa sababu wao wamekuwa daima wakiwadanganya na kuwaghushia Waislam.”

MATAMANIO NA TAMAA ZISIZO HALALI.

934.            Mtume Muhammad  Mustafa s.a.w.w., amesema Al-Kafi,

J. 2, Uk. 79:

“Baada yangu mimi, ninawahofia umma wangu katika vitu vitatu:

Upotofu baada ya kuelimika,

 matamanio yanayo potosha na

Tamaa ya tumbo na sehemu za siri.”

935.     Al Imam Muhammad al-Baquir a.s., amesema Al-Kafi, J. 2,

Uk. 80:

“Hakuna ‘ibada ya Allah swt iliyo na thamani zaidi kuliko usafi, uhalisi wa tumbo la mtu na sehemu zake za siri kutokana na matamanio au tamaa.”

936.            Mtume Muhammad  Mustafa s.a.w.w. Amesema, Makarim-ul- Akhlaq, 429 :

“Kwa mtu ambaye anakuwa na matamanio na maovu yanapokuwa daima yako tayari na yeye anayaepukana nayo kwa sababu ya hofu ya Allah swt,  basi Allah swt atamharamishia moto wa Jahannam na atamhakikishia kuwa hatakuwa na tishio kubwa ….”

937.            Mtume Muhammad  Mustafa s.a.w.w. amesema: Al-Muhajjat-ul-Baidha

“Yeyote yule anayejinusuru na maovu ya

tumbo,

ulimi, na

sehemu zake za siri basi kwa hakika amejinusuru kutoka madhambi.”

938.     Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s., amesema Nahjul Balagha

U. 553:

“Kumbuka (wakati wa kutenda dhambi), kuwa raha zinapotea wakati matokeo ( yatakayotokea )yake yanabakia.”

939.            Mtume Muhammad  Mustafa s.a.w.w. amesema, Al-Kafi, J. 5,

 Uk. 548:

“Yeyote yule anayembusu kijana wa kiume kwa matamanio ya kitamaa, basi Allah swt atamadhidhibisha na kumchapa kwa miale ya moto.”

940.     Al Imam Muhammad al-Baquir a.s. amesema, Al-Kafi, J. 2,

Uk. 79:

“Je kuna jitihada gani iliyo afadhali kuliko usahihi wa tumbo na wa sehemu za siri.”

MALI YA DUNIA NA ULIMBIKIZAJI KWA UROHO.

941.            Mtume Muhammad  Mustafa s.a.w.w. amesema, Bihar al-

Anwaar, J. 71, Uk. 173:

“Kwa yeyote yule ambaye siku zake mbili za maisha yakawa sawa (hakuna maendeleo ya kiroho) kwa hakika yupo katika hasara.”

942.     Al Imam Musa al-Kadhim a.s. amesema, Bihar al-Anwaar,

J. 78, Uk. 311:

“Mfano wa dunia hii ni sawa na maji ya bahari. Kiasi chochote yule anywacho mwenye kiu kutoka bahari, kiu chake kitaendelea kuongezeka hadi kinawez kumuua.”

943.     Al Imam Muhammad at-Taqi a.s. amesema, Bihar al-Anwaar,

J. 78, Uk. 368:

“Watu wanaheshimiwa humu duniani kwa kuwa na mali na Akhera watu wataheshimiwa kwa kuwa na matendo mema.”

944.         Mtume Muhammad  Mustafa s.a.w.w. Amesema, Makusanyo ya Waram:

“Maangamizo ya wanawake wangu yako katika mambo mawili:

Dhahabu na

mavazi yasiyo ya heshima;

Na maangamizo ya wanaume wafuasi wangu yapo katika

kuiacha elimu na

 kukusanya na kulimbikiza mali.”

DUNIA INAYO HADAA, MAVUTIO NA SUMU YAKE.

945.            Mtume Muhammad  Mustafa s.a.w.w., amesema Bihar al-

Anwaar, J. 6, Uk. 161:

“Wakati Jeneza maiti ya mtu inapoinuliwa na kuchukuliwa kwenda kuzikwa, basi Ruh yake inaifuata maiti na katika hali ya masikitiko makubwa inasema:

‘Enyi watoto na Jama’a zangu ! Jitahadharisheni sana kuwa ulimwengu huu hauwahadai nyie kama mulivyonifanyia mimi.

Mimi nimekusanya mali yote hii bila ya kujali uhalali au uharamu wake na nimeiacha nyuma huku kwa ajili ya wengine.

 Sasa mimi nimeondoka na mzigo juu yangu (kwa sababu ya kutenda kila aina ya madhambi ya uhalali na uharamu) wakati matunda yake wanafaidi watu wangineo; kwa hivyo, mujiepushe na hayo ambayo sawa na yaliyo nifika mimi.”

946.     Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s., amesema Bihar al-Anwaar,

J. 73, Uk. 166:

“Iwapo huyu mtu angeweza kuiona mauti yake na kasi yake inavyo mwelekea yeye basi kwa hakika angechukia na kuiacha dunia na matumaini yake yote.”

947.     Al Imam Musa al-Kadhim a.s., amesema Bihar al-Anwaar,

J. 78, Uk. 311:

“Mfano wa dunia ni kama nyoka ambaye ngozi yake ya nje ni laini na nyororo kwa kugusa wakati kuna sumu kali mno inayoua ndani mwake. Aliye na hekima wanajaribu kujiepusha nayo (lakini watoto wasio na fahamu kamili) wanapendezewa na kuvutiwa nayo na wanatamani kugusa na kucheza kwa mikono yao.[71]

948.            Amesema Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s., Al-Kafi, J. 2,Uk. 315:

“Mapenzi ya dunia hii itakayo angamia ndiyo chanzo cha maovu yote.”

WATUMWA WAPUUZAJI WA DUNIA HII INAYO HADAA.

949.         Amesema Al Imam Hussein ibn 'Ali ibn Abi Talib a.s.,  Tuhaful-'Uqul na Bihar al-Anwaar, J. 44, Uk. 374:

“Kwa hakika, watu ni watumwa wa dunia na imani yao haina misingi yoyote, ipo katika ndimi zao tu. Wao wanaitilia maanani ili mradi wanapata mahitaji yao wanayoyahitaji, lakini pale wanapojaribiwa, basi idadi ya waumini halisi inakwenda ikipungua.”

950.     Al Imam Hassan ibn 'Ali ibn Abi Talib a.s. amesema, Safinat-ul-Bihar, J. 2, Uk. 84:

“Mimi nastaajabishwa kuhusu yule mtu ambaye yuko mashughuli kwa ajili ya kula tu lakini hafikirii kwa ajili ya chakula cha akili yake. Hivyo yeye anajiepusha na kile kinachomdhuru tumboni mwake na papo hapo anaiachia akili yake ijae kwa yale yanayoangamiza.”

ULAFI NA MATUMAINI YA KIPUUZI.

951.     Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s., amesema Nahjul Balagha

Barua no. 52:

“Ingawaje uchoyo, uoga na uroho ni vitu vyenye sifa tofauti, lakini vyote viko sawa katika mambo ya kufikiria kwao kuhusu Allah swt.”

952.     Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema, Man la Yahdharul

Faqih, J. 4, Uk. 418:

“Iwapo mwanaadamu atakuwa na mabonde mawili ambamo kumejazwa dhahabu na fedha, basi yeye hatatosheka nayo bali atakwenda kuitafuta ya tatu.”

953.     Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s., amesema Al-Usul-i- Kafi, J. 2,

Uk. 320:

“Yeyote yule anaye uendekeza moyo wake kwa dunia hii basi atapatwa na hali tatu:

Mateso yasiyoisha,

kiu ya matamanio isiyoisha na

matumaini yasiyo timika.”

954.     Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s., amesema Ghurar-ul-Hikam,

Uk. 240:

“Wako kiasi gani cha watu ambao ni waovu na siku zao ziko zinahesabika lakini bado wanaendelea kwa juhudi zao zote za kuitafuta hii dunia.”

MAJIVUNO NA KIBURI.

955.     Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. amesema, Tasnif-i-Ghurar-ul-

Hikam,Uk. 443:

“Msiwe wakaidi (na msing’ang’anie kufuata vile mfikiriavyo nyie wenyewe), kwa sababu watu kama hawa hukumbana na maangamizo.”

956.     Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s., amesema Tasnif-i-Ghurar-ul-

Hikam,Uk. 308 na Bihar al-Anwaar, J. 6, Uk. 91:

“Yeyote yule ajionaye kuwa yeye ndiye mkubwa kabisa (hana mfano mwingine) basi si kitu chochote kile mbele ya Allah swt.”

957.     Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. amesema, Bihar al-Anwaar,

J. 72, Uk. 39:

“Mambo mawili yanasababisha watu kuangamia (na kutumbukizwa katika Jahannam):

Kuogopa umaskini, na

Kutaka ukubwa kwa kupitia majivuno.”

958.     Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. amesema, Ghurar-ul-Hikam, Uk. 298:

“Mjiepushe na kujifakharisha wenyewe, kwa kutegemea yale muyaonayo mazuri ndani mwenu na kwa kupenda kuzidishiwa sifa kwa sababu hayo ndiyo majukumu makubwa yakutegemewa na Shaytani.”

959.     Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s., amesema Al-Kafi, J. 2, Uk. 310:

“Yeyote yule aliye na kiburi hata kidogo moyoni mwake basi hataruhusiwa kuingia Jannat.”

KUBANA MATUMIZI.

960.     Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s., amesema Bihar al-Anwaar,

 J. 71 Uk. 346:

“Yeyote yule anaye panga matumizi yake basi kamwa hatakuwa fakiri.”[72]

961.     Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s., amesema Ghurar-ul-Hikam, Uk. 182:

“Sera bora kabisa ni katika kutekeleza ukarimu.”

962.     Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s., amesema Mustadrak-ul-Wasa'il, J. 15, Uk. 271:

“Matumizi ya kupita kiasi cha kile kinachohitajika, ni ufujaji.”

963.  Al Imam Musa al-Kadhim a.s., amesema Bihar al-Anwaar,

 J. 66, Uk. 334:

“Lau watu wangekuwa na tabia ya kula kwa kiasi, basi miili yao ingekuwa na nguvu.”

964.            Mtume Muhammad  Mustafa s.a.w.w. amesema, Irshad-ul-

Qulub…………:

“Hakuna mtu anayepita makaburini isipokuwa waliokufa wanamwambia:

‘Ewe uliye ghafilika ! Je unaelewa yale tulivyoeleweshwa sisi, itakufanya wewe damu yako ipoozwe.’”

USHAURIANO.

965.            Mtume Muhammad  Mustafa s.a.w.w. amesema, Irshad-ul-

Qulub…………:

“Hakuna mtu anayepita makaburini isipokuwa waliokufa wanamwambia:

‘Ewe uliye ghafilika ! Je unaelewa yale tulivyoeleweshwa sisi, itakufanya wewe damu yako ipoozwe.’”

966.         Mtume Muhammad  Mustafa s.a.w.w. amesema, Manhaj-us-Sadiqiin,Tafsiri, J. 2, Uk. 373:

“Iwapo watawala wenu ni watenda wema, na matajiri ni wale wenye kukushukuruni, na mambo yenu yanakwenda kwa ushauriano miongoni mwenu, basi kwenu nyinyi kuishi duniani ni vyema kuliko chini yake. Lakini iwapo watawala wenu ni waovu kwenu nyie, na matajiri ni mabakhili miongoni mwenu, na mambo yenu yanakwenda bila kushauriana, kwa hivyo kwenu nyie kutakuwa afadhali kuwa ndani ya ardhi kuliko kuishi juu yake.”

967.     Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. amesema, Ghurar-ul-Hikam, Uk. 336:

“Yeyote yule anayeshauriana pamoja na wenye busara na akili, kwa ajili ya kupata mwangaza ili aweze kupata mwanga katika masuala yake (na ataweza kuona sahihi kile kilicho sawa kutoka na kile kilicho potofu).”

968.     Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s., amesema Bihar al-Anwaar,

J. 75, Uk. 105:

“Yeyote yule anayeshauriana pamoja na watu wa maelewano, basi huonyesha maendeleo yake….”

969.      Mtume Muhammad  Mustafa s.a.w.w., amesema Nahaj-ul-Falsafa, Uk. 533;

“Hakuna muumin atakaye kuwa mwovu kwa ushauriano, na wala hakuna atakayefaidika kwa ukaidi wake.”

KUFANYA KAZI NA KUKAA BURE.

970.         Mtume Muhammad  Mustafa s.a.w.w., amesema At-Tahdhib, J. 6, Uk. 324:

“Ibada imegawanyika katika matawi sabini, na bora ni kule mtu kujitafutia riziki halali.”

971.     Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s., amesema Ghurar-ul-Hikam Uk. 197:

“Kamwe, Kamwe hakutapatikana raha na starehe za maisha kwa kubakia bila kazi au kuwa mvivu.”

972.     Al Imam Muhammad al-Baquir a.s., amesema Bihar al-Anwaar, J. 78, Uk. 175:

“Jiepusheni uvivu na kutokuridhika. Na haya mawili ndio ufunguo wa kila aina ya maovu.”

973.         Mtume Muhammad  Mustafa s.a.w.w.aliambiwa na Sa’ad Ansari kuwa mikono yake imekufa ganzi au imekuwa ngozi ngumu ni kwa sababu ya kufanya kazi kwa kutumia kamba na koleo kwa ajili ya kupata pesa kwa ajili ya kutumia  yeye, mke na watoto wake.

   Kwa kusikia hayo Mtume Muhammad  Mustafa s.a.w.w. aliibusu mikono yake (akionyesha heshima) na akasema, Usd-ul-Ghabah, J. 2, Uk. 269:

“Kwa hakika huu ndio mkono ambao moto wa Jahannam kamwe hautaugusa.”

SHAHIDI NA SHAHADA.

974.         Mtume Muhammad  Mustafa s.a.w.w., amesema Bihar al-Anwaar, J. 10, Uk. 100:

“Kuna jema kwa kila jema hadi wakati mtu anapouawa katika njia ya Allah swt na zaidi ya hapo hakuna tena jema lingine juu yake. (Kupigana dhidi ya maadui Waislam ambao wanawaua Waislam)”

975.     Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema, Furu'i al-Kafi, J. 5,

Uk. 54:

“Yeyote yule anayeuawa katika njia ya Allah swt kama shahidi, basi yeye kamwe hataulizwa chochote kuhusu madhambi yake. (Madhambi yake yote yatakuwa yamesamehewa kwa ujumla).”

976.         Mtume Muhammad  Mustafa s.a.w.w., amesema Bihar al-Anwaar, J. 75, Uk. 149:

“……………. kwa kiapo cha yule ambaye maisha na roho yangu iko mikononi mwake, iwapo viumbe vyote vya duniani na angani vikijumuika pamoja kumuua muumin ambaye hana kosa hata moja au watakapo shawishiwa kufanya hivyo, basi Allah swt atawatia wote kwa pamoja katika moto wa Jahannam.”

977.         Mtume Muhammad  Mustafa s.a.w.w., amesema Wasa'il ush-Shi'ah, J. 15, Uk. 14:

“Hakuna tone ambalo linalopendwa na Allah swt kuliko tone la damu ya yule, linalomwagika akiwa anakuwa shahidi katika njia ya Allah swt.”

MTARAJIWA AL-MAHDII A.S. NA UTAWALA WAKE WA HAKI.

978.         Mtume Muhammad  Mustafa s.a.w.w., amesema Sunan Abi Daud, J. 4, Uk. 107;

“Al Mahdi anatokana na kizazi changu kutokea kwa wana wa Fatma Bi Zahra a.s.[73]

979.         Mtume Muhammad  Mustafa s.a.w.w. amesema kuwa, Bihar al-Anwaar, J. 52, Uk. 129:

“Mwenye furaha ni yule ambaye ataweza kumfikia Al-Qaim a.s. wa Ahlul Bayt a.s. na kumfuata kabla ya kudhihiri kwake. Mtu huyu atawapenda wapenzi wa Imam Al Mahdi a.s. na atawachukia maadui wake, na atakubalia uongozi wa Maimam a.s. kabla ya kudhihiri kwake. Na hawa ndio marafiki zangu, na kwa hakika hawa ni watu halisi katika umma wangu ambao mimi ninawatukuza sana.”

980.         Mtume Muhammad  Mustafa s.a.w.w. amesema, Al-Musannif, J. 11 Uk. 371:

“Allah swt atamwinua mtu mmoja kutokana na kizazi changu, kutokea Ahlul Bayt a.s.  yangu, kwa kuja kwake ardhi hii itajazwa kwa uadilifu kama vile ilivyojaa sasa hivi kwa dhuluma na kukosekana kwa haki.”

981.         Mtume Muhammad  Mustafa s.a.w.w., amesema Musnad Ahmad ibn Hanbal, J. 2, Uk. 83 na J. 3, Uk. 446  na J. 4, Uk. 96; Sahih Bukhari, J. 5, Uk. 13 na Sahih Muslim, J. 6, Uk. 21, na No. 1849 ya Riwaya–25 na Marajeo mengine ambayo yameelezwa na Wanazuoni wa Kisunni:

“Mtu yeyote atakayekufa bila kumjua Imam wa Zama zake (Imam wa zama zetu hizi ni Al Imam Mahdi Sahibuz-Zamaan a.s.) Basi atakuwa amekufa kama vile walivyo kuwa wakifa katika zama za Ujahiliyyah.”

982.     Al Imam 'Ali ibn Abi Talib a.s. amesema kuwa, Bihar al-Anwaar, J. 52, Uk. 316:

“Atakapo dhihiri Al Qaim a.s., basi mbingu itanyesha mvua, ardhi itaotesha miti yake, uadui utakwisha kutoka mioyo ya waja (ili kwamba wote waweze kuishi kwa amani na mapenzi ya kindugu), na wawindaji na wanyama wataendelea kuishi kwa amani kwa pamoja…………”

983.  Abil Jarudi amesema, Al-Kafi, J. 1, Uk. 34:

“ Mimi nilimwuliza Al Imam Muhammad al-Baquir a.s. iwapo yeye alikuwa akijua kuhusu mapenzi yangu na utiifu wangu kwake, naye alinijibu kuwa alikuwa akijua. Nami nikamwambia kuwa nilikuwa na swala nililokuwa nikitaka kumwuliza ili aweze kunijibu, kwa sababu mimi nilikuwa kipofu na nilikua nikitembea kwa uchache sana, na hivyo nilikuwa siwezi kumtembelea kila mara. Naye alinitaka mimi nimwulize swala nililokuwa nikitaka kumwuliza. Hivyo mimi nilimwomba anijulishe dini au madhehebu yeye na Ahlul Bayt a.s. wanayoifuata na ambayo inapendwa na Allah swt, ili nami niweze kufanya ‘ibada ya Allah swt kwa mujibu wa madhehebu hayo.”

rudi nyuma Yaliyomo endelea