rudi maktaba >Akida >Yaliyomo >

HITIMISHO

Katika kitabu chake "Basic Christianity" (Ukristo wa Msingi) mwandishi John Stott anasema:

"Kimsingi Ukristo ni Kristo. Nafsi na kazi ya Yesu ni jiwe la msingi ambapo juu yake imejengwa imani ya Ukristo. Na kama siye alisema kuwa ni yeye (ikiwa sio yeye aliyejitangaza kuwa ni Yesu kristo). Na kama hakufanya yale aliyosema alikuja kufanya, jengo zima la Ukristo litaporomoka na kuanguka chini".[31]

Mtume Muhammad, baada ya miaka ya mapambano dhidi ya Wayahudi wa Madinah juu ya masuala ya dini, alisema thiolojia ni upuuzi wa kitoto - - adui wa dini. Uislamu, tofauti na mifumo mingine, ni dini rahisi ambayo haikuzikwa katika vichaka vya ububusa visivyokubaliana na akili na mantiki. Hakuna kundi la watu wanaoshughulika na masuala ya dini peke yake (clergy), hakuna madaraja ya dini, wala hakuna Sakramenti. Thiolojia haina nafasi katika Uislamu, kwa vile Uislam ni njia kamili ya maisha, na sio rundo la maneno tu.

Licha ya kwamba Uyahudi ulikwenda mrama katika sherehe (fafanuzi) za vitabu vyao vya sheria lakini bado wanayo imani ya msingi na kuu kabisa kuwa Mungu ni mmoja.

Uislamu una maana kujinyenyekesha chini ya taa na milki ya Mwenyezi Mungu, imani ya kuwa Mwenyezi Mungu mmoja tu asiyekuwa na mshirika ikiwa imani kuu na ya msingi kabisa.

Ukristo kwa upande mwingine unasema kwamba Bwana wake ni Yesu kristo. Kwa mujibu wa Fritz Ridenour:

"------ Tunajinyenyekesha chini ya mamlaka yake".[32]

Hebu tuangalie tena katika Mathayo 4: 10, ambapo Yesu anasema:

"Msimsujudie yeyote isipokuwa Bwana Mungu wenu. Na mwabuduni Yeye tu".

Dhahiri shahiri, hapa Yesu anatuambia kwamba ni Mungu peke yake ndiye tunayetakiwa kumwabudu.

Dini sio suala la kubahatisha na hotuba bali ni ukweli (fact) na muongozo. Dini ya kweli inajali na kuzingatia utii wa sheria, na utii huu ndio kipimo cha uchamungu wa muumini.

Ndugu zetu wa Kikristo wanatakiwa kuzingatia masuala haya katika nyoyo zao. Sio tu kwamba hawafuati miongozo ya dini zao isipokuwa Jumapili, bali pia wamepotea kabisa kutoka kwenye mafundisho ya mtu ambaye jina lake linaunda msingi wa imani yao. Na badala yake wamebugia imani na mila za kipagani ambazo wamezivisha joho la imani juu ya kuwepo kwa Mwenyezi Mungu Mmoja asiyekuwa na Mshirika (Monotheism). Marafiki zetu wa kikristo wana kazi kubwa zaidi ya kutafiti.

Waislam hawana budi kukumbuka maneno ya Mwenyezi Mungu katika Quran:

"Wayahudi na Wakristo hawatakuwa radhi nanyi mpaka mtakapofuata dini yao". (Quran 2:120)

Pia ni lazima tukumbuke maneno ya mwisho yaliyotolewa na Mwenyezi Mungu kwa Mtume Muhammad (SAWW):

"Leo nimekukamilishieni dini yenu (na) kukutimilizieni neema yangu juu yenu na Nimekuchagulieni Uislamu ndio iwe dini yenu". (Quran 5:3).

Baada ya kusema na kufanya yote, ni lazima tuyazingatie maneno muhimu yafuatayo kutoka kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu:

"Tunaubanisha na kuuthibitisha ukweli dhidi ya Uongo (Batili) mara Batili ikaondoka. Na adhabu inakungojeeni kwa haya mnayoyasema". (Quran 21:18)