rudi maktaba >Akida >Yaliyomo >

MWANZILISHI HALISI WA UKRISTO - PAULO WA TARSUS

Mmoja wa wanafunzi hawa waYesu (Wanazareti) aliyeitwa Stephano alielekeza mahubiri yake mbele zaidi ambapo alitoa mahubiri makali kukemea maovu mbele ya Mahakimu wa kiyahudi walioeleweka kama Sanhedrin. Wakifoka kwa hasira kwa sababu ya maneno yake ya "kishetani", mahakimu waliruka na kumkamata, kisha wakampeleka nje ya mji ambako walimpiga mawe mpaka kufa. Kisa hiki kinapatikana katika "Matendo ya Mitume", sura ya 7, katika Biblia.

Mauaji ya Stephano yalishuhudiwa na kijana mdogo wa kiyahudi aliyeitwa Saulo (Paulo). Paulo alizaliwa katika mji wa Tarsus, si muda mrefu sana baada ya Yesu. Saulo (Paulo) alikuwa amejiunga na moja ya madhehebu ya kiyahudi "Pharisees". Hawa Wapharisees waliojipa mamlaka na kujihalalishia kuwaua wanafunzi wa Yesu (Wanazareti), sasa hivi walikuwa na nia kubwa ya kuendelea kuwakamata na kuwaua wanafunzi wa Yesu. Kufuatia mauaji dhidi ya Stephano, Paulo mwenyewe alichukua na kufanya kazi muhimu katika kuendeleza mauaji haya dhidi ya wanafunzi wa Yesu.

Utendaji kazi wake katika kuendeleza mauaji haya ulikuwa mzuri mno kiasi kwamba alifanywa kuwa ni ajenti mkuu wa harakati hizi katika mji wa Jerusalem, na alipewa kumbukumbu muhimu ili kuendeleza safisha safisha hii katika miji ya jirani.

Ni takriban miaka ishirini na tano tangu kupaa kwa Yesu mbinguni, ambapo huyu muuaji na mpinzani mkubwa wa Yesu na wafuasi wake alipokuwa njiani kuelekea Damascus kwenda kuwasaka wafuasi wa Yesu ambapo aliona katika ndoto anayodai kuwa alimuona Yesu, aliyemuuliza kuwa kwa nini alikuwa anataka kumuua (Yesu) kwa kuwatesa watu wake (Yesu).

Maelezo mengi yametolewa kuonyesha nini kilimtokea Saulo siku hiyo. Kama vile ugonjwa unaotokana na kupigwa na miale ya jua kwa muda mrefu hasa kichwani, mawenge na hata kifafa. Lakini hakuna lenye yakini tukiachilia kwamba maelezo yote haya yanakusudiwa kumbadilisha muuaji wa wanafunzi na wafuasi wa Yesu na adui mkubwa wa ujumbe wa Yesu, na kuwa mhubiri mzuri wa Yesu asiyekuwa na mfano wake.

Saulo alibadilisha jina lake na kuwa Paulo na akaenda katika jangwa la Arabuni ili kutafakari ni jinsi gani angetekeleza amri aliyoamini kuwa imetoka kwa Yesu ya kwenda kuhubiri.

Nini hasa angefanya ilikuwa ni kitendawili kwake, hata hivyo, maadamu wayahudi walikuwa wamemkataa Yesu na ujumbe wake, Paulo hakuona uwezekano wa kuwashawishi kwa mahubiri na kuwapata. Baada ya kutafakari akaona itakuwa ni vizuri zaidi aache kushughulika na wayahudi na badala yake aeleze jitihada zake kwa wasio kuwa wayahudi (Gentiles). Ili kufanikisha hili busara na akili nyingi vilitakiwa kutumika.

Warumi na Wagiriki ambao hawakuwa Wayahudi ndio hasa Paulo aliowalenga kuelekeza mahubiri yake. Hawa walikuwa wapagani waliokuwa wakiabudu miungu wa kike na miungu wa kiume na iliyokuwa mingi sana. Majumba ya ibada za masanamu na masanamu yenyewe yalienea kwa wingi nchi nzima, na sheria ya kirumi iliwataka watu wote, isipokuwa Wayahudi, kusujudia na kutoa heshima kwa miungu hii ya kisanamu.

Paulo alielewa kwamba watu waliokuwa na imani ya kipagani iliyowakolea kiasi hicho wasingeweza kukubali kwamba neema ya Mungu na uokovu vingeletwa na mtu tu aliyeaminiwa kuwa muongofu na mtenda haki. Ili kupata mafanikio ya haraka katika kazi yake Paulo alielewa wazi kwamba alilazimika "kulegeza" mambo kidogo, akizingatia utamaduni wa Warumi na Wagiriki (Watu wa Mataifa).

Paul Maier, katika kitabu chake "Wakristo wa Mwanzo" (First Christians), anatuambia kwamba ilipita miaka kumi na tatu tanguwakati Paulo "alipopokea wito kutoka kwa Yesu" mpaka alipoanza kuhubiri. Katika hiyo miaka kumi na tatu, Paulo kwa kutumia ujanja na ubunifu wake wa hali juu alijifunza mambo mengi kuhusiana na mila na desturi za Warumi na Wagiriki, ambapo hatimaye alirudi Damaskas akiwa amejipatia silaha muhimu kwa kutambua kwamba Warumi na Wagiriki wangedai na kihitaji Mungu ambaye wangeweza kumuona na kumshika katika hii dini yao mpya, na alikuwa tayari kuwakubalia hili pindi wakihitaji.

Paulo lifanikiwa sana katika kazi yake hii na aliweza kuwapata Warumi na Wagiriki wengi mno. Japokuwa dini ya ukristo inachukua jina lake kutoka kwa Yesu kristo, Paulo mkazi wa Tarsus lazima atambulike na kueleweka kuwa ndiye mwanzilishi halisi wa Kristo, kwa vile yeye ndiye aliyebuni na kutunga misingi muhimu na imani za kikristo, na akajenga na kuimarisha Makanisa katika ulimwengu wote wa zama zake. Wakristo hawalikatai hili:

"Hakuna mtu yeyote katika historia ya ukristo mwenye athari kubwa na umaarufu kama Saulo mkazi wa Tarsus".[3]

Katika kitabu "The 100" (Watu 100) chenye orodha ya watu wenye athari kubwa ulimwengu na maarufu kuliko wote mia moja mwandishi wa kitabu hicho Michael Hart anasema:

"Hakuna mtu mwingine aliyefanya kazi kubwa ya kueneza ukristo kama Paulo."[4]

Kuna tatizo moja kuhusiana na jambo hili, kwamba mafundisho ya Paulo, mwanzilishi halisi wa ukristo, hayawiani na hayawezi kupatikana katika mafundisho ya Yesu wala katika mafundisho ya Mitume waliotangulia kabla yake.

Si hivyo tu, bali Paulo alionana mara chache sana na wanafunzi wa Yesu ambao wangeweza kumuongoza na kumuweka sawa, hawakukubaliana na mafundisho ya upotoshaji ya Paulo, na Paulo alilielewa hili. Hatimaye hata hivyo, Paulo alifanikiwa kwa sababu ya uwezo wake mkubwa wa kushawishi watu, mbali na ukweli kwamba yeye na wafuasi wake waliwazidi sana wanafunzi wa Yesu kwa nyadhifa zao kijamii, utajiri na elimu, aliweza kupata idadi kubwa ya wafuasi wa Kirumi na Kigiriki. Mafundisho ya Yesu yaliyokusudiwa kwa Wayahudi yaliyokuwa yakifundishwa na wanafunzi wake hayakuweza kufurukuta tena mbele ya mafundisho ya Paulo.

Hebu tujaribu kufanya uchunguzi wa makini juu ya uzushi ambao Paulo aliuingiza katika dini "yake" ya Ukristo.