rudi maktaba >Akida >Yaliyomo >

UTANGULIZI

Uchunguzi wa karibu, katika dini mbili kati ya hizi - Uyahudi na Uislamu - utaonyesha hili kuwa ni kweli: Wote Wayahudi na Wislamu wanamuabudu Mungu mmoja, Muumba wa Mbingu na Ardhi.

Hii dini nyingine, Ukristo, ina mushkeli kidogo, hususan wakati tunapoelezea maana ya imani ya kumuamini Mungu Mmoja asiyekuwa na mshirika tofauti na inavyoaminiwa na Ukristo.

Badala ya kumfanya Mwenyezi Mungu Mtukufu awe ndio kiini na msingi mkuu wa imani yao, Wakristo wamebadilisha muelekeo wao na kumfanya Yesu, anayeeleweka kwao kama "Yesu kristo" au "Yesu Aliyepakwa mafuta" kuwa ndio msingi mkuu wa imani. Kwa Wayahudi Yesu alikuwa "Kijana mzuri wa kiyahudi". Kwa Waislamu Yesu alikuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu lakini alikuwa binadamu; mmoja wa wajumbe wateule wa Mwenyezi Mungu Mtukufu. Kwa Wakristo, hata hivyo, Yesu ni zaidi ya hayo.

Ukristo, kiini chake kikuu ni Yesu Kristo. Dini hii imepata jina lake kutokana na jina la Yesu Kristo. Misingi na imani zote muhimu za kikristo kiini chake ni Yesu kristo. Sikukuu kubwa za Kikristo huwa ni kumbukumbu ya matukio katika maisha ya Yesu Kristo. Alama ya imani ya Kikristo, msalaba, ni alama ya Yesu Kristo. Sala na dua za Wakristo huelekezwa kwa Yesu Kristo, kwa vile wanaamini kuwa Mwenyezi Mungu Mtukufu Mwenyewe huwa hawezi kuombwa na binadamu wa kawaida.

Kwa mujibu wa Mwandishi wa Kikristo Fritz Ridenour: "Msingi wa Ukristo ni kwamba Yesu Kristo hasa ndiye sababu ya kuwepo Ukristo na kwamba yeye ndiye anayeushikilia na kuumiliki".[1]

Wakristo wengi leo wanashindwa kuelewa kuwepo kwa Mwenyezi Mungu bila ya Yesu kusimama mbele ya Mwenyezi Mungu badala yao. Bwana Ridenour anasema kwamba Ukristo ni: "...... Uhusiano na mwanadamu, Yesu Kristo"[2]. Na Wakristo wengi sana wana imani hii, hawamwelewi Mwenyezi Mungu Mtukufu kwa namna nyingine yoyote isipokuwa kwa kupitia kwa Yesu Kristo.

Wakristo wanasema mwabudu Mwenyezi Mungu, lakini Yesu pia picha yake iwepo akilini. Kwa jinsi wanavyomuona - kwa nyongeza ya Mwenyezi Mungu, kama Mungu halisi, Ukristo ni dini yenye miungu wawili, sio mmoja, na dini yenye Mungu zaidi ya mmoja sio dini inayompwekesha Mwenyezi Mungu Mmoja asiye na mshirika.

Hali hii ilikujaje? Ilikuwaje dini ya Ukristo imbadilishe Mtume wa Mwenyezi Mungu (ambaye ni binadamu) na kumfanya yeye Mwenyewe (Yesu kristo) kuwa Mungu?