rudi maktaba >Akida >

Rudi nyuma Yaliyomo endelea

NAFSI ILIYOPATA KUTU (al-Nafs-al-Ra’ina):

‘KUTU’ ni shida nyingineyo ambayo nafsi inaweza kupatwa kwani ni sawa na ule mfano wa kioo cha kujitazamia, iwapo ile poda itabanduka basi hutaweza kujitamazama kiooni. Basi kioo cha moyo ambavyo ni sehemu ya umuhimu kwa ajili ya Mwenyezi Mungu utukufu wa ukamilifu wake, fadhila zake zitamorudishwa kwake, hazitoweza rudishwa iwepo itashika kutu, na hatimaye itaweza kupoteza ile nguvu ya kupeleka ujumbe wako kwa Mwenyezi Mungu.

Ingawaje mwanadamu hawezi kumtazama Mwenyezi Mungu kwa macho yake, lakini anao uwezo wa kumwona Mwenyezi Mungu, Utukufu wake na Ukuu wake kwa kupitia NURU iliyomo katika Nafsi yake. Nafsi ile ambayo imeshakwisha shikwa na kutu ambamo sasa hakuna uwezo wa kurudishia (reflect ) kutoka na kwa Mwenyezi Mungu, basi bila shaka itatapatapa huko na huko ikimtafuta sheitani na hasa kwa mujibu wa matilaba yake. Qurani ikiwa inatumbusha kuwa:

“Sivyo hivyo! Bali yametia juu ya nyoyo zao (maovu) waliokuwa wakiyachuma.” (83:14)

Katika ‘aya hii twaelezewa vyema kabisa kuwa chanzo cha kupatwa kwa kutu kwa Nafsi ni kule kutenda madhambi. Kwa hivyo kila dhambi itatupia uzito (itatanda kiza juu ya moyo; na ifikiapo hali kama hii, inambidi mtu afanye Tawba mara moja kwa ajili ya kuyasafisha hayo matendo maovu na atende matendo mema ili kuzuia kupotea kwa nuru iliyotunukiwa Nafsi yake. Vile vile, twaambiwa katika hadithi Tukufu kuwa: “Mtu mwenye furaha kuu katika siku ya Kiama ni yule atakaye yaona maneno aliyokuwa akiyatamka ‘naomba msamaha wa Mwenyezi Mungu’ chini ya kila dhambi alilolitenda. Kwa Hivyo inambidi kila Mwislam mmoja wetu apige msasa kila ovu alilolitenda ama sivyo, Mwenyezi Mungu azitowazo onyo zake za upole zitabadilika na kuwa ghadhabu kubwa sana.

NAFSI AMURU (al-Nafs al- Ammara):

Nafsi isiyofunzwa hasa wakati wa ujana wa mtu, huamuru kutendwa kwa matnedo ya madhambi bila kiasi. Katika Qurani, kuhusu kisa cha Mtume Yussuf, Nafsi inasemwa:

“Nami sijitasi Nafsi yangu; kwa hakika (kila) Nafsi ni yenye kuamrisha sana maovu (12:53)

Sentensi hiyo inaonyesha kuwa ilitamkwa na Zuleikha aliyekuwa amependa Nabii Yussuf. Pale alipotoa ushahidi, alithibitisha kuwa ndiye chanzo cha uovu huo. Kwani Yussuf alikuwa hayupo wakati huo wa ushahid, lakini kwa kuwa Zuleikha alikuwa hana hila yoyote ile zidi ya Yussuf. Pia kuna uwezekano kuwa hayo yametamkwa na Yussuf au ni wote vyovyote vile, Qur’an inatuambia kuwa “Nafsi ni yenye kuamrisha sana maovu. (12:53)

Nafsi yoyote ile isiyokuwa imeongozwa kwa mujibu wa mfano ya Islam, huwa daima inavutwa popote pale penye madhambi na ma’asiyah kwani yote hayo yako yamedhalilishwa kabisa. Mfano wa Nafsi hii ni sawa na mtoto mchanga atakaye kila kitu kuchezea bila kutazama ubora wake, faida au hasara zake, iliramdi yeye apate kuchezea tu, Nafsi ya yule aliye na utamaduni mzuri, aliyekomaa na kubaleghe inavutika pale penye mema na hujiepusha na matilaba yake; na ile nafsi elimishwa na inavutika pale penye maovu ya kila aina na kwa hivyo lazima ifunzwe vyema, itasaidia kutakasisha hiyo Nafsi.

HATIMAYE: Kile kilichoelezwa hapo kinasema kuwa Nafsi inaweza kuwa bora kabisa ama mbovu kabisa au vinazidiana katika vina na ngazi. Kuna nafsi zifikiapo kuitwa ‘Nafsi halisi na ‘Nafsi ridhika’ n.k. na vile vile kuna zinapofifia hadi kufikia hali mbaya kabisa na matokeo yake ni majanga, majonzi na maovu na kufikia ile sifa ya “kupigwa mihuri” au ‘zilizopofuka’ na ‘zenye maradhi’ zikiwa ni kama mifano.

Hali hii inadhihiridha kuwa Nafsi zinapangwa na kila mtu anayo Nafsi moja tu.

JE UMEJING’AMUA UNA NAFSI YA AINA GANI UNDANI MWAKO??

(JITAHADHARISHE)!

3. DHULUMA ZA AINA TATU

Makala haya yametarjumiwa na:

Amiraly M.H.Datoo P.O.Box 838 Bukoba – Tanzania

Amesema al-Imam Muhammad al-Baquir a.s. : Al-Kafi, j. 2, uk.330

“Zipo aina tatu za dhuluma: “Aina ya kwanza ni ile ambayo Allah swt anatoa msamaha na ya pili ni ile ambayo haitolei msamaha na aina ya tatu ni ile ambayo yeye haipuuzi.”

Ama dhuluma ambayo anaisamehe ni ile ambayo mtu huitenda baina yake binafsi na Allah swt. Na dhuluma ambayo Allah swt haisamehe ni kukufuru na dhuluma ambayo haipuuzii ni ile ambayo inatendewa dhidi ya haki za watu.”

Ufafanuzi:

Aina ya tatu ya dhuluma ni ile ambayo mtu hukiuka na kuvunja haki za watu. Njia saheli ya kutaka kusamehewa ni kwanza kumridhisha yule ambaye haki zake zimekiukwa na kuvunjwa. Iwapo mtu huyo atamsamehe yule aliyemvunjia haki zake, basi hapo dhuluma hiyo itageuka kuwa dhuluma dhidi yake binafsi. Na hapo ndipo ataweza kuwa mstahiki wa kuomba msamaha wa Allah swt.

4. MAKUNDI MANNE YA WATU

Imenakiliwa kutoka Jaafer ibn Muhammad naye kutokea Baba, naye kutokea kwa Babu yake naye kutokea kwa Imam Ali ibn Abi Talib a.s. kwamba Mtume s.a.w.w. alisema katika wasia wake.

Alisema Mtume s.a.w.w. “ Ewe Ali ! Kuna makundi manne ambamo watu wanapatikana wamegawanyika kwa mujibu wa matendo yao humu duniani.[3]

A. Kupanda daraja

1. Kutawadha wudhuu katika baridi

Kwa hakika ni jambo gumu mno kuamka na kujiweka tayari kwa ajili ya ibada za Allah swt hasa kama utakuwapo kazita sehemu ambazo kuna baridi kali ambapo hata kunakuwa na hatari ya watu wengine kuathirika kwa baridi kali. Wakati huyo unakuwa ndio wakati mzuri wa kujipatia usingizi mnono na nguvu za Shaitani zinakuwa zikitushawishi sisi tutoe visingizio mbalimbali ili mradi tusiamke na kufanya ibada za sala hususan za Alfajiri.

2. Kusubiri sala baada ya sala .

Mumin wa kweli kwa hakika anakuwa akiusubiri wakati wa sala kuwadia kwa ajili ya kutaka kusali sala kwa mara nyingine. Fursa hii anaisubiri kwa hamu kwa sababu anapata fursa kwa mara nyingine kumwabudu na kumshukuru Allah swt na ni wakati mwema kwa ajili ya kuomba Tawba ya madhambi yake na vile vile ni wakati mwingine wa kujipatia neema na baraka za Allah swt. Kwa kifupi mumin huyoo amabye anausubiri wakati wa sala uwadie anakuwa na hamu ya kujipatia bahati ya kuweza kujiweka mbele ya Allah swt.

Tukiangalia mfano wa kidunia, iwapo mimi nitaambiwa kuwa nimepewa kibali cha kumzuru Raisi wa nchi yetu nyakati fulani fulani kwa siku. Hivyo mimi baada ya kumzuru mara ya kwanza kwa siku, nitakuwa na hamu na shauku ya kuwadia kwa muda wa mara pili na hivyo hivyo kwa mara zote. Kwa hakika nitaiona saa ikienda pole pole mno.

Na hivyo ndivyo inavyokuwa hali ya Mumin kwa ajili ya kutaka kuwa mbele ya Allah swt kwa nyakati angalau mara tano kwa siku.

3. Kutembea usiku na mchana kwa miguu kuelekea Jamaa’

Mumin kwa hakika daima hupenda kujumuika pamoja na jama’a yake katika mambo yote ya jumuiya yake na sala za jama’a .

Mtume s.a.w.w. amesema:

“Kwa hakika Allah swt hawakutanishi Ummah wangu katika upotofu, na mkono Wake uko pamoja na Ummah huo, kwa hakika atakayejitoa humo basi atambue kuwa amejitoa kwa ajili ya Jahannam….” Mizan al - Hikmah.

B. Kaffarah ya madhambi.

1. Kutoa na kupokea salaam kwa unyenyekevu.

Mumin huwa daima mwepesi wa kutoa salaam na kujibu salaam anazotolewa. Kamwe hawi mtu mwenye dharau wala kutegea kutolewa salaam au mwenye kiburi.

Allah swt anatuambia katika Quran kuwa tutolewapo salaamu ni faradhi kuijibu ama kwa kurejea salaam hiyo hiyo au kuijibu kwa ubora zaidi.

Mtume s.a.w.w. alikuwa akiviziwa na ma Sahaba wake kwa kujificha kiasi kwamba wapate fursa ya kutangulia kutoa salaam kwa sababu Mtume s.a.w.w. alikuwa ndiyo daima mtu wa kutoa salaa kwa mara ya kwanza. Sasa sisi tunayo kiburi cha nini ? Kwa hakika Allah swt anatuambia kuwa Salaam ni kauli itokayo Kwake.

2. Kuwalisha chakula wale wanaohitaji.

Mumin kwa hakika huwa na moyo wa huruma kiasi kwamba hawezi kula peke yake huku watu wengine wakiwa katika hali ya kubakia katika njaa. Na si hayo tu bali huwa na moyo wa kutaka kuwasaidia binadamu wenzake katika kila hali awezayo yeye.

Yeye huwa karimu na kamwe hawi bakhili ambaye yeye mwenyewe hula bila ya kuwapa wenzake.

3. Kusali sala za Tahajjud ( salat al - Layl au usiku wa manane ).

Mumin huwa anasali sala za usiku wa manane (Tahajjud ) wakati ambapo watu wanapokuwa wamelala usingizi mnono. Na husali kwa kutaka ridhaa ya Allah swt na wala si kwa kujionyesha kwa watu.

Kwa hakika sala hii huwa ikisaliwa na Mitume a.s. na Ma-Imamu a.s. kila siku bila ya kukosa. Hii ni ibada ambayo mtu huwa anamnyenyekea Allah swt wakati ambapo anakuwa ametulia kiroho na kiakili. Huwa hana mawazo au mambo yanayomsumbua huku na huko. Hivyo inamaanisha kuwa ibada hii inafanyika kwa roho khalisi na mtu hukubaliwa ibada zake haraka zaidi katika sala hizi.

Imam Hussain a.s. siku ya Aashura alimwusia dada yake Bi. Zainab binti Ali ibn Albi Talib a.s. kuwa : “Ewe dada yangu Zainab ! Naomba usinisahau katika sala zako za usiku i.e. Salat al-Layl.”

C. Waangamio

1. Tabia mbovu

Wale watu wote wanaoingia katika kikundi hiki cha wenye tabia mbovu kwa hakika mwisho hao hujikuta kuwa wameangamia na kupoteza maisha yao. Yaani maji yameshakwisha mwagiga hayazoeleki tena. Tabia kama hizi zinamwigiza katika upotofu na kiburi na kujiona kuwa wao ndio watu waliostaarabika lakini kumbe ni kinyume na hali hiyo kwani Allah swt hawapendi wale wanaojifakharisha na kutakabari.

2. Kutii nafsi zao

Iwapo mtu ataitii nafsi yake katika kumpotosha basi atakuwa kwa hakika amepotoka na kuangamia humu duniani na Aakhera kwa pamoja.

Amesema Mtume Mtukufu s.a.w.w.: “Yeyote yule atakayeitambua nafsi yake (mwenyewe) basi hakika amemtambua Allah swt.”

Vile vile amesema kuwa : “ Kwa hakika hodari kabisa ni yule ambaye ameighalibu nafsi yake.” Yaani nafsi yake haimpotoshi katika mambo mengi mno kama vile ulafi, uchoyo, ubakhili, uasherati, ukafiri, maasi n.k.

Iwapo mtu atatawaliwa na nafsi yake basi atakuwa mtumwa wa nafsi yake.

Msomaji anaombwa kusoma makala niliyoyatoa katika Sauti ya Bilal , P.O.Box 20033 DSM juu ya maudhui Maadili ya Kiislamu - sura izungumziayo juu ya sifa 18 za nafsi,Juzuu XXXI, Na. 5, Rabiul Aakhar 1418, Septemba 1997. (Iliyochapwa katika sehemu mbili.)

3. Kujifakharisha

Kwa hakika mtu anapoambukizwa ugonjwa huu basi atambue kuwa ameangamia humu duniani na Aakhera kwa pamoja. Mtu anapenda kujionyesha kuwa yeye ndiye mtu bora zaidi kuliko wengine kwa sababu ya kupata kwa mali zaidi au ilimu au wadhifa. Vitu vyote hivi ambavyo sisi tunavijua kuwa ni vyote vyeneye kuangamia na kupotea na tutaviacha humu humu duniani.

Mtu katika sura hizi anaanza kukufuru kwani anaanza kuwasema na kuwaona watu wenzake kama wanyama na waovu kiasi cha kuthubutu kusema ati wanamsumbua na kumpotezea wakati wake. Inambidi yeye kutambua kuwa Allah swt amemwingiza katika mtihani hivyo inambidi afanye mema ili aweze kufuzu.

D. Uokovu

1. Hofu ya Allah swt katika hali ya dhahiri na batini

Iwapo mtu atataka kupata uokovu inambidi awe na khofu ya Allah swt wakati akiwa peke yake na vile vile anapokuwa mbele ya watu. Isiwe kwamba mtu anapokuwa peke yake anaruhusiwa kufanya madhambi na wakati anapokuwa mbele ya watu kujionyesha kuwa ni mtu ambaye ana khofu ya Allah swt kupita watu wengine. Kutenda madhambi katika hali yoyote yanayo adhabu kali.

2. Kusudio madhubuti katika umasikini na utajiri

Mtu inambidi awe na makusudio yake madhubuti bila ya kuyumbishwa katika hali ya umasikini na utajiri pia. Kwa sababu anapokuwa na moyo wa kuwasaidia watu wenzake katika ufukara asiupoteze katika hali awapo tajiri. Iwapo alikuwa msalihina awapo katika ufukara basi aendelee vile vile kwani asije akatoa kisingizio cha kukosa wakati katika utajiri na biashara zake.

Vile vile mtu anapokuwa katika umasikini inambidi awe madhubuti katika imani yake ili asije akakufuru na kushuku uadilifu wa Allah swt kwa shida azipatazo maishani mwake. Kila mtu anakumbana na misukosuko mbalimbali humu duniani hivyo inambidi kuimarisha imani yake.Huo pia huwa ni wakati wa mtihani kutoka kwa Allah swt, na inambidi ajaribu kufuzu.

3. Uadilifu katika shida na raha

Inambidi mtu awe daima katika mizani ya kauli yake asije akatamka maneno ambayo yatamkufurisha wakati anapokuwa katika shida au raha. Anapokuwa katika shida asije akasema kuwa Allah swt amemtupa au hamjali wala hazisikii duaa zake (Allah swt atuepushe na wakati huo) na pale anapokuwa katika utajiri na starehe asije akakufuru kuwa yeye hana shida ya kitu chochote au mtu yeyote kwani anacho kile anachokihitaji, hivyo kujifanya maghururi na mwenye takabbur. Kwa hakika Allah swt hawapendi watu kama hawa.

Kwa wale walio matajiri inawabidi wafanye mambo mema kwa kutoa misaada kwa misikiti,madrasa masikini na mahala pote pale penye kupata ridhaa za Allah swt na wale walio masikini na mafukara inawabidi wakinai kwa kile walichonacho na wamshukuru Allah swt kwa kile anachowajaalia.

Maneno yetu yawe yamepimwa vyema kabla ya kuyatamka kwani isije tukasema mambo ambayo yatatufanya sisi tuwe mustahiki wa adhabu za Allah swt. Na wala tusiwaseme watu vibaya kwani na hayo pia yatatufanya sisi tuwe mustahiki wa Adhabu za Allah swt.

Hadith hii imesomwa na Sheikh Akmal Hussain kutoka Moshi, Tanzania.

Hadith hii imeshereshwa na: Amiraly M.H.Datoo 8th May 1998

Sehenu ya 2. Marejeo kuhusu Jannat na Jahannam

1. Qur’ani Tukufu

Jannat 11:35, 3:112, 3:113, 10:15, 10:13, 3:111, 10:14, 9:354, 14:119, 15:205, 17:315, 18;375, 18:129, 19:9, 19:123, 19:124, 19:137, 20:218, 20:213, 20:399, 14:83, 14:83, 14:84, 4:18, 4:20, 8:117, 8:123

Maana ya Jahiim j 5 uk. 256;

Jahannam : 11:20, 1:294, 14:357, 15:204, 17:232, 12:178, 18:130, 18:383, 19:141, 20:7, 20:412, 20:438, 8:350, 8:351, 8:352, 8:113, 8:114, 8:115, 20:9

(Namba inayotangulia ni ya Juzuu na inayofuata ni nambari za ukurasa.)

(Marejeo haya ni ya Al-Mizan fi tafsiril Qur’an, zipo juzuu 20. Chapa ya Intesharat Bayan, Teheran, Nasir khosru, Teheran. Jamhuri ya Kiislamu ya Iran)

2. Nahjul Balagha

Hotuba: 16; 27; 28; 64; 66; 79; 83; 157; 171; 167; 160; 75; 109; 106; 119; 120; 124; 128; 12; 144; 152; 156; 193; 176; 165; 183; 192; 191; 193; 199;

Msemo: 199;

Barua: 17; 27; 31; 28; 41; 76;

Wasia: 24

Misemo ya hekima: 31; 368; 228; 349; 387; 429; 456; 131; 42

(Marejeo haya ni ya Chapa ya Sub-hi Salehe, Beirut. Libanon)

Rudi nyuma Yaliyomo endelea