rudi nyuma Yaliyomo  

Ukinaifu ni sifa inayomfanya mwenye kuwa nayo ajitahidi kutafuta maisha yake kwa kadiri ya kutosheleza mahitaji yake tu. Ukinaifu humfanya apange maisha yake kwa kutumia akili na tadbiri na humzuia asiharibu ufanisi wake kwa kuhangaika burebure ili kwamba aridhike na atosheke kwa yale anayoyachuma kwa njia ya halali. Mwendo huu wa

257

kibusara ndio unaompa fursa kujitahidi katika kufikia lengo tukufu zaidi na kufaidika na wema na utu. Ukinaifu peke yake ni ukwasi, kwa sababu mtu anapotosheka moyoni mwake kwa kile anachokipata huhisi hana haja; na utajiri hasa ni kutohitajia.

Amirul Muuminin Ali AS ameashiria jambo hili kwa usemi murua:

"Mtukufu kuliko wote ni yule ambaye hukata tamaa (juu ya watu), hushika ukinaifu na uchaji, na huacha uroho na tamaa, kwani tamaa na uroho ni sawa na umaskini, na kukata tamaa (juu ya watu) na ukinaifu ni utajiri wa dhahiri."

(Ghuram 'l-Hikam, uk 255)

Anayejifanya mtumwa wa tamaa na uchu, huutia maradhi mwili na roho yake. Imam Ali AS amesema:

"Kila mwenye tamaa ni mgonjwa."

(Ghwaru 'l-Hikam, uk 544)

Dk. Marden amesema:

"Kuna baadhi ya fikra pia zinazotokana na tamaa na hisia duni ambazo mbali na kuathiri mwili huathiri nafsi na roho pia. Huleta maradhi, hutuharibia maisha yetu kwa kugeuza mwendo wake, na huangamiza sifa bora kabisa za tabia ya mwanadamu."

(Pinizi Fikr)

Imam Ali AS amesema:

"Tamaa huchafua nafsi, huharibu dini (imani) na huondoa uungwana."

(Ghuram 'l-ffikam, uk. 77)

258 

Mtume Muhammad SAW ametaja matatizo yanayotokana na tamaa:

"Mwenye tamaa husumbuliwa na matatizo saba mabaya: 1) Fikra inayomdhuru mwili wake na isiyomnufaisha: 2) hamu (hima) isiyokwisha; 3) taabu isiyompa raha ila baada ya kufa na wakati wa kupumzika huona taabu zaidi; 4) hofu isiyoacha kumhangaisha; 5) huzuni inayofanya maisha yake machungu bila ya kuwa na faida; 6) hesabu isiyomsalimisha na adhabu ya Mwenyezi Mungu ila asemehewe na Mwenyezi Mungu; na 7) adhabu asiyoweza kuikimbia wala kuiepuka."

(Miistadriku 'l-Wasa'il, jz. 2, uk. 435)

Tamaa ni tabia mbaya sana inayomshawishi mtu afuate tabia mbaya nyinginezo. Imam Ali AS amesema:

"Tamaa humsukuma mtu kwenye mabaya."

(Ghurant 'l-Hikam, uk. 16)

Vilevile amesema:

"Matokeo ya tamaa ni kumtia mtu katika aibu."

(Ghuram 'l-Hikam, uk. 360)

John Markoist ameandika:

"Hali ya kiroho ya mwizi ina matatizo machache zaidi kuliko wahalifu wengine. Huiba kitu asichokuwa nacho na hutamani kukimiliki. Wizi unatokana na tabia ya kutamani na uroho. Mtu mwenye kuwa na wazimu wa kuiba kwa kuiba, kwa mfano, jozi moja ya soksi katika kibanda kimoja cha sokoni, au kuimiliki baiskeli

259

aliyopewa amana, huwa kwa kweli ameingiwa na tamaa ya vitu hivyo. Tabia hiyohiyo ya kutamani ndiyo hasa inayomshawishi kuiba au kufanya hiana."

(Cheh Midanam)

Kwa hivyo, tunafikia hatima hii kwamba ugonjwa wa hatari wa uroho na tamaa hauwezi kupona ila kwa njia ya imani. Na utulivu wa roho na moyo wa kuridhika haupatikani ila kwa kuimarisha nguvu za kiroho na maadili mema.

17 - MABISHANO

263

Ubinafsi Kayaya

Kujipenda au ubinafsi ni mojawapo kati ya naumbile muhimu ya kiroho uliowekwa katika muundo wa dhati ya binadamu ambao daima humwelekeza kufanya hima na juhudi katika maisha yake na kujihifadhi. Kwa sababu hii, huyakimbia mambo yanayomdhuru na huyafuatia mambo yanayostawisha la kuimarisha maisha yake. Sehemu moja ya ukamilifu, utukufu na maendeleo ya mwanadamu imefadhiliwa na ufahari huohuo wa kinafsi; na utashi huu wa asili una athari muhimu katika mfumo wa maisha na katika kuendeleza ustaarabu wa wanadamu.

Lakini mtu huweza kupata ufanisi anapoyaangalia natamanio yake kwamba hayazoroti wala hayatii fora, na wala hayasalimu amri mbele ya silika yake. Kwa livyo, ili kuridhisha matakwa yake ya kinafsi kwa njia inayofaa na kupevua hulka na maadili mema, inabidi iweke mizani katika akili yake. Silika ya mtu si mwongozo wake, bali nguvu ya akili ndiyo inayoweza kukabiliana na matakwa ya kinafsi yaliyopindukia, na kuzuia uasi wa silika haribifu. Akili inatufanya sisi tuweze kuutambua ukweli kwa kutupambanulia baina ya njia sahihi na potofu. Akili ambayo ina wajibu mkubwa wa kujenga shakhsia ya mtu, inarekebisha pale palipopotoka na hutupa nguvu nyingi za kuchunga mienendo yetu.

Silika ya ubinafsi inapotoka kwenye njia adilifu na

264

ya kati na kuelekea upande mwingine kupita kiasi, huharibu mfumo wa akili na tafakuri, na huyafanya maendeleo yawe na ukweli wa maisha usiweze kutambulikana. Watu waliopatikana na upotofu huo wa kiroho na wakajitahidi kuyapata matakwa yao yasiyokuwa ya wastani, mwisho wao huwa ni kutumbukia katika jalala ya mashaka na ufisadi. Mabaya yote yanayotokana na ubinafsi yanasababisha kuzidi kwake bila ya kiasi na kutoka kwenye njia ya kati.

Kupanda au kuanguka kwa shakhsia ya mtu kunahusiana moja kwa moja na hali yake ya kiroho na kimaadili. Upotevu wa kimaadili ulitapakaa kwa sura mbalimbali katika vipindi vya maisha, na vilevile sehemu kubwa ya mashaka na matatizo ya kimaisha imesababishwa na makosa na maelekeo yetu yaliyoruka mipaka.

Ingawa kiwango cha uwezo wa mwanadamu ni kikubwa mno na kila mtu ana fursa nzuri ya kuyaelekeza kwa busara matamanio yake ya asili, lakini hakuna kitu chochote kilicho muhimu zaidi kwa mtu na kwa wakati huohuo kikawa kigumu zaidi kama kuidhibiti hisia yake ya ubinafsi isizidi kupita kiasi.

Kwa hivyo, ni lazima tujitahidi zaidi kusawazisha hali hiyo ya kinafsi, kwa sababu kujipenda na kujiona kunapotia fora, huwa hayumkiniki kupatikana maendeleo yoyote ya kimaadili na huwa ni muhali kupatikana mafanikio ya maisha kama hakuna nidhamu ndani ya moyo.

265

Tunapata Faida Gani Kubishana?

Mafanikio yetu ya kimaadili na kijamii yanategemea msingi ambao ni lazima tuujue, na tuupange mwendo wetu kufuatana na msingi huo. Nafasi ya mtu katika uhusiano wake na watu wengine, na kutambua masharti ya majukumu yake ni miongoni mwa masuala ambayo yanahusiana kwa kiwango kikubwa na kufanikiwa au kusumbuka kila mtu.

Katika kiini cha moyo wa kila mtu mna umbile la kutaka kupendana na kusikilizana na wengine. Kila mtu anapenda kuishi kwa masikilizano na wengine na anachukia kifungo kiza na roho ya ukiwa. Lakini ikiwa mtu hana roho tulivu wala moyo safi, hayumkiniki akaweza kusikilizana na watu wengine au hata akaweza kusikilizana na nafsi yake mwenyewe!

Amani na ushirikiano ni msingi muhimu kwa aina yoyote ya maisha ya kijamii. Sharti la kwanza kabisa la kuwepo upendano na masikilizano ni kuheshimu hisia na haki za watu unapoingiliana nao. Jambo hili ndilo linaloimarisha na kudumisha uhusiano kati ya kila mtu. Watu wasiokuwa na sifa kama hii husababisha kuvunjika masikilizano kati yao na kila mtu katika jamii, huregeza nguzo ya urafiki na upendo, na wala hawawezi kuhifadhi uhusiano wao na watu wengine katika hali inayokubalika.

Tabia mojawapo iliyo mbaya ambayo inaumiza sana ufungamano wa kirafiki na umoja kati ya watu ni ugomvi. Mgomvi hajui chanzo cha mwendo wake

266

mwovu, wala kitu gani kilichoathiri sana hisia zake na kuuchafua moyo wake. Lakini ni lazima aelewe kwamba ubinafsi wake uliopita kiasi ni miongoni mwa vitu muhimu vilivyozalisha tabia hiyo mbovu. Kwa kawaida, mmea wa ugomvi hukua kwa kutiwa na kushibishwa maji ya ubinafsi.

Mtu mkaidi na mbishi anapohudhuria katika mkutano wowote na anaposikia maoni yoyote yanayotolewa, huanza kubisha hapohapo bila ya kutaka kufahamisha au kusahihisha makosa yoyote, kwa sababu ubinafsi na ghururi humghasi moyoni mwake. Ni tabia ya mbishi kumpinga na kumbomoa msemaji bure bilashi, na kumtuhumu ujinga na kusema mapiswa, ili ajionyeshe kuwa ni bora kuliko wengine wote. Wakati mwingine huficha sura yake mbovu ya ubishi chini ya kisingizio cha kuuliza maswali, kukosoa au kusahihisha.

Mtu mwenye ukaidi kama huo hawezi kuamua kwa haki na huwa haogopi kumnyima mtu haki yake au kudhulumu. Haifai kudharau radiamali ya mkaidi au mbishi ambaye hadhi yake imedharauliwa, kwa sababu itambidi baadaye atakapopata fursa nzuri atumie nguvu zake kulipiza kisasi cha kudharauliwa kwake. Kuenea kwa sifa hii mbaya kati ya taifa moja huvunja umoja wa kifikra na kiitikadi na huleta mizozano isiyomalizika kati ya watu ambayo madhara yake hayawezi kurekebishwa kwa urahisi.

Mwanachuoni mmoja ameandika:

"Akili ni taa inayoangaza ambayo humwongoza mtu katika giza la ujinga na humwondoshea matatizo yake. Sisi daima tunajivunia kwamba tuna akili ambayo

267

hutujulisha vyanzo vya vitu vyote na uhusiano kati yao. Lakini ole wetu tukitaka kufichua ukweli kwa kubisha na kukaidi. Mashindano na mabishano hayaleti faida yoyote isipokuwa majuto na fazaa. Faida ya pekee ni kudhihirika ujinga na makosa ya pande mbili tu, lakini hayawezi kabisa kugeuza fikra za wengine na kuwafanya wazifuate fikra zao."

Tuzingatie Maneno ya Viongozi wa Kiislamu

Uislamu umezingatia vipengee vyote vya maisha ya kijamii na umechunguza kwa makini kabisa mambo yote yanayoleta na kuimarisha umoja na mapenzi, na umekataza kwa ukali kila jambo linalosababisha utengano kati ya Waislamu na kuregeza nguzo za masikilizano. Viongozi wa kidini huwafunza wafuasi wao wafuate mwendo wa usafi na ukweli na wazisafishe nyoyo zao kutokana na kila aina ya uchafu.

Mtume Mtukufu amesema:

"Miongoni mwa (alama za) uungwana ni mtu kunyamaza kimya na kumsikiliza ndugu yake anaposema."

(Nahju 'l-Fasahah, uk. 633)

Imam Baqir As amesema:

"Na jifunze kusikiliza vizuri kama vile unavyojifunza kusema vizuri, wala usimkatize mtu yeyote anaposema."

Viongozi wa Kiislamu wamekataza mara kwa mara tabia ya kufanya ugomvi, kwa kuwa matatizo yote na

268

misukosuko yote inasababishwa na tabia hiyo; na hata wamepiga marufuku kuzozana katika masuala ya haki.

Imam Sadiq AS amesema:

"Mja hataipata imani halisi mpaka atakapoacha ubishi hata kama ni haki."

(Safinatu 'l-Bihar, jz. 2, uk. 522)

Hakuna atakayetoka katika uwanja wa mabishano na ushindani akiwa mshindi, wala hakuna atakayemshinda mwenziwe katika mzozano huo.

Imam Hadi AS amesema:

"Ubishi huharibu urafiki wa muda mrefu, huvunja uhusiano ulio madhubuti, na sehemu ndogo ya kitu kinachopatikana ni mashindano—na mashindano yenyewe ni chanzo hasa cha kutosikilizana."

Dk. Dale Carnegie ameandika:

"Kati ya majadiliano kumi, washindani hutoka katika majadiliano tisa wakizidi kuamini fikra zao na kujifikiria wao wako katika haki. Hakuna mshindi yeyote katika mashindano hayo, kwa sababu ikiwa mmeshindwa basi ndiyo mmeshindwa tu, na ikiwa mmeshinda, pia huwa mmeshindwa. Vipi? Tuchukulie kwa mfano kwamba umeweza kumshinda mshindani wako na kumthibitishia kwamba yeye ni mjinga. Baadaye? Utapiga makofi na kushangilia kwa furaha. Lakini fikiri mshindani wako atakuwa katika hali gani? Ushindi wako umeweza kumfanya ahisi unyonge na ujinga wake na kuuumiza ubinafsi wake na kumtia uchungu moyo wake. Kushindana si mbinu ya kusadikisha. Viwili hivi- yaani kushindana na kusadiki-

269

havihusiani kabisakabisa. Mbinu ya kuwavuta watu katika fikra zako ni ghairi ya hiyo. Kutoelewana hakuondoki kwa kushindana na kugombana, bali ni lazima zitumike hekima, maarifa, siasa na tabia ya kupenda masikilizano. Vilevile inabidi mtu ajifikirie kwamba ikiwa yeye atakuwa katika nafasi ya mshindani wake atafanya nini?"

(How to Win Friends and Influence People)

Mtume Muhammad SAW amesema:

"Acheni kubishana, kwani manufaa yake ni machache na huchochea uhasama kati ya ndugu."

Bwana Auibury amesema"

"Mara nyingi mabishano na majadiliano hayatoi faida nzuri, kwa kuwa mshindani mmoja hubadilisha nia yake wakati hamaki inapompanda moyoni mwake anaposhindana, ingawa anaposema hujitahidi kutulia. Isitoshe kila tukijitahidi kumshinda mpinzani wetu, yeye huzidi kubisha. Katika hali hii huenda likamtoka tamko kali ambalo likaharibu urafiki daima. Kwa upande mwingine, hatuwezi kuwaridhisha wengine wakafuata fikra zetu kwa kushindana tu."

(DarJostojue Khoshbakhti)

Mbishi hawezi kuona raha moyoni mwake bali hukereka siku zote.

Imam Sadiq AS amesema:

"Epukaneni na mabishano, kwani huunguza moyo, huleta unafiki na husababisha chuki."

(Usulu 'l-Kafi, jz. 1, uk. 452)

270

kwa hivyo,tukiyafuata mafundisho matukufu ya dini ya kiislaam, tutaweza kuleta mabadiliko ya kimsingi katika sifa na hali za kiroho na tukafuata kwa dhati misingi bora ya ubinadamu na madili mema.

MSAMIATI

Maana ya maneno magumu yaliyotumika humu

 aali:  ahali ya juu

amiliana:  tendeana

anuwai:  namna kwa namna

asteaste:  kwa taratibu

baathi:  pewa utume

barakala:  mtu mwenye tamaa ya cheo

bariziana:  kabiliana katika vita

bidhaa:  matokeo mbay ya kitendo au hali

chumu:  bahati njema

dariji:  weka kwa mpango

dhaa:  ukosefu wa raha moyoni au akilini

ghaya:  upeo

ghera:  moyo wa kufanya jambo; ari

ghiba:  usengenyaji

ghusubu:  chukua kwa nguvu

hadi:  ukomo

hawili:  hamisha

hududi:  adhabu kuu za kiislam

hulka:  tabia au mwenendo wa mtu

iktisadi:  wastani

irada:  azma; kusudio

itibari:  muamana

kaida:  msingi; utaratibu

kauleni:  mnafiki

kayaya:  kupita kiasi

272

niiiadn:  meta; kitu ki.sichokuwa roho

maadili:  mwenendo mwema; tabia; elimu ya wcma na ubaya

nianmuma:  mlu asiyekuwa msomi wala mwanachuoni

majojo:  malata juu ya malata

rnnnliki:  ulumiaji sahihi wa akili

mapiswa:  maneno yasiyo na maana

muamana:  liali ya kuaminiana; uarninifu

ndumakuwili:  mnafiki

ndweo:  kiburi; majivuno

nyonda:  mapenzi

radiamali:  marudio au jawabu ya amali iliyotendwa

rughba:  hali inayompa mtu hamu au kuvutika na jambo fulani

ruliani:  enye asili ya roho

saiida:  bahati njeni.i; ufanisi

sliamirl:  'enea

shakhsia:  haiba, hadhi

ladbiri:  uendeshaji mzuri wa jambo

tiihinl:  jahbu

tatiaruki:  utovu wa ululivu na makini; mbabaiko

lashwishl:  hali ya kulokuwa na uhakika au makini

Ihakllisha:  pa laabu, mashaka au dhiki

tuluo:  hali ya kulokuwa na subira

ufanisl:  hali ya kupatikana kwa mafanikio; ustawi; saada

uklmwa:  ucliovu wa kufanya kitu kimoja kila siku

ukuba:  nuksi; baa

usongombwingo:  unafiki

ulashl:  liali ya kuwa na hamu ya kulaka

ullmbalcwlri:   u&alili

uzandiki:  unat'iki

uzlmbezimbe:  uvivu

wenzo:  (nyenzo) kitu kinachorahisisha kazi

dgizaga:  ovyoovyo

rudi nyuma Yaliyomo