Yaliyomo endelea

UCHUNGUZI WA MATATIZO YA KIMAADILI NA KINAFSI

Sayyid Mujtaba Musawi Lari

Mfasiri : Sayyid Muhammad Ridha Shushtary

Kwajina la Allah, Mwingi wa rehema, Mwenye kiirehemu

DIBAJI

Tunawajua watu au makundi ya watu ambao wanaonekana wakiishi katika mazingira yanayofanana, lakini wakati mwingine tunamwona mtu mmoja kati yao au taifa moja likifanya maendeleo ya haraka kwa kadiri ya kuwashangaza watu wote.

Maamuma wasiozoea kufikiri wanaposhindwa kupata majibu ya maswali kama hayo hutoa kwa haraka kisingizio cha "bahati", "nasibu", "sadfa", n. k. Wanapoona mambo hayo, husema: "Mungu atupe bahati!" au "Angalia sadfa hiyo!" au "Ajabu! Katika dunia hii hakuna kitu kinachotokea kwa sharti la kingine!"

Tukiangalia kwa makini tutaona kwamba hakuna bahati wala sadfa wala utovu wa sharti katika matukio hayo, bali nyuma yake kuna ushindi na mafanikio, au kushindwa na kutofuzu. Kuna sababu na misingi tofauti katika kila jambo, lakini mojawapo kati ya misingi muhimu ni "msingi wa kimaadili."

Kwa mfano, nchi ya Ujerumani ambayo baada ya Vita Vikuu vya Pili vya Dunia iligeuzwa kuwa jivu na vifusi, leo imekuwa ni nchi kubwa ya viwanda na iliyojengeka vizuri. Wataalamu wanasema kwamba

12

Wajerumani si watu wenye akili nyingi kuliko sisi wala hawana vipawa vya ajabu kuliko watu wengine, lakini sababu kuu ya kuendelea kwao ni kule kuwa na nidhamu na utambuzi wa wajibu ambao umekuwa ni tabia ya taifa zima.

Hapa tunaona waziwazi athari ya msingi wa kimaadili katika kuendeleza taifa moja. Tunaweza kusema kwamba kila maendeleo ya kiteknolojia waliyoyapata yanatokana na msingi huo.

Bila shaka, huu ni mfano mmoja mdogo unaohusiana na mafanikio katika sehemu moja tu ya maisha. Huenda zamani uhusiano baina ya maadili na maisha ya kijamii ulikuwa haufahamiki sana, lakini leo athari ya msingi wa kimaadili katika muundo wa maisha ya mataifa unaonekana waziwazi kwa kadiri kwamba hakuna shaka yoyote juu ya suala hilo.

Kwa upande mwingine, msingi wa shakhsia ya kila mtu umesimama juu ya thamani, sifa na hulka yake. Mtu mwenye hulka njema na sifa bora anastahiki kuitwa mwanadamu, na bila ya kuwa na sifa hizo huwa ni mnyama tu.

Sehemu kubwa ya thamani ya ubinadamu inapatikana katika maadili mema. Tusisahau kwamba sifa hii tukufu ya kiutu inaweza kupatikana kwa ukuzaji roho na malezi maalumu ya kinafsi na kimaadili. Kwa sababu hii, wanasaikolojia na wataalamu wa elimu ya maadili wamejadili kwa urefu jinsi ya kuzuia na kupambana na ufisadi wa kimaadili na namna ya kukuza sifa na tabia njema na tukufu; na kwa mara

13

nyingi wamesisitiza upande wa kimatendo.

Viongozi wakuu wa dini yetu ambao walikuwa ni walimu na walezi bora kabisa wa maadili ya wanadamu wametoa mwongozo mkubwa kwa ajili ya kukuza tabia njema. Vivyo hivyo, mwendo wa maisha yao umejaa mafunzo bora kabisa ya kimatendo ambayo tukiyafuata tunaweza kuwa ni watu wenye furaha na hadhi kubwa.

Kuna watu wengi wanaoteseka nafsi zao kwa sababu ya tabia zao mbaya na wanashindwa kupata dawa yake. Jambo hili linawahusu zaidi vijana, hasa wale wanaoishi kwa ujeuri na ujuba.

Kwa bahati mbaya, hakijaandikwa kitabu kizuri, kamili na chenye faida ambacho kingeweza kuwa ni mwongozo wa kifikra na kimatendo kwa vijana, na kama kipo, hakijaandikwa kwa lugha ya kisasa. Nafasi ya maudhui hii ni tupu. Hivyo, tulifikiria kutoa kitabu kizito kuhusu suala hilo kwa ajili ya vijana.

Kwa bahati nzuri, tumefanikiwa kutoa kitabu hiki ambacho kinachungua masuala muhimu ya kimaadili kwa kutumia mbinu mpya na kwa kuzingatia msingi wa elimunafsi ya kisasa. Jumuia ya Elimu Kuhifadhi Kizazi Chipukizi imechukua jukumu la kukichapisha na kukitangaza (chapa ya kwanza kwa lugha ya Kiajemi).

Vilevile kitabu hiki kimeandikwa kwa lugha safi na tamu na kinaweza kufahamika na watu wote, na kwa wakati huohuo kina uzito wa kitaalamu. Tunawakaribisha wale wote wenye hamu ya kurekebisha jamii wakisome kitabu hiki kwa makini na wakitumie katika jitahada zao za kupambana na ufisadi wa kutisha

14

ulioenea katikajamii hii ya leo.

Sisi tunawausia zaidi vijana watukufu wakisome kitabu hiki kwa kuwa wao wana fursa kamili ya kukuza sifa bora za uungwana, sifa ambazo huenda zikawapa mafanikio na fakhari kubwa katika maisha yao yote.

Jumuia ya EIimu Kuhifadhi Kizazi Chipukizi

Qum (Iran) 1387 Hijria (1966)

17

UTANGULIZI

Kila mtu katika dunia hii hutaka ufanisi na raha, na huhangaika usiku na mchana katika uwanja wa maisha kutafuta mahitaji yake. Katika uwanja huo ambao unafanana na uwanja wa vita, huendelea na juhudi zake hata kufikia mwisho wa uhai wake, akitaraji kwamba siku moja ndege wa bahati atamtandazia mabawa yake na ataweza kupitisha umri wake mfupi kwa raha na starehe chini ya kivuli chake.

Ni jambo la kusikitisha kuona kwamba licha ya watu kuwa na uwezo na suhula zote ambazo dhahiri yake huridhisha maisha yao, hata hivyo kuna mambo yasiyofahamika ambayo daima husumbua na hukera roho zao kwa kadiri kwamba huwa ni muhali kwao kupata ufanisi halisi. Mwisho wake, watu kama hao huchukuliwa na mawimbi ya machafuko na mashaka, huvunjika nyoyo zao, hujuta na huanguka katika bonde la umaskini.

, Kushindwa na kutofanikiwa huko kunatokana na tabia yao ya kupendelea ndoto badala ya uhakika na kupita katika njia kiza ya maisha bila ya kutumia taa inayong'ara ya akili na maarifa ambayo humwongoza binadamu katika kiza. Ndoto na mawazo ya namna kwa

18

namna wanayowazia watu huwaendesha mrama katika bahari iliyochafuka kwa mawimbi makali; na malengo duni na matarajio yasiyo na kikomo yanayotoka katika fikra zao yanakomea katika kiza totoro cha mashaka na huishia katika ukingo wa misukosuko.

Binadamu ambaye ni kiumbe bora kabisa Katika ulimwengu huu, ameumbwa akiwa na nguvu mbili zilizo bora-nguvu ya kimakanika na nguvu ya kiroho (kinafsi)-Tukiweka mbali mambo ya kimaada na sifa zinazolingana na wanyama wengine, binadamu ana mahitaji mengi ya kiroho ambayo yanapokidhiwa humfikisha kwenye ghaya ya ukamilifu. Wakati wowote nguvu mojawapo inapokuwa na nguvu zaidi kuliko ya pili katika dhamiri ya mtu, basi nguvu ya pili hudhoofika na hushindwa tu.

Katika ulimwengu wa leo, maendeleo ya kisayansi na kiteknolojia yamebadilisha sura ya maisha ya wanadamu. Maendeleo ya kiteknolojia yaliyoleta mabadiliko ya ajabu katika vipengee vyote vya maisha, yameyafumbua macho na kuyatatua matatizo mengi. Maendeleo ya binadamu yameenea katika ulimwegu mzima, kutoka katika kina cha bahari hadi upeo wa mbingu. Lakini udhaifu wa misingi ya imani na uchaji umekwenda sambamba na maendeleo ya kisayansi kwa sababu ya kuzingatia nguvu na fikra zote juu ya mambo ya kidunia tu. Kutokana na kuwepo hali hiyo, ufisaidi kila aina umepenya katika kila sehemu ya jamii, na idadi ya uhalifu, jinai, uvunjaji wa sheria na vitendo dhidi ya ubinadamu imezidi kwa kiwango kikubwa sana. Mambo yanayoleta ufanisi na urekebishaji katika Jimii

19

yamepiga magoti mbele ya rnadhihirisho ya ufisadi na ufasiki. Mabaki ya kiroho pia yanaunguzwa na kuangamizwa na moto wa tamaa za kinafsi za watu na sifa chafuchafu!

Tunaona waziwazi katika ulimwengu wa leo kwamba mambo yasiyo na maana yanapewa umuhimu zaidi kuliko maadili mema. Binadamu amejizatiti kwa nguvu bora kabisa ya kitaalamu, lakini malaika wa maadili mema ambae anapaswa kuilinda roho, anakandamizwa na matamanio maovu, na hisia za kibinadamu ziko katika hali ya kukata roho baada ya wema kufa.

Uwongo, uroho, unafiki, udhalimu, utimbakwiri na tabia mbaya nyinginezo ambazo kila moja imeweka kizuizi katika njia ya ukamilifu, utukufu na ufanisi wa binadamu, zimeifunga mikono na miguu ya watu na kuichafua sana jamii. Kuvunjika nguzo zinazosimamisha maadili mema na kuangamia hisia ya kutenda mema kumesababisha kutokeza kila aina ya masaibu na masumbuko na kumvama kila mtu na jamii nzima. Huu ni ukweli mchungu kwamba ikiwa binadamu wa sasa atanyimwa manufaa ya kimaada, basi hatakuwa na kitu chochote cha kukitegemea katika ulimwengu huu mkubwa. Akikosa  kitu kidogo tu huvunjika moyo wake, hukata tamaa na kupoteza nguvu za kiroho za kuvumilia. Wataalamu wa elimu ya maadili na elimunafsi huamini kwamba ubinadamu wa mtu huthibitika na kufikia kilele cha utukufu wakati anapokuwa na roho bora na maadili matukufu, na

20

wakati unapokuwepo aina maalumu ya usawa kati ya sifa na hisia zake. Rasilimali ya kiroho na kimaadili humzuwia mtu asipotoke, humtukuza na humfikisha kwenye kilele cha ukamilifu anao ustahiki.

Katika jamii mbalimbali za wanadamu, walitokeza watukufu ambao majina yao ya fakhari yalisajiliwa katika historia ya wanadamu kwa heshima kubwa kutokana na kuwa na fadhila za kiroho na maadili mema. Jamii isiyojizatiti kwa silaha nzuri za kimaadili na isiyotawaliwa na mafundisho ya kibinadamu katika mazingira yake, haistahiki kuendelea kuishi. Kuangamia kwa ustaarabu mkubwa na mataifa hakukutokana na kuzoroteka hali ya kiuchumi peke yake, bali sababu hasa ya kuangamia jamii hizo ni kuharibikiwa na hazina za kiroho na kimaadili. Kuregea kwa misingi ya kiroho na kimaadili kunaleta maangamizo makubwa kwa jamii kuliko mtetemeko wowote mwingine.

Sheria na mifumo ya wanadamu havikuweza kabisa kuvama katika roho za wanadamu na kuunda umoja na uhusiano wa kiroho kati ya watu wa jamii, mataifa na makabila mbalimbali. Sheria zilizotungwa kufuatana na fikra za wanadamu hazifai kabisa kumpatia mtu ufanisi wa kila aina kwa sababu ya kutegemea elimu ndogo, kutodhibiti uhusiano wa matokeo na kuathirika kwake na mambo mengineyo. Hivyo, sheria hizo huwa ni za muda tu na hubadilika kila sura ya jamii inapobadilika katika zama mbalimbali. Kwa hakika, kutokeza ufisadi na michafuko ya kila aina ambayo imewatatanisha na

21

kuwasumbua wanadamu, ni matokeo ya upungufu na kutokamilika kwa sheria na taratibu hizo za wanadamu.

Kwa upande mwingine, kuna dini takatifu ya Mitume ambayo inapata ufunuo wake kutoka chemchemi tukufu ya Mwenyezi Mungu na inategemea maarifa yasiyo na kikomo ya Mwenyezi Mungu. Dini hii imehifadhika kutokana na tufani ya mabadiliko na mapinduzi, na kwa sababu ya kuelewa uhusiano wa matukio na uhakika wa ulimwengu, imewaonyesha watu ratiba bora kabisa ya sera ya ukamilifu. Vilevile imewapangia watu ratiba ya kusafisha na kurekebisha nafsi zao na kuelekea kwenye utambuzi mkuu wa kinafsi. Hakuna mtu anayekataa umuhimu wa mafundisho ya dini, matokeo yake yanayomeremeta na athari yake ya haraka na kubwa katika mfumo wa jamii. Ikiwa katika dhati ya mtu mtakosekana mahakama, nyenzo za kuzuia matamanio na hisia ya kutambua wajibu, basi hapana shaka kwamba hatua yoyote ya kurekebisha nafsi itashindwa tu. Kwa hivyo, hayumkiniki kujenga ustaarabu kamili na kuleta mazingira ya amani na ufanisi katika jamii bila ya kuwekwa rasilimali ya kiroho na kimaadili.

Msingi wa dini ya daima ya Kiislamu- iliyoletwa na mwenye shakhsia na tabia bora kabisa katika historia  umesimamishwa juu ya imani na uchaji. Dini hii, mbali ya kuwa ni njia ya kumpatia mtu ufanisi wa Akhera, ni msingi wa furaha na utulivu katika maisha ya dunia hii pia. Shabaha ya mwito wa Uislamu ni kutukuza thamani ya binadamu na kustawisha itikadi safi na maadili yake mema. Uislamu huzitambua sifa

22

njema za kiroho na mwendo safi wa binadamu kuwa ni kipimo cha ubinadamu. Uislamu unapinga kufidiwa rnema kwa ajili ya matamanio ya nafsi na kupewa mgongo mambo ya kiroho. Unapambana vikali na wale watu wanaotia doa ubinadamu na heshima, na wanaodhoofisha msingi wa kuaminiana na kuelewana. Jamii iliyopangiwa uhusiano wake na Uislamu, watu wake huishi kwa mapenzi na amani, na huwepo moyo wa kuaminiana katika mambo yao yote. Usawa na uhusiano wa hali ya juu kabisa ndio unaowaunganisha watu wa jamii hiyo, na wote huwa ni sawa mbele ya sheria. Ikiwa jamii itakuwa na sifa kama hizo, basi umoja wa kiroho, mafundisho na taratibu za ukamilifu vinaweza kuleia mapinduzi makubwa ya kitabia katika mataifa na makabila mbalimbali ambavyo vitadhamini ufanisi na mafanikio katika vipengee vyote vya maisha.

Kitabu hiki kinazungumzia masuala ya kimaadili na kinaangalia mafundisho matukufu ya dini ya Kiislamu juu ya maadili.

Ingawa vitabu vya zamani vilivyoandikwa na wakubwa wetu kuhusu maadili ni hazina ya thamani kwetu, lakini kutokana na kupita kipindi kirefu tangu vichapishwe, vimekuwa havivutii tena; isitoshe, vitabu hivyo vilitumia. kaida za kinadharia ambazo hazitumiki sana sasa.

Mwandishi amejaribu kuichungua maudhui ya maadili kwa kutumia lugha ya kisasa na inayovutia.

23

Vilevile katika kujadili suala la tabia, ameyachungua baadhi ya masuala yanayohusiana na nafsi na adabu. Ameyanakili maoni ya kitaalamu ya wanavyuoni wa sasa wa nchi za Magharibi na kuyalinganisha na mafundisho ya viongozi wa kidini waliyotoa.zaidi ya karne kumi na tatu zilizopita.

Baadhi ya sura za kitabu hiki zilichapishwa katika gazeti zuri la kidini liitwalo Maktabe Islam. Mtungaji hana haja ya kuelezea umuhimu wa mambo yaliyojadiliwa humu. Tunawaachia wasomaji watukufu wenyewe waamue hilo watakapokuwa wakisoma maoni ya baadhi ya wataalamu katika kitabu kama hiki cha maadili ambacho kinatumia mbinu maalumu na mpya kabisa. Tunataraji kwamba sote tutazingatia nasaha zenye thamani za viongozi wa Kiislamu na wanavyuoni wa elimu ya maadili ili kwazo tuweze kupiga hatua za haraka katika kurekebisha nafsi zetu na kuzizuia zisiharibike na tuweze kupata mafanikio, ufanisi na raha halisi.

Sayyid Mujtaba Musawi Lari Aprili 1966 Qum

1 - HULKA MBAYA

27

Thamani ya Urafiki na Mapenzi

Kufanya urafiki ni mojawapo kati ya mahitaji ya asili katika maisha ya binadamu. Kufuatana na ukweli huu, kuna nguvu ya ndani inayomfanya mtu awapende watu wengine. Haiwezekani kupambana na haja hiyo ambayo ni hisia ya kimaumbile. Kwa hivyo, ni lazima kukidhi haja hiyo. Kila mtu huanzisha uhusiano wa kirafiki na kikundi cha aina yake, na hufaidika na uelewano wao.

Urafiki ni chimbuko la utulivu na ni mojawapo kati ya ladha bora kabisa ya roho. Baada ya kupita muda tangu kuanza, urafiki hustawi na hukamilika. Katika dunia hii iliyo pana, hakuna kitu kilicho na thamani zaidi kuliko urafiki.

Taabu ya kukosa rafiki na upweke huleta mashaka makubwa kwa mtu. Ikiwa ufungamano wa kimapenzi hautaweza kufungamanisha roho zetu na za wengine, na ikiwa wengine hawatapokea roho zetu kwa mikono miwili, basi bila shaka tutafazaika na kuwa na wasiwasi, na maisha yetu ya dunia yatakuwa ya dhiki na kiza. Mwanachuoni mmoja amesema:

"Siri ya ufanisi ni hii, kwamba uhusiano wetu na wengine uwe wa mapenzi badala ya uhasama. Ikiwa mtu hawezi kufanya urafiki na watu wenye tabia nzuri, basi hataweza kabisa kuishi bila kuwa na fazaa!"

Uhusiano ambao unaunganisha jamii katika sura bora kabisa unategemea msingi wa "kuwa na moyo

28

mweupe, upendo na mahaba." Mivutio ya roho mbili katika vitu vilivyo muhimu sana ndiyo inayoleta uelewano na mapenzi baina ya watu wawili; na kwa njia hii, husimama nguzo ya urafiki wenye heri na fanaka. Hata hivyo, ili kudumisha urafiki, ni lazima mtu aweke kando tofauti zake na asikilizane na wengine katika baadhi ya mambo ambayo wanayapinga kabisa.

Urafiki wa maana kabisa ni ule ambao hautokani na maslahi ya kibinafsi, bali unaambatana na hisia za kindugu na ule ambao unaweza kuridhisha roho ya mtu inayohitaji mapenzi na utulivu. Mtu anayejitambulisha mwenyewe kama ni rafiki mwaminifu, asikubali kuruhusu jambo lolote liharibu hisia zake juu ya rafiki yake, bali kwa hakika anatakiwa ajitahidi kuondoa matatizo na maumivu yanayomchoma moyo wa rafiki yake, na ampatie moyo wa matumaini na utulivu. Wale wanaowatarajia watu wengine kuwafanyia wao mapenzi, wao wenyewe waonyeshe hisia zao za mapenzi. Mwanachuoni mmoja amesema:

"Maisha yetu ni kama eneo la milima ambapo ikiwa patapigwa ukelele mmoja, mtu atasikia mwangwi wake ukirudi kwake; hivyo, wale waliojawa na mapenzi ya wengine katika nyoyo zao, wataona hali kama hiyo kutoka kwao. Ni kweli kwamba maisha yetu ya kidunia yamesimama juu ya mabadilishano na malipano. Hatutaki kusema kwamba maisha yetu ya kiroho pia yamesimama juu ya msingi huohuo, lakini vipi inayumkinika kutaraji kuona uaminifu kutoka kwa wengine bila ya wewe mwenyewe kuwa mwaminifu kwao? Na vipi mtu atake apendwe ne wengine bila yeye

29

mwenyewe kwanza kuwapenda wao?"

Kutendeana na wengine kunaweza kuleta madhara sana kama pande zote mbili zisitendeane juu ya msingi wa mapenzi na uaminifu.

Ikiwa unafiki utadhibiti nyoyo na maisha ya watu;

na ikiwa majivuno na majisifu yatachukua nafasi ya uaminifu na urafiki; uelewano na wema utadhoofika na moyo wa kushirikiana utatoweka katika jamii.

Bila shaka wengi kati yenu mnakutana na kuingiliana na watu ambao nyoyo zao hazina mapenzi ya kweli wala hisia njema, lakini wanajionyesha mbele yenu kuwa ni marafiki na wapenzi wenu. Mara nyingi mnaweza kuzitambua nyuso na hisia zao za ndani; na kutokana na maingiliano hayo, mnaweza kuzifunua nyuso hizo mbele yenu.

Kwa hakika, mojawapo kati ya masharti ya kupatikana furaha na ufanisi, na mbinu inayofaa ya maendeleo ya kiroho ni kuwa na urafiki wa kikweli na watu wema na wanyofu. Hii ni kwa sababu fikra za mtu binafsi hukua kuambatana na urafiki kama huo, ambapo roho hupanda kwenye daraja za unyofu na tabia aali. Kwa hivyo, ni lazima kumchungua mtu kabla ya kumkubali kuwa rafiki yako. Ni kosa kubwa kufanya urafiki na mtu yeyote kabla ya kuhakikisha uaminifu na unyofu wake, kwa sababu binadamu ameumbwa mwepesi wa kufuata tabia za wengine kutokana na maingiliano kati yao. Uhusiano usiofaa ni hatari na tishio kwa ufanisi wa wanadamu.

30

Hulka Mbaya Husababisha Chuki

Baadhi ya tabia na hulka zisizotakikana hudhoofisha misingi ya mapenzi, na wakati mwingine husababisha kuvunjika uhusiano mzuri kabisa. Watu wakali ambao hawawezi kuhifadhi mapenzi yao juu ya wengine, hujenga ukuta mgumu baina yao na jamii ambao huwazuia wasione mwanga wa mahaba. Kwa hivyo, tabia mbovu huharibu msingi wa furaha na hushusha thamani ya mtu.

Hakuna anayekataa kwamba tabia mbaya huwatenganisha na kuwaweka watu mbalimbali, kwa sababu mtu mzuri huchukia kufanya urafiki na mtu mbaya mwenye tabia mbovu. Hivyo, tabia mbaya huwalazimisha wapoteze suhula nyingi ambazo zingekuwa na manufaa makubwa kwa ajili ya maendeleo ya maisha yao lau wangelikuwa na tabia njema na wenye adabu.

Ni lazima kwa yule mtu anayetaka kuingiliana na jamii, kwanza ajifunze sanaa ya maingiliano, kisha akishaijua barabara, afuate kimatendo kufuatana na adabu za kijamii zinazokubaliwa. Bila ya njia hii, mtu hawezi kuishi kwa masikilizano na jamii yake, wala mwendo wake hauwezi kukamilika katika jamii hiyo. Kwa hivyo, mwendo mwema ni msingi mkuu wa furaha na ufanisi, vilevile, ni jambo muhimu katika kuboresha shakhsia na hadhi ya mtu.

Kwa hakika, mwenendo mzuri humwezesha mtu atumie vipawa vyake na kuweza kufaa katika kiwango

31

chote cha uendeshaji na ustawi wa jamii na maisha. Hakuna mwendo wowote ulio sawa na tabia njema katika kuvuta mapenzi na mahaba ya watu na katika kupunguza maumivu yanayoweza kuyakabili maisha.

Wale wanaobarikiwa tabia nzuri kama hizo hawadhihirishi kwa wengine hali yao ya huzuni; na huzuia isitoke nje ya maisha yao ya faragha. Watu kama hao hujitahidi kuleta mazingira ya furaha na ufanisi kati yao ili kwamba wale wanaoingiliana nao wasahau mashaka yao kwa kupewa hisia ya matumaini na utulivu. Wao pia huonyesha utulivu na raha yao ingawa wana matatizo, lakini kwa njia hii huzidisha uwezekano wao wa kupata ufanisi na ushindi.

Tabia nzuri ni nguzo madhubuti kabisa ya kujipatia mafanikio kwa watu wengi. Hapana haja kusema kwamba mafanikio ya kibiashara ya mashirika yanahusiana moja kwa moja na mwendo mzuri wa wafanyakazi wake.

Kwa kawaida, mkurugenzi wa shirika mwenye tabia nzuri huwa mwenye nishati na jitihada, na huvutia kwake maingiliano mengi. Kwa ufupi, hulka na tabia njema ni siri ya kupendwa na kukubaliwa na watu. Watu hawawezi kuwavumilia watu wenye tabia mbaya hata wawe na vyeo gani. Ukichungua mwenyewe utaona sababu ya baadhi ya watu kupendwa na wengine. Mwanachuoni mmoja wa Magharibi ameandika haya kuhusu uzoefu wake katika uwanja huu:

"Siku moja niliamua kufanya uchunguzi vipi furaha na ubashasha wa uso wangu unavyoathiri maisha yangu. Kabla ya siku hiyo nilikuwa na huzuni; na asubuhi

32

iliyofuatia nikaondoka nyumbani nikiwa na nia ya kuwa mchangamfu. Nikafikiri moyoni mwangu kwamba nimeona mara kadhaa kwamba sura changamfu na za ucheshi za watu zilinipa nguvu na nishati. Nilitaka mwenyewe kugundua ikiwa mimi mwenyewe ningeweza kuwaathiri wengine kwa namna hiyohiyo. Nilipokuwa nikielekea kazini nikakariri mwenyewe kwamba azma yangu ni kuwa mcheshi na mchangamfu. Hata nikajiaminisha kwamba nilikuwa mtu mwenye bahati sana. Na matokeo yake, nikahisi raha mwilini mwangu. Nikahisi kana kwamba nataka kuruka. Nikatazama pande zote kwa uso wa bashasha sana; bado nikaona ziko nyuso nyingi zinazoonyesha huzuni. Moyo wangu ulinichoma kwa ajili ya watu hao, nikatamani lau ningeliweza kuwapa chembe za furaha ya moyo wangu.

"Asubuhi hiyo niliingia ofisini na nikamwamkia mhasibu kwa namna ambayo hakuwahi kuamkiwa na mimi. Kabla yake sikuwa tayari kumwamkia kwa bashasha namna hiyo hata kwa kima cha kuokoa maisha yangu! Mhasibu hakuwa na budi ila kunijibu kwa ukunjufu na mapenzi. Wakati huo nikahisi kwamba furaha yangu imemuathiri barabara.

"Rais wa shirika langu ninapofanya kazi ni mtu ambaye hakiinui kabisa kichwa chake anapozungumza na wengine ni mtu mchapwa sana. Siku hiyo alinitolea ukali sana kuliko siku nyingine yoyote. Nisingeweza kumstahamilia, lakini kwa kuwa niliamua nisikereke kwa jambo lolote, nikamjibu kwa namna ambayo ikafanya mikunjo ya kipaji chake iondoke. Huo ulikuwa mkasa wa pili siku hiyo. Baadaye siku hiyo, nikajaribu

33

kuendelea kutabasamu na kuchangamka na wafanyakazi wenzangu.

"Kwa njia hiyo, nikaweza hutekeleza mbinu hiyo kwa familia yangu, na matokeo yake yakawa mazuri. Kwa hivyo, nikagundua kwamba ninaweza kuwa mchangamfu na mwenye furaha, na nikawafanya wenzangu wahisi vivyo hivyo.

"Jambo hili linawezekana kwako pia. Onana na watu kwa hali hii, uso wako uwe na bashasha, na utaona maua ya furaha yakichanua katika maisha yako kama vile mawaridi yanavyochanua katika majira ya machipuo; na utapata marafiki wengi watakaokuletea amani na utulivu wa daima."

Hakuna mtu anayekataa athari kubwa ya tabia hii katika kulainisha nyoyo za maadui. Heshima na tabia nzuri husaidia sana kuwasadikisha wapinzani wafuate itikadi fulani.

Mwandishi mwingine wa Magharibi amesema haya kuhusu jambo hili:

"Milango yote hufunguliwa yule anayetabasamu na akawa na tabia nzuri, lakini wale wenye tabia mbaya hubidi wagonge milango ili wafunguliwe kama vile wahuni. Mambo bora kabisa ni yale yanayohusiana na adabu, tabia nzuri na uchangamfu."

Hata hivyo, ningependa kuongeza kwamba tabia njema hulazimu furaha na huwaongoza kwenye ukamilifu watu wenye hulka nzuri, lakini kwa sharti kwamba tabia hizo ziwe zinachimbuka ndani ya moyo wa mtu bila ya kuwepo unafiki au kujidai.

Kwa maana nyingine, ni lazima hisia ya mapenzi

34

iwe ni madhihirisho ya yaliyomo moyoni. Uzuri wa nje peke yake si dalili ya ubora wa ndani na usafi wa mwendo wa mtu, kwa sababu inawezekana hiyohiyo mienendo mizuri ya kidhahiri ya mtu ikawa inakinzana na kuhitalifiana na moyo wake uliochafuka na uliopotea. Kwani kuna mashetani wengi wanaovaa nguo za malaika ili kuficha nyuso zao za kutisha nyuma ya pazia la uzuri.

Mtume Mtukufu Hutoa Kielelezo

Sote tunajua kwamba mojawapo kati ya sababu kubwa kabisa ya kuendelea Uislamu ni mwendo na tabia njema ya Mtume Mtukufu SAW. Kuenea Uislamu kutokana na maadili mema ya Mtume kumetajwa na Mwenyezi Mungu pia:                 '

"Na kama ungelikuwa mkali na mwenye moyo mgumu, bila shaka (watu) wangekukimbia."

(Aal 'Imraan, 3:159)

Mtume Mtukufu aliwakunjulia watu wote moyo wa mapenzi. Upendo wake mkubwa juu ya watu, upole na mvutio wake ulikuwa ukidhihirika kwenye uso wake wa kimalaika. Alikuwa akiwatendea vizuri na kuwakirimu Waislamu wote sawasawa.

"Mtume Mtukufu SAW alikuwa akiwashughulikia na akigawa wakati wake kati ya masahaba zake

sawasawa/

(Rawdhatu 'l-Kafi,uk. 268)

35

Mtume wa Uislamu alikuwa akikataza tabia mbovu, na alikuwa akisema:

"Tabia mbaya ni kisirani, na mtu mwovu kabisa kati yenu ni yule mwenye tabia mbovu."

(Nahju 'l-Fasahah.uk.. 311)

Mahali pengine amesema:

"Enyi wana wa Abdul Muttalib! Ninyi hamtaweza kamwe kuwaridhisha watu kwa mali zenu, hivyo, kutaneni nao kwa uso mchangamfu na mwendo mzuri." (Wasa'ilu 'sh-Shi'ah, jz. 2, uk. 222)

Aliyekuwa mtumishi wa Mtume Mtukufu, Anas bin Malik, alikuwa daima akikumbuka hulka nzuri ya Mtume Mtukufu, na alikuwa akiwaambia watu kwamba katika kipindi cha miaka kumi aliyomtumikia Mtume Mtukufu, hakuwahi kabisa kumwona ameukunja uso wake unaonawiri, wala hakuwahi hata mara moja kumwona amepandisha nyusi zake au ameonyesha uso wa hasira kwa sababu ya kufanya jambo lisilopendeza.

Tabia njema na uchangamfu ni katika sababu zinazozidisha umri wa mtu. Imam Sadiq AS amesema:

"Wema na tabia nzuri hustawisha ardhi na huzidisha umri."

(Wasa'ilu 'sh-Shi'ah, jz. 2, uk. 221)

Dk. Sanderson ameandika yafuatayo kuhusu mada hii:

"Uchangamfu ni mojawapo kati ya vitu muhimu vinavyozuia na kuponesha maradhi. Madawa mengi

36

baada ya kutoa nafuu ya haraka na ya juujuu tu huanza kuonyesha udhaifu wake, lakini ukunjufu na uchangamfu unaleta athari za kudumu ambazo huonekana mwilini mzima. Uchangamfu hunawirisha macho, huchangamsha viungo, huimarisha miguu na husafisha sauti. Watu wenye tabia nzuri na uchangamfu, furaha zao zote huzidi na hupata matumaini, damu huzunguka haraka sana viungoni mwao, hewa huingia kwa raha zaidi mapafuni mwao, afya na siha ya miili yao huimarika barabara na huvunja nguvu za ugonjwa!"

(Pintzi Fikr)

Jambo linalovutia katika usemi huo wa Imam Sadiq AS ni hili kwamba kutenda mema pamoja na tabia nzuri husababisha umri wa mtu kuzidi, kwa sababu mtenda mema katika kutenda mema na mazuri huhisi furaha na hupata ukunjufu maalumu katika nafsi yake, na kwa sababu hii kutenda mema kwa upande wa kiafya huleta athari na matokeo kama yale ya tabia njema. Vivyo hivyo, Imam ameihesabu sifa njema hii kuwa ni miongoni mwa vitu vinavyoleta bahati nzuri kwa binadamu:

"Tabia njema ni miongoni mwa ufanisi wa mtu."

(Mustadriku 'l-Wasa'il, jz. 2, uk.S3)

Samuel Smiles ameandika haya kuhusu maudhui hii:

"Kuna msemo maarufu unaosema kwamba  kadiri ustawi na ufanisi wa mtu katika maisha yake unavyohusiana na uwezo wa nafsi yake na kipawa chake cha kiasili, vivyo hivyo, kwa kadiri hiyohiyo huhusiana

37

na tabia njema, afya na siha yake pia."

Hulka nzuri husababisha kupanuka maisha ya mtu, kuzidi riziki na kupatikana mapenzi na masikilizano.

Imam Ali AS amesema:

"Tabia nzuri hupanua riziki na huvuta (nyoyo za) urafiki."

(Ghuraru 'l-Hikam, uk.279)

Bwana S. Marden ameandika haya katika kitabu chake kiitwacho, Khawishtan Sazi:

"Ninamjua meneja mmoja wa hoteli ambaye kutokana na mwendo na tabia yake nzuri amekuwa mashuhuri na amejipatia utajiri mwingi kwa kadiri kwamba wasafiri na watalii walikuwa wakifunga safari ndefu ili waje katika hoteli yake, kwa kuwa mazingira ya hoteli hiyo ilifanana na ya nyumbani kwao. Wageni wanapoingia katika hoteli hiyo hukaribishwa kwa furaha na tabasamu maalumu ambayo huoni katika hoteli nyinginezo. Kwa ufupi, hali ya kutokuwepo ukarimu na ubashasha katika hoteli nyinginezo haikuwepo hapo. Watumishi wa hoteli hiyo daima hujitahidi kama inavyomkinika kuweka uhusiano wa kiurafiki kati yao na washitiri. Watumishi huwahudumia washitiri wao kwa uso wa tabasamu na huwashughulikia kwa mapenzi yanayotokana na upendo wao. Huwafanya wageni wapendezwe na mwendo wao mzuri na waipende hoteli hiyo kwa kadiri kwamba watake kuja tena na wawasifie wenzao. Ni wazi kwamba mwendo huu huwavutia wageni wapya."

Mwandishi ameongeza:

38

"Adabu na tabia nzuri hazikuwa na thamani kubwa katika zama zozote kama sasa zilivyo. Katika zama hizi kuwa na shakhsia (hadhi), haiba na tabia nzuri, na kujitahidi kuwasaidia watu kumekuwa ni rasilimali ambayo kila mtu anataka kuwa nayo ili apate mafanikio katika maisha yake."

Kufuatana na maneno ya Imam Sadiq AS, uchangamfu ni alama ya uelevu na ukamilifu wa akili ya mtu. Amesema:

"Watu wenye akili kamilifu kabisa ni wale wenye tabia nzuri kabisa."

Watu wenye kutumia akili vizuri sana, tabia zao pia huwa ni bora zaidi kuliko watu wengine.

  Yaliyomo endelea