Kimekusanywa
na
kutarjumiwa
na
AMIRALY
M. H. DATOO
BUKOBA -
www.al-islam.org and ebooked by www.ShiaLibrary.com and www.islamkutuphanesi.com . May Allah be pleased with all. |
Namshukuru Allah
swt,Mtume Mtukufu s.a.w.w. pamoja na Ahli Bayt Tukufu a.s. kwa kunijaalia
niweze kufanikisha juhudi zangu hizi katika kukitayarisha kitabu hiki juu ya
maudhui haya ya
ndoa katika Islam.
Mnamo mwezi
April 1994 nilifanywa operesheni ya appendix
huko
Na takriban tarehe 28 mwezi Julai 1995 nilibahatika kumtembelea Chief Missionary wa Bilal Muslim Mission of Tanzania, Hujjatul-Islam Sayyid Saeed Akhtar Rizvi,na katika mazungumzo yetu kulitokezea mazungumzo juu ya kitabu cha ndoa katika Islam. Na nilimwambia kuwa nilikuwa nimekifanyia kazi kiasi fulani.
Kwa hakika yeye alivutiwa mno, na kuniomba nikikamilishe haraka iwezekanavyo kwani alikuwa akihitaji kuchapa kitabu juu ya maudhui hayo. Nami baada ya kurejea kwangu Bukoba,2.8.95 nilikalia kitabu hiki na kuweza kukikamilisha vyema kwa uwezo wangu mdogo hadi leo tarehe 28.8.95.
Hivyo ni matumaini yangu kuwa,utafiti nilioufanya kwa kiasi hicho kidogo,kitasaidia katika ndoa na masuala yanayohusiana nayo na wengi tutaweza kujirekebisha ili kuweza kujipatia matunda bora kabisa katika maisha ya ndoa.
Hata hivyo nitapenda kupokea maoni na ushauri na masahihisho kuhusu maudhui na kitabu hiki kwa ujumla ili n iweze kuendeleza sura zinginezo ambazo sikuzigusia,ingawaje ni nyingi.
Amiraly M.H.Datoo 28 August 1995
BUKOBA. -
Zipo riwaya nyingi mno ambazo zimenakiliwa kutoka Mtume s.a.w.w. na Maimamu a.s. ambazo zinasema kuwa mwenye kuoaanakuwa amejidhibiti vyema katika Islam na nusu ya sehemu ya imani inambidi afanye jitihada ili aweze kuiimarisha.Mwenye kuoa rakaa mbili za mwenye kuoa ni afadhali kuliko rakaa' sabini za mtu asiyeoa. Aliyeoa ni mpenzi wa Allah s.w.t.
Mtume s.a.w.w.
amesema kuwa mtu asifanye uchelewesho katika
kuoa
kwani watoto
watakaozaliwa watakuwa wakimtii na kumtukuza Allah s.w.t. ambapo ujira wake
utakuwa ukipatiwa wazazi wao
na mema
Iwapo mwanamke mimba yake itaanguka basi Siku ya Qiyama mtoto wake huyo atakataa kuingia Jannat (Peponi) hadi hapo wazazi wake waingizwe nae pamoja.Limetolewa onyo kuwa "kufa bila ya kuoa ni vibaya mno."
Imam Jaafer as-Sadiq a.s. amenakiliwa akisema kuwa "Iwapo nitakuwa na dunia pamoja na vitu vyake vyote vikawa vyangu bila ya kupitisha usiku mmoja bila mwanamke,basi mimi siridhii hayo yote.Ni afadhali kukosa vyote hivyo kuliko kukosa mwanamke. Vile vile sala ya aliyeoa ni afadhali kuliko sala za kila siku pamoja na saumu za asiyeoa."
Vile vile kuna riwaya isemayo kuwa mtu atakapo kujitakasa mbele ya Allah swt,basi inambidi afanye harusi na kuoa katika hali ya umasikini na ufukara ni kuthibitisha imani na uaminifu juu ya Allah s.w.t. kwani Allah s.w.t. amesema "Oeni hata katika hali ya umasikini na ufukara kwani nitawaghaniisha."
Ipo katika riwaya kuwa muoe wake wazuri na mtu atakayeoa mwanamke kwa sababu ya tamaa ya mali au uzuri,basi atakosa vyote.Na atakayeoa kwa kuangalia dini na imani ya mwanamke,basi atapata mali na uzuri vyote.
Katika kumsifu mwanamke,ni bora kuliko dhahabu na fedha na mwanamke mwovu ni mbaya sana kwani hata mchanga ni afadhali kuliko yeye. Mwanamke mwenye gharama ndogo na vilevile anazaa watoto kwa urahisi na mwanamke mwenye mahari ndogo basi ni mwema na mwanamke mwenye gharama kubwa na mwenye kuzaa watoto kwa mushkeli na mwenye mahari kubwa,basi mwanamke kama huyo si mwema.
Ni Sunnah kusoma nikah wakati wa usiku,kwani Allah s.w.t. ameufanya usiku kuwa mapumziko na starehe na inapoangukia Qamar dar Aqrab (nyota iwapo katika Nge) basi msifanya nikah na kunapokuwa joto kali,iwapo kutakuwapo na ndoa,basi kunauwezekano wa kuachana.Vile vile kusifanywe ndoa siku ya jumatatu kwani siku hiyo ni mbaya mno na iwapo itakuwa ni siku ya kuzaliwa kwa Ma'sum a.s. au Idd basi hakuna shida yoyote.Haifai kuoa katika tarehe 26,28 na 30 za kila mwezi.
Kuoa si faradhi lakini iwapo kuna hatari ya kutumbukia katika maasi,basi itakuwa ni faradhi kuoa,na kwa mjane kolewa si vibaya,kwani kubakia pekee mara nyingi inakuwa mushkeli kimaisha na hivyo haitakiwi kujitumbukiza katika magumu ya maisha ambapo tunaweza kujiepusha.Kwa hakika ni jambo la kusikitisha kuona katika jamii yetu wajane wakitupwa bila kujali na kudharauliwa kama ni wenye nuksi ambapo inatubidi sisi kuwajali na kuwatunza na kuwaoza inapowezekana ili wao nao waweze kuishi maisha kama wengineo wote.
Ipo Hadith inayosisitiza mno kabisa kumfanyia na kumgharamia mtu harusi na nikah kwani inayo thawabu adhimu.Kila neno litakalosemwa na kila tendo litakalotendwa na kila hatua itakayochukuliwa,Allah swt atampa thawabu za sala za usiku na saumu za mwaka mzima.Na huko Jannat atampatia Hur al-Ain elfu moja wakiwa na majumba yaliyorembeshwa kwa Yaquti na vito vya thamani.
Ipo riwaya inayosema kuwa atakayemwozesha mjane, basi Siku ya Qiyama atakuwa miongoni mwa wale
waliorehemiwa na Allah swt.
Atakaye suluhisha baina ya bibi na bwana,basi Allah swt atamjaalia thawabu za mashahidi elfu na hatua zozote zile atakazozichukua katika kufanyisha suluh na matamshi yote yatakayotoka atapatiwa thawabu za ibada za mwaka mzima.
SEHEMU YA
Iwapo mimi nitataka niwe daktari au niwe mhandisi basi itanilazimu kwa mfululizo kwa kiasi cha miaka miwili, au mitatu au mitano, kumi au kumi na tano nisome kwa kupitia vyuo mbalimbali, kufuatia mazoea tofauti tofauti hadi niweze kuwa daktari au mhandisi ambaye nitaweza kukabili hali ya kazi zangu bila matatizo na vile vile iwapo nitapata matatizo nitakuwa ninajua njia za kuweza kuyarekebisha, kusahihisha na kuleta maendeleo mazuri katika fani yangu.Lakini katika zama hizi ni jambo la kusikitisha mno kuona kuwa wanaume wanataka kufuzu na kupata stashahada ya kuwa yeye ni mume bila ya kupitia mafunzo na kujitayarisha vyema kwa ajili ya mustakabali huo mpya. Kwa hakika mwanamme au mwanamke akitaka kuwa bwana na mwanamke akitaka kuwa bibi inawalazimu wajifunze mambo mengi na namna ya kukabili mustakabali huo mpya hivyo inawabidi wapitie mawaidha, nasiha na mazungumzo ya wazee na kujionea maisha yalivyo na wakati waliopo, lakini tunaona wengine wanaoa kimchezo na baadaye maisha yanakuwa magumu huko mbeleni na hatimaye ndoa zao kuvunjika na hivyo maisha ya pande zote mbili kuharibika kujaa kwa chuki na kukosa raha kabisa.
Hivyo katika taarifa zinazofuata nitajaribu kuzungumzia namna ya kutengeneza ndoa yetu ikawa raha na mustarehe.
Ndoa ni sawa na
farasi wawili wakivuta kigari. Kama utakavyokuwa ukiwaona farasi wawili
wamefungwa kigari nyuma
Kwa hakika ndoa
iliyofanikiwa na yenye raha inamgeuza mtu akajihisi kama yuko peponi na hiyo
ndiyo baraka kubwa ya Allah swt, na neema kubwa wajitahidi kiasi wawezacho
kujionyesha kama kweli wao wako katika mazingara hayo ili mazungumzo
wanayozungumza, vitendo wanavyotenda vionekane kama ni kweli, mfano kunaweza
kuwekwa mchezo wa kuigiza vile watumwa walivyokuwa wakipigwa na kuteswa katika
zama za wakoloni, lakini vile vitendo wanavyovitenda pale wakiwa kwenye jukwaa
vinawavutia watu kiasi kwamba wanahisi kwamba kweli hivi ndivyo ilivyokuwa kwa
hiyo na sisi ili kuonyesha maisha yetu inatubidi tufanye kila njia kufikia hayo
malengo yetu ya maisha.Kwa hivyo mtu anaporudi kutoka ofisini inambidi aje
nyumbani na uso wenye bashasha hata kama amekumbana na mambo mengi
yaliyomuudhi, yaliyomvuruga wakati akiwa ofisini na kwa hakika akija na uso
wenye bashasha nyumbani, nyumba nzima watakuwa wachangamfu watakuwa wakicheka
atapenda aongee wajadiliane wazungumze wabadilishane mawazo na kwa hakika hiyo
itamfanya huyo bwana asahahu uchovu wake wa siku nzima, lakini fikiria ukija
umenuna,umevimba uso kama papai nyumbani wakishakuona tu umekuja umepandisha
wote watakukimbia, hata kama mmoja wa familia atakuwa amewazia ukija azungumze
kitu fulani hatazungumza mtu yeyote na wewe maana wanajua wakikuzungumzisha
wewe ni sawa sawa na kuwatemea moto; kwa hivyo mtu huyo mmoja tu ukija nyumbani
unaweza kuigeuza nyumba yako ikawa bustani nzuri au unaweza kuitengeneza nyumba
yako ikawa ni chumba cha adhabu kwa sababu kila mmoja anakuogopa wote wamenuna
umewatia katika adhabu na huu sio uadilifu kwa upande wa mwanamme. Na hakuna
sababu ya mwanamme kuleta hali mbaya
Mwanamme ni bingwa katika utumishi wake lakini mtumishi aliyebobea katika utumishi daima anatenda kiasi cha kumfurahisha mwanamke na kujiona yeye ni mtu maarufu.Bibi na Bwana wanaelewana vizuri kuliko mtumishi, lakini inawabidi wote wawili wawe ni watumishi waliobobea katika fani yao bibi kwa bwana na bwana kwa bibi. Kamwe usimfanye mke wako ahisi kuwa wewe unaelewa kasoro zake na wala asifanye hisia kuwa anaelewa kasoro zako daima kila mmoja awe akimfunika mwenzake.Kwa hakika maisha ya furaha yanaweza kupatikana katika ndoa pale bibi na bwana wanapokuwa na moyo wa kutoa na wala si wa kuchukua.
Ni jambo la lazima kuwapo na tofauti ya maoni na uhodari wa mabishano miongoni mwa watu waliokuwa wanaishi pamoja. Hasira ni jambo la kutokea lakini haibidi pande zote mbili kuwa na hasira labda wakati mmoja awe huyu wakati mwingine awe mwenzake (yaani mmoja awe na hasira kwa wakati mmoja, wote haiwabidi kuwa na hasira kwa wakati mmoja). Kwa hivyo yule anayeweza kwanza adhibiti na mara nyingine mwenzake. Kwa sababu mmoja anapokuwa ameingiwa na hasira na mwenzake akawa ametulia hapo balaa na maafa mengi yataweza kuepukwa. Kwa hakika nimeona maneno ya kupooza magomvi katika majumba yetu ni machache na matamu sana yaani kusema: "samahani nisamehe, "na kwa hakika mtu anayesema samahani nisamehe maneno hayo ni mtu mwenye busara sana na anahisi raha moyoni mwake, hasa wakati anajua yeye hayuko kwenye hatia hana makosa lakini anaomba msamaha; na kuna msemo mashuhuri usemao 'anayetoa msamaha kwa mwenzake ni mpenzi wa Mungu'. Kwa hakika mtu mwenye moyo mkubwa ni yule anayekubali makosa yake, anayekubali lawama na kuomba msamaha. Jambo lingine linalostahili kuandikwa kwa wino wa dhahabu ni kamwe usimlaumu mwenzako. Njia nionayo iliyo rahisi kwa ajili ya kuelewana katika magomvi kutoelewana sura mbali mbali ni kwanza ukubali maelewano japo kuwa liwe ni jambo dogo baada ya kutua na mambo kutulia mnaweza kuendelea mkafanya marekebisho na maongezi zaidi katika maelewano yenu hayo, na hatimaye kila mnapokuwa mkiendelea kupanua maelewano yenu itafika wakati mtaona kuwa mambo ambayo mliokuwa hamkuelewana yatatoweka kutakuwa na uelewano tu.
Kamwe usiwaseme
vibaya upande wa mke wako au upande wa mume wako:
Kwa sababu iwapo
mwanamme atakuwa akiwasema vibaya jamaa za
mke wake basi mke ataanza kuwachukia jamaa wa mume wake.
Kamwe usiwe na hasira dhidi ya mwenzako na
wala usikubali hisia
Kutofautiana kwa maoni na mawazo na magomvi ni sehemu ya maisha. Mshairi mmoja maarufu amesema: "Je maisha ni nini, Je mauti ni nini, na kufufuka ni nini?" Urafiki wako, magomvi yako, na kukutana kwako tena."
Kisha hakikisha
kuwa ugomvi wenu haubakii mpaka wakati wa chakula kinachofuata yaani mkigombana
asubuhi mpaka chakula cha mchana kiwe kimeshakwisha , na wewe hutakiwi kukwepa
mlo huo. Ni lazima ukubali kuwa Allah swt ametujaalia neema kubwa ya muda huo
wa kula chakula pamoja ambamo tunaongezea uhusiano wetu, uelewano na kumaliza
tofauti na ugomvi wetu, lazima tuwe tahadhari kuwa kamwe tusianze mazungumzo
ambayo yataleta ubishano mkali wakati tukiwa tunakula. Kwa sababu kunaweza
kuanza na mazungumzo ambayo yanaweza kuleta mzozo na watu wasiweze kula chakula
chao hivyo kila mtu aachilie mbali mazungumzo hayo hadi baadaye ili wote waweze
kula vizuri washibe
ili waweze kumudu
maisha
Kupendana na
kucheza kwa bibi na bwana ni moja ya siri kubwa ya ufanisi wa maisha ya ndoa na
kwamba inaweka hai moyo wa ndoa. Kamwe usijitupe ukajisahau bali inakubidi daima
uwe ukijiweka vyema, vizuri kiasi cha kumvutia mwenzako ili daima awe
akikutamani na kukupenda bila ya
kujali
umri wako. Kusuhubiana kwa bibi na bwana ni gurudumu moja muhimu katika mtambo
huu wa maisha ya ndoa.
Kusuhubiana
kutakuwa na mafanikio na raha zake zitapatikana pale bibi na bwana
watashirikiana katika mazingara hayo.
Inabidi ikumbukwe pia unapokuwa na mawazo mengi kunapokuwa na mvurugano
na mtu anapokuwa na matatizo raha na hamu ya kusuhubiana
hufa. Hivyo hamu na raha ya kusuhubiana
inapatikana katika hali ya mtu kuwa mchangamfu na namna ya kujiweka mwenye
raha.Mtu anapochokozana kimapenzi na mwenzake basi kimchezo mchezo mapenzi yao
yanaongezeka na hatimaye yanafika mbali mathalani bibi na bwana wanaweza kuwa
wamelala katika mazungumzo, wanaweza kuanza mapenzi ya mmoja kumbusu mwenzake
na wakawa na hamu wakaingiwa na hamu kwa wote wawili hadi kufikia hatua ya
kusuhubiana kwa furaha kwa sababu pande zote mbili wanakuwa na hamu.
Vile vile ni jambo la muhimu
Panapokuwa na watoto katika familia ni lazima kabisa kwa bibi na bwana kuheshimiana na kuonekana kuheshimiana mbele ya watoto wao na kamwe wasionyeshe tofauti zao mbele ya watoto. ugomvi na mzozano wa bibi na bwana mbele ya watoto unaathari mbaya kabisa kwa watoto kwa ajili ya siha ya akili zao jambo ambalo ni muhimu sana kwa watoto kuliko siha ya mwili.Vile vile matishio ya kumpiga mke ni mambo ambayo hayawezi kusameheka.
Hakuna faida ya kukalia makosa yaliyopita au mambo yaliyopita itakuwa ni vyema lau utasahau na kusameheana ili mjenge maisha mema.
Ukaidi hauleti manufaa yoyote kwa bibi na bwana na familia nzima kwa ujumla, lakini kuvumiliana na kupeana mkono kwa bibi na bwana ni jambo moja ambalo linasaidia kusukuma gurudumu la maisha bora na utengemano ambavyo hatima yake ni ya bibi na bwana kuelewana vyema na kuishi maisha ya starehe.
Nyumba ni mahala pa mke na biashara au kazi au taaluma ni maswala ya bwana.Hivyo kama mwanamke anaishi nyumbani tu anafanya kazi za nyumbani na mwanamme anafanya kazi za biashara au ofisini basi wasiingiliane bali kila mmoja amwachie mwenzake aendeshe kazi inayompasa hiyo haimaanishi kuwa bwana asiwe na picha ya mazingara ya nyumbani na mwanamke asiwe na picha ya mazingara ya kazi bali kila mmoja inabidi wasaidiane washirikiane waishi maisha mazuri ili bibi aweze kuendelea na kazi zake vizuri na bwana aweze kuendelea na kazi zake vizuri bila ya kuzozana.
Ni kweli kuwa umbali unavutia. Kwa hivyo utaona bibi na bwana wanatuvutia na wanaonekana kwamba wao wanaishi vizuri kuliko sisi kwa hiyo tukazane kuwa sisi hatuishi vizuri hatuelewani kama wale wanavyoishi kwa raha na starehe la sivyo hivyo inawezakana wao wakajua siri ya bibi na bwana kwa hivyo mbele ya watu hawaonyeshi bali wanaonyesha wako raha starehe na hakuna tofauti baina yao, kunaweza kuwepo raha na starehe pamoja na tofauti miongoni mwao hivyo kwa kuwatazama wengine tusianze kuzua magomvi kwetu vile vile usione wengine wanaishi maisha kifahari na sisi baada ya kuyaona tukatamani kuishi hivyo bila kujali hali ya uchumi wa waume wetu au matatizo mengine yanayokabili familia kwa ujumla.
Mtu anapoposa ni kipindi kimoja ambacho kila upande unafanya njia ya kuvutia mwenzake. Siku hizi tunazuzuliwa kwa kuiga mambo ya sinema kiasi kwamba wengine wanajifanya ni waigizaji wa sinema ili mradi wawavutie wenzao.
Baada ya ndoa
bibi na bwana wanakwenda kutembea safari ambapo ni bibi na bwana tu na hakika
Iwapo
kutokuelewana kwa kiasi kidogo kidogo kutakuwa kukiendelea na kuongezeka basi
yanakwenda yanazaana.
Milima
inatengenezwa kwa punje ndogo ndogo,na ukianza kuzikusanya utashtukia unapata
mlima.Hivyo mashitaka na tuhuma dhidi ya mwenzako yatajenga nyumba katika mioyo
ya bibi au bwana. Watu kama hawa ukiwashindilia kabisa na kuwauliza yaliyotokea
wiki iliyopita yaani juma lililopita utawasikia wakianza kutupiana lawama
ambazo zimewaka moto kweli kweli.Kwa kutokuelewana, kwa kutotosheka katika hali
Kutokuelewana kati ya bibi na bwana ni vitu vya kawaida katika ndoa ambapo shaka haijatokezea.Katika hali hiyo inatakiwa maswala kama haya yachukuliwe kwa busara na kuelezwa kwa kiakili sio kwa mtu mwenyewe bali kwa mwenzake pia.Mara nyingine hatua hii haiwezekani hivyo kuna wazee wanaoweza kusaidia katika maswala ya ndoa. Hivyo ndiyo maana Islam imetoa amri kuwa kabla ya kutoa talaqa ushauri wa watu wenye hekima katika mambo ya ndoa waingilie kati na kujaribu kusuluhisha tofauti baina ya bibi na bwana. Kwa ushauri bora kusiwe na upande wa mwanamke au upande wa mwanamme bali wawe ni watu wa nje ya watu hawa wawili kwa sababu mtu asiweze kuvutia upande wa jamaa zake.
Ninapenda
kuwasisitizia kuwa mawasiliano ni muhimu kabisa katika ndoa yenye furaha na
starehe. Bila ya mawasiliano baina ya bibi na bwana hofu inaendelea, mashaka
inaongezeka na hali ya kutokuelewana itatokezea. Hivyo kuelewana lazima kuwepo
na njia za kuwasiliana kuanzia wanapooana mwanzoni ili kwamba hata bibi na
bwana wakiwa ni watu mashuhuri
Katika maisha ya
ndoa sio lazima kuwa ni maongozi tu yanayotakiwa kila siku kwa wakati mwingine
hata kumgusa kidogo mwenzako au hata kuminya mkono kidogo yana mawasiliano ya
aina yake na yana athari zaidi kuliko ya maneno.Hivyo mnapokutana baada ya
bwana kushughulika ofisini na bibi kushughulika nyumbani mnapoonana mnazungumza
nakidogo kujichangamsha, jambo ambalo litaweka njia ya mawasiliano kuwa bora na
mazuri;na jambo lingine ambalo ni zuri kabisa katika mawasiliano ni hizi silabi
tatu:"mimi ninakupenda sana."
Na
lau utaongezea maneno mengine mawili ya
Shughuli za kuridhisha za chakula na maongezi yanaunganisha familia pamoja.Baba anaweza kuwafurahisha kwa kuhadithia ujana wake, akiongelea mambo mengi yenye faida kama kuendesha baiskeli,kuroa samaki na kupanda farasi siku za Jumapili, vile vile mama pia anaweza kuanzisha mazungumzo juu ya utoto wake na ujana wake.Katika majumba mengine muda unakwenda mwingi wakati wanapokuwa mezani wanakula kwasababu familia wanapokuwa wanakula pamoja wanazungumzia mambo ya siku yaliyotokea mwingine anaongelea aliyoyasikia au kuyaona na mambo mengineyo hata wengine huzungumzia matukio mengine na kuzungumzia matukio ya Qurani,Hadithi n.k.
Hivyo inabidi wakati wa kukaa kula mazungumzo yatakayotokea yawe yenye kufurahisha na kupendeza na ichukuliwe tahadhari kuwa mtu yeyote asianzishe mazungumzo yale ambayo yanaweza kusababisha kutokea ugomvi au kutokuelewana wakati wa chakula.
Wazazi wawaulize watoto wao walichofanya shuleni na wamefanya na akina nani, na walichojifunza nacho. Na hali hii itakuwa ni ya kufurahisha mno kwa mzazi na watoto kwa sababu watajikuta wazazi katika mazungumzo na watoto wao.
Kuwachukua
familia katika matembezi inawabidi wazazi watumie muda mwingi pamoja na familia
Inawabidi wazazi waangalie kwa makini mavazi ya watoto na usafi wao na yote hayo uyafanye kwa sauti ya kuvutia na kupendeza, uwafundishe wao namna ya kufanya vyema zaidi kwa kuvutia.
Kufikiria shughuli za siku nzima, usikalie kusoma magazeti tu au kuangalia matatizo yako inakubidi pia ufikirie kuhusu familia yako vile utakavyoweza kuiendeleza na kutatua matatizo na kuleta ushirikiano na uelewano mwema miongoni mwa familia nzima.
(a)Je unajua na kutambua kuwa wewe umechukua kitu bora kabisa kilichoumbwa na Allah swt? Roho,maisha ya mwanamke na mapenzi ya kiajabu kabisa !.
(b).Tumewafaradhishia wanaume kuwafanyia wema wazazi wao. Mama yake alimhimili katika maumivu na kumzaa katika maumivu.
(c). Macho yoyote yanayomwangalia mwanamke kwa nia mbaya ni sawa na kufanya zinaa.
(d) Bora miongoni mwenu kuliko wote ni yule mtu ambaye ni mwenye huruma na mwenye ukarimu kwa familia yake, na mimi niko vivyo hivyo kwa familia yangu.Mtume Mtukufu s.a.w.w.
(e) Wanawake wanaheshimiwa na wale watu tu ambao ni wanaume wenye huruma na wenye fahamu zao imamu na hakuna anayewakashifu na kuwatukana isipokuwa kwa wale ambao ni waovu na wapotofu.
Daima ukumbuke kuwa mwanamke ni kitu kimoja kilicho chepesi kuliko mwanamme hivyo inabidi ahifadhiwe katika kila hali ya maisha na apewe yale anayoyahitaji. Mume bora ni yule ambaye anathamini mahitajio ya mke wake na iwapo mke wake atamuomba bwana wake kitu chochote basi bwana afikirie kuwa amepewa heshima hiyo ya kumpatia mke wake alichoombwa.
Daima mfanye mke wako awe na hisia kuwa yeye ni mtu muhimu kabisa katika maisha yako na kamwe usiache kudhihirisha hivyo. Kwa kutoa lawama na kutumia lugha chafu na kuhamaki kila hapa na pale yaongezea katika uelewano mbaya baina ya bibi na bwana, na haisaidii chochote katika kuleta unyumba wenye raha na starehe.
Zawadi, lau
ikiwa ndogo kiasi gani, atakayopewa mke kutoka kwa bwana wake kwa hakika
itaongezea mapenzi na uvutano baina
Mwanamke ni kiumbe kilicho nyororo na hivyo ndivyo inavyobidi kumchukulia. Kwa kumdharau, kwa kutumia maneno maovu, kwa kumchukua vibaya kutasababisha uharibifu wa akili yake hapo mbeleni ingawaje kwa wakati huo haitajulikana hivyo.
Mwanamke ni kiumbe cha ajabu kwa hiyo kila utakavyomuwia vyema ndivyo atakavyokuwa na akili timamu siku za mbeleni na ukianza kuchafua akili zake, siku za mbeleni hiyo akili itaharibika na unyumba wako utaanza kuwa katika matatizo.
Usijaribu
kumfaidi mwanamke kwa sababu ya udhaifu wake na maumbile yake.
Kimaumbile mwanamke ni mama na daima anapenda
kuhifadhiwa na kutumika
Maisha mazima ya
mwanamke yanategemea juu ya bwana, maendeleo, afya, furaha yake n.k. Mara
nyingi utaona akivutiwa na mambo mengi
Mama kwa mtoto
ni muhimu
Itakubidi lazima ujifunze namna ya kuacha mawazo ya ofisini mwako wakati unapowasha gari lako ili uweze kukutana na familia yako kwa uso wenye bashasha na wenye furaha.
Uwe mwangalifu
(a) Kuwa mcheshi, kuimarisha na kufundisha. Na haya ndiyo maneno yenye busara kubwa.
(b) Unatakiwa uwe na uhusiano wa pembe tatu.Sio pembe tatu ile ya kidunia bali pembe tatu hiyo iwe imetengenezwa kwa kona tatu pembe ya kwanza ni Allah swt, bwana wako na wewe mwenyewe.
(c) Vita vikuu vya dunia vilivyopiganwa lau ukitaka nikwambie wapi na lini hautaipata katika ramani ya ulimwengu, ni vita vilivyopiganwa na akina mama kwa wanaume.
(d) Tafuta vitabu, magazeti, maprogramu na mambo ambayo yatakufanya wewe uwe mke mwema zaidi, mama mwema, rafiki bora na Mwislamu bora.
(e) Qurani Tukufu inatuambia sura An-Nisaa, 4 : 34
"....Basi wanawake
wema ni wale wenye kutii,wanaojihifadhi wasipokuwapo waume zao..."
Vile vile Qurani Tukufu inatuambia katika sura Al-Ahzab 33 : 59
"Ewe Mtume ! Waambie wake zako,na binti zako na wanawake wa Kiislamu, wajiteremshie uzuri nguo zao."
Kwa hakika katika siku yako ya harusi akili yako inageuka kwa siku za baraka zijazo. Ndoa nzuri ni muujiza wa maisha yote. Kwa hakika wewe na bwana wako hamuwezi kujua vile maisha yenye baraka na fanaka yatakavyokuwa mbeleni.
Mke mpenzi,
daima uwe ni kama mke kwa bwana wako na wala usiwe
Kwa hakika
mwanamme amezaliwa akiwa mjeuri, na hivyo mwanamke inambidi awe mcheshi ili
kuendesha maisha
Mwanamke hodari ni yule ambaye anaweza kumuathiri bwana wake kwa mbinu mbali mbali kiasi kwamba bwana wake asiweze kuhisi iwapo yeye anaelekezwa au anashutumiwa au anaburutwa na mke wake.Bwana yeyote hawezi kukubali kutii amri kutoka kwa mke wake na lau akichafuka mambo yanaweza kuwa mabaya kabisa kwa hivyo mwanamke mwenye busara anajaribu kujiepusha na majanga ya maisha ya ndoa ili yasiharibike bali yaendelee vizuri na yenye mustarehe.
Inambidi
mwanamke amfanye bwana wake ahisi kuwa mke wake ni mtu mmoja ambaye anamjali
kabisa maishani mwake.Unaweza kuwa na mawazo na matatizo mengine ya familia na
watoto lakini baba watoto lazima apewe nafasi ya kwanza, kiasi kwamba asihisi
kuwa yeye ametupwa,haumjali.Hivyo pamoja na kuwa na shughuli za nyumbani nyingi
zilizokutinga kamwe usisahau kumjali bwana wako pale anapoondoka kwenda kazini
katika harakati za kutafuta riziki, na kwa hakika mwanamke mwenye busara
atamsindikiza hadi mlangoni na ataweza kumuaga vyema. Vile vile atakaporejea
kutoka kazini uwe ni wakati muhimu katika maisha yako inakubidi umpokee kama
shujaa na unamkaribisha kama mgeni muhimu kwako huku ukijionyesha umefurahia
Kamwe, usianze
kuongea mambo ya matatizo yako pale bwana wako anaporudi kutoka kazini. Kwa
sababu bwana wako atakuwa ametoka katika vurugu za maisha matatizo na mawazo ya
siku nzima yaliyokuwa yakimzonga akilini huku akiwa amerudi nyumbani ikiwa
Kamwe usiwe mtu
mwenye mzozo, usiwe mtu mwenye kuzua mizozo na katika maswala nyeti na bwana
wako kamwe usiseme:“Je si nilikwambia
hayo .........".
Kamwe usiiache nyumba yako katika hali ya mzozo wowote ukaenda nyumbani kwa mama yako. Hii nyumba ni ya kwako hivyo itakubidi ufanye marekebisho kuliko kuiacha. Magomvi na mizozano yote itakuwa imepoteza makali yote siku inayofuata yaani mambo yatakwenda yanatulia kila muda utakavyokuwa unaendelea kupita.
Mwanamke aliyeelimika na kuerevuka lazima akumbuke kuwa iwapo yeye anataka familia, maisha ya kifamilia basi itambidi kujitolea mhanga ya utaalamu wake kwa sababu ya bwana wake na watoto wake yaani iwapo mwanamke ni mhandisi au mwalimu au ni mtaalam katika fani yoyote ile na iwapo anataka familia na lau itambidi abaki nyumbani kuitunza familia yake basi itambidi atoe mhanga wa utaalamu wake kwa ajili ya familia yake hiyo. Kwa hakika kimaumbile mwanamke ni mtu mwenye kuheshimiwa na makusudi ya maisha yake ya msingi ni kuzaa watoto, kuwalea na kutengeneza nyumba yake. Adhma yake katika maisha ni kuwa mke na mama.
Daima itakubidi uwe mwenye kupendeza na kuvutia mbele ya mme wako hakuna mtu yeyote anayeweza kujigeuza au kutokujali mbele ya mwanamke anayependeza na kuvutia yaani kila mwanamme anavutiwa kwa mwanamke anapopendeza na anapovutia lau wewe hautaweza kumuweka katika mvuto wako basi utambue wazi kuwa kuna mwingine atamvutia. Itabidi tukumbuke kuwa hakuna mwanamke aliye ovyo isipokuwa huyu mwanamke hajui namna ya kujirembesha na kujifanya mwanamke mwenye kuvutia na kupendeza.
Bwana wako
anaweza kufanya kila juhudi kwa uwezo wake ili akupatie kile kilichobora
kabisa. Lazima daima uwe unafikiria kuwa wewe uko katika hali ya afadhali
kuliko mwanamke mwingineyo.
Kitu
kikubwa, majumba ya fahari na gari ,havifanyi maisha ya bibi na bwana yakawa ya
furaha na mstarehe hata kidogo isipokuwa kinachofanya nyumba ya bibi na bwana
kuwa raha na mstarehe ni kule kuridhika hata kama kitakuwa ni kiasi kidogo kwa
sababu tumeona kuwa kuna familia nyingine matajiri kabisa lakini hawana raha
nyumbani, bibi ana njia yake na bwana ana njia yake. Pamoja na kuwa na gari,
majumba ya fahari kila kitu wanacho lakini ile raha ya maisha ya ndoa
hawana.
Na vile vile tumewaona watu
wengine wanatoa maisha kwa tabu tabu lakini wanaishi kwa mapenzi wanapendana na
humo ndimo kuna baraka za
Allah swt.Kwa
sababu wote wawili wanaishi maisha ya kutosheka wanakinai. Amesema Mtume
Mtukufu s.a.w.w. kuwa:"Asiyekinai
kwa kidogo hashibi kwa kingi." Inatubidi tutosheke, turidhike kwa kile
alichotupa Allah swt na hii ni neema moja kubwa ya Allah swt na wala
usisikitike kwa kile usichonacho.
Daima
uwe na moyo wa kusema kuwa wewe unacho kila kitu na moyo
Kamwe usijaribu mawazo yako potofu yakakufanya uwe mwenye fahari mbele ya mwenzako katika maisha ya unyumba, daima uishi vile nafasi yako juu ya familia ilivyo yaani isiwe wewe mwanamke unataka kujifanya wewe ukachukua nafasi ya mwanamme katika nyumba nafasi ya mwanamme iko nafasi yake na wewe mwanamke una nafasi yako hivyo kila mtu ana cheo chake. Na hii ndiyo itahakikisha maisha yawe mema kwa sababu tunaona magomvi makubwa ndiyo hayo, bwana ataanza kusema mimi mke wangu anataka kuniendesha anataka kunitawala ananitolea amri mbali mbali mimi siwezi mwanamke kama huyu na hatima yake ni kuachana na kuishi katika hali ya ugomvi na kutokuelewana.
Daima uwe
mcheshi pale unapomuona ametingwa na mawazo anamzigo kwenye akili yake ambao
unamzuzua. Lazima umpunguzie uzito wake mwilini pale unapoona amelemewa.Uwe
ukitoa mashitaka machache
Kwa kumtukuza ni
jambo muhimu
Kwa hakika hata mapenzi ya kweli hayana dhamana ya kukosa matatizo. Hata kama bibi na bwana wanapendana kiasi gani haiwezi kusemwa kuwa hakuna matatizo miongoni mwao, lakini jambo la ajabu ni kwamba wao pamoja na kuwa na makosa na matatizo miongoni mwao wameshikamana vyema na wanasonga mbele. Na hayo ndiyo maendeleo ya kweli.
Kujishughulisha na mambo ya vyakula unachukua masaa mengi kwa siku na kwa juma kuliko kazi nyingine zozote za nyumbani. Katika hali hii kuna sura mbili:
1. Ama kuchukia na kusababisha kupika chakula songa mbele.
2. Kufurahika na kazi ya mapishi na katika hali hii lau utapika mapishi kwa furaha na moyo mkunjufu basi utapika bila kuona tabu yoyote na utaweza kupika vyakula vya aina aina ambavyo vitafurahisha nyumba nzima .
Upishi
unaonekana kwamba ni jambo ambalo ni kubwa
Na kutaka kuwa mpishi mzuri au mtaalam kwanza itakubidi utambue umuhimu wake. Pili itabidi ujifunze na kutambua, na tatu inabidi utende kimatendo yaani uyapike hayo mapishi.
Je hatuelewi sisi umuhimu wa mapishi katika maisha ya ndoa ya
ustarehe na yenye fanaka?
Je hayana
umuhimu katika kujenga familia zinazoishi kwa raha?
Wanaume wengi
Mama anaweza
kuwaathiri watoto
Akina mama watambue wazi kuwa watoto wao wanapoolewa wanapokuwa na mikono yao myeupe haimfurahishi bwana isipokuwa kazi anazozifanya nyumbani na kutunza nyumba na ule mpango na akili na moyo wa kufanya na kufanyisha kazi ndio unaopendwa na bwana kwa hiyo mwanamke ambaye hafanyi kazi na nyumba inakuwa chafu na kupika hapiki au hajui kupika basi unyumba wake unamatatizo hali hii magomvi hayawezi kuisha.Inawabidi akina mama watumie akili na busara yao kutaka kuishi maisha mema wawafundishe mabinti wao vitu hivyo ili wao pia wakienda kwa mabwana wao waweze kuishi maisha mema na mazuri.Hakuna mama anayetaka binti wake akiolewa apate taabu huko, hivyo ili kuepukana na swala hili itabidi muwafundishe mabinti wenu mapishi, kazi za nyumbani, mapenzi ya bwana na ufamilia, ili kuhakikisha maisha yao yatakwenda vizuri. Watoto wa siku hizi wanalelewa vibaya na wazazi wao na hatimaye tunaona magomvi ya familia hayaishi, na mara nyingi watoto wengine wanarudishwa kwa wazazi wao kwa sababu ya kukosa uhodari katika fani hizo.
Akina mama inawabidi kufanya kazi, na miaka ya nyuma walikuwa wanafanya kazi ngumu na masaa mengi. Wanawake walikuwa wakifanya kazi katika maduka madogo au mashambani. Wanawake walikuwa wakifanya kazi pamoja na mabwana zao na watoto wao wote walikuwa wakifanya kazi kwa pamoja. Kwa hivyo kila wakati alikuwa pamoja nao. Yeye alikuwa daima akipatikana pale alipokuwa akihitajika na mtoto wake aliweza kuwaacha baba na watoto dukani akaenda nyumbani kumshughulikia mtoto wake. Na kazi yake ilikuwa ni kwa mujibu wa kutaka kuishughulikia familia yake na ilikuwa ni kazi za kifamilia.
Lakini kazi za siku hizi ni kazi tofauti kabisa ni mbali na nyumba, ni mbali na bwana (na kwa kawaida kazi hizo ni pamoja na mabwana wa wanawake wengine).Na mara nyingi wanaume wanapokosa mapenzi na uvutano wa wake zao, wanaingia katika mtego wa wanawake wengine.
Kwa hivyo walezi
wa watoto wanakaa wanabadilika mmoja baada ya mwingine. Kwa hiyo katika
maendeleo ya mtoto hafaidiki kiasi anachotakiwa na upole na mapenzi ya mama
hayapatikani pale mtoto anapokuwa mgonjwa au anapokuwa katika shida. Hali hizi
kwa siku hizi ndizo zinazoleta matatizo makubwa katika familia zetu hizi.
Lakini ninaona kuwa akina mama inawabidi watambue hivyo kabla ya kukubali
kufanya kazi
Ukitaka kusoma zaidi juu ya maudhui haya,rejea sehemu ya pili ya kitabu hiki juu ya muta'.
1. Uvumilivu, hisia na
kijana ambaye hana uzoefu anaweza kuona kuwa anajitwisha mzigo wa matatizo ulio
hafifu kuliko pale anapokuwa peke yake.Lakini ule moyo na hali wa kutaka mtu
kuunganisha na mwenzake ndio siri kubwa ya maisha ya ndoa ambayo itafanya
maisha hayo kuwa kama bustani ya
2.Katika maisha ya awali ya ndoa kunakuwa na mawazo kuhusu mapato ya familia hasa fedha za kununulia vitu vya nyumbani na gharama zinginezo. Na katika hali ya kushirikiana, maswala ya kifedha ni ya wote wawili na bibi na bwana wanaweza kuunganisha vichwa vyao kwa pamoja na kuweza kutatua maswala yao kwa pamoja yanayowazonga kimapango, kifedha n.k.Ni lazima tukumbuke kuwa mwanzoni mwa maisha ya ndoa hakuna mtu ambaye ana mapato ambayo yanaingia tu bila yeye kutafuta na kushughulikia na ni jambo la furaha mno kuona mtu anakusanya senti moja moja hadi hapo wanafanikiwa hata kujenga nyumba.Usisahau kuwa wazazi wako pia wameanza vivyo hivyo na wao kamwe hawakuwa na chochote kile wanachokihitaji pale ulipokuwa bado mdogo. Na kwa hakika ni jambo la kawaida kuwa sisi inatubidi tujue namna ya kuweka akiba na maswala ya akiba ni nyeti katika maisha ya familia ili kujenga maisha ya baadaye kwa ajili yetu na kwa ajili ya watoto wetu.
3. Katika kupunguza mawazo
na mvutano wa maisha, watu wengi wanakuwa na mapenzi katika mambo fulani fulani
ambayo kwa hakika hatuwezi kuelezea umuhimu wake katika maisha ya ndoa hususani
mapenzi au mazoea ya tabia baina ya bibi na bwana wanaweza kushirikiana kwa
pamoja. Lau tabia ya mapenzi
4. Katika umri wa kati
bibi na bwana wanakuwa katika umri wao mzuri
5. Hapo kunaanza kutokea matatizo ya watoto wanaokua lau itakumbukwa kuwa watoto ni matokeo ya ushirikiano wao na hivyo ni wajibu wa kila mmoja wao katika kuwaongoza na kuwaelekeza kwa hivyo hakutakuwa na matatizo yoyote katika umri huu na hivyo itafanya maisha yao yawe yameimarika zaidi.
6.Katika miaka ya kukua mwanamke anaweza kukabiliana na matatizo kwa sababu uzazi wake unakwisha na mwili wake inabidi ubadilike kwa ajili ya hali hiyo. Na katika hali hii ya kipindi kifupi anaweza kujisikia mzito asiye na raha na asiyejipenda na asiyependa hata maisha kwa sababu atakuwa haoni raha katika kila hali hivyo wakati huu ndiyo utunzaji bora na mapenzi ya bwana wake ndiyo yanayoweza kumsaidia akapita kipindi hiki ingawaje na daktari anaweza kusaidia katika swala hili.
Kwa kifupi, kila
mabadiliko ya mwili wa mwanadamu iwe bibi au bwana, wanatakiwa wawe tayari
7. Katika umri huu wa
katikati mwanamme ndio huwa yuko katika kilele cha wajibu wake kama bwana au
baba
akiwa kama mkuu wa familia kwa ujumla hivyo ataonekana yuko
mashughuli
Miaka hii ndiyo wakati mwanamme yaani mme au akiwa kama baba anaanza kuweka msingi wa maisha ya watoto ya baadaye wakati huu ndio bwana anamalizia mipango ya kujenga nyumba kwa ajili ya mke wake, na watoto wake na wakati huu ndio watoto wanapokuwa wamekua kidogo kwa hiyo yupo katika mipango ya kuwasomesha masomo ya juu zaidi au kuwatia katika masomo ya fani mbalimbali hivyo ndivyo vinavyomtinga kwa kipindi hiki. Namna ya kukabili mambo hayo yote na namna ya kutimiza adhma aliyokuwa akiipangia miaka yote iliyopita. Ushirikiano wa mke na watoto kwa bwana au baba katika hali hii ni jambo moja jema kabisa ambalo litamsaidia kutimiza malengo haya kwa uzuri na vyema kabisa, bila ya kuhisi kuwa amebeba mzigo huo peke yake.
8. Wakati huu ndio tunawaona wanawake wengi wakiwa wajane wanafiwa na mabwana zao hivyo tunawaona na tuombe kwa Allah swt asiwajaalie wake zetu kupata matatizo.
Kuna wajane
wengi
9.Kuna msemo wa wahenga
usemao kuwa:"Mwanamke ni mzee vile
aonekanavyo na mwanamme ni mzee
10.Ni jambo la kawaida kwetu sisi kuona mtu ameishi miongo sita au zaidi kuwa ni mzee na mambo ambayo tunaona kuwa huyu mtu anastahili kustaafishwa hata kazini. Kwa hakika hili zoezi sio sahihi. Tusiangalie mtu ameishi miaka mingapi ili tujue uzee wake bali tuangalie ameishi namna gani, ndilo jambo lililo la muhimu mno. Tunawaona watu wengi sana wanasayansi pia na watu wanaotoa mihadhara na wataalamu katika fani mbalimbali ambao wamechangia kwa kiasi kikubwa mno na kwa muda wa miaka mingi katika fani zao na wametoa michango yao katika kuiendeleza fani zao hizo ambao baada ya kupita miaka yao hiyo ya uzee sisi tunaouhesabia na bado wako wachangamfu na wakakamavu.
Kwa hiyo
11.Utafiti wa siku hizi umegundua kuwa mtu ambaye anajiweka mkakamavu kiakili na kimwili katika shughuli mbalimbali basi anakuwa amejiepusha na matatizo ya uzeeni, au hata mwisho wa maisha yake kwa ufunguo wa ujana wa milele na kuwa na nguvu ni kuendeleza shughuli katika hali yoyote ile, iwe ya kiakili au kimwili. Hivyo maisha ya ndoa ambayo yanaendelea daima ni baraka na neema kubwa ya Allah swt. Na kukua kwa watoto kusiwaletee hofu na mashaka kwa upande wao. Iwapo mtu atataka maisha yake yawe mema na mazuri zaidi atokane na tamaa ya umashuhuri,kujitakia nafasi, kutaka mamlaka au pesa kwa hakika raha ya maisha itaweza kupatikana na mwenzako ambaye ameshirikiana na wewe katika hali tofauti tofauti za maisha.
Inabidi mtu aende na maisha yake au aende na wakati mtu anapokuwa kijana anaweza kujitafutia nafasi, pesa, nguvu na umashuhuri n.k. kwa sababu ana uwezo wa kufanya mambo kama haya na anakuwa na nguvu za kukabiliana na mambo kama haya na matatizo yoyote yatakayotokana nayo na vile umri wake unavyoendelea kukua ile nguvu ya kustahimili ya kukabiliana na mambo kama hayo inapungua pia nguvu kama hizo zinapungua mwilini mwake.Hivyo yanapotokea matatizo yoyote yanamuathiri sana kiakili na kisiha mara nyingine katika hali ya uzee mtu anapata ugonjwa wa moyo,au hata kupoteza fahamu (akili) n.k.na kukosa usingizi ni mambo ya kawaida, hivyo inabidi mtu kupunguza kasi zake hizo za harakati za ujana ili anapozeeka akili yake isiwe inaathirika ambayo itahatarisha maisha yake ya uzeeni.
12. Lakini mara nyingine,
amani na udugu
13. Kama nilivyoelezea
awali kuna mapenzi katika fani mbalimbali hasa katika umri huu wakati mtu
anaona hana shughuli ya kufanya anapitia katika kipindi kigumu baada ya
kustaafu kwa kustaafishwa inambidi awe na mapenzi ya jambo fulani ili kupoteza
mawazo yake mfano mtu mwingine anakuwa na tabia au mapenzi ya uchoraji kuna
mfano wa mtu mmoja ambaye katika miaka ya mbeleni alikuwa mchoraji, na uchoraji
huu ameuanza alipokosa kazi maana mawazo yalikuwa yakimsumbua kwa hiyo
akajitafutia hoja ya kujituliza kimawazo akawa mchoraji na kwa hali hii
alinunua kibokisi kimoja cha rangi na brashi kidogo na makalatasi mengi na
akaanza kazi ya uchoraji. Na baada ya kutayarisha vitu hivi akajiingiza katika
fani hii ya uchoraji hivyo maisha yake yakawa yanaendelea vizuri bila
kuharibikiwa na akili.
mambo
14.Imesemwa kuwa ujana wenyewe unavutia lakini bora zaidi uko pale ni kuwa na shukurani katika uzeeni.
Allah swt anatuambia katika Qurani Tukufu sura Al-Baqarah, 2 : 187:
"...
Wao ni (kama) nguo
kwenu, na nyinyi ni
Familia inaanza katika bibi na bwana wenye mpangilio wa maisha ambayo yanawaelekeza wote wawili katika njia iliyobora hapo mbeleni, tunaona katika jamii ya siku hizi kuwa kuna mapambano katika jamii zetu, baina ya Mashariki na Magharibi mawazo haya yanatofautina au tunaweza kusema kuna tofauti baina ya mawazo ya Kiislamu na mawazo dhidi ya Uislamu, kwa sababu jamii ya Kiislamu imeeleza waziwazi vile mfumo wa familia unavyotakiwa kuwapo na kwa kuwa watu wanaacha tabia na tamaduni zao za Kiisilamu na kukimbilia tamaduni za kimagharibi au zile zisizo za Kiisilamu ndipo matatizo na upotofu unapoanza hivyo ni ushauri kwa wote kwanza wazingatie mfumo wa jamii katika Uislamu ndipo hapo baadaye wajaribu kuingia katika mfumo wa kimagharibi halafu shauri lake kama atapata kupotoka au atapenda kurekebisha maisha yake ili hadi mwisho wake, yawe yenye fanaka na baraka.
Ni wazi wazi kuwa Allah swt amemuumba mwanadamu,ana mambo mawili ya kuyafanya,
1.Kuendeleza kizazi ili kisiishe, binadamu waendelee kuzaana.
2. Kutimiza mahitaji
Kwa upande mwingine tunaona Allah swt amegawanya wanadamu katika makundi mawili mwanamme na mwanamke.Naona kwa maumbile mwanamme ameumbwa kwa ajili ya shughuli za nje za kutafuta mahitaji na kutafuta riziki kwa ajili yake na familia yake nzima wakati mwanamke hakupewa uwezo huo. Papo hapo tunaona kimaumbile mwanamke ametengenezwa makhsusi kwa ajili ya uzazi na malezi.
Itakuwa ni jambo lenye ugumu sana kwa mwanamme kufanya kazi za kulea na kutunza familia na kupika chakula na mambo mengineyo ambayo mwanamke anayafanya vyema zaidi na vile vile kimaumbile mwanamke inamuwia vigumu sana kufanya kazi ngumu za kupambana na maisha katika kuchuma fedha kwa ajili ya kuilisha familia yake. Na nyanja zote hizi mbili zinapingana.
Kwa mwanamme kubaki nyumbani na kulea watoto na kutunza nyumba na usafi n.k. anaweza akachoshwa katika muda wa madakika tu na papo hapo anaweza kukumbana na maswala magumu zaidi akiwa nje ya nyumba katika kutafuta riziki na kutafuta mahitajio ya familia yake hayo mambo mazito na magumu hatayajali bali atayakabili na kuyapita, na upande mwingine mwanamke kutoka nje ya nyumba kwenda kutafuta mapato kwa ajili ya riziki na mahitajio ya familia yake ni kazi moja ngumu sana kwake kimaumbile lakini anaweza kushinda nyumbani siku nzima, akilea watoto, akifanya usafi na mapishi n.k. bila kusikia uchungu au uchovu wowote.Hivyo mwanamme awe ni mwanamme na mwanamke abakie kuwa ni mwanamke.
Mazungumzo
yaliyotangulia yametuonyesha waziwazi katika maswala haya ya ndoa hivyo
tuendelee na mazungumzo yetu kuhusu faida za ndoa ni
Kazi anazoziweza
mwanamke na zile asizoziweza mwanamke, hivyo hizo ndizo faida za mkataba wa
ndoa katika mkataba wa ndoa mwanamme anachukua jukumu la kufanya shughuli
fulani na mwanamke anakubali kufanya shughuli fulani.
"...kama watakuwa
mafakiri,Allah atawatajirisha katika fadhila Zake..."
Imam Jaafer
Sadiq a.s. amesema kuwa riziki na baraka ipo pamoja na wanawake na wale
wanaowategemea. "Usemi huu unasema uhakika kuwa fani ya unyumba ni
uhifadhi wa mwanamke na kwa ufanisi wao katika fani hii wanaweza kufanya mapato
ya mwanamme yakafika mbali
Pande zote mbili baada ya kuungana kwa ndoa inawabidi wahakikishe uendelezaji na ubakiaji hai wa binadamu.Ingawaje mzigo mkubwa uliomuhimu katika hatua hii upo juu ya mabega ya mwanamke, lakini haiwezekani shughuli hii ikafanyika kuanzia mwanzoni iwapo mwanamme hatashirikishwa.
Ni faida hii ambayo Mtume Mtukufu s.a.w.w. amesema katika Hadithi mashuhuri, "Muoe,musaidiane, mustarehe na muongeze idadi yenu."
Faida ya tatu ya
ndoa ni kutimiza mahitajio ya hamu ya mwanadamu kwa njia zilizo za heshima
(tusiwe kama wanyama tukaanza kutumia njia
Ingawaje watu
wengi mara nyingine wanajaribu kutimiza mahitaji
Na kwa sababu
kama hizi na faida
Hivyo labda tunaweza kuilewa Aya ya Qurani Sura Al-Baqarah 2: 187
"...
Wao ni (kama) nguo
kwenu, na nyinyi ni
Kwa kutaja
mavazi
tunaelezwa madhumuni matatu
inapendeza, inafunika sehemu za mwili na inamuhifadhi mtu kwa baridi na joto.
Bibi na bwana
kwa kuungana pamoja wanajaribu kufunika maswala madogo madogo wanayokumbana
nayo, na umoja huu ndio unaowahifadhi dhidi ya magumu na matatizo ya mtu
anapokuwa peke yake;"nuru ya furaha na fanaka inang'ara katika maisha
Hadi sasa hivi sisi tumekuwa tukiangalia mipaka ya kikudura ya wajibu wa mwanamme na mwanamke (Yaani wajibu wa bibi na bwana).Sasa hebu tuangalie vile Uislamu unavyoweza kutuongoza katika mipaka ya Din.
Hadithi hii ifuatayo itawapa mfano wa kanuni za Kiislamu. Imam Muhammad Baqir a.s. amesema:
"Kwa hakika Fatima a.s. alichukua jukumu la wajibu wa kazi zote za nyumbani kama kusaga unga, kupika mikate, na usafi wa nyumba kwa ujumla; na Ali a.s. alichukua wajibu wa kazi zote za nje ya nyumba, kama kuleta kuni za kupikia na kuleta vitu vya kupika, n.k. "
(Biharul Anwaar, Jalada 10).
Kwa mujibu wa Hadithi hii tuliyoisoma tunaona mipaka baina ya wajibu wa bwana na bibi ni ukuta wa nyumba. Mwanamke ni mkuu katika chochote kile kilichopo katika kuta nne za nyumba na mwanamme ni mkuu katika mambo yote yaliyo nje ya kuta hizo.
Uislamu umemkomboa mwanamke dhidi ya matatizo na michafuko yote ya dunia;ili kwamba aweze kuzingatia na kutimiza wajibu wake vyema katika mambo ya unyumba.
Qurani Tukufu imekusanya kanuni zote za maisha ya nyumbani.Kama ilivyoelezwa hapo awali kimaumbile mwanamke ni jinsia dhaifu.Kwa hivyo asitegemewe kujitia katika machachari ya kutafuta maisha;badala yake mwanamme ndivyo inavyombidi atafute kwa ajili ya wote. Iwapo nyumba ni ufalme basi mwanamme ni mfalme na mwanamke ni waziri mkuu.Aya hii inatuelezea vitu vitatu vilivyo vya hakika.Hebu tujaribu kuangalia na kuchambua :-
Allah swt amempatia mmoja zaidi kuliko mwingine; Aya hii inatuelezea vile nguvu zilivyo za mwanamme katika kumlinganisha mwanamke.
Ni ilimu ya kawaida na inajulikana kisayansi kuwa mwili wa mwanamke kwa wastani uko dhaifu kuliko ule wa mwanamme. Ulinganishi ufuatao utasaidia kidogo kuelezea swala hili:-
Uzito wa moyo wa mwanamme ni baina ya gramu 280 hadi 340 wakati uzito wa moyo wa mwanamke ni kutoka gramu 230 hadi 280. Ujazo wa moyo wa mwanamme anapokuwa na umri wa miaka hamsini (50) anapofikia c.c.290, wakati upande wa mwanamke kwa baadhi yao ni 50c.c yaani chini ya 50c.c. (Gray's anatomy, chapa ya 28, 1945 ; uk. 672).
Farid Wajid Afind (Misri ) anaandika katika kitabu chake mwanamke nguvu na uwezo wa mishipa ya mwanamke ni nusu ya ile ya mwanamme; na huo ndiyo uwiano wa vile mishipa inavyofanya kazi.
Wastani urefu wa mwanamke upo chini ya sm 12 (kiasi cha inchi 4 3/4) kasoro ya mwanamme.
Kwa kawaida wastani wa uzito wa mwanamke ni kilo 5 kasoro ya uzito wa mwanamme.
Idadi ya chembe chembe nyekundu katika mraba wa milimita ya damu ya mwanamme ni milioni 5 na mwanamke ni milioni 4 1/2. (Gray's anatomi).
1.Farid Wajid Afind ananakili kwa mamlaka kuwa sehemu tano za hisia za mwanadamu (kuona, kusikia, kunusa, kuonja na kugusa, ambavyo ndivyo muhimu katika kuhisi) vya mwanamke ni dhaifu kuliko vya
mwanamme.
2. Akili, kwa wastani uzito wa akili ya ubongo wa mwanamme ni kiasi cha gramu 1380; na wa mwanamke ni kiasi cha gramu 1250 (Gray's anatomi, jalada la 28, 1945; uk. 1024) uwiano wa ubongo wa mwanamme kwa mwili wake mzima ni 1: 40; na wa mwanamke ni 1:44.
Lau vitu hivi vitano vya mwanadamu vitakuwa dhaifu basi bila ubishi tutaona kuwa huyo mwanamke ni dhaifu kabisa kimaumbile.
Farid Wajid
Afind ananakili kuwa akili ya mwanamke ni
Allah swt amemuumba mwanamke awe mwenye hisia kali kuliko mwanamme ni kwa sababu alivyoumbiwa yaani mama. Mwanamke anatoa maamuzi yake haraka kwa mujibu wa hisia zake bila ya kutumia busara, akili au uhodari wake. Na labda kwa sababu hizi na undani mwa swala hili ndio maana Qurani Tukufu inachukulia ushahidi wa wanawake wawili kuwa sawa na ushahidi wa mwanamme mmoja.
Ni jambo la
masikitiko
Je kushirikishwa huku kuna maanisha nini?
Mwanamke bado anahitajika kutimiza wajibu wake wa kimaumbile wa kushika mimba, kuzaa na kulea watoto.Wakati mwanamme hafanyi hivyo na wala mwanamme hawezi kushirikiana naye katika kumbebea mwanamke mimba, kunyonyesha watoto, kuwalea, au kuangalia watoto na kufanya kazi zote zinazojulikana kama kazi za akina mama; hali hii mwanamke ndiye anayebeba mzigo huu lakini pamoja na wajibu huu nyakati zote, mwanamme bado anamwambia mwanamke "tushirikiane kutafuta mapato ya kuendesha maisha yetu."Kwa kifupi jinsia mwenye nguvu amemkomboa jinsia dhaifu katika kubeba mzigo wake bila ya yeye kumsaidia mwanamke mzigo wake Masikini mwanamke bado anazuzuliwa kwa sauti zinazopaazwa za uhuru na ushirikishwaji wa wanawake bila ya kutambua njama na mbinu za mwanamme za kumtwisha mzigo wake.Kwa kweli sitakuwa na nafasi ya kuorodhesha maafa -kijamii,kinyumbani na kiuchumi -unaotokana na mwanamke kujiingiza katika harakati hizi za kuchuma mapesa.
Vyovyote vile,mwanamme amefanywa kuwa mlinzi wa mwanamke, kwa sababu ya mwili wake wenye nguvu na akili na busara yake na kwa sababu amewajibishwa kumstiri na kumshughulikia mke wake. Hivyo kwa sababu hizi na zinginezo mwanamke amelazimishwa kumtii bwana wake.
Mtume Mtukufu s.a.w.w. amesema:"Wanawake waliotukuzwa kuliko wote mbele ya Allah swt ni wale ambao ni watiifu kwa mabwana zao na ambao wanabakia katika mipaka ya nyumba zao."
Iwapo wanawake
watabakia katika mipaka
Tunaelewa kuwa leo taasisi yoyote au kikundi chochote kiwe cha siasa au hata michezo inahitaji kiongozi. Hivyo ni jambo la kustaajabisha mno kuona kwa wale wanaotetea usawa wa jinsia (yaani usawa wa mwanamke na mwanamme) wanapokanusha kuwa mwanamme si kiongozi katika unyumba.Je nyumba inakwenda kiholela au kuna mipango inayopangwa na kutekelezwa kwa ushirikiano wa wawili hivyo kuwapo kwa kiongozi mwenye maamuzi ya mwisho ni muhimu sana hata kama itakuwa ni maswala ya nyumbani.
Wataalamu wa mambo ya kale wanasema:"Katika zama za kale mwanamke alikuwa huru alikwenda alikotaka, alifanya kile alichokitaka yaani kwa kifupi alikuwa ni bwana mwenyewe. Lakini katika zama hizo za kale alikuwa hana heshima yoyote wala utukuzo wowote, kwa sababu kulikuwa hakuna familia kila mmoja alikuwa akiishi peke yake.
Lakini familia zilipoanza kutokezea,hali ilianza kubadilika kutokezea mizunguko ya familia, mwanamke alipoteza uhuru wake na ilimbidi akubali kanuni na vishindikizo vingine vya kifamilia, lakini papo hapo alijipatia heshima na utukuzo wa hali ya juu mambo ambayo alikuwa hakuyafikiria hapo kabla.
Katika nchi za
Magharibi
ushirikishwaji
wa mwanamke
umewafanya wanawake wengi
Mtu hawezi
kupanda jahazi mbili kwa wakati mmoja hivyo lau yeye atajiingiza katika mambo
ya kuchuma mapesa basi watoto wake watanyimwa haki
Mwanamke mmoja alimwuliza Mtume s.a.w.w.:"Ewe Mtume wa Allah swt, je ni nani anayo haki zaidi juu ya mwanamme?"Mtume s.a.w.w.alimjibu: "Wazazi wake."Baadaye alimuuliza:"Je nani mwenye haki zaidi juu ya mwanamke?" Mtume s.a.w.w. alimjibu: "Bwana wake."
Wakati mmoja walimwuliza Mtume s.a.w.w.:"Sisi tunawaona baadhi ya watu wakiwasujudia baadhi ya watu wao." Mtume s.a.w.w.aliwajibu:"Iwapo mimi ningekuwa na uwezo wa kumruhusu mtu yeyote kumsujudia mtu mwingine basi ningemwamurisha mwanamke amsujudie bwana wake."
Imam Jaafer
Sadique a.s. amesema: "Allah swt alimtumia ujumbe Mtume s.a.w.w., mwambie
Na kwa sababu
hii ndiyo maana Mtume s.a.w.w.alimwambia
"Ewe
Itatubidi lazima tukumbuke sheria iliyo ya uchokozi na udhalimu, kamwe hawezi kuwa sahihi. Hivyo misingi ya mamlaka ya bwana yamewekwa kwa mapenzi na wala sio vitisho na uonevu. Allah swt anatuambia katika Qurani Tukufu sura Ar-Rum 30:21
"..... naye Amejaalia
mapenzi na huruma baina yenu..."
Katika Aya hii tunaona maneno mawili mapenzi na huruma,yametumika katika mapenzi ya unyumba.Kwa kawaida mwanamke tukiongelea ukweli anampenda bwana wake zaidi mno. Yeye yuko tayari, kujitolea nafsi ,mwili wake kwa ajili ya mume wake. Hivyo mapenzi ndivyo yanavyotelezea hali hiyo.
Kwa upande mwingine mapenzi ya mwanamme kwa mke wake yana sura tofauti kimaumbile - hapo hakuna swala la kujitolea. Na hivyo ndivyo huruma inavyotumika.
Vyovyote vile mapenzi, utiifu na huruma ndio mambo ya kutimiza katika maisha ya mwanadamu: Kudhatiti mambo ya nyumbani na uzazi.
Ndipo hapo itambidi aweze kuweka malengo ya matumizi katika misingi hiyo. Mtume Mtukufu s.a.w.w. amesema: "Allah swt atamjalia nguo sabini elfu huko Jannah yule mke ambaye atakuwa ameridhika kwa kiasi cha mapato mume wake anachokipata kwa uwezo wake."
Kwa wale wanaokwenda kinyume na busara hii,Mtume Mtukufu s.a.w.w. amesema: -
"Hakuna mwanamke ambaye anamuomba mume wake zaidi ya uwezo wake, na asiyetosheka kwa kile anachopata cha kuishi - kiwe kidogo au zaidi - wala kutosheka na neema anayojaliwa na Allah swt, isipokuwa atakuwa ni miongoni mwa wale ambao matendo yao mema hayakubaliwi, na madhambi yao hayatasamehewa na Allah swt atakuwa daima akiwachukia hadi hapo hao wanawake watakapotubu."
Ni ukweli kwamba
matatizo ya kinyumbani yanamchukiza mtu
Iwapo mwanamke atatokwa na machozi wakati wa kupika kwa sababu ya
moshi, Allah swt atamwandikia thawabu za
shahidi
(waliouawa katika njia ya Allah swt)
ambao macho
Na iwapo mwanamke huyo anaye msaidizi katika mambo ya nyumbani na hivyo anapata fursa kidogo basi asiupoteze huo wakati; badala yake, muda huo utumike katika shughuli zingine zenye manufaa katika mipaka yake ya nyumbani.Mtume Mtukufu s.a.w.w.amesema:"Kazi nzuri kabisa ya mwanamke ni ufumaji; kwa sababu kwa kila uzi mmoja anasamehewa dhambi moja na kupewa thawabu moja."
Mwanamke amevutiwa katika utunzaji wa nyumba bora katika maneno yafuatayo:-
"Mwanamke yeyote katika nyumba ya mme wake, anapohamisha kitu kutoka nafasi moja hadi nafasi ya pili kwa nia njema, Allah swt anamwangalia (kwa baraka), na yeyote yule anayetazamwa na Allah swt kwa rehema, basi kamwe haadhibiwi."
Kwa hivyo tunaona katika maswala ya nyumbani mwanamke inambidi aangalie mambo yote mazuri kwa nia njema ya kuendeleza nyumba ya bwana wake na anayekuwa na nia mbaya ya kusema anachukua vitu nje ya nyumba yake bila ya bwana wake kujua kwa nia mbaya basi huyo naye atapata adhabu za Allah swt.
Uendelezaji wa binadamu na asili ya kuwapo kwake na kwa ujumla ni wajibu wa kila aina, vyote viko pamoja na mwanamke.
Kwa hakika
mwanamke amebarikiwa jambo
Uislamu
haujapitiwa vile mwanamke anavyobeba mzigo huu na maswala
Mwanamke anapata thawabu za kudumu katika kila hatua hizi, na kwa mujibu wa Mtume Mtukufu s.a.w.w. amesema:
Hatua ya kwanza:
"Wakati mwanamke anaposhika mimba, katika kipindi hicho ni sawa na yule anayefunga saumu daima,anayesali na anayepigana Jihad kwa nafsi na kwa mali yake katika njia ya Allah swt."
Hatua ya pili:
"Wakati mwanamke anapozaa, anapata thawabu kupita kiasi kwamba hatuwezi kuzielezea kwa sababu ya tendo hili jema."
Hatua ya tatu:
"Wakati mwanamke anapomnyonyesha mtoto wake maziwa, Allah swt anamjalia thawabu sawa na kumfanya huru mtumwa (kutoka kizazi cha Mtume Ismail a.s. ) kwa kila mara anaponyonyesha."
Hatua ya nne:
"Uleaji wa watoto - swala hili linazungumziwa zaidi katika maswala ya haki za watoto."
Taarifa ifuatayo
kutoka
Hadithi tukufu lazima isomwe
kwa uangalifu
"Ewe Fatima mwanamke asimletee chochote kile mbele ya bwana wake asichokipenda; daima awe mtunzi muhifadhi wake; lazima awe mkweli na mtiifu mbele na anapokuwa hayupo; aukate (ukali na majeraha) ya ulimi wake (dhidi ya bwana wake); amtazame vyema pale anapohitajika bwana wake kutazamwa na kutunzwa; amtimizie mahitaji yake yote na daima aangalie ahali yake; kwa sababu kumtazama bwana wake ni ibada; na kamwe asimkaribishe mtu katika chakula isipokuwa napokuwa ameruhusiwa na bwana wake; na daima mwanamke awe akiridhika na kile alichojaaliwa na Allah swt; na kamwe asimwache bwana wake, na kama atamwachia, basi sala zake, saum na zaka hazitakubaliwa na Allah swt hadi hapo bwana wake atakapokuwa amemridhia."
Quran Tukufu
inafafanua misemo ya kuwazulia Waislamu
juu ya utumwa wa wanawake katika Islam swala ambalo wanamagharibi
waliomajahili ndio wanaotumia
Kama iliyoelezwa hapo awali kwa mujibu wa akili na kwa mujibu wa sheria za Kiislamu, mwanamme ndiye anayewajibika kwa ajili ya kumgharimia na kumtafutia mahitaji yote ya mke wake, na katika mtazamo huu wa uwajibikaji ambao upo katika mapenzi.
Inaonekana kutoka juu kuwa chochote kile anachotaka mwanamke kwa ajili ya utulivu wa akili yake kuwa bora kiroho, na kuridhika na mahitajio yake, vinaweza kutenganishwa katika makundi mawili:
1. Mapenzi halisi.
2. Kutizamwa vyema.
Lau mtu atakaa kupitia orodha ya madai ya wale wenye kutetea ukombozi wa wanawake, basi utagundua kuwa haki hizo zote ambazo zinakubaliana kiakili utaona yako katika makundi haya mawili.
Islam imewaamrisha kwa kuwasisitiza wanaume kuwapa uhuru wake zao kufurahi haki zao bila ya kubugudhiwa vyovyote vile. Mtume Mtukufu s.a.w.w. amesema:
"Mwanamke yeyote atakayembughudhi mume wake kwa ulimi wake....atakuwa ni wa kwanza kuingizwa Jahanam. Na, vivyo hivyo, iwapo bwana wake hatamfanyia haki."
Imam Jaafer Sadiq a.s. amesema:
"Mimi nina uhakika kuwa mtu anapokuwa
bora zaidi katika imani na Islam basi vivyo hivyo ndivyo mapenzi ya wake zake
inavyozidi."
Aya isemayo: Allah swt ameweka mapenzi na huruma baina yenu, inaonyesha kuwa mapenzi ya kindoa ni baraka za Allah swt; na vile mtu atakavyokuwa na imani zaidi katika Allah swt, na ndivyo vivyo hivyo rehema na baraka zaidi za Allah swt zitakuwa juu ya jozi hiyo (yaani bibi na bwana ).
Na kwa sababu hii Imam Jaafer Sadiq a.s. amesema:”Miongoni mwa desturi za Mitume ni mapenzi ya
wanawake."
Mtume Mtukufu
s.a.w.w. amesema,
"Ijulikane mtu
bora miongoni mwenu ni yule ambaye ni bora kwa wake zake na mimi ni bora kwa
wake zangu."
Vivyo hivyo ,ameendelea kusema: "Rehema na baraka za Allah swt ziwe juu ya mtumwa wake ambaye anawafanyia wema baina yake na mke wake kwa hakika, Allah swt amempa mamlaka zaidi juu ya mke wake na kwamba amemfanya awe ni mtu mwenye kumhifadhi mke wake."
Kwa mujibu wa
sheria za Kiislamu, imesisitizwa kuwa mwanamme anapokuja nyumbani aje na uso
wenye bashasha, mchangamfu. Nyumba hiyo itakuwa ni Jannah iwapo sheria
Katika aya za
Qurani Allah swt anawaambia wanaume kuwatendea wema wake zao. Mbali na aya hiyo
ya hapo juu ipo aya nyingine inayosema: "Qurani,sura
An-Nisaa, 4 : 19
"...Na
kaeni nao kwa wema ..."
Kuwatendea wema
kwa mujibu wa Hadithi inamaanisha kuwa kile ambacho atapatiwa mwanamke, kwa
kiasi kinachowezekana, hali na desturi alivyokuwa akiishi katika majumba ya
wazazi wake; ili kwamba asipate kukabiliana na hali ya kutoishi kwa raha na
vile vile asipate ugumu wa kupata magonjwa ya akili kwa sababu ya kukosa raha
katika majumba ya mabwana zao.
Na iwapo bwana, kwa sababu za uchumi wake kuwa kiasi,anashindwa kumpatia hali hiyo bora basi hawezi kulaumiwa.
Qurani Tukufu
inatuambia katika sura
Al-Baqarah
2 : 236
"... Mwenye wasaa kadiri awezavyo,na mwenye dhiki kadiri awezavyo..."
Imam Jaafer Sadiq a.s. anatuambia: "Wale wote wanaomtengemea bwana ni wafungwa wake, na mtumwa wa Allah swt aliyebora kuliko wote mbele ya macho ya Allah swt ni yule ambaye anawatendea wema wafungwa wake."
Vivyo hivyo Imam Musa al-Kadhim a.s amesema:"Wale wote wanaomtegemea mwanamme ni watumwa wake. Kwa hivyo iwapo Allah swt anamjalia baraka zake mtu yeyote, basi itambidi na yeye aitumie zaidi kwa ajili ya wafungwa wake; na lau hatafanya hivyo, basi neema na baraka hiyo itatoweka.
Kwa mujibu wa Sharia za Kiislamu, malipo, matumizi au posho ya mwanamke ni malipo ya utiifu wake. Iwapo huyo mwanamke hamkatalii mume wake haki zake, basi ana haki zake zote za kuruzukiwa.Iwapo bwana, kwa sababu ya matatizo yake ya kiuchumi, anashindwa kumtimizia posho na ruzuku za mke wake, basi atabakia na deni hilo akidaiwa na mke wake; na hivyo itambidi kumlipa mara moja pale apatapo mapesa n.k.Kwa kifupi kumtimizia mwanamke haja zake ni juu ya misingi nipe na nikupe, na mwanamme itambidi alipe kwa hali yoyote ile.Imam Jaafer Sadiq a.s. amesema: "Amelaaniwa yule mwanamme ambaye hawajali wale wanaomtegemea."
Kwa upande mwingine mwanamme sio wa desturi hiyo kwa hivyo, Uislamu umemfaradhia mtu awe na subira na usamehevu wakati wa hasira za mke wake.Inambidi mwanamme amvumilie mke wake kwa kuweka maanani udhaifu wake na kwa kukumbuka kuwa mwanamke anatawaliwa na hisia zake.
Allah swt
anatuambia katika Qurani tukufu sura
An-Nisaa
4 :19
"... na kaeni nao kwa wema..."
Hatuwezi
kukanusha kuwa kazi hii ya kupewa ni ngumu
Allah swt
anatuambia katika Qurani sura
Al-Baqarah
2 : 201
"... Mola wetu! Tupe mema duniani na mema Aakhera,na utulinde na adhabu ya Moto."
Miongoni mwa ufafanuzi zaidi wa aya hii, Imam Amir -al- Muminiin Ali ibn Abi Talib a.s. amesema:
"Mema katika dunia
hii inamaanisha mwanamke mwenye silka nzuri,na
mema
katika Aakhera inamaanisha
hurul-ain
na
adhabu za moto inamaanisha
mwanamke mwenye silka mbaya."
(Tafsiri
-
Kusema kwa mwanamke mwenye tabia, silka na desturi mbaya, mke mwenye hasira kali ni adhabu ya motoni inawakilisha uhakika kwa njia inayowezekana. Lakini inatubidi sisi pia tuwe tukiitazama hii Hadith:-
"Kwa hakika Mtume Ibrahimu a.s. alimlalamikia Allah swt dhidi ya hasira za mke wake Sarah. Hapo Allah swt alimtumia ujumbe ukimwambia kuwa kwa hakika mfano wa mwanamke ni mfano wa ubavu;iwapo utajaribu kuunyoosha utavunjika; na lau iwapo utauachia ubavu wako ulivyo basi utafaidika nao."
Kwa kifupi aya
nyingi mno za Qurani tukufu na
Hadith
nyingi mno zinatuusia, zinatuamrisha kuwa muugano wa bibi na bwana uimarishe na
kufanya madhubuti mapenzi yao na umoja wao kiasi wanapokuwa wameungana kindoa,
hata kama itabidi mmoja ajinyime kiasi fulani na vile vile kujaza kwa subira
inayozidi uwezo wa mtu mwenyewe. Na kwa kufuata kwa kanuni
Uislamu unatambua waziwazi kuwa hii njia ya kubuni mambo tu haisaidii kuwa mema. Isipokuwa kanuni zinazotumika na desturi miongoni mwa bibi na bwana ndizo zinazoleta amani katika nyumba.Hotuba kubwa kubwa hazitamsaidia mtu wa kawaida iwapo hayatakuwa kwa mujibu wa akili na vile vile lau hazitakuwa katika uwezo wake.
Ndoa bora za Kiislamu ni zile ambazo bibi na bwana wanapendana na wanaheshimiana na kila mmoja kuheshimu haki za mwenzake.
Lakini dunia hii haipo na watu wacha mungu na wenye kufahamu tu bali imejaa zaidi kwa watu wenye mioyo migumu na wanawake wa aina hizo; wao hawajali uharibifu wanaouleta katika jamii ya Kiislamu kwa sababu ya matendo yao na kuchezea maamrisho ya Sharia za Kiislamu. Hivyo ilikuwa ni lazima kutengenezwa Sharia ili kurekebisha desturi zao.
Chanzo kikuu cha
magomvi ni kupuuzia kwa wajibu wa mtu mmoja kwa ajili ya mwenzake.Dharau hiyo
inawezekana ni upande wa bwana au upande wa mke, au pande zote mbili. Islam kwa
kuzingatia maswala nyeti
Iwapo mke
ataacha wajibu wake na kumsumbua bwana wake, basi Allah swt
anaelezea laana za aina tatu kwa ajili yake,
katika sura
An-Nisaa
4 : 34
"... Na wanawake ambao mnaona uasi wao kwenu waonyeni na waacheni peke
Hatua ya kwanza:
"Itambidi kwanza bwana ajaribu kumuelimisha mke wake na
kumshauri abadilishe desturi ya tabia zake. Mwanzoni nasiha na majadiliano
baina
Hatua ya
pili:
"Iwapo
Hatua ya
tatu:
"Lakini, iwapo upuuzaji wake huo umezidi, na mawaidha, nasiha
na mgomo wako huo haukumuathiri, basi matibabu madogo hayawezi kuwa na faida
yoyote.
Katika hali ya kuzidi kabisa
Lakini kumwijia kwa mabavu huko lazima kuwe ni kwenye hali nzuri na nidhamu bora. Imam Muhammad Baqir a.s. amesema:
"Kwa hakika, mjeledi kwa mswaki wa meno. Sharia inasema kuwa isiwe unampiga ngumi kiasi cha kuvunja mfupa au kuacha doa jekundu au michubuko, na kamwe mwanamme haruhusiwi kumpiga usoni mwanamke, na wala mahala pamoja kupigwa mara nyingi."
Iwapo matibabu haya yataondoa sababu za ugomvi, basi inambidi mwanamme (bwana ) amwie kwa wema na atimize haki zake zote kwa mara moja.Lau katika hali hii ya ugomvi na kujaribu kumrudisha mke katika hali yake akaomba msamaha na akatubu kosa lake basi inambidi mwanamme na hasira zake na ugomvi uishie pale pale, na mrudishie haki zote za mwanamke anazostahili yaani mapenzi, haki na mambo mengine yote kama tulivyokwisha kuelezwa hapo nyuma. Sentensi ya mwisho ya Aya ya hapo juu inatuambia hivi:
( baadaye, wanaporudi katika utiifu, basi usiwatendee tena hasira).
"... Na
Na iwapo kwa
upande mwingine bwana ndiye yuko katika makosa na amepuuzia wajibu wake kwa mke
wake, basi mwanamke itambidi kwanza ajaribu kuleta uelewano baina
Allah swt
anatuambia katika Qurani tukufu katika sura
An-Nisaa
4:128
"... Na kama mke akiona kwa mume wake kugombanagombana na
kutenganatengana,basi si vibaya kwao wakitengeneze baina
Na iwapo njia hii haitawezekana kuleta matunda mazuri basi mwanamke ana haki ya kuchukua mashitaka yake mbele ya Hakim-i-Sharia (kadhi au mujtahid ) ambaye ana mamlaka ya kila aina katika usuluhishi wa mfarakano kwa mujibu wa Sharia na maadili.
Iwapo bibi na
bwana watapuuzia haki zao, basi hapo kwa kweli kuna haja ya msaada wa mtu
mwingine ili kumaliza mzozo wao. Hivyo Allah swt ametuamrisha katika Qurani
tukufu sura An-Nisaa
4:35
"... Na kama mkijua kuwa kuna ugomvi baina ya mke na mume basi pelekeni, mwamuzi mmoja katika jamaa za mwanamme, mmoja katika jamaa za mwanamke."
Uadilifu na
maamuzi
1.Si haramu kusuhubiana na mke anapokuwa na mimbalakini iwapo kutakuwa na hatari kwake yeye au mtoto aliye tumboni,basi katika hali hii itakuwa ni haraam kusuhubiana.Hata hivyo wataalamu wanapinga kusuhubiana wakati mwanamke anapokuwa na mimba.
2.Wazee waliwauliza Maulamaa iwapo watoto watazaliwa vile yalivyoelezwa hapo awali,lakini walijibu kuwa hayo yote yapo mikononi mwa Allah swt.
3.Maelezo yote
yalivyoelezwa kama ni makruh (karaha) basi yachukuliwe ni karaha na
4.Iwapo mwanamke alikuwa katika hali ya janaba na hakuwahi kuoga ghusl-i-janaba na akaingia katika haidh,au baada ya kutoka haidh lakini kabla ya kufanya ghusli Haidh akaingia janaba (akatakiwa kufanya ghusli janaba) yaani anatakiwa kufanya ghusli zote mbili :Janaba na Haidh .Katika swala hili hatakiwi kufanya ghusli mbili mbalimbali isipokuwa atafanya nia moja tu ambayo itafaa kwa ghusli zote mbili.
5.Kutoa manii kwa mkono ni haraam na vile vile madaktari pia wanapinga mno kwani kunadhoofisha uwezo wa mtu na hatimaye kupoteza nguvu za kiume.
6.Kuingilia kwa njia ya nyuma ni haramu na ni yenye madhara makubwa sana.
7.Kutalazimika kufanya ghusl-i-janaba iwapo kutatokwa na manii kwa njia yoyote ile ya kutumia mkono,kusuhubiana au kuingilia kwa sehemu ya nyuma au katika usingizi.
8.Iwapo mtu ataota ndoto ya kusuhubiana na mwanamke lakini hakutokwa na manii,basi halazimiki kufanya ghusl-i-janaba.
9.Ni lazima kusuhubiana mara moja katika miezi minne lakini ni sharti kuwa kusiwepo na udhri wowote wa kisheria wala asiwe amekwenda safarini.
10.Ni swala mashuhuri miongoni mwa Maulamaa kuwa usiku saba ni makhsusi kwa ajili ya mwanamke aliyeolewa bikira na usiku tatu kwa mwanamke asiye bikira.
11.Ni hukumu kwa ajili ya
wanaume kutoziweka nywele
za sehemu zao za siri kwa zaidi ya siku arobaini (na wazikate
kabla
ya siku hizo) na wanawake
wasiziweke zaidi ya siku ishirini (na wazikate kabla ya siku hizo). Ipo riwaya
ya Imam Jaafer as-Sadiq a.s. isemayo:"Msiziweke nywele zenu za sehemu zenu
za mwili zinazotakiwa kukatwa i.e.mashurubu, kwapani
,na sehemu za siri,na muziondoe kwa kutumia
nurah.
12.Kuna faida mno kusuhubiana na mwanamke ambaye ametoka katika haidh na ameoga ghusl-i-haidh.
13.Wapinzani wa swala hilo juu wanasema ni vyema kujiepusha na mwanamke ambaye ametoka haidh kwa siku kumi ambavyo hatapata udhaifu na siku ishirini zilizobakia ni nzuri ambamo siku kumi za katikati ndizo nzuri mno.
14.Imeruhusiwa kumwoa msichana mdogo,lakini iwapo hatakuwa ametimiza umri wa miaka tisa au kuzidi basi ni haraam kusuhubiana naye.
15.Iwapo mwanamme atamwoa msichana asiyefikia au kutimiza umri wa miaka tisa na akasuhubiana naye basi atambue kuwa ametenda tendo la dhambi na iwapo amemjeruhi katika sehemu zake za siri yaani iwapo sehemu ya kike kuungana na sehemu ya haja ndogo au sehemu ya kike kuungana na sehemu ya choo (njia ya nyuma) basi atambue kuwa huyo mwanamke atakuwa haraam kwake yeye kwa umri mzima.Lakini Maulamaa wanasema kuwa nikah (ndoa) haivunjiki kwa hivyo kamwe hataweza kusuhubiana naye kwani atakuwa haraam kwake kusuhubiana naye.Na iwapo hali kama hiyo itatokea kwa mke wake ambaye amekwisha timiza umri wa miaka tisa au zaidi basi hatakuwa haraam kusuhubiana naye.
16.Mtu hawezi kumwoa dada wa mke wake aliye bado hai na iwapo atathubutu kufanya hivyo (yaani kuwaoa dada wawili wakiwa ni wake zake wawili) basi ni dhambi na nikah hiyo itakuwa batil na watoto watakaozaliwa watakuwa ni waladuz-zinaa.
17.Iwapo mwanamme atasuhubiana na mwanamke aliye na bwana ambaye yu hai au mwanamke ambaye hakumaliza kipindi chake cha Iddah basi kamwe hataweza kumwoa huyo mwanamke mbeleni.
18.Iwapo mtu alisuhubiana na mwanamke asiye na bwana (ingawaje ni dhambi la zinaa aliyojipatia) lakini iwapo atataka kumwoa,basi anaweza.
19.Iwapo mwanamke (mwenye bwana) atafanya zinaa na bwana mwingine nje ya ndoa yake au mwanamme (mwenye mke) atafanya zinaa na mwanamke mwingine nje ya ndoa yake basi wote wanakabiliwa na adhabau ya kukalishwa shimoni na kupigwa mawe hadi kufa. Na iwapo ni mwanamke asiye na bwana au mwanamme asiye na mke basi watachapwa viboko mia moja.
20.Iwapo ni mwanamke aliyepewa talaqa basi hakuna mtu atakayeruhusiwa kumwoa kabla hajamaliza kipindi chake cha Iddah na iwapo mtu yeyote atathubutu kufanya hivyo,basi mwenye kuoa, kuolewa na wote walioshiriki katika kufanikisha hivyo wanalaaniwa na Allah swt na wanajitafutia adhabu zake. Na iwapo watasuhubiana basi hiyo ni zinaa na mtoto akizaliwa atakuwa waladuz-zinaa na atambue waziwazi kuwa kamwe hawezi kumwoa hata kama atataka hivyo.
21.Iwapo mwanamme atafanya tendo la kubaka (atamwingilia kwa nguvu) mwanamke basi atambue waziwazi kuwa kamwe hawezi kumwoa (aliyebaka) huyo mwanamke wala hawezi kumwoa mama,dada na binti yake.
22.Mwanamme atakaye kuwa amempa mke wake talaqa tisa kwa mujibu wa Shariah,basi atakuwa haraam kwake daima.
23.Iwapo mwanamme atakuwa amesuhubiana na wifiau shanghazi yake,basi hawezi kuwaoa mabinti wao (watoto wa shanghazi na watoto wa wifi) .
24.Iwapo kutakuwa na mume ambaye ameishi na mwanamke kwa kipindi cha miaka thelathini au hamsini au hata zaidi ya hayo lakini kwa ndoa ya muda (muta') na atakapokufa mmoja wao basi hakuna atakayemrithi mwenzake.
25.Haki ya urithi wa kutoka mali ya baba kwa ajili ya watoto itakuwa sawa kabisa kwa mujibu wa Shariah za Dini iwapo watakuwa wamezaliwa na mama aliyeolewa kwa ndoa kamili,au ndoa ya muda au amezaliwa na kijakazi wa baba yake.
26.Iwapo mwanamme atampa mke wake talaqa,basi itabidi ishuhudiwe na waadilifu wawili ndipo hapo sigha hiyo itakaposomwa na nikah ya mwanamke haivunjiki hapo hadi mwanamke huyo kutimiza kipindi cha Iddah yake (ndipo hapo atakapokuwa huru kuolewa) na iwapo ataolewa,basi ndoa hiyo itakuwa haraam na iwapo watasuhubiana basi hilo ni tendo la zinaa.Hata hivyo siku hizi kuna mtindo wa kupeana talaqa za haraka haraka ilimradi mmojawapo anataka kuoa mwingine basi atafanya kila aina ya hila ya kujifanyia njia saheli ili mradi afanikiwe katika adhma yake,lakini ikumbukwe wazi kuwa iwapo Shariah za dini ya Islam kama hazikufuatwa na kutimizwa basi mambo yote yatakuwa ni haraam.Kutoa na kupewa talaqa kuna masharti maalum na yenye msimamo na mipangilio yake.
27.Iwapo bibi na bwana
walikuwa
mushrik na wote kwa pamoja
wakawa Waislaam,basi ndoa yao itahalalika na kuwa ya daima lakini iwapo mmoja
wao atakuwa Mwislaam na baada ya kupita kipindi cha
Iddah
hawi
Mwislaam basi
nikah inavunjika na haitawezekana kamwe
hadi awe Mwislam.
28.Iwapo bwana atakuwa Mumiin na mke akiwa
mushrik,na iwapo mke hatabadilisha imani
yake (akawa Mwislam) basi itakuwa ni swala kama la hapo juu kwani huyo bibi
hatakuwa mke halali
wala bwana hatakuwa
halali kisharia.Kwa kifupi
wote wanakuwa
wametoka katika
nikah.
29.Iwapo mke atakuwa Mumiin na bwana atakuwa mushrik,basi hukumu yake ni kama ilivyozungumzwa hapo juu katika na.28,yaani. uhusiano wao unakuwa umevunjika kindoa.
30.Bwana Mushrik anapokubalia Islam na akawa Mwislaam lakini mke akabakia mushrik, na baada ya kupita kipindi mke akawa Mwislaam,basi katika hali kama hii kwa mujibu wa Shariah,ndoa yao ilikuwa imekwishavunjika (hawakuwa na ndoa) na bwana haelewi masuala haya na anamchukulia mke wake kama yu halaali kwake,na siku atakapokuja kujua masuala haya kishariah basi itambidi afanye nikah haraka.
31.Watu wengi sana wanadai kuwa wao wamekuwa Waislaam lakini wake zao wanakataa kata kata kuwa Waislaam na ilhali wameshazaa nao watoto hivyo hawawezi kuwapa talaqa wake zao kwa sababu kama hizo na lawama na aibu kutoka kwa jamaa zao.Kwa hivyo "Mungu atatusamehe tu,sisi tufanyeje?".
Sisi tujiulize kuwa hapo kosa ni la nani na anayetakiwa kulaumiwa ni nani.Hivyo itawabidi wasiwachukulie wake kama hao kama ni wake zao na wala wasi suhubiane nao na hivyo tu ndivyo watakavyoweza kujiepusha na madhambi.
Sasa tuzungumzie
swala la
toharah kwani chakula
anachokipika ni
najis na nguo na vyombo
anavyoviosha pia ni
najis kwa hivyo
ni haraam na sala zitakuwa
batil
hivyo itambidi kuchukua hatua za kujitoharisha
kishariah na kuchukua hatua zote za
tahadhari ili aweze kusali na kufunga saumu bila ya kuhatarisha
amali
zake za
ibadah.
Iwapo hatafanya hivyo na kuishi na mke wake mushrik na vyote atakavyopatiwa na mke wake kwa ajili ya wudhuu,ghusli, sala na saumu basi vyote vitakuwa ni batil. Hivyo mwenyekujitakia hayo,itambidi atafute ufumbuzi wake. Ama sivyo matokeo yake yapo bayana.
Watu wengi wanasema "Je mwenye kukubali matendo yetu ni Allah swt au ni Mashekhe wetu?" Kwa kweli huku ndiko kujidanganya nafsi zetu na kujihadaa kwani Shariah kuhusu sala,saumu na mengineyo ni ya Allah swt na wala si yetu hivyo ni kwa mujibu wa hayo tu, hakuna Shariah ya aina yoyote ile ambayo mtu anayo ruhusa kuibadilisha kwa mujibu wa matakwa yake.Je ni Sheikh yupi ambaye anataka kujitumbukiza bure katika moto wa Jahannam kwa kumsingizia Allah swt,Mitume a.s. na Maimamu a.s? Hivyo sisi pia inatubidi kufanya utafiti zaidi juu ya masuala ya Din kwani ni fardhi yetu kujua masuala yote ya Din.
32.Ingawaje Islam
imeruhusu kuoa wake wanne kwa wakati mmoja lakini imeweka Shariah kali mno ya
kutimiza na kuhakikisha
uadilifu miongoni
mwao.Itambidi mtu atafiti zaidi juu ya masuala haya katika
fiqh.
33.Mke hawi haraam baada ya kumpatia talaqa, illa baada ya kupita kipindi cha Iddah.Iwapo mume atataka kumrejea mke wake kabla ya kipindi cha Iddah kuisha, na iwapo atakuwa na uhusiano wa mume na mke,basi talaqa itavunjika na hakuna haja ya kusoma nikah tena.
34.Iwapo mume atampa talaqa mke wake na baada ya kupita kipindi cha Iddah atataka kumrejea tena mke
wake basi itambidi kusomewa nikah tena.
Si lazima kuwa
mwanamke huyo aolewe na kusuhubiana na mwanamme mwingine na kupewa talaqa
ndipo bwana wa kwanza aweze kumrejea.
35.Mwanamme hawezi kumpa talaqa ovyo mwanamke kwa sababu zisizo na msingi kishariah.Hivyo itambidi mtu kutafiti vyema masuala ya talaqa katika Shariah kwa pande zote mbili kwani kuna mambo mengi ya kuzingatia na kuyatekeleza yakiwemo pamoja na haki ya mke na watoto.Hivyo tusidhani kuwa tutakapomwambia mke "nimekupa talaqa" basi siyo kwamba amepata talaqa bado anakuwa amebakia katika nikah au kwa kupewa talaqa mahakamani,kwani haki zake zote bado zipo juu ya bwana wake.Shariah za Kiislamu ni Shariah halali hivyo Shariah za nje ya Islam hazitabadilisha msimamo wa Islam.
Wanaume wengi mno wenye ndoa huwa na tabia ya kuingiliana pamoja na wanawake nje ya ndoa yao (malaya) ilhali wakijua kuwa kufanya hivyo ni kinyume na Shariah za Dini na ni ghunah-i-kabirah (dhambi kubwa mno).Pamoja na hayo kuna madhara mengi mno ya kimwili pia na hatimaye mtu kufikia hatua ya hatari kwa siha yake.Ni dhahiri kuwa raha na starehe za huyo malaya pia zinatolewa na mke wake na mke wa nyumbani huweza kutoa hata zaidi ya hayo.
Tumeona daima kuwa wanaume waendao na malaya huwa wanaadhiriwa na kudhalilika katika jamii inayothamini ndoa halali na hatima yao huwa mbaya kwani huwa wamefilisika kimali na vile vile miili yao pia inakuwa imekwisha.Yaani kudhoofika na kupatwa kila aina ya magonjwa kama magonjwa ya ngozi,ukhanisi na siku hizi ugonjwa wa ukimwi, kwani malaya huwa hana bwana mmoja illa kila mwenye chochote ndiye bwana wake,ukitoka wewe ataingia mwingine kwani wao wanataka kila wakati wapate 'kipya' nao pia hawataki kula pilau kila siku kama wewe unavyodai. Baada ya mwanamme huyo kujitumbukiza na kujiangamiza yeye mwenyewe katika magonjwa mabaya kabisa huwaambukiza wake na watoto wake na hata familia yake nzima inaweza kuteketezwa kwa kutokana na maovu yake.Hivyo inampasa kila mwanamme amwangalie mwanamke malaya kama nyoka mwenye sumu kali na hivyo inambidi kujiepusha naye kabla hajapata sumu hiyo mwilini na maishani mwake.
Mara nyingi mno sababu za kumfanya bwana aende kwa malaya huwa ni wake zao nyumbani.Kwani kwa kutokana na magomvi au kutoelewana vyema baina ya bwana na bibi au kwa kutokuwa na programu nzuri ya maisha ya nyumbani.Vile vile imewahi kuonekana kuwa huwa mmoja wao hataki kusuhubiana wakati fulani ambapo mwenzake anataka kwa nguvu,na katika hali kama hii ndipo inamfanya kufikiria njia ya kutaka kwenda nje kujiridhisha.
Hivyo inambidi bibi na bwana kuwajibika vyema katika masuala haya.Na daima tukumbuke kuwa katika maisha yetu yote mapenzi na bibi au bwana ni nguzo mojawapo ilipojengeka maisha yetu,na iwapo itadhoofika nguzo hiyo,basi itaweza kuporomosha maisha yetu.Na swala la kusuhubiana ni nyeti mno katika maisha ya ndoa.
Tujaribu kuelewa falsafa ya 'kuridhika' na 'kutosheka' ndipo maisha yetu yatatengemaa.Iwapo katika tembeatembea yako umeona gari moja ambalo limekupendezea na ukawa unao uwezo wa kulinunua,na ukalinunua hilo gari. Basi utajisikia una raha mno wakati ukiliendesha ambapo kabla yake ulikuwa unapata shida kubwa ya usafiri na huduma zinginezo. Lakini ikifika siku ukaanza kuidharau,basi utaanza kutukana badala ya kuisifu kama hapo awali na raha uliyokuwa ukiipata sasa itakuwa imegeuka kuwa udhia na kuanza kula kichwa chako.Utaanza kutamani magari mazuri mno ya watu wengine wakati uwezo hauna.Sasa jee utakwenda kuiba ambapo unajua hatima yake ni kule kushikwa gari na wewe kwenda kizimbani--maisha yako kupotea na kuteseka?
Maisha yetu kuhusu kusuhubiana huwa ni sawa na kula, kunywa na kulala.Iwapo mtu atakuwa mroho katika kula na kunywa ambapo kamwe haridhiki,basi utaona anapenda kula kila mahala na kila wakati yaani anakuwa mroho asiyekinaika.
Wataalamu na madaktari wanasema iwapo mtu atataka kuitunza siha yake vyema na kujilinda kabisa,basi inambidi asuhubiane mara moja kwa mwaka,lakini kipindi hiki ni kirefu mno ambapo nadhani hakuna mtu afanyaye hivyo.
Hata hivyo kumwaga manii mara moja kila siku ingawaje haishauriwi,lakini inawezekana kwani manii huwa inakusanyika sehemu tatu.Kumwaga mara moja kunapunguza sehemu moja ya manii iliyokomaa ambapo kunakuwa bado sehemu mbili zinazoendelea kukomaa.Na kumwaga kwa mara ya pili kunatokwa na manii iliyo bado kukomaa na kumwaga kwa manii mara ya tatu kunatokwa na manii changa kabisa na kumwaga kwa mara ya nne,ni kutoa damu tu.Hivyo kumwaga manii kwa zaidi ya mara moja kunamdhoofisha mwanamme na hatimaye kuwa khanisi .Kuna watu wengi mno ambao siku hizi hawaoni raha ya kusuhubiana na wake zao hadi hapo watazame filamu za watu uchi wakifanya hayo.Watambue wazi wazi kuwa mwelekeo wao ni mbaya. Bwana anaanza kuwatamani wake wa nje na bibi kuwatamani wanaume wa nje na vile vile kuna hatari kubwa mno ya mwanamme kupoteza nguvu zake za kiume.Sasa raha za dakika chache tu zikikufikisha katika hatari hiyo,je litakuwa ni jambo la busara? Hebu tukae na kutafakari swala hili vyema ili tusije tukajikuta tumeangamia kabisa.
Kama vile ilivyokwisha elezwa hapo awali,wazazi ambao wanapenda sana kusuhubiana, kizazi chao kitakuwa dhaifu na hivyo wazazi wanawajibika mno kuhakikisha kuwa vizazi vyao vinakuwa vyema na vyenye mustakbali mzuri.
Ni ghunah-i-kabiirah kuchezea sehemu ya uume wa mwanamme hadi kutokwa na manii kwa sababu tu siyo kuwa inadhoofisha mishipa yao bali inaleta madhara makubwa mno ambayo ni hatari zaidi kwa siha yao.Ikumbukwe vyema kuwa vijana wanamwaga na kuzitupa jawhari kutoka mwilini mwao.Na anapoingia katika tabia kama hii anakuwa ndiye muuaji wake mwenyewe bila hata ya yeye mwenyewe kutambua hivyo anajifurahisha kipuuzi kwa kupoteza uzima wa milele.
Tabia kama hiyo haina mipaka kwani kila wakati tu atakuwa akitamani kujitoa manii ambapo ni hatari kwa siha yake.Akifanya utafiti ataona kuwa anajitoa damu tu na jee kwa kujitoa damu si kutamponza tu? Sasa mwanamme mzima akiupoteza uume wake atakuwa na faida gani?Kwa kutokwa na manii kupita kiasi kutampatia tabia ya kutokwa na manii haraka mno wakati wa kusuhubiana ambapo atakuwa daima hakutimiza hamu ya kusuhubiana.Si kwamba yeye tu atakuwa hana raha vile vile mke wake atakuwa na hamu isiyotoshelezwa ,hivyo si kutamwelekeza mke wake kutafuta wanaume wengine? Je mtu atapendelea hivyo?
Fikiria wewe ni mtu mmoja uliyesoma sana na unaolewa na mwanamke ambaye anafurahi mno kusikia sifa zako.Lakini mutakapoingia kitandani kusuhubiana anakukuta hauna nguvu za kiume za kumridhisha.Je mwanamke si atajiambia kuwa "afadhali ningeolewa na jahili ambaye anaweza kunitimizia haja yangu kuliko huyu aliyesoma ambaye hawezi kuniridhisha?" Maisha yamepotea bure!
Kuna baadhi ya vijana wanatokwa na manii katika ndoto,mkojo au katika hali ya ugonjwa au mshtuko na hali kama hii inatokea miongoni mwa vijana kwa sababu ya ugonjwa ambao unatokana na:(1).kujitoa manii, (2).kujiweka pamoja na wanawake na (3).kuwa na mapenzi ya wanawake bila ya kuwapata.
Hivyo inawabidi vijana wote wajirekebishe na kuacha mbali tabia hizo mbaya ambazo zitamwangamiza na kupoteza nguvu za ujana wake.
Kile ukifanyacho sasa hivi bila ya kufikiria mbele ni hatari kwa maisha yako ya mbeleni,fikiria bado ni miaka mingapi utakayo ishi.Hebu chukua mfano wa mtu amwambie kijana wa miaka 18 kuwa amng'oe meno yake yote,sasa kijana huyo atafikiria iwapo atang'olewa meno umri huo basi ataufikiaje umri wa miaka 40 au 60 au zaidi bila ya meno?
Hivyo fikiria na uyajenge maisha yako kuanzia sasa
kabla haujachelewa!
Kwa mujibu wa Shariah za Kiislam,ulawiti na wanawake kuingiliana wenyewe kwa wenyewe ni matendo ya Ghunah-i-Kabira na hivyo kiviwekea adhabu kali mno hapa duniani na Aakhera . Iwapo kutapatikana watu wakifanya hivyo,basi wote wachinjwe. Hapo Hakim-i-Sharah (Hakimu wa Kidini) anaweza kutoa amri ya ya kuchinjwa kwa panga,kufungwa mikono na miguu na hatimaye kutupwa kutoka juu,au kuchomwa moto,kupigwa mawe hadi kufa au kuangushiwa ukuta. Vile vile anaweza kutoa adhabu zingine pamoja na kuchomwa moto.
Ulawiti baina ya mwanamke mmoja na mwanamke mwingine pia inachukuliwa na Shariah kuwa ni dhambi kubwa kabisa kama vile ilivyo ulawiti baina ya wanaume. Iwapo wanawake wenye kutenda hivyo ni wenye akili na fahamu timamu,basi wapigwe viboko mia moja kila mmoja. Adhabu hii imewekwa kwa ajili ya wanawake wote wale walioolewa na wasioolewa.
Iwapo mwanamke atapatikana na makosa kama haya kwa mara ya nne,basi atachinjwa. Na iwapo mwanamke atakapopatikana na kosa kama hili,na akakiri na kutubu,basi Imam anaweza kumsamehe au kumpangia adhabu.Vile vile Naibu wa Imam anayo mamlaka kama haya. Lakini siku hizi hakuna adhabu kama hizi.
Binadamu anafanya kila aina ya utafiti na jitihada ya kutafuta mwenzi wa kila moja kuwa watoto watakaozaliwa na farasi,ng'ombe na mbwa wawe madhubuti na wenye siha nzuri lakini jambo la kushangaza kuona kuwa sisi tumejipuuza kutafuta mwenzetu katika swala hili !
Lakini leo tunatafuta bibi na bwana kwa kuzingatia urembo na utajiri halafu hata kama mmoja wao atakuwa na tabia mbaya au magonjwa ya kuweza kurithiwa katika watoto.
Iwapo hawa watu wawili yaani mwanamme na mwanamke wanapotaka kuoana watakuwa ni watu wenye kasoro fulani za kitaalam ambazo zinajulikana basi hawashauriwi kuoana, huyu mwanamme asimuoe huyo mwanamke na huyo mwanamke asiolewe na huyo mwanamme. Hata hivyo watu wengi hawawezi kuelewa vile magonjwa ya kurithiwa yaliyomo miongoni mwao yaani mwanamme hawezi kuelewa mwanamke anayetaka kumuoa ana magonjwa gani ambayo yanaweza kurithiwa na watoto au mwanamke hawezi kuelewa mwanamme anayo magonjwa gani yanayoweza kurithiwa na watoto wao; basi watu wanaoana.
Umuhimu juu ya mali, kabila na mambo mengine na mara nyingi ndoa kama hizi ndiyo sababu kubwa za kuzaliwa kwa watoto waliodhaifu kwa sababu katika kuchagua, afya au siha iliachwa.Mwanamme aliye na siha nzuri anastahili kumuoa mwanamke aliye na siha nzuri, bila ya kujali kuwa huyo mwanamme ni tajiri au amesoma au ni mpumbavu, kwani jambo kubwa ni siha.
Ndoa ndiyo msingi wa furaha za maisha ni jambo la kipumbavu kupanga ndoa baina ya watu wawili bila ya kutazama mambo ya mbele na nyuma. Inabidi wahusika wa sehemu zote mbili watilie maanani siha zao tofauti kati ya umri na silka zao kabla ya kukubaliana baina yao kwa sababu siha na silka au tabia zinazooana baina yao ndizo zinazofanya maisha yakawa yenye furaha na kama siha na silka zao zitatofautiana basi maisha yao yamepotea na kila mara watakuwa katika mizozo. Mambo mengi sana yapo ya kuzingatia kabla ya mtu hajakubaliana na mwenzake kuoana. Litakuwa ni jambo la kipumbavu kutafuta msichana mwenye umbo zuri,kiuno kidogo mwembamba kama sindano ati huyo ndiye anaonekana mzuri.Hakika mwanamke kama huyo hawezi kuzaa watoto wenye afya nzuri.
Kwa kifupi mtu anapochagua mwenzake akiwa mwanamke au mwanamme asiangalie utajiri, urembo na ukabila ilimradi macho yake yanamdanganya, lakini inambidi amwangalie mwenzake ana siha gani. Na tabia zake zimeoana kama tabia zake, silka yake na silka ya huyo mwenzake ziko sawa ili waweze kuelewana hapo mbeleni. Na iwapo ataoa mwanamke mrembo au tajiri lakini asiye na siha nzuri,basi hatakuwa na faida naye.
Yaani watoto wanapokuwa wadogo katika mila nyingi wanapanga ndoa Uislamu haujakataza lakini kuna mambo mengi ya kuzingatia yaliyo na faida na yenye hasara katika hali hii.Ndoa hizi za kupangwa za utotoni zimesababisha vijana hawa wawili wakose kuendelea na masomo yao na maendeleo mengi hawawezi kuyafikia kwa sababu wanaoana bado wakiwa wadogo. Vile vile wanapokuwa wadogo wanaweza kuwa wanacheza pamoja, wanaweza kuwa marafiki sana kwa sababu wanakuwa na akili ya kitoto bado lakini vile wanavyoendelea kukua na baada ya kuwa wakubwa mara nyingi unaona wanatofautiana kwa mawazo na mmoja anakuwa na tabia tofauti na mwenzake na mara nyingine mmoja anaweza kumpenda mwenzake wakati mwingine anamchukia kwa sababu wakati huo wanaakili timamu kwa hivyo kuna uwezekano wa hali hiyo kutoendelea vyema. Kwa hakika ndoa kama hizi zinaishia katika hali ya vurugu na mara nyingi kupeana talaqa.
Kuna hali nyingine za ndoa ambazo zinapangwa na wazazi au ndoa zingine zinapangwa na wataalam katika fani hii ya kuoza na katika sura hii mwanamke na mwanamme yaani bibi na bwana mara nyingi sana wanakuwa hawana raha ya maisha kwa sababu mwanamme na mwanamke wanatoka mahala tofauti na inawezekana mara nyingi hawajuani wanashtukia wameshapangiwa ndoa au bibi ameshatafutiwa bwana au bwana ameshatafutiwa bibi,ilhali anaona wakubwa wake wameshamtafutia anakubali! Lakini mawazo na mapendo yao yanatofautiana, mwingine anakuwa na tabia tofauti na mwenzake kwa hiyo daima wanakuwa katika hali ya vurugu. Na katika maisha ambayo hayana raha, uelewano, mapenzi, uwiano baina ya bibi na bwana kuna sababisha watoto watakaozaliwa wasiwe watoto kamilifu kwa sababu watoto akiwa bado tumboni mama akili zake zinakuwa zimevurugika kwa sababu mama huwa hafikirii mambo mengi mazuri kila wakati utamuona mara ana hasira mara anafikiria matatizo anayoyapata sasa na vitu vinamuathiri mtoto na hata mtoto akishazaliwa hawezi kupata mapenzi ya baba na mama kwa sababu wote wawili wako katika hali ya mvurugano kwa hiyo hata watoto mawazo yao yanakuwa yameharibikiwa. Ama wao wale wanaoolewa wakiwa bado wadogo kabla ya kufikia ubaleghe hawawezi kuzaa ingawaje katika hali ya usichana msichana wa miaka kumi na moja imerekodiwa kuzaa watoto. Hata hivyo kifugo cha msichana wa umri huo haijatangamaa kikamilifu kwa hivyo tusitegemee kuwa mfuko wa mama huyo ambao haujatengamaa sawa sawa ukaweza kuzaa mtoto na kumlisha mtoto kikamilifu.Kwa sababu mfuko wake bado unakasoro sio madhubuti kwa hivyo mtoto huyo hatapata mahitajio yake sawasawa yungali tumboni.
Kwa mwanadamu kimaumbile alivyoumbwa na Allah swt anategemewa aishi kama binadamu na hivyo mwanamme au mwanamke anapokataa kuoa au kuolewa kwa hakika hapo ni kinyume na kimaumbile aliyoumbiwa na Allah swt.Wataalam wamedadisi kuwa watu wanaooa au wanaoolewa wanaishi maisha marefu zaidi kuliko wale ambao hawaoi wala kuolewa.Na wale wasiooa wana uwezekano wa kupata magonjwa mengi ya hatari kuliko wale wanaooa hivyo ni jambo la busara kuoa au kuolewa pale mtu anapoingia katika umri wake huo. Ni jambo la kudura za Allah swt kuwa mwanamme na mwanamke wanatamaniana.
Zipo Dua nyingi
mno kwa ajili ya mwanamke kushika mimba
na hapa chini nitawaleteeni
Dua chache ambazo zitakuwa zenye manufaa kwa wale bibi na bwana ambao kwa
bahati mbaya hawakujaaliiwa watoto ninatumaini na ni sala zetu pia kwa kusoma
duaa na kwa kufuata miongozo michache ifuatayo Allah swt atawajaalia hiyo
neema.
Mtume s.a.w.w.
amesema:
"Watoto ni sawa na maua ya
peponi kwa hivyo uwema wa mtu ni kutokana na vile anavyozaa watoto."
Mtu ambaye hajabahatika kupata watoto, aende katika hali ya sujuda na asome Dua ifuatayo:-
Rabbi habli min ladunka dhurriyatan tayyibatan Innaka samiud-Dua', Rabbi la-tadharni fardan wa anta Khayrul Warithiin.
Na mtu ambaye anataka mke wake ashike mimba basi inambidi baada ya sala ya Ijumaa asali rakaa mbili na katika kila rukuu na sujuda arefushe na baada ya sala asome Dua ifuatayo:-
Allahumma inni as-aluka
bima sa-alaka bihi Zakariyya:Rabbi la tadharni fardan wa anta khayrul
warithiin,habli minladunka dhurriyatan tayyibatan,Innaka akhadhtaha fa fadhayat
fi rahimiha waladan,fajalhu ghulaman mubarakan zakiyyan wala taj'al lishaytani
fihi shirkan wala nasiban.
Mtu mmoja alimwijia Imam Muhammad Baqir a.s. na kumwambia:"Ewe mjukuu wa Mtume! Mimi sina watoto," hapo Imam a.s. alimjibu kuwa : "Kila usiku au kila wakati wa mchana usome Istighfaar mara mia moja na Istighfaar ifuatayo ndiyo itakuwa vyema zaidi. 'Astaghfirullah rabbi wa-atubu ilaihi'.
Ili kutaka watoto kwa wale ambao hawajabahatika inawabidi daima asubuhi na jioni wafanye ifuatavyo: asome mara kumi
Astaghfirullah rabbi wa-atubu ilaihi na baadaye asome mara tisa Subahanallah na baadaye asome mara moja Astaghfirullah rabbi wa-atubu ilaihi.
Mwenye kuripoti mmoja anaelezea kuwa watu wengi wamefanya majaribio hayo na wameweza kuzaa watoto wengi.
Imam Jaafer Sadiq a.s. amesema kuwa mtu yeyote mwenye kutaka watoto, kila anapoamka asome Istighfaar mara mia moja na lau atasahau hapo baadaye asome kwa nia ya Qadhaa.
Mtu mmoja alisema:"Ewe Imam mimi sina watoto."Imam a.s. alimwambia:"unapopanga kusuhubiana na mke wako soma duaa ifuatayo : Allahumma inruzaktana dhakaran sammaytuhu Muhammadan.
Mtu mmoja alimwijia Imam Ridhaa a.s na kumwambia: "Ewe mwana wa Mtume ! Mimi daima huwa niko mgonjwa na sina watoto."Hapo Imam a.s alimjibu: "Uwe ukisoma adhaan nyumbani kwako kwa sauti kubwa. Yule mtu baada ya miaka kupita alimwijia Imam na kumwambia:"Mimi nilikuwa nikifanya hivyo na ninamshukuru Allah swt nimepona na nimekuwa mzima na sasa hivi nina watoto wengi."
Mtu mmoja alikuja kwa Imam Jaafer Sadiq a.s. na kuleta malalamiko yake, "Ewe mwana wa Mtume ! Mimi sipati mtoto wa kiume." Hapo Imam a.s. alimjibu: "Popote pale unapokuwa umepanga kusuhubiana na mke wako (kumuingilia mke wako) basi usome Aya ifuatayo mara tatu na baada ya kusoma mara tatu ndio usuhubiane na mke wako. Allah swt atakujaalia watoto wa kiume.Na Aya yenyewe ni hii ifuatayo:-Wadhannuni Idhdhahaba mughadhiban fadhanni an lan nakdir Ilayhi fanaada fidhdhulumaati,'an-Lailaha illa Anta Subhanaka inni kuntu minadhdhalimiin, fastajabna lahu wa najjainahu minal ghammi wa kadhalika nunjil mu'miniin,Zakariyya idhnaada Rabbahu Rabbi la tadharni fardan,wa anta Khayrul warithiin.
Katika Hadith inapatikana kuwa mtu yoyote ambaye hapati watoto inambidi afanye niyyat kama ifuatavyo:- "Iwapo mimi nitapata kijana wa kiume jina lake nitaliweka Ali" basi Allah swt atamjaalia mtoto wa kiume.
Imam Zeinul Abeidin a.s. amenakiliwa akisema mtu yeyote atakayesoma Dua ifuatayo atapata chochote kile akitakacho lau atataka mali, au watoto na wema wa dini na dunia, basi Mwenyezi Mungu atamjalia vyote hivyo na Dua yenyewe ni kama ifuatavyo:-
Rabbi la tadharni fardan,wa anta Khayrul warithiin wajalni minladunka wayarithuni fi hayati wayastaghfiruli baada mauti waj-alha khalqan sawiyyan wala taj-al lishaytani fiha nasiban.Allahumma Inni astaghfiruka wa atubu ilayka,Innaka antal ghafurur-Rahiim.
Na kwa hakika imependekezwa mno kusoma Dua hiyo mara sabini kwa ajili ya wale wanaotaka watoto.
Mtu mmoja alimwijia Imam Muhammad Baqir a.s. na alikuja akilalamika kuwa anao watoto wachache. Hapo Imam alimjibu: "Kila siku kwa muda wa siku tatu baada ya sala ya asubuhi na sala ya Isha usome subahanallah mara sabini na Astaghfirullah mara sabini. Na baadaye usome Dua inayofuata:- Astaghfiru Rabbakum Innahu kana Ghaffara,yursilussama' alaykum midraara,wa yumdidkum bi amwalin wa baniin wa yaj-alkum anhaara.
Baada ya kukamilisha utaratibu huo kwa muda wa siku tatu kwa usiku huo wa siku ya tatu ndio usuhubiane na mke wako na Allah swt atakujaalia watoto wema kwa ajili yako.
Mtu mmoja alikuja kwa Imam Jaafer Sadiq a.s. na kumwambia: "Ewe mjukuu wa Mtume! Allah swt amenijaalia wasichana wanane lakini mpaka leo sijabahatika kuona sura ya mtoto wa kiume. Imam a.s. alimwambia: "Wakati wa kusuhubiana, ukae katikati ya miguu ya mke wako, wakati huo mkono wako wa kulia uwe upande wa kulia mwa kitovu chake na usome sura ya Inna-An- zalnahu ... mara saba na baada ya kusoma ndio usuhubiane na mke wako.Mtu huyo anasema kwa kufanya hivyo Allah swt alimjaalia watoto saba wa kiume.
Imam Hasan a.s. amesema: "Yeyote yule anayependa kuzaa watoto wa kiume basi inambidi afanye Istighfaar kwa wingi kabisa."
Hapo tumeona duaa za kupata watoto vile vile kuna mambo mengine yanayochangia katika sura hii.
Wakati mzazi anapopata mimba hali yake ya kiakili na siha yake ya kimwili inaathiri sana mwili na akili ya mtoto aliyetumboni.
Inamlazimu mwanamke akae mbali na bwana wake katika kipindi cha haidh.Mfano wa gogo likitupwa mtoni halirudi nyuma bali linaendelea mbele (yaani halirudi kule maji yanakotoka bali huenda kule maji yanakokwenda), vivyo hivyo iwapo manii zitaingizwa ndani ya mwanamke haitafika katika sehemu za kushika mimba hivyo hakutakuwa na maana ya kusuhubiana. Na lau kimaajabu mwanamke akitokea akashika mimba katika hali hiyo ya kusuhubiana wakati akiwa katika kipindi chake cha damu ya siku za mwezini mtoto ataweza kufa azaliwapo. Iwapo mimba itashika siku ya pili mtoto atazaliwa akiwa na kasoro ya viungo na umri wake utakuwa mdogo sana. Na mimba itakayoshikwa baada ya kumalizika kwa damu hiyo mtoto atakuwa mzima mwenye siha nzuri na maisha mazuri.
Mwanamke anayokumbana nayo kiakili na kimwili akiwa na mimba yanamuathiri sana mtoto aliye katika tumbo.Hivyo inashauriwa sana kwa wanawake kuweka akili zao safi na wayaondoshe mawazo yao mabaya na wasijiingize katika mambo machafu, vile vile inawabidi wavae mavazi mazuri, masafi yenye kupendeza, wajipake manukato mazuri waonekane nadhifu,wajiepushe na harufu mbaya na mawazo ya kutisha.Mwanamke huyo asile vyakula vilivyoharibika au vilivyolala. Inambidi asitoke toke nje ila kikazi na aende katika mazingara ya kupendeza na kamwe asiende katika mazingara ambayo yanatisha yenye mashetani, majini n.k. na kamwe asipige makelele na mayowe na wala asijitaabishe kimwili pia, kwa muhtasari inambidi ajiepushe na kila aina ya tabia na hali ambayo itamuathiri vibaya mtoto tumboni.
Mwanamke mwenye mimba asilale juu ya vitanda virefu. Inambidi kitanda anacholalia kiwe na nafasi ya kutosha na ni lazima kuwa matandiko yawe mazuri na masafi. Na inambidi alale na mavazi mepesi, chakula chake kiwe cha kawaida na chenye afya yaani kiwe na mahitaji ya kutengeneza chakula cha mtoto tumboni.
Mwanamke mwenye mimba huwa na matamanio na yasipotimizwa yanamuathiri sana mtoto.Masikitiko,hasira, kutoridhika na mambo yote kama haya yanayoathiri akili na ubongo wa mtoto aliyetumboni.
Imeshauriwa sana kwa mwanamke kujiepusha na:-
1. Kupanda farasi au tembo.
2. Kupanda miinuko mikubwa.
3. Kufanya mazoezi magumu
4. Kwenda kwa mwendo wa haraka haraka au kuruka ruka
5. Magomvi ya kila aina
6. Kula vyakula vyenye harufu mbaya au kula vyakula vilivyo moto na kula
vitu vichachu sana na vile vile kula vyakula ambavyo ni vizito.
7. Kuchuchumaa na mambo kama hayo.
Inashauriwa ale matunda kwa wingi zaidi kiasi awezavyo.
Baada ya kushika mimbamwanamke anakuwa na hamu sana ya kula aina nyingi ya vyakula. Na lau matamanio yake hayo yatatimizwa basi atazaa mtoto mwenye siha nzuri sana, lau matamanio yake hayo hayatatimizwa basi inawezekana akazaa mtoto mwenye kasoro nyingi tu.
Wazazi tabia zao pia zinaathiri sana akili na hali ya watoto. Iwapo wazazi watakuwa wakigombana wakati wa kushika mimba ,basi kuna uwezekano wa mtoto atakayezaliwa atakuwa mgomvi.Walevi mara nyingi wanazaa watoto wenye kasoro na wasio na maendeleo.Inatokea pia kwa watoto wanaozaliwa mwanzoni wanakuwa wamepoa na wenye fikara kidogo za kinyuma nyuma wakati watoto wengine wanaoendelea kuzaliwa wanakuwa hodari na wenye siha nzuri.Sababu zote hizo tunaweza kuzipata katika mazungumzo tuliyoyazungumza huko nyuma na mengineyo mengi. Kwa hivyo inatulazimu sisi twende na wakati kwa sababu iwapo tutataka watoto wazaliwe wenye siha nzuri wenye akili nzuri wema wenye sifa nzuri basi itatubidi tujirekebishe katika kipindi hicho, tuwe tahadhari na hali ya baadaye.
Imefaradhishwa katika Islam kukata sehemu ya ngozi ya mbele ya uume wa mtoto mwanamme. Kufanya hivyo kuna faida nyingi sana ambazo zinaelezwa hata na madaktari wa siku hizi.Daima kunakuwa na maji yenye kunatanata na yenye harufu mbaya mbele ya uume wa mwanamme. Lau itaachwa hali hiyo uchafu huo uendelee kuwepo hapo basi kuna hatari ya kutokezea vipele na kuzuka magonjwa mabaya yatakayo athiri uume wa mwanamme. Hivyo iwapo hiyo ngozi ya mbele itakatwa basi hakutakuwa na utaratibu wa kubakia uchafu hapo mbele na hivyo sehemu ya uume wa mwanamme daima utakuwa msafi na utakuwa hauna hatari ya kupata madhara kama haya.
Mwanamme aliyetahiriwa yaani aliyekatwa ngozi ile ya uume ya mbele anatoa manii kwa nguvu zaidi ya yule mwanamme ambaye ngozi yake haijakatwa.Manii iliyomwagwa haibakii katika sehemu ya ngozi ya mwanamme sehemu ya mbele kwa wale waliokatwa ngozi na wale wasiokatwa ngozi uchafu huo unabaki pale pale na unaweza kuleta madhara makubwa zaidi. Wale wanaume ambao hawajakatwa ile ngozi ya mbele (kutahiriwa) hawawezi kusafisha ndani mwa sehemu hizo hivyo kuna hatari nyingi ya kufuga magonjwa hapo na vile vile kuna uwezekano mkubwa sana wa kufuga magonjwa yanayotokana sehemu za siri za mwanamke na mwanamme.
Hivyo Sharia za Uislamu zina hekima , zina busara, na zimefanywa kwa ajili ya masilahi na ubora wa binadamu kwa yeyote yule atakayeweza kufuata atapata mafanikio na wala hakuna hasara au ubaya ndani yake.
Katika Uislamu unywaji wa pombe na zinaa vyote hivi ni katika madhambi makubwa.
Unywaji pombe umezungumziwa sana katika Quran na Hadithi na riwaya mbalimbali kabla ya kutaka kuzungumzia madhara na maovu ya pombe kwa mujibu wa dini ya Kiislamu tujaribu kuangalia sayansi na matibabu yanasemaje kuhusu haya.
Daktari mashuhuri Arnel-Wared anaandika katika mpangilio wa sayansi kuwa yeye alipokuwa akifanya kazi katika Hospitali mashuhuri ya Edinberg, hospitali yake ilikuwa ikiwanywesha pombe wagonjwa wenye magonjwa ya Pneumonia hivyo ilibidi watumie mabilioni ya mapaundi kwa ajili ya kuwanunulia wagonjwa pombe. Baada ya miaka michache kupita Profesa Sir Thomas wa Edinberg University alizuia matumizi ya pombe katika kutibu ugonjwa huo hivyo gharama ya matumizi ya pombe ilipungua sana ikabakia katika paundi chache tu.
Sababu kubwa yakukatiza utumiaji wa pombe katika kutibu ugonjwa wa pneumonia ni kwamba: "Pombe hiyo ilikuwa ikiwadhoofisha Phagocytes ambao wanasaidia sana katika kuua vijidudu vya Pneumonia. Kwa hakika hao phagocytes wanapokuwa dhaifu basi kuna uwezekano mdogo sana kwa mgonjwa kupona na hivyo hatima yake ni kifo.Baada ya uvumbuzi huo hospitali nyingi za Ulaya ziliacha kutumia pombe katika matibabu ya ugonjwa huo na badala yake maziwa yalianza kutumika. Hata hivyo hawakosi madaktari wengi mno ambao bado wamekalia desturi ya kizamani ya kushauri wagonjwa wenye Pneumonia kutumia pombe. Hata hivyo katika hospitali nzuri na zenye maendeleo mazuri zinakataa utumiaji wa pombe kwa sababu pombe zinaaminiwa na inasadikiwa kuwa ni adui wa mwanadamu hadi leo hii.
Profesa Machincalf wakati wa maonyesho ya siha huko London katika mwaka 1906 alisema kuwa phagocytes ni kitu kimoja bora katika damu yetu, lakini inapopata sumu juu yake basi inaharibika. Vile vile amethibitisha kuwa pombe inaiteketeza hiyo nguvu yake kama vile opium inavyofanya.
Wakati mtu anapoumwa na mbwa kichaa au anapopigwa sindano ya kichaa cha mbwa basi huyo mtu ambaye si mlevi inamsaidia vyema kabisa kuliko yule ambaye ni mlevi na mara nyingi haiwasaidii. Utumiaji hata kiasi kidogo cha pombe kinawateketeza phagocytes. Kwa hakika kwa unywaji wa pombe sisi tunateketeza uwezo wa mwili wetu wa kututeketeza sisi wenyewe. Baada ya uvumbuzi huo madaktari waliokuwa wakiamini kuwa pombe inasaidia katika kuivisha chakula mwilini wameondoa mawazo hayo ya kuwa pombe ni yenye faida badala yake wameamini kuwa pombe inaleta madhara zaidi mwilini .
Pombe inaathiri vibaya sana hali ya uzalishaji wa kemikali katika tumbo. Kemikali hizi zinafanya kazi kubwa sana ya kutengeneza chakula chetu kuingia katika damu yetu. Hivyo kwa kunywa pombe kunaharibu nguvu za kemikali na hivyo kutukosesha sisi faida yote kutokana na vyakula vyote tunavyopata.
Miaka ya nyuma madaktari walikuwa wakiwashauri wanawake wanaonyonyesha maziwa watoto watumie pombe ili kuongeza maziwa katika matiti yao. Hata hivyo, wamebadilisha mawazo yao na maoni yao. Ni kweli kuwa pombe inaongeza kiasi cha maziwa katika matiti ya mama, lakini sio sababu nyingine isipokuwa ni sababu ya utumiaji wa maji, ambayo ndiyo inaongezea kiasi cha maziwa katika matiti ya mama. Kwa hivyo kuna vinywaji vingi sana vyenye afya na vyenye siha nzuri ambavyo vinaweza kutumika na vyenye manufaa zaidi kuliko pombe. Je kwa nini tuanze kumnywesha mtoto pombe yungali mchanga kwa kupitia katika maziwa ya mama?
Pombe inakausha maji maji mwilini. Na hii ndiyo maana tunawaona wanywaji wa pombe kuwa wanahitaji kunywa maji mengi sana na wanakuwa na kiu kingi kuliko mtu wa hali ya kawaida. Sababu nyingine ya kiu kikubwa kama hicho ni kwamba pombe inaathiri vibaya sana kemikali zinazotengenezwa na tumbo kwa ajili ya kuivisha chakula na kufanya chakula kisiweze kuiva vizuri chakula kinageuka kuwa sumu kwa mnywaji wa pombe. Na sababu hii ni mojawapo ya kusababisha sumu hii kuingia katika damu kumfanya awe na kiu hasa ya vinywaji baridi.Na vile vile tumeona kuwa mtu mwenye homa huwa ana kiu sana kwa sababu ya sumu hiyo inayoingia katika damu yake.Hata hivyo ukinywa maji hiyo sumu iliyoko ndani ya damu ya mtu mwenye homa inapungua hivyo kila sumu inavyozidi kupungua katika damu ndivyo vivyo hivyo homa inavyoendelea kupungua.
Mlevi wa pombe huwa anawashwa sana tumboni na ndio maana watu wengi utawaona wanakunywa pombe kwa kuiongezea maji na hii inakuwa na athari kidogo kuliko mtu anayekunywa pombe kavu kavu.Hata hivyo nawashauri hao watu waache kunywa pombe na wanywe maji tupu kwa sababu maji yanafaida sana kuliko pombe yao hiyo.
Sasa nitaomba tuangalie kidogo vipi Din yetu inatuambia nini kuhusu unywaji wa pombe.Sisi tumebahatika mno kuwa wafuasi wa Din ambayo imetuangalizia mambo mengi yenye faida na manufaa kwetu ambayo yote yanatuletea maendeleo katika maisha yetu.Vivyo hivyo Din yetu hii imetuambia mambo mengi yaliyo mabaya na maovu na yenye hatari kwa ajili ya maisha yetu. Wataalamu katika fani ya madawa katika miaka ya nyuma walikuwa wakiwacheka Waislamu kuwa Din yao imewanyima vitu vyenye faida kubwa kama vile pombe. Lakini baada ya utafiti kuendelea zaidi leo wanakubali kuwa Mtume Muhammad s.a.w.w. kwa hakika ametumia hekima na busara sana kwa kuwaharamishia Waislamu pombe kitu ambacho ni chenye madhara makubwa sana.
Mtume s.a.w.w. amesema kuwa : "Watu wa vikundi vitatu hawataingia kamwe peponi , nao ni:-
1. Wale wanaokunywa pombe daima
2. Wale wanaotumia uchawi
3. Wale ambao wanavunja uhusiano na majamaa zao .
Mtu yeyote anayetumia pombe atapewa kinywaji kutoka mto unaoitwa Guta. Kinywaji hiki kitakuwa kina uchafu na usaha kutoka kwa malaya na kitakuwa kikitoa harufu mbaya sana na kwa hakika kitakuwa kikiwauma sana wale wote watakaokuwa wakiishi Jahannam.
Mtume s.a.w.w. amesema kuwa:"Mtu yeyote atakayekuwa akiwauzia pombe Mayahudi, Wakristo, au makafiri basi huyo mtu atakuwa anapata madhambi sawa na yeye mwenye kuinywa pombe hiyo. Kwa hiyo mtu asiseme kuwa ninawauzia pombe makafiri hivyo mimi sina madhambi, pombe ni kitu kibaya kwa binadamu wa kila aina awe Mwislamu awe kafiri kwa hivyo atakayewauzia pombe hata makafiri atapata madhambi sawa sawa na mtu anayekunywa pombe yenyewe.Vile vile Mtume s.a.w.w. amesema kuwa:"Watu wasiende kumwangalia na kumjua hali mgonjwa ambaye ni mlevi na wala wasiungane katika mazishi ya mlevi huyo.Vile vile ameendelea kusema ushahidi wa mlevi usikubaliwe na wala msiwaoze watoto wenu kwa walevi.Ameendelea kusema Mtume s.a.w.w. kuwa: "Chochote kile kisikubalike kutoka kwa mlevi."
Imam Jaafer Sadiq a.s. amesema: "Mlevi siku ya Qiyama uso wake utakuwa umegeuka kuwa mweusi na ulimi wake utakuwa umevutwa ukining'nia mpaka mate yatakuwa yakimdondokea kifuani mwake. Mlevi huyo atakuwa akipatiwa maji au kinywaji kutoka kisima ambacho kitakuwa kimejaa usaha wa miili ya watendao maasi yaani malaya. Allah swt, Malaika, Mitume na waumini wote kwa pamoja wanawalaani walevi. Wakati mtu anapokuwa amelewa imani yake inamtoka na nafasi hiyo inachukuliwa na mashetani.
Imam Muhammad Baqir a.s. amesema: "Mtu yeyote anapolewa ibada zake za siku arobaini hazikubaliki. Na lau hatasali basi atapata adhabu mara mbili."
Imam Jaafer Sadiq a.s. amesema kuwa: "Mlevi sala zake za siku za arobaini hazikubaliwi na iwapo atakufa katika kipindi hicho basi ataingizwa katika Jahannam moja kwa moja."
Abu Salehe alimuuliza Imam Jaafer Sadiq a.s.iwapo kuna ubaya wowote katika kumnywisha mtoto mchanga azaliwapo pombe kwa sababu ilikuwa katika desturi na mila zao.Basi Imam a.s. alimjibu:"Allah swt atawanywesha maji moto sana yakitokota wale wote watakaowanywesha watoto wachanga pombe".
Imam Jaafer Sadiq a.s. amesema: "Mtu yeyote atakayemuoza binti yake kwa mlevi, basi huyo mtu amejiburuta katika Jahannam. Vile vile amesema mtu yeyote asimuoze binti wake kwa mlevi na wala asimkubali binti wa mlevi kwa harusi na wala mtu yeyote asiende kumwangalia mlevi anapougua. Mlevi siku ya Qiyama uso wake utaonekana mweusi, macho yake yakiwa majivu, uso wake ukiwa hauna sura nzuri ukiwa umeoza na ulimi ukiwa umening'inia chini. Amesema ni dhambi kabisa kunywa pombe. Mtu anapokunywa pombe anaacha sala, hamtambui mama, dada au binti yake na daima huwa amepoteza fahamu zake.
Ameendelea kusema iko nyumba ya maasi na nyumba hiyo ina mlango uliotiwa kufuli na ufunguo wa nyumba hiyo ni pombe. Kwa hiyo inamaanisha kuwa pombe ni mama wa maovu yote. Mtu yeyote anayekunywa pombe ni sawa na mtu anayeabudu miungu. Kwa sababu katika hali hiyo hakubali Quran kuwa ni kitabu kilicho kweli kwani lau akikubali kuwa ni Kitabu kilicho kweli na sahihi basi asingekunywa pombe kitu ambacho kimeharamishwa katika Quran tukufu.
Ameendelea kusema Imam a s. kuwa : "Mtu yeyote atakayempa mlevi punje ya chakula au hata tone la maji, basi Allah swt atamuwekea kaburini nge mkubwa sana mwenye meno ambayo yatakuwa marefu kiasi cha mikono mia moja na kumi na atakuwa akipatiwa maji kutoka Jahannam Kutimiza mahitajio ya mlevi ni sawa na kuwaua waumini elfu moja na kuibomoa Al-Kaaba kwa mara elfu moja. Malaika elfu sabini wanamlaani yule mtu anayemsalimia au anayemheshimu mlevi.Jibrail, Mikail, Israfil,Mitume na Maimamu wote wanawalaani wale watu wote ambao wanachukua pombe hata tone moja.
Siku ya Qiyama atatokezea nge mkubwa mno katika uwanja na atasema: "Wako wapi wale watu ambao walikuwa wakipigana na Allah swt na Mtume wake?" Jibrail atamuuliza ni akina nani alikuwa akiwatafuta. Nge huyo atasema: "Yeye alikuwa akiwatafuta watu wa aina tano."
1. Wale ambao wameacha sala
2. Wale walioacha kulipa zaka
3. Wale wanaopokea riba
4. Wale walio na tabia ya kunywa pombe
5.. Wale ambao wamezoea kuzungumzia mazungumzo ya dunia wakiwa misikitini.
Mtu mmoja alimwuliza Imam Jaafer Sadiq a.s. kuhusu kuwapo kwa pombe juu ya meza ya chakula. Imam alimjibu: "Ni haramu kula chakula juu ya meza hiyo." Vile vile Imam a.s. amesema: "Watu wasiwe wakikaa na walevi kwa sababu walevi daima huwa wanalaaniwa na wale wanaokaa nao pia wataathirika kwa laana hizo."
Imam Mohammad Baqir a.s. amesema kuwa Allah swt anawalaani watu wa aina kumi wanao shirikiana katika utengenezwaji wa pombe nao ni:-
1. Wale wanaopanda mbegu ya miti ambayo mazao yake yanatumika katika
kutengenezea pombe
2. Wale ambao wanaangalia na kuitunza miti hiyo.
3. Wale wanaotengeneza juisi yake
4. Wale wanaohudumia, wanaotawanya wanaogawa pombe
5. Wale wanakunywa hiyo pombe
6. Wale wanaopakia au kusafirisha hiyo pombe
7. Wale wanaochukua hiyo pombe
8. Wale wanaouza hiyo pombe
9. Wale wanaonunua hiyo pombe
10. Wale wanaolipia hiyo pombe.
Allah swt anazuia matendo mema yaliyofanywa na mtu katika kipindi cha miaka arobaini ya mtu ambaye anawasalimia au anawatolea heshima au anayepeana mikono na walevi. Ameendelea kusema: "Kumsaidia mlevi ni sawa sawa ni kuwasaidia wale ambao wanataka kuuvunja na kuuharibu Uislamu," na vile vile amesema : "Kumpatia mkopo mlevi ni sawa sawa na kumuua Mumiin."
Hivyo msomaji tumejaribu kuangalia kwa muhtasari tu kuhusu maovu na hatari na vile Uislamu unavyosema kuzungumzia pombe kwa kuwa kitabu hiki kidogo kinazungumzia mambo mengine kuhusu mambo ya ndoa n.k. hivyo hatuna muda wa kuzungumzia mambo juu ya pombe, hata hivyo maudhui haya yamezungumziwa na watu wengi Mashekh na madaktari kwa mapana zaidi na vile vile ukiweza kubahatika unaweza kutuandikia kwa anwani yetu juu ya kitabu kinachozungumzia mambo mawili ambayo yameunganishwa katika Quran: pombe na kamari maovu haya mawili katika jamii yetu ni maovu sana na mimi nimetunga kitabu kimoja juu ya kamari mbali peke yake na kipo kitabu kimoja kinazungumzia juu ya habari ya pombe,na anwani yangu ipo hapo nyuma katika ukurasa wa maneno machache.
Lau utapenda kupata kitabu hicho usisite kutuandikia tutajitahidi kukutumia.
Kama vile Uislamu unavyolaani pombe vile vile inalaani vikali sana zinaa, kwa uchache ninawaletea mazungumzo na Hadithi juu ya suala hili.
Allah swt ametuamrisha katika Quran kuwa siku ya Qiyama mwenye kutenda zinaa ataadhibiwa mara dufu na daima atakaa katika moto wa Jahannam.
Imeelezwa katika kitabu Tafsir-i-Safi kuwa miongoni mwa chemichemi za Jahannam moja inaitwa Asam ambamo badala ya maji inatiririka shaba iliyoyeyushwa. Maumivu ya chemichemi hizi inazidi hata adhabu za ahera na adhabu za Jahannam. Wale watakaotupwa katika chemichemi hii inayotokota ni wale ambao wanamwabudu mtu mwingine mbali na Allah swt, na wale ambao wamewaua wale watu ambao wameharamishwa kuuawa na wale watu watendao zinaa.
Imam Jaafer Sadiq a.s. amesema: "Allah swt ameweka adhabu sita kwa wale watendao zinaa ambapo adhabu za aina tatu wanazipata humu humu duniani na zinazobakia hizo tatu wanazipata huko Akhera.
Adhabu hizo zilizowekewa humu duniani ni:-
1.
Wanapoteza nuru
2.
Wanakuwa maskini
3.
Maisha yao yanakuwa mafupi.
Adhabu tatu zilizowekewa Akhera ni:-
1.
Allah swt
atakuwa amewakasirikia mno
2.
Watahesabiwa
siku ya Qiyama
kwa Sharia kali
3. Wataishi milele Jahannam.
Mtume Mtukufu s.a.w.w. amesema: "Manukato ya Jannat yataweza kusikika hadi umbali wa miaka. Hata hivyo yule mtoto ambaye amekanushwa na wazazi yaani wazazi wamesema sio mtoto wao tena, na mtu yule ambaye haonyeshi huruma kwa jamaa zake na yule mtu mzee anafanya zinaa, hao ndio watu hawataweza kusikia manukato ya Jannat."
Kuna Hadithi isemayo kuwa mwenye kufanya zinaa na mwenye kufanya Ulawiti watakuwa wakinuka kama nyama ya mizoga siku ya Qiyama hadi watakapoingizwa Jahannam. Na kwa kweli watu wataudhika na kudhurika kwa harufu zao hizo mbaya. Na wala hakuna matendo yao mema yeyote yatakayokubalika na kwamba matendo yao yote hayo yatakuwa yametupiliwa mbali.Watapigiliwa misumari katika masanduku ya maiti. Watakuwa wamepewa adhabu kubwa kweli kweli kiasi kwamba iwapo mishipa yao watafungwa watu laki nne wote watakufa kwa kuathirika na adhabu watakuwa wakipata watu kama hao.Na watu kama hao ndio watakaopata adhabu kubwa kabisa katika wakazi wa Jahannam.
Mtu yeyote iwapo ni mtumwa au mtu mwingine yeyote afanyapo zinaa na Mwislamu, Myahudi, Mkristo, au mwanamke mwingine, Allah swt atamfungulia milango laki tano katika kaburi ambamo wataingia nyoka, nge na miale ya mioto ambavyo vyote hivyo vitakuwa vikimuadhibu na kumteketeza humo hadi siku ya Qiyama wakati watu wote watakapokuwa wamekusanyika siku ya Qiyama, watu kama hawa watakuwa wakitoa harufu mbaya katika sehemu zao za siri, kiasi kwamba watu wengine wote watakuwa wakiona udhia, na harufu hii itaendelea kutoka hadi watakapoingizwa Jahannam.
Kuna wakati wanawake wanatokwa na maji meupe au ya rangi ya njano yaani maji maji hayo ni kama usaha kutoka sehemu zao za siri na maji haya yanakuwa yenye kuondoa raha mwilini nayo yanaitwa Leucorrhoea
wanawake walio na ugonjwa kama huo wanaweza kuingizwa katika makundi manne yaani:-
1. Wasichana wadogo
2. Mabinti waliokua
3. Wanawake walioolewa
4. Wanawake wenye umri mkubwa
Wasichana hawa wanaanza kutokwa na maji kama hayo kwa sababu ya uvimbe unaotokea katika sehemu zao za siri.Inaweza kuonekana iwapo msichana atalala kwa wima na ukiangalia sehemu yake ya siri utaona imevimba imekuwa rangi nyekundu na imejawa na usaha na maji maji kama haya na sababu kuu zinazofanya hali hii kutokea ni kama zifuatazo:-
(i)Kuna jarasimu
za aina nyingi sana juu ya ardhi ambapo uchafu umechanganyikana hivyo jarasimu
hizo zimeingia katika sehemu za siri za watoto kwa sababu wanapokuwa wakicheza
kwenye udongo nje na wanakuwa hawakuvaa chupi na matokeo yake ni uvimbe wa aina
hiyo.Na lau hali hii haitapewa umuhimu wa kutibiwa basi utaishia katika ugonjwa
Leucorrhoea.
(ii)Kuna vijidudu vya aina fulani ambavyo vinaishi katika majumba ambayo haina upepo wa kutosha.Na minyoo hiyo inawauma watu wanapokuwa wamelala hivyo minyoo hiyo inapouma sehemu za siri za msichana pia inaweza kusababisha ugonjwa huo.
(iii)Majeraha yanayopatikana kwa sababu ya ajali katika sehemu ya siri ya mwanamke pia inasababisha ugonjwa kama huo.
(iv) Hali ya baridi pia inachangia katika ugonjwa huu.
Katika kutibu sehemu hizi inabidi zioshwe vyema kabisa na kusafishwa na pamba au kitambaa safi kilichochovya katika maji ambamo borax imechanganywa. Borax ni aina ya dawa inayotumika katika matibabu kama haya na lau hakutaonekana dalili ya kupona ugonjwa huo basi inashauriwa kumuona daktari haraka sana iwezekanavyo.
Sehemu za siri za wasichana wasioolewa pia huwa inavimba na kutoa maji maji kama hayo wao pia hupata maumivu madogo madogo katika sehemu ya chini ya tumbo lao na huongezeka pale wanapokaribia vipindi vyao vya damu ya mwezi ( haidh ).Kwa sababu moja kubwa ya ugonjwa huo katika kikundi hiki kuwa matamanio yao yanakuwa hayakutimizwa.
Katika hali ya wasichana kama hawa hakuna matibabu yake.Hata hivyo wanatakiwa wapewe mapumziko, vyakula vizuri na vile vile wawe wakilala kwa kiasi wakiwezacho. Jambo tunaloshauri suluhisho kama hili ni kuwa msichana wa hali kama hii waozwe haraka iwezekanavyo.
Wanawake walioolewa wanapopata maumivu wakati wa kusuhubiana basi wajue kuwa ni onyo kuwa watapata ugonjwa huu. Hivyo waume zao inawabidi wawe wavumilivu na wenye subira kwa sababu kusuhubiana kupita kiasi kutaleta ugonjwa huu wa Leucorrhoea.
Wakati mwanamke anapozaa, mdomo wa kifugo chake unapanuka na moja ya sababu ya ugonjwa huo ni hiyo na lau mwanamke huyo atatibiwa vyema basi ataweza kuepukana na ugonjwa huo lakini kama hakupata matibabu sahihi basi ugonjwa huu hautaweza kutokezea.
Mwanamke kutopata haidh, kusuhubiana wakati huo na kushindiliana zaidi kunasababisha ngozi za sehemu za ndani ya sehemu za siri ya mwanamke kuvimba na hii pia ni sababu mojawapo.
Si kwamba wasichana wadogo na wanawake ndio wanaopata ugonjwa huu bali hata wanawake wa makamu wanaathirika na ugonjwa huu. Kutokujali vyema katika umri wa vijana, ugonjwa wa kisukari na mabadiliko katika umri wa mwanamke huyo inachangia katika ugonjwa huu kwa wanawake wa makamu.
Ugonjwa huu ni kwa sababu ya uvimbe unaotokana katika sehemu za siri ya mwanamke ndani mwake na sababu kubwa inatokana na damu yake kuwa chafu, kutoiva chakula vizuri tumboni, yabisi, n.k.Hivyo sababu hizi ziondolewe wakati huo huo kunapofanywa matibabu yaani dawa zake.
Inaonekana kuwa mwanamke anapata raha kidogo wakati anapochukua pamba iliyorowanishwa katika maji yenye kemikali ya borax na kuweka katika sehemu za siri za mwanamke kwa muda wa masaa ishirini na manne hadi arobaini na nane kwa hivyo iwapo hili halitamsaidia basi aonane na madaktari au awaulize wazee wanaoweza kumsaidia kwa madawa ya kienyeji ili akapona na aweze kujisikia raha starehe.
Imeonekana kuwa vijana wengi wana matatizo wa ugonjwa huo wa spermatorrhoea. Kuna malalamiko ya aina mbili katika kupungua nguvu kwa kiume katika kusuhubiana, nazo ni :-
1. manii inamwagika wakati mtu akiwa usingizini au katika mkojo
2. Mwanamme, ingawaje anakuwa na hamu ya kusuhubiana na mwanamke hawezi kuusimamisha uume wake au anapousimamisha, hatokwi na manii. Hivyo katika kufanya matibabu ya magonjwa kama haya inabidi mtu afanye dawa ambayo itamsaidia.Hata hivyo kabla ya kufanya matibabuhayo inabidi mtu mwenye magonjwa ya yabisi n.k. ayatatue kwanza.Itambidi mtu aangalie hali ya hewa ya wakati na hali ya mwili wake na mazingara kabla ya kuingilia matibabu ya matatizo yake hayo.
Kwa mujibu wa fatawa za Alhaji Sayyed Ali Huseyn Sistan, Najaf- Ashraf,Iraq.
Kwa sababu ya mkataba wa ndoa ndipo mwanamke anahalalishwa kwa mwanamme na vile vile mwanamme anahalalishwa kwa mwanamke,na mkataba huu upo wa aina mbili mkataba wa kwanza ni wa kudumu na mkataba wa pili ni muta'. Tofauti baina ya mikataba hii miwili ni kwamba katika mkataba wa daima mwanamke anapoolewa hautambulishwi muda fulani kwa hivyo inadumu umri wao mzima, na muta' humo kunatajwa muda wa kuishi kwa ndoa hiyo; yaani mtu wanaweza kuoana na mwanamke kwa mapatano ya kwa saa moja au siku moja au mwezi mmoja au mwaka mmoja au muda mwingine wowote; lakini muda huo usizidi umri wa mwanamke au umri wa mwanamme kwa sababu katika sura hii ndoa hii itakuja kuwa batil; na ndoa hii inajulikana kama ndoa ya muta'. Ndoa hii ya muta' itazungumziwa peke yake katika kitabu hiki katika sehemu ya pili hivyo kwa habari zaidi na undani zaidi vitapatikana katika sehemu ya pili ya kitabu hiki.
(2372) Ndoa iwe ya kudumu au ya muda mfupi ni lazima sigha isomwe , kwa mwanamke na kwa mwanamme kuwa radhi nakuandika kwao hakutoshi. Itambidi mwanamke na mwanamme wasome wenyewe hiyo sigha ya ndoa ama wamtafute wakili ambaye atasoma kwa niaba yao.
(2373) Wakili huyo sio lazima awe mwanamme vile vile mwanamke anaweza akawa wakili wa upande wowote huo.
(2374) Hadi hapo mwanamke na mwanamme watakapokuwa yakini kuwa mawakili wao wameisha soma sigha ya ndoa basi hapo huyo mwanamke na mwanamme watakuwa hawajahalalishwa na hivyo hawawezi hata kutazamana, na kwa kukisia kuwa mawakili wao wamesoma sigha vile vile haitoshelezi lakini mawakili wao wakisema tumesoma sigha lakini wao kama hawakuridhika au hawakuyakini basi kuamini ni swala la mashaka.
(2375) Iwapo mwanamke atamteua wakili wake amsomee sigha amsomee nikah na mtu fulani kwa muda wa siku kumi na hakumtajia mwanzo wa siku kumi hizo basi wakili siku atakayoichagua ndio itakuwa mwanzo wa siku kumi hizo, lakini iwapo wakili huyo atajua mwanamke huyo alikuwa akikusudia siku fulani au saa fulani basi itambidi asome hiyo sigha kwa mujibu wa yule mwanamke alivyotaka.
(2376)
Katika ndoa ya daima au ya muda mfupi
inawezekana mtu mmoja akawa wakili
wa upande wa mwanamke na mwanamme na vile vile mtu anaweza kuwa
wakili
wa mwanamke wakati yeye mwenyewe anamuoa huyo mwanamke lakini ni
ehtiyate mustahab
kuwa ndoa isomwe na
watu wawili.
(2377) Iwapo mwanamme na mwanamke watapenda wajisomee wenyewe sigha ya ndoa yao basi itawabidi kwanza watambulishe kiasi cha mahari yao na ndipo mwanamke aseme: "Zawwajtuka nafsi alaa sidaaqil ma'alum" yaani mimi kwa mahari ambayo imekubaliwa nimejifanya mke wako.
Hapo mwanamme atasema Qabiltu tazwija-yaani mimi nimekubali wewe kuwa mke wangu. Na katika sura hii ndoa yao ni sahihi.
Iwapo ndoa hii
sigha
ya ndoa hii itasomwa
na wakili
yaani iwapo jina la
mwanamme ni Ahmad na jina la mwanamke ni Fatima na hapo
wakili
wa mwanamke akasema:
"Zawwajtu muwakkilaka Ahmad muwakkilati Fatima 'ala sidaaqil
ma'alum"
na katika upande wa wakili
wa mwanamme atasema "Qabiltu tazwija li-muwakkili Ahmad 'alaa sidaaqil
ma'alum"
Na hapo ndoa hiyo
itakuwa sahihi.Vile vile ni
ehtiyat-i-mustahab
kuwa itambidi
mwanamme au wakili
wa mwanamme atamke maneno kwa mujibu wa maneno yaliyotamkwa na
mwanamke au wakili wake,mfano iwapo mwanamke atatamka "zawwajtu"
basi mwanamme naye itambidi aseme
"Qabiltu tazwija"
na wala
asiseme
'Qabiltu nikah.'
(2378)Iwapo mwanamme na mwanamke watapenda wajisomee sigha ya ndoa yao hivyo baada ya kuafikiana muda na mahari wanaweza kujisomea wenyewe. Hivyo mwanamke ataanza "zawwajtuka nafsi fi muddatil ma'alumat 'alaal mahril ma'alum" na hapo akimaliza mwanamme atasema "Qabiltu." Kwa hapo ndoa itakuwa sahihi na iwapo wataweka mawakili wao basi wakili wa mwanamke atamwambia wakili wa mwanamme "zawwajtu muwakkilati fil muddatil ma'alumati 'alaal mahril ma'alum." na hapo wakili wa mwanamme baada ya kusubiri kwa punde atasema: "Qabiltu tazwija limuwakkili ha-kadhaa " na ndoa yao itakuwa sahihi.
(2379). Ndoa ina masharti na machache ndiyo yameorodheshwa kama ifuatavyo:-
1. Katika misingi ya ihtiyat, sigha isomwe katika Kiarabu kilicho sahihi na lau mwanamke na mwanamme hawataweza kusoma katika Kiarabu basi wanaweza kusoma katika lugha nyingine wanayoijua wao vyema ambamo maana ya maneno zawwajtu au Qabiltu inafahamika vyema kwao. Na si lazima kuweka wakili.
2. Mwanamme au mwanamke au mwakilishi wao, ambaye anasoma nikah yao, awe na nia ya 'insha' (yaani ikifanywa kutekelezwa papo hapo). Katika maneno mengine iwapo mwanamme na mwanamke wanasoma wenyewe nia ya mwanamke anaposema zawwajtuka nafsi ikimaanisha kuwa amekuwa mke wake papo hapo; na mwanamme kwa kusema Qabiltu tazwija basi huyo mwanamme amemkubalia papo hapo huyo mwanamke kama mke wake.Na iwapo wakili wa mwanamke na mwanamme ndiye anaye soma nikah ndoa, nia zao wanaposema zawwajtu na Qabiltu ziwe kwamba mwanamke na mwanamme waliowateua wao kuwawakilisha, papo hapo wamekuwa mtu na mke wake.
3.Mtu yeyote asomaye nikah ama iwe yake mwenyewe au awe wakili wa mtu mwingine, lazima awe mtu mwenye akili na fahamu timamu, na kwa tahadhari, awe baleghe pia.
4.Iwapo nikah inasomwa na mawakili au walezi wa mwanamke na mwanamme, lazima wawatambulishe mwanamke na mwanamme kwa kuwataja majina yao au kwa kutoa ishara ya kuwatambulisha wao.Hivyo iwapo mtu ana mabinti zaidi ya mmoja na yeye akamwambia mwanamme: zawwajtuka ihda banaati (yaani nimekuoza mmoja wa mabinti wangu kuwa mke wako) na mwanamme akasema Qabiltu yaani nimekubali (hapo ndoa hiyo itakuwa batil kwa sababu hakuna msichana aliyetambulishwani msichana yupi.
5.Ni lazima mwanamme na mwanamke wawe radhi kuingia katika mkataba wa ndoa.Lakini iwapo mwanamke ataonekana akisita kutoa ruhusa ya ndoa hiyo, lakini inaonekana kuwa kimoyo amekubaliana nayo, basi ndoa hiyo iko sahihi .
(2380) Iwapo katika kusoma nikah hata herufi moja ikisomwa isivyo sahihi, kubadilika kwa maana, basi ndoa hiyo itakuwa batil.
(2381) Mtu yule ambaye anasoma nikah na anajaribu kuleta maana kwa ujumla, wakati akiwa na nia ya maana hiyo hiyo, hiyo ndoa itakuwa sahihi. Si lazima kwa mtu huyo kuelewa maana halisi ilivyo ya kila neno au kujua kanuni za lugha ya Kiarabu.
(2382) Iwapo ndoa ya mwanamke itasomwa bila ya ruhusa yake lakini baadaye mwanamme na mwanamke wakakubaliana na ndoa hiyo wakaridhiana, hiyo ndoa ni sahihi.
(2383) Iwapo mwanamme na mwanamke au mmoja wao, amelazimishwa kuingia katika mkataba huo, na wakaridhia baada ya nikah kusomwa basi ndoa hiyo itakuwa ni sahihi, ingawaje ni vyema iwapo nikah hiyo itasomwa tena.
(2384) Baba au babu wanaweza kufanya mkataba wa ndoa kwa ajili ya mvulana au msichana walio wadogo, au kwa niaba ya mvulana au msichana aliye na akili kasoro, lau watakuwa wamebaleghe na baada ya watoto kubaleghe au huyo mwenye akili kasoro akawa na akili timamu, basi wao wanauwezo wa kuiweka hiyo ndoa ikaendelea au kuikatisha iwapo kuna mambo maovu yaliyopo katikati.Lakini iwapo mmoja wa watoto hawa ambao bado hawajabaleghe watakataa hii ndoa, basi katika hali hii udharuri wa tahadhari talaqa au kusomwa tena kwa ndoa, hali itakayokuwapo lazima isomwe.
(2385) Iwapo msichana atafika wakati wa kubaleghe na bado yu bikira na yuko Rashida (yaani anaweza kuamua kwa ajili ya masilahi yake) anataka kuolewa, basi itambidi apate ruhusa ya baba wake au ya babu wake mzaa baba, ingawaje atakuwa yeye akijitazama mwenyewe katika maswala yake.Hata hivyo si lazima kwake kwa msichana huyo kupata ruhusa ya mama au kaka yake.
(2386) Katika sura zifuatazo haitakuwa lazima kwa mwanamke kupata idhini ya baba au babu mzaa baba kabla ya kuolewa:
1. Iwapo yeye si bikira
2. Iwapo yeye ni bikira lakini baba au babu mzaa baba yake wanamkatalia
idhini ya kuolewa na mwanamme ambaye ni mwema katika macho ya
Sharia na vile vile katika tamaduni na desturi zao.
3. Iwapo baba na babu mzaa baba hakubali kushiriki katika ndoa.
4. Iwapo baba au babu mzaa baba hawako katika hali ya kutoa idhini, mfano
hawana akili timamu, n.k.
5. Haiwezekani kupata idhini yao kwa sababu ya kutokuwapo kwao, au kwa
sababu zingine kama hizi, na mwanamke anataka kuolewa haraka.
(2387) Iwapo baba au babu mzaa baba watafanya mkataba wa ndoa kwa niaba ya mtoto wao wa kiume ambaye hajabaleghe bado na huyo mtoto wa kiume atakapobaleghe itabidi kumlipia gharama zote mke wake.Na hata kabla ya kubaleghe kiasi kwamba huyo anakuwa na umri wa kuweza kuona raha ya mwanamke huyo na mwanamke asiwe mdogo sana kiasi kwamba asiweze kuwa na uhusiano wa kusuhubiana na bwana wake. Na katika hali mbali na hizi, kuwe na dalili za kuthibitisha kuwa anahitaji kugharamiwa mume wake hivyo kuwepo na maafikiano ikiwa ni njia ya tahadhari.
(2388) Iwapo baba au babu mzaa baba wataingia katika mkataba wa ndoa kwa niaba ya mtoto wao asiyebaleghe itawabidi walipe mahari iwapo mtoto hana uwezo wake , au iwapo mmoja wao atakayechukua jukumu la kulipa mahari hayo. Katika hali nyingineyo, baba au babu mzaa baba wanaweza kulipa mahari kutoka milki ya mtoto, lakini kisizidi kiasi cha mahari ya kawaida inayotolewa katika sura kama hii.Lakini iwapo hali ya wakati huo itadai kulipiwa mahari zaidi, basi watalipa kutoka milki ya mtoto, na sivyo vinginevyo, hadi hapo mtoto mwenyewe atakapokubaliana nayo baada ya kubaleghe.
(2389) Iwapo mwanamme atakuja kujua baada ya kusomewa nikah (ndoa) kuwa mke wake wakati wa kusomewa mkataba wa ndoa alikuwa na kasoro mojawapo ya sita zifuatazo basi anaweza kubatilisha ndoa:-
1. Kichaa (hata kama kinakuja kwa muda fulani),
2. Ukoma
3. Magonjwa mabaya ya ngozi
4. Kipofu
5. Mlemavu, hata kama sio kiasi cha kutambaa ardhini,
6. Kuwapo kwa kipande cha nyama au mfupa katika ndani mwa sehemu za siri za mwanamke jambo ambalo linaweza au lisiweze mwanamke kuingiliwa au kushika mimba na iwapo mwanamme atatambua kuwa mke wake wakati wa kusomewa nikah, alikuwa ana ugonjwa unaoitwa Ifza' -yaani njia ya mkojo wake na vipindi vya damu vimekuwa moja au njia yakupitia damu ya haidh na njia ya kupitia choo imekuwa moja, katika sura hii mwanamme hawezi kubatilisha ndoa yake. Kwa tahadhari ya lazima itambidi kumpa talaqa iwapo itabidi kuvunja ndoa hiyo.
(2390) Mwanamke anaweza kubatilisha ndoa katika sura zifuatazo hata bila ya kupewa talaqa:
1. Iwapo atajua kuwa mume wake hana sehemu zake za siri (uume wa
mwanamme).
2. Iwapo atajua kuwa uume wa bwana wake umekatwa kabla au baada ya
kusuhubiana.
3. Iwapo bwana wake ana ugonjwa unaomfanya asiweze kusuhubiana, hata
kama ugonjwa huo umetokezea baada ya ndoa au baada ya kusuhubiana.
(2391). Iwapo mwanamke atavunja ndoa kwa sababu ya mume wake hawezi kusuhubiana naye, basi itambidi mume ampe nusu ya mahari waliyopatana. Lakini iwapo mwanamme au mwanamke atavunja ndoa kwa sababu ya kasoro moja au nyingine kama zilivyoelezwa hapo juu, na kama hawajasuhubiana, basi mwanamme hatatakiwa kumlipa chochote mwanamke.Lakini iwapo bibi na bwana walisuhubiana, basi itambidi mwanamme amlipe huyo mke wake mahari kamili.Iwapo mwanamme atavunja ndoa kwa sababu ya kasoro kama zilivyoelezwa katika mas'ala 2389, basi katika sura hii kama hawajasuhubiana mwanamme hatatakiwa kulipa chochote. Na iwapo mwanamme alisuhubiana na mke wake basi itambidi amlipe mahari kamili.
(2392) Wafuatao ambao ni mahram kwa mwanamme ni haramu kuwaoa, nao ni:- Mama mzazi, dada yake, binti yake, shanghazi na wifi wake,binti wa kaka yake, binti wa dada yake na mama mkwe.
(2393) Mwanamme anapomuoa mwanamke kuanzia hapo mama mkwe bibi mzaa mke wake, bibi mzaa baba yake na wanawake wote walio katika mstari huu ni mahram wake,( maana yake ni wale wasioruhusiwa kuolewa nayeye), hata kama huyo mwanamme atakuwa hakusuhubiana na mwanamke huyo aliyemuoa.
(2394) Mtu anapooa mwanamke, na akasuhubiana naye, basi watoto wa huyo mke wake na wajukuu wa mke huyo (wa wanaume au wasichana ) na kizazi mfululizo kinachotokana hapo kuanzia huyo mwanamme wote kwa pamoja wanakuwa mahram. Bila ya kujali kuwa hao wote walikuwapo wakati wa kusomwa ndoa au walizaliwa baada ya ndoa yao.
(2395) Iwapo mwanamme ataoa mwanamke, na hakusuhubiana, basi ni tahadhari ya lazima kuwa muda utakao dumu ndoa yao, asimuoe mtoto wa mke huyo.
(2396) Shanghazi na wifi wa mwanamme kwa upande wa baba na mama yake, na shanghazi na wifi kwa upande wa baba yake, na shanghazi na wifi wa mababu zake, na shanghazi na wifi wa mama yake na shanghazi na wifi wa bibi mzaa mama, na vile mfululizo unavyoendelea nyuma, hao wote ni mahram wake.
(2397) Baba na babu wa mume, hata mfululizo huu utakavyo kwenda ni mahram wa mwanamke wa bwana huyo.Vivyo hivyo watoto wa kiume na wajukuu wa kiume (watoto wa watoto wa kike ), vyovyote vile mfululizo huu utakavyokwenda chini, pia ni mahram wake, bila kujali iwapo hao walikuwapo wakati wa ndoa yake au walizaliwa baadaye.
(2398) Iwapo mwanamme atamuoa mwanamke, (iwapo ndoa yao ni ya kudumu au ndoa ya muta') kamwe hawezi kumuoa dada wa mke wake, wakati mwanamke huyo bado ni mke wake.
(2399) Iwapo mwanamme atampa mke wake talaqa inayoweza kurudiwa, kama vile itakavyokuwa inaelezwa katika Sharia zinazohusiana na talaqa, basi hawezi kumuoa dada wa mke wake wakati mke akiwa katika Iddah. Lakini iwapo hiyo ni talaqa inayoweza kurudiwa, basi anaweza kumuoa dada wa mke wake.Na kama ni Iddah ya muda mfupi (muta'),tahadhari ya lazima ni kuwa mtu hapaswi kumuoa dada wa mke katika kipindi hicho.
(2400) Mwanamme haruhusiwi kumuoa binti wa kaka au dada wa mke wake bila idhini ya mke wake. Na lau kama ataoa bila idhini ya mke wake, na hapo baadaye mke wake akaridhia ndoa hiyo, basi itakuwa ni sahihi.
(2401) Iwapo mwanamke atakuja kufahamu hapo mbeleni kuwa bwana wake ameoa binti wa dada yake au kaka yake huyo mwanamke na akakaa kimya, na hapo baadaye akaridhia ndoa hiyo, itakuwa ni sahihi. Na lau mwanamke huyo hataridhia hapo baadaye ,ndoa hiyo itakuwa batil.
(2402) Iwapo mwanamme kabla ya kumuoa binti wa shanghazi au wifi yake (Mungu atuepushe nayo ) akasuhubiana na mama mkwe, basi hawezi kumuoa huyo msichana kwa misingi ya tahadhari.
(2403) Iwapo mwanamme ataoa watoto wa wifi au watoto wa shanghazi wake na baada ya kusuhubiana na mke wake akasuhubiana na mama wa mke wake huyo, basi tendo hili halitakuwa sababu ya kuachana (ndoa yao itaendelea). Na Sharia kama hii itatumika iwapo huyo mwanamme atasuhubiana na mama wa mke wake baada ya kusomewa ndoa, lakini kabla hajasuhubiana na mke wake, ingawaje tahadhari iliyosisitizwa mno katika sura hii ni kwamba huyo mwanamme ajitoe mbali kwa kumpa talaqa.
(2404) Iwapo mwanamme atafanya zinaa pamoja na mwanamke mbali na shanghazi na wifi wake, ni tahadhari iliyosisitizwa mno kuwa asioe binti wa mama. Kwa hakika, na kama atamuoa, na atafanya zinaa na mama wa mke wake kabla ya kusuhubiana na mke wake, basi tahadhari iliyosisitizwa mno ni kwamba ajitenganishe naye, lakini iwapo huyo mwanamme akasuhubiana mke wake baada ya ndoa, na hapo baadaye ndipo akaja akafanya zinaa na mama wa mke wake, basi katika sura hii sio lazima kwake kutengana na mke wake.
(2405) Mwanamke wa Kiislamu hawezi kuolewa na mwanamme asiye Mwislamu, na vile vile mwanamme wa Kiislamu hawezi kumuoa mwanamke asiye Mwislamu ambao sio katika Ahlul kitab. hata hivyo hakuna ubaya kwa kuingia katika mikataba ya ndoa ya muda mfupi (muta'') pamoja na Mayahudi pamoja na wanawake wa Kiyahudi na wanawake Wakristo, lakini tahadhari ya lazima mwanamme wa Kiislamu asiwachukue hawa katika ndoa yao ya kudumu. zipo baadhi ya madhehebu kama Khawarij, Ghulat, na nasibi ambao wanajitambulisha na kudai kuwa wao ni Waislamu, lakini wametenganishwa kuwa si Waislamu. Wanaumme Waislamu na wanawake hawawezi kuoa au kuolewa ndoa ya kudumu au muta' pamoja na watu hao.
(2406) Iwapo mwanamme atafanya zinaa pamoja na mwanamke ambaye yupo katika Iddah ya talaqa inayoweza kurudiwa, kama tahadhari huyo mwanamke atakuwa ni haramu kwa ajili yake. Na iwapo huyo mwanamme atafanya zinaa pamoja na mwanamke ambaye yupo katika Iddah ya muda mfupi, au ndoa isiyoweza kurudiwa, au katika Iddah ya kifo cha mume wake, basi anaweza kumuoa huyo mwanamke hapo baadaye, ingawaje ni tahadhari iliyosisitizwa mno kuwa yeye asimuoe mwanamke huyo.
Maana za talaqa za kurudiwa na kutokurudiwa, na Iddah za muta'na Iddah za kifo, zinazungumziwa vyema katika vitabu vya fiqh katika sura za talaqa.
(2407) Iwapo mwanamme atafanya zinaa pamoja na mwanamke ambaye hajaolewa na ambaye hayuko katika Iddah yoyote ile, kama tahadhari huyo mwanamme hawezi kumuoa huyo mwanamke hadi hapo amefanya tawba ya Allah swt na ameomba msamaha kwake.Lakini iwapo atatokezea mtu mwingine wa kumuoa huyo mwanamke kabla ya mwanamke huyo hajafanya tawba ya kuomba msamaha kwa Allah swt,basi hakuna mushkeli. Iwapo mwanamke huyo akaja kujulikana kuwa ni malaya katika sura hii haitaruhusiwa kumuoa huyo mwanamke hadi hapo amefanya tawba wazi wazi na kuomba msamaha wa Allah swt. Na katika misingi hiyo hiyo haitaruhusiwa kuolewa na mwanamme ambaye anajulikana kuwa yeye anajihusisha katika mambo ya malaya hadi hapo huyo mwanamme atubu kidhahiri na aombe msamaha wa Allah swt.Na iwapo mwanamme atataka kumuoa mwanamke ambaye amejulikana kufanya zinaa pamoja naye au amezini pamoja na mwanamme mwingine basi itambidi kwa misingi ya tahadhari,asubiri hadi huyo mwanamke awe tohara kutokana na haidh.
(2408) Iwapo mwanamme atamuoa mwanamke ambaye yuko katika Iddah ya mwanamme mwingine, na lau wote kwa pamoja wanajua au mmoja wao anajua kuwa Iddah ya mwanamke huyo haijaisha, na wanatambua waziwazi kuwa kuoa mwanamke akiwa katika Iddah ni haramu, hivyo huyo mwanamke atakuwa ni haramu kwa milele kwa ajili ya mwanamme huyo hata kama huyo mwanamme baada ya kusomewa ndoa atakuwa hajasuhubiana na mwanamke huyo.
(2409)
Iwapo mwanamme atamuoa mwanamke ambaye yuko
katika
Iddah
ya mwanamme mwingine, na atasuhubiana naye, basi mwanamke huyo
atakuwa haramu kwa ajili yake milele, hata kama yeye mwanamme atakuwa hakujua
yeye mwanamke alikuwa katika
Iddah, au hakujua kuwa ni haramu kumuoa
mwanamke akiwa katika
Iddah.
(2410) Iwapo mwanamme atamuoa mwanamke huku akijua kuwa mwanamke huyo anaye bwana, basi itambidi ajitenganishe naye na asimuoe kamwe maishani mbeleni. Na Sharia kama hiyo ndiyo itatumika katika misingi ya tahadhari, kama yeye mwanamme hakujua kama yeye mwanamke ameolewa na anaye bwana, na vile vile huyo mwanamme alikuwa amesuhubiana na mwanamke huyo baada ya ndoa yake.
(2411) Iwapo mwanamke aliyeolewa akafanya zinaa, yeye katika misingi ya tahadhari, atakuwa ni haramu wa milele kwa mtu aliyefanya zinaa naye, lakini hatakuwa haramu kwa mume wake aliyeolewa na ndoa halali.Na lau huyo mwanamke hatafanya tawba, na ataendelea na tabia yake hiyo ya kufanya zinaa basi itakuwa ni afadhali kwa bwana wake ampe talaqa, ingawaje itambidi amlipe na mahari yake.
(2412) Katika sura ya mwanamke ambaye amepewa talaqa au mwanamme ambaye yuko katika ndoa ya muta' na bwana wake amekiachia kipindi kilichobakia, au iwapo kipindi cha ndoa ya muta' kimekwisha, na baada ya muda akaolewa na bwana mwingine na hapo akaijiwa na shaka iwapo wakati wa ndoa yake ya pili lau Iddah ya bwana wake wa kwanza ilikwisha au haikuisha, basi itambidi apuuzie shaka hiyo.
(2413) Iwapo mwanamme aliyebaleghe atafanya Ulawiti na kijana wa kiume, basi mama, dada na binti wa mtoto huyo atakuwa haramu kwa ajili yake. Na Sharia kama hii itatumika wakati ambapo mtu ambaye amelawitiwa ni mwanamme mtu mzima, au wakati mtu anayelawiti ni kijana ambaye hajabaleghe. Lakini iwapo mtu atakuwa na shaka iwapo kikofia cha uume wa mwanamme umeingia katika sehemu za choo au haikuingia, basi katika sura hiyo mwanamke katika kikundi cha hapo juu hawatakuwa haramu kwa ajili yake.
(2414) Iwapo mwanamme atamuoa mama au dada wa kijana mvulana, na akamulawiti huyo mvulana baada ya ndoa kwa misingi ya tahadhari hao watakuwa ni haramu kwa ajili yake.
(2415) Iwapo mwanamme ambaye yuko katika hali ya ihram (ni amri moja wapo inayotimizwa wakati wa kuhiji) akaoa mwanamke, basi ndoa hiyo ni batil, na lau alijua kuwa kuoa katika hali ya ihram ni haramu, basi mwanamme huyo hawezi kumuoa mwanamke huyo
(2416) Iwapo mwanamke ambaye yuko katika hali ya ihram ambaye hayuko katika hali ya ihram, basi ndoa yake ni batil. Na iwapo mwanamke huyo alielewa kuolewa katika ndoa ya Ihram ni haramu, katika misingi ya tahadhari ya faradhi, yeye mwanamke hawezi kamwe kuolewa na mwanamme huyo tena.
(2417) Iwapo mwanamme hafanyi tawaf-un-nisa (ni amri mojawapo ya kutimizwa katika Hajj na umra mufrada ) basi mke wake na wanawake wengine watakuwa haramu kwa ajili yake, vile vile iwapo mwanamke hatafanya tawaf-un-nisa, basi bwana wake na wanaume wengine watakuwa haramu kwa ajili yake .Lakini ,iwapo wao (mwanamme au mwanamke )watatekeleza tawaf-un-nisa hapo mbeleni, basi watakuwa halali.
(2418) Iwapo mwanamme atafunga ndoa pamoja na msichana ambaye bado hajabaleghe ni haramu kusuhubiana naye kabla hajatimiza umri wa miaka tisa. Lakini iwapo atasuhubiana naye basi huyo msichana ambaye ni mke wake hatakuwa haramu kwa ajili yake hapo atakapobaleghe, hata kama atakuwa amedhurika na Ifza (sura iliyoelezwa katika hukumu Na,2388) ingawaje katika misingi ya tahadhari itambidi, ampe talaqa.
(2419) Mwanamke ambaye amepewa talaqa mara tatu, atakuwa haramu kwa ajili ya mume wake. Lakini ataolewa na mwanamme mwingine, kwa mujibu wa Sharia na kanuni zinazoelezwa vyema katika vitabu vya fiqh katika sura ya talaqa, bwana wake wa kwanza anaweza kumuoa baada ya bwana wake wa pili kufariki, au kumpa talaqa mwanamke huyo na itambidi akamilishe kipindi cha Iddah.
(2420) Kwa mwanamke ambaye ameolewa katika ndoa ya kudumu, ni haramu kwa ajili yake kutoka nje ya nyumba yake bila ya idhini ya bwana wake, ingawaje kutoka kwake huko nje hakutavunja haki za bwana wake.Vile vile itambidi ajitolee kwa ajili ya kusuhubiana na bwana wake, na kamwe asimuzuie mume wake kusuhubiana naye bila ya kuwa na sababu ya kiadilifu. Na kiasi kwamba mwanamke huyo hataondoka katika misingi ya kutimiza wajibu wake, ni wajibu kwa mume wake kumpatia chakula, mavazi na nyumba ya kuishi. na lau bwana wake hatampatia vitu hivyo, bila ya kujali kama ana uwezo wa kumpatia vitu hivyo au hana basi atakuwa anadaiwa deni na mke wake.
(2421) Iwapo mwanamke hatimizi wajibu wake wa kindoa kwa mume wake, basi hana ulazimisho wa chakula, nguo au nyumba kutoka kwa bwana wake hata kama akiishi naye.Lakini iwapo atagoma kumtii katika nyakati mbalimbali basi hukumu ya kiakili yetu inasema kuwa huyo mwanamke hatakuwa na haki ya kudai chochote kutoka kwa bwana wake. Lakini hukumu hii ni swala la ishkal. Katika sura yoyote ile haimaanishi kuwa inapoteza haki zake za mahari.
(2422). Mwanamme hana haki ya kumlazimisha mke wake kufanya kazi za nyumbani.
(2423) Gharama za usafiri za mwanamke ni lazima zilipwe na bwana wake, iwapo zitazidi kuliko gharama za nyumbani na iwapo atakuwa amesafiri kwa ruhusa ya bwana wake. Lakini kwa gharama za kusafiri kwa gari au kwa ndege n.k. na gharama zinginezo ambazo ni dharura katika safari, zitachukuliwa na mke mwenyewe, isipokuwa wakati ambapo bwana mwenyewe atataka kumchukua mke wake pamoja naye katika safari, ambapo katika sura hii bwana ndiye atakayegharimia gharama zote.
(2424) Iwapo bwana ambaye anawajibika kumlisha na kumtunza mke wake, hatimizi wajibu huo kwa mke wake, basi mke huyo anaweza kutoa gharama zake za maisha kutoka kwa milki ya bwana wake hata bila ruhusa ya bwana wake. Na lau sura hii haitawezekana, na atalazimika mwanamke huyo kufanya kazi na kujilisha mwenyewe, na mwanamke huyo hawezi kupeleka swala lake mbele ya mujtahid (kadhi au Hakimu wa Sharia) ambaye atamlazimisha huyo mwanamme (hata kwa kumtishia kwa kifungo cha jela, kulipa gharama za mwanamke, basi kuanzia pale mwanamke huyo atakapoanza kuchuma maisha yake haitakuwa faradhi kwa mwanamke huyo kumtii bwana wake.
(2425) Iwapo mwanamme kwa mfano ana wanawake wawili na hupitisha usiku kwa mmoja wao, hivyo ni wajibu kwake yeye kupitisha usiku mmoja kati ya usiku nne kwa mke wa pili; katika hali mbali na hii,si wajibu kwa mwanamme kuwa pamoja na mke wake. Hivyo, ni lazima kwa mwanamme kutojitenga na mke wake kabisa. Na katika misingi ya tahadhari inambidi mwanamme apitishe usiku mmoja kati ya usiku nne akiwa pamoja na mke aliyemuoa kwa ndoa ya kudumu.
(2426) Hairuhusiwi kwa mwanamme kutokusuhubiana kwa zaidi ya miezi minne pamoja na mke wake kijana na ambaye ameolewa kwa ndoa ya kudumu isipokuwa wakati kusuhubiana kule kunaleta madhara kwake au inahitaji nguvu na juhudi zaidi, au wakati ambapo mwanamke mwenyewe anakubali kutokusuhubiana kwa kipindi hicho au sharti liliwekwa na bwana wakati wa kufunga ndoa.Na katika Sharia hii, hakuna tofauti ya sura ya bwana anakuwapo au anapokuwa safarini au mwanamke huyu ameolewa kwa ndoa ya kudumu au kwa ndoa ya muta'.
(2427) Iwapo katika ndoa ya kudumu mahari hayajaafikiwa, basi ndoa hii ni sahihi na katika hali hiyo bwana alisuhubiana na mke wake, basi itabidi amlipe mahari yote kamili ambayo itakuwa kwa mujibu kuwa mahari anavyolipwa mwanamke kwa kawaida kwa daraja lake. Ama kuhusiana na muta'' hata hivyo kama mahari haijaafikiwa kuanzia mwanzoni basi ndoa hiyo itakuwa batil.
(2428) Wakati wa nikah ya ndoa ya kudumu, kulikuwa hakujaafikiwa wakati wa kulipa mahari, basi mwanamke ana ruhusa ya kumzuia bwana wake asisuhubiane naye hadi hapo atakapomlipa mahari yake, bila ya kujali iwapo bwana wake anaweza kumlipa au hana uwezo wa kumlipa. Lakini iwapo huyo mwanamke atamkubalia mume wake asuhubiane naye kabla ya kupokea mahari, na mume wake akasuhubiana naye, basi kuanzia kusuhubiana kwao kwa mara ya kwanza mwanamke huyo kamwe hawezi kumzuia mume wake asisuhubiane naye bila ya kuwa na sababu za kuridhisha.
(2430)Kufanya muta' (ndoa ya muda mfupi) pamoja na mwanamke ama kwa ajili ya kutaka raha ya kusuhubiana, au kwa sababu nyingine yoyote ile, basi ni sahihi.
(2431)Ni tahadhari ya faradhi kuwa mwanamme asikose kusuhubiana naye mwanamke aliyefanya naye muta' kwa kipindi cha miezi minne yaani inambidi isipite kipindi hicho bila kusuhubiana na mwanamke aliyefanya naye muta'.
(2432)Iwapo mwanamme aliyefanya muta' na mwanamke, ataweka shuruti kuwa mume wake huyo hatasuhubiana naye basi ndoa hiyo itakuwa ni sahihi na vile vile shuruti lake hilo pia linakubalika, kwa hivyo mume atafaidika kwa starehe zinginezo tu bila ya kusuhubiana naye.Hata hivyo iwapo atakubali kusuhubiana naye hapo baadaye,mwanamke anaweza kusuhubiana na bwana wake huyo, na sharti hili linatumika katika ndoa ya kudumu.
(2433)Mwanamke aliyeolewa kwa muta'hawi mustahiki wa kupewa gharama zake hata kama atashika mimba .
(2434))Mwanamke aliyeolewa kwa muta' hastahiki kulala na bwana wake, na wala hana urithi na bwana wake na wala bwana wake pia hamrithi mke wake aliyeolewa kwa muta'.Hata hivyo iwapo mmoja wao anaweka sharti na kurithiana basi swala hilo ni ishkal, lakini hata hivyo lazima ichukuliwe tahadhari katika kuweka maanani na utekelezaji wake.
(2435)Iwapo mwanamke ambaye ameolewa kwa muta' alikuwa hajui kuwa yeye si mustahiki wa gharama wala kulala na bwana wake lakini ndoa yake itakuwa sahihi bado, na kutokujua huko yaani kubakia katika hali ya ujahili vile vile atakuwa na haki ya kudai chochote kwa bwana wake.
(2436) Iwapo mwanamke aliyeolewa kwa muta' atatoka nje ya nyumba bila ya ruhusa ya bwana wake na kwa vyovyote vile haki ya bwana wake itakuwa imevunjwa basi kutoka kwake nje ni haramu. Na iwapo haki ya bwana wake itakuwa imesalimika ichukuliwe tahadhari iliyosisitizwa kuwa mwanamke huyo asitoke nje ya nyumba bila ya ruhusa ya bwana wake.
(2437) Iwapo mwanamke atampa ruhusa mwanamme ya kuwa wakili wake katika kusoma nikah ya muta' pamoja na mwanamke huyo kwa kipindi fulani na kwa kiasi fulani cha mahari, na badala yake huyo mwanamme yaani wakili akasoma nikah ya kudumu pamoja na mwanamke huyo au anasoma nikah ya muta' pamoja na mwanamke huyo bila ya kubainisha wazi wazi kipindi cha muda au kiasi cha mahari, basi ndoa hiyo itakuwa batil. Lakini iwapo mwanamke ataridhia na kutoa ruhusa kwa mapatano hapo mbeleni basi ndoa hiyo itakuwa sahihi.
(2438)Ili kutaka kuwa
mahram
(yaani
ambaye huwezi kumuoa na anakuwa ni jamaa wako wa karibu ), baba
au babu
mzaa baba wanaweza kumuingiza mtoto wao asiyebaleghe au msichana wao
asiyebaleghe
katika ndoa pamoja na mtu
mwingine kwa kipindi kifupi,ili mradi haitatokezea ufisadi.Hata hivyo, iwapo
wao watamuoza mvulana mdogo au msichana mdogo ambaye kwa vyovyote vile hawezi
kupata starehe ya kusuhubiana katika kipindi hicho, basi katika sura hii
usahihi wa ndoa kama hiyo ni
ishkal.
(2439) Iwapo baba au babu mzaa baba wa mtoto asiyekuwapo, wakamuoza kwa mtu ili kutaka kuwa mahram, bila kujua iwapo mtoto yuko hai au amekufa, basi kusudi litapatikana iwapo katika kipindi katika ndoa, mtoto atakuwa na uwezo wa kusuhubiana. Iwapo hapo baadaye itakuja kujulikana kuwa mtoto huyo hakuwa hai wakati wa kusomwa ndoa hiyo basi itachukuliwa kuwa ni batil.Na wale wote ambao walikuwa ni mahram sasa watakuwa si mahram.
(2440)Iwapo bwana atakuwa amempatia zawadi bibi wake aliyemuoa kwa muta' katika kipindi hicho, na atakapokuwa amemuachia na kama alikuwa amesuhubiana naye basi itabidi ampatie vitu vyote vile alivyokuwa ameahidi kumpa. Na lau kama alikuwa hajasuhubiana naye basi itambidi ampe nusu ya mahari yake, ingawaje achukue tahadhari iliyosisitizwa mno kuwa itambidi ampe mahari kamili.
(2441)Iwapo mwanamme ataingia katika muta' pamoja na mwanamke na mwanamke atakapokuwa katika kipindi cha Iddah kabla ya kuisha basi inaruhusiwa mwanamme kumuoa mwanamke huyo kwa ndoa ya kudumu au ndoa ya muta'.
(2442) Ni haramu kwa mwanamme kutazama mwili au nywele kwa mwanamke ambaye siyo mahram bila kujali iwapo ana nia ya kuona raha au sivyo, na kama kuna hatari ya kuangukia katika tendo bovu la kutenda madhambi au siyo. Vile vile ni haramu kutazama juu uso na mikono mpaka kufika katika vipingili vya mkono wa juu, ya wanawake kwa nia ya kuona raha au kuna hatari ya kuangukia katika madhambi, na katika hatua ya tahadhari iliyosisitizwa ni kuwa mtu asitazame sura zao au mikono yao hata kama ni bila sababu kama hizo. Vivyo hivyo ni haramu kwa mwanamke kutazama mwili wa mwanamme asiye mahram kwake, isipokuwa sehemu zile ambazo kwa kawaida huwa hazifunikwi, kama uso,mikono, kichwa, shingo,na miguu. Mwanamke huyo anaweza kuona sehemu hizi za mwanamme bila ya kuwa au kutaka raha au iwapo kutakuwa au kama hakutakuwa na hatari ya kutumbukia katika matendo ya madhambi.
(2443)Kuangalia mwili wa mwanamke ambaye hajali kuhusu hijab hata kama atakuwa ameshauriwa si haramu, ili mradi haitamtumbukiza mtu katika matendo ya madhambi au raha ya kusuhubiana au kushangazwa, wala si kwa nia; na katika Sharia hii, hakuna utofautisho baina ya mwanamke wa Kiislamu au mwanamke asiye Mwislamu; na vile vile sehemu zile kama uso mikono ambayo kwa kawaida huwa haifunikwi,na sehemu zinginezo za miili yao.
(2444) Inambidi mwanamke afunike mwili wake na nywele zake kutokana na mwanamme ambaye sio mahram kwake na tahadhari iliyo faradhi,kuwa ajifunike mzima dhidi ya wavulana ambao hawajabaleghe na ambao wanaweza kutambua baina ya mema na mabaya na labda wanaweza kuvutiwa katika mambo ya kusuhubiana.Lakini anaweza kuacha uso wake na mikono mpaka juu kidogo viganja visifunikwe mbele ya mtu ambaye sie mahram kwake, ili mradi huku kusimpelekee mtu katika mtego wa madhambi, kwa macho mabaya au yeye kufanya jambo lolote ni haramu; kwa hali zozote hizi itambidi yeye afunike sehemu hizo zote.Ni haramu kutazama sehemu zake za siri za Mwislamu aliyebaleghe,hata kama itatazamwa nyuma ya kioo au kutokana na kioo kwa mbele, au maji safi yaliyotulia n.k.Kama tahadhari ya lazima, ni haramu vile vile kutazama sehemu za siri za mtu ambaye si Mwislamu,na kijana ambaye hajabaleghe na ambaye anaelewa mema na mabaya.Hata hivyo bibi na bwana wanaweza kutazama mwili wa mwenzake.
(2446)Iwapo mwanamme na mwanamke ambao ni mahram kwa kila mmoja, hawana nia ya raha ya kusuhubiana, wanaweza kuona mwili mzima wa mtu na mwenzake isipokuwa sehemu zake za siri.
(2447) Mwanamme hatakiwi kuangalia mwili wa mwanamme mwenzake kwa kupandwa na matamanio ya Ulawiti, na vile vile ni haramu kwa mwanamke kutizama mwili wa mwanamke mwenzake kwa nia ya kutaka kuingiliana naye.
(2448)Iwapo mwanamme anamfahamu mwanamke
ambaye siye
mahram
kwake, basi itambidi kama
tahadhari
asitazame hata taswira yake n.k.,ili mradi mwanamke huyo hayupo miongoni mwa
wanawake mwa wale wasiovaa
hijab.
(2449)Iwapo mwanamke anataka kumpiga enema mwanamke mwingine au mwanamme mbali na bwana wake, au kusafisha sehemu za siri za mwanamke au za mwanamme kwa maji, basi itambidi avishe kitu mikono yake ili mikono yake isiguse sehemu hizo za siri za mwanamke au mwanamme. Na vivyo hivyo inatumika kwa mwanamme ambaye anataka kumpiga enema mwanamme au mwanamke mwingine mbali na mke wake, au kusafisha sehemu za siri za mwanamke au mwanamme kwa maji.
(2450) Iwapo mwanamke atakuwa ameugua na anaweza kutibiwa na mganga wa kiume vyema zaidi, basi anaweza kutibiwa naye.Na iwapo daktari huyo mwanamme itabidi amtazame ili kumtibu, au kumgusa mwanamke huyo kwa sababu hizo basi hakuna ishkal yoyote.Hata hivyo,iwapo ataweza kumtibu kwa kumwangalia itambidi asimguse, na kama ataweza kutibu kwa kumgusa mwili wake, basi asimtazame mwanamke huyo.
(2451) Iwapo mtu itambidi atazame sehemu za siri za mgonjwa wake akiwa mwanamke au mwanamme kwa ajili ya matibabu, basi itambidi katika misingi ya tahadhari iliyo faradhi, aweke kioo mbele yake mbele ya mwanamke au mwanamme. Hata hivyo, na kama hakuna njia nyingine bila kuangalia moja kwa moja katika sehemu za siri za mwanamke huyo au mwanamme, basi hakuna mshikeli.Vivyo hivyo iwapo kutachukuliwa muda zaidi kuangalia sehemu hizo za siri kupitia kioo kuliko kumwangalia moja kwa moja, basi anaweza kumtazama moja kwa moja.
(2452) Iwapo mtu atakuwa ametumbukia katika matendo (zinaa) ambayo yameharamishwa kwa sababu ya kutokuwa na mke, basi ni faradhi kwake yeye kuoa.
(2453) Iwapo bwana ataweka sharti kabla ya ndoa kuwa mwanamke lazima awe bikira, na baada ya ndoa ikaonekana kuwa si bikira, basi anaweza kuvunja ndoa hiyo.Hata hivyo,anaweza kukata kiasi cha mahari yanayolipwa kwa kawaida kwa ajili ya mwanamke aliyebikira au asiyebikira.
(2454) Ni haramu kwa mwanamke na mwanamme ambao si mahram kuwa pamoja katika sehemu zile ambazo hakuna mtu mwingine, iwapo kuna hofu ya kutumbukia katika ufisadi, au hata kama ni mahari ambapo anaweza kutokezea mtu kwa ghafla. Lau kutakuwa hakuna hatari yoyote ya ubaya basi hakuna mushkeli wowote.
(2455)Iwapo mwanamme ndiye atakayepanga mahari ya mwanamke wakati wa ndoa, lakini hana nia ya kumlipa, basi ndoa hiyo itakuwa ni sahihi lakini atakuwa ana deni na mke wake.
(2456) Mwislamu ambaye anaukana Uislamu na kuingia katika dini ya wale wasio Waislamu, ni kafiri na hao ni wa aina mbili;fitri na milli . Kafiri fitri ni yule ambaye wazazi wake au mmoja wao alikuwa Mwislamu alipokuwa amezaliwa, na yeye mwenyewe alikuwa Mwislamu hadi hapo alipofika umri wa kutambua baina ya mema na mabaya na hapo baadaye akaja akawa kafiri. Na kafiri milli ni mtu aliyetofauti kabisa.
(2457) Iwapo mwanamke atakuwa kafiri baada ya ndoa, ndoa yake itakuwa batil,na iwapo mume wake atakuwa hajasuhubiana naye, basi hatakiwi kubakia katika Iddah. Na hali hii itakuwa vivyo hivyo iwapo yeye atabadilika baada ya kusuhubiana na mume wake, au yeye amefikia ugumba ( Ya'isa), au alikuwa bado mdogo. Na lau kama atakuwa hajafikia ugumba, basi itambidi atimize Iddah kama vile inavyoelezwa katika hukumu za talaqa. Na ni jambo la kawaida iwapo yeye atakuwa Mwislamu tena akiwa katika kipindi cha Iddah, ndoa yake itasalimika.Hata hivyo,inaweza kuchukuliwa kuwa sahihi, na hivyo tahadhari isiachwe. Mwanamke anayeitwa Ya'isa ni yule ambaye amefikia umri wa miaka hamsini (50) na kwa sababu ya umri huo mkubwa anaacha kupata haidh na wala hategemei kuyapata maishani mwake.
(2458) Iwapo mwanamme atakuwa kafiri fitri baada ya ndoa, mke wake atakuwa haramu kwa ajili yake; na huyo mwanamke hatakiwi kuingia katika Iddah baada ya kifo cha mume wake maswala ambayo yanaelezwa vyema katika Sharia za talaqa.
(2459)Iwapo mwanamme atakuwa kafiri milli baada ya ndoa, ndoa yake itakuwa batil. Na kama alikuwa hakusuhubiana na mke wake, au mwanamke huyo amekuwa Ya'isa, au kama bado ni mdogo basi hatatekeleza Iddah. Lau kama huyo mwanamme ataingia katika ukafiri baada ya kusuhubiana na mke wake, mke wake akiwa katika hali ya mwanamke yule ambaye anapata haidh kama kawaida, basi itambidi aingie katika Iddah ya talaqa, maswala ambayo yanaelezwa vyema katika maswala ya talaqa. Inachukuliwa kawaida iwapo bwana wake atakuwa tena Mwislamu kabla ya huyo mwanamke kumaliza Iddah basi ndoa yao itasalimika. Hata hivyo haitegemei kuwa hii itakuwa sahihi, lakini tahadhari isiachwe.
(2460) Iwapo mwanamke wakati wa ndoa ataweka sharti kuwa bwana wake asimchukue nje ya mji (utakaotajwa), na mwanamme akakubalia hilo sharti, basi asimchukue mke wake nje ya mji huo bila ya idhini yake.
(2461).Iwapo mwanamke ana mtoto wa bwana aliyemtangulia huyu bwana, basi huyo bwana anaweza kumuoza huyu binti kwa mtoto wake wa kiume, ambaye si mtoto wa mke huyo. Vivyo hivyo iwapo mke atamuoza mtoto wake kwa msichana, basi yeye akiwa kama baba anaweza kumuoa mama wa binti huyo.
(2462) Iwapo mwanamke atashika mimba kwa sababu ya zinaa, basi haruhusiwi kuangusha mimba hiyo.
(2463) Iwapo mwanamme atafanya zinaa na mwanamke asiye na bwana, wala yeye hayuko katika Iddah, na baadaye akamuoa na mtoto akazaliwa wakiwa bado pamoja na hawajui iwapo huyu mtoto ameingia katika mimba ya mama akiwa wamesuhubiana kihalali au kiharamu basi mtoto huyo atachukuliwa kama mwana halali.
(2464) Iwapo mwanamme hajui kuwa mwanamke huyo yu katika Iddah na akamuoa na mwanamke huyo vile vile hajui kuwa yeye yuko katika Iddah na mtoto akazaliwa kwao, basi huyo mtoto atakuwa ni mwana halali kwa mujibu wa Sharia ni mtoto wao wote. Hata hivyo iwapo mwanamke anajua kuwa yeye alikuwa katika Iddah, na katika kipindi hicho cha Iddah ndoa hairuhusiwi mtoto atakayezaliwa atakuwa ni mtoto wa baba,na kwa hali yoyote ile ndoa yao itakuwa batil na wao watakuwa ni haramu kwa kila mmoja.
(2465)Iwapo mwanamke atasema yeye kuwa amekuwa gumba (Ya'isa), maneno yake yasikubalike lakini akisema kuwa yeye hana bwana basi maneno yake yakubalike, isipokuwa pale anapojulikana kuwa haaminiki, katika hali hiyo uchunguzi utahitajika.
(2466)Iwapo mwanamme atamuoa mwanamke baada ya mwanamke kusema kuwa hana bwana, na ikatokezea mtu mwingine akaja akadai kuwa huyu ni mke wake basi madai yake hayatakubaliwa hadi hapo ithibitishwe kwa mujibu wa Sharia.
(2467) Hadi hapo msichana au mvulana anamaliza umri wa miaka miwili, baba yake hawezi kumtenganisha na mama yake.Na kama tahadhari, mtoto asitenganishwe na mama yake hadi umri wa miaka saba.
(2468) Iwapo mtu anayetaka kuoa anajulikana kwa wema na imani yake, basi inasisitizwa kuwa ombi lake hilo lisikataliwe.Mtume Mtukufu s.a.w.w. ameripotiwa kusema: "Popote utakaposikia, popote utakapopokea maombi ya kumuoza mtoto wako kwa mwanamme ambaye sifa zake na ucha Mungu wake unakufurahisha wewe, basi muoze mtoto wako. Na lau hautafanya hivyo, basi ufisadi na maovu yatajaza dunia."
(2469)Iwapo mwanamke ataafikiana na mume wake kuhusu mahari yake, kwa masharti kwamba mwanamme huyo hataoa mwanamke mwingine, basi ni faradhi kwa mwanamme kutokuoa mwanamke mwingine,na kwamba mwanamke huyo asidai mahari yake tena.
(2470)Iwapo mwanaharamu ataoa, na mtoto atazaliwa basi mtoto huyo atakuwa ni mwana halali.
(2471)Iwapo mwanamme atasuhubiana na mke wake katika funga za mwezi wa Ramadhani au wakati mwanamke huyo atakuwa katika vipindi vyake vya mwezi (haidh), mwanamme atakuwa ametenda dhambi lakini iwapo mke atashika mimba katika hali hiyo basi mimba hiyo ni halali.
(2472)Iwapo mwanamke atakuwa na uhakika
kuwa bwana wake amekufa akiwa safarini,na akaolewa na mwanamme mwingine baada
ya kukamilisha
Iddah
ya kifo,(mambo
yanayoelezwa vyema katika maswala ya talaqa) na baadaye mume wake wa kwanza akatokezea kutoka safari, basi
itambidi mwanamke huyo papo hapo ajitenganishe na bwana wake wa pili,na huyo
mwanamke atakuwa ni halali kwa bwana wake wa kwanza. Lakini iwapo bwana wake wa
pili atakuwa amesuhubiana naye, basi itambidi atekeleze
Iddah
na bwana wake wa pili itambidi ampe
mahari yake kamili kwa
mujibu wa mwanamke wa kikundi hicho, lakini hastahiki kulipiwa gharama na bwana
wake wa pili katika kipindi hicho cha
Iddah.
1.Mtume s.a.w.w. amesema:
"Msisuhubiane na wake zenu kama
kuku.Fanyeni
mapenzi ya kutosha,mubusu na hatimaye
munapojawa na raha ndipo musuhubiane”.
2.Watu wengi wanachukulia mambo ya kishetani katika kusuhubiana huku wakipuuza njia aliyoihalalisha Allah swt. Wao wanaingilia njia ya nyuma i.e. panapopitia choo kwa kisingizio cha kupata raha zaidi kumbe kunakujitumbukiza katika hatari ya kuweza kuambukizwa magonjwa hatari kabisa kwa sababu hiyo ni nafasi ya kupitia uchafu mtupu uliojaa magonjwa ya kila aina. Kwa msomaji ni ushauri wangu kuwa aonane na mganga ili aweze kupata ukweli na uhakika wa swala hili ili aweze kuelewa vyema falsafa ya Islam katika swala hili.
3.Manukato ya maua na mafuta mazuri yanaweza kuwafanya kustarehe zaidi katika kusuhubiana.
4.Kwa kubaki mbali na mke kwa kipindi kirefu bila ya kusuhubiana naye au kwa udhuru mwingine wa kisheria haifai kumtukana au kumuudhi kwani kunaweza kwa urahisi kumfanya mke aende nje kwa waume wengine na hapa bwana ndiye atakaye wajibika.
5.Wataalamu wanasema kuwa bibi na bwana wanaposuhubiana,inawabidi wasiingiliane tena illa baada ya siku tatu au hata zaidi.Ingawaje hakuna ushahidi wa kuleta madhara.
6.Haifai kusuhubiana wakati tumbo likiwa limejaa (ameshiba) au likiwa tupu (njaa) bali baada ya kula iwapo utakuwa umepita muda wakutosha,basi hakuna madhara.
7.Baada ya kusuhubiana kwa bibi na bwana,wasioshe sehemu zao za siri kwa maji baridi wala wasioge kwa maji baridi kwani kwa kufanya hivyo kutaweza kuwaingiza katika magonjwa mengi mno na kuna uwezekano mkubwa wa mishipa kulegea.Lakini kusafisha kwa kitambaa chenye maji si vibaya.Bibi na bwana hawatakiwi kusafisha sehemu zao za siri kwa kutumia kitambaa kimoja tu kwani kunapunguza mapenzi baina yao.
8.Baada ya kusuhubiana wote wawili wanashauriwa kujisaidia haja ndogo (kukojoa mkojo) na kwa kufanya hivyo mishipa haitalegea.
9.Kusuhubiana kwa kijana mwenye umri mdogo na mwanamke mwenye umri mkubwa ni hatari sana kwa siha ya mwanamme kwani ni sawa na sumu kali sana.
10.Umri wa mwanamke: kuanzia miaka kumi na miwili hadi ishirini ni kama bibi harusi,na katika umri huu anaweza kutoa uridhisho mzuri kabisa katika kusuhubiana.Vile vile kuanzia umri wa miaka ishirini hadi thelathini anaweza kutoa uridhiano mzuri na bwana pia anaweza kuridhika. Na mwanamke kuanzia thelathini hadi arobaini si mbaya. Kuanzia arobaini hadi hamsini huwa hisia zimekuwa sugu,hata hivyo hana madhara.
11.Mtume s.a.w.w. alimwambia Imam Ali a.s. "Ewe Ali! Unapomleta mke wako nyumbani mwako,ondoa viatu vyake ili aweze kuketi vyema na uoshe vikanyagio vya miguu yake na kumwagilia maji hayo mlangoni na kona zote na kuta za nje ya ya nyumba;kwa kwa kufanya hivyo kutaondoa mawazo na shida sabini elfu na kutakuletea baraka na rehema sabini elfu za Allah swt.Na vile vile kila kona ya nyumba itakuwa imebarikiwa na bibi harusi atakuwa amehifadhika na ugonjwa wa kichaa,kubabuka ngozi kichwani na ukoma.Usimpatie kwa siku saba za kwanza maziwa,siki,giligilani na tufahachachu.Alipouliza Imam Ali a.s. sababu yake,alijibiwa:"kwa kula vitu hivyo,mwanamke anapoteza nguvu za kushika mimba na hawezi kuzaa mtoto.Kipande cha mkeka kilichotupwa nyumbani ni bora kuliko mwanamke asiyezaa."
1.Ni haramu kusuhubiana na mwanamke anapokuwa katika haidh (mwanamke anapotokwa na damu ya kila mwezi) au nifas (damu inayotoka baada ya kuzaa),na vile vile si vyema kumgusa kuanzia sehemu zake za siri hadi magoti yake.
2.Hairuhusiwi kusuhubiana na mwanamke baada ya kufunga damu ya haidh na nifas na kabla ya mwanamke hajaoga (hajafanya ghusl) Maulamaa wengi wanasema kuwa ni haramu kusuhubiana na kwa hakika ndivyo inavyotakiwa lakini iwapo mtu atataka kusuhubiana,basi itawabidi wasafishe vyema sehemu hizo ndipo waweze kusuhubiana.
3.Iwapo mtu atapenda kusuhubiana na mwanamke aliye katika Istehadha (zisizozidi siku zaidi ya haidh) basi itambidi huyo mwanamke aoge istehadha na kukamilisha masharti yote ya istehadha ndipo hapo atakapoweza kusuhubiana naye.
4.Kila wakati mwanamme anaposuhubina na mke wake haruhusiwi kumwaga nje manii (shahawa au mbegu za kiume) nje ya uuke wa mke bila ya ruhusa ya mke wake na baadhi ya Maulamaa wanasema kuwa ni haramu kufanya hivyo.Lakini hata hivyo anaposuhubiana na kijakazi wake anayo ikhtiyari ya kufanya hivyo.Lakini wataalamu wanapinga kumwaga nje manii.
5.Haitakiwi kusuhubiana usiku wa kuamkia jumatano kwani iwapo atachukua mimba,basi kuna uwezekano wa kuanguka kwa mimba kabla ya kufikia muda wake na iwapo itakamilika basi kunaweza kuzaliwa kwa mtoto mwendawazimu au mwenye ugonjwa wa yabisi.
6.Haitakiwi kusuhubiana siku za mwanzoni,katikati na mwishoni mwa kila mwezi kwani vile vile kuna hatari ya kuanguka kwa mimba changa na iwapo atazaliwa mtoto basi kunauwezekano wa kuwa mwendawazimu au mwenye yabisi.
7.Wakati wa kusuhubiana haitakiwi kuzungumza kwani kunauwezekano wa kuzaliwa kwa mtoto kiziwi.
8.Wakati wa kusuhubiana hairuhusiwi kuangalia sehemu za siri kwani kunahatari ya kuzaliwa kwa mtoto kipofu,lakini katika riwaya nyingine inaelezea kuwa hakuna ubaya wowote ule.Mbali na wakati wa kusuhubiana,hapana makatazo ya aina yoyote ile katika kutazamana.
9.Iwapo kutakuwa kumepakwa khizaab,basi haitakiwi kusuhubiana.
10.Vile vile hairuhusiwi kusuhubiana wanapokuwa katika maji.
11.Hairuhusiwi kusuhubiana mbele ya watoto kwani kuna hatari ya kuzaliwa mtoto mzinifu.
12.Iwapo kutakuwa na aliye macho au asikiaye sauti za wakati wa kusuhubiana,basi haitakiwi kusuhubiana wakati huo.
13.Iwapo mtu atasuhubiana na kijakazi wake mmoja na kuwa na hamu ya kusuhubiana na kijakazi wa pili basi itambidi afanye wudhuu (kutawadha) kwanza.
14.Hairuhusiwi kuwalaza wanawake wawili (iwapo mtu atakuwa na wake wawili) kwa pamoja kitanda kimoja lakini anaruhusiwa kwa ajili ya vijakazi wawili.
15.Hairuhusiwi kusuhubiana huku uso au mgongo ukielekea Qibla.
16.Vile vile hairuhusiwi kusuhubiana wakati wanapokuwa wakisafiri katika meli au jahazi.
17.Iwapo mtu alitokwa na manii bila ya kusuhubiana, (akiwa usingizini au kwa sababu zinginezo) basi itambidi kwanza afanye ghusl-i-janaba, ndipo aweze kusuhubiana kwani bila ya kufaya hivyo kuna uwezekano wa kuzaliwa mtoto mwendawazimu.
18.Ni haramu kusuhubiana wakati wa kupatwa kwa jua na mwezi au kunapotokea mtetemeko au jua lionekanapo kuwa rangi njano.
19.Kusuhubiana wakati wa adhuhuri kunaweza kuzaliwa mtoto mwenye macho makengeza.
20.Imam Ali a.s. amesema:"Iwapo utamwona mwanamke wa nje na iwapo utaghalibiwa na Sheitani hata ukatamani kusuhubiana na mke wako,basi usithubutu kufanya hivyo kwani ujiambie kuwa kile alichonacho huyo hata mke wako pia anacho.Na iwapo atakuwa hana mke,basi inambidi asali rakaa mbili na kumwomba Allah swt amjaalie mke,naye atapata kuoa."
21.Iwapo watasuhubiana wakiwa wamesimama,basi kunauwezekano wa mtoto kuzaliwa akiwa na tabia ya kujikojolea kitandani hata akiwa na umri mkubwa.
22.Iwapo kutasuhubiwa katika usiku wa Idd ul-Fitr, mtoto atakayezaliwa atakuwa na maovu mengi mno.
23.Vile vile inabidi kujiepusha na kusuhubiana usiku wa Idd ul-Adh-ha kwa sababu kunauwezekano wa kuzaliwa mtoto mwenye vidole vinne au sita.
24. Kwa sababu ya kusuhubiana chini ya miti ya matunda, mtoto atakayezaliwa ataweza kuwa kiongozi wa dhalimu.
25. Haitakiwi kusuhubiana wakati miale ya jua ikiwaelekea kwani mtoto atakayezaliwa atakuwa mwenye wasiwasi hadi kufa kwake.
26. Hairuhusiwi kusuhubiana baina ya Adhaan na Iqamah mtoto atakayezaliwa atakuwa daima mwenye kutaka kumwaga damu yaani muaji.
27. Kutaka kusuhubiana na mwanamke mwenye mimba, inabidi mwanamme awe katika hali ya wudhuu kwani bila hivyo mtoto atakayezaliwa atakuwa mwenye roho ngumu na mchoyo.
28. Haitakiwi kusuhubiana usiku wa tarehe kumi na tano ya Shaaban, kwani mtoto atakayezaliwa hatakuwa
mwenye bahati na atakuwa na madoti meusi usoni mwake.
29. Hairuhusiwi kusuhubiana katika siku za mwisho za mwezi wa Shaaban kwani mtoto atakayezaliwa atakuwa jambazi na mwenye ukatili na kuna hofu ya kuwaua watu wengi mno.
30. Hairuhusiwi kusuhubiana juu ya paa za nyumba kwani mtoto atakayezaliwa atakuwa mlaghai na asiye na imani.
31.Haitakiwi kusuhubiana usiku wa kuamkia safari kwani mtoto atakayezaliwa atakuwa mwenye kutumia vibaya mali ya watu na watu kama hao ni ndugu wa masheitani.
32.Atazaliwa mtoto asiye na raha kwa sababu ya kusuhubiana wakati wanapokuwa wazazi katika safari isiyozidi siku tatu.
33.Iwapo kutasuhubiana wakati wa mwanzoni mwa usiku basi mtoto atakayezaliwa atakuwa mchawi na ambaye ataithamini dunia kuliko Aakhera.
34. Hairuhusiwi kusuhubiana mahala ambapo ni wazi kama chini ya mbingu.
35.Allah swt,Mitume na Aimma a.s.,Malaika pamoja na wanaadamu pia hulaani vikali mno kule kusuhubiana barabarani au njiani ambapo hupitwa na watu.
36.Iwapo mtu atakuwa anatakiwa kuoga ghusl-i-Mayyit basi hatakiwi kusuhubiana na iwapo atataka kufanya hivyo,basi itambidi afanye wudhuu
37.Iwapo mtu atapenda kusuhubiana kwa mara ya pili baada ya kwanza,basi itambidi afanye wudhuu.
38.Iwapo mtu atataka Shaitan asiwe mshiriki katika kusuhubiana kwao,basi aiseme kikamilifu "Bismillah".
39.Baada ya ndoa,haifai kusuhubiana kwa mara ya kwanza katika 'tahtush-shoaa' (usiku mbili au tatu za mwisho za mwezi ambapo mwezi hauonekani).
40.Ni haraam kusuhubiana wakati mwanamke anapokuwa katika haidh na nifas, na kwa kukiuka kunatakiwa kulipa kaffarah yake.
41.Mtume s.a.w.w. amesema iwapo atazaliwa mtoto mwenye ugonjwa wa ukoma,basi wazazi ndio watakaojilaumu.
42.Ipo riwaya iliyopokelewa kutoka kwa Imam Jaafer as-Sadiq a.s."Adui wetu sisi Ahlul-Bait a.s. ya Mtume Mtukufu s.a.w.w. ama atakuwa ni waladuz-zinaa au waladul-Haidh. Hivyo mtu akiona kuwa moyoni mwake anayo mapenzi ya Ahlul-Bayt a.s. basi amwombee kheri mama yake mzazi kwa kutomzaa mwana haramu." Ipo riwaya moja isemayo "alikuwa baba mmoja akisema kuwa mtu mwenye mapenzi ya Ahli Bayti a.s. ni mwana halali na mwenye uadui nao ni waladuz-Zinaa. Basi mtoto wake alimwambia baba yake kuwa yeye alikuwa adui mkubwa wa Ahli-Bayti a.s. Sasa jee yeye alikuwa ni waladuz-zinaa ?
Baba yake alimwambia akamwulize mama yake kwani yeye anavyoelewa, alikuwa kweli mwana haramu kwa sababu baba yake alifanya mapenzi na mama yake na walisuhubiana kabla ya ndoa, na mama yake akashika mimba . Baadaye walifanya tawba na kufunga ndoa.Hivyo,kwa kifupi alizaliwa kabla ya wao kufunga ndoa.
43.Haifai kusuhubiana
na
mke mmoja mbele ya mke wa pili lakini
haina shida iwapo kutasuhubiana na kijakazi mbele ya kijakazi mwingine.
44.Haifai kusuhubiana katika hali ya kuwa uchi kabisa bila kujifunika kwani kunawafukuza Malaika.Lakini walimwuliza Imam Musa al-Kadhim a.s. iwapo nguo ikisogea,naye alijibu kuwa hapakuwa na matatizo.
45.Iwapo mtu atasuhubiana na mwanamke aliyepakaa rangi kichwani,basi mtoto atakayezaliwa ataweza kuwa khanisi.
46.Inambidi mtu aondoe pete alizovaa ambazo zimechongewa majina matukufu au naqshi kabla ya kusuhubiana.
47.Haifai kusuhubiana iwapo kuna shida ya kupata maji kwa ajili ya kufanya ghusli
48.Ni makrooh (karaha) kusuhubiana wakati wa alfajiri kabla hapajapambazuka au kuchwa kwa jua kamili.
49.Ni vyema kufunga macho wakati wa kusuhubiana.
50. Hairuhusiwi kusoma Quran Tukufu katika kitanda ambapo wamesuhubiana bibi na bwana na bado hawajaoga ghusl-i-janabakwani kutaweza kusababisha adhabu ya Allah swt kuwaadhibu wote wawili.
1.Ni Sunnah kusuhubiana usiku wa kwanza wa mwezi wa Ramadhani.
2.Mtoto atakayezaliwa kwa kusuhubiana usiku wa jumatatu basi atakuwa (hafidhi Quran) mwenye kuihifdhi
Quran kwa moyo na Allah swt atakuwa amemwia radhi na kwa bahati yake njema.
3.Mtoto atakayezaliwa kwa sababu ya kusuhubiana usiku wa jumanne,iwapo ni mvulana atapata ufalme wa Din ya Islam yaani atakuwa mwema mno na roho yake itakuwa yenye huruma,mikono yake madhubuti na ulimi wake utakuwa umehifadhika na ghibah na buhtan (kusengenya na kusingizia) watu.
4.Kwa kusuhubiana usiku wa alhamisi (kuamkia ijumaa),na mtoto atakayezaliwa ataweza kuwa Hakimu wa Shariah au atakuwa Aalim.
5.Kwa kusuhubiana wakati wa mchana wa siku ya Ijumaa mtoto atakayezaliwa atakuwa amekaa mbali na Shaitan na Allah swt atamjaalia usalama wa Din na dunia.
6.Ukimwona mtoto ni mzungumzaji wa lugha tamu na msomaji wa khutbah basi ujue kuwa huyo ni matokeo ya kusuhubiana usiku wa Ijumaa.
7.Mtoto atakayezaliwa kwa kutokana kusuhubiana baada ya adhuhuri ya Ijumaa ,basi atakuwa akijulikana kwa ukarimu wake.
8.Kwa kusuhubiana baada ya salat al-'Ishaa ya siku ya Ijumaa,mtoto atakayezaliwa atakuwa ni mwenye wadhifa katika Din
Kuna baadhi ya mizozo na sura katika maisha ya ndoa ambazo zinashindikana kutatuliwa katika misingi mbalimbali, na hali ya maisha ya kifamilia inakuwa haivumiliki. Katika hali kama hizo, kunakuwa na njia mbili tu za kufanya ambazo zinakuwa zimebakia:
1.Kumwachia bibi na bwana katika hali hiyo hiyo walivyo, ambavyo kwa mujibu wa aya ya Qurani tukufu ni adhabu ya motoni
2.Kuwaachanisha na kuwatenganisha na mfungamano wa ndoa (talaqa), ili kwamba kila mmoja wao atafute mwenzake atakayeweza kupatana naye ili maisha yao yawe mema na mazuri.
Akili zetu zinakubaliana na utaratibu wa na. 2 na ndivyo vivyo hivyo Uislamu pia unaunga mkono.
Ukristo unapendelea hali ya kwanza yaani kuwalazimisha bibi na bwana waishi pamoja hata kama watachukiana kiasi gani,na hoja hii inatokana na maneno ya Yesu:-
Biblia inatuambia katika Mathayo, 5 : 31 - 32.
"...Kila mtu amwachaye mkewe,isipokuwa kwa habari ya uasherati,amfanya kuwa mzinzi; ...
Tujiulize sisi kama binadamu iwapo zinaa peke yake ndiyo inayoharibu maisha ya ndoa? Je hasira kali au kutafuna haki ya mwenzako au ndizo pia zinazoleta mfarakano katika maisha ya ndoa, Je kudharau kumjali mke kwa kumpa haki zake, uaminifu, kumgeuka mke au kutojali havitoshelezi kufanya nyumba yako ikawa Jahannam?
Ni lazima hapa sisi tujaribu kujua busara ya talaqa ilivyo katika maswala mengi yaliy onyeti, kama ilivyoruhusiwa katika Islam. Leo hata wale watu ambao hawakubaliani na talaqa wanaiambia Serikali katika bunge ipitishe Sharia na muswada kuhusu talaqa, katika Sharia za nchi, mambo ambayo mara nyingi yanapingwa na Kanisa na dini nyinginezo kwa sababu dini hizo hazina mwanya zaidi katika maswala haya.
Dini ya Hindu haitambui talaqa; nao pia katika nchi ya India wametengeneza Sharia na muswada katika Sharia zao za nchi.
Waangilikana nao pia wanapinga
talaqa; nao kwa kupitia
Sharia ya bunge (ambamo Askofu ndio mhusika mkuu -member) Wamekubali
kutenganishwa na mahakama yaani
talaqa.
jambo la kuvutia hapa ni kwamba mkuu wa nchi, mtawala ni mkuu wa Kanisa
Je kwa nini Mfalme Edward VIII alimuoa mwanamke aliyepewa talaqa, na papo hapo maelfu kwa maelfu ya raia wake walikuwa wakipewa talaqa chini ya mamlaka yake? Je inamaanisha kuwa dini ya Kikristo inasheria mbili ? Sharia zake; moja kwa ajili ya watu wakubwa na Sharia nyingine kwa ajili ya watu wa kawaida?
Kanisa la Roman Katholiki linapinga kabisa talaqa. Lakini wamelazimishwa kwa ukweli sugu wa maisha kiasi kwamba wametafuta njia ya kuvunja ndoa bila ya kuita talaqa. Iwapo mtu anasubira ya Job (Ayub) na fedha na mapesa ya Qarun anaweza kupata baada ya kuomba amri kutoka Vatikan, kuwa ndoa yake ilikuwa imekwisha na batil kuanzia mwanzoni.
Mastaajabisho au siyo? Jambo lililogumu hapa ni kwamba atakayepata ni yule tu ambaye yuko katika tabaka la matajiri."Katika miaka ya karibuni, Papa Paulo wa VI ameonyesha utaratibu .....kuwa inaweza kutatua hata ya kesi ya miaka 20. Pamoja na Vatikani za kuweka malipo, gharama za Rot zimebakia juu sana, mara nyingine katika maelfu ya dola na ikiwafanyia wale wenye utajiri."
Iwapo ndoa hiyo itasemwa kuwa hiyo ndoa tokea mwanzoni ilikuwa ni batil sasa watoto waliozaliwa katika kipindi hicho watakuwa na nafasi gani katika Sharia zao? Je tutasema watoto hao ni wana haramu?
Italia chini ya
shinikizo
Ndio tunaona binadamu anavyoweza kuteseka kwa kanuni na Sharia kama hizo.Sio kutaabika na kuteseka tu kunakotokea bali kunawashawishi na kuwasukuma watu kujiingiza katika madhambi (zinaa).Je inawezekana bibi na bwana walioachana kienyeji miaka 20 au 30 iliyopita wakabaki bado wako safi? Bila shaka kila mmoja wao yaani bibi na bwana watakuwa wametaka kutimiza haja zao za kijinsia pamoja na watu wa nje ambao hawakuolewa nao na wengineo humo watakuwa wamewazaa watoto wengi na bila shaka katika kipindi cha miaka 20 - 30 wengine wamekuwa mababu wa wajukuu na watoto wanaharamu ambao amezaa mtoto na mjukuu nje ya ndoa.
Kwa hiyo tukiangalia maswala kama hayo tunaona kweli kuwa Uislamu umetoa mwongozo ulio sahihi na mambo ambayo yanakubalika na akili yetu ili kufanya maisha yetu yakawa mazuri na fanaka.
Kwa kuwa kitabu hiki kinazungumzia mambo ya ndoa hivyo maudhui ya talaqa sitayazungumzia zaidi lakini nimeonelea nigusie kidogo ili tupate kidogo fununu juu ya desturi na Sharia za Kiislamu ni kwa ajili yetu na ubora wetu na kwa ajili ya mustakbali, hivyo msomaji iwapo atapenda kufanya utafiti juu ya swala la talaqa anaweza kujiendeleza au Insha Allah nikifanikiwa nitajaribu kutayarisha kitabu juu ya talaqa na mirathi.
T A M A T I .
[AMD1]SEHEMU YA PILI
Kuhusiana na somo hili la muta', nimejaribu kugawa hili somo katika sehemu tatu ambazo zote ziko zinashikamana kwani kila sehemu inaelezea jambo moja kwa kinaganaga.
Sehemu ya kwanza inahusiana sana na namna hii ya ndoa katika Islam ilivyokuwa na ambavyo ipo bado na masharti yake na kanuni zake na namna inavyobidi kutekelezwa kwa mujibu wa madhehebu haya. Shia Ithna Asheria na ambavyo inavyohukumiwa na 'Ulamaa wa Madhehebu haya. Sehemu ya pili pia inajishughulisha sana na kueleza ubora na umuhimu wa ndoa kama hii katika jamii ya Islam kwani inasaidia kukomesha uovu na uharibifu uliozagaa katika jamii ya Kiislamu na suluhisho lake, hatimaye sehemu ya tatu inaelezea uovu mwingine ambao umeikumba jamii ya Kiislamu ambavyo mwanamke anatoka nyumbani mwake na kwenda kufanya kazi nje kwa ajili ya mambo yasiyo na misingi na hatimaye nyumba inapoteza ule ubora na hadhi yake ya kifamilia, n.k.
Katika kusoma mapokeo na maandishi ya maarifa ya Sharia kuhusu ndoa hii ya kipindi kifupi, kuna mambo fulani fulani ambayo yanabidi kwanza yafikiriwe na yamefafanuliwa vyema kwa mujibu wa Fatawa za ulamaa wa Madhehebu ya Shia Ithna Asheria.
Katika mpokeo huo,kuhusu somo hili,neno muta' ndilo litumikalo sana. Inawezekana kusemwa kwa sababu ya habari zielezwamo katika Qurani kuhusu hii ndoa ya kukatiza. Katika aya hiyo, neno Istimuta limetumika na ambavyo neno Muta' limetokana nalo. Kutokana na mapokeo ya Ma-Imam a.s. au kwa kutokana na mapokeo ya Khalifa Omar, unalipata neno hilo la muta' kwa mfano Khalifa Omar amesema,"wake wawili wa vipindi vifupi wanaruhusiwa." Au Jabir ambaye asema,"sisi tulinufaika sana na ndoa ya muda mfupi wakati wa Mtukufu Mtume s.a.w.w."Vile vile katika mapokezi mengine yaliyo pokelewa na Shu'ba bin Muslim ambaye anasema,
"Mimi nilimwendea Asma binti Abu Bakr. Nilimuulizia kuhusu hii ndoa ya kukatiza nae”.
Kwa ujumla neno muta' linatumika zaidi sana hata kuliko wakati wa Mtume s.a.w.w. au nyakati za wafuasi wake na pia hata wakati wa Imam. Hata wale wanaoipinga hii ndoa pia wanalitumia sana hili neno.Maneno mengineyo yalinganayo na hayo pia hutumika kama vile tamatu' na istimuta'.Hilli analitumia neno hili katika maandishi yake yote na vile vile Shahrihni, lakini kila pale panapohusiana na ndoa ya kukatiza neno tamatu' na Istimuta' pia yanatumiwa.
Wale wanaolitumia neno muta'' wanadhania kuwa aina hii ya ndoa ni kwa ajili ya kusuhubiana. Watu wale watumiao ndoa ya kukatiza wanakuwa na mawazo mawili ya kuoa na kwa muda wa ndoa lazima ieleweke vyema.
Katika vitabu vya elimu ya Sharia za Sunni, kuna ubishano kuhusu hili jambo la ndoa ya kukatiza, iwapo aina hii ya ndoa ni ya muda uliodhaniwa wa kipindi kifupi. Bila shaka wote wanakubaliana kuwa ni aina moja na sawa kabisa, kwani isipokuwa Wahanafii, ambao wanasema kuwa iwapo neno tamatu' linatumika wakati wa kusoma ndoa basi hapo ndipo patakuwa sawa na aina hii ya ndoa ya kukatiza. Hata hivyo, somo hilo sio la muhimu kwao Sunni kwani ndoa iliyo haramu kwao ni ile iliyokatazwa na ambayo ni hii ya kukatiza.
Ilikuwa na picha iliyo wazi mbele yetu kuhusu neno hili la muta' (enye faida), basi inatubidi sisi hapa chini tuzungumzie maelezo kutoka kwa Madhehebu ya Shia na Sunni.
Sheikh Tusi katika kitabu chake Majma' ul Bayan, ambayo ni maelezo juu ya Qurani, anasema yafuatayo juu ya aya hii ya Qurani."Na wale wanaofaidika nao.." (4 :24) kwamba kufaidika na 'inamaanisha kuwaridhisha na matamanio na furaha ya mtu.Maana hii pia inaelezwa na Hassan Mujahid Ibn Zaid na Sa'di.Kwa hiyo maana ya aya hiyo ni kwamba kwa kuwa unafaidika kutoka kwao basi "uwape mahari yao kama mlivyopatana."
Imam Fakhru Razi katika maelezo yake juu ya aya hii anasema: "Kustareheka (Istimuta') maana yake ni kufaidika kutoka kwao. Kwa mathalani, inasemekana fulani bin fulani amefaidika kutokana na jitihada za mwanamke au fulani bin fulani amefariki akiwa yu bado kijana na hakuufaidia ujana wake. Allah, aliye mkuu wa kila kitu asema, "kwa hiyo wewe umestareheka (umefaidika) hisa yako," yaani wewe umefaidika bahati yako na utajiri katika dunia hii. Wewe umenufaika na wenzako wa dunia."
Ndoa isiyo ya kudumu inayo masharti manne ambayo kwa kutimzwa kwake ndiko kunako halalishwa:-sigha yake ambayo ni lazima isomwe; masharti yatimizwe kwa lazima na pande zote mbili zinazohusika; muda wa kudumu hii ndoa iidhinishwe na kuthibitishwa; na mahari yakubaliwe, lazima iwe kwanza.
Ndoa ya muta' inategemea mkataba, kwa hiyo makubaliano na uhakikisho ndivyo vitu vinavyohitajiwa sana.Uhakikisho hapa, kama ilivyo katika ndoa ya kudumu ni lazima itolewe na mwanamke. Mtunzi wa al-Mitajir anadai kuwa wote wawili:mwanamke na mwanamme ni lazima waukubali huo mkataba kwa hiari yao. Katika hali hii,mkataba wa ndoa ya aina hii basi itakamilika kati ya kanuni hizi:"Mimi naolewa na wewe;" Mimi ni mke wako wa muda......;" mimi nadaiwa na wewe (mimi ni wako nilivyo)."
Sayyid Murtaza anasema kuwa mkataba wa ndoa ya kukatiza inawezekana kukubalika baada ya kutamka neno ambalo linaweza ndoa hii kuwa ya kihalali, lakini hii haithibitishwi! Mtungaji wa as-Mis'alik anasema: "Mimi napendelea kuwa kanuni au matamshi yote matatu yasomwe." Kwa hivyo inaonekana kuwa hao watu wanakubaliana kwamba ndoa ya kukatiza haiwezi kukubalika iwapo mtu yeyote atatumia maneno ya kuwa nayo, kodisha, azima au mchango."
Kwa kukubali kwa mwanamme ni lazima atamke hayo maneno yanawezekana, "Mimi nakubali ndoa na faida zake. "Na iwapo mwanamme atasema,"Mimi nakubali na nimeridhika;" au maneno yale yaelezayo hayo, basi mkataba utakuwa sahihi.
Siyo lazima kuwa uhakikisho utangulie makubaliano kwani mkataba unahusiana na makubaliano kwanza ndipo kuhakikisha kinafuata.Lakini itakuwa ni sawa iwapo itatokea hivyo wote wanakubaliana nayo.Asema, "Iwapo mwanamme atasema,"Mimi nakuoa wewe na mwanamke akasema: "Mimi naolewa na wewe" basi ndoa hii itakuwa ni sahihi.
Kuhusiana na ndoa hii ya kukatiza na usomaji wake, Allamah Hilli, anasema kuwa ni lazima isomwe katika nyakati zilizopita lakini 'Ulamaa wengineo wanasema kuwa jambo la muhimu kwamba nia lazima iwe wazi inayoweza kueleweka kwa kweli, kuna maandishi mengi sana yanayoelezea aina hii ya ndoa na ambavyo inatubidi tuyajue hayo.
Kama vile inavyonakiliwa kutoka Imam Ja'afer - us- Sadiq a.s., ambapo Abu ibn Taghlub alipomwuliza Imam kuwa anapaswa amwambie nini mwanamke yule ambaye atakuwa naye katika faragha kwa muda mfupi,Imam alijibu: "Sema mimi nakupa wewe kwa muda (kadha wa kadha )kwa mujibu wa kitabu cha Mungu na mila na utamaduni wa Mtukufu Mtume s.a.w.w. bila ya urithi au kurithiwa kwa ajili ya siku kadha wa kadha na dirham kadha wa kadha."
Katika kunakiliwa kutoka ibn Yahya kwa kupitia kwa Hisham ibn Salim,
ilisemwa "Mimi niliuliza kuwa: "Je ndoa ya kukatiza ni nini?" Je
huo mkataba utatimizwa vipi?"Yeye alijibu:"Mimi nakuoa kwa muda wa
siku fulani kwa kiasi cha Dirham kadha wa kadha. Katika kuongezea zaidi katika
mapokeo ya maandishi na maelezo ya hapo awali, kuna mapokeo mengine manne
kuhusu ndoa ya kukatiza, kama ilivyoelezwa katika kitabu cha
al -
Wasa'il.
Katika mkataba huu, ni lazima makubaliano na kuhakishiwa yafaywe kati ya mtu mwenye kuoa na mwenye kuolewa au kwa wakili wao au baba yao Kwa hiyo inawezekana kwa baba mzazi kusema, "Mimi namwoza binti (kwa fulani bin fulani ) kwa maamuzi na maelewano kwa mujibu wa amri yake mwenyewe." Iwapo mtu atajifanyia mambo tofauti na hayo kinyume na Sharia, basi mkataba huo utakuwa sio kamili, batil.
Kwa sababu ya ndoa tu ndivyo mwanamke anakuwa halali kwa mwanamme. Na hivyo hii imegawanyika katika sehemu mbili:"Yeye kudumu na ile ya muda au kipindi kifupi."Ndoa ya kudumu ni ile ambamo muda kati ya mke na mume haujulikani.Mke anayechukuliwa katika ndoa ya namna hii anaitwa 'wa kudumu' mkataba wa kipindi kifupi ni ile ambamo muda wa mke na mume unajulikana. Tuseme mwanamke anaolewa kwa muda wa saa moja au siku moja au mwezi mmoja au mwaka mmoja au ziada ya hapo. Masomo ya ndoa kama hii ya muda wa kukatiza inaitwa sigha na yenyewe inaitwa muta'
(Nambari zilizoandikwa katika vifungu ni nambari za Fatawa zilizotolewa na Ulamaa wa Madhehebu ya Shia Ithna Asheria na ambazo zimetolewa na Mujtahid Sayyid Ali Husseini Sistani, Najaf-i-Ashraf, Iraq.
(2430) Kufanya muta' (ndoa ya muda mfupi) pamoja na mwanamke ama kwa ajili ya kutaka raha ya kusuhubiana, au kwa sababu nyingine yoyote ile, basi ni sahihi.
(2431) Ni tahadhari ya faradhi kuwa mwanamme asikose kusuhubiana naye mwanamke aliyefanya naye muta' kwa kipindi cha miezi minne yaani inambidi isipite kipindi hicho bila kusuhubiana na mwanamke aliyefanya naye muta'.
(2432)Iwapo mwanamme aliyefanya muta' na mwanamke, ataweka shuruti kuwa mume wake huyo hatasuhubiana naye basi ndoa hiyo itakuwa ni sahihi na vile vile shuruti lake hilo pia linakubalika, kwa hivyo mume atafaidika kwa starehe zinginezo tu bila ya kusuhubiana naye. Hata hivyo iwapo atakubali kusuhubiana naye hapo baadaye,mwanamke anaweza kusuhubiana na bwana wake huyo, na sharti hili linatumika katika ndoa ya kudumu.
(2433)Mwanamke aliyeolewa kwa muta'hawi mustahiki wa kupewa gharama zake hata kama atashika mimba .
(2434))Mwanamke aliyeolewa kwa muta' hastahiki kulala na bwana wake, na wala hana urithi bwana wake na wala bwana wake pia hamrithi mke wake aliyeolewa kwa muta'. Hata hivyo iwapo mmoja wao anaweka sharti na kurithiana basi swala hilo ni ishkal, lakini hata hivyo lazima ichukuliwe tahadhari katika kuweka maanani na utekelezaji wake.
(2435) Iwapo mwanamke ambaye ameolewa kwa muta' alikuwa hajui kuwa yeye si mustahiki wa gharama wala kulala na bwana wake lakini ndoa yake itakuwa sahihi bado, na kutokujua huko yaani kubakia katika hali ya ujahili vile vile atakuwa na haki ya kudai chochote kwa bwana wake.
(2436)Iwapo mwanamke aliyeolewa kwa muta' atatoka nje ya nyumba bila ya ruhusa bwana wake na kwa vyovyote vile haki ya bwana wake itakuwa imevunjwa basi kutoka kwake nje ni haramu. Na iwapo haki ya bwana wake itakuwa imesalimika ichukuliwe tahadhari iliyosisitizwa kuwa mwanamke huyo asitoke nje ya nyumba bila ya ruhusa ya bwana wake.
(2437)Iwapo mwanamke atampa ruhusa mwanamme ya kuwa wakili wake katika kusoma nikah ya muta' pamoja na mwanamke huyo kwa kipindi fulani na kwa kiasi fulani cha mahari, na badala yake huyo mwanamme yaani wakili akasoma nikah ya kudumu pamoja na mwanamke huyo au anasoma nikah ya muta' pamoja na mwanamke huyo bila ya kubainisha wazi wazi kipindi cha muda au kiasi cha mahari, basi ndoa hiyo itakuwa batil.Lakini iwapo mwanamke ataridhia na kutoa ruhusa kwa mapatano hapo mbeleni basi ndoa hiyo itakuwa sahihi.
(2438)Ili kutaka kuwa
mahram
(yaani
ambaye huwezi kumuoa na anakuwa ni jamaa wako wa karibu ), baba
au babu
mzaa baba wanaweza kumuingiza mtoto wao asiyebaleghe au msichana wao
asiyebaleghe
katika ndoa pamoja na mtu
mwingine kwa kipindi kifupi, ili mradi haitatokezea ufisadi.Hata hivyo,iwapo
wao watamuoza mvulana mdogo au msichana mdogo ambaye kwa vyovyote vile hawezi
kupata starehe ya kusuhubiana katika kipindi hicho, basi katika sura hii
usahihi wa ndoa kama hiyo ni
ishkal.
(2439)Iwapo baba au babu mzaa baba wa mtoto asiyekuwapo, wakamuoza kwa mtu ili kutaka kuwa mahram, bila kujua iwapo mtoto yuko hai au amekufa, basi kusudi litapatikana iwapo katika kipindi katika ndoa, mtoto atakuwa na uwezo wa kusuhubiana.Iwapo hapo baadaye itakuja kujulikana kuwa mtoto huyo hakuwa hai wakati wa kusomwa ndoa hiyo basi itachukuliwa kuwa ni batil.Na wale wote ambao walikuwa ni mahram sasa watakuwa na-mahram.
(2440)Iwapo bwana atakuwa amempatia zawadi bibi wake aliyemuoa kwa muta' katika kipindi hicho, na atakapokuwa amemuachia na kama alikuwa amesuhubiana naye basi itabidi ampatie vitu vyote vile alivyokuwa ameahidi kumpa. Na lau kama alikuwa hajasuhubiana naye basi itambidi ampe nusu ya mahari yake, ingawaje achukue tahadhari iliyosisitizwa mno kuwa itambidi ampe mahari kamili.
(2441)Iwapo mwanamme ataingia katika muta' pamoja na mwanamke na mwanamke atakapokuwa katika kipindi cha Iddah kabla ya kuisha basi inaruhusiwa mwanamme kumuoa mwanamke huyo kwa ndoa ya kudumu au ndoa ya muta'.
Leo wale wenye kuwa na mafikara ya Magharibi, baada ya uchunguzi na upekuzi wa historia na kwa kujionea maovu yaliyozagaa katika jamii za siku hizi, wamegundua na kuafikiana kuwa yale mafunzo ambayo wa-Mashariki wanayashikilia (eti maendeleo ya kuleta jamii nyuma ) na ambao wamezubaa, ndizo za kufuata na ambazo ndizo funguo za kukomesha maovu katika jamii za siku hizi na katika siku zijazo.
Jambo ambalo ni la maana la kulizungumzia hapa ni kuhusu hii ndoa ya muda -muta' ambayo itasaidia sana kuepusha balaa ya ndoa-na -talaqa za kila siku katika jamii zetu.Hali ya maisha inaonyesha na kutuambia kuwa binadamu anatenda mambo haraka vile wakati umwelekezavyo. Wanamafikara wa Magharibi na wana-Sharia wa Magharibi leo hii wanasema kuwa talaqa ni jambo ambalo lishughulikiwe haraka iwezekanavyo.Wao wanadhani kuwa talaqa haraka inatokana na ndoa iliyofungwa kwa urahisi na hivyo mtu anao uhuru wa kujiamulia vile aonavyo bora kwake bila ya kuzingatia ubora na heshima ya jamii, kwani kuoa na kuachana ni vitu viwili vilivyo pamoja. Na hivyo ikiwa harusi itakuwa na ugumu ndani yake basi hata talaqa pia itakuwa ni vigumu kutolewa. Lakini hata hivyo wao imewabidi kuamua na kuafikiana kuwa ndoa lazima iwe ni sawa na mkataba kama vile mikataba mingine yote. Na hivyo umuhimu kidogo pungufu upewe ule upande wa muda mrefu wa hisa ya mwanadamu.
Mtazamo huo unashabihiana sana na ule mkataba: Ndoa ya kukatiza ya muda uliokubaliwa kwani katika aina hii ya ndoa, siku zinakubaliwa na kiasi cha mahari kinaafikiwa na makubaliano pia yanaafikiwa.Katika utaratibu huu, mwanamme anayo haki ya kujichagulia mwanamke amfaaye na vivyo hivyo mwanamke anao uhuru na kwa hiari yake mwenyewe ya kumchagua bwana amtakaye mwenyewe kwa muda ule atako yeye/wao.Iwapo bwana na bibi wakipendana zaidi basi wanaweza kuurefusha muda wa mkataba wao.Iwapo patatokea matatizo, basi bwana anaweza kumrudishia siku zake mwanamke. Au iwapo mwanamke anaweza kumrudishia kiasi cha mahari ya siku zilizobakia na hapo akaachana nae. Vile vile katika ndoa ya kukatiza iwapo mtoto atazaliwa basi ni wa baba kama vile ilivyo katika ndoa ya muda mrefu. Lakini kama vile inavyopingana na ile ndoa ya muda mrefu (katika ndoa ya muda mrefu kuzaa mtoto ndiyo jambo la kwanza kutamaniwa na wazazi), ambavyo katika ndoa ya kukatiza haimaanishi kuzaa watoto bali kitu cha muhimu ni maana katika ndoa ya kukatiza ni kuepusha na kutokomesha umalaya katika jamii. Kwa hivyo, wale wasio na nia ya kuiendeleza hii ndoa au wale wasio na hakika nayo, basi ni lazima wafanye nia kutoka mwanzoni kuwa wao hawana lengo la kuzalisha watoto katika kipindi cha ndoa hii.
Kwa desturi, katika kila maendeleo na maumbile ya kila jamii,ndoa ni jambo la muhimu kabisa kwa sababu binadamu anajielekeza yeye mwenyewe kwa jambo la kuoa. Hii ni imani ya kila mtu na hata maumbile yake yanonyesha, kwani hata Mwenyezi Mungu (swt)alipoanza kuumba, alimuumba Adam na baadaye alimuumba Hawa kama mshiriki wake wa maisha. Anasema katika Qurani Tukufu:-
'Enyi watu mcheni Mola wenu
ambaye amekuumbeni katika nafsi (asli) moja.
Na akamuumba mkewe katika nafsi ile ile.
Na akaeneza wanaume wengi na wanawake kutoka katika wawili
hao......'(4:1)
Kwa kawaida mtu anapooa, yeye anakuwa na mabadiliko ya kiroho, kwani anatakasika, na kuanza maisha mapya. Kwa hiyo bwana na bibi wanaitwa pea au jozi. Kwa sababu binadamu wameumbwa kwa jozi, kwani kama kila jozi bila ya kuwa na nyenzie huwa haikukamilika. Ndivyo vivyo hivyo, Adam bila ya Hawa alikuwa hajakamilika na vile vile Hawa bila Adam alikuwa naye hajakamilika. Kwa hiyo mojawapo ya malengo ya ndoa ni kutafuta umbo kamili la binadamu kwa mtazamo wa kiroho kitakatifu.Anaelezea Allah swt katika Qurani:
'Na katika Ishara zake (za kuonyesha ihsani zake juu yenu) ni kuwa amekuumbieni wake zenu katika jinsi yenu ili mupate utulivu kwao, naye amejaalia mapenzi na huruma baina yenu. Bila shaka katika haya zimo Ishara kwa watu wanaofikiri.' (30:21 )
Hata Mtume Mtukufu s.a.w.w. amehimiza sana kuhusu ndoa hadi hapo aliposema wazi kuwa ndoa ni nusu ya dini. (Wasa'il vol 14 uk 5 seh:1 ). Imenakiliwa kuwa Mtume s.a.w.w. amesema:
"Mwenyezi Mungu aliye mkuu, amesema
'popote pale nitakapo kuongezea mambo mema ya duni hii na bora wa Waislamu,
mimi nitawapa moyo wa kunyenyekea, ulimi utakaokuwa ukimkumbuka Allah swt,
mwili imani ambao utakaokuwa unastahimili shida na taabu na yule
mwenzie
ambayo anayo imani ambayo
alikuwa akiiomba kwa machozi ya masikitiko, amfanye mtu kuwa furaha na starehe
.."
(Wasa'il :vol. 14; 23; seh.
:9).
Kwa mtizamo wa nidhamu, ndoa inaweza kutumika kama kampeni mojawapo ya kufuta umalaya na ile nidhamu isiyokubaliwa na jamii ambayo binadamu anapotaka kumaliza hamu yake ya uume au ya kike au nyege, basi inambidi kusuhubiana na mwenzake.Kwa kawaida tabia ya mwanadamu ya kujituliza nyege za kusuhubiana zinaweza kutulizwa tu kwa njia ya ndoa. Wakati ambapo wanyama wanakuwa na nyege za kusuhubiana kwa kufuatana na msimu tu na ndivyo kusema kuwa wanyama huwa hawana ile hamu ya kusuhubiana kila wakati watamanipo kusuhubiana, ila ni binadamu tu ambaye yuko tayari kabisa daima wakati wowote ule na mahali popote pale. Ile hamu ya kusuhubiana na msisimko huwa uko katika kila msimu na kila mahari.Basi iwapo hapatakuwapo na mwongozo au Sharia za Allah swt kati ya uhusiano wa mwanamme na ule wa mwanamke basi mwanadamu atakuwa ni mwovu zaidi hata kuliko wanyama kwa kufuatana na misisimko ya kutaka kusuhubiana na mwenzake.
Wakati uliopita, kila yule mwenye uwezo, alijenga kama ngome kwa ajili yake na humo aliweka wake wengi. Yeyote yule aliyekuwa hajiwezi kwa hamu ya kusuhubiana, basi alikwenda huo na kufanya umalaya. Katika nyakati za jahiliyyan katika Arabia na wakati wa ufalme wa Shah wa Iran, majumba kama hayo yalikuwa yamezagaa kila mahala. Siku hizi vyote vimeangamizwa huko Iran na Arabia.Ubaya na adhabu ya kutenda umalaya umerudiwa kila mara katika Qurani Tukufu adhabu kali imetolewa kwa kutenda uovu huo. Watu walianza kupinga na wale wenye imani hawakurudia kutenda hayo maovu tena. Mubadi katika maelezo yake ananakili mapokeo ya Hadith.Yeye anasema, "Abu Hureirah alisema kuwa Mtume s.a.w.w. amesema 'kwa watu wa aina tatu ambao Mungu atawasaidia......(miongoni mwao ni yule )mtu ambaye anaomba maghfirah kwa Mungu huku akitaka kuoa." Yeye pia amesema, "Popote pale nyie mumwonapo mtu mwenye tabia nzuri na ni mwenye imani, mwozeni mtoto wenu wa kike. Kwani, kwa kutofanya hivyo basi ufisadi utakuingilia."Mu'badi anasema,"Mtume Mtukufu s.a.w.w. amesema hayo na Shaf'i anathibitisha hayo, 'mtu ambaye anao uwezo wa kuoa na anataka kuoa na ni afadhali kuwa huyo mtu atafute mwanamke wa kumwoa na kwa kufanya hivyo ni afadhali kuwa huyo mtu atafute mwanamke wa kumwoa na kwa kufanya hivyo ni bora zaidi hata ya sala za usiku - nawafil. Hata hivyo hilo wimbi la tamaa na msisimko yanapotaka kumghalibu mtu basi yeye anaweza kutuliza kwa kufunga saumu. Mtume Mtukufu s.a.w.w. amesema, "vijana! Yeyote yule ambaye anaweza kujitunza mwenyewe, basi waoe kwani ndoa ni kinga ya macho yenu.Ndoa inamwepusha binadamu kwa kutenda matendo maovu, lakini iwapo mtu hana uwezo, basi afunge saumu, kwani saumu kwa mtu kama huyu haina madhara yoyote kwake. Lakini kwa mtu yule ambaye hana misisimko na tamaa za kila mara za kutenda maovu haya na hana mpango wa kuoa wakati huo, basi sala za usiku (nawafil) ni bora zaidi kwake yeye.Tabarasi katika maelezo yake ameleta zaidi ya Hadith ikiwemo ile iliyonakiliwa na Abu Hureirah kutoka kwa Mtume Mtukufu s.a.w.w.,"Iwapo mtu ana mtoto wa kiume basi ni lazima amtafutie mke na asipofanya hivyo na ambapo huyo mwana akatenda dhambi, basi wote wawili ni dhamana wa adhabu ya madhambi hayo."
Dunia ya siku hizi, kwa tahzibu na imani imezidi kurudia ile hali ya miaka ya ujinga. Kwa haraka sana inarudia hali ya kusonga nyuma, na hii sababu yake ni kuwa binadamu amefuata mkumbo unaopita bila hata ya kufikiria na wala kutojali hali bora ya maisha wa ustaarabu wao.Ile Ne'ema ya Mwenyezi Mungu ya kumpa binadamu fursa ya kutambua kipi ni kibaya na kipi ni kizuri imeshakwisha potea kabisa, kwani siku hizi mwanadamu hayuko tayari hata kuufuata utamaduni wao wala hathaminiki kuufuata tena. Mkumbo wa maisha haukuathiri maji na ardhi tu bali yamemfanya hata mwanadamu asiwe na akili za kufikiria, na kila hisa iongezekavyo ndivyo jamii pia huendelea kurudi nyuma vile vile na hata kupotoka.Katika nchi zile ambazo bado wanazingatia utamaduni na ustaarabu wao wa kale, hali hii ya upotofu ni mdogo kuliko ile ya nchi za mfumo wa Magharibi ambao hawana bahati ya kuyazingatia hayo. Kwani leo wao wanayoyazingatia ni ustaarabu wao wenyewe.Lakini sikitiko kubwa ni kwa wale vijana wenye akili timamu na fahamu timamu wanaoendelea na kuiga vioja viovu vya Magharibi.Wao wanachukulia ule uhusiano wa kiume na kike bila ya vizingiti ati ndiyo alama kubwa kabisa ya maendeleo ya jamii lakini hawatambui kuwa kufanya hivyo wao wanajidhihirisha wazi wazi uovu na ustaarabu wa jamii yao.
Katika nchi za Magharibi, maana halisi ya ndoa imetimuliwa mbali kutoka mizizi yake. Sharia ya kawaida imeiwakilisha ndoa na hii ni kwa sababu wa mkumbo wa maisha unaowafanya wapotezwe na zile kanuni zao za dini na mila hadi mtu kufikia hatua ya kutoamini kuwa kuna Mungu, au kuna siku ya Qiyama tu' Mapenzi ndiyo malipo yake kwani wao wanavutiwa na tamaa zao tu. Enzi za zamani pia watu walikuwa wakifanya aina hii ya mapenzi lakini malipo yao yalikuwa ni mapenzi ya Mungu kwani mapenzi ya mtu na Mungu ni thabiti wakati mapenzi kati ya mwanamme na mwanamke ni ya kulaghai tu. Iwapo tunawaona waumini wakituambia kuwa dunia hii siyo ya kudumu bali ni uwanja wa majaribio kwa hivyo wao wanajaribu kujijenga na kujitayarisha kuishi katika dunia itakayo dumu milele kwa kujiepusha na kila matakwa (yasiyo bora ) ya mioyo yao na kufuata maamrisho ya Mwenyezi Mungu swt, kama alivyosema Allah swt katika Qurani Tukufu.
"......Ambao
uwapatapo msiba husema:
"Hakika
sisi ni wa Mwenyezi Mungu, na kwake yeye tutarejea (atatupa jazaa
yake)."
(2:156)
Katika kila desturi na utamaduni na ustaarabu, uhusiano kati ya mwanamke na mwanamme hasa ni kwa kupitia ndoa tu ambayo inatimizwa kwa Sharia na kanuni za kidini au njia ile iliyo halali. Katika utamaduni zinginezo,sababu kuu ya kuoa ni kustawisha familia. Kama ilivyo (familia ) nyumba ni kiini cha shughuli na mafunzo yote ya jamii ambapo mafunzo wayapatayo memba wa familia na watoto ili siku zijazo warithi wazazi wao na kudumisha jina lao na sifa zao na za jamii nzima kwa ujumla - na hii ndiyo kiini cha ndoa. Kila mtu anataka abakie na ukumbusho wake baada ya kifo chake. Iwapo kila mtu na familia wakitambua wajibu wao na shughuli atakazo kuzifanyia familia yake kwa upendo na kwa kushirikiana vyema na wenzake, basi kutakuwa na usalama na amani na bongo tulivu miongoni mwao.
Ikiwa itatokea utaratibu na mazingara kama haya, basi wanawake wanafunza mafunzo bora kabisa watoto wao na pia wanatunza nyumba zao vyema na wanaume wao wanashughulikia mambo mengineyo ya jamii hii, pia ni lengo mojawapo la ndoa kwani jamii au familia inaumbika kwa mambo haya ya usalama na uwema wa jamii unatokana na upole na usalama wa akili, ya kila familia, na hapo ndipo nchi imara inajengeka kutokana na jamii bora kama hizi. kwa hiyo kutuliza akili na usalama wa mwili wa jamii ni usalama na ubora wa familia. Papo hapo ndipo panapotokea mategemeo ya maendeleo ya nchi na hii ndiyo sababu kuu kati ya chi na jamii ambayo yanatokana na mambo hayo hayo niliyoyalezea hapo awali.
Bila shaka tumesoma sehemu ya kwanza na ile ya pili katika mfululizo wa aina hii ya ndoa ya kukatiza au muta', kwa hivyo hadi hapa tumeona na kushuhudia namna vile wana wa Magharibi walivyopoteza ile imani ya ndoa kihalali na vivyo ndivyo walivyokosa ile imani na ubora wa familia. Kwa hakika hali hii ni mbaya na hatari kabisa. Katika hali hii pia kuna matumizi mabaya ya maisha ya mwanadamu kuhusu uhuru wa mwanamke kuwa sawa na mwanamme. Wote wanawake na wanaume wanasema ni lazima wanawake wawe sawa katika jamii. Kwa hakika hakuna tofauti yoyote kati yao kwani wote ni sawa kuanzia pale walipozaliwa, lakini wao hawakuelewa maana halisi ya usawa huu. Wao wanadhani kuwa mwanamke pia awe na kazi katika jamii kama vile alivyo mwanamme.Hiki ndicho chanzo cha kumfanya mwanamke kutoa mguu wake nyumbani na kwenda kufanya kazi pamoja na wanaume katika maofisi na wala sio nyumbani tena na ambavyo hawataki tena kubakia nyumbani kufanya kazi za nyumbani za kulea na kuwaelimisha watoto wao kwani ikiwa mwanamke atabakia nyumbani akitunza nyumba yake na akabakia kuwa mke mtiifu na mpole, basi heshima yake itakuwa ni dumi ya ile ya mwanamme ambavyo nikinyume cha Udemokrasia. Mawazo haya ni yale kutoka kwa miaka ya viwanda ambapo wanahitaji nguvu za wanawake (kuvutia ) kusukuma biashara yao mbele ya makampuni au viwanda. Upande mwingine wao wanasema kuwa mwanamke anayo haki sawa na ya mwanamme na pengine husema kuwa wanawake wako huru kwa hivyo mwanamke lazima aache nyumba yake na atoke nje kwenda kufanya kazi pamoja na wanaume kwani mambo haya mawili ni lazima katika haki ya upande wao.Kwa hivyo kila usikiapo 'Usawa na uhuru wa wanawake' basi uelewe kuwa wanaviwanda wanawatumikisha wanawake katika kazi zao za viwandani na sababu nyingine ni kwamba eti familia yao haijitoshelezi kimaslahi na hivyo ndivyo wanawake hawana budi kwenda kufanya kazi nje ya nyumba zao.
Hoja yangu kubwa ni kwamba wanawake wa dunia hii wasijaribu kuwaiga wale wanawake wa Magharibi kwa sababu nchi zao ni za viwanda na ili kuwa sawa wote inawabidi wanawake pia wajilazimishe kufanya kazi katika sekta hii ya uchumi na hivyo ndivyo adhaniavyo mwanamke wa Magharibi. Hapo ndipo migongano ya kila aina ya kupangiwa kazi huwa zinatokea. Huu ni ukweli kuwa hali hii ya namba hii ipo bado ingali ikiendelea katika nchi za Ukomunisti mwanamke kwanza kabisa inambidi achukue koleo nzito na aanze kutengeneza na kujenga barabara kwa mtazamo wa uchumi na wa viwanda, na hapo ndipo ajionapo yu sawa na wanaume.Upande mwingine,iwapo mwanamke inambidi kwenda kufanya kazi nje ya nyumba yake, basi ni lazima awaache watoto wake chini ya walezi wengine au chini ya ulezi wa serikali. Hapa utaratibu na shughuli za nyumbani zinagawanyika kati ya mwanamke na mwanamme na hapa ndiyo maana halisi ya nyumba inapofifia. Nyongeza ya hapo, wakati mwanamme na mwanamke wanapokuwa sawa katika kila sehemu, basi ule ubora na udhaifu wa mwanamme unaanza kuujongelea ule wa mwanamke na mwanamke mienendo yake inazidi kukaribia ile ya kiume. Hapo ndipo tutasema kuwa mwanamme si mwanamme halisi tena na mwanamke pia si mwanamke halisi tena. Itakuwa ni bora iwapo nitawadokezea ile Hadith ya Mtume Mtukufu s.a.w.w.:
"Mwenyezi Mungu atalaani kabila nne za watu na Malaika wataitikia 'aamin.' Moja ni yule mtu mwanamme ambaye anajigeuza au kujilinganisha au anafanya au kujilinganisha na ile mienendo ya mwanamke wakati ambapo Mungu amemuumba yu mwanamme na vile vile yule mwanamke ambaye anamuigiza mwanamme wakati ambapo yeye ameumbwa na Mungu kuwa mwanamke."
Mwenyezi Mungu alimuumba Adam kwanza na baadaye Hawa. Wanasema kuwa kabla ya kuumbwa Hawa, Adam alikuwa hajakamilika kama mwanamme na hapo baada ya kuumbwa kwa Hawa basi Adam alikamilika kuwa mwanamme kwa kuota ndevu.Kwa hiyo maana halisi ya maneno hayo ni kwamba mwanamme bila ya mwanamke hawezi kukamilika na vile vile mwanamke bila ya mwanamme pia hajakamilika na hivyo ndivyo tuseme kuwa mwanamme ni mwanamme tu na mwanamke ni mwanamke tu.Iwapo mmoja wapo atakosa basi hakutakuwapo na ukamili wowote kati yao kimaumbile. Jambo kuu la kuzingatia na kulitazama ni la uchi-uume na ukike.Na hapa ndipo Mungu anapomkumbusha mwanadamu kuwa, aheshimu maumbile yake kama ni mwanamme basi abakie kuwa ni mwanamme na kama ni mwanamke abakie kuwa ni mwanamke. Lakini wao wamejidanganya na kujigeuza kwao kwa vile walivyoumbwa.
Kwa hivyo huu usawa sio ule wana wa Magharibi wachukuliavyo bali ni vile kama desturi, mila na utamaduni za dunia zielezavyo. Hapa inamaanisha kuwa pale popote palipo, mwanamme anazo shughuli zake za kuzifanya na vile vile mwanamke pia anazo shughuli zake,hivyo kwa vyovyote vile shughuli zitakapoongezeka ndivyo mwanamme ataendelea kukomaza ile hadhi yake ya kiume na ambazo ni kwamba mwanamke ataendelea kuwalea na kuwafunza watoto wake kila jema, kwani kwa kadri ya uwezo wake na kutunza familia yake vyema kwani hapo ndipo kutampa moyo mumewe kufanya kazi zaidi kwa nidhamu katika jamii.
Je kuna heshima gani kati ya mwanamke na mwanamme iwapo wote watakuwa 'sawa?'Mtu mashuhuri wa India anasema kuwa:"Ile heshima ya mwanamke kuwa sawa na mwanamme ni sawa na kusema kuwa Muasia kujigeuza kizungu."(yaani Muasia anajisahau na kujigeuza kuwa yuko anaishi kizungu ambavyo yeye siyo Mzungu bali ni Muasia kwa asili yake).
Katika Sharia za kiungwana za Japan, shughuli za mwanamke nyumbani
ni sawa na kazi za mwanamme katika jamii na nusu ya mapato yote ya mwanamme ni
haki ya mwanamke.Kwa hivyo, wakati wa kuachana, nusu ya mali yote ile
aliyoichuma mwanamme baada ya ndoa na imekusanywa nyumbani, basi hiyo sehemu
nusu ni ya mwanamke.
Wao wanasema kuwa
ule ushindi uliopatikana katika vita vya pili vya dunia, vilitokana na utunzi
na malezi na mafunzo mema kabisa yaliyokuwa yakitolewa na mama zao na ambavyo
kusema kuwa wafunzi bora wa watu ni
mama.
Katika kila familia inayofuata mila na utamaduni, wazazi wana nguvu na sauti juu ya watoto wao.Nao watoto pia wanazo heshima, mapendo na uhusiano bora kabisa na wazazi wao. Hapa itabidi kusema kuwa yule mtu ambaye hataweza kuelewa huruma na mapenzi ya wazazi, basi hata baraka za Mwenyezi Mungu atazikosa. Inasemekana kuwa, "kwa mujibu wa Sharia za Manu, Mwalimu ni bora kuliko watu kumi wenye heshima.Baba mzazi ni sawa na walimu kumi kama hao lakini mama mzazi ni sawa na baba elfu moja kwa heshima na kama mwalimu."
Annealed kusema "Hata siku hizi, mama wa Ki-Hindu wana unyenyekevu na uwezo mkubwa wa kusema bado kuliko mama wazazi wengineo hata kama wakiwafananisha kiasi gani.Mama huwa anawahukumu wote hata kama wamekuwa wakubwa wala sio watoto tu kwani wanao uwezo zaidi wa kuhukumu nyumbani.Kwa maoni yangu mimi, wale watoto waliokulia katika desturi za Kizungu tu ndio wasio na adabu na heshima kwa wazazi kwa wazazi wao."
Ni heri iwapo tuanze kumalizia maneno yetu kwa kusema kuwa iwapo wanasheria katika nchi zisizo za Kiislamu wakijaribu kuingiza aina hii ya ndoa katika (ndoa ya kukatiza) Sharia zao, basi lazima uovu uliozagaa katika jamii zetu zitafutwa kwani hadi sasa wao wanazo zile Sharia zihusuzo ile ndoa ya muda mrefu (permanent marriage). Hii haimaanishi kuwa ndoa ya kukatiza iwakilishe ndoa ya kudumu, na popote pale mtu atakapo mpa mwenzake talaqa basi bila shaka Sharia wanazo tayari zilizotungwa na ambavyo ni imani kubwa. Lakini hili jambo la kuliingiza la ndoa ya kukatiza ni gumu sana kwani iwapo itakubaliwa basi lazima pia itolewe utaratibu halali wa kulitimiza.Kwa wakati huu, mimi sidhani iwapo aina hii ya ndoa ya kukatiza itawezekana au la.Hata hivyo mambo yafuatayo yanaweza kutupatia mwongozo wa kuyafafanua vyema.
Je nini maana halisi ya 'ndoa?' Je nini ukweli wa ndoa? Je ni nini maadhimio au mategemeo yake? Baada ya kuyajibu kwa ufasaha tu ndipo mtu anaweza kuelezea vyema ndoa ya kukatiza na nini mategemeo ya ndoa ya kukatiza na kuna tofauti zipi kati ya ndoa ya kukatizwa na ile ya muda mrefu.Kwa ufupi, kuandika haya kwa mifululizo sio kuthibitisha au kukanusha imani ilivyoeleweka kutoka kwa wanavyuoni na mtu asitende kinyume na maelezo yao. Kwani inavyojieleza wazi wazi msimamo wake wa ndoa hii ya kukatiza. Kwa mujibu wa wafuasi wa Madhehebu ya Shia Ithna-Asheria, ndoa ya kukatiza inaruhusiwa (halali) na ambavyo kwa mujibu wa Madhehebu ya Sunni, hii ndoa imeharamishwa. Mimi nimejaribu kuelezea vyote. Mimi azma yangu ilikuwa ni kuelezea wazi wazi ile ndoa ya kukatiza na msomaji atakuwa ameona kuwa hii ndoa inayo misingi mingi bora, sababu ya imani ambazo madhehebu yote mawili yanavyoelezea wazi wazi.
—A—
Adhaan, 91
Ahlul kitab, 75
amelawitiwa, 77
anayelawiti, 77
—B—
baba, 15, 23, 71, 72, 81, 86, 100, 101
babu, 71, 72, 81, 101
baleghe, 54, 71, 72, 77
batil, 47, 68, 71, 73, 75, 77, 80, 81, 84, 85, 86, 95, 100, 101, 102
bikira, 72
binti, 21, 46, 62
—D—
dada, 46, 77
Dua, 54
duaa, 57
—F—
fatawa, 68
filamu za watu uchi, 50
fiqh, 48, 76, 78
fitri, 84, 85
—G—
ghusli, 47
ghusl-i-janaba, 44, 90, 93
ghusl-i-Mayyit, 92
—H—
haidh, 44, 57, 67, 73, 76, 84, 85, 86, 88, 89, 92
haja ndogo, 45, 88
halaali, 47
hijab, 82, 83
Hindu, 95
Hur al-Ain, 5
—I—
Iddah, 45, 46, 48, 74, 76, 77, 78, 82, 84, 85, 86, 87, 102
Ifza, 78
Ifza', 73
ihram, 77
Iqamah, 91
ishkal, 80, 81, 83, 101, 102
Istehadha, 89
Istighfaar, 55
—J—
janaba, 44
—K—
kabila, 52
kaffarah, 92
kamari, 64
khanisi, 50, 93
Khatna, 58
kubaka, 46
kuchomwa moto, 51
kumpiga mke, 42
kuoa, 4, 29
kupigwa mawe, 45, 51
kuridhika, 49
kusuhubiana, 57, 72, 88, 98
kutooa, 54
kutosheka, 49
kuvunja ndoa, 72
kuwaoa dada wawili, 45
kuwaoa ni haramu., 73
—M—
maasi, 63
magonjwa, 66
mahari, 69, 70, 72, 73, 77, 79, 80, 81, 82, 84, 86, 87, 98, 99, 101, 102
mahram, 73, 74, 81, 82, 83, 84, 101, 102
malaya, 48, 61, 76, 105
mali, 4, 52
mama, 16, 18, 21, 46, 77
mama mkwe, 75
manii, 44, 50, 51, 57, 59, 68, 89, 90
Manukato, 65, 87
mashurubu, 44
matamanio, 58
matiti, 60
maziwa, 60
miaka tisa, 45, 78
milli, 84, 85
mimba, 4, 32, 36, 37, 43, 54, 57, 58, 73, 80, 85, 86, 88, 89, 91, 92, 101
mirathi, 96
mjane, 5
mkataba, 100
mkataba wa, 71
mroho, 49
msichana mdogo, 45
Msisuhubiane, 87
mujtahid, 79
Mumiin, 46, 47
mushrik, 46, 47
musuhubiane, 87
muta', 22, 46, 68, 74, 75, 76, 77, 79, 80, 81, 82, 97, 98, 99, 100, 101, 102
mwana halali, 85, 86, 92
—N—
najis, 47
nawafil, 105
ndoa ya utotoni, 53
nguvu za kiume, 51
nifas, 89, 92
nikah, 46, 47, 48
njia ya nyuma, 44, 87
njia ya nyuma, 45
nurah, 44
nyama ya mizoga, 65
nywele, 44
—P—
pete, 93
pombe, 59, 60, 61, 62, 63, 64
—Q—
Qamar dar Aqrab, 5
Qibla., 90
Qiyama, 4, 62, 63, 65
—R—
Rakaa, 4, 54, 90
Rashida, 72
riba, 63
Romani Katholiki, 95
—S—
sala, 63
samahani nisamehe, 8
shanghazi, 46, 73, 74, 75
sigha, 46, 69, 70, 98, 100
—T—
talaqa, 11, 45, 46, 47, 48, 53, 71, 73, 74, 75, 76, 77, 78, 84, 85, 86, 94, 95, 96, 102
tawaf-un-nisa, 78
tawba, 76, 77
tohara, 76
toharah, 47
—U—
uchawi, 61
uchi, 93
ukhanisi, 48
Ukristo, 94
Ulawiti, 51, 65, 77, 83
ummah, 4
umra mufrada, 78
urembo na utajiri, 52
urithi, 46, 80, 101
uume, 58, 68
uume wa mwanamme, 50, 58, 73, 77
—V—
viboko, 45, 51
vikanyagio vya miguu, 88
—W—
Waangilikana, 95
wachinjwe, 51
wake wanne, 48
wakili, 69, 70, 71, 81, 100, 101
waladul-Haidh, 92
waladuz-zinaa, 45, 92
wana haramu, 95
wanawake wawili, 90
Watapigiliwa misumari, 65
watoto wa shangazi, 46, 75
watoto wa wifi, 46, 75
wifi, 46, 73, 74, 75
wudhuu, 47, 91, 92
—Y—
Ya'isa, 84, 85, 86
—Z—
zaka, 63
zinaa, 14, 45, 46, 59, 64, 65, 75, 76, 77, 84, 85, 94, 96
NA KUTARJUMIWA NA
AMIRALY
M. H.
DATOO
- P.O. Box
838 - BUKOBA TANZANIA
1.
TAJWID
ILIYORAHISISHWA
2.
BWANA ABU TALIB
a.s. MADHULUMU WA HISTORIA
3.
FADHAIL ZA IMAM
ALI IBN ABI TALIB a.s.
4.
HUKUMU
ZILIZOTOLEWA NA IMAM ALI IBN ABI TALIB a.s.
5.
UHARAMISHO WA
KAMARI KATIKA ISLAM
6.
UHARAMISHO WA
VILEO KATIKA ISLAM
7.
MSAFARA WA IMAM
HUSAYN IBN ALI a.s. MADINA – KARBALA
8.
DALILI ZA
QIYAMA NA KUDHIHIRI KWA IMAM MAHDI a.s.
9.
KITABU CHA
TAJWID
10.
NDOA KATIKA ISLAM
11.
MAKALA MCHANGANYIKO
No. 1
12.
MAKALA MCHANGANYIKO
No. 2
13.
KESI YA FADAK
14.
UWAHHABI – ASILI NA KUENEA KWAKE
15.
TAWBA
16.
TADHWIN AL-HADITH
17.
HEKAYA ZA BAHLUL
18.
SHADA
19.
TAFSIRI YA JUZUU’ ‘AMMA
20.
HIARI NA SHURUTISHO KATIKA ISLAM
21.
WAANDISHI MASHIA KATIKA SAHIH NA SUNAN ZA AHL SUNNA
22.
USINGIZI NA
NDOTO
23.
MAJINA KWA AJILI YA WATOTO WAISLAMU
Page:
117
[AMD1] closed at 4.50 pm on 22/8/95