Makala haya yametarjumiwa na
Amiraly M.H.Datoo
Bukoba Tanzania
(12 March 2003 muafaka wa 8 Muharram 1424 Hijriyyah )
www.al-islam.org and ebooked by www.ShiaLibrary.com and www.islamkutuphanesi.com . May Allah be pleased with all. |
>>ASSALAMU 'ALAYKUM YA SHUHADAA-I-KERBALA<<
JARIBU
KUTEMBELEA JANGWA LA KARBALA, AMBAPO KUNA MAFURIKO YA DAMU, MVUA ZA MACHOZI NA
NYOYO ZINAZOLIA KILIO CHA KIU CHA AL ‘ATASH….
ENEZA UJUMBE WA
KARBALA … ENEZA DINI YA ISLAM …, DINI YA KWELI NA YENYE KUDUMU ….
Imam Hussain ( a.s.) awasili
Karbala huku akiuongoza msafara wake wa Wananyumba wa Mtume Muhammad s.a.w.w.
wakiwemo ndugu, jamaa, wanawake na watoto wakiwa jangwani
Imam Hussain (a.s.) akiongea na watu wa Kabila la Asad na akipatana nao kuhusu ununuzi
wa ardhi ya Karbala
Imam Hussain (a.s.) akilihutubia jeshi la ‘Umar ibn Sa'ad (AL) kabla ya kuanza kwa Vita
Imam Hussain (a.s.) akikubalia bay’a ya watu wawili. Hur (A) akiomba
msamaha na kujiunga na kambi ya Imam Hussain ( a.s.)
Imam Hussain (a.s.) akizileta maiti za waliouawa Shahidi katika mahema yao.
Vita pamoja na maadui (AL)
Ali al-Akber (a.s.) kijana mwenye umri wa miaka 18 mwana wa kiume wa Imam Hussain
( a.s. ) akifa Sahihidi mikononi mwa baba yake aliyekuwa amedhoofika.
Abbas (a.s.) akiwa katika mto Furati akiwaangalia vile majeshi ya adui ‘Umar ibn Sa'ad (AL) walivyokuwa wakikimbia
Imam Hussain (a.s.) akimwinua mtoto mchanga ‘Ali Asgher (A) kuelekea jeshi lisilokuwa na
aibu wala haya wala huruma, akimwombea maji mtoto huyo, ambapo jeshi kwa
kikatili lilimwua mtoto huyo kwa mshale wenye midomo miwili
Imam Hussain (a.s.) akiwaaga wakina mama katika hema. Al Wida' Al Akhir
(Kuaga kwa mara ya mwisho)
Imam Hussain (a.s.) akiwa vitani
Akiwa ameanguka Imam Hussain (a.s.) akisubiri mwito wa Allah (swt)
Zuljana akirejea kwa akina mama bila ya kuwa na mmiliki wake kurejea
hemani.
Wanawake watakatifu na watoharifu wa Nyumba ya Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. (
Ahlul Bayt a.s. ) wakijitupa miguuni mwa Zuljana ambaye amerejea bila ya
Imam Hussain ( a.s. ).
Wananyumba wakiwa pamoja na Zuljana asiye na bwana wake, wakilia juu ya
kifo cha Imam Hussain ( a.s. ).Wanawake wa wanayumba ya Imam Hussain ( a.s. ) wakilia
kwa maangamizo na mateso na dhuluma yaliyoyapata katika masaa machache yaliyo
pita.
Kiwiliwili bila kichwa cha Imam Hussain ( a.s. ) Kilichokuwa kimeachwa
katika jangwa la Karbala baada ya Vita
Maadui wa jeshi la ‘Umar Saad (AL) waanza uporaji na kuchoma moto mahema ya
wananyumba wa Ahlul Bayt a.s. ambamo waliobakia ni wanawake, watoto na wagonjwa
tu - Shame Ghariba
Katikati ya hofu na vitisho, wananyumba wa Imam Hussain ( a.s. ) wajikusanya mbele
ya Imam aliyeshika hatamu ya Uimamu, Al Imam – ‘Ali ibn Hussain Zayn al-‘Abidin
(a.s.)
Wakiwa wamefungwa minyororo mizito shingoni na miguuni na huku wakitembezwa kwa
miguu - Imam 'Ali Zaynul-‘Abidin
(a.s.), wanawake, watoto na wagonjwa wachukululiwa
mateka
Zainab (a.s.) na Imam ‘Ali Zayn Al ‘Abidin (a.s.) wakiwa katika baraza la
viongozi makatili na dhalimu
Imam ‘Ali Zayn al-‘Abidin (a.s.) akiwa katika baraza la Yazid ibn Mua'awiyaah (AL) huku kichwa cha
Imam Hussain (a.s.) kikionyeshwa
Imam ‘Ali Zayn Ali ‘Abidin (a.s.) akimhutubia Yazid (AL) katika baraza lake
Idumu milele bendera ya Islam ambayo iliokolewa na damu toharifu ya Mashahidi
wa Karbala
HUSSAIN YU HAI DAIMA...YEYE
JANA PIA ALIKUWA HAI NA LEO PIA YU HAI NA DAIMA ATAKUWA HAI …..
… DAMU YA HUSSAIN (
a.s. ),
SABR YA ZAINAB ( a.s. )
MAUAJI YA KARBALA,
NDIYO YALIYOOKOA
LA-ILAHA-ILLALLAH...
>>ILTIMAAS-E-DUA'A,
MO'MIN MOHTAAJ-E-DUA'A<<