YALIYOMO
|
|
Kimetungwa na:
(
Kimefasiriwa na:
Seyyid
Muhammad Mahdi Musawy
Shushtani
(
Kimetolewa na:
BILAL MUSLIM
P.O.
DAR ES SALAAM
Haki zote ziko kwa Bilal Muslim
Chapa ya kwanza, 1972, Nakala 2,000
Chapa ya pili, 1983,Nakala 2,000
Chapa ya tatu, 1987, nakala 5,000
ISBN
9976 956 26 6
Kimepigwa chapa na
Hii
ni tafsiri ya Kijitabu Kilichoandikwa kwa lugha ya Kiarabu, Kilichoandikwa na
Ayaatullah Seeyyid Muhammed Mahdi Shirazi wa
Hatuna budi kutamka hapa kuwa mujibu wa
imani yetu,
Mitume wote waalikuwa
wametumwa na Mwenyezi Mungu Kuwaongiza watu katika njia iliyo sawa.
Waalifanya hivyo kwa kuhubiri wema wao mkuu
na kwa matendo
Kufanya hivyo iliwapasa wawe waongofu
zaidi, waadilifu na kuwa wakamilifu katika uchaji wao kwa Mwenyezi Mungu.
Wasingeweza kusema uwongo iwapo wao
walifundisha watu kusema kweli.Wasingeweza
kumwomba Miungu, iwapo wao waliwataka watu kumwomba Mungu Aliye Mmoja
tu, na kadhalika.
Hata hivyo, Biblia inasingizia zote za maovu na madhambi kwa Mitume hao. Ama viongozi wa Kiyahudi na Wakristo walikuwa na madhambi makubwa kabisa, la sivyo, basi ni makosa ya Biblia yenyewe (inayoaminiwa kuwa si maandishi ya Musa wala Isa a.s)
Kwa hiyo,
ni juu ya msomaji mwenyewe kuteua yapi yanayomfaa na yapi yasiyomfaa.
Syed
saeed Akhtar Rizvi
Je, wewe unaona huyu
Mungu wa Biblia ni wa namna gani?
Kama Mungu nao mwili, nywele na vazi ,
anaishi katika mahala , hajui kitu kilichofichika nyuma ya mti , anadanganya
watu, huvunja ahadi yake, je binadamu yukoje?
Swali: Ati Mwenyezi Mungu ana sura ya binadamu?
Jibu:
Sivyo Kamwe. Lakini katika Biblia
kitabu cha kwanza kiitwacho Mwanzo, Sura ya 1, aya ya 26 na 27, Imeandikwa
hivi: “Mungu akasema, Na tufanye mtu kwa mfano wetu, Kwa sura yetu, Mungu akaumba mtu kwa mfano wake, Kwa mfano
wa Mungu na Mungu alimwumba, Mwanamume na Mwanamke aliwaumba.”
Swali: Ati
Mwenyezi Mungu anazo nywele? Anacho kivazi?
Jibu:
Sivyo kamwe. Lakini katika Biblia kitabu cha Danieli, Sura ya 7, Aya ya
9, imeandikwa hivi: “Ni katazama hata
viti vya enzi vikawekwa, na Mmoja aliye mzee wa siku (Mwenyezi Mungu) ameketi,
Mavazi yake yalikuwa meupe kama theeluji, na nywele za kichwa chake kama sufu
Swali:
Ati Mwenyezi Mungu anayo miguu miwili?
Jibu: Sivyo Kamwe. Lakini katika
Biblia kitabu cha kutoka sura ya 24, aya ya 10, Imeandikwa hivi: “Wakamwona
Mungu wa Israeli: chini ya miguu yake palikuwa na
Swali:
Ati Mwenyezi Mungu ana pahala ambapo anaonekana?
Jibu: Sivyo
kamwe. Lakini Biblia katika kitabu cha
ufunuo wa Yohana, Sura ya 4, aya ya 2, Imeandikwa hivi:” Na mara nalikuwa
katika Roho: na tazama, Kiti cha enzi kimewekwa mbinguni na mmoja ameketi juu
ya kiti: na yeye aliyeketi alionekana mithili ya jiwe laq yaspi na akiki, na
upinde wa mvua ulikizunguka kile kiti cha enzi, ukionekana mithili ya
zumaridi.”
Swali: Ati Mwenyezi
Mungu hutembea?
Jibu:
Sivyo kabisa. Lakini katika Biblia kitabu cha kwanza kiitwacho Mwanzo,
sura ya 2,aya ya 8, imeandikwa hivi: “Kisha wakasikia (Adamu na mkewe) sauti ya
Bwana Mungu, akitembea bustanini wakati wa jua kupunga: Adam na mkewe
wakajificha kati ya miti ya bustani, Bwana Mungu asiwaone."
Swali: Ati Mwenyezi Mungu hutembea?
Jibu: Sivyo Kamwe. Lakini katika Biblia kitabu cha Pili kiitwacho kutoka, sura ya 19, aya ya 20, imeandikwa hivi: “Bwana akaushukia mlima, Bwana akamwita Musa aende hata kilele cha mlima: Musa akapanda juu.”
Swali
: Ati Mwenyezi Mungu huteremka juu ya wingu na anakwenda mbele ya
mtu?
Jibu: Sivyo kabisa Biblia kitabu
cha pili kiitwacho “KUTOKA” katika sura ya 34 aya ya 5 na 6, imeaandikwa hivi:” bwana akashuka ndani ya
lile wingu, akasimama pamoja naye huko,
akalitantaza jina la Bwana. Bwana akapita mbele yake.”
Swali: Ati Mwenyezi Mungu huchagua mahala pa kukaa yeye?
Jibu: Sivyo
kabisa. Lakini katika Biblia kitabu cha
Zaburi ya 132, aya 13, imeandikwa hivi: “kwa kuwa Bwana ameitamani akae ndani
yake.”
Swali: Ati
Mwenyezi Mungu mjinga? Hapambanui kati ya milango ya wenyekuamini na makafiri
ila kwa alama?
Jibu: Sivyo Kabisa.
Lakini Biblia kitabu cha pili, Kiitwacho, KUTOKA, sura ya 12. aya ya 12
na 13, meandikwa hivi: “Maana nitapita kati ya nchi ya Misri usiku huo, nami
nitawapiga wazaliwa wa kwanza wote katika nchi ya Misri, wamwanadamu na
wanyama; nami nitafanya hukumu juu ya
miungu yote ya Misri; Mimi ndimi Bwana. Na ile damu itakuwa ishara kwenu katika
zile nyumba mtakazokuwamo nami nitakapoiona ile damu, nitapita juu yenu,
lisiwapate pigo lolote likawaharibu nitakapoipiga nchi ya Misri.”
Swali: Ati Mwenyezi Mungu hawezi kujua kwamba mtu amejificha katika mti?
Vile vile hajui nani amemfundisha binadamu?
Jibu: Sivyo kabisa. Lakini Biblia katika kitabu cha Mwanzo sura ya 3, aya 9-11, imeandikwa hivi,”Bwana na Mungu akamwita Adamu, akamwambia uko wapi? Akasema, Nalisikia sauti yako bustanini, nikaogopa kwa kuwa mimi ni uchi :nikajifificha.” Akasema, Ni nani aliyekuambia ya kuwa uchi?
Swali: Ati Mwenyezi Mungu anavunja ahadi zake?
Jibu: Sivyo kabisa. Kuvunja ahadi
ni aibu kubwa. Lakini Biblia katika kitabu cha kwanza cha cha Samweli, Sura ya
2, aya ya 30 na 31, imeandikwa hivi:”Kwa sababu hiyo,Bwana, Mungu wa Israel,
asema, Ni kweli, nalisema ya kuwa nyumba yako, na nyumba ya baba yako itakwenda
mbele zangu milele:lakini sasa Bwana asema, Jambo hili na liwe
mbalinami…Angalia, Siku zinakuja, nitakapoukata mkono wako, na mkono wa mbali
ya baba yako, hata nyumbani mwako hatakuwa mzee.” Mungu yu mbali na uzushi huu
juu yake.
Na vilevile katika sura ya
13,aya 13 imeandikwa hivi: “… Bwana angaliufanya ufalme wako kuwa imara juu ya
Israeli milele. Lakini sasa ufalme wako hautadumu.”
Mungu yu mbali na uzushi huu juu
yake
Swali: Ati upumbavu wa Mungu una hekima zaidi ya
wanadamu?
Jibu: Sivyo Kabisa. Mwenyezi Mungu
si mpumbavu kamwe, basi vipi itakuwa upumbavu wake una hekima zaidi ya
wanadamu: Lakini Biblia katika waraka wa kwanza wa Mtume Paulo kwa Wakorintho,
sura ya kwanza, aya ya 25, imeandikwa hivi:” Kwa sababu upumbavu wa Mungu una
hekima zaidi ya wanadamu.”
Swali: Mwenyezi Mungu hujuta akisha tenda jambo?
Jibu: Sivyo Kabisa. Lakini Biblia katika kitabu
cha kwanza cha Samweli, Sura ya 15, aya
ya 10 na 11, Imeandikwa hivi, “Ndipo neno la Bwana likamjia Samweli, Kusema,
“najuta kwa sababu nimemtawaza Sauli awe Mfalme.”
Swali:
Ati Mwenyezi Mungu husikitika na kuwa na majonzi kwa kitendo alichofanya?
Jibu Sivyo kabisa. Lakini katika Biblia kitabu cha Mwanzo, Sura
ya 6, aya ya 6 na 7, imeandikwa hivi: ‘Bwana akaghairi kwa kuwa amefanya mwanadamu duniani, akahuzunika
moyo. Bwana akasema, Nitamfuatilia mbali mwanadamu niliyemwumba usoni pa nchi.”
Swali: Ati Mwenyezi Mungu hushinda mweleka na mtu?
Jibu: Sivyo kabisa. Lakini Biblia katika kitabu cha Mwanzo, sura ya 32, aya ya 24 na 28, imeandikwa hivi: Yakobo akakaa peke: na mtu mmoja akaashindana naye mweleka hata alfajiri.. Akamwambia, Jina lako hutaitwa tena Yakobo, Ila Israeli, Maana unashindana na Mungu.”
Swali: Ati Mwenyezi Mungu husema uwongo halinyoka
husema kweli?
Jibu: Sivyo Kabisa. Lakini Biblia Katika kitabu cha Mwanzo, sura
ya 3, aya ya 3 hadi ya 6 , imeandikwa hivi:
Lakini matunda ya mti ulio katikati ya bustani Mungu amesema , msiyale
wala msiyaguse, msije mkafa. Nyoka akamwambia mwanamke, Hakika hamtakufa, kwa maana Mungu anajua ya
kwamba siku mtakayokula matunda ya mti huo, mtafumbuliwa macho, nanyi mtakuwa
Baadaye imeelezwa kwamba Adamu
na Hawa baada ya kula matunda ya mti huo, wakawa huko … yameelezwa mambo ambayo
si shani ya Mwenyezi Mungu kuambiwa hivyo.
Swali: Ati Mwenyezi Mungu hushuka kutoka mbinguni ili kuchafua umoja wa
watu ili wasisikilizane kwani anaogopa umoja wao?
Jibu: Sivyo, sivyo kabisa mara elfu. Lakini Biblia katika kitabu cha Mwanza, Sura ya 11, aya ya kwanza hadi 9, imeandikwa hivi:”Nchi yote ilikuwa na na lugha moja na usemi mmoja.
Ikawa watu waliposafiri pande za mashariki waliona nchi tambalale katika nchi ya Shinari: waakakaa huko. Waliambiana, Haya, na tufanye matofali tukayachome moto.
Walikuwa na matofali badala ya mawe, na lami badala ya chokaa. Wakasema, Haya na tujijengee mji, na mnara, na kilele chake kifike mbinguni tujifanye jinaa: ili tusipate kutawanyika usoni pa nchi yote. Bwana akasema, Tazama, watu hawa ni taifa moja, na lugha moja : na haya ndiyo wanayoanza kuyafanya, wala sasa hawatazuiliwa neno
Wanalokusudia kulifanya, Haya, na tushuke huko huko, tuwachafulie usemi wao ili wasisikilizane
maneno
Swali: Ati Mwenyezi Mungu husema kitu baadaye akafanya mengine?
Jibu: Sivyo Kabisa. Lakini Biblia katika kitabu cha Mwanzo, Sura ya 6, aya ya 3, inasemaa hivi: Bwana akasema, Roho yangu haitashindana na wanadamu milele kwa kuwa yeye naye ni nyama: basi siku zake zitakuwa miakaa mia na ishirini.”
Hayo yalikuwa mwanza wa kuumba Binadamu, hebu tutazame, Mungu
alifuata ahadi yake? Biblia inasema Mungu aligeuza maneno yake, Kwa hivyo watu
wengi waliishi juu ya umri alioahidi
Mungu. Kwa mfano, imeandikwa katika Mwanzo, Sura ya tisa, aya ya ishirini nia nne
(mwa
Mitume waalitumwa kufundisha watu wema na
ukweli. Mitume wa Biblia wanasema uwongo.:
Swali: Ati Yesu (Isa a.s) husema uwongo?
Jibu: Sivyo, Kamwe: Lakini katika Biblia, Injil ya Yohana
Mtakatifu, Sura ya 7, aya ya 2-3, Inasema hivi:
Na sikukuu ya Waayahudi, Sikukuu ya vibanda ili kuwaa karibu.
Basi ndugu zake wakamwambia, ondoka hapa, uende hapa, uende Uyahudi, wanafunzi
wako nao wapate kuzitazama kazi zako
unazozifanya. Kwa maana hakuna mtu afanyaaye nena kwa siri, naye mwenyewe ataka kujulikana.
Ukifanya mambo haya, basi jidhi hirishe kwa ulimwengu. Maana ana hata nduguze
hawakumwamini. Basi Yesu akamwambia, Haujaafika
bado wakati wenu siku zote upo.
Ulimwengu hauwezi kuwachukia ninyi: kwa sababu mimi naushuhudia ya kuwa kazi
zake ni mbovu. Kweni ninyi kwenda kula
sikukuu: Mimi si kweli bado kwenda kula sikukuu hii: kwa kuwaa haujatimia
wakati wangu. Naye alipokwisha kuwaambia
hayo, alikaa vibi hivi huko Galiliya.
Hata ndugu zake walipokwisha kuwa kuiendea
sikukuu, ndipo yeye naye alipokwea, si kwa wazi bali kana kwamba kwa siri.
Swali: Ati Yesu (Isa a.s.) hutengeneza
mvinyo, na anaweza kuwanywesha
Masahaba wake?
Jibu: Sivyo,
sivyo kabisa. Lakini katika Biblia
inasema hivyo, na isitoshe hayo inasema kuwa ndio ufunguo wa Utume wake, na
ndicho kitu alichotumia hadi akaaga
dunia:
Usiseme, hivyo huenda ikawa katika madhehebu ya Yesu (Isa a.s) pombe kuwa halali. Naogopa Mungu kwa
masingizio hayo, kwani Agano jipya zinabainisha uharamu wa mvinyo.
Basi
kwanza tueleze wazi amri ya uharamu wa mvinyo
katika Biblia na baadaye tueleza masingizio juu ya Yesu (Isa a.s)
Katika Biblia kitabu cha Hosea, Sura ya
nne, aya 10 na 11 imeandikwa hivi:
Nao watakula, lakini hawatashiba: watafanya
zinaa, lakini hawataongezeka:kwa sababu wameacha kumwangalia Bwana. Uzinzi na
divai na divai mpya huondoa fahamu za wanadamu.
Vile vile katika Isaya sura ya 5 , aya 11
na 12 na 13 li
Nasema hivi:ole wao waamkao asubuhi na
mapema, wapate kufuata kileo, wakishinda sana hata usiku wa manane mpaka mvinyo
umewaka kama moto ndani yao: Na kinubi, na zeze, na matari, na filimbi, na
mvinyo zote ziko katika karamu zao: Lakini hawaiangalii kazi ya Bwana wala
kuyafikiri matendo ya mikono yake. Kwa sababu hiyo watu wangu wamechukuliwa
mateka, kwa kukosa kuwa na maarifa.
Katika kitabu cha kumbukumbu la Torati,
sura 21, aya ya 18-21, inasema hivi: Mtu akiwa na mwana Mkaidi, mshupavu,
asiyetii sauti ya baba yake, wala sauti ya mama yake, nao wajapomwadhibu
hawasikilizi, ndipo babaye na mamaye na wamkamate, na kumpeleka kwa wazee wa
mji wake, katika lango la mahali pake: wawaambie wazee wa mji wake, Huyu mwana
wetu ni mkaidi, mshupavu hasikizi sauti yetu: Ni mwasherati, na tena ni Mlevi
Waume wote wa mji wake na wamtupie mawe, afe: ndivyo utakavyoondoa uovu
katikati yako : na Israeli wate watasikia na kuogopa.
Katika kitabu cha luku, sura ya 7, aya ya
33 na34, Inasema hivi:
Kwa kuwa Yohana Mbatizaji alikuja, hali
mkate wala hanywi divai, nanyi mwasema, Ana pepo. Mwana wa Adamu amekuja, ana
kula na kunywa: nanyi mwasema, Tazama, mlafi huyu, na mnywaji wa divai, rafiki
wao watoza ushuru na wenye dhambi.
Katika kitabu cha Yohana Mtakatifu, sura ya
pili, aya ya 1-11, inasema hivi: Na siku ya tatu palikuwa na arusi huko kana,
mji wa Galilaya: naye mama yake Yesu alikuwapo. Yesu naye alikuwa amealikwa
arusini pomoja na wanafunzi wake. Hata divai ilipowatindikia, mamaye Yesu
akamwambia Mama, tuna nini mimi nawe?
Saa yangu haijawadia. Mamaye akawaambia watumishi, Lolote atakalowaambia,
fanyeni.
Basi kulikuwapo huko mabalasi sita ya
mawe, nayo yamewekwa huko kwa desturi ya
Wayahudi ya kutawadha, kila moja lapata kadiri ya nzio mbili tatu. Yesu
akawambia, Jalizeni mabalasi maji. Nao wakayajaliza hata juu. Akawaambia, Sasa
tokeni mkampeleka. Naye mkuu wa meza alipoyaonja yale
Lakini
watumishi walijua, wale walioyateka yale maji), yule mkuu za meza
alimwiita bwana arusi akamwambia, Kila
mtu kwanza huandaa divai iliyo njema: hata sasa.
Mwanzo huo wa ishara Yesu aliufanya
huko kana ya Galilaya,
akaudhihirisha utukufu wake, nao
wanafunzi wake wakamwamini.
Jambo hili linadhihirisha kwamba kunywa
mvinyo haikuwa inafikiriwa kuwa
mwiko katika dini kwa mujibu wa Agano jipya. Angalia jinsi Isa (Yesu)
alivyotengeneza mvinyo akiwaambia wengine wainywe.
Tukio
lingine:
Katika kitabu cha Luka Mtakatifu, Sura 22,
aya 14-18 inasema hivi: Hata saa ilipofika aliketi chakulani, yeye na wale
miyume (kumi na wawili) pamoja naye. Akawaambia, Nimetamani
Je,
Mtume huzini? Hawezi. Je, Mtume humnywesha mtu mvinyo? Hawezi. Ati Mtume
humdanganya mtu ili amwue? Hawezi.
Lakinu katika Biblia Mtume Daudi (a.s)
amesingiziwa yote haya juu.
Tazama kitabu cha pili cha Samweli, sura
11, aya 2-27, yasema hivi:”Ikawa wakati wa jioni, Daudi akaondoka kitandani,
akatembea juu ya dari ya jumba la Mfalme: na alipokuwa juu ya dari aliona
Mwanamke anaoga: naye huyo Mwanamke alikuwa mzuri
Je, umesikia kisa namna alivyofanya hila ya
kumwua Uria; Na kwamba Daudi alizini na mke wa Uria baadaye akamlewesha ili
apate kulala na mkewe, jambo lisiloridhisha, na kumpeleka Uria vitani kwa hadaa
ili auawe, na wakatenda hata akauwawa?
Basi sasa sikia tokeo la hayo kwa yule
mwanamke mwenye mume aliyezini naye Daudi!
Tazama Injili ya Mateyo, sura 1, aya ya
6-9, inasema hivi: “ Yese akamzaa Mfalme Daudi. Daudi akamzaaa Sulemani kwa
yule mke wa Uria.”
Vile vile tazama kitabu cha pili cha
Samweli, sura 12, aya ya 9, inasema hivi:-
Bwana, Mungu wa Israeli asema hivi:
“Umempiga Uria, Mhiti, kwa upanga, nawe
umemtwaa mkewe awe mke wako?”
Basi sasa sikia iliokuwa ajabu zaidi!
Agano zote mbili za sema kwamba Mwenyezi
Mungu amemjaazi Mtume Daudi kwa kuwasalitisha wanawe juu ya wake zake hata
wakazini nao!
Tazama kitabu cha pili cha Samweli, sura
12, aya 11 na 12, inasema hivi:-
Bwana asema hivi, Angalia, nitakuondokesha
uovu katika nyumba yako, nami nitawatwaa wake zako mbele ya macho yako, na kumpa jirani yako, naye atalala na
wake zako mbele ya jua hili. Maana wewe ulifanya jambo hili kwa siri; bali mimi
nitalifanya jambo hili mbele ya Israili wote na mbele ya jua.
Tena tazama sura16, aya 22, inasema hivi”-
Basi wakamtandikia Absalomu hema juu ya
nyumba darini; naye Absalomu akaingia kwa masuria ya babaye machoni pa Israeli
wote.
Biblia haitoshelezi kusingizia kuwa licha ya kutenda uzinzi wa kawaida, Mtume alizini pia na binti zake
Swali: Je,
Mtume anaweza kuzini na binti zake au kulewa divai?
Jibu:
Haiwezekani kamwe mambo hayo,
yote ni masingizio tu. Kwani
mwenye akili
yeyote hawezi kufanya mambo
Basi tazama Biblia kitabu cha kwanza, sura
ya 19, aya ya 30-38, inasema hivi: lutu akapanda kutoka Soari akakaa mlimani na
binti zake wawili. Yule mkubwa akamwambia mdogo, Baba yetu ni mzee, wala hakuna
mtu mume katika nchi atuingilie
Baba yetu uzao. Wakamnywesha baba
Je, wadhani kuwa Mtume aweza kudanganya? Au
kumbusu mwanamke mgeni? Au wadhani Mwenyezi Mungu huweza kupigana mieleka na
Mtume Wake, na wala Asiwe Kumshinda?
Swali:
Ati inawezekana Mtume ambusu mwanamke asiyemhusu?
Jibu:
Mambo haya hafanyi mwenye akili yeyote sembuse Mtume wa Mungu.
Swali:
Ati Mtume hushindana mweleka na Mungu?
Jibu: Sivyo kabisa, kwani Mwenyezi
Mungu hana kiwiliwili hata mtu ashindana mweleka naye.
Swali:
Ati Mtume hudanganya?
Jibu:
Kudanganya ni aibu na Mtume amekamilishwa na Mwenyezi Mungu.
Lakini katika Biblia yote hayo
wamesingiziwa. Tazama kitabu cha Mwanzo, sura 29, aya 11, inasema hivi:
Yakobu akambusu Raheli, akainua sauti yake
akalia. Huyu Raheli akaolewa na huyu Yakobu baada ya miaka saba.
Vile vile tazama sura ya 32, aya ya 24-30
inasema hivi: Yakobu akakaa peke yake; na mtu mmoja akashindana naye mweleka
hata alfajiri…akamwambia, jina
Akambariki huko. Yakobu akapata mahali
pale, penueli, maana alisema, Nimeonana na Mungu uso ka uso na nafsi yangu
imeokoka.
Vilevile tazama sura27, aya1-35 inaseama
hivi: Ikawa Iseka alipokewa mzoe, na macho yake yamepofuka asione, akamwita
Esau mwanawe mkubwa, akamwambia, Mwanangu…. Basi, nakuomba chukua mata yako,
podo lako
Na upinde wako, ukaende nyikani uniwindie
mawindo; ukanifanyie chakula kitamu namna ile niipendayo, ukiniletea, ili nile;
na roho yangu ikubariki, kabla sijafa. Na Rabeka akasikia, Isaka aliposema na
Esau mwanawe… Kisha Rebeka akatwaa mavazi mazuri ya Esau mwana mkubwa,
aliyokuwa nayo nyumbani, akamvika Yakobu mwanawe mdogo… Akaja kwa baba yake,
akasema, Babangu. Akasema, mimi hapa, Unani
wewe mwanangu Yakobu akamwambia babaye, Mimi ni Esau, mzaliwa wako wa
kwanza nimefanya
Akakaribia akambusu. Naye akasikia harufu
ya mavazi yake, akambariki akasema… Ikawa Isaka alipokwisha kumbariki Yakobo
ndiyo kwanza ametoka mbele ya Isaka baba yake, mara Esau ndugu yake akaja
kutika katika kuwinda kwake … Isaka, baba yake, akamwuliza, U nani wewe?
Akasema, Mmi ni mwanao, Esau, mzaliwa wako wa kwanza.Isaka akatetemeka tetemeko
kuu
Ni ajabu mno na masingizio kwa Mtume
kumbusu mwanamke, na kuhadaa , au kushindana mweleka na Mingu na kuchukua utume
kwa nguvu na hadaa! Yaweza kuwa hayo ni kweli?
Jibu: Haimkiniki kamwe hivyo.
Swali: Je, inawezekana Mtu ajenge nyumba ya
kuabudia masanamu?
Jibu: Kabisa haiwezekani Mtume yeyote kufanya
hivyo.
Swali: Ati inamkinika moyo wa Mtume upotoke na
Mwenyezi Mungu?
Jibu: Haiwezekani Kamwe!
LAKINI:
Biblia katika kitabu cha Wafalme,Sura 11 , aya za kwanza inasema hivi:
Mfalme Suleman akawapenda wanawake wengi
wageni, pamoja na binti yake Farao… Na wa mataifa Bwana aliyowaambia wana wa
Israeli, Msiingie kwenu: kwa kuwa hakika wataigeuza mioyo yenu kuifuata miungu
Maana Ikawa, Suleimani alipokuwa mzee, wake
zake wakamgeuza moyo wake , afuate miungu mingine wala moyo wake haukuwa
mkamilifu kwa Bwanba, Mungu wake ,
Kwa kuwa Sulemani akamfuata Ashtorethi,
Mungu wa Wasidoni, na Milkomu, chukizo la waamoni. Sulemani akafanya yaliyo
mabaya machoni pa Bwana, wala hakumfumfuata Bwana kwa utimilifu,
Basi Bwana akamghadhibikia Sulemani kwa
sababu moyo wake umegeuka, naye amemwacha Bwana, Mungu wa Israeli, aliyemtokea
mara mbili, akamwamuru katika habari ya jambo lilo hilo asifuate miungu
mingine: lakini yeye hakuyashika aliyoyaamuru Bwana.
Je , umepata kusikia chuki baina ya Mwenyezi Mungu na Mtume Wake? Je, umepata kusikia kuwa Mtume ni dhalimu? La sivyo , basi soma haya:
Swali: Ati inamkinika iwe chuki
na uaduwi kati ya Mwenyezi Mungu
na Mtume wake hadi atake kumuua
Jibu:
Haimkiniki kamwe;
LAKINI: Biblia katika Agano jipya na
Agano la kale inasema
kiitwaacho KUTOKA, sura ya 4, aya mbali
mbali: Bwana akamwamia Musa, hapo utakaporudi Misri, angalia ukazifanye mbele
ya Farao zile ajabu zote nilizo-zitia
mkononi mwako.
Swali:
Je , inawezekana Mtume awe dhalimu na kuamrisha wauawe watoto na
mengineyo
Jibu: Mtume hawezi kuwa hivyo wala hawezi kamwe kutenda dhuluma.
Lakini Biblia katika Agono jipya na
Agono la kale husema
Tazama kitabu cha nne cha Musa, kiitwacho HESABU sura ya 31 aya mbalimbali:
Wana wa Israeli wakawachukua mateka
wanawake wa Midiani na watoto wao: na ngonbe zao wote na
Ukagawanye nyara mafungu mawili: Kati ya watu waliozoea vita, waliotoka nje
waende vitandani . . . wanadamu jumla
Basi sasa na tuulize idadi gani
waliangamizwa kwa kuona haram na uchungu? Bila ya shaka ni zaidi kuliko
waliowachwa hai !!
Kwa hivyo inatubidi tushukuru hiyo huruma na msamaha kwa kuwekwa hai watoto wa kike ambao hawakumjua mume kwa kulala pamoja naye: ijapokuwa tumeshajua kwamba (agano zote mbili) imesema katika kisa kingine ameuuwaua watu wote hata hawo watoto wa kike bikira?(Tazama kumbukumbu la Torati , sura 2 , kuanzia aya 31). Kisha Bwana akaniambia Tazama nimeanza kumtoa sihoni na nchi yake mbele yako: anza kuimiliki, upate kuirithi nchi yake. Ndipo Sihoni alipotutokea juu yetu, yeye na watu wake wote, kupigana huko Yahasa. Bwana, Mungu wetu, akamtoa mbele yetu, tukampiga yeye na wanawe, na watu wake wote. Tukatwaa miji yake yote wakati hou, tukaharibu kabisa kila mji uliokuwa na watu, pamoja na wanawake na wadogo :tusimsaze hata mmoja :ila ngombe zao tuliwatazama kuwa mawindo yetu, pamoja na nyara za miji tuliyoitwaa.
Agano zote mbili
ina haki ya kusema, kwa nini mnanilipizia kisasi? Kwa nini mimi ndio naliomsingizia Mtume Musa
kuwauwa watu waume, wake na watoto? Kwani hamwangalii vipi amesingiziwa
Mwenyezi Mungu, kwa kuwaamrisha wauwawe kila chenye roho hata wanyama? (tazama
kumbukumbu la Torati, sura 20, kuanzia aya 13) Na Bwana, Mungu wako, autiapo
mkononi mwako, mpige kila mume aliyemo kwa makali ya upanga: Lakini wanawake na watoto, na vilivyo mjini
vyote, navyo ni nyara zake zote ,
uvitwae viwe mateka kwako: Nawe utakula nyara za adui zako alizokupa Bwana
Mungu wako. Utaifanyia vivyo miji yote iliyo mbali
Swali:
je, inawezekana Mtume awe mkali anapozungumza na Mwenyezi Mungu na
kumtaka amfutiliye mbali katika Utume?
Jibu:
Haiwezekani kamwe: Lakini Biblia
katika kitabu cha pili cha Musa kiitwacho
KUTOKA sura 32, kuanzia aya 31 linasema hivi: Musa akarejea kwa Bwana,
akasema Aa ‘ watu hawa wametenda dhambi kuu , wamejifanyia miungu ya dhahabu.
Walakini sasa, ikiwa utawasamehe dhambi
Swali: Je, inawezekana Mwenyezi
Mungu amuamrishe Mtume wake atembee uchi kati ya watu kwa miaka na kwa nini?
Kwa ajili ya ubarudhuli kwa ilhani yeye ni wa kupigwa mifano?
Jibu: Haiwezekani kamwe kwa Mwenyezi Mungu
kuamrisha hivyo, kwa sababu Mwenyezi Mungu Anakataza kukaa uchi mbele ya watu!
Hii ni mambo ya kiwendawazimu lakini Biblia katika kitabu cha Nabii Isaya, sura
ya 20 aya ya pili hadi mwisho wa aya ya nne inasema hivi:
Wakati huo Bwana alinena kwa kinywa cha Isaya, mwana wa amozi, akisema, Haya, uvue nguu ya magunia viunoni mwako, na viatu vyako migu
Uni mwako. Naye akafanya hivyo akaenda
uchi, miguu yake haina viatu. Bwana akasema, kama vile mtumishi wangu Isaya
anavyokwenda uchi, hana viatu, awe ishara na ajabu kwa muda wa miaka mitatu juu
ya Misri na juu ya kushi:vivyo hivyo Mfalme wa Ashuru atawachukua uchi,
wafungwa wa Misri, na watu wa kushi waliohamishwa, watoto kwa wazee, hawana
viatu, matako yao wazi Misri iaibishwe.
Swali:
Ati inawezekana Mtume asisadiki Maneno ya Mwenyezi Mungu hadi akamtaka
thibitisho la ukweli wa maneno yake?
Jibu: Hasha Mtume kuwa na shaka juu ya maneno ya
Mwenyezi Mungu hata atake ushahidi!
Lakini agano mbili zamsingizia Mtume
Ibrahim kwa hayo! Tazama kitabu cha kwa kwanza cha Musa, kiitwacho, Mwanza,
sura ya 15 aya ya kwanza na ya saba, inasema hivi:
Baada ya mambo likamjia Abramu katika
njozi, likinena . . . . . .Mimi ni Bwana, niliyekuleta kutoka Uru wa Wakaldayo
nikupe nchi hii ili urithi. Akasema, Ee bwana Mungu, ni pateje kujua ya kwamba
nita Rithi? Akamwambia, Unipatie ndama wa miaka mitatu: na mbuzi mke wa miaka
mitatu, na hua na mwana njiwa Akampatia hao wote, akaweka kila kipande kuelekea
mwenzake, ila ndege hakuwapasua Hata tai walipotua juu ya mizoga Abramu
akawafukuza. Basi tazama vipi hivi? Kuna uhusiano gani kati ya maneno ya mbele
na baadaye. Naam (Agano) husimulia kisa namna hivyo ya kurukaruka na kutinga
haina uhusiano na mwenziwe.
Sasa, Mungu wa
Biblia anamwamuru Mtume mmoja kula mkate uliochanganywa na mavi ya mtu. Ubora
wa mafundisho haya ni upi?
Swali:
Ati Mwenyezi Mungu humuamrisha Mtume wake ale mkate uliokandwa na mavi
ya binadamu? Kwa nini hivyo kuamrishwa?
Jibu:
Haiwezekani kamwe Mola kamuamrisha Mtume wake hivyo!
Lakini Biblia inasema hivyo! Tazama kitabu
cha Nabii Ezekieli, sura ya 4, aya ya 12 inasema hivi:
Nawe (Ezekieli) utakila
Lakini Nabii Ezekieli alikuwa mwenye akili
. . . atakula vipi mkate uliokandwa na
mavi ya binadamu? Akataka msamaha kwa jambo hili la kuchekesha na Mwenyezi
Mungu alimkubalia na akatukuka na akabadilishiwa mavi ya binadamu kwa mavi ya
ngombe.
Na
katika sura hiyo hiyo, aya ya 14 na 15 , inasema hivi: Ndipo nikasema, Ee Bwana
Mungu, tazama roho yangu haikutiwa unajisi: maana tangu ujana waangu hata sasa
sijala nyamafu, wala nyama ichukizayo haikuingia kinywani mwangu. Ndipo
akaniambia, Tazama, nimekupa mashonde ya ngombe badala ya mashonde ya
mwanadamu, nawe utakipika chakula chako juu ya hayo.
Swali: Ati Mwenyezi Mungu humuamrisha
Mtume wake kunyoa kichwa chake na ndevu zake? Kwa nini hivyo? Kwa jambo la
upuzi tu! Lakini masikini Nabii Ezekieli
alifikiwa na mambo ya kuchekesha. Akawa anakula mavi ya ngombe baada ya
kuhurumiwa na
Nawe,
mwanadamu ujipatie upanga mkali,
Baadaye inaonyesha makusudi ya kutoa mfano
huo ni kuwajulisha kwamba, theluthi ya watu wa Orshibna watakufa kwa tauni, na
kwa njaa watakomeshwa, na theluthi watakomeshwa, kwa upanga, na theluthi
atawatawanya kwa upepo. Tazama mifano na wakatolewa mifino!
Angalia mfano huu na mwenye kufanyika kwake
mfano huo.
Swali: Ati inapendeza
kwa Mwenyezi Mungu amkufishe mke wa Mtume kwa ajili ya kuonyesha mfano ya
kijinga kwa ilhali ingewezekana kueleza kwa maneno tu?
Jibu: Ndio…
Mtume Ezekieli alipatwa na masaibu mawili (katika agano zote mbili) na akawa
mifano ya kiupuzi, bila shaka si halali kwa Mwenyezi Mungu na Mitume wake na
mambo
Neno la Bwana likanijia tena, kusema,
Mwanadamu, tazama, ninakuondolea kwa pigo moja tunu, mteule wa macho yako mke
wako) wa lakini hutaomboleza wala yasiohuruzike machozi yako. Ugua, lakini
si kwa sauti ya kusikiwa:usifanye
matanga kwa ajili yake
Yeye aliyekufa: jipige kilemba chako,
ukavae viatu vyako, wala usile chakula cha watu. Basi nalisema na watu asubuhi: Na jioni mke wangu akafa: nami nalifanya
asubuhi
Iwapo hayo hayatoshi, angalia jinsi Mwenyezi
Mungu anavyomwamuru Mtuma mmoja
kutwaa mwanamke na kuzini naye.
Na
baada Mtume Ezekieli agano zote mbili inamlenga mishale za mifano za upuzi
kumkusudia Mtume Hosea.
Basi natuulize.
Swali:
Ati inaelekea kwamba amuamrishe Mtume wake akatwae na kumwoa mke wa
uzinzi, na watoto wa uzinzi? Na kwa nini? Kwa sababu nchi ilifanya uzinzi, kwa
kumwacha Bwana. Au ilikuwa onyo na mawaidha kwa nyumba ya Israeli kwa kuwataja
majina ya watoto aliwazaa yule mwanamke, na kutaja vipi alizini?
Jibu: Hasha!
Mwenyezi Mungu kamwe hakumuamrisha
Mtume wake yeyote kufanya hivyo. Lakini
Biblia katika kitabu cha Mtume Hosea sura ya kwanza, toka aya ya pili hadi
mwisho wa aya ya nne, inasema:
Hapo kwanza Bwana aliponena kwa kinywa cha
Hosea, E nenda ukatwae mke wa uzinzi: kwa maana nchi hii inafanya uzinzi, na
watoto wa uzinzi: Kwa maana nchi hii inafanya uzinzi mwingi, kwa kumwacha Bwana. Basi akaenda akamwoa Gomeri, binti Didlaimu:naye akachukua mimba,
akamzalia mtoto mwanamume. Bwana akamwambia, Mwite jina
Damu ya Yezreeli, na kuukomesha ufalme wa
nyumba ya Israeli.
Msihini mama yenu, msihini; kwa maana yeye
si mke wangu, wala mimi si mume wake; na ayawekee mbali mambo ya uasherati wake
yasiwe mbele ya uso wake, na mambo ya uzinzi wake yasiwe kati ya maziwa yake;
nisije nikamvua nguo zake akawa uchi, nikamweka katika hali aliyokuwa nayo siku
ya kuzaliwa kwake, na kumfanya kama jangwa, na kumweka kama nchi kame. Na
kumfisha kwa kiu; naam , sitawaonea rehema watoto wake: kwa maana ni watoto wa
uzinzi. Maana mama
Na katika sura ya pili, aya ya pili
inaeleza hivi:
Bwana akanwambia, E nenda tena, mpande
mwamanke apendavye na rafiki yake, naye ni mzini;
Ingawa wanaigeukia miungu mingine, na
kupenda mikte ya zabibu kavu. Basi nikajinunulia mwanamke huyo kwa vipande kumi
na vitano vya fedha, na homeri moja ya shayiri, na nusu ya homeri ya shayiri;
nami nikamwambia, utatawa kwa ajili yangu siku nyingi; hutafanya mambo ya
ukahaba, wala ingawa wanaigeukia miungu
mingine, na kupenda mikte ya zabibu kavu. Basi nikajinunulia mwanamke huyo kwa
vipande kumi na vitano vya fedha, na homeri moja ya shayiri, na nusu ya homeri
ya shayiri; nami nikamwambia, utatawa kwa ajili yangu siku nyingi; hutafanya
mambo ya ukahaba, wala
hutakuwa mke wa mtu awaye yote; nami
nitakuwa hali iyo hiyo kwa ajili yako. Kwa maana wana wa Israeli watakaa siku
nyingi bila mfalme , wala mtu mkuu.
Kisa
kama hii ambao ni hasara kuandikwa vitabuni licha kuandikwa katika kitabu
(tukufu). Na ikiwa Mtume hafanyi hivyo
basi nini itakuwa kwa watu wengine?
Namikiwa mkubwa wa nyumba anapenda jambo
Fulani baya, basi hakuna shaka watu wa nyumbani wote wataingia katika maovu
yote Isitoshe hayo ampende mwanamke apaendwaye na rafiki naye ni mzini
Biblia Yapaswa ufundisha upweke wake Mwenyezi
Mungu. Lakini Mtume wake huabudu miungu! Je, hiki si kinyume?
Swali: Je
inamkinika Mtume kutengenza masanamu nakuwapoteza watu kwa kuabudu masanamu?
Jibu:
Haiwezekani kamwe kwani kuabudu masanamu ni
kazi ya makafiri na mushriki na Mwenyezi Mungu hapendezwi na hayo kabisa.
Lakini Biblia katika kitabu cha pili cha Musa, kiitwacho kutoka, sura ya 2
kuanzia aya ya kwanza hadi mwisho wa aya ya sita, inasema:
Hata
watu walipoona ya kuwa Musa amekawia kushuka katika mlima, wakakusanyana
wakamwendea Haruni, wakamwambia, Haya! Katufanyizie miungu itakayokwenda mbele
yetu, kwa maana Musa huyo aliyetutoa
katika nchi ya Misri hatujui yaliyompata. Haruni akawaambia, Zivunjeni pete za
dhahabu zilizo katika masikio ya wake zenu, mkaniletee. Watu wote wakazivunja
pete za dhahabu zilizo katika masikio
Swali: Ati Mwenyezi Mungu hufanya
hasira? Au Mungu kubishana na Mtume wake
na baadaye akajuta?
Jibu: Hasira na
kutetana si jambo zuri kabisa kwa hivyo haiwezekani kamwe Mwenyezi Mungu atende
tena na Mtume wake Mtukufu!
Lakini Biblie inaedelea kusema,kutoka aya ya 10,hadi mwisho wa aya ya
14:
Basi
sasa niache ili harisa zangu ziwake juu
Geuka katika hasira yako kali, ughairi uovu
huu ulio nao juu ya watu wako . . . .Na Bwana akaughairi ule uovu alisema ya
kwamba atawatenda watu wake.
Je,
aweza Mtume kuwa mwana wa haramu? Biblia inasema Sivyo Biblia inasema “Ndivyo!
Swali;
Je, aweza Mtume kuwa mwana wa haramu au mwana wa mwanamke kahaba?
Jibu: Hawezi kuwa kamwe. Kwa sababu
kuzaliwa haramu ni ‘aibu’ kwa mwana: Kunamwadhili mwana wa haramu machoni na
myoyonimwa watu.
Hivyo watu hawawezi kumsikiliza
wala kupokea maneno yake. Kwa vile jambo hili halilingani na kusudio la utume,
Mwenyezi Mungu hakutuma mtu yeyote wa aina hiyo akawa Mtume.
BIBLIA: Vile vile inasema wazi wazi
katika kumbukumbubu la Torati, 23:2,
‘Mwana wa haramu asiingie katika mkutano wa Bwana: Hata kizazi cha kumi
asiingie aliye wake katika mkutano wa Bwana.”
Kwa
hiyo, Mtume hawezi kuwa ‘mwana wa haramu.’
LAKINI: Biblia yenyewe hiyo inasema
kwamba baadhi ya Mitume walikuwa wana wa haramu!
(1)
Waamuzi, sura ya 11:1, inasema: Basi huyo Yeftha, Mgileadi, alikuwa mtu
shujaa
Na halafu inasema katika sura hiyo hiyo ,
aya ya 29, ‘Ndipo roho wa Bwana akamjilia juu yake Yeftha.’Hii ina maana kwamba
alikuwa Mtume!
(2) Mwanzo, 38:6-30, Yuda akamwoza mke ni Tamari. Naye Eri, mzaliwa wa kwanzawa
Yuda, alikuwa mbaya machoni pa Bwana: Na Bwana akamvua. Yuda akamwambia O nani,
Uingie kwa mke wa nani, Uingie kwa mke wa nduguyo, ukamwoe, ukamwinulie nduguyo
uzao. Onani
Alijua ya kwamba huo uzao hautakuwa wake,
ikawa, alipoingia kwa mke wa nduguye, akamwangalia chini asipe nduguye uzao.
Neno hili alilolifanya likawa baya machoni pa Bwana, basi akamwua yeye naye.
Yuda akmwambia Tamari mkwewe, Ukae mjane
nyumbani mwa baba yako hata shela
mwanangu atakapokuwa mtu mzima, maana alisema, asipate kufa yeye
Huyo Tamari akapewa habari, kusema, Mkweo anakwenda Timna . . . , akakaa mlangoni pa Enaumu,
Karibu na njia ya kuenda Timna. Yuda alipomwona alimdhania kuwa ni kahaba,
maana amejifunika uso. Akakaa mlangoni
pa Enaumu, karibu na njia ya kuendea Timna. Yuda alipomwona alimdhania kuwa ni
kahaba, maana amejifunika uso. Akamgeukia kando ya njia, akisema, Niruhusu
niingie kwako. Maana hakujua ya, kuwa ni mkwewe. Akamwuliza, utanipa nini?
Ukiingia kwangu? . . . . Basi akampa,
akaingiake, naye akapata mimba mitatu Yuda akapewa habari kwamba, Mkweo, Tamari
amefanya uzinifu, naye ana mimba ya haramu. Ikawa, wakati wake wa kuzaa
walikuwapo mapacha tumboni mwake . . . . kwa jina lake likaitwa Peresi. Akatoka
Ndugu yake baadaye, . . naye akaitwa jina
Na huyu Peresi ni babu yake Daudi kama
ilivyoelezwa wazi katika Biblia, kitabu cha Mambo ya Nyakati cha kwanza, sura
ya 2, aya ya 5, imeandikwa nasaba ya Daudi mwana wa Yese mwana wa Obedi mwana
wa salmoni mwana wa Nashoni mwana wa Aminadabu mwana wa Ramu mwana wa Hesroni
mwana wa Peresi.
Kwa hiyo, Daudi alikuwa Nabii na alikuwa
katika kizazi cha kumi asiingie aliye wake katika mkutano wa Bwana!!!”
(3)
Samue 11; sura 12;24, inasem;
Naye Daudi akamfariji Bath-sheba mkewe, akaingia kwake. Akalala naye; naye
akazaa mwana, akamwita jina
Kwa hivyo, Mtume Sulemani alikuwa mwana wa
Beth-
Na katika Samuel 11, Sura 11: 2- 27, yasema
hivi: Ikawa wakati wa jioni, Daudi akaondoka kitandani, akatembea juu ya dari
ya jumba la Mfalme: na alipokuwa juu ya dari aliona mwanamke anaoga: naye huyo
mwanamke alikuwa mzuri
Na kumpeleka Uria vitandani kwa hadaa ili
auawe, na wakatenda hata akauawa?
Tazama, Biblia inaonyesha utakatifu gani wa
Daudi na Beth-
(4)
Sasa tazameni kwamba Biblia inamsingizia. Yesu pia kutokana na Peresi
ambaye ni mwana wa haramu!
TAZAMA: Injili ya Mathayo Mtakatifu, sura 1, aya ya 1-16, yasema hivi: Kitabu
cha ukoo wa Yesu Kristo. Mwana wa Ibrahimu. Ibrahimu alimzaa Isaka, Isaka
akamzaa Yakobo , Yakobo akamzaa Yuda na ndugu zake; Yuda akamzaa Peresi na Zera
kwa Tamari: Peresi akamzaa Esromu; . . . . . . Yakobo akamzaa Yusufu mumewe
Mariamu aliyemzaa Yesu aitwaye Kristo.
Swali: Je, inamkinika Mweneyezi Mungu amuamrishe Mtume wake atengeze utepe
au nira na ajivike shingoni kwa nini? Kwa jambo la upuzi kwa ilhali yeye ni
mfano mzuuri.
Jibu:
Haiwezekani kamwe Mwenyezi Mungu kuamrisha hivyo. Lakini Biblia katika kitabu cha Nabii
Yeremia, sura ya 27, aya 1 hadi mwisho
wa aya ya nane inasema hivi:-
Swali: Ati Mtume
hunywa mvinyo na kulewa hadi akawa hoikuvua nguo na kuwa uchi?
Jibu: Haiwezekani
kamwe kufanya mambo yaliyokatazwa na Mwenyezi Mungu, wala mwenye akili yeyote
hawezi kufanya mambo
Lakini (agano zote mbili) BiIlia
inamsingizia Mtume Nuhu hayo, basi tazama kitabu cha kwanza cha Musa, kiitwacho
“Mwanzo” sura ya tisa, aya ya 20 inasema hivi:-
Neno hili likamjia Yeremia, kutoka kwa
Bwana, kusema, Bwana ameniambia hivi, Jifanyizie vifungo na nira, ukajivike
shingoni; ….. Naitakuwa, taifa lile na mfalme yule asiyetaka Nebukadneze, huyo
mfalme wa Babelia, na kutia shingo zao katika nira ya mfalme wa Babeli, mimi
nitaliadhibu taifa lile kwa upanga, na kwa njaa na kwa tauni.
Nuhu akaanza kuwa mkulima, akapanda
mizabibu, akanywa divai, akalewa; akawa uchi katika hema yake. Hamu, baba wa kanaani, akauona uchi wa baba
yake, akawaeleza ndugu zake wawili waliokuwa nje.
Swali: Ati Mtume husema uwongo?
Akamwambia,
karibu kwangu nyumbani, ule chakula. Naye akamwambia, siwezi kurudi pamoja
nawe, wala kuingia pamoja nawe; wala sili chakula wala simywi maji pamoja nawe;
kwani nimeambiwa kwa neno la Bwana, usile chakula wala usinywe maji huko, wala
usirudi kwa njia ile ulioijia. Akamwambia, Mimi nami ni Nabii kama wewe na
malaika akaniambia kwa neno la Bwana, husema, mrudishe pamoja nawe nyumbani
kwako, ale chakula, akanywe maji. Lakini alisema uongo.
Jibu:
Hasha! Mtume hasemi uwongo kamwe kwani Mtume akiwa mwongo atamsadiki
nani na kufuata dini yake?
Lakini kwa bahati mbaya Bilia inamsingizia
hivyo Mtume mmoja. Tazama kitabu cha
kwanza cha Wafalme, sura ya kumi na tatu, kutoka aya 11 hadi mwisho wa aya 19,
inasema hivi:-
Basi Nabii mmoja mzee alikuwa akikaa katika
Betheli; akamfuata Mtume wa Mungu, akamkuta ameketi chini ya mwaloni,
akamwambia, Je! Wewe ndiwe yule Mtume wa Mungu aliyetoka katika yuda?
Akamwambia, Mimi ndiye.
Swali: Ati
inamkinika Mtume atoe habari kwa ilhali yeye anafahamu kwamba ni
uwongo tu?
Jibu:
Haiwezekani kamwe Mtume kueleza jambo ambayo yeye anajua kwamba ni uongo
mtupu.
Lakini Biblia linamsingizia hivyo, tazama
kitabu cha pili cha Wafalme, sura ya 8, kutoka aya 7 hadi mwisho wa aya 15,
inasema hivi;
Kisha, Elisha akaenda dameski; na
Ben-hadadi, mfalme wa Shamu, alikuwa hawezi; akamambiwa ya kwamba, yule Mtu wa
Mungu ame fika. hapo. Mfalme akamwambia Hazeli, chukua zawadi mkononi mwako,
ukaende ili kumlaki yule mtu wa Mungu, ukamulize bwana kwa kimwachake, kusema,
je! Nitapona ugonjwa huu? Basi Hazaeli akaenda kumlaki, akachukua zawadi
mkononi mwake, zakila kitu chema kilichopatikana Dameski, kiasi cha mzigo ya
ngamia arobaini, akaenda akasimsimama mbele yake, akasema, Mwana wako
Ben-hadadi, mfalme wa sham, amenituma kwako, kusema, je! Nitapona ugonjwa
huu? Elisha akamwambia, E nenda
ukamwambie, bila shaka utapona; lakini Bwana umenionyesha ya kwamba Bila shaka
atakufa …… akarudi kwa bwana wake; naye akamwambia, Elisha alikwambiaje?
Akajibu, aliniambia kuwa bila shaka utapona ikawa siku ya pili yake akatwaa
tandiko la kitanda, akali chovya katika maji, akali tangaza juu ya uso wake,
hata akafa. Na Hazaeli akatawala badala yake.
KATIKA KITABU HIKI
1.
Kuhusu Mwenyezi Mungu
Jinsi Biblia inavyozungumzia kuhusu
Mwenyezi Mungu. Kiasi gani Biblia imetopewa kwa maovu na uwongo kuhusu Mwenyezi
Mungu aliyeumba Ulimwengu? Biblia anasema yasiyofaa juu ya Utukufu wa Mwenyezi
Mungu.
2.
Kuhusu Mitume
Mambo gani ambayo Agano jipya na Agano la
kale yameongopwa kuhusu Mitume wa Mwenyezi Mungu ? Mambo ambayo hayafai hata
kwa duni lichaa ya Mitume wa Mwenyezi Mungu, waliokuwa watukufu zaidi kuliko
binadamu wote. Mitume hao hawakutumwa
ila kuongoza, kutakasa na kutenda mema.
Lakini angalia jinsi Mitume hao walivyosimuliwa katika Biblia.