DHAMBI KUU LA KUTOKULIPA ZAKA, KHUMS NA SADAQAH

 

YALIYOMO

UTANGULIZI.. 3

1.  KUTOKULIPA ZAKA.... 4

2.  ASIYELIPA ZAKA NI KAFIRI... 7

3.  SABABU ZA KUFARADHISHWA KWA ZAKA. 9

4.  ZAKA NA SADAQAH HUONGEZA NEEMA.. 10

5.  AINA ZA ZAKA NA VIWANGO VYAKE.. 14

1.  zaka ya mali..... 15

(A).  ZAKA KATIKA WANYAMA. 15

(i)       VIWANGO  VITANO YA KONDOO NA MBUZI..... 15

(ii)       VIWANGO  VIWILI  VYA NG’OMBE..... 15

(iii)      VIWANGO  12  VYA NGAMIA. 15

(B).  VIWANGO 2 VYA DHAHABU NA FEDHA.. 16

1)        VIWANGO 2 VYA  FEDHA.. 16

2)        VIWANGO 2 VYA  DHAHABU.. 16

2.  ZAKAT-I-FITRAH... 17

6.  MATUMIZI YA ZAKA. 18

7.  ZAKA ZILIZO SUNNAH.... 19

8.  KUSALI SALA ZA MAREHEMU NI LAZIMA. 19

9.  KHUMS.... 20

1. KUONGEZEKA KWA NEEMA NA KUTOHARISHA MALI....... 20

2. KHUMS ILIYOFARADHISHWA, AINA NA MATUMIZI YAKE....... 21

10.  SADAQAH   NA   MISAADA:... 24

WANANYUMBA WANAOSTAHIKI MALIPO. 24

1.       SADAQAH ZILIZO SUNNAH. 24

2.       ZAWADI.... 24

3.       UGENI NA UKARIMU.... 24

4.  HAKI ILIYO MAALUMU NA ISIYO MAALUM..... 25

 

 

 

 

 

 

The .HTML version of this book is taken from
www.al-islam.org and ebooked by www.ShiaLibrary.com and www.islamkutuphanesi.com . May Allah be pleased with all.

 

 

 

Kimeandikwa na

SYED DASTAGHIB SHIRAZI

 

 

Kimetarjumiwa na kuhaririwa  na

AMIRALY  M. H. DATOO

BUKOBA - TANZANIA

 

 

 

 


UTANGULIZI

 

 

Hapa nitapenda kuzungumzia machache kuhusu sadaqah

 

 

 

 


1.  KUTOKULIPA ZAKA

Katika Madhambi makuu, dhambi la thelathini na saba ni kule kutokulipa Zaka zilizofaradhishwa na kama vile ilivyoelezwa katika Sahifa ya ‘Abdul ‘Adhim kwamba Maimamu Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s., Imam Musa al-Kadhim a.s. na Al Imam Muhammad at-Taqi a.s. wamesema kuwa hili ni dhambi kubwa kabisa kwani amesema Allah swt katika Quran: Surah al –Tawba

h, Ayah 34 – 35 :

Siku (mali yao) yatakapotiwa moto katika moto wa Jahannam , na kwa hayo vikachomwa vipaji vya nyuso zao na mbavu zao na migongo yao, “Haya ndiyo (yale mali) mliojilimbikia nafsi zenu, basi onjeni (adhabu ya ) yale mliyokuwa mkikusanya.”

 

Imeelezwa katika riwaya kuwa neno lililotumika katika Ayah hii kanz inamaanisha mali yoyote ile ambamo Zaka na haki zinginezo zilizofaradhishwa hazijatolewa.

 

Vile vile Amesema Allah swt katika Qur'an Tukufu, Surah Ali-Imran, 3 , Ayah 180 :

Wala wasione wale ambao wanafanya ubakhili katika yale aliyowapa Allah swt katika fadhila Zake kuwa ni bora kwao. La ni vibaya kwao. Watafungwa kongwa za yale waliyoyafanyia ubakhili – Siku ya Qiyamah.

 

Yaaani wale ambao wanamiliki mali kwa kipindi kifupi tu ambayo hatimaye watakufa na hakuna shaka kuwa hakuna kitakachobakia kingine isipokuwa Ufalme wa Allah swt. Hivyo inatubidi sisi tutumie mali hii vyema iwezekanavyo katika njia ya kutuletea baraka na uokovu Siku ya Qiyamah, kabla mali hii haijatutoka na tukaiacha humu humu duniani. Imeandikwa katika Minhaj-us-Sadiqiin kuwa imeelezwa katika Hadith kuwa :

‘Yeyote yule aliyebarikiwa na Allah swt kwa mali na utajiri, lakini kwa sababu za ubakhili wake hakutoa Zaka na malipo mengine yaliyofaradhishwa kwake, basi Siku ya Qiyamah mali hiyo itatokezea kwake katika sura ya nyoka, ambaye atakuwa mwenye sumu kali kwani hatakuwa na unywele wowote juu ya kichwa chake na atakuwa na alama mbili za rangi nyeusi chini ya macho yake na hii ndiyo dalili ya kutambulisha kuwa nyoka huyo ni mkali sana na hatarikabis. Basi nyoka huyo atajiviringisha shingoni mwa mtu huyo kama mnyororo na kujivingisha shingoni mwake. Katika hali ya kumsuta, nyoka huyo atasema: ‘Mimi ni mali yako ile ambayo wewe ulikuwa ukijivuna na kujifakharisha duniani.’

 

Al Imam Muhammad al-Baqir a.s. amesema katika Wasail-as-shiah, mlango 3, J.6, Uk. 11:

“Mtu yeyote ambaye hatatoa na kulipa Zaka ya mali yake basiSiku ya Qiyamah Allah swt atamwadhibu kwa miale ya mioto katika sura ya nyoka wakubwa ambao watakuwa wakinyofoa na kula nyama yake hadi hapo hisabu yake itakapokwisha.”

 

Vile vile Al Imam Muhammad al-Baqir a.s. amesema katika Tafsir Minhaj as-Sadiqiin kuwa :

“Iwapo mtu aliye na mali na utajiri atakapoijiwa na ndugu au jamaa yake kwa ajili kuomba msaada kutokea mali na utajiri huo alionao, na yeye kwa sababu ya ubakhili wake akimnyima, basi Allah swt atamtoa nyoka mkubwa kabisa kutokea mioto ya Jahannam ambaye huizungusha ulimi wake mdomoni ili kwamba mtu huyo amwijie ili aweze kujiviringa shingoni mwake kama mnyororo mzito.”

 

Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema katika Wasa’il as-Shiah, ZAKAT,mlango 3, Hadith 1, J.6, Uk. 11 Kafi :

“Mtu yeyote anayemiliki dhahabu na fedha na asipotoa Zaka yake iliyofaradhishwa (au Khums, kama vile inavyoelezwa katika Tafsir al-Qummi), basi Allah swt atamfunga kifungo katika mahala pa upweke na atamwekea nyoka mkubwa kabisa ambaye atakuwa amedondosha nywele zake kwa sababu ya sumu kali aliyonayo, na wakati nyoka huyoatakapotaka kumshika basi mtu huyo atakuwa akijarbu sana kukikmibia lakiniatkaposhindwa hatimaye atakapotambua kuwa hataweza kujiokoa basi atamnyooshea mikono nyake mbele ya nyoka huyo. Lakini nyoka huyo atazitafuna mikono hiyo kama vile anavyotafunwa mtoto mdogo wa ngamia na atajiviringisha shingoni mwake kama mnyororo. Na hapo Allah swt anatuambia kuwa ‘Yeyote yule anayemiliki mifugo, ng’ombe na ngamia na siyetoa Zaka ya mali yake, basi Allah swt Siku ya Qiyamah atamfunga kifungo cha upweke na kila mnyama atamwuma na kila mnyama mwenye meno makali atampasua na yeyote yule ambaye hatoi Zaka kutokea mitende, mizabibu na mazao yake ya kilimo, basi huyo siku ya Qiyamah basi atafungwa shingoni mwake kwa mnyororo wenye urefu wa takriban magorofa saba.”

 

Al Imam Muhammad al-Baqir a.s. amesema katika Wasa’il as-Shiah Mlango 3, J.6, Uk.11 :

 “Allah swt amefaradhisha Zaka pamoja na Sala. Ameamrisha kutekeleza Sala na kutoa Zaka hivyo iwapo mtu atasali bila ya kutoa Zaka, basi atakuwa hakukamilisha Sala .

 

Vile vile Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. Wasa’il as-Shiah, ZAKAT,mlango 3, Hadith 13, J.6, Uk. 11:

amesema kuwa :

“Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. aliingia katika Masjid an-Nabawi, na aliwataja watu watano kwa majina yao na akasema kuwa inukeni na mtoke humu Msikitini na wala msisali kwani nyinyi hamutoi Zaka.

(Wasiolipa Zaka wamefukuzwa kutoka Msikitini !)

 

Vile vile Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. anasema katika Wasa’il as-Shiah, ZAKAT,mlango 3, Hadith 24, J.6, Uk 14 :

“Mtu yeyote asiyelipa Zaka ya mali yake basi yeye wakati wa mauti yake atataka kurudishwa humu duniani ili aweze kutoa na kulipa Zaka, kama vile Allah swt anatuambia: ‘Ewe Allah swt nirudishe tena ili nikafanye mema niliyokuwa nimeyaacha !’ Yaani wakati wa kifo chake atasema kuwa arudishwe humu duniani ili akaitumie mali aliyoilimbikiza katika njia njema, lakini atajibiwa kuwa kamwe haitawezekana hivyo kurudi kwake.”

 

Vile vile Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. ameelezea tafsir ya Ayah isemayo kuwa : ‘Allah swt atawaonyesha matendo yao katika hali ya kusikitisha mno kuwa wao hawatatoka nje ya Jahannam’ kama ifuatavyo katika wasl Wasa’il as-Shiah,mlango 5, Hadith 5, J.6, Uk21 :

“Mtu yule ambaye anakusanya na kulimbikiza mali yake na anafanya ubakhili katika kuitumia katika mambo mema na kwa kutoa zaka n.k., basi anapokufa huku amewaachia mali hiyo wale ambao watatumia mali hiyo katika utiifu wa Allah swt au kwa kutenda madhambi, basiiwapo itatumiwa katika utiifu wa Allah swt basi atakuwa mtu wa kujivuna na iwapo itatumiwa katika maasi na madhambi basi itamdhalilisha.”

 

Riwaya hii imenakiliwa na ‘Ayyashi, Mufiid, Sadduq na Tabarasi katika vitabu vyao na vile vile wamewanakili Maimamu Al Imam Muhammad al-Baqir a.s. na Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s.

 

Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. amesema, Wasa’il as-Shiah,mlango 5, Hadith 5, J.6, Uk21 :

“Hakuna kitu kinachokimaliza Islam kama Ubakhili na njia ya Ubakhili ni sawa na njia ya sisimizi ambayo haionekanina yenyewe ipo kama Shirk ambayo inayo aina nyingi.”

 

Al Imam 'Ali ibn Abi Talib  a.s. amesema katika Safinat al-Bihar, J.1 Uk. 155 :

 “Watu watakapokataa kutoa Zaka, basi baraka itakuwa imeondolewa kutoka ardhini kwa kutoa mazao na matunda kutoka mashamba yao,na madini.”

 

Vile vile Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. amesema katika Wasa’il as-Shiah,Mlango 1, Hadith  13 :

“Muwatibu wagonjwa wenu kwa kutoa Sadaqah na mutokomeze balaa, maafa kwa Du’a na muhifadhi mali zenu kwa kutoa Zaka.”

 

Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema Wasa’il as-Shiah,mlango 5, Hadith 10, J.6, Uk23 :

“Allah swt anazo mahala pengi humu ardhini ambazo huitwa ‘kilipiza  kisasi’ hivyo Allah swt anapomjaalia mtu mali na utajiri, na huyo mtu haitumii kwa kutoa malipo aliyofaradhishiwa, basi huwekewa nafasi mahala hap. Mali ambayo anakusanya kwa mbinu zake zote,inampotoka na anaiacha kwa wengine.”

 

Na katika riwaya zinginezo imeelezwa kuwa mtu ambaye anafanya ubakhili wa kutumia mali yake katika njia njema basi itatokea kuwa ataitumia katika njia potofu na riwaya ambazo zimeelezwa katika mlango wa Zaka, zipo nyingi, lakini hadi hapa zinatosheleza.

 

 

 

 

2.  ASIYELIPA ZAKA NI KAFIRI

Kama tulivyokwisha ona hapo awali kuhusu masuala ya zaka na kutokulipa kwake ni dhambi kuu. Iwapo mtu atamlazimu kulipa Zaka na kwa sababu za ubakhili wake, halipi basi atakuwa kafiri na najis kwani Zaka ni slawa na kufaradhishiwa kutimiza kama Sala na swala moja muhimu katika Dini na kwa kutokutimiza misingi ya dini, basi kunamtoa mtu nje ya dini. Zipo riwaya nyingi ambazo zinazumngumzia kukufurishwa kwa mtu asiyetoa Zaka kwa sababu za ubakhili wake. Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema katika Wasa’il as-Shiah,mlango 4, Hadith 2, J.6, Uk 18 :

“Bila shaka Allah swt amewawekea hisa mafukara na wenye shida katika mali za matajiriambayo imefaradhishwa. Faradhi ambayo inapotimizwa inakuwa ni yenye kuwafakharisha matajiri hao na ni kwa sababu ya kutoa huko Zaka kunakoharamisha kumwagwa damu yao na wanaolipa zaka wanaitwa Waislamu.”

 

Yaani wenye mali iwapo hawatatoa Zaka iliyofaradhishwa kwa kukataa, basi hao si Waislamu na hivyo kumwagwa kwa damu yao haiharamishwi.

 

Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema, Wasa’il as-Shiah,, J.6, Uk18 :

 “Mtu yeyote yule ambaye hatatoa Zaka hata lau kwa kiasi cha Qirat (1.20 Dinar yaani punje nne za Shayiri) basi huyo si Mumin wala si Mwislamu na watu kama hawa ndivyo alivyoelezea Allah swt  kuwa watakuwa wakitaka warudishwe humu duniani ili watekeleze mema. “

 

Vile vile Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. ameeleza katika Wasa’il as-Shiah,, J.6, Uk18:

“Mtu yeyote yule ambaye hatatoa Zaka hata kwa kiasi cha Qirat moja (sawa na punje nne za Shayiri) basi huyo atakuwa  bila imani na kufa kwa mauti ya Myahudi au Mnasara.”

 

Amesema vile vile Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. katika Wasa’il as-Shiah, ZAKAT, mlango 3, Hadith 1, J.6, Uk. 19 na  Kafi :

“Allah swt ameruhusu kumwagwa damu ya watu wa aina mbili ambapo hukumu hii itatekelezwa pale atakapodhihiri Al-Imam Muhammad Mahdi, sahibuz-zamaan, a.s. na hivyo mmoja miongoni mwa watu hao wawili ni yule anayefanya zinaa ilhali anayo mke wake hivyo atauawa kwa kupigwa mawe hadi kufa kwake na wa pili ni yule asiyetoa Zaka, huyo atakatwa kichwa.”

 

Vile vile amesema, katika Wasa’il as-Shiah,mlango 5, Hadith 8, J.6, Uk20 :

“Mali haipotei katika majangwa na Baharini ispokuwa ile isiyolipiwa Zaka na atakapodhihiri Al-Imam Muhammad Mahdi, sahibuz-zamaan, a.s. basi wale wote wasiolipa Zaka watasakwa na kukamtwa na watakatwa shingo zao.”

 

Amesema Allah swt katika Quran: Surah al –Fussilat, 41, Ayah 6 – 8 :

“Ole wao wanaomshirikisha, ambao hawatoi Zaka na wanaikataa Aakhera.” 

 

Amesema Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. , katika  Al-mustadrak :

“Kwa kiapo cha Allah swt ambaye anayoanayo roho ya Mtume Wake katika kudura yake, kuwa hakuna mtu anayemfanyia khiana Allah swt isipokuwa Mushrikina kama hawa ambao hawatoi Zaka kutoka mali zao.”

 

Vile vile Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. alimwambia Al-Imam ‘Ali ibn Abi Talib a.s., katika Al-Khisal, Uk. 450, Mlango Kumi :

“Ya Ali ! Katika Ummah wangu wapo makafiri wa makundi kumi

1.       Mfitini na mchonganishi 

2.       Mchawi

3.       Dayyuth yaani mwanamme yule ambaye anajua kuwa mke wake anazini lakini hajali bali anapuuzia,

4.       Mwanamme yule ambaye anauroho wa kiharamu wa kutafuta wanawake mbalimbal kwa kulawiti,

5.       Anayewalawiti wanyama 

6.       Anayezini pamoja na wale walioharamishwa kwake yaani ambao ni mahram kwake,

7.       Anayechochea na kuzidisha moto wa fitina na chuki miongoni mwa watu, 

8.       Anayewasaidia makafiri kihali na mali kupigana dhidi ya Waislamu,

9.       Asiyetoa Zaka

10.    Asiye Hijji ilhali ana uwezo kamili na kutimiza masharti yake na akifa katika hali hiyo.”

 

Kwa kuzingatia riwaya kama hizi tunaona kuwa kutokusali, kutokutoa Zaka na kutokuhiji wakati hali inaruhusu, kwa misingi ya ujauri wetu wenyewe, basi huyo ni kafiri na atakosa baraka na neema za Aakhera ambayo ni kumwokoa kutoka Jahannam   na vile vile humu duniani hatakuwa toharifu kama Waislamu na hataruhusiwa kurithi, kuoana pamoja na waislamu, n.k., lakini iwapo mtu hatoi Zaka kwa ubakhili wake (Ingawaje hakatai wala kupinga Zaka) basi huyo hawezi kuwa kafiri.  Ingawaje kidhahiri yeye ni Mwislamu lakini kiundani mwake anayo sifa mojawapo ya ukafiri na iwapo atakufa , basi atatumbukizwa katika adhabu kali mno, kama vile ilivyoahidiwa.


 

3.  SABABU ZA KUFARADHISHWA KWA ZAKA

 

Katika kufaradhisha utoaji wa Zaka na Sadaqah zinginezo zinahekima ndani yake ambazo hazipo dhahiri mbele yetu. Hata hivyo baadhi yao zimeletwa bele yetu (ambavyo ni kutokea Allah swt ) mtihani kwa wenye mali na utajiri kwa kujiuliza je kwao Allah swt ni mpenzi zaidi kuliko mali zao ambazo zitakwisha siku moja ?  Na je kwa kweli wana imani kamili juu ya Thawabu, Jannat, Jazaa ( malipo ) au hawana imani ? Je kwa kweli wanafanya ibada ya Allah swt kwa moyo mkweli au sivyo ? 

 

Faida ya pili ni kuwaondolea shida na taabu wale wanaostahiki misaada hiyo ili waweze kuishi vizuri, na kwa hayo Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema katika kuzungumzia faida za utoaji wa Zaka, katika Kafi Wasail, Mlango 1, Hadith 9 :

“Bila shaka Zaka imefaradhishwa kwa ajili ya kuwajaribu (mtihani) matajiri na wenye mali na kuwatimizia mahitaji ya wenye shida na kwa yakini, iwapo watu wangalikuwa wakitoa Zaka ipasavyo, basi kusingalikuwapo na Waislamu masikini na wenye shida na wala kusingalikuwa na mmoja kumtegemea mwingine na wala kusingalikuwapo na wenye kuwa na njaa au wasiokuwa na nguo. Lakini taabu na shida zote walionazo masikini ni kutokana na wenye mali na utajirikutotimiza wajibu wao wa kutoa Zaka na Sadaqah. Hivyo Allah swt humtenga mbali na neeema na baraka Zake yule ambaye hatimizi wajibu wake huo. Nami naapa kwa kiapo cha Allah swt ambaye ameumba viumbe vyote na anawapatia riziki zao, kuwa hakuna kinachopotea katika mali katika nchi kavu au majiniisipokuwa ile isiyotolewa  Zaka.

 

Faida ya tatu, Nafsi[1] yetu inatoharishwa kwa udhalilisho wa ugonjwa sugu wa ubakhili na hivyo inatubidi sisi lazima tuutibu ugonjwa huu unaoangamiza na kutumaliza.

 

Hivyo Amesema Allah swt katika Quran: Surah al-Tawbah, Ayah 103 :

Chukua sadaqah katika mali yao, uwasafishe na kuwatakasa kwa ajili ya hizo (sadaqah zao na kuwataja kwa vizuri (mbele yangu) na uwaombee dua. Kwa hakika kuwaombea kwako kutawapa utulivu, na Allah swt ndiye asikiaye na ajuaye.”

 

Vile vile Amesema Allah swt katika Quran: Surah al – Hashri, 59,  Ayah 9 :

“Na walio na maskani zao na Imani yao kabla yao, wanawapenda waliohamia kwao, wala hawaoni choyokatika vifua vyao kwa waliyopewa (Wahajiri), bali wanawapendelea kulikoa nafsi zao, ingawa wao wenyewe ni wajitaji.  Na mwenye kuepushwa uchoyo wa nafsi yake, basi hao ndio wenye kufanikiwa.”

 

Hivyo tumeona kuwa matibabu ya uginjwa uitwao ubakhili ni kule kutoa Zaka, misaada na Sadaqah na tuwetukitoa kila mara kiasi kwamba iwe ndiyo tabia yetu na kwa kuzingatia ustaarabu na adabu tukitoa Sadaqah basi tunaweza kuokoka na ugonjwa huu unaotuangamiza.

 

4.  ZAKA NA SADAQAH HUONGEZA NEEMA

 

Faida kuu mojawapo ya kutoa Zaka ni kuongezeka kwa neema na baraka ya mali yetu iwapo itatolewa kwa kuzingatia kanuni na ustaarabu wa kutoa hivyo, na ni kinyume na mawazo na mipango ya Ki-Shaytani, kwani mabakhili hufikiria daima kuwa kwa kutoa mali yako kwa ajili misaada na Sadaqah na Zaka, basi mali yao hupungua na hivyo wanaweza kuwa masikini na kwa hakika hayo ndiyo mawazo na upotofu wa Shaytani.

 

Amesema Allah swt katika Quran: Surah al –Baqarah, Ayah 28 : “Allah swt huongezea katika Sadaqah” yaani huongezea baraka humu duniani na vile vile kutakuwapo na malipo mengine huko Aakhera na amesema Allah swt katika Quran: Surah al – Saba,34, Ayah 39 : ‘Chochote kile mtakachokitoa (katika njia yake), basi Atawalipeni (humu humu duniani) malipo yake, Naye ni Mbora wa wanao ruzuku.’

 

Amesema Allah swt katika Quran: Surah al –Rum, 30,  Ayah 39 :

‘Na mnachokitoa kwa riba ili kiongezeke katika mali ya watu, basi hakiongezeki mbele ya Allah swt . Lakini mnachokitoa kwa Zaka kwa kutaka radhi ya Allah swt, basi hao ndio watakaozidishiwa.’

 

Katika Ayah hizo, tumeona kuwa kuongezeka zaidi mno na vile vile Baraka pia itakuwamo, vyote kwa pamoja. Katika kusisitiza hayo, zipo riwaya nyingi mno.

 

Amesema Bi. Fatimah az-Zahra bintie Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. katika hotuba aliyoitoa kuzungumzia Fadak [2] katika Bihar al-Anwaar, J.8, Uk 109 :

 “Kwa ajili ya kujitakasa na dhambi la Shirk, Allah swt ametufadhishia kuikamilisha imani yetu ( yaani mtu yeyote anayetaka kujitakasisha na unajisi basi inambidi kuleta imani kwa moyo wake kamilifu), na Sala inamwepusha na magonjwa ya kiburi na kujifakharisha, na Zaka inamwepusha mtu kwa magonjwa ya ubahili ili mwanadamu awe mkarimu na mpenda kutoa kwa ajili ya mema ili atakasike) na hii pia ndiyo sababu kuu katika kujiongezea riziki .”

 

Al Imam 'Ali ibn Abi Talib  a.s. ameripotiwa akisema katika Al-Kafi:

“Yeyote yule anayetumia kutoka mali yake katika njia ya kheri, basi Allah swt anamlipa mema humu duniani na kumwongezea katika malipo yake.”

 

Vile vile ameripotiwa akisema Al Imam 'Ali ibn Abi Talib  a.s.  katika Wasa’il as-Shiah : Mlango Sadaqah, Hadith 19, J.6, Uk. 259 :

“Tafuteni riziki yenu kwa kutoa Sadaqah.”

 

Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. ameripotiwa katika Kitab ‘Uddatud-Da’I kuwa  alimwuliza mtoto wake :”Je nyumbani kuna kiasi gani kwa ajili ya matumizi ?”

 

Naye alimjibu : “Zipo Dinar arobaini tu.” 

 

Imam a.s. alimwambia “Dinar zote hizo zigawe Sadaqah.”

 

Kwa hayo mtoto wake alimwambia Imam a.s. “Ewe Baba ! Mbali na Dinar hizi arobaini, hatutabakia na akiba yoyote.”

 

Imam a.s. alimwambia : “Nakuambia kuwa zitoe Dinar zote Sadaqah kwani ni Allah swt tu ndiye atakayetuongezea kwa hayo. Je wewe hauelwei kuwa kila kitu kina ufunguo wake ? Na ufunguo wa riziki ni Sadaqah ( kutolea mema ).”

 

Kwa hayo, mtoto wake aliyekuwa akiitwa Muhammad, alizitoa Sadaqah Dinar hizo na hazikupita siku kumi, Imam a.s. alitumiwa Ddinar elfu nne. Hapo Imam a.s. alimwambia mwanae : “Ewe Mwanangu ! Sisi tulitoa Dinar arobaini tu na Allah swt ametupa Dinar elfu nne badala yake.”

 

Al Imam 'Ali ibn Abi Talib  a.s. amesema katika Nahjul Balagha kuwa :

“Mtu anapokuwa masikini au mwenye shida basi fanyeni biashara pamoja na Allah swt kwa kutoa Sadaqah.”

 

Al Imam ‘Ali ar Ridha  a.s. alimwambia mfanyakazi wake : “Je leo umeshagawa chochote katika njia ya Allah swt .”  Mfanyakazi huyo, “La, bado sijagawa.”  Kwa kuyasikia hayo Imam a.s. alimjibu, “ Sasa kama haukufanya hivyo, basi Allah swt atatulipa nini badala ya tendo letu ? Hivyo hatutapata baraka wala neema yoyote kutoka kwa Allah swt . Tukitoa chochote ndipo Allah swt atatulipa kwa wingi badala yake.”

 

Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. ameelezea Hadith katika Al-kafi, Kitab ad-Du’a, J. 2, Uk.595  moja kwa kutokea Ayah Fahuwa Yukhlifuhu (yaani chochote kile kinachotolewa katika njia ya Allah swt , basi hulipa malipo yake kwa haraka sana ). Na Hadith yenyewe ni :

“Je utadhaniaje kuwa Allah swt anakiuka ahadi aliyoitoa ?”

 

Basi mwandishi  akajibu : “La ! Sivyo hivyo.”

 

Ndipo Imam a.s. alimwuliza : “Sasa je kwanini wewe haupati malipo yako kwa yale unayoyatoa na kugawa ?”

 

Naye akajibu, “ Kwa hakika mimi sijui sababu zake.”

 

Imam a.s. alimjibu, “Iwapo miongoni mwenu yeyote atakayekuwa akiipata riziki yake kwa njia zilizo halali, na kama ataitumia hata Dirham moja katika njia zilizo halali, basi lazima mtapata malipo yake na kwa wingi zaidi.  Na iwapo mkiona kuwa hamkupata chochote katika malipo yenu basi mutambue kuwa mali hiyo ilichumwa kwa njia zilizo haramu au ilitolewa na kutumiwa katika njia iliyoharamishwa.”

 

Kuhusiana na swala hili zipo Ayah na riwaya nyingi mno, lakini tunatua hapa. Marehemu Nouri katika kitabu chake Kalimah at-Tayyibah amezungumzia mengi na kwa mapana na undani zaidi kuhusu kutoa Sadaqah katika njia ya Allah swt  na amedondoa hekaya takriban arobaini ambamo ‘Alim rabbani akhwand Mullah Fath ‘Ali amenakili kisa cha jamaa yake ategemewae ambaye amesema,

“Mwaka mmoja ambapo hali ya ughali ilikuwa imekithiri, nilikuwa na kipande kimoja cha ardhi ambapo nilikuwa nimepanda Shayiri na ikatokea kuwa shamba langu hilo likawa na mavuno mengi mno kuliko mashamba menginey. Kwa kuwa hali ilikuwa ni mbaya kwa watu wengineo, hivyo tamaa ya kujitafutia faida zaidi katika mazingara hayo niliyatoa kutoka nafsi yangu. Hivyo mimi nilkwenda moja kwa moja Msikitini na kutangaza kuwa mazao yote yaliyo shambani mwangu nimeyaacha kwa masharti kwamba yeyote mwenye shida tu ndiye aende kuchukua na masikini na mafukara waendekuchukua kwa ajili ya chakula cha familia zao. Wote wachukue kiasi wanachokihitaji. Hivyo masikini na mafukara na wenye shida walikuwa wakichukua mavuno kutoka shambani mwangu huku wakisubiri mavuno yao kukomaa. Kwa hakika nafsi yangu ilikuwa imetulia vyema kabisa kwani sikuwa na wasiwasi kwani nilikuwa nimeshajitenga navyo.

 

Wakulima wadogowadogo wote walipovuna mazao yao, nami nikavuna kutoka mashamba yangu mengineo na nikawaambia wafanyakazi wangu waende katika shamba ambalo nilikuwa nimeligawa kuwasaidia wenye shida wakati huo, wakaangalie kama kumebakia chochote ili waweze kuvuna.

 

Kwa hakika hao walipokwenda shambani humo walikuta shamba zima limejaa Shayiri kupita kiasi na baada ya kuvuna na kusafisha nilikuta kuwa nimepata mavuno mara dufu kuliko mashamba yangu mengineyo. Ingawaje humo watu wote walikuwa wakivuna kwa ajili ya chakula chao na familia zao, ilitakiwa kuwa tupu kumbe Allah swt amerudishia mavuno tena mara dufu.

 

Vile vile sisi tulikuwa ukipanda mwaka mmoja na kuipumzisha ardhi mwaka mmoja, lakini shamba hilo halikuhitaji kupumzishwa wala kuwekewa mbolea na badala yake nimekuwa nikilima na kupanda nafaka kila mwaka na nilikuwa nikipata mavuno mara dufu kila msimu.

 

Mimi kwa hakika nilistaajabishwa mno kuona hayo na nikajiuliza isije hiki kipande cha ardhi kikawa ni kitu kingine na mavuno yanapokuwa tayari, hupata mavuno mengi kabisa kuliko mashamba mengine yangu na ya watu wengineo.

 

Mbali na hayo, Merehemu amenakiliwa kuwa :

‘Yeye alikuwa na shamba moja la mizabibu kandoni mwa barabara na kwa mara ya kwanza kulipozaa zabibu katika matawi yake, alimwammuru mtunza shamba wake kuwa zabibu zote zilizopo kando ya barabara aziache kwa ajili wapitao njia. Hivyo kila mpita njia alichuma na kula zabibu zilizokuwa hapo na wengine hata walichukua pamoja nao. Msimu ulipokwa ukiisha aliwaamuru wafanyakazi wake waende kuangalia kama kulibakia zabibu zilizokuwa zimefichika nyuma ya majani au pembeni. Lakini jambo la kustaajabisha ni kwamba, wafanyakazi waliporudi, walikuwa wamevuna zabibu mara dufu ya mashamba yake mengineyo pamoja na kwamba kila mpita njia alikuwa akichuma zabibu hapo.’

 

Vile vile imenakiliwa kuwa :

‘Kila msimu alipokuwa akivuna ngano na kuzisafisha, alikuwa akizileta nyumbani kwake na hapo ndipo alipokuwa akitoa Zaka yake. Lakini safari moja alipovuna na kusafisha, akiwa akielekea nyumbani kwake aliwaza kuwa inambidi alipe Zaka haraka iwezekanavyo, kwani si vyema kuchelewesha ulipaji wa Zaka. Ni ukweli kwamba ngano ipo tayari na mafukaraa na masikini pia wapo. Hivyo aliwajulisha mara moja mafukaraa na masikini waje kuchukua ngano, na hivyo akapiga mahisabu yake na kuwagawia sehemu yao na hivyo sehemu iliyobakia aliileta nyumbani kwake na kujaza madebe makubwa makubwa na alikuwa akijua ujazo wao. Lakini alikuja kuangalia hapo baadaye akakuta kuwa idadi ya ngano imeongezeka mara dufu pamoja na kwamba likuwa amepunguza kwa ajili ya kuwagawia mafukaraa na masikini.Na hivyo alikuta idadi ya ngano ipo pale pale kabla ya kutoa Zaka.’

 

Katika kitabu kilichotajwa, Alhaj Mahdi Sultan Abadi amenakili kuwa :

‘Mwaka mmoja mimi nilipovuna mavuno, nilipima uzito wa ngano na nikatoa na kuigawa Zaka yake. Na nafaka hizo zilibakia mahala hapo hapo kwa muda wa mwezi mmoa ambapo anyama pamoja na mapanya walikuwa wakila humo. Na nilipokuja kurudia kupima uzito wake nikakuta kuwa uzito wa ngano ulikuwa vile vile kama siku ya kwanza yaani kiasi nilichokitoa Zaka na kilicholiwa na wanyama na mapanya hakikupungua hata chembe kidogo.’


 

5.  AINA ZA ZAKA NA VIWANGO VYAKE

 

Zaka imegawanywa katika makundi mawili

·         Zaka  iliyofaradhishwa

·         Zaka iliyo Sunnah

 

Na Zaka iliyofaradhishwa pia imegawanywa katika makundi mawili :

·         1.  Zaka ya mali

·         2.  Zaka ya Mwili  ( Zakati Fitrah )

 

Zaka iliyofaradhishwa inayo aina tisa za mali na aina nne za nafaka ( ngano, Shayiri, tende na zabibu ), aina tatu za wanyama (kondoo au mbuzi, ng’ombe na ngamia ) na aina mbili za madini (dhahabu na fedha ).

 

Mahisabu ya aina nne za nafaka :

  1. Ngano, Shayiri, tende na zabibu zitastahiki kutolewa Zaka iwapo zitafikia kiwango maalum ambavyo ni Saa 300 au mann 280 Tabrizi na ni pungufu kwa mithqal 45 ambayo ni sawa na takriban Kiligramu 847 .
  2. Na iwapo ( ngano, Shayiri, tende na zabibu )  zinalimwa kwa umwagiliaji wa maji ya mvua au mito au kwa urutubisho wa ardhi (kama zilivyo baadhi ya mazao huko Misri ) basi Zaka yake itakuwa ni asilimia 10  ( 10 % )
  3. Na iwapo inamwagiwa kwa maji ya kisima basi Zaka yake itakuwa asilimia 5. ( 5% )

 

1.  zaka ya mali

(A).  ZAKA KATIKA WANYAMA

                                                                                                       (i)     VIWANGO  VITANO YA KONDOO NA MBUZI

 

  1. Idadi yao iwapo arobaini (40 ) basi Zaka yake ni kondoo au mbuzi mmoja ( 1 ) na iwapo hawatafika arobaini basi hakuna Zaka.
  2. Idadi yao iwapo mia moja na ishirini na moja ( 121 ) basi Zaka yake itakuwa ni kondoo au mbuzi wawili ( 2 )
  3. Iwapo idadi yao ni mia mbili na moja ( 201 ) basi Zaka yao itakuwa ni kondoo au mbuzi wanne ( 3 ).
  4. Iwapo idadi yao ni mia tatu na moja ( 301 ) basi Zaka yao itakuwa ni kondoo au mbuzi wanne ( 4 ).
  5. Iwapo idadi yao ni mia nne ( 400 ) au zaidi basi Zaka yao itakuwa ni kondoo au mbuzi mmoja kwa kila kondoo au mbuzi mia moja  ( 1 ).

                                                                                                                       (ii)     VIWANGO  VIWILI  VYA NG’OMBE

  1. Kiwango cha kwanza ni ng’ombe 30. Iwapo mtu atakuwa na ng’ombe 30 basi itambidi alipe Zaka ambayo ni ndama dume mmoja wa ng’ombe ambaye ameingia katika umri wa mwaka wa pili. Na iwapo watapungua ng’ombe chini ya 30, basi hawatakiwi kulipa Zaka.
  2. Kiango cha pili ni ng’ombe 40 na Zaka yake ni ndama jike wa ng’ombe ambaye ameshaingia katika mwaka wa tatu .

 

·         Iwapo mtu atakuwa na ng’ombe kati ya 30 na 40  ( mfano ng’ombe 39 ) basi anatakiwa alipe Zaka za ng’ombe 30 tu.

·         Na iwapo anao ng’ombe 60 basi atalipa Zaka ya  ndama 2 ambao wameingia katika mwaka wa pili.

·         Na iwapo anao ng’ombe 70 basi atalipa Zaka ya  ndama 1 ambaye ameingia katika mwaka wa pili na ndama jike mmoja ambaye ameingia katika mwaka wa tatu.

·         Kwa kila idadi itakavyoongezeka basi itabidi kupigia hisabu kwa 30 au 40 na Zaka itatolewa hivyo.

                                                                                                                                  (iii)     VIWANGO  12  VYA NGAMIA

 

  1. Iwapo mtu atakuwa na ngamia 5 basi Zaka yake ni mbuzi au kondoo mmoja. Iwapo idadi ya ngamia 5 haitafika basi hatatakiwa kulipa Zaka.
  2. Ngamia 10 na Zaka yake ni mbuzi au kondoo 2
  3. Ngamia 15 na Zaka yake ni mbuzi au kondoo 3
  4. Ngamia 20 na Zaka yake ni mbuzi au kondoo 4
  5. Ngamia 25 na Zaka yake ni mbuzi au kondoo 5
  6. Ngamia 26 na Zaka yake ni ngamia mmoja ambaye ameingia mwaka wa pili
  7. Ngamia 36 na Zaka yake ni ngamia mmoja ambaye ameingia mwaka wa tatu
  8. Ngamia 46 na Zaka yake ni ngamia mmoja ambaye ameingia mwaka wa nne
  9. Ngamia 61 na Zaka yake ni ngamia mmoja ambaye ameingia mwaka wa tano
  10. Ngamia 76 na Zaka yake ni ngamia wawili ambao wameingia mwaka wa tatu
  11. Ngamia 91 na Zaka yake ni ngamia wawili ambao wameingia mwaka wa nne
  12. Ngamia 121 na Zaka yake itahesabiwa ama kwa makundi ya ngami 40, na atatoa Zaka ngamia mmoja aliyeingia mwaka wa tatu na kila kikundi cha ngamia 50 atatoa ngamia mmoja aliyeingia mwaka wa nne.

(B).  VIWANGO 2 VYA DHAHABU NA FEDHA[1]

1)        VIWANGO 2 VYA  FEDHA
  1. Kiwango cha kwanza ni Mithqaal  105, sawa na uzito wa Gramu 483.88  na kama fedha hiyo imebadilishwa katika sarafu kwa ajili ya kufanyiwa biashara na zimewekwa mahala kwa muda wa mwaka mmoja basi Zaka yake itakuwa ni asilimia 2.5  (2.5 % ) Na iwapo kiwango hicho kitapungua basi hakuna Zaka itakayolipwa.
  2. Kuongezeka kwa Mithqaal 21 katika Mithqaal 105 zikawa jumla ya Mithqaal 126, basi itambidi alipe Zaka ya Mithqaal 126. Na iwapo itakuwa chini ya Mithqaal 126 ( kama haitafikia iMithqaal 21 ) basi itambidi alipie Zaka katika Mithqaal 105. Hivyo itambidi alipe  sehemu 1 / 40 ya jumla. Lakini lazima iwe imefikia Mithqaal 21 na kama itapungua basi kiwango hicho kitabaki kilipofikia. Mfano iwapo mtu atatakiwa kulipia Mithqaal 110 basi yeye atalipia Mithqaal  105 ambayo ni sawa na 2. 5 % ( au 2.625 Mithqaal) na mara nyingine itambidi alipie  Mithqaal 5zilizozidi ambayo si faradhi.
2)          VIWANGO 2 VYA  DHAHABU
  1. Kiwango cha kwanza ni Mithqaal 20 (Shar’ee) katika sura ya sarafu zitumiwazwo katika kufanyia biashara na zikakaa kwa muda wa mwaka mmoja mahala moja bila kutumiwa ambapo Mithqaal  1 ni sawa na uzito wa  3.456 gramu na hivyo inapofikia kiwango cha 20 Mithqaal ( ispofikia hivyo, hakuna Zaka )  inambidi mtu alipe Zaka kwa kiwango cha  sehemu  1/40 ambayo ni sawa na uzito wa 1.728 gramu.
  2. Kiwango cha pili ni kule kunapoongezeka kwa dhahabu zaidi ya Mithqaal  20 Shar’ee,  iwapo kutaongezeka Mithqaal  4 Shar’ee juu ya Mithqaal  20 Shar’ee basi  inambidi mtu alipe Zaka kwa kiwango chote kwa ujumla kwa kiwango cha  2. 5 %  na iwapo kiwango cha nyongeza kitakuwa ni pungufu ya 4 Mithqaal  basi Zaka italipwa kwa 20 Shar’ee Mithqaal  tu na haitamlazimu kulipia Mithqaal  iliyozidi ambayo ni pungufu ya 4 Mithqaal .

 

 

2.  ZAKAT-I-FITRAH

Mtu yeyote yule ambaye katika usiku wa kuamkia Idd-ul-Fitr ( usiku wa kuamkia tarehe mosi ya Mwezi mtukufu wa Shawwaal ) baada ya kuzama kwa jua akabalehe, akawa na akili timamu na ghanii ( yaani ambaye anajitimizia mahitaji yake ya dharura ya kila mwezi, huitwa ghanii, yaani si mwenye dhiki ) basi ni faradhi juu yake na kutoa Zakat-i-Fitri yake binafsi na wale wote wanaomtegemea kimaisha na kichakula hata wale watoto wachanga wanaonyonya na vile vile kama kutatokezea mgeni basi awalipie nao pia. Kiwango cha  Fitrah ni Sa’a imoja ambayo ni sawa na kiasi cha kilogramu 3 za ngano, zabibu, tende, mchele au choc hote kile anachokitumia yeye kama chakula chakecha kila siku na itambidi awape wale wanaostahiki au anaweza kutoa thamani yake kifedha, nayo inafaa.

Tukumbuke kuwa faida ya papo hapo ya fitrani kule kubakia katika kunusurika na mauti ambazo si za kawaida kama vile ajali n.k. na imeripotiwa na Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. kuwa :

“Alimwambia wakili wake wa matumizi kuwa aende akatoe Zakat-i-Fitrah ya wananyumba yake wote bila hata ya kumsahau mmoja wao kwa sababuiwapo hatatoa Zaka yao basi atakuwa na hofu ya kufa kwao na thawabu zake ni sawa na kukubaliwa kwa saumu za mwezi mzima.

 

Vile vile Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema :

“Zakat-i-Fitrah inakamilisha saumu za mwezi Mtukufu wa Ramadhani.”


 

6.  MATUMIZI YA ZAKA

 

Amesema Allah swt katika Quran: Surah al – Tawbah,  9, Ayah 60 :

“Wa kupewa Sadaqah ni mafakiri, na masikini, na wanaozitumikia, na wa kutiwa nguvu nyoyo zao, na katika kukomboa watumwa, na wenye madeni, na katika Njia ya Allah swt , na wasafiri. Huu ni wajibu uliofaradhiwa na Allah swt . Na Allah swt ni Mwenye kujua Mwenye hikima.”

 

Mali ya Zaka inaweza kugawiwa sehemu nane kama ilivyoelezwa katika ayah hii ya Qur'an Tukufu :

  1. Fakiri

Ni mtu yule ambaye yeye hana uwezo wa kujilisha yeye pamoja na familia yake kwa muda wa mwaka mzima. Ambaye kwa hakika hana uwezo wa kurejesha sasa hivi au hata hapo mbeleni. Lakini yule mtu ambaye anamiliki majengo, milki au mali haitwi fakiri.

  1. Masikini

 Ni yule ambaye hali yake ni ngumu kuliko hata fakiri.

  1. Wanaozitumikia

 Ni mtu yule ambaye anakusanya Zaka kwa niaba ya Al-Imam Muhammad Mahdi, sahibuz-zamaan, a.s. na kumfikishia Naibu wa Imam a.s. au wanaostahiki.

  1. Wa kutiwa nguvu nyoyo zao

 Ni Waislamu wale ambao imani zao ni dhaifu hivyo kwa kuwasaidia na kuwapa nguvu kimaisha.

  1. Kukomboa watumwa

 Kutumia mapato ya Zaka kwa ajili ya kumfanya huru mtumwa ambaye yupo katika hali ya kuteswa mno au kumnunua na kumfanya awe huru

  1. Wenye madeni

Kuwasaidia mapato ya Zaka wale wasiojiweza kulipa madeni wanayodaiwa.

  1. Njia ya Allah swt

 Mapato ya Zaka yanaweza kutumia katika kila shughuli zenye kuifaidisha Dini mfano ujenzi wa Misikiti au Madrassah ili Waislamu waweze kufaidika kwa kufanyia ‘ibada na vile vile kutolewe mafunzo ya Dini , au kutengeneza madaraja au kusuluhisha makundi mawili au watu wawili waliotafarukiana au kusaidia katika ‘ibada, n.k.

  1. Wasafiri :

 Kumsaidia msafiri ambaye amekumbwa na matatizo akiwa safarini ambaye hawezi kuchukua deni au kuuza kitu alichonacho kwa ajili ya kurudi nyumbani kwake hata kama yeye hatakuwa  fakiri nyumbani kwake.


 

7.  ZAKA ZILIZO SUNNAH

 

Vitu saba vina Zaka Sunnah :

  1. Mali ya biashara au mtaji

Mali ambayo mtu anataka kuitumia katika kufanyia bishara

  1. Aina za nafaka :

Mfano mchele, dengu, dengu iliyoparazwa. Lakini mbogamboga kama vile biringanya, matango, matikimaji, maboga hayana Zaka.

  1. Farasi jike
  2. Vito vya dhahabu na mawe

Vitu vilivyotengezwa vya kuvaa na mawe kama almasi n.k.

  1. Mali iliyozikwa au kufichwa

Iwapo mtu atakuwa na mali aliyoizika au aliyoificha ambayo hawezi kuitumia basi kwa misingi ya uwezo inambidi kutoa Zaka ya mwaka mmoja.

  1. Kukwepa kutoa Zaka

Iwapo mtu atauza sehemu ya mali kiasi fulani kabla ya kuisha kwa mwaka kwa misingi ya kukwepa kulipa Zaka, basi itambidi uanzapo mwaka mpya, alipie Zaka sehemu hiyo aliyokuwa ameuza kwa ajili ya kukwepa Zaka yake.

  1. Mali ya kukodisha

Mtu anayepokea malipo kutokana na kukodisha majumba, maduka, mashamba, mabustani au hamaamk (mabafu yanayotoza malipo kwa kutumia ).

 

 

 

8.  KUSALI SALA ZA MAREHEMU NI LAZIMA

Haifai kabisa kufanya uvivu katika Sala zilizofaradhishwa na iwapo kutabakia kwa Sala ambazo zimekuwa Qadhaa za marehemu basi ni wajibu kake kufanya wusia kuwa sala zake hizo zitimizwe baada kufa kwake. Na marehemu anapofanya wusia kama huo basi ni wajib juu ya mwusiwa kutekeleza na kutimiza usia huo kutokea sehemu ya tatu ya mali ya marehemu huyo.

 

 


 

9.  KHUMS

Baada ya Zaka iliyofaradhishwa inakuja Khums iliyofaradhishwa ambayo Allah swt amewawekea kwa ajili ya Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. pamoja na Ahlul Bayt a.s., ambapo Zaka kwao ni haramu. Na iwapo mtu yeyote hatalipa Khums hata kwa Dirham moja au chini yake, basi huyo atakuwa ni mdhulumaji wa haki ya watajwa hapo juu. Na iwapo atajihalalishia kwa ajili yake mwenyewe na kukataa kutoa khums, basi naye pia atakuwa miongoni mwa Makafiri kwani hali kama hizo zimekwishaelezwa kwa undani katika kurasa zilizopita lakini katika Qur'an Tukufu imeelezwa kuwa ni shuruti la imani juu ya Allah swt  kama vile Allah swt anavyotuelezea katika Sura al-Anfaal, 8, Ayah 41 :

NA JUENI ya kwamba ngawira mnayoipata, basi khums (sehemu moja katika tano) ni kwa ajili ya Allah swt na Mtume, na jamaa, na mayatima, na masikini, na wasafiri, ikiwa nyinyi mmemuamini Allah swt na tuliyoteremsha kwa mja wetu(Muhammad) siku ya kipambanuo (katika Vita vya Badr), siku ( Waislamu na Makafiri ) yalipokutana majeshi mawili. Na Allah swt ni Muweza wa kila kitu.

 

Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema, katika Man la yahdhurul Faqihi, J.2, uk.41

“Kwa kuwa Allah swt ametuharamishia Zaka sisi Ahlul-Bayt a.s.hivyo ametuwekea Khums kwa ajili yetu na hivyo Sadaqah pia ni haram kwetu na zawadi imeruhusiwa kwa ajili yetu.”

 

Al Imam Muhammad al-Baqir a.s. amesema, katika Usuli Kafi, J. 1, Uk.545 :

 “Hakuna mtu yeyote anayeruhusiwa kununulia chochote kutoka kifungu ambacho Khums haijalipwa na hadi pale wasipoifikisha kwa wanaostahiki kwetu.”

 

Vile vile Al Imam Muhammad al-Baqir a.s. amesema, katika Al-Kafi, J.1, Uk. 546 :

 “Siku ya Qiyamah wakati ule utakuwa mgumu kabisa pale wanaostahiki Khums watakapotokezea kudai haki zao kutoka wale wasioilipa.”

 

 

1. KUONGEZEKA KWA NEEMA NA KUTOHARISHA MALI

Miongoni mwa marafiki tajiri mmoja kutokea Uajemi alimwandikia barua Al-Imam ‘Ali ar-Ridha a.s. na alimwomba Imam a.s. ruhusa ya kuitumia mali ile ambayo khums haijatolewa. Basi Imam a.s. alimwandikia majibu kama ifuatavyo :

Imenakiliwa kutoka Al-Wafi, Al-Kafi na Tahdhib

“Bila shaka Allah swt ni Wasi’ na Mkarimu na amechukua dhamana ya kumlipa thawabu na malipo mema  yule mtu ambaye atatekeleza hukumu zake na ameweka adhabu kwa yeyote atakayekwenda kinyume ya hayo. Bila shaka mali iliyo halali kwa ajili ya mtu ni ile ambayo Allah swt ameihalalisha na kwa hakika Khums ni dharura yetu na ni hukumu  ya Dini yetu na ni njia ya kujipatia kipato kwa jili ya riziki sisi na wenzetu na imewekwa kwa ajili ya kulinda hishima zetu dhidi ya wapinzani wetu. Hivyo kamwe musiache kutoa na kulipa Khums. Na kila inapowezekana kusijikoseshe Du’a zetu na kwa hakika kwa kutoa Khums kunazidisha riziki yenu na  kutoharisha na ni hazina kubwa kwa ajili ya Siku ile ambayo kutakuwa na taabu tupu na mateso (Siku ya Qiyamah. Na kwa hakika Mwislamu sahihi ni  yule ambaye amemwahidi Allah swt kwa ahadi na ‘ibada, basi atimize kwa ukamilifu. Na iwapo atakubali kwa mdomo tu ilhali moyoni anakataa na kupinga basi atambue kuwa yeye si mwislamu.

 

Al-Imam Muhammad Mahdi, sahibuz-zamaan, a.s. kwa kupitia Naibu wake makhsusi Muhammad bin ‘Uthman , alimwandikia barua Abul Hasan Asadi, kama ifuatavyo, katika Akmalud-Diin Saduq, Mlango Tawqi’at, Uk. 563 :

“Bismillahir Rahmanir Rahiim.

Allah swt , Malaika na watu wote wanamlaani mtu yule ambaye anajihalalishia hata kwa Dirhamu moja kutoka haki yetu.”

 

Kwa kusoma barua hiyo Abul Hasan Asadi  anasema :

“Mimi nilifikiri kuwa mtu yeyote anayjihalalishia kwa kuila mali ya Imam a.s. (na wala si yule mtu ambaye anaila bila kujua kuwa kujihalalishia na katika maharamisho yote ya hukumu za Allah swt ni kwamba kuhalalisha kile alichokiharamisha Allah swt , basi mtu huyo atakuwa mustahiki wa laana hizo zote, na hivyo kwa misingi hiyo hiyo hakuna tofauti baina ya hukumu zingine na ile ya kula mali ya Imam a.s.)

 

Lakini kwa kiapo cha Allah swt ambaye amembashiria Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. ! Mie nimeona katika yale yaliyokuwa yameandikwa katika barua hiyo ya Imam a.s. na nikashtuka mara moja na kwa hakika madhumuni ya barua hiyo ilikuwa ni yenye maana kuwa Allah swt pamoja na Malaika na watu wote wanamlaani yule mtu ambaye anaila hata Dirhamu moja kutoka mali yetu (haki yetu sisi Saadat). Hata kama hatakuwa akidhani kuwa ni halali kwa ajili yake.

 

Pamoja na hayo zipo hukumu za Khums zipo riwaya nyingi mno.

 

 

2. KHUMS ILIYOFARADHISHWA, AINA NA MATUMIZI YAKE

Khums imefardhishwa katika vitu saba :

  1. Ngawira (mali inayopatikana vitani kwa kushinda)

 

  1. Hazina inayopatikana kwa kutumbukia majini

 

  1. Hazina

 

  1. Faida itokanayo na biashara

 

  1. Mali halali iliyochanganyikana na mali haramu na kiasi chake kisijulikane.

 

  1. Ardhi ile ambayo Kafiri Dhimmi anainunua kutoka Mwislamu.

 

  1. Madini kama dhahabu, fedha, chuma, shaba, mafuta, Firozah, ‘Aqiiq, chumvi n.k.

 

Kila kifungu kina hukumu zilizoelezwa kwa marefu na mapana katika vitabu vya Fiq-hi.

 

Khums inatakiwa kugawiwa sehemu mbili :

1.       Sehemu ya kwanza ni haki ya Saadat ambao ni masikini, mafukara au ambaye ameishiwa katika safari

2.       Sehemu ya pili ni ya Al-Imam Muhammad Mahdi, sahibuz-zamaan, a.s. ambaye kwa sasa yupo ghaib na hivyo kumfikishia Naibu wake ambaye ni Mujtahid Jame’ Sharait au kutumiwa katika kazi ambazo Mujtahid Jame’ Sharait ameruhusu.

 

Katika kitabu cha Kalimat Tayyibah kumeandikwa hekaya zaidi ya arobaini ambazo zinaonyesha namna ya kufanya uwema pamoja na Saadat na faida zilizopatikana kwa kufanya mapenzi na meam pamoja nao. Sisi tunawaleteeni hekaya moja ambayo imenakiliwa kwa kupitia mifululizo mingi ya walioyoifikisha katika Muntakhab Ad-diin, Kitabu fadhail Shaadhaan na Tohfatul Azhar na wasilatul al-Mal kuwa :

‘Ibrahim bin Mahran kwamba katika mji wa Kufah kulikuwa na jirani yangu aliyekuwa akiitwa Abu Ja’afar, mtu mwenye heshima kubwa sana. Kila Sayyed aliyekwenda kwake kumwomba chochote, yeye aliwapa na alipolipwa alipokea na pale ambapo alikuwa halipwi, alikuwa akimwambia karani wake aandike kuwa Al Imam 'Ali ibn Abi Talib  a.s. amekopa kiasi hicho. Hivi ndivyo ilivyokuwa ikiendelea kwa muda mrefu, na kwa bahati mbaya ulimwijia wakati mbaya ambapo yeye alifilisika na kuwa fakiri.

 

Siku moja alipokuwa amekaa nyumbani kwake huku akiangalia daftari lake la madeni aliyokuwa akiwadai watu. Kwa kila jina la mtu aliyekuwa hai, alimtuma karani wake kwenda kufanya madai na kwa yule aliyefariki, iwapo ameacha mali, basi aliwaomba jamaa wamlipe. Na kwa yule ambaye hana arithi wala hakuacha chochote cha kuweza kufanya madai yake, yeye alikuwa akichora mstari.

 

Katika siku hizo hizo, siku moja alipokua ameketi nje mlangoni mwake huku akiliangalia daftari lake la madeni, kulipita mpinzani wake mmoja ambaye alimdhihaki kwa kumwambia ,”Je Al Imam 'Ali ibn Abi Talib  a.s. amekufanyiaje, je amekulipa madeni yako ?”

 

Kwa kuyasikia hayo, alihuzunika mno na akaondoka zake.  Basi usiku huo alimwota Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. akiwa pamoja na Al-Imam hasan a.s. na Al-imam Hussayn a.s. katika ndoto yake. Mtume s.a.w.w. aliuliza ‘Je baba yenu yuko wapi ? Al Imam 'Ali ibn Abi Talib  a.s. ambaye alikuwa yupo nyuma ya Mtume s.a.w.w. alijibu. ‘Naam, nipo hapa.Ewe Mtume wa Allah swt !’

 

Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. alimwuliza Al Imam 'Ali ibn Abi Talib  a.s. , “Je ni kwanini haumlipi huyu mtu haki yake ?”

 

Al Imam 'Ali ibn Abi Talib  a.s. alijibu’ “Ewe Mtume wa Allah swt ! Mimi nimemletea haki yake yote.”

 

Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. akamwambia, “Basi mpe achukue.”

 

Al Imam 'Ali ibn Abi Talib  a.s. alitoa mfukoa mmoja mweupe na  kumpa huyo mtu na kumwambia, “Hii ndiyo haki yako.”

 

Hapo Mtume Muhammad Mustafa s.a.w.w. akasema , “Pokea haki yako na siku yoyote utakapoijiwa na watoto wake kwako kwa kukuomba chochote, na unacho basi uwape na kamwe usiwanyime. Nenda kamwe hautakuwa na shida wala dhiki ya aina yoyote ile.”

 

Mtu huyo analezea kuwa alipofumbua macho yake kutoka usingizini, aliukuta mfuko ule ule ukiwa mkononi mwake na alimwamsha mke wake na kumwambia awashe taa. Anasema, “Nilipofungua mfuko huo, kulikuwa na Ashrafii elfu moja kamili.” Mke wangu aliniambia kuwa inawezekana mimi nimekopa mali hiyo kutoka kwa matajiri, nikamwambia kuwa sivyo na hapo nilimsimulia kisa kizima. Baadaye nilikichukua kidaftari changu na kuanza kupiga hisabu ya deni la Al Imam 'Ali ibn Abi Talib  a.s. ambalo nilikuwa nikiwapa Saadat na nikakuta kuwa jumla yake imekuwa ni Ashrafii elfu moja kamili kama alivyonilipa Al Imam 'Ali ibn Abi Talib  a.s.  Hakukuzidi wala kupungua !


 

10.  SADAQAH   NA   MISAADA: 

 

WANANYUMBA WANAOSTAHIKI MALIPO

Wanaostahiki malipo ni mke ( wa ndoa ya kudumu ) mtiifu na watoto wake na watoto wa watoto wake na vile inavyoendelea kuteremka chini na ambao anahitaji msaada basi ni faradhi. Vile vile baba na mama na babu mzaa baba na mama mzaa mama na vile itakavyoendelea juu na iwapo wanahitaji msaada wake na watu wngineo basi na kwa kiasi cha uwezo wake kama anao na iwapo hatawapa basi atatazamwa miongoni mwa watu kama qata’ rahmi . Na jambo hili limezungumziwa katika makala mengineyo.

 

 

 

1.      SADAQAH ZILIZO SUNNAH

Zipo aina nyingi za malipo yaliyo Sunnah. Katika Ayah na riwaya nyingi mno kumesisitizwa mno kuwa sadaqah itolewe hususan katika siku ya Ijumaa, Siku ya ‘Arafah, katika mwezi Mtukufu wa Ramadhani itolewe kwa makhususi ya majirani, majamaa n.k. Vile vile Sadaqah ni dawa ya ugonjwa, huondoa balaa, huleta riziki, huzidisha mali na huepusha vifo vya kutisha kama kuungua moto, kuzama maji  na kuwazuia Majinni na kwamba huondoa balaa sabini. Kila utakavyotoa sadaqah zaidi basi matokeo yake pia yatakuwa ni mazuri zaidi. Wala haina kiwango kidogo, kiasi chochote mtu atakachokitoa kitatosha walau hata kama atatoa kokwa moja ya tende basi itatosha !

 

 

2.      ZAWADI

Ni kitu ambacho mtu mmoja anampa mtu kwa ajili ya kuongezea urafiki ama awe masikini au tajiri. Na iwapo hivyo itakuwa kwa nia ya kutaka furaha ya Allah swt, basi itakuwa ni ‘ibada bora kabisa.

 

Imeripotiwa kutoka Al Imam 'Ali ibn Abi Talib  a.s. katika Al-Kafi J.5, Uk. 144  kuwa :

“Iwapo mimi nitapenda kumpatia kitu rafiki yangu basi mimi nitampa zawadi kwani ninaipenda zaidi kuliko Sadaqah.”

 

3.      UGENI NA UKARIMU

Zipo riwaya nyingi mno kuhusu kuwakarimu wageni na kamba hiyo ndiyo tabia njema ya Mitume a.s. Ipo riwaya moja kuwa Al Imam 'Ali ibn Abi Talib  a.s. kwa muda wa siku saba hakupata mgeni nyumbani kwake basi alisema huku akilia :

“Nasikitika mnona ninakhofu kuwa isije Allah swt akaniondolea rehema na baraka zake.”

 

 

4.  HAKI ILIYO MAALUMU NA ISIYO MAALUM

Inatubidi sisi tuwe tumepanga viwango maalumu vya kila siku au kila wiki au kila mwezikatika mali zetu kwa ajili ya wale wenye shida na kwa ajili ya majamaa zetu ili kukidhi mahitaji yao.

 

Amesema Allah swt katika Quran: Surah al- Ma’arij,   , Ayah 24 – 25 :

xxxxxx

 

Al Imam Musa bin Ja’afer a.s. amepokelewa riwaya kuwa  :

“Katika ukoo wa Bani Israil kulikuwa na mtu mwema ambaye alikuwa mke aliye mwema pia. Siku moja aliota ndoto ambamo aliambiwa kuwa Allah swt amempangia kiasi fulani cha umri wake ambapo nusu ya umri huo utapita katika raha na mustarehe wakati nusu ya umriuliobakia utapita katika shida na dhiki na umasikin.

 

Hivyo Allah swt amekupa fursa wewe kuchagua iwapo utapenda kupitisha umri wako wa nusu ya awali ya raha na mustarehe na baadaye dhiki na umasikini ? Hivyo chagua mojawapo. Kwa hayo mtu huyo alijibu kuwa : ‘Mimi ninaye mke wangu aliye mwema na hushirikiana naye katika maswala yote, hivyo nitapenda kupewa muda wa kuweza kuongea naye kabla sijatoa uamuzi wa chaguo langu.’

 

Mke wake alimshauri mumewe kuukubalia umri ule wenye neema uwe ndio wa kuanzia kwani: ‘Inawezekana Allah swt anataka kututeremshia neema na baraka zake hivyo tukaongoka.’

 

Hivyo usiku uliofuatia, bwana huyo aliulizwa jibu alilifikia katika uamuzi wake. Naye akajibu : ‘Mimi ninataka kuupitisha nusu ya umri wangu katika neema, raha na mustarehe.’ Kwa hayo akajibiwa kuwa hivyo ndivyo itakavyokuwa kwa mujibu wa chaguo lake. Kuanzia hapo yeye alijaaliwa kila aina ya raha na akawa tajiri mkubwa mwenye mali na milki nyingi.

 

Katika kutajirika huku, mke wake akamwambia, ‘Ewe Bwanangu! Usiwasahau kuwasaidia na kukidhi haja za majamaa zetu na mafukara na masikinina uwe na uhusiano mwema pamoja na. na uwazawadie watu fulani fulani wakiwemo majirani na marafiki, zawadi mbalimbali.’

 

Mtu huyo alizingatiana kutekeleza ushauri uliokuwa umetolewa na mke wake. Na hivyo alifungua milango ya kugawa mali yake katika masuala hayo hadi ulipofika akati wa kuisha kwa nusu ya umri wake wa awali.

 

Kuisha huku kwa nusu ya kwanza ya umri wake, aliota ndoto tena ambamo aliambiwa kuwa :’Kwa kutokana na uwema wako wa kuwasaidia wenye shida na dhiki imekuwa kipaumbele kwako, basi Allah swt amekubadilishia sehemu hii ya pili kuwa katika raha na mustarehe kama ilivyo sasa.’”

 

 

 5.  HAKI YA UVUNAJI

Wakati wa mavuno kwa kiwango kile ambacho bado Zaka haijapigiwa hisabu, inagawiwa kwa kuchota mkono moja kwa wapita njia kama vile alivyosema Allah swt katika Quran: Surah 69, Ayah 141 :

xxxx

Katika aina za Sadaqah, aina hizi mbili za sadaqah ni Sunnah kwani Ayah ya Qur'an Tukufu pamoja na riwaya nyingi zimezungumzia na kusisitiza na ndio maana zimezungumziwa mbalimbali.

 

 

6.  KUKOPA MADENI

Yaani kuwakopa Waislamu ambao wanashida ya kukopa deni ili kukidhi masuala yao. Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema, katika Al-Kafi :

“Katika mlango wa Jannat kumeandikwa ‘Yapo mema kumi kwa mtoa Sadaqah na mema kumi na nane kwa mkopeshaji madeni.’”

 

Vile vile Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. amesema, katika  Al-Wafi :

“Wakati Mumin mmoja anapomkopesha Mumin mwenzake deni kwa ajili ya kutaka ridhaa ya Allah swt , basi Allah swt anihisabia deni hilo katika Sadaqah hadi kulipwa kwake.”

 

Kila mara mtu atakapokuwa akimpa muhula mdaiwa wake kulipa deni lake, basi Allah swt atakuwa akimwandikia kuwa ametoa Sadaqah kiasi hicho kwani yeye alikuwa na haki kamili ya kufanya na kulazimisha malipo lakini hakutumia nguvu kudai na badala yake amemwongezea muda mdaiwa wake, hivyo inamaanisha kuwa amemkopa mara mbili katika mali hiyo. Hivyo mtu huyo anakuwa mustahiki wa kupata thawabu za kutoa Sadaqah ka mara ya pili.

 

Vile vile Al Imam Ja'afer as-Sadiq a.s. ameripotiwa akisema kuwa :

“Kwa kupuuzia ‘Ma’un’ (mambo ya nyumbani ) ambayo Allah swt ameahidikatika Qur'an Tukufu  adhabu, basi si Zaka inayozungumziwa, bali ni kuwasaidia kwa kuwakopa wale wenye shida na wanaodai kuwapa vitu vya nyumbani.”



[1]  Viwango hivi vimeletwa mbele yenu kwa kimukhtasari tu ili kuweza kuwapa mwanga juu ya masuala haya na hivyo inatubidi sisi turejee vitabu vya Fiq-hi ili tuweze kujua hukumu za Shariah kwa undani zaidi katika masuala haya na mengineyo.



[1]       MAADILI YA ISLAM:    Nafs  aina na sifa zake

Masomo ya akhlaq- maadili katika Islam ni mojawapo ya bora ya sayansi na inamwelekeza asomaye hadi katika elimu ya kujielewa nafsi yake mwenyewe ambayo Islam inaamini kuwa ni fardhi. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema: “Yeyote yule aliyeitambua nafsi yake (mwenyewe) basi hakika ametambua Allah.”

 

Hivyo hivyo kuna mapokezi mengi ya habari kuhusu umuhimu wa somo hili hata Mtume Mtukufu (s.a.w.w) amebainisha kuwa: “Mimi nimetumwa kuja kukamilisha maadili.

 

Tuanze kuzichambua aina za nafsi alizonazo mwanadamu vile alivyo:

 

Hapana shaka kuwa mwanadamu hana zaidi ya moja, lakini hii nafsi au roho inayo masharti fulani fulani. Kwa hiyo, hali ya kuonyesha kama ‘nafsi ya kujilaumu’ ‘au nafsi ya kuamrisha’ ‘nafsi inayotosheka’ (kama vile vielezwavyo katika Qu’rani), na hivyo haidhihirishi idadi ya nafsi. Upande mwingine, yote haya ni miongoni mwa ngazi za sifa ambazo zinaleta kwa ukamilifu na ustawi wa hali ya nafsi, pamoja na yale yanayoozesha nafsi na kuleta maovu.

 

NAFSI SAFI AU THABITI (nafsi au thabiti.)

 

Katika Qur’rani Tukufu, aina mbili hizo za masharti za nafsi zinaelezwa:-“Isipokuwa mwenye kuja kwa Mwenyezi Mungu na moyo safi” (26:89)

 

Uhalisi huu ni aina ya moyo, na moyo halisi (safi) ni ule ambao haufungamani na upande wa kuhangaika wala upande ule wa wapotofu.

 

Imenakiliwa kutoka kwa Imamu Sadique (a.s) kuwa: “Moyo ulio msafi- halisi ni ule   ambamo hakuna chochote kile ila Allhah (s.w.t) tu”

 

Katika hali hii, Nafsi imetunukiwa hatua mojawapo ya umuhimu kuwa kamilifu. Hivyo inamaanisha kuwa hakutakuwa na mapenzi mbali na ile ya Allhah tu.

 

Kuna habari nyigine iliyonakiliwa kutoka kwa Mtume Mtumfu (s.a.w.w.) ambamo twaambiwa: “Imani ya mtu haitokamilika hadi hapo mimi niwe mpenzi wake kuliko hata baba yake, mama yake, watoto wake mali yake na hata kuliko maisha yake.”

 

Ndivyo hivyo, nafsi safi ni nafsi ambamo hakuna mapendo mengine yoyote yale isipokuwa Allah (s.w.t.) na wale wapendwao kwa ajili ya Allah (Mtume na Ahali yake)

 

NAFSI YENYE KUTUBU (al-Nafs al- Muniib).

 

Sharti lingine la moyo au Nafsi ni ‘kutubu’ na hivyo huitwa moyo wenye kutubu au nafsi yenye kutubu. Hivyo huwa daima inarudi kwa Mwenyezi Mungu.

 

“.. Na anayemuogopa ( Mwenyezi Mungu Mwingi wa kurehemu, na hali ya kuwa humuoni na akaja kwa m oyo ulioelekea ( kwa Mwenyezi Mungu).” (50:33)

 

Kuwa na khofu ya Mwenyezi Mungu pale mtu awapo peke yake ni mojawapo ya masharti bora ya nafsi, na hii ina maanisha kuwa nafsi imemtambua Allah (s.w.t) kiasi kile kuwa hakutakuwa na tofauti yoyote itakapokuwa pekee yake au katika kundi la watu. Hata kama hakutakuwa na mtu yeyote karibu nayo, basi ile khofu ya Allah (s.w.t.) imo ndani yake thabiti. Hii haipo katika kundi la zile nafsi zilizo ghafilika katika maasi na matendo maovu wakiwa katika kundi la watu au wakati wengine watakapokuja julishwa, na hawatajizuia nayo na hata kama iwapo watakapopewa habari zilizo bainika. Hii ni ile aina ya nafsi ambayo haielewi kuwa Mwenyezi Mungu yupo anaangalia yote na Aliye dhahiri popote pale na kwa hakika aina hii ya nafsi haipo pamoja na Allah na wala haitorudi kamwe kwa Allah.

 

NAFSI MWONGOZI (al- Nafs al- Muhtadi).

Sharti lingine la nafsi ni ile iongozwayo. Qur’rani inatuambia: (64:11).

 

“..Anayemuamini Mwenyezi Mungu huuongoza moyo wake”

 

Mtu ambaye moyo wake ukiwa umeongozwa na kujitosa katika habari ya imani na sheria Tukufu za Allah (subahana wa Tala), yeye anaielewa njia yake vyema kabisa. Zile imani atakazokubalia na matendo yake yale yampasa kuyatenda huwa ni dhahiri kwake kuelewa vyote hivyo kwa uadilifu.

 

NAFSI ILIYO RIDHIKA (al-Nafs al- Mutmaina)

Sharti lingine lijulikanalo vyema la moyo au nafsi ni “kuridhika. Qur’an:

“ Sikiliza: Kwa kumkumbuka Mwenyezi Mungu nyoyo hutulia. “(13:28)

 

Na vile vile mwishoni mwa sura al-Fajr twaabiwa (89:28)

“Ewe nafsi yenye kutua”!

“Rudi kwa Mola wako, hali ya utaridhika...”

 

Nafsi iliyo ridhika ni ile iliyokwisha ridhika, ina maanisha kuwa mtu yupo anapigana vita vikali na matakwa yake na kwa kuyatimiza yale yaliyo fardhi kwake katika dini na kujiepusha na yale yaliyoharamishwa, na anajipa umuhimu kwa kuelimisha na kuikamilisha nafsi yake hadi hapo yeye hapindukii kutii chochote kile isipokuwa Allah (swt) tu. Ni marufuku kwake kuelekea pale penye madhambi na huwa ni mwenye kupenda amani na utulivu na huwa ni mwenye kujiridhikia mwenyewe hadi hapo yeye huwa thabiti kama jabali madhubuti. Hakuna madhambi, matakwa ya ubinafsi, tamaa, mvutano wa dunia, mapenzi ya mali au cheo yatakayoweza kuja kumpotosha yeye na kumwelekeze pengine na vile vile hakuna sheitani atakayeweza mghalimu na kumpotosha yeye.

 

Hali ya juu kabisa ya sharti hili kama ilivyokuwa katika Mtume mtukufu (s.a.w.w.) na ma - Imamu (a.s.), waliokuwa halisi kuwa hata mawazo ya kutaka kutenda madhambi hayakutokea kamwe.

 

AL-NAFS AL-MUTTAQI (nafsi ya tahadhari ya uadilifu):

 

Sifa nyigine ya nafsi inajulikana kama uangalifu wa uadilifu wa nafsi, (The virtuosly cautious self) nafsi ambayo imejaa kwa khofu na tahadhari. Hali hiyo inatokana na nyakati fulani kwa kupotoshwa na (kwa akili na roho) huzungukwa na uchafu na ubovu ili nafsi iingie sharti sawa sawa na itahadharishwe na madhambi. Nafsi ikiwa katika hali  hiyo huitwa nafsi ya tahadhari ya uadilifu:-

“.......Anayezihishimu alama za (dini ya ) Mwenyezi Mungu, basi hili

ni jambo la katika utawala wa nyoyo. “(22:32)

 

Kwa mtu yule ambaye imani yake inafikia kiwango hiki cha “Taqwa” kiwango cha tahadhari ya uadilifu, huheshimu na kumthamini Allhah (s.w.t.) na yele yote yaliyotolewa ishara nae kama Dini, Msikiti, sheriah, waumini wake Makka Ka’aba Tukufu n.k. kwa ufupi. Chochote kile kinachohusika na Mungu huwa kina kuwa na umuhimu na ta ‘adhima kubwa kwa mtu kama huyu wa namna hii. Na hii ndiyo kwa hakika matokeo ya  ‘taqwa’

 

NAFSI NYENYEKEVU (al- Nafs al- Mukhbit)

 

Hali nyingineyo ya Nafsi ni unyenyekevu (uvumilivu), yaani humaanisha kuwa mtu mwenye nafsi hali hii huwa mnyenyekevu mbele ya maamrisho ya Allah (swt)

 

Kwa mara nyingine tena twaambiwa katika Surah al Halj: (22:54)

“..waiamini, na ili zinyenyekee kwake nyoyo zao”

 

Kwa sababu nyoyo hizi hujiimamisha chini mbele ya Mungu na maamrisho yake, na wale wenye kuwa na nyoyo hizo hujiwakilisha kwa Allhah s.w.t  hawavunji kamwe maamrisho  ya Mwenyezi Mungu na wala hazisaliti au kuzipinga.

 

NAFSI HALISI (al-Nafs al-Zakiyyah):

 

Aina nyigine ya nafsi ni ile nafsi au roho iliyo mtakatifu (the pure self). Katika Qur’ani Tukufu, Mwenyezi Mungu anakula kiapo cha jua, mwezi mbingu, ardhi na vitu vingine na baadaye akisemea nafsi, anatuambia:

“Bila shaka amefaulu aliyeyeitakasa (nafsi yake) na bila shaka amejihasiri aliyeiviza (nafsi yake)” (91:9 & 10)

 

Ni dhahiri kuwa inambidi mtu afanye jitihada ili kufikia hatua hii. Kabla ya yote yale mengineyo, nafsi lazima iwe huru kutoka sifa zote zile zilizo ovu na hapo ndipo uwanja utakuwa tayari kwakuzitambulisha sifa zilizo nzuri na bora kabisa na kwa uanzishaji na uendelezaji. Mtu ambaye nafsi yake itatakasika, basi amehakikishiwa msamaha (ukovu) na kufikia kipeo cha furaha ya milele. (The person whose self become purified is assured of salvation and bliss!)

 

NAFSI YA KUKARIPIA - LAUMU (al-Nafs al- Lawwama).

Inawezekana wakati mwingine kuwa hivyo kwa vyovyote vile na kiasi chochote kile cha madhambi ayafanyayo, mtu  hajisikii chochote cha kutenda kosa, wala hasikitiki, wala hajilaumu mwenyewe. Nafsi kama hiyo ni ile iliyoshindikana. Hata hivyo, ile nafsi baada ya kuanguka na kutenda madhambi na itajikaripia yenyewe na kujishutumu yenyewe, kabla ya yeyote yule kufanya hivyo, basi imeingia katika sharti tukufu mojawapo la nafsi itakiwavyo kuwa. Qur’ani Tukufu inatuelezea:

“Naapa kwa siku ya Kiama. Tena naapa kwa nafsi inayojilaumu; (kuwa mtafufuliwa na mtalipwa)”. (75:1-2).

 

Ni dhahiri kuwa iwapo Mwenyezi Mungu akiapia kwa vitu, basi kuna utukufu wake humo. Nayo pia ni wazi kuwa yeyote yule aifunzae nafsi yake vyema hadi ule wakati wa kutenda madhambi, yenyewe (nafsi) hujaa masikitiko na kujilaumu, basi imefikia mojawapo ya vina vya utakatifu.

 

NAFSI ILIYOFUNGULIWA HERI (al-Nafs al-Mulham):

Sharti lingine la nafsi ni kuongozwa na Mungu. Twaambiwa kaika Qur’ani:

“ Kisha akaifahamisha uovu wake na wema wake”  (91:8)

 

Maongozi haya ni kutia moyo kwa nafsi wakati itapokuwa katika hali ya kutakasika- ‘Nafsi halisi si’ ambayo tumeishaizumgumzia. Ni lazima iwapo nafsi itaelekezwa kwa mujibu wa madhambi basi muongozo na kufunguliwa kwa heri kutoka kwa Allah (swt) yatafikia kikomo chake.

 

Kwa kupingana na sifa na masharti ya nafsi ambazo ni sababu ya furaha ya milele na utakatifu, baadhi ambazo zimekwisha tajwa hapo awali, pia hapo hapo kuna sifa na masharti yanayosababisha maovu ya nafsi, sasa tuziangalie.

 

NAFSI YENYE MADHAMBI (al-Nafs al-Athima):

 

Iwapo roho au nafsi ya mtu ikiwa na tabia ya kutenda madhambi, basi huitwa yeye madhambi. Qur’ani inazungumzia kulipa kwa amana:

“Na atakaeficha basi hakika moyo moyo wake ni wenye kuingia

       dhambini.”(2:283)

 

Hii inathibitisha kuwa nafsi ya yeyote yule ambaye ameshajizoelesha madhambi ni nzito na ni wazi na tayari kwa kutenda madhambi wakati wowote ule.

 

NAFSI ILIYO SINZIA (al-Nafsal-Ghafil)

 

Sababu mojawapo ya kushidwa na kufifia kwa nafsi ni kulegea au kusinzia au kuwa zembe. Kwa kutenda mambo maovu na kwa kuendelea kutenda madhambi ndiko kunakosababisha nafsi kuelekea palipo paovu na kutomsikia Allah (swt). Anaelezea Mwenyezi Mungu katika Qur’ani Tukufu

 

“Wala usiwatii wale ambao tumezighafilisha nyoyo zao wakafuata

          matamanio yao...” (18:28)

 

NAFSI ZILIZOTIWA MUHURI (al-Nafs al- Matbu)

 

Hapa inamaanisha kufungwa muhuri juu yake na hivyo ndivyo hatua ya mwisho  ya kungwa, inatuambia:

“Na watakaokuwa na uzani khafifu, basi hao ndio waliozitia hasarani nafsi zao    kwasababu ya kuzifanyia ujeuri Aya zetu.”

 

Popote pale mtu anapokuwa fidhuli au juvi kuelekea Allhah (swt) hadi kudharau na kutokubali ujumbe wake na maamrisho ya Allah ambayo Mwenyezi Mungu ambazo amewekea mbele yake, au , iwapo yeye atazikubalia, anazipa umuhimu kidogo na kuwa na kosa la upinzani basi hapo moyo wake unaingia katika hatua ile ambayo ni sawa na kama tahadhari, maamrisho Matukufu na yale yaliyo haramishwa hayatakuwa na athali yoyote ile kwake yeye. Na hii ni hatua mojawapo ya kudidimiza kwa nafsi na kushindwa kwake.

 

NAFSI ILIYO POFUKA ( al-Nafs al- Amya):

 

Hali nyingine ya Nafsi ni kupofuka. Qur’ani inatuambia kuwa:

“Kwa hakika macho hayapofuki, lakini nyonyo ambazo zimo vifuani ndizo zinapofuka. (22:46)

 

Nyoyo hizi zinaona vingine mbali na Allah (swt) na hazimwoni Mwenyezi Mungu. Nyoyo za aina hizi huona yale tu yatakayo yenyewe bila ya kuyazingatia yale maamrisho ya Allah (swt) na kwa hakika ndizo zilivyo kama vile vimepofuka tu.

 

NAFSI YENYE MARADHI (al-Nafs al-Maridha):

“Nyoyoni mwao mna maradhi, na Mwenyezi Mungu amewazidishia maradhi.”(2:10)

 

Ugonjwa wa aina hii inawezekana kuonekana mioyoni mwetu kwa sababu ya yale madhambi tuyafanyayo sisi siku hadi siku. Kama vile mtu mgojwa huwa hana hamu ya vyakula wala madawa ambavyo ni vyenye manufaa kwake na vile vile vyakula vizuri havitakuwa na ladha yoyote kwake, ndivyo vivyo hivyo kuhusu NAFSI iliyougua, kwani inapatikana kuonywa ( na Mwenyezi Mungu) na kukaribia kwa upole kwa mapendo na matakwa yake ya humu ulimwenguni na akhera kuwa yenye adhabu kali sana na yenye kutisha mno. Kilicho zaidi ni kwamba mtu aliyeugua hivyo ni yule mwenye, kuipendelea kwa ajili ya nafsi yake yale yote yaliyo mabaya na maovu, kwani huwa avutiwa navyo kama kambwa ndivyo vyenye kumfaa yeye. Kwa hakika hii ndiyo ile nafsi ilikwisha ugua; kama vile ilivyo kifo kwa mtu hatakayetibiwa magonjwa yake na hivyo ndivyo vinaweza kutokea kwa ajili ya aina hii ya nafsi iwapo haitoweza kutibiwa kabla ya ugonjwa kuenea pote na hatimaye mtu aweza kuangamia.

 

Popote pale mtu aonapo kuwa yeye hatamani chochote kile atakiwacho kukifanya yaani kumkumbuka Mwenyezi Mungu katika sala na kutii Sheria Tukufu za Dini ambazo hazimfai na ambazo ni chungu kwake, kwa hivyo ni wazi kabisa kuwa atambua kuwa huo moyo wake umeshaanza kuugua maradhi, na bila ya kisita inambidi afanye kila hila awezayo ili ajielekeze kwa mujibu wa aya za Qur’rani Tukufu, kwa watawa na walio waumini halisi na wale walio hodari katika elimu na ujuzi huu: waganga waa moyo, i.e.., wanavyuoni waelewao na wafuatao mienendo ya Mtume Mtukufu (s.a.w.w.), ili waweze kuitibu nafsi  ya aina hiyo iliyopatwa na maradhi.

 

NAFSI INAYOKWENDA UPANDE (al-Nafs al-Za’igha):

 

Moyo au Nafsi pia inaweza kusemwa kuwa inakwenda upande au inapotoka. Aina hii ya Nafsi ni ile ichaguayo upotofu wakati ipatiwapo chaguo katika hali mbili ya wema na uovu.

 

Kama mategemeo yote ya maisha, katika sehemu zote za Imani, maadili na matendo, mambo yake yote yaliyo dhahiri na yale yote yaliyo batili mwake, mwanadamu daima anakubwa na mgawanyiko wa njia mbili mbele yake , mtu ambaye amefaulu na kufurahika ni yule ambaye daima anachagua njia ile aitakayo Mwenyezi Mungu. I.e njia iliyo nyooka (Sirat al-Mustaqeem) ya dini katika kila hali. Hata hivyo, mtu ambaye moyo wake unampotosha, huwa daima ndiye achanguaye njia ya upotofu

 

Katika Qur’ani, kuzungumzia mifano na mafumbo ya aya na kwa kuelezea wazi wazi, Mwenyezi  Mungu anatuambia:

“Wale ambao nyoyoni mwao mna upotofu wanafuata zile zinazobabaisha kwa kutaka kuwaharibu watu kutaka na kujua hakika yake vipi.”(3:7)

 

Hivi kwa kuchagua mfano (mutashabih au allegorical) wa aya za Qur’ani ili kuitumia Qur’ani kwa kuhakikisha matakwa ya mtu binafsi ni sampuli ya ile nafsi iliyopotoka.

 

NAFSI YA MOYO MGUMU (al-Nafs al-Qasiya)

 

Sharti lingine la nafsi kuwa hivyo ni kutokana na moyo mgumu na katili.

“....Na tukazifanye nyoyo zao kuwa ngumu” (5:13)

“....Kwa hivi nyoyo zao zikiwa ngumu” (57:16)

 

Hali kama hii inaelezewa katika aya zinginezo pia. Nyoyo kama hizi zina sifa kama zile za jiwe na chuma, kuwa hakuna chochote kile kiwezacho kuathiri au kuacha alama yoyote juu yake ila kwa mshindo mkali tu moto. Hadi kufikia hali ya moyo kuwa mgumu kiasi hiki ni dhahiri ikionekana vile maovu yalivyo mteka huyo mtu hadi akawa mtumwa wa matakwa na maovu yake. Kwa hakika imepotoka!

 

NAFSI WASIWASI (al-Nafs al-Murtaba):

 

Nafsi ya aina hii imo katika hali hii ya wasiwasi kuhusu vile vitu iipasavyo kuvijua na kuviamini. Shaka kuhusu mizizi ya dini ya Islam kama vile kushuka kuwapo kwa Allah (swt), akhera, Unabuwa na vile vile Uimamu (a.s.), na kushuku matawi ya Dini kama vile sala, saumu na mema na mengineyo mengi.

 

“Nyoyo zao zina shaka; kwahivyo wanasitasita kwa ajili ya shaka yao.” (9:45)

 

Hii ni mojawapo ya sababu ya upotofu wa Nafsi na ni fardhi kwa watu wale walio katika hali kama hii kujielekeza hadi aya za Quarani na hadithi Tufuku za Mtume (s.a.w.w.) na ma -Imam (a.s.) na kwa wanavyuoni wa dini ili kuweza kutokomeza hali hii kabla ya kutanda juu ya Nafsi nzima undani mwake. Ama sivyo, iwapo hali kama hii haitashughulikiwa na badala yake ikapuuzwa na kubakia Nafsini, basi itamwelekeza mtu katika hali ya kukatiza na kukataliwa (kupuuzwa na kudhoofika).

 

NAFSI ILIYOPATA KUTU (al-Nafs-al-Ra’ina):

 

‘KUTU’ ni shida nyingineyo ambayo nafsi inaweza kupatwa kwani ni sawa na ule mfano wa kioo cha kujitazamia, iwapo ile poda itabanduka basi hutaweza kujitamazama kiooni. Basi kioo cha moyo ambavyo ni sehemu ya umuhimu kwa ajili ya Mwenyezi Mungu utukufu wa ukamilifu wake, fadhila zake zitamorudishwa kwake, hazitoweza rudishwa iwepo itashika kutu, na hatimaye itaweza kupoteza ile nguvu ya kupeleka ujumbe wako kwa Mwenyezi Mungu.

 

Ingawaje mwanadamu hawezi kumtazama Mwenyezi Mungu kwa macho yake, lakini anao uwezo wa kumwona Mwenyezi Mungu, Utukufu wake na Ukuu wake kwa kupitia NURU iliyomo katika Nafsi yake. Nafsi ile ambayo imeshakwisha shikwa na kutu ambamo sasa hakuna uwezo wa kurudishia (reflect ) kutoka na kwa Mwenyezi Mungu, basi bila shaka itatapatapa huko na huko ikimtafuta sheitani na hasa kwa mujibu wa matilaba yake. Qurani ikiwa inatumbusha kuwa:

 

“Sivyo hivyo! Bali yametia juu ya nyoyo zao (maovu) waliokuwa wakiyachuma.” (83:14)

 

Katika ‘aya hii twaelezewa vyema kabisa kuwa chanzo cha kupatwa kwa kutu kwa Nafsi ni kule kutenda madhambi. Kwa hivyo kila dhambi itatupia uzito (itatanda kiza juu ya moyo; na ifikiapo hali kama hii, inambidi mtu afanye Tawba mara moja kwa  ajili ya kuyasafisha hayo matendo maovu na atende matendo mema ili kuzuia kupotea kwa nuru iliyotunukiwa Nafsi yake. Vile vile, twaambiwa katika hadithi Tukufu kuwa: “Mtu mwenye furaha kuu katika siku ya Kiama ni yule atakaye yaona maneno aliyokuwa akiyatamka ‘naomba msamaha wa Mwenyezi Mungu’ chini ya kila dhambi alilolitenda. Kwa Hivyo inambidi kila Mwislam mmoja wetu apige msasa kila ovu alilolitenda ama sivyo, Mwenyezi Mungu azitowazo onyo zake za upole zitabadilika na kuwa ghadhabu kubwa sana.

 

NAFSI AMURU (al-Nafs al- Ammara):

 

Nafsi isiyofunzwa hasa wakati wa ujana wa mtu, huamuru kutendwa kwa matnedo ya madhambi bila kiasi. Katika Qurani, kuhusu kisa cha Mtume Yussuf, Nafsi inasemwa:

“Nami sijitasi  Nafsi yangu; kwa hakika (kila) Nafsi ni yenye kuamrisha sana maovu (12:53)

 

Sentensi hiyo inaonyesha kuwa ilitamkwa na Zuleikha aliyekuwa amependa Nabii Yussuf. Pale alipotoa ushahidi, alithibitisha kuwa ndiye chanzo cha uovu huo. Kwani Yussuf alikuwa hayupo wakati huo wa ushahid, lakini kwa kuwa Zuleikha alikuwa hana hila yoyote ile zidi ya Yussuf. Pia kuna uwezekano kuwa hayo yametamkwa na Yussuf au ni wote vyovyote vile, Qur’an inatuambia kuwa “Nafsi ni yenye kuamrisha sana maovu. (12:53)

 

Nafsi yoyote ile isiyokuwa imeongozwa kwa mujibu wa mfano ya Islam, huwa daima inavutwa popote pale penye madhambi na  ma’asiyah kwani yote hayo yako yamedhalilishwa kabisa. Mfano wa Nafsi hii ni sawa na mtoto mchanga atakaye kila kitu kuchezea bila kutazama ubora wake, faida au hasara zake, iliramdi yeye apate kuchezea tu, Nafsi ya yule aliye na utamaduni mzuri, aliyekomaa na kubaleghe inavutika pale penye mema na hujiepusha na matilaba yake; na ile nafsi elimishwa na inavutika pale penye maovu ya kila aina na  kwa hivyo lazima ifunzwe vyema, itasaidia kutakasisha hiyo Nafsi.

 

HATIMAYE: Kile kilichoelezwa hapo kinasema kuwa Nafsi inaweza kuwa bora kabisa ama mbovu  kabisa au vinazidiana katika vina na ngazi. Kuna nafsi zifikiapo kuitwa ‘Nafsi halisi na  ‘Nafsi ridhika’ n.k.  na vile vile kuna zinapofifia hadi kufikia hali mbaya kabisa na matokeo yake ni majanga, majonzi na maovu na kufikia ile sifa ya “kupigwa mihuri” au ‘zilizopofuka’ na ‘zenye maradhi’ zikiwa ni kama mifano.

 

Hali hii inadhihiridha kuwa Nafsi zinapangwa na kila mtu anayo Nafsi moja tu.

 

     JE UMEJING’AMUA UNA NAFSI YA AINA GANI UNDANI MWAKO??

                                         (JITAHADHARISHE)!

 

 

 

 

[2]Fadak 

Fadak kilikuwa ni kijiji kimoja chenye rutuba karibu na Madina huko Arabia na vile vile ilikuwa na ngome iliyokuwa ikiitwa ash-Shumrukh. (Mu'jamal buldan,j.4,uk.238;Mu'jam masta'jam,al-Bakri,j. 3,uk.1015;ar-Rawdhal-mi'tar,al-himyari,uk.437;Wafaa' al-wafaa,j. 4,uk.1280). Fadak ilikuwa ni milki ya Mayahudi katika mwaka wa 7 baada ya Hijri na umilikaji wake ulitoka kwao ukawa chini ya Mtume s.a.w.w. kwa mujibu wa mkataba wa amani.Sababu ya mkataba huu ni kwamba baada ya kuanguka kwa Khaybar,Mayahudi waliitambua nguvu na uwezo halisi wa Waislamu,na ushawishi wao kijeshi ulipungua na walishuhudia kuwa Mtume s.a.w.w. aliwasamehe baadhi ya Mayahudi walipoomba hifadhi,vilevile wao walituma ujumbe wa amani kwa Mtume s.a.w.w. na walionyesha nia yao kuwa Fadak ingeliweza kuchukuliwa kutoka kwao na kwamba eneo lao lisingeligeuzwa kuwa uwanja wa vita.Kwa hivyo,Mtume s.a.w.w. alilikubali ombi lao na kuwapatia amani,na ardhi hiyo ikawa ndiyo milki yake binafsi ambamo hakuna aliyekuwa na hamu na wala kusingaliwezekana kuwa na hamu;kwa sababu Waislamu wanayo haki ya kugawana katika milki zile ambazo wanazoweza kuzipata baada ya kupigana Jihad,ambapo milki inayopatikana bila jihad inaitwa fay' ambayo ndiyo milki ya Mtume s.a.w.w.peke yake na kwamba hakuna mtu mwingine yeyote aliyekuwa na haki humo.

 

Kwa mujibu wa kesi ya 'dai la Fadak' ni kwamba Bi.Fatimah az-Zahra a.s. alidai kuwa baba yake Mtume Mtukufu Muhammad s.a.w.w. alikuwa amempatia Fadak kama Zawadi (hibah)na alikuwa ni mrithi wa sehemu iliyopatikana ya baba yake ya khums ya khaybar na mali yake huko Madina.Tukio hili limeandikwa kama ifuatavyo katika Sahih Bukhari:

 

Imeripotiwa na Abdul Aziz bin Abdullah,Ibrahim bin Sa'd , Saleh na Ibn Shihab kuwa  wamepewa habari na Urwah bin Zubayr kuwa  imeripotiwa kutoka  Aisha kuwa baada ya kifo cha Mtume s.a.w.w. Bi.Fatimah a.s. alimwambia Abubakr ampatie ile haki  ya urithi wa Mtume s.a.w.w. ambao umepewa na Mwenyezi Mungu.Hapo Abubakr aliielezea hadith isemayo kuwa 'sisi Mitume hatuachi urithi,na sehemu yetu ni sadaqah' na hapo binti yake Mtume s.a.w.w. alighadhabika mno na tangia hapo aliacha kuzungumza na Abubakr mpaka kufariki kwake,kwani baada ya kifo cha babake,aliishi muda wa miezi sita tu. Aisha anaelezea kuwa Bi.Fatimah a.s. alidai urithi wa Khaybar na kiunga huko Madina,lakini Abubakr alikataa katakata kumpatia. Anaendelea Aisha kusema kuwa Abubakr alisema kuwa yeye hakuwa tayari kamwe kuachia kile alichokuwa Mtume s.a.w.w. akikifanyia kazi,bali nami pia nitaendelea kukifanyia kazi. Mimi ninaogopa katika kutahkiki iwapo nitaliachia katika amri za Mtume s.a.w.w. basi nitatoka katika haki na kuingia katika batili.Lakini ni dhahiri kuwa baada yake Abubakr,urithi wa Madina ulipewa Imam Ali a.s na Abbas. Lakini alibakia na Khaybar na Fadak huku akidai kuwa hivyo vilikuwa ni Sadaqah ya Mtume s.a.w.w. Mambo hayo yalikuwanayo hao wawili kwa mujibu wa matakwa yao."

 

Katika Sahih Bukhari kisa hiki kimeripotiwa mahala pengi (1) Kitabul Khums,mlango faradh khums, (2)Kitabul Fadhail As-habin Nabii katika  mazungumzo ya Abbas bin Abdul Muttalib (3) Kitabul Maghazi,mlango  wa Ghazwah Khaybar, (4) Kitabul Maghazi,mlango Hadith Bani Nadhiir, (5) Kitabul Faraidh,mlango Qaul Nabii  s.a.w.w.: hakirithiwi tunachokiacha Sadaqah. (6) Kitab al-I'tisaam bil kitaan wa Sunnatah.

 

Katika Bukhari,sehemu moja baada ya kuelezea kisa hiki cha dai la Fadak,imeelezwa hivi:

"Bi.Fatimah az-Zahra a.s. alikasirishwa mno na alimghadhabikia mno Abu Bakr kwa kumkatalia urithi wake,na kamwe hakuongea naye mpaka alipofariki,baada ya miezi sita tangu baba yake kufariki.Baada ya kifo chake,bwana wake Imam Ali a.s. alimzika wakati wa usiku na Abubakr hakuruhusiwa kushiriki katika mazishi na alimsalia mwenyewe.Watu walikuwa wakimstahi Imam Ali a.s katika uhai wa Bi Fatimah a.s. lakini baada ya kifo chake,watu walimgeuka Imam Ali a.s. na kwa sababu hiyo Imam Ali a.s alifanya Bay'a ya Abubakr baada ya miezi sita" (Sahih Bukhari:Kitabul Maghazi,mlango gazwa Khaybar)

 

Vivi hivi,kisa hiki kimeelezwa katika Sahih Muslim.Angalia Kitabul Jihad wal Siira,mlango kauli Nabii s.a.w.w.:La nurith maa tarakna fahuwa sadaqah yaani haturithiwi kile tulichokiacha,illa ni Sadaqah.

 

Kwa kuwa kisa hiki  kinapatikana katika 'sahihain" (vitabu viwili sahihi:Muslim na Bukhari) basi wanahadith wanaafikiana na kukubalia.Sasa nitapenda mutafakari juu ya kisa hicho hicho katika kitabu mojawapo maarufu  'tabaqaatil Kubra' kama vilivyo maarufu Sahih Muslim na Bukhari.

 

"Abubakr hakumpatia chochote Bi.Fatemah a.s. kutoka kile alichokuwa ameacha Mtume s.a.w.w. na kwa sababu hiyo Bi.Fatimah a.s. alimghadhabikia mno Abubakr na kamwe hakuzungumza naye hadi kufariki kwake.Bi Fatimah a.s. aliishi kwa muda wa miezi sita baada ya kifo cha Mtume s.a.w.w. Jaafer anaripoti kuwa Bi.Fatimah a.s. alimwijia Abubakr na kudai haki za urithi kutokana alivyoviacha Mtume s.a.w.w. na vile vile alikuja Abbas kuja kudai urithi wake. Imam Ali a.s. alikuwa nao.Hapo Abubakr aliwajibu kuwa Mtume s.a.w.w. alisema kuwa 'sisi mitume haturithiwi kwa kile tunachokiacha,huwa Sadaqah' na mimi ninafanya kile alichokifanya Mtume s.a.w.w.. Hapo Imam Ali a.s. alimjibu kuwa katika Quran Tukufu imeandikwa kuwa urithi wa Mtume Daud a.s. ulichukuliwa na Mtume Suleyman a.s. na Mtume Zakariyyahh a.s. aliomba dua ajaaliwe mtoto wa kiume ili aweze kuwa mrithi wake na wa Ale Yaaqub. Abubakr alimjibu kuwa ndivyo vivyo hivyo unavyotamka wewe lakini wewe unajua kile nikijuacho mimi. Imam Ali a.s. alimwambia kuwa hiki ni Kitabu cha Allah  kinachosema katika haqi yetu.Lakini Abubakr alikataa katakata na hapo wote watatu waliondoka kwa ukimya." (Tabaqaat Ibn Sa'ad,j.2,uk.86)

 

Vile vile Imam Tabari ameelezea kwa mapana zaidi katika historia yake.Rejea Tarikh al-Umam wal Muluuk,j.3,uk.202. Allamah Baladhuri ameongezea mwangaza zaidi katika swala hili:                      

"Abdullah ibn Maimun al-Maktub,Fasiil bin 'Iyaar na malik bin Jawza wamenakiliwa wakiripoti kutoka kwa baba yao kuwa Bi.Fatimah az-Zahra a.s. alimwambia Abubakr kuwa Mtume s.a.w.w. alimpatia zawadi na hivyo amrejeshee.Na katika kuthibitisha hivyo,Imam Ali a.s. alitoa uthibitisho wake na hapo ndipo Abubakr alitaka kuletwa mashahidi wengineo.Ummi Aiman alitoa shahada katika dai la Bi.Fatimah a.s. Hapo Abubakr alimwambia Bi.Fatimah a.s. kuwa "unaelewa vyema kuwa ushahidi haukubaliki hadi kuwepo na ushahidi wa wanamme wawili au mwanamme mmoja na wanawake wawili." Hapo Bi.Fatimah a.s. alirudi na kunijulisha hayo. Ruh al-Karabisi amenakili kwa mlolongo wa walioripoti kutoka  kwa Jaafer ibn Muhammad kuwa amesema kuwa Bib.Fatimah az-Zahra a.s. alimwambia Abubakr amrejeshee Fadak kwani Mtume s.a.w.w. alishamzawadia (hiba)Hapo Abubakr alidai aletewe mashahidi.Hapo Bi.Fatima a.s. aliwaleta Ummi Ayman na Rubah,mtumwa wa Mtume s.a.w.w. kutoa ushahidi nao walitoa ushahidi wa kuthibitisha dai la Bi.Fatimah a.s. Hapo Abubakr alisema kuwa ushahidi huo utakubaliwa pale  atakapo patikana mwanamme mmoja na wanawake wawili."

 

"Ameelezea Ibn Aisha Maitami kutoka Himad bin Salmah,kutoka Muhammad bin Saib Kalbi ambaye kutoka kwa Abu Salha ambaye ameelezea kutoka kwa Ummi Haani ambaye ameripoti kuwa Bi.Fatimah az-Zhra a.s. bintiye Mtume sa.w.w. alikwenda katika baraza la Abubakr na kumwambia 'utakapokufa wewe urithi wako ataupata nani?' Abubakr alijibu kuwa 'watoto na ahali yangu' Sasa je umekuwaje kuwa umechukua urithi wa Mtume s.a.w.w. na unakatalia kunipatia mimi mustahiki wake? Hapo Abubakr alimjibu kuwa 'mimi sijachukua dhahabu au fedha katika urithi wa baba yako na wala sikuchukua hiki au  wala kile.' Bi.Fatimah az-Zahra a.s. alimwambia'kuna hisa katika Khaybar na Fadak ni zawadi na milki yangu' Hapo Abubakr alimwambia:"Ewe Binti wa Mtume s.a.w.w.!  Mimi nilimsikia Mtume s.a.w.w. akisema kuwa Fadak ni kitu ambacho kinazalisha na kulisha ambapo Allah swt hunipatia humo riziki katika uhai wangu na pale nitakapofariki,itagawiwa Waislamu wote."

(Futuh al-Bayaan.Allamah Abul Hasan Bilazuri,chapa ya Misri,uk.44-45)