UTETEZI WA SHERIA ZA KIISLAMU

 

Muhtasari nne juu ya

Sheria mbali mbali binafsi Za kiislamu

 

Kimeandikwa na:

Allamah Sayyid Saeed Akhtar Rizvi

 

Kimetafsiriwa na:

Dr. Mohamed S. Kanju

 

Kimechapishwa na:

BILAL MUSLIM MISSION OF TANZANIA

P.O.Box  20033

Dar es Salaam

Tanzania

 
 

The .HTML version of this book is taken from
www.al-islam.org and ebooked by www.ShiaLibrary.com and www.islamkutuphanesi.com . May Allah be pleased with all.

 

 

 

Haki ya kunakili imehifadhiwa na:

ã Bilal Muslim Mission of Tanzania

 

 

 

 

 

ISBN    9987  620  26  4

 

 

 

Toleo la Kwanza: 2001,   Nakala:  2000

 

 

 

Kimetolewa na kuchapishwa na:

BILAL MUSLIM MISSION OF TANZANIA

S.L.P. 20033

DAR-ES-SALAAM

TANZANIA 

 

 

 

 

 

YALIYOMO

 

1.                Dibaji                                                                            4

 

2.                Historia Fupi Ya Mwandishi Wa Kitabu Hiki        5

 

 

3.                Utangulizi                                                                  11

 

 

4.                Muhtasari juu ya Sheria za ndoa uliwasilishwa

 

mbele ya Tume ya Serikali ya Kenya juu ya

           Sheria za ndoa n.k                                                     17

 

6.           Muhtasari juu ya Sheria za mirathi uliwakilishwa

          mbele ya Tume ya Serikali ya Kenya juu  ya

           Sheria za ndoa n.k                                                     28

 

7.           Muhtasari juu ya Waraka wa Tanzania juu ya

Sheria ya ndoa inayofanana sawa kwa wote       Imechapishwa katika Standard (DSM)

           Jumatatu, 8 Desemba 1969                                      42

 

8.           Muhtasari juu ya Hijabu na Mirathi

           uliwasilishwa kwa Mheshimiwa Al-Haj

           Sheikh Ali Hassan Mwinyi                                      56

 

9.           Barua ya Wizara ya Elimu Juu ya Hijabu             64

 

10.     Mahkama ya Kadhi: Baadhi ya Mapendekezo

Imechapishwa katika The Democrat (DSM)                                   17-23, Aug, 1999                                          65

 

 

DIBAJI

 

           Tunamshukuru Allãh (s.w.t.) na kwa baraka za Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na Ahlul~Bayt (a.s.) kwa kutujaalia kuweza kufanikisha juhudi zetu hizi katika kuchapisha kitabu hiki juu ya sheria za ki-Islamu.

 

           Kitabu hiki kilochopo mikononi mwako ni tafsiri ya kitabu cha kiingereza kiitwacho In Defense of Islamic Laws kilicho andikwa na Allamah Al-Haj Sayyid Saeed Akhtar Rizvi, Muasisi na Mhubiri Mkuu wa Mission hii.Kitabu hiki kimekua maarufu katika ulimwengu wa ki-Islamu.Watu wengi kutoka Afrika ya Mashriki wametuomba kukitafasiri katika lugha ya kiswahili.

 

           Tunamshukuru Dr, Mohammad Salehe Kanju kwa kukitafsiri kitabu hiki katika lugha ya kiswahili.

 

           Kwa manufaa ya wasomaji wetu tumeongeza makala juu ya Mahakama ya Kadhi ambayo ilitayarishwa na Mwandishi baada ya kitabu cha asili ya kiingereza kuchapishwa.

 

           Mission inatoa shukurani zake za dhati kwa Bwana Mahmood Khimji ambaye kwa juhudi zake kitabu hiki kinawafikia wasomaji wetu mikononi na Sayyid Murtaza Rizvi kukipanga vizuri katika kompyuta na wale wote wanaotuunga mkono kwa njia moja au nyingine kwa kufanikisha kuchapishwa kitabu hiki, Tunamuomba Mwenyezi Mungu (s.w.t.) awalipe malipo mema hapo Duniani na baadaye huko, Akhera.

 

Wamaa Tawfeeqi Illah Billah

 

BILAL MUSLIM MISSION OF TANZANIA

 

 

                                               

HISTORIA FUPI YA

MTUNZI WA KITABU HIKI

ALLAMAH SAYYID SAEED AKHTAR RIZVI


Hujjatul Islam Wal Muslimin Allamah Al-Haj Sayyid Saeed Akhtari Rizvi, alizaliwa katika Familia ya Maulamaa mwezi Mosi Rajab 1345 A.H. (5th Januari 1927 M.) katika mji wa Ushri Khurd, Wilaya ya Siwan, Bihar, India. Mazazi wake Marehemu Ustadul Ulamaa Sayedul Hukama Maulana Al-Haj Sayyid Abdul Hassan Rizvi (radhi za Mwenyezi Mungu Zimshukie) alikuwa Mmoja wa Maulamaa wakubwa wa India.

 

            Allamah Rizvi alianza masomo yake katika mji wa Gopalpur makazi ya jadi yake na kuendelea huko Patna na Banaras. Alifaulu Shahada ya juu katika mtihani wa lugha za Kiarabu, Kiajemi na Kiurdu kutoka (Chuo Kikuu cha) Allahabad Board, U.P., na akafanikiwa kupata Shahada ya juu zaidi ya elimu ya dini - "Fakhru 'L-Afadhil" kutoka chuo cha Jami'ul 'Uloom Jawadia, Banaras.

Kuanzia ujana wake, alikuwa akijishughulisha kikamilifu katika jamii, elimu na kuinua dini ya Jumuiya. Katika mwaka wa 1948, alichukuwa nafasi ya baba yake kama Imamu wa Jumuiya huko Hallaur katika wilaya ya Basti, U.P. na akaendelea na nafasi hiyo hadi mwaka wa 1951. Kuanzia 1952 - 1959 alifanya kazi kama Mwalimu wa Urdu na Kiajemi katika shule ya Sekondari ya juu ya Husainganj (huko) Husainganj, Siwani.

 

            Muda wa miaka yote hii alitumia likizo zake na wakati wake katika shughuli za Jumuiya kama kuendeleza shughuli za Anjumani Wazifa-e-Sadat-wa Momineen na Anjuma-e-Tarraqi-e-Urdu.

 

            Katika Mwezi Desemba 1959, alikwenda Tanzania (wakati huo ikijulikana kama Tanganyika) ambako alihudumia kama Imam wa Jumuiya huko Lindi (1959-1962) Arusha (1963-1964) na Dar es Salaam (1965-1969).

 

            Baada ya juma moja tu kuwasili kwake Afrika, alianza kujifunza lugha ya Kiswahili na kuangalia hali ya nchi kwa mtazamo wa kubalighisha Uislamu wa kweli miongoni mwa jamii ya wazawa (wa asili). Katika nyakati hizo kulikuwa hakuna Shia-Ithna-asheri hata mmoja mwenye asili ya Kiafrika katika bara lote. Katika mwaka wa 1962 alitayarisha mpango kwa ajili ya tablighi na akaupeleka kwa sekritariati ya Halmashauri Kuu ya Khoja Shia Ithnaasheri wakati huo ikiwa Arusha. Katika mwaka wa 1963 mpango huu ulijadiliwa kwa urefu. Katika hatua hiyo haukuweza kutekelezwa kama ilivyoshauriwa, lakini mwelekezo wa taratibu uliwekwa katika utekelezaji. Katika mwaka 1964 Sekritariati ilitayarisha taarifa (memorandum) iliyotegemea juu ya msingi wa taratibu yake ambayo iliwekwa katika agenda ya mkutano wa tatu wa mwisho wa mwaka wa muungano wa Jamati za Khoja Shia Ithna-asheri za Afrika (Federation of Khoja Shia Ithna-Asheri Jamaats of Africa) uliofanyika Tanga. Hivyo Bilal Muslim Mission ilizaliwa.

 

            Kuanzia siku hiyo, Allamah Rizvi alitumia muda wake katika shughuli za Tabligh. Katika mwaka 1963 Bilal Muslim Mission of Tanzania ilisajiliwa. Wakati kazi ilipoongezeka, Marehemu Ayatullah Al-Uzma Sayyid Muhsin Al-Hakeem (Najaf, Iraq) aliamuru Halmashauri Kuu ya Khoja Shia Ithna-asheri ya Afrika kumtoa katika majukumu ya Jamaat, na kuanzia hapo gharama zote za Allamah Sayyid Rizvi zilichukuliwa na marehemu Ayatullah Al-Uzma Sayyid Muhsin Al-Hakeem na baada yake zikachukuliwa na marehemu Ayatullah Al-Uzma Sayyid Abul Qasim Al-Khu'i.

 

            Kwa juhudi zake katika Mission hii makumi ya maelfu ya Waafrika wamekubali imani ya Shia pole pole kupitia mafundisho, maandishi na masomo kwa njia ya Posta, sasa Jumuiya ya Shia imestawi nchini Guyana chini ya Bwana Lateef Ali ambaye amefanikiwa kueneza ujumbe mpaka Trinidad na Tobago.

 

            Mission ina kituo kwa ajili ya kufundishia Mubalighina mjini Dar es Salaam ambacho vile vile kina Bweni lenye nafasi. Kuna shule za chekechea, Msingi, Secondary na Madrasah ya Qur’ãn na Misikiti. Kwa nyongeza, Mission inaendesha masomo aina nne kwa njia ya Posta ambayo kwayo mwanga wa Ushia umefika mbali kwa marefu na mapana. Mission imechapisha vitabu zaidi ya miamoja na ishirini kwa Kiingereza na Kiswahili, sehemu kubwa ikiwa ni ya vitabu vya Allamah Rizvi au tarjuma yao.

 

            Kuna Bilal Muslim Mission nchini Kenya (imeanzishwa sawia na Misheni ya Tanzania) Burundi, Malagasy na Msumbiji. Yakitiwa moyo na Bilal Muslim Mission of Tanzania, Mashirika yenye majina kama haya yameanzishwa nchini Seneghal,Naijeria,Ghana,Sweden na Marikani.

 

            Katika mwaka wa 1978 alirudi na kukaa nchini India ambako alianza kuandika tarjuma ya Kiingereza ya Tafsir al-Mizan cha Marehemu Allamah Sayyid Muhammad Husayn at-Tabataba'i. Juzuu kumi za tarjuma hii zimekwisha chapishwa na World Organization For Islamic Service (WOFIS)  Tehran Iran.

 

            Mwezi Desemba 1980, alikwenda London kwa mualiko wa (Shirika la)  Imam Sahebuz Zaman Trust. Kule London alikua pamoja na marehemu Hujjatul Islam Al-Mujahid Sayyid Mhadi al-Hakeem katika kuanzisha World Ahlul-Bayt (A.S.) Islamic League (WABIL) ni mmoja wa wadhamini watatu wa Shirika hili. Alikuwa Mkurugenzi wa Kamati ya maandalizi ambayo ilirasimu katiba ya WABIL na ilipanga mkutano wake wa kwanza wa katiba. Mkutano huu ulifanyika mwezi Augosti 1983 ambao kwayo wajumbe 80 kutoka nchi 30 walishiriki. Katika mkutano huo alichaguliwa kuwa mkurugenzi mkuu (wa shirika hilo).

 

            Alirudi Tanzania mwaka 1986 kuendeleza shughuli za Bilal Muslim Mission of Tanzania na sasa hugawanya wakati wake kati ya Tanzania, India, na Canada.

 

            Mwaka wa 1991 Ilianzishawa Ahlul~Bayt (A.S.) World Assembly (ABWA) Tehran,Iran na Allamah Rizvi alichguliwa mmoja wa wana kamati ya Halmashuri kuu na mjuube. Na vile vile ni Muasis na Mwenye Kiti wa Ahlul~Bayt (A.S.) Assembly of Tanzania.

 

Mwaka wa 1993 ameanzisha Bilal Charitable trust of India,Gopalpur. Hadi sasa zaidi ya Misikiti 25 na Hussaeinia zimejengwa na zaidi ya nyumba 30 za kuishi kwa watu ambao hawana makazi na vile vile shule za chekechea, Msingi, Secondary na teknolojia zimeanzishwa na Tasisi hii.

 

            Allamah Rizvi ameanzisha Madrasa nyingi za Kidini na kufungua Markazi za Tablighi katika sehemu mbalimbali ulimwenguni, kati ya sehemu hizo ni India, Marekani, Uingereza, Canada, na nchi za Kiafrika.

 

            Kufikia sasa ameandika vitabu 124 (78 kwa Kiingereza, 29 kwa Kiurdu, 11 kwa Kiarabu na 6 kwa Kiswahili) ambavyo 91 vimekwisha chapishwa na 6 vinachapishwa.Kwa muda huu, anajishughulisha katika kuandika vitabu 3 vya Kiingereza, Kiarabu na Kiurdu. Baadhi ya vitabu vyake vimetafsiriwa kwa lugha za Ki-Japan Ki-Indonesia, Ki-Thai, Ki-Burma, Ki-Urdu, Ki-Hindi, Ki-Gurjati, Ki-Sindhi, Ki-Ajemi, Ki-Swahili, Ki-Hausa, Ki-Shona, Ki-Taliani, Ki-Faransa Ki-Swidish Ki-Bosni Ki-Arabi Ki-Holanzi.

 

 Vile vile amefanya kazi na baadhi ya Maulama wa Qum kuweka vizuri na kusahihisha Adh-Dhariah fi Tasanif As-shia, Kitabu kikubwa cha habari za vitabu na watungaji wake kilichoandikwa na marehemu Ayatullah Agha Buzrg at-Tehrani.

 

            Amepewa Ijazat (Mamlaka) na Ma-Ayatullah wakongwe kumi na Tisa wa Najaf (Iraq) na Qum (Iran) kwa simulizi ya hadithi (riwayah) kwa mambo ya hukumu kwa Shariah na vile vile kushughulikia suala lolote ambalo kwalo ruhusa ya Mujtahid ni muhimu.

 

            Ni mtaalam wa lugha. Huandika, huzungumza na kutoa mihadhara kwa Ki-Urdu, Ki-Arabu, Ki-Ingereza, Ki-Swahili na Ki-Ajemi. Vile vile anayo elimu (ya maandishi) ya Ki-Hindi na Ki-Gujarati. Mbali na ukubwa na upana (wa eneo) anaoshughulikia, na ziara za mara kwa mara ndani ya Afrika Mashariki, amezuru kama nchi 45 za Asia, Afrika, Ulaya na Marekani.

 

ORODHA YA BAADHI ZA VITABU

 VYA

 ALLAMAH RIZVI

 

Kwa Kiingereza


1     Islam

2.    Need of Religion                         

3.         God : An Islamic

       Perspective

4.    Justice of God

5.    Prophethood

6.    Imamate

7.    Qur’an and Hadith

8.    Day of Judgement

 9.   What a Muslim Should

       Know & Believe

10.  The Return of Al-Mahd

11.  Elements of Islamic

       Studies

12.  Fast                 

13.    Family Life of Islam

14.    Charter of Rights

15.     Hijab

16.    Muhammad (S.A.W.) is the

       Last Prophet

17.    The Holy Prophet

18.    Four California Lectures

19.    Taqiya

20.    Inner Voice

21.    Rulings On Morden Problems

22.    Islamic Laws

23.    In Defence of Islamic Laws

24.    Wahhabis’ Fitna Exposed

25.    On To The Right Path

26.    Pork

 

 

 

 

 

 

 

27.    Slavery

28.    Sects of Islam

29.    Shi’ite Sects

30.  Your Questions Answered  1

31.  Your Questions Answered  2

32.  Your Questions Answered  3

33.  Your Questions Answered  4

34.  Your Questions Answered  5

35.  Your Questions Answered  6

36.  Your Questions Answered  7

37.    Your Questions Answered  8

38.    A Few Questions Answered

39.  Fadak

40.  The Ideal Islamic Government

41.  Meaning & Origin of Shiism

42.  The Quran Its Protection from

       Alteration

43.  Prophecies About the Holy

       Prophet of Islam in Hindu       

       Christian & Jewish Scriptures

44.    Some East African Ithna- 

       Asheri Jamaats

45.    The Khoja Shia Ithna-Asheri

       Community in East Africa

46.    A Correspondence Between a

       Christian and a Muslim

47.    Selected Articals  Vol  1

48.    Selected Articals  Vol  2


 

 

 

 

 

UTANGULIZI

 

 

 

 

Katika mwaka wa 1964, Bunge la Tanganyika lilipitisha  Sheria ya “ki-Islamu” (Taarifa mpya) ambayo ilimpa uwezo Waziri anayehusika na mambo ya Sheria kutengeneza na kutangaza Taarifa ya Sheria ya ki-Islamu baada ya kushauriana na Wasomi wa sheria katika madhehebu za ki-Islamu.  Kwa mujibu wa Gazeti la Standard Tanzania (13/ 7/67) liliandika : “Inafahamika kwamba Tanganyika ni nchi ya kwanza kupata kutekeleza zoezi la kupanga kanuni ya sheria ya ki-Islamu katika mfumo wa sheria iliamriwa halali. Taarifa hizi zitasaidia sana Mahakama ambazo hutegemea juu ya vitabu vya kiada”.

 

Khoja shia Ithna-asheri territorial council of Tanzania (Jumuiya  ya Khoja shia Ithana-sheri) walilichukulia uzito suala hili.  Bwana Mohamed G. Dhirani, aliyekuwa wakati huo Rais wa Baraza ya Jumuiya iliyotajwa, alinichukuwa mpaka kwenye Ofisi za Mwanasheria Mkuu, ambako nilimkuta wakili mkuu wa mradi huo.  Alikuwa ni mwislamu wa Zanzibar.  Alinishauri niandike kwa Kiingereza, sheria zote za Shi’a zihusikanazo na masuala haya kwa matumizi ya Ofisi yake.  Hivyo niiandika “sheria za ki-Islamu zinazohusika na ndoa, kuvunjika kwa ndoa, makubaliano ya ndoa, wosia, mirathi na waqf”.  Bwana Fida Hussein Abdallah Hameer, aliyekuwa Katibu wa Baraza wakati huo alitayarisha Sekretariati kwa ajili ya kusaidia.

 

Miwishowe makaratasi (yenye taarifa) yalimfikia Bwana Bashir Rahim, aliyekuwa mrasimu wa Bunge Muandamizi ambaye alikamilisha sura nne za ndoa (kama inavyokubalika na madhehebu makubwa matatu ya Sheria ya Uislamu - Shafii,Hanafi na Shi’a).  Ilichapishwa chini ya mamlaka ya bwana Rashid Kawawa, aliyekuwa wakati huo  makamu wa rais wa Tanzania, ambaye alikuwa anapasika vile vile  na Idara ya Sheria.  Ilitokea kama sheria ndogo zilizotungwa chini ya Taarifa rasmi mpya ya Sheria ya ki-Islamu (Na. 56 ya 1964) (Katika) Nyongeza ya Gazeti (La Serikali Na. 34 la 27 Juni 1967).  Ilieleweka zile sura zilizobakia zinazohusu utunzaji wa watoto na talaka nk.  zitachapishwa mwishoni mwa mwaka, na kisha hapo Sheria zitaanza kutekelezwa.

 

KUELEKEA KENYA

 

Sasa mandhari inahamia Kenya.  Serikali ya Kenya wakati huo iliunda  Tume juu ya sheria za ndoa, talaka na mirathi, chini ya uwenyekiti wa Mheshimiwa Jaji Spry wa Mahakama Kuu ya Kenya.  Tume ilitakiwa  itoe mapendekezo kwa ajili ya sheria mpya yenye uwezo mkubwa na kwa kadiri itakavyoweza kutumika kama sheria inayofanana ya ndoa, na talaka itumikayo kwa watu wote nchini Kenya. Ambayo itakuwa badala ya Sheria iliyopo juu ya suala lihusianalo na  Sheria ya mila, Sheria ya “ki-Islamu”, (haswa ya kwetu) Sheria ya  Baniani na Sheria za Bunge zinazohusika na kutayarisha rasimu ya Shria mpya; ikitoa kipaumbele mahususi kwa hadhi ya wanawake kuhusiana na ndoa na talaka katika jamii huru ya kidemokrasia.

 

Nilikwenda Mombasa Julai 1967 kwa mintaarafu fulani mingine na  wahusika wa Supreme Council (Halmashauri Kuu ya Shia Ithna-asheri) walinichukuwa nikaonane na wakili ambaye alikuwa bingwa katika sheria binafsi za Uislamu.  Kwa kuelezewa matukio ya Tanzania, aliniomba nimplekee nakala ya Sheria za “Ki-Islamu” ambayo nimeiandika kwa ajili ya Tanzania.  Nami niliahidi hivyo.

 

Kabla ya hii,  niliandika majibu kwa maswali ya Tume ambayo yalipelekwa kabla kwenye Tume.

 

Kurudi Dar es Salaam, nilikusanya taarifa ya Sheria za “Ki-Islamu” zilizotajwa (karibu karatasi ndefu mia moja, kurasa zilizopigwa mashine kwa karibu karibu) zikiwa zimerudufiwa, na kutumwa Halmashauri Kuu ya Khoja Shia Ithna-asheri.

 

Katika juma la tatu la Augusti 1967, niliitwa haraka Mombasa  ambako tume ilikuwa ikae kwa ajili ya kusikiliza kuanzia 21/8/1967.  Niliandika muhtasari (au taarifa) kwa ajili ya kuwasilisha mbele ya tume, ambayo ilikamilishwa baada ya majadiliano na maofisa wakuu watendaji (wa Halmashauri Kuu).

 

Muhtasari  ule uliwasilishwa  kwenye tume na  kisha ukachapishwa katika “The Light” ya Julai – Augusti 1967. (Marehemu) Haji Mohamedali Meghji, Rais wa Halmashauri Kuu ya Khoja Shia Ithna-asheri aliandika barua  iliyoambatanishwa ya maelezo (ya ziada) dondoo ambayo imechapishwa marudufu kabla ya muhtasari wa kwanza.

Mheshimiwa Jaji Spry alisikika akiwaambia wenzake baadae kwamba “watu hawa walijua kuhusu walichokuwa wakiongea”.

 

Muhtasari mwingine juu ya Sheria ya Mirathi ambao ulioandikwa na mimi, ulitumwa kwenye tume na kuchapishwa katika “The Light” ya Januari – Aprili 1968.  Ni Muhtasari wa pili katika mkusanyo huu.

 

KURUDI TANZANIA:

 

Wakati matukio hayo hapo juu yalipokuwa yanafanyika nichini Kenya, ghafla Serikali ya Tanzania ilisimamisha zoezi la upangaji wa Kanuni (wa Sheria ya “ki-Islamu”).

 

Tume ya Kenya iliwasilisha taarifa yake na mapendekezo wakati Fulani katika mwaka wa 1969.  Tarehe 10/9/69 Serikali ya Tanzania ilichapisha waraka (White Paper) No. 1 wa 1969 uliosema kwamba inataka kutunga Sheria ya Ndoa iliyo sawasawa (kwa wote),  na ikatoa maelezo ya masharti iliyoyataka yawekwe kwenye Sheria iliyokusudiwa.

 

Pamoja na kuchapishwa kwa waraka, Serikali ilikaribisha maoni na mapendekezo kutoka kwenye Jumuiya na watu binafsi.  Wakristo, Mabaniani na Maismailiya walichapisha maoni yao katika magazeti.  Niliwafuata Bakwata kwa madhumuni haya; walikataa kwa mkato kabisa kuingilia mpango wa Serikali.  Nilikuwa sina njia nyingine bali kuandika kwa niaba ya Shi’a Ithna-sheri tu.  Maoni yalikuwa ya ukweli na pengine kifungu cha mwisho kilikuwa kikali kidogo.  Nilipeleka mswada kwa Bwana Anverali M. Rajpar, aliyekuwa wakati huo Rais wa Khoja Shia Ithna-sheri Territorial Council of Tanzania, aliniambia niendelee na niuchapishe kwenye Gazeti la Standard kwa niaba ya Tanzania Council.  Ilitokea katika Standard (Dar es Salaam) tarehe 8 Desemba 1969 (Jumatatu) na baadaye dondoo zake zilichapishwa katika “The Light” ya Desemba 1969.  (Mswada) huu hutokea kama muhtasari wa tatu katika kijitabu hiki.

 

Wakati wa miezi ya baadaye, Halmashauri Kuu (Supreme Council) ilinitumia taarifa mbili za tume ya Kenya, nilishagazwa kuona kwamba karibu mapendekezo mengi ya waraka wa Tanzania yaliondolewa kutoka kwenye mapendekezo ya Tume ya Kenya.

 

Wakati naandika muswada wa Sheria ya Ndoa ya mwaka 1971, katika mwanga wa waraka wa Serikali na maoni niliyopokea, Bwana Bashir Rahim, aliyekuwa wakati huo msawidi mkuu wa Bunge, alijaribu kwa uwezo wake kuingiza masharti ya Sheria za “ki-Islamu”.  Kabla ya kukamilisha muswada huo, ulionyehswa kwa wanachuoni wa kila dini na madhehebu, na mabadiliko fulani yalifanywa kwa kutegemea juu ya ushauri wao.

 

HALI ILIYOPO SASA:

 

Serikali ya Tanzania sasa inataka kutunga Sheria ya Mirathi iliyo sawa kwa wote; ambayo itawapa wanawake kigawanyo sawa na kile cha wanaume.  Wakati wanachuo wa “ki-islamu” (sio Bakwata) walipotoa  kauli zao dhidi ya sheria hiyo, aliyekuwa wakati huo Rais (wa Jamhuri ya Tanzania) Mheshimiwa Al – Haji Ali Hasani Mwinyi aliwahakikishia kwamba rai haikuwa kubadilisha sheria ya “ki-Islamu”, bali kuweka haki ya mirathi kwa wanawake wale ambao hawana haki kama hizo kabisa – bali wao wenyewe wanachukuliwa kama bidhaa za mirathi.

 

Wakati huo huo katika mwaka wa 1990, mashirika mabalimbali ya “ki-Islamu” (Mbali na Bakwata) yalianza kufanya  kampeni kwa ajili ya washichana wa “ki-Islamu”  kuruhusiwa kuvaa Hijab mashuleni.  Wawakilishi wao walikutana mara nyingi, na kutegemea juu ya majadiliano yao, niliandika Muhtasari juu ya Hijab na mirathi, ambao hatimaye uliwasilishwa kwa Rais Al-Haj Ali Hassan Mwinyi.  (Muhtasari huo) umewekwa katika kijitabu hiki kama Muhtasari wa nne.  Inafurahisha kuona kwamba Rais alitamka katika hotuba ya hadhara tarehe 10/8/1995 kwamba wasichana wa “ki-Islamu” sasa wanaruhusiwa kuvaa Hijab mashuleni; na Kaimu Kamishina wa Elimu alitoa mwongozo kwenye suala hili kwa taasisi za Elimu, ambao barua yake halisi yaweza kuonekana  katika ukurasa ufuatao, na tarjuma yake ya kiingereza imetolewa mwiso wa kitabu hiki.

 

Bilal Muslim Mission of Tanzania inaona kwamba muhtasari hizi zina hoja zilizo wazi kuthibitisha kwamba Sheira za “ki-Islamu” zilizoanzia kutokana na hekima ya Mungu haziwezi kubadilishwa, na kwamba Sheria ya “ki-Islamu” ni mfumo pekee ambao huweza kutoa haki na uhuru katika jamii.

 

Ni kwa sababu hii kwamba Misheni hii imeamua kuchapisha Muhtasari nne pamoja katika kijitabu hiki.  Nawashukuru kwa ari hii, na kuomba kwa Allah Subhanahu wa Ta’ala kuwapa tawfiq zaidi, na akifanye kitabu hiki kuwa  njia ya mwongozo kwa Waislamu na kwa  wasio Waislamu hali kadhalika.

 

Dar es Salaam                           Sayyid Saeed Akhtar Rizvi

31st October  1998                         

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

1

MUHTASARI JUU YA SHERIA ZA NDOA*

 

 

Dondoo kutoka barua iliyoambatanishwa :  Muhtasari ufuatao uliandikwa na Maulana Sayyid Saeed  Akhtar Rizvi kwa ajili  ya kuwasilisha mbele ya  tume juu ya  Sheria  za Ndoa, talaka na Mirathi, iliyowekwa na Serikali ya Kenya chini ya uweneyekiti wa Mheshimiwa Jaji Spry wa Mahakama Kuu ya Kenya.

 

Masharti ya Rejea kwa ajili ya Tume ni:-

 

“Kufikiria Sheria iliyopo ihusikananyo na Ndoa, Talaka na mambo yahusianayo na hayo;” “Kutoa mapendekezo kwa ajili ya Sheria mpya itoayo uwanja mpana na, kwa kadiri itakavyoweza kutekelezwa sheria ya Ndoa sawa kwa watu wote, na talaka itumikayo kwa watu wote nchini Kenya, ambayo itachukuwa nafasi ya sheria iliyopo juu ya suala  lihusianalo na Sheria ya mila, Sheria ya  ki-Islamu, Sheria ya ki-baniani na amri zinazohusika za Bunge na kutayarisha muswada wa Sheria mpya.”

 

“kutoa kipaumbele mahususi kwa hadhi za wanawake kaitka kuhusiana  na ndoa na talaka katika jamii huru ya kidemokrasia”.

 

Tume ilituma maswali mapema kwa pande zote zinazohusika, na Halmashauri Kuu (Supreme Council) ikapeleka  majibu yao (yalioandikwa na Maulana Sayyid  Saeed Akhtar Rizvi) kwenye  Tume kabla.

 

Tume ilikaa kwa ajili ya kusikiliza mjini Mombasa kuanzia tarehe 21 Augasti 1967.  Ujumbe wetu ulitokea mbele ya tume tarehe 22 Augasti.  Pamoja na Muhtasari, taarifa iliyobeba mambo mengi ya shria za ki-Islamu na mkusanyo wa hotuba juu ya Usul-Din “Islam” zote zikiwa zimeandikwa na kukusanywa na Maulana Sayyid Saeed Akhtar Rizvi, ziliwasilishwa mbele ya Tume.

 

Ni wazi kwamba juhudi ya Maulana katika suala hili imestahiki kusifiwa mno, na sisiti kukiri kwamba uwasilishaji ufuatao usingelifanikiwa bila muongozo na msaada wake.

 

Wajumbe wa msafara walikuwa, Maulana Sayyid Saeed Akhtar Rizvi,Mulla Asgherali M. M. Jaffer (Hon. Gen.Secretary – Mh. Katibu Mkuu),Bw. Hassan A. M. Jaffer (Mh. Mhazina  Mkuu) Maulana Sheikh Maqbool Hussain (Mombasa) Bw. Bashir H. Pira na mimi mwenyewe.

 

Mh. Katibu Mkuu wa Halmashauri Kuu ya Khoja Shia Ithna-asheri Mulla Asgheri M. M. Jaffer aliwasilisha kama msomaji wa Shia Ithna-asheri, na alisoma wasilisho mbele ya Tume.Vile vile alijibu maswali yaliyoulizwa na Tume, na kufafanua nukta mbali mbali zinazohusika na Ndoa, Talaka n.k. kwa mujibu wa madhehebu ya Shia.

 

 

MOHAMEDALI MEGHJI:

Rais, Shia Ithna-ashri-Halmashauri Kuu (ya Khoja)

P. O. Box 1085, Mombasa.

*****

 

1.Kwa niaba ya Jumuiya ya shia Ithna-asheri ya Kenya, tunachukuwa fursa hii ya kufanya uwasilishaji huu kwa ajili ya kufikiriwa na Tume.

 

2.Katika uwasilishaji huu, tunakomea maelezo yetu kwenye Sheria za dini zilizofungana na Ndoa, Talaka, wosia na mirathi ya Madhehebu ya ki-Islamu ya Shia Ithna-asheri.

 

3.Inafahamika kwamba matatizo ya kijamii aina mbalimbali yatokeayo kwa kutmia vibaya au tafsiri potofu za mila, desturi au sheria za dini katika utekelezaji wa jumla, hutoa sababu kwa uwajibikaji wa makini kwa Serikali, na Serikali katika hamu yake kuwapatia watu wake ustawi katika suala hilo inakabiliwa na  jukumu ngumu la Serikali  la kutokomeza maovu ya kijamii.  Juhudi yoyote katika muelekeo huu yafaa kuungwa mkono na hustahiki ushirikiano wote.  Lakini tunahisi kwamba wazo la kutunga Sheria ya wote kuchukua mahali pa Sheria ya ki-Islamu iliyopo sasa sio sahihi.

 

Hata desturi za kimila (zisizo na mamlaka ya kidini) ni ngumu kubadilisha.  Hii  huwa hatari mno zaidi katika suala kama la  Sheria ya ki-Islamu ambayo ni sehemu muhimu ya dini yetu, ambayo  haikomei kwenye ibada tu.  Sheria hizi haziwezi kuvunjwa bila ya kupata  hisia ya hatia na dhambi.

 

Kwa hiyo, tunahisi kwamba njia nzuri “itakuwa kuacha mamia ya maua kuchanua.”  Umoja wa Kitaifa hauhitaji kwamba raia wote  yawapasa kuwa na lahaja inayofanana au imani ya dini inayofanana.  Hivyo kwa nini inafikiriwa kwamba ni muhimu kuwa na Sheria ya Ndoa inayofanana na talaka ya kutumika kwa watu wote wa Kenya.

 

4.Sheria zetu za Shia Ithna-asheri hazikutegemezwa juu ya “Rai” (maoni) au “Qiyas” (anolojia).  Zimetegemea kabisa juu ya Qur’an Tukufu  na Hadith za Mtukufu Mtume na Maimamu wetu Kumi na Mbili.

 

Kwa vile tume inahusika na mambo ya Ndoa na Mirathi, lazima  tuonyeshe kwamba kanuni za msingi na mambo mengi namna kwa namna  ya mirathi yanaelezwa katika Qur’an Tukufu.  Kusema kweli, maudhui hii imeshughulikiwa zaidi kwa ukamilifu katika Kitabu Kitukufu.  Hali kadhalika, kanuni za msingi za ndoa na talaka zimetegemezwa juu ya Qur’an Tukufu.

 

Mambo ambayo hayako wazi katika Qur’an Tukufu yanaelezwa katika Hadithi kama ilivyotajwa hapo juu.

 

Wanachuoni wetu ambao wanaitwa MUJTAHID hawatoi hukumu yoyote kwa maoni yao, analojia (Qiyas) au (kwa) ijimai.  Hakuna mamlaka kama hayo yaliyotolewa kwa yeyote katika Sheria ya madhehebu yetu.  Wanaweza kutofautiana katika kutafsiri Hadith fulani zinazohusu baadhi ya mambo madogo, lakini hata hivyo tofauti hiyo ni tofauti katika tafsir, sio ya maoni.

 

Madhehebu ya Shia Ithna-ashri hufuata katika mambo yote ya dini hukumu za Mujtahid mkubwa wa zama.  Anachukuliwa  kuwa yeye ni mwakilishi wa Imamu wetu wa Kumi na Mbili na ni mtu wa mwisho juu ya mambo  yote ya dini. Kwake yeye amekabidhiwa katika masuala fulani, mamlaka za ulezi wa watoto, ulinzi katika ndoa na talaka, utekelezaji wa Wosia na mali ya marehemu na mambo kama hayo.

 

5.Sheria ya ki-Islamu ya madhehebu ya Shia Ithna-asheri ni chombokilichofumwa vizuri. Hatuwezi kubadilisha au kurekebisha, moja au mbili ya mambo yake bila kuharibu ufumaji wote.

 

Kwa Mfano:-

 

[1]       Hukumu za Ndoa na Talaka zinabeba uzito wa moja kwa moja juu ya uhalali au vinginevyo wa mtoto; juu ya wema au dhambi ya pamoja ya mwanaume na mwanamke; katika haki ya wao wenyewe kwa wenyewe ya mirathi na ile ya mtoto; mbali na kutokana na jamii na shida za kisheria.

 

[2]       Katika sheria za ki-Islamu mtu hawezi kutumia kitu chochote kilichopatikana kiharamu (kwa maana ya kidini) amma kwa kilimwengu au kwa madhumuni ya kidini.  Kwa hiyo, kama mabadiliko yanafanywa katika sheria za mirathi na mtu fulani anapewa zaidi kuliko mgao wake kwa mujibu wa Qur’an Tukufu, maisha yake yote yatakuwa  duni.  Maisha yake ya kila siku yatakuwa ni orodha ndefu ya kuchupa mipaka, Sala zake, Hija, chakula na mavazi vitakuwa haramu katika maana ya kidini.

 

Hivyo ni wazi kwamba mfumo wa Sheria ya ndoa, talaka na mirathi hauwezi kubadilishwa; vinginevyo hii itaanzisha muingilio wa moja kwa moja katika dini yetu.

 

6.Kuhusu hamu ya Tume “Kutoa kipaumbele kwa hadhi ya wanawake katika kuhusiana na Ndoa na Talaka katika jamii huru ya kidemokrasia”. 

 

            Tunataka kuwakilisha kama ifuatavyo:-

 

(a)       katika sheira ya madhehebu yetu mwanamke anazo haki hizo upendeleo na ulinzi wa salama tangia Karne ya Kumi na nne, nyingi ya hizo hazikufikiriwa katika Jamii zisizo za ki-Islamu mpaka Karne iliyopita na baadhi ya hizo ziko mbele ya inayoitwa zama ya kisasa.

 

(b)       Uislamu kwa mujibu wa madhehebu ya Shia, umempa mwanamke haki ya kufanya mkataba yeye mwenyewe katika Ndoa kama ni mtu mzima na makanifu.

 

(c)        Uislamu umempa mwanamke kitambulisho cha

kujitegemea.  Mwanamke wa ki-Islamu anamiliki mali yake mwenyewe hata baada ya kuolewa, na mume hawezi kuingilia.

 

(d)       Mwanamke anaweza kumfungulia mume wake mashtaka, anawezakutoa ushahidi dhidi yake.  Anarithi kutoka kwa mume kwa haki na mwanaume kutoka kwa mwanamke.

Haki hii, ya wote pamoja ya mirathi (kurithiana) ilitolewa wakati hakuna jamii kamwe ilifikiria kuhusu haki hii.

 

7.Mgao wa mwanamke kwa kawaida ni, nusu ya ule (mgao) wa mwanaume. Lakini hii ni mantiki kabisa.  Uislamu umemfanya mwanaume kuwa na jukumu la kutunza familia.  Hakuna mzigo kama huo  uliowekwa  juu ya mwanamke.  Hata mke tajiri anahusika kupata matunzo yake kutoka  kwa mume wake ingawa anaweza kuwa ni maskini.  Kwa vile matunzo ya familia ni jukumu la mwanaume, amepewa mgao marudufu karibu katika mirathi yote.

Vile vile, mwanamke hupata mahari ambayo hutoka kwa mume  kwenda kwa mke.  Kwa hiyo uwiyano wa mgao uliowekwa katika Qur’an Tukufu ni wa haki zaidi.

 

8.Sheria ya Uislamu ihusianayo na Wosia haimruhusu mtu kuusia zaidi ya thuluthi moja ya mali yake kamili.  Hivyo hali ya kifedha ya wale watakao kuwa warithi siku zote inalindwa na mbali ya kutwaliwa kokote isivyo haki na yeyote.  Usalama huu bado unakosekana katika jamii nyingi ambazo huruhusu mtu kutoa mali yote kwa mgeni haswa.

 

9.Sasa tunakuja kwenye baadhi ya mambo ya Ndoa:-

 

(a)MITALA : Jamii ya Waafrika ilikuwa, na kwa kiwango fulanini jamii ya kimitala.  Uislamu vilevile huruhusu mitala.  Umeruhusu wake wanne kwa wakati mmoja na imeamuru usawa  katika kuwahudumia wake wote.

 

(b)Yapasa ikumbukwe kwamba mitala sio kitu cha lazima wala sio kitu kinachotetewa.  Ni ruhusa tu pamoja na ukomo Fulani na masharti.  Na katika baadhi ya mazingira ruhusa hii imethibitisha manufaa mazuri mno.

 

Kwa mfano, kama mke ana ugonjwa sugu au ni mgumba au kwa sababu nyingine fulani haiwezekani kwa wawili hao kuishi kama mume na mke.  Suluhisho litolewalo na jamii fulani ni kumtaliki mke na kuoa mwingine.  Lakini je, hii ni haki?  Je, ni wema au uadilifu kumfukuza mwanamke katika hali ya uzee au katika umri wake wakati kutoka kwenye nyumba yake, kwa sababu  ame kuwa mgonjwa siku zote au ametokea kuwa mgumba? Uislamu hupinga ukatili huo kwa kuruhusu mitala.

 

10.(a) TALAKA:  Hakuna haja kusisitiza kwamba katika hali fulani talaka ndio suluhisho pekee lililobakia kwa wawili hao (mume na mke). Manufaa ya mfumo wa talaka yanaweza kuonekana kutokana na ukweli kwamba hata Baniani na Wakristo wengi wamelazimika kwa nguvu ya moja kwa moja isio epukika kutnga sheria za talaka.

 

(b) Ni lazima tuonyeshe kwenye wakati wa mwanzo kwamba madhehebu ya Shia-Ithanaseri ya ki-Islamu imeweka kanuani ngumu zilizotegemea juu ya Qura’n Tukufu na Hadithi, kuhusiana na talaka.

                                                                                                 

(c) Talaka imetangazwa na Mtukufu Mtume kuwa ni kitu kilichotwezwa katika halali zote.

 

(d) Qur’an Tukufu imeweka mfumo wa usuluhisho wakati wowote kukiwa kuna kutokuelewana kati ya mume na mke.

 

(e) MASHARTI YA TALAKA: Talaka inaruhusiwa mradi tu inatamkwa mbele ya watu wawili mashahidi.  “Adil” (watu wamuelekeo thabiti) ambao husikiliza maeneno na kuelewa asili au chanzo cha talaka.  Talaka lazima itamkwe katika utaratibu uliothibitishwa,

 

 Zaidi ni lazima vile vile kwamba mume awe mtu mzima, mwenye akili timamu  na mwenye  kuelewa vizuri  atendaye kwa utashi wa uhuru wake mwenyewe, na sio katika mshituko wa hasira au kutishwa.  Nakwamba lazima awe na nia ya dhahiri ya kuvunja ndoa.

 

Kwa kadiri mwanamke anavyohusika,yeye wakati wa Talaka lazima awe katika hali ya tohara na kwamba talaka haiwezi kutamkwa hata wakati wa tohara ambao kwamba mume amekutana naye kimwili.

 

Kama moja ya masharti yaliyotajwa hapo juu yakivunjwa  Talaka itakuwa batili na kutenguka.

 

(f) Talaka tatu haziwezi kutolewa kwa wakati mmoja.  Kama mtu atasema kwamba  anatoa talaka tatu, hata moja haitakuwa halali.

 

(g) Katika hali nyingi, talaka inaweza kutenguliwa, na mume ana lazimika kumtunza mke aliyetalikiwa wakati wa kipindi cha “Iddat” (kwa kawaida ni miezi mitatu) katika nyumba yake; vinginevyo ahiari kutoka (mwenyewe).

 

(h) Wakati wa kipindi kilichotajwa cha “IDDAT”  mume   anayo haki ya kutengua talaka kwa maneno au kitendo na kutakuwa hakuna haja ya taratibu zozote.

 

Kanuni hizi ngumu zimekuwa siku zote zikitekelezwa na madhehebu yetu.  Shukurani kwa Shariat yetu, talaka katika madhehebu ya Shia-Ithanasheri ziko mara chache sana.

 

            11.HAKI YA MWANAMKE KUHUSIANA NA UVUNJANI WA NDOA: Mwanamke hakupewa haki ya kumpa talaka mume wake.  Sababu  yeneyewe sio ngumu sana kuelewa.  Familia ni msingi wa jamii ya binadamu na kwa vile kila jamii huhitaji mamlaka ya mwisho kuiweka katika mpango ulioandaliwa vizuri. Familia lazima vile vile ipate kiongozi mkuu.  Sheria ya ki-Islamu imetoa  nafasi hiyo kwa mume, na mume amepewa haki ya kutoa talaka.

 

 Lakini mke ana haki ya kudai talaka katika hali nyingi: Km:

 

            (1)       Anaweza akaomba Khula ambayo inaweza kukubalika juu yake na mume;

 

(2)       Anaweza kumuomba Mujtahidi kumpa talaka katika hali ambako mume ametoweka, au akapuuza kumtunza.

 

(3)       Katika hali ya mume yakuwa mwenda  wazimu,  imma imetokea kabla au baada ya ndoa, ana haki ya kuifuta ndoa bila haja yoyote ya kupeleka kesi kwa Mujtahid.

 

(4)       Na anaweza kuibatisha Ndoa baada ya kuipeleka kesi kwa Mujtahid, kama mume ni hanithi.

 

12.Katika uwasilishaji wetu, tulionyesha mapema kwamba sheria sawa kwa wote katika jamii ya kilimwengu kama hii ya Kenya haina umuhimu kwa umoja wa kitaifa.  Sasa tunaomba kuwasilisha kwamba kuishi pamoja, kwa amani na urafiki miongoni mwa watu walioambatanishwa kwenye imani za dini mbalimbali na sheria kunaweza kupatikana tu kama uhuru utatolewa kwao kutekeleza  sheria kama hizi, na kutenda kimujibu (kama itakikanavyo).

 

Haitakuwa nje ya sehemu (ya maudhui) kutaja hapa kwamba  Uislamu una seti ya theolojia inayojumuisha mambo yote ya maisha.  Na kwamba amri zake na maelekezo hayakomei kwenye ibada za sala za kila siku na maombi pekee.  Ni mfumo wa maisha ambao hutoa huduma ya mipangilio namna namna kwa jaamii, ndoa, maadili, na hali kadhalika uendeshaji wa biashara katika maisha ya kibinadamu.

 

Pengine itakuwa ni kitu cha kuvutia kwamba hivi karibuni Tanzania imechapisha “Taarifa ya sheria ya ki-Islamu. “ Huu ni utungaji mdogo wa Sheria chini ya “Taarifa mpya ya shria ya ki-Islamu” (No. 56 ya 1964).  Nyongeza ya Gazeti  (la Srikali) No. 34 ya 27 Juni, 1967 yahusika. Hatua hii iliyokuja wakati mzuri katika Tanzania imethibitisha kwamba nchi yoyote inayopigania uhuru wa kuabudu na utekelezaji wa dini inaweza kwa usalama kuweka sheria mbali mbali kuhusiana na Ndoa, Talaka, Mirathi au mambo yoyote kama hayo.  Vile vile huonyesha kwamba hatua kama hiyo inatekelezeka.  Tunaweza kuongeza kwamba vile vile hudokeza kwamba mpangilio kama huo unasaidia kwenye kuelewa vizuri na uhusiano katika nchi ambako  mazingira ya maridhia  yanatakiwa yafanyike, na tunaweka mikononi mwa tume kupendekeza hatua kama hiyo nchini Kenya.

 

13.Kujaribu kuweka mpaka kati ya Qur’an Tukufu na Sheria ya ki-Islamu kamwe hakuwezi kufikirika.  Jaribio lolote la kuvuruga au katika maneno ya masharti ya rejea ya Tume, “Kubadilisha Sheria ya ki-Islamu” kutakuwa hakukubaliki.  Kama ilivyoelezwa hapo juu, sheria ya ki-Islamu imetegemezwa juu ya Qur’an Tukufu na  kubadilisha Sheria ya Kiislamu ni sawa sawa na kubadilisha Qur’an Tukufu.

 

14.Tumewasilisha maswali yaliyotumwa na Tume yakiwa yamekamilishwa ipasavyo sambamba pamoja na mpangilio wa sheria ya ki-Islamu (katika Kiingereza) kwa mujibu wa Sheria ya Madhehebu ya Shia kuhusiana na Ndoa, uvunjaji wa Ndoa, Wosia, Mirathi, Makubaliano na Wakf; na tutafurahi kujibu maswali yoyote yajitokezayo kutoka humo na kuwasilisha ufafanuzi utakiwao.

 

MOMBASA, 22 AGOSTI 1967.


 

 

 

 

 

 

2

MUHTASARI JUU YA SHERIA ZA MIRATHI:*

 

ANGALIA: Tuna furaha kufunga pamoja na huu muhtasari uliowasilishwa kwenye tume juu ya sheria ya mirathi iliyoteuliwa hivi karibuni na Serikali ya Kenya.  Masharti ya rejea  yakiwa, kufirikiria sheria zilizopo sasa zinazohusu ndoa, talaka na mambo yanayohusika pamoja na hayo na kupendekeza Sheria inayofanana ya kutumika kwa watu wote wa Kenya ikitoa kipaumbela kwenye hadhi ya wanawake kuhusiana na ndoa na talaka katika jamii huru  ya kidemokrasia.

 

Sekritariati hii ina wiwa na Maulana Sayyid Saeed Akhtar Rizvi mwanachuo mkazi wa Dar es Salaam, Muasisi na Mhubiri Mkuu, wa Bilal Muslim Mission of Tanzania kwa juhudi zake kubwa katika kuandaa muhtasari huu.  Vile vile tuna viwa na Mulla Hussein A. Rahim M. B. E. wa Zanzibar, kwa muongozo wake wenye thamani.

 

Tunaomba Allah ( S.A.W.) kwamba awalipe kwa wingi hapa duniani na kesho akhera.

 

ASGHARALI M. M. JAFFAR,

Mh. Katibu Mkuu,

Halmashauri Kuu K. S. Ithna-Asheri

P. O. Box 1085, MOMBASA

*****

 

 

1. Kwa niaba ya Jumuiya ya Shia Ithna-Asheri ya Kenya tunaomba ruhusa ya kutoa uwasilishaji huu kw aajili ya kufikiriwa na Tume.

 

2. Maelezo yetu yanakomea kwenye Sheria za dini zinazohusika na wosia na Mirathi kwa mujibu wa madhehebu ya ki-Islamu  ya Shia Ithna-Asheri, isipokuwa ambako palipokuwa na maana kutoa maoni ya madhehebu nyingine ili kuifanya nukta yetu kuwa wazi.

 

3. Tayari tumewasilisha maswali yaliyotumwa na Tume yakiwa yamekamilishwa ipasavyo pamoja na mpangilio wa sheria za ki-Islamu (kwa Kiingerza) kwa mujibu wa Sheria ya Madhehebu ya ki-Islamu ya Shia Ithna-Asheri ihusianayo na Mirathi na Wosia miongoni mwa mambo  mengine.  Katika wasilisho hili tutajitahidi kueleza kanuni za msingi chini ya hukumu hizo.

 

4. Tunaelewa kwamba tume hii itatoa kipaumbele kwenye hadhi ya wanawake.  Tunajasiri kutumaini kwamba Sheria ya ki-Islamu inayotajwa kwa mujibu wa madhehebu ya Shia, itakuwa ya msaada mkubwa kwa Tume katika kazi yake juu ya suala hili.

 

Haitakuwa nje ya sehemu (ya maudhui) kutaja kwamba mila ya ki-Arabu ya zamani ilikuwa na lengo moja la msingi katika mtizamo, yaani, uzuiaji wa kudumu wa mali katika familia. Pamoja na lengo hili katika mtizamo, urithi ulikomea kwa ndugu wa kiume pekee tu, na hata miongoni mwao ni kwa wale tu ambao walikuwa na uwezo wa kubeba silaha.

 

Hatukusudii kushughulika sana juu ya nukta hii; itoshe tu kusema kwamba tabia kama hii, zaidi au kidogo ilikuwepo katika jamii zote katika wakati huo na imebakia katika jamii nyingi mpaka sasa.  Uislamu ulitoa kwa kudhihirisha uwekaji wa sheria ya haki ya kurithi kwa wale ambao walienguliwa na taasisi za zamani.  Moja ya matokeo ya faida ya sheria mpya ya Mungu ilikuwa kunyanyua hadhi ya wanawake katika mizani ya ustaarabu, kwa kunyanyua uchumi wao na nafasi ya kijamii, na kuwapa wajane, mama, mabinti na dada na ndugu wengine wa kike haki ya kurithi.

 

5. Moyo huu umehifadhiwa katika Sheria ya madhehebu ya Shia ambayo, kwa kunukuu maneno ya mwanachuoni mkubwa Sayyed Amir Ali, “Ni ya wepesi mkubwa mno na haihusishi mjadala wowote kuhusiana na haki za ndugu wa kiume na wa kike - “Asabah na Zav-il-Arham”. Kisha aliendelea kusema kwamba “Tofauti kubwa, kusema kweli, kati ya Shia na Sheria ya mirathi ya Sunni iko katika suala la jinsia ya Kuumeni.  Shia wanakataa kwa kupinga itikadi ya  Taasib au jinsia ya Kuumeni; hatimaye uhusiano wa Kuumeni wa jinsia ya kiume, au inayoitwa “Asbah Sahihi” katika fikihi ya Sunni (Sheria ya Sunni), hawana upendeleo maalum wala hawafadilishwi kwenye kuunganisha mahusiano na marehemu kupitia wanawake. Kwa mfano, Shia wanaona ni kinyume cha uadilifu kuwatoa watoto wa binti kwa kupendela kizazi cha mbali cha kaka, kwa msingi wa kubunia kwa kuwa kwao kuungana na marehemu kupitia mahusiano ya kuumeni.  (Mohameden Law, by Ameer Ali Vo. 2; P. 128).

 

Kwa mfano:

 

(a) Kama Muislamu Sunni akifa akiacha nyuma yake binti wa binti yake pamoja na mtoto wa kiume wa kaka yake, mtoto wa kiume wa kaka yake atachukuwa urithi wote kama ASABAH (ndugu wa kuumeni wa jinsia ya kiume).  Kwakumuondoa mjukuu mwenyewe wa marehemu.  Chini ya Sheria ya Shia Inthna-Asheri, mjukuu wa kike (anayezaliwa na binti yake) wa marehemu, kama mtoto kwa nasaba, huchukuwa mali yote kwa kumuondoa mtoto wa kiume wa kaka yake.

 

(b) Kama Muislamu Sunni akifa, akiacha nyuma binti na kaka, binti huchukuwa mgao ulioainishwa, yaani moja kwa mbili za mwanaume na inayobakia huenda kwa kaka kama Asabah. Chini ya Sheria ya Shia Ithna-Asheri, huchukuwa mali yote, nusu kama kiainisho cha mgao wake, na nusu nyingine kwa itikadi ya kurudisha.

 

6. Kanuni zinazoongoza zinaweza kuelezwa kwa ufupi katika maneno yafuatayo:-

 

(a) Mrithi mwenye uhusiano wa karibu na marehemu hurithi kwa kumfadhilisha zaidi kuliko yule mwenye kufungamana naye kwa mbali;

 

(b) Yeyote yule anayehusiana na marehemu kupitia mtu yeyote harithi wakati mtu yule anaishi;

 

(c) Kaka na dada wa kuzaliwa mama mmoja, baba mmoja wanapendelewa kuliko kaka na dada wa kinasaba; lakini kaka na dada wa tumbo mmoja watarithi pamoja nao.

 

 (d) Wakati uhusiano ni sawa, mwanamume kwa kawaida hupata marudufu ya mgao wa mwanamke, isipokuwa katika hali ya warithi wanaohusiana kwa mama ambao kwa ujumla hugawanya urithi miongoni mwao kwa sawa sawa bila tofauti ya jinsia.

 

Inaweza ikaulizwa kwa nini mgao wa mwanamke, kwa kawaida ni nusu ya ule wa mwanaume?  Kusema kweli, ni yenye mantiki kabisa. Uislamu umemfanya mwanaume kuwajibika kwa ajili ya matunzo ya familia.  Hakuna mzigo kama huo uliowekwa juu ya mwanamke.  Hata mke tajiri anapasika kupata matunzo yake kutoka kwa mume wake ingawa anaweza akawa masikini.  Kwa vile anatakiwa kubeba gharama zote, amepewa mgao marudufu karibu katika kila mirthi.  Vile vile mwanamke hupata mahari ambayo hutoka kwa mwanaume kwenda kwa mwanamke.  Hivyo uwiyano wa migao uliowekwa na Qur’an  Tukufu ni wa haki zaidi.

 

7. MAKUNDI NA TABAKA ZA WARITHI:

 

Katika Shriat za Shia Ithna-Ahsri, warithi wamegawanywa katika makundi mawili, yaani, wale ambao hurithi kwa haki ya “Nasab” (nasaba); na wale ambao wanarithi kwa haki ya ‘Sabab’ ambao kwamba muhimu ni wa ndoa (kuoana).  Makundi yote hurithi kwa pamoja.

 

Kundi la kwanza yaani mahusiano ambayo yanapasika kurithi kwa sababu ya unasaba limegawanyika katika tabaka tatu:-

 

(a) Tabaka la Kwanza:

 

(i) Wazazi na            (ii) Watoto (au katika kukosekana kwao, wajukuu-wowote kwenda chini-yaani: kilembwe, kitukuu na kuendelea).

(b)              Tabaka la Pili:

 

Kama hakuna mrithi kabisa katika tabaka la kwanza, basi wazazi na dhuria wa wazazi wa marehemu watarithi: Ina maana:

 

(i) Babu zake marehemu (wowote kwenda juu).

 

(ii) Kaka na Dada (au katika kukosekana kwao-dhuria wa kaka na dada).

 

(c)       Tabaka la Tatu:

 

Kama hakuna mrithi aliyepo si katika tabaka la kwanza au la pili, basi dhuria wa mababu (wowote kwenda juu) watarithi.  Ina maana: ndugu  wa upande wa kiume na upande wa kike wa marehemu, ami, wajomba na shangazi wa marehemu (au katika  kukosekana kwao, basi watoto wao kwenda chini).

 

Kama ilivyoelezwa hapo juu mume au mke au wakeze marehemu watarithi pamoja na tabaka zote hizi.

 

            8. Dhul – Fardh na Dhul Qarabat:

 

Ni muhimu kutaja kwamba, chini ya sheria ya Shia, warithi katika kundi au tabaka lolote watakalokuwa wamegawanywa katika mafungu matatu, kuhusiana na haki ambayo wanapasika wao kushiriki katika mirathi:-

 

(1) DHUL-FARDH: wale ambao wana haki kwenye mgao ulioainishwa katika mirathi ni hawa:

(a) Mama

(b) Mume

(c) Mjane au Wajane

(d) Mtu au watu wanaohusiana kwa mama yuleyule tu.

 

(2) DHUL-QARABAT: Wale ambao huchukuwa urithi kwa sababu ya uhusiano wao na marehemu, lakini ambao mgao wao hushuka na kupanda kwa kutegemea idadi ya warithi na mazingira.  Hawa ni:-

 

(a) Mtoto au watoto wa kiume

(b) Kaka kamili au katika kutokuwepo kwao ndugu kwa upande wa baba (mama mbali mbali)           

(c) Mababu

(d) Ami na Shangazi

(e) Wajomba na mama wadogo.

 

(3) DHUL – FARDH WAL-QARABAT; Hawa ni warithi ambao wakati mwingine hurithi kwa sababu ya uhusiano wao na wakati mwingine hutegemea migao yao iliyopangwa; hawa ni:

 

 (a) Baba ambaye hurithi mgao uliopangwa kama kuna mtoto wa marehemu; na huchukuwa kwa uhusiano kama hakuna mtoto wa marehemu.

 

 (b) Binti au Mabinti ambao hupata mgao wao uliopangwa bila kuwepo baba wa marehemu au kaka yake au kaka zao wenyewe; na wanachukua kwa ushusiano wakati wakiwa pamoja na yeyote kati yao.

 

(c) Dada kamili au dadaze au katika kutokuwepo kwao, dada wa nasaba au dadaze, ambao hupata mgao uliopangwa wakati bila kuwepo babu au kaka, kakaze wa daraja moja kama wao wenyewe, na huchukuwa kwa uhusiano wakati wakiwa pamoja na yeyote kati yao.

 

Angalia :  Wakati kukiwa na mrithi mmoja tu, imma Dhul-Fardh au Dhul-Qarabat, au mwenye kupasika kwa sababu ya uhusiano maalum wa Sabab (kuoana-ndoa), mrithi kama huyo huchukuwa mirathi yote.  Kwa mfano, binti pekee huchukua mgao wake uliopangwa, yaani, nusu moja na iliyobakia huenda kwake kwa kurudisha.  Mtoto wa kiume pekee huchukua mali yote kwa haki ya Qarabat, hakuna mgao ulioainishwa uliowekwa kwake kwa Sheria.  Wakati marehemu ni mwanamke na hakuacha nyuma yake jamaa anayehusiana na yeye isipokuwa mume, ambaye anahusika na kurithi kwa sababau ya ndoa, anachukuwa urithi wote kwanza kama mgao wake ulioainishwa, na uliobakia kwa kurudisha.

 

            9. MIGAO: Kwa kadiri migao inavyohusika iko sita kwa idadi, yaani:-

 

(1)  Nusu moja (2) Moja ya nne (3) Moja ya Nane

(4) Moja ya tatu (5) Mbili ya tatu (6) Moja ya sita.

 

(1)              NUSU MOJA : Wafuatao wanapasika kwenye nusu moja ya urithi:

 

(a)              Mume wakati mke hakuacha mtoto;

(b)              Binti wakati hakuna mtoto wa kiume;

(c)              Dada kamili kwa kukosekana warithi wengine ambao wametajwa mapema;

(d)              Dada wa nasaba wakati hakuna kaka na dada kamili.

 

(2)              MOJA YA NNE : Wafuatao wanahusika kwenye moja ya nne:

 

(a)              Mume, wakati kuna nasaba ya dhuria ya mke;

(b)              Mke, wakati hakuna nasaba ya dhuria ya mume;

 

 

(3)              MOJA YA NANE : Hii huchukuliwa na mjane au wajane wakati kuna nasaba ya dhuria ya mume.

 

(4)              MOJA YA TATU : Wafuatato wanapasika kwenye moja ya tatu:-

 

(a)              Mama, wakati hakuna nasaba ya dhuria ya marehemu, wala hakuacha kaka wawili, au dada wanne au kaka mmoja na dada wawili.

(b)              Kaka na dada tumbo moja, wakati wakiwa wawili au zaidi katika idadi.

 

(5)              MBILI YA TATU : Wafuatao wanapasika kwenye mbili ya tatu:

 

(a)              Mabinti wawili au zaidi, wakati hakuna mtoto wa kiume;

(b)              Dada kamili wawili au zaidi wakati hakuna kaka kamili au hakuna kakaze (baba mmoja mama mabali mbali).

 

(6)       MOJA YA SITA : Moja ya Sita inachukuliwa na wafuatao:

 

(a)              Wote baba na mama wakati marehemu ameacha nasaba ya dhuria.

(b)              Mama, wakati wanakuwepo pamoja naye kaka wawili au zaidi wa damu kamili au kaka mmoja na dada wawili au dada wanne wa damu kamili (au kwa baba yule tu, baba yule akiwa yupo).

(c)              Kaka mmoja au dada wa tumbo moja.

 

10. MGAWANYO WA MALI: Wakati kuna mmoja tu  wa warithi waliotajwa hapo juu akiwa mwanaume au mwanamke hupata mali yote.  Kama ni Dhul-Qarabat, huipata kwa sababu ya uhusiano; kama ni Dhul-Fardh, kwanza anapata mgao wake uliopangwa, na kisha mabaki anapewa yeye kama kurudisha (Radd).

 

Kama wako warithi wawili au zaidi, itagawanywa katika utaratibu ufuatao: Kwanza mume; au mke au wake  watachukuwa mgao wao; kisha ndugu Dhul – Fardh watapata mgao wao; kisha mabaki yatagawanywa miongoni mwa warithi  Dhul-Qarabat.

 

Mfano: Kutoa mfano  wa utaratibu  wetu, ngoja nichukulie kwamba mtu anakufa anamuacha baba yake, mama, mke, watoto wanne wa kiume, mabinti watano, wajukuu watatu, babu, kaka watatu na shangazi wawili.

 

Kwa vile ameacha wazazi na watoto wakiume na mabinti, ambao wanahusika na tabaka la kwanza la warithi, babu na kaka (ambaowanahusika na tabaka la pili) na mashangazi (ambao wanahusika na tabaka la tatu) wataondolewa kwenye urithi.

 

Hali kadhalika, wajukuu wataondolewa kwa sababu ya kuwepo watoto, juu ya msingi wa karibu kuwaondoa wa mbali zaidi.

 

Mfumo huu wa kuondoa hutuacha na warithi wafuatao: mke, Baba, Mama, Watoto wanne wa kiume na mabinti watano.

 

Mke atapata 1/8 ya mali kwa sababu marehemu ameacha watoto; Baba na Mama wote watapata kila mmoja, moja ya sita 1/6.

 

Kigawanyo cha kawaida cha 8 na 6 itakuwa 24. Hivyo mali itagawanywa katika migao 24 – ambapo kutoka hiyo mke atapata 3 (yaani 1/8), baba 4 (yaani 1/6) na mama vile vile 4 (yaani 1/6). Itaonekana kuwa baba ameshughulikiwa hapa kama Dhul – Fardhi, sio kama  dhul – Qarabat, kwa sababu ya watoto wa marehemu, na mama kupata mgao pungufu (yaani 1/6 badala ya 1/3) kwa sababu ya mantiki hiyo hiyo.

 

Vyovyote vile, baada ya kupunguza 3 + 4 + 4 (yaani 11/24) tumebakiwa na migao 13.  Hii itagawanywa miongoni mwa watoto, mtoto wa kiume akipata marudufu ya mgao wa binti.  Ina maana kwamba – kila mmoja wa watoto wanne wa kiume atachukuwa migao miwili (kufanya 8) na kila mmoja wa mabinti atapata mgao mmoja (kufanya 5).  Hivyo migao yote imekwisha.

 

            11. DHUL-FARDH LAZIMA WAPATE MGAO WAO ULIOPANGWA:

 

Katika mfano wa hapo juu, migao imelingana na mahitaji ya manfungu ya mirathi.  Lakini kuna weza kuwa na hali wakati migao iliyopangwa yaweza kuzidi kigawanyo cha kawaida cha migao. Kwa mfano, kama mwanamke ataacha mume nyuma yake mabinti wawili na mama, migao yao kwa kuhusiana itakuwa moja ya nne, mbili ya tatu na moja ya sita.  Kigawanyo cha kawaida 3, 4, na 6 ni 12, ambacho huwakilisha migao ambayo kwayo mali itagawanywa – 3 ikiwa mgao wa mume, 8 wa mabinti na 2 wa mama.  Lakini 3 + 8 + 2 hufanya 13, sio 12.

Masunni hugawa mali kwenye migao 13, na kuleta upungufu kwa wote.  Lakini miongoni mwa Shia, Mama na mume, wao wakiwa ni dhul-Fardh, lazima wapate mgao wao kamili, yaani 3 + 2.  Na mabaki yaani 7/12 yatagawanywa sawa sawa miongoni mwa mabinti, kwa sababu watoto vile vile ni miongoni mwa Dhul-Qarabat.

Hivyo wakati wowote kunapokuwa na upungufu katika migao iliyopangwa, huangukia juu ya Dhul – Qarabat, ambao migao yao hupasika na kupanda na kushuka, sio juu ya Dhul- Fardh.

 

            12. IMAM : Mrithi wa Marehemu asiye na mrithi:

 

Kama hakuna mrithi katika tabaka yoyote na makundi yaliyotajwa hapo juu, Imam atakuwa mrithi wake.  Kwa vile Imamu wetu yuko kwenye ghaibu kwa wakati huu, Mujtahid atapokea mali ile kwa niaba ya Imamu na ataitumia katika utangazaji wa imani na unyanyuaji wa dini ya Jumuiya ya Shia kwa kupendelea zaidi katika eneo lile lile alilokuwa akiishi marehemu.

 

Mtu ambaye hana mrithi isipokuwa Imamu, ameruhusiwa katika Sheria ya Shia kutoa kwa wosia mali yake yote ili mradi utoaji huo ni kwa ajili ya faida ya Shia Ithna-asheri masikini, Ithna - asheri mayatima au Ithna-Asheri  wasafiri mafukara tu.

 

            13. KUONDOA KUTOKA  MIRATHI :

 

Hakuna  mwandishi wa wosia  mwenye haki yoyote ya kumzuiya  yeyote katika warithi wake kutokana na haki yake ya mgao wa mirathi.  Hata kama anafanya wosia kuhusu suala hili, utakuwa umetenguka na batili katika sheria.  Lakini mrithi atazuiwa kutoka kwenye mirathi kama akitokea kuwa sio Mwislamu au kwa makusudi na kwa dhulma amemuua marehemu ambaye kwamba mali yake angerithi.

 

            14. HATI ZA WOSIA :

 

Ufanyaji wa wosia unatambuliwa na kuhimizwa na Sheria ya Ki-Islamu. Wosia unaweza ukawa wa mdomo au katika maandishi. Mwandishi wa Wosia ameruhusiwa kurithisha mpaka theluthi moja ya mali yake halisi.  Kurithisha kokote kunakozidi theluthi moja ni batili, vinginevyo mpaka ikubaliwe na warithi.  Mpangilio ya hukumu juu ya suala hili unatolewa katika kitabu kilicho andamana “ISALAMIC LAW-Sheria za Ki-Islamu” na sio muhimu kueleza kwa kinaganaga hapa.

 

            15. ULIPAJI WA MADENI NA GHARAMA KUTOKA KWENYE MALI:

 

Inaweza kuonyeshwa hapa kwamba katika hali zote, madeni ya halali yampasayo marehemu pamoja na gharama fulani fulani lazima yapewe umuhimu wa kwanza katika ulipaji wa urithi na migao ya warithi.

 

Neno “Deni”, Maana yake madeni ya kawaida ailiyoyaingia mwenyewe au kwa niaba ya marehemu na hujumuisha vile vile madeni ya kidini kama Zakat (kodi ya maskini) Khumus (hutolewa moja ya tano) Kaffara (malipo ya kosa au fidia), Nazar (nadhiri) nk., na neno “gharama” hujumuisha wajibu wa kupeleka wakili kwa gharama za mali ya marehemu, kutekeleza Hija Makka kama ilikuwa wajibu juu ya marehemu na haikutekelezwa na yeye wakati wa uhai wake.  Gharama za mazishi vile vile zinatakiwa kupewa umuhimu wakulipwa.

 

Baada ya kulipa madeni yaliyotajwa na gharama na urithi ulioelekezwa  na wosia wa marehemu kufikia mwisho wa theluthi moja ya mali halisi, mabaki yatagawanywa miongoni mwa warithi.

 

16. Katika kuhitimisha, tungependa kurudia tuliyoyasema mapema mbele ya Tume juu ya Sheria ya mambo ya Ndoa.  Tunahisi kwamba wazo la kutunga Sheria ya wote kuchukua mahali  pa Sheria ya ki-Islamu iliyopo sasa sio makosa tu bali ni kufuru kwa mtizamo wetu wa kidini.  Itakuwa ni sawa sawa na kuweka dini inayofanana juu ya wote ambapo litakuwa ni wazo lisilo na maana.  Sheria za ki – Islamu ni sehemu ya dini yetu. Sheria hizi haziwezi kubadilishwa au kuvunjwa bila kupata hisia ya hatia na dhambi.

 

17. Hukumu zinazohusu mirathi zimewekwa kwa usahihi wa juu mno na Qur’an Tukufu na zinaelezewa kiukamilifu kwa uwazi katika Hadithi za Mtukufu Mtume na Maimamu kumi na mbili na hakuna shaka hata kidogo kwamba hukumu hizi ni kwa mujibu wa kanuni pana ya undugu wa mtu ambao Uislamu unataka kuanzisha.

 

18. Sheria ya ki-Islamu ya madhehebu ya Shia Ithna-Asheri ni kitu kilichofumwa vizuri.  Hatuwezi kubadilisha au kurekebisha moja au mambo yake mawili bila kuharibu ufumaji mzima.  Kwa mfano, katika Sheria ya Ki-Islamu mtu hawezi kutumia kitu chochote kilichopatikana kiharamu (katika maana ya kidini) amma kwa kidunia au kwa madhumuni ya kidini.  Kama kwa mfano mabadiliko yanafanywa katika sheria ya mirathi, mtu fulani kwa maana hiyo kikawaida atapata zaidi kuliko haki ya mgao aliogawiwa na Qur’an Tukufu na pato hili la haramu litafanya maisha yake yote kuwa duni.  Maisha yake ya kila siku yatakuwa ni orodha ndefu ya kuchupa mipaka; Sala zake, Hija yake, hata chakula chake na mavazi vitakuwa haramu, katika maana ya dini.  Hivyo hawezi kutegemea amani katika maisha ya kesho akhera.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

3

MUHTASARI JUU YA WARAKA WA TANZANIA

JUU YA SHERIA YA NDOA INAYOFANANA

(SAWA) KWA WOTE*

 

ANGALIA: Muhtasari huu kwa kutoepukika imeunganisha baadhi ya ibara kutoka kwenye Muhtasari uliowasilishwa kwenye Tume ya Serikali ya Kenya.

 

*****

 

Kwa niaba ya Jumuiya ya Shia Ithna-Asheri ya Tanzania, tunachukuwa fursa hii ya kuwaslisha maoni yafuatayo kwa mapendekezo ya Serikali juu ya shria inayofanana kwa wote ya Ndoa (Waraka wa Serikali Na. 1 wa mwaka 1969).

 

Madhumuni yaliyodaiwa na mapendekezo haya ni kuondoa hali iliyopo ambayo kwayo “Sheria zilizopo hazitambui Ndoa zote zilizofungwa chini ya Sheria tofauti kama zinazolingana sawa”.

 

Lakini je, ni lazima kwa madhumuni haya kutunga sheria ya ndoa inayofanana kwa wote?  Je, suala hili haliwezi kufikiwa kirahisi kwa kuleta pamoja Ndoa zote chini ya mamlaka ya kisheria ya mahakama moja chini ya rejesta moja?

 

Katika mwaka wa 1964 “Taarifa mpya ya Sheria za ki-Islamu” ilipitishwa inayosema kwamba hukumu za sheria za ki-Islamu za Ndoa ziwekwe katika mpango ulio wazi.  Sheria ndogo chini ya amri hiyo ilichapishwa kama nyongeza ya Gazeti Na. 34 la 27 Juni 1967.  Hii ndio ilikuwa iwe ni awamu ya kwanza.

 

Tunashangaa kwa nini sera  hii haikuweza kuendelezwa, au angalau kupanuliwa kujumlisha tofauti za sheria za ndoa za kimila hali kadhalika na za ki-Baniani na za Kikiristo.  Sheria hizi zingeweza kupangiwa kanuni na kuwekwa chini ya mamlaka ya kisheria ya Mahakama moja.

 

Hapo, na hapo tu, sura yenye mambo mengi ingeweza kuongezwa kushughulikia migongano ya sheria; (ni) baadhi ya mifano ambayo kwamba imetolewa katika Waraka wa Serikali.

 

Tunatambua kwamba matatizo mabalimbali ya jamii yanayojitokeza ya matumizi mabaya au tafsiri potofu za sheria za kimila au zakidini kwa ujumla hutoa sabau kwa Serikali kuhusika kwa makini.  Serikali katika juhudi za kuwapatia watu wake ustawi katika suala hilo, inakabiliwa  na jukumu la kutokomeza maovu ya kijamii.

 

Juhudi yoyote katika muelekeo huu yafaa kuungwa mkono na kustahiki ushirikiano wote.  Lakini tunahisi kwamba wazo la kutunga Sheria ya wote kuchukuwa mahali pa taarifa mpya ya shria ya Ki-Islamu sio sahihi.

 

Hata desturi zakimila (zisizo na mamlaka ya ki-Mungu) ni ngumu kubadilisha.  Hii huwa hatari mno zaidi katika suala la sheria ya ki-Islamu ambayo ni sehemu muhimu ya dini yetu.  Sheria hizi haziwezi kuvunjwa bila kupata hisia ya hatia na dhambi.

 

Kwa hiyo tunahisi kwamba njia nzuri ingelikuwa “kuacha mamia ya maua kuchanua.”  Umoja wa kitaifa hauhitaji kwamba raia wote lazima wawe na lahaja inayofanana au imani ya dini inayofanana. Hivyo  kwa nini inafikiriwa kwamba  ni muhimu kuwa na Sheria ya Ndoa na Talaka inayofanana ya kutumika kwa watu wote wa Tanzania?

 

Sheria zetu za Shia Ithna-Asheri hazikutegemezwa juu ya “Ra’i (maoni) au “Qiyas” (analojia).  Zimetegemezwa kabisa juu ya Qur’an Tukufu na Hdithi za Mtukufu Mtume na Maimamu wetu Kumi na Mbili.

 

Kwa vile waraka unahusika na mambo ya Ndoa, lazima tuonyeshe kwamba kanuni zetu za msingi za Ndoa na Talaka zimetegemezwa juu ya Qur’an  Tukufu.  Mambo ambayo hayako wazi katika Qur’an yanaelezwa katika  Hadithi.

 

Wanachuoni wetu ambao wanaitwa MUJTAHID  hawatoi hukumu yoyote kwa maoni yao, analojia (Qiyas) au (kwa) ijimai.  Hakuna mamlaka kama hayo yaliyotolewa kw ayoyote katika sheria ya madhehebu yetu.  Wanaweza  kutofautiana katika kutafsiri Hadithi fulani zinazohusu baadhi ya mambo madogo, lakini hata hivyo tofauti hiyo ni tofauti katika tafsir, sio ya maoni.

 

Shia Ithan-Asheri hufuata katika mambo yote ya dini hukumu za Mujtahid mkubwa wa zama.  Anachukuliwa kuwa yeye ni muwakilishi wa Imamu wetu wa kumi na mbili na ni mtu (mwanachuoni) wa mwisho juu ya mambo yote ya kidini.

 

Kwake yeye mumewekwa ndani yake masuala fulani, uwezo wa ulezi wa watoto, ndoa na talaka, utekelezaji wa wosia na mali ya marehemu na mambo kama hayo.

 

Sheria ya ki-Islamu ya madhehebu ya Shia Ithna-Asheri ni chombo kilichofumwa vizuri.  Hatuwezi kubadilisha au kurekebisha moja au mbili ya mambo yake bila kuharibu ufumaji wote.

 

Kwa mfano, hukumu za ndoa na talaka zinabeba uzito wa moja kwa moja juu ya uhalali wa mtoto; juu ya dhambi ya pamoja ya mwanaume na mwanamke katika haki ya wao kwa wao wenyewe ya mirathi na ile ya mtoto. Mbali na mambo mengine ya jamii na matatizo halai.

 

Katika sheria ya ki-Islamu mtu hawezi kutumia kitu chochote kilichopatikana kiharamu (kwa maana ya kidini) amma kwa kidunia au kwa madhumuni ya kidini.  Kwa hiyo, kama mabadiliko yanafanywa katika sheria za mirathi, kwa mfano, mtu fulani anapewa zaidi kuliko  haki ya mgao wake kwa mujibu wa Qur’an Tukufu maisha yake yote yatakuwa duni.  Maisha yake ya kila siku yatakuwa ni orodha ndefu ya kuchupa mipaka, Sala zake, Hija, chakula na mavazi vitakuwa haramu katika maana ya dini.

 

Hivyo ni wazi kwamba mfumo wa Sheria ya ndoa, talaka na mirathi hauwezi kubadilishwa.  Vinginevyo hii itaanzisha muingilio wa moja kwa moja katika dini yetu.

 

Kuhusu haki ya mwanamke katika sheria ya ki-Islamu tunataka kuwakilisha kwamba:

 

Katika sheria ya madhehebu yetu mwanamke anazo haki hizo, upendeleo na ulinzi kwa muda wa Karne Kumi na Nne zilizopita, nyingi ya hizo hazikufikiriwa katika jamii zisizo za ki-Islamu mpaka kwenye Karne iliyopita na baadhi ya hizo mbele ya inayoitwa zama ya kisasa.

 

Uislamu kwa mujibu wa madhehebu ya Shia umempa mwanamke haki ya kufanya mkataba yeye mwenyewe katika ndoa kama ni mtu mzima na makanifu.

 

Uislamu umempa Mwanamke kitambulisho cha kujitengemea.  Mwanamke wa ki-Islamu anamiliki mali yake mwenyewe hata baada ya kuolewa, na mume hawezi kuiingilia.

 

Mwanamke anaweza kumfungulia mume wake mashitaka, anaweza kutoa ushahidi dhidi yake.  Anarithi kutoka kwa mume kwa haki na mwanaume kutoka kwa mwanamke.  Haki hii ya wote pamoja ya mirathi (kurithiana) ilitolewa wakati hakuna jamii kamwe ilifikiria kuhusu haki hii.

 

Mgao wa mwanamke kwa kawaida ni nusu ya ule (mgao) wa mwanaume.  Lakini hii ni mantiki kabisa.  Uislamu umemfanya mwanaume kuwa na jukumu la kutunza familia.  Hakuna mzigo kama huo uliowekwa juu ya mwanamke.

 

Hata mke tajiri anahusika kupata matunzo yake kutoka kwa mume wake ingawa anaweza kuwa ni masikini.  Kwa vile matunzo ya familia ni jukumu la mwanaume, amepewa ngao marudufu karibu katika mirathi yote.

 

Mwanamke hupata Mahr (sio bei ya kuziba pengo ambalo ni geni kwenye fikira za Ki-Islam) ambayo hutoka kwa mwanaume kwenda kwa mwanamke.  Uwiyano wa mgao uliowekwa katika Qura’an Tukufu kwa hiyo ni wa haki  zaidi.

 

Sheria ya Uislamu ihusikanayo na Wosia hairuhusu mtu kuusia zaidi ya thuluthi moja ya mali yake kamili.  Hivyo hali ya kifedha ya wale watakaokuwa warithi (pamoja) na mke siku zote inalindwa na kutwaliwa isivyo haki na yeyote.  Usalama huo bado  unakosekana katika jamii nyingi ambazo huruhusu mtu kutoa mali  yake yote hata kwa mgeni.

Sasa tukija kwenye waraka wa Serikali wenyewe, kuna pendekezo moja ambalo katika  mfumo wake uliopo, hukata ndani kabisa kwenye mzizi wa dini zote.  Ni ule ushauri wa kwamba, “kama mwanaume ana kaa na mke kinyumba kwa muda wa zaidi ya miaka miwili basi atachukuliwa kwamba amemoa mwanamke huyo, na kama wamepata watoto, (basi) watoto hao watachukuliwa kuwa watoto halali  wa mume na mke huyo.”

 

Kama nia ni kutoa usalama kwa mke halisi ambaye Ndoa yake haikusajiliwa au ambaye Cheti chake cha Ndoa kilipotea, neno kinyumba halileti maana.

 

Itapaswa libadilishwe kwa (maneno), “Kuishi pamoja kama mume na mke katika mazingira ya kifamilia, mradi inawezekana kwa wao kuoana na mmoja wao akadai ndoa ambayo haikukataliwa na mwingine; au katika hali ya kifo cha mmojawapo, kwa kawaida inajulikana kwamba walikuwa wameoana na haithibitishwi kwamba hakukuwa na ndoa kabisa.”

 

Vile vile, tulitaja mapema, katika Uislamu mke hana wajibu wa kumtunza mume.  Hivyo, makusudio ya Waraka kumfanya mke apasike kumtunza mume wake inakwenda kinyume kabisa na mamrisho ya Qur’an Tukufu.

 

Kwa vile mjadala unaendelea juu ya suala la mitala, ni muhimu kuthibitisha tena kwamba tumeridhishwa vya kutosha na hali yenye kutaka kwa hakika umuhimu wa mitala katika hali nyingi. Jamii ya ki-Afrika, kama Waraka kwa usahihi unavyothibitisha, ni jamii ya ki-Mitala.  Uislamu unakubaliana nao.  Lakini Uislamu umeweka mpaka kwa wake wanne kwa wakati mmoja na umeamrisha, kwa taratibu makhsusi, usawa katika huduma na haki ya wake wote kama waraka unavyotaka iwe.

 

Inapasa ikumbukwe kwamba mitala sio kitu cha lazima wala hakitetewi.  Ni ruhusa tu yenye mipaka fulani na mashariti.  Na katika baadhi ya mazingira ruhusa hii imeonyesha kuwa yenye manufaa mno.

 

Kwa mfano: kama mke ana ugonjwa sugu, au mgumba au kwa sababu nyingine fulani haiwezekani kwa wawili hawo kuishi kama mume na mke.  Suluhisho litolewalo na jamii fulani ni kumtaliki mke na kuoa mwingine.  Lakini, je ni haki?  Je, ni wema au uadilifu kumfukuza mwanamke katika hali ya uzee, katika umri wake wa kati kutoka kwenye nyumba yake, kwa sababu amekuwa mgonjwa siku zote au ametokea kuwa mgumba?.

 

Uislamu hupinga ukatili huo kwa kuruhusu mitala.

 

Hii ni mbali kabisa na utafiti wa kitakwimu kwamba wanawake wanawazidi wanaume katika Tanzania, wanawake 100 kwa wanaume 95; au katika ile misiba fulani kama vita, wanaume hukumbana na kifo zaidi kuliko wanawake.  Kama mitala hairuhusiwi na jamii, italazimisha aslimia tano ya wanawake nchini kujiingiza katika ukahaba.

 

Tunafikiri kiasi hiki kitatosha kuonyesha hekima ya Waraka wa Serikali katika kutambua mitala kama halali na desturi yenye “manufaa”.  Lakini, katika mfumo wake wa sasa, Waraka hautakidhi madhumuni yanayohitajiwa.  Je, itatokea nini kama pamoja na hali kuruhusu ndoa ya pili, mke wa kwanza akakataa kwa “hiari na kwa uhuru kukubali kuigeuza ndoa ya mke mmoja”  kuwa ya mitala?  Je; haitamlazimisha mwanaume kuwa “kwenye hali ambapo amma amtaliki mke wake wa kwanza au akae kinyumba (isvyo halali) na mke mwingine”,  pamoja na athari zake zote zisizofaa zisizoepukika?.

 

Njia nzuri ni kumtaka mwanaume aende kwenye baraza (au mahakama) iliyopendekezwa ya ndoa au kamati ya jumuiya yake na kuwathibitishia haja zake.  Kama wakikubali, kukataa kwa mke wa kwanza hakupasi kufikiriwa kabisa.

 

Tunachukulia kwamba, kwa vile hakuna suala la kubadilisha asili ya ndoa  katika ndoa ya Mwislamu, Mwislamu hatahitaji idhini ya mke wa kwanza  (au wake) kabla ya kuoa mke mwingine.

 

TALAKA: Hakuna haja ya kusisitiza kwamba katika hali fulani talaka ndio suluhisho pekee lililobaki kwa wanandoa.  Manufaa ya mfumo wa talaka yanaweza kuonekana kutokana na ukweli kwamba hata mabaniani na wakristo wamelazimika kwa nguvu ya moja kwa moja isiyoepukika kutunga sheria za talaka.  Waraka umetambua hoja hii.  Vile vile lazima ikumbukwe kwamba Uislamu, wakati ambapo unakubali hoja hii katika hali fulani, umetamka kwamba ni “Sheria halali yenye kuchukiza mno”.  (makuruhu), itumikayo tu katika hali zilizo ngumu mno.

 

Qur’an Tukufu imeweka chombo cha usuluhisho na jumuiya nyingi za ki-Islamu zina kamati kama hizo.  Kwa bahati mbaya baadhi ya pande fulani hawakupendelea kabisa mfumo huu muhimu.  Matumizi haya mabaya ya uhalali wa talaka lazima yaachwe na jaribio la waraka kudhibiti hali hii linakaribishwa sana.

 

Masharti ya Talaka: Lazima tuonyeshe katika mwanzo kwamba madhehebu ya Shia Ithan-asheri ya Sheria ya ki-Islamu imeweka kanuni ngumu zilizotegemezwa juu ya Qur’an Tukufu na Hadithi kuhusiana na talaka.  Talaka inaruhusiwa mradi tu inatamkwa mbele ya watu wawili mashahidi “Adil” (watu waliothibitishwa uaminifu wao) ambao husikia maneno na kuelewa chanzo cha talaka.  Talaka lazima itamkwe katika utaratibu uliothibitishwa.

 

Zaidi, ni lazima vile vile kwamba mume awe mtu mzima, mwenye akili timamu na mwenye kuelewa vizuri, atendaye kwa utashi wa uhuru wake mwenyewe na sio katika mshituko wa hasira au kutishwa, na kwamba lazima awe na nia ya dhahiri ya kuvunja ndoa.

 

Kwa kadiri mwanamke anavyohusika, yeye wakati wa talaka lazima awe katika hali ya tohara na kwamba talaka haiwezi kutamkwa hata wakati wa tohara ambao kwamba mume amekutana naye kimwili.

 

Kama moja ya mashariti yaliyotajwa hapo juu yakivunjwa, talaka itakuwa batili na kutenguka.

 

Sheria ya ki-Islam haimpi mwanamke haki ya kutoa talaka, maoni yoyote kwamba mwanamke apasa kupewa haki ya kumtaliki mumewe yatakuwa ni kuingilia maadili ya dini, ambayo waraka umekariri kusema, sio nia ya Serikali.

 

Familia ni msingi wa jamii, na kama ilivyo kila jamii, huhitaji mamlaka ya mwisho kuhifadhi nidhamu na ustawi wa jamaa (wa familia).  Uislamu umetoa nafasi hiyo kwa mume ambaye amepewa haki ya kutoa talaka.

 

Lakini mwanamke wa ki-Islamu anapasika kutoa maombi ya kuvunja ndoa au kuibadilisha yeye mwenyewe katika mazingira yafuatayo:-

 

·        Anaweza kuomba (Khula) ambayo yaweza kukubaliwa juu yake na mume.

 

·        Anaweza kumuomba Mujtahid (ambaye ni Kadhi katika Sheriat za Shia Ithna – Asheri) kumpa talaka kama mume maetoweka, au anakataa kumtunza.

 

·        Anaweza kuifuta ndoa kama mume ni mwenda wazimu au akawa mwenda wazimu baada ya ndoa.

 

·        Na anaweza kuibatilisha ndoa (baada  ya kupeleka suala lake kwa Mujtahid) kama mume ni hanithi.

 

Itakuwa muhimu, wakati wa kuandika hati ya rasimu, kutambua talaka iliyotolewa na Mujtahid na ubatilisho wa ndoa kwa kadiri ambavyo ndoa za Shia Ithna-Asheri zinavyohusika.

 

Hukumu zilizotajwa hapo juu zinauhusiano juu ya masharti ya waraka kuhusiana na mume aliyetoweka.  Kutoa talaka kwa Mujtahid (au hakimu katika suala la wasio kuwa Shia Ithna – Asheri au wasiokuwa Waislamu) ni sahihisho bora zaidi kuliko kudhania kwamba mume kafa (kwa madhumuni ya ndoa yake) na kudhani anaishi (kwa madhumuni mengine, pamoja na ndoa nyingine kama ipo yoyote) wakati mmoja na huo huo!

 

Kwa vile Waraka kwa usahihi hutambua talaka iliyotolewa na mume mwislamu kama mwisho (wa ndoa), na kuitaka mahakama kusajili talaka hiyo bila uchunguzi wowote zaidi, tunataka kusisitiza kwamba talaka kama hiyo iwe inafanya kazi kuanzia tarehe ya kutamkwa kwa utaratibu wa talaka na mume, na sio tarehe ya kusajiliwa.

 


Waraka humtaka Mwislamu akusudiaye kutoa taarifa ya kusudio lake siku 21 kabla kwa “Sheikh aliyeruhusiwa na Waziri kufungisha Ndoa.”

 

(Waraka) umepuuza ukweli kwamba Mvulana wa ki-Islamu na msichana wanaweza kufunga Ndoa wao wenyewe bila kuwa na haja ya “kumwita Sheikh na kumuomba afungishe ndoa”.  Tuna hakika sio nia ya Serikali kutengeneza Sheria mpya ya Uislamu ambayo ingelianzisha wachungaji kama wa Kikristo.  Basi nini hii maana ya kutajwa Sheikh aliyeruhusiwa na Waziri?  Ni wazi kwamba wazo hili linakwenda kinyume kabisa na Uislamu.

 

Vile vile tunashindwa kuona haja yoyote kwa ajili ya pendekezo hili la taarifa ya siku 21.  Tuchukulie msichana kutoka Kigoma na mvulana kutoka Pangani (wote wanaishi Dar es Salaam).  Wakamjulisha Sheikh wa Jumuiya yao mjini Dar es Salaam kwamba wanataka kuoana.  Sheikh yule hatarajiwi kuchapisha au kutangaza kusudio la ndoa katika magazeti au radio.  Basi, vipi ataweza kujua kama kuna kikwazo chochote cha halali dhidi ya ndoa ile?

 

Na hata hivyo, hakutakuwa hata ndoa moja kama hiyo ya kusudio la kiharamu katika ndoa elfu moja.  Tunafikiri, ni bora kuiondoa sheria hii na kuibadilisha na nyingine kwa maana kwamba kama itakuja kufahamika hata baada  ya kuona  kwamba wasingeweza kuona kihalali, ndoa itakuwa batili na kutenguka kuanzia mwanzo.

 

Kwa kadiri usajili wa Ndoa na Talaka unavyohusika, katika Jumuiya yetu rejesta za ndoa zimekuwepo kwa zaidi ya miaka 125 na tunatoa vyeti kwa wanandoa.

 

Lakini lazima tusisistize kwa nguvu sana kwamba uhalali wa ndoa au talaka hauwezi kufanywa kwa kupasishwa na usajili.  Yaweza ikafanywa kuwa ni kosa kwa zile ambazo hazikusajiliwa; lakini isije ikaathiri uhalali wa ndoa au talaka.

 

Hivyo hivyo, katika hali nyingine pia, kama ndoa ni sahihi kwa mujibu wa dini, isije ikachukuliwa kuwa ni batili kama inapingana na masharti yoyote yaliyowekwa na waraka.  Vinginevyo, itakuwa ni uingiliaji wa moja kwa moja katika dini.

 

Madhumuni ya muhtasari huu ni kuidhihirishia Serikali kwamba utungaji wa sheria lazima ufanye juhudi ya kuhifadhi sheria za dini za Jumuiya mbalimbali zinazoishi chini ya bendera moja,  hususani wakati sheria hizo zikiwa ni zenye athari nyingi juu ya misingi hiyo kama ndoa na maisha ya kifamilia.

 

Kama tulivyoonyesha mapema, katika Uislamu Sheria na dini havitenganishwi, kwa vile sheria zetu zimeanzia kutoka kwenye Qur’an Tukufu ni wazi kwamba kama sheria yoyote inatungwa ambayo imma hupingana na maamrisho ya Qu’ran au Hadithi; kwa kawaida itasababisha  vurugu kubwa katika akili za Umma wa ki-Islamu na kwa hiyo Jumuiya yote ya Uislamu itakuwa katika usumbufu.

 

Mwishoni, tunapenda kufanya muhtasari wa maoni yetu kwa ifuatavyo:

 

Tunahitaji kwamba badala ya kutunga Sheria inayofanana kwa wote, “Amri ya Taarifa mpya ya Sheria za “ki-Islamu” lazima ziwe katika matumizi kwa ajili ya Waislamu na uandikwe muswada wa Sheria ndogo chini ya Amri hiyo, uchapishwe na ifanywe itumike kwa mapema iwezekanvyo.

 

Kwa kadiri mapendekezo ya Waraka yanavyohusika tunakubali kabisa kwamba “Ndoa lazima iwe muungano wa hiari” (ibara ya 6 ya waraka maelezo ya Kiingerza) kwamba wanandoa wasije wakawa ndani ya hadhi iliyokatazwa ya undugu au unasaba (ibara ya 9); kwamba yeyote kati ya mume au mke anweza kumiliki mali yake mwenyewe.” (ibara ya 19);  kwamba mke awe na uwezo wa kutoa ushahidi dhidi ya mumewe (ibara ya 21); kwamba kuwe na masharti ya talaka “kama ndoa imevunjika kabisa” na kwamba “Talaka zisishughulikiwe juu juu (ibara ya 24); na kwamba kuwe na mabaraza ya usuluhisho” na “utambulisho kamili upewe mabaraza kama hayo ambayo yapo katika Jumuiya mbali mbali kabla ya sheria hii mpya unayokusudiwa” (ibara 25).

 

Tunakubaliana na mapendekezo yafuatayo pamoja na masharti na sifa fulani:-

 

Umri wa chini wa miaka 15 na 18 kwa wasichana na wavulana mtawalia (ibara ya 7) na usajili wa ndoa (ibara ya 17), na wa talaka (ibara ya 27) ni mambo mazuri tunakubaliana nayo ilimradi, kuvunja au kukiukwa kwao hakufanyi ndoa au talaka batili na kutenguka.

 

Matamshi ya Mwislamu ya Utaratibu (formula) ya talaka yanatambuliwa na Waraka kama ushahidi wa kuvunjika kabisa kwa ndoa na mahakama inapaswa “kutoa cheti cha kuvunja ndoa”.

 

Tunakubali pendekezo hili, ilimradi cheti kinachosemwa kinaanzia nyuma kuanzia tarehe ya kutamkwa kwa utaratibu wa talaka na mume.

 

Tuko katika maafikiano kamili na pendekezo kuruhusu Ndoa ya mke mmoja kubadilishwa kuwa ya mitala.  Lakini hatufikirii kuwa ni busara kusisistiza juu ya idhini ya mke wa kwanza (ibara ya 12).  Mume anapaswa kuwa na haki ya kwenda kwenye baraza la Ndoa lililopendekezwa na uamuzi wao utakuwa wa mwisho.

 

Vile vile, tunaona kwamba Ndoa ya Mwislamu ikiwa yenye uwezekano wa mitala, mume wa ki-Islamu hatatawaliwa na sharti hili.

 

Tunafikiri kwamba pendekezo la kudhania mume (aliyetoweka kwa muda wa miaka 5) kama aliyekufa sio la busara.  Njia nzuri ni kumruhusu Hakimu (au Mujtahid) kutoa talaka kama mazingira yatahitajia hivyo.

 

Haki ya mwanamke kudai talaka au kuvunja au kutengua ndoa lazima ikomee kwenye mazingira yaliyotajwa mapema katika muhtasaari huu.  Utungaji wowote wa sheria  uendao kupita mpaka huo, utakuwa ni uingiliaji wa moja kwa moja katika dini yetu.

 

Tunakataa kwa nguvu pendekezo kwamba kukaa kinyumba na mwanamke kwa muda wowote (mpaka wa miaka 2 ni wa kiholela kabisa) huwafanya hao wawili mume na mke kihalali.  Vinginevyo mpaka utamkaji unabadilishwa kama, ilivyopendekezwa katika ibara ya 11 ya muhtasari huu, pendekezo hili haliwezi kukubaliwa.

 

Tunakataa kabisa pendekezo la kumfanya mke kuwajibika kumtunza mume wake (ibara ya 19).

 

Tunafikiri kwamba pendekezo la kutaka taarifa ya siku 21 halina maana kabisa, na kuunganisha katika hali ya Waislamu pamoja na usemi “taarifa itapelekwa kwa Sheikh, ambaye ameruhusiwa na Waziri kufungisha ndoa” huhitaji kuangaliwa kwa tahadhari sana, kwani huonyesha kuanzishwa kwa sheria mpya ya uchungaji ambao ni kinyume kabisa na misingi ya Ki – Islamu.  Kwa hiyo hatuwezi kukubaliana nalo.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

4

MUHTASARI JUU YA HIJABU NA MIRATHI*

 

 

Mheshimiwa Rais,

 

1. Kwa niaba ya Jumuiya na mashirika mbali mbali ya ki-Islamu, tunachukua fursa ya kufanya wasilisho hili kwa ajili yako wewe Mheshimiwa kulifikiria kwa huruma.

 

2. Kaika wasilisho hili tunakomea wenyewe kwenye masuala mawili ambayo yalikuwa yakikera akili zetu kwa muda mrefu.  Nayo ni:  Hijabu kwa ajili ya wasichana wa ki-Islamu katika taasisi za elimu na Sheria za ki-Islamu zinazohusu Wosia na Mirathi.

 

3. Mheshimiwa:  Sisi wote ni raia wa nchi huru, na tumejipa katiba ambayo, pamoja na mambo mengine kuhakikisha uhuru wa kuabudu, dini, muungano na kuzungumuza.  Hususan tanarejea kwenye Ibara 18 (1), 19 (1) (2) na 20 (1) ya Katiba ambazo ni kama ifuatavyo:-

 

18 (1) Bila chuki kueleza shria za nchi, kila mtu anao Uhuru wa kutoa maoni na kuzungumza, na kutaka, kupokea, kugawa au kusambaza habari na maoni kupitia chombo chochote cha habari bila kujali mipaka ya kitaifa, na vile vile ana haki kutokana na kuingiliwa mawasiliano yake.

 

19 (1) Kila mtu ana haki ya Uhuru wa mawazo au dhamira, itikadi au imani, na hiari katika mambo ya dini, pamoja na uhuru wa kubadili dini au imani yake.

 

19 (2) Bila chuki kwenye sheria zinazohusika za Jamhuri ya Muungano, taluma ya dini, ibada na utangazaji wa dini utakuwa huru na jambo la binafsi la mtu binafsi, na mambo na uendeshaji wa vyombo vya Dini hautakuwa sehemu ya shughuli za mamlaka ya Dola.

 

20 (1) Kila mtu ana haki ya kupewa uhuru, kutegemea Sheria za nchi, kukusanyika kwa uhuru na kwa amani, kuunganika na kushirikiana na watu wengine, kutoa maoni hadharani, na muhimu zaidi kuunda au kujiuunga na mashirika au vyama (vikundi) vilivyoundwa kwa madhumuni ya kuhifadhi au kuendeleza itikadi zake au masilahi yoyote mengine.

 

4.  Allah (SWT) amesema katika Qur’an Tukufu

neno lake la mwisho:

 

“Na sikuwaumba majini na watu isipokuwa kwamba wanitumikie mimi”. (Sura 51, aya 56) Waislamu wote kuanzia mwanzo kabisa wanakubali kwamba neno “li ya budun” ambalo linatokana na (neno) “Ibadah” na linatafsiriwa hapa kama “tumikia”, maana yake unyenyekevu kamili.

 

Mheshimiwa: Hakuna awezaye kufahamu zaidi kuliko busara zako nzuri kwamba “Ibadah” katika Uislamu sio kawaida ya baadhi ya ibada zenye kutekelezwa katika nyakati au siku makhususi.  Huzunguka maisha yote ya Mwislamu.  Uislamu maana yake kujisalimisha kwenye majaaliwa ya Allah (SWT) na wakati tunapoahidi kufanya hivyo tunaitwa Waislamu (ili) kutuongoza katika maisha yetu ya kidunia, na kutusaidia kufika karibu Yake katika maisha ya kesho akhera Allah (SWT) ametuma kwetu kupitia kwa Mtume Wake wa mwisho (s.a.w.) mfumo wa sheria wenye mambo mengi unaojumuisha mambo yote ya maisha … ya nyumbani, ya kijamii ya kifedha, ya kimaadili na ya kiroho.

 

5. Mheshimiwa unajua vizuri sana kwamba Qur’an Tukufu haikushughulikia suala lolote la sheria kwa ufafanuzi zaidi (na uanagalifu) na katika namna ya utaratibu kwama sheria ya ndoa, wosia, mirathi na mambo mengine yanayohusika nayo, pamoja na adabu ya mavazi kwa wanawake.

 

6. HIJAB:  Ni lazima iwekwe wazi kuanzia mwanzo  kwamba hukumu zinazoelekeza Wanawake kuvaa katika namna ambayo hufunika mwili wote na kuhifadhi muruwa wao zimetajwa kwa wazi katika Qur’an Tukufu.  Ni urithi wa kawaida kwa Waislamu wote na haukukomea kwenye madhehebu au Jumuiya fulani.  Vile vile, sio mila ya kitamaduni, ni sheria ya lazima ya Mungu, na haiwezi kuachwa bila kupata hisia ya dhambi na hatia.

 

7. Kuna aya si chini ya tisa katika sura mbali mbali za Qur’an Tukufu zinazofafanua hukumu ya Hijab. Kwa ruhusa yako Mheshimiwa tunanukuu mbili ya hizo hapa chini:-

 

“Nasema (Ewe Mtume) kuwaambia waumini wanawake wainamishe macho yao, na wazilinde tupu zao, wala wasidhihirishe viungo vyao isipokuwa vinavyodhihirika; na waangushe shungi zao mpaka vifuani mwao, na wasionyeshe mapambo yao ila kwa waume zao, au baba zao,  au baba za waume zao, au watoto wao, au watoto wa waume zao, au kaka zao, au wana wa kaka zao, au wana wa dada zao, au wanawake wenzi wao, au wale iliyowamiliki mikono yao ya kuume, au watumishi wanaume wasio na matamanio ya kijinsia au watoto wadogo ambao hawajapata elimu ya siri za wanawake; wala wasipige miguu yao ili yajulikane wanayoyaficha katika mapambo yao; na tubieni nyote kwa Allah; enyi waumini, ili mpate kufudhu (kesho akhera)”. (Sura 24 Aya 31).

 

‘Ewe Mtume’.  Waambie wake zako, na binti zako na wanawake wa waumini wateremshe chini “Jilbab” zao, ili kwamba wapate kuhishimiwa ….” (Sura 33, Aya 59).

 

(Jilbab = Joho Kubwa kuliko shela na fupi kuliko kashida, ambayo hufunika kichwa na kifua cha mwanamke).

 

8. Kwa kutegemea  juu ya aya hizi na aya nyingine za Qur’an Tukufu na Hadithi sahihi za Mtukufu Mtume (SAW) Wanachuoni wa ki-Islamu, bila utengano wowote wa hitilafu, wameamuru kwamba:-

 

(a) Wanawake wa ki-Islamu lazima wafunike mwili mzima wakati wanapotoka majumba yao.  Uso tu (lakini sio kichwa na nywele ) na viganja vya mikono vinaweza kuwa wazi.

 

(b) Kuna hukumu maalum nz za shuruti za mavazi kwa ajili ya Sala na Hajj.

 

(c) Nguo isiwe yenye kubana kuonyesha mikunjo kunjo ya mwili, wala nyepesi, (na kuonekana) kuyashinda madhumuni ya vazi (kama ilivyokusudia).

 

(d) Wanawake hawapaswi kuvaa vazi ambalo kwa ujumla hutumiwa na wanaume, wala wanaume kuvaa za wanawake.

 

9. Mheshimiwa! Wizara ya Elimu katika nchi yetu imechagua sare kwa ajili ya wasichana wa shule za msingi, ambayo ni mfano wa vazi la kimagharibi.  Tunashangaa kwa nini uamuzi kama huo ulichukuliwa.  Blauzi na sketi sio vazi la ki-Afrika, wala si la kikristo au la ki-Islamu.  Kwa nini mtindo huo ni mtakatifu mno kiasi kwamba hauwezi kubadilishwa?  Ingelikuwa vizuri zaidi kuwa na hamu yetu yakitaifa badala yake kuamuru (kuvaa) gauni refu na bui bui.  Kwa vile ni vazi linalovaliwa na mamilioni ya wanawake wa ki-Afrika.  Je, si wakati muafaka kwamba wenyewe tunaondokana na tabia kwamba yote yale yanayokuja kutoka nchi za Ulaya (Magharibi) ni mazuri kwetu, ambapo maadili yetu wenyewe ni ya “kishenzi”?

 

10. Kwa mtazamo wa ukweli hapo juu, kwa unyenyekevu Mheshimiwa tunaomba uielekeze Wizara ya Elimu kuagiza (uvaaji) wa sare kama hizo kwa wasichana wa shule zenye kufunika vichwa vyao na mwili mzima, kuacha wazi nyuso na viganja. Inaweza kurahisishwa kwa kuvaa:      skafu, gauni, suruali na soksi.

 

Tunaamini kwamba itakuwa ni sare yenye heshima zaidi, na itaruhusu hata wasichana kushiriki katika riadha na michezo kwa uhuru bila hofu ya kuonekana aibu yoyote.

 

            11. Mheshimiwa:

 

Kama kwa sababu yoyote ni vigumu kuanzisha sare hizi kwa wasichana wote, basi  wasichana wa ki-Islamu waruhusiwe nchi nzima kuvaa sare hizo bila pingamizi au kizuizi chochote, kwa vile ni sheria ya dini yao na sio kikabila au mila ya kitamaduni.

 

12. Kabla hatujaendea masuala mengine, tungependa kwa huruma zako Mheshimiwa kutoa taarifa kwako kwamba wasichana wa ki-Islamu wanaoishi Uingereza na Ufaransa wamepata haki yao ya kuvaa Hijab mashuleni, ingawa ilichukuwa hatua za kimahakama (na katika suala la Ufaransa, uingiliaji kati ya Tume ya haki za binadamu ya  Uingereza) kuipata haki hiyo.  Karibu na nyumbani nchini Kenya,mwaka huu (1990) msichana Mwislamu wa ki-Afrika alishinda kesi mahakamani dhidi ya mamlaka za shule wakati zilipokataa kumruhusu kuingia shule na Hijab. Gazeti rasmi la KANU (liitwalo) the Kenya times (Nairobi) liliandika tahariri tarehe 2/2/1990 ambayo kwayo pamoja na mambo mengine liliandika:

 

“ Kwa nchi ya Kidemokrasia kama hii yetu, ambako uhuru wa kuabudu kwa dini zote umehifadhiwa katika Katiba, ni vigumu kuamini kwamba baadhi ya watu wanaona ni sawa kuwanyima wengine uhuru huu”.

 

“Dini, kama tujuavyo, ni jambo lililo karibu sana na mioyo ya baadhi ya watu kuwanyima uhuru wa kuelezea hisia zao wakati wowote wanapotaka kufanya hivyo ni kuwa dhidi ya juhudi zote katika  kujenga jamii yenye amani na upendo”.

 

“Chukuwa Uislamu kwa mfano, ni mfumo kamili wa maisha.  Kumtaka mfuasi yeyote muaminifu wa dini hii kuacha baadhi ya mambo ya maisha haya, hakika ni kumuambia akatae yale yalioandikwa katika Qur’an Tukufu.  Na sisi ni nani, katika wadhifa wowote ule uwao tunaoundesha, kuingilia maisha ya ndani ya watu wengine na dini zao?  Suala la msichana huyu wa ki – Islamu kuambiwa afunue  kichwa chake wakati akiwa katika eneo la Shule halipaswi  kutokea.  Hali kadhalika kuwanyima watoto haki yao ya elimu kwa sababu wanavaa vilemba si ya kuvumiliwa.”

 

13. SHERIA YA KIISLAMU YA MIRATHI:

 

Tumepata kuelewa kwamba Serikali inakusudia kufanya mabadiliko katika sheria ya ki-Islamu ya mirathi. Tulikerwa mno na habari hizi:  Kama tulivyo wasilisha mapema, Qur’an Tukufu imeweka kwa usahihi na uwazi mno zaidi hukumu zinazohusiana na mirathi, kwa ufafanuzi kabisa ikitoa kwa warithi mbali mbali migao yao katika mali ya Mwislamu marehemu.  Sheria ya ki-Islamu ni chombo kilichofumwa vizuri.  Hatuwezi kubadilisha au kurekebisha moja au mbili ya mambo yake bila kuharibu ufumaji wote.  Kwa mfano, katika sheria ya ki-Islamu mtu hawezi kutumia kitu kilichopatikana kiharamu (katika maana ya dini), amma kwa kidunia au kwa madhumuni ya kidini.  Kwa hiyo kama madiliko yanafanywa katika Sheria ya mirathi, kwa maana hiyo mtu fulani kwa kawaida atapata zaidi kuliko mgao wake  (ule ambao amegaiwa na Qur’an Tukufu).  Pato hilo la haramu litafanya maisha yake yote kuwa duni.  Maisha yake ya kila siku yatakuwa ni orodha ndefu ya  madhambi na kuchupa mipaka.  Sala zake zitakuwa batili; Hija yake itakuwa batili na kutenguka; hata chakula chake na mavazi vitakuwa  haramu katika maana ya dini.  Mtu kama huyo kamwe hawezi kutarajia amani katika maisha ya kesho akhera.

 

14. Hatujui ni nini maana halisi ya zoezo hili.  Kwa hiyo hatuwezi kusema zaidi kwa sasa.  Lakini tunarudia kusema kwamba sheria hizi zimeegemezwa juu ya Qur’an Tukufu na haiwezekani kuweka mpaka baina ya Sheria hizi na Qur’an Tukufu.  Jambo lolote la kubadilisha migawanyo ya ki – Qur’an itakuwa sawa na kubadilisha Qur’an Tukufu .

 

15. Hata hivyo, katika mintaarafu hii, tungetaka kuvuta nadhari yako Mheshimiwa kwenye Amri ya Taarifa mpya ya Sheria ya ki-Islamu ya Serikali ya Tanzania (Na. 56 ya 1964), ambayo chini yake, kazi ilianzishwa ya kupanga kanuni za Sheria za ki-Islamu, ikitoa utambulisho halisi kwa madhehebu.  Sura nne zinazo husika na Ndoa, Ulinzi wa watoto n.k. zilichapishwa pia kama sheria ndogo chini ya sheria hiyo katika nyongeza  ya Gazeti Na 34 la 27 Juni 1967.  Ilikuwa ni hatua ambayo ilifurahisha Umma wote wa Ki-Islamu wa nchi hii. Kwa bahati mbaya mpango ule uliachwa.  Bado, kama mpango ule utahuishwa, ambao kwayo hukumu za kila Madhehebu zinatambuliwa kama Sheria zitumikazo kwenye Jumuiya hiyo, na  sheria  hizo zikapangiwa kanuni katika juzuu moja kwa rejea za urahisi kwa Mahakama za Sheria, itakuwa hatua ya kusifia sana ambayo kwamba Umma wote wa Waislamu wa Tanzania watakuwa siku zote na shukurani kwako wewe Mheshimiwa.

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

MAHAKAMA YA KADHI:

BAADHI YA MAPENDEKEZO*

 

Waislamu nchini kwa muda mrefu wamekuwa wakidai kuwepo na Mahakama ya Kadhi katika Tanzania itakayoangalia na kushughulikia mambo maalum ambayo yanajumuishwa zaidi na Sharia za Kiislamu kuliko Sheria za Mahakama za kawaida.

 

Ukweli kwamba tayari ipo Mahakama ya Biashara (Uchumi), ni uthibitisho tosha kwamba mambo maalum (ya aina moja) yanahitaji kushughulikiwa na Mahakama maalum ambayo vitabu vya Sheria vya kawaida huyafafanua kwa nadra (uchache).

 

Hata hivyo, tayari inakubalika kimsingi kwamba hakuna utata katika suala hili, kwani Rais Benjamin Mkapa ameshasema atayashughulikia matatizo yote yanayowakera Waislamu na kuhakikisha kuwa Waislamu wote nchini hawajisikii kunyanyaswa kwa vile sera ya Chama tawala (Serikali) ni Usawa miongoni mwa Wananchi wake, bila kujali jinsia, rangi (Utaifa), au Dini.

 

Kwa mantiki hii, mapendekezo kadhaa yanatolewa kuisaidia Mahakama ya Kadhi iweze kufanya kazi zake kwa ufanisi na kupatikana madaraka kamili ya kisheria ya Mahakama ya Kadhi.

 

Ili Mahakama iweze kupata hadhi yake, haya ni mapendekezo ambayo yangeweza kusaidia kufikia lengo hilo.

 

 Mswada unalenga kuanzishwa kwa Mahakama ya Kadhi katika kila Wilaya ya Tanzania, ili kuangalia mambo yote yahusianayo na Sharia ya Kiislamu katika masuala ya Ndoa, talaka, haki ya kulea watoto, mgawanyo wa mali, Urithi n.k. pale ambapo wahusika wa utata huo ni Waislamu, waliooana kwa mujibu wa sharia na desturi ya ndoa za Kiislamu.

 

Ukweli ni kwamba makusudio ya mswada huu ni mazuri, lakini upo uwezekano mkubwa kwamba kutokana na ukosefu wa Kitabu makhususi cha Sheria za Kiislamu, Makadhi katika wilaya mbali mbali wakifikia kwenye uamuzi wa kesi zinazofanana, wanaweza wakatoa hukumu zinazopingana.

 

Hivyo, upo umuhimu wa kukiandaa kitabu makhsusi kitakachotumika kama Mwongozo wa Makadhi ili kuiepuka migongano.

 

Hapo zamani mwaka 1964, Bunge la Tanganyika kwa wakati huo  lilipitisha “Sharia ya Kiislamu (Sheria ndogo)” iliyompa madaraka Waziri aliyehusika na mambo ya Sheria kuandaa na kuchapisha kipengele cha Sharia ya Kiislamu baada ya kushauriana na wanachuoni wa Sharia za Madh-hebu za Kiislamu.

 

Katibu Mkuu wa Bunge wakati huo, alikamilisha kuandika Mswada wa ndoa wenye sehemu 4 (kama ulivyokubaliwa na wanachuoni wa Sharia za Kiislamu kutoka Madh-hebu matatu Kiislamu Shafi’i, Hanafi na Shia).

 

Mswada huu uliotolewa kama Sharia ndogo chini ya kifungu kidogo cha Sharia ya Kiislamu (Na: 56 ya mwaka 1964) ikiwa ni sehemu ndogo ya Gazeti la Serikali na Na: 34 la tarehe 27, Juni, 1967.

 

Ilifahamika kuwa sehemu zilizosalia, kuhusiana na kuwalea watoto na talaka n.k. zingechapishwa mapema. Lakini zoezi hili lilisitishwa na badala yake serikali ilitunga sheria ya ‘Ndoa’ kupitia Mswada wa Ndoa wa mwaka 1971.

 

Hata hivyo, kanuni ya Sheria ya Ki-Islamu 1964 bado haijafutwa na bado ni sehemu ya Kitabu cha Bunge. Na kwa sababu sasa serikali inakusudia kuanzisha Mahakama za Makadhi katika kila Wilaya, ni wakati muafaka wa kufufua tena mswada wa sheria ya Kiislamu ya mwaka 1964 ili ufanyiwe kazi na kazi hii ianzie pale ilipoachiwa.

 

Jambo muhimu hapa ni kuepusha uwezekano wa Makadhi kutoa hukumu zitakazoleta utata. Vinginevyo, mzigo wa kazi za Mahakama Kuu utaongezeka kwa kuwa rufani kutoka Mahakama za Makadhi zitajazana kwenye Mahakama ya Rufaa.

 

Madhehebu za Makadhi wa Wilaya:

 

Kwa vile Waislamu wengi wa Tanzania ni wafuasi wa Madhehebu ya Shafii ni vizuri makadhi wa Wilaya watokane na Madhehebu ya Shafii.

 

Lakini iwapo wahusika au mhusika wa mgogoro ni wa Madhehebu isiyo ya Shafii, inapendekezwa kuwa Kadhi wa Wilaya asaidiwe na wanachuoni wa madh-hab inayohusika.

 

Hii itafuta uwezekano wa kutolewa hukumu isiyo sawa na itawapa imani ya kutendewa haki wahusika au mhusika. Wasaidizi wa Kadhi wa Wilaya waliotajwa hapo juu itabidi watayarishwe katika kila Wilaya na wanaweza kuangaliwa upya (kuteuliwa) muda baada ya muda.

 

Iwapo mapendekezo mawili muhimu yaliyotajwa hapo juu katika makala haya yatakubalika na kufanyiwa kazi, itakwenda hatua kubwa kuwatendea haki na usawa Waislamu wote nchini.

                          

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 



* Uliwasilishwa mbele ya Tume ya Serekali ya Kenya juu ya Sheria za Ndoa, Talaka na Mirathi; kwa niaba ya Khoja Shia Ithna – asheri (Supreme Council of Africa, Mombasa) 22/8/1967

 

 

* Uliwakilishwa mbele ya Tume ya Serikali ya Kenya juu ya Sheria za Ndoa, Talaka na Mirathi: kwa niaba ya Khoja Shia Ithna-Asheri Supreme Council of Afrika Mombasa, 1967.

 

 

* Imechapishwa katika Standard (Dar es Salaam) Jumatatu, 1969 kwa niaba ya Khoja   Shia Ithna-Asheri Territorial Council of Tanzania.

 

* Uliwasilishwa kwa Mheshimiwa Al-Haj Sheikh  Ali Hassan Mwinyi, Rais wa Muungano wa Jamhuri ya Tanzania, kwa niaba ya wawakilishi wa Mashirika (Taasisi) mbali mbali ya Ki-Islamu ya Dar es Salaam mwaka 1990

* Imechapishwa katika  The Democrat (Dar es Salaam) Aug 17-23,1999.