WALID NA HARUN RASHID

Na haikukomea hapo tu. Inaonyesha kuwa matendo haye yalikuwa yakitendeka mara kwa mara. Walid bin Yazid bin Abdul Malik alikuwa Khalifa mwingine wa ukoo wa Bani Umayyah. Yeye alikuwa mlevi. Usiku mmoja alikesha akinywa pombe na mmoja wa suria wake hadi waliposikia Adhana ya Sala ya Alfajiri. Walid akaapa kuwa yule suria wake atasalisha. Hivyo yule suria akavaa joho Ia Khalifa na akasalisha katika hali ile ya ulevi na uchafu.

Siku moja Walid alimwona binti wake msichana wa miaka kumi hivi ambae bado hajaolewa na akamkera sana kwa kumtaka mapenzi. Mwanamke mtumishi wake alikuwepo pale kakaa. Yule mwanamke akasema kuwa (hakuwa Uislamu ule alioufanya Khalifa bali) ilikuwa dini ya Majus. Walid akajibu:

"Mtu anayejali ndimi za watu, hufa katika hali ya masikitiko; na mtu athubutuye kupata fahari zote."

Harun Rashid, Khalifa mashuhuri atajwaye katika kitabu kiitwacho "Alfu leIa-u-lela" anayedhaniwa na wanahistoria wa Kiislamu kuwa ni mmoja wa Makhalifa wakubwa, alitaka kulala na suria wa baba yake aliyefaiki. Yule mwanamke alisema kuwa isingeiIiwezekana kwa sababu alikuwa mama yake wa kambo. Harun Rashid alimwita Qadhi Bwana Abu Yusuf na kumtaka atafute njia ya kumtoshelezea haja yake. Qadhi huyo akasema:

"Yeve (mwanamke) alikuwa mjakazi tu. Je, wewe utakubali vyo vyote vile asemavyo? Hapana. Usikubali kila asemacho kuwa ni kweli."

Hivyo Khalifa huyo alitosheleza matakwa yake na mwanamke huyo. Bwana lbn Mubaraka anasema:

"Sifahamu ni nani miongoni mwa watu hawa watatu aliyekuwa akishangaza sana, Khalifa anayechovya mkono wake katika damu na mali za Waislamu na ambaye hakumstahi mama yake wa kambo; au mjakazi aliyekataa kutosheleza haja ya Khalifa; au Qadhi aliyemruhusu Khalifa kumfedhehesha baba yake na kulala na yule Suria aliyekuwa mama yake wa kambo".

Nasi twaambiwa kuwa watu hao walikuwa 'Ulul Amr' waliotajwa katika aya hii.

Hebu ngoja tuirudie ile sentensi iliyoandikwa mwanzoni mwa habari hii. Kama Allah angetulazimisha kuwatii wafalme kama hawa, hali mbaya ingetokea kwa Waislamu. Waislamu wangeghadhibikiwa na Allah, kwa cho chote kile wakifanyacho. Iwapo watawatii watawala hawa, watakuwa wameasi Amri ya Allah isemayo;

"Wala msimtii miongoni mwao mwenye dhambi........"

(Qur'ani 76:24).

Na iwapo watawaasi watawala hao, watakuwe vile vile wameiasi amri ya Allah ya Watii watawala wa Kiislamu".

Sasa, kama tukiikubali tafasiri ya Masunni, itaonekana kuwa Waislamu watapata laana ya milele iwapo watawatii au watawaasi watawala wao wasio 'Ma'asum.'

Vile vile wako watawala we Kiislamu wa imani na madhehebu mbali mbali. Wako Shaafi, Mawahhabi, Maliki, Hanafii na vile vile wako Shia na lbadhi. Kwa kutegemeana na tafsiri hii, Masunni waishio katika nchi ya Sultani we Kiibadhi (kama vile Masqat) itawabidi wafuate mafundisho ya Kiibadhi; na wale waishio katika nchi ya Kishia (kama vile Iran) itawabidi wafuate mafundisho ya Kishia.

Je, watu hawa wanao uthibitisho wa nia zao wa kuifuata tafsiri yao kwa kadri ya hoja zake?

'Mufassir' mashuhuri wa Kisunni lmamu Fakhruddin Razi, ilimbidi akubali katika kitabu chake kiitwacho 'Tafsiir Kabir', kuwa aya hii inathibitisha kuwa 'Ulul Amr' ni lazima wawe 'Ma'asum'. Hoja alizozitoa ni kuwa Allah Amewaamrisha wanaadamu kuwatii "Ulul Amr" bila ya kutoa masharti yoyote; hivyo basi ni lazima "Ulul Amr" wawe 'Ma'asum'. Kwa sababu, iwapo upo uwezekano wa wao kufanya dhambi yoyote ile (na hali kufanya dhambi kunakatazwa) ingekuwa na maana kuwa mtu angelazimika kuwatii na vile vile kuwaasi katika tendo hilo (lililo dhambi),na hali jambo hili haliwezekani. Hivyo Bwana Fakhruddin Razi akabunia njia nyingine yakusemakuwa taifa Ia Kiislamu kwa ujumla ni 'Ma'asum'.

Tafsiri hi ni yake yeye tu, maana hakuna mwanachuoni mwingine wa Kiislamu aliyeitumia njia hii, na wala haimo mwenye msingi wa Hadithi yoyote ya Mtume [s].

Hakika inashangaza kuona kuwa, lmamu Fakhruddin Razi anakubali kuwa kila mtu wa taifa lile (yaani taifa Ia Kiislamu) si Ma'asum; na vivyo bado anadai kuwa jumla yao ni Ma'asum.

Hata mtoto wa shule ya msingi anafahamu kuwa 200a + 200a itakuwa 400a na wale si lx.

Lakini tunatakiwa tuamini kuwa watu milioni 70 wasio Ma'asum ukiongeza wengine milioni 70 wasio Ma'asum utapata Ma'asum mmoja. Mshairi mmoja wa pande za Asia, Bwana Iqbal alisema:

"Akili za punda 200 heziwezi kutoa wazo Ia mtu mmoja."

Ni wazi kuwa uamuzi wa lmamu Razi kuwa 'Ulul Amr' ni lazima wawe Ma'asum, unatokana na elimu aliyokuwa nayo, lakini usemi wake kuwa "Ma'asum" meana yake ni taifa Ia Kiislamu, unatokana na chuki fulani.

Vile vile hakuacha kuonyesha wazi kuwa Aya yenye neno 'Minkum' (toka miongoni mwenu) inaonyesha kuwa hao 'Ulul Amr' watakuwa ni sehemu ya taifa Ia Kiislamu, na wala sio taifa zima Ia Kiislamu.

Na kama taifa zima Ia Kiislamu lingetiiwa, basi ni nani ambaye angelibakia kutii?

Sasa turudi kwenye tafsiri sahihi ya Aya hiyo hapo juu.

lmamu Ja'far Sadiq [a] alisema kuwa aya hii iliteremsha kuhusu Hadhrat Ali bin Abi Talib [a], lmamu Hasan [a] na lmamu Husayn [a].

Mtu mmoja alipomsikia lmamu Ja'far As-Sadiq [a] akisema hivyo, alisema kuwa watu husema kuwa mbona Allah Hakuyataja majina ya Ali na jamii yake katika kitabu chake?

lmamu Ja'far [a] akasema: "Waambie kuwa, ililetwa amri ya Sala, lakini Allah hakutaja rakaa 3, au 4 na ilikuwa ni kazi ya Mtume wa Allah [s] kueleza kwa kirefu. Na tena Zakaat iliamrishwa lakini Allah hakueteza kuwa ilikuwa itolewe dirham moja katika kila dirham arobaini; na ni Mtume wa Allah [s] aliyeeleza. Hija iliamrishwa vile vile, lakini Allah Hakuamrisha kufanya Tawafu mara 7. Mtume wa Allah [s] ndiye aliyeeleza kuwa tufanye Tawaf tufanyapo Hija. Aya hii izungumziayo juu ya 'Ulul Amr' mfano wake ni kama aya zihusuzo mambo tuliyoyataja hapo juu.

"Mtiini Allah na mtiini Rasuli na wala walio na mamlaka toka miongoni mwenu" na (hii aya) iliteremshwa kuhusu Hadhrat Ali [a] na Hasan [a] na Husayn [a]. (Uthibitisho huu umeandikwa katika kitabu kiitwacho 'Tafsiir Safi kama ulivyonakiliwa kutoka katika kitabu kiitwacho Kafi na kitabu kiitwacho Tafsiir Ayyashi.)

Katika kitabu kiitwacho "Kifayat-ul-Athar" iko hadithi iliyopokewa kutoka kwa Jabir bin Abdallah Ansari, ielezayo aya hii. Hadithi hiyo inasema kuwa, ilipoteremshwa aya hii Bwana Jabir alimwuliza Mtume [s] akisema:

"Tunamjua Allah na Mtume [s]lakini ni nani watu hawa walio na madaraka ambao utii kwao umeungwa pamoja na utii kwa Allah na wewe - Mtume [s] akamjibu: "Hao ni makhalifa wangu na Maimamu wa Waislamu baada yangu. Wa Kwanza ni Ali, kisha Hasan, Kisha Husayn, kisha Ali bin Husayn, kisha Muhammad bin Ali ambaye katika Taurat ameitwa Baqir. Ewe Jabir! Wewe utamwona. Umwonapo nitolee salaamu zangu kwake. Atarithiwa na mwanewe Ja'far Sadiq - Mkweli, kisha atafuatia Musa bin Ja'far, kisha Ali bin Musa, kisha Muhammad bin Ali, kisha Ali bin Muhammad, kisha Hasan bin Ali, kisha Muhammad bin Hassan.

"Yeye (Muhammad bin Hasan) atauteka ulimwengu wote toka Mashariki hadi Magharibi. Wakati wote atakoakuwa katika Ghaibu (kutoonekana katikamacho ya wafuasi na maratiki zake, imani ya Uimamu wake itabakia katika nyoyo zile tu ambazo Allah kazijaribu kuhusu imani zao."

Hadithi hii imenakiliwa kutoka vitabu vya Kishia. Waandishi wa Kisunni wameiandika Hadithi hii kwa kifupi, lakini ziko Hadithi nyingi za Kisunni zizungumziazo kuhusu hawa Maimamu kumi na wawili. Msomaji anaombwa asome Sura ya 77 ya kitabu kiitwacho 'Yanabi-uI-Mawaddah' cha Sheikh Hafidh Sulaiman bin Ibrahim Qanduzi Hanafi, aliyefariki mnamo mwaka 1294 Hijiriya.

Kwanza kabisa Sheikh huyo ameinakili ile Hadithi mashuhuri sana isemayo:

"Watakuwepo Makhalifa kumi na wawili, wote kutoka miongoni mwa Makuraishi".

Hadithi hii imeandikwa katika vitabu vingi sana miongoni mwa vitabu hivyo vikiwemo vitabu vya Mabwana Bukhari, Muslim, Abu Dawuud na Tirmidhi.

Kisha amenakili Hadith nyingi sana zithibitishazo kuwa, Mtume [s] alisema:

"Mimi, Ali, Hasan, Husayn na watu tisa kutokana na kizazi cha Husayn ni Safi na Ma'asum".

Vile vile amenakili Hadithi isemayo kuwa Mtume [s] alimwambia Imamu Husayn [s]:

"Wewe ni Sayyid mwana wa Sayyid, ndugu wa Sayyid; Wewe ni lmamu, mwana wa lmamu, ndugu wa lmamu, wewe ni uthibitisho (wa Allah), ndugu wa uthibitisho wa AlIah na baba wa thibitisho tisa (za Allah), ambao wa tisa wao atakuwa Mahdi."

Baada ya kunakili hadithi nyingi za aina hiyo, anaendelea kusema:

"Wanachuoni wengi wamesema kuwa Hadithi (zionyeshazo kuwa Makhalifa baada ya Mtume [s] watakuwa kumi na wawili) ni mashuhuri, zitokanazo na Asnaad (nyororo ye watu waliosikia Hadithi hiyo mmoja toka kwa mwingine) nyingi. Sasa kutegemeana na muda upitavyo na matokeo ya kihistoria, tunajua kuwa, kwa Hadithi hii, Mtume [s] alikuwa na maana ya Maimamu kumi na wawili kutokana na Ahlul-Bait na Dhuria wake."

Kisha ametoa sababu zithibitishazo kuwa Hadithi hizi haziwezi kuwa zinazungumzia kuhusu Khalifa Rashidiin wane, wala wafalme kutoka katika nyumba ya Umayyah wala wale watokao katika nyumba ya Abbas.

Mwisho kabisa anasema:

"Hivyo basi, njia ifaayo tu, kwa kuitafsiri Hadithi hi ni kukubali kuwa inazungumzia kuhusu Maimamu kumi na Wawili kutokana na Ahlul-Baiti wa Mtume [s] na Dhuria wake, kwa sababu walikuwa watu waliokuwa na Elimu zaidi katika zama zao, waliomwongopa Allah zaidi, wachamungu zaidi, waliokuwa wa kiwango cha juu sana katika nasaba yao, wabora zaidi katika matendo, watukufu zaidi mbele ya Allah, na Elimu yao ilitokana na jadi zao (Mtukufu Mtume [s]), kupitia kwa baba zao, na kwa njia ya kurithi na mafunzo ya moja kwa moja kutoka kwa Allah."

Sasa tunajua ni nani wale 'walio na mamlaka", na sasa tunaweza kuona wazi wazi kuwa suula la kuwatii watawala waonevu na dhalimu halihusiani hata kidogo na aya hii. Waislamu hawawajibishwi kwa aya hii kuwatii, "Watawala wenu" ambao wanaweza wakawa wadhalimu, waonevu, wajinga, wachoyo na waliojitumbukiza katika uasherati Waislamu wanaamrishwa na aya hii kuwatii Maimamu 12 ambao wote walikuwa watakatifu na wote walitakasika na kila aina ya mawazo au matendo mabaya. Kuwatii Maimamu hawa hakuna hatari yoyote. Kunatuliano kutokana na hatari ya aina yoyote; kwa maana Maimamu hawa hawatatoa amri yoyote kinyume cha Penzi la Allah na watawafanyia banaadamu wote upendo, haki na usawa.