"ULUL AMR" NI NANI?

Allah Anasema katika Kitabu chake kitukufu:

"Enyi mlioamini Mtiini Allah, na mtiini Rasuli (Wake Muhammad) na Wale waliopewa mamlaka kutoka miongoni mwenu, ......

(Qur'ani, 4:59)

Aya hi inawawajibisha Waislamu aina mbili za utii. Kwanza, kumtii Allah; Pili kumtii Rasuli. Hii ina maana kwamba ni lazima "Ulul Amr" wawe na heo kama kile cha Rasuli; au sivyo Allah Asingekuunga kuwatii wao na kule kumtii Rasuli, katika Aya hii.

Kabla hatujaamua ni nani hao "Ulul Amr", ingetusaidia sana kama tungeitazama ile amri ya kumtii Rasuli [s], ili tuone jinsi amri hii inavyozunguka na kuenea kote-kote, na jinsi mamlaka ya Rasuli wa Allah [s] ilivyo kuu.

Allah Anasema katika Qurani Tukufu:

"Na Hatukumtuma Rasuli yeyote ila atiwe kwa idhini ya Allah..."

(Qur'ani 4:64)

Ilibidi Manabii na Marasuli watiiwe na kufuatwa, sio kwamba hao wafuasi walitegemewa kukicheki kila kitendo cha Nabii na kuamua kipi kitiiwe na kipi kisitiiwe. Hii inathibitisha wazi wazi kwamba, Manabii na Marasuli walikuwa Maasumiin (Wasiotenda madhambi wala kukosea); na lau isingekuwa hivyo, Allah Asingewamrisha watu kuwatii Marasuli bila ya masharti yoyote.

Ziko Aya nyingi za Qur'ani Tukufu ambazo ndani yao Allah Anatuamrisha kumtii Rasuli, Akisema:

"Enyi mlioamini: Mtiini Allah na mtiini Rasuli........"

Tena Allah Anasema:

"Na mwenye kumtii Allah na Rasuli........."

(Qur'ani 4:69)

Sura hiyo hiyo inathibitishwa kwamba:

"Mwenye kumtii Rasuli amemtii Allah........"

Katika aya zote hizi za Qur'ani Tukufu na nyinginezo nyingi, utii kwa Allah umefanywa kuwa sawa na uti kwa Rasuli. Uthibitisho huu usingewezekana kama Manabii wasingekuwa Ma'asumiin na Watakatifu.

Sasa hebu ongezea aye hii ifuatayo katika aya tulizozitaja hapo juu:

"...Wala usimtii miongoni mwao mwenye dhambi."

(Qur'ani 76:24)

Sasa picha imekamilika. Inabidi kuwatii Manabii. Watendao madhambi wasitiiwe: Hivyo, uamuzi ni kwamba, Manabii si watenda madhambi. Kwa usemi myingine ni kwamba, Manabii ni Ma'asumiin (Watakatifu) na Wasiotenda Madhambi.

Hebu fikiria ni hali gani ambayo ingetokea kama Nabii yeyote yule angewasihi wafuasi wake wafanye kosa fulani au dhambi. Kwa vyo vyote vile hawa wafuasi waovu wangelaaniwa na kuipata ghadhabu ye Allah. Kama wakimtii Nabii yule na kuitenda ile dhambi wangekuwa wameihalifu amri ya Allah na hivyo wangefedheheshwa. Na kama kwa upande mwingine, wakimwasi yule Nabii, vivyo wangekuwa wameiasi amri ya Allah tuliyoitaja hapo juu yenye kuhusu kumtii Nabii. Hivyo yaonekana kwamba Nabii asiye Ma'asuum asingeweza kuwaletea watu wake cho chote kile iIa fedheha na laana tu.

Tukimtazama hasa Mtukufu Mtume wetu [s] tunaona kwamba Allah Ametuamrisha Akisema:

"...Na anachokupeni Rasuli basi kipokeeni; na anachokukatazeni jiepusheni nacho...."

(Qur'ani, 59:7)

Hii ma maana kwamba, kuruhusiwa au kukatazwa na Mtukufu Mtume [s] kila mare kulikuwa kukitegemeana na Mapenzi ya Allah na kila mara Alikupenda. Hii inathibitisha kwamba Mtukufu Mtume [s] alikuwa Ma'asum. Hakuna mtu awezaye kuwa na uhakika kabisa kabisa juu ya amri azitoazo mtu asiye Ma'asum.

Iko aye nyingine isemeyo:

"Sema (ewe Rasuli wetu Muhammad); Kama ninyi mwampenda Allah, basi nifuateni (na) Allah Atakupendeni na Atakughofirieni madhambi yenu...."

(Quran, 3:31)

Katika aya hii, kumpenda Allah kumetegemezwa na kumfuata Mtukufu Mtume [s]. Pande zote mbili za mapenzi zimejumlishwa ndani yake. Kama unampenda Allah basi mfuate Mtume [s] kama ukimfuata Mtume [s] Allah atakupenda. Je, hii haionyeshi kwamba Mtukufu Mtume [s] alikuwa katoharika kabisa na kila aina ya dosari?

Si matendo yake tu, bali hata maneno yake yalikuwa ni amri ya ya Allah. Allah Anasema katika Qur'ani Tukufu:

"Wala hasemi (huyu Rasuli Wetu Muhummed) kwa matamanio yake. Sio hayo ila ni ufunuo uliofunuliwe kwake."

(Qur'ani, 53:3-4)

Katika aya hizi tunaiona daraja ya hali ya juu sana ya Utakatifu awezayo kuifikiria mtu.

Vile vile ziko aya kadhaa katika Qur'ani Tukufu ambazo ndani yake maneno yafuatayo yametumiwa kwa ajili ye Mtukufu Mtume wetu [s].

".... Rasuli kutoka miongoni mwao, awasomee ishara zake na kuwatakasa na kuwafunza Kitabu na Hekima......"

(Qur'ani, 62:2)

Vipi Nabii ataweza kuwatakasa watu kutokana na madhambi na dosari iwapo yeye mwenyewe si Mtakatifu. Vipi mtu ataweza kuwefundisha wenzie hekima ikiwa yeye mwenyewe hana hekima imwezeshayo kupambanua baina ye ukweli na uwongo - Au lililo baya zaidi, pale akosapo uwezo wa nia ye kujizuia kutenda uovu pale anapoufahemu - Kazi ya Mtukufu Mtume [s] ilikuwa kuwafundisha watu Kitabu cha Allah. Hii ina maana kwamba yeye Mtukufu Mtume [s] alizijua amri za Allah.

Ilikuwa kwamba awatakase na kuwafundisha hekima; hii ina maana kwamba yeye mwenyewe alikuwa ne hekima na tohara.

Uthibitisho wa ukamilifu wa tabia zake unapatikana katika Qur'ani Tukufu, katika aye isemayo:

"Na hakika (Wewe Rasuli Wetu Muhammad) une tabia njema adhimu"

(Qur'ani, 68:4)

Mtu atendaye maovu hawezi kuistahili sifa hii. Aya zote hizi zaonyesha mambo mawili:

Jambo Ia Kwanza: Mamlaka ye Mtukufu Mtume [s] juu ya Waumini haina kikomo na ni yenye kuenea kote kote. Amri yoyote aitoayo, katika hali yoyote ile, mahali popote pale, na wakati wowote ule, ni wajibu kuitii bila ya swali lolote lile.

Jambo Ia Pili:
Ni kwamba, yeye alipewa mamlaka kubwa sana kwa sababu ni "Ma'asum" (Mtakatifu) na katoharika kutokana na makosa, na madhambi. Isingekuwa hivyo, Allah Asingetuamrisha kumtii bila ya masharti yoyote yale.

Sasa katika aya hii (Qur'ani, 4:59), hawa "Ulul Amr" wamepewa mamlaka iliyo sawa kabisa na hii juu ya Waislamu, kwa sababu wote, "Rasuli" na hawa "Ulul Amr" wametajwa kwa pamoja, chini ya neno moja, Ati-'uu" (Mtiini) jambo ambalo laonyesha kwamba kuwatii "Ulul Amr" kuna maana ile ile ya kumtii Rasuli.

Hii yaonyesha kwamba "Ulul Amr" nao ni lazima wawe "Ma'asum" (Watakatifu), na waliotakasika kabisa kutokana na kila aina ya makosa, ne madhambi, au sivyo amri ye kuwatii wao isingeungwa na amri ya kumtii Rasuli [s].

lmamu wetu wa kwanza AmiruI Muminiin Ali bin Abi Talib [a] alisema:

"Yeyote yule amwasiye Allah asitiiwe; na hakika utii ni wa Allah na Rasuli Wake na wale waliopewa mamlaka. Hakika Allah ameamrisha kumtii Rasuli kwa sababu yu Ma'asum, aliyetoharika na ambaye katu hatawaamuru watu kumwasi Allah; na hakika Ameamrisha kuwatii wale waliopewe mamlaka kwa sababu wao (nao) si watenda madhambi; wametoharika na hawawezi kuwaamuru watu kumwasi Allah."

(Kifungu hiki kimenukuliwa kutoka kitabu 'Ilalu Sharaye", kama kilivyonakiliwa katika Tafsiir Safi).

Kabla hatujaendelee zaidi, inatulazimu tueleze kuwa Waislamu wengi (Masunni) huyatafsiri maneno haye "Ulul Amr" kuwa na maana ye 'Watawala kutoka miongoni mwenu, yaani watawala wa Kiislamu. Tafsiri hii haina msingi wo wote wa kihoja. Hoja yake imesimama katika msingi wa upotoshaji wa historia ya Kiislamu. Waislamu wengi wamekuwa vibaraka wa wafalme na watawala wakiutafsiri Uislamu na Qur'ani kwa kurudia ili kuwaridhisha watawaIa wa kila zama.

Ulikuwepo wakati ambao ufalme ulikuwa aina ya pekee ya utawala iliyotumika. Katika zama hizo wanachuoni wa Kiislamu walikuwa wakiwatukuza wafalme na milki zao kwa kusema kuwa "Mfalme ni kivuli cha Allah" (Kana kwamba Allah ana kivuli). Siku hizi demokrasi ndio mtindo wa serkali na wanachuoni wa Kisunni hawachoki kuthibitisha katika maandishi yao, vitabu vyoa na matoleo yao kuwamsingi wa Utaratibu wa serikali ya Kiislamu ni demokrasi. Huendelea hata kuthubutu kusema kuwa demokrasi ilianzishwa na Uislamu, wakisahau kabisa Jamhuri za miji ya Uyunani (Ugiriki) za zamani sana hata kabla ya Uislemu. Katika nusu ya pili ya karne hii, ujamaa na ukomujisti vinazidi kuenea katika nchi zinazoendelea na wala sitashangaa kusikia kuwa wanachuoni wa Kiislamu wanajaribu kila wawezacho ili kuthibitisha kuwa Uislamu unafundisha na kujenga Ujamaa. Baadhi ya watu katika nchi ye Pakistani na mahali penginepo wamezua usemi usemao "Ujamaa wa Kiislamu." Maana hasa ya huu "Ujamaa wa Kiislamu", mimi sijui. Lakini mtu asishangae kuone kuwa katika muda wa miaka ishirini ijayo watu hawa hawa wataanza kudai kuwa Uislamu unafundisha Ukomunisti.

Mambo yote haya hubadilika ili kuudhihaki utawale wa Kiislamu.

Miaka michache iliyopita katika mkutano wa Waislamu uliofanyika katika nchi ya Kiafrika, ambao rais wa nchi hiyo alikuwa mgeni wa heshima, kiongozi wa KiisIamu alisema katika hotuba yake kuwa Uislamu unafundisha "Mtiini Allah, Mtiini Rasuli na watawala wenu'.

Katika Jibu lake, rais huyo (ambeye aliheshimiwa ulimwenguni pote kuwa yu kiongozi mwenye hekima na ambaye alikuwa ni Mkristo wa Kanisa Katoliki), alisema kuwa alipendezewa sana na hekima iliyomo katika amri ye kumtii Allah na Rasuli wa Allah, lakini hakuweza kuelewa hoja za amri ya kuwatii watawala wenu. Je, vipi iwapo mtawala huyo atekuwa mdhalimu na mwonevu? Je, Uislamu unaamrisha kumtii mtawala huyo kabisa kabisa bile ye kumpinga?

Hakika swali hili Ia kihekima linahitaji jibu Ia kihekima vile vile, wala haliwezi kutupiliwa mbali. Ukweli ni kuwa kiongozi yule wa kidini aliyesema vile, kasema kutokana na kuitafasiri vibaye Qur'ani. Historia ya Kiislamu imejaa majina ya watawala ambao udhalimu wao, uasherati wao na uonevu vimeiiharibu jina Ia Uislamu. Watawala kama hao kila mara wamekuwepo na bado wapo na watakuwepo hata pengine zaidi ya hao.

Ili kukupa mifano michache:

Yazidi bin Muawiyyah: Alikuwa Khalifa wa Uislamu. Lakini imani yake na tabia zake viIikuwaje? Yeye alikataa kabisa kumwamini Mtukufu Mtumte [s]. Alionyesha wazi wazi imani yake katika Shairi lake lisemalo:

"Bani Hashim (Mtume [s] na AhIul-Bait wake) walivumbua mbinu za kupatia milki. Kwa hakika hakukuwepo na habari zozote zitokazo kwa Mwenyezi Mungu wala Ufunuo wowote."

Yazid hakuamini siku ya Mwisho. Anasema:

"Enyi wapenzi wangu (msiamini kuwa mtakutana nami baada ye kufa kwangu maana) yale walivokuambieni kuhusu kufufuliwa baada ya kufa, kwa ajili ye Hukumu ni uzushi uufanyao moyo uzisahau fahari (za ulimwengu huu wa kweli)."

Baada ya kuupata Ukhalifa, aliidhihaki Sala ya Kiislamu waziwazi; akaonyesha kutoiheshimu dini kwa kuwavisha mbwa na ngedere mavazi ya viongozi wa kidini. Kamari na kucheza na madubu vilikuwa michezo yake ya kawaida. Alitumia muda wake wote katika kunywa kila mahali bila ya kusita; hekuwa na heshima kwa mwanamke ye yote na hata 'mahramu' wake kame vile mama, umbu, shangazi, mama mdogo na binti. Hawa wote walikuwa sawa na wanawake wengine mbele yake.

Mauwaji ya watu wa Nyumba ya Mtume [s] aliyoyafanya yanajulikana sana. Ulimwengu unafahamu kabisa yale yaliyotokea huko Karbala na jinsi lmamu Husayn [a] na masahabe wake na ndugu zake (akiwemo mtoto mwenye umri wa miezi sita) na jinsi wote hawa walivyokufa kishahidi mnamo tarehe 10 ya Muharram (Mfunguo 4) mwaka 61 A.H. jinsi watukufu hao walivyowekwa na njaa na kiu tangu tarehe 7 hadi 10 ya mwezi huo; jinsi mahema yao yalivyochomwa na jinsi familia yake (wakiwemo wanawake, watoto na mwanawe aliyekuwa mgonjwa sana) walivyofanywa mateka na kupelekwa Kufa na baadaye kupelekwa Demeski; jinsi walivyotiwa jela kwa mwaka mzima kabla ya kufunguliwa. Mambo haya yanajulikana sana na hayana ulazima wa kuelezwa kwa kirefu hapa.

Baada ye mauwaji ya Karbala, Yazid alituma jeshi lake kwenda Madina. Mji huo Mtakatifu wa Mtume [s] ulitekwa nyara. Wasichane bikira mia tatu; achilia mbali wanawake wengine, walinajisiwa. "Quarii" (Wasomaji wa Tajwiidi) wa Qur'ani mia tatu na masahaba mia saba wa Mtume [s] waliuwawa kikatili. Msikiti Mtakatifu wa Mtume [s] ulifungwa kwa muda wa siku kadhaa; jeshi Ia Yazid liliutumia msikiti huo kama banda la farasi wao. Mbwa waliingia msikitini humo na Mimbari ya Mtume [s] ilinajisiwa na wanyama hao. Mwisho amiri jeshi wa Yazid aliwalazimisha watu wa Madina kumkubali Yazid kwa kuapa kwa meneno haya:

"Sisi tu watumwa wa Yazid; ni juu yake kutupa uhuru au kutuuza katika soko Ia watumwa."

Wale waliotaka kuapa kiapo cha utii kwa Yazid chini ya masharti ya kuwa 'Yazid afuate Qur'ani na Hadithi za Mtume [s] waliuawa.

Baada ya hapo, kwa amri ya Yazid jeshi lilikwenda Makkah. Mji huo wa Allah ulio mtakatifu kuliko yote duniani, ulizingirwa. Jeshi hilo halikuweza kuingia mjini humo, hivyo ikabidi askari watumie teo (fumbewe au kombeo-silaha ya kivita ya zamani sana iliyotumika kwa kutupia mawe mazito katika sehemu zilizo mbaIi).

Kwa kutumia teo walitupa mawe na vijinga vya moto katika Kaaba. 'Kiswa' (yaani nguo iifunikayo Kaaba ikaungua na sehemu ya jengo hilo takatifu ikaanguka.

Na sisi tunategemewa kuamini kuwa Yazid alikuwa mmoja wa 'Ulul Amr' ambae kumtii kulikuwa wajibu kama kule kwa Mtume [s].